Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

CCM YAPATA UGENI KUTOKA PALESTINA

$
0
0
 Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akimlaki Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, alipowasili asubuhi hii, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya Kichama, hapa nchini. Pamoja naye ni Wajumbe wa NEC wa PLO, Jehad Zneed na Saleh Raafat.
 Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, alipowasili asubuhi hii, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julisu Nyerere, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya ziara ya Kichama, hapa nchini. Pamoja naye ni Wajumbe wa NEC wa PLO, Jehad Zneed na Saleh Raafat (Kushoto). Wapili kulia ni Balozi wa Palestina hapa nchini  Dk. Nasri Abujasir.
Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, akizingumza Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayaseer Khalid ambaye pia ni mjube wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam. Kiongozi huyo anatarajiwa kuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuanzia saa 3.30 asubuhi hii, kwenye hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

REDD'S MISS KINONDONI 2013 WATEMBELEA WAGONJWA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR

$
0
0
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwa na mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakiwaongoza warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (katikati) akiwa na mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo wakitoa maelekezo kwa warembo mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiwagawia warembo vifaa kwa ajili ya kujikinga na vumbi mara baada ya warembo hao kutembelea hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kutembelea wagonjwa na kufanya usafi.
Warembo wajielekezana namna ya kuvaa vifaa vya kujikinga na vumbi kabla hawajaanza zoezi la kufanya usafi.
 Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiwaongoza warembo kuchukua vifaa kwa ajili ya kuanza zoezi la kufanya usafi.
 
Warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013 wakiwa katika zoezi la kufanya usafi.
 Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dokta Gunini Kamba (kulia) akiongea na vyombo vya habari. 
Mrembo wa Redd's Miss Tanzania 2012/13 ambaye alitokea Redd'd Miss Kinondoni 2012 akiongea na vyombo vya habari.
  Mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013, Ssebo akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika zoezi la kufanya usafi.
Bw. Ssebo alisema kuwa mchakato wa kumtafuta Redd's Miss Kinondoni umeanza kwa kishindo ambapo warembo hao ambao walishaanza kambi tokea mwishoni mwa wiki iliyopita jana waliweza kutembelea hospitali ya Mwananyamala  na kufanya usafi.

Warembo hao ambao wanajumuisha vitongoji vya Dar Indian Ocean, Sinza na Ubungo baada ya kufanya usafi hospitalini hapo walijionea hali mbaya iliyokuwepo pale na kuamua kufanya harambee ya kuchangisha hela kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds).

Harambee hiyo imepangwa kufanyika siku ya alhamis tarehe 13, katika ukumbi wa Ambassador kuanzia saa moja jioni huku mgeni rasmi akiwa ni meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda. Warembo hao leo watafanya usafi hospitali ya Sinza na kutembelea mradi wa mabasi yaendayo kwa kasi.

Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku walowa yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.

Launch parties with ZIFF and Fashion Week Zanzibar.

warsha ya tanapa na wahariri wa vyombo vya habari yaendelea leo mkoani iringa.

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi Mipango,Miradi ya Maendeleo na Huduma za Utalii TANAPA,Dkt.Ezekiel Dembe akijibu changamoto mbalimbali zilizokuwa zikiulizwa na washiriki wa Warsha ya TANAPA na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusiana na mada zilizohusu masuala ya utalii ndani ya hifadhi za Wanyama na Miradi ya ujirani mwema.Warsha hiyo ya siku nne iliyofunguliwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii,Balozi Khamis Kagasheki inaendeleo leo ikiwa ni siku ya pili katika ukumbi wa mikutano wa Siasa na Kilimo,Manispaa ya Iringa mkoani Iringa.Warsha hiyo imebeba kauli mbiu inayohusu wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Ubunge Ardhi,mazingira na Maliasili,Mh James Daudi Lembeli akifafanua jambo mbele ya washiriki wa Warsha ya siku nne ya shirika la Hifadhi ya Mbuga za Taifa (TANAPA) na Wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali  kwenye mada mbili zilizohusu masuala ya utalii ndani ya hifadhi za Wanyama pamoja na Miradi ya Ujirani mwema.Warsha hiyo imebeba kauli mbiu inayohusu wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukabiliana na Ujangili katika hifadhi za Taifa, unaoendelea kwenye ukumbi wa Siasa na Kilimo,Ofisi za Manispaa ya Iringa,Mkoani Iringa.
 Waziri Kivuli (kambi ya Upinzani) Wizara ya Maliasili na Utalii,Mh Mch.Peter Simon Msingwa akichangia kwenye moja ya mada iliohusu Masuala ya utalii ndani ya hifadhi za Wanyama,kulia kwake ni Mkurugenzi wa TANAPA,Bwa.Allan Kijazi na shoto ni Dkt.Ayoub Rioba.
 Mmoja wa Wahariri,Charles Misango kutoka gazeti la Tanzania Daima akiuliza swali kwenye warsha hiyo mapema leo asubuhi.
 Mmoja wa Wahariri wa gazeti la The Guardian on Sunday,Rodgers Luhwago akiuliza swali kwenye moja ya mada ya leo iliyohusu Masuala ya Utalii ndani ya hifadhi za Wanyama,mapema leo asubuhi.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha hiyo ya siku nne wakifuatilia kwa makini yanayojiri ukumbini humo.

WATANZANIA WAKARIBISHWA SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI, IJUMAA TAREHE 14 JUNI, 2013

$
0
0
Inline image 1
Tanzania kupitia Mpango wa Damu Salama Tanzania itaungana na nchi nyengine Duniani katika sherehe za Kuwashukuru na kuwatambua Wachangia Damu Duniani siku ya Ijumaa ya tarehe 14 Juni, 2013 ambapo kitaifa sherehe hizo zitafanyika katika viwanja vya Mkendo Wialyani Musoma, mkoani Mara huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Waziri mwenye dhamana Katika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Mh. Dk. Hussein Mwinyi.
Kwa Mujibu wa Mpango wa Damu Salama Tanzania, wananchi ambao wako katika mikoa mengine nje ya kanda ya ziwa wanaweza kujumuika na vituo vya Damu Salama vilivyo katika kanda zao ili kuweza kusheherekea na kujitolea damu siku hiyo.
Aidha, sehemu zilizoanishwa na Mpango wa Damu Salama Tanzania ambapo sherehe hizo zitafanyika Kimkoa ni Makao Makuu ya Mpango wa Damu Salama Tanzania, Ilala Mchikichini kwa Mkoa wa Dar es salaam, Viwanja vya Tangamano kwa Mkoa wa Tanga, Mkoani Tabora Katika Kituo cha Damu Salama Kitete, Viwanja vya Luanda Nzovwe Jijini Mbeya, Kwa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi sherehe zitafanyika katika Bustani ya Mkapa, Morogoro katika Kituo cha Damu Salama Rwegosore, na Mkoani Lindi katika kituo cha Damu Salama Ilulu.
Sherehe hizo za Kila mwaka zinalengo la kuamsha ari pamoja na kuongeza uwelewa juu ya mahitaji ya damu na umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji damu duniani ikiwa pamoja na kuwashukuru na kuwapongeza wachangia damu wote duniani.

Kidunia sherehe hizi zitafanyika Jijini Paris, Ufaransa chini ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ikishirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (IFRC), Shirikisho la Kimataifa laTaasisi za Kuchangia Damu (IFBDO), na Jumuiya ya Kimataifa Mpango wa Damu Salama (ISBT). Ujumbe wa Mwaka huu ni TOA ZAWADI YA MAISHA. CHANGIA DAMU.
Rafiki wa Damu Salama Tanzania inawaomba watanzania wote kujitokeza kwa wingi siku ya Ijumaa kuweza kujumuika pamoja katika sherehe hizi muhimu ambazo zinagusa moja kwa moja maisha ya mwanadamu. Mahitaji ya damu nchini bado ni makubwa na wahitaji wamekuwa wakiongezeka kila siku kutokana na Uzazi kwa kina mama, ajali na magonjwa ya saratani. Kama asilimia 1% tu ya watanzania watajitolea kutoa damu kwa mwaka basi Tanzania itaweza kuondokana na tatizo hili la upungufu wa damu.

Ijumaa Hii na Kila Ijumaa ya Pili ya Mwezi GROOVEBACK Team Iko Mafian Lounge!!

UJUMBE WA PLO WAKUTANA NA KINANA

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia), akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Tayseer Khalid (wapili kushoto) katika mazungumzo maalum yaliyofanyika kwenye hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, leo Juni 12, 2013. Wapili kulia ni Katibu wa HKT ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. Wengine, Watatu kushoto ni Balozi wa Palestina nchini, Dk. Nasri Abujais. (Picha na Bashir Nkoromo).

MJUMBE WA NEC AKUTANA NA MWENYEKITI WA SACCOS KUBWA YA WANAWAKE (TEWO)

$
0
0
Mjumbe wa NEC Phares Magesa akisalimiana na Mwenyekiti wa WAZAZI Temeke mama Sophia Kinega ambaye pia in Mwenyekiti wa TEWO Saccos mara baada ya mazungumzo yenye lengo la kusaidia kuimarisha Saccos hiyo kwa miradi ya kiuchumi kwa faida ya Watanzania wote. UMOJA NI USHINDI !!!!

Msikilize Mh.James Lembeli akizungumza kuhusiana na ujangili wa meno ya tembo

$
0
0
Mwenyeki wa Kamati ya Bunge Ardhi,Mazingira na Maliasili,Mh James Lembeli akizungumzia kuhusiana na suala la Ujangili wa meno ya Tembo,wakati wa warsha ya TANAPA na Wahariri wa Vyombo vya Habari,inayofanyika mkoani Iringa.

KAMPUNI YA BIA YA SERENGETI YATUNUKUIWA CHETI NA SHIRIKA LA VIWANGO LA KIMATAIFA(ISO)

$
0
0
  Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi akiwa amebeba cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO) mara baada ya kumaliza mkutano na wanahabari jana jijini Dar es Salaam. 
 Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Taylor pamoja na Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi wakionesha cheti walichotunukiwa na Shirika la Viwango la Kimataifa(ISO) kwa wana habari jana katika ofisi za kiwanda cha bia cha Serengeti jana jijini Dar es Salaam.
 Meneja mawasiliano ya ndani wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Imani Lwinga akizungumza jambo katika mkutano na wana habari jana jijini Dar es Salaam.
Meneja viwango wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Kitambi, akizungumza na wana habari, kuhusu kutunukiwa cheti 9001:2008 na shirika la viwango la kimataifa (ISO) baada ya kukidhi vigezo vya shirika la Det Norske Veritas (DNV)linaloaminika kimataifa katika kutoa huduma za ukaguzi na uhakiki wa utendaji wa viongozi na wafanyakazi katika makampuni, mkutano huo ulifanyika jana katika ofisi za Kiwanda cha bia cha Serengeti jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Mark Taylor .

TAMASHA LA USIKU WA MATUMAINI 2013 KUWEKA HISTORIA

FLAVIANA MATATA FOUNDATION STATIONERIES .......COMING SOON!!

MAANDALIZI YA MTANANGE WA KUKATA NA SHOKA KATI YA NMB NA WABUNGE UWANJA WA JAMHUR

$
0
0
 Mheshimiwa Kassim Majaliwa akipokea jezi kwa ajili ya mechi hiyo kati ya Wabunge na NMB  kutoka kwa Nahodha msaidizi wa timu ya NMB, Hezbon Mpate. Makabidhiano haya ya Jezi zenye thamani ya shilingi milioni tatu na laki saba yamefanyika katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Mheshimiwa Fatma Mikidadi akipokea jezi za mpira wa pete kutoka kwa nahodha wa timu ya mpira wa pete ya NMB Josephine Kulwa. Mechi zote zinatarajiwa kuchezwa siku ya jumamosi katika viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma.
 Waheshimiwa wabunge pamoja na maofisa wa NMB wakizifurahia jezi mara baada ya makabidhiano rasmi.

Timu ya Benki ya NMB ipo kwenye maandalizi makubwa ya mechi kati yao na wabunge ambayo itachezwa siku ya jumamosi kwenye viwanja vya Jamhuri  hapa Dodoma. Ili kufanikisha mtanange huo Benki ya NMB imekabidhi jezi kwa Nahodha wa timu ya Bunge ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Kassim Majaliwa. Ni mtanange wa kukata na shoka ambao umesubiriwa kwa hamu na kwa muda mrefu na mashabiki wa timu hizo mbili.

uzinduzi wa Kill Music Tour wafanyika leo jijini Dar.

$
0
0
 Waimbaji wan a washindi wa tuzo za kili wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro wakati wa uzinduzi wa Kili Muzic Tour uliofanyika katika Hotel ya Holiday Inn Dar es Salaam.
 Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi wa Kili Music Tour unaotarajiwa kuanza wiki hii Mkoani Dodoma ,uliofanyika katika Hoteli ya Holiday Inn Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba na Muimbaji wa nyimbo za kizazi kipya, Diamod Platnam.
 Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platinam (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour ulifanyika Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na Rais wa Bendi ya Mashujaa,Charles Baba
 Rais wa Bendi ya Mashujaam,Charles Baba(kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour ulifanyika Dar es Salaam.Kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe na Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platnam
Mwimbaji wa nyimbo za kizazi kipya,Kala Jeremiah (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tour ulifanyika Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Rais wa Bendi ya Mashujaa,Charles Baba, Mwimbaji wa nyimbo za nyimbo za kizazi kipya,Diamond Platnam na Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe

ORIJINO KOMEDI WASAINI MKATABA MNONO WA USIMAMIZI

$
0
0
  Mkuu wa kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara kutoka  ROCKSTAR4000,Christine “Seven” Mosha , akifafanua jambo mbele ya Wanahabari kwenye mkutano wao uliofanyika jijini Dar kuhusiana na Kundi la kipaji cha televisheni “Orijino Komedi”  kuingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa  kushirikiana na Rockstar 4000.
 Pichani shotoni ni Mpoki akizungumza machache kwenye mkutano huo, kati ni Joti na  Mkurugenzi mkuu wa Nexus, Bwana Bobby Bharwani
 kutoka kushoto ni Mpoki, Joti, Bobby, Seven, Seki, Masanja na Maclegan
Mpoki, Kitenge, Maulid, Joti, Seki, Masanja na Maclegan

=========== ====================

KUNDI LA KIPAJI CHA TELEVISHENI KINACHOONGOZA TANZANIA 

 ORIJINO KOMEDI WASAINI MKATABA MNONO WA USIMAMIZI 

Kundi la kipaji cha televisheni “Orijino Komedi” linaloongoza nchini kwa vipindi vyake  kupitia television imeingia mkataba na Kampuni ya Nexus Consulting Agency kwa  kushirikiana na Rockstar 4000. Mkataba huu unakuwa wa kwanza kwa wasanii wa  luninga kupitia kampuni hii ya Nexus

Nexus imenunua haki zote za usimamizi wa biashara na uongozi wa kundi hilo ambalo  linajulikana sana nchini kupitia vichekesho vyake kupitia vituo vya televisheni na  matamasha mbali mbali ambapo mkataba huu utakuwa ni kwa ajili ya kusimamia kipindi  hiki cha vichekesho kinachoundwa na wachekeshaji saba wajulikanao kama; Joti,  Maclegan, Masanja, Wakuvanga, Mpoki, Vengu na David Seki ambacho kimekuwepo  hewani kwa mfululizo wa miaka sita.


 Kushirikiana na Orijino Komedi ni kitu cha muhimu kwa Nexus kwani siku zote  imekuwa ikitamani kufanya kazi kwa karibu na kundi hilo na kuthamini kazi zao  kutokana na vipaji vya hali ya juu walivyokuwa wakionyesha wasanii wa kundi hilo;  alisema Mkurugenzi mkuu wa Nexus, Bwana Bobby Bharwani. 

“Nimefurahishwa sana kufanya kazi na watu wenye vipaji vya hali ya juu na kuiingia  mkataba na Kampuni ya Nexus Agency. Kwa pamoja tumedhamiria kukuza na  kubadilisha dhama ya vipaji na sanaa kutoka ilipo na kuwa ya kimataifa” alisema  Christine “Seven” Mosha , Mkuu wa kitengo cha Vipaji na Uendelezaji wa Biashara kutoka  ROCKSTAR4000.

Muandaji wa vipindi vya Orijino Komedi, Sekioni Davis ‘Seki’ amesema wanafuraha  kuingia mkataba wa kazi na kampuni ya Nexus Agency na Rockstar 4000 Africa, mbapo ameahidi kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kukidhi haja ya soko.


Kwa kushirikiana na Rockstar 4000, nexus inatambua na kuthamini vipaji hivyo  itahakikisha inaendeleza vipaji vya wasanii wa kundi hilo ili vipaji vyao viweze kufikia  kiwango cha juu vya ufanisi ndani ya Afrika na kimataifa kwa ujumla. 


Jiunge na kufuatilie Orijino Komedi kwenye:

Website 

www.orijinokomedi.com

YouTube

www.youtube.com/orijinokomedi

Twitter

www.twitter.com/orijinokomedi

Facebook


Ndani ya Ruaha national park maelekezo yakitolewa

$
0
0

Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakipata maelekezo mafupi kutoka kwa Muhifadhi Mwandamizi wa Ruaha National park,Bwa.Paul Bang mapema leo asubuhi

NAIBU WAZIRI AWAASA WASTAAFU WA NSSF

$
0
0
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, akisoma hotuba yake wakati wa sherehe ya siku ya wanachama wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Meneja Kiongozi Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Crescentius Magori. 
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza wakati wa sherehe ya siku ya Wanachama wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo.. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu, Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga na Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume. 
Mstaafu wa NSSF, Justina Lyela akitoa ushuhuda wa athari za fao la kujitoa wakatti wa sherehe za wastaafu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Mstaafu akichangia wakati wa sherehe hizo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF, Abubakar Rajabu (katikati), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kulia) na  Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume wakibadilishana mawazo wakati wa sherehe ya siku ya wanachama wastaafu (Pensioners) wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. 
 Wastaafu.
 Wastaafu wakijiandikishankabla ya kuingia katika ukumbi wa Karimjee leo.
Baadhi ya wastaafu wakimsikiliza mgeni rasmi Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk. Makongoro Mahanga.

Dar es Salaam, Tanzania

WASTAAFU nchini wametakiwa kuwa mabalozi wazuri kwa familia na jamii inayowazunguka, kuelewa faida na hasara ya Fao la Kujitoa, linalokimbiliwa na wanachama wa Mifuko ya Pensheni kwa Wastaafu, licha ya ukubwa wa athari zake.


Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Milton Mahanga, wakati wa sherehe ya Siku ya Wanachama Wastaafu (Pensioners) wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) wa mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee, jijini.


Mahanga alisema kuwa, Fao la Kujitoa ni changamoto ni changamoto kubwa inayoikabili mifuko mingi ya pensheni nchini likiwamo NSSF na kwamba, jamii inapaswa kuepuka kukimbilia kujitoa pale wanapobadilisha ajira kutoka sehemu moja kwenda nyingine au ajira zao zinapokoma.


“Ni vema wastaafu au wanachama wanaohama au kubadili ajira zao wakaendelea na kuchangia hata wanapokuwa katika ajira binafsi, kuliko kukimbilia kujitoa ili kuchukua kilicho chao, ambacho umaliza muda mfupi baadaye na kuishi maisha ya kuhangaika,” alisema Mahanga.


Mahanga akawahikikishia wastaafu maisha bora baada ya kazi na kusema kuanzishwa kwa Mamlaka ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kumebeba dhima ya kufanikisha hilo, ambapo kazi zake ni kusimamia mifuko yote ya jamii nchini ili iweze kutoa huduma bora kwa wanachama wake.


“Hakuna anayeweza kubisha kuwa maendeleo tuliyonayo sasa nchini yametokana na kazi nzuri ya wastaafu katika sekta ya umma na binafsi na nguvu zao ndio zimelifikisha hapa taifa kimaendeleo, hivyo kuwathamini wastaafu ni kujali mchango wao, aliongeza Mahanga.


Aidha, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Cresentius Magori aliwashukuru wastaafu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuhudhuria sherehe hizo, huku akiahidi hirika kuendelea na juhudi za kuwaelimisha waajiri ili kila mmoja ajue wajibu alionao kwa wanachama wake na haki zake katika NSSF.


Magori aliongeza kuwa, nia ya kuwa na siku kama hiyo ni kuonesha namna ushirikiano baina ya wastaafu na NSSF ulivyo na wigo mpana usio na mwisho, ambapo hafla za kukutana baina ya pande hizo hizo mara moja kwa mwaka huzaa awazo endelevu yenye tija kwa kila upande.

KAPIGENI KURA USALAMA WA KUTOSHA-NAPE

$
0
0
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Kimandolu wakati wa kampeni za udiwani . 
Mgombea wa kiti cha udiwani, Ndugu Edna Jonathan Sauli akisalimia wakazi wa kata ya Kimandolu wakati wa kampeni za udiwani.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ,akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea wa kiti cha udiwani cha kata ya Kimandolu,Arusha.

MANGULA ALA CHAKULA CHA JIONI NA UJUMBE WA PALESTINA

$
0
0
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula akimkaribisha Makamu Mwenyekiti Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Palestina (PLO), Tayseer Khalid,kwenye chakula cha jioni, alichomwandalia mgeni huyo na ujumbe wake, kwenye hoteli ya Protea Courtyard, jijini Dar es Salaam, Jini 12, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Mangula akifurahi hapa na apale na wageni kabla ya chakula
 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Chama Cha PLO,Jehad Abu Znead (kushoto) akimsalimia Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Tanzania, Khamis Dadi kwenye hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, wakati wa chakula cha jioni ambacho Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula aliuandalia ujumbe wa PLO uliopo nchini, Juni 12, 2013. Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi Amina Makilagi, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa
Kimataifa CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Kiongozi wa zamani wa Makao Makuu ya CCM, Hulda Kibacha.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akimsalimia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya chama cha PLO, Jehad Abu Znead wakati wa chakula cha jioni alichouandalia ujumbe wa PLO ulipo nchini, kwenye hoteli ya Courtyard jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa NEC,
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula akizungumza wakati wa chakula cha jioni alichouandalia ujumbe wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) kwenye Hotel ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, Juni 12, 2013. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya PLO, Jehad Abu Znead  na Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Balozi wa Palestina hapa nchini, Dk. Nasri Abujais na  Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid.
 Makamu Mwenyekiti wa PLO Tayseer akizungumza kwenye chakula hicho.
 Mkao mzima uliokuwa hivi
 Mangula na Tayseer wakiongoza kuchukua chakula
 Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi cha Palestina (PLO) Tayseer Khalid akimpa zawadi maalum, Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Mangula kwa ajili ya ujumbe wa PLO uliopo nchini, katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, Juni 12, 2013.
 Naam zawadi hii ni nzuri: Mangula akifurahia zawadi hiyo
Balozi wa Palestina hapa nchini, Dk. Nasri Abujais (kulia) akitoa neno la kumshukuru Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula ( wapili kushoto), kwa achakula cha jioni alichouandalia ujumbe wa PLO uliopo nchini, katika hoteli ya Protea Courtyard jijini Dar es Salaam, Juni 12, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na Wapili kulia ni Makamu Mwenyekiti wa PLO, Tayseer Khalid PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

redds miss kinondoni 2013 watembelea ofisi ya wakala wa mradi wa mabasi yaendayo kasi jijini dar leo

$
0
0
Bango la ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART) lililoko Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam.
Msimamizi wa mradi huo, akitoa maelezo kwa warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013 ambao waliambatana na Madiwani wa Viti Maalum kutembelea ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka zilizoko Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam. Ziara ya warembo hao ilikuwa na nia ya kuwajengea uwezo warembo hao waweze kutambua miradi mbali mbali inayoendeshwa na serikali.
Warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013 wakimsikiliza Kaimu Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi. Astelia Mrambo mara baada ya kutembelea ofisi kwake.
 Kaimu Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi. Astelia Mrambo akitoa maelezo kwa warembo wa Redd's Miss Kinondoni 2013 juu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka unaotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwaka 2014 ambapo mpaka sasa baadhi ya vituo na karakana zimeshaanza kukamilika.

Kaimu Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi. Astelia Mrambo akiwa na mratibu wa shindano la Redd's Miss Kinondoni 2013 wakiwaongoza warembo kuangalia ujenzi wa vituo vya mabasi yaendayo kwa haraka kituo hicho kilichokatika hatua za mwisho kukamilika kipo Manzese jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi. Astelia Mrambo akiendelea kutoa ufafanuzi juu ya mradi huo.
Maelezo yakiendelea kutolewa...
Kaimu Mtedaji Mkuu wa ofisi ya wakala wa Usafiri wa Haraka (DART), Bi. Astelia Mrambo akifanya mahojiano na vyombo ya habari.
Mshiriki wa Redd's Miss Kinondoni 2013 akieleza machache waliyojifunza. Mashindano ya Redd's Miss Kinondoni yanatarajiwa kufanyika June 21, huku mashindano hayo yakiwa yamedhaminiwa na Redd's Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, Mrokim Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog, DjChoka Blog na Kajunason Blog.
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images