Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AWASILI ARUSHA KUFUNGUA MKUTANO WA SITA WA WADAU WA NSSF

$
0
0



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha Oktoba 20, 2016 ambako alifungua mkutano wa sita wa Wadau wa NSSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC). Katikati ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama , Jenista Mhagama (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha ambako alifungua mkutano wa Sita wa NSSF kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Longido, Godfrey Chongolo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Arusha Oktoba 20, 2016 ambako alifungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) . Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI (NEC) JAJI MSTAAFU DAMIAN LUBUVA AKUTANA NA KUAFANYA MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI WA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA LEO

$
0
0
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Nyanduga (kulia) aliyetembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dar es salaam. Katikati ni Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Asina Omari.
 Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Nyanduga (wa pili kutoka kulia) aliyetembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dar es salaam. Wengine ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe , Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi - NEC, Asina Omari (wa pili kutoka kushoto) na Afisa Uchunguzi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Nancy Ngula (wa tatu kutoka kulia).
  Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akisisitiza jambo wakati akizungumza na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Nyanduga (wa pili kutoka kulia) aliyetembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dar es salaam.
 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Nyanduga (katikati) akimweleza jambo jambo Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) mara baada kutembelea Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe na Kushoto Bi. Nancy Ngula, Afisa Uchunguzi wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) jaji Mstaafu Damian Lubuva ( kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mhe. Bahame Tom Nyanduga (aliyekaa kulia). Waliosimama mstari wa nyuma ni Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Asina Omari (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Kisheria wa NEC, Bw. Emmanuel Kawishe na Maafisa kutoka NEC na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. Picha / Aron Msigwa - NEC.

BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI LAKUTANA KUJADILI MAENDELEO YA MKAKATI WA KUPUNGUZA AJALI

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wajumbe wa baraza hilo wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam.
6
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani nchini  ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akifungua kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani.Kushoto ni  Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam.
7
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiongoza kikao cha kujadili maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani. Kushoto  ni Katibu Mtendaji wa baraza ambaye pia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mohamed Mpinga.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara hiyo, Dar es Salaam.(
8
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Mossi Ndozero, akiwasilisha taarifa ya maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani kwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani  ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya mkakati huo, kilichofanyika katika ukumbi wa wizara, Dar es Salaam.
9
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Hamza Kasongo(kulia), akichangia mada wakati wa kujadili  taarifa ya maendeleo ya Mkakati wa Kupunguza Ajali za Barabarani wakati wa kikao cha kujadili maendeleo ya mkakati huo.Kushoto ni mjumbe wa baraza hilo Henry Bantu. Kikao hicho  kilifanyika katika ukumbi wa wizara, Dar es Salaam.
(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AZINDUA KITABU KINACHOELEZEA MAHUSIANO NA URAFIKI WA TANZANIA NA USWISI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely muda mfupi kabla ya kuzindua kitabu kiitwacho A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake,Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely pamoja na Balozi wa Uswis katika Afrika Mashariki Mhe. Arthur Mattli (kushoto) muda mfupi kabla ya kuzindua kitabu kiitwacho A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake, kushoto ni Balozi wa Uswis katika Afrika Mashariki Mhe. Arthur Mattli,Ikulu jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely , Balozi wa Uswis katika Afrika Mashariki Mhe. Arthur Mattli (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano Bi. Romana Tedeschi na Maafisa wengine muda mfupi kabla ya kuzindua kitabu kiitwacho A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake,Ikulu jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akipokea kitabu cha A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake kutoka kwa Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely muda mfupi kabla ya kuzindua kitabu hicho, Ikulu jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akifunua ukurasa wa kitabu cha A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake kama ishara ya kukizindua kitabu hicho mbele ya Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Florence Tinguely , Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mwaka huu Swaziland na Tanzania inatimiza miaka 50 ya mahusiano ya kidiplomasia baina baina ya nchi hizi mbili. Katika kuadhimisha shughuli hii, Ubalozi wa Swaziland umezindua kitabu kinaitwa A-Concise Study of Contemporary Art kinachoelezea mahusiano na urafiki uliodumu baina ya nchi hizi mbili na watu wake. Kitabu hiki kimezinduliwa rasmi na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS DKT SHEIN AZUNGUMZA NA WIZARA YA KAZI,UWEZESHAJI,WAZEE,VIJANA,WANAWAKE NA WATOTO

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto katika  kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
z2
Viongozi katika Wizara ya  Viongozi katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto  wakiwa katika  kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
z3
Waziri wa Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto  Mhe,Moudline Cyrus Castico akisoma   utekelezaji wa Mpango kazi wa mwaka 2016-2017 katika  kikao siku moja cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) (kulia) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee.
z4
Katibu Mkuu Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Bi.Fatma Gharibu Bilali (kulia) akifafanua vifungu vya utekelezaji wa Mpango kazi wa   mwaka 2016-2017 katika kikao siku moja cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),(kushoto) Mshauri wa Rais ushikiano wa Kimataifa,Fedha na Uchumi Ikulu Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa,
z5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abdulhamid Yahya Mzee (katikati) wakati akichangia katika kikao cha utekelezaji wa Mpango kazi wa   mwaka 2016-2017 cha robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja (kushoto) Waziri wa Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto  Mhe,Moudline Cyrus Castico,
z6
Mkurugenzi wa Ajira Ameir Ali Ameir katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto akielezea mifumo na utaratibu wa Ajira wakati katika kikao cha utekelezaji wa Mpango kazi wa   mwaka 2016-2017 katika   robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016, kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 20/10 /2016.

WATANZANIA WATAKIWA KUONGEZA THAMANI NA UZALISHAJI KATIKA SEKTA YA VIWANDA NCHINI.

$
0
0
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akisisitiza jambo kwa wawakilishi wa masharika ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo pichani) wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa KAIZEN Tanzania Bw. Takao Kikuchi akielezea mikakati ya KAIZEN kwa wawakilishi wa masharika ya kiserikali na makampuni binafsi (hawapo pichani) wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi wakipokea tuzo zao wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (watatu toka kushoto waliokaa) pamoja na Balozi wa Japan nchini na Mwakilishi wa JICA Tanzania wakiwa katia picha ya pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi walioshinda tuzo wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN Tanzania kwa mashirika ya kiserikali na makampuni bifsi mapema hii leo jijini Dar es salaam.

Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

Na. Eliphace Marwa – Maelezo

Watanzania watakiwa kuongeza thamani na uzalishaji katika sekta ya viwanda nchini.

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewataka watanzania kuongeza thamani ya bidhaa na uzalishaji ili kuongeza fursa za ajira.

Mwijage ameyasema hayo wakati akizungumza na wawakilishi wa mashirika ya kiserikali na makampuni binafsi wakati wa sherehe za utoaji tuzo za pili za KAIZEN zinazoratibiwa na Shirika la uhusiano wa kimataifa laJapan (JICA).

“Tuko hapa hii leo kushuhudia sherehe za utoaji wa tuzo katika sekta ya viwanda ambayo ni matunda ya dhana za KAIZEN kwani tuzo hizi zinatolewa kwa makampuni yaliyofanya vizuri katika kutekeleza mbinu za KAIZEN ili kuweza kutoa changamoto kwa makampuni mengine” alisema Mh. Mwijage

Kwa upande wake Mwakilishi Mkuu wa JICA ofisi ya Tanzania Bw. Toshio Nagase aliipongeza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji pamoja na kitengo cha KAIZEN Tanzania kwa kuandaa sherehe yenye mafanikio kwa mara nyingine kufuatia ili iliyofanyika mwaka jana.

“Baada ya uzinduzi wa mpango wa miaka mitano, sisi sote tumetambua umuhimu wa kukuza viwanda ili kufikia maendeleo ya kiuchumi na kijamii hapa Tanzania”, alisema Bw. Toshio

Aidha Bw. Toshio alibainisha baadhi ya maeneo ambayo KAIZEN imefanikiwa kuwa ni pamoja na kuhakikisha ubora wa bidhaa na kubadilisha tabia pamoja na kutoa motisha kwa wafanyakazi.

Kwa upande wake Mwakilishi wa KAIZEN Tanzania Bw. Takao Kikuchi amesema kuwa anaamini kuitangaza KAIZEN nchini Tanzania ni jambo la muhimu ili kutengeneza viwanda vyenye ushindani na kufanikisha lengo la kukuza viwanda kuelekea mwaka 2025.

TANZANIA YAWAKILISHWA VYEMA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA MAKAZI NA MAENDELEO ENDELEVU YA MIJI (UN HABITAT III) – QUITO, ECUADOR

$
0
0

Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila akitoa Hotuba katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Makazi na Maendeleo Endelevu ya Miji (UN-HABITAT III, Quito – Ecuador) .
Meza Kuu katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Makazi na Maendeleo Endelevu ya Miji (UN-HABITAT III, Quito – Ecuador) wakifuatilia Hotuba iliyokuwa ikitolewa na Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila.
Katibu Mkuu, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila baada ya kutoa Hotuba, akipongezwa na Profesa Anna Tibaijuka; Mbunge wa Muleba Kusini, wengine ni Immaculata Senje; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Sada Sekiete- Afisa Mipango Miji Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Katibu Mkuu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila akiwa na viongozi wa UN-HABITAT Africa Region kutoka Nairobi wakifanya mazungumzo kuhusu kufufua shughuli za shirika hilo nchini Tanzania.
Katibu Mkuu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila, Immaculata Senje; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Sada Sekiete Afisa Mipango Miji Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika picha ya pamoja na viongozi wa UN-HABITAT Africa Region kutoka Nairobi
Wajumbe kutoka Tanzania, kutoka kushoto ni; Katibu Mkuu; Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Dkt. Yamungu Kayandabila, Nehemia Mchechu Mkurugenzi Mkuu katika Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Immaculata Senje; Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mipango Miji na Vijiji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Fatma chullo Mkurugenzi wa sheria wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wakifuatilia Mkutano wa wa Umoja wa Mataifa wa Makazi na Maendeleo Endelevu ya Miji (UN-HABITAT III, Quito – Ecuador)

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano – Wizara ya Ardhi

SERIKALI YAPUNGUZA DENI LA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali tayari imeshalipa sh. bilioni 722.7 kati ya sh. bilioni 964.2 za madeni ya michango ya jumla ambayo Serikali inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii nchini.

Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Oktoba 20, 2016) wakati akifungua Mkutano wa Sita wa wadau wa NSSF ulioanza leo kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), Arusha na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 600.

Amesema sekta hiyo imekua kwa asilimia 15 kutoka sh. trilioni 8.9 mwaka 2015 hadi kufikia sh. trilioni 10.2 mwaka 2016. “Hadi kufikia Juni 2016, takwimu zinaonesha idadi ya wanachama imeongezeka na kufikia milioni 2.1. Rasilmali za mifuko zimefikia shilingi trilioni 10.28 na mafao yaliyolipwa kwa kipindi cha mwaka kinachoishia Juni 2016 ni shillingi trilioni 2.93. Michango ya wanachama kwa mwaka ni shilingi trilioni 2.15 uwekezaji katika nyanja mbalimbali umefikia kiasi cha shilingi trilioni 9.29,” ameongeza.

Waziri Mkuu pia amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara awaandikie barua waajiri wote wanaodaiwa na shirika hilo na kuwataka wawasilishe fedha wanayodaiwa mara moja na wale ambao hawatalipa ndani muda utakaowekwa wafikishwe mahakamani na yeye apewe taarifa.

“Kumekuwepo na changamoto ya muda mrefu ya baadhi ya waajiri kutolipa michango kwa wakati hali inayoleta usumbufu mkubwa kwa wanachama hasa wanapofikia muda wa kustaafu. Suala hili halikubaliki, hivyo natoa maelekezo kwa waajiri wote nchini waheshimu sheria na wawasilishe michango yao kwa wakati,” amesisitiza.

Mbali ya kuwabana waajiri, Waziri Mkuu pia amewataka wanunuzi wa nyumba za shirika hilo na wapangaji wote wanaodaiwa wakamilishe malipo yao na wasipofanya hivyo ndani ya muda uliopangwa wafikishwe mahakamani.

“Nimeambiwa pia lipo tatizo la wadaiwa wa nyumba yaani wanunuzi na wapangaji. Suala hili lilitolewa maelekezo na Waziri wa Nchi, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu. Nataka nisisitize kuwa watu wote walionunua nyumba za NSSF na bado hawajakamilisha malipo na wale waliopanga lakini hawalipi kodi wanatakiwa kulipa haraka au wakabidhi nyumba hizo kwa NSSF ziuzwe kwa watu wengine, vinginevyo nao wafikishwe mahakamani.”

Akizungumzia utendaji wa shirika hilo, Waziri Mkuu amewapongeza viongozi wa shirika hilo na Bodi ya Wadhamini kwa uamuzi wake wa kuwekeza kwenye uzalishaji wa sukari nchini. Amesema kiwanda kitakachojengwa, kinatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 kwa Watanzania na hivyo kuongeza wanachama katika mfuko wa NSSF.

Nimefurahishwa na uamuzi wa NSSF na PPF kuungana ili kukabiliana na tatizo la sukari nchini. Tumeelezwa hapa kuwa mashirika haya yatashirikiana kujenga Kiwanda cha Sukari kitakachozalisha tani 200,000 kwa mwaka. Kiwanda hicho kitajengwa katika eneo la Mkulazi lililopo mkoani Morogoro,” amesema.

Mapemaakielezea utendaji wa shirika hilo, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara alisema limeboresha mafao ya wanachama wake kutoka sh. 80,000 hadi sh. 100,000 kwa mwezi.

Alisema limeanza kufanya upembuzi yakinifu wa kujenga nyumba za watumishi Dodoma ili kuendana na uamuzi wa serikali kuhamia Dodoma. “Upembuzi bado unaendelea lakini tumeshabaini kuna uwezekano wa kujenga nyumba 200 hadi 300 mkoani Dodoma,” alisema.

Kuhusu uwekezaji kwenye ujenzi wa Daraja la Mwalimu Nyerere lililopo Kigamboni, Dar es Salaam, Prof. Kahyarara alisema uwekezaji huo unalipa kwa sababu makusanyo ya tozo kwa watumiaji yamefikia asilimia 109. “Tuna uhakika kwamba fedha tulizowekeza zitarudi,” amesisitiza.

Wakati huohuo, Waziri Mkuu amepokea msaada wa tani 45 za saruji ambazo ni sawa na mifuko 900 yenye thamani ya sh. milioni 15 kwa ajili ya waathirika wa tetememo la ardhi mkoani Kagera. Amepokea msaada huo kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Prof. Samuel Wangwe.

Akiwasilisha msaada huo, Prof. Wangwe alisema wameguswa na tatizo lilitokea mkoani Kagera na wameamua kutoa mchango ili kusaidia juhudi za Serikali kukabiliana na maafa hayo. Pia alisema wamekamilisha ahadi yao ya madawati 6,000 yenye thamani ya sh. milioni 400 ambayo waliitoa awali.

Waziri Mkuu aliwashukuru kwa misaada hiyo na kuwahakikishia kwamba itafikishwa kwa walengwa.

                             
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, OKTOBA 20, 2016.

Kongamano la Nne Gesi na Mafuta lafanyika Dar

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kushoto) akifugua kongamano la nne linalohusu gesi na mafuta lililoambatana na maonesho , lililokutanisha wadau mbalimbali kutoka makampuni yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, vyuo vikuu, wizara na taasisi za serikali jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kushoto), akibadilishana mawazo na Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile (kulia) katika kongamano hilo
Kutoka kulia; mwakilishi kutoka Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Profesa Abraham Temu, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, James Andilile na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika kongamano hilo.
Washiriki kutoka makampuni yanayohusika na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, vyuo vikuu, wizara na taasisi za serikali wakifuatilia hotuba iliyokuwa inatolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (hayupo pichani) katika kongamano hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Kapuulya Musomba (kushoto) akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) kwa mchango wa shirika hilo katika kufanikisha kongamano hilo.
Mwakilishi kutoka Benki ya Standard Chartered, Thomas Bisonga (kushoto) akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) kwa mchango wa benki hiyo katika kufanikisha kongamano hilo.
Mwakilishi kutoka kampuni inayojihusisha na ujenzi wa mabomba ya gesi kutoka China (kushoto) akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) kwa mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha kongamano hilo.
Meneja Mawasiliano kutoka kampuni ya utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta nchini ya Statoil, Genevieve Kasanga (kushoto), akipokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (kulia) kwa mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha kongamano hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Kapuulya Musomba akieleza jambo katika kongamano hilo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo (katikati waliokaa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa kongamano hilo.



Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Kongamano la Nne linalohusu sekta ndogo ya mafuta na gesi lililoambatana na maonesho kuhusu sekta hiyo na kukutanisha Wadau mbalimbali ikiwemo Kampuni zinazojishughulisha na utafiti na uchimbaji wa mafuta na gesi, Vyuo Vikuu, Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali limeanza kufanyika jijini Dar es Saalaam.

Kongamano hilo lilifunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dk. Juliana Pallangyo ambapo aliwaeleza wadau hao kuwa, usimamizi madhubuti wa sekta ndogo ya gesi na mafuta utaleta mapinduzi makubwa kwenye ukuaji wa viwanda na kuiwezesha Tanzania kuingia kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Katika kongamano hilo linalofanyika kuanzia tarehe 20 – 21 Oktoba, 2016, Dk. Pallangyo alisema kuwa kutokana na kiasi kikubwa cha gesi kilichogunduliwa ambacho ni futi za ujazo trilioni 57.2, kampuni mbalimbali za kigeni zimeanza kujitokeza na kuwekeza katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo gesi imegunduliwa

Alisema kutokana na uwekezaji katika shughuli za gesi na mafuta, kumekuwepo na mabadiliko ya kiuchumi katika mikoa hiyo kama vile kuongezeka kwa fursa za ajira, malazi na utoaji wa huduma kwa wawekezaji.

Aliongeza kuwa ni vyema wananchi hususan wa maeneo hayo kujiandaa na uwekezaji mkubwa katika mikoa hiyo ambapo kwa sasa katika mikoa ya Lindi na Mtwara kunatarajiwa kujengwa viwanda vikubwa vya mbolea, vitakavyoleta neema katika mikoa hiyo.

Alisema katika kujiandaa na kasi ya ukuaji wa sekta za gesi na mafuta nchini serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kunakuwepo na sera na sheria zitakazowezesha wazawa kuwa sehemu ya umiliki wa uchumi wa gesi na mafuta.

Alitaja mikakati mingine ni pamoja na uanzishwaji wa kozi zinazohusu masuala ya gesi na mafuta katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Aliongeza kuwa, Serikali imekuwa ikipeleka nje ya nchi kusomea masuala ya gesi na mafuta katika ngazi ya shahada ya uzamili (masters degree), wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo ya sayansi katika ngazi ya shahada.

“Lengo letu kama Serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa na wataalam wa kutosha watakaoshiriki katika uchumi wa gesi na mafuta kwa kuajiriwa kwenye makampuni yanayojihusisha na utafiti na uchimbaji wa gesi na mafuta,” alisema Dk. Pallangyo.

Wakati huo huo akizungumza katika kongamano hilo, mwakilishi kutoka Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Profesa Abraham Temu alisema kuwa lengo la kongamano hilo lilikuwa ni kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu sekta za gesi na mafuta nchini.

Alisema mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na uelewa kuhusu sekta za gesi na mafuta, sera na sheria za mafuta na gesi, ushirikishwaji wa wazawa kwenye sekta za gesi na mafuta, changamoto na matumizi endelevu ya mafuta na gesi na rushwa.

Kongamano hilo liliandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na Taasisi ya Wahandisi Tanzania (IET), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

KESSY RUKSA KUCHEZA YANGA-TFF

$
0
0
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Shirikisho la soka nchini TFF limeweka wazi kuwa beki wa kulia wa Yanga Hassan Kessy, aliyetokea Simba ruksa kucheza katika ligi kuu ya vodacom kutokana na  kanuni za ligi hiyo kwa kuwa swala kesi ni madai .

Afred amesema kuwa swala mchezaji huyo aliwezi kumzuia mchezaji huyo kucheza kwakuwa tayari swala hilo lipo katika hatua ya usuluhushu .

"Lakini ikitokea usuluhishi alijafikiwa maamuzi hivyo kamati itachukua maamuzi kwa mujibu wa kanuni zinavyoeleza na majibu nitakuja kuwapatia"amesema lucas.

Amesema kuwa Simba katika mkataba wake waliweka kipengele cha kulipa zaidi ya dola 600 kama faini hivyo tunasubiri maamuzi hayo hivyo kesi anapaswa kucheza mpaka hapo kamati itakapo toa maamuzi.

KIKOSI KAZI CHA JESHI LA WANANCHI(JWTZ)CHA WASILI KAGERA KWAAJILI YA KUJENGA MIUNDOMBINU ILIYOATHIRIKA NA TETEMEKO LA ARDHI

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Missenyi

KIKOSI kazi cha jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ)kutoka makao makuu ya Jeshi kimewasili Mkoani Kagera kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya serekali iliyoathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoana hapa septemba 10 mwaka huu.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Kabambyaile Kata ya Ishozi Wilaya ya Missenyi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu alisema kuwa kikosi hicho kinawataalamu wa fani zote za ujenzi na wamekuja na vifaa vyote vya ujenzi.

"Hiki kikosi kitafanya kazi kwa masaa 24 yaani watajenga usiku na mchana taasisi zote za umma zilizoathiriwa na tetemeko ikiwa ni pamoja na mashule na zahanati ili watoto waende shule na wagonjwa waendelee kupata matibabu"alisema.Alisema mpaka kufikia july mwakani ujenzi wa miundombinu utakuwa umekamilika kwa robo tatu na aliwataka wananchi wawape ushirikiano maeneo yote watakayopita kujenga miundombinu ya umma.

Kiongozi wa kikosi hicho Meja Buchadi Kakura alisema kuwa kikosi hicho kimekuja Kagera kusaidia serekali ya Mkoa kurudisha miundombinu yote ya umma iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi katika hali yake ya kawaida.

"Ni vigumu kusema lini tutakamilisha ujenzi ila sisi tutafanya kazi usiku na mchana ili ujenzi huu ukamilike ndani ya muda mfupi"Alisema Meja Kakura.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu(mwenye Suti)akisikiliza maelezo juu ya kikosi kazi cha askari waliokuja kujenga miundo mbinu ya umma iliyoathiriwa na tetemeko la ardhi


Kikosi kazi cha askari wa Jeshi la wananchi(JWTZ)kutokaakao makuu ya Jeshi kilichowasili Mkoani Kagera kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya umma iliyoathirika na tetemeko la ardhi.

Greda la Jeshi likiandaa eneo linalotarajia kujengwa kituo cha afya kituo cha afya cha Ishozi kijiji cha Kyabaile.
 

WAZIRI KAIRUKI AFANYA ZIARA DAR, KINONDONI KUKAGUA MRADI WA TASAF

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairuki leo amefanya ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAF.

Mh. Kairuki alianza ziara hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na kupokelewa na Kaimu Mkuu wa mkoa hua Mh. Ally Hapi.
Akiwa ofisini hapo Mh. Kairuki alisaini kitabu cha wageni na kusalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Ally Hapi, wakuu wa wilaya za Ilala, Temeke, Kigamboni na Katibu tawala wa mkoa wa Dar es salaam.

Mara baada ya kusaini kitabu cha wageni, Mh. Angela Kairuki alifanya mkutano na wakuu wa wilaya, wakurugenzi na waratibu wa TASAF Mkoa na manispaa za Dar es salaam ambapo alipokea taarifa mbalimbali za manispaa na Mkoa mradi wa kuondoa umasikini wa TASAF.

Katiba hotuba yake Mh. Kairuki amewataka waratibu wa TASAF wa Mkoa na manispaa kujipanga vema, kusimamia mradi kwa makini na kuondoa wale wote wasiostahili kupata fedha hizo katika orodha ya wanufaika wa TASAF.

Akitoa salam za Mkoa, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Ally Hapi amemshukuru Mh. Kairuki kwa ziara hiyo na kumfahamisha kuwa Mkoa wa Dar es salaam unakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa mradi wa TASAF ikiwemo watu wasiostahili majina yao kuingizwa miongoni mwa wanufaika, kuingizwa kwa majina hewa, kubaguliwa kwa baadhi ya wananchi masikini kwa itikadi za kisiasa na ufuatiliaji duni unaofanywa na waratibu wa TASAF ngazi mbalimbali.

Ziara ya Mh. Angela Kairuki iligusa pia maeneo ya Kata za Kigogo na Msasani ambako Mh. Waziri alipata nafasi ya kuongea na wananchi wanufaika wa TASAF katika mikutano ya hadhara mitaa ya Kigogo Kati na Mikoroshini (Msasani).

Wananchi waliojitokeza wameishukuru serikali kwa mradi huo ambao umekua msaada mkubwa kwao katika kujikwamua na umasikini.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairukia akizungumza na mmoja wa wakazi wa Kinondoni,
mara baada ya kufanya ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAFkushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala bora Mh. Angela Kairukia akiwa sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,akiendelea na ziara katika Mkoa wa Dar es salaam kukagua maendeleo ya mradi wa kusaidia kaya masikini TASAFkushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh. Ally Hapi

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA MKUTANO WA 6 WA NSSF JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Waziri Mkuu Mhe.  Kassim Majaliwa akishiriki kuimba wimbo wa taifa kabla ya kufungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama na  kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akizungumza   kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kufungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba  20, 2016
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipiga makofi baada ya kupokea tani 45 za saruji  zenye thamani ya shilinigi milioni 15 zilizotolewa na NSSF  kabla ya kufungua  Mkutano wa  Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mkutano wa Sita wa Wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC) Oktoba 20, 2016. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.


MBUNGE WA KIEMBESAMAKI ZANZIBAR AKABIDHI MADAWATI 80 SKULI YA KISAUNI

$
0
0
 Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Zanzibar Mhe. Ibrahim Raza akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Kisauni alipofika kukabidhi madawati katika skuli hiyo na kuona changamoto zao.
v2
Mwalimu wa Biology wa Shule ya Kisauni Muh’d Ali Muh’d akimueleza Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza juu ya uhaba wa vifaa vya maabara katika skuli hiyo.
v3
Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza akimkabidhi msaada wa Madawati 80 Mwalim Mkuu wa Shule ya Kisauni Machalila Kulima Ndega kwajili ya shule hiyo.
v4
Sehemu ya madawati 80 yaliyotolewa na  Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza.
v5
Mbunge wa Jimbo la Kiembe Samaki Mhe. Ibrahim Raza akizungumza na walimu  na wanafunzi wa Skuli ya Kisauni baada ya kukabidhi madawati katika shule  hiyo.

Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

WAZIRI LUKUVI AVAMIA OFISI YA ARDHI MOROGORO,ATOA AGIZO ZITO.


TOYOTA RAV4 INAUZWA

$
0
0
Make:toyota
Model:Rav4
Bodytype:station wagon
Color:black
Year of man:2006
Contact:+255754710458 or +255755311477

KAMATI YA BUNGE YAENDELEA KUUJADILI MUSWADA WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI.

Madiwani Hanang’ waridhia mashamba kukodishwa kwa wananchi.

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, Bryceson Kibasa, akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Katesh Wilayani Hanang’ Mkoani Manyara, Peter Lowry akizungumza kwenye kikao cha Bazara la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.

Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang’ Mkoani Manyara, wakifuatilia kikao cha Baraza lao lililofanyika mji mdogo wa Katesh.

MAONESHO YA KATUNI NA VIBONZO YAFUNGULIWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

.Mgeni Maalum,Masoud Kipanya akiwa na Rais wa Chama cha Wasanii na Wachongaji Tanzania (CHAWASAWATA), Bw. Adrian Nyangamalle,Mwenyekiti wa Chama cha Wachoraji Katuni Tanzania,Nathan Mpangala wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa maonesho ya katuni na vibonzo jana jioni katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

Mgeni Maalum,Masoud Kipanya akizungumza na wadau mbalimbali (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa maonesho ya katuni na vibonzo jana jioni katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wachoraji Katuni Tanzania,Nathan Mpangala akizungumza juu ya hafla ya uzinduzi wa maonesho ya katuni na vibonzo jana jioni katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam Oktoba 20-2016.



Baadhi ya Wadau wakiafuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo.
Ankal pichani Kati nae alikuwepo kushuhudia ufunguzi rasmi wa maonesho ya katuni na vibonzo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaa,Pichani kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wachoraji Katuni Tanzania,Nathan Mpangalaa akimueleza jambo Ankal Muhidin Michuzi kuhusiana na ufunguzi huo


Wadau mbalimbali wa Katuni wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya katuni na vibonzo jana jioni katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam OKTOBA 20-2016.

RC GAMBO AWAACHIA TABASAMU WANANCHI WA TERRATI – ARUSHA

$
0
0

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kwanza kulia) akizungumza na wananchi wa Kata ya Terrati kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya Msingi Mkonoo.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Terrati waliohudhuria Mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia (aliyesimama) akiwatambulisha wakuu wa Idara za Jiji (hawapo Pichani) kwenye Mkutano wa hadahara.
Mhandisi wa barabara Jiji la Arusha Fordia Mwankenja (anayepunga mkono) akiwasalimia wananchi wa Kata ya Terrari kwenye Mkutano wa hadhara

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Fabian Gabriel Daqarro akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuzungumza na wananchi wa Kata ya Terrati kwenye Mkutano wa hadhara.



Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilaitayoki Mhe. Long’ida Lomayani Kupitia Chadema akiwasilisha kero za mtaa wake kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha

……………………………………………………………………………

Nteghenjwa Hosseah – Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amechangia Lita 600 za mafuta kwa ajili ya greda la Halmashauri ili liweze kutengeneza miundombinu ya barabara kwenye maeneo yote korofi yanayozunguka kata ya Terrati.

Rc Gambo amefanya hivyo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Terrat uliofanyika kwenye Shule ya Msingi Terrat wenye lengo la kufahamu changamoto za muda muda mrefu zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo.

Katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa alianadamana na watalaamu wa Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma katika Mkoa huu pamoja na menegiment ya Jiji ili kuwezesha upatikanaji wa majawabu ya kero zote zilizo wasilishwa na wananchi hao ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa haraka ili kumaliza kabisa changamoto hizo.

Wananchi wa Kata hiyo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na kero ya ubovu wa miundombinu ya barabara, kukosekana kwa maji safi na salama pamoja na umeme katika eneo hilo na pia walitoa shukrani zao kwa Mkuu wa Mkoa kwa kuwapa kipaumbele katika ziara zake za kutambua changamoto za Mkoa wake.

Sisi wakazi wa huku tumekua kama hatuishi kwenye Jiji la Arusha kwa sababu huduma zote muhimu zimekuwa kikwazo sana kwetu mpaka zinasababisha kudorora kwa uchumi kwa wakazi wa maeneo haya kwa kuwa hapavutii wafanyabiashara kuja kuwekeza wala wanunuzi kutoka mjini hivyo tumekua tukiuziana sisi kwa sisi ambao wote tuna vipato duni alisema Jumanne Juma Kingu.

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa Jina la Eliakim Mason kutoka Mtaa wa bondeni kati alisema kuwa Gari lakubebea wagonjwa katika kituo cha Afya Mkonoo limeharibika kwa kipindi kirefu sana na wanapata tabu ya kusafirisha mgonjwa hadi kufikia kwenye Hospital za Mjini Arusha inawalazimu kukodi Gari kwa gharama kubwa ili kunusuru maisha ya ndugu zao pia alilalamikia uhaba wa watumishi katika Kituo cha Afya Mkonoo na kudai kwamba inakuwa vigumu kupata hudma bora wagonjwa wanapokua wengi katika kituo hicho.

Akitoa majibu ya malalamiko hayo Mkuu wa Mkoa wa Arusha alisema changamoto hizi zimekuwa za kipindi kirefu lakin hivi sasa zimefika mwisho kwa sababu Serikali ya Awamu ya Tano ni ya kutatua kero na vitendo ndivyo vinavyotawala hivyo ndani ya muda mfupi eneo hili litakua sehemu nzuri ya kuishi kwa kuwa kero hizi zitakuwa historia.

Rc Gambo alimuagiza Maneja wa Tanesco Mkoa kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wa Kata ya Tarati ndani ya miezi mitatu pia aliwataka viongozi wengine wa Taasisi zinazolalamikiwa kutolea ufafanuzi na mikakati ya haraka ya kumaliza kabisa matatizo ya wananchi wa Terrat.

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani Kihamia aliahidi mbele ya Mkutano huo kwamba ndani ya wiki mbili gari la kubebea wagonjwa kwenye Kituo cha Afya Mkonoo litakuwa limeshatengenezwa na kuanza kutoa huduma na pia ataongeza watumishi wa kutosha ili kuboresha utoaji wa huduma za Afya katika Kituo hicho.

Eng. Ruth Koya ni Mkuu wa Idara ya Maji safi na maji Taka (AUWSA) alieleza kuwa Taasisi yake imeanza kutekeleza mradi mkubwa wa uboreshaji wa miundombinu pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama na Kata ya Terrati ni miongoni mwa maeneo ambayo yatafikiwa na mradi huo na utamaliza kabisa changamoto hii ya maji.

Mkutano huu ulihudhuriwa na wananchi wa chama cha demokrasia na maendeleo akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa wa Ilaitayok Mhe. Long’ida Lomayani.
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images