Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1015 | 1016 | (Page 1017) | 1018 | 1019 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Mkazi wa eneo hilo, Lukia Khalid (aliye kaa), akiwa amekaa nje na vyombo vyake baada ya kubolewa nyumba yake.
   Wananchi wa Tegeta A Kata ya Goba wakiwa wamesimama chini ya mti Dar es Salaam jana, baada ya nyumba zao kubomolewa na Kampuni ya Udalali ya Yono kwa madai ya kuvamia eneo hilo. Hata hivyo wamekanusha kuvamia eneo hilo. Zaidi ya nyumba 150 zilibomolewa. Wananchi hao leo wanaandamana kwenda kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo kupeleka malalamiko yao.
   Askari polisi wakiwa eneo hilo kuimarisha ulinzi.
   Watoto wakiangalia nyumba yao baada ya kubomolewa.
   Mkazi wa eneo hilo akiwa kando ya nyumba yake iliyobomolewa.
   Mkazi wa eneo hilo akiangalia nyumba yake baada ya kubomolewa.
  Magodoro yakiwa yamefunikwa na paa la nyumba baada ya kubomolewa kwa nyumba hizo.

  Na Dotto Mwaibale

  KAMPUNI ya Udali ya Yono Aution Mart imebomoa nyumba zaidi ya 150 za wakazi wa Tegeta A Kata ya Goba jijini Dar es Salaam kwa madai ya kujengwa eneo ambalo sio lao huku Kaya zaidi ya 450 zikikosa makazi ya kuishi.

  Hata hivyo ubomojai huo umepingwa na wananchi hao wakidai eneo hilo ni lao na wapo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

  Zoezi la ubomoaji wa nyumba hizo lililofanyika Dar es Salaam jana, ulisimamiwa na askari polisi waliokuwa na silaha za moto na mabomu ya machozi huku wakiwa katika magari yenye namba PT, 3475, 1986 na  3675 huko kukiwa na askari hao zaidi ya 15.

  Mmoja wa wananchi hao, Macarios Turuka  akizungumza na Jambo Leo eneo la tukio alisema eneo hilo kwa kipindi kirefu lilikuwa halitumiki na lilikuwa ni vichaka vya wahalifu kwani wanawake walikuwa wakibakwa na kutumiwa na watu kwa uhalifu ndipo walipoingia na kujenga.

  Aliongeza kuwa baada ya kuanza ujenzi ndipo alipo ibuka Benjamini Mutabagwa na kueleza kuwa ni lake ndipo walipofungua kesi mahakama ya Kimara ambapo alishindwa kupeleka vielelezo vya umiliki wa eneo hilo.

  Mwanasheria anayewatetea wananchi hao, Moses Chunga alisema kitengo cha kubomoa nyumba hizo ni kukiuka sheria za mahakama kwani kuna kesi ya msingi namba 188/ 2016 waliyofungua mahakama kuu ya ardhi ambapo walitakiwa tarehe 31 mwezi huu kwenda kuisikiliza lakini wanashangaa kuona nyumba hizo zikibomolewa.

  Alisema wananchi hao wanajipanga kudai fidia ya uhalibifu huo na kuwa kabla ya yote wanahitaji kumuona rais kuona wanapata haki yao.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, Yono Kevela alisema kampuni ya ke imevunja nyumba hizo kwa amri ya mahakama na polisi walikuwepo kusimamia zoezi hilo.

  "Mwenye eneo hilo ambaye ni Kanisa la Winers alishinda kesi mwaka mmoja uliopita na leo jana ulikuwa ni utekelezaji wa kuwaondoa wavamizi hao" alisema Kevela.

  Mkazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Hamisi alisema kitendo walichofanyiwa si cha uungwana hata kidogo kwani wao wapo katika eneo kwa siku nyingi mpaka wamefikia hatua ya kujenga nyumba hizo hizo mmiliki huyo alikuwa wapi kwa siku zote hizo.

  "Kwa kweli hawa watu wanatufanya tusiipende serikali yetu tunaomuomba rais atusaidie katika jambo hili" alisema Hamisi.

  Hamisi alisema kesho leo wanatarajia kwenda kwa mkuu wa wilaya ya Ubungo kupeleka kilio chao na kama akishindwa watakwenda kwa mkuu wa mkoa na kama napo hawatapata ufumbuzi watakwenda kumuona waziri Lukuvi na Rais.

  Hawa Musa alisema baada ya kuvunjiwa nyumba zao wapo katika wakati mgumu na hawajui wataisheje na watoto wao.

  Alisema wamepanga vitu vyao nje na mvua yote iliyonyesha jana imelowanisha vyombo vyao yakiwemo magodoro na hawajui huyo mtu anayedai ni eneo lake nyuma yake yupo nani.

  Alisema nyumba yake iliyobomolewa ilikuwa inathamani ya sh. 700,000.

  "Tangua tufungue kesi mahakama ya Kimara hakuwahi kufika kama yupo kweli kwanini anashindwa kuhudhuria mahakamani " alihoji Musa.

  Musa aliongeza kuwa kabla ya kubomoa nyumba hizo walipaswa kutoa notsi lakini wao hawajafanya hivyo wamefika saa mbili asubuhi na kuanza kubomoa bila hata ya kuwa shirikisha vipongozi wa eneo hilo.

  Mkazi mwingine wa eneo hilo Juma Abdallah amelalamikia jeshi la polisi kwa kuchukua TV, king'amuzi na sh. 80,000 zilizokuwepo ndani kabla ya nyumba yake kubomolewa.

  "TV yangu na king'amuzi na sh.80,000 zimechukuliwa wakati wa zoezi hilo" alisema Abdallah.

   Katika hatua nyingine wananchi hao wamemtupia lawama Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Tegeta A  kuwa amekuwa akiwakumbatia watu wanaodai kuwa eneo hilo ni lao wakati anaelewa fika ukweli halisi wa eneo hilo.

  Mwenyekiti huyo Marko Vaginga alipopigiwa simu ili kuzungumzia suala hilo hakuwa tayari kuzungumza chochote zaidi ya kumtaka mwandishi kwenda ofisini kwake kwa mazungumzo zaidi.

  "Nakuomba uje ofisini tuzungumze kwa leo sipo tayari kuzungumza chochote" alisema Vaginga na kukata simu.

  Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni alipopigiwa simu alisema polisi walikuwa eneo hilo kwa ajili ya kusimamia amri ya mahakama.

  0 0


  0 0

  Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi viti 142 vyenye thamani ya shilingi milioni 6 katika Shule ya Sekondari Kisungu iliyopo kata ya Kinyerezi jijini Dar es Salaam. 

  Meneja Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemu akikabidhi viti hivyo kwa niaba ya Mkurungezi Mtendaji wa TPDC amesema viti hivyo vitasadia kutatua changamoto ya wanafunzi kukosa viti shuleni hapo. 

  Amengoze kuwa mchango huo wa viti ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha wanafunzi wanakuwa na mazingira rafiki ya kujifunzia. 

  Shirika hilo limekuwa na utaratibu wa kuchangia jamii katika nyaja za afya, elimu, maji, utawala bora na michezo kupitia programu yake kuwajibika kwa jamii.
  Mkuu wa shule ya Sekondari Kisungu, Mkama Mgeta (kulia) na wanafunzi wa Shule ya Sekondari wakipokea kiti kutoka kwa Meneja Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemu (kushoto) katika hafla fupi ya kupokea viti 142 kutoka TPDC.
   Meneja Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemu akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC katika hafla fupi ya kukabidhi viti 142 vyenye thamani ya shilingi milioni 6 katika kwa Shule ya Sekondari Kisungu iliyopo kata ya Kinyerezi jiji Dar es Salaam.
   
  Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisungu, Philimina Casimr akisoma taarifa ya Shule hiyo kabla ya kupokea viti kutoka TPDC.
   Sehemu ya viti 142 vilivyotolewa na TPDC.


  0 0


  Ngoma ya Kioda na kundi la JKT wakitumbuiza kwenye hafla fupi ya uwekaji wa jiwe la msingi

  0 0
  Jokate Mwegelo akiwasili katika shule ya Sekondari ya Majani Ya Chai ya Vingunguti. Kulia kwake ni Mkuu wa shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi.

  Jokate Mwegelo akitoa hotuba yake katika Mahafali ya Nane ya Kidato cha Nne ya Shule ya secondari ya Majani ya Chai. Katika Hotuba yake, Jokate alitoa ahadi ya kuwajengea uwanja wa michezo na matundu ya Vyoo shuleni hapo. Ujenzi huo utaanza baadaye.
  Mkuu wa Shule ya ya Sekondari ya Majani ya Chai, Kasango Pascal Ngozi akitoa neno la shukrani baada ya ahadi ya Jokate Mwegelo wa kujenga uwanja wa michezo na matundu ya vyoo.
  Jokate Mwegelo akimkimkabidhi zawadi ya kuwa mwanamichezo bora wa wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim katika mahafali ya nane ya shule hiyo. Anayeshuhudia (wa kwanza) ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi.

  Jokate Mwegelo akimkimkabidhi zawadi mwanafunzi mwenye nidhamu bora kwa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Khalid Ibrahim katika mahafali ya nane ya shule hiyo. Anayeshuhudia (wa kwanza) ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi.

  Jokate Mwegelo akiserebuka na wanamuziki wa bongo fleva wanaosoma katika shule ya sekondari ya Majani ya Chai wakati wa Mahafali ya Nane yaliyofanyika juzi. Jokate ameahidi kuijengea shule hiyo uwanja wa michezo na matundu ya vyoo.  Mrembo mwenye vipaji lukuki, Jokate Mwegelo kupitia kampeni yake yake ya kuchangia jamii ijulikanayo kwa jina la “Be Kidotified” ameahidi kujenga uwanja wa michezo kwa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti jijini.

  Akizungumza katika Mahafali ya Nane ya shule hiyo, Jokate alisema kuwa ameguswa na changamoto mbalimbali zinazo ikabili shule hiyo na kuamua kusaidia kwa kupitia kampeni yake hiyo.Tayari Jokate amekabidhi viwanja vya netiboli na mpira wa kikapu kwa shule ya Sekondari ya Wasichana wa Jangwani.

  Jokate ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, alisema kuwa serikali peke yake haitaweza kutatua changamoto mbalimbali katika sekta ya elimu na nyinginezo na hivyo inahitaji msaada kutoka kwa sekta binafasi na wadau.

  “Nashukuru kwa kunichagua kuwa mgeni rasmi katika mahafali haya, hii imenipa faraja kubwa sana, nimesikia changamoto mbalimbali, kwa kuanzia nitaanza kujenga uwanja wa michezo na matundu ya vyoo,” alisema Jokate.

  Alisema kuwa ameamua kuonyesha mfano kupitia ‘Kidoti Brand’ kuchangia maendeleo ya michezo nchini hasa kwa katika shule ambazo ni kiini cha maendeleo ya sekta hiyo hapa nchini. Mbali ya michezo, pia Kidoti Brand inajihusisha zaidi na maendeleo ya elimu hapa nchini.

  Mkuu wa Shule hiyo, Kasango Pascal Ngozi alisema kuwa wanalazimika kutumia viwanja vya shule jirani katika kufanikisha masuala ya michezo ambayo ni moja ya masomo muhimu sana.Ngozi alisema kuwa wanatambua kuwa kuna vipaji kibao vya michezo katika shule yao, lakini kutokana na kukosa viwanja bora wameshindwa kuvitambua.

  “Tunashukuru Jokate kwa ahadi ya kutujengea uwanja wa michezo na matundu ya vyoo, hii itatoa hamasa kwa wanafunzi wenye vipaji katika michezo mbalimbali kutambuliwa na vile vile kuendelezwa, bado tuna tatizo la jengo la utawala, samani za ofisini na kumalizia uzio wa shule, tunawaomba wadau watusaidie kufanikisha hayo,” alisema Kasango.

  Mahafali hayo yalipambwa na burudani mbalimbali za muziki wa bongo fleva, singeli, ngoma kutoka kwa wanafunzi wa shule hiyo.Kati ya wanafunzi zaidi ya 290 wanaomaliza kidato cha nne, Kkhalid Ibrahim alitwaa tuzo ya mwanamichezo bora huku Latifa Kihiyo akitwaa tuzo ya mwanafunzi mwenye nidhamu.

  0 0


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Irani nchini Mhe.Mehdi Agha Jafari (kushoto)ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais,Ikulu jijini Dar es Salaam leo na kuaga baada ya muda wake wa kazi kumalizika nchini
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Irani nchini Mhe.Mehdi Agha Jafari (kushoto)ambaye alifika ofisini kwa Makamu wa Rais,Ikulu jijini Dar es Salaam leo na kuaga baada ya muda wake wa kazi kumalizika nchini.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ikiendelea na majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba (kulia) akielezea jambo kwa wajumbe wa Kamati yake na viongozi na watendaji wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye 
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kushoto) akijibu hoja mbalimbali za wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Peter Serukamba 
  Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akisisitiza jambo kwa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.
  Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson (kushoto) akifafanua jambo wakati wa majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.
   
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akijibu hoja zilizotolewa na baadhi ya wajumbe ambao wanashiriki kuuchambua Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari leo Oktoba 21,2016 Mjini Dodoma.
  Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia majadiliano na hoja mbalimbali katika kikao cha kuujadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari kinachoendelea Mjini Dodoma leo Oktoba 21,2016.Picha zote na Idara ya Habari MAELEZO

  0 0

  Jengo la ofisi linalojengwa na vijana wa kikundi cha Sarorya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana. Wa Pili Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari ambaye aliongoza ujumbe wa NHC katika uhakiki wa shughuli zinazofanywa na vijana hao baada ya kupewa msaada wa mashine.
  nc2
  Kanisa lililojengwa na vijana wa kikundi cha Hope Revival - Manispaa ya Musoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana.
  nc3
  Kanisa lililojengwa na vijana wa kikundi cha Hope Revival - Manispaa ya Musoma ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana.
  nc4
  Meneja wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Benedict Kilimba ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kufyatua matofali yanayofungamana kupitia ufadhili wa na NHC wa msaada wa mashine ya kufyatua matofali kwa vijana wa Manispaa ya Ilemela – Mwanza.
  nc5
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari akiwa katika mahojiano na vyombo vya habari baada ya kuhakiki vikundi vya vijana wa Ukombozi Vijana Magu kwenye eneo lao la kazi wanalotegemea kujenga nyumba.
  nc6
  Moja ya kazi za vijana wa kikundi cha Sarorya - Halmashauri ya Rorya ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa vijana wa kutengeneza matofali ya kufungamana kupitia mashine zilizotolewa na NHC kama msaada kwa vijana.
  nc7
  Moja ya Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana - Halmashauri ya Magu.
  nc8
  Moja ya Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana - Halmashauri ya Magu.
  nc9
  Nyumba iliyojengwa na kikundi cha Ukombozi Vijana Magu.
  nc10
  Nyumba iliyogengwa na vijana Ukombozi Vijana Halmashauri ya Magu.
  nc11
  Nyumba iliyojengwa na vijana wa kikundi cha JOMUGI Maswa.
  nc12
  Nyumba iliyojengwa na vijana wa Misungwi.
  nc13
  Nyumba ya mwananchi iliyojengwa na vijana Rorya.
  nc14
  Picha ya pamoja na vijana wa kikundi cha Ukombozi Vijana Magu mble ya mojawapo ya nyumba ziliyojengwa na vijana hao
  nc15
  Eneo jingine la kazi ya vikundi cha Ukombozi Vijana Magu.
  nc16
  Eneo la kazi la kufyatua matofali ya vijana wa Misungwi.
  nc17
  Eneo la kazi la kufyatua matofali ya vijana wa Misungwi.
  nc18
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na timu yake ya NHC akikagua matundu kumi vya choo vilivyojengwa na vijana wa kikundi Jiendeleze - Halmashauri ya Musoma Vijijini.
  nc19
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya wa ya Magu Bw. Lutengano Mwalwiba.
  nc20
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Bw. Juma Hamsini.
  nc21
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii, Susan Omari na Ujumbe wa NHC wakipata maelekezo kutoka kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya  Biutiama Bi. Anna Nyamubi.
  nc22
  Ujumbe kutoka NHC ukizungumza na Mkurugenzi Halmashauri ya Mji wa Tarime Bw. Fidelica Myovella.
  nc23
  Ujumbe wa NHC ukipata maelekeo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rorya Bw. Gasper Mago.

  0 0

  Na Daudi Manongi,MAELEZO.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Sal
  aam Profesa Haji Semboja amewataka wamiliki na wadau wa tasnia ya habari hapa nchini kuusoma na kuelewa madhumuni ya Muswada wa Huduma za Habari kwa ajili kusaidia maoni ambayo yataboresha muswada huo.

  Profesa Semboja asema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi. Amesema ni vema wanahabari na wadau wa habari wakausoma kwa kina na kutoa maoni yao kwani hakuna sababu ya kuuchelewesha muswada huo kwa ajili ya kuimarisha tasnia ya habari.

  Profesa Semboja ameipongeza Serikali kwa kuwa na uwazi katika kuuleta muswada huu kwa jamii ili wauone na kuulewa na waweze kutoa maoni yao ili tupate kitu kilicho bora. Amesema kuwa baadhi ya maeneo yaliyomo katika muswada huo yatasaidia wanahabari kuboresha taaluma yao na kuwa na wanahabari wanaotambulika.

  Profesa Semboja amewataka wana habari kuusoma vyema muswada huo na kuacha kuwa na mawazo hasi huku akisisitiza ushiriki wao uwe mkubwa kwani muswada huu unapatikana kwenye mitandao na hivyo unamfikia mtu yeyote kwa urahisi kabisa.

  Muswada wa Vyombo vya Habari ulichapishwa na kuwekwa hadharani tangu Septemba 2016, pamoja na mambo mengi mazuri wadau wakuu wote walishiriki katika hatua za ndani za serikali kutoa maoni na kwa sasa wanashiriki katika hatua ya Kamati ya Bunge

  0 0

  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali akifungua Mkutano wa Majaji Wafawidhi na Majaji waliosikiliza Kesi za Uchaguzi wa mwaka 2015 unaofanyika jijnini Arusha.

  Baadhi ya Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye Mkutano wa Kutathmini usikilizwaji wa kesi za uchaguzi unaofanyika jijini Arusha.

  Baadhi ya Waheshimiwa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa kwenye Mkutano wa Kutathmini usikilizwaji wa kesi za uchaguzi unaofanyika jijini Arusha.

  ………………………………………………………….

  Na Lydia Churi- Mahakama

  Majaji wa Mahakama Kuu nchini wametakiwa kufanya kazi yao kwa kuzingatia maadili ya taaluma hiyo wakati wote kwa kuwa watanzania wanaitegemea Mahakama kuwatendea haki kwa sawa na kwa wakati.

  Akifungua Mkutano wa Majaji Wafawidhi na Majaji waliosikiliza kesi za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 unaotathmini usikilizwaji wa kesi hizo leo jijini Arusha, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali alisema watanzania wana imani na Mahakama hivyo ni muhimu kwa Majaji hao kutenda haki wakati wote.

  Alisema Majaji hao wamekutana ili waweze kupata nafasi ya kujadili changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa kusikiliza kesi zilizohusu uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kubadilishana mawazo namna ya kuzimaliza kwa haraka kesi zihusuzo uchaguzi kwa siku za mbeleni.

  Alisema jumla ya kesi 53 za Ubunge zilizotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 zilifunguliwa katika Mahakama Kuu kanda za Dar es salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya, Moshi, Mtwara na Mwanza. Kanda nyingine ni Shinyanga, Songea, Sumbawanga, na Tanga.

  Jaji Wambali alisema kati ya kesi hizo, kesi 31 zilimalizika katika hatua za awali na kesi 22 ziliendelea. Mpaka sasa kesi 19 zimemalizika. Aliongeza kuwa kesi tatu bado ziko mahakamani.

  Jaji Wambali alisema ni jambo la kujivunia kwa Mahakama ya Tanzania kwa kuwa kesi zote 196 zilizotokana na uchaguzi wa madiwani zilimalizika mapema katika Mahakama mbalimbali za Hakimu Mkazi nchini.

  Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kufanyika kwa uchaguzi Mkuu nchini, zaidi ya asilimia 94 ya kesi za uchaguzi zilizofunguliwa kwenye Mahakama Kuu zimemalizika wakati asilimia 100 ya kesi zote za udiwani zimemalizika.

  Jaji Kiongozi amewapongeza Majaji na Mahakimu wote kwa kumaliza kesi kwa ufanisi na kwa wakati licha ya changamoto mbalimbali wanazozipitia Watumishi hao wa Mahakama wakati wanaposikiliza kesi zainazotokana na uchaguzi.

  Aidha Jaji Kiongozi alishukuru shirika la Umoja wa Mataifa-UNDP kwa kufadhili mafunzo mbalimbali ya Majaji na Mahakaimu yaliyotolewa kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Mkutano wa siku nne wa Majaji Wafawidhi pamoja na Majaji waliosikiliza kesi za uchaguzi ulioanza leo jijini Arusha umefadhiliwa na shirika hilo.

  0 0

   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhami ya NSSF, Profesa Samuel Wangwe kabla ya kupondoka kweye uwanja wa ndege wa Arusha kurejea Dar es salaam  Oktoba 21, 2016.  Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, GAbriel Daqalo na watatu  kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius  Kahyarara. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, Gabriel Daqalo kwenye uwanja wa ndege wa Arusha kabala ya kurejea jijini  Dar es salaam Oktoba 21, 2016 . Jana alifungua Mkutano wa sita wa wadau wa NSSF kwenye Kituo cha Kimataifa cha `mikutano cha Kimataifa cha Arusha AICC. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Profesa Samuel Wangwe na Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa  Godius Kahyarara. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  SUALA la wizi na ujambazi kwa wakazi wa Bunju Beach kubakia kuwa historia baada ya Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni kuahidi kujenga kituo cha Polisi kitakachokuwa na uwezo wa kuchukua Askari zaidi ya 40.

  Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, ACP Suzan Kaganda alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya kuzindua umoja wa Wakazi wa Bunju “Bunju Beach Community Support” .RPC Kaganda amesema kuwa wezi na majambazi wamekula kwao na kuongeza kuwa suala la ulinzi na usalama ni la kila raia kwa mujibu wa sheria.

  Awali akisoma risala ya Jumuiya hiyo Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya kusaidiana ya Wakazi wa Bunju (Bunju Beach Community Support), Vanessa Milinga alisema kuwa Jumuiya hiyo ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa na lengo la kuimarisha ulinzi na usalama wa mali na familia za wakazi wa Bunju Beach.

  Vanessa amesema kuwa mwaka 2011 walipata usajili ambapo pia wanachama wameongezeka na kupelekea kubadili kuongezeka kwa malengo ambayo ni pamoja na kuanzishwa kwa SACCOSS.

  Akizungumzia historia ya Bunju Beach Community Support, Mmoja wa waanzilishi wa Jumuiya hiyo Profesa. Joas Rugemalila amesema kuwa umoja huo umeanzishwa kwa lengo la kuimarisha ulinzi shirikishi, usalama, amani na maendeleo.
  RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda akizungumza na wanajumuiya ya Bunju Beach Community Support wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato, OCD Kawe, John Malulu na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
  Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakazi wa Bunju Beach,Bunju Beach Community Support Bi. Vanessa Milinga akisoma risala ya Jumuiya hiyo wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
  RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya wakazi wa Bunju Beach (Bunju Beach Community Support) Bi. Vanessa Milinga mara baada ya kumkabidhi risala wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
  Muasisi wa Jumuiya ya Bunju Community Support Profesa. Joas Rugemalila (kushoto) akigonga cheers na RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.
  RPC wa Kinondoni Suzan Kaganda wakigonga cheers wakati wa hafla ya kujumuika pamoja kwa wanajumuiya hao hivi karibuni Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Bunju Mhe. Phocas Nato na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw. Kheri Nassor Missinga.


  0 0

  Na Asteria Muhozya, DSM

  Wizara ya Nishati na Madini, imeandaa Mkutano ambao pamoja na masuala mengine utapokea Taarifa kuhusu maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga, ambao utahudhuriwa na Mawaziri wanaosimamia sekta hiyo kutoka Uganda na Tanzania.

  Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Jijini Tanga tarehe 24 hadi 26,Oktoba, 2016, utatanguliwa na mkutano wa Wataalam kutoka Serikali ya Tanzania na Uganda na kisha kufuatiwa na mkutano wa Makatibu Wakuu wa sekta hizo, na tarehe 26 Oktoba, 2016, utafanyika Mkutano wa Mawaziri wa nchi husika.

  Mbali na Wataalam kutoka Tanzania na Uganda, mkutano huo pia utashirikisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Wawekezaji katika mradi huo kutoka Kampuni za Total E&P ya Ufaransa, Tullow Oil ya Uingereza, China National Offshore Oil Company (CNOOC) na kampuni za Mafuta za Taifa za Tanzania na Uganda.

  Mradi wa bomba hilo una urefu wa kilomita zipatazo 1,443 kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga. Bomba hilo linatarajiwa kupita katika mikoa ya Kagera, Geita, Tabora, Shinyanga Dodoma na Tanga.

  Mradi huo ambao uliridhiwa na Baraza la Mawaziri kutekelezwa nchini Tanzania mnamo tarehe 29/09/2016, katika kikao kilichoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, utakua na manufaa makubwa kwa Tanzania kwa kuongeza kasi ya kukua kiuchumi.

  Bandari ya Tanga itapata fursa za kuongeza kiwango cha kufanya biashara na nchi za Uganda, Rwanda na Burundi na hivyo kuweza kufungua mkuza wa kiuchumi baina ya Mikoa ambayo bomba hili litapita na nchi Jirani za Afrika Mashariki.

  Mradi huo unaotajwa kuwa mradi mwingine wa kihistoria, utagharimu kiasi cha Dola za Marekani takribani Bilioni 3.5, ambapo utakapokamilika unatarajiwa kuwa na uwezo wa kusafirisha jumla ya mapipa Laki Mbili (200,000) kwa siku. Mradi utakua na Manufaa kwa Taifa ikiwemo kutoa ajira za muda mfupi na mrefu.

  0 0


  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Augustine Mahiga akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye Mkutano wa majadiliano ya amani na ulinzi kati ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) unaofanyika katika Hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine Mkutano huo unarajia kujadili kuhusu masuala yafuatayo; Aina za chaguzi na jinsi zinavyosimamiwa miongoni mwa nchi wanachama, Vijana wa Afrika wanaokimbilia Ulaya kutafuta maisha, tishio la amani ya Kanda na Dunia.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima (katikati) akifuatilia Mkutano. Kulia ni Katibu Mtendaji wa SADC Dkt. Stergomena Tax na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (kushoto)
  Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wakimsikiliza Waziri Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
  Sehemu ya Wajumbe wa Mkutano na Watendaji wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi kutoka SADC na EU.
  Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika mahojiano na wanahabari

  0 0

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman akizungumza na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (hawapo pichani) leo jijini Arusha. Katika Mkutano huo, Jaji huyo aliwapongeza Majaji kwa kuziendesha vizuri kesi zilizohusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015PICHA NA LYDIA CHURI-MAHAKAMA

  ………………………………………………………………

  Na Lydia Churi-Mahakama

  Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Majaji wengine wamepongezwa kwa kumaliza vizuri kesi za uchaguzi zilizofunguliwa katika Mahakama Kuu kanda mbalimbali nchini na pia kutenga muda wa kujadili changamoto zilizotokana na kesi hizo.

  Akizungumza na Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania leo jijini Arusha, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amewapongeza Majaji hao kwa kujitoa katika kusikiliza kesi hizo na kuzitolea hukumu kesi nyingi kwa kipindi kifupi licha ya kesi chache kubakia mahakamani.

  Jumla ya kesi 53 za Ubunge zilizotokana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 zilifunguliwa katika Mahakama Kuu kanda za Dar es salaam, Dodoma, Iringa, Mbeya, Moshi, Mtwara na Mwanza. Kanda nyingine ni Shinyanga, Songea, Sumbawanga, na Tanga. Kati ya kesi hizo, kesi 31 zilimalizika katika hatua za awali na kesi 22 ziliendelea, mpaka sasa kesi 19 zimemalizika. kesi tatu bado ziko mahakamani.

  Hata hivyo kesi zote 196 zilizotokana na uchaguzi wa madiwani zilimalizika mapema katika Mahakama mbalimbali za Hakimu Mkazi nchini. Katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kufanyika kwa uchaguzi Mkuu nchini, zaidi ya asilimia 94 ya kesi za uchaguzi zilizofunguliwa kwenye Mahakama Kuu zimemalizika wakati asilimia 100 ya kesi zote za udiwani zimemalizika.

  Aidha, Jaji Mkuu amewataka Majaji hao kuweka mikakati ya kuhakikisha kasi ya kupunguza kesi mahakamani hasa zile za muda mrefu inaongezeka ili kupunguza malalamiko yanayotokana na kuchelewa kutoa hukumu na kutopatikana kwa nakala za hukumu kwa wakati.

  Mheshimiwa Chande amewataka Majaji kusimamia suala la maadili ndani ya Taasisi hiyo ili kurejesha imani ya wananchi kwa Mahakama yao.

  Kuhusu suala la Maadili kwa Mahakimu, Jaji Mkuu amesema wameomba ushauri Tume ya Utumishi wa Mahakama kuwa endapo hakimu atashtakiwa kwa kosa la rushwa ataondolewa kazini kwa maslahi ya Umma hata kama atashinda kesi hiyo.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi watatu kutoka (kulia), Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wanne kutoka (kulia) watatu kutoka kushoto, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wanne kutoka (kushoto), Mtendaji mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Arch. Elius Mwakalinga wakwanza (kulia) Pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Joseph Nyamhanga wakwanza kushoto.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Elimu, Sayansi Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara. Hosteli hizo zitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 3840 na ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa hosteli za wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania TBA Arch. Elius Mwakalinga akitoa ufafanuzi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuhusu ujenzi wa Hosteli hizo za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga tumba katika bendi ya Msondo Ngoma mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mke wake Mama Janeth Magufuli, Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa Rwekaza Mukandara wakipiga makofi wakati brass bendi ya JKT ilipokuwa ikitumbuiza mara baada ya kukamilika kwa tukio la kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati akiwasili katika viwanja vya hosteli mpya za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


  Taaswira ya moja ya moja ya hosteli hizo za wanafunzi ambazo ujenzi wake umefikia asilimia 75 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.PICHA NA IKULU.

  0 0

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakimkabidhi Afisa Mtendaji wa Kata ya Muhandu ilipo shule hiyo, vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

  Mbali na vifaa hivyo, pia wanafunzi hao ambao miongoni mwao ni wafanyabiashara na watumishi wa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi, wametoa vifaa vya michezo kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ikiwemo mipira na jezi, pamoja na zawadi mbalimbali kwa ikiwemo kompyuka kwa baadhi ya waliokuwa waalimu wao kipindi hicho.
  Na BMG

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakiwakabidhi baadhi ya waalimu pamoja na kamati ya shule hiyo, vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakikabidhi vifaa mbalimbali vya kurudufu taarifa ambavyo ni printa pamoja na kompyuta walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza, wakiwakabidhi vifaa vya michezo wanafunzi wa shule hiyo walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza, wakiwakabidhi vifaa vya michezo wanafunzi wa shule hiyo walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza, wakiwakabidhi vifaa vya michezo wanafunzi wa shule hiyo walivyovitoa kwa ajili ya shule yao hii leo.

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kulia), wakimkabidhi zawadi ya kompyuta aliyekuwa mwalimu wao, Mwalimu Nicholaus Magashi (kushoto).

  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu mwaka 1993 (1987-1993) Shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza (kushoto), wakimkabidhi zawadi mmoja wa aliyekuwa mwalimu wao, Mwalimu Elizabeth Makonda (kulia).

  Kaimu Mkuu wa shule ya Msingi Nyakato Jijini Mwanza, Florence Sam, akisoma taarifa ya shule hiyo kwa wanafunzi waliohitimu shuleni hapo mwaka 1993 walipoitembelea na kutoa vifaa mbalimbali ikiwemo kompyuta pamoja na printa.

  Mwalimu Benadetha Athanasi, akitoa taarifa fupi kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza mwaka 1993.

  Atley Kuni akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza mwaka 1993, namna wazo kusaidia shule ya msingi waliyosoma lilivyoanza kwenye mitandao ya kijamii (kundi la whatsupp).

  Baadhi ya Waalimu wa shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza, kamati ya shule pamoja na baadhi ya waaliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule hiyo.

  Baadhi ya Waalimu wa shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza, kamati ya shule pamoja na baadhi ya waaliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule hiyo, wakiimba wimbo wa Taifa.

  Mmoja wa wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza akijitambulisha.

  Mmoja wa wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza akijitambulisha.

  Mmoja wa wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza akijitambulisha.

  Mwalimu Nicholaus Magashi, aliyekuwa mwalimu wa shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza akijitambulisha

  Mwalimu Elizabeth Makonda, aliyekuwa mwalimu wa shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza akisalimia

  Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza, 2016

  Moja ya darasa walilosoma wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwnza.

  Moja ya darasa walilosoma wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwnza.

  Picha ya pamoja kati ya wanafunzi waliohitimu darsa la saba shule ya Nyakato Jijini Mwanza, pamoja na waalimu wa shule hiyo.

  Na George Binagi-GB Pazzo
  Wadau wa elimu mkoani Mwanza wametakiwa kushirikiana na serikali katika kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za waalimu katika shule ya msingi Nyakato Jijini Mwanza.

  Kaimu Mkuu wa shule hiyo, Florence Sam, ametoa rai hiyo wakati wa hafla ya kupokea vifaa mbalimbali ikiwemo kompyuta pamoja na printa, vilivyotolewa na wanafunzi waliohitimu darasa la saba katika shule hiyo mwaka 1993.

  Mwalimu Sam amesema shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 1,800 huku vyumba vilivyopo vikiwa ni 18 hali inayosababisha kuwa na upungufu wa vyumba 32 ambapo ametumia fursa hiyo kuwaasa wadau mbalimbali kusaidia kukabiliana na changamoto hiyo.

  Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliohitimu darasa la saba mwaka 1993 katika shule hiyo, Mwalimu Benadetha Athanasi, amesema wanafunzi hao wameamua kusaidia kutatua baadhi ya changamoto za shule hiyo ili kutoa mwamko kwa wadau wengine kusaidia utatuzi wa changamoto za elimu nchini.

  Vifaa vilivyotolewa na wanafunzi hao ni pamoja  na vifaa vya michezo kwa wanafunzi,kompyuta pamoja na printa ambavyo vimegharimu Zaidi ya shilingi Milioni Mbili.

  0 0


  Afisa masoko Platinum Credit Tanzania, Gideon Lufunyo (kushoto) akikabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji ambayo ni sawa na tani 15 kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu ikiwa ni msaada wa taasisi hiyo kwa waathirika wa tetemekonla Ardhi mkoani humo.
  Kampuni ya Platnum Credit Tanzania Leo imekabidhi msaada wa mifuko 300 ya sumenti kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salum Kijuu kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoani humo.

  Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo leo, Ofisa Masoko wa Kampuni hiyo,Gideon Lufunyo alisema  tetemeko hilo limeleta madhara makubwa ambayo yamewagusa na kuamua kusaidia serikali katika kurejesha miundombinu yake hasa katika mshule katika hali nzuri ili masomo yaendelee na watoto wapate elimu.

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza alipokutana na Balozi wa Finland Nchini, Pekka Hukka (kushoto). Balozi Hukka alimtembelea Waziri Muhongo Ofisini kwake, Makao Makuu ya Wizara ya Nishati na Madini Jijini Dar es Salaam ili kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa Sekta ya Nishati nchini.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza wakati wa kikao na Balozi wa Finland Nchini, Pekka Hukka (katikati). Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
  Balozi wa Finland Nchini, Pekka Hukka (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akipeana mkono na Balozi wa Finland Nchini Tanzania, Pekka Hukka wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Muhongo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akizungumza katika kikao na Balozi wa Finland Nchini, Pekka Hukka (kushoto).

  0 0

  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel anatarajiwa kufungua kongamano kuhusu mabadiliko ya mifumo ya uendeshaji katika klabu za soka nchini.
   
  Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Jumamosi Oktoba 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuhusu mifumo ya kiuendeshaji ambayo klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zipo mbioni kuingia na limeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
   
  Kongamano hilo litaanza saa nne na nusu asubuhi na litarushwa live (mubashara) na kituo cha televisheni cha Azam kupitia chaneli yake ya Azam Two.Dhamira kubwa ya kongamano hilo ni kupata maoni ya kitaalamu kuhusu mifumo hiyo, ambapo Simba ipo mbioni kuingia mambo ya hisa, wakati Yanga utaratibu wa kukodishwa.
   
  Baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ni namna ya kuendesha klabu za soka kibiashara, uwekezaji, mambo ya hisa na masuala ya uthamini kukiwa na watalaamu kutoka taasisi mbalimbali nchini.
   
  Pia kutazungumzwa umuhimu wa mabadiliko katika klabu hizo na harakati za kuzibadili zilivyoanza miaka ya nyuma na matokeo yake yalivyokuwa.
   
  Lengo ni kujadili kitaalamu bila ushabiki wa namna yoyote kwani nia ni kujenga na kuimarisha soka na michezo kwa ujumla hapa nchini na ndiyo sababu tumealika wataalamu wa kada mbalimbali, viongozi wa zamani wa soka kwa tofauti na baadhi ya wadau wa soka.
   
  Nawasilisha,
   
  Amir Mhando
  Katibu Mkuu TASWA
  21/10/2016

older | 1 | .... | 1015 | 1016 | (Page 1017) | 1018 | 1019 | .... | 1898 | newer