Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1001 | 1002 | (Page 1003) | 1004 | 1005 | .... | 1898 | newer

  0 0  0 0


  0 0

   Wataalamu wa Masuala ya Uchumi na Fedha kutoka Tanzania wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, wakifuatilia mazungumzo ya mkutano kati ya Shirika la Fedha Duniani-IMF na Wizara ya Fedha na Mipango, mkutano uliofanyika katika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
   Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (Kulia) wakiwa katika kikao cha kazi na uongozi wa juu wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, ambapo masuala kadhaa yanayohusu hali ya uchumi na maendeleo ya miradi inayofadhiliwa na shirika hilo ilijadiliwa, Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, Jijini Washington DC, Marekani.
   Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (wa tatu kutoka kushoto) akiwa kwenye mkutano na Magavana kutoka nchi mbalimbali za kiafrika wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, Jijini Washington DC nchini Marekani, akielezea juu ya ukuaji wa uchumi katika shughuli za mawasiliano, madini,  huduma ya fedha, bima na huduma za uzalishaji wa viwandani pamoja na changamoto zilizopo..
   Naibu Gavana wa Benki Kuu Dkt. Natu A. Mwamba akifafanua juu ya changamoto zinazoikumba Tanzania katika kukuza  uchumi hasa katika sekta ya Elimu, Afya na Miundombinu, akiwa mmoja wa wachokoza mada wengine kutoka nchi kadhaa za Kiafrika kwenye mkutano uliojadili kuhusu hali ya Afrika,  Jijini Washington DC –Marekani.
   Baadhi wa wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria mkutano wa hali ya ukuaji wa uchumi katika Nchi za Afrika wakati Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania alipokuwa akiwasilisha mada, Jijini Washington DC-Marekani.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James akiwa na Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndullu wakibadilishana mawazo baada ya kushiriki mikutano ya siku ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, nje ya ukumbi wa mikutano ya Benki ya Dunia Jijini Washington DC- Marekani.

  0 0

    Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama akipata maelezo kuhusiana na Elimu ya Mpiga Kura alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) leo mkoani Simiyu.

   Baadhi ya Wanachi wakifuatilia ufunguzi rasmi wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere wilayani Bariadi mkoani Simiyu leo.
   Watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiandaa vipeperushi vya Elimu ya Mpiga Kura tayari kuwagawia viongozi na wananchi wanaotembelea Banda la Maonesho la NEC.
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama (katikati) akikata utepe kufungua rasmi maadhimisho ya Wiki ya Vijana leo mkoani Simiyu.   Kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo Mhe. Anthony Mavunde, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka (wa pili kutoka kushoto), Waziri Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Titus Kamani na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia).Picha na Aron Msigwa – NEC.
  Wananchi wilayani Bariadi mkoani Simiyu wakipata elimu ya Mpiga Kura kwenye banda la Maonesho la NEC leo.


  Na. Aron Msigwa –NEC.
  9/10/2016. Bariadi –Simiyu.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imepongezwa kwa kuanzisha programu endelevu  za utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura kwa kuwafikia wananchi moja kwa moja katika maeneo yao kote nchini.

  Akitoa pongezi hizo mara baada ya kutembelea Banda la Maonesho la Elimu ya Mpiga Kura la NEC wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika Bariadi mkoani Simiyu,  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Muhagama amesema kuwa hatua ya NEC  kutoa elimu ya mpiga kura kupitia maonesho hayo inawasaidia wananchi kujifunza masuala mbalimbali kuhusiana na chaguzi za Tanzania.

  “ Nawapongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuanzisha utaratibu huu wa kushiriki maonesho mbalimbali, mnafanya kazi nzuri, endeleeni hivyo hivyo kuwaelimisha wananchi” Amesema Mhe. Jenista.

   Ameeleza kuwa ushiriki wa NEC katika maadhimisho ya Wiki ya Vijana unawapa fursa vijana wengi kupata elimu sahihi kuhusu wajibu wao na majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kuratibu na kusimamia Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani.

  Kwa upande wake Afisa Habari wa Idara ya Elimu ya Mpiga Kura ya NEC Bi. Margareth Chambiri amwemweleza Waziri huyo kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanzisha program endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura kwa kuhakikisha kuwa wananchi moja kwa moja katika maeneo mbalimbali nchini.

  Amesema NEC inatoa elimu hiyo kwa wananchi ili kuwawezesha kuwa na uelewa sahihi kuhusu utendaji wa Tume na masuala mbalimbali yanayohusu upigaji wa kura, sheria, taratibu na kanuni zinazosimamia uchaguzi, taarifa za wapiga kura na maelekezo ya namna ya kufanya endapo kadi zao za kupigia kura zimepotea au kuharibika, mwananchi kuhama eneo moja kwenda jingine kutokana na sababu mbalimbali.

  Baadhi ya wananchi waliolitembelea banda la NEC wameeleza kufurahishwa ufafanuzi  na elimu ya Mpiga kura inayoendelea kutolewa na Maofisa wa Tume hiyo  kupitia majibu ya maswali mbalimbali wanayouliza hususan uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kwa mujibu wa Sheria ambao utakaowapa fursa ya kuhuisha taarifa zao pia kupewa elimu kuhusu uendeshaji wa chaguzi mbalimbali hapa nchini.

  Aidha, wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuendelea kutoa elimu ya Mpiga kura katika maeneo  mengine nchini kwa ili kuwawezesha wananchi wengi zaidi kupata elimu sahihi kuhusu utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.


  0 0

   Mwanafunzi bora wa somo la bailojia kitaifa kwa mwaka 2016, Bi. Anab Faisal Issa (katikati) akiwa katika picha na wazazi wake, Bw. Faisal Issa (wa pili kulia) na Bi. Beng’i Issa (wa pili kushoto) pamoja na walimu wa shule ya sekondari Feza mara baada ya kupokea tuzo katika hafla fupi iliyoandaliwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali kwa lengo la kuwatambua na kuwapa moyo wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.  Hafla hiyo ilifanyika Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Afisa tawala wa wizara ya afya Bw Michael John akikabidhi cheti kwa mwanafunzi bora wa somo la bailojia kitaifa kwa mwaka 2016 kutoka shule ya Feza  Bi.Anab Faisal Issa katika hafla iliyoandaliwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali kwa lengo la kuwatambua na kuwapa moyo wanafunzi wengine kupenda masomo ya sayansi.

  0 0

  Afisa Mkuu Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Frank Kanyusi akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.  Alionya wafanyabiashara ambao hawajasajili majina ya biashara kufanya hivyo katika kipindi cha miezi miwili kuanzia sasa au kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetoa muda wa miezi miwili kwa wafanyabiashara wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajiliwa wafanye hivyo haraka.

  Akizungumza na waandishi wa waandishi wa jijini Dar es salaam  jana, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Frank Kanyusi alisema katika zoezi la kutoa elimu na kurasimisha majina ya biashara na kampuni linaloendelea katika mikoa mbalimbali imebainika kuwa wafanyabiashara wengi wanatumia majina ya biashara pasipo kuyasajili.

  “Sheria ya majina ya biashara inamtaka mfanyabiashara kusajili jina la biashara yake ndani ya siku 28 toka aanze kulitumia,” alisema Bw.Kanyusi na kuongezea kuwa kinyume na hapo atakuwa amevunja sheria ya majina ya biashara.

  Alisema baada ya muda huo kupita, patakuwa na msako nchi nzima ili kuwabaini wale wote wanaotumia majina ya biashara pasipo kusajili na kuwafikisha katika vyombo vya sheria au kuwatoza faini.

  Alisema kuwa sasa usajili wa majina ya biashara umerahisishwa kwani unafanywa kwa njia ya mtandao kwa kutembelea tovuti ya wakala huo ambayo ni www.brela.go.tz ili kupata maelezo yote ya namna ya kusajili jina la biashara.

  Aliwataka wafanyabiashara wasiishie kusajili tu jina la biashara bali pia waende katika Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa ajili ya kupata namba ya Mlipa Kodi (TIN) pia waendele katika halmashauri zao kupata leseni ya biashara.

  “Kwa kurasimisha biashara serikali itapata mapato kwani wigo wa walipa kodi utaongezeka na pia itakuwa faida kwa wafanyabiashara katika kujengewa mazingira bora ya kufanya biashara,” alisisitiza Bw.Kanyusi.

  Alisema BRELA imejipanga kuzunguka mikoa yote nchini ili kutoa elimu juu ya urasimishaji wa majina ya biashara na makampuni kwani imeonekana wananchi hawana uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa urasimishaji.

  Hadi sasa BRELA imefanya ziara katika mikoa ya Mwanza, Mara, Geita na Simiyu na wiki hii watakuwa mkoani Shinyanga kwa muda wiki moja katika kuhamasisha wafanyabiashara kurasimisha biashara zao.

  Alisisitiza kuwa ni lazima kuhakikisha kuwa biashara zinarasimishwa ili serikali iweze kuwatambua walipa kodi wake ambao watachangia pato la taifa na kuiwezesha Tanzania kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

  0 0


  Mkuu wa gereza la Karanga, mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro, ambako ndiko kilipo kiwanda cha kutengeneza viatu, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP), Hassan Bakari Mkwiche, (kushoto), akionyesha kitu, wakati Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (wakwanza kulia), alipotembelea kiwanda hicho ili kuona eneo lililotengwa kwa ujenzi wa kiwanda kipya cha kisasa cha viatu, Oktoba 9, 2016. Wengine pichani ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, (wapili kushoto), Mkuu wa magereza mkoani Kilimanjaro, Kamishna Msaidizi wa Polisi, (ACP), Anderson Kamtera.
  Bw. Erio, na maafisa wake, wakipatiwa maelezo na maafisa wa Jeshi la Magereza alipokagua moja ya maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho

  NA K-VIS MEDIA, MOSHI

  MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio, ametembelele kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga mjini Moshi mkoani Kilimanjaro Oktoba 9, 2016, ili kuona eneo ambalo kitajengwa kiwanda kipya na cha kisasa.

  Bw. Erio ambaye alifuatana na Mkurugenzi wa Uwekezaji wa Mfuko huo, Bw. Steven Alfred, na Meneja Uhusiano, Bi.Lulu Mengele, pia alipata fursa ya kupokea taarifa ya uendeshaji wa kiwanda cha sasa na changamoto zinazokikabili. Bw. Erio alisema, ziara yake inalenga kujua mambo mawili ambayo ni kuona eneo patakapojengwa kiwanda kipya cha kutengeneza bidhaa za ngozi, lakini pia kupata uelewa wa nini kifanyike ili kuboresha kiwanda cha sasa ambacho kilijengwa mwaka 1977.

  Maafisa wa kiwanda hicho, walimuonyesha maeneo mawili ambayo yanafaa kujengwa kiwanda hicho. “Kama mtakumbuka, wiki iliyopita mimi na Kamishna Jenerali wa Magereza, (CGP), John Minja tulisaini makubaliano ya ushirikiano kati ya PPF na Jeshi la Magereza katika kukiboresha kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga, lakini pia kujenga kiwanda cha kisasa cha kuchakata ngozi na kutengeneza bidhaa zitokanazo na ngozi.” Alianza kwa kusema.

  Alisema, nia ya Mfuko ni kuona kazi ya ujenzi wa kiwanda kipya inakamilika ifikapo Desemba 2018 ili kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda. “Wakati tukisubiri ujenzi wa kiwanda kipya ukamilike, lazima pia tuboreshe hiki cha sasa kwa kuimarisha miundombinu iliyopo, na hivyo kuongeza uzalishaji na kupanua masoko ” alisema Bw. Erio.

  Aliagiza wataalamu wa PPF kwa kushirikiana na wenzao wa Magereza (kiwanda cha Karanga), wakutane haraka ili kuainisha chamngamoto zinazokikabili kiwanda cha sasa, ili uboreshaji wa mitambo uweze kufanyika kwa haraka.” Alifafanua.

  Awali Kaimu Mkuu wa kiwanda cha viatu Karanga, Naibu Mrakibu wa Magereza,( ASP), Michael Minja, alisema kiwanda cha sasa kinakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na uchakavu wa mitambo, ambapo alisema baadhi ya mashine zimepitwa na wakati na zingine zimeharibika na hivyo zinahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa.

  “Mambo yanayotakiwa kufanyiwa kazi ili kuwezesha uendeshaji bora wa kiwanda, ni pamoja na kununua vipuri kwa ajili ya ukarabati wa baadhi ya mashine, lakini pia kuna upungufu wa baadhi ya mashine hivyo tunahitaji kuongeza idadi yake.” Alisema ASP Minja.

  Akizungumza kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza, Kamishna wa Magereza, (CP), Editha Malya, alisema, Jeshi la Magereza limefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na PPF katika kushirikiana katika uendeshaji wa kiwanda cha viatu Karanga ikiwa ni pamoja na ujenzi wa kiwanda kipya na cha kisasa.

  “Tutashirikiana kwa karibu ili kuhakikisha azma yetu inatimia kwa haraka,” alisema CP Malisa. Kiwanda cha viatu Karanga, kilichoko kwenye eneo la Gereza la Karanga mjini Moshi, kilizinduliwa na Rais wa awamu ya kwanza, Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Juni 3, 1977 na wateja wakubwa wa bidhaa za kiwanda hicho ni taasisi cha kijeshi, ikiwa ni pamoja na JWTZ, JKT, Magereza na Jeshi la Polisi.
  Kamishna wa Magereza, (CP), Editha Malya, aliyemuwakilisha Mkuu wa Jeshi la Magereza Nchini, (CGP), akizungumza wakati wa kikao cha kupeana taarifa na ujumbe wa PPF ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu Erio Oktoba 9, 2016
  Bw. Erio, akizungumza wakati wa mkutano huo mfupi kabla ya kukagua maeneo hayo ya ujenzi
  Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, (katikati), akizungumza jambo wakati wa mkutano huo. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele, na kushoto ni Kamishna wa Magereza, Editha Malya
  Afisa magereza ambaye ni fundi viatu wa kiwanda cha viatu cha gereza la Karanga, akishona viatu
  Bw. Erio, akiongozwa na mama Malya, na maafisa wengine akitembelea kiwanda
  Kaimu Mkuu wa Kiwanda cha kutengeneza viatu cha Karanga, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, (ASP), Michael Minja, akitoa taarifa ya utendaji wa kiwanda
  Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. Erio, na Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Alfred, wakiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo
  Bw. Erio(kushoto), akiangalia moja ya viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo
  Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Bw. Steven Alfred, akionyeshwa namna kiatu kinavyotengenezwa, (katikati) ni mwakilishi mkuu wa ofisi ya PPF mkoani Kilimanjaro, Bw. Jacob Cornel Sule
  Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. Erio, na Mkurugenzi wa Uwekezaji Bw. Alfred, wakiangalia viatu vilivyotengenezwa kiwandani hapo. Kushoto ni Mkuu wa Gereza la Karanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, (ACP), Hassan Bakari Mkwiche
  Mkuu wa kitengo cha umeme wa Kiwanda cha viatu Karanga, Staff Surgent, Aulelia Mushi, akziungumzia mahitaji ya umeme kiwandani hapo
  Maafisa wa wa Jeshi la Magereza, wakisikiliza mazungumzo hayo
  Picha ya Pamoja baada ya kutembelea kiwanda
  Ukaguzi wa moja ya maeneo ya ujenzi wa kiwanda
  Jiwe la msingi aliloweka Mwalimu Nyerere wakati wa ufunguzi wa kiwanda Juni 3, 1977
  Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu Mengele, (watatu kushoto), akiangalia moja ya viatu vinavyotengenezwa kiwandani hapo, Kushoto ni Kamishna wa Magereza, Editha Malya, Mwakilishi Mkuu wa PPF, Mkoani Kilimanjaro, Jacob Cornel Sule, Mkuu wa Magereza mkoani Kilimanjaro, (RPO), Kamishna Msaidizi wa Magereza, Anderson Kamtera, na maafisa wengine
  Bw. Erio akisalimiana na Kamishna wa Magereza, Editha Malya

  0 0


  0 0

  Kituo cha EFM kimeendelea na harakati zake za kuwasaidia na kuwainua vijana wanaojihusisha na muziki. Kwa kutumia shindano maalumu la singeli michano linalofanyika kila siku ya jumamosi kuanzia saa nne hadi saa sita mchana, EFM radio inasaka wasanii chipukizi wenye vipaji vya kuimba nyimbo za singeli na baadae kuwaendeleza katika muziki huo. 

  Zoezi hili ni endelevu na litadumu kwa muda wa wiki 12 katika maeneo mbalimbali ya Dar es salaam na Pwani ambapo muziki mnene utafika. 

  Jumla ya wasanii 5 huibuka na ushindi na washindi hawa hupatikana kila eneo ambapo zoezi hili la kusaka vipaji vipya vya singeli (Singeli Michano) hufanyika. 

  Meneja matukio na mawasiliano ya efm redio Neema Mukuarsi amesema baada ya zoezi hili wasani hawa chipukizi watapata nafasi ya kupata semina kutoka kwa TCRA, BASATA na TRA pale Dar live siku ya ijumaa ya tarehe 14.10.2016 saa 8;00 mchana ili waweze kupata elimu ya kulipa kodi,waweze kuimba nyimbo zenye maadili na kuhakikisha nyimbo zao zinakuwa na maadili katika jamii. 

  Msaani chipukizi, Jfari Salumu a.k.a Winnero akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka vipaji vya kuimba nyimbo za singeli jijini Dar es Salaam.
  Msaani chipukizi,Ramadhani Iddi a.k.a Sindano Simba akionesha uwezo wake jukwaani katika tamasha la kusaka vipaji vya kuimba nyimbo za singeli jijini Dar es Salaam.
  Mashabiki wa mziki wa nyimbo za singeli wakiendelea kupagawa katika tamasha la kusaka vipaji vya kuimba nyimbo za singeli jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wakuu wa Taasisi na Idara za wizara (hawapo pichani), wakati wa kikao cha  kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kulia ni Naibu Waziri  Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akizungumza na wakuu wa Taasisi na Idara za wizara wakati wa kikao cha  kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya wizara. Kulia ni Naibu Waziri Mhandisi Hamad Masauni. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, akizungumza wakati  wa kikao cha  kujadili masuala mbalimbali ya mipango na maendeleo ya  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Idara zake. Kikao hicho kiliongozwa na Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba (hayupo pichani). Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Minja. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara, jijini Dar es Salaam.
  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.

  0 0  0 0

   Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili unapenda kuutarifu Umma kwamba haijamzuia Bi. Mwajuma Ramadhani Kimweri kutoka hospitalini kwa madai ya kushindwa kulipa pesa za matibabu kama ilivyoandikwa na Gazeti la Jambo Leo lenye namba ISSN 7826 No 2589, hivyo taarifa hizo si za kweli.

  Katika ukurasa wa mbele, gazeti hilo limechapisha taarifa yenye kichwa cha habari kinachosema “Mgonjwa saratani azuiwa Muhimbili miezi miwili ni baada ya kushindwa kulipa deni la Sh. 330,000”.

  Bi. Mwajuma Ramadhani Kimweri kwa mara ya kwanza alilazwa Muhimbili Agosti 29, 2016  akitokea mkoani Morogoro na kuruhusiwa Septemba 10, 2016  na  Septemba 23, 2016  alilazwa tena na kuruhusiwa Septemba 24, 2016.

  Baada ya vipimo vya awali kufanyika Septemba 29, 2016 alilazwa tena na kufanyiwa  upasuaji Septemba 30, 2016 na kuruhusiwa Oktoba 04, 2016 baada ya taratibu za matibabu kukamilika.

   Mgonjwa  aliingizwa kwenye utaratibu wa msamaha na kuchangia Shilingi 70,000 tu, kati  ya Shilingi 400,142.33. Hivyo si kweli kwamba mgonjwa alilipa Shilinngi 380,000 kama ilivyoandikwa na gazeti hilo.

  Kuhusu tiba ya mionzi, Bi. Mwajuma Ramadhani Kimweri amefanyiwa vipimo vingine hivyo atatakiwa kurejea baada ya wiki tatu kwa ajili ya majibu na si kweli kwamba Muhimbili imezuia uhamisho wake kwenda Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kwa ajili ya tiba hiyo.
  Imetolewa na;

  Uongozi wa  Hospitali ya Taifa Muhimbili
  Oktoba  10, 2016.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hall of Fame Boxing Promotions Jay Msangi (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusiana na pambano la bondia Ibrahim Class ambaye atapambana na bondia Jason Bedeman wa Afrika Kusini kuwania mkanda wa Light wa uzito wa Chama Cha WBF na Abdallah Pazi (Dulla Mbabe) ambaye atapambana na bondia , Zheng Chengbo wa China katika pambano la kimataifa.
  Bondia Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ (kulia) akizungumza katika mkutano huo. Pazi atapambana na bondia Zheng Chengbo wa China katika pambano la kimataifa la uzito wa Super Middle. Kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Hall of Fame Boxing and Promotions, Jay Msangi
  Bondia Ibrahim Class (kulia) akizungumza katika mkutano huo. Class atapambana na bondia Jason Bedeman wa Afrika Kusini kuwania mkanda wa Light wa uzito wa Chama Cha WBF. Kushoto ni bondia Abdallah Pazi

  Bondia nyota nchini, Abdallah “Dulla Mbabe” Pazi atapanda jukwaani Oktoba 28 kupambana na bondia kutoka China, Zheng Chengbo katika pambano la kimataifa uzito wa Super Middle. Mbali ya Mbabe, bondia mwingine wa Tanzania, Ibrahim Class ambaye ni bingwa wa kimataifa wa World Professional Boxing Federation (WPBF) na Universal Boxing Organization (UBO) naye atapanda ulingoni kuwania ubingwa wa kimataifa wa WBF kwa kupambana na bondia kutoka Afrika Kusini Bedeman ambaye ni bingwa wa zamani wa uzito wa light wa vyama vya WBA na IBO. 

  Akizungumza jijini jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Hall of Fame Boxing Promotions Jay Msangi alisema kuwa mapambano hayo yatafanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee hall na mabondia hao watawasili nchini wiki moja kabla ya pambano. Msangi alisema kuwa maandalizi ya mapambano hayo yamekamilika na mabondia wote walikuwa kwenye maandalizi makali chini ya makocha wao. 

  Alisema kuwa Mbabe kwa sasa anasimamiwa na kocha wake, Shomari Kimbau wakati Class yupo chini ya kocha nyota nchini, Habib Kinyogoli na bingwa wa zamani wa Dunia, Rashid Matumla. “Maandalizi yapo vizuri na mabondia wote wapi katika morali ya juu, Mbabe anataka kudhihirisha ubora wake nchini katika uzito wa Super Middle kwa kumchapa Mchina ambaye kwa sasa yupo katika timu ya Olimpiki ya China na ni moto wa kuotea mbali,” 

  “Class baada ya kumchapa Cosmass Cheka na kutwaa ubingwa wa UBO mwaka huu na kuchmapa Mzambia Mwasa Kabinga kwa TKO raundi ya tisa, sasa anataka kuonyesha kuwa ni nyota mpya ya ngumi za kulipwa nchini kwa kumchapa bondia huyo wa Afrika Kusini,” alisema Msangi. Kwa upande wake, Mbabe alisema kuwa amejiandaa vizuri na anasubiri siku ya pambano lenyewe ili kuwapa raha Watanzania. 

  “Namsubiri Mchina kwa hamu sana, hatofika raundi ya tatu, sitataka adumu jukwaani kwa zaidi ya dakika 15,, nataka kumpa kipigo cha kihistoria ili aende kuwaambia wenzake kuwa kuna bondia hatari sana na wa kuogopwa hapa nchini,” alisema Mbabe. 

  Class alisema kuwa hana shaka na pambano na ushindi ni jadi yake. “Nipo fiti kwa ajili ya pambano, nipo tayari kwa changamoto, najua naye anajiandaa kama mimi, sitawaangusha Watanzania siku hiyo,” alisema Class.

  0 0

  Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imeanza utekelezaji wa zoezi la kubomoa kuta za nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya Mto Msuka katika eneo la Kilimahewa, kwa ajili ya kupanua mto huo ili kuondoa athari za mafuriko zinazojitokeza wakati wa mvua za masika. Wananchi wametakiwa kutojenga maeneo yasiyo rasmi.
  Na BMG
  Zoezi ka ubomoaji likiendelewa ambapo limesimamiwa na mgambo wa halmashauri hiyo ya Manispaa ya Ilemela
  Mto huu unapaswa kupanuliwa zaidi na kujengewa kuta maana wakati wa mafuriko huwa unapitisha maji mengi yanayosababisha mafuriko kwa wakazi wa eneo hili la Kilimahewa.
  Miongoni mwa kuta zilizoingia eneo la hifadhi ya mto Msuka baada ya kubobolewa
  Miongoni mwa kuta zilizoingia eneo la hifadhi ya mto Msuka baada ya kubomolewa
  Na George Binagi-GB Pazzo 
  Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza imeanza utekelezaji wa zoezi la kubomoa kuta za nyumba zilizojengwa kwenye hifadhi ya Mto Msuka katika eneo la Kilimahewa, kwa ajili ya kupanua mto huo ili kuondoa athari za mafuriko zinazojitokeza wakati wa mvua za masika.


  Mhandisi wa Manispaa hiyo, Jacob Mwakyambiki, amesema zoezi hilo limefanyika baada ya tahadhari kutolewa kwa wakazi wa eneo hilo kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita na kwamba mpango uliopo ni kujenga mtaro mkubwa katika mto huo ili kusaidia maji yake kutosababisha mafuriko wakati wa mvua za masika.


  Amesema tayari mkandarasi ameanza kazi hiyo na kwamba ujenzi wa mto huo utakapokamilika, utasaidia maji yake kutiririka moja kwa moja hadi ziwa Victoria badala ya kumwaga maji kwenye makazi ya watu kama ilivyokuwa hapo awali na kusababisha athari za kimafuriko.


  Hata hivyo baadhi ya wakazi wanaoishi katika eneo linalopitiwa na mto Msuka wamesema zoezi hilo limefanyika wakati ambao bado hawajui hatima yao kwani wakati wanajenga makazi yao katika eneo hilo walipata vibali vyote ikiwemo hati miliki za viwanja vyao ambapo wamependekeza kulipwa fidia licha ya Manispaa ya Ilemela kuwatahadharisha kwamba hakuna fidia itakayotolewa kwa waliojenga katika hifadhi ya mto.


  Licha ya malalamiko hayo, baadhi ya wakazi wa Kata ya Ibungilo wanaoishi katika maeneo jirani na mto Msuka wamepongeza zoezi la upanuzi wa mto huo kwani wamekuwa wakipata athari kubwa ikiwemo mali zao kusombwa na maji wakati wa mvua za masika kutokana na makazi ya wananchi yaliyojengwa kwenye karibu na mto huo.


  Katika misimu kadhaa ya mvua za masika, athari mbalimbali ikiwemo vifo vya watu na mifugo kutokana na mafuriko ya mto Msuka, zimekuwa zikitokea katika eneo la Kilimahewa kutokana na wananchi kujenga makazi yao hadi kwenye hifadhi ya mto huo hivyo upanuzi na ujenzi wake unaelezwa kuwa mwarobaini wa kadhia hiyo.


  0 0

  Na Ally Daud-MAELEZO

  DAWA muhimu za binadamu zinapatikana kwa wingi katika Bohari kuu ya dawa MSD kwa masaa 24 zikiwemo dawa za kutibu Malaria, Kifua kikuu, Ukoma ,ARV , dawa za kutuliza maumivu pamoja na Anti- biotic ili kutimiza na kutekeleza sera ya mpango wa Afya wa awamu ya tano.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya , Maendeleo ya Jamii, Wazee , Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika leo jijini Dar es salaam ili kuzungumzia hali ya upatikanaji wa dawa na chanjo nchini.

  “Dawa zote muhimu kwa binadamu zinapatikana kwenye bohari kuu ya dawa kwa masaa 24 kinyume na watu na Taasisi zisizo za kiserikali kusambaza maneno kuwa MSD imeishiwa dawa kitendo ambacho sio cha kweli dawa zipo na zinasambazwa kwenye vituo vyote vya afya” Alisema Mhe. Ummy.

  Aidha Ummy amesema kuwa ili kutekeleza mpango wa sera ya afya ya Serikali ya tano ,jumla ya shilingi bilioni 251 zimetengwa ili kuweza kuhakikisha dawa za binadamu zinapatikana kila wakati pindi zinapohitajika kutoka MSD ili kutoa huduma bora kwa watanzania.

  Aliongeza kuwa Serikali imetenga Bilioni 85 kwa ajili ya kulipa deni linalodaiwa na MSD ili kuhakikisha Bohari hiyo inajiendesha vizuri na kutokaukiwa dawa pindi zinapohitajika katika vituo vya afya na kutoa huduma za matibabu kwa muda muafaka kwa watanzania.

  Mbali na hayo Waziri huyo amesema kuwa tatizo la chanjo kwa sasa limepata ufumbuzi kwani zimeagizwa chanjo za watoto za kifua kikuu dozi milioni 2, chanjo za Pepopunda dozi milioni 1.2 na chanjo za Polio ambazo ni dozi 2 ili kuimarisha hali ya matibabu nchini.

  “Tulikuwa na tatizo la chanjo kama wiki nne zilizopita lakini tumejitahidi na tumeweza kuleta chanjo zote muhimu pamoja na kuagiza chanjo za surua ambazo zinatarajiwa kuja hivi karibuni ili kuhakikisha chanjo zinapatikana kwa wingi nchini” alisisitiza Waziri huyo.

  Aidha amesisitiza kuwa wanahitaji kununua na kufanya uzalishaji wa dawa katika viwanda vya ndani ili kuweza kuchangia uchumi wa viwanda vya ndani ili tufikie uchumi wa kati.

  Waziri Ummy aliwataka Wakurugenzi wa Vituo vya Afya pamoja na Waratibu wa Afya wa Wilaya kuagiza dawa MSD mapema bila ya kusubiri ziishe kabisa kwenye vituo vyao ili kuweza kuondoa usumbufu kwa wagonjwa.

  0 0

  Mkaguzi wa Ndani wa Serikali Bi Joan John akimwelekeza Bw.Benedict kalaguza jinsi ya kujaza fomu za uhakiki wa wastaafu wanaolipwa kupitia Wizara ya Fedha na Mipango.Zoezi hilo limeanzia mkoa wa Pwani wilaya ya Kibaha leo na litafanyika nchi nzima.
  Baadhi ya wastaafu mbalimbali wakiwa tayari kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki mkoani Pwani.Uhakiki huu unahusisha wanaolipwa kupitia Wizara ya Fedha na Mipango Pekee.

  Na Daudi Manongi,MAELEZO.

  Wizara ya Fedha na Mipango imeanza zoezi la Uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa na wizara hiyo katika mkoa wa Pwani, Kibaha. Uhakiki huu hautausisha wastaafu wanaolipwa kupitia mifuko ya hifadhi za jamii kama vile PSPF, NSSF, PPF na GEPF.

  Hayo yamebainishwa na Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Bw.Mohamed Mtonga alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari kuhusu mpango huo wa uhakiki ulioanza leo mkoani Pwani.

  “Uhakiki huu unatokana na utaratibu uliojiwekea Wizara ya Fedha na Mipango wa kufanya uhakiki wastaafu ili kuhuisha orodha ya malipo ya wastaafu na inasaidia kubaini mabadiliko ya taarifa za wastaafu kama vile kufariki na hivyo kuepuka kulipa wasiostahili”Alisema Bw.Mtonga.

  Aidha akizungumzia kuhusu utaratibu wa uhakiki huu amesema kuwa zoezi hili litafanyika nchi nzima na limeanzia katika Mkoa wa Pwani wilaya ya Kibaha na litafanyika kuanzia leo tarehe 10 mpaka tarehe 14 mwezi huu na kuendelea kwenye wilaya zote za mkoa wa pwani mpaka tarehe 21 mwezi huu.

  Baada ya uhakiki katika mkoa wa Pwani zoezi litaendeshwa kikanda nyanda za juu kusini katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Njombe, Songwe na Katavi kuanzia tarehe 31 Octoba mpaka tarehe 11 Novemba mwaka huu.

  Pia zoezi litafanyika katika kanda ya kati likijumuisha mikoa ya Dodoma, Morogoro na Singida kuanzia tarehe 21 mpaka 25 Novemba.

  Akizungumza na waandishi wa habari mwakilishi wa wazee wastaafu Bw.Benedict Kalaguza amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kufanya uhakiki huu wa wastaafu na kwamba zoezi limekuwa ni zuri lisilokuwa usumbufu wowote na limeboreshwa zaidi kwa kutumia teknolojia nzuri zaidi.

  Aidha Wastaafu wanaohakikiwa wanatakiwa kufika kwenye vituo hivyo wakiwa na nyaraka kama Kadi ya Benki, Picha za passport mbili, Barua ya Ajira ya Kwanza, Barua ya Kustaafu au kupunguzwa kazi kazini, barua ya Tuzo la Kustaafu, Nakala ya Hati ya Malipo ya kiinua mgongo au mkupuo, kitambulisho cha pensheni na barua ya Kudhibitishwa kazini.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f2
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang mara baada ya kupokea Hati yake za Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f3
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi mteule wa Ghana hapa nchini Kwame Asamoah Tenkorang Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f4
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f5
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya utambilisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f6
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini  Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya utambilisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f7
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini  Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f8
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na Balozi mteule wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini  Mahjoub Ahmed Abdallah Sharfi mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f9
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f10
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini Yevhemsi Tsymbalik mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f11
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi mteule wa Ukraine hapa nchini  Yevhemsi Tsymbalik mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f12
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati ya Utambulisho kutoka kwa balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia  Frantisek Dlhopolcek Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f13
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Frantisek Dlhopolcek mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  f14
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na balozi mteule wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Frantisek Dlhopolcek mara baada ya kupokea Hati yake ya Utambulisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
  PICHA NA IKULU

  0 0

   
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 10 Oktoba, 2016 amepokea hati za utambulisho za mabalozi wanne wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

  Mabalozi waliowasilisha hati zao za utambulisho Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Balozi wa Jamhuri ya Sudan hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi, Balozi wa Jamhuri ya Slovakia hapa nchini Mhe. Frantisek Dlhopolcek, Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk na Balozi wa Jamhuri ya Ghana Mhe. Kwame Asamoah Tenkorang.

  Rais Magufuli amezungumza na Mabalozi hao kwa nyakati tofauti baada ya kupokea hati zao za utambulisho, ambapo wamesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo kwa kujikita zaidi katika biashara na uwekezaji.

  "Mhe. Balozi najua nchi yenu ya Sudan ina utajiri wa mafuta na imefanikiwa kujenga uchumi wake kupitia mafuta, sisi pia hapa nchini tumebaini uwepo wa mafuta na gesi asilia katika maadhi ya maeneo, ningependa uhusiano na ushirikiano wetu sasa ujielekeza katika kubadilishana uzoefu na ujuzi wa namna tunavyoweza kunufaika na mafuta na gesi"  amesema Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Sudani hapa nchini Mhe. Mahjoub Ahmed Abd Allah Sharfi.

  Dkt. Magufuli pia ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka nchi za Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo Mafuta na gesi, Kilimo, Uvuvi, Mbuga za wanyama, Madini na ufugaji.

  "Hivi sasa Tanzania ipo katika mpango wa ujenzi wa viwanda na pia tunatekeleza mpango wa pili wa maendeleo, hivyo nakuomba Mhe. Balozi uwahamasishe wafanyabiashara na wawekezaji wa Ukraine waje wawekeze katika viwanda kwani soko la uhakika la bidhaa lipo" amesisitiza Dkt. Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ukraine hapa nchini Mhe. Yevheni Tsymbaliuk.
  Aidha, Rais Magufuli amewasihi Mabalozi wa Slovakia, Ukraine na Ghana ambao makazi yao ya Ubalozi yapo Mjini Nairobi nchini Kenya kuanzisha Ubalozi wao hapa nchini ili kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano katika masuala ya biashara na uwekezaji.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  10 Oktoba, 2016

  0 0

   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimpa mkono wa pole Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa leo huko Bagamoyo leo 
  sal6
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwafariji watoto wa Marehemu Mariam Saburi ambaye ni  Shemeji wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa leo huko Bagamoyo leo .
  sal1
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akilakiwa na Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete alipowasili kwenye msiba wa Marehemu Mariam Saburi,  shemeji yake Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa leo huko Bagamoyo leo 
  sal2
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimfariji Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa leo huko Bagamoyo leo 
  sal3
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na  Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete alimfariji Bi Maguno Binti Athumani ambaye ni mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)  Marehemu Mariam Saburi aliyefariki jana na kuzikwa leo huko Bagamoyo leo 
  sal4
   Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mkwewe Bi Maguno Binti Athumani kwenye  msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam saburi  aliyefariki jana na kuzikwa leo huko Bagamoyo leo
  PICHA NA IKULU

  0 0

  *Wapanga kulizindua kabla ya Krismas mwaka huu

  KAMPUNI ya Simba Motors imesema ina mpango wa kujenga kiwanda cha kuunganisha magari aina ya pick-up ambacho kitaanza kuzalisha magari kabla ya Desemba 30, mwaka huu.

  Ahadi hiyo imetolewa leo mchana (Jumatatu, Oktoba 10, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Jitesh Ladwa mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.

  “Tumeamua kuunda magari aina ya pick-up kwa sababu ya mahitaji makubwa yaliyopo nchini. Takwimu zinaonyesha kuwa, kwa mwaka Tanzania inanunua magari ya aina hii zaidi ya 4,000. Katika nchi za SADC mahitaji ni pick-up 35,000 kwa mwaka. Tutaanza na mtaji wa dola za Marekani milioni 200 na tumeomba ekari 200 katika eneo la EPZ,” amesema.

  “Eneo la kiwanda cha kuunganisha magari peke yake linahitaji ekari 50, kwa hiyo tukiweka na yadi za kupaki magari, eneo la viwanda vingine, eneo la kushusha na kupakia makontena yatakayokuwa yakisafirishwa kwenda nchi jirani, ni lazima tutahitaji eneo kubwa zaidi,” amesisitiza.

  Amesema mradi huo wa majaribio, utaanza kwa kutengeneza magari 20 kila mwezi na kwamba kazi ya utengenezaji magari itaongezeka na kufikia 1,000 na baadaye 5,000 kwa mwaka. “Tunataraji gari la kwanza litazinduliwa kabla ya Krismasi, mwaka huu,” amesema.

  Bw. Ladwa amesema uundaji wa magari hayo aina ya Foton-Tunland utafanyika kwa ubia baina ya kampuni yao, SUMA-JKT na kampuni Foton International ya China kwa kutumia teknolojia ya Kichina na kwamba magari hayo yanayotumia 4-Wheel Drive, yana uwezo wa kupita kwenye barabara za aina zote.

  Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni hiyo, Bw. Aatish Ladwa, amesema mradi utakapoanza, mbali ya kutoa ajira kwa Watanzania, utawezesha pia kujengwa kwa viwanda vingine vitakavyotengeneza matairi ya magari, vioo, taa, bumpers, viti na filters.

  “Tunataraji kujenga uwezo wa wahandisi wazawa, uhamishaji wa ujuzi kwa mafundi wa Kitanzania (technology transfer), kupunguza bei kwa mlaji wa mwisho, kupunguza gharama za uzalishaji, kutekeleza amza ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa ni nchi ya viwanda, kuongeza ajira kwa wanajeshi, na kuwezesha upatikanaji wa vipuri vya magari kwa urahisi na kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.”

  “Kiwanda kitaajiri wafanyakazi 1,500 kwa kuanzia ambao watakuwemo mafundi na watoa huduma mbalimbali, lakini katika kipindi cha miaka mitatu hadi mitano, tunataraji kuongeza wafanyakazi wengine 5,000 wakati uzalishaji ukiwa umepamba moto,” amesema.

  Kwa upande wake, akizungumza mara baada ya kulikagua gari la mfano aina ya Foton-Tunland, Waziri Mkuu amesema anawakaribisha kwenye uwekezaji huo hasa ikizingatiwa kuwa magari hayo yana uwezo wa kupita kwenye maeneo ya vijijini ambako barabara zake siyo nzuri.

  “Ofisi za Serikali zinayahitaji zaidi haya magari, hospitali zetu za wilayani nazo pia zinayahitaji haya magari ili yaweze kutoa huduma za chanjo kwa watoto, huduma za UKIMWI, kampeni za kupambana na malaria, na huduma kwa mama wajawazito huko vijijini,” amesema.

   (mwisho)

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  JUMATATU, OKTOBA 10, 2016  

older | 1 | .... | 1001 | 1002 | (Page 1003) | 1004 | 1005 | .... | 1898 | newer