Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AELEKEA MKOANI DODOMA KWA ZIARA YA SIKU TATU

$
0
0
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi wa Chalinze Mkoani Pwani leo Octoba 15,2016 alipokua njiani kuelekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu.
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wananchi wa MlandiziMkoa wq Pwani leo Octoba 15,2016 alipokua njiani kuelekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya  kikazi ya siku 3.
 
Baadhi ya Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akiwahutubia,maeneneo ya Mlandizi Mkoa wa Pwani leo Octoba 15,2016 alipokua njiani kuelekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya  kikazi ya siku 3

TAARIFA

Viongozi wa Umma watakiwa kuwa na maadili mema ili kumuenzi Mwali Julius Kambarage Nyerere

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mhe. Phillip Mangula akiwasilisha mada kuhusu Maadili ya Viongozi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki dunia.
kig4
Balozi mstaafu Ibrahim Kaduma akiwasilisha mada kuhusu Maadili ya Viongozi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki dunia.
kig5
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere wakifuatilia mada kutoka kwa wawasilishaji ambao ni Mhe. Phillip Mangula, Joseph Butiku, Ibrahim Kaduma na Dkt. Harun Kondo, mada zilizowasilisha ni pamoja na Miiko ya Uongozi, Azimio la Arusha na Maadili ya Viongozi.
kig1
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akimpongeza Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bara, Mhe. Phillip Mangula mara baada ya kuwasilisha mada kuhusu Maadili ya Viongozi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA).Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Profesa Shadrack Mwakalila, Mwenyekiti wa Kongamano hilo ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri msaafu Mhe. Anne Makinda.
kig2
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku akiwasilisha mada kuhusu Miiko ya Uongozi wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki dunia.

kig6
kig7
Mchumi Mwandamizi Profesa Ibrahim Lipumba akichangia mada wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki dunia.
kig8
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Stella Marios cha Mtwara Padre, Dkt. Charles Kitima  akichangia mada wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki dunia.
kig9
Watoa mada wakinukuu michango ya washiriki wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki dunia.Kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM – Bara, Mhe Phillip Mangula, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku, Balozi mstaafu Ibrahim Kaduma na Mwanasiasa Mkongwe Mhe. Wilson Mkama.
kig10
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere wakiangalia baadhi ya maandiko na machapisho aliyoandika Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere enzi za uhai wake yanayochapishwa na Mkuki na Nyota Publisher leo Jijini Dar es Salaam wakati wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA). Maadhimisho hayo yamefanyika ikiwa ni kumbukumbu za miaka 17 tangu Baba wa Taifa Mwl. Nyerere afariki dunia.
kig11
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stella Manyanya akiteta jambo na mmoja wa washiriki wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA).Naibu Waziri huyo ndiye alikuwa mgeni rasmi katika Kongamano hilo. Lililokuwa limebeba nukuu ya Mwalimu Nyerere isemayo “Viongozi ni lazima wawe mfano mzuri kwa wananchi kwa maisha yao na vitendo vyao pia”.
kig13
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Kongamano la Maadhimisho ya Kumbukizi za Mwalimu Julius Nyerere lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere(MNMA) akiagana na washiriki.

Picha na. Frank Shija, MAELEZO.

Video: Kagera All Star Ft Baghdad - Inaanza Na Wewe (Tetemeko Kagera)

Shule ya ATLAS yafanya Mahafali ya Darasa la Saba, Wazazi na Walezi Watakiwa kutowakatishaTamaa Watoto

$
0
0


Shule ya Atlas Madale iliyopo Jijini Dar es Salaam imefanya mahafali ya Darasa la saba, ambapo Mgeni rasmi kwenye mahafali hayo alikuwa ni ndugu Rogers Shemwelekwa, ambae ni Afisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni.



Mkuu wa Shule ya Atlas Madale Justus Kagya akizungumza katika Mahafali hayo ameeleza kuwa kila mwaka ifikapo Oktoba 14 shule hiyo imejiwekea utaratibu wa kufanya mahafali ili Kumuenzi baba wa Taifa Mwalimu JULIUS NYERERE.




Makamu mkuu upande wa Taaluma kwenye shule hiyo Joseph Mjingo amewataka Wazazi kuacha kuwakatisha tamaa Watoto, hususani kwenye Somo la Hesabu, ambalo limekuwa likionekana kuwa ni gumu tofauti na masomo mengine


Aidha Mahafali hayo yamehudhuriwa na Wazazi pamoja na walezi wa wanafunzi hao.

Afisa Elimu wa manispaa ya Kinondoni, Rogers Shemwelekwa akizungumza na Wahitimu wanaomaliza Darasa la Saba katika Shule ya Atlas madale iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shule ya Atlas madale, Justus Kagya akitoa nasaha zake kwa wahitimu wanaomaliza Darasa la Saba, wakati wa Mahafali yaliyofanyika kwenye Shule hiyo, ambapo Mgeni rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Afisa elimu wa Manispaa ya Kinondoni ndugu Rogers Shemwelekwa.
Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakipata maelezo ya kina kutoka kwa mkuu wa Shule ya Atlas madale, ndugu Justus Kagya wakati wa mahafali ya wahitimu wa Darasa la saba kwenye shule, ambayo pia yalihudhuriwa na wazazi na walezi wa wanafunzi hao.
Wazazi wa wanafunzi wanaohitimu elimu ya msingi katika Shule ya Atlas madale ya Jijini Da es Salaam wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kwenye Shughuli hiyo.
Baadhi ya Wahitimu wanaomaliza elimu ya msingi katika shule ya Atlas madale wakionesha nyuso za furaha, baada ya kusikia nasaha kutoka kwa Afisa elimu wa manispaa ya Kinondoni ndugu Rogers Shemwelekwa pamoja na mkuu wa shule hiyo ndugu Justus Kagya. 
Sehemu ya Wanafunzi wa Atlas madale waliohudhuria Mahafali ya wahitimu wa Darasa la Saba kwenye Shule hiyo.
Baadhi ya watumishi wa Shule ya Atlas Madale wakiwa wamepanda Jukwaani wakati wa mahafali ya Darasa la Saba kwenye shule hiyo, yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakiwemo Wazazi na walezi wa wanafunzi wanaohitimu elimu ya Msingi kwenye Shule ya Atlas madale, wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kupata chakula cha Mchana kilichoandaliwa maalum na uongozi wa shule hiyo.  

DAWASCO NA DAWASA SHIRIKIANENI KUONDOA KERO YA MAJI JIJINI DAR ES SALAAM-MHADISI MBOGO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba akizungumza katika uzinduzi wa Semina ya pamoja ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) Mkoani Pwani 
 Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA,Meja Jenerali Mstaafu Samwel Kitundu akizungumz machche kwenye uzinduzi wa Semina ya pamoja ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) Mkoani Pwani 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji,Mhandisi Mbogo Mfutakamba pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA,Meja Jenerali Mstaafu Samwel Kitundu wakiwa kwenye picha ya pamoja na DAWASCO na DAWASA Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji wakati amezindua Semina ya pamoja ya mafunzo kwa wafanyakazi wa Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO) pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASA) iliyofanyika mjini Bagamoyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Mbogo Mfutakamba amezitaka taasisi hizo kuongeza ushirikiano,haswa kwa wafanyakazi kwa kuwaandalia semina za mafunzo kwa pamoja ili waweze kufahamiana na kushirikiana kwa pamoja katika kuondoa kero ya Maji iliyopo jijini Dar es salaam.

“Mimi faraja yangu ni kuona DAWASCO na DAWASA mnashirikiana haswa wafanyakazi kwa kuwa kitu kimoja katika kutimiza majukumu yao, muone tatizo la Maji ni lenu wote ,naamini mkipendana na kuwa wamoja mtasaidia sana kuondoa kero ya Maji kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam” alisema Mfutakamba.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASCO na mjumbe wa bodi ya DAWASA Meja Jenerali Mstaafu Samwel Kitundu amemshukuru katibu mkuu kwa kufika na kuzindua semina hiyo na pia amewataka washiriki hao kutumia elimu watakayopata kutoa huduma bora kwa wananchi wanaowahudumia na kutatua kero ya Maji kwa jiji la Dar es salaam.

“Kwa niaba ya DAWASCO na DAWASA tunakushukuru katibu mkuu kwa kuweza kushiriki nasi kuzindua semina hii ya mafunzo kwa wafanyakazi wa taasisi hizi mbili tunaona upo pamoja nasi hivyo na mimi napenda kuwa sisitizia washiriki wa semina hii kutumia elimu na ujuzi watakaopata kuboresha huduma ya Maji kwa kuwa wabunifu kwenye maeneo yao ya kazi nakuondoa kero ya Maji kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na Mkoa wa pwani” alisema Kitundu.

Serikali yatangaza vigezo mikopo elimu ya juu 2016/2017

$
0
0
·          *Vitatumika kwa wanaonza masomo na wanaoendelea

Serikali imetangaza vigezo vitakavyotumika katika kupanga na kugawa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2016/2017 vitakavyotumika kwa wanafunzi wa mwaka wa kwaza na wale wanaoendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari jioni ya leo (Ijumaa, Oktoba 14, 2016) katika Ofisi za Bodi ya Mikopo (HESLB) zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya amesema vigezo hivyo vinazingatia mahitaji ya kitaifa, uhitaji wa waombaji na ufaulu katika kozi za kipaumbele.

“Kozi za kipaumbele ni kama fani za sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa kilimo, gesi na mafuta na nyinginezo,” amesema Naibu Waziri Manyanya.

Kwa mujibu wa Mhandisi Manyanya, fani hizi zinatokana na mahitaji ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Sera ya Elimu na Mafunzo ya 2014 ambazo zinasisitiza umuhimu wa kuzalisha watalaamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani hizo.

Naibu Waziri huyo ametaja vigezo vingine kuwa ni uhitaji wa waombaji hususani wale wenye mahitaji maalum kama wenye ulemavu na yatima.

Aidha, waombaji wenye ufaulu wa juu na wanachukua kozi za kipaumbele nao watafikiriwa, amesema Naibu Waziri Manyanya katika mkutano huo uliohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Maimuna Tarishi na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru.  

Kuhusu kutolewa kwa orodha ya waombaji waliofanikiwa kupata mikopo kwa 2016/2017, Naibu Waziri huyo amesema Bodi imekamilisha uchambuzi wa majina ya waombaji ambao wana sifa zilizoainishwa hapo juu na majina ya wanufaika wapya yatatangazwa leo tarehe 14 Oktoba, 2016.

Aidha, kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao (means tested) katika vipengele vyote vya mikopo.

DC Makete Atoa Maagizo Mazito kwa Walimu wanaotembea na Wanafunzi

$
0
0
Katika kuadhimisha miaka 17 ya kifo cha baba wa taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere, wanafunzi wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kusoma kwa bidii kwa kuwa taifa linawategemea ikiwemo kuja kushika nyadhifa mbalimbali baada ya kuhitimu masomo yao

Kauli hiyo imetolewa jana na Mgeni Rasmi katika maadhimisho ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa taifa mwalimu Julius Nyerere ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessi yaliyoadhimishwa kiwilaya katika shule ya Sekondari Lupalilo

Aidha Mkuu huyo ametoa Onyo kali kwa walimu wote wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi na kusema sheria zipo wazi kwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua, huku akiwataka wanaofanya hivyo kama wapo kuacha vitendo hivyo mara moja

Naye diwani wa kata ya Tandala Mh Egnatio Mtawa ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete akishukuru kwa hotuba ya mgeni rasmi amesisitiza maagizo hayo wahusika wayafanyie kazi ili kuepusha madahara yatakayoweza kujitokeza endapo maagizo hayo yatapuuzwa

Awali katika maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine wanafunzi wa shule ya sekondari Lupalilo wamepatiwa elimu ya Virusi vya Ukimwi na UKIMWI kazi iliyofanywa na Mratibu wa Ukimwi sekta zote Wilaya ya Makete Bi Ester Lamosai ambapo pamoja na mambo mengine amemueleza mgeni rasmi jinsi ambavyo shule nyingi hazipo salama kwa sasa

Na Edwin Moshi

Undergraduate scholarships

WANAUME WA KATOLIKI JIMBO LA DAR ES SALAAM WATEMBELEA MASISTA WA DADA WADOGO WA MTAKATIFU FRANSISKO MBAGALA

$
0
0

Waumini wa Kanisa Katoliki wakiandamana wakati wa kuanza ibada ya Masista wa Jimbo la Dar es Salaam wa Shirika la Dada Wadogo la Mbagala Misheni baada ya kutembelewa na Umoja wa Wanaume wa Kanisa Katoliki (Uwaka), Dar es Salaam leo asubuhi, ambao jukumu lao kubwa ni kuwalea watawa hao.
Monsinyori Padri Deogratius Mbiku . wa Parokia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) (katikati), akiongoza ibada ya misa takatifu. Kushoto ni Padri Msaidizi wa Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph, Edward Sabbas na kulia ni Katibu wa Jimbo hilo, Aidan Mubezi.
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo (kulia), akishiriki sakramenti takatifu wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya waumini wa kanisa hilo wakinunua mvinyo wa Arovela.
Waumini wakisali mbele ya msalaba nje ya kibanda maalumu cha msalaba wa Yesu.
waumini wakiwa kwenye ibada hiyo.
waumini wakitafakari katika ibada hiyo.
Makofi yakipigwa wakati maandamano yakiingia kabla ya kuanza kwa ibada hiyo.
Picha zikipigwa katika ibada hiyo.
Kwaya ya Mtakatifu Kizito ya Kanisa Katoliki Mbagala Kizuiani wakiimba katika ibada hiyo.

Ma padri mbalimbali waliohudhuria ibada hiyo.
Masista wa shirika hilo wakiwa kwenye ibada hiyo.
Ibada ikiendelea.
Waumini wa kanisa katoliki wakiwa katika ibada hiyo.


Kiongozi wa kwaya hiyo, Fednandi Constantino akifanya vitu vyake.
Ibada ikiendelea.
Monsinyori Mbiku akiongoza ibada hiyo.
Waumini wakipokea sakramenti ya Ekaristi Takatifu.
Kinanda kikipigwa.
waumini wakipiga picha za matukio mbalimbali.
Mapadri na watumishi wa kanisa wakitoka kwenye ibada hiyo.

Na Dotto Mwaibale

WATANZANIA wametakiwa kuacha tabia ya kuchagua kazi na kudharau kazi zingine kwani mbele za mungu kazi zote ni sawa na zinaheshimika.Hayo yameelezwa na Monsinyori Padri Deogratius Mbiku katika ibada takatifu ya kuombea Umoja wa Wanaume Katoliki (Uwaka) kuwasaidia kwa hali na mali masista wa Shirika la Dada Wadogo wanaoishi eneo la Mbagala Misheni jijini, Dares Salaam.

Akitoa mahubiri katika ibada hiyo, alisema binadamu anapenda kuchagua kazi huku akionya kuwa watu waache kudharau kazi yoyote inayofanywa na mwingine ilimradi iwe ya halali.“Tusidharau tufanye kazi na asiye fanya kazi hastahili kula. Hata familia yaYesu ililala njaa…hata ukilala njaa usidharau kazi,”alisema.Akimzungumzia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, PadriMbiku alisemaalikuwa mtu wa kwanza kuwaomba masista kuombea nchi ilipovamiwa na majeshi yaIdd Amin wa Uganda.

“Nyerere aliwashukuru sana watawa masista kwa kushinda vita ile dhidi ya Idd Amin. Tanzania haikuzoea vita.“Hivyo aliomba masista wasali sana. Tanzania ikashinda. Nyerere alisema waziwazi na washukuru masista kwa kushinda vita,” alisemaMbiku.Vita kati ya Tanzania na Uganda iliibukamwaka 1978 nakufikia tamati mwaka 1979 baadayamajeshi ya Amin kuchakazwa vibaya na Jeshi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ).Kutokana na umuhimu wa sala za masista hao, Padri Mbiku aliwaomba Uwaka kuhakikisha wanawasaidia masista kwani wanamchango mkubwa kwa taifa na kanisa.

“Masista wanajitoleakuombea kanisa na watu wote wapate wokovu pasipo kubagua dini zao. Sala yao nimuhimu, ina nguvu na Mungu anaisikiliza kwa kujitoa kwao,” alisema.Kwa msingi huoaliwaomba Uwaka ambao kaulimbiu yao “Nguzo Imara Hekalu la Bwana”

AFANDE SELE AIBUKIA MSAFARA WA MAKAMU WA RAIS MH SAMIA SULUHU HASSANI MKOANI MOROGORO LEO.

$
0
0
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi wa Morogoro mjini.kijiji cha Msamvu alipokua njiani akielekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu leo Octoba 15,2016
 Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Afande Sele akizungumza jambo mbele ya Makamu wa Raisi na wananchi,mara baada ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kusalimiana na wananchi wa Morogoro mjini kijiji cha Msamvu alipokua njiani akielekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu leo Octoba 15,2016. Pichani kulia ni MKuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen.
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi wa Morogoro katika kijiji cha Msamvu leo Octoba 15,2016. 
MKuu wa mkoa wa Morogoro, Dkt Kebwe Stephen akizungumza jambo na Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya atambulikae kwa jina la kisanii Afande Sele mapema leo mchana,Mara baada ya Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kusalimiana na wananchi wa Morogoro mjini kijiji cha Msamvu alipokua njiani akielekea Mkoani Dodoma kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu leo Octoba 15,2016.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKARIBISHA WAWEKEZAJI KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA VIWANDA HAPA NCHINI

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea shukurani kutoka kwa mwakilishi wa Shehe mkuu wa Bohara  kutoka Mumbai Shehe Badrul Jamali baada ya kufungua kongamano la uwekezaji lililo andaliwa na Jumuiya ya Dawoodi Bohora linalo elezea furusa za uwekezaji nchini Tanzania kushoto ni Waziri wa Viwanda  Biashara na Uwekezaji Chales Mwijage  Kongamano hilo lilihudhiriwa na Bohara zaidi ya mianne wasekta mbalimbali kutoka zaidi ya Nnchi 40 kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano  Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam
waw3
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mwakilishi wa Shehe  mkuu  wa Bohora kutoka Mumbai Shehe  Badrul Jamal katikati ni muandaaji wa kongamano la wafanya biashara wa Dhehebu la Dawood Bohora Bwana Mustafa Hassanali kongamano hilo lilikuwa likielezea furusa za uwekezaji zilizopo Tanzania

waw1
Waziri Mkuu Kassim  Majaliwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la uwekezaji lilo andaliwa na jumuiya ya Dowoodi Bohora lililo fanyika hapa nchini katika ukumbi wa mwalimu Nyere jijini Dar ess salam linalo lenga kutangaza fursa za uwekezaji Tanzania  kongamano hilo liliuhudhuriwa na wafanya biashara sekta mbali mbali kutoka zaidi ya nchi 40 duniani
Picha na Chris Mfinanga
KONGAMANO HILO LIMEFANYIKA MWISHONI MWAWIKI HII

SAFARI ZA NDEGE MPYA AINA YA BOMBADIER JIJINI ARUSHA KUINUA SEKTA YA UTALII NCHINI

$
0
0
Moja ya Ndege mpya ya serikali iliyokodishwa kwa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombadier  Dash 8 Q400 ikitua kwa mara ya kwanza katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha wakati maafisa wa Mamlaka ya Anga(TCAA) walipokua wakifanya ukaguzi kabla ya kuanza rasmi safari za kibiashara nchini.
Maafisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA)wakilakiwa katika uwanja mdogo wa ndege wa Arusha mara baada ya kuwasili kwa ajili ya kufanya ukaguzi kabla ya safari kwa ndege hizo kuanza.
Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ,Ibrahim Mussa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini(TANAPA)akizungumza na waandishi wa habari juu ya faida za utalii zitakazotokana na kukua usafiri wa anga nchini.
  Baadhi ya watumishi wa uwanja mdogo wa ndege wa Arusha wakifurahia ndege aina ya Bombadier baada ya kupata nafasi ya kuingia ndani ya ndege hiyo na kujionea mandhari yake.
  Mkuu wa kitengo cha usalama wa Shirika la ndege Tanzania (ATCL) ,John Chaggu akijiandaa kuingia ndani ya ndege kwa ajili ya kuendelea na ukaguzi katika viwanja vingine nchini ambavyo ndege hiyo itatoa huduma.
  Baadhi ya wananchi waliokua wakipita kando ya barabara walilazimika kuishudia ndege hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 

TAMASHA LA UTAMADUNI LA NAMASTEE TANZANIA LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa ufunguzi rasmi wa Tamasha la Utamaduni la India liitwalo Namastee Tanzania (Habari Tanzania) lililofanyika Oktoba 14,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
ia2
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwasha mshumaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Tamasha la Utamaduni la India liitwalo Namastee Tanzania (Habari Tanzania) lililofanyika Oktoba 14,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
ia3
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi akiwasha mshumaa kuashiria ufunguzi rasmi wa Tamasha la Utamaduni la India liitwalo Namastee Tanzania (Habari Tanzania) lililofanyika Oktoba 14,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
ia4
Baadhi ya vikundi vya Utaamduni wa kihindi vikitumbuiza katika uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni la India liitwalo Namastee Tanzania (Habari Tanzania) lililofanyika Oktoba 14,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.
ia5 ia6
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe. Ally Hassan Mwinyi (kulia)akimsikiliza Balozi wa India nchini Mhe. Sandeep Arya (katikati)  wakati wa onesho la uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni la India liitwalo Namastee Tanzania (Habari Tanzania) lililofanyika Oktoba 14,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam kulia ni  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye.
ia7
Wageni waalikwa wakifatila burudani mbalimbali wakati wa onesho la Tamasha la Utamaduni la India liitwalo Namastee Tanzania (Habari Tanzania) lililofanyika Oktoba 14,2016 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar es Salaam.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WHUSM

Asasi Ya Vijana Ya TYVA yawakutanisha vijana kujadili haki na wajibu wao katika Jamii

$
0
0
Meneja Mradi, Ushirikishwaji wa Vijana - TYVA, Alfred Kiwuyo  akiwaelezea washiriki dhima ya kongamano la vijana waliokutana kujadili haki na wajabu kwa vijana katika maendeleo ya Taifa. (Picha na Geofrey Adroph)

TYVA  ni asasi ya vijana ambayo imejikita na Kujipambanua kupigania jamii yenye haki na usawa, amani na misingi ya kidemokrasia na yenye ushiriki hai na wenye tija kwa vijana katika shughuli za maendeleo imeandaa kongamano hili kuwawezesha vijana kujadili Haki na Wajibu kwa Vijana na mstakabali wa Taifa kwa ujumla. Kongamano hili pia lilikuwa na dhima ya kupanua uelewa na umuhimu wa vijana kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendele ya Taifa kwa ujumla.
Wakili Chikulupi Kasaka, akitoa mada ya Haki na Wajibu wa Vijana kwa vijana mbalimbali wa vyoni na mtaani waliokuta kujadili haki na wajibu wao katika jamii iliyofanyika katika ukumbi wa British Council jijini Dar es salaam iliyoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA .

Mwenyekiti wa Bodi ya washauri ya Vijana(YAB) Femina Hip, Hassan Pukey akitoa mada kwa vijana waliofika katika kongamano lililoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA ili kujadili haki na wajibu wa vijana na katika jamii.

Makamu Mwenyekiti wa TYVA, Kamala Dickson akizungumzia mchakato wa baraza la vijana na jinsi vijana walivyoshirikishwa katika kutoa maoni ya mchakato mzima iliyoandaliwa na Taasisi la Vijana la TYVA na kufanyika katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam leo
Baadhi ya vijana wakichangia mada zilizokuwa zikihusu wajibu na haki kwa vijana 

Baadhi ya vijana waliofika katika kongamano la kujadili haki na wajibu wa vijana katika jamii
Victoria Charles  ambaye alikuwa ni Mwongozaji wa Mjadala wa Vijana akizungumza na waandshi wa habri leo katoka kongamano lililofanyika katika ukumbi wa British Council jijini Dar es Salaam
Zulekha Ibrahim kutoka Taasisi la Vijana la TYVA akizungumza jambo
Katibu Mtendaji wa TYVA Saddam Khalfan Ahmed akifunga kongamano la vijana lililowakutanisha vijana ili kujadili haki na wajibu wa vijana. Alisisitiza vijana watafute maarifa na taarifa za maendeleo. Aligusia pia umuhimu wa ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika sekta mbalimbali za maendeleo na vyombo vya maamuzi.
Picha ya Pamoja

DC NDEJEMBI ASIMAMISHA UCHIMBAJI MADINI KATIKA KIJIJI CHA SILWA KATA YA PANDAMBILI NA KUMUAGIZA MKURUGENZI KUMSIMAMISHA KAZI MTENDAJI WA KIJIJI CHA SILWA.

$
0
0
Leo (jana) baada ya shuguli ya kuadhimisha miaka 17 toka Mwalimu Nyerere afariki, DC Ndejembi na Mkurugenzi wa Halimashauri ya Wilaya ya Kongwa Ndg Izengo walifanya ziara ya kushtukiza katika Kijiji Cha Silwa kata ya Pandambili Baada ya kupata taarifa kuna uchimbaji wa madini aina ya KONISUPHIRE unaofanyika na wafanyabiashara bila kua na vibali vyovyote. 

Baada ya kufika eneo la tukio wakabaini mtendaji wa kijiji Ndg Michael Boniface Magenje alitoa eneo bila kutoa nakala kwenye Kata wala Halmashauri na hakuhusisha serikali ya kijiji. Hivyo DC akachukua hatua kusimamisha uchimbaji na kumuagiza Mkurugenzi kumsimamisha kazi mtendaji huyo mara moja kwa kutokufuata taratibu.

ATEMBEA SIKU 21 KWENDA DODOMA KUMFUATA WAZIRI MKUU ILI KUFIKISHA MALALAMIKO YAKE YA KUPORWA ARDHI.

$
0
0
Mkazi wa Kilindi, Tanga Angela Basso , aliyetembea kwa miguu kwa muda wa siku 21 pamoja na Watoto wake Janeth Peter (9) na Happy Peter (7) kuja Mkoani Dodoma kuonana na Waziri mkuu ili kupeleka malalamiko yake ya kudhulumiwa mashamba yake ya hekari 30 na kuchomewa nyumba .

MKAZI wa Kilindi mkoani Tanga, Angela Basso, akiwa na watoto wake wawili Happy(7) na Janeth Peter(9), amelazimika kutembea kwa mikuu kwa siku 21 hadi mkoani Dodoma kwa lengo la kumuona Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ili amsaidie kurudishiwa hekari 30 za mashamba yake aliyozoporwa.

Basso alifika mjini Dodoma akiwa na watoto wake hao, ambapo alisema aliona ni vyema kwenda Dodoma kuonana na Waziri Mkuu kutokana na kuporwa mashamba na kuchomewa nyumba yake katika kijiji cha Kwendigole wilayani Kilindi na wanaume wawili ambao waliojitokeza kwa nyakati tofauti wakidai ni maeneo yao.

Alisema alipita hatua zote zinazotakiwa kuomba mashamba, ambapo awali alipatiwa hekari 10 na kijiji na akazifanyia shughuli za kilimo na kujenga nyumba yake ya kuishi, lakini baada ya kwenda kujifungua alikuta mazao yamefyekwa na yeye kutakiwa kuondoka kwenye eneo hilo.

Mwanamke huyo alisema baada ya kunyang’anywa alifikisha malalamiko yake kuanzia uongozi wa kijiji hadi wilayani na baadaye akapatiwa eneo jingine la hekari 20, lakini alijitokeza mtu mwingine na kudai eneo hilo ni mali ya kanisa, licha ya kumiliki kihalali eneo la Hembekali.

“Nilikwenda kushtaki kwa serikali ya kijiji, kata na baadaye kwenda kwa mkuu wa wilaya ambako iliamuliwa nirudishiwe mashamba yangu, lakini hawakufanya hivyo mwisho wa siku nikafukuzwa kabisa kuishi kwenye eneo hilo,” alisema Basso

Mwanamke huyo alisema baada ya kutimuliwa alianza kuishi maisha yake kituo cha mabasi Muheza na baadaye alifukuzwa kituoni hapo kwa madai watu hawaruhusu kulala ama kuishi hapo na ndipo akaamua kuanza safari ya Dodoma baada ya kusikia Waziri Mkuu amehamia Dodoma.

Akisimulia machungu ya safari yake, Basso alisema akiwa njiani walikuwa wakila mahindi ya kukaanga na maji ya kunywa na kulala porini muda mwingine giza linapowakuta katikati ya pori.“Naomba kusaidiwa jamani nimeanza kufuatilia tangu mwaka 2012 lakini bila mafanikio jambo ambalo limechangia familia yake kusambaratika kutokana na kukosa pa kuishi huku watoto wangu hawa wakikosa elimu kwa kutangatanga,”alisema Mwanamke huyo

Basso aliomba Serikali itende haki ili yeye aweze kupata haki yake ya kurejeshewa mashamba yake na kurudi katika eneo hilo ili watoto wake wawili wapate nafasi ya kusoma. Mwanamke huyo alisema kwa sasa amekuwa kama mkimbizi kutokana na kukosa hana mahali pa kuishi huku mumewe naye akiikimbia familia yake baada ya kuporwa ardhi hiyo ambayo ilikuwa kama kitega uchumi chao.

WAZIRI WA ARDHI MH. WILLIAM LUKUVI AZINDUA RASMI KAMISHENI YA TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDHI LEO JIJINI DAR

$
0
0
Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi akizindua rasmi Kamisheni ya Tume ya Mipango na Matumizi ya Ardhi katika ukumbi wa Tume Jijini Dar es salaam leo.
Dr. Stephen Nindi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi ya Ardhi Tanzania akitoa utambulisho wakati wa uzinduzi wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi
Mwenyekiti wa Kamisheni Mstaafu Bw. Abubakar Rajabu akizungumzia hatua walizofikia wakati akiwa mwenyekiti mpaka walipofikia kabla ya kumaliza muda wake na kumpongeza hatua zinazoendelea kwa sasa katika Tume hiyo.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Moses Kusiluka akimkaribisha Mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi.
Mwenyekiti mpya wa Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi Bw. Fidelis Mutakyamilwa akitoa neno la Shukurani kwa Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi baada ya uzinduzi rasmi wa tume na kuleleza kuwa wanaanza kuyafanyia kutekeleza mara moja maelekezo waliyopewa na Mh. Lukuvi
Makamishna wateule, Pamoja na Menijimenti ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi wakiwa katika uzinduzi huo.
Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume pamoja na Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi
Mh. William Lukuvi (MB) , Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi,Mwenyekiti,Katibu pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo
Makamishna wateule Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi(aliyeketi katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi

Picha zote na Fredy Njeje/Blogs za Mikoa

 

WAZIRI MUHONGO AKAGUA NYUMBA ZILIZOATHIRIWA NA UPEPO MKALI ,MUSOMA MKOANI MARA

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter M. Muhongo akiongea na baadhi ya Wananchi ambao Nyumba zao ziliathirika na Upepo Mkali katika kijiji Cha Kiemba Kata ya Ifulifu. Taarifa zinaeleza kuwa mnamo tarehe 11/10/2016 majira ya saa 3 Usiku upepo mkali ukiandana na mvua uliezua nyumba zipatazo 44 na kusababisha madhara makubwa
 Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo ambaye pia ni Mbunge wa Musoma Vijijini akikagua baadhi ya nyumba zilizoathirika na upepo mkali katika kijiji cha Kiembe Kata ya Ifulifu Wilaya ya Musoma. Taarifa zinaeleza kuwa mnamo tarehe 11/10/2016 majira ya saa 3 usiku upepo mkali ukiandamana na mvua uliezua nyumba zipatazo 44.
Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter M. Muhongo na Mbunge wa Jimbo la Musoma vijijini akiwa amekaa kwenye moja ya nyumba akikagua baadhi ya Nyumba zilizoathirika na Upepo Mkali katika kijiji Cha Kiemba Kata ya Ifulifu Wilaya ya Musoma Mkoani Mara. 

Taarifa zinaeleza kuwa mnamo tarehe 11/10/2016 majira ya saa 3 Usiku upepo mkali ukiendana na mvua uliezua nyumba zipatazo 44. Nyumba Nyingi zilizoathirika ni zile za mgongo wa Tembo. Katika kukagua athari za uharibifu ilibainika myumba Tano ziliathirika vibaya kiasi cha kusababisha wamiliki wake kulala Nje.

Hata, hivyo ilielezwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Musoma na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kushirikiana na Viongozi wa Halmashauri walitembelea eneo hilo baada ya kupata taarifa za athari za kuezuliwa paa na kuahidi kuagiza tathmini ifanyike ili Serikali iweze kutoa masaada kwa Wananchi hao.

kuongea na Wananchi hao, Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo hilo la Musoma Vijijini aliiwaambia Wananchi hao kuwa Serikali ya Rais Magufuli ipo pamoja nao na ametumwa kuwapa pole kutoka kwa Viongozi wa juu wa Serikali. "Ndugu wananchi, nimetumwa na Rais wetu Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli niwape pole sana kwa kukutwa na kadhia hii ya kuenguliwa Nyumba Zenu na upepo, aidha, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu wanawapa pole pia na wanawatakia heri wale wote walioathirika"

Prof. Muhongo aliwaelekeza Viongozi wa kijiji hicho kuwa wahakikishe wanafanya tathmini ya kweli kwa kupita kila Nyumba iliyoathirika na yoyote atakaegundulika Amedanganya ili alipwe zoezi zima litaahirishwa na kurudiwa upya, pia wahusika watachukuliwa hatua za kinidhamu.

Aidha, aliwaahidi Wananchi hao kuanza kupewa misaada Baada ya kikao Cha Halmashauri kupitia taarifa ya tathmini jumatatu tarehe 17/10/2016 na kuwaelekeza Viongozi wa Halmashauri kufanya kazi hiyo kwa haraka.

Prof. Muhongo alikuwa Mkoani Mara kwa ziara ya kikazi ya kukagua umeme Sambamba na kushiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwalimu J. K. Nyerere iliyofanyika nyumbani kwake Butiama tarehe 14/10/2016

HABARI PICHA KWA HISANI YA ANNA NKINDA

VIJUSO VYA BAADHI YA NAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 16,2016

Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images