Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 998 | 999 | (Page 1000) | 1001 | 1002 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu misaada iliyotolewa na Bohari ya Madawa (MSD) waliotoa Dawa na Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 30.
  c4
  Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu mashuka 250 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
  c1
  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akitoa taarifa kwa Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kuhusu hatua iliyofikiwa na serikali katika kurejesha hali baada ya tetemeko lilitokea mkoani humo ambapo pia alimshukukuru Waziri Ummy kwa Misaada aliyoitoa wakati wanakabiliana na maafa ikiwemo, Madawa, Vifaa tiba na madktari iliyowezesha kusaidia kwa kiasi kikubwa waathirika wa tetemeko.
  c2
  Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiongea na Mkuu wa Mkoa wa Kagera na kuipongeza kamati ya mkoa kwa namna walivyojipanga kukabiliana na athari za tetemeko pamoja na kuwahudumia waathirika.


  0 0

  Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Mhe. Chum Kombo Khamis akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Makumbusho ya watu wa zamani yaliopo Kuumbi Jambiani, Mkoa Kusini Unguja.

  Baadhi ya wananchi na wafanyakazi wa Idara ya Makumbusho na Mambo ya Kale walioshiriki
  ufunguzi wa Makumbusho ya Watu wa zamani Kuumbi wakifuatilia sherehe hizo.

  Mtafiti wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Professa Felix Chami kwanza (kulia) akitoa maelezo
  juu ya utafiti uliofanywa na kupelekea kuanzishwa kwa makumbusho ya Kuumbi Jambiani.

  Mkuu wa Divisheni ya Mambo ya Kale Zanzibar Abdallah Khamis Ali akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Habari, Utalii Utamaduni na Michezo Chum Kombo Khamis wa kwanza (kushoto) wakati wa ufunguzi wa makumbusho ya Kuumbi.

  Naibu Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Chum Kombo Khamis akizungumza na wananchi na wafanyakazi wa Idara ya Makumbusho wakati wa ufunguzi wa Makumbusho ya Kuumbi, Jambiani Mkoa Kusini Unguja.  Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar

  0 0

  Wafanyakazi wa Benki ya CRDB na viongozi na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu wakifurahia jambo baada ya benki hiyo kukabidhi madawati 200 katika wiki ya huduma kwa wateja, kupitia kauli mbiu ya tunakusikiliza karibu tukuhudumie.  Meneja wa CRDB Tawi la Babati Mkoani Manyara, Ronald Paul (kushoto) na Mkurugenzi wa mji wa Mbulu Anna Mbogo wakiwa kwenye moja kati ya madawati 200 yaliyotolewa na benki hiyo katika sherehe za wiki ya huduma kwa wateja.  Wafanyakazi wa benki ya CRDB na wanafunzi wa shule ya Imboru ya Halmashauri ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara, wakishangilia baada ya benki hiyo kukabidhi madawati 200 kwenye halmashauri hiyo.

  HALMASHAURI ya Mji wa Mbulu Mkoani Manyara, imekabidhiwa msaada wa madawati 200 na Benki ya CRDB kwa ajili ya kutumiwa na wanafunzi wa shule tano za msingi, ambapo kila shule itapatiwa madawati 40.

  Meneja wa CRDB Tawi la Babati, Ronald Paul akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo 200 alisema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja wamejitolea msaada huo kama mchango wao kwa jamii.

  Paul alisema benki hiyo ya CRDB imetoa madawati hayo 200 ambayo yatagawanywa kwa wanafunzi wa shule tano za halmashauri ya mji wa Mbulu, ambapo kila moja ya shule hizo zitatolewa madawati 40.

  “Tukiwa kwenye wiki ya huduma kwa wateja tunahakikisha tunarudisha kile kidogo tunachopata kupitia jamii, sisi tutaendelea kutoa mchango wetu kwa jamii ili kuhakikisha tunaunga mkono suala zima la maendeleo,” alisema Paul.

  Alisema kwa muda wa miaka miwili tangu CRDB ianze kutoa huduma zake katika mkoa wa Manyara, wananchi wa mji wa Mbulu wamechangamkia fursa ya uwepo wao, kwa kuweka fedha, kutoa na kuchukua mikopo ya benki hiyo.

  Mkurugenzi wa mji wa Mbulu Anna Mbogo akizungumza wakati akipokea madawati hayo aliushukuru uongozi wa CRDB kwa kutoa msaada huo kwani utawasaidia wanafunzi wa shule hizo kusoma kwa ufasaha.

  Mbogo alisema awali walikuwa na upungufu wa madawati 3,179 ila walijitahidi na kuhakikisha madawati hayo yanapatikana na hadi sasa wana madawati 999 ya ziada ambayo yamehifadhiwa kwa ajili ya kutumika baadaye.

  Alitoa ombi kwa CRDB kuendelea kutoa msaada wa miundombinu ya shule za eneo hilo kwani hivi sasa wana mpango wa kujenga madarasa mengine ya shule ya msingi Imboru, yenye madarasa mawili pekee.

  “Awali wanafunzi wa shule hii walikuwa wanatembea umbali mrefu wa kilometa tatu kutoka nyumbani hadi shuleni kila siku hivyo ili kukomesha hali hiyo kwa watoto hawa wadogo ndipo tukaamua kuijenga,” alisema Mbogo.

  Alisema lengo lao ni kuhakikisha wanaendelea kuiboresha shule hiyo mpya kwa kujenga madarasa mengine zaidi ili baada kwani hivi sasa wanafunzi hao wanapata elimu kwa urahisi kwa sababu ipo karibu na makazi yao.

  0 0

  Jumapili Oktoba 09, 2016 katika Kanisa la "EAGT Lumala Mpya International Church" Sabasaba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza, linatarajiwa kufanyika tamasha kubwa la Kusifu na Kuabudu.

  Mchungaji Kiongozi wa Kanisa hilo, Dkt.Daniel Moses Kulola, amewahisi watu wote kufika kwenye tamasha hilo kwani kwenye kusifu na kuabudu, ana uhakika wa kuisikia sauti ya Mungu na huwa huru na kujitenga na dhambi ikizingatiwa kwamba kuna nguvu ya Mungu kwenye kusifu na kuabudu.

  Mratibu wa tamasha hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Vijana, Max Kemmy, amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake na kwamba litaanza kuanzia majira ya saa nane kamili mchana likiwa na ujumbe usemao, "Njoo Tuabudu Pamoja".

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wajumbe katika Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), lililofanyika mkoani Dodoma.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Saba la Wafanyakazi akitoa taarifa ya utendaji kazi wa Wakala huo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani). Baraza hilo limefanyika mkoani Dodoma.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika Baraza hilo.
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (kushoto) akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa katika Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala huo lililofanyika mkoani Dodoma.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS).
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza mmoja wa wajumbe waliohudhuria katika Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), mkoani Dodoma.  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameuagiza Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kuboresha Idara ya Mipango na Usanifu katika wakala huo ili kupata matokeo mazuri katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.

  Prof. Mbarawa ameutaka wakala huo kuboresha kanuni zinazosimamia aina ya vyombo vya moto vinavyotumia barabara zote nchini ikiwemo ili kuweza kusaidia miundombinu hiyo kudumu muda mrefu.

  Akizungumza mkoani Dodoma katika ufunguzi wa Baraza la Saba la Wafanyakazi wa Wakala huo Prof. Mbarawa amesema kuwa wakala unabidi uanze kubadili aina ya mfumo wa usanifu uliokuwa ukitumika awali na badala yake utumike usanifu wa kisasa unaoendana na mahitaji halisi ya watumiaji wa barabara hizo.

  “Kama mnaona kuna mabadiliko yoyote mnayohitaji kuyafanya ili barabara zetu zidumu, boresheni kanuni na mlete kwangu ili nizifanyie kazi”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Ameongeza kuwa katika kuboresha utendaji katika wakala huo, Serikali ina mpango wa kuwapa fursa za ajira wahandisi hususani wanawake ili na kuwajengea uwezo na kuweka uwiano katika taalamu hiyo.

  Aidha Waziri Prof. Mbarawa ameahidi kuongeza fedha za uendeshaji kwa wakala huo ili kuuwezesha kutekeleza miradi mbalimbali inayoendelea nchini.

  “Kumbukeni majukumu ya Wakala yameongezeka sasa hamtajenga barabara pekee, mmeongezewa jukumu la kujenga miundombinu ya viwanja vya ndege hivyo ni muhimu kujipanga kutekeleza kazi hii”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

  Naye, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng. Patrick Mfugale ameahidi kushughulikia ujenzi wa viwanja vya ndege ikiwemo kufanya kazi kwa weledi na uadilifu kama ambavyo wakala huo unatekeleza miradi yake ya barabara.

  Ameongeza kuwa Wakala unaendelea kufanya kazi na Makandarasi wenye uwezo na wanaozingatia thamani ya fedha katika miradi yote inayotekelezwa nchini.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya TANROADS, Eng. Hawa Mmanga amemuahidi Waziri Prof. Mbarawa kufanya kazi kwa uadilifu, bidii, na kuzingatia thamani ya fedha katika miradi yote inayotekelezwa na wakala.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0


   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akimfariji Said Ally, ambaye ametobolewa machomara baada ya kumaliza mazungumzo na waandish wa Habari
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akipewa mkono wa shukurani na Said Ally, ambaye ametobolewa macho hivi karibuni na mtuhumiwa ambaye tayari amekwishakamatwa,picha kati  Mkewe Zara Sudi mara baada ya kumaliza mazungumzo na waandish wa Habari

  Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii

  Siku chache mara baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa koasa la kumtoboa macho ndugu Said Ally wa Buguruni kwa Mnyamani mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda ameamua kuendelea kumsaidia kijana huyo katika hatua zake zote za matibabu na mtaji wa Shilingi Milioni kumi.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kijana huyo kufika katika ofis za mkoa , Makonda alisema kuwa mara baada ya kufanyika uchunguzi na madaktari Bingwa wa Muhimbili imeonekana kuwa bado Said hataweza kupata nafasi ya kuona,hivyo anahitaji matibabu ya ziada.

  “Serikali ya mkoa imetoa gari ambayo atatumia kwa kipindi chote akiwa anaenda kupatiwa matibabu na shughuli zingine ambazo atakuwa anafanya mpaka hapo atakapokuwa sawa”alisema Makonda.

  Kwa upande Ndugu Said Ally amesema kuwa anawashukuru madaktari kwa juhudi zote walizofanya na shukrani kubwa sana ziende kwa Gea Habibu wa Clouds Media na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa moyo wake aliounyesha kwa kujitoa kwa hali na mali.

  “Kiukweli nimeona Mungu akiwa katika upande wangu kwa msaada ninaondelea kupata kutoka kwa mkuu wa Mkoa na watu wa Clouds na madakatari naomba mungu aweze kuwapa maisha marefu” alisema Said.

  Makonda alimaliza kwa kusema kuwa Serikali ya mkoa inandaa utaratibu kwa ajili ya watu wengine ambao wanahitaji kujitolea kumsaidia Said hivyo jumatatu atatangaza rasmi.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania, (TANESCO), Felchesmi Mramba, (kushoto), akibadilishana hati za mkabata na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton baada ya kusini, mradi wa ujenzi wa njia ya umeme (transmission line) itakayounganisha Tanzania na Kenya, makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2016. Shirika hilo limeingia mkataba na makampuni matatu kutekeleza mradi huo (KTPIP), wa Msongo wa KV400 unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya dola za Kimarekani
  309.26
   NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
  SHIRIKA la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), limesaini mkataba na makampuni matatu kujenga njia ya umeme, (Transmission lines), wa Msongo wa Kilovolti 400 utakaounganisha Tanzania na Kenya.

  Hafla ya kutiliana saini mikataba hiyo, imefanyika leo Oktoba 7, 2016 makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, ambapo Shirika hilo la Umeme linalomilikiwa na serikali, limetiliana saini mikataba hiyo na makampuni ya Bouygues Energies Service, Energoinvest na Kalpa-Taru.Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Felchesmi Mramba, alisema, Ujenzi wa Mradi huu wenye urefu wa Kilomita 414, utaanzia Mkoani Singida,-Babati-Arusha hadi Namanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.

  Kisha Mradi utaunganishwa na njia ya Msongo wa Kilovolti 400 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka eneo la Isinya, Nairobi, nchini Kenya hadi eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya, (Namanga) ambapo utaunganisha na njia ya umeme wa wa Msongo wa Kilovolti 400kv kwa upande wa Tanzania.
  Napana niwahakikishie, kuwa huu ni mfululizo wa miradi mikubwa inayotekelezwa na TANESCO na utawezesha usafirishaji wa umeme wa Mgawati 2000 katika pande zotekenya na Tanzania”. Alifafanua Mramba.
  Akifafanua zaidi, Mhandisi Mramba alsiema, utekelezaji wa mradi huu unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB), na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya Dola za Kimarekani, Milioni 309.26 utakamilika katika kipindi cha miezi 24, sawa na miaka 2.

  “Dola za Marekani Milioni 258.82, zitatumika kujenga upande wa Tanzania na  Dola za Kimarekani Milioni 50.45 zitatumika kujenga mradi upande wa Kenya,” alifafanua Mhandisi Mramba. Hata hivyo Mkurugenzi huyo Mtendaji alitoa onyo kwa wakandarasi waliopewa kazi hiyo kuitekeleza kwa wakati kwa mujibu wa mkataba. “Angalizo, kwenu ninyi wakandarasi, kamilishini mradi ndani ya muda kama ambavyo tumekubaliana kwenye mkataba, kushindwa kukamilisha ujenzi kwa mujibu wa mkataba ni kushindwa kufanya kazi na sisi kama TANESCO hatutakubaliana na hilo.”Alionya Mhandisi Mramba. 

  Naye mwakilishi Mkazi wa (AfDB), Tonia Kandiero, alitoa hakikisho kuwa benki hiyo itaendelea kusaidia miradi mikubwa kama hii, kwa manufaa ya eneo lote la Afrika. Kwa upande wake, MAfisa Miradi msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, naye aliungana na AfDB, kutoa hakikisho la ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na JICA, katika kusaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kama huu uliosainiwa leo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton wakisaini mkataba huo
   Mhandisi Mramba, (kushoto), na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, wakisaini mkataba
   Mhandisi Mramba, akibadilishana hati na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, baada ya kusaini mkataba
   Mhandisi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakisaini mkataba kutekeleza mradi huo
   Mhandisi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakibadilishana hati
   Mkurugenzi Mkazi wa AfDB nchini, Tonia Kandiero, akizungumza kwenye hafla hiyo
   Mhandisi Mramba, (kulia) na Kandiero, wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo
   Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Bibi. Kandiero
   Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, (kushoto), akizungumza
  Mhandisi Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Bi. Rosina wa JICA
   Mhandisi Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, akizungumza kwenye hafla hiyo
   Mratibu wa Miradi wa Shirika la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Khalid James, (kulia), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba.
   Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Mramba, (wasaba kushoto), akipongezwa na Mwakilishi mkazi wa AfDB, hapa nchini, Tonia Kandiero, wakati wa picha ya pamoja na wawakilishi wa makampuni yaliyopata kandarasi ya ujenzi wa mradi huo
   Kutoka kushoto, Patrick Canton, S.K. Sarotra, Apolei Rosina, Mhandisi Mramba, Tonia Kandiero na Bisera Hadzialjevic, wakiwa katika picha ya pamoja mwishoni mwa hafla hiyo
   Afisa Mawasiliano na Uhusiano wa TANESCO, Henry Kilasila, (kualia), akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Felchesmi Mramba.
   Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, (Uwekezaji), Mhandisi Decklan P.Mhaiki, akiwakaribisha wageni kwenye hafla hiyo.
  Meneja mradi huo wa KTPIP, Mhandisi Mhandisi Lewanga Tesha, (kulia), akiwa na wawakilishi wa kampuni ya KALPA-TARU

  0 0


       Bodi ya Filamu Tanzania leo imemkabidhi cheti na hundi yenye thamani ya shilingi Laki Mbili mwanafunzi Omary Maganga aliyefanya vizuri kwenye masomo ya filamu na runinga kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA).

       Makabidhiano hayo yamefanyika kwenye ofisi za bodi hiyo ambapo Afisa Uhusiano na Mawasiliano Abuu Kimario alimkabidhi cheti hicho na hundi kwa niaba ya Katibu Mtendaji Joyce fisoo.

       Baada ya kukabidhiwa zawadi zake bwana Maganga aliishukuru Bodi hiyo ya filamu kwa kutambua juhudi za wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo yao. Pia ameziasa taasisi zingine za Serikali na zisizo za kiserikali kuwatambua wanafunzi wanaofanya vizuri kwani kwa kufanya hivyo kunaongeza morali na ushindani.

       Wakati huo Afisa Uhusiano na Mawasiliano Abuu Kimario kwa niaba ya Katibu Mtendaji wa bodi hiyo ametoa ahadi ya kuendelea kutoa zawadi kwa wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo yenye uhusiano na tasnia ya filamu.

  Kwa sasa Bodi ya Filamu Tanzania iko kwenye utekelezaji wa programu ya kutambua na kukuza vipaji vya wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo ya tasnia ya filamu nchini. Program hii ilianzishwa ikiwa na lengo la kukuza ubora wa filamu za Kitanzania.

  0 0  0 0

  Na Eleuteri Mangi-MAELEZO

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu ameahidi kutuma timu ya wataalam kutoka Idara ya Magonjwa ya Mlipuko ili kuja kushirikiana na timu ya Mkoa ili kufanya tathmini ili kuweza kuepusha magonjwa ya mlipuko hasa katika kipindi hichi ambacho mvua zimeanza kunyesha mkoani humo.

  Akiongea wakati akikabidhi misaada kwa mkoa wa kagera Meja jenerali Mstaafu Salum Kijuu Waziri Ummy amesema anatambua kipindi hiki cha mvua huwa ni tishio kwa magonjwa ya mlipuko hivyo wizara itachukua hatua ya kutuma wataalam pamoja na kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga na magonjwa hayo.

  “Nafahamu tuko kwenye kipindi cha mvua nyingi ambacho mara nyingi magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu huibuka, hivyo kabla ya hayo kutokea kama tahadhari sisi kama wizara tutatuma wataalam kuja kufanya tathmini na kutoa elimu ya namna ya kujikinga” Alisema Waziri Ummy.

  Aidha Waziri Ummy amekabidhi misaada ya Dawa na Vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 30 vilivyotolewa na Bohari kuu ya Dawa (MSD) kwa mkuu wa mkoa wa kagera Meja jenerali Mstaafu Salum Kijuu kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko mkoani humo.

  Pia Waziri Ummy amekabidhi mashuka 250 yaliyotolewa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa ajili ya Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati mkoani kagera.

  Akiwa katika ziara kutembelea maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi Waziri Ummy amewataka watumishi katika sekta ya afya mkoani humo kuweka mkakati wa kuweka mazingira safi kwenye maeneo yote yaliyoathiriwa na tetemeko

  Wakati huo huo Waziri Ummy ametembelea Kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Kiilima kilichopo katika Halmashauri ya Bukoba na kuagiza wazee hao kupatiwa chakula cha milo mitatu ili kulinda afya zao.

  Akizungumza baada ya kupokea misaada hiyo mkuu wa mkoa wa kagera Meja jenerali Mstaafu Salum Kijuu amewaomba wadau wengine kuendelea kutoa misaada kwa ajili ya kurejesha hali baada ya maafa kutokea.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji  wa Hakielimu,John Kalage, akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya hatua zilizo chukuliwa na Serikali kwa Walimu wa Mbeya Day.

  Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii

  Tasisi isiyo ya kiserikali inayosimamia mwenendo wa Elimu hapa nchini ya Hakielimu imeipongeza Serikali kwa hatua za kinidhamu zilichokuliwa kwa wale wote waliohusika kutoa adhabu ya kikatili kwa mwanafunzi wa kidato cha 3 ,Sebastian Chinguku wa shule ya sekondari ya Mbeya day.

  Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini dare s Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa wa tasisi hiyo, John Kalage amesema kuwa wamepokea taharifa hiyo kwa masikitiko makubwa sana mara baada ya kuona ukatili uliopotiliza.

  “tunaipongeza Serikali kwa kuchukua hatua za awali zikiwemo kuliagiza jeshi la polisi nchini kuchukua hatua za haraka dhidi ya walimu waliohusika katika tukio hili. Aidha tunampongeza Mwalimu aliyethubutu kukemea na kufichua ukatili huu uliopotiliza hivyo tunaomba mamlaka husika zichukue hatua madhubuti za kulinda uhai hata ajira ya mwalimu huyu jasiri” amesema Kalage.

  Ameongeza kuwa Haki elimu inaitaka Serikali kuhakikisha suala hili linashughulikiwa kwa uapana wake na kuendelea kuitaharifu jamii juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya walimu waliohusika na ukatili huu.

  Alimaliza kwa kusema kuwa licha ya tukio la Mbeya linaonekana kuchukua mjadala mpana hapa nchini kwa sasa, tunapenda kuitaharifu serikali kuwa matukio ya ukatili dhidi ya watoto wa mwaka 2011 imeonesha kuwa kuna ukatili wa kutisha sana kwa watoto katika shule nyingi hapa nchini vikiwemo vya kimwili na kingono.

  Aliweka wazi kuwa adhabu kama hizi zinapotolewa kwa watoto, husababisha wato kutafuta namna ya kukwepa adhabu hiyoo na kupelekea kukimbia masomo yao na hatimaye kuacha shule kabisa.

  0 0

  Dar es Salaam.

  Wadadisi au wakusanyaji taarifa za kitakwimu rasmi katika tafiti mbalimbali zinazoratibiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wametakiwa kuwa wamehitimu Mafunzo ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi angalau kwa ngazi ya cheti.

  Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa imesema matakwa hayo ni kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Na. 9 ya mwaka 2015 inayoipa mamlaka ofisi hiyo ya kuratibu na kusimamia ukusanyaji wa Takwimu rasmi nchini.

  Taarifa hiyo imefafanua kuwa utumiaji wa wadadisi ambao wamepitia mafunzo ya ukusanyaji takwimu angalau kwa ngazi ya cheti kutasaidia kuboresha zaidi upatikanaji wa takwimu rasmi nchini. 

  Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa Mafunzo ya Ukusanyaji Takwimu Rasmi yanatolewa na Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika "Eastern Africa Statistical Training Centre (EASTC) kilichopo Changanyikeni jijini Dar es Salaam.

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu ina jukumu la kukusanya, kuchambua na kusambaza Takwimu Rasmi Nchini kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015.

  0 0

   Jaji Mkuu wa  Australia  ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kushoto), akipokea zawadi  ya picha  kutoka kwa  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) katika halfla fupi iliyofanyika  leo  tarehe 7.10 .2016 kwenye ukumbi wa maktaba wa   Mahakama  ya Rufani  ya Tanzania .


   Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto)akizungumza  na Jaji Mkuu wa  Australia  ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis(katikati) na (kulia) ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,Bi.  Katarina  Revocati katika mkutano  huo ulifanyika leo tarehe 7.10 .2016 kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Katiba  na Sheria uliopo jijini Dar es Salaam.
   Jaji Mkuu wa  Australia  ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis (kulia) akizungumza kuhusu ziara yake ya siku tatu aliyoifanya nchini na kubadilishana uzoefu wa masuala mbalimbali ya mafunzo, sheria na shughuli za kimahakama baina ya nchi hizo mbili. (Kushoto) ni Waziri wa Katiba na Sheria,Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe. Mkutano  huo ulifanyika leo tarehe  7.10.2016 kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Katiba  na Sheria uliopo jijini Dar es Salaam.
  Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini, Mhe. Christopher Kourakis akiangalia na kupata  maelezo juu  ya mfumo wa kielektroniki wa kusajili  mashauri kutoka kwa Karani wa Mahakama ya Hakimu  Mkazi  Kisutu, iliyopo jijini Dar es Salaam Bw. Abdalla Bugalo wakati alipoitembelea leo tarehe 7.10 .2016  .PICHA NA MAHAKAMA YA TANZANIA

  0 0

   .Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo akizungumza na viongozi mbalimbali wa NHIF kuhusu kujifunza kutokana na uzoefu wa kuendesha Mfuko wa bima ya afya, katika ziara ya mafunzo makao makuu ya NHIF leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu).
   Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) akitoa maelezo mafupi kuhusu shughuli za Mfuko huo, leo kwenye makao makuu ya ofisi za mfuko huo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo.
    Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga akitoa maelezo mafupi kuhusu shughuli za Mfuko huo leo  kwenye makao makuu ya ofisi za mfuko huo jijini Dar es Salaam.. Kulia ni Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo.
   Meneja Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Elentruda Mbodoro akitoa walezo mafupi kwa Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo kuhusu utunzaji wa nyaraka za wanacha wa mfuko huo leo jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) leo alipo tembelea Makao makuu ya mfuko huo.
  Waziri wa Afya wa Zanzibar Mh.Mahamud Thabit Kombo akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa NHIF leo makao makuu ya ofisi hizo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umepokea ugeni kutoka Wizara ya Afya ya Zanzibar katika ziara ya mafunzo iliyoongozwa na Mh.Mahamud Thabit Kombo ambaye ni Waziri wa Afya wa Zanzibar.

  Katika ziara hiyo, yenye lengo la kushiriki uzoefu wa utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo, Waziri na timu yake walipata melezo na kujionea shughuli mbalimbali za Mfuko huo.

  Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mh.Kombo alisema "tunahitaji kujifunza kutokana na uzoefu wenu wa kuendasha Mfuko wa bima ya afya, hatukuona haja ya kwenda mbali kwani tuna kaka na dada zetu hapa karibu na wana uzoefu wa kutosha".

  Mh. Kombo alisema kuwa Wizara ya Afya ya Zanzibar ina ushirikiano mkubwa sana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto na kusisitiza kuwa Wizara hizi zinafanya kazi kwa karibu sana na hii inasaidia kufanikisha maendeleo ya sekta ya afya kwa pande zote.

  Akiwakilisha mada ya Utekelezaji wa shughuli za Mfuko,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga aliongelea umuhimu wa Bima ya Afya katika maendelea ya sekta ya afya nchini na kuanisha utekelezaji wa majukumu ya Mfuko huo ambapo alielezea pia mifumo imara ya uendeshaji wa Mfuko ikiwemo ya Tehama lakini pia mifumo ya kubaini udanganyifu ili kuudhibiti.

  Naye Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF, Bi. Anne Makinda (Spika Mstaafu) lielezea umuhimu wa Mfuko kujipanga kimuuondo katika kuhakikisha unaweza kufikia azma ya Serikali ya kuhakikisha afya bora kwa wote. "Pamoja na mambo mengine, elimu kwa umma ni suala la msingi sana katika utekelezaji wa shughuli za Mfuko na kuwapa nafasi wadau kuuliza na kujibiwa hoja zao"alisema.

  Akitoa shukrani zake kwa NHIF katika ziara hiyo ambayo pia ilihudhuriwa na Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari, Waziri Kombo alishukuru Mfuko na kusema kwamba utabakia kwenye historia ya maendeleo ya sekta ya afya Zanzibar lakini pia alisisitiza umuhimu wa kuwa na bima ya afya kwa kusema "Bima ya afya ni Mkombozi wa wanyonge" .

  0 0


  Kijana Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu Henjelewe maarufu kama Scorpion (katikati), akisaidiwa na ndugu zake wakati akiingia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda kuzungumza na waandishi wa habari.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya kumpa fursa kijana Said kuzungumza na wanahabari.
    Kijana Said Mrisho (kulia), akizungumza na wanahabari. Kulia kwake ni mke wake Stara Soud.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akiwa ameinama kwa uchungu wakati kijana huyo alipokuwa akizungumza na wanahabari.
   Kijana Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu Henjelewe maarufu kama Scorpion (kulia), akilia kwa uchungu wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo. Kushoto ni mke wake, Stara Soud
   Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magembe (kushoto), akimfariji kijana Said Mrisho.
   Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akimfariji kijana Said Mrisho.
   Mama yake Said Mrisho, Halima Lwiza Abdallah  akilia.
   Ndugu zake Said Mrisho wakitoka ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es Salaam baada ya kuzungumza na wanahabari. Kushoto mbele ni mama yake Said, Halima Lwiza Abdallah  na kulia ni mke wake, Stara Soud.
  Said Mrisho akisaidiwa kushuka ngazi wakati akitoka kuzungumza na wanahabari ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
  …………………………………………………………………………..
  Na Dotto Mwaibale
   
  MAJONZI na vilio vilitawala ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati Kijna Said Mrisho anayedaiwa kujeruhiwa na kutobolewa macho na Salumu Henjelewe maarufu kama Scorpion Buguruni Sheli alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mbele ya mkuu wa mkoa Dar es Salaam leo asubuhi kuwa hata ona tena katika maisha yake kufuatia kujeruhiwa vibaya kwenye mishipa ya macho na mtuhumiwa huyo na kupoteza uwezekano wa kuona.
   
  “Nilijua ipo siku moja nitakufa lakini sikutegemea kuwa nitakuja kutolewa macho yangu kikatili kiasi hiki sijui mungu anampango gani na mimi wala sijui nini ya hatima ya maisha yangu” alisema Mrisho ambapo ukumbi mzima uligubikwa na ukimya sanjari  simanzi huku mke wake Stara Soud akishindwa kujizuia kulia.
   
  Mrisho alisema anamshukuru sana Rais John Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa jitihada walizofanya za kumsaidia kupata matibabu lakini imeshindika kwa kuwa mishipa yote yenye uwezo wa kumfanya aweze kuona imeharibiwa vibaya na mtuhumiwa huyo hivyo ataweza kuona tena katika maisha yake.
   
  “Iwapo kama mishipa isingeharibiwa kwa visu mama yangu kipenzi Halima Lwiza Abdallah alikuwa yupo tayari kutoa jicho lake moja kwa ajili ya kunisaidia niweze kuona lakini kwa bahati mbaya hilo halitawezekana baada ya madaktari kunieleza kuwa mishipa ya macho yangu imeharibiwa” alisema Mrisho kwa huzuni na kuanza kulia.
   
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wamepokea kwa huzuni taarifa hiyo ya madaktari na kumuomba Mrisho asikate tamaa kwani serikali itaangalia jinsi ya kumsaidia.
   
  Makonda alisema serikali itatoa sh.milioni 10 kama mtaji ili ziweze  kumsaidia wakati wakiangalia namna ya kuwashirikisha watu wengine kwa ajili ya kumsaidia.
   
  Makonda alisema serikali itamsaidia kufanyiwa upasuaji wa kuwekewa macho ya bandia ili awe katika mwonekano wa kawaida ingawa hatakuwa haoni.
   
  “Pamoja na kumpatia kiasi hicho cha fedha katika kipindi hiki cha mpito ambacho atakuwa akihitaji kwenda katika matibabu na sehemu zingine tutakuwa tukimsaidia usafari wa kwenda maeneo hayo” alisema Makonda.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akiongea na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2016
   
   Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe Jack Mugendi Zoka akichangia mada wakati wa mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na  Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe Jack Mugendi Zoka baada ya kuongea na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2016
   ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kanda na Kimataifa, Balozi  Dkt. Augustine Mahiga na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hamisi Kigwangwalla katika picha ya kumbukumbu   na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2016.PICHA NA IKULU


  0 0

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (katikati) alipofanya ziara ya kukagua mazingira katika kiwanda cha kutengeneza viroba vya mifuko Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina (kushoto) mara baada ya kuwasili na kutembelea kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga cha Murzer kilichopo jijini Dar e s salaam.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akikagua sehemu ya kuyeyushia viroba ya mifuko katika kiwanda cha Unberg International kilichopo jijini Dar es salaam mapema hii leo.

  ………………………………………………………

  Kiwanda cha kutengeneza mifuko maarufu kama viroba cha UNBERG INTERNATIONAL cha jijini Dar es Salaam kinachomilikiwa na Raia wa China kilichopo katika eneo la viwanda Mandela Road jijini Dar es salaam, kimetozwa faini ya shilingi milioni ishirini na tano kwa kukiuka vibaya sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake.

  Kiwanda ambacho kilikuwa hata hakijulikani kinachotengeneza mifuko itumikayo kufungia bidhaa mbali mbali kama sabuni, saruji na sukari, kimeonekana kufanya kazi ya uzalishaji katika mazingira hatarishi kwa wafanyakazi kiwandani hapo pamoja na mazingira.

  Hayo yamebainika katika siku ya pili ya hitimisho ya ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpiga alipokua akikagua baadhi ya Mazingira ya jiji la Dar es Salaam na viwanda, ndipo alipoingia kiwandani hapo kwa kushtukiza na kujionea namna ambapo raia hao wa China wanavyotiririsha uchafu wa kinyesi cha binadamu katika mto msimbazi.

  Naibu Waziri Mpina alisema, “Tunawapenda na kuwajali wawekezaji ila kwa Uchafuzi huu mnaoufanya hapa hata kama ingekuwa nchini kwenu hii isinge ruhusiwa, nilitaka kiwanda hiki kifungwe kabisa lakini lazima taratibu za kisheria zifuatwe. Kiwanda hakina hata cheti kimoja kinachowaruhsu kuanya kazi hizi” Alisisitiza Mpina. Pamoja na uchafu wa maji baada ya kuswafisha malighafi ya mifuko hiyo kiwandani hapo ambayo nimifuko ya bidhaa mbali mbali ikirejelezwa bila kujali wala kutibu maji na kuyaachia katika mazingira.

  Akitaja adhabu katika kiwanda hicho mratibu wa kanda ya mashariki kutoka baraza la taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC Bw. Jafari Chimgege, amesema kuwa kiwanda kinatakiwa ,kulipa faini hiyo ndani ya siku saba na kuacha kutiririsha maji pamoja na kurekebisha wa usafishaji viroba kiwandani hapo, kupata cheti chatathmini ya athari za mazingira pamoja na vibali vingine vya uwekezaji nchini.

  Kwa upande wake mtaalam wa maji Ardhini kutoka bonde la Wami Ruvu Bw. Msuda,amewataka wawekezaji na wenye viwanda nchini kufika katika ofisi za Bonde zilikzopo Ubungo maji jijini Dar es Salaam ili waweze kufanya mchakato wa kupata vibali na vyeti vya kutiirisha maji machafu yaliyotibiwa kwa njia sahihi.

  Naibu waziri mpina amehitimisha ziara yae ya siku mbili jijini Dar es salaam ya kukagua baadhi ya viwanda na mazingira.

  0 0

  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha hotuba kuhusu ni jinsi gani Tanzania imejipanga kukabiliana na tatizo la utapiamlo na udumavu wa akili kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano, alipomuwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Jijini Washington DC, Marekani.
  Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akimpogeza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, baada ya kuwasilisha hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika mkutano huo kuhusu watoto kupata lishe bora wakati wa kuzaliwa na kusisitiza wakinamama wanyonyeshe watoto ipasavyo ili kuondokana na tatizo kubwa la utapiamlo ambalo mara nyingi huwakumba watoto wanapokuwa wadogo na kusababisha kupoteza nguvu kazi ya Taifa, Jijini Washington DC.
  Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim akiwa na Mawaziri wa Fedha wa Afrika akiwemo na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philiph Mpango(wa nne kutoka kulia),Jijini Washington DC.


  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, wa kwanza kushoto akisikiliza kwa makini hotuba ya Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, katika mkutano uliowahusisha Mawaziri wa Fedha kutoka nchi kadhaa duniani kama vile Cameroon, Ethiophia, Senegal na Indonesia ambapo rais huyo aliwataka mawaziri hao wasimamie rasilimali fedha vizuri hasa katika suala la kukabiliana na changamoto ya utapiamlo na udumavu wa akili kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano, mkutano uliofanyika Jijini Washington DC, Marekani.
   
  Benny Mwaipaja, MoFP 
  Washington DC 
  7.10.2016 

  MAKAMU wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameitaka Benki ya Dunia na wadau wengine wa maendeleo kuwekeza kiasi kikubwa cha fedha ili kutatua changamoto ya utapiamlo na udumavu wa akili kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano kwenye nchi masikini na zinazoendelea ili kujenga kizazi chenye afya kwa maendeleo endelevu ya mataifa hayo. 

  Makamu wa Rais ametoa wito huo Mjini Washington Marekani kwenye hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, wakati wa mkutano ulioandaliwa na Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Kim, ulioshirikisha mawaziri wa Fedha na wadau wengine kutoka nchi zaidi ya 180 wanaoshiriki mkutano wa Mwaka wa Benki hiyo na Shirika la Fedha Duniani-IMF 

  Amesema kuwa licha ya Tanzania kufanikiwa kupunguza utapiamlo na kiwango cha udumavu kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka 5 kutoka asilimia 42 hadi kufikia asilimia 34, bado idadi kubwa ya watoto wanaokadiriwa kufikia milioni 2.7 wamedumaa akili huku wengine laki sita wakikabiliwa na utapiamlo mkali. 

  Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema kuwa kwa kutambua changamoto hiyo, serikali imepanga kutumia kiasi cha dola Milioni 115 sawa na zaidi ya shilingi Bilioni 254 kukabiliana na tatizo hilo katika kipindi cha miaka mitano kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa miaka Mitano, kuanzia mwaka 2016/2021 

  Ameitaka jumuiya ya Kimataifa kuunga mkono juhudi za mataifa masikini na zinazoendelea ili kuwaokoa mamilioni ya watoto wanaokabiliwa na tatizo hilo hivyo kuathiri mustakabali wa watoto kielimu na kimaisha. 

  Kwa upande wake Rais wa Benki ya Dunia, Dkt. Jim Kim, amesema kuwa asilimia 43 ya watoto waliochini ya umri wa miaka mitano wanaokadiriwa kufikia milioni 250 katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati wamedumaa na kukabiliwa na utapiamlo mkali unaoletelezwa na umasikini pamoja na ukosefu wa elimu kuhusu umuhimu wa kuwapatia watoto lishe bora na unyonyeshaji wa maziwa ya mama, 

  Ameahidi kuwa Benki hiyo itatenga fedha kupitia miradi mbalimbai inayotekelezwa kwa ufadhili wake na kushirikisha sekta binafsi ili lengo la kunusuru watoto katika hali hiyo ya utapiamlo na udumavu wa akili liweze kupatiwa ufumbuzi wa haraka. 

  Ameyataka Mataifa kuwekeza fedha katika ujenzi wa miundombini ya sekta ya afya, elimu, maji, na usalama wa chakula, kuwajali na kuwapenda watoto ili malengo ya kukomesha tatizo hilo yafikiwe kama yalivyopangwa. 

  0 0

   Ajali hii imetokea leo katika eneo la Emaus, Mkoani Dodoma ambapo imehusisha gari kubwa mbili na moja dogo aina ya Toyota Noah. Inadaiwa kuwa Mtu mmoja amepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa. Chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika mpaka sasa.
   Askari Polisi wakiwa eneo la tukio kuokoa majeruhi.


  0 0


  Afisa Utawala wa Wizara wa Afya, Michael John akikabidhi cheti kwa mshindi wa kwanza wa masomo ya Sayansi kwa Wanaume Mugisha Lukambuzi kutoka shule ya Sekondari ya Bendel Memorial ya Moshi
  Afisa Utawala wa Wizara wa Afya, Michael John akikabidhi cheti kwa mshindi wa kwanza wa masomo ya Sayansi kwa Wanawake Naomi Sarakikya kutoka shule ya S't Mary's Mazinde juu.
   
   
  Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii

  SERIKALI imesema itaendelea kuisadia ofisi ya Mkemia mkuu kuwa na Vifaa vya kisasa ili iweze kupambana na changamoto mbalimbali za upimaji.

  Hayo yamesemwa jioni ya leo na Naibu Waziri wa Afya ,Dk Hamisi Kigwangwala katika hotuba yake iliyosomwa na afisa utawala wa Wizara hiyo,Michael John katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi Kidato cha nne na cha Sita Mwaka jana.

  “Tunashukuru kwa kazi mnayofanya na sisi kama serikali tunajipanga kwa kila namna kuhakikisha kuwa ofisi hii ya mkemkia mkuu inakuwa bora zaidi licha kutangazwa kuwa ndio bora kwa Afrika Mashariki” amesema

  Alimaliza kwa kuwataka wanafunzi wote waliofanya vizuri katika masomo yao kuwa bado wanakazi kubwa ya kuongeza juhudi hili kufikia malengo waliyojipangia.

older | 1 | .... | 998 | 999 | (Page 1000) | 1001 | 1002 | .... | 1897 | newer