Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46313 articles
Browse latest View live

SERIKALI KUWAKAMATA NA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATU WOTE WALIOSHIRIKI MAUAJI YA WATAFITI-DKT.MWAKYEMBE

$
0
0




Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mh. Harrison Mwakyembe akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu mauaji ya wataalamu wa utafiti yaliyotokea hivi karibuni mjini Dodoma, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Amon Mpanju. (Picha na Benjamin Sawe- Maelezo).


Na Beatrice Lyimo- MAELEZO

Dar es Salaam.

SERIKALI imesema itahakikisha kuwa wahusika wa mauaji ya Watafiti mkoani Dodoma wanakamatwa na kufikishwa mahakamani ili waweze kujibu mashtaka yanayowakabili.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri ya Mambo ya Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya mauaji ya Wataalamu hao yaliyotokea wilayani Chamwino.

Amesema kuwa Serikali imesikitishwa na hatua iliyochukuliwa na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Iringa Mvumi wilayani Chamwino kuwaua watafiti hao ambao walikuwa kazini.

Kufuatia hali hiyo amewaagiza Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kushirikiana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) katika kufanya upelelezi wa mauaji ya wataalamu hao ili wahusika waweze kufikishwa vyombo vya usalama haraka na haki iweze kutendeka.

Amesema kuwa ushirikiano huo utasaidia kuimarisha upepelezi ambao utawezesha uandaaji wa mashtaka ili wahusika wote waweze kufikishwa Mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayowakabili.

“Wizara inawataka Mkurugenzi wa Mashtaka DPP ajihusishe kikamilifu na upelelezi wa kesi hii ya mauaji ya watafiti kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai DCI kwa mujibu wa Sheria ya Huduma ya Uendeshaji wa Mashtaka” alifafanua Dkt. Mwakyembe.

Ameongeza kuwa ili kukomesha wimbi la wananchi kuchukua sheria mkononi, Wizara itachukua hatua kali kuhakikisha waliohusika kwa namna moja ama nyingine kwa kushawishi, kuhamasisha au kuchochea, kupanga, kushambulia kwa mapanga na kushiriki kuchoma moto gari wanafikishwa mahakamani ili Sheria ichukue mkondo wake.

Katika hatua nyingine, Waziri Mwakyembe amewataka baadhi ya waandishi wa habari kubadilisha mfumo wa kutoa taarifa za matukio zinazochochea uvunjifu wa amani kama vile kuandika kuwa “wananchi wenye hasira kali” maneno ya aina hii hushawishi wengine kufanya hivyo kwa kisingizio cha hasira.

Mbali na hayo Waziri huyo amevitaka vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria kwa wote waliohusika na vitendo vya kuchukua sheria mkononi ikiwemo kuwafikisha mahakamani.

WIZARA YA UJENZI, MAWASILIANO NA USAFIRISHAJI WAFANYA MAZUNGUMZO NA WAANDISHI WA HABARI ZANZIBARI

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliyano na Usafirishaji Zanzibari Mustafa Abuod Jumbe akizungumza na waandishi wa Habari  hawapo pichani huko Ofisi ya Shirika la Meli Malindi Mjini Zanzibar.
Waandishi wa Habari wakichukuwa maelezo  ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji  Mustafa Aboud Jumbe wakati walipofika Ofisi ya Shirika la Meli Malindi Zanzibar.Picha na Miza Othman-  Habari Maelezo Zanzibari.

Na Ali Issa na Mwashungi Tahir / Maelezo Zanzibar 06/10/2016

MELI mpya ya Mapinduzi II inatarajiwa kuondoka nchini Jumaatatu ijayo kuelekea Mombasa chelezoni kwa kufanyiwa ukaguzi wa kawaida baada ya dhamana ya mwaka mmoja iliyowekwa kati ya Serikali na mtengenezaji wa meli hiyo.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mustafa Abuod Jumbe wakati akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisi ya Shirika la Meli Malindi Zanzibar

Amesema upelekaji wa meli katika chelezo ni suala la kawaida na halijaalishi kwa upya wa mwaka mmoja au miwili ispokuwa ni maamuzi ya Shirika kufanya hivyo.

Amesema wamepeleka chelezoni meli hiyo baada ya dhamana aliyotoa mtengenezaji ya mwaka mmoja kumalizika, hivyo ilipaswa kuchunguzwa kabla ya dhamana huyo kumalizika muda wake Disemba mwaka huu.

Aidha amesema meli hiyo katika ukaguzi wake utakao fanywa nipamoja na kutia rangi ,ukaguzi wa viokozi ,mashine ukungu na mambo mengi yatayonekana kurekebishwa.

Amesema gharama ya matengenezo hayo yanatarajiwa kufikia dolazaidi ya 90 elfu ambapo zitagawiwa thuluthi tatu ,thuluthi moja mjenzi wa meli na sehemu mbili zilizo bakia zitatoa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hata hivyo aliwataka wananchi kuondosha hofu na wasiwasi kwa kuikosa meli hiyo kwa kipindi kifupi na badala yake Shirika la Meli la Zanzibar limefanya mazungumzo na uongozi wa meli ya seling ili kuhudumuia usafiri kwa muda huo kwakwenda Pemba na Daresalaam mara tatu kwa wiki.

Pamoja na hayo Katibu huyo aliwambia wandishi wahabari kua Serikali ina mpango wa kununua meli mpya mbili ambayo moja itahudumia abiria pamoja na mizigo na nyengine itakuwa meli ya mafuta.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

BENKI YA DUNIA KUIPIGAJEKI TANZANIA RUZUKU NA MKOPO WENYE MASHARTI NAFUU DOLA BLN 1 NUKTA 6

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philiph Mpango akifurahia jambo na Bi. Bella Bird ambaye ni Mkurugenzi Mkazi anayeiwakilisha Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia wakati wakisubiri kuingia kwenye mkutano Jijini Washington DC.(Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Dotto James akisalimiana na Bi. Bella Bird ambaye ni Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anaewakilisha benki hiyo katika nchi za Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia akiwa pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Jijini Washington DC.
Bi. Bella Bird, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anaewakilisha Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia akifafanuliwa masuala mbalimbali ya Tanzania na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Dotto James (kulia) pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango(katikati) Jijini Washington DC.
Kaimu Kamishna wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya Nishati na Petroli Bw. James Andilile akimweleza Kaimu Kamishma wa Sera Bw. Agustine Ollal (kushoto) na Kamishna wa Bajeti Bw. John Cheyo (kulia) kuhusu Tanesco inavyopiga hatua katika uimarishaji wa nishati kwa wananchi, wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Benki ya Dunia na IMF unaoendelea Jijini Washington DC, Marekani.
Wajumbe kutoka Tanzania waliohudhuria Mkutano wa Benki ya Dunia wakiwa kwenye Mkutano wa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia, Kanda ya Afrika Jijini Washigton DC.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akieleza ni jinsi gani Benki ya Dunia inafurahia utendaji kazi wa nchi ya Tanzania hasa katika kukuza uchumi, kulia kwake ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dkt. Natu Mwamba anaemfuatia ni Bw. Johson Nyela Mkurugenzi wa Sera Uchumi na Utafiti na Bw. Dickson Lema Meneja Masuala ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania Jijini Washgton DC, Marekani.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop akifafanua masuala mbalimbali namna Benki hiyo ilivyojipanga kushirikiana na Tanzania katika utekelezaji wa miradi yake mbalimbali ya kipaumbele wakati wa mazungumzo kati ya Benki hiyo na Ujumbe kutoka Tanzania unaohudhuria mkutano wa mwaka wa Benki hiyo na Shirika la Fedha la Kimataifa-IFM, unaofanyika Washington DC nchini Marekani
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndullu akimweleza jambo Mkurugenzi Msaidizi wa Benki ya Dunia ya Afrika Bw. Makhtar Diop (Hayupo pichani) juu ya miradi mbalimbali ambayo Benki ya Dunia inaweza Kusaidia Tanzania katika Sekta mbalimbali kwani kwa sasa uchumi wa Tanzania umekuwa kwa kiasi cha kuridhisha kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango akifuatiwa na Waziri wa Fedha wa Zanzibar Dkt. Khalid Salum Mohamed, Jijini Washington DC, Marekani
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndullu akimwonesha kitabu waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango walipokuwa kwenye mkutano na Mkurugenzi Msaidizi wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Jijini Washigton DC, Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifurahia jambo na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bw. Albert Zeufack alipotoka kwenye mkutano, Jijini Washigton DC, Marekani.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifurahia jambo na Mchumi Mkuu wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Bw. Albert Zeufack alipotoka kwenye mkutano, Jijini Washigton DC, Marekani.

........................................................

Benny Mwaipaja, MoFP-Washington DC

BENKI ya Dunia inakusudia kuipatia Tanzania ruzuku na mkopo wenye masharti nafuu wa dola Bilioni 1 nukta 6 sawa na zaidi ya shilingi Trilioni 3 nukta 5 kwaajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo nishati ya umeme, kilimo biashara na ukarabati wa miundombinu ya reli ya kati.

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu amesema Jijini Washington DC, Marekani ambako Ujumbe wa wataalamu wa masuala ya uchumi na Fedha kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki mkutano wa mwaka wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF kwamba mazungumzo kuhusu mkopo huo yako katika hatua za mwisho.

Prof. Ndulu amesema kuwa upatikanaji wa mkopo huo utaisaidia serikali kuboresha miundombinu yake mbalimbali ili kuharakisha maendeleo ya sekta ya viwanda kwa kuimarisha pia mazingira ya sekta binafsi kufanyabiashara na kuwekeza mitaji na teknolojia.

“Mbali na mkopo huo ambao ni muhimu kwa taifa, tunajadili pia namna ukuaji wa uchumi unavyotakiwa kuakisi maisha ya kawaida ya wananchi wetu kwa kupiga hatua kimaisha na kuondokana na umasikini” alisema Gavana Prof. Ndulu.

Aidha, amesema kuwa Benki ya Dunia imesifu hatua zilizofikiwa na serikali ya Tanzania katika kukuza na kusimamia uchumi wake ambao licha ya uchumi wa dunia kushuka viwango vyake vya ukuaji uliotarajiwa wa asilimia 3.3 na kukua kwa asilimia 1.5 tu, Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi ya asilimia 7.

“Tanzania ni miongoni mwa nchi nne zinazoendelea ambazo uchumi wake unakua kwa kasi na unatarajia kukua zaidi kutokana na kuvumbuliwa kwa gesi na kushuka kwa mfumuko wa bei” Alisisitiza Prof Ndulu

Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa mkopo utakao tolewa ni pamoja na dola milioni mia 2 kwaajili ya kulijengea uwezo shirika la ugavi wa umeme nchini Tanzania-Tanesco ili liondokane na nakisi inayosababishwa na madeni makubwa yanayolikabili shirika hilo

Dkt. Mpango Amefafanua kuwa mkopo huo pia utaiwezesha serikali kulipa madeni inayodaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii baada ya kufanyika kwa uhakiki wa kina wa madeni hayo ili kuiwezesha mifuko hiyo itoe huduma inayostahili kwa wananchama wake.

Amesema kuwa kiasi kingine cha fedha hizo kitatumika kuijengea uwezo sekta binafsi iweze kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa Taifa pamoja na kuimarisha kilimo kwa kuwawezesha wakulima kulima kilimo cha kibiashara na kuondoa kodi zenye kuleta kero katika sekta ya kilimo.

“Wakati tunatekeleza mpango huo tutaangalia pia namna ya kupitia upya kodi zinazolalamikiwa katika sekta ya utalii” amefafanua Dkt. Mpango

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Mohamed, ameishukuru Benki ya dunia kwa kuisaidia nchi hiyo kupitia miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa visiwani humo ikiwemo uboreshaji wa rasilimali watu, miundombinu ya barabara, kiwanja cha ndege na kuboresha mazingira yatakayochangia kukua kwa sekta ya utalii visiwani humo.

Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Makhtar Diop, amesema kuwa benki hiyo itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania ili iweze kufanikiwa kiuchumi na kijamii.

Amesifu juhudi na hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli kwa kurejesha nidhamu ya kazi na kupambana na vitendo vya ufisadi hatua ambayo inaungwa mkono na benki yake ili kuharakisha maendeleo ya nchi na wananchi wake kwa ujumla.

Diop amebainisha kuwa Benki yake inataka kuona Shirika la Umeme Tanzania Tanesco linaboreshwa na kuwa la kisasa kwakuwa nishati ni nyenzo muhimu ya kukuza uchumi wa viwanda na kwamba wangependa kusaidia eneo hilo namengine ya kuboresha rasilimali watu kwa kuwekeza kwenye elimu na kuwainua wananchi kimapato kupitia mradi wa TASAF na mingine itakayoanzishwa.

RAIS MAGUFULI ATOA MIEZI 2 KWA TANESCO ILI KUFIKISHA UMEME KATIKA KIWANDA CHA BAKHRESA

$
0
0

Na: Frank Shija, MAELEZO

TENESCO yapewa miezi miwili kuhakikisha inafikisha huduma ya umeme katika kiwanda cha kusindika matunda na kuzalisha juisi na vinywaji baridi cha Bakhresa Food Products Ltd kilichopo Mwandege wilayani Mkuranga, Mkoani  Pwani.

Agizo hilo limetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kiwanda hicho iliyofanyika leo wilayani Mkuranga, Mkoani Pwani.

Amesema kuwa ni ajabu kwa mwekezaji kuanza ujenzi hadi anamaliza na baadaye anaanza uzalishaji halafu suala la nishati ya umeme linakuwa kikwazo hali inayomlazimu mwekezaji kutumia nishati mbadala (Jenereta) kitu kinachosababisha gharama za uendeshaji kuwa kubwa.

“Ninaagiza hakikisheni mnafikisha umeme katika kiwanda hiki kabla ya mwezi wa 12, nia ajabu sana mtu anaanza kujenga mnamuangalia tu, anamaliza mnamuangalia, Meneja wa TANESCO upo? Hakikisha umeme unafika kama kuna mtu ana kukwamisha niambie”. Alisema Rais Magufuli.

Aliongeza ni imani yake kuwa baada ya umeme kufikishwa katika kiwaanda hicho gharama za undeshaji zitapungua na kupelekea kufanya maboresho ya maslahi ya wafanyakazi wake.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli ametumia wasaa huo kumuomba Mwenyekiti  wa Makampuni ya Bakhresa Said Salim Bakhresa kuangalia uwezekano wa kufanya uwekezaji kama huo katika maeneo mengine ya kikanda hili kutoa fursa kwa wananchi wanaoishi katika maeneo hayo kupata soko la bidhaa zao.

Kwa upande wake Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema kuwa uwekezaji uliofanywa na Makampuni ya Bakhresa unasaidia kuchochea kilimo cha matunda na kutoa fursa ya soko la uhakika kwa wakulima.

Mwijage alisema kuwa Sekta ya Viwanda nchini imeendelea kukuwa, aliongeza kuwa adhima ya kufikia Tanzania yenye uchumi wa kati kutokana na viwanda itatimia endapo wafanyabiashara wenye viwanda  watakua wazalendo kama Bakhresa.

Naye Mwakilishi wa Kampuni ya Bakhresa Food Production Ltd Bw. Yusuph Bakhresa ameishukuru Serikali kwa kutoa ushirikiano kwa wafanyabiashara wenye viwanda nchini, hali ambayo itasaidia kufikia lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ya kuitaka Tanzania kuwa nchi yenye viwanda ifikapo mwaka 2025.

WATAALAMU WA MAJENGO WA DIT KUFANYA UTAFITI UHARIBIFU WA MAJENGO KAGERA.

$
0
0

Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya akiongea na Wataalamu wa majengo kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT), (hawapo pichani) ambao wapo mkoani Kagera kufanya utafiti wa uharibifu wa majengo uliosababishwa na tetemeko la ardhi ili kujua hali halisiilivyo hadi sasa.
Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya akiongea na Wataalamu wa majengo kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wakiongozwa na Mhandisi Dkt. Johnson Malisa (wa kwanza kulia) ambao wapo mkoani Kagera kufanya utafiti wa uharibifu wa majengo uliosababishwa na tetemeko la ardhi ili kujua hali halisiilivyo hadi sasa. Wa kwanza kushoto ni Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Nesphory Bwana akifuatiwa na Dkt. Asinta Manyele na Mhandisi Dkt. Johnson Malisa wa DIT.(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)

Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba

Timu ya wataalamu wa majengo kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) wamewasili mkoani Kagera kufanya utafiti wa uharibifu wa majengo uliosababishwa na tetemeko la ardhi ili kujua hali halisiilivyo hadi sasa.

Timu hiyo iliyyongozwa na Dkt. Asinta Manyele na Mhandisi Dkt. Johnson Malisa wa DIT wapo mkoani humo ili kuwajionea hali halisi ya majengo katika wailaya zilizoathiriwa na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10 mwaka huu na hali ilivyo hadi sasa baada ya tukio hilo.

Wakiwa katika kituo cha kukabiliana na maafa mjini Bukoba, wataalamu hao wamemwabia Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya kuwa utafiti wao unalenga kufanya tathmini ya kujua namna nyumba zinavyopaswa kujengwa ili kukabiliana na atahri za tetemeko la ardhi ambalo kwa Tanzania ni tukio la kwanza ambalo limekuwa na madhara mengi yakiwemo majengo ya taasisi za umma na za watu binafsi, nyumba za watu binafsi, miundombinu ya maji, umeme pamoja na barabara.

Zaidi ya hayo, watafiti hao wamemwambia Brigedia Jenerali Msuya kuwa nia yao pia ni kuchunguza aina za udongo katika mkoa wa Kagera na kutoa ushauri wa aina za majengo yanayotakiwa kujengwa kwa kuzingatia tahadhari za athari za tetemeko la ardhi.

Aidha, watafiti hao wametoa ushauri kwa waandaaji wa sera, waandae sera inayohusu maelekezo ya ujenzi wa majengo ambayo yolenga kuhimili athari za tetemeko la ardhi ili yaweze kustahimili nguvu ya tetemeko la ardhi endapo litatokea.

Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya amewataka wataalamu hao watumie elimu waliyonayo kuelimisha jamii katika kujua aina ya majengo wanapojenga nyumba zao ili ziwe imara.

Katika kurejesha hali baada ya tetemeko hilo, Brigedia Jenerali Msuya amesema kuwa kituo chake kinashirikiana na Kamati ya Maafa ya Mkoa kwa kuwa na mikutano kila siku pamoja na kuratibu mambo mbalimbali ikiwemo kupokea na kugawa misaada inayotolewa na wananchi, taasisi za kidini na za watu binafsi na mataifa mengine yakiwemo Kenya, Burundi, Uganda, India na Uingereza.

Halmashauri za mkoa wa Kagera ambazo zimeathiriwa na tetemeko la ardhi ni Bukoba Vijijini, Manispaa ya Bukoba, Muleba, Kyerwa, Misenyi na Karagwe

TAMASHA LA VYAKULA VYA VINYWAJI KUFANYIKA LEADERS CLUB OKTOBA 8 JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ya EM & U Investiment, Edward James akizungumza na waandishi wahabari juu ya tamasha la vinywaji na vyakula litakalofanyika viwanja Leaders Club jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mratibu wa Tamasha hilo, Zahara Michuzi ,Kulia Meneja Mafunzo na Uwezeshaji, Rashid Chenja.
 Mratibu wa Tamasha hilo, Zahara michuzi juu maandalizi juuya tamasha la vinywaji na vyakula litakalofanyika viwanja Leaders Club jijini Dar es Salaam,
 
KAMPUNI ya EM & U Investiment imeandaa tamasha la Chakula na Vinywaji litakalofanyika (Dar es Salaam Food & Drink Festival) Oktoba 8 katika viwanja vya leaders Club jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Edward James amesema tamasha hilo litakuwa la aina yake kwa kushirikisha wapikaji wa wa vyakula vya asili ikiwa ni kufanya watanzania kupenda hivyo.

James amesema kuwa watu wengi wanapenda kula vyakula vya asili lakini hawajui watapata wapi hivyo tamasha litafungua ukurasa mpya juu ya watu wanaweza kupata chakula hicho sehemu gani .

Amesema katika tasha hilo kutakuwa na wapishi katika kila kabila kupata chakula chake cha asili katika mikoa yao hiyo itakuwa ni sehemu kuwajengea utamdauni wa kuepnda chakula cha asili.

James amesema katika tamasha hilo wananchi watapima magonjwa yote bure ikiwa ni kutaka watanzania kujua afya zao.katika Tamasha hilo wasanii mbalimbali watatumbuza katika tamasha hilo.

BWENI LA WASICHANA MORETO SEKONDARI LA TEKETETEA KWA MOTO

$
0
0
BWENI la wanafunzi wasichana katika shule ya sekondari ya Moreto iliyopo tarafa ya Msoga wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, baada ya kuungua kwa moto na kusababisha mali zote za wanafunzi hao kuteketea kwa moto. (Picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo

MBUNGE wa jimbo la Chalinze, mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete, ametoa magodoro 50, yenye thamani ya sh.mil 2.225 kwa wanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Moreto, waliounguliwa na bweni lao na kusababisha mali zote kuteketea kwa moto.

Wanafunzi hao wapatao196, katika shule hiyo iliyopo kata ya Lugoba tarafa ya Msoga, wilaya ya Bagamoyo, wamenusurika kifo baada ya bweni hilo kuteketea kwa moto siku ya oktoba 5.

Moto huo umeteketeza mali zote zilizokuwemo ambazo hadi sasa hazijajulikana thamani yake.Kufuatia kutokea kwa tukio hilo, Ridhiwani alifika shuleni hapo kutembelea na kutoa pole kwa kutokea janga hilo.

Alisema wakumshukuru ni mungu kwani pamoja na kutokea kwa hasara ya kuteketea kwa mali lakini hakuna madhara kwa wanafunzi yaliyotokea.

Ridhiwani aliwapa pole walimu na wanafunzi kijumla na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kwenda kusaidia pale watakapojaaliwa.

Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Moreto, Justine Lyamuya alielezea kuwa, tukio hilo limetokea oktoba 5,majira ya asubuhi ambapo walianza kuona moshi mzito katika bweni mojawapo wanaloishi wasichana wa shule hiyo.

Alisema wakati moto huo unazuka wanafunzi hao walikuwa kwenye masomo yao darasani."Tulifuatilia na kukuta moto umeshashika kwenye bweni hilo na jitihada za kuuzima zilishindikana"alisema mwalimu Lyamuya.

Lyamuya alisema mali zote za wanafunzi wanaolala kwenye bweni hilo zimeteketea kwa moto hivyo kwa sasa wanafanya tathmini kujua gharama zilizopotea.

Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoani Pwani linafanya uchunguzi wa tukio hilo ili kubaini chanzo cha moto.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, Boniventure Mushongi, alielezea kuwa mazingira ya jengo hilo ni yenye kutumia nishati ya solar power hivyo ni lazima kufanya uchunguzi wa kina kujua kiini cha kuzuka kwa moto huo.

Alisema bweni hilo linakadiriwa kuwa na wanafunzi 196.
Kamanda Mushongi alisema thamani za mali za wanafunzi katika moto huo bado hazijafahamika.

NDEGE ZA AIR TANZANIA (ATCL) KUANZA SAFARI ZAKE OKTOBA 15,2016


Waziri Simbachawene aagiza kuvuliwa madaraka kwa Mwl. Mkuu wa Shule ya kutwa ya Sekondari Mbeya.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mhe. George Simbachawene akisisitiza jambo wakati wa mahojiano maalum juu ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kufuatia tukio la Walimu wa mazoezi katika Shule ya Sekondari ya kutwa Mbeya leo Jijini Dar es Salaam.


Na: Frank Shija, MAELEZO.

MAMLAKA husika ya nidhamu kwa walimu imeagizwa kumvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kutwa ya Sekondari ya Mbeya, Mwl. Magreth Haule kufuatia kutotoa taarifa juu ya tukio la kushambuliwa kwa mwanafunzi Kidato cha tatu Shule hiyo Sebastian Chingulu.

Ikizungumza na mwandishi maalum kutoka Idara ya Habari –MAELEZO, leo Jijini Dar es Salaam ambapo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. George Simbachawene amesema kuwa tukio hilo ni la kweli lilitokea tarehe 28 Septemba, 2016 lakini Mwalimu Mkuu huyo akutoa taarifa, hadi ziliposambaa kwenye mitandao ya kijamii.

“Ninaagiza mamlaka husika za kinidhamu kumvua madaraka mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mbeya Kutwa Mwl. Magreth Haule avuliwe madaraka kutokana na kukaa kimya huku kukiwa na tukio la unyama dhidi ya mwanafunzi”. Alisema Simbachawene.

Alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa za awali zilizopatikana tukio hilo lilitokea huku ikidaiwa chanzo chake ni mwanafunzi Sebastian Chingulu kugomea adhabu aliyopewa na mwalimu wake.

Aliongeza kuwa walimu waliohusika na tukio hilo ni wa mazoezi kutoka Chuo Kikuu cha Elimu Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ambapo walishirikiana kumshambulia mwanafunzi huyo.

SImbachawene aliwataja walimu hao wa mazoezi kuwa ni pamoja na Frank Msigwa kutoka DUCE, ambaye ndiye chanzo kikubwa kufuatia madai ya mwanafunzi huyo kugoma kufanya adhabu aliyopewa na mwalimu huyo.

Wengine ni John Deo na Sante Gwamoka kutoka DUCE,mwingine ni Evans Sanga kutoka Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Awali akielezea hatua ambazo tayari Serikali imekwisha zichukuwa, alisema kuwa ni pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mbeya kuendelea na ufuatiliaji wa karibu suala hilo ambapo mpaka sasa vyombo vya dola vinaendelea kuwahoji baadhi ya walimu washule hiyo.

Hatua nyingine ni pamoja na kuendelea kuwasaka wahusika wa tukio hilo kwa kuwa mara baada ya kufanya shambulio hilo walitoweka kusikojulikana, hata hivyo halisisitiza kuwa hakuna hatakaye kwepa katika hili.

Katika hatua nyingine Simbachawene aamewaagiza Wakuu wa Shule za Serikali nchini kuzingatia kanuni za utoaji wa adhabu kwa wanafunzi badala ya kufanya kazi kwa mazoea.

WLAC WAZINDUA AWAMU YA TATU YA KAMPENI YA ‘TUNAWEZA’ JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Masue (wa pili kulia) na Mkurugenzi waKituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo (wa tatu kulia), wakikata utepe kuzindua rasmi Awamu ya Tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ wakati wa hafla ya uzinduzi huo uliofanyika leo kwenye Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam. Kulia ni Jacckline Mlay wa Kitengo cha haki za Jinsia Oxfam na (kushoto) ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kivulini ya jijini Mwanza, Yassin Ally.
 Mgeni rasmi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Masue (wa pili kulia) na Mkurugenzi waKituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo (wa tatu kulia), na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kivulini ya jijini Mwanza, Yassin Ally (wa pili kushoto) Mkaguzi wa Polisi Prisca Komba wa Dawati la Jinsia Polisi Kinondoni (kushoto) na Jackline Mlay wa Kitengo cha haki za Jinsia Oxfam, kwa pamoja wakiinua vipeperushi baada ya mgeni rasmi kuzindua Awamu ya Tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ iliyofanyika kwenye Viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam, leo. Picha na Mafoto Blog
 Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Theodosia Muholo, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Sehemu ya wadau na mashuhuda waliohudhuria uzinduzi huo.
 Specioza Sylvester, mkazi wa jijini Mwanza akitoa ushuhuda wa Ukatili jinsi alivyomwagiwa Tindikali na vijana waliotumwa na mumewe kwa ajili ya mali.
 Rukia Hamis, mkazi wa Mbagala Kijichi, akitoa ushuhuda jinsi alivyokatwa mkono na mumewe.
 Rukia akiuvaa mkono wake wa bandia baaada ya kutoa ushuhuda
 Jacckline Mlay wa Kitengo cha haki za Jinsia kutoka Shirika la Oxfam, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
 Mkaguzi wa Polisi Prisca Komba wa Dawati la Jinsia Polisi Kinondoni, akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi.
 Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya,  akizungumza.
 Mgeni rasmi Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Flora Masue, akihutubia wakati wa hafla hiyo.
 Baadhi ya wadau na viongozi wakiwa Jukwaa Kuu.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Mwacity Almas, akiimba na kucheza pamoja na baadhi ya kinamama waliohudhuria uzinduzi wa Awamu ya tatu ya Kampeni ya ‘Tunaweza’ ya Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), iliyozinduliwa leo kwenye Viwanja vya Biafra jijini Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
 Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Hisia Theatre Group, wakitoa burudani. 
 Wasanii wa kikundi cha Ngonjela cha Aha Organization, wakighani mashahiri yao ya Ngonjela.
Wasanii wa Kikundi cha Sanaa cha Hisia Theatre Group, wakitoa burudani. 

RC MWANZA AWAFUNDA VIJANA KUPITIA MKUTANO WA BARAZA KUU MAALUMU LA UVCCM WILAYA YA NYAMAGANA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela (wa tatu kulia), akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa BarazaKu Maalumu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, uliofanyika "Gandhi Hall" Jijini Mwanza.

Mongela amewataka vijana kubuni njia mbalimbali halali za kuwaingizia kipato ikiwemo ujasiriamali badala ya kukaa bila kazi huku wakijivunia kuwa kwenye vyama vya siasa.

Amesema ni vyema wanaoingia kwenye siasa wakahakikisha wana shuguli za kufanya ambapo amewasihi wajasiriamali wakiwemo Machinga kuwa tayari kufanya biashara zao katika maeneo yaliyoainishwa na kwamba watakaotii hilo, watanufaika moja kwa moja na mikopo inayotolewa na halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Naye Katibu wa UVCCM wilayani Nyamagana, Odila Batimayo, kwa niaba ya umoja huo, amempongeza Rais John Magufuli kutokana na utendaji wema wa kazi ikiwemo kuanza kutimiza ahadi zake ndani ya miezi tisa ya uongozi wake kama vile ununuzi wa ndege, mabehewa, ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na mpango wa elimu bure nchini.

Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nyamagana, Hussein Kimu, amebainisha kwamba lengo la mkutano huo ni kuyapongeza makundi mbalimbali yakiwemo machinga, mamantilie na bodaboda kutokana na mchango wao katika kufanikisha ushindi katika uchaguzi wa mwaka jana, ambapo pamoja na mambo mengine wajumbe wa mkutano huo wamepata fursa ya kuchangia damu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela (katikati), akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Mkutano wa BarazaKu Maalumu la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, uliofanyika "Gandhi Hall" Jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongela, akizungumza kwenye mkutano huo
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nyamagana, Hussein Kimu, akizungumza kwenye mkutano huo
Katibu wa UVCCM wilayani Nyamagana, Odila Batimayo, akisoma taarifa ya UVCCM Nyamagana kwenye mkutano huo.
Wajumbe mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo
Viongozi mbalimbali wa UVCCM mkoani Mwanza
Viongozi mbalimbali wa UVCCM mkoani Mwanza
Wajumbe pamoja na Viongozi mbalimbali wa UVCCM mkoani Mwanza
Taswira ya mkutano wa Baraza Kuu Maalumu ya UVCCM Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, ikiwa ni sehemu ya kuelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya kuanzishwa kwa umoja huo, "UVCCM DAY" kitaifa.
Imeandaliwa na BMG

WAZIRI MKUU ABAINI MADUDU UUZAJI VIWANJA CDA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Watumishi wa Mamalaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kwenye ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Oktoba 6, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu CDA wakimsikilizwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Oktoba 6, 2016.
Baadhi ya Watumishi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Mkuu CDA wakimsikilizwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao, Ofisini kwake jijini Dar es salaam Oktoba 6, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


*Kiwanja chauzwa kwa sh. milioni 240 lakini zilizoingia CDA ni milioni 6 tu
*Ahimiza kasi ya upimaji viwanja, asema waliolipa nusu wasinyang’anywe

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Bunge), Bw. Uledi Mussa afuatilie malipo ya kiwanja kilichouzwa na CDA kwa sh. milioni 240 lakini fedha iliyoingia ofisini ni sh. milioni 6 tu.

“Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, ninataka ufuatilie mauzo ya kiwanja namba 26 block AA eneo la Kikuyu East ambacho kimeuzwa kwa sh. milioni 240 lakini fedha iliyoingia CDA ni sh. milioni 6 tu. Nataka kujua nani ameingiza milioni 6 na nani kachukua hizo sh. milioni 234,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Oktoba 6, 2016) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) kwenye ukumbi wa Hazina ndogo mjini Dodoma.

Bila kutoa ufafanuzi zaidi, Waziri Mkuu amesema eneo hilo lilipaswa kuwa na kituo cha mafuta na akataka apatiwe taarifa mapema iwezekanavyo.

Pia amemwagiza Katibu Mkuu huyo afuatilie mkataba wa upangishaji wa jengo la CDA ambalo wamepangishwa taasisi ya Tunakopesha Limited kwa madai kuwa mhusika alipewa bure na sasa anataka kulipangisha tena ili apate cha juu.

Waziri Mkuu amewaonya watumishi hao pamoja na viongozi wao waache tabia ya kushirikiana na madalali kuuza viwanja na akawataka wachape kazi wakijielekeza na kasi ya Serikali ya kuhamia Dodoma.

“Tabia ya watumishi kushirikiana na madalali kuuza ardhi sasa basi. Hata hivyo, nimefarijika kukuta mmeanza kuweka mfumo wa kielektoniki katika baadhi ya huduma. Ni lazima mauzo ya viwanja sasa hivi yafanyike kwa njia ya kieletroniki, madalali hawana nafasi,” amesisitiza.

Ameutaka uongozi wa CDA uongeze kasi ya upimaji viwanja kwa sababu mahitaji ni makubwa lakini akaonya kuwa wakati zoezi hilo likifanyika, wananchi walionunua viwanja na bado hawajamalizia kuvilipia, wasinyang’anywe kwa kigezo cha kutaka kuwauzia wengine.

“Mimi nataka idadi ya viwanja vilivyopimwa iongezeke. Lakini pia msitumie fursa hii kuwanyang’anya watu wenye umiliki halali eti kwa sababu Serikali inataka idadi ya viwanja vilivyopimwa iongezeke,” amesema.

“Kama mtu amepewa offer au hati yake asinyang’anywe hata kama amelipia nusu asinyang’anywe. Ahimizwe kumalizia hilo deni na ninyi kazi yenu ni kupima viwanja vingine,”  amesisitiza.

“Natambua mnayo benki ya viwanja, lakini inabidi muongeze idadi ya viwanja vingi zaidi. Tumeita wawekezaji waje kujenga nyumba za kuishi watumishi, mahoteli na viwanda na maeneo yote haya inabidi yatengwe rasmi,” amesema.

Amesema jumla ya viwanja 70,000 vimepimwa tangu CDA ianzishwe mwaka 1973. Amesema kama wataendelea na kasi hiyo wakati mahitaji yameongezeka, itawachukua zaidi ya miaka 40 kukamilisha mahitaji ya viwanja 100,000 ambavyo vinatarajiwa kuanza kupimwa hivi karibuni.

Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa CDA, Eng. Paskasi Muragili amesema usanifu wa upimaji viwanja 20,000 umekamilika na kwamba wana lengo la kupima viwanja vingine 100,000 ifikapo Juni 2017.

Waziri Mkuu alitembelea Ofisi ya CDA na kukagua mfumo wa utunzaji mafaili wa zamani pamoja na uhamishaji wa taarifa za wenye viwanja kwenye mfumo wa kompyuta. Pia alikagua mifumo ya uuzaji viwanja kwa njia ya mtandao ambayo hata hivyo bado haijakamilika.

Wakati huo huo,Waziri Mkuu amepokea mchango wa zaidi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Wilaya wa Kongwa, Bw. Deogratius Ndejembi zikiwa ni kwa ajili ya wakazi wa mkoa wa Kagera walioathirika kwa tetemeko la ardhi lilitokea Septemba 10, mwaka huu.

Pia Waziri Mkuu amepokea mchango mwingine wa zaidi ya sh. milioni tano kutoka kwa makundi mbalimbali ya wafanyabiasha wa Manispaa ya Dodoma wakiwemo wamiliki wa hoteli, nyumba za kulala wageni, waendesha bodaboda na madereva wa daladala.

Akipokea msaada huo, Waziri Mkuu amewashukuru wafanyabiashara hao na kuwahakikishia kwamba fedha hizo zitapelekwa mkoani Kagera na kuwafikia walengwa kama ilivyokusudiwa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
S. L. P. 980,
DODOMA.
ALHAMISI, OKTOBA 6, 2016

SHULE YA SEKONDARI TUSIIME YAPIGWA FAINI YA MILIONI KUMI KWA UCHAFUZI WA MAZINGIRA

$
0
0
 Naibu Wziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina alipokuwa akifanya ziara ya kukagua mazingira katika shule ya secondary Tusiime iliyopo tabata jijini Dar es salaam mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi ya utililishaji maji taka kwenye makazi ya watu kutoka shuleni hapo.                
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina (katikati)  akipata maelezo ya jinsi gani mfumo wa utililishaji  maji taka unavyofanya kazi katika shule ya secondary Tusiime.                    
Naibu Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuipiga faini ya million kumi shule ya secondary Tusiime iliyopo Tabata jijini Dar es salaam kwa uchafuzi wa mazingira

DC LONGIDO DANIEL CHONGOLO ASHIRIKI UJENZI WA MADARASA MAWILI

$
0
0


Mkuu wa Wilaya ya longido Ndugu Daniel Godfrey Chongolo akishiriki ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Lanchi iliyopo wilayani humo.

Ndugu Daniel Godfrey Chongolo ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Longido akiweka Jiwe kwenye msingi wa nyumba wakati akishiriki Ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Lanchi.
....................

Mkuu wa wilaya ya Longido Bw. Daniel Godfrey Chongolo ameshiriki ujenzi wa madarasa mawili katika shule ya msingi Lanchi iliyopo wilayani Longido. Shule hiyo ambayo ina wanafunzi mpaka wa darasa la tano, ilikuwa na madarasa mawili tu jambo lililosababisha shughuli za utoaji elimu kwa wanafunzi kuwa ngumu.

Katika kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa, Mkuu wa Wilaya akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido Bw. Jumaa Mhina wamefanya kazi ya ujenzi kwa kushirikiana na wananchi siku nzima ya leo. Katika hatua nyingine mkuu huyo wa Wilaya ya Longido aliendesha harambee iliyofanikisha kupatikana kwa jumla ya shilingi milioni 10.
Wananchi wilayani Longido wakiwa katika harakati za Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa kwenye shule ya Msingi Lanchi, baada ya kuhamasishwa na mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Daniel Godfrey Chongolo.

Kazi ya Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Msingi Lanchi wilayani Longido ikiendelea..
Mkuu wa Wilaya ya Longindo Ndugu Daniel Godfrey Chongolo akiendelea kushiriki Ujenzi wa vyumba viwili vya Madarasa katika Shule ya Msingi Lanchi.

ISHU YA WALIMU WALIOMPIGA MWANAFUNZI MBEYA DAY,MKUU WA SHULE AVULIWA MADARAKA


TAZAMA SHUGHURI NZIMA YA TUKIO LA RAIS DKT. MAGUFULI ALIPOFUNGUA RASMI KIWANDA CHA KUSINDIKA MATUNDA CHA BAKHRESSA FOOD PRODUCTS LTD. MKURANGA, MKOANI PWANI LEO

$
0
0
 Waziri wa viwanda,  Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage (kushoto) na katibu Mkuu wake Dkt. Adelhelm Meru wakiongea na Mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa Group Mzee Said Salim Bakhresa wakati wakimsubiri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili kwenye sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
 Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Bakhressa Bw. Abubakar Bakhresa (kushoto) akibadilishana mawazo na maafisa waandamizi wake wakati wakimsubiri Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili kwenye sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage kwenye sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na  Mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa Group  Mzee Said Salim Bakhresa kwenye sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe Filberto Hassan Sanga  alipowasili kwa ajili ya  sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na  Katibu Mkuu Waziri wa viwanda,  Biashara na Uwekezaji  Dkt. Adelhelm Meru  alipowasili kwa ajili ya  sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Joseph Malongo
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na Mbunge wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Bakhressa Bw. Abubakar Bakhresa 
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Bakhressa Bw. Abubakar Bakhresa 
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na Mtendaji Mkuu (CEO) Wa  Bakhresa Food Products LTD Bw. Salim Aziz Salim  
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na mmoja wa Watendaji wa Bakhresa  Group Bw. Aziz Salim  
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na mmoja wa maafisa waandamizi   Bakhresa Food Products LTD 
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akilakiwa na mmoja wa maafisa waandamizi   Bakhresa Food Products LTD 
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, kamanda Boniventure Mushongi 
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na viongozi wa mkoa wa pwani
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuzindua rasmi  kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
 Mbunge wa Mkuranga Mhe Abdallah Ulega akifurahia baada ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuzindua rasmi  kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa baada ya kukizindua rasmi  kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa baada ya kukizindua rasmi  kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa baada ya kukizindua rasmi  kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na kupata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufian Ally kuhusiana na hatua mbalimbali za usindikaji wa matunda katika kiwanda hicho kilichopo Mwandege mkoani Pwani.
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa baada ya kukizindua rasmi  kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
  Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufian Allyakitoa muhtasali  wa shughuli wakati wa ufunguzi  rasmi wa kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Products kijijini Mwandege wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani leo Oktoba 6, 2016
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiteta jambo  na  Mwenyekiti wa makampuni ya Bakhresa Group  Mzee Said Salim Bakhresa
 Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Bakhresa Bw. Abubakar Bakhresa akisoma risala kwenye shere hizo
 Mbunge wa Mkuranga Mhe abdallah Ulega akisema machache
 Wafanyakazi na wageni waalikwa
 Wafanyakazi na wageni waalikwa
 Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akisoma ripoti kuhusu viwanda na uwekezaji mkoani humo
 Mshereheshaji Charles Hilary akiwa kazini
 Wafanyakazi na wageni waalikwa
 Waziri wa viwanda,  Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage akiongea machache kabla ya kumkaribisha Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuhutubia
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia wakati wa sherehe hizo
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia wakati wa sherehe hizo

 Wafanyakazi na wageni waalikwa wakimsikiliza Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akihutubia wakati wa sherehe hizo

 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiendelea kuhutubia wakati wa sherehe hizo

 Wafanyakazi na wageni waalikwa
 Wafanyakazi na wageni waalikwa
 Wafanyakazi na wageni waalikwa
 Wafanyakazi na wageni waalikwa
 Wafanyakazi na wageni waalikwa
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiendelea kuhutubia wakati wa sherehe hizo

  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiendelea kuhutubia wakati wa sherehe hizo

  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiendelea kuhutubia wakati wa sherehe hizo
 Mbunge wa Mkuranga Mhe Abdallah Ulega akimshukuru  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  kwa kutambua mchango wake katika kuleta maendeleo jimboni wakati akiendelea kuhutubia

 Mbunge wa Mkuranga Mhe Abdallah Ulega akimshukuru  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  kwa kutambua mchango wake katika kuleta maendeleo jimboni wakati akiendelea kuhutubia
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na    Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufian Ally  baada ya kuzindua rasmi kiwanda hicho na kisha kuhutubia wakati wa sherehe hizo
     Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiaga baada ya kuzindua rasmi kiwanda hicho na kisha kuhutubia wakati wa sherehe hizo
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya kumbukumbu na meza kuu
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya kumbukumbu na meza kuu na baadhi ya viongozi wa mkoa wa pwani
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya kumbukumbu na meza kuu na baadhi ya viongozi wa mkoa wa pwani
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya kumbukumbu na meza kuu na maafisa waandamizi  wa Bakhressa Group
 Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya kumbukumbu na meza kuu na wafanyakazi wa Bakhressa Food Products Ltd. 
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya kumbukumbu na meza kuu na wafanyakazi wa Bakhressa Food Products Ltd. 
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya kumbukumbu na meza kuu na wafanyakazi wa Bakhressa Food Products Ltd. 
  Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya kumbukumbu na meza kuu na wanahabari waliohudhuria na wa Azam Media
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  katika picha ya kumbukumbu na meza kuu na wanahabari waliohudhuria na wa Azam Media

   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana na Bw. Charles Hilary wa Azam TV Bw. Dunstan Tido Mhando
   Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiagana Bw. Dunstan Tido Mhando. PICHA NA IKULU

TANESCO YATILIANA SAINI MIKATABA YA KUJENGA NJIA YA UMEME WA KILOVOTI 400.

$
0
0

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said.
SHIRIKA la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), limesaini mkataba na makampuni matatu kujenga njia ya umeme, (Transmission lines), wa Msongo wa Kilovolti 400 utakaounganisha Tanzania na Kenya.

Hafla ya kutiliana saini mikataba hiyo, imefanyika leo Oktoba 7, 2016 makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, ambapo Shirika hilo la Umeme linalomilikiwa na serikali, limetiliana saini mikataba hiyo na makampuni ya Bouygues Energies Service, Energoinvest na Kalpa-Taru.

Akizungumz wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Felchesmi Mramba, alisema, Ujenzi wa Mradi huu wenye urefu wa Kilomita 414, utaanzia Mkoani Singida,-Babati-Arusha hadi Namanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.

Kisha Mradi utaunganishwa na njia ya Msongo wa Kilovolti 400 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka eneo la Isinya, Nairobi, nchini Kenya hadi eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya, (Namanga) ambapo utaunganisha na njia ya umeme wa wa Msongo wa Kilovolti 400kv kwa upande wa Tanzania.

“ Napana niwahakikishie, kuwa huu ni mfululizo wa miradi mikubwa inayotekelezwa na TANESCO na utawezesha usafirishaji wa umeme wa Mgawati 2000 katika pande zotekenya na Tanzania”. Alifafanua Mramba.

Akifafanua zaidi, Mhandisi Mramba alsiema, utekelezaji wa mradi huu unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB), na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya Dola za Kimarekani, Milioni 309.26 utakamilika katika kipindi cha miezi 24, sawa na miaka 2.

“Dola za Marekani Milioni 258.82, zitatumika kujenga upande wa Tanzania na  Dola za Kimarekani Milioni 50.45 zitatumika kujenga mradi upande wa Kenya,” alifafanua Mhandisi Mramba.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo Mtendaji alitoa onyo kwa wakandarasi waliopewa kazi hiyo kuitekeleza kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.
“ Angalizo, kwenu ninyi wakandarasi, kamilishini mradi ndani ya muda kama ambavyo tumekubaliana kwenye mkataba, kushindwa kukamilisha ujenzi kwa mujibu wa mkataba ni kushindwa kufanya kazi na sisi kama TANESCO hatutakubaliana na hilo.” Alionya Mhandisi Mramba.

Naye mwakilishi Mkazi wa (AfDB), Tonia Kandiero, alitoa hakikisho kuwa benki hiyo itaendelea kusaidia miradi mikubwa kama hii, kwa manufaa ya eneo lote la Afrika.

Kwa upande wake, MAfisa Miradi msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, naye aliungana na AfDB, kutoa hakikisho la ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na JICA, katika kusaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kama huu uliosainiwa leo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania, (TANESCO), Felchesmi Mramba, (kushoto), akibadilishana hati za mkabata na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton baada ya kusini, mradi wa ujenzi wa njia ya umeme (transmission line) itakayounganisha Tanzania na Kenya, makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2016. Shirika hilo limeingia mkataba na makampuni matatu kutekeleza mradi huo (KTPIP), wa Msongo wa KV400 unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya dola za Kimarekani
309.26.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton wakisaini mkataba huo
 Mhandisi Mramba, (kushoto), na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, wakisaini mkataba
 Mhandisi Mramba, akibadilishana hati na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, baada ya kusaini mkataba
 Mhandisi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakisaini mkataba kutekeleza mradi huo
 Mhandisi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakibadilishana hati
 Mkurugenzi Mkazi wa AfDB nchini, Tonia Kandiero, akizungumza kwenye hafla hiyo
 Mhandisi Mramba, (kulia) na Kandiero, wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo
 Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Bibi. Kandiero
 Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, (kushoto), akizungumza
Mhandisi Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Bi. Rosina wa JICA
 Mhandisi Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, akizungumza kwenye hafla hiyo
 Mratibu wa Miradi wa Shirika la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Khalid James, (kulia), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Mramba, (wasaba kushoto), akipongezwa na Mwakilishi mkazi wa AfDB, hapa nchini, Tonia Kandiero, wakati wa picha ya pamoja na wawakilishi wa makampuni yaliyopata kandarasi ya ujenzi wa mradi huo
 Kutoka kushoto, Patrick Canton, S.K. Sarotra, Apolei Rosina, Mhandisi Mramba, Tonia Kandiero na Bisera Hadzialjevic, wakiwa katika picha ya pamoja mwishoni mwa hafla hiyo
 Afisa Mawasiliano na Uhusiano wa TANESCO, Henry Kilasila, (kualia), akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Felchesmi Mramba.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, (Uwekezaji), Mhandisi Decklan P.Mhaiki, akiwakaribisha wageni kwenye hafla hiyo.
Meneja mradi huo wa KTPIP, Mhandisi Mhandisi Lewanga Tesha, (kulia), akiwa na wawakilishi wa kampuni ya KALPA-TARU
TANESCO YATILIANA SAINI MIKATABA YA KUJENGA NJIA YA UMEME WA KILOVOTI 400 UTAKAOUNGAMISHA MIJI YA SINGIDA, ARUSHA NA NAMANGA NCHINI KENYA.

SHIRIKA LA ENGENDER HEALTH WAMKARIBISHA RAIS WAO HAPA NCHINI ALIPOTEMBELEA.

$
0
0
 Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la EngenderHealth, Ulla Muller akizungumza na wadau wa afya pamoja na wadau wa elimu katika hafla fupi ya kumkaribisha hapa nchini.
Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la EngenderHealth, Ulla Muller akizungumza na wadau wa afya na wadau wa Elimu  kuhusiana na Uzazi wa Mpango wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwaajili ya Kumkaribisha hapa nchini.
Naibu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la EngenderHealth, Feddy Mwanga akizungumza na wadau wa Afya na elimu wakati wa kumkaribisha Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la EngenderHealth, Ulla Muller jijini Dar es Salaam.
 Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la EngenderHealth, Ulla Muller akizungumza na wadau wa afya pamoja na wadau wa elimu katika hafla fupi ya kumkaribisha hapa nchini.
 Mkurugenzi Mkazi wa shirika la EngenderHealth hapa nchini, Richard Killian akibadilishana mawazo na baadhi ya wadau wa afya na elimu katika hafla ya Kumkaribisha Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la EngenderHealth, Ulla Muller hapa nchini.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA JAMHURI YA CZECH ATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

$
0
0

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni(kulia), akimsikiliza Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek wakati wa mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia njia za mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu.Mazungumzo yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akizungumza na Ujumbe
kutoka Jamhuri ya Czech, ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(wa kwanza kushoto), wakati wa mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu. Mazungumzo yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.

Mjumbe kutoka Jeshi la Polisi,Kamishna Albert Nyamhanga akijitambulisha kabla ya kuanza mazungumzo kati ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Czech na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu.Meza kuu ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Hamad Masauni(kushoto) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek.Mazungumzo yalifanyika jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, akipokea zawadi kutoka
kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech, Ivan Jancarek(kushoto), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana na uhalifu. Mazungumzo yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Jamhuri ya Czech nchini Kenya, Pavel Rezac, akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni(kulia), baada ya kumaliza mazungumzo yaliyohusu kuimarisha uhusiano katika masuala ya usalama kupitia mafunzo, teknolojia na mbinu za kukabiliana
na uhalifu.Katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje kutoka Jamhuri ya Czech,
Ivan Jancarek Mazungumzo yalifanyika ofisini kwa naibu waziri,jijini Dar es Salaam.

(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

WAFANYABIASHARA WA CONGO WAIPONGEZA SERIKALI YA TANZANIA.

$
0
0
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Congo (DRC) nchini Tanzania Bw. Sumail Edward (kulia) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa wafanyabiashara wa Congo kutumia Bandari ya Dar es Salaam baada ya Serikali kuondoa vikwazo, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bw. Tiganya Vincent.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Congo (DRC) nchini Tanzania Bw. Sumail Edward (mwenye suti) wakati alipokuwa akielezea kuridhika na uamuzi wa Serikali ya Tanzania kuondoa vikwazo katika Bandari ya Dar es Salaam na kupelekea wafanyabiashara wa Congo (DRC) kuendelea kuitumia bandari hiyo.

Picha na Eliphace Marwa – Maelezo

Na: Frank Shija, MAELEZO.

WAFANYABIASHARA kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wafurahishwa na hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuondoa vikwazo vya usafirishaji wa mizigo kupitia Bandari ya Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Wafanyabiashara wa Congo waishio nchini Tanzania Bw. Sumaili K. Edward alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kurejea kwao na kutumia Bandari hiyo leo Jijini Dar es Salaam.

Sumaili amesema kuwa miaka ya nyuma kulikuwa na changamoto nyingi ambapo alizitaja kuwa ni mizani na sehemu za ukaguzi kuwa nyingi pamoja na siku za kuhifadhi mizigo kuwa chache.

Alisema kuwa wamefikia uamuzi wa kuendelea kutumia Bandari ya Dar es Salaam baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kutatua changamo hizo ambapo sasa vizuizi vimepungua.

“Naipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua ya kutuondolea usumbufu sisi wafanyabiashara wa Congo tuliokuwa tunafanya shughuli zao Bandari ya Dar es Salaam, tumerejea na tutapitishia mizigo yetu hapa”. Alisema Sumaili.

Adhai alisema kuwa wamefarijika kuona sasa siku za kuhifadhi mizigo kabla ya kuongezeka kutoka siku 15 zilizokuwepo awali hadi kufikia 30 kama ilivyobainishwa wakati wa ziara ya siku tatu ya Rais wa Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila mapema wiki hii.

Akijibu swali la la mwandishi wa habari aliyetaka kujua sababu zilizowafanya kusitisha kwa muda kutumia Bandari ya Dar es Salaam, Rais huyo alisema kuwa kitu kikubwa kilicho wafanya wachukue uamuzi wa kusitisha ni gharama kuwa kubwa hivyo kupelekea kufanya biashara isiyokuwa na faida.
Viewing all 46313 articles
Browse latest View live




Latest Images