Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu awataka Jumuiya ya Bohora kuwekeza katika Viwanda nchini

$
0
0
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii.

Waziri mkuu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Kassim Majaliwa ameiasa Jumuiya  ya Bohora kuja kuwekeza katika nyanja ya viwanda kutokana na Sera nzuri zilizowekwa za uwekezaji na mahusiano mazuri yaliyopo baina ya jamii ya mabohora Duniani kote na tangu kuanzishwa kwa Taifa hili.

Waziri  Mkuu amesema hayo jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akifunga Kongamano la Biashara lililoandaliwa na jumuiya ya Bohora nchini na kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu nyerere, Dar es Salaam.

"Mazingira ya nchi ya Tanzania ni rafiki kwa biashara na uhakika wa soko kutokana na eneo ilililopo kijiografia, kwani nchi yetu inahudumia nchi zaidi ya nane kwa kutumia Bandari ya Dar es Salaam, hivyo kuwa sehemu ya kipekee yenye uhakika wa biashara katika ukanda wa Afrika ya Mashariki" amesema Waziri mkuu Majaliwa.

Amesema kwa sasa serikali yake imejipanga kuziwezsha sekta binafsi zote zinazo hitaji kuwekeza Tanzania hasa katika upande wa Viwanda, hivyo kuwaalika wote ambao wana nia ya kuwekeza kuja hapa nchini na watapata msaada wa kutosha.

Kwa upande wake muwakilishi wa Bohora nchini ,Murtza Adam Jee alimuhakikishia Waziri mkuu kuwa kwa maneno waliyoambiwa na Rais pamoja na yeye sasa viwanda vitakuja, kwani wamejua kuwa hapa ni mahali salama pa kufanya biashara na kujenga Viwanda.

Amesema kuwa kila mfanyabiashara aliyefika hapa nchini amejionea mwenyewe kwa namna gani nchi hii ilivyojiandaa katika uchumi wa viwanda .
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana kiongozi wa Jumuiya ya Bohora Badrul Jamal Bhausaad wakati alipokuwa akiwasili katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar Es Salaam.
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyabiashara wa jumuiya wa Bohora kutoka nchi mbalimbali.
Wafanyabiashara wa Jumiya ya Bohora wakimsikiliza Waziri mkuu katika kongamano la Wafanyabiashara.

WAZIRI DK. POSSI: UELEMAVU NA UZEE SIO LAANA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Abdallah Possi akiongea na wageni waalikwa hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es salaam.

……………………………………………………..

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO

Watafiti wa masuala mbalimbali ya kijamii nchini wametakiwa kuhakikisha wanafanya tafiti ambazo zitawasaidia watu wenye ulemavu kupata vifaa saidizi ili waweze kumudu kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Walemavu Dkt. Possi Abdallah alipokuwa akizindua taarifa mpya ya utafiti inayobainisha hali halisi ya ulemevu na uzee nchini jijini Dar es salaam.

“Serikali inafarijika inapoona watu wanafanya utafiti ili kuwasaidia watu wenye ulemavu waweze kupata vifaa saidizi na ni kitu gani kifanyike ili NGOs ziweze kujikwamua kiuchumi na kuwasaidia wenye mahitaji” alisema Dkt. Possi.

Kuhusu suala la unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu, Dkt. Possi amesema kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu hapo tayari kuona wananchi wananyanyapaliwa huku akisisitiza kuwa watu wote ni sawa na ofisi hiyo ina “zero tolerance” kwa watu wanaowanyayapaa mlemavu.

Katika masuala ya kisheria kwa watu wenye ulemavu, Dkt. Possi amesema kuwa inapotokea mlemavu au mzee amefanyiwa kosa taarifa itolewe mara moja ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya waliofanya makosa hayo na haki iweze kutendeka.

Naibu Waziri Dkt. Possi pia amezitaka Asasi zinazoshughulika na watu walemavu wafanye kazi kwa pamoja ili kuwasaidia walengwa ambao ni walemavu, watoto na wazee na kuwataka kutumia fursa waliyonayo ya kupata msaada kisheria bure kutoka kwenye taasisi za sheria ikiwemo Chama cha Mawakili (Tanganyika Law Society), TAMWA pamoja na taasisi nyingine za kisheria wakati masuala ya jianai amewataka wayapeleke kwenye polisi kwa hatua zaidi za kisheria huku akisisitiza kumshirikisha inapobidi kufanya hivyo.

Akitoa maelezo ya utafiti huo wakati wa uzinduzi, mtafiti kutoka Taasisi ya Afya Ifakara (IHI) Bakar Fakih amesema kuwa utafiti huo umewashirikisha watafiti rika mbalimbali wakiwemo wazee na watu wenye ulemavu na kubainisha kuwa bado kuna imani potofu kwenye jamii juu ya wazee na watu wenye ulemavu.

Utafiti huo unaoongozwa na kaulimbiu “Ulemavu na uzee sio laana” umebainisha kuwa watu wenye ulemavu na wazee nchini wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupata elimu, huduma za afya, unayanyasaji wa kingono na kuvunjika kwa ndoa, kutokujaliwa na familia pamoja na kutengwa kwa watu wenye ualbino kutokana na mila potofu.

Kwa upande wake mtafiti rika Blandina Isaya amesema kuwa walemavu waachwe wafanye maamuzi yanayohusu maisha yao ikiwemo masuala ya ndoa wawe huru kuchagua wenza wao badala ya kuchaguliwa na familia zao kwa kuwa wanahaki kama watu wengine wasio na ulemavu.

Katika kuhakikisha familia zinakuwa imara kiuchumi, Blandina amesema kuwa familia zenye watu wenye ulemavu na wazee wapewe elimu ya ujasiriamali ili waweze kuwa na uwezo wa kuendesha maisha yao kwa kulea familia ipasavyo na kuomba Seriklai za mtaa ziwe na takwimu za wazee na watu wenye ulemavu.

Rais Magufuli apokea Mchango wa Dola 250,000 kutoka Jumuiya ya Madhehebu ya Bohora

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakimshukuru Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016 .

Jumuiya ya Madhehebu ya Dawoodi Bohra imetoa mchango wa Dola za Marekani laki mbili na nusu (Usd. 250,000) sawa na Shilingi Milioni Mia Tano Arobaini na Tano za Kitanzania (Ths. 545,000,000) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea katika Mkoa wa Kagera tarehe 10 Septemba, 2016.

Kiongozi Mkuu  wa Madhehebu ya Bohra Duniani Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin amekabidhi mchango huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, walipokutana na kufanya Mazungumzo leo tarehe 13 Oktoba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kati ya fedha hizo Dola za Marekani laki moja (Usd. 100,000) zimetolewa na Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mwenyewe, Dola za Marekani laki moja (Usd. 100,000) zimetolewa na Viongozi wengine wa Madhehebu ya Bohra na Dola za Marekani Elfu Hamsini (Usd. 50,000) zimetolewa na wana Jumuiya ya Bohra wa Tanzania.

Pamoja na kutoa mchango huo, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin ameahidi kuwa Jumuiya hiyo ambayo inamiliki hospitali kubwa zilizopo maeneo mbalimbali duniani ikiwemo India, itajenga hospitali hapa nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu.

Pia Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin ameahidi kuwa Jumuiya ya Bohra itatoa udhamini wa masomo ya udaktari kwa vijana wa Tanzania na pia itadhamini matibabu kwa wagonjwa 20 watakaopelekwa nchini India kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kwa Upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemshukuru Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na Jumuiya nzima ya Dawoodi Bohra kwa mchango walioutoa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera na pia kwa kufanyia mkutano wao wa mwaka hapa nchini uliowaleta wageni takribani 31,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani.

“Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin nakushukuru sana kwa kuja hapa nchini kwetu na kutuletea mkutano huu mkubwa, ujio wenu umeimarisha uhusiano kati ya Bohra na Tanzania na pia umechangia uchumi wa nchi yetu.

“Nakushukuru pia kwa nia yenu ya kujenga hospitali hapa nchini, kuwasomesha madaktari na kudhamini matibabu ya wagonjwa huko India, naomba nikuhakikishie kuwa mchango mlioutoa utatusaidia sana na pia mkijenga hospitali na kufundisha madaktari mtakuwa mmesaidia kuokoa fedha nyingi ambazo Serikali ingetumia” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewaalika wanajumuiya ya Dawoodi Bohra kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo viwanda, kilimo, usafirishaji, madini na uvuvi na amewahakikishia kuwa Serikali itawaunga mkono wote watakaokuwa tayari kuja kuwekeza Tanzania.

Jumuiya ya Madhehebu ya Dawoodi Bohra Duniani imeadhimisha mwaka mpya wa Kiislam na kumbukumbu ya kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (S.A.W) aitwaye Imamu Hussein ambapo maadhimisho yake ya kidunia yaliyoambatana na tamasha la zaidi ya wiki mbili yamefanyika hapa nchini kuanzia tarehe 01 Oktoba, 2016 hadi tarehe 11 Oktoba, 2016.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
13 Oktoba, 2016

Vijana jitokezeni kupima ukimwi kujenga taifa lililo na afya bora – Mkwinda

$
0
0
 Mratibu kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Bw. Joseph Muhoja (kulia) akizungumza na vijana wenye umri chini ya miaka 18 kuhusu namna kijana anavyopaswa kujitambua na maambukizi ya virusi vya ukimwi leo katika viwanja vya Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.
Baadhi ya vijana wenye umri chini ya miaka 18 wakifuatilia mada iliyokua ikitolewa na Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi leo katika viwanja vya Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.
Mjumbe kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Bibi. Happiness Malamala (kulia) akitoa elimu ya namna ya kutumia kinga kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa vijana waliotembelea banda la NACOPHA leo katika viwanja vya Sabasaba kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoani Simiyu.
Mwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Bw. Hamidu Mkwinda (kulia) akitoa elimu ya kujitambua na namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi wakati wa ziara ya wajumbe kutoka NACOPHA walipotembelea katika kituo cha mabasi cha Somanga leo katika Mkoa wa Simiyu kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.
Vijana wakifanya mashindano ya kula biskuti na kunywa soda wakati wa ziara ya wajumbe kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) walipotembelea kituo cha mabasi cha Somanga kutoa elimu ya nanma ya kujitambua na kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi leo Mkoani Simiyu kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru.

…………………………………………………

Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Vijana nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ili waweze kujitambua na kupata mbinu mbadala zitakazowazesha kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi ili kujenga taifa lililo na afya bora.

Hayo yamesemwa na Mwezeshaji kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Bw. Hamidu Mkwinda alipokua akizungumza na vijana waliojitokeza kupata elimu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi wakati wa wiki ya vijana kitaifa na kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru leo katika Viwanja vya Sabasaba Mkoani Simiyu.

“Vijana wanatakiwa kujitambua na kujua haki zao ili wasije wakaangukia katika wimbi la ulaghai na anasa ambazo zitawapelekea kutokufikia malengo yao na wakati mwingine kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi bila kutarajia” amesema Bw. Mkwinda.

Aidha Bibi. Happiness Malamala kutoka NACOPHA amewataka vijana kutokukata tamaa pale wanapojitambua kuwa wamepata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwani kuwa na virusi vya ukimwi sio mwisho wa maisha bali watambue kwamba virusi vya ukimwi ni kama magonjwa mengine yasiyotibika kama vile kisukari, kansa na presha.

Naye Mratibu kutoka Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (NACOPHA) Bw. Joseph Muhoja amesema kuwa NACOPHA inashiriki katika Wiki ya Vijana kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru kuhakikisha vijana wanajua haki zao za msingi hususani vijana wa kike waliopata jukumu la kuwa wazazi katika umri mdogo wajue aina ya ukatili wa kijinsia na jinsi ya kukabiliana nao.

Bw. Muhoja amesema kuwa NACOPHA imejipanga kutoa amasa kwa vijana kuhusu ushauri nasaha na kupima ili wajue hali yao ya kiafya na jinsi ya kujikinga na kuwakinga wengine, lakini pia kupitia maonesho haya vijana wanapata elimu ya afya ya uzazi na makuzi ili vijana waweze kujikinga na mimba zisizotarajiwa au kupata watoto katika wakati usio sahihi.

NACOPHA kupitia ufadhili wa watu wa Marekani (USAID) inatekeleza mradi wa SAUTI YETU, mradi unaojihusisha na masuala ya ufuatiliaji, utendaji wa serikali na masuala ya utawala bora, na pia kuwajengea uwezo wananchi waishio na VVU na UKIMWI ili sauti zao zisikike, waweze kushirikishwa katika mambo ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wa kutambua haki za msingi, kisheria na kuchangia mawazo katika utekelezaji wa sera na sheria mbalimbali.

MHE ANASTAZIA WAMBURA ATEMBELEA JAKAYA MRISHO KIKWETE YOUTH PARK NA KUBARIKI MASHINDANO YA YOUTH DEVELOPMENT CUP 2016

$
0
0
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akipiga mpira ikiwa ni ishara ya kubariki fainali za mashindano ya Youth Development Cup yaliyofanyika katika viwanaja vya kituo cha michezo Jakaya Mrisho Kikwete leo Oktoba 13, 2016.
yuo9
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya vijana ya Home Team Academy  kutoka Temeke kabla ya kuanza kwa fainali ya mashindano ya Youth Development Cup 2016 leo Oktoba 13,2016.
yuo2
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na Mkurugenzi wa Ufundi wa kituo cha Michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park Bw. Ray Power kilichopo Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam leo Oktoba 13,2016.
yuo3 
yuo4
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akitembelea na kujionea viwanja mbalimbali vya michezo katika kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park  kilichopo Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam huku akipata  maelezo kutoka kwa  Mkurugenzi wa Ufundi wa kituo hicho Bw. Ray Power leo Oktoba 13,2016.
yuo5
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Alex Nkenyenge akiuliza maswali kwa Mkurugenzi wa Ufundi wa kituo cha michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Bw. Ray Power  ili kujua mambo muhimu kuhusu kituo hicho leo Oktoba 13,2014.
yuo6
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na wachezaji wa timu ya vijana ya Home Team Academy kutoka Temeke kabla ya kuanza kwa fainali ya mashindano ya Youth Development Cup 2016 leo Oktoba 13, 2016.
yuo7
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akisalimiana na wachezaji wa timu ya vijana ya Bom Bom kutoka Ilala kabla ya kuanza kwa fainali ya mashindano ya Youth Development Cup 2016 leo Oktoba 13, 2016.

TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA UMMA KUTOKA MKOA WA MWANZA

$
0
0
Tarehe 12.10.2016 majira ya saa 16:35 katika eneo la busenga “a” kata ya Buswelu wilaya ya Ilemela jiji na mkoa wa Mwanza, askari walifanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la juma biria miaka 42, mfanya biashara na mkazi wa mtaa wa Busenga akiwa na vifaa vya kutengeneza noti bandia ambavyo ni kemikali ikiwa ndani chupa kubwa, sabuni ya maji iliyowekwa ndani ya chupa ndogo, karatasi zilizokatwa mfano wa noti ya shilingi elfu kumi pamoja na unga ambao bado haujafahamika ni wa kitu gani, kitendo ambacho ni kinyume na sheria na taratibu za nchi .

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa tajwa hapo juu akishirikiana na wenzake amekuwa akifanya shughuli hiyo ya uhalifu, ndipo zilipatikana taarifa za kiintelejensia kuhusiana na uhalifu huo, ndipo askari waliweza kufuatilia na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa huyo.

Aidha kwa sasa jeshi la polisi lipo katika mahojiano na mtuhumiwa, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili hatua za stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake. aidha jitihada za kuwasaka wenzake wanaodaiwa kushirikiana na mtuhumiwa huyu katika uhalifu huo bado zinaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi ahmed msangi anatoa rai kwa wakazi wa jiji na mkoa wa mwanza, akiwataka kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na wahalifu wa aina kama hii, ili waweze kufikshwa katika vyombo vya sheria, kwani jeshi la polisi linaamini endapo wananchi wataendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi lao, tutaweza kukomesha uhalifu katika mkoa wetu.

imetolewa na:

DCP: Ahmed Msangi

Kamanda wa polisi (m) Mwanza


WAKAZI WA WILAYA YA CHEMBA KUADHIMISHA MIAKA 17 YA KIFO CHA BABA WA TAIFA KWA KUSHIRIKI KUFANYA KAZI ZA KIJAMII KWA PAMOJA

$
0
0
Katibu tawala wilaya ya Chemba,Ndugu Nyakia Ally
Katika kuadhimisha kumbukizi ya miaka 17 ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere, Maadhimisho ya kilele cha wiki ya Vijana pamoja na Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru hapo kesho tarehe 14/10/2016. 

Hayo yameelezwa na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Ndugu Nyakia Ally,alipokuwa akizungumza na Globu ya Jamii kwa njia ya Simu,leo.

Nyakia amesema kuwa Wilaya ya Chemba imepanga kufanya yafuatayo katika kuenzi harakati na juhudi za Muasisi huyu wa Taifa letu.

Ikumbukwe Mwl Nyerere katika maisha yake alipigania ukombozi wa Tanzania katika 1.  Kupambana na adui ujinga. 2. Adui Maradhi. 3. Adui Umasikini na 4. Adui njaa.

"Hivyo Wilaya yetu itaadhimisha siku hii kwa kushiriki kwa kusafisha eneo itakapojengwa Zahanati ya Wilaya ya Chemba na wananchi watachangia matofali ya ujenzi wa Zahanati hiyo. Vile vile zoezi hilo litaendana na uchangiaji wa damu katika benki ya damu hapa Wilayani Chemba",alisema Nyakia

Amesema kuwa baada ya kufanyika kwa shughuli mbalimbali za kijamii,baadae Kutakuwepo na Michezo mbalimbali ya kuvuta kamba  baina ya Watumishi wa Serikali na Wananchi wa Kijiji cha Chemba,Kukimbiza kuku na mwisho kutakuwa na mchezo wa bao kati ya Wazee wa hapa Chemba katika kumuenzi Mwl Nyerere ambaye alikuwa mpenzi mkubwa wa mchezo huu.

Amesema kuwa Washindi katika mchezo wa kuvuta kamba na nao watajinyakulia zawadi ya Mbuzi na ule wa kukimbiza kuku kwa upande wa wanawake na wanaume watajinyakulia kuku watakaye mkamata.

Katibu Tawala wamewaomba wananchi wa Chemba na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi bila kukosa katika tukio hili la kipekee la kuenzi juhudi za Baba wa Taifa katika kuwaletea wananchi maendeleo majira ya saa 2:00 asubuhi ya kesho katika viwanja vya michezo shule ya Msingi Chemba.

TAZAMA PICHA MBALIMBALI ZA MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI ALIPOTEMBELEA KITUO CHA WAZEE FUNGAFUNGA MKOANI MOROGOROZEE.

$
0
0
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na viongozi wa mkoa mara baada ya kuwasili mkoani Morogoro kwa ajili ya ziara ya kikazi ya kutembelea vituo vya kulea wazee na watu wasiojiweza vya Chazi na Fungafunga vyote vilivyopo Mkoani huko.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni Ikulu Ndogo Mkoani Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na baadhi ya watoto alipofika kutembelea makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisaini kitabu cha wageni alipofika katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro.
Baadhi ya Viongozi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro wakimuonesha Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli maeneo ya miradi yaliyo katika makazi hayo.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akisalimiana na wazee wanaoishi katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro.
 Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Regina Chonjo akiongea na wazee makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga  na kuwataka viongozi wa kituo hicho kuwasiliana mara kwa mara na viongozi wa mkoa pale wanapohitaji msaada ili kusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili wazee katika kituo hicho.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akicheza ngoma ya asili na baadhi ya viongozi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga
Kaimu Afisa Mfawidhi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw.Rashid Omar akishukuru Mama Janeth Magufuli kwa uamuzi wake wa kuja kukitembelea kituo hicho kwani ni faraja kwa wazee na watu wenye ulemavu hasa kwa kupokea msaada wa chakula.
Kaimu Afisa Mfawidhi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw.Rashid Omar akimkabidhi Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli hotuba.
Baadhi ya Wazee wakimsikiliza Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na Wazee katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro ambapo amezitaka Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa kadri iwekenavyo.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi ya Chakula Mwenyekiti wa Wazee wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw. Joseph Kaniki.
Mwenyekiti wa Wazee wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga Bw. Joseph Kaniki. Akimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa msaada wa chakula na kuwataka wadau wengine kuiga mfano huo kwani kusaidia wazee ni kulisaidia taifa pia.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akipokea zawadi ya kuku kutoka kwa mmoja wa kiongozi wa makazi ya wazee ya Fungafunga.
Baadhi ya Nyumba Wanazoishi wazee katika Makazi ya Fungafunga yaliyopo Manispaa ya Morogoro.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akibadilishana mawazo na mmoja ya wazee katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mama Janeth Magufuli akiwaaga baadhi ya Wazee na watu wenye mahitaji maalum katika makazi ya Kulea Wazee na watu wenye mahitaji maalum ya Fungafunga
PICHA/HABARI NA HASSAN SILAYO


Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu kwa kadri iwekenavyo.

Hayo yamesemwa na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli wakati akiongea na wazee na watu wenye ulemavu alipotembelea kituo cha wazee na watu wenye mahitaji maalum cha Fungafunga kilichopo Mkoani Morogoro.

“Kundi hili ni moja kati ya makundi yaliyokatika hatari kubwa sana na kwa kiasi kikubwa ni kundi ambalo limekuwa likisahaulika sana na kuwafanya kukosa mahitaji muhimu wanayopaswa kuyapata hivyo rai yangu kwa Wizara, Taasisi za Serikali Mashirika ya ndani na nje ya nchi, watu binafsi na wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza katika kuwasaidia wazee na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha kuhakikisha wanapata huduma zote muhimu”. Alisema Mama Janeth.

Pia Mama Janeth alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli inatambua kuwa wazee ni rasilimali na hazina kubwa katika kukuza uchumi wa nchi hivyo serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha wazee na watu wasiojiweza wanapata huduma zote muhimu.

Aidha, Akiongea wakati wa kukabidhi msaada wa Mchele kilo 875,Unga Kilo 875, Sukari Kilo 175, Maharage Kilo 350  na Mafuta ya watu wenye ulemavu wa ngozi boksi 1 Mama Janeth aliwataka viongozi wa kituo hicho kuhakikisha chakula hicho kinawafikia walengwa kama ilivyopangwa.

Akiongea wakati akimkaribisha Mama Janeth Magufuli, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bi. Regina Chonjo aliwataka ameataka viongozi wa kituo hicho kuwasiliana mara kwa mara na viongozi wa mkoa pale wanapohitaji msaada ili kusaidia kuondoa changamoto zinazowakabili wazee katika kituo hicho.

Naye Kaimu Afisa Mfawidhi wa Kituo hicho Bw.Rashid Omar alimshukuru Mama Janeth Magufuli kwa uamuzi wake wa kuja kukitembelea kituo hicho kwani ni faraja kwa wazee na watu wenye ulemavu hasa kwa kupokea msaada wa chakula.


RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AAGANA NA KIONGOZI MKUU WA MADHEHEBU YA BOHORA DUNIANI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akisalimiana na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiongea na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake wakimsikiliza Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiongea jambo Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiongea na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakipokea mfano wa hundi ya dola za kimarekani Laki moja kama msaada toka kwa jumuiya ya Bohora Duniani kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani kagera toka kwa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakipokea mfano wa hundi ya dola za kimarekani Laki moja kama msaada toka kwa Jumuiya ya Bohora Tanzania kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera toka kwa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakipokea mfano wa hundi ya dola za kimarekani 50,000 ukiwa msaada wa Jumuiya ya Bohora Dar es salaam kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera toka kwa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa katika dua na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakimshukuru Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016 .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakiagana na Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohora duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 13, 2016

NAIBU WAZIRI MPINA AMUWAKILISHA MAKAMU WA RAIS KATIKA MKUTANO WA CLIMATE CHANGE JIJINI MWANZA

$
0
0
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina kushoto aliyeshika nafaka mkononi, akipata maelezo toka kwa Bi. Leokadia Vedastus Program manager wa kikundi cha sauti ya wanawake Tanzania toka Ukerewe, nafaka iayotengenezwa kwa kuzingatia utunzanji wa mazingira. Naibu Waziri Mpina alimuwakilisha Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hasan katika mkutano ulohusu mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi katika ziwa Victoria, jijini Mwanza Leo.
Picha ya Pamoja ya Washiriki wa Mkutano ulohusu mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi katika ziwa Victoria ambapo Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, alimuwakilisha Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hasan Mkutano huo umefanyika jijini Mwanza leo. (Picha na Evelyn Mkokoi)

KIPINDI CHA WAZIRI MKUU ALIPOTEMBELEA CHUO CHA MUHIMBILI MLOGANZIRA KIBAMBA

Mbunge wa Mkuranga aendelea na ziara ya kijiji kwa kijiji kusikiliza na kutatua kero zao.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Mkuranga.

Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, amesema kuwa anataka wananchi wamtume cha kuzungumza bunge lijalo juu ya changamoto zao.

Hayo ameyasema katika ziara ya kijiji kwa kijiji katika vijiji Picha ndege pamoja na vikindu, amesema wananchi bila kumtuma hana cha kuzungumza.

Amesema muda wake pasipo kuwa na Bunge utatumika katika kusikiliza kero za wananchi ambao ndio dhamana yake ya ubunge.Ulega amesema wananchi katika kutekeleza  miradi ni lazima wachangie ndipo serikali iweze kuunga mkono.

Aidha katika changamoto ya umeme ameliomba shirika la Umeme nchini kumaliza changamoto hiyo kutokana na kusubiri kwa muda Mrefu.
 .mbunge wa mkuranga, Abdallah Ulega akitoa Maelezo kwa kaimu meneja wa tanesco juu ya kushughulikia changamoto ya umeme.
Mbunge wa mkuranga ,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha vikindu, mkuranga.


ZIARA YA MFALME WA MOROCCO NCHINI KUKUZA DIPLOMASIA YA UCHUMI

$
0
0

Na. Immaculate Makilika, MAELEZO

Serikali imesema kuwa ziara ya Mfalme wa Morocco nchini Mohammed  wa VI ina lengo  la kukuza diplomasia ya uchumi kati ya nchi hizi mbili, na kamwe haitaathiri  msimamo wa Tanzania katika mgogoro unaoendelea kati ya Morroco na Sahara Magharibi.

Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambapo taarifa hiyo imesisitiza kuwa ziara hiyo itakuza ushirikiano katika masuala ya uchumi.

“ Lengo la ziara hiyo ni kukuza zaidi uhusiano kati ya Tanzania na Morocco hususani katika masuala ya kiuchumi na kibiashara kwa faida ya watu wa nchi hizi mbili, na kamwe  haitaathiri msimamo wa Tanzania katika mgogoro unaoendelea kati ya Morocco na Sahara Magharibi”.

Hata hivyo taarifa hiyo imesisitiza kuwa , msimamo wa Tanzania ambao umekuwa ukisimamiwa na Awamu zote za uongozi  zilizopita na Awamu hii, upo sambamba na ule wa Umoja wa Afrika (AU) unaoutaka Umoja wa Mataifa (UN) ambao ndio wamepewa jukumu la kusimamia mgogoro huo, kuongeza kasi ya kutatua mgogoro huo ili  kupata suluhu ya kudumu.

Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco anatarajiwa kuwasili nchini Oktoba 19 mwaka huu kwa ziara ya siku nne, ambapo atatembelea Zanzibar pamoja na Hifadhi ya Ngorongoro kwa ajli ya kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Aidha, mara baada ya kumaliza ziara yake nchini, Mfalme Mohammed VI atatembelea nchi za Rwanda, Ethiopia na Kenya.

KAMANDA CHOUGHULE: VIJANA TUMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE KWA KUFANYAKAZI ZA KUJIAJIRI

$
0
0
Sharik Chughule
Mwenyekiti wa CCM, Shina la Pamba Road, Dar es Saaam, Sharik Choughule, amewaasa vijana kumuenzi Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa kufanya kazi za kujiajiri.

Amesema, kufanya hivyo kutawawezesha vjana wengi kuwa na ajira za uhakika, badala ya kusubiri ajira za serikali au taasisi mbalimbali kwa kuwa nafasi za ajira katika sekta hizo ni chache huku mahitaji yakiwa ni makubwa.

Choughule ambaye pia ni Kamanda wa Vijana Kata ya Kivukoni, Dar es Salaam, amesema hayo leo wakati akizungumzia kumbukumbu ya miaka 17 ya Kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambayo Maadhimisho yake yanafayika leo Kitaifa mkoani Simiyu kwa shughuli ya kuzima Mwenge.

Amesema, ili kuweza kufanya kazi za kujiajiri, vijana ni lazima kwanza kuondoa woga, ili kujiamini kuwa wanaweza kwa kuwa ajira binafsi zipo nyingi hasa ikizingatiwa kwamba wengi siku hizi wana elimu za kutosha hadi za viwango vya Chuo Kikuu.

"Vijana lazima tujiamini kwa kuwa sisi ndiyo tegemeo la taifa, hivyo siyo busara vijana kuanza kulalamika kuwa hatuna ajira kwa lengo la kutarajia kuwa Taifa ndilo tulitegemee kutupatia ajira, hayo si mawazo mwafaka kwa afya ya nchi yetu", alisema Shoughule.

Alisema, hatua ya vijana kuanza kuweka kisingizio cha ukosefu wa ajira za kuajiriwa, kinawadumaza vijana na kukosa maamuzi ya kubuni au kukosa ubunifu wa kubuni miradi aina tofauti tofauti kwa manufaa yao.

Choughule alisema, hivi sasa umefikia wakati wa vijana kuachana na mawazo mgando, kwa wasababu baadhi ya vijana ambao wameonyesha uthubutu, wameweza kujiajiri katika sekta za mitandao ya mawasiliano ambayo ni sekta imeenea duniani kote.

Alisema, mfano mzuri wa kuigwa ni vijana walipo Jeshi la Kujenga Taifa, JKT, ambao wamekuwa wakionyesha kufanya kazi nyingi ambazo siyo za kuajiriwa ikiwemo kuanzisha shughuli za kilimo cha kisasa, ufugaji na ufundi wa aina mbalimbali ikiwemo kutengeneza samani na ujenzi wa nyumba.

Choghule amesema, hatua ya vijana kufanyakazi za kujiajiri siyo tu watakuwa wamemuenzi Baba wa taaifa Mwalimu Nyerere, lakini pia watakuwa wamemuunga mkono Rais Dk John Magufuli katika azma yake ya kukuza uchumi wa taifa kwa kaulimbiu yake ya 'Hapa kazi tu'.

TEMESA SHINYANGA YAZIDAI MILLIONI 163 HALMASHAURI, MASHIRIKA NA TAASISI ZA SERIKALI.

$
0
0
Mtendaji Mkuu TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (wa pili kulia) akitoa maelekezo kwa watendaji wa kituo cha Shinyanga alipotembelea kituoni hapo katika ziara yake katika vituo vya TEMESA Kanda ya Ziwa.
Mtendaji Mkuu TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (menye shati la rangi ya bluu)akiangalia gari la TANESCO Shinyanga, linaloshikiliwa na TEMESA Shinyanga kwa sababu ya deni la Sh Millioni 96 kushoto ni Meneja wa TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki Lukali.Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Shinyanga.

Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu(kushoto) akisikiliza taarifa kuhusu kituo cha TEMESA Mkoa wa Shinyanga kutoka kwa Meneja wa TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki Lukali, alipotembelea kituoni hapo katika ziara yake katika vituo vya TEMESA Kanda ya Ziwa.
Mtendaji Mkuu TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu akikagua chumba cha kuhifadhia vipuri vya matengenezo ya magari TEMESA Mkoa wa Shinyanga, alipotembelea kituoni hapo katika ziara yake katika vituo vya TEMESA Kanda ya Ziwa.
………………

Na Theresia Mwami TEMESA Shinyanga

Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Mkoa wa Shinyanga inazidai Halamashauri, Mashirika na Taasisi za Serikali mkoani humo jumla ya shillingi 163,269,269.82 kutokana na kupata huduma ya matengenezo ya magari.

Katika taarifa yake kwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Meneja wa TEMESA Shinyanga Mhandisi Riziki Lukali amesema madeni hayo ni ya mwaka wa fedha 2016/2017 na wamesha wasilisha madai yao kwa wahusika na wanasubiri kulipwa.

Mhandisi Riziki Lukali aliwataja wadaiwa hao kuwa ni TANROADS Shinyanga Sh 24,193,733.21, TANESCO Shinyanga Sh Milioni 96,267,987.63, DED Kishapu Sh 6,753,735.03, RAS Shinyanga Sh 2,742,097.36, KUWASA Kahama Sh 9,855,714, KASHUWASA Shinyanga Sh 1,992,430, TBA Shinyanga Sh 5,103,062.56, Mahakama Kuu Shinyanga Sh 5,470,628.91, Uhamiaji Shinyanga Sh 896,333.63, DAS Kishapu Sh 1,071,573.57, NSSF Shinyanga Sh3,798,184 pamoja na RMO Shinyanga shilingi 5,123, 789.92 milioni na jumla ya madeni hayo yote ni Sh 163,269,269.82.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amefurahishwa na utaratibu wa TEMESA Shinyanga wa kuzuia magari ya taasisi, halmashauri na mashirika yanayodaiwa na kituo hadi hapo yatakapolipiwa gharama za matengenezo.

Na pia amemuagiza Meneja wa TEMESA Shinyanga kutoa taarifa kwake kama kuna Taasisi za Serikali ambazo hukiuka Sheria kwa kutopeleka magari yake kwenye karakana za TEMESA na kupeleka magari hayo kwenye karakana binafsi zilizomo mkoani humo ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Dkt Mgwatu amesisitiza watumishi kuendelea kujituma kufanya kazi kwa weledi na kwa ubora zaidi ili karakana iweze kuvuta wateja wengi na kuongeza pato la kituo.

Aidha TEMESA Shinyanga kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 kituo kimepanga kukusanya jumla ya Sh 458,160,000 kutokana na madeni na huduma zinazoendelea kutolewa kituoni hapo.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kutembelea vituo vya TEMESA vilivyopo Kanda ya Ziwa ili kubaini changamoto mbali mbali zilizomo na kuzitafutia ufumbuzi.

WAZIRI MBARAWA AWAPIGA TAFU WAHANDISI WASHAURI

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Kivuko cha MV. Chato, Eng. Fredinand Mishamo (Wa kwanza kushoto), alipokagua kivuko hicho, wilayani Chato, mkoani Geita. 
Fundi wa Kivuko cha Mv Chato kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme Nchini (TEMESA), Bw. Mbondo Jackson, akimweleza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, namna injini ya Kivuko cha MV. Chato inavyotumia mafuta, alipotembelea kivuko hicho, wilayani Chato, Geita. 
Muonekano wa Kivuko cha MV Chato kilichopo Wilaya ya Chato mkoani Geita. 
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga, akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (mwenye shati la blue), ramani inayoonesha mtandao wa barabara za mkoa wa Geita, alipomtembelea Ofisini kwake. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisisitiza jambo kwa wafanyakazi wanaofanya kazi kwenye Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (hawapo pichani), alipoongea nao Mkoani Geita. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akisalimiana na wafanyakazi wa Sekta ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, mara baada ya kuongea nao Mkoani Geita. 



Serikali kupitia Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), imeanzisha Kitengo maalum cha Wahandisi Washauri (TECU), ili kuwajengea uwezo wahandisi wazawa kusimamia miradi ya ujenzi wa barabara nchini na hivyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha ambacho kingetumika kuwalipa wahandisi washauri kutoka nje ya nchi. 

Akizungumza mkoani Geita mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga-Biharamulo yenye urefu wa KM 112 ambayo pia inasimamiwa na Wahandisi Washauri Wazawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema mpaka sasa wahandisi wazawa wanasimamia miradi mbalimbali ya barabara katika mikoa ya Kagera, Mwanza, Geita na Kilimanjaro ambapo kupitia miradi hiyo serikali imeokoa dola za kimerani milioni mbili ambazo zingetumika kulipa wahadisi kutoka nje ya nchi. 

“Nitahakikisha ninakijengea uwezo kitengo hiki ili kuweza kuokoa fedha nyingi zaidi. Nimeridhishwa na usimamizi wa wahandisi hawa katika barabara hii ambayo ipo katika hatua nzuri”, amesema Prof Mbarawa. 

Waziri Mbarawa ameongeza kuwa Serikali itahakikisha kuwa miaka mitano ijayo miradi yote mikubwa nchini itasimamiwa na Wakala huo ili kuokoa fedha za ndani na badala yake fedha hizo kuelekezwa kwenye miradi mingine ya ujenzi. 

Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS, mkoa wa Geita Eng. Harun Senkuku amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara ya Uyovu-Bwanga umefikia asilimia 47 na Bwanga – Biharamulo umefikia asilimia 42 na ujenzi wake unagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 90. 

Aidha, Eng. Senkuku amemuahidi Waziri huyo kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili wananchi wa mikoa ya kagera na Geita kuweza kutumia barabara hiyo. 

Naye, Mhandisi Msahauri kutoka TECU Eng. Gladson Yohana amesema kuwa kusimamia miradi mikubwa kama hiyo kumewasaidia kujifunza zaidi kwa vitendo na amemuhakikishia Waziri huyo kusimamia barabara hiyo kwa kuzingatia ubora na viwango vinavyotakiwa. 

Katika hatua nyingine Waziri Prof. Mbarawa amekagua kivuko cha MV. Chato na kumuagiza Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), mkoa wa Geita Eng. Fredinand Mishamo kuhakikisha kuwa kivuko hicho kinajiendesha chenyewe kutoka kwenye mapato yanayopatikana. 

Prof Mbarawa amemtaka Meneja huyo kuhakikisha kuwa mapato yatokanayo na kivuko hicho yanaongezeka ili kuweza kusaidia changamoto ndogondogo katika kivuko hicho. 

Eng.Mishamo amemuelezea Waziri huyo changamoto zinazokabili kivuko hicho kuwa ni kukosa maegesho katika baadhi ya maeneo. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilian

WATANZANIA TUFANYE SHUGHULI ZENYE MANUFAA KWA JAMII INAYOTUZUNGUKA KWA AFYA YA NCHI-DC HAPI

$
0
0
Na Humphrey Shayo -Globu ya Jamii.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi, ametoa wito kwa wakazi wa Kinondoni na Tanzania kwa ujumla kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa kufanya shughuli zenye manufaa kwa jamii inayotuzunguka.

Hapi ameyasema hayo leo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika fukwe za Coco beach Dar es Salaam wakati wa zoezi la kufanya usafi katika fukwe hizo,ikiwa ni sehemu ya ishara ya kumuenzi Mwalimu kwa urithi aliotuachia.

"Hii ni moja ya sehemu ambazo tunapasa kujivunia, kwani mwalimu aliamua kutenga maeneo haya kwa watu wa hali ya chini kuja kujiburudisha tena pasipo kulipia chochote,  hivyo kamwe matajiri hawatopata fursa ya kuja kujipenyeza katika kunyakua eneo hili ambalo kila Mtanzania anakuja kujidai nalo" amesema Hapi.

Alimaliza kwa kusema kuwa usafi ni jambo la msingi na linapaswa kufanywa kila siku,tusingojee mahadhimisho au sikukuu,pia alichukua fursa hiyo kuwashukuru wakazi wa Kinondoni kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo.
 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni,Ally Hapi, akisukuma mkokoteni wenye taka.
 Baadhi ya Wanafunzi wakiwa na walimu wao katika zoezi la usafi lililofanyika CocoBeach Dar es Salaam.
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni  Ally Hapi, akimwaga takataka  kwa kutumia  toroli wakati wa zoezi la usafi kitika fukwe za Coco Beach.
Mkuuwa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akiweka taka kwenye mfuko ulioshikwa na Mkandarasi wa fukwe za Kinondoni Elizabeth Mhlanga kutoka  kampuni ya Flamingo,wakati wa  zoezi la usafi katika fukwe za Coco Beach.

MCHANGO WA MWL.NYERERE KATIKA KUIMARISHA UHUSIANO WA TANZANIA NA NCHI ZA NJE

$
0
0
 
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Kati ya mafanikio makubwa ya Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Rais wa Awamu ya Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kujenga umoja wa taifa kati ya watu wa makabila na dini tofauti, na hivyo kudumisha amani ya muda mrefu tofauti na hali ya nchi nyingi za jirani na hiyo imeifanya Tanzana iitwe “Kisiwa cha Amani”.

Mwl. Nyerere amepanua wigo wa siasa ya Tanzania na mataifa ya nje ambapo ameimarisha uhusiano, ushirikiano na kuunga mkono vyama halisi vya Ukombozi wa Afrika kama vile FRELIMO ya Msumbiji, ZANU-PF ya Zimbabwe, ANC ya Afrika Kusini na MPLA ya Angola bila kusahau SWAPO ya Namibia pamoja na mataifa yaliyopo mabara ya Ulaya, Amerika na Asia.

‘Tukiimarisha kushirikiana kwetu, tukielewa kuwa vita vyao ni vita vyetu, tutaongeza sana nguvu zetu za kuleta ukombozi wa Afrika nzima’ anasema Mwl. Nyerere.

Katika nukuu za Mwl. Nyerere, amewahi kusema “Uhuru wetu hauwezi kuwa kamili kama jirani zetu hawajapata uhuru.” Hii inadhihirisha jinsi gani muasisi huyu wa Tanzania alivyokuwa na dhamira ya dhati ya kushirikiana na mataifa mengine ya kiafrika.

Katika Azimio la Arusha Mwl. Nyerere amewahi kusema Tanzania iko tayari kushirikiana kirafiki na nchi yoyote yenye nia njema bila kujali kama nchi hiyo ni ya upande wa Mashariki, kwa maana ya nchi zenye mlengo wa Kijamaa au Kikomunisti au Magharibi, zenye mwelekeo wa kibepari.

Aidha, Mwl. Nyerere amesisitiza juu ya wajibu wa kuimarisha ushirikiano na kuungana mkono nchi za kimapinduzi za Afrika, kwa vile aliamini kuwa nchi zote zimo katika jahazi moja, yenye safari moja, akiwa na maana ya mazingira na hali za kufanana za nchi hizo.

Katika kipindi cha Utawala wake wa Awamu ya Kwanza na hata baadae Mwl. Nyerere ameshiriki katika jitihada mbalimbali za kusaidia mataifa ya kiafrika kujipatia Uhuru wake, pamoja na kutatua migogoro iliyokuwepo katika nchi hizo. Amekuwa Mwenyekiti wa nchi zilizokuwa mstari wa mbele katika ukombozi wa Afrika pia amekuwa msuluhishi wa migogoro ya Burundi.

Hali hiyo imesaidia Tanzania kuwa nchi yenye mahusino mema na nchi mbalimbali duniani bila kujali itikadi zao wala miongozo yao.

Kutokana mchango na jitihada za Mwl. Nyerere, Tanzania imekua kivutio cha wageni wengi kutoka nje, kuanzia wanasiasa wa kimataifa na wasomi kutoka Marekani, Ulaya Magharibu na kwingineko.

Wasomi hao wa Kimataifa kutoka maeneo mbalimbali walikuja kujionea na kufanya utafiti juu ya sera ya Tanzania siri iliyomwezesha Mwl. Nyerere kuiweka Tanzania katika ramani ya Dunia.

“Pembuzi zao nyingi zilimwelezea Mwl. Nyerere kama “Roho ya Afrika na tumaini la wasomi, wanasiasa wa Afrika na Dunia nzima”, kila neno lake lina thamani kubwa, lenye kupimwa na kuchanganuliwa kwa makini na nchi za Magharibi na za Mashariki.

Kitendo hicho cha jamii ya kimataifa kumfananisha Mwl. Nyerere na wafalme wa nchi za ustaarabu wa kwanza Duniani, kama Julius Ceasar, Suleimani na Richard wa II, ni uthibitisho tosha kwamba kipaji chake kilivutia wengi.

Baadhi ya viongozi waliofurahishwa na uwezo wa Mwl. Nyerere ni pamoja na Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter ambaye mwaka 1977 alimsifia na kumwelezea Mwl. Nyerere kama “ Rais Mwandamizi, msomi, mwanafalsafa aliyetukuka na mwandishi mahiri”.

Imewahi kuelezwa kuwa Rais Carter alichukua daftari (notebook) na kuandika kila kitu alichokuwa akisema Mwl. Nyerere na baadae gazeti moja nchini humo liliandika “Inapotokea Rais wa Taifa kubwa kumnukuu Rais wa Kiafrika” inaonesha ni jinsi gani busara ya Mwl. Nyerere ilivyoheshimika na mataifa makubwa.

Mwl. Nyerere ameimarisha mahusiano baina ya nchi kadhaa na Tanzania katika harakati za ukombozi wa nchi hizo na uhusiano huo umezaa matunda ambayo ni msaada katika kukuza uchumi wa nchi husika pamoja na kuchangia maendeleo kwa kutoa fursa mbalimbali ikiwemo ajira, masuala ya kidiplomasia ama utatuzi wa migogoro, sekta za viwanda, afya, kilimo, elimu, teknolojia na biashara.

Mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika ambazo bado zilikua zikikaliwa kimabavu na wakoloni katika nchi za Zimbabwe, Msumbiji , Angola, Namibia na Zimbabwe zimeimarisha uhusiano kati ya nchi hizo na Tanzania.

Kuwapatia hifadhi salama vyama vya ukombozi vya mataifa, pamoja na rafiki wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Dr. Kenneth David Kaunda (aliyekuwa rais wa Zambia) ulisaidia jitihada za kuikomboa Afrika hususani Kusini mwa Afrika.

Aidha, kupitia uhusiano uliojengwa wakati huo kati ya Mwl. Nyerere na Kenneth Kaunda ulifanikisha azma ya biashara ya nchi ya Zambia iliyokuwa ikiuza shaba kwa kiwango kikubwa katika nchi za China, Ujerumani na kwingineko kwa kujenga reli ya TAZARA kutokana na ufadhili wa Serikali ya China kutoka Dar es Salaam hadi ukanda wa shaba nchini Zambia.

Reli hiyo ni mradi mkubwa wa kwanza kufanywa na China nje ya mipaka yao, lakini pia ndiyo reli bora zaidi kujengwa Duniani baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Mwl. Nyerere hakuishia Afrika pekee, ameimarisha mahusiano baina ya Tanzania na China ambayo kwa hakika yamekua yakileta faida kubwa kwa nchi zote mbili.

Ni kutokana na mahusiano hayo mema kati ya Tanzania na China, ndio kumezaa matunda yaliyochangia juhudi zilizofanywa na Meya wa Mji wa Musoma Bw. Kisusura Malima na aliyekuwa Balozi Mdogo wa China nchini Li Xuhang alipokuwa mkoani Mara kuadhimisha miaka 50 ya Urafiki wa Tanzania na China.

Juhudi hizo ni katika kuwaenzi wanamapinduzi, Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na muasisi wa Taifa la China, Mao Zedong, kwa kuunganisha mji wa Musoma kilipo kijiji cha Butiama alipozaliwa Mwalimu na Jiji la Xiang Tan nyumbani kwa Mao mwasisi wa China.

Miji hiyo inaungana kuifanya Butiama na Mara kuwa kivutio cha utalii, uwekezaji kibiashara na kitaaluma kwa kushirikiana Xiang Tan jiji lenye maendeleo makubwa.

Mahusiano mazuri ya Mwl. Nyerere yalishamiri pia katika taasisi mbalimbali duniani, kwa mfano Robert Mac Namara, Rais wa zamani wa Benki ya dunia aliita Tanzania “kipenzi” chake cha Afrika.

Naye, Gavana Jerry Brown wa Marekani alipotembelea Tanzania, alikaa juu ya magoti ya Mwl. Nyerere kwa kile alichosema “aweze kujifunza maajabu ya bara la Afrika kutoka kwa bingwa wa masuala ya Afrika na Dunia”.

Ikumbukwe kuwa Mwl. Nyerere amekuwa na ushawishi mkubwa na alitoa wazo la kuunda mashirika mbalimbali yanayoziunganisha nchi za Afrika ikiwa ni hatua mojawapo ya kuelekea kuunda Afrika moja, hivyo mashirika kama vile SADC, ECOWAS, COMESA, EAC na kadhalika yaliundwa katika kufikia azma ya kuunganisha nchi za Afrika, na hivyo mashirika hayo yamekua yakiendelelea kufanya kazi hadi sasa.

Ni dhahiri kuwa Tanzania imendelea kuaminika na kuwa kinara katika masuala ya diplomasia na amani duniani kote na kuifanya kuwa na mahusiano yaliyoimarika katika nchi mbalimbali . Na hiyo ikiwa ni juhudi zilizofanywa na Mwl. Nyerere wakati wa utawala wake na hata baada.

Hakika mchango wake wa kukuza uhusiano wa Kimataifa na Tanzania utakumbukwa vizazi hadi vizazi.

TAASISI YA LECRI CONSULT YAENDESHA WARSHA KWA VIJANA YAWATAKA WASITEGEMEE KUAJIRIWA

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Legal and Child Right Consult, Edna Kamaleki (kushoto), akizungumza na vijana wasomi katika warsha ya siku moja ya kuwaongezea uwezo iliyofanyika Dar es Salaam leo. Warsha hiyo iliandaliwa na taasisi hiyo.
Mdau Julius Kionambali (kushoto), akizungumza katika warsha hiyo.
Miriam Mnada (kulia), akichangia mada
Vijana wasomi wakiwa kwenye warsha hiyo.
Warsha ikiendelea.
Vijana wakisikiliza mada kwa makini



Na Dotto Mwaibale


VIJANA wasomi wametakiwa kuacha kutegemea kazi za kuajiriwa badala yake wawe wabunifu katika masuala mbalimbali kulingana na elimu yao ili kujikomboa kiuchumi.

Mwito huo umetoewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Lecri Consult, Edna Kamaleki Dar es Salaam leo katika warsha ya siku mbili ya kuwaongezea uwezo vijana iliyoandaliwa na taasisi hiyo. 

"Kijana umesoma kwanini upoteze muda wako kwa kuzunguka kutafuta kazi wakati fursa nyingi zipo" alisema Kamaleki.Kamaleki aliwataka vijana waoshiriki warsha hiyo kubadili na kuthubutu kuanza kufanya kitu chochote kulingana na elimu walizosomea vijana hao.

Akizungumzia taasisi yake hiyo alisema imejikita kutoa huduma za kisheria kwa jamii na ushauri katika mambo mbalimbali yanayohusu haki za watoto."Tuna amani kwamba haki za watoto ni muhimu kwa maendeleo na ustawi wa watoto, pia watoto wanapaswa kuishi katika jamii ambayo haki za binadamu na sheria zinaeleweka vizuri na kuheshimiwa na kila raia" alisema Kamaleki.

Alisema taasisi hiyo inatoa ushauri na huduma ya kisheria kwa jamii wakiwemo watoto, watu binafsi na taasisi mbalimbali na kuandaa nyaraka mbalimbali za kisheria na mikataba ya kisheria.

Aliongeza kuwa shughuli zingine zinazofanywa na taasisi hiyo ni kushauri namna ya kufungua kesi katika masuala ya jinai, madai, ndoa, ardhi na usimamizi wa mirathi pamoja na kuwawakilisha wateja wao mahakamani katika shauri lolote la kisheria.

Alitaja kazi nyingine ya taasisi hiyo kuwa ni kuwasaidia watu binafsi kuunda na kusajili kampuni au taasisi na kujenga uwezo wa taasisi au watu binafsi kuhusu sheria mbalimbali za nchi na kimataifa na kufanya tafiti mbalimbali kuhusu masuala ya kisheria. 

Kwa mawasiliano na taasisi hiyo wasiliana nao kwa facebook lecriconsult, twitter lecriconsult na instrag ni lecriconsult1601 na simu namba 0767855174 na 0657023585.

Dk.Kigwangalla na Mwigulu Nchemba waombewa dua na Sheikh Mkuu wa jumuiya ya Bohora Duniani

$
0
0
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla jana jioni (Oktoba 13.2016), amekaribishwa na dhehebu la Bohora na kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Jumuiya ya Bohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin katika msikiti wa dhehebu hilo Upanga Jijini Dar es Salaam.

Mbali na kutoa dua kwa Dk. Kigwangalla, Sheikh Dkt. Syedna ameahidi kuleta wawekezaji wa Kibohora kutoka sehemu mbalimbali Duniani kwa ajili ya kuwekeza kwenye ujenzi wa Mahospitali ikiwemo Hospitali za Rufaa za kisasa pamoja na Viwanda vya Dawa hali ambayo itapunguza idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kufuata matibabu.

Pia viwanda vya dawa vitashusha gharama za dawa nchini na kupunguza ucheleweshaji unaosababishwa na kuagiza dawa nje ya nchi.

Aidha, katika tukio hilo, usiku huu, Dk.Kigwangalla ameweza kushuhudia ndoa za Vijana zaidi ya 50 zikifungishwa na Sheikh Mkuu wa Mabohora Duniani, Dkt. Syedna.

Mbali na Dk.Kigwangalla kuombewa dua maalum na Sheikh Mkuu wa Bohora Duniani, Dkt. Syedna, Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba aliungana katika kuombewa na Shehe huyo.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akibusu mkono wa Sheikh Mkuu wa Bohora Duniani, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin isharara ya kupokea dua katika tukio hilo
Waziri wa mambo ya ndani nchini ,Mwigulu Nchemba akiombewa baraka na kiongozi Dawood Bohora Duniani Dkt Syedna Mufaddal Saifuddin katika msikiti wa mabohora Upanga.
Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi, Mh. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa tukio hilo.

Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images