Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1000 | 1001 | (Page 1002) | 1003 | 1004 | .... | 1896 | newer

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya Afrika Louis Rene Peter Larose (hayupo Pichani), makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Washington DC, Marekani, kulia kwake ni Katibu Mkuu w Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James.(Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango).
   Ujumbe wa wataalamu wa Fedha, Sera na Uchumi kutoka Tanzania wakifuatilia kwa makini Mazungumzo ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose (hawapo Pichani), Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Washington DC, Marekani, ambapo unafanyika Mkutano wa Mwaka wa Benki hiyo ambayo Tanzania ni Mwanachama, wa kwanza kushoto ni Kamishna wa Sera Augustine Ollal, Kamishna wa Bajeti John Cheyo na Kaimu Kamishna wa Fedha za Nje Mamelta Mutagwaba.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose walipokutana ofisini kwake Jijini Washington DC, Marekani, ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Tanzania na namna Benki hiyo ilivyojipanga kuhakikisha kuwa inaiwezesha Tanzania kufikia ndoto yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025
   Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakishikana mikono kuonesha umoja na mshikamano mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo kati ya ujumbe huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose, Jijini Washington DC nchini Marekani, ambako ujumbe huo unahudhuria Mkutano wa Mwaka wa Benki hiyo.
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Katikati, Akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia kanda ya Afrika mara baada ya viongozi hao kumaliza mazungumzo yaliyogusia Nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi, Jijini Washington DC, nchini Marekani, ambapo Tanzania inashiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF.
   Baadhi ya wajumbe wa Tanzania wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, baada ya kumalizika kwa kikao kati ya ujumbe huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose, wakiwa nje ya Majengo ya Benki hiyo Jijini Washington DC nchini Marekani. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Kamishna wa Fedha za nje, Wizara ya Fedha na Mipango, Mamelta Mutagwaba, Kamishna wa Bajeti, John Cheyo, Kamisha wa Madini James Andilile na Kamishna wa Sera Augustine Ollal.
   Wajumbe kutoka takribani nchi 180 duniani kote, wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, wakiwa katika Siku ya kwanza ya Mkutano wa Mwaka wa Taasisi hizo Jijini Washington DC nchini Marekani, Tanzania inawakilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt, Philip Mpango ambaye ameongoza ujumbe wa wataalamu wa Fedha na Uchumi katika mkutano huo.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James (wa kwanza kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (wa pili), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BOT, Prof Benno Ndulu (wa tatu kutoka Kushoto), Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BoT Dkt. Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Kamisha Msaidizi wa Nishati, Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile, wakiangalia ripoti iliyotolewa na timu ya wataalamu wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini Tanzania kwa ufadhili na mkopo kutoka Taasisi hizo.
  Ujumbe wa Tanzania na badhi ya  viongozi wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF wakikatisha Mitaa ya Jiji la Washington DC nchini Marekani kuwahi vikao mbalimbali vinavyoendeshwa na Taasisi hizo kabla ya kufikiwa kwa kilele cha Mkutano wa Mwaka wa Taasisi hizo Oktoba 9 mwaka huu.

  0 0  0 0

  Kongamano la mtoto wa kike lililofanyika leo mjini Shinyanga limeitaka serikali kuweka juhudi za makusudi kupinga vitendo vya ukatili wa Kijinsia hasa kwa watoto wanaoozeshwa ndoa za utotoni kutoka kwa wazazi na walezi wao.

  Maadhimisho haya yanaendelea kufanyika mjini Shinyanga ili kuungana na Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike inayoendelea kuadhimishwa Mkoani hapa ambayo kilele chake ni tarehe 11 Oktoba 2016.

  Maadhimisho hayaufanyika kila mwaka ikiwa ni mwitikio wa Azimio la Umoja huo lililopitishwa mwezi Desemba mwaka 2011.

  Akiongea katika kongamano la watoto mkoani shinyanga Mkurugenzi wa Watoto Bi. Magereth Mussai kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amelaani wale wote wanaoozesha watoto ambao wako katika umri wa kwenda shule kwasababu ndoa za utotoni uwafanya watoto hawa kushindwa kufikia ndoto zao ikiwemo haki ya kupata elimu ya juu.

  Wakati huo huo watoto wawili ambao hawakutaka majina yao kutajwa kwasababu ya kulinda haki za watoto wametoa ushuhuda wao wa ni namna gani ndoa za kulazimishwa wakiwa wadogo zilivyoelekea kukatiza ndoto yao kabla ya kuokolewa na shirika la AGAPE kuwaokoa
  na kuwaendeleza kielimu.

  Mmoja wa Watoto hao ambaye jina limeifadhiwa amesema ndoa yake ya utotoni iligubikwa na vipigo vya mara kwa mara kutoka kwa mme wake ambaye alimpatia ujauzito na baadae kumtelekeza yeye na mtoto.

  Alendelea kusema kuwa inamuuma sana kama mlengwa kuwa mzazi na wakati huo kuwa mwanafunzi anayesoma kwa msaada wa mashirika yasiyo ya kiserikali huku baadhi ya wazazi na walezi wakiendeleza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.  

  Watoto wao kwa pamoja wameitaka serikali na vyombo vya habari kuwekeza nguvu zao kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ndoa za utotoni ambazo zimekuwa kikwazo kwa mtoto wa kike kufikia ndoto zake.

  Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA), inakadiriwa kuwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo wasichana wapatao milioni moja wanatarajiwa kuwa wameolewa katika umri wa chini ya miaka 18 duniani kote.
  Mkurugenzi wa Watoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Magereth Mussai akiongea na Watoto hawapo pichani katika kongamano la mtoto wakike linaoendelea mjini Shinyanga.


  Baadhi ya Watoto Wakifuatilia jambo katika kongamano la watoto linaloendelea leo jijini Shinyanga
  Afisa Maendele ya Jamii Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Anna Muhina akiongea na Watoto hawapo pichani katika kongamano la mtoto wakike linaoendelea mjini Shinyanga.

  0 0

  MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Mhe Deogratius Ndejembi

  MKUU wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Deogratius Ndejembi amekifunga Chuo cha Ualimu cha Nkuruma kilichopo Mkoka na kuagiza uongozi wa chuo kurudisha fedha zote za ada walizolipa wanafunzi ili ziwasaidie kulipia vyuo vingine.

  Alitoa agizo hilo wakati wa mkutano na wanafunzi pamoja na uongozi wa chuo hicho kuhusu kutafuta suluhu ya mgogoro ambao ulianza Septemba 16, mwaka huu. Chuo hicho kilidahili wanafunzi 77 kwa lengo la kuwafundisha ualimu, walipofika wakaambiwa wanasoma masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

  “Baadaye wakaambiwa wanabadilishiwa masomo sasa wanasoma Maendeleo ya Jamii, hii yote wamefanya kwa kuwa chuo hakina usajili wowote.Ada wamechukua na hakuna kinachoendelea,” alisema Ndejembi.

  Ndejembi alifikia hatua ya kukifunga chuo kutokana na wanafunzi kugoma kufanya mitihani ya chuo ya kumaliza mwaka wa masomo kwa madai chuo hakitambuliwi na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).

  Alisema kukifungia chuo pekee haitoshi wanatakiwa kurudisha fedha zote za ada walizolipwa na wanafunzi katika mwaka huo wa masomo uliopita ili kuwasaidia kulipa vyuo vingine.

  “Kuwarudishia fedha sio mwisho wa jambo hili kwa sababu mmepotezewa muda wenu na haki yenu ,mmeonewa, mmedhulumiwa kwa kusema hivyo namwagiza Mkuu wa Polisi wa Wilaya na timu yake kuwakamata sasa hivi na wafikishwe kwenye vyombo vya kisheria ili haki iweze kutendeka,” alisema.

  Amewataja wanaotakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria kuwa ni mmiliki wa chuo, Mathew Nkurlu, Msajili wa Chuo, Yohana Michael, Mhasibu Elieth Ruben, wakufunzi Pendael Petro na Christopher Mabatian.

  Ndejembi alitaja sababu za kuagiza wakamatwe viongozi hao wa chuo ni kuwa walihusika kushiriki katika kufanya udanganyifu na kuwatapeli wanafunzi hao huku wakijua kinachoendelea.Aidha, alisema serikali itawasaidia katika utaratibu wa kupata vyuo vingine kwa wale wenye sifa za kujiunga na vyuo katika kozi ambayo walianza kusoma.

  Alisema kama ikitokea chuo hakina fedha za kuwarudishia wanafunzi, majengo yao yatatumika kama dhamana ya ada kwa vyuo ambavyo vitawapokea wanafunzi hao. Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho, Mhoja Matando aliishukuru serikali kwa kuwasaidia kujua hatma ya kutimiza ndoto yao ya kielimu.

  0 0

  Meneja wa Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo, akizunguza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.

  Siku ya Posta duniani huadhimishwa ifikapo Oktoba 09 kila Mwaka ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya Siku ya kuanzishwa kwa Umoja wa Posta Duniani ulioanzishwa mwaka 1874 katika mji wa Berne nchini Switzerland ukijumuisha mataifa 192 duniani.
  Na BMG

  Maadhimisho hayo yamekwenda sambamba na zoezi la kukabidhi zawadi kwa Washindi wa Uandishi wa barua Kitaifa kutoka mkoani Mwanza ambapo washindi watano kati ya 10 bora kitaifa wametoka Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.

  Washindi hao na nambari walizoshika kwenye mabano ni, Denis Bahati Stephen (01), Samwel Lufungulo Somelo (02), Vitalis Aloo Awasi (03), Kizito Eliakimu Paschal (04) na Fredrick Elias Mayunga (08).

  Washindi wa Tano na Sita wametoka Shule ya Mazinde Juu mkoani Tanga, Mshindi wa Saba ametoka Shule ya Lugalo mkoani Iringa, huku Washindi wa Tisa na 10 pia wakitoka Shule ya Mazinde Juu mkoani Tanga.

  Meneja wa Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo amesema shindano la uandishi wa barua huwashirikisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wasiozidi umri wa miaka 15 ambapo shule za msingi lugha ya kiswahili na kiingereza hutumika na kiingereza pekee kwa shule za sekondari. 

  Amebainisha kwamba wanafunzi huandika barua yenye mane kati ya 500 na 1,000 kulingana na mada iliyotolewa na kwamba mwaka huu mada ilikuwa ni "Jiandikie barua ukiwa na miaka 45" ambapo barua ya mshindi wa kwanza itakwenda kushindanishwa na barua za washindi wengine kutoka nchi 191 wanachama wa Umoja wa Posta Duniani ambapo mshindi wa kwanza nchini ataliwakilisha taifa kwenye shindalo hilo nchini Switzerland.
  Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu, Jimbo Kuu la Mwanza, Alex Masasi, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo akizungumza ambapo amewahimiza wanafunzi kuongeza bidii katika masomo yao hususani kuwa bora kwenye kusoma, kuandika na kuzungumza lugha nyingi tofauti na kiswahili na kiingereza.
  Wanafunzi wakimsikiliza kwa umakini Katibu Mtendaji wa Idara ya Elimu, Jimbo Kuu la Mwanza, Alex Masasi, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho Siku ya Posta yaliyofanyika leo Jijini Mwanza.
  Mkuu wa Shule ya Saint Mary's (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani. Siku ya Posta duniani hufanyika kila mwaka Oktoba 08, hivyo yamefanyika leo Oktoba 07 kutokana na ratiba ilivyopangwa.
  Mshindi wa Nane Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Fredrick Elias Mayunga kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.

  Mshindi wa Nane amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Elfu Arobaini (40,000).
  Mshindi wa Nne Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Kizito Eliakimu Paschal, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.


  Mshindi wa Nne amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Moja na Elfu Ishirini (120,000).

  Mshindi wa tatu Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Vitalis Aloo Awasi, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.


  Mshindi wa Tatu amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Mbili (200,000)

  Mshindi wa Pili Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Samweli Lufungulo Somelo, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.


  Mshindi wa Pili amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Tatu (300,000)

  Mshindi wa Kwanza Kitaifa kwenye Mashindano ya Uandishi wa barua, Denis Bahati Stephen, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akipokea zawadi yake.


  Mshindi wa kwanza amepokea Cheti cha utambuzi, Tisheti, Kamusi ya Kiingereza, begi la kubebea daftari, Kikokoteo pamoja na fedha Laki Nne (400,000)

  Mkuu wa Shule ya Saint Mary's Seminary, Maximillian Buluma, akipokea zawadi ya shule hiyo baada ya kuwa shule iliyotoa washindi kitaifa pamoja na washiriki wengi. Amepokea mpira pamoja na Cheti kutoka Shirika la Posta.
  Kulia ni Meneja wa Posta Mwanza, Julius Chifungo, akimkabidhi mgeni rasmi zawadi
  Washindi wa shindano la kuandika barua nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Posta Mwanza, Waalimu wa Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza, Mgeni Rasmi pamoja na Wazazi.
  Washindi wa shindano la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wazazi wao.
  Washindi wa shindano la kuandika barua nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la Posta Mwanza.
  Washindi wa shindano la kuandika barua nchini, wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza, Mgeni Rasmi pamoja na Meneja wa Posta Mwanza.
  Washindi wa shindano la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza.
  Washindi wa tatu bora katika shindano la kuandika barua nchini kutoka shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza
  Afisa Masoko, Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Mponda, akizungumza kwenye maadhimisho hayo
  Mwalimu Victor Mgisha anayefundisha somo la Kiingereza shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizungumza kwenye Maadhimisho hayo.
  Waalimu wa Shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza wakielezea furaha yao baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuibuka washindi wa shindano la uandishi wa barua linaloandaliwa na Umoja wa Posta duniani na kufanyika kwa nchi wanachama 191 kote duniani.
  Mwalimu wa Shule ya Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza, akisoma barua iliyompa ushindi, mshindi wa kwanza kwenye shindano la uandishi wa barua nchini.
  Meneja wa Shirika la Posta mkoani Mwanza, Julius Chifungo, akizunguza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
  Mshindi wa kwanza Kitaifa kwenye shindano ya uandishi wa barua, Denis Bahati Stephen, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizunguza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
   Mshindi wa pili Kitaifa katika shindano ya uandishi wa barua, Samweli Lufungulo Somelo, kutoka Saint Mary's Seminary Jijini Mwanza akizunguza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Posta Duniani ambayo kimkoa yamefanyika leo katika Shule ya Saint Mary's Seminary (Nyegezi Sekondari) Jijini Mwanza.
  Bonyeza HAPA Kutazama Mwanza walivyoibuka kidedea kwenye Shindano la Uandishi wa barua mwaka 2015 Kitaifa.

  0 0

   Mshambuliaji wa Ndanda FC, Omary Mponda akichuana na kiungo wa African Lyon, Omary Salum katika mchezo wa LigiKuu Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. African  Lyon ilishinda 1-0. (Picha na Franis Dande)
   Mshambuliaji wa Ndanda FC, Omary Mponda (kushoto) akiwania mpira na beki wa African Lyon, William Otong.
   Beki wa African Lyon, Milaji Seleman (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa Ndanda, Riphat Hamis.

  0 0    Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose walipokutana ofisini kwake Jijini Washington DC, Marekani, ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Tanzania na namna Benki hiyo ilivyojipanga kuhakikisha kuwa inaiwezesha Tanzania kufikia ndoto yake ya kuwa nchi yenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025


  Benny Mwaipaja, MoFP
  Washington DC, Marekani
  8.10.2016

  WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa Serikali imedhamiria kuimarisha sekta ya kilimo na Utalii ili ziweze kutoa mchango mkubwa kuinua uchumi wa Taifa pamoja na kuwaondoa wananchi wake kutoka katika lindi la umasikini.

  Waziri Mpango ameyasema hayo Jijini Washington DC, nchini Marekani, wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose, ambapo viongozi hao wamezungumzia masuala yanayohusu utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na taasisi hiyo.
  Amesema kuwa kilimo kinaajiri asilimia kubwa ya watanzania hivyo mapinduzi yanayokusudiwa katika sekta hiyo ni kuendesha kilimo biashara kwa kuongeza uzalishaji na  thamani ya mazao ya wakulima.

  Kuhusu sekta ya Utalii, Dkt. Philip Mpango anayeongoza ujumbe wa wataalamu wa Uchumi na Fedha katika Mkutano wa Mwaka ulioandaliwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani, IMF, amesema kuwa serikali inakusudia kupitia upya kodi zinazoleta kero mbalimbali katika sekta hiyo pamoja kilimo.

  Eneo jingine alilotaka Benki ya Dunia kuingilia kati, ni kuipatia Tanzania Mkopo na ruzuku utakaosaidia kukabiliana na madeni yake makubwa inayodaiwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja madeni ya Shirika la Ugavi wa Umeme nchini, TANESCO, ili shirika hilo liweze kujiendesha kwa faida na kuchangia ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa haraka.

  Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Louis Rene Peter Larose, ameihakikishia Tanzania kuwa pamoja na miradi mingine, itafadhili mradi mkubwa wa kilimo wa ukanda wa kusini “Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT)” ili kukifanya kilimo kuwa na tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

  “Mimi nimefika Tanzania na ninaifananisha nchi hiyo kuwa itafikia ama kuzidi hadhi ya Dubai kutokana na rasilimali nyingi ilizonazo ambazo zikisimamiwa vizuri zitaibadili kabisa nchi hiyo kimaendeleo” alisema Larose.

  Ameitaka Tanzania kutosita kuitumia ipasavyo benki hiyo kufanikisha malengo yake ya maendeleo na kwamba yeye mwenyewe binafsi pamoja na kwamba anaongoza kundi la nchi 22 za kiafrika katika Benki hiyo, atahakikisha Tanzania kama zilivyo nchi nyingine, inanufaika na uwepo wa Taasisi hiyo.

  Mkurugenzi huyo Mtendaji amepongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, namna anavyosimamia mambo kwa nguvu zake zote na ametoa pole kwa nchi hiyo kutokana na madhara iliyoyapata kufuatia tetemeko kubwa la ardhi lililoukumba mkoa wa Kagera na mikoa mingine jirani.

  Ameahidi kuwa Benki hiyo itatuma wataalamu watakaosaidia kufanya utafiti na kuishauri nchi kitaalamu na kimiundombinu namna ya kukabiliana na majanga ya matetemeko pamoja na vifaa vitakavyosaidia kutoa tahadhari kabla ya kutokea kwa majanga kama hayo.

  0 0


  Msanii wa Muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Wanaume Family, Chege Chigunda akiweka sawa baadhi ya zawadi alikuwa ameziandaa kwa ajili ya Wagonjwa Temeke Hospitali.
  Msanii wa Muziki kutoka kundi la Wanaume Family, Chege Chigunda akizungumza jambo na mmoja ya wauguzi wa Temeke Hospitali jijini Dar.
  Chege na Temba wakiteta jambo mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Temeke


  Chege Chigunda akizungumza na Waandishi wa habari
  Chege Chigunda na baadhi ya Wasanii kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe wakielekea wodini
  Chege Chigunda akiwasiliana na baadhi ya watu kabla ya kuingia wodini
  Msanii wa Muziki wa Bongofleva Mheshimiwa Temba akitoa zawadi kwa wagonjwa
  Chege Chigunda akitoa baadhi ya Zawadi kwa wagonjwa
  Mh Temba akiingia wodini kupeleka zawadi kwa Wagonjwa
  Mhe. Temba akigawa zawadi kwa wagonjwa
  Baadhi wasanii kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe akitoa zawadi kwa wagonjwa


  Chege Chigunda akiwa amembeba mtoto Hadija Abdalah akiwa na Mama yake Mwanahawa Juma.
   
  Na Humphrey Shao, blog ya Jamii 
   
  MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva kutoka kundi la Wanaume Family Chege Chigunda , leo ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kutembelea hospitlai ya Rufaa ya Temeke na kugawa zawadi mbalimbali katika wodi ya Watoto waliozwa hapo kutokana na matatizo mbalimbali. 
   
  Akizungumza na Mwandishi wa blog hii Mapema leo Hospitalini hapo chege alisema kuwa imekuwa tofauti sana kwa watu kupenda kusheherekea katika nyumba za starehe lakini yeye ameamua kukaa na watoto hao wagonjwa hili kurudisha kile ancho kipata kwa jamii. “Chege Chigunda aezaliwa leo hivyo ndio maana nipo hapa motto wa Mama Said kushherekea siku yangu ya kuzaliwa na wagonjwa kwa kutoa zawadi mbalimbali kama mnavyoziona Pampers , Dawa za Mswaki na Dawa kwa ajili ya wagonjwa ambao awana uwezo wa kujijinunuli a hivyo katika siku ya leo wamepata fursa ya kununuliwa madawa na mimi” anasema Chege. 
   
  Anasema kuwa maisha yamebadilika sana na inapaswa watu kurudi nyuma na kufanya yale yaliyoa mazuri yanayompendeza Mungu kwa kusheherekea siku zao za kuzaliwa na watu ambao wanamatazo na wenye uhitaji hili kuweza kuwapa faraja ambayo wakuwa wameikosa kwa muda kutokana na matatizo yaliyowakuta. Alimaliza kwa kutoa wito kwa wasanii na watu maharufu kuwa na utamaduni wa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mablimbali kila wanapopata nafasi na kiasi kidogo kwani kutoa akuhitaji kuwa na utajiri mkubwa bali ni moyo tu.

  0 0


  Waziri huyo akiangalia zahanati ya Ishozi ambayo imeharibika kabisa na kufanya huduma za afya kufanyika kwenye Tenti  la muda nyuma kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Luteni Kanali Denis Mwita.
  umula1
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikagua kituo cha afya cha Kabyaile kilichokuwa hakijakamilika ujenzi wake Wilayani Misenyi mkoani Kagera wakati alipotembelea na kujionea hali halisi ya madhara yaliyosababishwa na Tetemeko la Ardhi, Kuua watu 17 na kujeruhi wengine mkoani humo

  umula2
  Hapa ni mahali palipohamishiwa Zahanati hiyo
  umu1
  Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiongea na akina mama waliofika kliniki ya afya ya uzazi ya mama na mtoto kwenye kituo cha afya cha Rwamishenyi kilichopo mkoani Kagera
  umu2
  Waziri Ummy akiongea na watoto waishio kwenye kituo cha watoto waishio kwenye mazingira magumu cha Uyacho
  umu3
  Akina mama hao wakimsikiliza Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,alipokuwa akiwahamasisha kujiunga na mfuko wa afya ya jamii(CHF) pamoja na uzazi wa mpango
  umu4
  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto akisalimiana na mtoto ambaye nyumba yao ilianguka kwa tetemeko na sasa wanaishi kwenye Tenti

  0 0


  Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Uwezeshaji (UTT-AMIS), Daud Mbaga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu huduma yao mpya ya usimamizi wa mali. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji, Issa Wahichinenda.

  MFUKO wa Uwekezaji wa Pamoja (UTT-AMIS) umesema kutokana na utafiti walioufanya kwa muda wa miaka 10, unaonyesha Watanzania walio wengi hawana uelewa wa kuwekeza fedha zao kwenye hati fungani (bond).

  Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa UTT, Daudi Mmbaga , alisema watu wengi wanakuwa na fedha nyingi lakini hawajui jinsi ya kuwekeza fedha zao.Alisema kutokana na changamoto iliyopo kwa Watanzania ya kutokuwa na uelewa wa jinsi ya kuwekeza , wameamua kuanzisha huduma ya Usimamizi wa Mali itakayomsaidia mwananchi jinsi ya kuweza kuwekeza fedha zake na kutengeneza faida.

  “ Watu wengi wanakuwa na fedha nyingi lakini zimelala tu, na wengine wamewekeza kwenye maeneo yasiyowapa faida ndio maana tuamua kuanzisha huduma itakayowasaidia kuwekeza fedha yao inayoitwa Usimamizi wa Mali,” alisema.Aidha, alisema huduma hiyo kwa sasa imeshaanza kutumika na mwelekeo ni mzuri kutokana na watu wengi kupenda kuwekeza fedha zao, ambapo kiwango cha kuanzia ni sh. Milioni tano.

  Mmbaga alisema kiwango cha elimu nchini kikijikita vizuri kitasababisha kuwepo na soko la uhakika na kusababisha kuwepo na maendeleo ya kiuchumi.Hata hivyo aliwashauri wananchi kujitahidi kuwekeza katika mifuko ya uwekezaji kwa kuwa kutasaidia kuwa na imani na fedha zao.

  0 0


  CCM Mkoa wa Dodoma pamoja na Jumuiya ya Wanawake Katoliki Tanzania (WAWATA) mkoa wa Dodoma muda huu wapo kwenye tukio la kutoa heshima za mwisho kuuaga mwili wa  Salome Kiwaya aliyefarika juzi kwa ajali ya gari.

  Heshima hizo za mwisho zinatolewa mbele mwili huo uliowekwa ndani ya kanisa kuu la Jimbo Katoliki hapa mjin Dodoma.Marehemu Salome Kiwaya hadi mauti yake alikuwa M/k wa UWT mkoa pamoja na WAWATA Jimbo Kuu la Dodoma.

  Ibada ya misa kuuaga mwili huo, inategemewa kuanza saa 9:00 alasiri na baadae kusafirishwa kwenda Mkoa wa Njombe jioni hii, ambapo utazikwa huko kesho jumatatu.Hapa wapo viongozi wa ngazi ya juu wa Serikali akiwamo RC Dodoma, Spika wa Bunge la Tanzania, Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda na mkwe.

  Pia yupo M/k wa CCM mkoa wa Dodoma, Alhaji Adam Kimbisa na wengine wengi.

  Kati ya hawa watatoa salamu za chama na serikali hapo baadae na watakachosema, nitakituma huko kwa ajili ya habari za kesho.

  Mungu ampumzishe kwa Amani.

  0 0

  Mtendaji Mkuu TEMESA Dr. Mussa Mgwatu (katikati) akikagua chumba maalumu kwa ajili ya injini (Engine Room) kulia ni msaidizi wa Meneja Bw. Charles Mbegete na kushoto ni Kaimu Meneja TEMESA Kagera Bw. Wilson Nyitwa.
  Mtendaji Mkuu TEMESA Dr. Mussa Mgwatu (wa tatu kushoto) akiongea na baadhi ya watumishi wa TEMESA Kagera alipotembelea kituoni hapo kukagua jinsi Ofisi inavyofanya kazi na kuzungumza na wafanyakazi.

  Mtendaji Mkuu TEMESA Dr. Mussa Mgwatu (wa pili kushoto) akisikiliza Kaimu Meneja wa TEMESA Kagera Bw. Wilson Nyitwa(wa pili kulia) alipotembelea ofisi hiyo na kuzungumza na baadhi ya watumishi wa TEMESA Kagera kushoto ni Msaidizi wa Meneja wa TEMESA Kagera Bw. Charles Mbegete na kulia ni Mhasibu Bi. Joviness Samson.Picha Na Theresia Mwami TEMESA (Kagera).

  ………………………………………………….

  Na Theresia Mwami TEMESA Kagera

  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu amewataka watumishi wake kuacha kufanya kazi kwa uzembe na mazoea badala yake waongeze ubunifu katika miundombinu iliyopo ili kuweza kuzalisha zaidi ikiwa ni sanjali na kuweka mikakati madhubuti ya kukusanya madeni siku hadi siku.

  Ameota agizo hilo alipotembelea na kujionea hali ya karakana ya TEMESA mkoani Kagera na kumuagiza Kaimu Meneja wa TEMESA Kagera Bw.Wilson Nyitwa kusimamia kwa makini utekelezaji wa majukumu ya Wakala huo mkoani hapo.

  “Inatupasa kuanza na hiki kidogo tulicho nacho kwa kuziba mianya ya uzembe na muongeze uadilifu na ufuatiliaji katika kazi tulizo nazo tufanikishe utendaji wa kazi zetu” alisema Dkt. Mgwatu.

  Dkt Mussa Mgwatu ameongeza kuwa watendaji wanapaswa kupambana ili kulinda soko lililopo kwa sasa na hata kuongeza wateja zaidi. Kwa sasa wateja wa TEMESA ni taasisi za serikali ambazo zinapeleka magari na mitambo kutengenezwa katika karakana zao.

  Aidha kwa upande wake Kaimu Meneja wa TEMESA Kagera Bw.Wilson Nyitwa alieleza kuwa Kituo chake mbali na kuwa na karakana na kutengeneza magari na vifaa vya umeme,kukodishaji mitambo na usimikaji umeme katika majengo mbali mbali ya serikali pia kinasimamia uendeshaji wa vivuko viwili vilivyopo Kyanyabasa na Ruvuvu.

  Alieleza kuwa TEMESA Kagera ina changamoto nyingi zikiwemo uchakavu wa Karakana yake iliyojengwa tangu mwaka 1958 pamoja na kukosa vitendea kazi muhimu pamoja na magari kwa ajili ya matumizi ya ofisi lakini bado wanafanya kazi kwa kujituma na kuzalisha zaidi ya Shillingi Million 50 kwa mwezi.

  “Nakuomba Mtendaji Mkuu utusaidie gari moja kwa ajili ya matumizi ya kituo nyongeza ya mafundi, vitendea kazi vya kisasa vya karakana ,ukarabati wa karakana ya mkoa ili kutuwezesha kutekeleza majukumu yetu na kuzalisha zaidi.

  Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yupo katika ziara ya kikazi Kanda ya Ziwa na atatembelea vituo vya TEMESA vilivyopo ili kubaini changamoto na kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo na kwa kuanzia yupo Mkoani Kagera.

  0 0

  Jana Oktoba 08, 2016 kuamkia leo jumapili Oktoba 09, 2016 ilikuwa Shangwe kubwa kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake kwenye tamasha kubwa la "The Nyama Choma Festival" lililofanyika kwenye viunga vya Rock City Mall.

  Msanii AY aliwapagawisha wakazi wa Jiji la Mwanza huku wakipata nyama zilizochomwa kwa ustadi wa hali ya juu huku #LakeFmDjz wakidondosha burudani pamoja na DjK3 kutoka Jijini Dar es salaam. Kumbuka 102.5 Lake Fm ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa waliofanikisha tamasha hilo.
  Na BMG
  Mkali AY akidondosha burudani jukwaani
  Shangwe kutoka kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake
  Shangwe kutoka kwa wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake
  "Nafurahi kwa namna Mwanza wanavyosupport kazi zangu, baada ya show hii nitarudi tena Mwanza kwa ajili ya kuwapa burudani zaidi". Anasem AY (kushoto) wakati akizungumza na Vesterjtz wa BMG
  Mmoja wa wakazi wa Jiji la Mwanza (kushoto) akizungumza na Hyroun Tambwe (kulia) ambaye mtangazaji wa 102.5 Lake Fm Mwanza kwenye The Nyama Choma Festival
  Wananzengo kutoka Lake Fm Mwanza
  Lake Fm Team
  Wananzengo wa Lake Fm Mwanza
  Bonyeza HAPA Kujua Zaidi

  0 0

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akiwa kwenye studio za televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) visiwani Zanzibar kutoa elimu ya mpiga kura juzi.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo kwenye studio za televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) visiwani Zanzibar wakati akitoa elimu ya mpiga kura juzi.
  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo kwenye studio za televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) visiwani Zanzibar wakati akitoa elimu ya mpiga kura juzi.Kushoto ni muandaaji wa vipindi wa ZBC, Salha Mohamed akiongoza kipindi cha Alasiri Yetu.

  Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani, akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Iman Osmond (katikati) na Naibu MkurUgenzi Mkuu wa Shirika hilo Nasra Mohamed baada ya kumaliza kipindi cha Alasiri Yetu, kutoa elimu ya mpiga kura.

  Picha na Hussein Makame,NEC

  …………………………………………………………..

  Hussein Makame, NEC

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarajia kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura ifikapo mwaka wa fedha wa 2017/2018 kwa mara ya kwanza baada ya uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2015.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati akitoa elimu ya mpiga kura kupitia kipindi cha Alasiri Yetu kinachorushwa na televisheni ya Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC).

  Alisema kuwa baada ya uboreshaji huo wa mwaka 2017/2018, Tume hiyo inategemea kuboresha kwa mara ya pili daftari hilo ifikapo mwaka wa fedha 2019/2020.

  Bw. Kailima alifafanua kuwa uboreshaji huo unafanyika kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinachoielekeza NEC kuboresha daftari hilo mara mbili.

  “Kwa mujibu wa kifungu namba 5 cha Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kinasema Tume ya Taifa ya Uchaguzi itapaswa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura mara mbili, baada ya uchaguzi mara moja na kabla ya uchaguzi ujao mara moja” alisema Bw. Kailima na kuongeza kuwa:

  “Kwa hiyo tumemaliza uchaguzi mwaka jana na kabla ya uchaguzi wa mwaka 2020, Mungu akituweka hai tunategemea mwaka 2017/2018 tuboreshe daftari na mwaka 2019/2020 tufanye hivyo”

  Mbali na kuzungumzia uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Bw. Kailima aleleza jinsi tume hiyo inavyotekeleza mikakati ya kutoa elimu ya mpiga kura na kwamba NEC itajipanga ili kwenda kutoa elimu hiyo visiwani Zanzibar.

  Alisema NEC inapanga kwenda kutoa elimu hiyo kwenye Chuo Kikuu Zanzibar (State University) mjini Unguja na baadaye kwenda kisiwani Pemba na pia inategemea kushiriki Jitimai ili kutoa elimu ya mpiga kura kwa washiriki wa mjumuiko huo.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa lengo la kuandikisha kila raia mwenye sifa za kupiga kura na kutunza taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

  Inaelezwa kuwa kuwepo kwa Daftari sahihi la Wapiga Kura linaloaminiwa na wadau ni kigezo muhimu cha kufanikisha chaguzi huru, wazi, zenye kukubalika na za haki zaidi.

  0 0


  Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lushoto ambaye ni Afisa Tarafa ya Lushoto,Asha Kikoti akifungua mkutano wa uzinduzi wa chama cha wazee wastaafu wilayani Lushoto kushoto ni MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu kulia kwake ni Mwenyekiti wa Chama cha Wazee wilayani humo Paul Kirua.
  MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu akizungumza na wazee wastaafu wilayani Lushoto
  MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu akizungumza na wazee wastaafu wilayani Lushoto
  Meneja Matekelezo wa PSPF Franscis Mselemu akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa chama hicho kulia kwake ni MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu

  MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu wa kwanza kuhoto katikati ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Asha Kikoti kulia ni Katibu wa chama cha wazee wastaafu wilayani Lushoto(Chawasewili)Paul Kirua
  MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu akimkabidhi Katibu Mkuu wa Chama cha wazee Wastaafu wilayani Lushoto (Chawasewili) Paul Kirua katiba ya Chama hicho mara baada ya kukizundua kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Asha Kikoti

  Katibu Mkuu wa Chama cha wazee Wastaafu wilayani Lushoto (Chawasewili) Paul Kirua akionyesha juu katiba ya Chama hicho mara baada ya kukizunduawilayani humo kushoto ni MKURUGENZI Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu
  Wazee Wastaafu wilayani Lushoto wakimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu

  Mmoja kati ya Wazee Wastaafu wilayani Lushoto,Yohana Wiliamu akiuliza swali katika mkutano huo wa uzinduzi wa chama hicho
  Mzee Mstaafu wilayani Lushoto,Judica Mandia akiuliza swali kwenye mkutano huo
  Juma Rashidi ambaye ni miuongoni mwa wazee wastaafu wilayani Lushoto akiuliza swali kwa mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF,Adam Mayingu
  MKURUGENZI wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF hapa nchini, Adam Mayingu amesema kuwa wazee wastaafu wanauwezo wa kuwa mabilionea na kuibadilisha nchi kwa kutengeneza ajira ,kubuni miradi inayoweza kuwaingizia kipato baada ya kulitumikia taifa katika nafasi mbalimbali walizokuwa nazo.

  Alisema kwani asilimia kubwa wanaweza kuanzisha miradi mbalimbali ambayo inaweza kuwasaidia kujiongezea kipato hali itakayopelekea vijana kuweza kuinua maisha yao kitendo ambacho pia kitasaidia kuongeza pato la serikali.

  Mayingu aliyasema hayo wakati wa wiki ya huduma kwa wateja Duniani ambapo mfuko huo unakutana na wadau wake ili kuweza kubaini changamoto ambazo ikiwemo kuangalia namna ya kukabiliana nazo.

  Wiki hiyo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa chama cha wazee wastaafu wilayani Lushoto (Chawisewilu) chenye makazi yake mjini hapa waliokuwa wakifanya kazi na baadae kustaafu waliweza kuhudhuriwa kwa wingi na kutoa mapendekezo yao.

  “Ukiangalia wazee wastaafu wanapokuwa wamepata fedha zao za kiunua mgongo badala ya kwenda kuzitumia katika matumizi yasiyokuwa ya lazima badala yake waone namna ya kuzitumia kubuni miradi itakayokuwa chachu kwao kupitia hatua kubwa za kimaendeleo “Alisema.

  “Sisi kama Mfuko wa Pensheni wa PSPF tunaunga mkono chama chenu lakini pia niwaambie Sido wapo tuzungumze nao ikiwemo kuweka utaratibu mzuri ili muweza kuona namna ya kuweza kunufaika na uwepo wao “Alisema.
  “Lakini pia msisite kuwatumia wataalamu kwenye masuala mbalimbali ya ujasiriamali kwani hiyo ndio njia ambayo inaweza kuwa chachu ya kuweza kufikia malengo yenu hasa katika kipindi hiki kwa kushirikiana “Alisema.

  Aidha pia aliwataka kupitia umoja wao kutumia fursa nyingi zilizopo kwenye maeneo yao kwani wanao umri wa kuishi mkubwa badala yake yaondokana na dhani ya kuwa watu wanapokuwa wakistaafu wanafariki kitendo ambacho sio hakina ukweli wowote.

  Lakini pia aliwataka kutumia fursa hiyo waliyoipata kuieli misha jamii huku akiwaomba kupitia chama chao kuwahimiza vijana wao kujiunga ma mfuko wa Pensheni wa PSPF ili waweze kunufaika na mafao yanayotolewa.

  Awali akizungumza wakati akifungua kikao hicho,Kaimu Mkuu wa wilaya ya Lushoto,Asha Kikoti aliwataka wazee wastafu kuhakikisha fedha wanazozipata za kiunua mgongo kuweka mpango mzuri wa kuzitumia kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili waweze kujiingizia kipato.

  “Kiuhalisia wazee wastaafu wanapopata fedha zao wanaona kama vile ni nyingi na kuzitumia bila kwa haraka bila kufikiria hata kuzianzishia miradi ambayo inaweza kuwasaidia kupambana na ukali wa maisha “Alisema huku akiwasisitizia wabadilike.

  Sambamba na hayo aliwataka pia kuwa na mpango mzuri wa matumizi ya fedha zao za kiinua mgongo ili ziweze kuwasaidia kutumiza ndoto zao katika maisha ikiwemo kuwa na maisha mazuri.

  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0


  Mpiga Golf Sara Denis Amina wa Klabu ya Golf ya Lugalo Jijini Dar Es Salaam akiwa katika Mazoezi kujiwinda na Mashindano ya Arusha Open yanayotarajiwa kufanyika Hivi karibuni Jijini Arusha Nyuma ni Amina Hamisi,Sophia Mathias wachezaji wenziei wa klabu hiyo
  Nahodha wa Klabu ya Golf ya Lugalo Kapteni Japhet Masai (katikati) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Operation na Mafunzo wa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu(OTO) Brigedia Jenerali Jairos Mwaseba alipotembelea viwanja vya golf vya Lugalo Jijini Da r es Salaam katika mashindano ya CDF Trophy 2016.
  Mnaadhimu Mkuu Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzani Luteni Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) Akisalimiana na Meneja wa Klabu ya Golf Lugalo Kanali Gerlard Omary, alipowasili katika Klabu hiyo Jijini Dar es Salaam kusuhudia mashindano ya Mkuu wa majeshi yaliyomalizika hivi karibuni Katikati ni Mwenyekiti wa klabu hiyo Brigedia Jenerali Michaele Luwongo
  Mnaadhimu Mkuu Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzani Luteni Jenerali Venance Mabeyo (kushoto) Akisalimiana na Mwenyekiti wa klabu Golf ya Lugalo Brigedia Jenerali Michaele Luwongo mara alipowasili katika klabu hiyo Jijini Dar es Salaam kushuhudia CDF Ttophy iliyomalizika hivi karibuni.
  Baadhi ya Wachezaji Wanawake wa Klabu ya Golf ya Lugalo ya Jijini Dar es Salaam wakiwa katika Mazoezi kujiwinda na Mashindano ya Arusha Open yanayotarajiwa kufanyika Hivi karibuni Jijini Arusha ( Picha na Luteni Selemani Semunyu)


  Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ


  Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange ambaye ni Mlezi wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo Golf Club ameimarisha safu ya uongozi wa klabu hiyo kwa kuwateua Naibu katibu Mkuu na Mkuu wa Miundombinu kujaza nafasi zilizoachwa wazi.

  Jenerali Mwamunyange amemteua Kanali Rajabu Mohamed Mwenyumbu kuwa Naibu Katibu wa klabu na Kapteni Kitego Kuwa Mkuu wa Miundombinu ya Klabu(Ground Member) kuchukua nafasi ya Kanali Jackson Nsigaye aliyehamia Bukoba kikazi.

  Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mwenyekiti wa Klabu hiyo Generali Michael Luwongo alisema Hatua hiyo inalenga kuboresha klabu hiyo ambayo inamikakati mikubwa ya kuboreshwa na kuwa kitovu cha Michezo cha kisasa che nye hadhi ya Kimataifa.

  Wakati huo huo wachezji wa Timu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo ya Jijini Dar es Salaam wako katika maandalizi ya mwisho kujiwinda na Mashindano ya Arusha open yanayotarajiwa kufanyika Hivi karibuni Jijini Arusha.

  Akiongea na Waandishi wa Habari katika Klabu hiyo Kapteni Japhet Masai alisema mashindano hayo ambayo ni muhimu katika kupandisha viwango vya wachezaji yanatarajiwa kufanyika Jumamosi na Jumapili ya Oktoba 15 na 16 huku ikihusisha wachezaji wasio wa kulipwa (Amature).

  Alisema Klabu ya Lugalo inatarajia kuingiza wachezaji wa Daraja la A,B,C senior huku wachezaji watoto ambao ni Junior watashindwa kushiriki kutokana na kuwa mashuleni katika kipindi hichi.

  “ Mashindano haya ni Muhimu kwa Wachezaji wetu lakini pia itatupa fursa kwa wachezaji wetu wenye viwango kupata nafasi kuchezea timu ya Taifa iwapo wataonekana. Alisema Kapteni Masai.

  Kapteni Masai alisema kumbukumbu ya Matokeo mazuri katika mashindano ya Tanzania open kwa kuchukua ushindi wa Kwanza na wa Pili gross huku Daraja B ikichukua Ushindi wa Kwanza na katika mashindano ya Moshi Open kuchukua nafasi ya Kwanza Mshindi wa Jumla.

  Kwa upande wake Afisa Utawala wa Klabu hiyo Kapteni Amanzi Mandengule alisema Jumla ya wachezaji 10 wanatarajiwa kwenda kushiriki michuano hiyo wakiwemo wanawake watatu na wanaume Saba.

  Aliongeza kuwa kikosi cha wachezaji hao Kitaongozwa na Kapteni Amanzi Mangengule, Kapteni Japhet Masai, Kapteni Kibuna Shabani, Juma Likuli,Noel Mheni,Nicolous Chitanda ,Michael Obare, Amina Hamisi,Sara Denis na Sophia Mathias.

  Afisa huyo wa Utawala alisema maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni Baraka za Mwenyeki wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo ili kuhakikisha wanakwenda kuwakilisha vyema Jeshi kwa kurejea na Ushindi.

  0 0

   Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Manyara, Isaya Shekifu akizungumza na wakazi wa Kata ya Dongobesh Wilayani Mbulu baada ya kukabidhi jana mabati 100 kwa ajili ya upauaji wa jengo la upasuaji wa kituo cha afya.
   Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, Chelestino Mofuga akizungumza na wakazi wa Kata ya Dongobesh baada ya kukabidhiwa mabati 100 ya jengo la upasuaji wa kituo cha afya na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Manyara.
  Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mkoani Manyara, Flatey Massay akizungumza jana na wakazi wa Kata ya Dongobesh baada ya kukabidhiwa mabati 100 ya jengo la upasuaji wa kituo cha afya na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Manyara. Picha na Joseph Lyimo.

  0 0


  Askofu wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Iringa Dkt Owdenburg Mdegela katikati akiwatambulisha mbele ya waumini wa kanisa kuu askofu mteule wa dayosisi hiyo mchungaji Blaston Gavile wa pili kushoto na mkewe pamoja na msaidizi wa askofu huyo mchungaji Himid Saga wa pili kulia na mkewe.
  Askofu wa Dododa Mwamasika kushoto akiwa na askofu mteule wa dayosisi ya Iringa Blaston Gavile na mkewe wakimsikiliza askofu wa dayosisi hiyo Dkt Mdegela
  Katibu wa dayosisi ya Iringa Chavala kulia akimfuatilia kwa makini askofu wa Dodoma
  Askofu Mwamasika kulia akimpongeza mke wa askofu mteule wa dayosisi ya Iringa katikati ni askofu Dkt Mdegela
  Mchungaji wa usharika wa kanisa kuu Mbogo akiweka sawa mic
  Askofu wa doyosisi ya Iringa Dr Mdegela kulia akimtambulisha rasmi askofu mteule wa dayosisi hiyo mchungaji Blaston Gavile na mkewe mbele ya waumini wa kanisa kuu leo


  Askofu Dkt Mdegela akitoa maelezo kwa waumini wa kanisa kuu

  Mmoja wa wageni akimpongeza askofu dkt Mdegela kwa kufanya uchaguzi wa kihistoria

  Viongozi wa kwaya ya vijana wakiwa katika picha ya pamoja
  Mwalimu wa kwaya ya vijana Lupyana Samweli kulia akimpongeza askofu Dkt Mdegela

  Askofu Dkt Mdegela akiwa na wanandoa watarajiwa kulia ni Debora Lubava mtunza hazina wa kwaya ya vijana na ubavu wake mtarajiwa kulia

  Askofu Dkt Mdegela akihoji jambo kwa mwimbaji wa kwaya ya vijana Onno Mella


  Na MatukiodaimaBlog

  ASKOFU wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa Dkt. Owdenburg Mdegela amewapongeza waumini wa dayosisi hiyo kwa kumpata askofu mpya atakayechukua nafasi yake pasipo kuwepo kwa vurugu za aina yoyote tofauti na maeneo mengine ambayo pindi linapotokea zoezi la uchaguzi wa askofu huwa na vurugu kubwa .

  Huku akisema kuwa hana ugomvi wowote na askofu wa dayosisi kusini Isaya Mengele kama ambavyo watu wanasema na kuwa mgogolo unaoendelea kati ya askofu huyo na waumini wake wa jimbo la Mufindi utatuzi wake ni maombi na sio kutumia nguvu hivyo alisema tayari amepokea maombi ya waumini wa jimbo la Mufindi kutaka kuhamia dayosisi ya Iringa na hana sababu ya kuwakataa kuwa pindi watakapokuwa tayari atawakaribisha .

  Askofu Dr Mdegela aliyasema hayo leo wakati wa ibada maalum ya kumtambulisha askofu mteule mchungaji Blaston Gavile na msaidizi wake Himid Saga mbele ya waumini wa kanisa hilo usharika wa Kanisa kuu ,kuwa uchaguzi mkuu uliofanyika ijumaa umemalizika kwa amani na utulivu mwingi na kupelekea heshima kubwa kwa dayosisi ya Iringa na Tanzania kwa ujumla .

  " Tumemaliza uchaguzi wetu kwa amani na utulivu mwingi na hadi sasa hapa nimepokea salamu za pongezi kutoka Dayosisi mbali mbali na hata nje ya Tanzania wakipongeza kwa jambo hilo kufanyika pasipo kuwepo kwa vurugu zozote ....hii ni heshima kuwa imewekwa na yote haya yamewezekana kutokana na kazi nzuri ya waumini kufanya maombi "

  Alisema kuwa hakuna jambo lolote alilolifanya vema pasipo kumtanguliza roho mtakatifu hivyo ombi lake kwa wale waliopewa kazi na Mungu ya kuongoza dayosisi hiyo ni kuepuka kusikiliza maneno ya watu wanayoyasema barabarani na badala yake kumtanguliza Mungu na kusikiliza kile kinachosemwa na viongozi wa dayosisi kwani maneno ya mitaani ni ya hivyo hivyo.

  " Mimi yamesemwa mengi ila nawasamehe bure wale wote waliosema ila nawaomba baadae wote wakatubu wapo ambao walikuwa wakifanya kazi ya kunichafua katika vyombo vya habari na mitaani kwa kusema mambo ya aibu dhidi yangu ila kiuharisia sivyo hivyo ....kuna wengine ni maaskofu walipata kutamka kuwa mimi natumia vibaya fedha za chuo kikuu cha Iringa wakati wao ni wasomi na wanajua kabisa kuwa chuo kinakaguliwa na kuna taratibu nzuri tu za kifedha ila kwa kuwa walikuwa wanafanya hivyo kwa kufurahisha nafsi zao na kupotosha nasema ni wakati wa wote kutubu na wakitubu waje kuniomba msamaha "Akifafanua juu ya ajenda ya waumini wa Kanisa hilo jimbo la Mufindi kutaka kuhama Dayosisi yao ya Kusini na kuhamia Dayosisi ya Iringa alisema kuwa kuwa ajenda hiyo ilizungumzwa na aliyewasilisha ajenda kwenye mkutano mkuu huo alikuwa ni yeye mwenyewe.

  " wapo watu wanapotosha kuwa ajenda ya Mufindi kuhamia Dayosisi ya Iringa hakuzungumzwa kwenye mkutano mkuu nawaambia kuwa ajenda hiyo imezungumza na mimi ndie niliyeiwasilisha usiku wa octoba 6 mbele ya wajumbe kwa kutoa maelezo maana ajenda ya askofu ni ajenda ya mkutano mkuu hivyo sikuipeleka Halmashauri kuu wala kamati ya utendaji nilitoa taarifa kwenye mkutano huo kuwa Mufindi wameamua kuhamia Iringa tulipowauliza kuwa wanataka dayosisi walisema hapana wao wameamua kuhamia Dayosisi ya Iringa hivyo niliwaambia wajumbe kuwa hamuwezi ninyi kuwaambia wasihamie maana dayosisi ni mali ya Mungu si mali ya mwanadamu na wakihamia kuhamia popote wao wanaweza hivyo wajumbe wa mkutano huo walikubali kuwapokea ..... hoja ya pili wajumbe walisema kutokana na jambo hilo kuwa bado linasumbua kanisa waliniomba mimi Mdegela kuendelea kuliratibu jambo hilo hadi mwisho ila kuna uzushi umetokea kuwa katibu mkuu anasema ajenda hiyo haikuwepo ni kweli kabisa ajenda kubwa ilikuwa ni uchaguzi mkuu lakini ile nilisimama nikasema kama mimi kwa hiyo mimi nawajibika kusema mbele ya wajumbe na pia nawajibika kubaki na majibu ya ule mkutano mkuu yanayosema maamuzi ya waumini wa Mufindi ndio tutakaouheshimu ndio kauli ya mkutano mkuu "

  Askofu Dkt Mdegela alisema kuwa watu wanasema kuwa msemaji wa dayosisi ya Iringa ni katibu mkuu wapo hao ni wapotoshaji na wanapaswa kupuuzwa kwani hadi sasa yeye Askofu ni msemaji mkuu wa dayosisi ya Iringa hadi hapo januari mwakani siku ambayo askofu mpya atasimikwa rasmi japo katibu mkuu anapaswa kusema kwa ruksa kutoka kwake hivyo anawataka waumini wa jimbo la Mafinga kupokea majibu ya maombi yao kuwa yamepokelewa rasmi .

  Alisema kuwa waumini wa Mufindi waliomba kuhamia dayosisi ya Iringa baada ya kudai kuwa hawapendi kuendelea kubaki dayosisi ya kusini na hivyo walikuwa njia panda kwanza iwapo wangekataliwa Irinda walipanga kuanzisha kanisa lao ama kuanzisha dayosisi yao lakini si kubaki dayosisi ya Kusini .


   Mimi ni mtaalam wa Imani hivyo niliwajibu kwa barua kuwa cha kwanza kuwapatanisha na katibu mkuu na askofu wa dayosisi ya kusini pia kuombana msamaha pale walipokosana ......mimi sina chuki hata kidogo na askofu mwenzangu wa kusini Mengele amekuwa ni rafiki yangu siku zote walipokosana wakristo wa Mufindi na askofu wao Mengele ni pale walipokamatwa na kuwekwa mahabusu kijiji cha Mdandu na kunyimwa dhamana na kukosa kushiriki mkutano mkuu ambayo ni mamlaka kuu ya dayosisi na Halmashauri kubaki kimya juu ya suala hilo sasa mimi nasimamia ukweli kuwa mimi kama askofu sikutumwa kufunga watu polisi nimetumwa kuwakomboa wakristo ndio wanaochagua viongozi na wanayohaki ya kusikilizwa sio kufungwa gerezani sasa kama haya yanamkwaza mwenzangu sina jinsi huu ndio ukweli lakini tujiulize kama Yesu angewakuta pale mahabusu mdandu angefanya nini "

  0 0


   Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema (kulia), akizungumza na wajumbe wa baraza  la ardhi wa wilaya hiyo Dar es Salaam juzi, wakati wakipeana mikakati ya kazi kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya migogoro ya ardhi.
   Mkutano ukiendelea.
   DC Sophia Mjema (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Dar es Salaam, mama Mary Chipungahelo (kulia) na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo.
  DC Mjema akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza hilo.

  Dotto Mwaibale

  WAJUMBE wa Baraza la Ardhi wa Wilaya ya Kinondoni wametakiwa kutobweteka badala yake waende kwa wananchi ili kujua changamoto za ardhi katika wilaya hiyo.

  Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Sophia Mjema Dar es Salaam juzi alipokuwa akizungumza na wajumbe hao ofisini kwake.

  "Ninyi ni watu muhimu sana katika kuibua changamoto za ardhi katika kata zetu zote za  wilaya ya Kinondoni nawaomba msiwe watu wa kukaa nendeni kwa wananchi huko kuna changamoto nyingi za ardhi" alisema Mjema.

  Mjema aliwataka wajumbe hao kwenda kutoa elimu kwa wananchi ili wajue haki zao kuhusu masuala ya ardhi jambo litakalosaidia kupunguza migogoro ya ardhi.

  Aliongeza kuwa migogoro mingi ya ardhi iliyopo katika wilaya hiyo mingi inasabaishwa na wananchi kutojua masuala ya ardhi na elimu.


  0 0


  Zawadi zikipangwa. Kutoka kushoto ni Meneja wa tawi hilo, Seka Urio, Asha Mayuva, Raphael Mlute na Magreth Lwiva. ' Hapa ni Kazi Tu kwa kwenda'
  Taswira ya keki maalumu kwa ajili ya watoto hao ' Hakika NMB Tawi la Mlimani City mmeonesha upendo wa hali ya juu kwa watoto hao barikiweni sanaaa'
  Mwonekano wa wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na watoto hao.
  Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wakiwa kwenye hafla hiyo fupi.
  Hapa ni furaha tupu.
  Hapa ni nani kama baba?
  Meneja wa tawi hilo, Seka Urio (kulia), akizungumza katika hafla hiyo.
  Wafanyakazi wa benki hiyo Tawi la Mlimani City wakiwa katika picha ya pamoja na watoto hao.
  Keki maalumu kwa ajili ya watoto hao ikikatwa.
  Hapa ndipo unapoweza kuutambua utamu wa keki.
  "Hapa ni kama wanafikiria sijui tuondoke na mtoto huyu"


   Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Mlimani City, Seka Urio 
  akiwa amembeba mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo  cha Yatima cha Chakuwama kilichopo Sinza wakati wa hafla fupi ya kutoa msaada iliyofanyika Dar es Salaam leo.
   Katibu Mtendaji wa Kituo hicho, Hassan Hamisi (kulia), akitoa historia fupi ya kituo hicho.
   Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo, wakiwa wamewabeba watoto katika hafla hiyo.
  Mfanyakazi bora wa benki hiyo, kuanzia mwezi Januari hadi Oktoba, Amani Mgweno akishiriki kubeba zawadi za watoto hao.
  Meneja wa tawi hilo, Seka Urio (kushoto), akishiriki kutelemsha zawadi hizo kutoka kwenye gari.
  Zawadi zikiendelea kutelemshwa.
  Zawadi zikitelemshwa. Kulia ni mtoto wa mfanyakzi wa benki hiyo, Asha Mayuva, akionesha upendo kwa watoto wenzake kwa kuwapelekea zawadi.
  Wafanyakazi wa benki hiyo wakiwa wamewabeba watoto mapacha wanaolelewa katika kituo hicho.
  Na Dotto Mwaibale

  BENKI ya NMB Tawi la Mlimani City imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa Makao ya  Kulea Watoto Yatima ya Chakuwama yaliyopo Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni  moja ya njia ya kujumuika na jamii inayo wazunguka.

  Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo ambao ni vyakula na vifaa vya shule kwa ajili ya wanafunzi Meneja wa benki hiyo wa tawi hilo, Seka Urio alisema ni kawaida kwa benki hiyo kushiriki shughuli za kijamii na kutoa faida wanayoipata kwa wananchi ambao ndio wateja wao.

  "Tunajisikia faraja kutoa vitu vichache kwa watoto wetu ambao mnawalea katika kituo hiki pia ni kurudisha faida tunayoipata kwa jamii" alisema Urio.

  Urio alisema vitabu vyote vya dini vinaelekeza kuwajali na kuwafariji wenzetu wenye uhitaji ikiwa ni agizo lake mwenyezi mungu.

  Katibu wa Kituo hicho, Hassan Hamisi alisema kituo hicho chenye watoto 60,000 wakike wakiwa 25 na kiume 35 tangu kianzishwe kwake mwaka 1998 kimepata mafanikio ya kupata nyumba yao ya kuishi watoto hao, malezi huduma za elimu na afya.

  "Kwa kweli tukiangalia tulipoanzisha kituo hiki na sasa tumepiga hatua licha ya kuwepo changamoto kwani tunasomesha watoto katika shule mbalimbali za sekondari na msingi na wengine wapo vyuo vikuu ni jambo la kujivunia" alisema Hamisi.

  Alisema watoto wengine wamepata kazi baada ya kuhitimu elimu katika ngazi mbalimbali na baadhi yao wameoa na kuolewa na sasa wanaendesha familia zao.

  Hamisi alimshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kuanzisha utaratibu wa wanafunzi kupata elimu bure kwani umewapunguzia changamoto ya kuwalipa ada wanafunzi 47 wanao walea katika kituo hicho.

  Hamisi alisema pamoja na kupiga hatua bado wanachangamoto mbalimbali kama chakula na nyumba kwani kila siku watoto wamekuwa wakiongeza katika kituo hicho kutokana na migogoro ya kifamilia, wazazi au walezi kufariki na kuwaacha watoto na watoto kutelekezwa hivyo akawaomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia kama ilivyofanya benki hiyo.

  Hafla hiyo ilihudhuria na wafanyakazi wa benki hiyo ambapo waliwafariji watoto yatima kwa kuwapa vitu mbalimbali na kuzungumza nao ambapo waliwasisitizia kuzingatia masomo. 

older | 1 | .... | 1000 | 1001 | (Page 1002) | 1003 | 1004 | .... | 1896 | newer