Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live

Serikali yaanza utafiti wa kuangalia hali ya upatikanaji wa nishati nchini

0
0
Mwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bw.Ephraim Kwesigabo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya utafiti watakaoufanya kwa pamoja na Wakala wa Nishati Vijijini(REA) ukiwa na lengo la kukusanya takwimu rasmi zinazohusu hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme katika maeneo ya vijijini.Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini(REA) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga akizungumza na waandishi wa habari juu ya utafiti ambao serikali itaanza kufanya kuangalia hali ya upatikanaji wa Nishati nchini hasa maeneo ya Vijijini.Kulia ni Mwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw.Ephraim Kwesigabo.
 
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Dar es Salaam

Serikali imeanza utafiti wa kuangalia hali ya upatikanaji wa Nishati Tanzania katika mikoa 26 ya Tanzania bara wa mwaka 2016 kuanzia Octoba 10, hadi Novemba 15 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwakilishi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa utafiti huo unafanya na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini(REA) kwa kushirikiana na kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS).

Dkt Kwesibago alisema kuwa lengo la utafiti huo ni kukusanya takwimu rasmi zinazohusu hali ya upatikanaji wa Nishati umeme katika ngazi ya jumuiya na kaya, matumizi ya umeme na nishati jadidifu pamoja na faida zake kwa maendeleo.

Sambamba na ukusunyaji wa takwimu hizo, Dkt Kwesibago alisema kuwa utafiti huo utahusisha ukusanyaji wa takwimu za kidemografia na za kiuchumi za wanakaya zikijumuisha umri, jinsia, hali za ndoa, elimu, shughuli za kiuchumi, matumizi ya muda pamoja na ushiriki wa jinsia katika shughuli za kiuchumi na kijamii.

Aliongeza kuwa utafiti huo utahusisha jumla ya maeneo 676 ya vijiji na mijini yaliyochaguliwa kitaalam katika mikoa yote ya Tanzania bara na kuhusisha jumla ya kaya binafsi 10,140 pamoja na viongozi wa vijiji na mitaa 676 ambao watahojiwa kuhusu miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopatikana katika maeneo yao.

Aidha, alisema kuwa timu ya wadadisi wapatao 130 watahusika katika zoezi hilo la ukusanyaji taarifa ambapo kila mkoa utakuwa na wadadisi watano, msimamizi mmoja na wataalamu wengine kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu makao makuu.

Vile vile alisema kuwa upatikanaji wa takwimu hizo utasaidia katika kuandaa taarifa kuhusu hali halisi ya upatikanaji na usambazaji wa nishati ya umeme nchini na hivyo kuweza kupima na kuhakiki maendeleo yaliyofanikiwa na mafanikio ya juhudi za Serikali.

Pia taarifa za utafiti huo zitatumika katika kuendeleza mipango ya usambazaji wa umeme vijijini kupitia miradi mbalimbali itakayotekelezwa na Serikali kwa ajili ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa nishati bora vijijini.

Mbali na hayo wananchi wameombwa kutochukua sheria mkononi kwa kuwadguru wadadisi wanapokuwa wakifanya tafiti mbalimbali kwa ajili ya kusaidia nchi yetu kupata takwimu rasmi zinazosaidia katika kutunga sera na kupanga mipango ya maendeleo.
 

SADC ORGAN TROIKA MINISTERIAL ASSESSMENT MISSION

0
0


The Southern African Development Community (SADC) Troika of the Organ on Politics, Defence and Security Cooperation undertook an assessment mission to the Democratic Republic of Congo (DRC) from 10th to 13th October 2016. The objective of the mission was to conduct an assessment of the political and security developments in the DRC aimed at assessing the on-going efforts related to peace and political stability of the DRC. H.E. John Pombe Joseph Magufuli, President of the United Republic of Tanzania in his capacity as the Chairperson of the Organ on Politics, Defence and Security cooperation mandated the Mission.

The assessment mission was led by Hon. Dr. Augustine P. Mahiga, Minister of Foreign Affairs and East African Cooperation of the United Republic of Tanzania and Chairperson of the Ministerial Committee of the Organ (MCO), who was accompanied by Hon. Georges Rebelo Chikoti, Minister of External Relations of the Republic of Angola and Deputy Chairperson of the MCO, Hon. Patricio Jose, Deputy Minister of National Defence of the Republic of Mozambique representing the outgoing chairperson of the MCO. The Mission was supported by the SADC Secretariat led by H.E. Dr. Stergomena Lawrence Tax, Executive Secretary of SADC. The mission also included SADC Ambassadors accredited in the DRC.

The Mission consulted with various stakeholders, including SADC Ambassadors accredited to the DRC, H.E. Edem Kodjo, African Union Facilitator of the National Dialogue, Hon. Raymond Tshibanda, Minister of Foreign Affairs and International Cooperation of DRC, Mr. Corneille Nangaa, and Mr. Nobert Katintima, Chairperson and Deputy of the Independent Electoral Commission (CENI) respectively, Senior Officials of the DRC Government, Representatives of Opposition Outside the  Dialogue (Rassemblement), Representatives of Opposition in the Dialogue, political parties in the Presidential majority led by Hon. Aubin Minaku, civil society and religious groups.

Following consultations and exchange of views with the various stakeholders, the Organ Troika Ministerial Mission:

1.   Noted the encouraging progress in the on-going AU-led National Dialogue and voters’ registration;

2.   Commended all stakeholders participating in the National Dialogue and noted progress made so far. Further urged all stakeholders who are not part of the National Dialogue to join the process;

3.   Encouraged all stakeholders to put the interest of the country and the people of the DRC first in the National Dialogue in order to ensure consensus on outstanding issues;

4.   Strongly condemned the violence that took place on 19th to 20thSeptember 2016, which resulted in the loss of lives of innocent civilians and police officers as well as destruction of property. Further called on all stakeholders to act responsibly and avoid any actions that would result in any acts of violence;

5.   Strongly discouraged any attempts and threats that are aimed at undermining the process of Dialogue.

6.   Urged all stakeholders to create a conducive environment for free, fair democratic, peaceful, transparent and credible elections in the interest of peace, national unity, stability and socio-economic development of the country and to uphold the principles; ideals and aspirations of the Congolese people as enshrined in the Constitution and in accordance with SADC and AU principles and guidelines governing democratic elections;

7.   Urged all eligible Congolese voters to fully participate in the on-going voters registration process in order to exercise their democratic right as enshrined in the Constitution in the next elections;

8.   Called upon all stakeholders in the DRC, the international community and the Support Group to continue supporting the Africa Union-led National Dialogue and the electoral process, with a view to ensure sustainable peace, security and stability in the DRC; and

9.   Re-affirmed SADC’s support to the ongoing National Dialogue and pledged its full support to the final outcome.



Done in Kinshasa, Democratic Republic of Congo
12th October 2016

WAZIRI LUKUVI. HAKUNA MAKAZI HOLELA YATAKAYOBOMOLEWA JIJINI MWANZA.

0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akimkabidhi hati ya umiliki wa ardhi na makazi mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza ambaye makazi yake yamerasimishwa kutoka makazi holela baada ya zoezi la upimaji kufanyika.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akimkabidhi hati ya umiliki wa ardhi na makazi mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza ambaye makazi yake yamerasimishwa kutoka makazi holela baada ya zoezi la upimaji kufanyika.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akizungumza na watendaji mbalimbali Jijini Mwanza (Ilemela na Nyamagana).
Baadhi ya Watendaji na Madiwani wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza
Baadhi ya Watendaji na Madiwani Jijini Mwanza
Pia Waziri Lukuzi amempandisha cheo aliyekuwa Afisa Mipango na Maendeleo ya Jiji la Mwanza, Deogratius Kalimerize, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mipango Miji na Vijijini Kanda ya Ziwa. 

Ni baada ya kuridhishwa na kazi yake ya usimamiaji na uandaaji wa Mpango Kabambe wa Jiji la Mwanza wa mwaka 2015-3015 ambao umelenga kulifanya Jiji la Mwanza kuwa kitovu cha kiuchumi na biashara katika nchi za maziwa makuu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye mkutano huo baina ya waziri Lukuvi na watendaji mbalimbali wa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
Watendaji na wananchi wa Kata ya Buhongwa wakimsikiliza waziri Lukuvi (hayupo pichani).
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, alipofanya ziara Jijini Mwanza hii leo.

Waziri ameziagiza halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, kuhakikisha zinakamilisha zoezi la upimaji na urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela hadi ifikapo june 30 mwakani.
Na BMG
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, alipofanya ziara Jijini Mwanza hii leo.

**********************
Na George Binagi-GB Pazzo
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, ameziagiza halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, kuhakikisha zinakamilisha zoezi la upimaji na urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela hadi ifikapo june 30 mwakani.

Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo hii leo Jijini Mwanza alikofanya ziara ya kujionea utekelezaji wa urasimishaji makazi yaliyoendelezwa kiholela Jijini Mwanza ambapo amebainisha kwamba Serikali haina mpango wa kuwavunjia wananchi makazi yaliyojengwa kiholela na badala yake imeandaa mpango huo ili kutambua makazi hayo na kuwapatia wananchi hati miliki ya makazi yao.

Aidha amewatahadharisha wananchi kwamba, mpango wa kurasimisha makazi yaliyojengwa kiholela hautayahusisha makazi yaliyojengwa kwenye maeneo hatarishi ikiwemo kwenye mabonde, miinuko, mafuriko pamoja na hifadhi za barabara.

Baadhi ya wananchi Jijini Mwanza ambao makazi yao yamerasimishwa na kupewa hati ya umiliki, wameipongeza serikali kwa hatua hiyo ambapo wameomba kasi ya zoezi hilo kuongezeka ili wananchi zaidi ya elfu 35 ambao makazi yao hayajapimwa, yaweze kupimwa na kupatia hati za umiliki kwa wakati kama Waziri Lukuvi alivyoagiza.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amemuhakikishia Waziri Lukuvi kwamba hadi kufikia mwezi Januari mwaka ujao, zoezi la kupima makazi yaliyojengwa kiholela na kuyarasimisha katika Jiji la Mwanza na Maspaa ya Ilemela, litakuwa limekamilika.

POPOTE PALE ULIPO UNAKARIBISHWA KWA MAHITAJI YA HUDUMA HIZI

0
0
Nakukaribisha Mac Travel Agency Tanzania  Kwa mahitaji ya huduma za Usafiri wa Ndege  local and International flights,Tunafanya kazi masaa 24/7 ,Pia tunasaidia kuprocess visa za Dubai kwa uharaka ndani ya masaa 24 & Visa za China & Turkey utapatiwa msaada wa kupata kwa uharaka.Kwa mawasiliano nasi piga namba hizi:- 0715 120 222 / 0715 000 890 /0752 120 128

Book your flight by email us :reservations@mactravel.co.tz
      Info.mactravel@gmail.com

 Tunapatikana Sinza - Mori near GBP petrol station.Karibuni sana✈✈✈

Tufollow leo Instagram upate offer @mactravelagency @mactravelagency @mactravelagency @mactravelagency

#Mac Travel Agency Tanzania
#Hotline-0715 000 890
#Tunafanyakazisiku7kwaWiki
#Flywithconfidencewithus.

Wasomi kutembelea Nyumba ya Mwalimu Nyerere Magomeni Kesho

0
0

Mratibu wa ziara ya viongozi wa vyuo vikuu mkoa wa Dar es Salaam,Marco Bujiba ,akizungumza na waandishi wa wahabari katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam,kulia mratibu msaidizi Boniface Macheta.

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Umoja wa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka vyuo mbalimbali wamejipanga kuadhimisha siku ya Nyerere Day kwa kutembelea nyumba ya kihistoria aliyowahi kuishi mwalimu Nyerere iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa safari hiyo Rais wa Chuo cha Sayansi na tiba Muhimbili,Marco Bujiba amesema kuwa wameamua kufanya hivi hilinkupata muda wa kutafakari kwa upana juhudi za baba wa Taifa katika kulikomboa Taifa dhidi ya Wakoloni kupambana na umaskini ,Ujinga na maradhi ambavyo alivitaja kama maadui wakubwa wa Taifa letu pamoja na kupinga vita rushwa ,ubaguzi miongoni miongoni mwa watanzania kwa tofauti za makabila ,dini,rangi au maeneo yanayotoka.

"Kama viongozi vijana katika nchi yetu ,tutatumia fursa hiyo kutathimini hatua za kimaenedeleo tulizifanya kama taifa kwa kurejea mpango wa Taifa wa kuondoa umaskini na kukuza Uchumi ili kujua kwa kwa kiasi gani taifa letu limeenzi fikra za Mwalimu kwa vitendo katika kupambana na adui namba moja wa Tanzania ,yaani umaskini" amesema Marco.

Aliongeza kuwa kwa kufanya hivi itaongeza chachu ya kujituma kujenga taifa namkusaidia kuhamasisha vijana wote Tanzania kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa umaskini hivyo kutimiza kwa vitendo kauli mbiu ya Serikali ya Hapa Kazi.

Pia alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wote ambao ni viajna kuenzi fikra za baba wa taifa katika kulitumikia taifa .

Timu ya Halotel Tanzania yashiriki katika mashindano ya kombe la Viettel 2016.

0
0

Timu ya Halotel Tanzania ikipambana na timu ya Mytel wakati wa michuaono ya kombe la dunia la Viettel yanayoendelea katika mji wa Hanoi, nchi Vietnam.
Wachezaji wa timu ya Halotel Tanzania wakisalimiana na wachezaji wa Mytel kabla ya mechi yao kwenye michuaono ya kombe la dunia la Viettel yanayoendelea katika mji wa Hanoi, nchi Vietnam.
Sherehe za ufunguzi za michuano ya Viettel World Cup 2016 nchini Vietnam, ambako timu ya Halotel Tanzania inashiriki kwa mara ya kwanza.



Timu ya Halotel kutoka Tanzania inashiriki katika mashindano ya dunia ya “Viettel World Cup 2016”, yanayofanyika nchini Vietnam katika mji mkuu wa Hanoi yakijumuisha timu 17 kutoka nchi 11 ambazo kampuni ya Viettel imewekeza.

Mashindano hayo yanayohusisha zaidi ya wafanyakazi 10,000 kutoka katika mabara ya Africa, Asia na Latin America huku kilele chake kikitarajiwa kuwa tarehe 15 ya mwezi huu wa kumi.

Toka yalipoanzishwa mwaka 2014, mashindano ya Viettel, yamekuwa yakifanyika kila baada ya miaka miwili, na katika hatua za mwanzo za mashindano hayo yanafanyika kakika nchi zote ambazo Viettel imewekeza.

Dhumuni kubwa la mashindano hayo ni kudumisha ushirikiano miongoni mwa wafanyakazi wa Viettel na pia kutoa fursa ya kujifunza tamaduni za jamii tofauti tofauti kama njia mojawapo ya kuishi kama familia.

Akiongelea kuhusu mashindano hayo, Mkuu wa Masoko wa Halotel, bwana Ngo duy Truong, amesema mashindano hayo yataimarisha uhusiano miongoni mwa wafanyakazi na pia kuongeza hamasa ya kufanya kazi kama timu moja.

‘Kama kauli mbiu yetu inavyosema ‘Pamoja katika Ubora’ tunaamini kuwa kupitia mashindano haya, wafanyakazi wetu watajifunza umuhimu wa kufanya kazi kwa pamoja na kwa kushirikiana”, akisema bwana Truong.

Mashindano ya kombe la dunia ya Viettel 2016 yanatarajia pia kutoa fursa kwa wafanyakazi wa Viettel kujifunza kuhusiana na tamaduni, historia na geographia ya nchi ya Vietnam.

Hii ni mara ya kwanza kwa timu ya Halotel kuingia kwenye mashindano hayo, ambayo yameenda sambamba na maadhimisho ya mwaka mmoja wa Halotel toka ilipoanza kutoa huduma zake nchini Tanzania

WANANCHI WAASWA KUTOA TAARIFA WANAPOPATWA NA MADHARA YA DAWA.

0
0
Afisa wa Uthibiti wa Majaribio na Usalama wa Dawa (TFDA)Dkt. Alex Nkayamba kushoto akimpa maelekezo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kuhusu mfumo wa wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa unavyopatikana kwenye simu za mkononi wakati wa hafla yauzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam, Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akiangalia jinsi mfumo wa wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa unavyofanya kazi katika kutoa tarifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo, wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo.
Wadau mbalimbali wa vyakula na dawa wakifuatilia kwa makini maelezo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa mfumo wa wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa uliyofanyika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.
 
Na Ally Daud-MAELEZO

WANANCHI waaswa kutoa taarifa pale wanapohisi wamepata madhara ya dawa wanazozitumia ili kuirahisishia Wizara ya Afya kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kuchukua hatua stahiki zidi ya watengenezaji wa dawa hizo ili zisiendelee kuwadhuru wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kwenye hafla ya uzinduzi wa mfumo wa kielektroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa uliofanyika jijini Dar es salaam.

Waziri Ummy amesema kuwa wananchi wawe mstari wa mbele katika kutoa taarifa pindi wanapohisi kupatwa na madhara ya dawa wanazozitumia ili kuirahishia TFDA kuchukua hatua stahiki kutokana na taratibu na sheria zilizopo za kuondoa madawa feki nchini.

“Napenda kusisitiza kwa wananchi wote kutoa taarifa pale wanapohisi wamepata madhara ya dawa ili kuirahishia TFDA kuchukua hatua stahiki kutokana na utaratibu na sheria zilizowekwa” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa bila taarifa hizi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia TFDA itashindwa kuchukua hatua muafaka na za haraka katika kudhibiti madhara yanayotokana na matumizi ya dawa na hivyo kuendelea kusababisha athari kwa watumiaji.

Waziri Ummy amesema kuwa wataalam wa afya na wananchi wote kwa ujumla wanatakiwa kutoa taarifa za madhara ya dawa kwa wakati, kwa wale wenye simu zilizounganishwa kwenye “internet” watumie simu hizo kutoa taarifa za madhara ya dawa, na wale wenye kompyuta zilizounganishwa kwenye “internet” watumie kompyuta hizo na wale wasio na simu wala kompyuta zilizounganishwa kwenye “internet “waendelee kutoa taarifa kwa kutumia fomu za njano na kijani.

Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa ujazaji wa taarifa hizo kwa kutumia njia za kielektroniki kunasaidia kujua dawa zipi ni sahihi na zipi si sahihi kwa matumizi ya binadamu na hivyo kuchukua hatua inayostahili.

“Napenda kuwaambia wananchi wajaze fomu hizo ili kutoa taarifa za madhara ya dawa wanazozitumia ili kufahamu dawa zipi ni sahihi kwa matumizi ya binadamu na kama sio sahihi basi tuzichukulie hatua zinazostahili” alisema Bw. Sillo.

Aidha Bw. Sillo amesema kuwa moja ya hatua ambayo zitachukuliwa pindi taarifa za madhara ya dawa zinapotolewa ni kufungia kiwanda kinachotengeneza aina hiyo ya dawa au kusimamisha matumizi yake ili kuondoa dawa zinazoleta madhara kwa watanzania.
 

TAKUKURU MKOANI MWANZA YAMNASA ASKARI FEKI WA JESHI LA WANANCHI JWTZ.

0
0
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Mwanza, Ernest Makale, akitoa taarifa ya kukamatwa kwa mwanamke aitwaye Felister Mathias Mawe, kwa tuhuma za kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na jeshi hilo kupitia maofisa anaofahamiana nao.
Na BMG

Makale ameeleza kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kujipatia kiasi cha shilingi 240,000 kati ya shilingi 500,000 alizokuwa ameomba kutoka kwa mmoja wa walioomba kujiunga na JWTZ.

Amebainisha kwamba mtuhumiwa mmoja ambaye ni mstaafu wa JWTZ aitwaye Sophia Chacha amekuwa akimsaidia mtuhumiwa huyo kwa kumuunganisha na watu waliokuwa wakihitaji kujiunga na jeshi ambapo ili kupata nafasi hiyo mtuhumiwa amekuwa akihitaji kiasi cha shilingi 500,000.

Mtuhumiwa alikamatwa Oktoba 10 mwaka huu katika hoteli moja iliyopo Kirumba Jijini Mwanza kufuatia mtego wa maofisa wa TAKUKURU.

"Kitendo cha mtuhumiwa kujifanya afisa wa jeshi hakihusiani na makosa yaliyo chini ya sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namaba 11/2007, hivyo jalada lenye tuhuma hiyo namba PCCB/MZ/ENQ/40/2016 limehamishiwa kwa wakili wa serikali mfawidhi ili mtuhumiwa aweze kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili". Alifafanua Makale.

Aidha Makale ameongeza kwamba TAKUKURU wilayani Misungwi imemfikisha mahakamani Katibu wa Idara ya Utumishi wa Waalimu TSD wilayani humo kwa kosa la tuhuma za kupokea rushwa shilingi 400,000 kutoka kwa Kitoki Mgaya ili asimchukulie hatua za kinidhamu kazini.
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Mwanza, Ernest Makale, akitoa taarifa ya kwa wanahabari kuhusu kukamatwa kwa mwanamke aitwaye Felister Mathias Mawe, kwa tuhuma za kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ kupitia maofisa anaofahamiana nao.
Mtuhumiwa Felister Mathias Mawe, anayetuhumiwa kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ.
Kushoto ni mtuhumiwa Felister Mathias Mawe, anayetuhumiwa kujifanya askari wa Jeshi la Wananchi JWTZ na kuchukua fedha kwa baadhi ya watu Jijini Mwanza ili awasaidie kupata nafasi ya kujiunga na JWTZ. Kulia ni Sophia Chacha ambaye ni mstaafu wa JWTZ anayetuhumiwa kumsaidia mtuhumiwa huyo kwa kumuunganisha na watu waliokuwa wakihitaji kujiunga na JWTZ.
Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza

Polisi Dar yaua wanne waliopora Benki ya CRDB-Mbagala.

0
0
Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwaua majambazi wanne waliokuwa wamejichimbia katika pori la Mbande jijini Dar es Salaam mara baada ya mapigano makali na majibizano ya risasi yaliyojiri kwa zaidi ya dakika arobaini.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Simon Siro, amesema kuwa jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mmoja wa Majambazi aliyehusika na tukio la ujambazi CRDB Mbagala

"Polisi mara baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na tukio hilo akiwa na wenzie saba hivyo aliwaambia askari kuwa anawapeleka sehemu walipo wenzake kwenye pori la Dondwe ambapo wanafanya mazoezi ya kivita.

"Walipofika katika eneo hilo la mipakani Chanika gafla majambazi hayo yalianza kufyatua risasi kwenye uelekeo wa askari na mtuhumiwa alikimbia na askari wakaanza kujibu mashambulizi na askari wakafanikiwa kujeruhi majambazi wanne na kufanikiwa kupata bunduki ya kijeshi aina ya SMG iliyofutwa namba za usajili ikiwa na risasi 22 ndani ya Magazine" Amesema Siro.

Amesema kuwa majeruhi hao walikimbizwa hospitali ya Taifa Muhimbili na wakati wanapatiwa matibabu wote kwa bahati mbaya walifariki Dunia kutokana na majeraha ya risasi.

Ameongeza kuwa uchunguzi huo umebaini kuwa Bunduki hiyo ni moja ya zile zilizoporwa wakati askari wakibadilishana lindo.

RC MRISHO GAMBO ATEKELEZA AGIZO LA RAIS DKT MAGUFULI LA KUSITISHA SAFARI YA KWENDA MKOANI SIMIYU KUHITIMISHA KILELE CHA MWENGE

0
0

Wachimbaji wa Madini watakiwa kujipatia Elimu na Teknolojia sahihi.

0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof.Justin Ntalikwa na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa wakipata maelezo toka kwa Bi Shamsa Diwani wa kikundi cha MIVA kinachojiusisha na uchimbaji mdogo wa madini na usio rasmi leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano kazi wa wadau wanawake katika sekta ya madini.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof.Justin Ntalikwa na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa wakipata maelezo toka kwa Bi Susan Fred wa TAMICUSO ambao wanajiusisha na uchimbaji mdogo wa madini ya Tanzanite jijini Arusha.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof.Justin Ntalikwa akiuliza swali kwa Bi Martha Kayaga wa kikundi cha WAWACHISI tokea singida jinsi wanavyochimba madini ya gypsum na kuyahifadhi katika mkutano wa wadau wanawake katika sekta ya madini.Kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa akizungumza na wanawake wachimbaji madini wadogo wadogo(hawapo pichani) leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere walipokutana katika mkutano kazi wa wadau wanawake katika sekta ya madini.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Prof.Justin Ntalikwa akizungumza jambo na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa,Bi Tertula Swai wa UN women na Kessy Edward wa Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Picha na Daudi Manongi,MAELEZO


Na Daudi Manongi,MAELEZO.

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa ametoa wito kwa wachimba wadogo wadogo wa madini kuongezea juhudi katika uchimbaji wa madini ikiwa ni pamoja na kujipatia elimu ya uchimbaji sahihi wa madini na kutumia teknolojia nzuri ambayo itawasaidia kuongeza tija katika shughuli zao.

Profesa Ntalikwa ameyasema hayo wakati akifungua mkutano kazi wa wadau wanawake katika sekta ya madini wanaojihusisha na uchimbaji ambao sio rasmi na mdogo uliofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

“Mimi wito wangu kwa wachimbaji hawa ni kwamba nawaomba wajipatie elimu na teknolojia sahihi ili waweze kujiongezea kipato katika uchimbaji huu”,Alisema Prof Ntalikwa.

Aidha Katibu Mkuu uyo aliwataka wachimbaji wadogo wadogo hao kuwasiliana na Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi(NEEC) kwa ajili ya kuwasaidia sehemu ambazo ambazo wanaweza kupata mitaji maana suala la mtaji ni muhimu sana ili waweze kuboresha shughuli za uchimbaji.

Pia amesema kuwa serikali imeanza kutoa ruzuku kwa awamu kwa wachimbaji hawa wadogo wa madini na hivi sasa wanajipanga kutoa awamu ya tatu ya ruzuku ikiwa na lengo ya kuwasaidia kununua vifaa vya uchimbaji na teknolojia sahihi itakayorahisisha uchimbaji wa madini na kuongeza kuwa kwa sasa wameshapokea maombi kutoka kwa wachimbaji mbalimbali na wanayafanyia kazi ili wapate washindi watakaojipatia ruzuku.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi kiuchumi Bi.Beng’i Issa amesema kuwa wao kama baraza watatengeneza programu ya jinsi ya kupata uongozi kwa wachimbaji hao ambao utasaidia kuwakilisha mawazo yao serikali na pia program ya kuwajengea uwezo pale ambapo wachimbaji hawa wana mapungufu na pia kuwaunganisha na masoko kama vile viwanda vya ndani ili visinunue malighafi kutoka nje na badala yake wanunue hapa nchini malighafi yanatotokana na uchimbaji wa madini.

Waziri Muhongo akutana na Balozi Mpya wa Canada nchini

0
0

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa na Balozi Mpya wa Canada nchini, Ian Myles (kushoto) na Kamishna wa Biashara katika Ubalozi huo, Anita Kundy mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na Balozi Mpya wa Canada nchini, Ian Myles mara baada ya kumaliza kikao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akijadiliana jambo na Balozi Mpya wa Canada nchini, Ian Myles wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam.
Balozi Mpya wa Canada nchini, Ian Myles akitia saini katika kitabu cha Wageni mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kamishna wa Biashara katika Ubalozi huo, Anita Kundy .
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akiwa katika kikao na Balozi Mpya wa Canada nchini, Ian Myles (kulia kwa Waziri ) na Kamishna wa Biashara katika Ubalozi huo, Anita Kundy (kulia kwa Balozi). Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watendaji wa Wizara na Taasisi zake. Kushoto kwa Waziri ni Kaimu Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga na wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini, Julius Sarota.












Waziri Muhongo akutana na Balozi Mpya wa Canada nchini
ü Wazungumzia uendelezaji Chuo cha Madini, Miradi ya Nishati na Madini



Na Teresia Mhagama

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Balozi Mpya wa Canada nchini, Ian Myles kuzungumzia masuala mbalimbali ya uendelezaji wa Sekta za Nishati na Madini nchini.

Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Wizara ya Nishati na Madini jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara ya kwanza kwa Balozi huyo kufika wizarani tangu alipowasili nchini mwezi Agosti mwaka huu ili kuiwakilisha nchi ya Canada.

Awali Balozi Myles alimweleza Profesa Muhongo kuwa nchi hiyo imeshiriki katika shughuli mbalimbali za uendelezaji wa sekta za Nishati na Madini nchini.

Mathalani, kupitia Shirika la Maendeleo la Canada (CIDA) nchi hiyo ilikuwa ikitoa fedha kwa Wakala wa Ukaguzi wa Madini nchini (TMAA) katika mwaka wa Fedha wa 2012/2013 hadi 2015/2016 ili kuuwezesha Wakala huo kufanya shughuli zake za ukaguzi kwa ufanisi pamoja na kujengewa uwezo kupitia mafunzo ambapo jumla ya fedha zilizotolewa ni Dola za Canada 2500.

"Katika Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini, Gesi Asilia na Mafuta (TEITI), Canada ilishiriki katika kusaidia mchakato wa maandalizi ya kupata Sheria ya kuongoza Tasnia ambayo ilipitishwa na Bunge mwaka 2015. Pia tunawajengea uwezo wataalam ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi," alisema Balozi Myles

Aidha, alisema kuwa Tanzania ni moja ya nchi zinazopewa kipaumbele na Serikali ya Canada katika masuala mbalimbali ikiwemo utoaji wa misaada ya kifedha.

kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, alisema kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili ulianza tangu miaka ya 1960 na kwamba nchi hizo zimekuwa zikishirikiana katika masuala mbalimbali ikiwemo Kilimo na Elimu.

Alisema kuwa katika Sekta ya Madini, kampuni kubwa zinazofanya shughuli za uchimbaji wa madini nchini, nyingi zinatoka nchini Canada na kutoa mfano wa kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia na kwamba kodi zinazolipwa na kampuni hizo kwa Serikali, zinasaidia kuendeleza miradi mingine ya maendeleo.

Kuhusu uendelezaji wa Chuo cha Madini Dodoma (MRI), Profesa Muhongo alimweza Balozi Myles kuwa mazungumzo kati ya Wizara na Ubalozi huo kuhusu kukiendeleza Chuo hicho kuwa katika ngazi ya Polytechnic yalikwishaanza hivyo alimweleza Balozi huyo kuwa ni vyema utekelezaji wa suala hilo ukaanza.

" Tunataka Chuo hiki kiwe cha kimataifa, kisiwe kinatambulika hapa nchini tu na pia kiwe kinabadilishana wataalam na Vyuo vingine vya nje ili kuboresha elimu inayotolewa katika Taasisi hiyo na pia kijitegemee, badala ya kuwa chini ya mwavuli wa Wizara ya Nishati na Madini,” alisema Profesa Muhongo.

Aidha alitumia fursa hiyo kuwaalika Wawekezaji kutoka Canada kuja kuwekeza katika utafiti na uchimbaji wa madini ya metali aina graphite na lithium kutokana na umuhimu wake duniani na kutoa mfano kuwa madini ya graphite yanatumika kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo betri.

"Madini haya ya metali yana umuhimu sana kwa sasa mfano ifikapo mwaka 1920-40 asilimia 40 ya magari duniani yatakuwa yakitumia umeme hivyo ili kuwezesha hilo wanahitaji madini haya," alisema Profesa Muhongo

Pia alizialika kampuni za Canada kuja kuwekeza katika uchimbaji wa madini adimu (rare metals) ambayo yanahitajika katika teknolojia ya kisasa kama vile madini ya titanium ambayo yanatumika katika kutengeneza mitambo mbalimbali ikiwemo inayotumika kuzalishia umeme.

Pamoja na kualika makampuni ya Canada kuja kuzalisha umeme nchini, Profesa Muhongo alitumia fursa hiyo kumueleza Balozi Myles ombi la Tanzania la kupeleka wataalam wake nchini Canada kusomea masuala ya mafuta na gesi.

TASAF NA WADAU WA MAENDELEO WAHITIMISHA MKUTANO WA KUPITIA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI-PSSN.

0
0
 1Baadhi ya watumishi wa TASAF wakisikiliza moja ya taarifa zilizotolewa kwenye mkutano uliopitia shughuli za Mpango wa Kunusuru Kaya maskini.
 Baadhi ya wadau wa maendeleo wakifuatilia taarifa utekelezaji wa shughuli za  Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
Baadhi ya wadau wa maendeleo wakifuatilia taarifa utekelezaji wa shughuli za  Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.
      Baadhi ya watumishi wa TASAF wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo wakisikiliza taarifa za utekelezaji wa Mpango huo kwenye mkutano wa kupitia utekelezaji wake.
 Baadhi ya wadau wa maendeleo wakifuatilia taarifa utekelezaji wa shughuli za  Mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF.

1.     Baadhi ya watumishi wa TASAF wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa taasisi hiyo wakisikiliza taarifa za utekelezaji wa Mpango huo kwenye mkutano wa kupitia utekelezaji wake.

1Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga(aliyeshika kipaza sauti) akizungumza wakati wa kufunga mkutano wa mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini kwenye ukumbi wa mikutano wa TASAF jijini Dar es salaam.



Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF – umehitimisha mkutano wa wadau wa Maendeleo ambao wamepitia utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru kaya maskini unaotekelezwa nchini kwa  lengo la kuona utekelezaji wake katika kipindi cha miezi sita iliyopita.

Licha ya kuwa na mkutano , wadau hao wa maendeleo, maafisa kutoka baadhi ya wizara, taasisi za serikali na mashirika yasiyokuwa ya  kiserikali na watumishi wa TASAF walipata fursa ya kutembelea wilaya za Mbarali, Muheza,Chato,Mkulama na Pemba na kukutana na walengwa wa Mpango huo na kuona namna wanavyonufaika na ruzuku ya fedha inayotolewa kwa kaya maskini.

Majumuisho ya mkutano huo yameonyesha kuwa kuna  mafanikio makubwa katika utekelezaji wa shughuli za Mpango ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku kwa walengwa kwa wakati, kuhamasisha walengwa kubuni miradi ya kujiongezea kipato na kushirikisha jamii katika utekelezaji wa shughuli za Mpango.

Aidha imeelezwa kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika mahudhurio ya wanafunzi wanaotoka katika kaya maskini na kuongezeka kwa mahudhurio ya watoto katika kupata huduma za kliniki mambo ambayo ni miongoni mwa masharti kwa walengwa kupara moja ya ruzuku zinazotolewa na Mpango wa Kunusuru kaya maskini.

Akizungumza mwishoni mwa mapitio hayo ambayo hufanyika kila baada ya miezi sita, Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga ametaka jitihada zaidi ziendelee kuchukuliwa na wafanyakazi wa TASAF na wadau wengine wanaotoa huduma kwa kaya maskini ili walengwa waweze kunufaika na huduma za mpango.

Kwa upande wake Msimamizi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bwana Abdulahi Muderis amesema mafanikio yaliyoanza kuonekana katika utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini ni kielelezo thabiti kinachoonyesha kuwa serikali ya Tanzania  imo katika jitihada kubwa za kupambana na umaskini  

SERIKALI YA CHINA YAAHIDI KUIPATIA TANZANIA MSAADA WA FEDHA WA SH.BILIONI 97 TOKA CHINA

0
0

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Charles Mwijage akizungumza katika mkutano kati yake na Naibu wa Viwanda wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Dkt. Qian Keming.Mazungumzo yao yalijikita katika kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na China katika kuboresha miundombinu.
Sehemu ya ujumbe ulioambatana na Dkt. Keming wakimsikiliza kwa makini Dkt. Mwijage hayupo pichani.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Kushirikiana katika masuala ya uchumi na teknolojia
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda (wa kwanza kushoto), Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Ramadhani Muombwa Mwinyi (katikati), na Mwakilishi kutoka Kituo cha Uwekezaji wa Tanzania kwa pamoja wakishuhudia uwekwaji saini katika mkataba huo.

Dkt. Mwijage na Dkt. Keming wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mkutano.
 
 ***********************************************************

Serikali ya Watu wa China imeahidi kuipatia Tanzania msaada wa fedha wa kiasi cha Shilingi bilioni 97 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Kauli hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage (Mb) baada ya kukutana na ujumbe kutoka China unaongozwa na Naibu Waziri wa Biashara wa nchi hiyo, Mhe. Dkt. Kian Keming.

Dkt. Kian na ujumbe wake upo nchini ambapo pamoja na mambo mengine walishiriki kikao cha tano cha Kamati ya pamoja ya Uchumi, Biashara, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kiteknolojia kilichofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Fedha na Mipango.

Mhe. Mwijage alieleza kuwa katika kikao hicho walijadili masuala mbalimbali ikiwemo uwekezaji katika viwanda, miundombinu na nishati. Alisema Serikali ya awamu ya tano imeweka mkazo katika maeneo hayo ili kufikia lengo la nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Alieleza kuwa katika harakati za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2020, viwanda viwili vya chuma na marumaru vilivyojengwa na wawekezaji kutoka China vinatarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka ujao. Kiwanda cha tatu kitaanza kujengwa na wawekezaji wa China muda wowote watakapopewa eneo kwa ajili ya ujenzi huo.

Kiwanda cha kwanza ni cha chuma kilichopo Mlandizi mkoani Pwani ambapo kitakapoanza kazi, kitazalisha tani 1,200,000 za chuma kwa mwaka. Aidha, kiwanda kingine cha marumaru kilichopo Mkuranga mkoani Pwani kinatarajiwa kuingiza pato la Dola za Marekani nilioni 150 kwa mwaka, kitakapoanza uzalishaji.

Kiwanda kinachosubiri kujengwa ni cha nguo ambacho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mita milioni 240 kwa mwaka. Mhe. Waziri alieleza kuwa juhudi za kupata ekari 700 kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho kwenye Wilaya ya Mkuranga zinaendelea na hivi karibibuni eneo hilo litakabidhiwa kwa wawekezaji hao.

Kwa upande wake, Dkt. Kian aliihakikishia Serikali ya Tanzania kuwa China itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania ya kufikia malengo ya kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Aidha, aliwakaribisha makampuni ya Tanzania kushiriki maonesho ya biashara yanayofanyika nchini China ili kuzitangaza bidhaa za Tanzania kwa madhumuni ya kupata soko nchini humo.

Mawaziri hao wawili waliweka saini Mkataba wa Makubaliano ya Kushirikiana katika masuala ya uchumi na teknolojia.

Dkt Shein awasili Mwanza leo kuelekea Simiyu kuzima Mwenge kesho.

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,John Mongela mara alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akielekea katika Mkoani Simiyu kushiriki sherehe za uzimaji mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika kesho.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifutana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe,John Mongela (wa pili kulia) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Jenister Muhagama (wa pili kushoto) na Waziri wa kazi,uwezeshaji Vijana,Wazee Wanawake na Moudeline Cyrus Castico (kushoto)baada ya mapokezi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza akielekea katika Mkoani Simiyu kushiriki sherehe za uzimaji mbio za Mwnge wa Uhuru Kitaifa zinazotarajiwa kufanyika kesho,[Picha na Ikulu.]

KONGAMANO LA HAKI YA AFYA YA UZAZI LAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

0
0
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kwa Umma Bw. Justus Mulokozi akifungua kongamano la Kitaifa la Haki ya Afya ya Uzazi katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam ambapo wadau mbalimbali wamehudhuria katika kongamano hilo wakiwemo Wanasheria , Wanasiasa, Wanafunzi Waandishi wa habari pamoja na waalikwa mbalimbali.
002
Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA Bi. Tike Mwambipile akizungumza katika kongamano hilo wakati alipokuwa akifafanua mambo mbalimbali kuhusu Haki ya Afya ya Uzazi.
02
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mama Anne Makinda akiwa katika kongamano hilo pamoja na washiriki wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kwa Umma Bw. Justus Mulokozi, Mwenyekiti wa TAWLA Bi. Attanasia Soka na Jaji Winnie Korosso.
2
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) Bi. Attanasia Soka na Jaji Winnie Korosso akimkaribisha mgeni rasmi ili kufungua kongamano hilo.
3
Baadhi ya wanasheria wanawake na wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika kongamano hilo.
4
Kutoka kulia Mgeni rasmi katika Kongamano hilo Mkurugenzi wa Huduma za Sheria kwa Umma Bw. Justus Mulokozi, akiwa na Mkurugenzi wa TAWLA Bi. Tike Mwambipile na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Bi. Pindi Chana.
5
Watoa mada wa kongamano hilo wakifuatilia kongamano hilo.
6
Baadhi ya wadau mbalimbali katika picha tofauti wakionekana kufuatilia na kuandika mambo muhimu yanayojadiliwa katika kongamano hilo.
7891011
Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA Bi Tike Mwambipile akiwa katika picha ya pamoja na Nasieki Kisambu Kutoka TAWLA na Salome Argan Mtoa mada wa Kongamano hilo kutoka Legal Advicer For Africa Center for Reproductive Rights.
12
Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake TAWLA Bi Tike Mwambipile akifurahia jambo na Jaji Winnie Korosso.

JAFO AWAAGIZA WAHANDISI WA MAJI KUSIMAMIA VYEMA MIRADI YA MAJI

0
0
Halmashauri alizofanya ziara yake ni pamoja na halmashauri ya wilaya ya kilindi Kiteto, Babati Mji, Babati, Mji Mbulu na Halmashauri ya Mbulu vijijini.Katika ziara hiyo pia alifanikiwa kuzungumza na watumishi na kutembelea miradi ya Elimu, Afya, Maji na Miundombinu ya barabara.

Akizungumza na watumishi, Jafo aliwaagiza wahandisi wa maji kusimama imara katika kusimamia miradi ya maji inayo endelea kujengwa ili miradi hiyo iweze kuwa na ubora unaokusudiwa ili kuondoa changamoto za upatikanaji wa maji katika jamii.

“Kila mradi wa Maji lazima uwe chini ya usimamizi wa chombo cha watumia maji ili miradi hii iwe endelevu,”amesema Jafo.
 Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akiwa katika Ukaguzi wa ujenzi wa Lambo la kuvuna maji ya mvua wilayani kilindi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo akikagua ujenzi wa barabara za halmashauri na ujenzi wa madaraja Katika halmashauri ya wilaya ya kilindi.
Naibu waziri Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi)akisaini kitabu cha wageni alipokuwa akikagua hospitali ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Seleman Jafo, amefanya ziara katika Halmashauri 6 za mikoa ya Tanga na Manyara huku akiwaagiza Wahandisi wa maji wa Halmashauri hizo kusimamia vyema miradi ya maji inayoendelea kujengwa katika halmashauri hizo.

ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA UONI DUNIANI

0
0
Mtaalamu wa macho kutoka China Dkt. Zhao Wei akimpima macho Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kwenye maadhimisho ya siku ya uoni Duniani yaliyofanyika kitaifa kituo cha Afya cha Magogoni, Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupima macho kwenye maadhimisho ya siku ya uoni Duniani yaliyofanyika Kituo cha Afya Magogoni wakiendelea kuangaliwa macho.
Mratibu wa huduma za macho Zanzibar Dkt. Rajab Mohammed Hilal akisoma risala ya kitego cha matibabu ya macho kwenye maadhimisho ya siku ya uoni Duniani yaliyofanyika Kituo cha Afya Magogoni, Mjini Zanzibar.
Mwakilishi wa Shirika la Sightsaver Tanzania Andrew Kilewela akibadiliishana mawazo na Mratibu wa Mradi wa Afya ya macho Zanzibar Dkt. Fatma Juma Omar wakati wa maadhimisho ya siku ya uoni Duniani katika Kituo cha Afya Magogoni.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa Kituo cha Afya Magogoni kwenye maadhimisho ya siku ya uoni Duniani yaliyofanyika katika Kituo hicho.

………………………………………………………………………

Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amewataka wananchi kuendelea kuvitumia vituo vya afya vilivyo karibu nao vinavyotoa huduma za macho katika jamii ili kupambana na upofu usiowalazima.

Amesema vituo vingi vya Afya hivi sasa vimewekewa huduma muhimu za uchunguzi wa maradhi mbali mbali, ikiwemo uchunguzi wa macho, na hakuna haja ya wananchi kukimbilia Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.

Waziri Mahmoud ameeleza hayo katika maadhimisho ya siku ya uoni Dunini yaliyofanyika Kitaifa kituo cha Afya Magogoni Wilaya ya Magharibi B.

Amesema madaktari wanapohisi tatizo ni kubwa na haiwezekani kupata matibabu katika vituo vidogo wanaamua kumpeleka mgonjwa Hospitali Kuu hivyo hakuna haja ya kuwa na wasiwasi na viituo hivyo.

Amesema tatizo la uoni limekuwa kubwa duniani kote na inakisiwa hivi sasa kuna watu wasioona wapatao milioni 285 na asilimia 37 kati yao hawaoni kabisa.

Kwa upande wa Zanzibar amesema inakisiwa kuwa na watu 10,000 ambao wanamatatizo ya uoni na asilimia 50 kati ya hao hawaoni kabisa kutokana na sababu mbali mbali.

Waziri wa Afya ameongeza kuwa wataalamu wa maradhi ya tiba ya macho nchini kwa kushirikiana na Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) pamoja na taasisi mbali mbali duniiani wako katika mikakati ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya maradhi ya macho.

Hata hivyo amesisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya inajitahidi kuendeleza huduma za matibabu ya macho katika nyanja zote katika vijiji mbali mbali Unguja na Pemba kupitia Kitengo chake cha Afya ya msingi ya matibabu ya macho vijijini.

Amewataka wananchi kufanya juhudi kuepuka maradhi ambayo yanapelekea matatizo ya macho na kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara kwani ni moja ya tiba ya kujiepusha na maradhi mengi.

Aidha alilishukuru Shirika la Kimataifa la Sightsaver kwa ushirikiano wake wa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na misaada ya kitaalamu na dawa wanazosaidia kitengo cha matibabu ya macho.

Katika risala ya wafanyakazi wa Kitengo cha matibabu ya macho iliyosomwa na Mratibu wa Kitengo hicho Dkt. Rajab Mohammed Hilal wamesema wanakabiliwa na udogo wa nafasi ya kutekeleza katika kitengo hicho.

TWANGA, PAPII, BABU SEYA KUTUMBUIZA TAMASHA LA WAFUNGWA UKONGA KESHO

0
0
papii
Wanamuziki wakongwe wanaotumikia kifungo cha maisha ndani ya Gereza la Ukonga, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.

TAMASHA kubwa la wafungwa linatarajiwa kuunguruma kesho kuanzia saa 2 asubuhi na habari njema ni kwamba, Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ itatumbuiza sambamba na wanamuziki wakongwe wanaotumikia kifungo cha maisha ndani ya Gereza la Ukonga, Nguza Viking ‘Babu Seya’ na Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.Pia msanii wa Singeli, Msaga Sumu ataporomosha burudani.

Tamasha hilo lenye lengo la kuwatia moyo wafungwa na kuwaonesha kwamba wapo pamoja na Watanzania wenzao ambao wanaishi huru litakuwa la aina yake kwani mbali na burudani kamambe kutoka kwa Twanga Pepeta, mhamasishaji mashuhuri Afrika Mashariki na Kati, Eric Shigongo atakuwepo kuwatia moyo wafungwa.
twanga
Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ 

Shigongo ambaye ndiye Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers, Wachapishaji wa Magazeti ya Ijumaa Wikienhemda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, amesema anatambua wafungwa waliopo gerezani nao wanahitaji faraja na kutiwa moyo kwa namna moja au nyingine, kwani nao walikuwa na ndoto zao hivyo kuwatia moyo ni jambo jema.

“Hii si mara ya kwanza kwa Global kuandaa tamasha la namna hii, mwaka 2008 tuliandaa, tunapozungumza pamoja na ndugu zetu waliopo gerezani huwa nao wanafarijika.

“Wanaona tuko nao pamoja. Mtu kufungwa haimaanishi kwamba hana maisha tena, haimaanishi kwamba hawezi kutimiza ndoto zake, haimaanishi kwamba alikuwa mkosaji sana asiyefaa katika jamii.“Bado mfungwa ana nafasi ya kujitunza, kuwa na malengo, kujiandaa na kutimiza ndoto zake pindi wakitoka gerezani. Mifano ninayo mingi tu, kuna wafungwa ambao tulizungumza nao mwaka 2008, kesho hii wameshatoka na wanakuja ofisini kwetu kutushukuru.
live3
Msanii wa Singeli, Msaga Sumu.
“Wanasema kupitia tamasha lile tuliwatia moyo na walibadilika na sasa wanaishi vizuri katika jamii zinazowazunguka na wanafanya biashara mbalimbali na wana mafanikio makubwa tu,” alisema Shigongo.
Mratibu wa tamasha hilo, Juma Mbizo, amesema mbali na burudani kali kutoka kwa Twanga, kutakuwepo na michezo mbalimbali kama ya mpira wa miguu, kuvuta kamba na mingineyo ambapo zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washindi.

“Kama unavyojua Ijumaa itakuwa ni Nyerere Day, hivyo tutamkumbuka muasisi wa taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kuimba, kucheza pamoja na wafungwa.“Twanga wataporomosha nyimbo zao kali. Wanamuziki wote wakali wa Twanga watakuwepo, wataimba pamoja na wanamuziki waliopo gerezani.

“Kuna wanamuziki maarufu waliotamba enzi hizo kama Papii Kocha na Babu Seya ambao wanatumikia kifungo chao cha maisha, nao watatumbuiza siku hiyo, tutapata fursa ya kuwaona live ndani ya Gereza la Ukonga,” alisema Mbizo.

Pamoja na maneno mazuri ya kutia moyo yatakayotolewa na Shigongo, Mkuu wa Gereza la Ukonga, ACP Stephen Mwaisabila naye anatarajiwa kutoa neno katika tamasha hilo sanjari na viongozi wengine wa magereza.

TRA WAVUKA MALENGO YA UKUSANYAJI MAPATO ARUSHA

0
0
Meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Arusha, bwana Apili Mbaruku.


Mamalaka ya mapato mkoa wa Arusha (TRA) imekusanya shilingi bilioni 64.6, ikiwa imevuka malengo yake iliyojiwekea awali ya kuweza kukusanya shilingi bilioni 63.1. Ongezeko hilo, ni sawa na asilimia 102, kulingana na meneja wa Mamlaka ya mapato (TRA) mkoani Arusha, bwana Apili Mbaruku. 

Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa Globu ya Jamiii mapema leo,Meneja wa mamlaka hiyo mkoa wa Arusha Apili Mbaruku alielezea kuwa ongezeko hilo linatokana na majumuisho ya makusanyo ya mwezi Julai na Agosti mwaka huu. 

“Ni kweli tumeweza kukusanya kiasi hiki cha fedha, na hii inatokana na
kukua kwa mwamko wa ulipaji kodi mkoani hapa japokuwa bado zipo
changamoto kadhaa za baadhi ya wafanyabisahara kutokuelewa umuhimu wa kulipa kodi,” alisema meneja huyo. 

Apili ametaja sekta ya utalii kuongoza katika ulipaji huo wa kodi. 
“Tumekuwa tukitoa elimu kwa wafanyabiashara waweze kuelewa umuhimu wa kulipa kodi na kukwepa usumbufu usio na lazima,” alishauri meneja
huyo. 

Hata hivyo, Mbaruku aliweka wazi kuwa ofisi yake ilishindwa kufikia
malengo ya ukusanyi wa mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16. 
“Kwa mwaka uliopita malengo yetu yalikuwa kukusanya shilingi 329.5
lakini kwa bahati mbaya tulipata shilingi bilioni 324.6 tu”. 
Na Woinde Shizza,Arusha.

Akifanunua zaidi kuhusu makusanyo ya mwaka huu, Mbaruku alisema kuwa
kiasi cha bilioni 30.3 zilitokana na makusanyo ya ndani wakati
shilingi bilioni sita zilitokana na malipo ya ushuru. Aidha, Mbaruku ameongeza kuwa ofisi yake inatarajia kukutana na
maofisa wa jiji la Arusha kuanza kukusanya makusanyo ya kodi za
majengo. 

Kulingana na meneja huyo wa TRA, ofisi yake inalenga kukusanya kodi
kutoka kwenye majengo 20, 536 mkoani hapa. Mamlaka ya mapato mkoni
Arusha(TRA) imevuka lengo la makusanyo yake kwa mwaka wa fedha
2016/17. 

“Nia yetu ni kuanza kukusanya kodi kutoka kwenye majengo hayo, na
tayari tumeshafanya mawasiliano na maofisa wa jiji na kuweza
kubainisha majengo hayo,” aliongeza meneja huyo wa TRA mkoani Arusha.
Viewing all 46201 articles
Browse latest View live




Latest Images