Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1009 | 1010 | (Page 1011) | 1012 | 1013 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akisalimiana na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhanidisi Gerson Lwenge alipowasili katika Mamlaka hiyo kwa ajili ya uzinduzi wa bofi mpya ya MUWSA.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Mamlak ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) kwa ajili ya uznduzi wa bodi.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya Mamlaka hiyo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Moshi (MUWSA) Prof ,Faustine Bee akizingumza katika hafla hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya utamburisho wa wageni waliohudhuria hafla hiyo.
  Baadhi ya Viongozi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
  Mbunge wa jimbo la Moshi vijijini ,Anthony Komu akisalimia mara baada ya kutamburishwa katika hafla hiyo.
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya akisalimia mara baada ya kutamburishwa.
  Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro,Aisha Amour (katikati) akiwa na wakuu wa wilaya,kulia ni Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa wakiwa katia hafla hiyo.
  Baadhi ya viongozi wa Mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiki akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akitoa taarifa ya Mamlaka kwa mgeni rasmi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakurugenzi wa Mamlaka hiyo.
  Baadhi ya wageni waliohudhuria hafla hiyo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA) Sharry Raymond (MB) akizungumza wakati wa kuaga rasmi kwa niaba ya wajumbe wenzake wa bodi waliomaliza muda wake.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Moshi mjini ,Jafary Michael.katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa MUWSA,Prof ,Faustine Bee.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Mamlaa ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
  Waziri wa Maji na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Mhandisi Gerson Lwenge akionesha zawadi ya Tablet zilizotolewa kwa wajumbe wa bodi waliomaliza muda wake.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Tablet Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof Faaustine Bee.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru zawadi ya Tablet.
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael aliyekuwa mjumbe wa bodi ya MUWSA , zawadi ya Tablet.
   Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi ambaye pia ni mjumbe wa bodi hiyo,Hajira Mmambe zawadi ya Tablet.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala ya jinsia na wanawake (KWIECO) Bi Elizabeth Minde zawadi ya Tablet.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof Faustine Bee.
  Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Prof Faustine Bee akionesha vitendea kazi alivyokabidhiwa.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru vitendea kazi kama mjumbe wa Bodi ya mamlaka hiyo .
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro ,Aisha Amour vitendea kazi kama mjumbe mpya Bodi ya mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA).
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiwa na wajumbe wa bodi mpya ya Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) mara baada ya kuzinduliwa.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi iliyomaliza muda wake.ya Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) .
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiwa katika picha  ya pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) .
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akiwa katika picha  ya pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya Mamlaka ya majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) . 

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  WAJUMBE WA BODI MPYA YA MUWSA
  1. BIBI ELIZABETH MINDE
  2. ENG: ABDALLA MKUFUNZI
  3. BW: BONIFACE MARIKI
  4. BW: FILBERT KAHETA
  5. BIBI HAJIRA MMAMBE
  6. Mh. RAYMOND MBOYA
  7. Eng. AISHA AMOUR
  8. BW. MICHAEL MWANDEZI
  WAJUMBE WA BODI ILIYOMALIZA MUDA WAKE
  1. Mh. SHALLY RAYMOND (MB)
  2. Mh. JAPHARY MICHAEL (MB)
  3. Eng. ALFRED SHAYO
  4. BW. JESHI LUPEMBE

  0 0

  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa katika zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya Mama na mtoto,jimboni humo.
  Mbunge Ridhiwani akipimwa mapigo ya mojo kabla ya kutoa damu,upimaji wa mapigo ya moyo ni muhimu katika zoezi la utoaji damu.
  Mbunge Ridhiwani akipata maelekezo kutoka kwa wahudumu wa afya katika zoezi hilo la kuchangia damu.

  Mbunge Ridhiwani Kikwete wa katikati akiwa na Mwenyekiti wa CCM kata ya Chalinze wa kushoto Bwana Nassar Tamim na Mratibu wa zoezi hilo la uchangiaji damu Bwana Lazaro.
  Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akiwa na Diwani wa kata ya Pera wa kulia,na Mwenyekiti wa wakinamama Kata ya Pera Bi.Esther Laban  wakitembea kuangalia lambo la maji lililojaa matope.

  Viongozi hao wakiangalia Lambo hilo la maji.
  Mbunge wa Chalinze wa tatu toka kulia akisikiliza maelezo kutoka kwa viongozi hao hatua walizochukua baada ya lambo hilo kujaa matope.
  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akipokolewa na kinamama wa jamii ya wafugaji wa kabila la Kimaasai alipofika kuwatembelea na kuzungumza nao.
  Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akisikiliza mmoja wa kina mama aliyesimama kuzungumza kuhusu kero wanazopata katika shughuli zao za kifugaji .


  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha wafugaji aliyesimama akizungumzia athari zizokanazo na sheria namba 10 ya mwaka 2010 katika kikao na Mbunge wa jimbo la Chalize Ridhiwani Kikwete.

  Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete,ameshiriki katika zoezi la kuchangia damu linalotambulika ‘’Changia Damu Salama kwa Mama na Mtoto’’lilifanyika jimboni humo ili kusaidia upatikanaji wa damu salama.

  Akizungumza katika zoezi hilo Ridhiwani amesema kuwa amevutiwa na zoezi hilo na kuamua kujitolea kuchangia damu ili kumkomboa mama na mtoto.

  Katika tukio lingine Ridhiwani amekutana na kufanya  mazungumzo na wakinamama wa jamii ya wafugaji wa kabila la wa Maasai ili kuangalia ni namna gani atasaidia kutatua changamoto zinazowakabili wafugaji katika jimbo hilo.

  Aidha amepata nafasi ya kutembelea Lambo la maji lililojaa matope katika eneo la Pera ili kujionea hali halisi ya eneo hilo ili kusaidia kurudisha lambo hilo katika hali yake ya kawaida.

  0 0

  Serikali imewataka baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) walioshirikiana na wenzao wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitisha makontena zaidi ya 100 bila kukaguliwa na shirika hilo katika Bandari ya Dar es Salaam kujisalimisha haraka.

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw.Charles Mwijage alitoa agizo hilo mwishoni mwa juma wakati akizindua baraza la wafanyakazi wa Shirika hilo.“Nimeanza kukusanya orodha ya majina ya watu waliosaidia kupitisha makontena haya na nikija nayo hawatapona,” alisema.

  Aliwataka wote wanaojijua kuhusika kujisalimisha mapema na kutubu ili wasamehewe kabla haya hatua hiyo.Makontena hayo yalipitishwa katika bandari ya Dar es Salaam hivi karibuni bila ya kuthibitishwa na shirika hilo.

  Pia aliitaka TRA kuacha kutoa makontena bila ya shirika hilo kuthibitisha au kukagua ubora wa bidhaa zinazoingizwa hapa nchini sababu mwenye mamlaka hiyo ni TBS.

  Alisema watakaotubu kuwa walishiriki waseme walishiriki vipi na lini, walishirikiana na nani na wataje sehemu yalikopelekwa makontena hayo ili serikali iweze kusaidia kukomesha hali hiyo.Alisema anaamini kuwa waliofanya hivyo katika mamlaka hiyo walifanya kwa utashi wao bila ya ushiriki wa viongozi wao na kwamba sasa wakati umefika wa kukomesha tabia hiyo.

  Alilitaka baraza hilo kushirikiana na menejimenti na kuhakikisha matatizo yanayojitokeza yanapatiwa ufumbuzi kwa maslahi ya nchi na kwamba serikali itahakikisha inaongeza vitendea kazi na watumishi ili kufikia malengo ya shirika.

  Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Egid Mubofu, baraza hilo lina wajumbe 48 wanaotoka katika vitengo mbalimbali na litakaa kwa muda wa miaka mitano.“Baraza hili linaundwa kutokana na mkataba wa menejimenti na Chama cha Wafanyakazi (RAAWU),” alisema Dkt. Mubofu na kuongeza kuwa menejimenti itashirikiana na baraza kufanyakazi za shirika kwa tija.

  Alisema wafanyakazi wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na uadilifu katika majukumu yao ya kila siku.Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi (TBS), Prof. Mekanya Maboko alilitaka baraza hilo kufanya kazi kwa kushirikiana na menejimenti na bodi kuhakikisha shughuli za udhibiti wa ubora zinafanyika kwa ufanisi.

  “Bodi itaendelea kuisimamia menejimenti na kuishauri ifanye kazi kwa kuzingatia sera na sheria,” alisema.

  0 0

  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg Abdulrahman Kinana ameitumia salamu za rambirambi familia ya Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Iringa Mzee Tasili Mung’wenya Mgoda aliyefariki dunia jana tarehe 14 Oktoba, 2016 katika Hospitali ya Wilaya ya Mafinga.

  Mzee Mgoda amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya TANU baadae CCM na Serikalini ambapo amekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Mafinga, Katibu wa CCM ngazi ya Wilaya na Mkuu wa Wilaya Mstaafu.

  Katika Salamu hizo Ndg Kinana amesema amepokea kwa majonzi na masikitiko makubwa kifo cha Mzee Tasili Mgoda ambaye alikuwa ni sehemu ya hazina ya wazee wa CCM na kwamba anaungana na familia ya marehemu, ndugu na jamaa katika kipindi hiki kigumu cha huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao.

  WanaCCM tunamuomba Mwenyezi Mungu aiweke peponi roho ya Marehemu Mzee Tasili Mung’wenya Mgoda.  Amina

  Imetolewa na:-

  SELEMAN Y. MWENDA
  Kny: MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
  15/10/2016


  0 0  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mery Majaliwa wakimsalimia Bahati Omary kutoka kijiji cha Nangao Wilaya Liwale ambaye amejifungua mtoto wa kike katika Hospitali ya wilaya ya Nachingwea  Waziri mkuu alifika katika Hospitali hapo kujionea jinsi huduma za afya zinavyo tolewa kwa wagonjwa waziri mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Ruwangwa  Mkoani Lindi
  luw2
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na watumishi wa Hospitali ya Nachingwea pamoja na wananchi waliofika katika Hospitali ya nachingwea Waziri Mkuu alifanya ziara ya kutembelea hospitalini hapo kwa ajili yakuona na kusikiliza wagonjwa wanavyo pata huduma  
  luw3

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Liwale Sarah Chiwanga ambaye nimiongoni wa viongozi wa mkoa wa Lindi waliofika katika kiwanja cha ndege Nachingwea kumpokea Waziri mkuu na mkewe Mary Majaliwa na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ambao wamewasili katika Mkoa wa Lindi kwa ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Ruwangwa

  0 0

  Hussein Makame, NEC

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka vyombo vya habari kuialika tume hiyo iwapatie elimu ya mpiga kura ili kukuza uelewa wa vyombo hivyo juu ya sheria, kanuni, na taratibu zinazoongoza uchaguzi na kufahamu majukumu ya tume hiyo.

  Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati akieleza tathmini yake juu ya elimu ya mpiga kura inayotolewa na tume hiyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

  Alisema NEC imejipanga kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima na iko tayari kupokea maombi ya kwenda kutoa elimu hiyo kwa wamiliki wa vyombo vya habari, wahariri na wafanyakazi wote wa vyombo hivyo ili kukuza uelewa wa sekta hiyo.

  “Niwaombe vyombo vya habari, tumeanzisha programu ya elimu ya mpiga kura tualikeni kwenye vyombo vyenu vya habari, mtualike tuje tuzungumze na nyinyi vyombo vya habari kimoja baada ya kingine” alisema Bw. Kailima na kufafanua kuwa:

  “Sisi tunataka kuzungumza na wewe mmiliki wa chombo na watumishi wako na viongozi wenzako wote ili tukueleweshe kuhusu Sheria ya Taifa ya Uchaguzi na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, utaratibu mzima wa uchaguzi na uijue Tume ili unapoandika ujue ninachoandika si cha kubahatisha”

  Bw. Kailima alisema elimu hiyo kwa vyombo vya habari pia itaviwezesha kuwa na uelewa mpana juu ya masuala mbalimbali ya uchaguzi na kutoa changamoto kwa mtendaji huyo wa NEC pindi anapopata na nafasi ya kuzungumza nao.

  Katika kutekeleza mkakati endelevu wa kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima, Bw. Kailima ameanza kutoa elimu hiyo kupitia televisheni mbalimbali nchini na kwamba yuko tayari kuzungumza na vyombo mbalimbali kutekeleza mkakati huo.Kwa upande mwingine, Bw. Kailima amewataka Watanzania wakisikia kuna maonesho au mkutano ambapo Tume inashiriki wafike banda la NEC waulize maswali wapate ufahamu na watapata uelewa mkubwa juu ya mchakato wa uchaguzi.

  Akizungumza kwa nyakati tofauti, Bw. Kailima alisema NEC itahakikisha inatumia maonesho, mikutano na mikusanyiko mbalimbali ikiwemo mikutano ya kidini ili kutoa elimu ya mpiga kura ikiwemo shule za sekondari nchini.Alisema lengo kuu la kutekeleza hayo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 wananchi wawe wamepata uelewa wa kutoa kuhusu taratibu za uchaguzi na kufahamu majukumu ya Tume ili kupunguza malalamiko na upotoshaji unaofanywa katika kipindi cha uchaguzi.

  Tayari Bw. Kailima ameshatoa elimu ya mpiga kura kupitia televisheni za Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC) na Televisheni ya Afrika Mashariki (EATV) na amesema NEC inajipanga kutoa elimu hiyo kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.Alisema aidha NEC itatoa matangazo kwenye vyombo vya habari kuziomba Asasi za Kiraia zinazoweza kutoa elimu ya mpiga kura kutuma maombi ili kupatiwa ridhaa ya kutoa elimu hiyo kwa umma.

  0 0

  Na Emmanuel Matinde-Kigoma

  VIJANA wametakiwa kufuata mafundisho ya Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, juu ya uwajibikaji katika kazi,kuwa wazalendo, kudumisha amani na kuwa walinzi wa amani ya nchi yao.

  Mbunge wa Vijana kutoka Mkoa wa Kigoma, Mh.Zainabu Katimba, metoa wito huo juzi katika kijiji cha Katanga wilayani Kakonko, mkoani Kigoma, wakati akihitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani humo katika siku ya kumbukumbu ya miaka 17 tangu kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

  Alisema wakati wa uhai wake Mwalimu alihubiri uwajibikaji, uzalendo, amani na upendo na kupinga rushwa, hivyo vijana wana wajibu wa kuyazingatia yote hayo kwa manufaa ya taifa.“Tuendelee kufanya kazi ili kumuenzi mwalimu kama vile rais wetu Magufuli anavyofanya kwa vitendo,”alisea Mh.Zainabu.

  Kuhusu suala la amani Mh.Zainabu, ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Chipukizi Sekondari na vyuo vikuu, alisema vijana hasa waishio mpakani na nchi jirani wanalo jukumu kubwa la usalama wan chi yao kwa kushirikiana na vyombo vya usalama na kutoa taarifa pindi wanapoona watu wanaowatilia mashaka.

  Kauli ya mbunge huyo inakuja siku moja tu baada ya askari polisi wakishirikiana na askari wa jeshi la wananchi kuwaua majambazi wawili waliokuwa wanajiandaa kufanya uhalifu katika kijiji cha Muhange wilayani Kakonko baada ya kukabiliana nao kwa risasi.Nao baadhi ya vijana katika kijiji cha Katanga wakiwemo Nestory John na Honorata Petro, walieleza utayari wao katika kuhakikisha kwamba wanafichua mtu yeyote mwenye nia ya kuhatarisha usalama katika maeneo yao.

  Katika ziara yake Mh.Zainabu Katimba, alilenga kukutana na vijana, kusikiliza changamoto zao na kuhamasisha vijana kuanzisha na kujiunga katika vikundi vya ujasiriamali na yeye kuahidi kushirikiana nao ili kupata fedha za kuanzisha miradi ya ujasiriamali ikiwemo asilimia 5% ya fedha zitolewazo na halmashauri kwa ajili ya vijana.

  Vile vile alitoa kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajili ya kuwezesha usajili wa vikundi 18 vya vijana katika wilaya za Kigoma vijijini, Buhigwe, Kasulu, Kibondo na Kakonko.
  Mbunge wa Vijana kutoka Mkoa wa Kigoma, Mh.Zainabu Katimba.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makundi mbalimbali ya Wakazi wa Dodoma ambao shughulizao zinahusiana na mazingira kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Jengo la Hazina ndogo, Makulu mkoani Dodoma ambapo alisisitiza dhambi ya kuharibu mazingira haisameheki hivyo kuwataka kila mmoja awe mstari wa mbele katika kutunza mazingira.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makundi mbalimbali ya Wakazi wa Dodoma ambao shughulizao zinahusiana na mazingira kwenye mkutano uliofanyika ukumbi wa Jengo la Hazina ndogo, Makulu mkoani Dodoma.
   Vijana wa DOYODO ni sehemu ya makundi yaliohudhuria mkutano wa Makamu wa Rais mjini Dodoma.
   Wazee Mashuhuri wa mji wa Dodoma ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   Dampo la kisasa lililopo Chidaye ambalo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan alitembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa dampo hilo.
   Kaimu Mkuu wa Idara ya Mazingira na Taka ngumu wa Manispaa ya Dodoma Bw. Barnabas Faida (kushoto) akielezea utaratibu utakaotumika wa kutupa taka katika dampo la kisasa la Chidaye kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alitembelea na kujionea maendeleo ya ujenzi wa dampo hilo ambalo linatarajiwa kuanza kutumia mwezi novemba.
  Mhandisi wa Majengo Bi. Gladness Pesha akimuelezea Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan mgawanyo wa ofisi katika jengo la Mkuu wa mkoa wa Dodoma.
    Jengo la Ofisi ya Mkoa wa Dodoma lililopo eneo la Makulu ambalo lipo kwenye hatua za mwisho za kukamilika.

                                        .................................................................
  MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan, ametaja vigezo vinavyokwamisha Dodoma kuwa Jiji ikiwa ni pamoja na uharibifu wa mazingira na uzembe wa ukusanyaji mapato.

  Kauli hiyo aliitoa jana alipokuwa akizungumza na wazee, wafanyabiashara, vikundi vya usafi wa mazingira na viongozi mbalimbali wa serikali, mjini hapa.

  Alisema serikali inapohamia Dodoma lazima kuwe Jiji na ili kupata hadhi hiyo mambo mengi yanahitajika ikiwa ni pamoja na usafi wa mazingira.

  Samia alisema mkoa huo umeathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo kwa asilimia kubwa yamesababishwa na shughuli za kibinadamu kwa kukata miti ovyo na kuifanya Dodoma kubadilika tofauti na ilivyokuwa awali.

  “Wakati nakuja Dodoma mwaka 2002 kulikuwa na baridi sana nakumbuka wakati ule kwa nyumba za zamani ambayo hata ninayoishi kwasasa hazikuwa na kiyoyozi na feni zenyewe zilipachikwa tu hazitumiki maana hali ya hewa ya Dodoma haihitaji kiyoyozi lakini kwasasa joto lipo na baridi ipo ya msimu,”alisema Samia


  0 0

  Kila Baada ya Mwezi kikundi cha Tandale Youth Development Centre hufanya Jukwaa la Vijana ambapo vijana hukutana na kujadili mambo mbalimbali yanayohusiana na wao. Katika jukwaa la mwezi huu kulikuwa na mada inayosema: "Nafasi  ya mtoto wa kike katika jamii" ambapo majadiliano yalilenga zaidi kutambua nafasi hizo, changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike pamoja, namna ya kuzitatua na jinsi gani mtoto wa kike anavyoweza kusimamia malengo yake kufanikiwa.

  Aidha katika jukwaa hilo la vijana Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation  kupitia Mkurugenzi Mkazi wa hapa nchini, Martha Nghambi alitoa pia elimu ya nafasi ya mzazi katika kudumisha  amani ndani ya familia, ambapo alisema kuwa ili amani iweze kudumishwa na watu waishi bila kuwepo na mifarakano ni lazima kujenga mahusiano mazuri kuanzia chini yaani wanafamilia kuweza kuelewena kwa kuwahusisha wazazi na watoto ambapo hawa wakiishi vema basi hakutakuwa tena na uvunjifu wa amani na kusisitiza kuwa kila mtu analojukumu la kulinda amani.
  Mwendeshaji wa Jukwaa la Vijana lililofanyika Tandale leo Jamal Magabilo akitoa neno la utangulizi na kuwakaribisha wageni waalikwa wote katika jukwaa
  Mkurugenzi wa Gida Rahma Bendera akiitambulisha rasmi mada katika Jukwaa la vijana inayosema nafasi ya mtoto wa kike katika jamii
  Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Bi. Martha Nghambi akitoa Elimu kwa kina juu ya nafasi ya mzazi katika kudumisha amani kwenye familia ambapo aligusia mambo mengi ikiwa ni pamoja na visababishi vya uvunjishi wa amani pamoja na namna ya kuzuia uvunjifu huo wa amani katika familia.
  Mwandaaji wa Matukio wa TYDC Imani akitoa neno la shukurani kwa wote waliohudhulia jukwaa hilo
  Afisa Mahusiano wa TYDC Anna Emmanuel akielezea historia fupi ya umoja wao
  Mdahalo ukiwa umeanza
  Loveness Msuya akizungumzia mada inayohusu jinsi gani mtoto wa kike anaweza kusimama kwenye ndoto na malengo yake na mwisho wasiku kufanikiwa, alieleza njia na mbinu mbalimbali zinazoweza kumfikisha mtoto wa kike kule anapo pataka.
  Anna Mwalongo kutoka DUCE akisisitiza kwa nguvu na kupaza sauti ya kuwasihi Mabinti kujitambua ili waweze kuepukana na vishawishi mbalimbali vinavyo sababishwa na vijana.
   Ni Binti Mdogo mwenye umri wa miaka 12 na mwenye upeo mkubwa Zurpha Issa yeye alitaka kujua ni namna gani anaweza vipi kujizuia na mabadiriko yake? ambapo pia alieleza kuwa yeye anandoto ya kuwa msanii hapo baadae.
  Mkurugenzi Mkazi wa Global Peace Foundation Tanzania Bi. Martha Nghambi  akifuatilia kwa makini mdahalo huo
  Steven Mfuko Maarufu kwa Jina la Babu Zero akichangia mada katika mdahalo huo ambapo alizungumzia changamoto za mabinti kuvunja ungo wakiwa katika umri mdogo na kuelezea namna vijana wanavyo warubuni na kuwadanganya mabinti wadogo.
  Muongozaji Mdahalo huo wa Nafasi ya Mtoto wa Kike kwenye Jamii Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) Ndg. George David maarufu kwa  Ambassador Angelo(wa pili kulia) akiendelea kutoa mwongozo
  Bi. Mwafine Kimwaga mkazi wa Tandale akielezea namna alivyo mpokonya simu mwanae kwa kuhofia kuwa inaweza kuwa ni chanzo cha kumharibu kisha kumpa adhabu kali
  Bi Stella Francis Mganga akielezea jinsi mabadiliko makubwa ya Teknolojia yalivyo na yanavyo endelea kuporomosha maadili ya vijana wengi na kutumia muda wao mwingi huko kulipo kufanya maswala mengine.
  Mhandisi Eliwanjeria James  kutoka Kikundi cha Mainjinia wanawake Tanzania  akichangia mada katika jukwaa hilo
  Asha Furaha mkazi wa Tandale akieleza mambo mbalimbali yanayowakabili mabinti na kuwasihi kuendelea kupata elimu zaidi juu ya usichana wao
  Madam Sophie Mbeyela akitoa mchango wake wakati wa kujadili mada ya Nafasi ya Mtoto wa kike kwenye jamii
  Vijana, Wazazi na wadau mbalimbali wakiwa katika jukwaa hilo
   Picha ya Pamoja
  Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

  0 0


  Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo (aliyesimama), akiwasalimia wafungwa (hawapo pichani) wa gereza la Ukonga katika Tamasha la Kuadhimisha Siku ya Nyerere (Nyerere Day) Oktoba 14, Ijumaa iliyopita jijini Dar es Salaam.
  Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza Dkt. Juma Malewa akitia saini kitabu kitabu cha wageni gerezani Ukonga katika Tamasha la Michezo wakati wa kuadhimisha Nyerere Day. Kutoka kulia ni Mkuu wa Gereza la Ukonga Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP) Stephen Mwaisabila, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu, Thom Nyanduga, Mkurugenzi wa Global Publishers Eric Shigongo na Abdalah Mrisho ambay ni Meneja wa Global Publishers.Baadhi ya wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia kwa magunia katika tamasha hilo.Mmoja wa wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia na yai katika kijiko.Sehemu ya wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kukimbia mita 100.Wafungwa walioshiriki katika mchezo wa kuvuta kamba.Hapa ni mchezo wa kushikana mieleka.Eric Shigongo (wa pili kulia) aliyekuwa mgeni rasmi, akisalimiana na wachezaji wa soka wa timu ya Tailors kabla ya mchuano mkali ulioshuhudia timu ya Bush ikiishinda Tailors kwa penalti baada ya kutoka sare ya 2-2.Shigongo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Bush kabla ya mchuano wa soka.
  ...Viongozi meza kuu wakifurahia jambo.
  Sehemu ya zawadi zilizoletwa na Global Publishers.
  Baadhi ya viongozi wa Jeshi la Magereza na wageni mbalimbali wakishiriki chakula cha mchana pamoja na wafungwa (hawapo pichani).Baadhi ya wachezaji wa timu iliyoibuka mshindi (Bush) wakishangilia baada ya kupachika bao la kusawazisha katika dakika mbili za mwisho na kufanya mchezo kuwa 2-2.
  Nahodha wa timu iliyoshinda, Johnson Nguza (Papii Kocha) akibeba kombe kwa niaba ya timu yake (Bush) baada ya kulipokea kutoka kwa Eric Shigongo.

  Johnson Nguza aka Papii Kocha (wa pili kushoto) akitumbuiza na wanamuziki wa Twanga Pepeta wakati wa tamasha hilo.
  Timu ya Bush walioibuka washindi.


  Katika kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, Gereza Kuu Ukonga kwa kushirikiana na Kampuni ya Global Publishers limefanya tamasha la michezo mbalimbali kwa wafungwa wa gereza hilo.

  Akiongea katika tamasha hilo, Mkurugenzi wa Global Publishers aliyekuwa pia mgeni rasmi, Eric Shigongo, amewaambia wafungwa kuwa dhamra ya ujio wao gerezani hapo ni katika kuonyesha kuwathamini, kuwahurumia na kuwatia moyo kwamba kuwa kwao gerezani siyo kwamba wametengwa na dunia.

  Shigongo aliwatia moyo wafungwa hao kuwa hawatakiwi kukata tamaa na bado wanayo nafasi ya kubadilika na kuwa raia wema.“Kila mwanadamu anao wajibu wa kubadili maisha yake, Mwalimu Nyerere tunayemuadhimisha leo alizaliwa kama mimi na wewe na kutengeneza maisha yake na leo tunamkubuka, kwa nini wewe ushindwe?” aliuliza Shigongo.

  Aliongeza: “Najua wengi wenu mko hapa mkiwa mmeitwa majina mengi kwa kuwa mmehukumiwa, hizi ni hukumu za wanadamu, mnao uwezo wa kuandika kurasa mpya katika maisha yenu na siku mkitoka duniani waseme mtu mwema ameondoka. Siku moja inatosha kubadili maisha yako, kila siku andika ukurasa mpya wa maisha yako na Mungu atakuongoza."

  Wadau wengine walioungana na Global Publishers katika tukio hilo ni pamoja na Tume ya Haki za Binadamu nchini ikiongozwa na mwenyekiti wake Thom Nyanduga na Rajab Maranda (aliyewahi kuwa mfungwa gereza hilo la Ukonga) ambao kwa pamoja walileta zawadi mbalimbali kwa wafungwa hao vikiwemo vifaa kama sabuni, soda na kikombe ambacho kilitolewa kwa timu iliyofanya vizuri katika mpira wa miguu.

  Katika tamasha hilo wafungwa walishiriki michezo ya kukimbia katika magunia, kukimbia na yai katika kijiko, mbio za mita 100 vijana kwa wazee, mita 400 kupokezana vijiti, kuvuta kamba, mieleka, mpira wa miguu, mashairi, kuonesha vipaji vya uchekeshaji, kuimba kwa mtindo wa kufokafoka, ngoma za jadi na burudani kwa kushirikiana na baadhi ya wanamuziki wa bendi ya Twanga Pepeta.

  Picha zote na ASP Deodatus Kazinja wa Jeshi la Magereza.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiongozana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru wakati alipowasili katika chanzo cha maji cha Shiri kwa ajili ya zoezi la kuotesha miti ikiwa ni kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa ,Hayati Mwl Julius Nyerere.
  Wakuu wa wilaya za Hai na Moshi ,Gelasius Byakanwa (wa pili toka kulia) na Kippi Warioba (wa tatu toka kushoto waliungana na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro katika zoezi hilo.kulia ni Katibu tawala wa mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Aisha Amour.
  Eneo lilipo jirani na chanzo cha maji cha Shiri ambalo liliandaliwa kwa ajili ya kuoteshwa miti.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiki akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi la uoteshaji miti.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiotesha mti katika eneo la chanzo cha maji la Shiri Njoro lililopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa akiotesha mti katika eneo hilo.
  Katibu tawala mkoa wa Kilimanjaro,Aisha Amour akiotesha mti katika eneo hilo.
  Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kipi Warioba akiotesha mti katika eneo hilo zoezi ambali lilishirikisha watumishi wa idara mbalimbali za serikali na wafanyakazi wa Mamlaka ya Majsafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi(MUWSA).
  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) Joyce Msiru akiotesha mti katika eneo hilo.
  Baadhi ya watumishi wa idara za serikali wakishiriki katika zoezi hilo.
  Meneja Biashara wa MUWSA,John Ndetiko akiotesha mti katika eneo hilo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki akiongozana na viongozi wa wilaya pamoja na wananchi wengine kutembelea chanzo cha maji cha Shiri Njoro .
  Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa(kushoto) Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba (anayefuatia pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wakitizama eneo ambalo kunafanyika mgawanyo wa maji katika chanzo cha maji cha Shiri Njoro.
  Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba (kulia) akiwa pamoja na Mkuu wa wilaya ya Hai,Gelasius Byakanwa.
  Chanzo cha maji cha Shiri.
  Baadhi ya watumishi wa serikali wakitizama chanzo cha maji cha Shiri njoro.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Said Meck Sadiki akizungumza katika chanzo hicho.
  Meneja Biashara wa MUWSA ,John Ndetiko akizungumza katika chanzo hicho.
  Mkuu wa mkoa akijiadaa kuvuka katika eneo lenye maji katika chanzo hicho.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

  0 0


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI
                

   


   
                 

  Mkutano  wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika wapitisha Mkataba wa Afrika wa Usalama wa Usafiri Baharini na Maendeleo ya Afrika.

  Mkataba wa Afrika wa Usalama wa Usafiri Baharini na Maendeleo (The African Charter on Maritime Security, Safety and Development) umepitishwa katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi za Afrika (The AU Extraordinary Summit) uliofanyika tarehe 15 Oktoba, 2016 Lome, Togo. Kupitishwa kwa Mkataba huu kumefuatia makubaliano yaliyofikiwa katika Mikutano ya Kilele ya Wakuu wa Nchi za Afrika iliyofanyika Younde Juni, 2013 na Visiwa vya Shelisheli Februari,2015.

  Tanzania imewakilishwa katika Mkutano huo na Mhe. Balozi. Dkt. Augustine P. Mahiga (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye hakuweza kuhudhuria Mkutano huu kwa sababu ya Majukumu mengine ya Kitaifa.

  Akihutubia Mkutano huo Balozi Dkt. Mahiga alisema, Mkataba huo ni kati ya nyaraka muhimu zitakazoelimisha kuhusu kutunza amani ya Dunia, usalama na maendeleo katika karne hii ya 21. Alisisitiza kwamba Bara la Afrika liko kati ya bahari kuu mbili yaani Atlantic na Hindi ambazo ni kati ya bahari zilizo na shughuli nyingi sana za usafirishaji duniani. 

  Tanzania ikiwa katika nusu ya ukanda wa pwani ya Mashariki na pwani ya Magharibi ya Bahari ya Hindi yenye urefu wa Kilomita 1400, Mkataba huu ambao Balozi Mahiga ametia sahihi kwa niaba ya Tanzania ni muhimu sana hivyo amewasihi wanachama wengine kuhakikisha wanafanya hivyo.

  Sambamba na hilo Balozi Dkt. Mahiga amesema Mkataba huu si muhimu tu kwa Afrika kulinda bahari na rasilimali zake bali ni muhimu kwa dunia nzima. Balozi. Dkt. Mahiga ameomba Nchi zote na Mashirika ya Kimataifa kuunga mkono utekelezaji wa mkataba huu. Kufuatia kupitishwa kwa mkataba huu ameiomba Sekretariati ya Umoja wa Afrika kupeleka Mkataba huu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na katika Jumuiya ya Kimataifa ili kuweza kutambuliwa.

  Aidha, Balozi Mahiga amesisitiza kuwa bahari ni hadhina muhimu si tu ya samaki na gesi bali rasilimali nyinine za thamani kama vile madini ambazo zimekaa tu chini ya bahari hivyo ni jukumu la kila mwana Afrika kuhakikisha analinda rasilimali muhimu tulizo nazo zikiwemo hizi ambazo zinapatikana baharini.

  Akimalizia hotuba yake Balozi. Dkt. Mahiga alisisitiza “Hivi karibuni bahari hizi ( Atlantic na Hindi) zitakuwa chanzo muhimu cha nishati, hivyo kusaidia jitihada za  kuleta maendeleo kupitia rasilimali za bahari, naamini mkataba huu utakuwa ni silaha muhimu katika kulinda rasilimali hizi za bahari kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo”. Balozi. Dkt. Mahiga ameusihi Umoja wa Afrika na Wanachama wote kuendelea kuuboresha Mkataba huu na kupitisha viambasho muhimu na hatimaye kuharakisha kuuridhia Mkataba huu ili utekelezaji wake uanze bila kuchelewa.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
  Dar es Salaam, 16 Oktoba, 2016.

  0 0

  luw2
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na watumishi wa Hospitali ya Nachingwea pamoja na wananchi waliofika katika Hospitali ya nachingwea Waziri Mkuu alifanya ziara ya kutembelea hospitalini hapo kwa ajili yakuona na kusikiliza wagonjwa wanavyo pata huduma  

  WAZIRI MKUU AAGIZA MAPATO YA HOSPITALI YA NACHINGWEA  YAKUSANYWE KWA NJIA YA KIELEKTRONIKI

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, Bw. Bakari Mohammed kuhakikisha hospitali ya wilaya hiyo inakusanya mapato kwa kutumiamfumo wa kielektroniki.

  Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 16, 2016) wakati alipotembelea hospitali ya wilaya ya Nachingwea akiwa kwenye ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Lindi.

  Waziri Mkuu amesema Serikali ilishaagiza taasisi zote za umma kutumia mfumo wa kielektroniki katika ukusanyaji wa mapato kwa lengo la kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma.

  Amesema taasisi ambazo tayari ziameanza kutumia mfuko huo katika ukusanyaji wa mapato zimeweza kuongeza kiwango cha makusanyo kutoka sh. 300,000 hadi milioni nne kwa siku.

  Pia aliwaagiza viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ambao utawawezesha kupata huduma ya matibabu bure katika kipindi cha mwaka mzima.

  Akizungumzia kuhusu matibabu kwa wazee, Waziri Mkuu amemuagiza Bw. Mohammed kuhakikisha anafungua dirisha la kuwahudumia wazee ili kuwarahisishia upatikanaji wa huduma wanapofika hospitalini hapo.“Mkurugenzi hakikisha watendaji wako wa kata na vijiji wamebaini wazee wote katika maeneo yao na kuwatengenezea vitambulisho vitakavyowawezesha kupatibiwa bure,” amesema.

  Naye Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk. Samwel Laizer amesema muamko mdogo wa jamii kujiunga na CHF ni moja kati ya changamoto zinazowakabili katika utoaji wa huduma za afya.Dk. Laizer amasema kati ya kaya 30,000 zilizoko wilayani Nachingwea ni kaya 7,133 tu ndizo zilizojiunga na mfuko wa CHF.

  Awali Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa Chuo Cha Walimu na kuwataka wabadilike ili waweze kuwatumikia wananchi kwa uadilifu bila ya kujali itikadi zao za kidini na kisiasa.

  Amesema Serikali haitamvumilia mtumishi yeyote atakayeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuwatumikia wananchi. “Serikali haitaridhika kuona wananchi wakizagaa kwenye ofisi za halmashauri hiyo bila ya kusikilizwa,” amesema.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, OKTOBA 16, 2016

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Shule ya ST. Emmanuel High School, Ernest Masaka, akizungumza katika mahafali ya saba ya Kidato cha Nne yaliyofanyika Chamazi jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba, Diwani wa Kata ya Chamazi, Hemedi Karata  ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahali hayo, Katibu wa Diwani huyo na Lucy Peter, mke wa Mkurugenzi wa shule hiyo.
   Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba, akizungumza katika 
  mahafali hayo. Kutoka kulia ni Makamu Mkuu wa Shule, Ally Mkamba, Diwani wa Kata ya Chamazi, Hemedi Karata na Katibu wa Diwani.
   Taswira ya meza kuu kwenye mahafali hayo.
   Wahitimu wa kidato cha nne wakionesha vyeti vyao.
   Mahafali yakiendelea.
   Ndugu na Jamaa yake mhitimu Winfrida Komba wakiwa kwenye mahafali hayo.
   Walimu wa shule hiyo wakishiriki kwenye mahafali hayo.
   Wazazi na walezi wa wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
   Wahitimu hao wakionesha jinsi ya kujifunza somo la Sayansi.
   Wanafunzi wa shule hiyo wakipata burudani kupitia madirishani.
   Burudani zikiendelea kutolewa na wahitimu hao.
   Wageni waalikwa wakiwa kwenye sherehe hiyo.
   Katibu wa Diwani (kulia), akitoa vyeti kwa niaba ya diwani huyo.
   Mwanafunzi akikabidhiwa cheti na Katibu wa Diwani wa Kata ya Chamazi.
  Katibu wa Diwani wa Kata ya Chamazi, akimkabidhi cheti mhitimu, Winfrida Komba katika mahafali hayo. Kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba.

  Na Dotto Mwaibale

  WAHITIMU wa Kidato cha Nne mwaka 2016 katika Shule ya St. Emmanuel iliyopo Chamazi jijini Dar es Salaam wametakiwa kuzingatia elimu ili kutimiza ndoto za maisha yao badala ya kujihusisha na vitendo viovu na utoro.

  Mwito huo umetolewa na Diwani wa Kata ya Chamazi, Hemedi Karata wakati akiwahutubia wanafunzi hao kwenye  mahafali ya saba ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyofanyika Dar es Salaam jana.

  "Zingatieni masomo yenu ili mtimize ndoto za maisha yenu ya baadae, wazazi wenu wanawalipia ada ni vizuri mkawaonesha mafanikio yenu katika elimu na sio tabia mbaya," alisema Karata ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.

  Alisema kwa maisha ya leo bila ya kuwa na elimu kuna changamoto kubwa ya maisha hivyo aliwaasa wahitimu hao kufanya bidii ya kusoma hata watapokuwa kidato cha tano na sita na elimu ya juu.

  Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Ernest Masaka aliwaomba wazazi kushirikiana na uongozi wa shule katika kuwalea wanafunzi hao wawapo nyumbani na shuleni.

  "Ushirikiano baina ya wazazi, wanafunzi na walimu ni muhimu sana katika kuwajengea wanafunzi mazingira mazuri ya kupata elimu bora hivyo nawaombeni tuendelee kushirikiana," alisema Masaka.

  Mkuu wa shule hiyo, Khalid Simba alisema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kutokana na ushirikiano uliopo kati ya wazazi, walimu na wanafunzi wenyewe.

  Alisema licha ya shule hiyo kuwa na mafanikio, changamoto ndogo ndogo zinakuwepo lakini wanajitahidi kuzitatua kwa kushirikiana kwa pamoja na wazazi.

  0 0

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashali akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya kuhusiana na tukio la kuunasa mtandao wa wizi wa Bajaji na Pikipiki (BodaBoda) Mkoani Mbeya.(JamiiMojaBlog) 
  Mkutano wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya na Waandishi wa habari.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashali akionesha baadhi ya Bjajai na Pikipiki ziizokmatwa katika msako uliofanywa na jeshi hilo la POLISI Mbeya. 
  Askari Polisi wakiwa wamebeba moja ya bajaji iliyokamatwa mara baada ya Jeshi la Polisi Kufanya masako . 
  Bajaji zilizokamatwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kufanya msako. 
  JESHI la Polisi Mkoani Mbeya limefanikiwa kuunasa mtandao uliokuwa ukihusika na matukio mbalimbali ya wizi wa bajaji na Pikipiki (bodaboda) katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.

  Mtuhumiwa anayehusika na matukio hayo imefahamika kwa jina la Getruda Mwakyusa Mkazi wa Mtaa wa Manga Veta jijini hapa. Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari amesema jeshi la polisi limeendelea kufanya misako katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ili kudhibiti uhalifu . 

  Amesema Octobar 13 katika misako hiyo jeshi hilo la polisi lilifanikiwa kuunasa mtandao wa wizi wa bajajai na pikipiki ambapo mtuhumiwa wa matukio hayo alifanikiwa kutoroka ambapo nyumba yake mara baada ya kufanyiwa upekuzi zilikutwa pikipiki 3,bajaji 3,bodi 7 za bajaji . 

  Amesema kati ya mali hizo pikipiki mbili tayari zimekwisha tambuliwa na wamiliki wake kuwa ziliibiwa wilayani Chunya septemba25 mwaka huu katika kijiji cha Isenyela kata ya Mbugani. Aidha Kamanda wa Polisi Mkoani humo ametoa wito kwa jamii husasani vijana kuacha tabia ya kutaka mali kwa njia ya mkato badala yake wafanye kazi kihalali ili kijipatia kipato sanjali na kutumia fursa zilizopo ili kujitafutia ajira.

  0 0

   Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo (Kushoto) akiwa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dkt Mariam Malliwadh mara baada ya kuwasili katika kampuni ya New Habari Corparation
   Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo akisikiliza kelele hizo ambazo zimekuwa zikiwasumbua wafanyakazi wa kampuni hiyo
  Kelele ziosizo za kawaida huenda zikawasababishia wafanyakazi wa Kampuni ya New Habari Corparation matatizo ya kutesikia kutokana na kutokuwa na vifaa madhubuti vya kuzuia kelele hizo.

  Hayo yamebainika wakati wa Ziara ya ghafla iliyofanywa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Mhe John L. Kayombo ambapo miongoni mwa mambo yaliyobainika ni pamoja na kelele hizo zisizo za kawaida ambazo zinazotolewa na mtambo wa kutengeneza magazeti katika kampuni hiyo ambazo zinahatarisha uwezo wa wafanyakazi wa kusikia .

  Ziara ya Mkurugenzi Kayombo ya kutembelea katika kampuni hiyo imekukuja muda mfupi baada ya kusikia vilio vya wananchi na wafanyabiashara wanaoishi jirani na kiwanda hicho. Baadhi ya wananchi wanaofanya biashara jirani na eneo hilo wamesema kuwa kwa muda mrefu wametoa malalamiko yao lakini hayakufanyiwa kazi, hivyo kuamua kufikisha kwa kiongozi shupavu mwenye nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi Mh. John Kayombo.

  Baada ya malalamiko ya wananchi kumfikia ,bila kupepesa macho Mkurugenzi Kayombo akaenda New Habari House bila kutoa taarifa kwa uongozi wa kiwanda kwa nia ya kuona hali halisi.Akiwa kiwandani hapo Mkurugenzi Kayombo alikagua maeneo mbalimbali yanayozunguka kiwanda na hatimaye akafika kwenye mashine inayochapisha magazeti yanayotolewa na kampuni hiyo.

  Mashine hiyo ilikuwa inapiga kelele hali ambayo sio rahisi kwa binadamu kukaa eneo hilo lakini alikuta wafanyakazi wakiwa hapo tena bila kifaa chochote cha kuzuia au kupunguza sauti hizo.'' Hili jambo sio zuri haiwezekani mashine ipige kelele kiasi hiki huku wafanyakazi wakiendelea kuzalisha magazeti,huu ni ukatili na ni kwenda kinyume na haki za binadamu"alisema Kayombo.

  0 0


  0 0

   Mtoto Juma Ramadhan mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi ya Tabata Kimanga, akiwa amembeba mdogo wake Sara Sadiki wakati wakipita katika daraja la miti linalounganisha wakazi wa Tabata Kimanga na Tabata Chang'ombe Dar es Salaam , ambapo wakazi wa eneo hilo wanaiomba Manispaa ya Ilala iwajengee daraja la kudumu.
  Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Amani, Jonathan Mlay akimuonesha mwandishi wa mtandao huu, daraja la miti wanalolitumia lililojengwa kwa nguvu za wananchi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hiyo.


  Na Dotto Mwaibale

  WANANCHI wanaoishi mpakani mwa Tabata Kimanga na Chang'ombe katika Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wameomba kujengewa daraja ili waweze kutumia muda mfupi wa kufika katika maeneo hayo badala ya kupitia Tataba Mawenzi.

  Ombi hilo wamelitowa Dar es Salaam jana wakati wakizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com kuhusu changamoto mbalimbali zilizopo katika eneo hilo ikiwemo ya kujengewa daraja hilo lililopo Mtaa wa Amani.

  Akizungumzia changamoto ya daraja hilo, mkazi wa eneo hilo Tusekelege Ambonisye alisema wamekuwa wakitumia muda mwingi wa kuzunguka na gari kupitia Tabata Bima na kwenda Tabata Chang'ombe lakini kama daraja hilo linalounganisha maeneo hayo lingejengwa lingewarahisishia" alisema Ambonisye.

  Aliongeza kuwa adha kubwa waliyonayo ni pale ikinyesha mvua kwani maji yanajaa na barabara hiyo kushindwa kupitika ikiwa ni pamoja na kuhatarisha maisha ya watu wanaojaribu kupita kaika eneo hilo.

  Alisema kutokana na adha waliyokuwa wakiipata wananchi wa eneo hilo walikusanya nguvu na kujenga daraja la miti la muda ambalo linatumika lakini sio salama kwa watumiaji.

  Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo wa Amani, Jonathan Mlay alisema changamoto ya daraja hilo ni ya muda mrefu kwani waliwahi kuiwasilisha kwa wabunge wa jimbo hilo waliopita na wa sasa Bonah Kaluwa lakini bado halijapatiwa ufumbuzi wowote.

  "Kupitia vikao vyetu vya kamati ya maendeleo ya mtaa changamoto hii tuliipeleka kwa wabunge waliopita pamoja na huyu wa sasa tupo tunasubiri matokea yake" alisema Mlay.


  0 0

   Msaani chipukizi,Mussa  Mkumba a.k.a Dogo Jet akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka  vipaji vya waimbaji wa nyimbo za singeli katika viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.
   Msaani chipukizi,Idd Issa a.k.a Mauwezo akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka  vipaji vya waimbaji wa nyimbo za singeli katika viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.


  Mashabiki wakipagawishwa na wasanii waimbaji wa nyimbo za singeli katika  viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.

  Mashabiki wakipagawishwa na wasanii waimbaji wa nyimbo za singeli katika  viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

  0 0

   Msaani chipukizi,Mussa  Mkumba a.k.a Dogo Jet akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka  vipaji vya waimbaji wa nyimbo za singeli katika viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.
   Msaani chipukizi,Idd Issa a.k.a Mauwezo akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka  vipaji vya waimbaji wa nyimbo za singeli katika viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.


  Mashabiki wakipagawishwa na wasanii waimbaji wa nyimbo za singeli katika  viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.

  Mashabiki wakipagawishwa na wasanii waimbaji wa nyimbo za singeli katika  viwanja vya Kisemvule mkoani Pwani.
  Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

older | 1 | .... | 1009 | 1010 | (Page 1011) | 1012 | 1013 | .... | 1896 | newer