Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 999 | 1000 | (Page 1001) | 1002 | 1003 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwahutubia Wanasayansi watafiti (Hawapo pichani) walioshiriki kongamano la 30 Jijini Dar es Salaam wakati wa kufunga kongamano hilo la siku tatu.
   Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela akielezea machache kabla ya kumwalika mgeni rasmi  kufunga mkutano huo
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpa shada la maua mmoja wa Staff member kwa namna walivyoweza kuandaa kongamano hilo
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi shada la maua mmoja wa wafanyakazi wa NIMR kwa namna walivyoweza kufanikisha shughuli hiyo.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimpongeza mmoja wa Wanasayansi Vijana waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hilo
   NNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi tuzo mmoja wa Wanasayansi waliofanya vizuri katika tuzo zinazotolewa kila mwaka na kongamano hino hilo
   Baadhi ya washiriki wakifuatilia kongamano hilo
  Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefunga rasmi Kongamano la 30 la Kimataifa la Wanasayansi Watafiti lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) lililokuwa la siku tatu Jijini Dar es Salaam.  Naibu Waziri Dk. Kigwangalla amewaeleza wanasayansi hao watafiti kuwa Serikali inashirikiana nao bega kwa bega katika jukumu la maendeleo hapa nchini hivyo  uwepo wao ni kielelezo tosha cha maendeleo ya Taifa na watu wake hasa katika Nyanja za kiuchumi, Afya, Mazingira na mambo mengine  ya kimaendeleo.  Aidha, amebainisha kuwa changamoto za magonjwa ya virusi yanayotokana na Mbu ambapo ameahidi amewahidi wanasayansi hao na Wizara yake kushirikiana nao katika kulipitia ufumbuzi.  Dk.Kigwangalla amewahakikishia Wanasayansi hao  kuwa, masuala yote ya kuimalisha huduma za Maabara katika ngazi za msingi kwani suala hilo amekuwa akilifanya kila mahala anapokwenda kwenye ziara zake juu ya upatikanaji wa huduma  Maabara bora kwenye sehemu za Afya.  “Nimependa maombi yenu haya juu ya kuimalisha huduma za Maabara kwenye ngazi za msingi. Suala hili nimekua nikilifuatilia kila ziara zangu kwenye vituo vya Afya na Hospitali zote hivyo nitalibeba hili na nitaendelea nalo kwa sababu nina aamini kutoa huduma za afya bila kuwa na huduma madhubuti za Maabara ni kuchezea afya za watanzania wenzetu, Ni lazima tuwe na huduma bora za Maabra zetu na suala hili tutakaa mimi na Mh. Waziri kuona namna ya kufanyia maboresho zaidi.” Amesema Dk.Kigwangalla.  Aidha,  Dk. Kigwangalla aliwatunukia vyeti maalum wanasayansi  Vijana walioshiriki kwenye kongamano hilo.  Kongamano  hilo  la siku tatu, Oktoba 4-6, awali lilizinduliwa na Makamu wa Rais Mh. Mama Samia Suluhu Hassan ambaye pia aliwahakikishia Wanasayansi Watafiti hao  kuwa Serikali inatambua mchango wao na wataendelea na juhudi za kuwalinda kwani ni nguzo muhimu ya kufikia malengo ya millennia ya ukuaji wa kiuchumi.  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dk. Mwele Malecela amesema kufikia tamati ya kongamano hilo ni ishara tosha maandalizi yake yalikuwa mazuri na washiriki wote walioshiriki wamejifunza mengi  huku wakiwa ni mfano wa kuigwa kwa elimu walioipata hapo.  Nchi  mbalimbali za Afrika, Ulaya na Amerika ambapo  washiriki zaidi ya 300 wameshiriki  huku mada zaidi ya 220 zikiwasilisishwa na kujadiliwa kwa pamoja na wataalam hao.  Nchi ambazo zinashiriki kongamano hilo kuwa ni Afrika Kusini, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda, Australia, Denmark, Ubeljiji, Uholanzi, Uingereza, Ujerumani, Uswis, Kanada, Sweden, Norway, Marekani, Bangladesh, Thailand na wenyeji Tanzania.

  0 0


  0 0   

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akiongea na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje ya nchi alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 7, 2016   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 07 Oktoba, 2016 amekutana na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani ambapo pamoja na mambo mengine ametaka utekelezaji wa diplomasia ya uchumi utiliwe mkazo katika uwekezaji kwenye sekta ya viwanda.

  Katika Mkutano huo uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Magufuli aliyehutubia na kuongoza majadiliano juu ya masuala mbalimbali ya shughuli za mabalozi, amesema Tanzania imeweka dhamira ya kuikuza sekta ya viwanda kutoka ukuaji wa asilimia 7.3 hadi kufikia asilimia 15 ifikapo mwaka 2021 na kuzalisha ajira kwa asilimia 40.

  "Sasa nimeona niwaite waheshimiwa Mabalozi ili tuelewane, mjue mwelekeo tunaoutaka na mjue ni namna gani mtakavyoshiriki kuhamasisha uwekezaji wa viwanda.

  "Nataka badala ya kubaki mmejifungia ofisini, mtoke mwende mkawatafute wawekezaji waje wawekeze katika viwanda ili nchi yetu inufaike kwa watu wetu kupata ajira, Serikali kukusanya kodi na tuinue maendeleo yetu"amesema Rais Magufuli.

  Maeneo mengine ambayo Rais Magufuli ametaka Mabalozi wayafanyie kazi ni kutangaza na kuwavutia watalii kuja hapa nchini, kufanyia kazi fursa zote zenye manufaa kwa Tanzania katika nchi wanakowakilisha, kulinda mali za nchi zilizopo katika nchi hizo na kufuatilia utekelezaji wa mikataba ya biashara na uwekezaji inayofanywa kati ya Tanzania na nchi wanakowakilisha.

  Pia Rais Magufuli amewataka waheshimiwa Mabalozi wote kufanya kazi kwa juhudi, kuondoa kasoro za utendaji kazi ambazo zimekuwa zikilalamikiwa katika ofisi zao na kubana matumizi ya fedha yasiyokuwa ya lazima.

  Dkt. Magufuli ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kujipanga na kudhibiti mianya yote ya matumizi mabaya ya fedha za umma ambazo zimekuwa zikitumika katika safari za nje ya nchi na matumizi mengine yasiyo ya lazima, pamoja na kuhakikisha watumishi wote ambao wapo katika ofisi za ubalozi kwenye nchi mbalimbali bila sababu za msingi wanarejeshwa nchini ili kupunguza mzigo wa gharama kwa Serikali.

  "Kuna wafanyakazi wapo kwenye Balozi zetu wakati hata sifa za kuwa katika nafasi wanazoshikilia hawana, ilifika mahali mtu akiharibu hapa nyumbani anapangiwa ubalozini.
  "Wakati mwingine unakuta ubalozi wa Tanzania kwenye nchi fulani una idadi kubwa ya wafanyakazi kuliko mahitaji ya ubalozi huo, haiwezekani"amesisitiza Rais Magufuli.

  Hata hivyo Dkt. Magufuli amewapongeza Mabalozi wote wa Tanzania kwa kazi wanazozifanya kwenye nchi wanazowakilisha na amewahakikishia kuwa Serikali ina matumaini nao na inawategemea kuwa wataendelea kuiwakilisha na kuitangaza vizuri Tanzania.

  Mkutano huo pia umehuduriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa Taasisi mbalimbali na Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  07 Oktoba, 2016

  0 0

   Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alipotembelea wodi ya wanawake
  Watumishi, wauguzi na madaktari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alipozuri katika hospitali ya Manispaa ya Ubungo kwa ziara ya kikazi
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasili Ofisi za Manispaa ya Ubungo.
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Akitoa maelekezo wakati akikagua ufanisi wa kazi katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini maelezo ya jinsi wanawake wanavyohudumiwa katika wodi ya wanawake

  Na Mathias Canal, Dar es salaam

  Duka la Dawa za Binadamu lililopo katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo iliyopo katika Mtaa wa Sinza Jijini Dar es salaam limekutikana na unadhilifu wa fedha za Umma kinyume na utaratibu wa matumizi ya fedha hizo.

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ameyabaini hayo baada ya kukagua mapato na matumizi ya Duka hilo na kugundua uwapo wa ubadhilifu huo mdogo mdogo ambao ameahidi kutuma mkaguzi wa ndani ili kukagua hesabu za duka hilo.

  MD Kayombo amebainisha hayo wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Hospitali hiyo mara baada ya kuzuru na kuwa na kikao cha pamoja ili kukumbushana majukumu ya kazi ikiwa ni pamoja na kujitambulisha ili kisikiliza kero za watumishi hao na kuzitafutia ufumbuzi.

  Kayombo amebaini kuwa Duka hilo la Dawa za binadamu katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo lina Account mbili zilizofunguliwa kwa ajili ya matunzo ya fedha za mauzo jambo ambalo sio sahihi kisheria katika Taasisi moja ya serikali kuwa na Account mbili za Bank.

  MD Kayombo ameahidi kubadilisha Mfumo wa kukusanya Mapato katika Hospitali hiyo kuhamia mfumo wa kisasa ili Serikali iweze kukusanya fedha za kutosha ambapo mfumo wa sasa mapato mengi yanapotea kwani kufanya hivyo itarahisisha Hospitali hiyo kuweza kujisimamia katika maswala ya matumizi madogo madogo na kuweza kuongeza uwezo wa kunua dawa za kutosha kwa mahitaji husika.

  Kuhusu kutoa na kupokea Rushwa MD Kayombo amesema kuwa hakuna asiyetambua kuwa jambo hili linawanyima haki wananchi wengi wanyonge hivyo watumishi wote katika Hospitali hiyo wameonywa kujihusisha na kadhia hiyo kwani endapo mtumishi yeyote atabainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo ili kuwa fundisho kwa wengine.

  "Watumishi wote mnatakiwa kuwa Clean Officials katika mazingira ya kazi hivyo ni lazima kujiepusha na ubadhilifu wa fedha za Umma kwani kila mmoja anapaswa kuridhika na kipato anachopata, Pia nawaahidi kila mmoja kumpatia Extra Duty Allowance kulingana na Bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017.

  MD Kayombo ametembelea Wodi zote Hospitalini hapo na kujionea hali halisi ya utoaji huduma ambapo pia ametembelea Ofisi zote zinazotoa huduma na kukutana na wataalamu mbalimbali ambapo wameelezea changamoto zao jambo ambalo Mkurugenzi huyo ameahidi kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo kwani lipo ndani ya uwezo wake.

  Md Kayombo Amewaonya Wakuu wa Idara kuacha tabia ya kuwanyanyasa na kuwagawa watumishi katika sehemu za kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi katika kuwahudumia wananchi.

  Kwa upande wao baadhi ya watumishi katika Hospitali hiyo wamempongeza Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Ubungo kwa ziara yake katika Hospitali hiyo kwani amekuwa Mkurugenzi wa kwanza kuzuru Hospitalini hapo na kujionea hali halisi ya utoaji huduma na sio kusimuliwa.

  MD Kayombo ametoa namba ya simu kwa ajili ya matumizi ya dharura kwa watumishi hao ili waweze kuripoti matukio ya haraka ambayo yanakuwa nje ya uwezo wao.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano,January Makamba kushoto akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso wakati alipofanya ziara wilaya ya Pangani kuangalia maeneo kutakapojengwa ukuta wa mto Pangani na Upandaji wa Miti ya Mikoko.

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano,January Makamba akisisitiza jambo kwa watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Pangani kuhusu kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa ili kuweza kusaidia ukuaji wa uchumi kulia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano,January Makamba akisisitiza jambo kwa watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Pangani kuhusu kufanya kazi kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Pangani(CCM) Jumaa Aweso kulia ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano,January Makamba akisisitiza jambo kwa watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Pangani kuhusu kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Issa
   Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Mayungi akisisitiza jambo kwaWaziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano,January Makamba kuhusu hatua wanazochukua kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo Mto Pangani
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano,January Makamba katikati akitazama namna mto Pangani ulivyoliwa kutokana na mabadiliko ya Tabia ya nchi wakati alipofanya ziara ya kuutembelea leo kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso kulia ni Afisa Misitu na Kiungo wa Mradi huo wilayani Pangani Twahiru Mkongo
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano,January Makamba katikati akitazama namna mto Pangani ulivyoliwa kutokana na mabadiliko ya Tabia ya nchi wakati alipofanya ziara ya kuutembelea leo kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso kulia ni Afisa Misitu na Kiungo wa Mradi huo wilayani Pangani Twahiru Mkongo
   Afisa Misitu na Kiungo wa Mradi huo wilayani Pangani Twahiru Mkongo akimuonyesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano,January Makamba katikati maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mabadiliko ya tabia ya nchi kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso kulia ni

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba  wa pili kutoka kushoto akitembelea maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mabadiliko ya tabia ya nchi kwenye katika Pangani kushoto  ni  Afisa Misitu na Kiungo wa Mradi huo wilayani Pangani Twahiru Mkongo
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba wa pili kutoka kushoto akiangalia maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mabadiliko ya tabia ya nchi


   Hili ni miongoni mwa maeneo ya ukuta wa mto Pangani yaliyo athiriwa na mabadiliko ya tabia ya nchi
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba akitembelea maeneo mbalimbali kujionea athari za mabadiliko ya tabia ya nchi
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea kujionea namna ukuta wa mto Pangani ulivyoliwa kutokana na mabadiliko ya nchi


   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba katikati akiangalia taarifa ya mradi wa Ujenzi wa Ukuta wa Mto Pangani mara baada ya kuutembelea leo  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba kushoto akiwa amekaa kwenye jahazi mara wakati alipofanya ziara ya kutembelea wilayani Pangani na Ukata wa Mto Pangani ambao umeliwa na maji kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi


   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba kushoto akisisitiza jambo Waziri Amiri ambao walikutwa wakiendelea na shughuli zao pembezoni mwa mto Pangani   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba wa tatu kutoka kushoto akimsikiliza kwa umakini Diwani wa Kata ya Pangani Mashariki Akida Boramimi 

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba kushoto akisisitiza jambo kwa Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso wakati wa ziara hiyo katikati ni  Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Mayungi

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano, January Makamba akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara yake hiyo leo hii
  </ Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam kwa minajili ya kuzungumza na Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akingia kwenye ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam kwa minajili ya kuzungumza na Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje
   Sehemu ya makatibu wakuu na mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje wakiwa ukumbini
   Sehemu ya mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje wakiwa ukumbini
   Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Luteni Jenerali Venance Mabeyo (kati) na  Bw. Alphayo Kidata, Kamishna Mkuu wa TRA (kulia) na maofisa wengine waandamizi wakiwa ukumbini
    Sehemu ya mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje wakiwa ukumbini
    Sehemu ya maofisa Ubalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje wakiwa ukumbini
   Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari (kulia) na maofisa wengine ukumbini hapo
    Sehemu ya maofisa Ubalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje wakiwa ukumbini
   Kaimu  Mkurugenzi  Idara ya Itifaki Bw.. James Bwana akiwa na mabalozi wakurugenzi wa Idara mbalimbali Wizarani
   Balozi wa Tanzania nchini Urusi Luteni Generali Wyjones Kisamba akisimama wakati mabalozi wakitambulishwa 
    Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Mhe,Wilson M.Masilingi akitambulishwa
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe Angela Kairuki, Katibu mkuu wake Dkt. Laurian  Ndumbaro, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad na viongozi wengine wakiwa ukumbini

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Ponary Mlima akiwatambulisha mabalozi
   Sehemu ya mabalozi hao
   Wajumbe wa mkutano huo
   Mabalozi
   Wajumbe wa mkutano
   Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
   Maofisa toka Sekretarieti ya Maadili,
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisoma risala yake
   Wajumbe wakifuatilia kwa makini
   Waziri Mkuu Mhe Kasssim Majaliwa akiongea na wajumbe
    Waziri Mkuu Mhe Kasssim Majaliwa akiongea na wajumbe
   Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na wajumbe
   Sehemu ya Mabalozi ambao ni wakurugenzi wa Idara mbalimbali
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wajumbe
   Sehemu ya mabalozi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
   Mabalozi wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea na hotuba
   Mabalozi wakinakiri kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
   Mabalozi wakinakiri kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
   Mabalozi wakinakiri kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
   Mabalozi wakinakiri kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
   Kila mtu alikuwa makini wakat wa hotuba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
   Kila mtu alikuwa makini wakat wa hotuba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
   Kila mtu alikuwa makini wakat wa hotuba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo

   Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe. Dorah Msechu akisimama baada ya kupongezwa na Rais Dkt. Magufuli kwa juhudi zake za kupatia makazi watumishi ubalozini
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipongezwa na Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa baada ya kuhutubia
   Wajumbe wakipongea hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo
   Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka akichangia katika mjadala kuhusu changamoto zinazozikabili balozi zetu nje ya nchi 
   Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa wakurugenzi 
   Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davies Mwamunyange akichangia katika mjadala
   Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu akitoa mchango wake
   Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba akichangia 

   Kamishana wa Tume ya Maadili ya Viongozi, Jaji Mstaafu, Salome Kaganda akichangia
   Mabalozi akifuatilia uchangiaji katika mkutano huo
   Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad akichangia
   Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akfafanua jambo
   Naibu waziri, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangwalla akichangia
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Ponary Mlima akichangia

   Kamimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari akitoa ufafanuzi wa masuala ya uwekezaji
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko 
   Mabalozi wakifuatilia michango
   Mabalozi wakifuatilia michango
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko 
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi akiongea meza kuu
   Mabalozi wakifuatilia
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiongea meza kuu
   Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea meza kuu
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wajumbe
   Wajumbe wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad baada ya mkutano kwisha
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe Angela Kairuki
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Kamishana wa Tume ya Maadili ya Viongozi, Jaji  (Mstaafu) Salome Kaganda
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kaimu Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Victoria Lembeli 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na  Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Dkt Modestus Francis Kapilimba
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davies Mwamunyange
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Tanzania mchini Ujerumani Mhe.Philip Marmo 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Zambia Mhe. Mhe.  Grace Mujuma
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Sweden Mhe Dorah Msechu
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe. Naimi Aziz
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na mwakilishi wa kudumu wa Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu waziri, wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangwalla 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Tanzania Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Kuwait Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi Radhia Msuya
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe  Rajabu Hassan Gamaha
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Balozi wa Tanzania Marekani Mhe. Wilson Masilingi
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Tanzania Urusi Luteni Generali (mst.) Wyjones Kisamba 

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi  wa Tanzania nchini Canada Mhe. Jack Mugendi Zoka 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mabalozi
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na balozi
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe Mathias Chikawe 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Dorothy Mwanyika
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Ponary Mlima 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi 
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha na meza kuu na mabalozi

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha na meza kuu na mabalozi

    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha na meza kuu na wakuu wa Taasisi mbalimbali

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika picha na meza kuu na Wakurugenzi wa Wizara ya mambo ya Nje.
  PICHA ZOTE NA IKULU


  0 0

  Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Dangotte, Harpreet Duggal (kulia) akimwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) sehemu ya kiwanda hicho.
  w2
  Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Dangotte, Harpreet Duggal (kulia) akimwonesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (kushoto) roboti maalum ya kuchukua sampuli mbalimbali  za kemikali/udongo  kwenye maabara ya kiwanda hicho (haipo pichani)
  w3
  Mtalaam kutoka Kiwanda cha Saruji cha Dangotte, Reuben Malambugi (kushoto) akielezea shughuli za kiwanda hicho.
  w4
  Kutoka kulia; Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa, Kamishna Msaidizi wa Madini – Kanda ya Kusini Mhandisi Benjamin Mchwampaka na Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Dk. Shufaa Al- beity  wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Dangotte, Harpreet Duggal (hayupo pichani).
  w5
  Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Saruji cha Dangotte, Harpreet Duggal akielezea shughuli za kiwanda  hicho mbele ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa pamoja na wawakilishi kutoka Wizara  ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Nchini (TANESCO)  na Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) ( hawapo pichani)

  0 0


  Na Humphrey Shao, Blog ya Jamii

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amekutana na wajumbe wa baraza la ardhi la wilaya hiyo na kupanga mikakati ya kutatua migogoro katika kata mbalimbali.

  Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake jana Mjema alisema kuwa kuanzia sasa ataanza kuzunguka na wajumbe hao wa baraza katika kata mbalimbali ili waweze kujionea kwa macho tatizo la migogoro ya ardhi linalo wakabili.

  “Hiki ni kikao cha kawaida tu chenye lengo la kupanga mipango mbalimbali ya kutatua changamoto zinazo wakabili wakazi wa Ilala haswa Migogoro ya ardhi” anasema Dc Mjema

  Alisema lengo la ziara ni pamoja na kujenga mshikamano wa kikazi baina ya wananchi na Watendaji wa Serikali katika kutatua kero zao.
   

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii,Mkuranga 

  MBUNGE wa Mkuranga, Abdallah Ulega, amezindua kisima katika Shule ya Msingi Lupondo, kilichojengwa na African Reflection Foundation. 

  Akizungumza Mara baada ya kuzindua Kisima hicho, amesema kuwa kijiji cha Lupondo kilikuwa na changamoto ya maji kwa muda mrefu. Amesema kuwa wananchi hao walikuwa wakitafuta maji umbali wa kilomita tano na kufanya kuumiza kichwa katika kuwapata wafadhili wa mradi huo. 

  Ulega amesema katika kipindi cha miezi tisa ameweza kupata miradi ya maji katika vijiji sita na kuahidi kuendelea kutafuta miradi ya maji katika vijiji vilivyosalia.Hata hivyo katika uzinduzi huo Mh.Ulega ametoa msaada wa mifuko 10 ya saruji katika msikiti wa kijiji hicho. 

  Nae mratibu wa African Reflection foundation, Shiraz Mohamed, amesema wataendelea kufadhili miradi ya maji katika vijiji vyenye changamoto hiyo. 
  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega,(katikati) akikata utepe wa uzinduzi wa kisima jana katika kijiji cha Lupondo.
  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa kijiji cha Lupondo jana mkoa wa Pwani
  Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Lupondo kabla ya uzinduzi wa kisima cha maji katika kijiji cha Lupondo jana mkoa wa Pwani.

  0 0

  Wananchi wa Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Wilayani Ngorogongoro wakiwa wamefunga barabara kuzuia msafara wa Mkuu wa Mkoa ili waweze kutatuliwa mgogoro ardhi ya Shule ya Msingi pamoja na Zahanati ya Samunge iliyoporwa na wavamizi.
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(tatu kulia) akisikiliza mgogoro wa wananchi wa Samunge baada ya wananchi hao kuzuia msafara wake.
  Mtendaji wa Kata ya Samunge Zacharia Antony (aliyeshika file) akimuonyesha Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo(tatu kulia) barua iliyoandikiwa kinyume cha taratibu na Mkuu wa Kituo cha Polisi Loliondo kumhalalisha mvamizi katika eneo hilo na kuwaamuru wanakijiji kuacha kutombughudi Lemindi Njuda (Mvamizi).
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akienda kukagua eneo la shule ya Msingi Samunge lililovamiwa na Bw. Lemind Njuda (hayupo pichani).
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha (pili kushoto) akionyeshwa mipaka ya eneo la Shule ya Msingi Samunge na viongozi wa kijiji cha Samunge.
  Wadau wa Habari katika picha ya pamoja na Babu wa Samunge Mchungaji Ambilikile Mwasapila(pili kulia) maarufu kama Babu wa Kikombe.
  Babu wa Samunge Mch. Ambilikile Mwasapila (kushoto) akiwa na Nteghenjwa Hosseah mdau wa Habari. Babu wa Samunge ni miongoni mwa wananchi waliozuia Msafara wa Mkuu wa Mkoa.

  ………………………………………………………….

  Nteghenjwa Hosseah ,Loliondo

  Migogoro ya ardhi katika wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha juzi iliingia katika sura mpya baada ya wananchi wa kata ya Samunge wilayani humo akiwemo babu wa kikombe cha dawa, Mchungaji Ambilikile Mwaisapile waliandamana na kufunga barabara na kuzuia msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ili watatuliwe mgogoro wa ardhi ya shule iliyoporwa na diwani mstaafu wa kata hiyo.

  Wananchi hao wakiwa na mabango na majani mabichi walizuia msafara huo ili waweze kusikililizwa kilio chao cha muda mrefu baada ya baraza la kata kuamuru katika kesi yake aprill mwaka huu kuwa ardhi hiyo ni mali ya shule lakini jeshi la polisi Ngorongoro limekuwa likimlinda na kumkingia kifua mvamizi huyo na kukataa kutekeleza amri ya baraza la ardhi kata iliyomtaka kuondoka katika eneo hilo la shule.

  Baadhi ya mabango hayo yalikuwa yakisomeka ” tumeporwa ardhi yetu Mkuu wa Mkoa tusaidie” lingine likisema ”wenye fedha wamepora ardhi ya shule na polisi inawalinda na kuwakingia kifua” na bango lingine lililosomeka ”Mkuu wa Mkoa tunaomba ushuke utusikilize viongozi wa wilaya wote wamenunuliwa”

  Kabla ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha kuteremka kuwasikiliza aliteremka Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashid Taka na Mkuu wa polisi wa wilaya hiyo OCD Warioba kwa lengo la kuwatuliza na kuwasihii kuacha mukari ili waeleza kero zao kwa utulivu na amani bila ya vurugu zozote.

  Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa kata hiyo, Mtendaji wa kata hiyo Zakaria Antony alisema kuwa eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 15 limeporwa na mfanyabiashara na diwani mstaafu Lemindi Njuda ambaye amefanya kilimo cha migomba na shughuli nyingine za kijamii.

  Antony alisema kuwa uamuzi wa kuondolewa kwa diwani huyo wa zamani katika eneo la shule ulitolewa na baraza la ardhi kata aprill mwaka huu lakini jeshi la polisi wilaya ya Ngorongoro limekuwa likimlinda na kugoma kutekeleza amri baraza na badala yake limeandika barua ya kutobugudhiwa katika shamba hilo na hatua kali zinachukuliwa kwa mwananchi atayekiuka amri hiyo.

  Mtendaji huyo aliendelea kusema kuwa wananchi wanashindwa kufanya shughuli za maendeleo hususani ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu kutokana na ufinyu wa eneo la shule hivyo walimuomba Mkuu wa Mkoa kusaidia mgogoro huo ili haki iweze kutendeka kwani polisi imewekwa mfukoni na tajiri huyo.

  Naye Mchungaji Ambilikile Mwaisapile alisema kuwa yeye yuko mstari wa mbele kuhakikisha shule inarudishiwa eneo lake lililoporwa na watu wenye fedha na nguvu za ushawishi kwani mungu hapendi vitu vya dhuruma.

  Mchungaji alisema yeye pamoja na wananchi wa kata hiyo walikuwa wakisaka haki kila ofisi ya wilaya ya Ngorongoro lakini haki hiyo walishindwa kuipata kutokana na mapokezi mabovu ya viongozi wa serikari wilaya ya Ngorongoro.

  Mkuu wa Mkoa Gambo kwa alimwamurisha OCD kufuta nakala ya barua aliyoandika mkuu wake wa kituo cha polisi Loliondo kwani yeye hana mamlaka ya kufanya hivyo bali anapaswa kutekeleza amri ya mahakama ya baraza la kata na sio vinginevyo.

  Gambo pia alimwagiza Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro pamoja na kamati yake ya ulinzi na usalama kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa amri hiyo ili shughuli za maendeleo ya shule hiyo ziweze kufanyika mara moja.

  Alisema na kusikitishwa kuona wananchi wana kero ya kutaka maendeleo lakini viongozi wa serikali kwa kujali matumbo yao na kuendekeza rushwa wako mstari wa mbele kuzuia wananchi kufanya shughuli za ujenzi wa shule.

  Pia Mkuu huyo aliwataka viongozi wa wilaya kumaliza mgogoro mwingine wa ardhi uliopo karibu na zahanati ya kata hiyo ili wananchi waweze kufanya shughuli nyingine za maendeleo na kuacha kukesha kufikiria migogoro ya ardhi kila kukicha ambayo mingi inasababishwa na viongozi.

  Baada ya maelezo hayo wananchi walionyeshwa kufurahishwa na uamuzi huo na kuahidi kutoa ushirikiano wa hali na mali katika shughuli za maendeleo.

  0 0


  0 0

  Hospitali ya rufaa ya Haydom iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, imepatiwa msaada wa mashuka 100 na benki ya CRDB ambayo yatatumiwa na wagonjwa wa hospitali hiyo.

  Akizungumza wakati akikabidhi mashuka hayo 100 kwa mkurugenzi wa hospitali hiyo Dk Emanuel Nuwass, Meneja wa CRDB Tawi la Babati Ronald Paul alisema wanatoa msaada huo ili kurudisha hisani kwa jamii.

  Paul alisema wamekabidhi mashuka hayo ili kutoa asante kwa jamii kwenye wiki ya huduma kwa wateja, kwa kurudisha kwao kile kidogo wanachopata kwa ajili ya kuboresha mahusiano zaidi baina ya benki hiyo na wateja wake.

  “Tutaendelea kushirikiana na kusaidiana kwenye masuala mbalimbali ya kijamii kwani tunatambua jitihada na changamoto ya hospitali ya Haydom ambayo inatoa huduma kwa watu wa Manyara na waliopo mikoa ya jirani,” alisema.

  Hata hivyo, mkurugenzi wa hospitali hiyo Dk Emanuel Nuwass alisema hii ni mara ya tatu kwa benki hiyo kutoa msaada kwenye hospitali ya Haydom, hivyo iendelee kuwa karibu nao kwa ajili ya kupeana ushirikiano wa kusaidia jamii.

  Dk Nuwass alisema awali benki hiyo ilitoa mchango wa maendeleo wa sh1 milioni kwa ajili ya siku ya Haydom, kisha wakawapa zawadi ya ng’ombe mmoja mkubwa wa siku ya familia na mashuka 100 yatakayotumiwa na wagonjwa.

  Alisema hivi karibuni bodi ya hospitali hiyo ilikubaliana na mpango wa malipo kwa wagonjwa kupitia njia ya kadi ya CRDB na zoezi hilo linatarajia kuwarahisishia watu wote watakaopata huduma katika eneo hilo la Haydom.

  Kwa upande wake, meneja masoko mwandamizi wa benki hiyo Fredrick Siwale alisema benki hiyo itandelea kutoa huduma nzuri kwa wateja wao huku ikiboresha maeneo ambayo huduma haipatikani kwa kuhakikisha wanakuwepo.

  “Kupitia kauli mbiu yetu ya ulipo tupo kama hatupo tutakuja na kama hatujaja utusubiri, tunalenga kuwahudumia watanzania wote na kupitia hilo ndiyo sababu tukafika kutoa mashuka haya kwani tunaithamini jamii,” alisema Siwale.
   

   

  0 0  0 0

   
  Jeshi la Polisi Tanzania, Kikosi cha Usalama Barabarani (T), Baraza la Usalama la Taifa Tanzania, kwa pamoja linatoa Shukrani nyingi kwako/kwenu kwa kujitokeza katika kusaidia Kikosi cha Usalama Barabarani, kutoa Elimu kwa Waendesha Pikipiki Maarufu kama Bodaboda, Kupitia Michezo Vijana mbalimbali zaidi ya 6,000 wameweza kupata Elimu kupitia Mashindano yanayoendela ya Mpinga Cup.

  Hata hivyo ukiwa kama Mdau wa Michezo yetu ya Mpinga Cup 2016, tunapenda Kukufahamisha kwamba, Sasa tunaingia mzunguko wa pili baada ya kumaliza mzunguko wa kwanza.
  Tulikuwa na Timu 128 zilizocheza hatua ya kwanza ya mtoano ambapo baada ya kucheza zimebaki timu 64 ambazo zinaanza mzunguko wa pili kwa njia ya mtoano.
  mzunguko huu utafanyika kwenye Viwanja Vitatu vya KAMPALA GONGOLAMBOTO, VINGUNGUTI SHULE YA MSINGI NA BENJAMINI MKAPA SEKONDARI.
  Inaanza tarehe 8/10/2016 na kumalizika tarehe 23/10/2016 na baada ya hapo tutabakiwa na timu 32 Bora zitakazocheza Raundi ya Tatu.Baada ya Raundi ya Tatu Tutabakiwa na Timu 16 Bora ambazo zitapewa Vifaa vya Michezo kwa ajili ya kucheza Ligi ya Mzunguko itakayokuwa katika Makundi mawili.

  Tutapata Timu za Robo Fainali, Nusu Fainali na FAinali.
  Kwa Kuwa Michezo ni Gharama kubwa na Pia Mahitaji ni Mengi, tunakuomba kwa Moyo wa Uzalendo uweze kujitokeza kwa mara nyingine kuweza kuchangia baadhi ya Mahitaji ili kuweza kufanikisha Mashindano yetu ambayo yameanza kwa ubora wa hali ya juu huku yakiwa pia ni mashindano ya kwanza kuandaliwa kwa kushirikisha timu nyingi kuliko mashindano yoyote Tanzania.

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika tamasha la madhehebu ya Bohora leo Oktoba 08, 2016, ambayo yanafanya maadhimisho ya dunia ya sikukuu ya mwaka mpya wa Kiislam Jijini Dar es Salaam.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Oktoba, 2016 amehutubia katika tamasha la madhehebu ya Bohora ambayo yanafanya maadhimisho ya dunia ya sikukuu ya mwaka mpya wa Kiislam Jijini Dar es Salaam.

  Maadhimisho hayo yamewaleta nchini wafuasi zaidi ya 30,000 kutoka nchi mbalimbali duniani na kuongozwa na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb (TUS).

  Akihutubia wafuasi wa Bohora katika Msikiti wa Hakimi uliopo Upanga Jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amemshukuru Kiongozi Mkuu wa Bohora kwa kukubali kufanya maadhimisho ya mwaka mpya wa madhehebu hayo hapa nchini na amewashukuru na kuwapongeza wafuasi wa madhehebu hayo kwa kukubali kuja hapa nchini na kukaa kwa siku zote za maadhimisho yaani kuanzia tarehe 02 Oktoba, 2016 walipoanza hadi tarehe 11 Oktoba, 2016 watakapomaliza.

  Rais Magufuli, amewapongeza viongozi na wafuasi wa madhehebu ya Bohora kwa kutumia maadhimisho haya kuhimiza amani, upendo na mshikamano na pia amewashukuru kwa kushiriki katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ikiwemo mchango Dola za Marekani 53,000 zilizotolewa na Kiongozi Mkuu wa Bohora kwa Serikali kwa ajili ya kuchangia kampeni ya utengenezaji wa madawati, na kuwaleta madaktari kutoka Hospitali ya Saifee ya India waliotoa matibabu bure kwa wananchi wa Arusha.

  Aidha, Rais Magufuli amewakaribisha wafuasi wa Bohora duniani kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Uvuvi, Misitu, Mifugo, Madini na Gesi kwani soko la uhakika lipo ndani ya nchi, katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) yenye watu takribani milioni 400.

  Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb (TUS) amemshukuru Rais Magufuli kwa kuungana na wafuasi wa madhehebu ya Bohora katika maadhimisho hayo na amesema wafuasi wote wa Bohora wanahimizwa kushirikiana na mamlaka zilizopo katika nchi wanazoishi, kuwa raia wema na kufuata sheria.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  08 Oktoba, 2016

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akisalimiana na Kiongozi wa Jumuiya ya 
  Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin mara alipowasili kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam  ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akiwasili  kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga 
  jijini Dar es salaam ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akihutubia mbele ya  Kiongozi wa Jumuiya ya 
  Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako 
  alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akiagana   Kiongozi wa Jumuiya ya 
  Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako 
  alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akisalimiana na Kiongozi wa Jumuiya ya Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin mara alipowasili kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam  ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akisalimiana na Kiongozi wa Jumuiya ya
  Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin mara alipowasili kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam  ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akihutubia mbele ya  waumini na  Kiongozi wa Jumuiya ya  Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akihutubia mbele ya  waumini na  Kiongozi wa Jumuiya ya  Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akimuaga  Kiongozi wa Jumuiya ya 
  Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako 
  alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John pombe Magufuli akihutubia mbele ya  waumini na  Kiongozi wa Jumuiya ya  Mabohora Duniani, Dk Seydna Mufaddal Saifuddin kwenye msikiti wa Bohora ulioko Upanga jijini Dar es salaam ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za Mabohora kuadhimisha Mwaka Mpya wa Kiislamu wa 1438 leo Oktoba 8, 2016

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni endelevu ya Fahari Tanzania, iliyoambatana na utoaji wa Tuzo kwa Bidhaa 50 bora za Kitanzania zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
   Waziri wa Viwanda,Bisahara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akihutubia kwenye uzinduzi wa kampeni endelevu ya Fahari Tanzania, iliyoambatana na utoaji wa Tuzo kwa Bidhaa 50 bora za Kitanzania.
   Meneja wa kampeni ya Fahari ya Tanzania Bw. Emmanuel Nnko akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo ambapo alifafanua umuhimu wa kununua bidhaa za Tanzania.
   Picha ya Tuzo 50
  Vijana wa Kimaasai wakionyesha umahiri wao wa kuimba na kucheza kwa kuruka wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Fahari ya Tanzania kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Afisa Habari wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Margareth Chambiri (kulia) akiwakaribisha kwenye banda la Maonesho la NEC, Naibu Mawaziri Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wilayani Bariadi mkoani Simiyu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inaendelea na program endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura kote nchini.
  Naibu Mawaziri Mhe. Anthony Mavunde Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu wakipata ufafanuzi kutoka kwa Maafisa wa NEC kuhusu utendaji wa Mashine za BVR katika uchukuaji na uhifadhi wa taarifa za Wapiga Kura leo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wilayani Bariadi –Simiyu. 
  Afisa TEHAMA wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Sanif Khalifan akitoa ufafanuzi kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Bariadi kuhusu taratibu za uchaguzi na hatua za uandikishaji wa wapiga kura kupitia TEHAMA leo mjini Baridi wakati wa Tume hiyo ilipokuwa ikitoa Elimu kwa Mpiga Kura kuhusu masuala mbalimbali.   Baadhi ya Askari wa JKT wakipita mbele ya Banda la Maonesho la NEC na wengine wakipata ufafanuzi kuhusu masula mbalimbali walipotembelea Banda la Maonesho ya Elimu ya Mpiga Kura wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Vijana wilayani Bariadi, mkoani Simiyu. 
  Naibu Mawaziri Mhe. Anthony Mavunde - Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana na Mhe. Abdallah Possi (Mwenye Kofia) Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu wakifurahia jambo mara baada ya kupata ufafanuzi kutoka kwa Maafisa wa NEC kuhusu utendaji wa Mashine za BVR katika uchukuaji na uhifadhi wa taarifa za Wapiga Kura leo kwenye maadhimisho ya Wiki ya Vijana na Kumbukumbu ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wilayani Bariadi –Simiyu. 
  Mkazi wa Bariadi akipata ufafanuzi kuhusu karatasi zenye majina ya wagombea zinazotumika kupigia kura alipotembelea banda la maonesho na Elimu ya mpiga kura la NEC leo wilayani Bariadi mkoani Simiyu.Picha na Aron Msigwa – NEC.

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( wa pili kulia) akifurahia jambo na Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson (kulia) wakati wa KUFUNGA Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ( katikati) akicheza moja ya ngoma za kiutamaduni Wwakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016 kulia ni Naibu Spika Mhe. Tulia Ackson na kushoto ni Katibu Mtendaji BASATA Geodfrey Mngereza.
  Kikundi cha Utamaduni cha Ikama kikitoa burudani wakati wa kufunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 liliofanyika wilayani Rungwe mkoani Mbeya leo Oktoba 08,2016. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM.


  Na Kitengo cha Mawasiliano WHUSM -Mbeya

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewashauri vijana kutumia ngoma za asili kujiajiri kwani ni fursa mojawapo ya ajira kwa sasa.

  Ametoa ushauri huo leo Mjini Mbeya alipokuwa akifunga Tamasha la Utamaduni la Tulia Tradition Festival 2016 na kuwahimiza vijana kutosubiri kuajiriwa ikiwa wanaona wana uwezo wa kufanya kitu ambacho kitawasaidia kupata kipato na kuendesha maisha yao.

  “Ngoma za asili ni chanzo cha ajira kwa vijana na sisi kama Serikali tutashirikiana na wadau wa Sanaa na Utamaduni ili kutengeneza ajira na kudumisha mila na desturi za nchi yetu” alisistiza Mhe. Nnauye.

  Aidha kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson amesema kuwa fursa pekee kwa vijana kujiajiri kupitia shughuli za Sanaa na Utamaduni kwani ndio sekta ambazo zimetoa ajira kwa vijana wengi duniani kwa sasa.

  “Nawashauri vijana wa kitanzania kuangalia na upande huu wa Sanaa na Utamaduni kuna ajira pia na sisi tupo pamoja nao na tutawapa ushirikiano ili wafikie malengo” alisema Mhe. Tulia.

  Tamasha hili liliondaliwa na Naibu Spika Mhe.Tulia Ackson linafanyika kwa siku mbili na limeshirikisha vikundi vya ngoma za asili vipatavyo 62 kutoka mikoa mbalimbali nchini.

  0 0

  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera

  MAMA mmoja na watoto wake wanne wakazi wa kijiji cha Nyamilanda kata ya Kyebitembe wilaya ya Muleba Mkoani kagera wamefariki dunia jana baada ya kula chakula aina ya ugali unaosadikiwa kuwa na sumu.

  Mwenyekiti wa kijiji cha Nyamilanda Trasias Baltromeo amesema watu hao waliofariki ni mama na watoto wake wanne ambao walikula ugali majira ya saa tisa mchana na kuanza kutapika na hatimaye kufariki dunia wakipelekwa Kituo cha Afya Kimeya kilicho jirani na kijiji hicho

  Baltromeo amewataja waliofariki kuwa ni mama wa watoto Julitha Julius (35) Haujeni Julius (14) Superius Julius (12), Gabriel Julius (4) na Paschazia Julius mwenye umri wa miezi sita

  Mwenyekiti huyo alisema katika tukio hilo mama aliandaa mboga aina ya dagaa na kwenda kwa mama mkwe wake nyumba jirani kutafuta unga wa muhogo na walipomaliza kula yeye na watoto wake wakaanza kutapika na kuanza kuhangaika hatimaye wananchi wakafika lakini juhudi za kuokoa maisha yao hazikuzaa matunda.

  "Nilipofika nilikuta hali ni mbaya wakitapika na kuamua kwenda kutoa taarifa polisi Kyebitembe lakini walipofika wakati wanawakimbiza hospitali ndogo ya kimeya wakawa wamefariki watoto wanne na mama yao”Alisema Mwenyekiti

  Tukio la Kifo kama hilo limetokea mwaka jana kata ya Kasharunga tarafa ya Kimwani jimbo la Muleba kusini wilayani humo ambapo watu saba wa familia moja walikula chakula chenye sumu na kuokoka watu watatu pekee wanne walifariki dunia.

  Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi ameongea na mtandao huu naye pia amekiri kupokea taarifa hiyo na kwamba hadi sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusishwa na vifo hivyo lakini uchunguzi wa wataalamu wa afya unaendelea ili kujiridhisha na kutambua aina ya sumu iliyotumika hadi watu hao wakapoteza maisha yao.

  Mkuu wa wilaya ya Muleba mhandisi Richadi Ruyango amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba jopo la wataalamu wa afya na jeshi la polisi limekwenda kituo cha Afya Kaigara na Hospitali ya Rubya kufanya uchunguzi kwa miili ya marehemu hao.

  Mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi katika tarafa ya7 kimwani kuwa makini na vyakula wanavyokula kwani hilo ni tukio la tatu la familia kula vyakula vyenye sumu na kupoteza maisha kijijini hapo

older | 1 | .... | 999 | 1000 | (Page 1001) | 1002 | 1003 | .... | 1898 | newer