Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ASIKITISHWA NA MWEKEZAJI KUBADILI MATUMIZI YA KIWANDA NA KUKITELEKEZA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakiangalia kiwanda  cha ILULU kilichokuwa kinatengeneza mafuta ambacho muekezaji amekifanya kuwa Ghala nakukitelekeza na watu kuiba vifaa na kufanya uharibifu mkubwa Kiwanda hicho kipo wilaya ya Rungwe Mkoani Lindi Waziri Mkuu yupo katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Nachingwea na Rungwe Mkoani Lindi(Picha na Chris Mfinanga)
koro2
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia baadhi ya magari yalivyo haribika ambayo yalikuwa yanamilikiwa nakiwanda cha kukamua ufuta  ILULU kiwanda hicho kipo wilani Nachingwea Mkoani lindi ambapo mwekezaji aliye kichukua amebadili matumizi na kukifanya Ghala lakuhifadhia bidhaa kushoto kwa waziri mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi    picha na Chris Mfinanga.


DHIBITINI BIASHARA ZA MAGENDO-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi kuhakikisha anadhibiti wafanyabiashara wanaonunua korosho kwa njia ya magendo na atakayekamatwa achukuliwe hatua.

Pia amewataka wananchi wa mkoa huo kutouza korosho zao kwa walanguzi maarufu kangomba na badala yake wazipeleke kwenye masoko rasmi ili waweze kupata tija.

“biashara ya kangomba ni mwiko atakayekamatwa amebeba korosho za kangomba atachukuliwa hatua za kisheria na chombo chake cha usafiri kitataifishwa” amesema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Oktoba 17, 2016) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Ruangwa katika mikutano iliyofanyika kwenye vijiji vya Mibure, Namakuku, Ng’imbwa, Chienjele, Mkata, Mitope na Kitandi

“Marufuku kuuza korosho kwa kangomba kwani mnapata hasara kipimo kinachotumika si rasmi. Mkoa kamateni na taifisheni korosho na chombo cha usafiri kitakachotumika kubeba korosho za magendo,” amesema.

Amesema ni vema wakulima wakaachana na biashara ya kangomba kwa sababu haina tija na badala yake wasubiri na kwenda kuuza korosho zao katika minada kwa bei nzuri.

“Mwaka huu korosho itauzika kwa bei ya juu zaidi isiyopungua sh.3500, msikubali kuuza korosho mlizizitolea jasho kwa walanguzi wanaotumia kangomba kwa sh. 1000 huu ni wizi, kwani kile kipimo cha wanachotumia ni sawa na kilo mbili, hivyo unapoteza zaidi ya sh. 6000”. amesema

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu aliwasisitiza wananchi hao kuongeza idadi ya mazao ya biashara na kuanza kulima alizeti ambapo wataweza kupata faida ya zaidi ya sh. milioni moja kwenye shamba la ukubwa wa ekari moja.

Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi ametoa miezi miwili kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Bw. Andrea Chezue kuhakikisha ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Mibure unakamilika. “Ndani ya miezi miwili Zahanati iwe imekamilika, tuache kuzungumza sasa ni vitendo tu”amesema.

Awali Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha kukamua mafuta ya ufuta na karanga cha Ilulu kilichoko wilayani Nachingwea na kukuta kimetelekezwa. Ameagiza uongozi wa kiwanda kumpelekea nyaraka zote za umiliki. Kiwanda hicho kilibinafsishwa kwa marehemu Abbas Gulamali na sasa kinasimamiwa na familia yake.

“Nawahitaji Dodoma Oktoba 22 waje na nyaraka zao ili nijue walipokabidhiwa kiwanda hiki walitaka kufanya nini,” alimuagiza Msimamizi wa Kiwanda hicho Dinna Mavumbi kuwajulisha wahusika.

Waziri Mkuu alisema haiwezekani kiwanda hicho kilichojengwa kwa fedha za umma kikatelekezwa bila ya kuendelezwa. Alisema baada ya kupitia nyaraka zao ataangalia namna ya kurudisha majengo hayo ya kiwanda kwa Serikali. “Hatuwezi kuacha raslimali hii ikiwa imetelekezwa msituni inaharibika.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, OKTOBA 17, 2016

WATANZANIA WATAKIWA KUTUMIA MABARAZA YA ARDHI

$
0
0
Kaimu Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya, Bibi. Amina Rashid Ntibampemba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Mabaraza hayo leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mboza Lwandiko.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Mboza Lwandiko akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hali ya Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya wilaya leo Jijini Dar es Salaam.

………………………………………………………..

Na Georgina Misama – MAELEZO

Wizara ya Ardhi, Nyumba naMaendeleo ya Makazi imewataka watanzania kutumia Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya katika kutatua matatizo mbalimbali yanayohusu Nyumba na Makazi.

Hayo yamesemwa leo na Kaimu Msajili Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya Bi Amina Rashidi wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari Maelezo.“Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ndiyo chombo pekee kilichoundwa kwa ajili ya kutatua matatizo yote yanayohusu ardhi na nyumba” alisema Amina.

Akitaja baadhi ya mashauri yanayosikilizwa kwenye Mabaraza hayo Amina alisema mashauri yanayotokana na milki pandikizi (double allocation) au mashauri ya wananchi wanaopakana kwa mmoja wao kutaka kujipanulia eneo. Yapo pia mashauri ya wenye nyumba na wapangaji yanayofunguliwa kwa kukiukwa kwa mikataba.

Aidha, Amina alifafanua kwamba uendeshaji wa mashauri katika Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ni wakirafiki nasio unaofuata taratibu za Mahakama za kawaida. Wajumbe wa Baraza wanatoka miongoni mwa wanajamii wa eneo ambalo Baraza limeundwa.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi Bi. Mboza Lwandiko alitolea ufafanuzi wa dhamira ya wizara yake katika kuhakikisha inapambana na ongezeko la mashauri kwa kuunda Mabaraza mapya yapatayo 20 kila mwaka.

“Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Wizara itakamilisha taratibu za kuunda Mabaraza(44) kati ya Mabaraza mapya 47 yaliyoundwa na tangazo la serikali la mwezi Aprili, 2016” alisema Mboza.Tayari takribani mashauri elfu 43 yamesikilizwa kati ya mashauri elfu 59 yaliyofunguliwa kwa kipindi cha kuanzia Oktoba 2004 na Septemba 2016.

Mwenyekiti wa(RFB) nchini, Bw. Joseph Haule awasilisha ripoti ya ukaguzi ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478)

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB), Bw. Joseph Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni. Jijini Dar es Salaam.
uje2
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini Bw. Joseph Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni. Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Meneja wa Mfuko huo Bw. Eliud Nyauhenga.
uje3
Baadhi ya Watendaji wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB) wakimsiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Bw. Joseph Haule (hayupo pichani), wakati alipotoa ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni.Jijini Dar es Salaam.

LUKUVI ATOA HATI KWA WANANCHI WA MAKAZI HOLELA MOROGORO.

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi katika ziara yake ya mkoani Morogoro (17-10-2016) ameendelea kutekeleza program ya kurasimisha makazi holela kwa wananchi 116, ambapo amegawa hati 60 za awali na kumuagiza Afisa ardhi kuhakikisha anatoa hati zilizobakia ndani ya mwezi mmoja.

Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika mpango wake wa kuboresha maendeleo ya wananchi na makazi yao, imeanzisha program ya kurasimisha makazi holela kwa wananchi. Mpango huu ni wakupima, kupanga na kuwapatia hati wananchi waliojenga katika makazi yasio na mpangilio rasmi.

Akiwa mkoani morogoro Mhe. Waziri alitembelea baadhi ya makazi ya wananchi hao katika kata ya Bigwa na kujionea jinsi wananchi wanavyounga mkono juhudi za serikali katika kurasimisha makazi holela.Wananchi hao wa Bigwa kwa umoja wao walipima ardhi zao na kufuata utaratibu wa mipango miji kwa mujibu wa taratibu za serikali.

Aidha, Lukuvi alifanya ziara ya kushtukiza katika Masijara ya Ardhi ya Manispaa ya Morogoro, na kukuta idadi kubwa ya hati za wananchi zimekaa zaidi ya mwaka mzima bila ya kuwafikia wahusika. Alihoji juu ya suala hilo, na kutoa agizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa hati hizo kuwafikia walengwa ndani ya mwezi mmoja.

Baada ya ziara hiyo Mheshimiwa Waziri aliongea na wananchi wa Morogoro katika ofisi za Manispaa ya Morogoro na kusikiliza kero zao mbalimbali za ardhi na kuzitatua papohapo. Katika mazungumzo yake aliwataka wananchi waunge mkono juhudi za serikali kurasimisha makazi yao ili waweze kuishi katika makazi salama yanayotambulika na pia waweze kufaidika na ardhi yao kama kupata mikopo Benki au katika mambo mengine ya maendeleo yao.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimuhoji Afisa ardhi Manispaa ya Morogoro Bw. Abenance Kanomoga (wa kwanza kushoto), kwanini amekaa na hati za wananchi kwa zaidi ya mwaka mmoja bila kuwajulisha wahusika kuja kuzichukua.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akigawa hati kwa wakazi wa Bigwa mkoani Morogoro..

 Baadhi ya wananchi wa mkoani Morogoro wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.
1.       Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ajiongea na wananchi wa mkoani Morogoro.

BALOZI WA TANZANIA NCHINI KOMORO AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA KOMORO, MHE. AZZALI OUSMAN

$
0
0
Balozi Chabaka Kilumanga akipokea zawadi kutoka kwa Rais. Azzali Ousman
Kutoka Kushoto Rais Azali Ousman, Balozi wat Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka Kilimunga, Bw. Mudrick Soragha Mkuu wa Afisa Ubalozi na Bi. Sheehat Kassim Mkalimani .
Mhe. Chabaka Kilumanga Balozi wa Tanzania ndani ya Muungano wa Visiwa vya Komoro leo tarehe 17 Oktoba, 2016 alikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Col. Azzali Ousmani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Komoro katika Ikulu ya Bait Salam. Hii ni mara ya kwanza kwa Mhe. Rais Azzali kufanya mazungumzo na Balozi huyo kutoka Tanzania tangu kuingia kwake madarakani Tarehe 25 Mei, 2016. 

Katika mazungumzo yao Mhe. Chabaka Kilumanga alichukua fursa hiyo kumpongeza Rais Azzali kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuongoza Wanakomoro na kuelezea kuwa Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano wake kwa Komoro hasa kwa kuzingatia mahusiano yakaribu yaliyopo baina ya hizo mbili. 

Kwa upande wake Mhe. Azzali Ousmani, Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Visiwa vya Komoro alimshukuru Mhe. Balozi kwa ushirikiano ambao amekuwa akiupata kutoka kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Komoro na kueleza kuwa Komoro inajifunza mambo mengi kutoka kwa ndugu zao wa Tanzania. 

Aidha aliezea kuwa uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Komoro ni wa Kihistoria na ni matarajio yake kuwa uhasiano huo utaendelea kukuzwa na kudumishwa kwa manufaa ya nchi zote mbili. Wakati wakimaliza mazungumzo yao, Mhe. Azzali alieleza dhamira yake ya kutaka kufanya ziara nchini Tanzania na kwamba ni matarajio yake kuwa ziara hiyo itafanyika mapema iwezekanavyo.

BODI YA MFUKO WA BARABARA YASITISHA UFADHILI WA UJENZI WA BARABARA KWA MANISPAA YA KINONDONI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB), Bw. Joseph Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni. Jijini Dar es Salaam.
uje2
Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini Bw. Joseph Haule akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni. Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Kaimu Meneja wa Mfuko huo Bw. Eliud Nyauhenga.
uje3
Baadhi ya Watendaji wa Bodi ya Mfuko wa Barabara nchini (RFB) wakimsiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Bw. Joseph Haule (hayupo pichani), wakati alipotoa ripoti ya ukaguzi wa kiufundi kwa kazi ya Ujenzi wa barabara ya Masjid Quba (KM 2.478) kwa kiwango cha lami katika Manispaa ya Kinondoni.Jijini Dar es Salaam


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Bodi ya Mfuko wa Barabara umesitisha ufadhili miradi ya barabara kwa Manispaa ya Kinondoni baada kubainika kutengeneza barabara chini ya kiwango pamoja na ukiukaji sheria za manunuzi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Joseph Haule amesema kusitisha ufadhili kwa barabara kwa Manispaa ya Kinondoni kumetokana manispaa hiyo kujenga barabara chini ya kiwango ikiwemo Barabara ya Masjid-Quba iliyopo Sinza.

Haule amesema barabara barabara hiyo mkandarasi anafanya kazi huku Bodi ikiwa imetoa Sh.Bilioni 3.3 lakini Manispaa imemlipa Mkandarasi sh.milioni 200 ambapo ni kinyume na sheria ya manunuzi ya kulipwa sh.milioni 801 kwa mkupuo wa kwanza.

Amesema barabara hiyo ilitakiwa kuisha mwaka jana lakini bado wanaendelea kujenga ambapo ni kinyume cha mkataba na kuhoji kuwa mkandarasi huyo anaendelea kujenga kwa mkataba gani wakati muda wake wa ujenzi ulikuwa umeisha.

Bodi imeuagiza Katibu Mkuu wa Tamisemi kuwachukulia hatua wote waliohusika na mkataba wa barabara ya Masjid Kuba pamoja kubadili mfumo manispaa jinsi kuweza kufanya fedha ya serikali inayotengwa na Barabar inakuwa salama.

Aidha bodi hiyo imetaka Halmashauri zote kuhakikisha zinasimamia fedha za barabara ipasavyo na pamoja na barababaea kujengwa kwa ubora unaotakiwa..

YALIYOJIRI MAGAZETINI LEO October 18, 2016.

JE WAZIJUA FAIDA 10 ZA KULA MATANGO NA MATIKITI MAJI? SOMA HAPA UFAIDI ZAIDI

$
0
0

TIKITI MAJI
TANGO

Ulaji wa matango na matikiti maji husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa cha maji ambayo husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali ambazo miili yetu huzipata kupitia vyakula, madawa na hata vinywaji.

(1)Husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kutokana na kuwa na asili ya nyuzi nyuzi au, fibres, humfanya mlaji ajisikie kushiba bila ya kuongeza vitu mwilini ambavyo husababisha mtu aongezeke uzito hivyo kuzuia magonjwa mbalimbali.

(2)Hupunguza (hangovers),uchovu, mawengewenge pamoja na hali ya kujisikia vibaya kutokana na unywaji wa kilevi. Hii ni kutokana na kuwa na vitamini B na maji mengi ambapo, baada ya mtu kunywa kilevi na kisha akaja kula matango kabla ya kulala, itamfanya asubuhi asiamke huku akiwa na hangovers

(3)Husaidia katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya tumbo kama vile kuvimbiwa, tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo na mengineyo hupungua kutokana na ulaji wa matango, husaidia kuondoa sumu tumboni na kurahisisha ufyonzwaji wa protein mwilini kutokana na uwepo wa kiwezeshaji cha kibaiolojia kinachoitwa, erepsin enzyme.

(4)Husaidia kuondoa msongo wa mawazo kwani yana kiwango kikubwa cha vitamini B ambayo husaidia kuboresha utendaji kazi wa mishipa mbalimbali ya fahamu mwilini na hivyo kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo wa mawazo unaosababishwa na maisha ya kila siku.

(5)Husaidia kuondoa hatari ya mtu kupata kansa. Yana kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye asili ya mimea viitwavyo, lignans, ambavyo pamoja na vitamini c, 

(6)husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya mwili na hivyo kuepusha hatari ya mtu kupata kansa.

(7)Husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani. Kwa kukiweka kipande cha tango mdomoni kwa dakika kadhaa, huuwa bakteria mbalimbali wasababishao magonjwa mbalimbali ya kinywa na harufu mbaya mdomoni.

(8)Husaidia mtu kupata choo laini na huzuia kukosa choo.

(9)Huzuia kuganda kwa mafuta katika mishipa ya damu ili kuwezesha mzunguko sahihi wa damu kaitika pande zote za mwili sambamba na kurekebisha mapigo ya moyo
(10)Huwepo wa vitamini katika matunda haya husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini na presha.

WABUNGE VITI MAALUM MKOA WA PWANI WACHANGIA UJENZI WA DARAJA LA USIMBE -MAPARONI WILAYANI KIBITI

$
0
0
Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu wakikagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala wilaya mpya ya Kibiti.
...............................................................
Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu wamefanya Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala lililopo Wilaya Mpya ya Kibiti na kukabidhi kiasi cha milioni moja 1.000.000/= huku shilingi milioni Nne na elfu Hamsini zikiwa zimeingizwa kwenye akaunti na kufanya jumla ya fedha ya mchango walioutoa katika ujenzi wa daraja hilo kufikia shilingi Milioni Tano na Elfu Hamsini 5.050.000/=.

Msaada huu unafuatia Ahadi iliyotolewa na Wabunge hao wakati wa Kampeni katika kusaidia Wananchi wa Maeneo ya vijiji hivyo ambao kwa sasa wanatumia Daraja la Muda lililojengwa kwa miti na wananchi wenyewe ili kuwawezesha Kuvuka mto .Ni muda mrefu sasa hawana daraja ambapo kipindi cha mvua Maji hujaa na kuwapa shida wananchi hasa Kina Mama Wajawazito na Wanafunzi hushindwa Kuvuka na baadhi yao wamepoteza Maisha kwa kusombwa na maji kutokana na tatizo la kukosekana kwa Daraja hilo.

Bajeti ya Ujenzi wa Daraja hilo imefika Milioni Kumi ambapo wabunge hao wamewashukuru Wadau wote waliowaunga Mkono katika kutimiza Ahadi hii ya kusaidia Wananchi wa Vijiji takriban saba hususan Kina Mama Wajawazito na Wanafunzi ili kuvuka usalama wanapokwenda Kupata huduma mbalimbali zikiwemo Afya na Elimu nk.

Wabunge hao waliwaomba wadau mbalimbali walioahidi kuchangia ujenzi wa daraja hilo katika Kata Mbili za Maparoni na Msala na Wilaya ya Mafia kukamilisha ahadi zao mungu awajaalie wafanikiwe kupata chochote ili waweze kuchangia ili tuweze kukamilisha ujenzi huo ambapo bado unahitaji shilingi milioni 5.000.000 zingine ili kukamilisha bajeti ya ujenzi wa daraja hilo ambayo ni shilingi milioni kumi 10,000.000.

"Tunaamini mtakapo pata fursa Mtachangia Mwenyezi Mungu Awawezeshe Amiin" Alisema Mh. Subila Mgalu huku akimaliza kwa kuwashukuru Viongozi wa Chama, Jumuiya zake , Serikali Ngazi ya Wilaya na Kata kwa mashirikiano makubwa na mapokezi Mazuri .

Daraja litakapokamilika litasaidia Vijiji Saba Kipoka , Usimbe ,Maparoni ,Msala ,Twasalie ,Kihasi ,Kiechuru ,Kibanjo Kata Tatu na pia Njia hii inatumiwa Kufika mpaka Mafia. ambapo kwa sasa kumekuwa na athari yingi hasa kwa akina Mama wengi wajawazito wanashindwa kuvuka Maji yanapojaa na kupelekea kujifungua Njiani.
mgal02
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Khamis Mgalu akifurahia jambo wakati wa Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala
mgal2
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Khamis Mgalu wakionyeshwa vipimo vya daraja na wananchi wakati wa Ziara ya Kukagua Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala
mgal3
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu akiwa amekaa na wakina mama wakati wa ziara hiyo wilaya mpya ya Kibiti
mgal4
Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu na Subira Khamis Mgalu wakikabidhi fedha taslimu shilingi milioni moja kwa kwa ajili ya Ujenzi wa Daraja la Usimbe -Maparoni - Msala wilaya mpya ya Kibiti.
mgal8
Hali ya Vyombo vya Usafiri waliyoikuta wabunge hao wakati walipofanya ziara Mwaka Jana 3/10/2015 ambayo iliwagusa na kuwahamasisha kutafuta Michango ya ujenzi wa daraja hilo Daraja
mgal6
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Khamis Mgalu akizungumza na wananchi wakati wa ziara hiyo.
mgal7
Mbunge Viti Maalum Mkoa wa Pwani Zaynab Matitu Vullu akizungumza na wananchi wakati wa ziara hiyo.

SIKILIZA ALIYOYAZUNGUMZA RAIS DKT MAGUFULI WAKATI WA KUAGA MWILI WA MAREHEMU DKT MASABURI VIWANJA VYA KARIMJEE JANA

DC ILALA AGOMA KUPOKEA RIPOTI YA SOKO LA SAMAKI FERRY

$
0
0
Na Humphrey Shao,Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, amegoma kupokea ripoti ya soko la Samaki Ferry kutoka kwa Meneja wa soko hilo,baada ya kubainika ''MADUDU'' yaliyomo ndani ya ripoti hiyo.

DC Mjema aliamua kufanya hivyo mara baada ya kubaini kuwa makusanyo ya ushuru yaliyomo ndani ya ripoti hiyo ni ya udanganyifu na kwamba mifumo ya uendeshaji iliyopo ndani soko hilo ni dhaifu na haikidhi viwango vya ubora,jambo ambalo linaishushia hadhi soko hilo  ambalo ni maarufu katika  ukanda huu wa Afrika Mashariki na kusini mwa Jangwa la Sahara.

"Katika soko hili lazima mmfanye mpango mpya wa kuhakikisha mnaongeza makusanyo ya ushuru kutoka milioni tatu kwa siku na ziadi ili kuhimili huduma zinazohitajika kutolewa kwa wadau wa soko"amesema Mjema.

Mjema aliagiza kuwa ndani ya miezi mitatu lazima bodi na uongozi wa Soko hilo kuhakikisha wanajenga matundu ya vyoo Ishirini tofauti na sasa ambapo kuna matundu mawili tu, ambayo yanahudumia watu zaidi ya 4000 katika soko hilo.
Pia aliweka wazi kuwa bodi ya soko hilo ina mzigo mzito wa kuhakikisha soko hilo linarudi katika mstari kama lilivyo kabidhiwa na serikali ya Japan kwa Tanzania. 
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema akikagua sehemu ya soko akiwa ameambatana na Naibu Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala ,Sophia Mjema akiangalia moja ya Chemba ya maji taka ambayo haina mfuniko wakati kwenye ripoti inaonyesha kuwa chemba hizo zina mifuniko.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema, akizungumza na mmoja wa wachuuzi wa Samaki katika soko la Samaki Ferry.

Mrembo wa Dodoma Anna Nitwa awa miss Photogenic

$
0
0
Shindano dogo la kumtafuta mrembo mwanamitindo TOP MODEL limefanyika mkoani Arusha Jumamosi iliyopita huku mrembo wa Sinza Sia Pius kutoka Kanda ya Kinondoni akiibuka mshindi katika shindano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Triple A jijini Arusha.

Jumla ya warembo 30 walipanda jukwaani kuwania taji hilo ambalo ni la pili kushindaniwa kati ya Mataji 5 yanayo shindaniwa kabla ya shindano kubwa la Fainali za Miss Tanzania lililopangwa kufanyika jijini Mwanza tarehe 29 Oktoba 2016.

Washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wameingia kambini tangu tarehe 30 Septemba 2016 jijini D’salaam , na baadae kuanza ziara rasmi ya kutembelea mikoa ya Dodoma, Singida, Arusha na kumaliza ziara yao jijini Mwanza.

Wakiwa Makao Makuu ya Chama na Serikali mkoani Dodoma warembo hao 30 walishiriki katika shindano dogo la kumtafuta mrembo anaevutia katika picha. (Miss Photogenic) ambapo mrembo wa Dodoma Anna Nitwa aliibuka mshindi katika shindano hilo akifuatiwa na Sia Pius kutoka Kanda ya Kinondoni.

Washindi hao 2 Miss Photogenic Anna Nitwa na Top Model Sia Pius tayari wamejipatia tiketi ya kuingia katika hatua ya pili ya nusu Fainali (Top 15) huku mataji mengine 3 bado yanagombaniwa na washiriki hao 30

Mashindano hayo madogo yaliyobaki ni

Mrembo mwenye kipaji – Miss Talent

Mrembo mwanamichezo – Top sports woman

Mrembo chaguo la watu – Miss Personality

Mataji hayo madogo yote yatashindaniwa jijini Mwanza wiki hii kabla ya Fainali za Taifa zilizopangwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2016. Katika ukumbi wa Rock City Mall uliopo jijini Mwanza.

KAMA UNAWEZA KAMFUNGIE MUMEO-KHADIJA KOPA

NEWZ ALERT:Rais Magufuli atengua uteuzi wa DED Mkinga aitwaye Emmanuel Mkumbo

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga ajulikanae kwa jina la Emmanuel Mkumbo.

Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Emmanuel Mkumbo kuanzia leo tarehe 18 Oktoba, 2016.

Uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga atakayejaza nafasi ya Emmanuel Mkumbo utafanywa baadaye.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
18 Oktoba, 2016

Klabu ya Rotary ya Oyster Bay Yajenga Ukuta katika Shule ya Msingi Msasani A na Msasani B

$
0
0
Klabu ya Rotary ya Oyster Bay ya jijini Dar es Salaam imekabidhi rasmi ukuta uliojengwa na klabu hiyo katika Shule ya Msingi ya Msasani A na Msasani B. Ukuta huo umejengwa ili kuimarisha usalama kwa wanafunzi wa shule hizo pamoja na kulinda mali za shule. Kabla ya ujenzi wa ukuta huo, mazingira ya shule hizo yalikuwa hatarishi kwa wanafunzi kutokana na watu wasiohusika kupita katika eneo la shule bila udhibiti.

Ujenzi wa ukuta huo wenye thamani ya takribani Tshs Milioni 35 umewezeshwa na fedha zilizopatikana kutoka kwenye mojawapo ya shughuli za uchangishaji fedha zinazofanywa na klabu hiyo ambapo wadau mbalimbali walichangia ili kufanikisha zoezi hilo.

Ukuta huo ni muendelezo wa jitihada mbalimbali zinazofanywa na Klabu ya Rotary ya Oyster Bay katika kuboresha mazingira ya shule hiyo. Jitihada nyingine zilizofanyika ni pamoja na ujenzi wa maktaba mbili pamoja na kuweka vitabu vya aina mbalimbali, maji safi na salama ya kunywa, kambi ya siku moja ya huduma za bure za upimaji na matibabu ya magonjwa mbalimbali, mafunzo kwa walimu pamoja na upandaji wa miti.

Hafla hiyo fupi ilihudhuriwa na wanachama wa klabu ya Rotary ya Oyster Bay pamoja na viongozi wa ngazi ya juu wa Muunganiko wa Klabu za Rotary katika nchi za Tanzania na Uganda. Kiongozi Mkuu wa mkusanyiko wa klabu za Rotary Tanzania na Uganda, bwana Jayesh Asher alikuwa mgeni rasmi katika makabidhiano hayo na alipongeza juhudi za klabu ya Oyster Bay katika kusaidia shule hizo.


NEWZ ALERT: MAHAKAMA KUU KITENGO CHA ARDHI YATUPILIA MBALI KESI YA MBOWE HOTELS DHIDI YA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC)

$
0
0
UPDATES.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Mahakama kuu kitengo cha Ardhi imetupilia mbali kesi ya maombi ya kurejea katika jengo iliyokuwa ofisi ya Tanzania Daima pamoja na ukumbi wa Bilcanas.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, Sivangilwa Mwangezi ambaye amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa kuondoa vitu katika jengo hilo.

Amesema katika hukumu hiyo hakuna mtu aliyevunjiwa haki yake ya msingi kutokana na kufuatwa kwa Sheria dhidi ya madai ya Shirika la Nyumba NHC, kwa Mbowe HotelS.

Wakili wa upande wa NHC, Aliko Mwamnenge amesema kutokana na hukumu hiyo Mbowe hotelS wanadaiwa sh. Bilioni 1.7 na NHC.Amesema vitu haviwezi kurudishwa mpaka pale mlalamikiwa atakapolipa deni lake kwa NHC.

Nae Wakili upande Mbowe Hotel, John Malya amesema wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi.Amesema kuwa nakala wakiipata wanaweza kuamua katika kukata rufaa.

Wakili wa NHC, Aliko Mwamnenge akizungumza na waandishi habari baada ya kutoka katika hukumu ya kesi iliyokuwa ikihusu maombi ya Mbowe hotels kurejea katika ofisi zake,ambapo hukumu yake imetolewa leo katika  mahakama kuu kitengo cha Ardhi,jijini Dar.
 Wakili wa Mbowe Hotels, John Malya akizungumza na waandishi wa habari juu ya hukumu iliyotelewa na Mahakama kuhusiana na maombi ya kurejea Mbowe hotels na Mali zake,  katika mahakama kuu kitengo cha ardhi leo jijini Dar es salaam.
 Mawakili wakitoka mahakamani leo mara baada ya hukumu ya kesi hiyo kutolewa. picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi imefuta kesi iliyofunguliwa na Mbowe Hotels Ltd. dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ,kuwa Shirika hilo liliitoa kampuni hiyo katika jengo lake jijini Dar es salaam kwa kufuata taratibu zote na kuzishikilia mali zake kihalali.

Uamuzi huo umetolewa asubuhi hii na Jaji Sivangilwa Mwangesi, ambaye amesema madai ya Mbowe kwamba aliingia mkataba na NHC hayana mashiko na kwamba mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.

Mlalamikaji alikuwa wakidai kwamba wakati NHC inamtoa  kwenye nyumba alikuwa ndani ya Mkataba wa Ubia na NHC, lakini Jaji alikataa hilo na kusema ingawa Mkataba wa Ubia Ulikuwepo lakini kwa kuwa haukutekelezwa ipasavyo. 

Na wakati wa NHC kumtoa kwenye nyumba Walikuwa na Mahusiano ya Mwenye Nyumba na Mpangaji, Mahusiano ambayo yako wazi kisheria juu ya Utekelezaji wake.

Mawakili wa Mbowe Hotels Mhe. John Mallya na Mhe. Peter Kibatala (pichani ) wakiongea na waandishi wa habari mara tu baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kutoka, wakidai kwamba hawakuridhika na uamuzi wa kufutiliwa mbali kwa kesi ya mteja wao.

RAIS DK. SHEIN AZUNGUMZA NA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika  kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
eli2
Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali katika ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakiwa katika  kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,
eli3
Makamo Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Zanzibar SUZA Prof.Idrissa Rai (kulia) akiwa na Viongozi katika  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali katika  kikao cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
eli4
Viongozi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali wakiwa katika  kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
eli5

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi.Khadija Bakari Juma (kushoto) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika  kikao siku moja cha Mpango kazi wa mwaka 2016-2017   katika  utekelezaji wa  robo mwaka ya kwanza ya  Julai-Septemba 2016 kilichofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 18/10 /2016.

VIDEO:NAPE AKIWASILISHA MUSWADA WA HABARI KUIBADILI TAALUMA

MKE WA WAZIRI MKUU MARY MAJALIWA AMEIOMBA JAMII MASHIRIKA NA MAKAMPUNI KUWASAIDIA WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI HAPA NCHINI (ALBINO)

$
0
0
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa kwa niaba ya familia yake ametoa mchango wa fedha zaidi ya shilingi laki sita kwa Mama Hakika Swalehe kwa ajili ya kuwasidia watoto wake wenye ulemavu wa ngozi (ALBINO) Rashidi  Juma (5)na Iklamu Juma (miezi 9) Mama Majaliwa amehidi kuwasidia watoto hao vifaa vingine vya kutunza ngozi kwa ajili ya  Watoto hao wanaoishi katika kijiji cha Mtope wilaya ya Ruwangwa Mkoani Lindi  .Picha na Chris Mfinanga
niw5
Mama Majaliwa akimsalimia mtoto Iklamu Juma mweye ulemavu wa ngozi Kushoto ni Rashidi Juma (5)kaka wa Iklamu
niw4
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akiagana na  Mama Hakika Swalehemara baada ya kuzingumza naye

MBUNGE LEMA AZUA TAHARUKI UZINDUZI WA UJENZI WA HOSPITALI YA MAMA NA MTOTO JIJINI ARUSHA LEO.

$
0
0


VURUGU kubwa zimeibuka baina ya mkuu wa mkuu wa mkoa Arusha Mringo Gambo na mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayojengwa eneo ya buruka nje kidogo ya jiji la Arusha.

Vurugu hiyo zimeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho gambo kuvuruga ratiba iliyokuwa imepagwa na waandaaji wa hafla hiyo ambapo kwa mujibu wa ratiba iyo ilikuwa imepagwa kuwa hotuba ya mkuu wa mkoa ingetanguliwa na waandaji wa shughuli hiyo akiwemo waandaji wa hafla hiyo,wafadhili pamoja na mbunge Lema.

Kabla ya vurugu hizo mkuu wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexzanda Mnyeti swala ambalo liliibua mzozo mkubwa kwa wananchi walikuwa wamefika kushuudia tukio hilo la uzinduzi wakiwemo wafadhili waliofadhili mradi ambao ni shirika la kuhudumia afya ya mama na mtoto (maternity Afrika ).

Baada ya kuanza kuhutubia mkuu huyo wa mkoa akielezea historia ya mradi huo ikiwe upatikanaji wa eneo la kujenga mradi wa hospitali hiyo gafla mbunge lema alipo simama na kupinga hotuba hiyo hiyo na kudai imejaa upotoshwaji na siasa ndani kwani yeye ndie aliyetafuta eneo hilo la ujenzi wa hospitali hiyo kutoka katoka kampuni ya mawala Advocate na sio kweli eneo hilo limetokana na maono aliyokuwa nayo Marehemu Advocate Nyaga Mawala ya mda mrefu .
Picha ikionyesha wa kushoto mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anatulizwa na mchungaji Wilfred Mlayi ,Wa kwanza kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiwa anatulizwa na mfadhili wa Mradi huo ambaye ni daktari bigwa wa magonjwa ya kina mama na Mtoto Duniani Edru Broun
Wananchi waliohudhuria uzinduzi wa ujenzi wa hospitali ya mama na mtoto ambaye akupenda kutaja jina lake akiwa anamuomba mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema kutulia na kumuaacha mkuu wa mkoa aendelee kutoa hutuba.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images