Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 98 | 99 | (Page 100) | 101 | 102 | .... | 1898 | newer

  0 0
 • 06/08/13--07:57: Viberiti vyetu

 • 0 0

  Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine.
   Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (aliyesimama) akifunga mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramdahani Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Viatnam, kwenye Ofisi za CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo.
   Mjumbe wa Chama Cha Kimomunisti cha China, akimpa zawadi Madabiba baada ya mazungumzo yao.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akimkabidhi cheti, Mkurugenzi wa ITV na Radio One, Joyce Mhaville, cha kutambua mchango wa wake katika kufanikisha matembezi ya hisani ya ‘Step Ahead’ kwa ajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Barclays Tanzania, Kihara Maina
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Montage Ltd,Teddy Mapunga akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Barclays Tanzania, Kihara Maina mara baada ya kupokea Cheti cha kutambua mchango wa wake katika kufanikisha matembezi ya hisani ya ‘Step Ahead’ kwa ajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo,kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro. 
  Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (pili kushoto) akiongoza Mazoezi kabla ya kuanza kwa Matembezi ya hisani ya ‘Step Ahead’ kwa ajili ya kusaidia afya ya mama na mtoto yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.


  0 0

  IMG_0103

  Mwendesaji wa semina ya “How To Find Your Destiny” Hoyce Temu akisikiliza utambulisho kutoka kwa washiriki waliohudhuria semina hiyo ambao baadhi yao ni wajasiriamali, waajiriwa wa serikali, Mentors na wanafunzi wa vyuo. Semina hiyo imefanyika kwenye Taasisi ya Mara Foundation ya jijini Dar.
  IMG_0131
  Pichani juu na chini ni Mwendeshaji wa semina ya “How To Find Your Destiny” Hoyce Temu aki-share experience ya maisha yake mpaka hapo alipofika baada ya kupitia vikwazo vingi, kuvuka mabonde na malima wakati wa semina hiyo.
  IMG_0133
  IMG_0121
  Pichani juu na chini ni Washiriki wa semina ya “How To Find Your Destiny” wakifuatilia kwa umakini shuhuda na mifano mbalimbali ya maisha iliyokuwa ikitolewa na Mwendeshaji wa Semina hiyo Hoyce Temu(hayupo pichani).
  IMG_0130
  IMG_0171
  Mwendeshaji wa Semina ya “How To Find Your Destiny” Hoyce Temu akigawa kitabu chake kinachoelezea historia ya maisha yake kinachoitwa "Nayakumbuka Yote" ambacho kinauzwa katika maduka mbalimbali ya vitabu jijini Dar na Pesa inayopatikana katika mauzo hayo asilimia 80 inakwenda kulipia ada za shule kwa wasichana ambao ni mayatima na asilimia 20 inakwenda kwa mchapishaji.
  IMG_0175
  Mmoja wa washiriki akimpongeza Hoyce Temu kwa ujasiri aliokuwa nao na mateso aliyopitia katika maisha yake mpaka kufikia hapo alipo.
  IMG_0184
  Hoyce Temu akisaini autograph kwa mmoja washiriki.
  IMG_0195
  Hoyce Temu akishow love na Mmiliki wa Beutylicious Saloon iliyopo Mikocheni B Irene Juliet Mbuya.
  IMG_0194
  Pichani juu na chini ni Baadhi ya washiriki wakipata picha ya ukumbusho na Mrembo wa zamani aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu.
  IMG_0188
  Vijana jijini Dar es Salaam wamepata fursa ya kushiriki katika semina iliyoandaliwa na Mikono Business Consult kwa ajili ya kuwapa hamasa na kuwataka wasikate tamaa ili wajipange na kuangalia nini wanachotaka kukifanya katika maisha yao.

  Semina hiyo iliyoendeshwa na Miss Tanzania wa zamani na Communication Analyst wa Umoja wa Mataifa Tanzania Bi. Hoyce Temu ilifahamika kwa jina la “How To Find Your Destiny” imeonekana kuwavutia washiriki waliohudhuria kutoka sehemu mbalimbali.

  0 0

   Miss Sinza 2012-2013, Brigitte Alfred (kushoto) akimvisha Taji Redd's Miss Sinza 2013, Prisca Element, baada ya kutangazwa mshindi wa taji hilo katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Meeda Club, Sinza jijini Dar es Salaam. 
   Redd's Miss Sinza 2013, Prisca Element (katikati) akiwa na Mshindi wa pili Happynes Maira (kulia) na Mshindi wa tatu, Sarahy Paul, wakiwa na furaha mara baada ya kutangazwa washindi katika shindano lao lililokuwa likishikiliwa na Redd's Miss Sinza na Miss Tanzania 2012-2013, Brigitte Alfred. 
   Warembo wa Redd's Miss Sinza, wakicheza shoo ya ufunguzi wa shindano lao.
  ********************************************
  Na www.sufianimafoto.com
  Prisca Element usiku wa kuamkia leo alitwaa taji la mrembo wa Redds Miss Sinza 2013 katika kinyang'anyiro kilichowashirikishwa jumla ya warembo 12, kwenye ukumbi wa Meeda Club na kurithi taji la kwanza la Redds Miss Tanzania, Brigitte Alfred.

  Haikuwa kazi rahisi kwa Prisca kutwaa taji hilo kutokana na ushindani mkubwa kutoka kwa warembo bora 11 walioshiriki mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Redds Original, Dodoma Wine, Fredito Entertainment, Chilly Willy Energy Drink, Sufiani Mafoto blog, Salut5 na CXC Africa.

  Hata hivyo, Prisca aliweza kuwazidi kete wanzake na kutwaa taji hilo sambamba na zawadi ya Kitita cha Sh. 400,000 zilizotolewa na waandaaji wa mashindano hayo  Calapy Entertainment chini ya ukurugenzi wa Majuto Omary. 

  Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sinza A, Juma Mgendwa alikabidhi zawadi hiyo kwa Prisca ambaye alisema kuwa amefurahi kushinda taji hilo na kazi yake kubwa ni kutwaa taji la Miss Kinondoni.

  "Kwangu ni historia kutokana na ukweli kuwa nimerithi taji la Redds Miss Tanzania Brigitte Alfred, na ninaahidi kufanya kweli katika mashindano yanayofuata na kutwaa mataji ya Miss Kinondoni na vile vile taji la Redds Miss Tanzania, nitashirikiana na waandaji wangu ili kufanya maandalizi ya kina ili kufikia malengo hayo," alisema Prisca.

  Nafasi ya pili ilichukuliwa na Happiness Maira ambaye alizawadiwa sh. 300,000 alizokabidhiwa na Mratibu wa Masoko na Biashara wa kinywaji cha Dodoma Wine, Frank Matonda na zawadi ya mshindi wa tatu ilikwenda kwa Sarahy Paul na kukabidhiwa zawadi ya shs 200,000 na Swabir Abdulrehman ambaye ni Mkurugenzi wa Usambazi wa Kampuni ya TSN Distribution kupitia kinywaji cha Chilly Willy.

  Nafasi ya nne ilichukuliwa na Nicole Michael na tano ilichukuliwa na Nasra Hassan ambao wote walizawadiwa shs 150,000 kila mmoja na  Mkurugenzi wa Mashindano hayo, Majuto. Warembo hao watano wataiwakilisha Sinza katika mashindano ya Miss Kinondoni 2013.

  Mashindano hayo yalishuhudiwa na umati mkubwa wa mashabiki wa urembo na kupambwa na burudani safi ya bendi bora nchini, African Stars maarufu kwa jina la Twanga Pepeta ambayo ilitambulisha baadhi ya nyimbo zake mpya za albamu ya Nyumbani ni Nyumbani.Twanga Pepeta ilifanya mambo makubwa jukwaani huku ikiwa ikitumbuiza kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha mwaka mmoja na zaidi.
   Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (katikati) akiwa na Albert Makoye (kushoto) na Miss Tanzania 2013, Brigitte Alfred, wakishuhudia shindano hilo.
   Shoo ya utangulizi ikiendelea...
   Warembo wakisebeneka na shoo ya ufunguzi.
   Shoo ya ufunguzi, warembo wakiendelea kuwabamba mashabiki wao..

  ..
   Mshiriki, Catrina Laurence, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
    Mshiriki, Nasra Hasan, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
    Mshiriki, Maua Abdul, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
    Mshiriki, Doris Mwaipopo, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
    Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza 2013, Prisca Element, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
    Mshiriki, Jaqueline Robert, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
    Mshiriki, ambaye ni mshindi wa pili, Happynes Maira, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
    Mshiriki, ambaye ni mshindi wa tatu, Sarahy Paul, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
    Mshiriki, Martha Joseph, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
    Mshiriki, Nicole Michael, akipita jukwaani na vazi la ubunifu.
   Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza 2013, Prisca Element na Doris Mwaipopo wakipita jukwaani na vazi la Ufukweni.
   Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza namba 2 Happynes Maira (kulia) na wenzake wakipita jukwaani na vazi la ubunifu.
   Mshiriki, ambaye ndiye Redd's Sinza 2013, Prisca Element, (kulia) na Jaqueline Robert wakipita jukwaani na vazi la usiku.
   Washiriki, wakipita jukwaani na vazi la usiku.
   Warembo wote waliochuana wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kutanzwa warembo watano bora.
   Warembo watano Bora, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi, kutoka (kushoto) ni Sarahy Paul, Nasra Hassan, Nicole Michael, Prisca Element na Happynes Maira.
   Mratibu wa shindano hilo Majuto Omary wa pili (kulia) akiwa meza kuu na Mkurugenzi wa Kamatio ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga na wengineo.
   Kalala Junior, akiwaongoza wanenguaji wa Twanga, kushambulia jukwaa wakati wa shindano hilo.
   Warembo watatu wa Miss Ubungo, wakipita jukwaani wakati wakitambulishwa ukumbini hapo, warembo hawa ndiyo wataungana na warembo wa Miss Sinza kuwania Taji la Miss Kinondoni.
   Mkurugenzi wa Usambazi wa Kampuni ya TSN Distribution, Swabir Abdulrehman (katikati) akimkabidhi zawadi mshindi wa tatu, Sarahy Paul. Kulia ni Meshack Nzowa Ofisa uhusiano wa kinywaji cha Chilly Willy.
   Mratibu wa Masoko na Biashara wa kinywaji cha Dodoma Wine, Frank Matonda, akimkabidhi zawadi mshindi wa pili, Happynes Maira.
  Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Sinza A, Juma Mgendwa, akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza, Redd's Miss sinza 2013, Prisca Element.

  0 0

  WANAWAKE  wa mkoa wa Iringa wameaswa kuachana na mila potofu na kujishughulisha katika ujasiriamali na kujiunga katika vikundi ili kujiinua kiuchumi . 
   
  Hayo yameelezwa na kaimu mkurugenzi wa manispaa ya mkoa wa Iringa bi Immaculate Senje wakati wa uzinduzi wa mradi wa kuwajengea uwezo wanawake katika utawala uliofanyika katika  ofisi za ccm maeneo ya viwanja vya kihesa sokoni. 
   
  Senji amesema kuwa mwanamke anatakiwa ajiamini ili apate uwezo wa kugombea vyeo mbalimbali katika utawala na kuondokana na dhana potofu iliyojengeka hapo nyuma.  
   
  Amesisitiza kuwa mradi huo utakuwa chachu ya maendeleo ya wanawake kwa sababu maendeleo ya mwanamke ni maendeleo ya jamii nzima. 
   
  Kwa upande wake waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na watoto Sophia Simba ambaye alikuwa ni mgeni rasimi katika hafla hiyo amebainisha kuwa serikali inatambua umuhimu wa mradi huo na inashirikiana na mashirika mbalimbali katika kuwainua wajasiriamali.
   

  0 0

  IMG_0566
  Mshindi wa Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu (katikati) akila pozi katika picha ya ukumbusho na mshindi wa pili Latifa Mohamed( wa pili kushoto) na Mshindi wa tatu Irene Rajab ( wa pili kulia) pamoja na mshindi wa nne na wa tano.
  IMG_0555
  Miss Kigamboni 2012 Edda Slyvester aliyemaliza muda wake akimvisha taji mshindi wa shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu (aliyeketi) wakati wa shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Navy Beach Kigamboni jijini Dar.
  IMG_0526
  Miss Kigamboni 2012 Edda Slyvester anayemaliza muda wake akisubiri kukabidhi taji kwa Redd's Miss KIgamboni 2013.
  IMG_0570
  IMG_0588
  Mgeni rasmi katika shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akitoa nasaha zake kwa mshindi wa taji la Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu mara baada ya kuibuka kidedea wa taji hilo ambapo amemtakia Baraka zote kuiwakilisha vyema Kigamboni.
  IMG_0596
  Mgeni rasmi katika shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akimkabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 500,000/mshindi wa taji la Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu iliyotoka mfukoni kwa Mbunge huyo.
  IMG_0601
  Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya akikabidhi zawadi ya fedha taslimu shilingi 250,000/ kwa mshindi wa tatu wa Redd's Miss Kigamboni 2013 Irene Rajab.


  IMG_0605
  Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel katika pozi na mshindi wa pili wa shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Latifa Mohamed mara baada ya kumkabidhi zawadi ya fedha taslim shilingi 300,000/.
  IMG_0612
  Redd's Miss Kigamboni 2013 Magdalena Olotu katika pozi na kitita chake cha fedha taslim shilingi 500,000/ zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile
  IMG_0307
  Picha juu na chini ni Washiriki 11 wa Redd's Miss Kigamboni wakifungua shindano hilo kwa show ya aina yake.
  IMG_0319
  IMG_0203
  Wanenguaji wa Bendi ya FM ACADEMIA maarufu kama Wazee wa Ngwasuma wakitoa burudani wakati wa shindano la kumsaka Redd's Miss Kigamboni 2013 lililofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Navy Beach Kigamboni jijini Dar.
  IMG_0369
  Pichani juu na chini washiriki wa Redd's Miss Kigamboni wakipita jukwaani mavazi ya ubunifu.
  IMG_0372
  IMG_0403
  Washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013 ndani ya Beach Wear.
  IMG_0433
  Mmoja wa majaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa CXC Tours and Safari Bw. Charles Hamka akitangaza majina ya warembo waliofanikiwa kutinga tano bora.
  IMG_0450
  Washiriki wa Redd's Miss Kigamboni waliofanikiwa kutinga tano bora.
  IMG_0485
  Aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye pia ni Somo wa washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013 akiwauliza maswali washiriki waliofanikiwa kutinga tano bora kwenye shindano hilo.
  IMG_0472
  Washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013 wakijibu maswali.
  IMG_0506
  Wadau wa tasnia ya urembo wakishangilia baadhi ya washiriki waliokuwa wakijibu maswali yao bila kutetereka.

  IMG_0606
  Raia wa kigeni kutoka China aliyehudhuria shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 akichukua picha ya ukumbusho ya mshindi wa taji hilo.
  IMG_0586
  Mwandaaji wa shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Angella Msangi (kulia) na Mratibu wa shindano hilo, Somoe Ng’itu pamoja na Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya (kushoto) wakati wa zoezi la kukabidhi zawadi kwa washindi.
  IMG_0220
  Raia wa Kigeni kutoka china ndani Redd's Miss Kigamboni 2013.
  IMG_0222
  VIP Table... Alikuwepo Bw. William Malecela a.k.a LEMUTUZ, Katibu Mkuu wa kamati ya Miss Tanzania, Bw. Bosco Majaliwa, Aliyewahi kuwa Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu (Somo wa washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013), Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel wakati wa shindano la kumtafuta Redd's Miss Kigamboni lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Navy Beach Kigamboni.
  IMG_0238
  Picha juu na chini ni baadhi ya Wadau wa tasnia ya masuala ya Urembo kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar waliohudhuria shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013.
  IMG_0239
  IMG_0517
  IMG_0508
  Nyomi ya Ukweli... Clouds Tv walikuwepo kuhakikisha shindao hilo linaruka Live.
  IMG_0533
  Aliyewahi kushika taji la Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu ambaye pia ni Somo wa washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013 akifurahi jambo na baadhi ya wageni waalikwa.
  IMG_0615
  Wadau wa tasnia ya Urembo wakishow love mara baada ya shindano hilo kumalizika.
  IMG_0227
  Mgeni rasmi katika shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akiwa ameambatana na Meneja Masoko Taifa wa shirika la ndege la Precision Air Bw. Ibrahim Bukenya wakiwasili ukumbini.(Picha zote na Zainul Mzige wa Dewjiblog).
  IMG_0233
  Mgeni rasmi katika shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akisalimiana na Aliyewahi kuwa Miss Tanzania 1999 Hoyce Temu (Somo wa washiriki wa Redd's Miss Kigamboni 2013). Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel.
  IMG_0234
  Mgeni rasmi katika shindano la Redd's Miss Kigamboni 2013 Mbunge wa jimbo la Kigamboni Mh. Dr. Faustine Ndugulile (CCM) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania, Bw. Prashant Patel mara baada ya kuwasili ukumbini.
  IMG_0244
  Meza ya Majaji ikiongozwa na Chief Judge Mwandaaji wa Miss Temeke Bw. Benny Kisaka (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa CXC Tours and Safari Bw. Charles Hamka ( wa pili kulia), Mratibu wa Miss Ilala Juma Mabakila (Kushoto) na Mkuu wa Radio France nchini Bw. Victor Willy (kulia).
  IMG_0284
  Mwandaaji wa mashindo ya Redd's Miss Kigamboni 2013 Angella Msangi akiteta jambo na Chief Judge wa mashindano hayo.

  0 0

  Mshindi wa shindano la BE FORWARD PHOTO CONTEST ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Makelele nchini Uganda,Bwa.Sunday Robert akifanya mahojiano mafupi mbele ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali,namna alivyojishindia gari aina ya Landcruiser Prado kupitia shindano hilo la mtandao wa kijamii wa facebook.
  Meneja mauzo  wa kampuni ya BE FORWARD .JP ambao ni wasafirishaji wa magari kutoka Japan kwenda nchi mbalimbali,Bwa.Eiichi Mizuyama akimkabidhi Bwa.Sunday Robert mfano wa funguo mara baada ya kujishindia gari aina ya   Landcruiser Prado kupitia shindano hilo la  BE FORWARD PHOTO CONTEST lililofanyika kwa njia ya Mtandao wa kijamii wa facebook.

  Bwa. Eiichi Mizuyama alisema kuwa pamoja na kumpata mshindi huyo wataendelea kufanya shindano hilo na kuwapata washindi wengine,katika suala zima la kuhakikisha kampuni hiyo ya BE FORWARD .JP inaendelea kuwajali wateja wake kwa namna mbalimbali,ikiwemo na suala la umakini mkubwa katika kusafirisha bidhaa zao zikiwa salama mpaka mlangoni kwa mteja wao.

  Bwa. Eiichi ameeleza kuwa pamoja na kuwa kampuni hiyo makao yake yako Japan,lakini pia wamefungua tawi la kampuni hiyo hapa nchini katika suala zima la kuwahudumia wateja watakaokuwa wanahitaji huduma zao za uhakika.

  0 0


  Washiriki wanaowania taji la Redds Miss Mwanza 2013, wameanza tambo na majigambo ya kunyakua Taji hilo, huku kila mmoja akieleza sifa za kushinda taji hilo. 

  Wakiongea kwa nyakati Tofauti wanyange hao walioweka kambi katika Hotel ya New Mwanza, wamesema mwaka huu pamoja na uwepo wa ushindani katika baadhi ya mikoa hapa nchini, lakini mkoa wa Mwanza umeonekana kuwa na warembo wenye ushindani zaidi kufuatia kila mrembo kuwa na vigezo vinavyo stahili, kupelekea kushindwa kutabili nani atabeba taji la Redds Miss Mwanza 2013.

  Baadhi ya warembo wamefunguka zaidi na kusema, mikoa ya kanda ya ziwa inayoleta warembo wao katika Kanda mkoani Mwanza, wajipange zaidi kwani Mwaka huu, Taji la kanda litabaki Mwanza na hata taji la Miss Tanzania litarejea Mwanza, kwani historia inaonyesha mkoa wa Mwanza ndio wenye Historia ya kuchukua Taji la Miss Tanzania mara mbili Mfululizo, ambapo Mwaka 2008 alilichukua Nasreem Karim na mwaka 2009 Miriam Gerald akalichukua tena.

  Jumla ya warembo 14 watapanda jukwaani katika ukumbi wa Yatch Club Mwanza siku ya Ijumaa ya terehe 14/06/2013 kuanzia saa 2 usiku.

  Warembo hao ni pamoja na Catherine Steven (21), Rose Peter (22), Victoria Newton (22), Clara Henry (20), Everlyn Charles (22), Esta Perfect (19), Edna Celestine (18), Judith Josephat (20), Lucy Charles (23), Nasra Muna (20), Suzan Ikombe (20), Khadija Suddy (20), Angel Lawrence (22), na Hajra Mohammed (22).

  0 0


  0 0

  Mwanamuziki TID ambaye yuko nchini UK kwenye tour iliyoandaliwa na Victor DJRule BongoUk amefunguka leo kupitia ukurasa wake wa facebook na kumshtumu promoter huyo aliye mleta nchini huma kuto kumlipa baada ya kufanya show kama walivyo kuwa wamekubalina. TID amaandika kifuatacho:

  My mind is not some stupid promota is trying to rob me,am not goin to let it happen am calling my balozi why a Kenyan artist hajamzingua......ndo maana hatuendelei
  Like ·  · Share
  ...

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, akiongoza kikao cha Maalum ya CCM 'Kamati Kuu' kilichokutana jana usiku mjini Dodoma kwa ajili ya kuipokea Rasimu ya Katiba mpya, iliyosomwa hivi karibuni.
   Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe 10/06/2013 chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya.

  Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekutana jana tarehe 10/06/2013 chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete. Kikao hicho kilikuwa cha siku moja na maalum kwa ajili ya kupokea rasimu ya katiba mpya.

  Kamati Kuu inaipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini kwa kazi nzuri na kukamilisha kazi kwa wakati.

  Kamati Kuu imepokea rasimu hiyo na kuelekeza kuwa; Kwa kuwa rasimu hii ni ya kwanza ambayo inapelekwa kujadiliwa tena kwa wananchi kupitia mabaraza mbalimbali ya katiba baada ya kuisha kwa hatua ya kutoa maoni.

   Kamati Kuu imekiagiza Chama kijipange kuijadili rasimu hiyo ndani ya Chama kama baraza la kitaasisi la katiba na kuwataka wanachama na wapenzi wa CCM wajitokeze kwa wingi na kushiriki kwenye mabaraza haya.

  Ushiriki huu wa CCM baada ya kupokea rasimu umekusudia kushirikisha wanachama wetu kwenye ngazi ya tawi, wilaya, mkoa na Taifa.

  Lakini pia Jumuiya za CCM zimekusudia kushiriki kama mabaraza ya Katiba na hivyo kuongeza ushiriki wa wanachama na wapenzi wa CCM katika mchakato huu.

  CCM kama baraza la katiba la kitaasisi litaipitia rasimu iliyowasilishwa kifungu kwa kifungu na kwa kuzingatia maoni ya CCM yaliyotolewa mwanzoni kabisa mwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba, wanachama wetu watashiriki kutoa maoni yao.

  Pamoja na kazi nzuri ya Tume ya Mabadiliko ya katiba, Kamati Kuu inaiomba Tume hiyo kueleza vizuri mchakato mzima kutoka rasimu ya kwanza mpaka rasimu ya mwisho ili kuondoa mkanganyiko kwa wananchi juu ya mchakato mzima hasa baada ya rasimu ya kwanza kutoka.

  Kamati Kuu inawasihi Watanzania kushiriki tena kwenye kutoa maoni kupitia mabaraza ya katiba kwa rasimu ya kwanza, bunge maalum la katiba kwa rasimu ya pili na kupitia kura ya maoni kwa rasimu ya tatu, kwa amani,utulivu na kuvumiliana ili mwisho wa siku tupate Katiba nzuri ya nchi yetu kwa masilahi ya Watanzania walio wengi.  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Moses Nnauye, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo mchana kuhusu kikao hicho cha Kamati Kuu ya CCM, kilichokutana jana usiku.
   Baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, waliohudhuria kikao hicho jana usiku.
   Sehemu ya Wajumbe wa Kikao hicho ambao wengi wao ni Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Mwigulu Nchemba, akiperuzi 'mambo flani' katika simu yake ya mkononi, wakati akiwa ukumbini humo kwenye Kikao cha Kamati Kuu kilichokutana jana usiku.

  0 0
 • 06/11/13--05:30: ANAFUATILIA JAMBO.


 • 0 0

  Waziri wa Nchi ya Ofisi ya Waziri mkuu (Sera,Uratibu na Bunge)William Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa ofisa wa benki ya NMB  Diana Kimaro mara alipotembelea banda la NMB katika maonyesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge.
  Mbunge wa viri maalum, Mh. Zainabu Vulu akipata maelezo kutoka kwa Meneja Huduma za Ziada, Alluthe Nungu wakati walipotembelea banda la NMB.
  Baadhi ya maofisa wa benki ya NMB waliopo kwenye maonyesho ya taasisi za kifedha mjini Dodoma.

  Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale (wa pili kushoto) akitoa maeleza kwa mbunge wa viti maalum, Mathew Mlacha na Mbunge wa Busega, Titus Kamani  juu ya huduma mbambali zinazotolewa na benki ya  NMB.

  Benki ya NMB inashiriki maonyesho ya huduma za kibenki yanayoendelea katika viwanja vya Bunge mkoani Dodoma. Lengo la maonyesho hayo ni kuelezea huduma mbali mbali zitolewazo na benki ya NMB kwa wateja wake.

  0 0


  0 0


  0 0

  Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare akiingia katika chumba cha ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kabla ya kupata dhamana katika kesi yake inayomkabili ya kula njama ya kutaka kumzuru kwa sumu Mhariri wa gazeti la wananchi.
   Wilfred Lwakatare akiwa na furaha pamoja na wakili wake baada kupata dhamana katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni mshtakiwa wa pili katika kesi inayomkali akiwa amerudi rumande baada ya kushindwa kukamilisha masharti ya dhamana.
  Wakili wa Wilfred Lwakatare, Peter Kibatara akiwa katika picha ya pamoja na mteja wake Wilfred  Lwakatare pamoja na wadhamini wake muda mfupi baada ya kuachiwa kwa dhamana na mahakama leo.
  Baada ya kupata dhamana safari ya kuelekea uraiani ilianza.
   Lwakatare akipandishwa katika Pickup.
   Akiwashukuru wanachama na wafuasi wa chama chake.
   Msafara ukiondoka katika maeneo ya Mahakama.
   Wafuasi wa Chadema wakiwa nje ya Mahakama ya Kisutu.
  Ulinzi pia ulikiwa mkali

  0 0

   Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu alivikabidhi vikundi vitano vya Kuweka na Kukopa (VICOBA, kila kimoja msaada wa sh. 500,000 na kikundi cha ulinzi shsirikishi sh. 500,000 za kutunisha mifuko hiyo.
   Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akikumbatiana na mmoja wa wanachama wa kikundi cha Vicoba cha Tuyangatane waliofurahi kupatiwa msaada wa sh. 500,000 za kutunisha mfuko wa kikundi hicho.
   Wanachama wa Tuyangatane wakifurahia kupata hundi hiyo.
   Mtemvu akikipatia kikundi cha Vigoba cha Tumaini msaada wa sh. laki tano
   Kikundi cha Tupendane kikipatiwa laki tano

   Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), kulia, akimkabidhi hundi ya sh. 500,000 Mweka Hazina wa Kikundi cha Saccos cha Pambazuko, Sophia Said, kwa ajili ya kutunisha mfuko wao, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu alivipatia pia kiasi kama hicho vikundi vingine vitano.
   Mtemvu akimvisha filimbi Juma Mlanzi ambaye ni miongoni mwa walinzi shirikishi  56 waliohitimu mafunzi ya kijeshi. Pia walikabidhiwa vyeti.
   Juma Kambona akikabidhiwa cheti baada ya kuhitimu mafunzo hayo
   Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (CCM), wa pili kulia, akimpatia cheti Mwanaisha Gea ambaye amekuwa miongoni mwa vijana 56 waliohitimu mafunzo ya Ulinzi Shirikishi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Azimio, Tandika, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. Mtemvu alikikabidhi pia kikundi hicho cha Ulinzi Shirikishi sh. 500,000 za kuanzishia Saccos yao. Kulia ni Diwani wa Kata ya Azimio, Hamis Mzuzuri.
   Jumanne Jumbe naye akikabidhiwa cheti baada ya kuhitimu mafunzo hayo
   Mma Mkazi wa Kata ya Azimio akilalamika mbele ya Mtemvu, kuhusu mchezo wa Kangha Mbendembende au kangamoko unavyowadhalilidha wanawake ambapo aliomba upigwe marufuku kwa vile auendani na maadili ya kitanmzania.
  Mgambo Said Amiri akilalamikia kitendo cha mabosi wake wa Kituo cha Polisi cha Tambuka Reli kinavyowalea vibaka na majambazi katika eneo hilo.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

  0 0


  Meneja wa Biashara wa benki ya CRDB tawi la UDOM, Danford Muyango akitoa mada kongamano la kimataifa la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuhusu ujasiriamali, ubunifu na uongozi. Vijana wasomi walikutana katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kupata fursa ya kuelimishwa kuhusu ujasiriamali toka kwa watoa mada mbalimbali. Kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AISEC) na kudhaminiwa na Benki ya  CRDB.
  Meneja wa Benki ya CRDB tawi la UDOM, Emmanuel Chaburuma akifafanua jambo kuhusu kongamano hilo. 
   Rais wa AISEC Tanzania, Frank Mushi
   Mwanafunzi wa mwaka wa tatu  UDOM, Lulu Molel akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kongamano hilo. 
   Baadhi ya wanafunzi wakionesha vipaji vyao 
  Wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali wakiwa katika kongamano la kimataifa la vyuo vikuu vya Afrika Mashariki kuhusu ujasiriamali, ubunifu na uongozi. Vijana wasomi walikutana katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kupata fursa ya kuelimishwa kuhusu ujasiriamali toka kwa watoa mada mbalimbali. Kongamano hilo liliandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AISEC) na kudhaminiwa na Benki ya  CRDB.


  0 0
 • 06/11/13--21:49: WARAKA WA MATUKIO CHUMA
 • Nawasalimu kutoka katika ardhi jadidu ya mrefu ukaitwa mlima Kilimanjaro, nikipigwa upepo murua unukiao marashi yakaitwa karafuu, visiwa Unguja nayo Pemba kutengeneza Zanzibar, alipoishi binadamu akawa wa Kwanza, Ngorongoro kati ya vingi vya kujivunia na fahari kuitikia.

  Labda tumekuwa tukisikia neno Kioo cha Jamii, na ama baada tukawa tunapeleka fikra zetu moja kwa moja kwa wale maarufu tunaowaona, kuwasikia ama kuwashabikia, iwe katika Nyanja ya sanaa, burudani, siasa, biashara, teknolojia na mengineyo kadha wa kadha. Lakini je tumewahi kuwaza kuwa Kioo cha Jamii ni kila mmoja wetu kwa nafasi yake, iwapo hutajiheshimu na kuiheshimu jamii uliyopo, kuanzia nyumbani, jirani, shuleni, kazini, chuoni, ibadani ama kwingine popote ulipo, wale wakutizamao watawezaje kukua na kuweza kuwa Kioo cha Jamii kile unachotaka wewe kukiona ama ikiwa hata kwako hukuwahi kukitanabahi?

  Ujana – Maji Ya Moto

  Umeshawahi kuusikia msemo huu, umewahi kukaa chini na kutafakari maana yake na kisha umuhimu wake? Wale tuwaonao leo na kuwakebehi, kuwadhihaki na labda kuwacheka kama si kuwadhalilisha kwa kufikia walipofikia pasipo labda mafanikio ama walichostahili kwa ukubwa leo umri wao, ushawahi kutambua kuwa nao waliwahi kuwa vijana, damu zikichemka, mihemko ikihemka na yaliyomo na yasiyomo kujitwisha na kabla hawajatanabahi jua likazimika na giza kuingia likawafika?

  Umaarufu, Jeuri, Makidai na Maisha Yetu

  Ushawahi kusikia mtoto akisema nataka kuwa maarufu akiwa mkubwa? Si kosa wala si vibaya, lakini swali kubwa unataka kuwa Maarufu kwa sababu gani, ili iweje na kwanini? Ushawahi kusikia ujumbe wa wimbo ukisema chuo kikuu cha umaarufu bongo ni dharau, jeuri, kiburi na majigambo? Umewahi kujiuliza kama wewe ni mmojawapo wa wahanga wa chuo hicho ambacho wakati mwingine ni kigumu mno kuepukika wakati wa ujana na hasa Umaarufu ama Mafanikio yanapokuja katika umri mdogo?

  Maisha YETU, CHAGUO LETU

  Maisha ni uchaguzi na labda huwezi kuchagua uzaliwe katika hali ipi ya kipato, makazi ama ndugu na wazazi, lakini kwa hakika Hatima zetu tunapokuwa na kuwa na maamuzi yetu, NI UCHAGUZI WETU. Ushawahi kufikiri ni wangapi wanaoishi kwa maisha ya kuigiza alimradi waonekane wapo juu, wana fedha nyingi ama mafanikio mengi sana (hata kama mengine bado ni ndoto wanazoota), wajitutumuao kukidhi starehe, matumizi na manunuzi yasiyo na chembe ya uwekezaji bali ufujaji, huku bila kujua wakiendelea kujiongezea msongo wa mawazo, mateso, maisha yasiyo na hata chembe ya furaha ya kweli na mahangaiko yaliyojaa wingi wa makwazo na maigizo? Kuwa mmoja kati yao si lazima, ni CHAGUO LAKO, ni MAISHA YAKO.

  KIPAJI / KIPAWA/ KARAMA vs TAALUMA, MALENGO NA USIMAMIZI

  Labda mara nyingi kumekuwa na kuchanganywa kati ya mtu kuwa na kipaji, kipawa ama karama fulani ikiwezekana hata zaidi ya moja na kusahau umuhimu wa taaluma, malengo na uongozi na usimamizi ili kuweza kuchochea, kulinda na kustawisha mafanikio na uendelevu wa kilichopo kipaji, kipawa ama karama.  Si lazima mtu awe amesoma sana ili afanikiwe na vilevile kusoma haimaanishi moja kwa moja ni lazima ufanikiwe, katika kila jambo tunahitaji upambanuzi yakinifu, KUJITAMBUA, nia madhubuti, usimamizi ama uongozi sahihi na kubwa zaidi kutambua THAMANI YA UWEPO WETU na kuwainua wengine kupitia vipawa, uwezo, mafanikio ama mamlaka yetu.

  Uwiano kati ya NAFSI na MIILI yetu

  Umewahi kuwaza umuhimu wa uwiano kati ya nafsi yaani ile iliyopo ndani yetu na miili yetu yaani kile kila mwanadamu mwingine anachokiona kwa macho kwetu? Mara nyingi tumejikuta tukichanganya sana muonekano wetu mbele za watu, kwa maana ya miili, mavazi, mapambo, mali n.k na kusahau kabisa Nafsi zilizopo ndani yetu, na mwisho wa siku kukosa mawasiliano wala uwiano na kabla hatujajua kutumbukia kwenye matumizi mabaya ya vilevi, madawa, vitu vya kutuchangamsha ama kutuondolea na aibu na kuendelea kutopea kwenye dimbwi la furaha isiyo halisi na kusahau nafsi zilizo ndani yetu kabala hatujajua tukikimbilia umauti badala ya kuishi, ushawahi kutathmini umuhimu wa imani, dini, ushauri na maisha yenye malengo katika kulisha sio tu mwili bali pia nafsi na roho zetu?

  Umaarufu wa leo, kutumika kwa leo, KILIO CHA KESHO

  Kwa nini ukubali kutumika kwa sababu tu ya fedha ama maslahi Fulani na kusahau utu, thamani na uendelezaji za tasnia zilizotuweka pale tulipo? Na kwanini tujisahau kiasi kuwa wale waliotufikisha pale tulipo leo hii tukawasabahi ama kuwajulia hali kwa kiburi, dharau, makidai na jeuri, wale tuliokuwa tukiwasihi watuunge mkono ili tusonge leo wakawa si kitu kwani wako wengi wanaotutambua na kutufahamu (Mwinyi mwenye KITU asie na kitu kinyama cha MWITU?)
  SHUKRANI

  Kwa kila tukifanyacho, tukumbuke kutoa shukrani kwa wale waliotusaidia kwa njia moja ama nyingine, HAITUPUNGUZII BALI INATUONGEZEA zaidi na zaidi, tusikubali kushukuru tu alimradi tumepewa ama kuahidiwa kitu Fulani bali tujifunze kutoa SHUKRANI kwa KILA ANAESTAHILI.


  Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M Chuma ukiniita Mwafrika kwa FAHARI NITAITIKA.

older | 1 | .... | 98 | 99 | (Page 100) | 101 | 102 | .... | 1898 | newer