Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1002 | 1003 | (Page 1004) | 1005 | 1006 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akilakiwa na Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete alipowasili kwenye msiba wa Marehemu Mariam Ramadhani Saburi, shemeji yake Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo  Oktoba 10, 2016

  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akilakiwa na Bw. Mohamed Kikwete  alipowasili kwenye msiba wa Marehemu Mariam Ramadhani Saburi, shemeji yake Rais Mstaafu Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo   Oktoba 10, 2016. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Majid Hemed Mwanga, 
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiifariji wana familia wa Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemejie  (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Ramadhani Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimfariji akifariji wana familia wa Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemejie  (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Ramadhani Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akimfariji Bibi Maguno Binti Athumani ambaye ni  mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)   Marehemu Mariam Ramadhani Saburi   aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na  Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete (kulia) akimfariji Bi Maguno Binti Athumani ambaye ni mkwe wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)  Marehemu Mariam Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
  Mawaidha yakitolewa msibani
  Bw. Yusuph Kikwete akielekeza waombolezaji sehemu ya kukaa wakati wa msiba huo
   Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mnbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete alipowasili kwenye  msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo.
   Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mkwewe Bi Maguno Binti Athumani kwenye  msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) Marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo 
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiongea jambo na  Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu)  Marehemu Mariam Ramadhani Saburi aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
   Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimpa mkono wa pole Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo 
  Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine  kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo 
  Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine  kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo 
   Sehemu ya waombolezaji   kwenye msiba wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa  huko Bagamoyo leo
  Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na waombolezaji wengine wakibeba mwili wa shemeji  yake (Rais Mstaafu) marehemu Mariam Ramadhani Saburi  aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo 
  Waombolezaji wakimswalia maiti 
  waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa  marehemu Mariam Ramadhani Saburi  kuelekeza makaburini huko Bagamoyo leo

  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwafariji watoto wa  shemejie Rais Mstaafu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete, Marehemu Mariam Ramadhani Saburi,    aliyefariki jana na kuzikwa huko Bagamoyo leo Oktoba 10, 2016
  Sehemu ya waombolezaji msibani
  Waombolezaji wakijiandaa kupata chakula cha mchana kabla ya maziko.
  Picha na IKULU

  0 0


  Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii

  MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amepiga marufuku ukusanywanji wa ushuru wa biashara katika soko jipya la Pugu Kigogo fresh.

  Akizungumza wakati wa ziara yake katika Kata ya Pugu na Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam , Mjema alichukua

  hatua hiyo mara baada ya kusikiliza kero za Wafanyabiashara na Wananchi wa eneo hilo ambao walifika kumsikiliza katika mkutano uliofanyika Sokoni hapo.

  “Hapa kuna mambo mengi yanapswa kushughulikiwa hili pawe sawa hivyo Halamsahauri nawapa muda wa miezi mitatu wakurekebisha utaratibu huo hivyo kwa kipindi chote hicho ni marufuku kukusanya pesa kutoka katika soko hili mpaka hapo miundombinu mtakapo iweka sawa”amesema Dc Mjema.

  Aliongeza kuwa ni wajibu wa Halmashauri kutengeneza mazingira mazuri hili kuweza kurahisisha ufanyikaji wa biashara wenye tija ambao autarishi afya za watu na Mazingira kwa ujumla.

  Katika hatua nyingine mkuu huyo wa Wialya amefuta vikundi vyote vya ulinzi shiriki vya kata ya Pugu kwa kumtaka OCD wa kituo cha Staki Shari kusimamia agizo hilo hili kuweza kusuka upya mfumo wa ulinzi katika eneo kutokana malalamiko ya Wananchi wa kata hiyo

  Amesema kuwa wakazi wa kata ya Gongolamboto awana imani kabisa na vikundi vya ulinzi shirikishi vilivyopo katika eneo hilo ndio maana anataka ufanyike utaratibu upya kwa mujibu wa katiba amabo utawasaidia kupata vijana walio waminifu.

  0 0

  Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-

  DAR ES SALAAM

  SERIKALI imesema imejipanga kuhakikisha kuwa idadi kubwa ya wananchi waishio  vijijini na mijini hapa nchini wananufaika na huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama ili kuwaondolea kero ya uhaba wa maji  watanzania ifikapo mwaka 2020.
   
  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge wakati wa uzinduzi wa Bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Maji.


  Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuongeza huduma ya upatikanaji wa maji vijijini kutoka asilimia 72 hadi asilimia 85 na mijini kutoka asilimia 86 hadi asilimia 95 ifikapo mwaka 2020.


  Waziri Lwenge amesema ili kufikia lengo hilo Serikali itahakikisha inafanyakazi kwa juhudi na weledi na maarifa ili kuondokana na kero hizo.


  “Katika kufikia malengo ya Serikali kuwa ifikapo mwaka 2020 huduma ya maji inawafikia wananchi waishio vijijini kwa asilimia 85 kutoka asilimia 72 ya sasa na mijini kwa asilimia 95 kutoka aslimia 86 ya sasa,” alifafanua waziri Lwenge.


  Katika kufanikisha hilo Waziri Lwenge ameiagiza Bodi hiyo kuwa wabunifu, waadilifu na wachapakazi ili kuleta mabadiliko ambayo yataiwezesha nchi kuwa nchi ya Uchumi wa kati na ya Viwanda hasa katika Sekta ya Maji.


  Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mbogo Futakamba alisema kuwa matumaini ya Serikali katika kuimarisha hali ya huduma ya maji vijijini na mjini ni kuona mfuko huo unasimamia ili kutoa matunda yaliyokusudia.


  Aidha, Mhandisi Futakamba alisema kuwa Bodi ya Wadhamini imekasimiwa jukumu la kusimamia na kulinda maslahi ya Taifa katika kuhakikisha Sekretarieti ya Mfuko inatekeleza majukumu kwa mujibu wa Sheria, Kanunu na Taratibu zilizopo.

  0 0


  Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (kushoto) akisalimiana na Afisa Mkuu wa Kampuni ya StarTimes Bw. Leo wakati alipokutana naye kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano leo 10/10/2016 Jijini Dar es Salaam.


  Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura akiongea na wawekezaji wa Makampuni matatu kutoka China leo 10/10/2016 Jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya Viongozi na watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na wawekezaji wakifuatilia mazungumzo hayo leo 10/10/2016 Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wawekezaji pamoja baadhi ya Viongozi na watendaji wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo leo 10/10/2016 Jijini Dar es Salaam. Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM).

  Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura amekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji wa makampuni matatu kutoka China, lengo la ziara la wawekezaji hao likiwa ni kufanya utafiti kujua ni namna gani Kampuni ya StarTimes inapiga hatua katika kusaidia kukuza maendeleo katika sekta ya habari Tanzania. 

  Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika leo Wizarani hapo, Mhe. Wambura amesema kuwa Serikali iko mbioni kujenga Jengo Maalum kwa ajili ya shughuli za Kiutamaduni (Cultural Complex) ambalo linatarajiwa kujengwa Bagamoyo na ndani ya jengo hilo kutawekwa vitu mbalimbali vinavyohusu utamaduni wa Tanzania. 

  Ameeleza kuwa, Tanzania imekuwa ikishirikiana na China katika masuala mbalimbali yakiwemo ya michezo, utamaduni na Sanaa ambapo baadhi wa wageni kutoka China wamekuwa wakifika kutalii na kuwekeza, lakini pia baadhi ya Watanzania nao wamekuwa wakipata fursa ya kutembelea China kujionea maendeleo na kujifunza mambo mbalimbali. 

  “Tanzania inapenda kushirikiana na China katika mambo mbalimbali kama vile kutengeneza filamu, michezo na hata utamaduni, kwakweli ushirikiano huu umekuwa wa manufaa kwetu sisi Watanzania kwani unapanua wigo wa kukuza maendeleo”, alisema Mhe. Wambura. 

  Ameongeza kuwa, Kampuni ya StarTimes ni moja kati ya Makampuni yaliyoisaidia Tanzania kuhama toka Analojia kwenda Dijitali ambapo kampuni hiyo iliweza kuwekeza nchini kwa kuleta ving’amuzi vyenye bei nafuu kiasi cha kumwezesha Mtanzania wa hali ya chini kumudu kununua na kuweza kupata habari kupitia runinga yake. 

  Aidha, amewashauri wawekezaji hao kutengeneza makala mbalimbali zinazohusu utamaduni wa Kitanzania kwa kushirikiana na Watanzania kwani inaweza kuleta soko zuri ndani na nje ya nchi. Kwa upande wake Kiongozi wa msafara wa wawekezaji hao ambaye pia ni Afisa Mkuu wa Kampuni ya Star Media (T) Ltd Bw. Leo amesema kuwa, China itaendeleza ushirikiano na Tanzania ambapo iko mbioni kutoa nafasi kwa Watanzania kutoka Shirika la Utangazaji TBC na Wizara kwenda kujifunza namna ya kutengeneza habari ikiwemo Makala na upigaji picha ili taaluma hiyo ije kuwasadia wengine.  

  Mbali na kuja kutafiti namna Kampuni ya StarTimes inavyofanya vizuri katika kuleta maendeleo Tanzania, ujio wa wawekezaji hao nchini pia unafungua milango zaidi ya kibiashara baina ya Tanzania na China na kuendeleza ushirikiano wenye lengo la kuleta maendeleo.

  0 0

   Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza katika mdahalo wa siku ya wazee kiwilaya iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri kulia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wazee Muheza
  Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (DAS) akizungumza neno kwenye kwenye mkutano huo
  Mwenyekiti wa Halmasahuri ya wilaya ya Muheza akizungumza
   Afisa Ustawi wa Jamii na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri akizungumza kwenye kikao hicho.
   Mwenyekiti wa Chama cha Wazee wilayani Muheza (UWAWAMU) Seif Athumani akizungumza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajati,Mhandisi Mwanasha Tumbo akifuatilia kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,
  baadhi ya Wazee wilayani Muheza wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa wilaya hiyo,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo.
  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akigawa zawadi ya sabuni kwa mmoja kati ya wazee wilayani humo wakati wa siku ya wazee dunia kiwilaya iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri wilayani humo
  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akigawa zawadi ya sabuni kwa mmoja kati ya wazee wilayani humo wakati wa siku ya wazee dunia kiwilaya iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri wilayani humo
  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akigawa zawadi ya sabuni kwa mmoja kati ya wazee wilayani humo wakati wa siku ya wazee dunia kiwilaya iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri wilayani humo.habari kwa hisani ya blog ya kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akizungumza na wanachama wa mtandao huo wakati wa mkutano wa kuchangia maafa ya tetemeko la ardhi, Kagera.Picha na Mpiga picha wetu.
  Mwanachama wa SHIWATA, Hamisi Kiondo akichangia hoja ya namna ya kusaidia waliopatwa na maafa Kagera. 

  Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) unatarajia kukabidhi mchango wa maafa ya tetemeko la ardhi kwa wananchi wa mkoa wa Kagera baada ya siku ya awali iliyokuwa imepangwa ya Oktoba 14, 2016 ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kfo cha Mwalimu Nyerere kuingiliana na ratiba nyingine za kitaifa.

  Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib akizungumza katika mkutano wa wanachama jana alisema mpaka sasa fedha ambazo zinatarajiwa kukabidhiwa ni sh. 600,000 ambazo kati ya hizo 100,000 zimechangwa na wanachama katika mkutano huo.

  Alisema wakati maandalizi ya kukabidhi fedha hizo ukiendelea siku hiyo ambayo SHIWATA imetenga kwa ajili ya kufanya kazi za kumuenzi baba wa Taifa, Nyerere viongozi wa kitaifa ambao walikuwa wapokee mchango huo watakuwa mkoa wa Simiyu katika sherehe ya kuzima Mwenge wa Uhuru.

  Katika mkutano huo wanachama waliahidi kuendelea kuchangia matukio yote ya kijamii na wengi wameahidi kuwasilisha vifaa mbalimbali na nguo kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Kagera.

  Wakati huo huo SHIWATA imetoa ofa ya Sh. Mil. 3.2 kwa wanachama wake watakaojenga nyumba za kuishi katika kijiji chao cha Mwanzega Mkuranga.

  Akifafanua kuhusu ofa hiyo, Taalib alisema gharama za kusafirisha vifaa vya ujenzi, gharama za kusafisha eneo la kujenga na ekari moja ya kulima bustani watapewa bure.

  Alisema kasi ya wanachama kujenga na kuhamia kijijini inaridhisha mpaka sasa nyumba 200 zimekamilika na nyingine zinaendelea kujengwa.

  Taalib huduma za jamii kijijini hapo zinafanyiwa kazi ambapo huduma ya maji safi na salama ya kisima kirefu itapatikana mapema.

  0 0

    Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba (katikati), Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia) na Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga , wakionesha jarida la kupinga adhabu ya kifo wakati wa uzindi wake Dar es Salaam leo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo- Bisimba (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akisoma tamko la kupinga adhabu ya kifo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio na kushoto ni Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga.
   Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji, Imelda Urio (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
   Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Anna Henga akizungumza katika mkutano huo.
   Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
  Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.
  ………………………………………………………..
  Na Dotto Mwaibale
   
  KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimefungua kesi ya kikatiba kuhusiana na ulinzi wa haki ya kuishi na urekebishwaji wa sheria ya kanuni ya adhabu juu ya ulazima wa kutolewa kwa adhabu ya kifo katika makosa ya uhaini na mauaji.
   
  Kesi hiyo imefunguliwa dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali  wakitaka ufafanuzi zaidi juu ya adhabu ya kifo, wakibainisha kuwa adhabu hiyo haimpi nafasi mtuhumiwa kujirekebisha bali ni ya kulipiza kisasi.
   
  Kituo hicho kimesema endapo Tanzania itatekeleza hukumu ya kifo  kwa sasa inamaanisha watu wapatao 228 na zaidi watapoteza maisha yao huku  wengine 244 wanasubiria maamuzi ya rufaa zao.
   
  Akizungumza wakati akitoa tamko la kupinga adhabu ya kifo  Dar es Salaam leo Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Hellen- Kijo Bisimba alisema hadi  mwaka 2015 jumla ya watu 472 walikuwa wamehukumiwa kunyongwa.
   
  Alisema kituo kinaiomba serikali kurekebisha sheria ya kanuni ya adhabu na sheria ya ugaidi yenye kutoa adhabu ya kifo kwa makosa ya mauaji, uhaini na ugaidi.
   
  Dk. Bisimba alisema kituo  kina sababu za kupinga adhabu hiyo ya kifo na  hawafurahii watu kuua wengine na ndio maana hawapendi pia hata muuaji auawe.
   
  “Adhabu ya kifo ni vigumu kuhakikisha kuwainatekelezwa tu  kwa wale watu ambao huwezi kuirekebisha kwani mfumo wa utoaji haki huwa pia na mianya ya makosa na hivyo maisha ya mtu yanaweza kupotea bure,” alisema Dk. Bisimba na kuongeza kuwa hakuna ushahidi wowote kuwa adhabu hiyo inaweza kuzuia watu wengine kutokutenda makosa  kama hayo.
   
  Alisema licha ya adhabu  hiyo kutokutekelezwa nchini kwa takriban miaka 22 , taaarifa zinaonesha kuwa watu 72 ambao walishawahi kunyongwa kutokana na adhabu hiyo.
   
  Hata hivyo aliiomba serikali kutengeneza utaratibu wa kuelimisha jamii juu ya kuheshimu haki za binadamu hususani haki zakuishi na kuweka mazingira ya kuiheshimu haki hiyo, pia ibadilishe sheria  kwa kuondoa adhabu ya kifo na kuweka adhabu mbadala kwenye makosa ya jinai na kwa wafungwa waliopo mfano vya muda mrefu  gerezani.

  0 0

   Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar eas Salaam leo, kuhusu mfumuko wa bei ya taifa kwa mwezi Septemba 2016. 
   Mkutano na wanahabari ukiendelea.
   waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
  Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo

  Na Dotto Mwaibale

  MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Septemba, 2016 umepungua hadi asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.9 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

  Hayo yabebainishwa na Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Ephraim Kwesigabo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar eas Salaam leo. 

  " Hii inamanisha kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi ya upandaji ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti 2016 " alisema Kwesigabo.

  Alisema  Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 103.05 mwezi Septemba 2016 kutoka 98.64 
  mwezi Septemba 2015.Kwesigabo aliongeza kuwa mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi mwezi Septemba 2016 umepungua hadi asilimia 6.0 kutoka asilimia 7.0 ilivyokuwa 
  mwezi Agosti 2016.

  Alisema  kupungua kwa mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia mwezi Septemba 2016 zikilinganishwa na bei za mwezi Septemba 2015.

  Alisema mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula zilizoonesha kupungua ni pamoja na bei za dagaa kwa asilimia 11.6 na viazi vitamu kwa asilimia 3.2.

  "Kwa upande mwingine mwenendo wa bei za baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilionesha kupungua ni pamoja na bei za gesi kwa asilimia 10.4, dizeli kwa asilimia 2.9 na petrol kwa asilimia 2.8.

  Akizungumzia mabadiliko ya bei kati ya mwezi Agosti na Septemba 2016 fahirisi za bei zimepungua hadi 103.o5 mwezi Septemba 2016 kutoka 103.28 mwezi Agosti 2016.

  Alisema kupungua kwa fahirisi za bei kumechangiwa na kupungua kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na bidhaa zisizo za vyakula.

  Alitaja baadhi ya bidhaa zilizochangia kupungua kwa fahirisi ni pamoja na mchele kwa asilimia 2.6, unga wa mahindi kwa asilimia 1.0, dagaa kwa asilimia 3.0 na mbogamboga kwa asilimia 4.3.

  Alisema kwa upande mwingine baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei ni pamoja na dizeli kwa asilimia 2.9, petroli kwa asilimia 2.8 na mafuta ya taa kwa asilimia 2.9

  Akizungumzia thamani ya shilingi ya Tanzania kwa mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 alisema uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia sh.97 na senti 04 mwezi Septemba 2016 kutoka mwezi Desemba 2015 ikilinganishwa na shilingi 96 na senti 83 ilivyokuwa mwezi Agosti 2016.

  Kwesigabo akizungumzia mfumuko wa bei kwa bidhaa ya nchi za Afrika Mashariki nchini Kenya mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 umeongezeka kidogo hadi asilimia 6.34 kutoka asilimia 6.26 mwezi Agosti 2016.

  Alisema nchini Uganda mfumuko wa bei wa mwezi Septemba 2016 umepungua hadi asilimia 4.2 kutoka asilimia 4.8 mwezi Agosti 2016.

  0 0

  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba akizungumza na wateja wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba ( wa kwanza kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo na wateja kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kushoto) akimsikiliza mmoja wa wateja wa kampuni ya TTCL mwenye asili ya China juzi kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Peter Ngota akizungumza na wateja wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Peter Ngota (wa pili kulia) akijumuika na baadhi ya wateja na wafanyakazi wa kampuni ya TTCL kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa kampuni hiyo na wateja kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akibadilishana mawazo na mmoja wa wateja wa kampuni ya TTCL mwenye asili ya China juzi kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba ( wa tatu kushoto) akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi na viongozi wa kampuni hiyo na wateja kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
   KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) imesema itaendelea na utekelezaji wa kuboresha miundombinu ya mtandao wake wa simu za mezani, mkononi pamoja na huduma za data ili kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wake na kufikia kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano nchini. Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki na Kaimu 

   
  Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Waziri Kindamba alipokuwa akizungumza na wateja mbalimbali kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Kaimu Afisa huyo wa TTCL, alisema kuwa maboresho ya miundombinu yanayofanywa kwa sasa katika shirika hilo yanaliwezesha kukabiliana na changamoto zilizokuwepo awali na kuwapa wateja weke fursa ya kufurahia huduma mpya na za zamani zinazotolewa kisasa na kwa umahiri mkubwa hivi sasa. 
   
  "Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) inaendelea na utekelezaji wa uboreshaji wa miundombinu ya mtandao wa simu za mezani, simu za mkononi na huduma za Data ili tuweze kutoa huduma iliyo bora zaidi kwa wateja wetu na kufikia kiwango cha hali ya juu katika kutoa huduma za Mawasiliano," alisema Waziri Kindamba. 
   
  Aidha alifafanua kuwa TTCL inawaahidi wateja wake na taifa kwa ujumla kwamba itaendelea kutoa huduma bora, za uhakika na gharama nafuu katika kutengeneza mazingira mazuri ya kiteknolojia, kwani baada ya mabadiliko watumishi wake wameazimia kuongeza kasi ya kufanya kazi kwa bidii, uadilifu, ubunifu na uzalendo wa hali ya juu ili kwenda sambamba na mahitaji ya sasa na baadaye ya wateja wa sekta ya Mawasiliano. Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki,ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya TTCL aliyefanya vizuri katika kutoa huduma kwa wateja. Zoezi hilo lilifanyika juzi kwenye hafla ya hitimisho la kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 zilizofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam.
   
  Pamoja na hayo Kindamba aliwataka wateja hasa taasisi na makampuni mbalimbali ya nje na ndani ya nchini kukitumia Kituo cha Taifa cha Kutunzia kumbukumbu (National Internet Data Centre) ambacho Ujenzi wake umekamilika na kimeanza kufanya kazi hiyo, huku kikiwa cha kisasa na chenye hadhi ya kimataifa.

   "...Niwashukuru sana wateja ambao wameishakubali kuifadhi taarifa zao kwenye Kituo. Nafahamu kwamba mazungumzo yanaendelea kati yetu na Wateja wengine na ninaamini kuwa tutakubalina na kufanya kazi pamoja...natoa wito kwa Wateja na Wadau wote wa ndani na nje ya nchi, tutumie kituo hiki chenye ubora wa Kimataifa na hadhi ya juu kabisa hapa nchini na eneo zima za Afrika Mashariki," alisema Kindamba. 
   
  Aliongeza kuwa kwa sasa kampuni ya TTCL imejipanga vyema kufanya kazi kwa ufanisi, huku ikitekeleza kwa vitendo falsafa ya Serikali ya awamu ya tano ya Hapa Kazi Tu. TTCL pia imedhamiria kutumia kwa uaminifu mkubwa rasilimali zilizopo ili iweze kutoa mchango stahiki katika mageuzi yanayoendelea ya kuifanya Tanzania kupiga hatua kuelekea kuwa Nchi ya Uchumi wa Viwanda.
   
  "Lengo hili la kuifanya Nchi kuwa ya Uchumi wa Viwanda, litafikiwa kwa uhakika zaidi endapo huduma za Mawasiliano zitakuwa za uhakika. TTCL tupo tayari na tunao uwezo wa kufanikisha lengo hili pasi na shaka yoyote. 
   
  Sote tunafahamu nia ya dhati ya Serikali yetu ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu Mpendwa Dkt John Pombe Magufuli. Serikali yetu inataka kazi kwa vitendo, inataka huduma bora kwa Wananchi," alisisitiza Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Kindamba. Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Nicodemas Thomas Mushi (wa pili kulia) akipata picha na baadhi ya wageni waalikwa kwenye hafla ya kilele cha Wiki ya Huduma kwa wateja wa TTCL, 2016 iliyofanyika ndani ya Banda la Maonesho ya Biashara la kampuni hiyo lililopo Viwanja vya Mwalimu Julias Nyerere, Sabasaba jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Ofisa Uhusiano wa TTCL, Edwin Mashasi.

  0 0

  KAMPUNI ya Simba Motors imesema ina mpango wa kujenga kiwanda cha kuunganisha magari aina ya pick-up ambacho kitaanza kuzalisha magari kabla ya Desemba 30, mwaka huu.

  Ahadi hiyo imetolewa leo mchana (Jumatatu, Oktoba 10, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Jitesh Ladwa mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam.

  “Tumeamua kuunda magari aina ya pick-up kwa sababu ya mahitaji makubwa yaliyopo nchini. Takwimu zinaonyesha kuwa, kwa mwaka Tanzania inanunua magari ya aina hii zaidi ya 4,000. Katika nchi za SADC mahitaji ni pick-up 35,000 kwa mwaka. Tutaanza na mtaji wa dola za Marekani milioni 200 na tumeomba ekari 200 katika eneo la EPZ,” amesema.

  “Eneo la kiwanda cha kuunganisha magari peke yake linahitaji ekari 50, kwa hiyo tukiweka na yadi za kupaki magari, eneo la viwanda vingine, eneo la kushusha na kupakia makontena yatakayokuwa yakisafirishwa kwenda nchi jirani, ni lazima tutahitaji eneo kubwa zaidi,” amesisitiza.

  Amesema mradi huo wa majaribio, utaanza kwa kutengeneza magari 20 kila mwezi na kwamba kazi ya utengenezaji magari itaongezeka na kufikia 1,000 na baadaye 5,000 kwa mwaka. “Tunataraji gari la kwanza litazinduliwa kabla ya Krismasi, mwaka huu,” amesema.

  Bw. Ladwa amesema uundaji wa magari hayo aina ya Foton-Tunland utafanyika kwa ubia baina ya kampuni yao, SUMA-JKT na kampuni Foton International ya China kwa kutumia teknolojia ya Kichina na kwamba magari hayo yanayotumia 4-Wheel Drive, yana uwezo wa kupita kwenye barabara za aina zote.

  Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Kampuni hiyo, Bw. Aatish Ladwa, amesema mradi utakapoanza, mbali ya kutoa ajira kwa Watanzania, utawezesha pia kujengwa kwa viwanda vingine vitakavyotengeneza matairi ya magari, vioo, taa, bumpers, viti na filters.

  “Tunataraji kujenga uwezo wa wahandisi wazawa, uhamishaji wa ujuzi kwa mafundi wa Kitanzania (technology transfer), kupunguza bei kwa mlaji wa mwisho, kupunguza gharama za uzalishaji, kutekeleza amza ya Serikali ya kuifanya Tanzania kuwa ni nchi ya viwanda, kuongeza ajira kwa wanajeshi, na kuwezesha upatikanaji wa vipuri vya magari kwa urahisi na kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.”

  “Kiwanda kitaajiri wafanyakazi 1,500 kwa kuanzia ambao watakuwemo mafundi na watoa huduma mbalimbali, lakini katika kipindi cha miaka mitatu hadi mitano, tunataraji kuongeza wafanyakazi wengine 5,000 wakati uzalishaji ukiwa umepamba moto,” amesema.

  Kwa upande wake, akizungumza mara baada ya kulikagua gari la mfano aina ya Foton-Tunland, Waziri Mkuu amesema anawakaribisha kwenye uwekezaji huo hasa ikizingatiwa kuwa magari hayo yana uwezo wa kupita kwenye maeneo ya vijijini ambako barabara zake siyo nzuri.

  “Ofisi za Serikali zinayahitaji zaidi haya magari, hospitali zetu za wilayani nazo pia zinayahitaji haya magari ili yaweze kutoa huduma za chanjo kwa watoto, huduma za UKIMWI, kampeni za kupambana na malaria, na huduma kwa mama wajawazito huko vijijini,” amesema.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  2 MTAA WA MAGOGONI,
  S. L. P. 3021,
  11410 DAR ES SALAAM.
  JUMATATU, OKTOBA 10, 2016 

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhisho ya siku ya magonjwa ya akili Duniani iliyoadhimishwa katika hospitali ya rufaa ya maginjwa ya akili ya mirembe mjini Dodoma
  Mganga mkuu hospitali ya rufaa ya magonjwa ya akili ya mirembe Dr Erasmus Mndeme akitoaa taarifa ya matatizo yanayochangia magonjwa ya akili wakati wa maadhimisho ya siku ya afya Duniani yaliyofanyika mkoani Dodoma leo katika hospitali hiyo.
  Mganga mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr James Charles akitoa maelezo kwenye maadhimisho ya siku ya afya ya akili Duniania iliyoaadhimshwa kitaifa katika hospitali ya rufaa ya magonjwa ya akili ya mirembe mjini Dodoma.
  Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Christina Mndeme akikagua bidhaa zinazozalishwa na wagonjwa wa akili katika hospitali ya rufaa ya mirembe mjini Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya magonjwa ya akili Duniani yaliyofanyika kitaifa mkoani Dodoma katika hospitali hiyo
  Baadhi ya Washiriki wa maadhimisho ya siku ya afya ya akili Duniani wakiwa kwenye picha ya pamoja iliyofanyika kitaifa mjni Dodoma leo

  Watanzania wameungana na wenzao duniani kote kuadhimisha siku ya Afya ya Akili duniani huku Tanzania ikitajwa kuwepo kwa zaidi ya wagonjwa laki nne na nusu wanaougua maradhi hayo nchini.

  Aidha mkoa wa Dar es salaam ndio unaongoza kwa kuwa na wagonjwa ambapo sababu kubwa inatajwa kuwa ni matumizi ya kupindukia ya madawa ya kulevya ikiwa ni pamoja na Bangi.

  Kadhalika, mkoa wa Dodoma watu 12 wanapokelewa kila siku katika hospitali ya rufaa ya wagonjwa wa akili ya Mirembe kutokana na tatizo hilo.

  Maadhimisho hayo ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Dodoma katika hospitali ya taifa ya magonjwa ya akili Mirembe ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 10 ya mwezi wa kumi.

  Kauli mbiu ya maandimisho hayo ni “utu katika afya ya akili, huduma za kisaikolojia na afya ya akili kuwa huduma ya kwanza kwa wote”

  Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme amewataka watanzania kuungana katika kupiga vita unyanyasaji na ukatili kwa wagonjwa wa akili na badala yake wapelekwe hospitali kwa ajili ya kupata matibabu.

  Amesema tatizo la akili huathiri kufikiri,kuhisi,kutambua na kutenda na tatizo la akili kwa sasa linaongezeka ambapo takribani watu milioni 35 wanaishi na ugonjwa huo.
  Mkuu wa wilaya huyo amesema kwa mujibu wa taarifa ya akili na dawa za kulevya ya mwaka 2013/2014 za shirika la afya duniani(WHO)o mkoa unaoongoza kuwa na wagonjwa wengi ni Dar-es-salaam ambayo ina asilimia 2 ya wagonjwa ikifuatiwa na Mwanza yenye asilimia 1.2 huku mkoa wa mwisho ukiwa ni Rukwa wenye asilimia 0.2

  Naye Mganga mkuu wa Mkoa wa Dodoma, DK. James Kiologwe, amesema kwa mkoa wa Dodoma wagonjwa 1256 walipatikana katika kipindi cha mwaka 2015 na kila siku wanapokea wagonjwa 12 ambao wanaugua ugonjwa huo wa akili ambao wanatoka katika maeneo mbalimbali.

  Kwa upande wake, Mganga mkuu wa Hospitali ya rufaa ya wagonjwa wa akili Mirembe, Erasmus Mganga, ameeleza sababu kuu mbili zinazosababisha ugonjwa wa akili, kuwa ni ile ya mtu kuzaliwa na vinasaba vya ugonjwa huo ambapo vinakuwa ni vya kurithi na pia inatokana na magonjwa ambayo yanashambulia kwenye ubongo ambapo mtu anaweza kuugua ugonjwa wa Maralia, uti wa mgongo na mapafu ambapo huathiri ubongo.

  Amebainisha mgonjwa huyo akishatibiwa na kupona anabaki na tatizo kwenye ubongo na hivyo kupatwa na ugonjwa wa kichaa, kutokana na namna alivyoumwa.

  0 0

      Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO, Ifakara

  Wasichana wanaoishi Ifakara, Wilaya ya Kilombero, Mkoani Morogoro wameiomba Serikali kuongeza adhabu kwa wanaume wanaosababisha mimba za utotoni ili kukomesha tatizo hilo.

  Maombi hayo yametolewa leo na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ifakara Jackline Mwalusako ambaye amekaimu nafasi ya Meneja Miradi wa Shirika la Plan International- Ifakara kama ishara ya kuadhimisha Siku ya Msichana Duniani itakayofanyika Oktoba 11 mwaka huu.

  Mwalusako amesema kuwa mila potofu pamoja na ndoa za utotoni ndio chanzo kikubwa kinachosababisha kuongezeka kwa mimba za utotoni kwahiyo kuna haja ya kubuni mbinu mpya zitakazotokomeza tatizo hilo.

  “Pamoja na adhabu zilizowekwa kwa ajili ya kuwaadhibu wanaume wanaosababisha mimba za utotoni bado idadi ya wasichana wanaopata mimba za utotoni inaongezeka, hivyo tunaiomba Serikali iwaongezee adhabu wanaofanya makosa hayo ili kuzuia tatizo hili”, alisema Mwalusako.

  Mwalusako ameongeza kuwa wazazi pia wanachangia wasichana kupata mimba za utotoni kwani wanakubali kuwaozesha watoto wao wakiwa bado wadogo kwahiyo nao wanatakiwa kupewa adhabu ili waachane na tabia ya kuwaozesha kabla ya muda muafaka.

  Kwa upande wake mwanafunzi anayekaimu nafasi ya Mratibu wa Miradi ya Shirika la Plan International, Deborah Mtiko ametoa rai kwa shule mbalimbali kuongeza utoaji wa elimu kuhusu mimba za utotoni ili kuwapa uelewa wasichana waliopo mashuleni.

  Mkoani Morogoro, Shirika la Plan International - Tanzania linaadhimisha Siku ya Msichana Duniani katika Kijiji cha Ihenga kilichopo mkoani humo kuanzia saa  tatu kamili asubuhi.

  0 0

   Baadhi ya wafanyakazi wa UBA Bank wakiwa katika Mazoezi ya viuongo
   Baadhi ya wafanyakazi wa UBA Bank wakiwa katika mbio za pole
   Baadhi ya wafanyakazi wa UBA Bank wakiwa katikamchezo wa kuvuta kamba katika bonanza la robo tatu ya mwaka
   Baadhi ya wafanyakazi wa UBA Bank wakiwa katika mchezo wa mpira wa miguu katika Tamasha lao la robo tatu ya Mwaka chuo kikuu cha Dar es Salaam
   Baadhi ya Wafanyakazi wa UBA Bank wakiwa katika mchezo wa mbio za magunia

  Wafanyakazi wa Bank ya UBA wanao zaliwa mwezi october wakikata keki kwa ajili kusheherekea siku yao ya Kuzaliwa

  0 0

  Benny Mwaipaja, MoFP-Washington DC, Marekani

  MAWAZIRI wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi mbalimbali za kiafrika, wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, wamekutana Jijini Washington DC, Marekan,i na kuzitaka Taasisi hizo kuweka mipango inayoakisi na kutatua changamoto zinazolikabili bara hilo ikiwemo, uhalifu, umasikini, mizozo ya kivita na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi

  Aidha, Viongozi hao wamezitaka taasisi hizo kuweka uwiano wa uwakilishi wa uongozi wa juu ili kuhakikisha kuwa maslahi mapana ya nchi hizo yanalindwa na maendeleo endelevu yanafikiwa kwa haraka.

  Akizungumza kwenye moja ya mikutano hiyo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ambaye kiutaratibu ni mmoja wa Magavana wa Benki ya Dunia na IMF, amesema kuwa mashirika hayo ya fedha ya kimataifa yanamchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi za kiafrika ikiwemo Tanzania.

  Hata hivyo amesema kuwa mdororo wa uchumi duniani, ambao unaonesha kuwa viwango vya ukuaji wa uchumi vilivyokadiriwa kufikiwa kwa asilimia 3, havitafikiwa ambapo takwimu zinaonesha kuwa ukuaji wake hivi sasa ni asilimia 1.5 tu, unaashiria namna nchi wanachama zinatakiwa kujipanga kuhakikisha kuwa uchumi unapanda.

  Dkt. Mpango amesema kuwa uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi kwa wastani wa asilimia 7 kwa mwaka lakini changamoto kubwa iliyopo ni kuhakikisha kuwa uchumi huo unaonekana katika maisha ya kawaida ya wananchi wake

  “Kila mara utasikia malalamiko ya wananchi kwamba uchumi wetu unakua kwa namba tu hawaoni ni kwa kiasi gani uchumi huo wanauona katika maisha yao ya kawaida kwa hiyo ili uchumi uhesabike kuwa unakua ni lazima uwe jumuishi na ushirikishe watu wengi” alisema Dkt. Mpango

  Amesema kuwa hali hiyo itawezekana ikiwa sekta zinazochangia maendeleo kwa kasi zaidi kama kilimo, uvuvi, biashara ya miamala ya simu, miundombinu na viwanda, zitaimarishwa ili kukuza ajira na kuongeza kipato cha wananchi.

  “Tunataka kilimo kiwe cha kisasa na cha kibiashara kwa kutumia zana na pembejeo bora za kilimo, uongezaji wa thamani ya mazao na kuwa na masoko ya uhakika ili kukuza ajira nyingi hususani kwa vijana” Aliongeza Dkt. Mpango

  Amebainisha kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano mzuri uliopo kati yake na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF na kuwataka watanzania waelewe kuwa mikopo na ruzuku zinazotafutwa na serikali yao ni kwaajili ya kuwaletea maendeleo kwa kuwekeza kwenye miradi yenye tija.
   Wajumbe wa Tanzania waliohudhuria mkutano wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, wakimsikiliza kwa makini Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim (hayupo pichani) wakati Mawaziri wa Fedha na makatibu wakuu (Magavana) kutoka nchi wanachama wa Taasisi hizo kutoka Bara la Afrika, walipokutana kama kamati, Jijini Washington DC, Marekani. 
   Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dotto James, wakifuatilia kwa makini mkutano wa Magavana wa Benki ya Dunia kutoka Barani Afrika uliohudhuriwa na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, Jijini Washington DC, Marekani. 
   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Katibu Mkuu Bw. Dotto James (kulia) wakiandika pointi muhimu wakati Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Yong Kim, alipowahutubia Mawaziri wa Fedha na Makatibu wakuu (Magavana) kutoka nchi za Kiafrika wanaoshiriki Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani-IMF, Jijini Washington DC-Marekani. 
   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Waziri wa Fedha wa Swaziland kushoto kwake walipokuwa kwenye mkutano na  Mkurugenzi Mtendaji Bi. Christine Lagarde Jijini washington DC- Marekani. 
   Wataalamu wa Fedha na Uchumi Kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wakisikiliza kwa makini mkutano wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, ukisimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bi. Christine Lagarde (Hayupo Pichani) ambaye  aliwambukusha wajumbe wanaoziwakilisha nchi zao kuwa umasikini bado ni changamoto kubwa na  unasababisha vikwanzo vingi katika kukuza maendeleo na ustawi wa nchi wanachama, Jijini Washington DC-Marekani.
   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, wakibadilishana mawazo kabla ya kukutana na uongozi wa Juu wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, Kanda ya Afrika, Jijini Washington DC nchini Marekani.
   Waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Kenya Bw. Patrick Ngugi Njoroge alipokutana nae kwenye mikutano ya Benki ya Dunia Jijini Washington DC- Marekani.
   Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akifafanua jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani-IMF, Kanda ya Afrika, Bi. Chileshe Mpundu Kapwepwe Hayupo pichani), Jijini Washington DC-Marekani. Kushoto kwake ni Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Prof. Benno Ndulu akifuatiwa na Naibu Gavana wa Benki hiyo Dkt. Natu Mwamba.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha Duniani –IMF, Kanda ya Afrika Kundi la Kwanza,  Chileshe Mpundu Kapwepwe (katikati), akisisitiza jambo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, alipokutana na Ujumbe huo Ofisini kwake Jijini Washington DC, Marekani.
   Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu (aliyenyoosha mkono) akielezea jambo wakati Ujumbe wa Tanzania Ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, kulia kwake, walipokutana na kufanya mazungumzo na  Mkurugenzi Mtendaji wa IMF Africa Group I Bw. Abebe Aemro Selassie (Hayupo pichani) ambapo Gavana  alieleza kuhusu uchumi wa sasa wa Tanzania pamoja na Hali ya uchumi unavyokua kwa kiasi cha kuridhisha, Jijini Washington Marekani.
   Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Hiroshi (Hiro) Kato, akimwonesha Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, Kitabu Chenye maelezo mbalimbali ya miradi inayotekelezwa nchini Tanzania kwa ufadhili wa shirika hilo, ambapo Japani imeahidi kuendelea kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha kuendeleza miundombinu ya barabara na sekta ya kilimo cha umwagiliaji.
  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James (kushoto) wakimsikiliza kwa makini  Makamu wa Rais wa Shirika la Maendeleo la Japan-JICA, Hiroshi (Hiro) Kato, wakati Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango ulipokutana na Mkurugenzi huyo ambaye ameahidi kuwa Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii, Jijini Washington DC, Marekani.
  (Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango)

  0 0

  Na Hussein Makame, NEC

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema itafikisha Elimu ya Mpiga Kura mpaka katika ngazi ya vijiji ili kuhakikisha wananachi wanaoishi vijijini wanapata elimu hiyo.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC Bw. Kailima Ramadhani wakati akitoa Elimu ya Mpiga kura kupitia kipindi cha Hot Mix cha televisheni ya Afrika Mashariki (EATV) juzi usiku.

  Bw. Kailima alikuwa akijibu swali la mtazamaji wa kipindi hicho aliyetambulika kwa jina moja la Jumanne, aliyeiomba Tume iwe na wafanyakazi wengi kwani Elimu ya Mpiga kura inahitaji kufika hadi vijijini.

  Msikilizaji huyo alisema Elimu hiyo ni muhimu kwani hata mwananchi wa kijijini anaihitaji kwa kuwa anahusika katika kuchagua viongozi kwenye chaguzi mbalimbali nchini.

  Akijibu swali la mtazamaji huyo, Bw. Kailima alisema moja ya mikakati ya NEC kuwafikia wapiga kura kwa sasa, ni kuwatumia wenyeviti wa vijiji na tayari imeshaandika barua Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuiomba iiwezeshe Tume kutekeleza hilo.

  Alisema Tume imeiomba TAMISEMI iipatie ratiba za mikutano ya kamati za halmashauri za mikoa, Wilaya na kamati za maendeleo za kata ambazo wajumbe wake ni wenyeviti wa mikutano mikuu ya vijiji ambao ni wenyeviti wa vijiji.

  “Kamati ya Halmashauri ya mkoa inakusanya watu wengi pale kwenye mkoa, tunataka tukawaelimishe pale.Katika mkutano mkuu wa kijiji mjumbe wake ni kila mwananchi mwenye umri wa miaka 18, kwa hiyo tutafika mpaka kwenye ngazi ile ya chini” alisisitiza Bw. Kailima na kuongoeza kuwa:

  “Tuwaombe tu kwamba wakisikia Tume ipo kwenye mkutano wa kijiji kabla hawajaanza mkutamo wao, basi waje tuwasikilize.Lakini pia tutawafuata viongozi wa dini tuweze kutoa elimu ya mpiga kura”.

  Alibainisha kuwa kupatia viongozi wa dini, Tume itawaomba wanapojumuika kwa ajili ya ibada zao kwenye makanisa au misikiti waialike NEC iwaelimishe waumini wao kuhusu elimu ya mpiga kura.

  “Kwa hiyo tutakwenda katika kila kona taratibu hadi kufikia mwaka 2020, Mungu akituweka hai nchi itabadilika na mwananchi atafahamu utaratibu mzima wa kuandikisha wapiga kura, kupiga kura na shughuli za Tume.” alisema Bw. Kailima.

  Alifafanua kuwa miakakati hiyo ikifanikiwa kutekelezwa itapunguza kwa kiwango kikubwa upotoshaji unaofanywa kuhusu mchakato wa Uchaguzi kwani wananchi watakuwa wanafahamu majukumu ya NEC na majukumu ya kwenye Uchaguzi.

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatekeleza mikakati wa kutoa Elimu ya Mpiga nchi nzima na sasa inashiriki kwenye Wiki ya Vijana, Sherehe za Uzimaji wa Mwenge wa Uhuru na Kumbukumbu ya Kifo cha Mwalimu. Julias Nyerere mkoani Simiyu.

  Hivyo Bw. Kailima aliwataka wananchi wafike kwenye banda la NEC kwenye uwanja wa Halmashauri ya Bariadi zinapofanyika shughuli hizo ili kuapata Elimu ya Mpiga kura inayotolewa.

  0 0  0 0

          Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba akiongea na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na kilimo nchini (FAO) Bwana Fred Kafeero alipomtembelea  WaZIRI Mkamba Ofisini kwake mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam.
   .       Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mbarak Abdulwakil pamoja na Mkurugenz i Msaidizi Idara ya Mazingira toka Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Magdalena Mtenga wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba ( hayupo pichani) alipokuwa akiongea na mWakilishi wa FAO Nchini.
  1.       Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mh. January Makamba akifurahia jambo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na kilimo nchini (FAO) Bwana Fred Kafeero wakati wa mazungumzo juu ya shughuli za mazingira yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

  0 0  0 0

   Imetokea mapema leo mchana maeneo ya Millienium Tower,Kijitonyama jijini Dar.ta  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda, akizindua utafiti huo katika Kituo cha Utafiti cha Makutupora mkoani Dodoma juzi.
   Watafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), na Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi wakiwa tayari kwa upandaji wa mbegu hizo katika Kituo cha Utafiti cha Makutopora mkoani Dodoma.
   Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi, akishiriki kupanda mbegu hizo.
   Mkurugenzi wa Sayansi Hai wa Costech, Dk.Flora Tibazarwa akishiriki katika zoezi hilo la upandaji mbegu hizo.


  Mshauri wa Mradi wa WEMA, Dk. Alois Kullaya  (kushoto) na Meneja mradi huo Mr  Silvester  wakishiriki kwenye upandaji wa mbegu hizo.


   Watafiti wakichoma masalia ya vifungashio vya mbegu za mahindi kama sheria ya GMO inavyoelekeza baada ya zoezi hilo.

  Na Dotto Mwaibale

  KWA mara ya kwanza Tanzania  imeanza kufanya utafiti wa mbegu ya mahindi meupe kwa kutumia teknolojia ya uhandisi jeni (GMO) ambao utachukua takriban miaka mitatu ili kupata matokeo ya mbegu nzuri itakayostahimili mabadiliko ya hali ya hewa ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa wakulima.

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dk. Hassan Mshinda alisema kuanza kwa utafiti huo ni hatua nzuri kwa nchi katika kuinua kilimo nchini.

  Alisema utafiti huo ambao unafanyika katika nchi tano za Afrika, kwa hapa nchini unafanyika katika kituo cha Makutopora mkoani Dodoma na kuwa nchi hizo  nyingine ni Kenya, Uganda, Africa ya Kusini na Msumbiji. 

  Mtafiti na Mshauri wa mradi wa mahindi yanayostahimili ukame ( WEMA) Dk. Alois Kullaya, alisema Tanzania ilikuwa ikifanya tafiti katika hatua ya maabara, na sasa kwa mara ya kwanza wapanda kwenye mazingira halisia. " Ni kweli tarehe tano ya mwezi huu, tulipanda mahindi meupe katika hatua ya utafiti kwenye mazingira. Tunataka tujiridhishe na uwezo wa mahindi hayo katika kustahimili ukame". Matokeo ya utafiti huu, utatoa nafasi kwetu kama watafiti na viongozi wetu kufanya maamuzi yenye tija kwa taifa badala ya kuwa watazamaji na kushambikia marumbano tusiyofahamu chanzo chake" alisema Kullaya.

  Mtafiti Kiongozi wa masuala ya bioteknolojia kutoka Costech Dk. Nicholas Nyange aliishukuru serikali kwa kuruhusu watafiti wake kuweza kufanya majaribio ya uhandisi jeni hapa nchi. Hii ni hatua nzuri katika nchi yoyote inayoamini katika maendeleo ya sayansi na teknolojia. 
  "Tumekuwa tukitishiwa kama watoto  Usiguse GMO utakufa, wakati nchi nyingine wanazalisha nakufanya biashara. Tunafanya biashara kubwa na India, China, Marekani na Afrika ya Kusini, na hawa wote wanatumia teknolojia ya uhandisi jeni". 

   "Tufanye utafiti, tuone kama tutakufa kweli au tutatoka kimasomaso" aliongeza Nyange kwa tabasamu. 

  Itakumbukwa kuwa Mradi wa WEMA hadi sasa  umezalisha mbegu 11 za mahindi kwa njia za kawaida. Na baadhi ya mbegu hizo zimeingia sokoni mwaka huu kwa bei ya kawaida. Hivyo, uzalishaji wa Mahindi ya GMO itakuwa ni hatua mbele katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi. 

older | 1 | .... | 1002 | 1003 | (Page 1004) | 1005 | 1006 | .... | 1898 | newer