Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

TANZANIA YAONGOZA UKUAJI WA UCHUMI AFRIKA-MAJALIWA

$
0
0


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi saba Barani Afrika ambazo uchumi wake unakua kwa kasi zaidi hivyo amewakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza kwenye sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda.


Tanzania ni nchi ya pili kwa kasi ya ukuaji wa uchumi Barani Afrika ambapo uchumi wake unakuwa kwa asilimia 7 ikiongozwa na Ivory Coast inayokua kwa asilimia 8.5, Senegal  ya tatu (asilimia 6.6), D’jibout ya nne (asilimia 6.5), Rwanda ya tano (asilimia 6.3), Kenya ya sita (asilimia 6.0) na Msumbiji ya saba (asilimia 6.0).


Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamis, Oktoba 13, 2016) wakati akifungua kongamano la Jumuiya ya Dawoodi Bohora lililohusu fursa za uwekezaji.

Amewakaribisha wanajumuia hiyo kuja kuwekeza nchini. Kongamano hilo lilifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere.“Tanzania ina sera nzuri za kiuchumi ambazo zimesababisha uchumi wake kuendelea kuwa imara kwa zaidi ya miongo miwili  sasa.  Naikaribisha jumuiya ya Bohora kuja kuwekeza na kufanya biashara Tanzania,” alisema.



Waziri Mkuu alisema makampuni yatakayowekeza nchini yatafaidika na uwepo wa malighafi za kutosha, sera nzuri uwekezaji pamoja na uhakika wa usalama wa mali zitakazowekezwa nchini kwa sababu ya hali ya amani na utulivu iliyoko nchini.



Alisema licha ya Tanzania kuwa maeneo mazuri kwa ajili ya uwekezaji pia ina soko la uhakika kwa sababu ya kuwa mwanachama wa jumuiya mbili ambazo ni Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zenye watu takriban milioni 600.



“Tanzania ni kitovu cha biashara kwani inapakana na nchi nane ambazo  kati yake nchi sita zinatumia bandari ya Dar es Salaam kusafirisha mizigo yake. Mizigo hiyo husafirishwa kwa njia ya reli na barabara,” alisema.



Nchi zinazopakana na Tanzania ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC). Zinazotumia bandari ya Dar es Salaam ni Uganda, DRC, Rwanda, Burundi, Malawi na Zambia. 


Kwa upande wake Mratibu wa Kongamano hilo la kidini (Ashara Mubarak) lililowakutanisha Mabohora kutoka duniani kote  Bw. Murtaza Adamjee ameahidi kushirikiana na Serikali katika kutangaza fursa za uwekezaji zilizoko nchini.

Bw. Adamjee alimuhakikishia Waziri Mkuu kwamba Mabora dunia nzima wanakuja Tanzania kuwekeza katika sekta mbalimbali hususan ya viwanda. “Tutafikisha ujumbe kwa Mabohora dunia kote kwamba Tanzania ni sehemu salama ya kuja kuwekeza,”




IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

2 MTAA WA MAGOGONI,

S. L. P. 3021,

11410 - DAR ES SALAAM.

IJUMAA, OKTOBA 14, 2016. 

DKT. SHEIN ASISITIZA WANANCHI KUENDELEA KUPEWA ELIMU YA MPIGA KURA.

$
0
0

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuwasili uwanja wa sabasaba kutembelea mabanda ya maonesho ya Taasisi na Vikundi mbalimbali vya maendeleo ya vijana wakati wa maadhimisho ya Kilele cha Wiki ya vijana mkoani humo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kuhusu Elimu ya Mpiga Kura kutoka kwa Afisa Habari Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bi. Margareth Chambiri mara baada ya kutembelea banda la maonesho la Tume hiyo kwenye viwanja vya sabasaba wilayani Bariadi uemkoani Simiyu.

Baadhi ya Watumishi wa Tume ya Taifa ya Takwimu waliokuwa wakitoa Elimu ya Mpiga Kura wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana Mkoani Simiyu.






Na. Aron Msigwa –NEC, Bariadi-Simiyu.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa elimu ya mpiga kura inayoendelea kutolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika maeneo mbalimbali nchini ni vema ikawa endelevu kwa kuwa inaongeza uelewa na kukuza Demokrasia nchini.

Dkt. Shein ameyasema hayo leo mjini Bariadi mkoani Simiyu mara baada ya kutembelea banda la maonesho la Elimu ya Mpiga Kura la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakati wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Vijana na kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere mkoani Simiyu.

Amesema hatua ya NEC kuwa na programu endelevu za kuwapatia wananchi elimu ya mpiga katika maeneo yao ni muhimu katika kukuza Demokrasia na kuwafanya waelewe wajibu wao katika kudumisha amani na utulivu nchini kwa kupiga kura kwa uhuru kuwachagua viongozi wanaowataka.

“Hongereni sana, mnapotoa elimu hii mapema mnafanya kazi nzuri, hii inaongeza uelewa miongoni mwa wananchi na kuwafanya muwafikie wananchi wengi zaidi kabla ya uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020” Amesisitiza Dkt. Shein.

Kwa upande wake Afisa Habari Mwandamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Margareth Chambiri amemweleza Dkt. Shein kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeshiriki maadhimisho ya Wiki ya Vijana mkoani Simiyu ili kutoa Elimu kwa wananchi hususan vijana wa mkoa huo.

“NEC tumeshiriki maadhimisho haya ili kuwaeleza wananchi namna ambavyo chaguzi mbalimbali zinazofanyika nchini zinaendeshwa kwa uhuru na uwazi kabisa, katika kufanikisha jambo hili Idara mbalimbali zimeshiriki ikiwemo Idara ya Elimu ya Mpiga Kura, Idara ya TEHAMA, Idara ya Daftari la Wapiga Kura, Idara ya Uchaguzi na Idara ya Sheria” Ameeleza Bi. Margareth.

Amesema tangu kuanza kwa maonesho hayo Oktoba 8, mwaka huu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefanikiwa kutoa Elimu ya Mpiga kura kwa wananchi waliokuwa wakilitembelea banda la maonesho la NEC, kutoa elimu hiyo kupitia majukwaa ya wazi ya burudani pamoja na kutoa elimu ya mpiga kura kwa wanafunzi wapatao 2100 wa shule za Sekondari mkoani humo.

MAMA JANETH: MUENZINI MWALIMU NYERERE KWA KUWAHUDUMIA WAZEE.

$
0
0
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na Wazee katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro ambapo amezitaka Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa kadri iwekenavyo


Na Hassan Silayo-MAELEZO

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli amewataka watanzania kumuenzi kwa vitendo Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwahudumia Wazee nchini kwa kuwapatia mahitaji ya muhimu kwa ajili ya ustawi wa maisha yao.

Akiongea na Wazee katika Kambi ya kulea wazee ya Chazi iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro Mama Janeth amesema kuwa watanzania wanapaswa kutambua Wazee ni kundi muhimu kwa ustawi wa nchi kwani miongoni mwao walishiriki katika ukombozi wa taifa leo hivyo tuitumie Siku kama ya leo na nyingine kumuenzi Hayati mwalimu Julius Nyerere akiwa kama mzee aliyetangulia mbele za haki.

"Leo ni siku muhimu sana katika taifa letu siku ambayo tunaenzi siku aliyofariki muasisi awa Taifa letu Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, hivyo ni rai yangu kwa watanzania kwa ujumla kumuenzi kwa kushiriki kwa pamoja katika kuwahudumia wazee na kuwapatia mahitaji yao muhimu" Alisema Mama Janeth.

Aidha, Mama Janeth alisema kuwa amesikia changamoto zinazokabili Makazi hayo na ameahidi kuendelea kushirikiana na wadau kwa kadri iwezekanavyo ili kuhakikisha wanapunguza na kuondoa kabisa changamoto hizo iwe makazi ya wazee Chazi na yote nchini yawe sehemu salama ya kuwahudumia wazee.

Katika kutembelea kituo hicho Mamam Janeth Magufuli ametoa zawadi ya mchele, Maharagwe,unga na mafuta ya kupikia kwa ajili ya wazee na watu wasiojiwezakatika kituo hicho.

Akimkaribisha Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe amesema kuwa serikali ya mkoa wake inatekeleza kwa vitendo maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. john Pombe Magufuli ya kuwahudumia wazee na kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ndani mkoa wameshaanza kutatua baadhi ya kero na wataendelea kufanya hivyo ili kuyaimarisha makazi ya wazee mkoani humo.

Pia Dkt. Kebwe amewataka watu wote waliovamia makazi ya wazee kuondoka mara moja na kutafuta maeneo mengine na atakayekiuka agizo hilo serikali itamchukulia hatua kali za kisheria.

Akiwasilisha Risala ya Makazi ya Ya wazee ya Chazi kwa Mama Janeth Magufuli Kaimu Afisa Mfawidhi wa Makazi hayo Bw. Richard Kamwana amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa misaada aliyoitoa kwa wazee wa kituo hicho wakati wa sikukuu ya Eid.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Bw. Florent Kiombo amemuhakikishia Mama Janeth Magufuli wataendelea kushirikiana na taasisi nyingine katika kukiendeleza kituo hicho ikiwamo kuwapatia wazee wote kadi za CHF kwa ajili ya kuwasaidia wazee hao kupata huduma ya Afya popote waendapo.

Samaki mkubwa akutwa amekufa katika ufukwe wa bahari ya Kilwa masoko leo,ana urefu wa ft 30

$
0
0

 
 Baadhi ya Wananchi wakiwa juu ya mgongo wa huyo samaki mkubwa ambaye mpaka sasa hakufahamika jina lake mara moja
Sehemu ya mwili wa samaki huyo

MAKAMU WA RAIS AHANI MSIBA WA MASABURI LEO

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapa pole ndugu marehemu Dk. Didas Masaburi mapema leo Chanika,jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole Bw. Deogras Didas Masaburi (Ojambi) ambaye ni mtoto wa  Marehemu Dk. Didas Masaburi na Diwani wa  kata ya Chanika,jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Profesa Philemon Sarungi mara baada ya kukutana kwenye msiba wa Marehemu Dk. Didas Masaburi mapema leo Chanika,jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole na kumfariji Bi.Janeth Masaburi ambaye ni mke wa  Marehemu Dk. Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi wakimpa pole na kumfariji Bi.Janeth Masaburi ambaye ni mke wa  Marehemu Dk. Didas Masaburi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitia saini kwenye kitabu cha maombelezo cha marehemu Dk. Didas Masaburi  nyumbani kwa marehemu Tabata Segerea,jijini Dar es salaam. 
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

BONANZA LA MWALIMU NYERERE ARUSHA LAFANA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akizungumza kwenye Bonanza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jiji Arusha,kushoto ni Afisa Michezo wa Jiji,Benson Maneno na kulia ni Katibu Tawala wa wilaya(DAS)David Mwakiposa.

Katibu Tawala wilaya ya Arusha,David Mwakiposa akizungumza kwenye Bonanza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jiji Arusha,katikati ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro akifatilia kwa makini na kushoto ni Afisa Michezo wa Jiji,Benson Maneno .
Katibu Tawala wilaya ya Arusha,David Mwakiposa akiangalia michoro yenye sura ya hayati Mwalimu Nyerere ilichorwa na vijana wazalendo kwenye Bonanza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jiji Arusha.
Watoto wakichuana kukimbia mbio za mita 50 kwenye Bonanza hilo.
Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro(wa pili kushoto)akiwa na Mwenyekiti wa mchezo wa Karate mkoa wa Arusha,Richard Kitoro pamoja Sensei Dad na Sensei David wakifatilia michezo iliyokua ikiendelea.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Edmund Rice akionyesha umahiri wake kwenye mchezo wa Karate

Kikundi cha Karate kikonyesha mbinu za mchezo huo


Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa kushirikiana na wadau wa michezo pamoja na wananchi wa Jiji wameadhimisha siku ya Mwl. Nyerere kwa kuandaa na kushiriki kwenye Bonanza la Michezo lililopewa Jina la Bonaza la Mwalimu Nyerere lililofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini hapa leo tarehe 14.10.2016.

Tamasha hili limeandaliwa maalumu kwa ajili ya kumuenzi baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyenyere aliyefariki miaka kumi na saba iliyopita sambamba na kusherekea kilele cha Mwenge wa Uhuru ambao ulipita katika Wilaya ya Arusha mwishoni mwa mwezi wa nane na kuzindua miradi ya Afya, Maji, Elimu, Uwezeshaji wananchi, uwezeshaji makundi maalumu, Ujenzi na Usafi wa Mazingira yenye thamani ya zaidi ya TshBil 1.5.

Akiongea na wanamichezo walioshiriki katika Bonanza hilo Mkuu wa Wilaya ya Arusa Mhe. Gabriel Fabian Daqarro alisema Tamasha hili ni kwa ajili ya kumuezi Mwl. Nyenyere ambapo litasaidia vijana na wananchi kuweka miili yao safi, kujiepusha na maradhi pamoja na makundi yanayoweza kusababisha kujiingiza kwenye madawa ya kulevya, ulevi na uzururaji.

Pia tuitumie siku hii kutafakari mafundisho na maelekezo ya Mwalimu Nyerere aliyoyatoa wakati wa uhai wake, wapi Nchi imetoka, Misingi imara ya Uongozi bora na namna gani tunaweza kuenenda ili kuleta maendeleo katika Taifa letu, na vijana kama nyie ndio mnaotakiwa kuwa chachu katika kupambana na umasikini katika Nchi yetu alisema Dc Daqarro.

Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Arusha Bw. David Mwakiposa alielezea Tamasha hilo kuwa limeshirikisha michezo mbalimbali kama Netball, Football, Volleyball, Basketball, mchezo wa Bao, kukimbiza kuku, Baiskel, kuvuta kamba, Karate, Taekondo, Uchoraji pamoja na riadha.

Bonaza hili pia limetumika kama jukwaa la kuendelea kuelimisha na kueneza ujumbe kwa vijana kupitia kauli mbiu ya Mwenge mwaka 2016 inayosema “Vijana ni nguvu kazi ya Taifa washirikishwe na wawezeshwe”.

Nteghenjwa Hosseah
Afisa Habari, Halmashauri ya Jiji
Arusha

14.10.2016.

BARABARA YA DODOMA-MAYAMAYA KUKAMILIKA NOVEMBA

$
0
0
Muonekano wa Barabara wa Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 ikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake. Barabara hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Novemba Mwaka huu.
Meneja Mradi wa Barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 Eng. Yusuf Karera, akitoa maelezo ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kushoto), alipokagua ujenzi wake, Mkoani Dodoma.
Muonekano wa tabaka la kwanza la Barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 ambayo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akiweka mchanga katika tabaka la kwanza la ujenzi wa barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 alipokagua mkoani Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akielekezwa namna ya kushindilia mchanga katika barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa KM 43.65 mkoani Dodoma.

…………………………………………………………..

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Ujenzi ya Sinohydro Corporation anayejenga barabara ya Dodoma-Mayamaya yenye urefu wa kilometa 43.65 kukamilisha ujenzi huo ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kukagua barabara hiyo mkoani Dodoma na kuridhishwa na ujenzi wake Prof. Mbarawa amesema kuwa barabara hiyo ni muhimu kwani ni kiungo kikuu kwa watu wanaosafiri kati ya mkoa wa Dodoma, Manyara, Arusha na nchi za Ukanda wa Kusini mwa Afrika.

“Kamilisheni kipande hiki kilichobaki haraka kwani barabara hii ni kiunganishi cha nchi za Kaskazini na Kusini mwa bara la Afrika hivyo kukamilika kwake kutasaidia kufungua fursa za kibiashara na kukuza uchumi wa nchi”, amesema Waziri Mbarawa. 

Amemtaka mkandarasi huyo kuzingatia viwango bora vya ujenzi wa barabara kama ilivyosainiwa kwenye mkataba na kuhakikisha thamani ya fedha katika ujenzi huo unaonekana.

Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Mkoa wa Dodoma Eng. Leonard Chimagu amemhakishia Waziri huyo kusimamia barabara hiyo kwa mujibu wa sheria za barabara ikiwemo kuzuia wananchi wasivamie miundombinu ya barabara na kuzuia mifugo kuswagwa kwenye barabara.

“Nahakikisha nitasimamia sheria za barabara, kwani mradi huu ni mkubwa na Serikali imetumia gharama kubwa katika ujenzi wake, hivyo ni lazima niutunze ili kudumu muda mrefu”, amefafanua Eng. Chimagu.

Barabara ya Dodoma – Mayamaya ni sehemu ya mradi mzima wa barabara ya Dodoma – Babati yenye urefu wa kilometa 188.15 na umegharimu shilingi bilioni 40.

WAZIRI MKUU APOKEA MSAADA WA SH. MILIONI 27.62

$
0
0
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akisalimiana na Ahmed Olotu(Mzee Chilo) mara baada ya kupokea shilingi laki sita na ishirini kutoka kwa Mtandao wa wasanii(SHIWATA) ikiwa ni msaada wa kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.Wengine pichani ni Mkurugenzi Idara ya uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Gen.Mbazi Msuya na Caasim Taalib(wa tano kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa mtandao wa wasanii.

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na wafanyabiashara ndogondogo solo la kariakoo mara baada ya kupokea msaada wa nguo mchanganyiko,midoli na kanzu wenye thamani ya shilingi milioni 2 ikiwa ni msaada wa kusaidia waathirika wa tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.

……………………………………………………………….

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea fedha taslimu sh. milioni 25.62 pamoja na nguo zenye thamani ya sh. milioni mbili kutoka kwa wadau mbalimbali.

Makabidhiano ya michango hiyo yamefanyika leo (Ijumaa, Oktoba 14, 2016) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Akiwashukuru wadau hao Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.

“Nawashukuru kwa kuamua kutumia siku ya leo ya kukumbuku ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere kuwachangia wenzetu waliopatwa na maafa,” amesema.

Waziri Mkuu amesema michango hiyo ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo baina ya Watanzania.

Misaada hiyo imetolewa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) sh. milioni 20, Mtandao wa Wasanii Tanzania sh. 620,000 na nguo mifuko miwili, Chama cha Makatibu Mahsusi (TAPSEA) sh. milioni tano.

Wengine ni Umoja wa Wafanyabiashara Ndogondogo soko la Kariakoo ambao wametoa marobota mawili ya nguo (suruali, kanzu na nguo za akinamama na moja la wanasesere kwa ajili ya watoto waliopatwa na maafa vyote vikiwa na thamani ya sh. milioni mbili.

Fedha na nguo hizo vimetolewa kwa ajili ya wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.

Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali .

MAMA JANETH: MUENZINI MWALIMU NYERERE KWA KUWAHUDUMIA WAZEE

$
0
0

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Chama Mkoani Morogoro alipofika kutembelea makazi ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro. 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akitembelea na kukagua makazi ya Wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro 
Baadhi ya Misaada iliyokabidhiwa kwa wazee wanaoishi katiika makazi ya Chazi yaliyopo
Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro 
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni alipofika kutembelea makazi ya kulea wazee ya Chazi yaliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Stephen Kebwe.

GOLF LUGALO YAWASILI ARUSHA KWA AJILI YA ARUSHA OPEN

$
0
0
Na Luteni Selemani Semunyu Arusha.

Wachezaji wa timu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo wamewasili salama jijini Arusha na wamefanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Gymkana utakaotumika kwa ajili ya michuano ya wazi inayotari wa kuanza kesho jumamosi.

Wachezaji hao ambao wanafikia 14 wakiwemo wanawake watatu wanawake wamesema ni matumaini yao kurejea na ushindi mnono ili kuwapa faraja mashabiki wa klabu yao ambao wanamatumani makubwa nao.

Kwa upande wake bingwa wa Moshi Open mashindano yaliyomalizika hivi karibuni kutoka Lugalo Nicholous Chitanda amesema anajivunia kuwa na mwalimu mzuri hivyo atatumia mafunzo mazuri aliyopata kutoka kwa mwalimu wake kutetea ubingwa aliopata Arusha Open katika kundi lake.

Kwa upande wake mkuu wa msafara wa timu ya Lugalo Kapteni Amanzi Mandengule amesema kikosi chote cha timu ya Lugalo kimefika salama hakuna majeruhi na wachezaji wana ari kubwa ya kuhakikisha wanaibuka na ushindi mnono.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka klabu ya Gymknana ya Arusha ambao ndio wenyeji wa michuano hii ya Arusha Open mwaka 2016 jumla ya washiriki 102 wamethibitisha kushiriki.

Wachezaji hao kutoka klabu ya jeshi ya Lugalo ni 14,wawili toka mkoani Morogoro,16 kutoka klabu ya TPC ,nane kutoka klabu ya Gymkhana ya Dar es salaam, saba toka Moshi na wenyeji kutoka klabu ya Gymkhana ya Arusha 55.

Mashindano ya wazi ya Arusha Open yanatarajiwa kufanyika kwa siku mbili kwa kuanza na jumamosi na jumapili ambapo mara baada ya kumalizika kwa michezo sherehe ya ugawaji zawadi kwa washindi itafanyika kwa makundi yote ambayo ni A,B,C Senior,Junior,na wanawake
 WACHEZAJI WA KLABU YA GOLF YA LUGALO WAKIJADILIANA JAMBO WAKATI WAKIFANYA MAZOEZI KABLA YA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN YANAYOTARAJIA KUFANYIKA OKTOBA 15 NA 16 MWAKA HUU JIJINI ARUSHA .
MPIGA GOLF NICHOLOUS CHITANDA WA KLABU YA GOLF YA LUGALO AKIWA KATIKA MAZOEZI KUJIANDAA NA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN YANAYOTARAJIWA KUFANYIKA OKTOBA 15 NA 16 JIJINI ARUSHA (PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)
AFISA TAWALA WA KLABU YA LUGALO KAPTENI AMANZI MANDENGULE MWENYE FULANA NYEUPE AKIJADILIANA JAMBO NA MCHEZAJI MWENZIE WA KLABU HIYO PROSPER EMANUEL (KULIA) NA JUMA LIKULI( KUSHOTO )KATIKA MAZOEZI YA KUJIWINDA NA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN .
WACHEZAJI WA KLABU YA GOLF YA LUGALO WAKIJADILIANA MATOKEO WAKATI WAKIFANYA MAZOEZI KABLA YA MASHINDANO YA ARUSHA OPEN YANAYOTARAJIA KUFANYIKA OKTOBA 15 NA 16 MWAKA HUU JIJINI ARUSHA (PICHA NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU WAZIRI WA BIASHARA WA JAMHURI YA WATU WA CHINA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming  aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo.
 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini  Dkt. Lu youqing  Ikulu jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming .
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya EXIM ya China Sun Ping ambaye aliambatana na Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming, pamoja na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu youqing.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming watatu kutoka kulia  aliyefika Ikulu pamoja na ujumbe wake kwa ajili ya mazungumzo. Wengine katika picha ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakwanza (kushoto) Makamu wa Rais wa Benki ya EXIM ya China Sun Ping wapili kutoka (kushoto) Balozi wa China hapa nchini Dkt. Dkt. Lu youqing watatu kutoka (kushoto),Pamoja na  Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage wapili kutoka kulia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa China Qian Keming mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi wa China hapa nchini  Dkt. Lu youqing mara baada ya kumaliza mazungumzo ya pamoja na ujumbe wa Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa Jamhuri ya China uliofika Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi wa China hapa nchini  Dkt. Lu youqing mara baada ya kumaliza mazungumzo ya pamoja na ujumbe wa Naibu Waziri wa Biashara kutoka Jamhuri ya Watu wa Jamhuri ya China uliofika Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU,




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 14 Oktoba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Biashara wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe.Qian Keming ambapo viongozi hao wamekubaliana kuharakisha miradi inayotekelezwa kwa ushirikiano wa nchi hizo mbili ukiwemo mradi wa ujenzi wa reli ya kati.


Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam Rais Magufuli amemueleza Mhe. Qian Keming kuwa Serikali yake ya awamu ya tano inataka kuona mambo yakifanyika na kutoa matokeo bila kupoteza muda na kwamba angependa wadau wa maendeleo hasa nchi ya China ambayo ni ndugu na rafiki mkubwa wa Tanzania iende katika kasi hiyo hiyo.

Rais Magufuli ameuzungumzia mradi wa ujenzi wa reli ya kati ya kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma na kuunganisha nchi za Rwanda na Burundi ambao Tanzania imetenga Shilingi Trilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi katika bajeti hii, kwa kutaka China ambayo imekubali kushiriki katika ujenzi iendane na kasi ya Serikali yake.

“Mhe. Qian Keming sisi tumeamua kuanza ujenzi na tayari Wakandarasi 32 wamejitokeza kuomba kujenga reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro umbali wa kilometa 200 za mwanzo na tutatumia fedha zetu wenyewe.

“Kazi hii tunataka ianze mwaka huu wa fedha, kwa sababu upembuzi yakinifu na usanifu umeshafanyika, kwa hiyo na nyie ongezeni kasi ili mradi huu wote ukamilike, nataka uwe umekamilika kabla sijaondoka madarakani” amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli ameongeza kuwa mradi huo una manufaa makubwa kwa Tanzania na nchi nyingine nane zinazotegemea bandari ya Dar es Salaam na kwamba kukamilika kwake kutatoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ambayo imedharia kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Biashara wa China Mheshimiwa Qian Keming amempongeza Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kukuza uchumi wa Tanzania, kupiga vita rushwa na kwa namna ya kipekee kwa dhamira yake ya kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na China na ameahidi kuwa Serikali ya China itaongeza msukumo katika uharakishaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli ya kati.

“Mheshimiwa Rais Magufuli nimeielewa dhamira yako na kiu uliyonayo, naona kabisa kwamba dhamira ya kisiasa ipo ya kutosha, tunachotakiwa kukifanya ni kuwasukuma wataalamu wetu waongeze kasi, na mimi nakuahidi kuwa tulikuwa tunakwenda kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa, sasa tutaongeza na kwenda kilometa 200 kwa saa” amesema Mhe. Qian Keming.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing, Makamu wa Rais wa Benki ya Exim ya China Bw. Sun Ping, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles John Mwijage na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
14 Oktoba, 2016
 

MBUNGE WA SINGIDA MJINI AMUENZI MWALIMU NYERERE KWA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akimkabidhi mganga mkuu wa zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai kifaa maalumu kwa ajili ya kipimo cha ugonjwa wa Malaria
Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 ikiwa imefunguliwa kwenye Boksi maalumu ili wananchi waione kwa karibu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mtamaa kupitia mkutano wa hadhara

 Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisisitiza jambo wakati wa Mkutano wake

 Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa makini Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima
 Shukrani na Pongezi
 Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akishiriki kucheza ngoma ya Kinyaturu
Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Kijijini Mtamaa kwa ajili ya mkutano na kukabidhi kifaa maalumu kwa ajili ya kupimia Malaria

 Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Mtamaa
 Baadhi ya wananchi wakifurahia kifaa cha kupimia Malaria
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima akisisitiza jambo wakati wa Mkutano

Na Mathias Canal, Singida

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mussa Sima ameadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuwarahisishia huduma za upimaji wa Maralia wananchi wa Kijiji cha Mtamaa.

Tatizo hilo sugu limepatiwa ufumbuzi mara baada ya Mbunge huyo kuwapatia Mashine ya Kupima Maralia (Binocular Microscope) Mega 7 iliyonunuliwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni mbili nchini Kenya.

Mhe Sima amemkabidhi mashine hiyo Mganga Mkuu wa Zahanati ya Mtamaa Godson Charles Swai mara baada ya mkutano wake na wananchi wa kijiji hicho ambapo pia ametumia mkutano huo kuwashukuru wananchi hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Octoba Mwaka jana.

Sima alisema kuwa ameamua kuitumia siku hii ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwani wakati wa utawala wake alisisitiza uwajibikaji kwa viongozi kwa kuwatumikia zaidi wananchi kuliko kujilimbikizia mali.

Sima Alisema kuwa Mwalimu Nyerere atakumbukwa zaidi kwa kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwaunganisha watanzania, kutetea usalama wa taifa katika vita vya Kagera dhidi ya Nduli idd Amin, na kufanya uhuru wa kazi na uhuru wa maendeleo.

Alisema kuwa Mwalimu Nyerere katika mambo aliyoyaamini sana na kuyapa mkazo ni pamoja na kupamabana na masuala ya haki usawa kwani alijenga imani katika misingi ya utu,haki na usawa kwa kila Raia wa Tanzania.

Sima ameahidi kuendelea kufanya mikutano mingi katika maeneo mbalimbali ya Jimbo lake ili kuelezea namna ilani ya uchaguzi inavyotekelezwa kwa vitendo sambamba na kushiriki shughuli za maendendeleo ya wananchi.

Kuhusu kadhia ya uduni wa upatikanaji wa Maji katika Kijiji cha Mtamaa A Mbunge huyo amesema kuwa hadi kufikia mwezi aprili mwakani maji yatakuwa yameanza kutoka ili kumaliza kadhia hiyo kwani mradi mkubwa wa maji utakuwa umemalizika.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida Mbua Gwae Chima ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mtamaa ametoa shukrani zake kwa mbunge huyo kwa kufanya mkutano wa tatu katika eneo hilo tangu aingie madarakani huku akiwasaidia wananchi katika kuboresha shughuli za maendeleo.

Chima amesema kuwa Mbunge huyo ni muwakilishi mzuri wa shughuli za wananchi wake na ameonyesha uwezo mkubwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutetea hoja na kusimamia misingi ya uwajibikaji.

Naye mganga mkuu wa zahanati ya Mtamaa Bw Godson Charles Swai amesema kuwa kifaa hicho maalumu kilichotolewa kwa ajili ya upimaji wa Malaria ni madhubuti na imara hivyo kinatarajia kuwasaidia wananchi wengi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisafiri umbali wa karibu kilomita 20 kwenda kupima ugonjwa huo.

Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa tarehe 13, April 1922 katika Kijiji cha Butiama Wilaya ya Musoma Mkoani Mara.

Maadhimisho ya Mwalimu Nyerere hufanyika kila mwaka ambapo watanzania popote ulimwenguni huadhimisha kwa sala na matembezi mbalimbali kama ishara ya heshima kwa muasisi wa Taifa lao.

KAMPENI YA BINTI WA KITAA YAZINDULIWA RASMI ENEO LA PAKACHA KATA YA TANDALE JIJINI DAR

$
0
0
Baadhi ya waliofanikisha uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa Kitaa wakiwa wanaonesha #tag  Binti ya Kitaa.
Baadhi ya wadau na Mabinti wa Kitaa wakiwa katika uzinduzi huo
Bwana  Godfrey Nteminyanda ambaye ni Mkurugenzi wa Applemackbooks_tz akielezea namna alivyo ipokea kampeni hiyo na wao kuahidi kuisapoti kwa hali na mali 
Mkurugenzi Mtendaji wa (CVF) Ndg. George David maarufu kwa  Ambassador Angelo akizindua rasmi kampeni ya Binti wa Kitaa
Binti Zawadi Mansende  akizungumzia anayesoma Shule ya Sekondari ya Manzese Kidato cha Tatu akizungumzia changamoto mbalimbali wanazokutana nazo kama wasichana wa mtaani ikiwa ni pamoja na kurubuniwa na Vijana jambo linalowapelekea kukumbia majumbani mwao na wengine kupata Mimba za utotoni, wakati wa uzinduzi Rasmi wa Kampeni ya Binti wa Kitaa.
Baadhi ya Mabinti waliokati ya umri wa miaka 14 na kuendelea wakiwa wanafuatilia kwa makini uzinduzi wa Kampeni ya Binti wa Kitaa iliyofanyikia Tandale

Baadhi ya akina mama wa Tandale pamoja na waendeshaji wa Kampeni ya Binti wa kitaa wakiwa katika uzinduzi
Mama Consalva Genes Samba ambaye ni Mkazi wa mda mrefu wa Tandale akielezea namna mabinti wamekuwa wakirubuniwa na kudanganywa .
Baadhi ya wawezeshaji, na wakazi wa Tandale wakionesha Mabango ya Binti wa Kitaa
Madam Sophia Mbeyela akizungumza jambo wakati wa Uzinduzi huo
Ulifika Muda wa kupata mambo ya Kitaa yaani Bagia, Vitumbua Chachandu na Ujii ilikuwa ni safi sana
Hawa ni Baadhi ya Timu ya waandaaji wa Kampeni ya Binti wa Kitaa
Hii ni timu nzima ya kitengo cha habari cha Kampeni ya Binti wa Kitaa wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi kuisha
Tukio likiwa linaendelea
Pamoja na kuwa ni Kampeni ya Binti wa kitaa wanaume nao wamehamasika kuisapoti mwanzo mwisho hapa wakiwa pamoja na Mabinti wengine wanaosapoti.
Picha ya pamoja  .Picha zote na Fredy Njeje/Story na Mwana Libeneke wa Funguka Live Dickson Mulashani

Asasi isiyo ya kiserikali ya Community Voices In Focus (CVF)  imezindua kampeni kwa jina BINTI WA KITAA eneo la Pakacha kata ya Tandale wilaya ya Kinondoni itakayodumu kwa mwaka mmoja yenye lengo la kuelimisha jamii ili kupunguza na kuondoa tatizo la mimba pamoja na ndoa za utotoni  nchini Tanzania.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa (CVF) Ndg. George David amesema kama mtanzania ameguswa na tatizo hili ambalo limedumu kwa muda mrefu katika jamii hata katika kipindi hiki cha utandawazi hivyo anaamini kupitia kampeni hii, elimu itawafikia walengwa kwa namna ya tofauti na licha ya kupunguza tatizo hili itasaidia kulimaliza kabisa.

"Inauma sana kuona nchi yetu inatajwa kati ya nchi 5 duniani  zinazotambulika kwa janga la mimba pamoja na ndoa za utotoni, hivyo ni dhahiri kuwa huu ni wakati wa kuunganisha nguvu na kuhakikisha mabinti kwenye jamii yetu wanafikia malengo yao kwa wakati husika na sii vinginevyo" alisema  George.

BINTI WA KITAA  imelenga mabinti kuanzia umri wa miaka 12 hadi 17 sio tu kwa wale waliopo shuleni bali hata wale waliopo mitaani na inatarajiwa kuzuru mikoa zaidi ya 10 nchini huku ikiwa na agenda ya kuwafikia mabinti katika mitaa wanayoishi ili kuwapa fursa hata wazazi kuweza kushiriki katika kuwa sehemu ya ukombozi wa binti wa Kitanzania.

Kwa kuwa kwa kiasi kikubwa changamoto zinazowapelekea mabinti kupata mimba na kuolewa zipo katika jamii hasa mitaani,hii ndio iliyosababisha kampeni hii kuzinduliwa mtaa wa Pakacha Tandale kwani.

Kadhalika mmoja kati ya mabinti waliohudhuria katika uzinduzi huo Zawadi Isihaka ameomba wazazi kufuatilia maendeleo na kuwa karibu na watoto wao ili kuweza kuyagundua mapema mabadiliko ya tabia pamoja na kuwapa elimu ya makuzi sambamba na kutokuwa wakali kupitiliza kwa lengo la kujenga mahusiano mazuri.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wadau mbalimbali ikiwemo waratibu wa eneo ambao ni Tandale Youths, Applemacbooks Company,wakazi wa eneo la Pakacha ,Tandale, waandishi wa habari pamoja.

Sambamba na uzinduzi huo katika kata ya Tandale,Ndg. George David ametoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono kampeni hii  ili kuweza kuwasaidia mabinti kwani ni wazi kuwa hili limekuwa sehemu kubwa ya kuzalisha wimbi kubwa la watoto wa mitaani, vifo wakati wa kujifungua, athari za kisaikolojia na kiuwanyima mabinti nafasi ya kupata haki yao ya msingi ya elimu.

KONGAMANO LA KUMUENZI MWALIMU J.K NYERERE LAFANYIKA WILAYANI IKUNGI

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akishiriki kuandaa bustani kwa ajili ya mbogamboga zitakazotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko.
  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa amembeba mmoja ya mwanafunzi wa shule ya Msingi Ikungi mchanganyiko
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikabidhi mahitaji kwa wanafunzi walemavu mara baada ya kuwasili shule ya msingi Ikungi mchanganyiko
 Baadhiya washiriki wa Kongamano wakisikiliza kwa makini mada zikiwasilishwa kwenye mdahalo

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akiwa na baadhi ya viongozi wa ngazi ya Wilaya wakati kongamano likiendelea

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimsalimu Bi Fumbo Shishiwa aliyejifungua salama mtoto wa kiume na kumuita Magufuli
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimiana na wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Ikungi mchanganyiko

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi akichangia mada iiliyokuwa inajadiliwa kwenye Kongamano la Kumuenzi Mwalimu J.K Nyerere kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisalimia na Bi Faidha Athumani mara baada ya kumkuta akisubiri matibabu katika Kituo cha afya Ikungi
 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akishiriki kuandaa bustani kwa ajili ya mbogamboga zitakazotumiwa na wanafunzi wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko
 Baadhi ya washiriki wakifatilia kwa makini Kongamano

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua Chumba cha kuhifadhia maiti katika Kituo cha Afya Ikungi

 Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikagua Mashine ya vipimo vya magonjwa mbalimbali ikiwemo ini katika kituo cha afya Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimuelekeza Mganga Mkuu wa kituo cha Afya Ikungi kuhakikisha anasimamia ujenzi wa upanuzi wa chumba cha kuhifadhia maiti


Na Mathias Canal, Singida

Uongozi wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida umeungana na Watanzania kote ulimwenguni kuadhimisha kumbukizi ya miaka 17 ya kifo cha Mwasisi wa Taifa na Rais wa Kwanza wa Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyefariki dunia Octoba 14, 1999 katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza.

Katika Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi limejumuisha Viongozi wa kada tofauti wakiwemo viongozi wa serikali, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vitongoji na vijiji, Viongozi wa siasa, Wazee wa mji wa Ikungi, Maafisa Tarafa na Watendaji, Madiwani, Walimu na wanafunzi ambapo wote kwa pamoja wamepata nafasi ya kuchangia mada na kupitisha maadhimio zaidi ya kumi na tano yatakayotoa taswira ya namna ya kumuenzi Mwalimu Nyerere mwakani.

Mgeni rasmi katika Kongamano hilo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amewasihi wananchi kwa umoja wao kumuenzi Mwalimu Nyerere katika matendo makubwa na muhimu aliyokuwa anayafanya hususani misingi ya Haki, Ukweli na uwajibikaji.

Amewataka watanzania kuishi katika matakwa ya Mwalimu Nyerere ikiwa ni pamoja na kutokubali kutoa na kupokea Rushwa kwani hayo ni miongoni mwa mambo mengi aliyoyahubiri wakati akiwa waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu nafasi hiyo na hatimaye kuyahubiri na kuyaishi kipindi akiwa Rais wa kwanza wa Tanzania.

Dc Mtaturu alisema kuwa Tanganyika wakati wa uhuru ilikuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo maradhi yatokanayo na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza, Pia kulikuwa na ujinga uliosababishwa na ukosefu wa elimu bora kwa kiasi kikubwa kwani watanganyika wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu walikuwa ni zaidi ya asilimia 90.

Alisema kuwa sambamba na hayo pia kulikuwa na umasikini mkubwa na uliokithiri kwani asilimia kubwa ya watanzania walikosa mahitaji ya msingi kama vile malazi, Chakula, na Mavazi ambapo Mwalimu Nyerere alifanikiwa kupingana na maadui hao watatu kwa kuongeza udahili kwa kiasi kikubwa katika shule muhimu za Sekondari Kilakala, Kibaha na Mzumbe.

Mtaturu alisema kuwa pia Mwalimu Nyerere alitaifisha taasisi zote za watu binafsi ili kuleta usawa katika jamii pamoja na kuimarisha upatikanaji mzuri wa huduma za afya katika zahanati,  vituo vya afya, na Hospitali ili kuboresha afya za watanzania na kuwafanya kuweza kufanya kazi vizuri na kwa ufasaha.

Dc Mtaturu Amewataka washiri wote wa Kongamano hilo na watanzania kwa ujumla kuendelea kuwa viungo muhimu katika kudumisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Kudumisha Lugha ya Kiswahili, Kukuza Utu na uadilifu katika kazi na jamii inayotuzunguka.

Zaidi amesisitiza wakulima kwa kushirikiana na maafisa kilimo kulima kilimo chenye tija ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ili kuhakikisha wanakuwa na mavuno mengi yenye faida kubwa na kuwaongeza uchumi wao kwani wastani wa pato la Mtanzania aishie Wilaya ya Ikungi ni shilingi elfu mbili kwa siku ambapo kwa mwezi ni shilingi elfu sitini.

Hata hivyo Dc Mtaturu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo hususani kusimamia vyema mapato ya serikali, Kupambana katika misingi ya utu, haki na usawa kwa kila Raia wa nchi hii, Kupinga Rushwa na matumizi mabaya ya fedha za Umma.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Ndg Dandala Mzunguor ameyataja baadhi ya maadhimio yaliyojadiliwa katika kongamano hilo kuwa ni pamoja na Kupata viongozi wa Haki na halali katika chaguzi zetu, Jamii kuwa na moyo wa uzalendo na kujitolea katika kufanya kazi.

Mengine ni kuepuka kejeli na dharau katika maisha ya kila siku, Kuboresha mazingira ya kufundishia, Jamii na viongozi kuweka miiko ya uongozi, Kudumisha umoja na mshikamano wa Taifa letu.

Naye katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi Aluu Segamba amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuamua kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kufanya kongamano kwani imekuwa taswira njema kwa wakazi wa Wilaya hiyo ambao hawajawahi kushiriki katika kongamano kama hilo tangu kuanzishwa kwa Wilaya hiyo.

Baadhi ya wachangiaji katika kongamano hilo la kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wamependekeza kuwa na siku moja ambayo Mkuu wa Wilaya atakutana na wananchi wote kwa ajili ya kujadili kwa pamoja namna ya kuiboresha Wilaya hiyo ikiwa ni pamoja na shughuli za kijamii hususani kuboresha kilimo, Uchumi na Miundombinu.

Wengine wamependekeza bendera kupeperushwa nusu mlingoti ni kuenzi na kutoa heshima kubwa kwa Baba wa Taifa kwani kufanya hivyo itakuwa njia sahihi ya kuongeza uwajibikaji na nidhamu ya Taifa.

Kabla ya Kongamano hilo mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi akishirikiana na viongozi wote wa Wilaya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama alitembelea Shule ya Msingi mchanganyiko Ikungi ili kutoa baadhi ya mahitaji kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwemo Wenye ulemavu wa ngozi, Walemavu mchanganyiko na wasioona.

Sambamba na hayo pia amewatembelea wagonjwa katika Kituo cha afya Ikungi kwa kuzuru katika wodi za wanawake waliojifungua, sambamba na Wodi ya wanaume na Wanawake.

Dc Mtaturu amemuagiza mganga Mkuu wa Zahanati hiyo kuhakikisha anafanya utaratibu wa kujenga Sehemu ya kuhifadhia maiti kutoka na sehemu iliyopo kuzidiwa kwani ina sehemu mbili tu za kuhifadhia maiti.

Aidha Dc Mtaturu alipotembelea kituo cha Afya cha Ikungi alipitia maagizo yake aliyowahi kuyatoa hivi karibuni ya kupanua chumba cha maabara na kuagiza kutengenezwa kwa mashine ya kupimia magonjwa mbalimbali ndani ya muda mfupi ili kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wanaotumia kituo hicho kwa ajili matibabu.

Akifunga Kongamano hilo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesisitiza kuwa katika kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni lazima kuhakikisha huduma za Afya, Elimu, Uchumi, Kilimo na Miundombinu zinaboreshwa.

VIJUSO VYA BAADHI YA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OKTOBA 15,2016


BENKI YA POSTA TANZANIA (TPB) YAMALIZA TATIZO LA UHABA WA VYOO KWA WALIMU WA SHULE YA MSINGI IPINDA KYELA

$
0
0
Meneja Mahusiano kwa Umma benki ya Posta Tanzania (TPB) Noves Moses akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya mradi wa vyoo vya walimu vyenye matundu matano katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya ambavyo ujenzi wake umeghalimu kiasi cha shilingi milioni 8kwa msaada wa benki hiyo ya Posta Tanzania. 
Baadhi ya wananchi,walimu na wazazi pamoja na wanafunzi shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vilivyo jengwa kwa msaada wa benki ya Posta Tanzania TPB. 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Ipinda Wilayani kyela Mkoani Mbeya wakitoa burudani katika hafla ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vyenye matundu matano ambavyo vimejengwa kwa msaada wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa thamani ya shilingi milioni 8. 
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ipinda Subira Gwakabale akishukuru kwa kupatiwa msaada na benki ya Posta Tanzania (TPB) kwa kujengewa vyoo vya walimu vyenye matundu 5 kwa thamani ya shilingi milioni 8 ,ambapo pia katika katika shukrani zake ameelezea changamoto mbalimbali walizonazo ikiwa ni pamoja na Idadi kubwa ya wananfunzi kuliko vyumba vya madarasa walivyo navyo ambapo kwa sasa wana jumla ya wanafunzi 948 huku vyumba vya vya madarasa vikiwa 8 tu hali ambayo inawawia vigumu katika utoaji wa huduma kwa wanafunzi hao. 
Meneja wa Benki ya Posta Tanzania Tawi la Mbeya ,Humphrey Julias akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vyenye matundu matano ambavyo vimejengwa na benki hiyo katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela.
Afisa Taaluma Wilaya ya Kyela Lucasian Kavishe akiwaasa wananchi waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya vyoo vya walimu vilivyojengwa katika Shule ya Msingi Ipinda kwa Msaada wa Benki ya Posta Tanzania (TPB)kwa kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa wadau mbalimbali wanaojitolea katika miradi mbalimbali ya kusaidia sekta ya elimu ili kuendelea kuwapa moyo zaidi wa kusaidia 
Meneja wa benki ya Posta Tanzania (TPB)Mkoa wa Mbeya kulia ,Humphrey Julias akiteta jambo na Meneja Mahusiano kwa Umma wa benki hiyo Noves Moses kabla ya kukabidhi rasmi mradi wa vyoo vya walimu vyenye matundu matano vilivyojengwa katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani Kyela Mkoani Mbeya kwa Msaada wa benki hiyo kwa thamani ya shilingi milioni 8. 
Meneja Mahusiano kwa Umma wa benki ya Posta Tanzania TPB,Noves Moses akizindua na kukabidhi rasmi mradi wa vyoo vya walimu vyenye matundu Matano ujenzi ambao umeghalimu kiasi cha shilingi milioni8 katika shule ya Msingi Ipinda Wilayani kyela Mkoani Mbeya Otobar 13 mwaka huu,kushoto ni mwenyekiti wa kijiji cha Ipinda Saadat Sam (katikati)Afisa elimu taaluma Lucasian Kavishe na mwalimu Mkuu wa shule hiyo Subira Gwakabale kulia . 
Muonekano wa jengo la vyoo vya walimu katika shule ya Msingi Ipinda lenye matundu matano ambalo ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni8. 

Meza kuu katika Picha ya pamoja na walimu na wajumbe wa bodi ya shule ya Msingi Pinda.
Meza kuu na wafanyakazi wa benki ya Posta Tanzania TPB tawi la Kyela na Mbeya. 
Meza kuu katika picha ya pamoja na wadau na viongozi wa serikali ya kijiji cha Ipinda Wilaya ya Kyela. 
Vyoo vilivyokuwa vikitumiwa na walimu wa shule ya Msingi Ipinda kabla ya kujengewa vyoo vipya na benki ya Posta Tanzania (TPB).PICHA E.MADAFA

JAFO AWAFAGILIA WATENDAJI NA VIONGOZI TEMEKE KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YA SERIKALI.

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za mitaa, Selemani Jafo akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Kilamba, kushoto ni Mbunge wa Mbagala, Issa Mangungu.

…………………………………………………………
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amewapongeza viongozi na watendaji wa wilaya ya Temeke kwa kutekeleza maagizo yake aliyoyatoa mwezi mmoja aliopita ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi wanakaa kwenye madawati na kuongezwa vyumba vya madarasa.

Mnamo mwezi Septemba mwaka huu, Jafo alizitembelea shule nne za wilaya ya Temeke zilizopo eneo la mbagala na kukutana na changamoto lukuki, zikiwemo kutotembelewa shule hizo na Afisa elimu wilaya toka mwaka huu uanze kitendo kilicho sababisha kutobainika kwa changamoto ili zipatiwe ufumbuzi.

Shule alizozitembelea ni pamoja na shule za msingi Chemchem, Nzasa, Charambe, na Kilamba ambapo Jafo alikuwakuta watoto wa darasa la saba pekee kwa shule ya Chemchem ndio waliokuwa wakikalia madawati.Katika shule ya nzasa, Naibu Waziri huyo aliwakuta watoto wamejazana huku kukiwa hakuna mpango wowote wa ujenzi wa madarasa.

Aidha aliwakuta walimu wakiwa hawana ofisi ya walimu licha ya shule hizo kuwa katika jiji la biashara lenye mapato mengi.Hata hivyo, Shule ya Kilamba pekee ndiyo ilikuwa katika hali ya kuridhisha, na baada ya ziara hiyo alitoa maagizo kwa mkurugenzi wa Temeke kuzifanyia kazi changamoto alizo zibaini kwa kipindi cha mwezi mmoja.

Jafo alifanya tena ziara kwenye eneo hilo ili kubaini utekelezaji wa maagizo yake na katika safari hiyo ya pili alifanikiwa kuzitembelea shule alizozitembelea awali pamoja na shule mbili nyingine za Kiburugwa na Kingugi.Alipofika alikuta watoto wote wakiwa katika madawati pamoja na kuanza kwa harakati za kuongeza madarasa na ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule hizo ambazo baadhi zilikuwa hazina.

Kadhalika, Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke, alimpa taarifa Jafo kuwa shule ya Nzasa itapata jumla ya vyumba saba, Chemchem vyumba vitano, chalambe vyumba vinne na ofisi ya walimu na kilamba kujengewa fensi ya shule.Naibu Waziri huyo aliwashukuru na kuwapongeza viongozi wote wa temeke kwa kujali matatizo ya jamii.

Katika ziara hiyo Jafo aliongozana na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Mbunge wa jimbo la Mbagala Issa Mangungu, Meya ya Temeke Chaurembo, Mkurungenzi wa Manispaa ya temeke na wakuu wake wa idara huku akisema viongozi hao ni mfano wa kuigwa.

MIGOGORO YA ARDHI JIJINI MWANZA MBIONI KUMALIZIKA

$
0
0
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa jijini humo wakati wa ziara ya kutembelea maeneo ya ardhi yenye migogoro pamoja na makazi yaliyojengwa kiholela kabla ya kuyafanyia urasimishaji na kutoa hati ya makazi kwa wamiliki wake.

Kiomoni alifanya ziara ya kutembelea Kata za Buhongwa na Luchelele na kuzungumza na wakazi wa kata hizo juu ya maeneo yenye migogoro na ambayo bado wananchi wanadai fidia ili kutatua changamoto hizo.
Na BMG
Diwani wa Kata ya Buhongwa, Joseph Kabadi (mwenye suti) akizungumza kwenye ziara hiyo na kuelezea maeneo yenye migogoro ya ardhi katika Kata yake kwa ajili ya kutafutiwa ufumbuzi kabla ya urasmishaji wa makazi yaliyojengwa kiholela kufanyika katika kata hiyo. 
Wengine ni viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwemo watendaji wa idara ya ardhi.
Mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa ambaye kiwanja chake kina mgogoro akitoa malalamiko yake mbele ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza. Hatimaye Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza aliahidi kumpatia kijana huyu kiwanja kingine ili kuondokana na kiwanja hicho chenye mgogoro.
Wakazi wa Kata ya Buhongwa Magharibi Kata ya Buhongwa wakiwa kwenye kikao baina yao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza kilicholenga kutatua migogoro ya ardhi katika kata hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Luchelele ili kutatua changamoto za migogoro ya ardhi ikiwemo madai ya fidia katika Kata hiyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akizungumza na wakazi wa Kata ya Luchelele ili kutatua changamoto za migogoro ya ardhi ikiwemo madai ya fidia katika Kata hiyo.
Wakazi wa Kata ya Luchelele Jijini Mwanza
Diwani wa Kata ya Luchelele, Vicent Lusana, akizungumza katika mkutano huo ambapo alihimiza halmashauri ya Jiji la Mwanza kulipa fidia kwa wakazi wa kata hiyo kwani ni muda mrefu tangu zoezi la uthamini wa ardhi ulipofanyika katika Kata hiyo.
Alfredy Ngendelo ambaye ni Mthamini wa Jiji la Mwana, akifafanua jambo kwa wakazi wa Kata Luchelele kuhusiana na taratibu za ulipaji fidia baada ya uthamini kufanyika.
Afisa ardhi mteule Jijini Mwanza, Halima Nassor, akifafanua jambo kwenye mkutano huo.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Luchelele wakiuliza maswali ikiwemo kulipwa fidia baada ya zoezi la uthamini wa ardhi yao kukamilika muda mrefu bila kulipwa fidia, ambapo waliombwa kulipwa fidia zao mapema ili waondoke katika maeneo yao ambayo yamepimwa kwa ajili ya miradi ya kijamii.
Baadhi ya maeneo hatarishi yenye miinuko ambayo Mkurugenzi wa Jiji Mwanza amezuia ujenzi wake kuendelea.
Mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa akitoa malalamiko yake kwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa akitoa malalamiko yake kwa Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba.

Na George Binagi-GB Pazzo
Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeanza zoezi la kutembelea maeneo ya ardhi yenye migogoro pamoja na makazi yaliyojengwa kiholela ili kuyafanyia urasimishaji.


Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, amesema zoezi hilo limelenga kuondoa migogoro yote ya ardhi na kutoa hati ya makazi kwa wananchi ambao makazi yao yaliyojengwa kiholela yatarasimishwa.

Amesema wale waliojenga katika maeneo hatarishi ikiwemo milimani, hawatahusika katika zoezi hilo hivyo wasiendelee na ujenzi wa makazi hayo.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Buhongwa na Luchelele, wameomba migogoro yote ya ardhi inayowakabili ikiwemo kulipwa fidia katika maeneo yao, itatuliwe kwa halmashauri ya Jiji la Mwanza kufanya tathmini upya na katika maeneo yenye migogoro na kutoa hati za umiliki.

Zoezi hili limejili ikiwa siku chache baada ya Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Willium Lukuvi, kufanya ziara Jijini Mwanza na kumtaka Mkurugenzi wa Jiji hilo kutembelea maeneo yote yenye migogoro na makazi holela kabla ya zoezi za usaminishaji kufanyika.

RC MWANZA AZINDUA MELI MPYA NA YA KISASA YA MV NYEHUNGE II.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto), jana amezindua Meli mpya na ya kisasa (Kivuko) ya MV NYEHUNGE II yenye uwezo wa kubeba abiria 500 pamoja na mizigo inayofanya safari zake kati ya Jiji la Mwanza na Wilaya ya Ukerewe.

“Naamini kivuko hiki kitakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Ukerewe kwani uhitaji wa wakazi wa Ukerewe kuhitaji huduma nzuri na salama ya usafiri ni mkubwa hivyo tunaamini  kivuko hiki kitatumika kwa maeneleo ya wanaUkerewe”. Alisema Mongella na kuongeza kwamba hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Ukerewe kutumia Kivuko hicho katika shughuli mbalimbali za kibiashara.
Na BMG
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto), jana amezindua Meli mpya na ya kisasa ya MV NYEHUNGE II yenye uwezo wa kubeba abiria 500 pamoja na mizigo inayofanya safari zake kati ya Jiji la Mwanza na Wilaya ya Ukerewe.
Mmoja wa watoto akisalimiana na viongozi waliohudhuria uzinduzi wa meli hiyo
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo
Mama  Gertrude Mongella (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi.Mary Tesha, wakati wa uzinduzi huo.
Mama  Gertrude Mongella (katikati), akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Bi.Mary Tesha (kulia), pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dkt.Leonard Masale (kushoto) wakati wa uzinduzi wa Meli hiyo.
“Naamini kivuko hiki kitakuwa ni mkombozi kwa wakazi wa Ukerewe kwani uhitaji wa wakazi wa Ukerewe kuhitaji huduma nzuri na salama ya usafiri ni mkubwa hivyo tunaamini  kivuko hiki kitatumika kwa maeneleo ya wanaUkerewe”. Alisema John Mongella (katikati) na kuongeza kwamba hiyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Ukerewe kutumia Kivuko hicho katika shughuli mbalimbali za kibiashara.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Nyehunge, Said Mohamed (kushoto), alisema Meli hiyo itakuwa mkombozi kwa wasafiri wa Ukerewe ambapo kutakuwa na Meli tatu kwa siku zitakazokuwa zikifanya safari zake za Jiji la Mwanza na Ukerewe huku nauli ikiwa ni nafuu kabisa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, George Nyamala, akielezea umuhimu wa meli hiyo kwa wakazi wa wilaya yake.
Mmoja wa wakazi wa Ukerewe akielezea furaha yake baada ya uzinduzi wa Meli ya Mv Nyehunge II
Mwonekano wa ndani wa Meli ya Mv Nyehunge II

Abiria wakiingia kwenye Meli ya Mv Nyehunge baada ya uzinduzi kwa ajili ya kusafiri kutoka Jijini Mwanza kuelekea Ukerewe.

Wasanii wa Muziki wa Singeli waaswa kuzingatia mafunzo ya sanaa ya ujasiliamali

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Joyce Hagu akifafanua jambo wakati wa ufunguzi wa semina ya wasanii wa muziki wa singeli jana Jijini Dar es Salaam,kulia ni Meneja Mkuu wa EFM Bw.Denis Ssebo na kushoto ni Mkurugenzi wa EFM Bw. Francis Ciza.
Mkuu wa Matukio ya Sanaa wa Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA),Bw.Kuwijira Maregesi akiongea na waasanii kuhusu maadili ya utunzi wa mashairi wa nyimbo zao wakati wa ufunguzi wa semina ya wasanii wa muziki wa singeli iliyoandaliwa na uongozi wa Radio ya EFM jana Jijini Dar es Salaam kushoto ni Afisa Sanaa Bi. Bona Masenge na kulia ni Mkurugenzi wa Radio EFM Bw.Francis Ciza. 
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Bw.Innocent Mungi akiwasisitiza wasanii (hawapo katika picha) matumizi sahii ya mitandao ya kijamii wakati wa semina ya wanamuziki wa singeli iliyoandaliwa na uongozi wa Radio ya EFM jana Jijini Dar es Salaam. 
Meneja Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bibi.Valentina Baltaz akiongea kuhusu umuhimu wa wasanii kulipa kodi kupitia kazi zao za sanaa ili kuchangia pato la taifa wakati wa semina la wasanii wa muziki wa singeli iliyoandaliwa na uongozi wa Radio ya EFM jana Jijini Dar es Salaam kulia ni Mhariri Mkuu wa EFM Bi.Scholastica Mazula. 
Afisa Sanaa kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bi.Bona Masenge akiongea na wasanii(Hawapo katika Picha) kwa kuwataka kutunza na kuendeleza utamaduni wa kitanzania kwa kufuata taratibu na sheria katika kazi zao za sanaa wakati wa semina ya wasanii wa muziki wa singeli leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Bw.Innocent Mungi na kulia ni Mkuu wa Matukio ya Sanaa wa Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA),Bw.Kurwijira Maregesi 
Baadhi ya Wasanii wa Muziki wa Singeli waliohudhuria semina iliyoandaliwa na uongozi wa radio EFM kwa lengo la kuwapata somo la kuifanya sanaa kuwa ujasiliamali ikiwemo kupata mbinu mbalimbali za uwekezaji . 
Baadhi ya Wasanii wa Muziki wa Singeli waliohudhuria semina iliyoandaliwa na uongozi wa radio EFM kwa lengo la kuwapata somo la kuifanya sanaa kuwa ujasiliamali ikiwemo kupata mbinu mbalimbali za uwekezaji . 
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Joyce Hagu(wa tano kutoka kushoto waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wasanii wa muziki wa singeli baada ya semina iliyokuwa imeandaliwa na uongozi wa Radio EFM jana Jijini Dar es Salaam. Picha na Lorietha Laurence 


Na Lorietha Laurence-WHUSM 

Wasanii wa Muziki wa Singeli wameaswa kuzingatia mafunzo ya sanaa ya ujasiliamali yatakayowasaidia kuongeza weledi na mbinu za kukuza kazi zao na hatimaye kuwa na sanaa bora kwa ukanda wa Afrika Mashariki. 

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari Utamaduni,Sanaa na Michezo Bi.Joyce Hagu wakati wa ufunguzi wa semina ya wasanii wa muziki wa singeli jana Jijini Dar es Salaam. 

Bi Joyce aliongeza kwa kusema kuwa sanaa ya muziki ni kazi kama kazi nyingine hivyo ni budi kusimamia misingi iliyo bora inayoendana na utamaduni wa kitanzania katika utunzi wa tungo za singeli. 

“Utamaduni ni mali ya jamii hivyo ni jukumu letu sote kupenda,kuthamini na kuendeleza utamaduni wetu kupitia kazi za sanaa na hii itasaidia kutekeleza kwa vitendo Sera ya Taifa ya Utamaduni” alisema Bi.Joyce. 

Aidha aliupongeza uongozi wa EFM kwa kuandaa semina hiyo ambayo imewapa fursa wasanii kupata elimu ya msingi kuhusu muziki na kuifanya kazi ya sanaa kuwa ya thamani kwa jamii. 

Naye Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Bw.Innocent Mungi amewataka wasanii hao kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kuuza kazi zao za mziki na hivyo kuwa na soko la kimataifa na sio kutumia mitandao kwa ajili ya kuchafuana. 

Kwa Upande wake Mkuu wa Matukio ya Sanaa wa Baraza la Sanaa la Taifa(BASATA),Bw.Kuwijira Maregesi amewakumbusha wasanii hao umuhimu wa kuzingatia maadili pale wanapofanya utunzi wa nyimbo zao ili kuepuka usumbufu wa kufungiwa. 

Mbali na mada ya maadili wasanii walipata fursa ya elimu ya mlipa kodi kutoka kwa Meneja Elimu kwa Mlipakodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bibi.Valentina Baltaz ambapo aliwaeleza wasanii umuhimu wa kulipa kodi kupitia kazi zao za sanaa kulingana na sheria na taratibu za nchi ili kuchangia katika kukuza pato la taifa.
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>