Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

HIVI NDIVYO MAMBO YALIVYOKUA KATIKA TAMASHA LA KANDANDA

$
0
0
TIMU ya soka ‘Team Ismail’ imefanikiwa kuwagaragaza wapinzani wao wa jadi 'Team Dizo Moja' kwa kipigo cha mabao 4-1, katika tamasha la Kandanda day, lililofanyika Jumamosi katika Viwanja vya Jakaya M Kikwete Youth Park.


Kipigo hicho kwa 'Team Dizo', ni mfululizo wa matokeo mazuri ya Team Ismail,ambayo mwaka huu imeonekana kulipiza kisasi cha kuchapwa idadi hiyo ya mabao kama walivyofanya Team Dizo katika msimu wa mwaka 2014.

Mabao ya Team Ismail,yaliwekwa kimiani na Freddy Pastor aliyeweka kimiani mabao mawili,huku Gerald Bernald na Noah Katepa wakifunga bao moja moja na lile la kufutia machozi kwa timu Dizo likifungwa na mchezaji wao waliyemchukua kwa mkopo toka timu Ismail Wilfred Kadege.

Mwaka jana katika tamasha hilo, Timu Ismail,iliwatandika wapinzani wao kwa mabao 2 kwa mtungi,jambo ambalo mwaka huu liliongeza upinzani mkubwa ndani na nje ya uwanja kutoka kwa mashabiki wa timu hizo mbili.

Mbali na mtanange huo,mechi nyingine iliyovuta hisia za mashabiki waliohudhuria tamasha hilo ni mchezo wa fainali ya makundi ulizokutanisha timu za Dar City Fc na Coca Cola,ambapo katika mchezo huo, Coca waliigaragaza Dar City kwa mabo 3 kwa bila.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati,Patrick Dumulinyi,aliwashukuru wadhamini wote pamoja na timu shiriki kwa kufanikisha lengo la tamasha la mwaka huu lililobeba kauli mbiu ya Mpira na Dawati kufana kwa kiasi kikubwa.

“Ningependa kuwashukuru wadhamini wetu na timu shiriki,kwa kuungana kutimiza ndoto zetu za mwaka huu za kuisaidia jamii kwa kukusanya fedha za madawati,ambayo kabla ya kuisha kwa mwezi huu tunatarajia kuyakabidhi katika shule husika,”alisema Dumulinyi.

Mshambuliaji wa 'Team Ismail', Nassor Bin Slum akijiandaa kuachia shuti kali kuelekea langoni mwa 'Team Dizo Moja', katika tamasha la wapenzi wa mchezo wa soka nchini 'Kandanda Day 2016', lililofanyika Jumamosi Oktoba 15, 2016 katika Viwanja vya Jakaya M Kikwete Youth Park, Jijini Dar es salaam.


MAKAMBA AHIMIZA UHIFADHI ENDELEVU WA MAZINGIRA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe. Waziri Makamba yuko Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba, wa tatu kutoka kulia akiangalia chanzo cha maji kilichovamiwa katika Mto Mambogo
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Parakuyo wakisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba kabla ya kufanya mkutano wa hadhara kijijini hapo.
Sehemu ya Wananchi wa waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Parakuyo Wilayani Kilosa. Wananchi hao walimweleza Waziri (hayupo pichani) changamoto zinazowakabili juu ya Hifadhi ya mazingira
Sehemu ya Wananchi wa waliojitokeza katika Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Parakuyo Wilayani Kilosa. Wananchi hao walimweleza Waziri (hayupo pichani) changamoto zinazowakabili juu ya Hifadhi ya mazingira

Na Lulu Mussa- Morogoro

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba ameitaka jamii ya watu wa Parakuyo katika Wilaya ya Kilosa kuishi kwa amani, uvumilivu na upendo miongoni mwao kwani ndio misingi ya watanzania.

Rai hiyo imetolewa leo katika Mkutano wa hadhara uliojumuisha jamii za wakulima na wafugaji ambazo zimekuwa na migogoro ya mara kwa mara. Waziri Makamba alizitaka jamii hizo kuishi kwa amani na kuhifadhi mazingira kwa faida ya sasa na vizazi vijavyo.

Miongoni mwa changamoto zilizobainishwa na jamii hiyo ni kutokuwa na elimu juu ya mabadiliko ya Tabianchi na athari zake pamoja na kutokuwepo na matumizi bora ya ardhi.

Waziri Makamba ameuagiza uongozi wa Wilaya na Kijiji kushirikiana pamoja kuunda kamati ya ‘Amani’ itakayokuwa na wajumbe kutoka pande zote mbili za wakulima na wafugaji na viongozi wa madhehebu ya dini ili kutafuta suluhu ya kudumu baina ya pande mbili ambazo zimekua na migogoro ya mara kwa mara. “Undeni Kamati hii mapema na Ofisi yangu itagharamia mafunzo kwa Kamati husika juu ya namna bora ya kutatua migogoro” alisisitiza Waziri Makamba.

katika jitihada za kukuza uelewa wa masuala ya mazingira na changamoto zake, Waziri Makamba ameitaka Serikali ya Kijiji kuunda Kamati ndogondogo za Mazingira ambazo zipo kwa mujibu wa sheria ya Mazingira na kuahidi kuipati mafunzo Kamati hizo ikiwa ni pamoja na kutengeneza sheria ndogo ndogo zitakazotumika kama nyenzo ya kuhifadhi na kusimamia Mazingira ya maeneo yao.

Aidha, Waziri Makamba amesema kuwa mpango wa matumizi bora ya ardhi ni muhimu sana na kuitaka jamii ya Parakuyo na Twa twa twa kushiriki kikamilifu katika zoezi la kuhakiki na kuhesabu mifugo yako ili kubaini ni ardhi kiasi gani inahitajika kwa wakulima na kiasi gani kwa wafugaji. “ndugu zangu niwasihi, Serikali ina nia ya dhati ya kuhakikisha kuna kuwa na matumizi bora ya ardhi, hivyo nawashauri mmshiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kupata uwiano wa idadi ya mifugo na ardhi iliyopo” Makamba aliongezea.

Awali katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Morogoro Waziri Makamba pia alitembelea chanzo cha maji na kujionea changamoto za kimazingira katika mto Mambogo.

ARUSHA OPEN YAMALIZIKA LUGALO YANYAKUA NAFASI TANO KATI YA 13 SAWA NA ASILIMIA 53

$
0
0
Mshindi wa Kwanza wea Division A wa Mashindano ya Wazi ya Arusha Open Kapten Shaban Kibuna akiwa katika harakati za mchezo huo katika mashindano yaliyomalizika Jumapili Oktoba 16 Jijini Arusha .(Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Mshindi wa Kwanza wa kundi la Wadogo Junior wa Mashindano ya Wazi ya Arusha Open Almadious Simon akiwa katika harakati za mchezo huo katika mashindano yaliyomalizika Jumapili Oktoba 16 Jijini Arusha .(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Mchezaji wa Golf wa Timu ya JWTZ ya Lugalo Nicholous Chitanda akiwa katika harakati za Mashindano ya Wazi ya Arusha Open katika mashindano yaliyomalizika Jumapili Oktoba 16 Jijini Arusha .(Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Mashindano ya Wazi ya Golf Arusha open yamemalizika jijini Arusha Oktoba 16 huku Timu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo ikifanya vizuri kwa kunyakua ushindi katika makundi kwa asilimia 53 huku ushindi wa Jumla ukichukuliwa na Mchezaji kutoka klabu ya Kilimanjaro.
Mpiga golf wa Timu ya Kilimanjaro issack Wanyeche akiibuka mshindi wa jumla wa mashindano hayo yaliyokuwa yakishindanishwa kwa mtindo wa Mikwaju ya Jumla Net kwenye makundi na Gross kwa ushindi wa Jumla. 

Katika Division A Mshindi ni kapteni Shaaban Kibuna kutoka Klabu ya Liugalo akifuatiwa na Richard Mtweve naye wa Lugalo ambaye walifungana kwa Mikwaju ya Jumla 145 kila mmoja lakini kutokana na kapteni kibuna kucheza vizuri siku ya mwisho akamshinda Mtweve kutokana na kucheza net ya 70 kwa 75 wakatik siku ya kwanza ilikuwa 75 kwa 70 ya Mtweve. 

Kundi B ambalo Timu ya Lugalo haikuingiza mchezaji katika kundi hilol imechukuliwa na N Matsouka wa Arusha aliyepata mikwaju ya Jumla 143 akifuatiwa na mshindi wa pili ni Musadiq Versi aliyepiga mikwaju ya Jumla 147. 

Divisheni C Mshindi ni Talib Chagani aliyepiga Mikwaju ya Jumla 148 akifuatiwa na kapteni Amanzi Mandengule wa lugalo aliyepiga mikwaju ya jumla 149. 

Kwa upande wa Kundi la wadogo Junior mshindi ni Almadiuos Simon kutoka Klabu ya Jeshi ya Lugalo kwa kupiga Mikwaju ya Jumla 131 huku mshindi wa Siku ya kwanza ni Salim Sharif aliyepata Net ya 70 na Mshindi wa Siku ya Pili ni Clemence Mutavangu wa Lugalo aliyepiga Net ya 69. 

Kwa Upande wake Nahodha wa Klabu ya jeshi ya Lugalo ambaye ni Mshindi wa Divisheni A kapten Shaban Kibuna amesema wamefanya vizuri kutokana kuingiza wachezaji 14 na kunyakua nafasi tano ukilinganisha na Arusha waliongiza wachezaji zaidi ya 50 na TPC walioingiza wachezaji 17 na kutoka bila ushindi. 

Alisema kinachofuata sasa ni klabu yake kujiandaa na mashindano yaliyoko mbele yao ya Oktoba 22 Mwaka huu lakini pia wanatarajiwa kuwa na mshindano ya Waitara Trophy na Miaka 10 ya Klabu mwezi Desemba.

MCHUNGAJI KULOLA ARINDIMA KWENYE HITIMISHO LA MKUTANO MKUWA WA INJILI KANISA LA EAGT POSTA B MABATINI JIJINI MWANZA

$
0
0
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani), kwa siku tatu mfululizo hadi jana jumapili Oktoba 16, 2016 alihudumu katika Kilele cha Mkutano Mkubwa wa Injili uliofanyika Kanisa la EAGT Posta B, Mabatini Jijini Mwanza, uliofanyika kwa juma zima kuanzia Oktoba 09 hadi Oktoba 16 mwaka huu.

Ulikuwa Mkutano uliojaa Neema ya Mungu ambapo makumi kwa mamia ya wakazi wa Jiji la Mwanza, walimgeukia Kristo na kuokoka huku waimbaji mbalimbali ikiwemo Kwaya ya Havillah, Mwanyamaka, Emmanuel Mgogo, Elineema Babu pamoja na waimbaji wengine wengi wakihudumu katika mkutano huo.

Mchungaji Kulola aliwahimiza wakristo kuweka dini zao pembeni na kumtumikia Mungu kwa roho na kweli huku wakiacha tabia ya kumuonea Kristo aibu.

"Tujivunie maamuzi tuliyonayo ya kuokoka maana hatukufanya makosa na kwa kuwa tunaye Yesu Kristo ambaye neno lake linakatakata kama upanga naomba wote tuwe vichaa kwa ajili yake". Alisisitiza Mchungaji Kulola akiwataka waliokoka kumtumikia Mungu bila hofu yoyote.
Na BMG
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiendelea kunena neno la Mungu katika mkutano huo
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiendelea kunena neno la Mungu katika mkutano huo
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola akiendelea kunena neno la Mungu 
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Posta B, Mabatini Jijini Mwanza, Lameck Nkumba, akiomba kwenye Mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wa Kanisa akiwemo Mchungaji wa Kanisa la EAGT Posta B, Mabatini Jijini Mwanza, Lameck Nkumba (kulia).
Waumini wakifuatilia mkutano huo
Baadhi ya waumini wakifuatilia mkutano huo
Waumini wakifuatilia mkutano huo
Bonyeza HAPA Kuhusu Mkutano Huo.

MFUKO WA PENSHENI WA PSPF UMEENDELEA KUWAFIKIA WATU WENGI KUPITIA MPANGO WA UCHANGIAJI WA HIARI (PSS)

$
0
0


Afisa Mwendeshaji  kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary akiwaeleza wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage juu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF ikiwa ni pamoja na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) ambapo mtu yeyote mwenye umri wa kuanzia miaka 18 anaweza kujiunga na kunufaika na mafao mengi.

Baadhi ya viongozi na watumishi wa Hoteli ya Heritage wakiwa wanasikiliza kwa makini somo kutoka kwa Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary kuhusu mafao yatolewayo na mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS)


Mmoja wa wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage akiwa anasoma jarida kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF


Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary akigawa vipeperushi na majarida yanayoelezea kwa kina huduma mbalimbali zitolewazo na mfuko huo.


Wafanyakazi wa Hotel ya Heritage wakiwa wanachukua fomu kwa ajili ya kujiunga na Bima ya afya ya NHIF itolewayo kwa Bei nafuu kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS)

Baadhi ya watumishi wa Hoteli ya Heritage Jijini Dar es salaam wakiendelea kusoma vigezo masharti na mambo mbalimbali juu ya Bima ya afya ya NHIF inayotolewa kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari (PSS)

Wafanyakazi wa Hoteli ya Heritage wakiendelea kupata maelezo juu ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF kutoka kwa Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary  
Picha na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa 




Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia mpango wake wa uchangiaji wa Hiari (PSS) umeendelea kuyafikia makundi mbalimbali kujiunga na mpango huo. 

Hayo yamesemwa na  Afisa Mwendeshaji  kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF Hadji Jamadary alipokuwa akitoa maelezo na mafunzo juu ya mfuko huo na wafanyakazi wa  Hoteli ya  Heritage iliyopo Jijini Dar es salaam  ambapo pamoja  na kutoa maelezo juu ya mfuko huo na kutoa  elimu ya juu ya mpango huo wa uchangiaji wa  hiari ambapo  mwanachama atatakiwa kuwa na umri wa kuanzia miaka 18 ,  atakuwa huru kuchagua muda wa kuchangia kutegemea kipato chake huku kiwango cha chini kikianzia Shilingi 10,000 ambayo mwanachama anaweza kulipia kupitia benki na huduma za simu.

Bwana Hadji alisema kuwa mpango huo wa hiari unakaribisha raia na mtu asiye raia bila kusahau mjasiriamali na mfanyakazi wa serikali  na kuongeza kuwa  mwanachama anayejiunga katika mfuko huo huweza kupata mafao ya aina sita ambayo ni; Fao la Elimu, Fao la Ujasiriamali, Fao la Uzeeni, Fao la Kifo, Fao la Ugonjwa/Ulemavu, Fao la Kujitoa, na Fao la Matibabu.

Akifafanua kuhusu Fao la Matibabu, Bwana Hadji alisema kuwa kupitia mpango wake wa uchangiaji wa hiari wanashirikiana na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ambapo mwanachama ataweza kupatiwa huduma bure katika hospitali na maduka ya madawa yaliyosajiliwa na NHIF kote nchini.

“Mwanachama anaweza kuwasajili pia wategemezi wake watano na kuendelea kupata mafao yetu bila shida yoyote,” alisema Hadji

Wakizungumza kwa nyakati mbalimbali wafanyakazi hao walionesha kufurahia unafuu wa mfuko huo na kuwataka PSPF kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili wananchi wengi wajiunge kwa kuwa hupoteza fedha nyingi ambazo wangeweza kuziokoa kwa kujiunga na mfuko huo.

Aidha Hadji aliwaambia wafanyakazi  hao kuwa PSPF ina wawezesha  wanachama wake na jamii kwa ujumla kumiliki nyumba zilizopo Dar , Morogoro, Tabora, Mtwara, Shinyanga na Iringa ambapo wataweza kununua kwa mkopo au malipo ya mara moja pamoja na mikopo ya viwanja vilivyo sehemu mbalimbali nchini.

WANANCHI WILAYANI RUFIJI WAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUINGILIA KATI MGOGORO WA ARDHI BAINA YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

$
0
0
 Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha mloka katika mkutano wa adhara kwa lengo la kuweza kujadili changamoto mbali mbali inazowakabili
 Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akiwahutubia wananchiwa kijiji cha mloka katika mkutano wa adhara.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha mloka wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Rufiji Mohamed Mchengwerwa wakati  wa mkutano huo wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha mloka.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)   .


NA VICTOR MASANGU, RUFIJI

WANANCHI wa kijiji cha Mloka kata ya Mwaseni  wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani wamemwomba Rais wa awamu ya tano Dr.John Magufuli kuingilia kati haraka iwezekanavyo migogoro  ya kugombania  ardhi baina ya wafugaji na wakulima ya  ili kuweza kuepeukana  vurugu na mapigano ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara na kusababisha baadhi ya watu kupoteza maisha yao na uvunjifu wa amani.

Kilio hicho wamekitoa kwa mbunge wa jimbo la Rufiji wakati wa mkutano wa adhara  katika kijiji cha Mloka kata ya Mwaseni  ulioandaliwa  kwa lengo la kuweza kubaini changamoto mbali mbali zinazowakabii wananchi kwa lengo la kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

 Wanakijiji hao akiwemo Juma Katoto na  Salum Mlanzi walisema kwamba kulingana na kukithiri kwa mapigano ya wakulima na wafugaji serikali inapaswa kulitafutua ufumbuzi suala hilo kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kufanya utaratibu wa kuipunguza mifugo iliyozidi kwani ndio chanzo cha kusababisha vurugu hizo.

Aidha katika hatua nyingne walisema  kuwa jamii ya wafugaji wamekuwa wakiingiza mifugo yao katika mashamba na kula mazao yao hali ambayo  kwa sasa imesababisha kuwepo kwa njaa katika baadhi ya maeneo kutokana  na kukosa chakula .

“Kwa kweli kwa sasa sisi wananchi wa kijiji hiki cha mloko bado tunakabiliwa na changamoto ya wakulima na wafugaji, maana tatio kubwa ni jamii ya wafugaji kuingiza mifugo yao katika mashamba yaetu na kua mazao yote kama vile, mahindi, mpunga, mboga mboga amabo ndizo tunategemea katika chakula, hivyo serikali inapaswa kuwachukulia hatua kali a kisheria,”alisema wananchi hao.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la rufiji Mohamed Mchengerwa ameahidi kulivalia njuga suala hilo kwa kushirikiana  bega kwa bega na serikali ya awamu ya tano  katika  kuhakikisha wanatenga maeneo maalumu   kwa ajili ya wagugaji na wakulima ili kuepukana na  mapigano ambayo yamekuwa yakijitokeza kwa wananchi wake.

Mchengerwa aliesma kwamba anatambua kuwepo kwa changamoto hiyo ya wafugai kuingiza migugo kiholela katika maeneo ya mashamba, lakini ameshaana kufanua jitihada  hali na mali kuhakikisha kuwa serikali inatenga maeneo maalumu kwa ajili ya wakulima na wafigaji ili kuweza kuondokana na virugu amabo imekuwa ikijitokeza.

“Katika jimbo langu la rufiji kwa sasa kuna zaidi ya mifugo kama laki tatu na nusu hadi laki nne kwa hivyo kikubwa aidi hapa mii nitahakikisha kwamba vurugu hizi zinamalizika kwa kushirikiana  na serikali ili kuweza kuona jinsi ya kutoa elimu kwa jamii ya wafugaji na wakulima ,ii wananachi wawee kuishi kwa amani bila ya kuwepo kwa mapigano ya aina yoyote,”alisema Mchengerwa.

WILAYA  ya rufiji kwa sasa ambayo inakadiriwa kuwa na mifugo zaidi ya laki tatu na nusu  bado inakabiliwa na changamoto  ya migogoro ya ardhi kwa kipindi cha muda mrefu kutokana  na jamii ya wakulima kuamua kuingiza mifugo yao katika maeneo ya mashamba na kula mazao hali ambayo inasababisha kuibuka kwa matukio ya mapigano na uvunjifu wa amani .

MBONI MASIMBA NDANI YA 102.5 LAKE FM MWANZA AKIZUNGUMZIA KONGAMANO LA SAUTI YA MWANAMKE.

$
0
0
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, Mboni Masimba (kushoto) akizungumza na Caroline Mwaipungu ambaye ni Mtangazaji wa 102.5 Lake Fm Mwanza kuhusu Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Na BMG
Konagamano hilo limelenga kuwahamasisha wanawake kujikomboa kiuchumi ambapo wanawake mbalimbali waliofanikiwa kiujasiriamali, kibiashara na kielimu watakuwepo kuzungumza na wanawake Jijini Mwanza ambapo kiingilio itakuwa elfu 40 tu na utapata elimu, burudani pamoja na chakula.

"Atakuwepo Shekha Nasser ambaye ni mmiliki wa Shear Illusion na Mwanzilishi wa Manjano Foundation ambaye amefanikiwa kwenye biashara, atakuwepo Mkandarasi Maida Waziri ambaye amekuwa mkandarasi na amefanikiwa pamoja na Biubwa Ibrahim ambaye ana Kampuni inaitwa Namaingo Agri_Busness Agency ambayo inawawezesha watu mbalimbali katika masuala ya kilimo na wengine wengi". Amefafanua Masimba.
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, Mboni Masimba akiwa ndani ya 102.5 Lake Fm Mwanza akizungumzia Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu ndani ya Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.
Mtangazaji wa Kipindi cha "The Mboni Show" kinachoruka kupitia runinga ya TBC1, Mboni Masimba (kushoto) akizungumza na Caroline Mwaipungu ambaye ni Mtangazaji wa 102.5 Lake Fm Mwanza kuhusu Kongamano la Sauti ya Mwanamke linalotarajiwa kufanyika Novemba 06 mwaka huu Gold Crest Hotel Jijini Mwanza.

JARIDA LA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO


Usalama wa chakula, uzalishaji kuboreshwa—Dkt.Turuka

$
0
0
Serikali imesema iko makini na itahakikisha kuwa nchi inakuwa na usalama wa kutosha wa chakula kwa kuongeza uzalishaji ili kuendana na idadi ya watu inayoongezeka.

Akiongea wakati wa mkutano wa wadau wa mbolea toka ndani na nje ya nchi uliofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, alisema pamoja na juhudi nyingine zinazofanyika, wanasayansi na watafiti wametakiwa kuhakikisha kuwa taarifa zinazopatikana kuhusu udongo zinatumika ipasavyo ili kutoa suluhisho linalotakiwa pale inapohitajika.

“Taarifa hizi zitasaidia kufahamu maeneo yenye rutuba kidogo, sumu na hivyo kupata majibu yanayotakiwa,” alisema.

Katibu Mkuu huyo alitaja moja ya mikakati ya kuongeza uzalishaji wa mazao kama ushirikiano kati ya serikali na taasisi inayojulikana kama Africa Soil Information Services (AfSIS) na kitengo kipya katika Wizara hiyo kinachoitwa Tanzania Soil Information Services (TanSIS) ambapo ardhi yote nchini itapimwa na kufanyiwa tathmini ili kujua ubora wake.

Alisema mkakati huo utasaidia kujua mahitaji ya maeneo husika na kuwasiliana na kampuni za kuzalisha mbolea.Aliiomba taasisi ya African Fertilizer and Agribusiness Partnership (AFAP) na wadau wengine kushirikiana na TanSIS ili kuhakikisha kuwa panakuwa na matumizi bora ya mbolea nchini.
 
Takwimu zinaonyesha kuwa matumizi ya mbolea bado ni madogo sana katika eneo la Afrika kusini mwa jangwa la Sahara.
 
Mwaka 2005 hadi 2010, wastani wa matumizi ya mbolea Afrika ilikuwa metriki tani milioni 3.2 kwa mwaka ikilinganishwa na metriki tani milioni 74.1 (Asia), 19.5 (Marekani) and 13.0 (Ulaya).

Kwa mujibu wa Dr. Turuka, matumizi haya madogo ya mbolea yanatakiwa kuboreshwa haraka kama kweli Afrika inataka kuzalisha chakula cha kutosha watu wake.“Maboresho katika sekta ya kilimo hayana budi kuimarishwa sasa kuliko kipindi chochote kutokana na idadi ya watu inayoongezeka na mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema.

Wakati wa uhuru mwaka 1961, Tanzania ilikuwa na watu takribani milioni 9.  Idadi hiyo imeongezeka kufikia karibu watu milioni 50 mwaka 2016 katika eneo la ukubwa wa ardhi lile lile la kilometa za mraba 945,000,000.

Wataalamu wanakubaliana kwamba matumizi ya mbolea yenye virutubisho vingi kama njia ya kuongeza tija na kuboresha mazingira katika uendeshaji wa kilimo.

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA MAELFU KUAGA MWILI WA MEYA WA ZAMANI WA DAR ES SALAAM DKT. DIDAS MASABURI

$
0
0
 VIONGOZI MBALIMBALI WAMEJITOKEZA KUAGA MWILI WA DKT DIDAS MASABURI,VIWANJA VYA KARIMJEE JIJINI DAR LEO .
SANDUKU LENYE  MWILI WA MAREHEMU DKT DIDAS MASABURI LIKIWASILI VIWANJA VYA KARIMJEE,JIJINI DAR ES SALAAM ASUBUHI HII KWA AJILI YA KUTOLEWA HESHIMA ZA MWISHO,AMBAPO RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI ALIWAONGOZA WANANCHI WALIOFIKA KUSHIRIKI KUAGA MWILI WA DKT DIDAS MASABURI.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea machache kwenye hafla ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016.
 Sehemu ya wafiwa kwenye hafla ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe wakitoa heshima zao za mwisho na kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe wakiwapa pole wafiwa baada ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe wakiwapa pole wafiwa baada ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe wakiwapa pole wafiwa baada ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016.
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho na kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016.
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwapa pole wafiwa baada ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016
 Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakiwapa pole wafiwa baada ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016
 Makamu wa Rais Mstaafu Dkt Mohamed Gkalib Bilali, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi na Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya mwita wakitoa heshima zao za mwisho na kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016
 Mama Salma Kikwete akitoa pole kwa wafiwa baada ya kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masabburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho kikwete na viongozi wengine wakiwa jukwaa kuu katika shughuli ya kutoa heshima za  mwisho na kuaga mwili wa Meya wa Dar es salaam wa zamani Dkt. Didas Masaburi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam leo Oktoba 17, 2016


PICHA NA IKULU


 Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Kiserikali na Kichama wakiongozwa na Rais Dkt John Pombe Magufuli (wa tano kulia) wakiwa katika viwanja vya Karimjee mapema leo asubuhi kutoa heshima ya mwisho na kuaga mwili wa Marehemu Dkt Didas Masaburi,aliyefariki wiki iliopita katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili,wakishiriki 
 Baadhi ya waombolezaji wakisubiri kuaga mwili wa mpendwa wao Dkt Didas Masaburi  
 Baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama na serikali pamoja na wananchi mbalimbali waliojitokeza kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Dkt Masaburi,mapema leo viwanja vya Karimjee,jijini Dar Es Salaam.
Sanduku lililobea mwili wa Marehemu Dkt Masaburi likiwasili katika viwanja vya Karimjee,jijini Dar kwa ajili ya kutolewa heshima za mwisho

ATCL YATOA OFA YA MWEZI MMOJA KWA SAFARI ZA MWANZA.

$
0
0


Na Daudi Manongi-MAELEZO.

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetoa ofa ya mwezi mmoja kwa abira wanaosafiri kutoka Dar es salaam kwenda Mwanza kulipa nauli ya shilingi 160,000/- kwa safari moja.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na na Kaimu Afisa Mawasiliano wa Kampuni Bi.Lily Fungamtama wakati akiongea na Idara ya Habari.
Amesema Ndege za Kampuni zimeanza kutoa huduma kuanzia Jumamosi ya wiki iliyopita ya tarehe 15 ya mwezi huu kama ilivyobainisha kupitia vyombo vya Habari.

Safari hizo zilianza kwa kutoa huduma ya kusafirisha abiria kuelekea nchini Comoro na hapa nchini itoa safari katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Kigoma.

Bi.Fungamtama amesema kwa kuanzia walianza na mazoezi ya vitendo kwa marubani na wafanyakazi wa ndani ya Ndege ambapo hatimaye walianza safari za biashara ya kusafirisha abiria mnamo tarehe 15 Oktoba kama ilivyopangwa.

Ameongeza kuwa ATCL imeboresha huduma zake kwa kiasi kikubwa kwa kuwapatia wateja wake ofa ya kubeba kilo 20 za mizigo na kilo 7 za mzigo wa mkononi bure   pamoja na kutoa vinywaji na ubadilishaji wa tiketi ni bure ndani ya mwezi.

Aidha, Kaimu Afisa Mawasiliano wa Kampuni Bi.Lily amekanusha taarifa potofu kuwa zimekwama kuanza safari zilizopangwa.
Amesema kuwa habari hizo sio za kweli kwani hivi sasa wameshaanza huduma katika mikoa hiyo mitatu.

Kampuni ya Ndege ya ATCL kwa sasa ina ndege tatu,zikiwemo mbili aina ya Dash8-Q400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja na Dash8-Q300 moja yenye uwezo wa kubeba  abiria 50. 

FNB YAZINDUA MASHINE ZA MALIPO KWA NJIA YA KADI

$
0
0

Meneja Masoko wa First National Bank Tanzania, Bi. Blandina Mwachang’a (Kushoto), na Mkuu wa kitengo cha bidhaa na huduma za kimtandao, Bw. Silvest Arumasi ( kulia) wakionyesha Mashine za malipo kwa njia ya kadi ambazo benki hiyo imezindua ili kuimarisha matumizi kadi za benki kama mbadala wa fedha taslimu Katikati ni Meneja wa Huduma za Kadi, Bi. Emma Kilimba akiwa ameshikilia tuzo ya ufanisi wa mashine hizo za malipo kwa mwaka 2016. 

Na Cathbert Kajuna. 

First National Bank Tanzania (FNB) imezindua rasmi mashine za malipo kwa njia ya kadi (POS Devices) jijini Dar es salaam kama hatua ya kuimarisha matumizi ya kadi za benki kwa ajili ya malipo ya bidhaa na huduma kwa njia salama, rahisi, na kwa gharama nafuu na zitatumika kama mbadala wa fedha taslimu. Mkuu wa bidhaa na huduma za dijitali wa benki hiyo, Silvest Arumasi alisema benki itatoa mashine za kuweka maeneo mbalimbali ya biashara kubwa na biashara ndogo au za rejareja. 

Vilevile benki hiyo itatoa mashine ndogo za kubeba kama simu ambazo zitatumika kwenye sekta ya utalii na mahoteli pamoja na biashara nyingine hasa zile zinazohama hama kwani mashine hizo zinatumia mtandao wa Intaneti kama simu. “Biashara yoyote inaweza kutumia mashine za malipo kwa njia kadi (P0S Device) kupokea malipo ya bidhaa au huduma. 

Huduma hii inatarajiwa kuongeza tija kwenye maeneo ya biashara kwa kupunguza hatari zitokanazo na utunzaji fedha taslimu na pia itapunguza safari za wafanyabiashara kwenda katika matawi ya benki kuweka fedha na sasa wataweza kutumia muda mwingi zaidi kuendesha biashara. 

Mashine za malipo kwa njia ya kadi zinaweza kuwekwa sehemu ya kudumu karibu na wateja au kubebeka kulingana na mahitaji ya mteja” alisema. Alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo kutaboresha huduma za kidijitali za benki hiyo kwani sasa wateja wataweza kuangalia na kupakua taarifa za mihamala na fedha kila siku na za kila mwezi jambo ambalo litawasaidia wafanyabiashara katika kutunza mahesabu. Uzinduzi wa mashine hizo ni sehemu ya mkakati wa FNB kuwa kiongozi katika huduma za benki na sehemu ya mpango wa benki hiyo kuchangia ukuaji wa uchumi kwa kuwawekea wafanyabiashara mazingira mazuri ya kuendesha shughuli zao. 

Arumasi alisema kuwa sambamba na uzinduzi huo, benki hiyo imepokea tuzo ya ufanisi wa kadi za fedha na malipo za VISA kwa mwaka 2016 baada ya kuwa imekidhi viwango vya ubora kimataifa na kuwa benki bora nchini katika utoaji wa huduma kupitia kadi hizo. Hii ni kutokana na huduma bora kwa wateja, ufanisi, na mfumo wa kuaminika katika kuendesha shughuli za kibenki. 

Programu ya tuzo za viwango vya ubora za VISA kimataifa ilianzishwa mwaka 1992 ili kutambua taasisi za kifedha dunia nzima zinazotoa huduma bora kwa watumiaji wa kadi za VISA kwenye maeneo mbalimbali. Kila mwaka tuzo hizo utolewa kwa taasisi hizo kutokana na kukidhi viwango vya ubora katika utendaji, ufanisi na mifumo madhubuti ya kudhibiti udanganyifu.

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WAGANGA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA MJINI DODOMA

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma
 Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya  uliofanyika kwenye Chuo Cha Mipango mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa mwaka wa Waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kwenye ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma .

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

RAIS AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA ARDHI,MAJI,NISHATI NA MAZINGIRA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiongoza kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 cha Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
ari2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 cha Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
ari3
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiongoza kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 cha Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
ari4
Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali katika Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
ari5
Baadhi ya Viongozi wa   Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
ari6
Baadhi ya Maafisa wa Idara mbali mbali katika  Wizara ya Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira wakiwa katika kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2017-2017 katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ikulu.] 17/10 /2016.

OMEGA MINISTRY CHURCH OF ALL NATIONS YAANDAA SEMINA YAKUOMBEA TAIFA

$
0
0
Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la Omega Ministry akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Semina ya kuliombea taifa leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mchungaji Samson Shango Donalds wa Kanisa la Ukombozi Missions Kanda ya Ziwa.
Mchungaji Samson Shango Donalds wa Kanisa la Ukombozi Missions Kanda ya Ziwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Semina ya kuliombea taifa leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Nabii Samson Rolinga wa Kanisa la Omega Ministry.

…………………………………………………………..

Lilian Lundo, MAELEZO.

KANISA la Omega Ministry of All Nations lenye makao yake Makuu Mbezi Afrikana, Jijini Dar es Salaam limeandaa Semina ya Injili ya Neno la Mungu la kuiombea Taifa na Viongozi wa Nchi, inayotarajiwa kufanyika Urafiki Nyangumi Jijini Dar es Salam Octoba 21 mpaka 23 mwaka huu.

Nabii Samson Rolinga ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu Semina hiyo yenye lengo la kuiombea Taifa, Viongozi wa Nchi na kuwafungua watu katika vifungo mbalimbali.

“TutaliombeaTaifa lirudi katika misingi ya Mungu, vile vile tutawaombea watu waliofungwa na nguvu za giza na magonjwa kama vile kanda, ukimwi na utasa,” alifafanua Nabii Rolinga.Amesema magonjwa yapo lakini pia yapo magonjwa ambayo yanatengenezwa na watu ilikumdhoofisha mtu, hivyo katika semina hiyo kutafanyika maombi ya kuombea magonjwa hayo pamoja na matatizo yote yanayotokonana roho za kurithi.

Vile vile amesema kuwa kumekuwa na matatizo mengi sana ambayo watu hawana majibu ya matatizo hayo mfano vijana wengi kutokuwa na kazi na kukata tama huku wakijraribu kupambana na matatizo hayo kwa njia ya mwili.Nabii Rolinga amesema kuwa lengo lake nikuonyesha chanzo cha matatizo na kuyatatua kwa njia ya maombi pamoja na kueleza namna ufalme wa giza unavyofanya kazi.

Kwa upande wake Nabii Donald kutoka Mwanza amesema kuwa atakuwepo katika semina hiyo ambayo itashughulikia matatizo ya Roho, kuvunja yanayoonekana katika ulimwengu wa Roho pamoja na kuombea nchi na Utawala wa nchi.

Aidha amesema kuwa watumishi wa Mungu wana jukumu kubwa la kuwaombea Viongozi wa Nchi na Rais ili Mungu awasimamie katika majukumu yao ya kila siku ya kuliongozaTaifa.

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI AMTEMBELEA PROFESA MUHONGO

$
0
0


Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akielezea fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nishati kwa Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke (kushoto).
Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke akielezea mikakati ya nchi yake katika kuisaidia Tanzania katika uboreshaji wa sekta ya nishati nchini.
Watendaji kutoka kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani).
Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke (kushoto) akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akibadilishana mawazo na Balozi wa

Uingereza Nchini, Sarah Cooke (kushoto) mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo ofisini kwake.



Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) na Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja.

………………………………………………………………

Na Greyson Mwase, Dar es Salaam

Balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke amemtembelea Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujadili namna Serikali ya Uingereza inavyoweza kufanya kazi na Tanzania kwenye uboreshaji wa sekta za Nishati na Madini.

Balozi Cooke alifanya mazungumzo na Profesa Muhongo pamoja na Watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA)

Akielezea kuhusu Sekta ya Nishati nchini, Profesa Muhongo alisema kuwa Serikali imeweka mikakati ya matumizi ya vyanzo vya nishati ya umeme kama vile gesi, maji, jotoardhi, makaa ya mawe, upepo, jua na kukaribisha wawekezaji kutoka Uingereza kushirikiana na Serikali kwenye uzalishaji na usambazaji wa umeme nchini hususan katika maeneo ya vijijini.

Aliongeza kuwa, Serikali imeanza kutumia gesi yake iliyogunduliwa kwa wingi kwa kiwango cha futi za ujazo trilioni 57.2 kwa kujenga bomba la gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es Salaam na kuendelea kusema kuwa Serikali imeweka mkakati wa kusambaza gesi mikoani pamoja na nyingine kuuzwa nje ya nchi.

“Kuna nchi zilizopo Ukanda wa Afrika Mashariki zimeomba bomba la gesi liende kwao; hii itatuwezesha sisi kufanya biashara pamoja nao na kuingiza fedha za kigeni,” alisema Profesa Muhongo

Aliongeza kuwa, mikakati mingine inayofanywa na Serikali ni pamoja na ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi kimiminika ( Liquefied Natural Gas Plant) na kiwanda cha mbolea katika eneo la Kilwa mkoani Lindi na kiwanda kingine cha mbolea katika mkoa wa Mtwara.

Alisisitiza kuwa, bado Serikali inaendelea na shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi katika maeneo mbalimbali nchini na kuomba kampuni za Uingereza zenye uzoefu kujitokeza na kuwekeza nchini.

Aidha, Profesa Muhongo alimwomba Balozi wa Uingereza kusaidia nchi ya Tanzania katika uendelezaji wa rasilimaliwatu kupitia nafasi za ufadhili zinazotolewa na ubalozi huo kwa ajili ya kusomea shahada ya uzamifu katika masuala ya sheria na uzimamizi katika sekta za gesi na mafuta.

Naye, balozi wa Uingereza Nchini, Sarah Cooke alisema serikali yake inaunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ya kufanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na kumhakikishia Waziri, kuwa atashawishi kampuni za Uingereza kuwekeza kwenye sekta za nishati na madini.

MASAUNI ATAKA IFUTWE G.N.U NDANI YA KATIBA YA Z'BAR.

$
0
0
Na Is-haka Omar, Zanzibar.

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wameshauriwa kuondosha mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) katika Katiba ya Zanzibar ya Mwaka mwaka 1984.

Ushauri huo umetolewa na Katibu  wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa Kamati Maalum ya NEC, CCM Zanzibar,  Hamad Yussuf Masauni katika Majumuisho ya ziara yake ya kuimarisha uhai wa Chama huko katika Ukumbi wa Amani Mkoa wa Mjini, Unguja.

Alisema huu ndio wakati mwafaka wa kuondosha mfumo huo kwani hauna tija katika maendeleo ya nchi badala yake ukiachwa itakuwa ni fursa kwa wapinzani kurudi tena katika serikali baada ya kufanyika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.

Alieleza kwamba nia ya CCM kukubali kuingia katika mfumo wa Serikali ya Umoja wa kitaifa (SUK) ni kushirikiana na vyama vya upinzani katika mipango ya maendeleo ya nchi pamoja na kumaliza siasa za chuki, hali ambayo CUF haikutaka kubadilika hivyo hakuna haja ya kubakisha mfumo huo katika Katiba ya Zanzibar.

Masauni aliwasihi Wawakilishi wa CCM kuhakikisha wanalinda kwa vitendo  maslahi ya Chama kwa kuandaa taratibu zote za kisheria kwa kufuta kipengele ndani ya Katiba kinachoeleza uwepo wa mfumo huo.

Alisema hatua ya mwisho itakuwa kurudi kwa wananchi kupiga kura ya maoni ya kukubali ama kukataa kuendelea na SUK, jambo ambalo kwa sasa ni rahisi kwani wananchi wengi hasa wafuasi wa CCM hawataki kuendelea na serikali hiyo.

“ Huu ni wakati mwafaka wa kuifuta CUF katika siasa za Zanzibar kwani hatuwezi kuendelea kuwa na ushirikiano na Chama kinachojali maslahi binafsi pamoja sera za utengano badala ya kuwaunganisha wananchi.

Hakuna haja ya kuendelea na SUK kwani katika miaka mitano ya mfumo huo wenzetu walionyesha udhaifu mkubwa na kupelekea nchi kuanza kuyumba kwani hata viongozi wao wa majimbo hawakufanya chochote kwa wananchi na mzigo wote waliwasukumia viongozi wa CCM.”, alisema Masauni na kuongeza kuwa serikali iliyopo sasa inaendelea kuwatumikia wananchi wote bila ya ubaguzi.

Aliwapongeza Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa juhudi zao za kufanya mabadiliko ya baadhi ya sheria ndani ya Katiba ya Zanzibar zilizokuwa zikiwajengea ngome ya kujiamini chama cha CUF katika Baraza hilo.

Akizungumzia Uchaguzi wa ndani ya CCM unaotarajiwa kufanyika mwaka 2017, Masauni alikemea tabia na vitendo vya kuendekeza siasa za makundi ndani ya CCM kwani  hali hiyo aliitaja kuwa  inasababisha kupatikana kwa viongozi wasiokuwa waadilifu ndani ya chama hicho.

Alisema baadhi ya viongozi wa CCM wanatakiwa kuwakataa watu watakaoingia ndani ya Chama hicho kuwania nafasi za uongozi kupitia nguvu za fedha na umaarufu kwani watu hao ndiyo chanzo cha kujengeka makundi yasiyokuwa na lazima ndani ya chama chetu.

“ Sote tunakumbuka athari mbaya ya makundi iliyojitokeza katika chaguzi zilizopita na kuendelea kutusumbua mpaka sasa kwani kuna baadhi ya wanachama waliweka mbele maslahi ya watu binafsi badala ya CCM.”, alifafanua Masauni.

Masauni ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, alieleza kwamba serikali haitovumilia kuona vitendo vya uhalifu vinaendelea katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar, na wanaofanya vitendo hivyo waache kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.

Aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kupunguza kesi za uhalifu unaotokea katika maeneo mbali mbali nchini kwani kuna baadhi ya wananchi wanakataa kutoa ushahidi kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu.

Mapema akizungumza Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini, Bora afya Silima Juma aliwapongeza baadhi ya viongozi wa Majimbo wanaotekeleza vizuri Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa wananchi.

Alisema tokea kumalizika kwa Uchaguzi wa Marudio hali ya kisiasa ndani ya Mkoa huo imeimarika kwani kila mwanachama na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakifanya kazi za kujitafutia kipato bila ya usumbufu.

Nao wanachama wa Chama hicho, waliahidi kutoa ushirikiano kwa mambo mbali mbali yatakayoiwezesha CCM kurudi madarakani katika uchaguzi Mkuu ujao.

Walipongeza juhudi zinazofanywa na Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kwa kutekeleza ahadi mbali mbali walizoahidi wananchi katika kampeni za Uchaguzi uliopita.

 Akizungumza Katibu wa Idara ya Siasa na Uhusiano wa kimataifa wa Kamati Maalum ya NEC, CCM Zanzibar,  Hamad Yussuf Masauni , na wafusi wa CCM katika mkutano wa majumuisho katika ziara yake aliyofanya Wilaya za Amani na Mjini Kichama Zanzibar.
Baadhi ya wafuasi wa CCM wakifuatilia kwa makini mkutano wa majukuisho ya Ziara ya Masauni uko katika ukumbi wa Mkoa wa Mjini kichama uliopo Amani Zanzibar.

DKT. CHARLES MWIJAGE AITAKA NBS KWA KUSHIRIKIANA NA WADAU WA MAENDELEO KUFANYA TAFITI YA VIWANDA VIDOGO NCHINI

$
0
0
Wazi wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akiwa ameshika vitabu mbalimnbali vya taarifa ya utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kushoto) akimkabidhi taarifa ya kitabu cha utafiti kuhusu matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 kwa Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia viwanda (UNIDO), Gerald Runyoro leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam


Baadhi ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.

Baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi mbalimbali nchini wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.



Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhelm Meru akizungumza wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (katikati) akifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa na wadau mbalimbali wakati uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage (kulia) akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Adelhelm Meru wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Charles Mwijage akizungumza na wadau mbalimbali wa maendeleo na Viongozi waandamizi wa Serikali wakati wa uzinduzi wa matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa Wandamizi wa Serikali kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwakilishwa wakati wa uzinduzi matokeo ya sensa ya uzalishaji viwandani ya mwaka 2013 leo Oktoba 17, 2016 Jijjini Dar es Salaam.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO)

……………………………………………………..

Na Beatrice Lyimo

MAELEZO-Dar es Salaam

SERIKALI imeitaka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushrikiana na wadau wa maendeleo nchini ikiwemo Shirika la Maendeleo ya Viwanda Duniani (UNIDO) na Shirikisho la Viwanda Nchini (CTI) kuendelea kufanya utafiti ili kubaini idadi na maendeleo ya viwanda vidogo vilivyopo nchini.

Hayo yamesemwa leo Jijini NA Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt Charles Mwijage wakati wa uzinduzi wa matokeo ya Sensa ya Uzalishaji bidhaa Viwandani mwaka 2013.

Dkt Mwijage alisema kuwa katika mataifa yanayoendelea duniani ikiwemo Korea Kusini, Malaysia na Singapore uchumi wa nchi hizo umeweza kukua kwa kiwango kwa juu zaidi kutokana na kuweka mkazo katika kuendeleza viwanda vidogo na vya kati.

Alisema katika kuharakisha kasi ya maendeleo ya vidogo yanapatikana nchini, Wizara yake imekusudia kuwajengea hamasa Watanzania kupendelea kujenga viwanda vidogo vidogo na vya kati, kwani kukua kwa sekta ya viwanda nchini kutaisaidia kuinua uchumi wan chi.

“Asilimia 25- 40 ya mazao ya kilimo yanayovunwa huharibika kabla ya kufikishwa kiwandani, katika kukabiliana na hali hiyo Serikali imekusudia kujenga viwanda vidogo vidogo ili kuwawezesha wakulima wapate sehemu nzuri zaidi za kuhifadhi mazao yao” alisema Mwijage.

Aidha, Dkt Mwijage alisema, sekta ya viwanda vidogo vidogo nchini imeendelea kukua kwa kasi nchini ambapo hadi sasa kuna jumla ya viwanda 3800 vilivyoanzishwa nchini kuanzia Novemba 2015 hadi octoba, 2016.

Katika hatua hiyo Dkt Mwijage alisema kuwa Wizara yake inaendelea kuhamasisha Sekta binafsi kuwekeza katika Sekta ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa ikiwa jukumu kuu la Serikali ni kuhakikisha nchi inakuwa salama na inajenga mazingira wezeshi kwenye sekta binafsi kuzalisha na kufanya biashara.

Naye Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt Albina Chuwa alisema kuwa matokeo hayo yanaonyesha mafanikio katika sekta ya viwanda ikiwemo kuongezeka kwa ajira zipatazo 264,223 nchini na kuchangia uchumi kwa takribani Shilingi bilioni 8.0 kwa mwaka 2013.

Alisema kuwa Takwimu za matokeo ya sense ya uzalishaji viwandani ni rasmi na kuwataka watunga sera, wanasiasa, viongozi, sekta binafsi na watu binafsi kutumia matokeo hayo kwa lengo la kuboresha Sekta ya viwanda nchini.

RAIS DKT MAGUFULI AUNGANISHA FAMILIA YA MAREHEMU DKT MASABURI,WANAFAMILIA NA WANANCHI WAFURAHIA

Waziri Mahiga akutana kwa mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa UN Ukanda wa Maziwa Makuu

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ukanda wa Maziwa Makuu, Mhe.Said Djinnit. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Oktoba, 2016 .
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Omary Mjenga (wa kwanza kushoto), Katibu wa Waziri, Bw. Gerald Mbwafu (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Ally Ubwa kwa pamoja wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Waziri Mahiga na Bw. Djinnit (hawapo pichani). 
Mkutano ukiendelea. 
Dkt. Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Bw.Djinnit mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images