Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 49473 articles
Browse latest View live

BANK OF AFRICA TANZANIA APPOINTS NEW MANAGING DIRECTOR


KIONGOZI MBIO ZA MWENGE WA UHURU KITAIFA AZINDUA DARASA LA TEHAMA SHULE YA WASICHANA YA JOKATE MWEGELO KISARAWE MKOANI PWANI

$
0
0




Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi (katikati) akimueleza jambo Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation Sandra Oswald (kulia) mara baada ya kuzindua darasa la Tehama kwenye shule ya wasichana ya Jokate Mwegelo iliyopo wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani mwishoni mwa wiki. Vodacom Tanzania kupitia taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imetoa kompyuta 15 kwa shule hiyo ikiwa na lengo la kuhakikisha wanafunzi wanapata maudhui ya elimu bure kupitia tovuti ya e-fahamu. 

 Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Luteni Josephine Mwambashi (katikati) akimueleza jambo Meneja wa Vodacom Tanzania Foundation Sandra Oswald (kulia) mara baada ya kuzindua darasa la Tehama kwenye shule ya wasichana ya Jokate Mwegelo iliyopo wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani mwishoni mwa wiki. Vodacom Tanzania kupitia taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imetoa kompyuta 15 kwa shule hiyo ikiwa na lengo la kuhakikisha wanafunzi wanapata maudhui ya elimu bure kupitia tovuti ya e-fahamu.  


NMB Marathon 2021 yazinduliwa, mapato kutibu wagonjwa Fistula CCBRT

$
0
0

  

Benki ya NMB, imesaini makubaliano ya ushirikiano na Hospitali ya CCBRT, yanayolenga kukusanya kiasi cha Sh. Bilioni 1 za matibabu ya Fistula kwa kina mama wasio na uwezo, kupitia Mbio za Hisani za NMB Marathon, zitakazofanyika kwa mara ya kwanza Septemba 18, 2021 jijini Dar es Salaam.

 Kupitia mbio hizo ambazo mwaka huu zitafanyika chini ya kaulimbiu ya: 'Mwendo wa Upendo,' Benki ya NMB na CCBRT wanatarajia kukusanya zaidi ya Sh. Milioni 250 kila mwaka kwa miaka minne ambazo zitasaidia matibabu ya wagonjwa wa fistula, miongoni mwa mamia ya kina mama wanaoteseka kwa maradhi hayo.

 Akizungumza wakati wa utilianaji saini wa makubaliano hayo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, alibainisha kuwa, Fistula ni maradhi yanayotesa kina mama wengi nchini, na akawataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kujisajili kushiriki mbio hizo, ili kufanikisha lengo la kukusanya fedha ya matibabu ya wagonjwa hao.

 Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi, alisema taasisi yake inajisikia faraja kubwa kufanikisha utilianaji saini wa makubaliano hayo, sambamba na uzinduzi wa NMB Marathon 2021, huku akieleza kuwa mashindano hayo yana maana kubwa kwa maelfu ya kina mama wa Kitanzania.

 NMB Marathon zitakuwa na sehemu tatu ambazo ni mbio za kilomita 21 (nusu marathon), kilomita 10 na kilomita 5, ambako washindi wa kwanza hadi wa 10 watapata medali na fedha taslimu.

 Kwa mujibu wa Mratibu wa NMB Marathon 2021, David Marealle, ada ya kujisajili kushiriki mbio hizo ni Sh. 30,000 kwa kilomita 21 na Sh. 20,000 kwa mbio za kilomita 10 na kilomita 5.

 Washindi wa mbio za kilomita 21 wanaume na wanawake watajinyakulia Medali ya Dhahabu na fedha taslimu Sh. 1,400,000, huku washindi wa pili wakitarajiwa kutwaa Medali za Fedha na Sh. 1,100,000, wakati washindi wa tatu wakitengewa Sh. 700,000 na Medali za Shaba.

 Huku kwa mbio za kilomita kumi, 700,000 na medali ya dhahabu, 500,000 na medali ya fedha pamoja na 300,000 na medali ya Shaba kwa mshindi wa kwanza, pili na tatu kwa wanaume na wanawake.

 Katika mbio za kilomita 5, washindi upande wa wanawake na wanaume watajipoza na Medali za dhahabu na Sh. 250,000, washindi wa pili medali za fedha na Sh. 150,000, huku washindi wa tatu wakiambulia medali za shaba na Sh. 100,000 taslimu.

Tayari kampuni za Bima za UAP na SANLAM wameshachangia jumla ya shilingi milioni 100 (sawa na Sh. Mil. 50 kila moja)

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki y NMB, Ruth Zaipuna na Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi  wakionyesha mkataba  wa maelewano baada ya kutiliana saini mkataba wa maelewano wa mbio za NMB Marathon zenye lengo la kuchangia bilioni mmoja ndani ya miaka minne kwa ajili ya kuwatibu akinamama wenye Fistula. Kulia ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa UAP Insurance, Nelson  Rwihula na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance,  Julius Magabe. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki y NMB, Ruth Zaipuna na Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi wakibadilishana  wa maelewano wa mbio za NMB Marathon zenye lengo lakuchangia bilioni mmoja ndani ya miaka minne kwa ajili ya kuwatibu akinamama wenye Fistula. Kulia ni  Afisa Mtendaji Mkuu wa UAP Insurance, Nelson Rwihula na kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Life Insurance, Julius Magabe 

 


 

NANI ATAFANIKIWA KUCHEZA LIGI YA UEFA NA EUROPA MSIMU HUU?

$
0
0

 


*Msimu Mpya, Vibe Jipya Viwanjani, Dakika 90 Kuamua Nani Mbabe!


Ni mwendo wa burudani kila pembe ya ulimwengu. Barani Ulaya, mambo yanazidi kutaradadi ukiwa ni msimu mpya wa 2021/22. Baadhi ya timu zimeshafuzu moja kwa moja mashindano ya Ligi ya Mabingwa, baadhi kuingia viwanjani wiki hii kuisaka tiketi hiyo. Mambo yapo hivi;


AS Monaco uso kwa uso dhidi ya Shakhtar Donetsk jumanne hii. Hizi ni timu mbili ambazo zinauzoefu mkubwa linapokuja suala la kucheza mashindano ya Uefa. Kazi kubwa itakuwa ndani ya uwanja, nani ataipata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa na nani ataikosa kwa msimu huu? Meridianbet tumekuwekea Odds ya 1.65 kwa Monaco.


Kule Ujerumani, kutachezwa mchezo wa DFB Super Cup. Huku moto utawaka pale ambapo Borussia Dortmund watachuana na Bayern Munich. Timu mbili zinazochuana kwa ubora ndani ya Bundesliga, ni dakika 90 pekee kuamua matokeo! Huku Haaland, kule Lewandowski. Ifuate Odds ya 2.15 ndani ya Meridianbet.


Jumatano hii, Benfica atakua nyumbani kuwaalika PSV Eindhoven katika mchezo wa kuisaka tiketi ya Ligi ya Mabingwa. Miamba ya uholanzi vs wababe wa ureno. Ni burudani isiyokifani wiki hii. Meridianbet tumekusogezea Odds ya 2.25 kwa Benfica.


Alhamisi itakuwa ni zamu ya timu zinazowania nafasi ya kucheza Ligi ya Europa. Randers FC vs Galatasary, ni msimu mpya na vibe jipya ndani ya viwanja barani Ulaya. Meridianbet tunakwenda pamoja nawe. Ifuate Odds ya 2.25 kwa Galatasaray wiki hii.


Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!

Wafanyabiashara wa Zanzibar waaswa kutumia vyema wigo wa biashara ya mtandaoni (e-commerce) kuuza na kutangaza bidhaa zao katika masoko ya ndani na nje ya nchi

$
0
0

Wafanyabiashara wa Zanzibar wameaswa kutumia vyema wigo wa biashara ya mtandaoni (e-commerce) kuuza na kutangaza bidhaa zao katika masoko ya ndani na nje ya nchi ili kukuza biashara zao na mitaji.

Hii ni kutokana na kuwa na uwanja mpana wa masoko ya mtandaoni kwa wafanyabiashara kuuza bidhaa na huduma zao katika muda mfupi na kwa gharama ndogo za uendeshaji.

Meneja Masoko wa  Zantel-Zanzibar, Rukia Mtingwa alisema wakati wa warsha ya Biashara-Mtandao iliyoandaliwa na Zantel kujadili fursa na changamoto za biashara za mitandaoni kwamba; wafanyabiashara watapata wateja wengi wapya kutoka masoko mapya ya mtandaoni na kuongeza mauzo yao na mitaji.

Warsha hii ya siku mbili iliyofanyika Agosti 14 na 15, 2021 Zanzibar, iliwaleta pamoja wawakilishi wa serikali, wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa biashara. Wafanyabiashara pia walipata fursa ya kuonyesha na kutangaza bidhaa zao mbalimbali.

“Kwa kutumia simu ya mkononi au kompyuta yako, unaweza kutangaza bidhaa au huduma yako kupitia kurasa zote za mitandao ya kijamii kama WhatsApp, Instagram, Facebook, Twitter na YouTube. Pia unaweza kufungua duka lako mtandaoni na ukauza bidhaa zako katika masoko ya ndani na nje ya Zanzibar,” alisema.

Aliongeza “Biashara-mtandao pia huokoa muda na kupunguza gharama za uendeshaji. Mfano, ukiwa na duka la mtandaoni, hauna haja ya kukodi eneo la kufanyia biashara; maana unaweza kuwa na bidhaa nyumbani kwako au kwenye chombo cha usafiri na ukafanya biashara yako vizuri sana.”

Kwa walio na biashara zao masokoni, wakulima na wavuvi; wanaweza kutangaza biashara zao mtandaoni na kuelekeza wateja wao mahala walipo.

“Warsha hii ni muendelezo wa kuiishi dhamira ya Zantel, ambayo inalenga kuendeleza matumizi ya intaneti na mfumo wa kidijitali katika masoko yetu.  Tunaendelea kuboresha mtandao wetu wa intaneti kutoka kasi ya 2G na 3G na kuweka mtandao wa 4G katika baadhi ya maeneo,” alisema.

Warsha hii pia ni muendelezo wa kampeni yake kabambe ya PASUA ANGA KI ZANTEL 4G inayolenga kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa intaneti katika kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Biashara na Masoko kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda – Zanzibar, Khamis Shauri, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo Mohamed Mwalim alisema warsha hii ya biashara za kimtandao (e-commerce) ni mwanzo mzuri wa kusaidia kukuza sekta ya biashara nchini.

Aliwaasa wafanyabiashara kutumia vyema wigo mpana wa soko la kimtandao ambalo kwa mujibu wa takwimu za za Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), idadi ya Watanzania wanaotumia mtandao wa intaneti imeongezeka kutoka milioni 26,83 mwaka 2020 hadi milioni 29.07 mwezi Aprili 2021.

“Biashara za mitandao zinasaidia wafanyabiashara kupata idadi kubwa ya wateja, urahisi wa kutangaza biashara, kupata bidhaa kwa manunuzi, kuokoa wakati na gharama ndogo,” alisema.

Aliongeza “Kulingana na mlipuko wa janga la ugonjwa wa mapafu (Covid-19), dunia yote imehamishia biashara zake kwenye mitandao ambapo biashara hufanyika bila mteja na muuzaji kukutana. Hivyo, ni lazima na sisi wana Zanzibar tubadilike”

Kutokana na umuhimu wa e-commerce, alisema, serikali imeweka sheria na miongozo mbalimbali ili kuweza kuboresha na kusimamia ufanyaji wa biashara za aina hiyo. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo Mohamed Mwalimu akimkabidhi hundi ya Sh300,000 mshindi wa kwanza wa Shindano la vijana wanaotumia mtandao wa intaneti kujiingizia kipato, Ahmad Masoud Seif katika warsha ya biashara-mtandao (e-commerce) iliyofanyika Kisonge Zanzibar.Katikati ni Afisa Meneja Masoko Zantel-Zanzibar Rukia Mtingwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Vipimo Mohamed Mwalimu (kushoto) na Meneja Masoko wa Zantel-Zanzibar, Rukia Mtingwa (pembeni) wakimsikiliza mfanyabiashara akielezea biashara yake katika warsha ya biashara-mtandao (e-commerce) iliyofanyika Kisonge Zanzibar. 


 

 

Benki ya NBC Yazindua huduma ya Bima ya Afya Kwa Familia na Vikundi.

$
0
0

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma za mpya ijulikanayo ‘Bima ya Afya na Maisha’ ikilenga kuwezesha ushirikishwaji wa jamii katika kupata huduma za bima jamii  kupitia familia na vikundi mbalimbali vya kijamii ikiwemo vya vicoba, saccos, wafanyakazi, vikundi  vya whatsApp na vyama vya ushirika .

Huduma hiyo inayopewa amana na Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance Tanzania inahusisha Bima ya ‘Afya  Salama’ mahususi kwa ajili ya wana familia pamoja na Bima ya ‘Nia Njema’  ambayo ni mahususi kwa ajili ya wana vikundi mbalimbali vya kijamii pamoja na familia zao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam mapema hii leo, Mkuu wa Idara ya Bima, Benki ya NBC Bw Benjamin Nkaka alisema huduma hizo  zinalenga kusaidia nia ya serikali katika kuhakikisha kwamba huduma ya bima ya afya inamfikia kila mtanzania.

“Kupitia huduma ya Bima ya Nia Njema  tunalenga kuwalinda watanzania katika vikundi vyao vya kijamii na kiuchumi na wakati huo huo kuwezesha  ushirikishwaji wa jamii katika mifumo fedha kwa kupitia  bima za jamii ikiwemo vikundi vya vicoba, saccos, wafanyakazi , vikundi vya wafanyakazi, Wajasiriamali, taasisi, vyama vya ushirika, makundi ya WhatsApp, na vikundi vingine vya namna hiyo,’’ alitaja.

Alifafanua kuwa bima ya vikundi inahusisha idadi ya wanachama kuanzia watano na kuendelea ambao wanaweza kuwa wanandugu, wanamtaa au muunganiko wowote huku akibainisha kuwa gharama ya kujiunga kwa mwaka ni Tsh 18,000.

“Utofauti wa bima hii ni kutoa huduma ya bima ya maisha kwa wanakikundi pamoja na familia zao, kwa gharama nafuu, uharaka na kwa utalaamu wa bima za jamii.’’

“Huduma hizi zinapatikana katika mikoa yote nchini na mafao ya bima hutolewa ndani ya masaa 24 hadi 48 baada ya kuwasilisha taarifa na viambatanisho sahihi kutoka kwa uongozi wa kikundi na kujaza fomu ya madai. Utaratibu wa kujisajili ni kupitia kikundi,’’ aliongezea.

Alitaja faida ya za bima hiyo ya kikundi kuwa ni pamoja na kuboresha mafao ya kikundi kwa mahitaji ya wanakikundi, kupunguza usumbufu wa kuchangishana miongoni mwa wanakikundi, kupatikana kwa fedha ndani ya muda mfupi na kupunguza michango ya mara kwa mara kwa wanakikundi

Kuhusu Bima ya Afya Salama Bw Nkaka alisema inalenga kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kiafya kwa wana familia na inatumika katika hospitali  zaidi ya 372 kote nchini ikiwemo hospitali za serikali na hospitali binafsi.

“Huduma hii inawalenga watu wote wenye umri chini ya miaka 64. Kwa upande wa familia inahusisha watu sita akiwemo mteja anayechukua bima  pamoja na mke au mume wake na watoto wao wanne walio chini ya miaka 18,’’ alifafanua.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Bima kupitia Mabenki kutoka Kampuni ya Sanlam Bi Klispinana Shirima aliwahakikishia wateja wa huduma hizo kuwa ni bora na zinalenga kuwagusa wana jamii moja kwa moja huku akibainisha kuwa kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha huduma hiyo inatolewa kwa kukidhi matakwa na malengo ya kuanzishwa kwake.

Wakizungumza kwenye hafla hiyo Mabalozi wa huduma hizo, Bi Dina Marios ambae ni mdau mashuhuri wa habari nchini pamoja na mtaalamu wa afya na mdau wa habari nchini Dk Isaac Maro walisema ushiriki wao katika kuzinadi huduma hizo unatokana na umuhimu na uhitaji wake kwenye mazingira ya kijamii kwa sasa.

“Kupitia teknolojia hii mawasiliano kwasasa tuna vikundi vingi vya kijamii kupitia simu zetu na hivyo tumejikuta tupo karibu zaidi katika kusaidia kwenye mambo mbalimbali ya kijamii kupitia michango mbalimbali. Ujio wa huduma kama hii ya bima ya Nia Njema ni suluhisho sahihi,’’ alisema Bi Marios ambae ni balozi wa huduma ya Bima ya Nia Njema.

“Kwasisi ambao tunatumia muda mwingi katika kutoa huduma za kiafya kwa jamii ndio tunaweza kufahamu zaidi umuhimu wa Bima ya afya kwasababu tunashuhudia kwa macho yetu faida za kuwa na bima ya afya na athari  za kutokuwa na bima ya afya. Huduma kama hii ya ‘Afya Salama ni mkombozi kwa wana jamii kiafya na kiuchumi,’’ aliongeza Dr Maro ambae ni balozi wa huduma na Bima Afya Salama.

Mkuu wa Idara ya Bima, Benki ya NBC Bw Benjamin Nkaka (Katikati) na Mkuu wa Idara ya Bima kupitia Mabenki kutoka Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance Tanzania Bi Klispinana Shirima (Kulia) wakizindua rasmi huduma mpya ijulikanayo ‘Bima ya Afya na Maisha’ inayowalenga wana familia na vikundi mbalimbali vya kijamii ikiwemo vya vicoba, saccos, wafanyakazi, vikundi  vya whatsApp na vyama vya ushirika. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Mawasiliano wa NBC Bw David Raymond (Kulia) na Mabalozi wa huduma hizo, Bi Dina Marios (wa pili kushoto) na Dk Isaac Maro (wa pili kulia)


Kwa mujibu wa Mabalozi wa huduma hizo, Bi Dina Marios (kushoto) ambae ni mdau mashuhuri wa habari nchini pamoja na mtaalamu wa afya na mdau wa habari nchini Dk Isaac Maro, ushiriki wao katika kuzinadi huduma hizo unatokana na umuhimu na uhitaji wake kwenye mazingira ya kijamii kwa sasa.

Mkuu wa Idara ya Bima kupitia Mabenki kutoka Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance Tanzania Bi Klispinana Shirima (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu huduma  hiyo.

Mmoja wa mabalozi wa huduma hizo, Bi Dina Marios (katikati) akizungumza kuhusu huduma ya Bima ya ‘Nia Njema’ inayowalenga wana vikundi vya kijamii na kiuchumi vikiwemo vikundi vya vicoba, saccos, wafanyakazi , vikundi vya wafanyakazi, Wajasiriamali, taasisi, vyama vya ushirika, makundi ya WhatsApp, na vikundi vingine vya namna hiyo wakati wa hafla hiyo.

Mmoja wa mabalozi wa huduma hizo, Bw Isaac Maro (katikati) akizungumza kuhusu huduma ya Bima ya ‘Afya Salama’ inayolenga kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kiafya kwa wana familia huku ikitumika katika hospitali  zaidi ya 372 kote nchini ikiwemo hospitali za serikali na hospitali binafsi wakati wa hafla hiyo.

Mkuu wa Idara ya Bima, Benki ya NBC Bw Benjamin Nkaka (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu huduma  mpya ijulikanayo ‘Bima ya Afya na Maisha’ inayowalenga wana familia na vikundi mbalimbali vya kijamii ikiwemo vya vicoba, saccos, wafanyakazi, vikundi  vya whatsApp na vyama vya ushirika. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Bima kupitia Mabenki kutoka Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance Tanzania Bi Klispinana Shirima (wa pili Kulia), Mkuu wa Mawasiliano wa NBC Bw David Raymond (wa pili kushoto) na Mabalozi wa huduma hizo, Bi Dina Marios (kulia) na Dk Isaac Maro (kushoto).

VODACOM TANZANIA PLC YAWEZESHA MAFUNZO YA TEHAMA KWA WASICHANA

$
0
0


Afisa Utumishi kwa kampuni ya teknolojia na mawasiliano Vodacom Tanzania Plc Gervas Mfubusa akitoa zawadi kwa mwakilishi wa kikundi cha Tanzania Safari Adventures Keziah Mafuru baada ya kushinda nafasi ya kwanza kwenye mafunzo ya TEHAMA yaliyopewa jina la ‘Code like a girl’, mpango unaoendeshwa na kampuni hiyo kupitia taasisi ya dLab ili kuhamasisha wasichana kupenda masomo ya Sayansi. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.


Afisa Rasilmali Watu wa kampuni ya teknolojia na mawasiliano Vodacom Tanzania Plc Gervas Mfubusa akiongea na washiriki wa mafunzo ya TEHAMA yaliyopewa jina la ‘Code like a girl’, mpango unaoendeshwa na Vodacom Tanzania kupitia Taasisi isiyo ya Kiserikali ya dLab ili kuhamasisha wasichana kupenda masomo ya Sayansi. Mafunzo hayo yamefanyi

Afisa Utumishi wa kampuni ya teknolojia na mawasiliano Vodacom Tanzania Plc Gervas Mfubusa akikabidhi zawadi kwa mwakilishi wa kikundi cha TEF’s Orphanage Center Farida Maside baada ya kikundi chao kuibuka kuwa na nidhamu bora wakati wa mafunzo ya TEHAMA yaliyopewa jina la ‘Code like a girl’, mpango unaoendeshwa na Vodacom Tanzania kupitia Taasisi isiyo ya Kiserikali ya dLab ili kuhamasisha wasichana kupenda masomo ya Sayansi. Mafunzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam.


SLOTI MPYA YA KUVUTIA KWENYE KASINO YA MERIDIANBET. HUU NI MCHEZO WENYE SIFA ZA KIPEKEE IKIWA NI PAMOJA MIZUNGUKO YENYE BONASI KUBWA!

$
0
0

   



Safari ya Kuvutia ndani ya Circus Fever Deluxe

 

Stadi za wacheza sarakasi ikiwa ni sambamba na uwezo wa wanyama, siku zote imekuwa ni safari ya kuvutia kwa wanasarakasi.

Huu ni mchezo ambao unapatika kwenye Kasino ya Meridianbet pekee. Inamithili ya mazingirza yanayokuonesha upekee wa kuangalia michezo ya sarakasi inayojumuisha watu na wanyama. Kuna watani kwenye kila kona ikiwa ni sambamba na kikundi ambacho kipo tayari kuingia uwanjani na kunogesha zaidi mchezo.

Unaweza kuicheza sloti hii bure au kwa pesa halisi kwenye Kasino ya Meridianbet. Tunashauri uanze na mchezo wa majaribio kwanza kwasababu sio sloti ambayo imezoeleka kwa wachezaji.

Safari ya Kibingwa na Hatari

 

Sloti ya Circus Fever Deluxe ina mchezo maalumu unaoitwa Plinko pamoja na michezo miwili ya bonasi – kugeuza kete na sarafu. Ni mchezo ambao haujazoeleka kwenye sloti. Hautokuta reels kwenye mchezo huu lakini utakuta vikwazo ambavyo mpira lazima uvipita ili ufike kwenye sehemu zenye namba. Ni mchezo ambao upo katikati ya sloti ya mtandaoni na mashine ya kurusha mipira, huku mcheza sarakati ndio nafasi kubwa.

Kwenye mchezo wa Plinko, mchezaji anaweza kubashiri kwenye namba 1 kati ya 5. Namba hizo ni 1,2,4,6 na 9. Unaanza kwa kuweka thamani ya chip kuanzia upande wa kulia wa sloti. Ongeza ubashiri kufikia kiwango unachohitaji na kisha bonyeza kitufe cha cheza “play”. Jokeri litaangusha mpira kutoka mdomoni mwake, lakini kabla ya hilo kutokea, hizo nafasi mbili za chini, zitachagua chip na kizidishio bila kupanga. Kama unabahati ya mpira kupita kwenye vikwazo na kuifikia nafasi hiyo, utabiri wako utazidishwa mpaka mara 20x ya dau lako.

Utapata malipo kama mpira utatua kwenye eneo linalotakiwa. Pia, kuna kofia za maajabu. Kofia ya rangi nyekundu ni kwaajili ya mchezo wa kete wakati ile ya rangi ya zambarau ni kwaajili ya bonasi ya mzunguko wa kugeuza sarafu.

 

Mizunguko Miwili ya Bonasi Kabambe

 

Kama ilivyoelezwa, utaona kofia mbili za maajabu ambazo zinatumika kwenye michezo miwili ya bonasi. Kama mpira utaangukia kwenye kofia nyekundu, utaingia kwenye mchezo wa kete.

Kama jina linavyoelekeza, bonasi ya mzunguko wa kete inaanza na kete mbili zinazozunguka na meza inayoonesha malipo. Bonyeza kitufe cha zungusha “roll button” unapokuwa tayari na kete itaanza kuzunguka ikionesha namba, Uwezekano wa malipo unatokea kati ya 2x na 50x ya dau lako, hii ni bonasi inayovutia.

Mzunguko wa pili wa bonasi unaitwa Geuza Sarafu. Inapatikana pale ambapo mpira utaanguka kwenye kofia ya zambarau. Huu ni mzunguko mrahisi wa bonasi ambao unazungusha sarafu na unasloti mbili. Malipo yanatokea kwenye pande zote mbili za sarafu, unapata ambacho kinasadifu kilichotokea kwenye sarafu. Uwezekano wa malipo ni chini kidogo ya yale ya kwenye bonasi ya kete, yanatokea kati ya x2 na x30 ya dau lako.

 

Safari Kabambe Kwenye Sarakasi

 

Hakukua na matoleo mengi yenye mithili ya sarakasi kwa siku nyingi, lakini Circus Fever Deluxe kutoka Studio za Exapanse ni mchezo wa kipekee. Unapatikana kwenye Kasino ya Meridianbet kwa bure au kwa pesa halisi, ni mchezo ambao unapaswa kuujaribu.

Utafurahia muonekano wa kipekee wenye zawadi kabambe. Ukiwa na bahati, unaweza kupata faida kubwa kwenye Plinko na kufurahia zawadi kedekede ambazo zinaweza kukupa faida maradufu.





Waziri wa Teknolojia azindua Huduma ya NMB Mkononi Plus *150*68#

$
0
0
Benki ya NMB imezindua huduma mpya ya NMB Mkononi Plus, ambayo Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Faustine Ndugulile, ameitaja kama muarobaini wa upotevu wa pesa na kichocheo cha kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za Bima na za kibenki kwa njia ya mtandao.

Uzinduzi NMB Mkononi Plus 'Ya Wote,' huduma inayotolewa kwa wateja na wasio wateja wa NMB, umefanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Ndugulile na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA), Neema Lutula.

Akizungumza kabla ya kuzindua huduma hiyo, Waziri Ndugulile alisema NMB Mkononi Plus ni huduma inayoakisi jitihada za benki hiyo katika kwenda na kasi ya Serikali, ambayo imejikita katika kutokomeza foleni za kihuduma maofisini, sambamba na kuongeza idadi ya watumiaji wa huduma za Bima na fedha kwa njia za mtandao.

"Ubunifu uendelee zaidi na NMB msiishie hapa, kwa sababu uzinduzi huu unaakisi utayari wenu katika kwenda na kasi ya Serikali, ambayo furaha yake ni kuona inaongeza idadibya watumiaji wa Bima na kutokomeza upotevu wa fedha, foleni za huduma maofisini, ambalo kwetu sisi sio jambo la sifa kamwe.

"NMB Mkononi Plus, ni muarobaini wa changamoto za kidijitali na tunaamini unaenda kuongeza kasi ya mafanikio yenu, ambayo ni kielelezo cha ubora wa huduma zenu uliowapa tuzo mbalimbali na pia unadhihirisha uimara wa uongozi wa benki hii chini ya watendaji wazalendo," alisema Waziri Ndugulile.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi Benki ya NMB, Filbert Mponzi, alibainisha kuwa NMB Mkononi Plus ni huduma chanya kwa watumiaji wa huduma za simu za mkononi, bila kujali kama ni wateja ama sio wateja wa benki hiyo, ambayo imeanza kwa kutoa huduma tatu kubwa na muhimu.

Mponzi alizitaja huduma zilizo ndani ya NMB Mkononi Plus ni Bima Xpress (inayohusu huduma za bima), Dunduliza (inayohusisha Usajili Bima ya Afya) na Pamoja Akaunti (inayowezesha ufunguaji wa akaunti za vikundi), na kwamba huduma zaidi zitaongezwa katika mwamvuli huo kulingana na mahitaji ya wateja na wasio wateja.

Leo hii kupitia NMB Mkononi Plus, NMB imethibitisha ubora na ubunifu walionao. Mkononi Plus ni ya wote, wateja na hata wasio wateja wa benki hiyo, hii ni tofauti na ile huduma ya NMB Mkononi, ambayo ni maalum kwa wateja wao.

"Wito kwa wateja ni kuwataka kuendelea kupata huduma bora na rafiki zitolewazo NMB, na wasio wateja wetu, tunawaomba waungane nasi kuhudumiwa na benki yetu, ambayo imeshinda tuzo kadhaa za kitaifa na kimataifa, huku tukijivunia kuwa wabunifu wa masuluhisho mbalimbali kupitia uwekezaji mkubwa wa kidijitali tuliofanya," alisisitiza Mponzi.

Naye Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA), Neema Lutula, aliipongeza NMB kwa ubunifu uliozaa huduma hiyo, anayoamini itakuwa chachu ya kuongeza idadi ya Watanzania wanaotumia huduma za bima, ambao kwa sasa ni wachache.

"Sisi kama wasimamizi na bima nchini, tumefurahishwa na ujio wa NMB Mkononi Plus, tukiamini unaenda kuchagiza watu wa kada zote kutumia huduma za bima na wito wetu kwa benki ni kuimarisha mahusiano mema na ushirikiano chanya na Kampuni za Bima nchini ili kurahisisha utoaji huduma kwa Watanzania," alisema Lutula.
Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Dk. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa tatu kulia), wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa huduma ya NMB Mkononi Plus uliofanyika Makao Makuu ya NMB - jijini Dar es Salaam. kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA), Neema Lutula. Wapili kulia ni Kaimu Afisa Mkuu Teknolojia na Mabadiliko ya Digitali wa NMB Kwame Makundi na Mkuu wa kitengo cha Bima NMB Martine Massawe.


Waziri wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Dk. Faustine Ndugulile (wa pili kushoto), Afisa Mkuu wa Biashara na Wateja Binafsi Benki ya NMB, Filbert Mponzi (wa tatu kulia), wakipiga makofi wakati wa uzinduzi wa huduma ya NMB Mkononi Plus uliofanyika Makao Makuu ya NMB - jijini Dar es Salaam. kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Usimamizi na Ukaguzi wa Mamlaka ya Bima Tanzania (TIRA), Neema Lutula. Wapili kulia ni Kaimu Afisa Mkuu Teknolojia na Mabadiliko ya Digitali wa NMB Kwame Makundi na Mkuu wa kitengo cha Bima NMB Martine Massawe.

NI MSIMU MPYA WENYE VIBE JIPYA VIWANJANI

$
0
0

 



Bashiri na Meridianbet, Uwe Miongoni Mwa Mabingwa!

 

Baada ya michezo ya wiki ya kwanza kunako soka barani Ulaya, wiki ya pili hii hapa! Burudani inaendelea wikiendi hii ndani ya viwanja mbalimbali, Meridianbet mambo yapo hivi;

 

Ijumaa hii tunaanzia kule Ubelgiji. Standard Liege kuchuana na KV Oostende kunako First Division A. Unaweza kuianza wikiendi yako kwa kuifuata Odds ya 2.25 kwa Liege ukiwa na Meridianbet.

 

Jumamosi hii tutakuwa pole Villa Park katika muendelezo wa EPLAston Villa kuchuana na Newcastle United. Timu zote mbili zilipoteza michezo yao ya kwanza, hii haimaanishi ni wanyonge. Tembelea Odds ya 1.95 kwa Aston Villa ndani ya Meridianbet.

 

Uhondo wa msimu mpya utanoga zaidi pale Emirate Stadium. Naam! Ni London Derby katika wiki ya pili ndani ya EPLArsenal vs Chelsea, vibe la mchezo wa majirani huwa ni burudani ya aina yake. Usipotoshwe na matokeo ya mchezo wa awali, lolote linaweza kutokea kwenye mchezo huu. Meridianbet tumekuwekea Odds ya 1.85 kwa Arsenal jumapili hii.

 

Wikiendi itahitimishwa kwa mtanange wa West Ham United vs Leicester City. Miongoni mwa timu ambazo zinatoa upinzani kwa miamba ya EPL, basi timu hizi hazikosekani kwenye nafasi hizo. Dakika 90 kuamua – ni Brendan Rogers au David Moyes kuondoka na pointi muhimu? Ifuate Odds ya 2.55 ndani ya Meridianbet.


TANZANIA MWENYEJI MAADHIMISHO YA KAIZEN 2021

$
0
0

  


Meneja wa KAIZEN kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Jane Lyatuu akitoa mada kwa waandishi wa habari na wasanii kuhusiana na falsafa ya KAIZEN na maadhimisho yake yanayotarajiwa kufanyika wiki ijayo nchini na kukutanisha nchi zipatazo 20 barani Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Festo Kapela akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari na wasanii kuelekea maadhimisho ya siku ya KAIZEN barani Afrika 2021 yatakayofanyika nchini.

Mjadala ukiendelea.


MAADHIMISHO Ya Falsafa ya KAIZEN kwa mwaka 2021 yanatarajiwa kufanyika nchini Tanzania kwa siku tatu ambapo nchi zipatazo 20 zinatarajiwa kushiriki maadhimisho hayo na kubadilishana uzoefu katika kukuza sekta ya viwanda na biashara.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari na wasanii Meneja wa KAIZEN kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Jane Lyatuu amesema, kwa mwaka huu Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo yatakayofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 26 Agosti na yatafunguliwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Tanzania bara kufungwa na Waziri wa Viwanda na Biashara kutoka Visiwani Zanzibar.

Amesema, nchi zipatazo 20 zitashiriki maadhimisho hayo kwa njia za mtandao huku washiriki wengine wakishiriki kwa kukutana na kueleza kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa watanzania katika kuvutia wawekezaji, kutangaza bidhaa pamoja na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini pamoja na kuhamasisha nchi nyingine za Afrika ambazo hazijaanza kutumia falsafa ya KAIZEN kuanza kuitekeleza.

Vilevile amesema kuwa,  kupitia maadhimisho hayo Tanzania inapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa nchi hizo mbinu bora za kutumia falsafa ya KAIZEN katika kukuza sekta ya viwanda na biashara.

Katika mkutano huo kutakuwa na majadilano maalum na Tanzania itapata wasaa wa kuwasilisha sera na uendelezaji wa falsafa ya KAIZEN nchini pamoja na washiriki kupata nafasi ya kutembelea viwanda na kujionea namna falsafa ya KAIZEN inavyotekelezwa.

 KAIZEN ni neno la kijapani lenye maana ya 'badilika' kwa ubora/uzuri na hutumika katika biashara, KAIZEN huusu shughuli endelevu zinazofanyika ili kuboresha kazi, mfumo, michakato na nyanja zote za kuendesha biashara.

Rais Samia apokea Kombe la Ubingwa wa CECAFA -2021 kutoka kwa Timu ya Taifa ya Vijana U23 Ikulu Jijini Dar es Salaam

$
0
0

  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea Kombe la Ubingwa wa Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA U23 kutoka kwa Nahodha msaidizi wa Timu ya Taifa ya Vijana U23 Reliant Lusajo leo tarehe 22 Agosti, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea Kombe la Ubingwa wa Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA U23 kutoka kwa Nahodha msaidizi wa Timu ya Taifa ya Vijana U23 Reliant Lusajo leo tarehe 22 Agosti, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali wa michezo, Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana U23, Wanariadha walioshiriki michezo ya Olimpiki (Japan) mara baada ya kupokea Kombe la Ubingwa wa Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA U23 leo tarehe 22 Agosti, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali wa michezo, Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana U23, Wanariadha walioshiriki michezo ya Olimpiki (Japan) mara baada ya kupokea Kombe la Ubingwa wa Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati CECAFA U23 leo tarehe 22 Agosti, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. 

Baadhi ya Wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana U23 wakiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wachezaji wa timu ya Taifa ya Vijana U23 wakiwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya Pamoja na Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Vijana ya U23 mara baada ya kukabidhiwa kombe la Ubingwa wa CECAFA U23 Challenge Cup leo tarehe 22 Agosti, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa pamoja na  Rais wa TFF Wallace Karia.
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya U23 wakiwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 22 Agosti, 2021. PICHA NA IKULU

Wafanyakazi Benki ya NBC waungana na Waziri Jafo, Klabu ya Rotary kusafisha fukwe Dar.

$
0
0

Wafanyakazi wa Benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi hii leo wameungana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo, Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula  pamoja na wakazi wengine wa jiji hilo katika kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Waziri Jafo pamoja na kuwapongeza wadau hao kwa jitihada hizo pia aliagiza Manispaa za Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni kuhakikisha zinatatua changamoto mbalimbali zinazokabili fukwe zilizopo kwenye manispaa hizo ikiwemo ukosefu wa vyoo.

“Suala la kuboresha huduma muhimu kwenye fukwe zetu si tu kwamba ni jukumu la Manispaa husika bali pia ni mojawapo ya chanzo cha mapato na ajira kwao. Manispaa zinapoboresha huduma hizi muhimu pia hata wananchi watajitokeza kwa wingi kwenye maeneo haya na pia watatumia huduma hizi kwa kuchangia kiasi cha fedha ambazo zitaongeza makusanyo kwa manispaa husika,’’ alisema.

Aidha Waziri Jafo aliongeza kuwa bado serikali hairidhishwi sana na usafi wa mazingira kwenye fukwe nyingi hususani jijini Dar es Salaam na jitihada za kukabiliana na changamoto hiyo zinaendelea kupitia watalaam pamoja na wadau mbalimbali wanaoshirikiana na serikali kutatua changamoto hiyo.

“Ndio maana nawapongeza sana Klabu ya Rotary kwa namna wanavyojitoa kushirikiana na serikali kutatua changamoto kama hizi kwa kushirikiana na wadau wengine kama vyuo vya elimu ya juu, makampuni binafsi na taasisi za kifedha ikiwemo benki ya NBC…huu ni mfano wa kuigwa hongereni sana,’’ alisema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye zoezi hilo muhimu ni muendelezo wa utaratibu wa kawaida wa benki hiyo kujitolea ama msaada au kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kijamii ili kujenga ushirikiano kwa jamii wanayoihudumia.

Alisema fukwe hizo zinatumiwa na wananchi mbalimbali ambao pia ni wateja wa Benki hiyo hivyo wana kila sababu kusaidia kuboresha usafi wake ili kutoa fursa kwa watumiaji kupumzika katika mazingira safi na salama kwao.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira Taifa Bw Seif Ali Seif pamoja na kuipongeza serikali kwa namna inavyoshirikiana na wadau mbalimbali katika kuboresha hali ya mazingira nchini pia alitoa wito kwa jamii kwa ujumla kuhakikisha kwamba kila mmoja anakuwa askari wa kulinda usafi wa mazingira na uharibu wa miundombinu ya mazingira.

“Ni vema sana ikiwa jukumu la usafi wa mazingira likiwa shirikishi kwa maana ya kwamba kila mmoja wetu anakuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba havumilii uchafuzi wowote utakaofanywa na mwenzie,’’ alishauri.

Awali akizungumza kwenye zoezi hilo Rais wa Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula Dr Edmund Issae ambae klabu yake ndio iliratibu zoezi hilo, alisema wamejipanga kuhakikisha washirikiana vema na wadau muhimu ikiwemo serikali ili kutatua changamoto zinazoikabili jamii ikiwemo suala zima la mazigira.

“Pamoja na kuwashukuru wadao wote waliotuunga mkono kufanikisha hili, nitoe wito kwao kwamba kwa pamoja tusichoke hadi tufike malengo yetu changamoto bado ni nyingi wadau zaidi wajitokeze,’’ alisema.

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wakiokota takataka wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hii leo. Zoezi hilo liliratibiwa na Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi akiokota takataka wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hii leo. Zoezi hilo liliratibiwa na Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo (Kushoto) akishirikiana na wadau mbalimbali akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (Katikati) na Mwenyekiti wa Kamati ya Mazingira Taifa Bw Seif Ali Seif (Kulia) kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hii leo. Zoezi hilo liliratibiwa na Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wakijipongeza kwa furaha mara baada ya kukamilisha zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hii leo. Zoezi hilo liliratibiwa na Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi (Katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo mara baada ya kukamilisha zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hii leo. Zoezi hilo liliratibiwa na Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo (wa tano Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Theobald Sabi (Kushoto kwake) mara baada ya kukamilisha zoezi la kufanya usafi wa mazingira kwenye ufukwe wa Msasani uliopo Mikocheni jijini Dar es Salaam hii leo. Zoezi hilo liliratibiwa na Klabu ya Rotary Dar es Salaam Peninsula na kudhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo benki ya NBC.



Tamasha la Zuchu Home Coming na Zantel lafana Zanzibar

$
0
0

Mcheza kwao hutunzwa! hivyo ndivyo unavyoweza kueleza jinsi tamasha la Zuchu Home Coming na Zantel lilivyokonga nyoyo za watu wengi katika Viwanja vya Amani Zanzibar usiku wa jana.

 Tamasha hilo liliofanyika jana lilipambwa na wasanii wa muziki kutoka Zanzibar ‘Zenjifleva’ akiwamo Sultan King, Berry black, Cholo na malkia wa mipasho Khadija Kopa.Pia, lilishuhudia wasanii wa Bongo fleva akiwamo Mr.Blue, Lavalava, Mbosso,Chege, Jux,Lulu diva na Queen Darleen.

 Moja ya wasanii walioonekana kukonga nyoyo za wengi ni pamoja na mama mzazi wa Zuchu Khadija Kopa ambaye alitumbuiza kwa miondoko ya Taarabu na kupata shangwe kubwa kutoka kwa watu waliokuwapo uwanjani hapo.

 Zuchu alianza kwa kutumbuiza nyimbo zake maarufu ikiwamo wimbo wa itawachoma, nisamehe na baadaye kuhitimisha kwa shangwe kubwa alipoimba wimbo wake wa Sukari.

 Awali, Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Zantel Aneth Muga alisema tamasha hilo pamoja na mambo mengine lililenga kutambua vipaji mbalimbali vya muziki kwa kuwapa wasanii hasa wachanga nafasi ya kuonesha vipaji vyao.

 Huu ni mwendelezo wa Kampeni yetu ya Pasua Anga Ki Zantel 4G ambayo inalenga kutoa elimu juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G katika kuleta manufaa ya kijamii na kiuchumi.

 “Sote tunafahamu kwamba Zuchu ni mtoto na kipaji wa nyumbani kwetu Zanzibar na kupitia tamasha hili Zuchu anarudi nyumbani kwa kutoa burudani ya aina yake hapa Uwanja wa Amani.Pia, kupitia tamasha hili, wanamuziki wa Zenjifleva watapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao ili na wao waweze Kupasua Anga kama ambavyo Zuchu amefanya,” alisema.

 Aliongeza kuwa kupitia intaneti ya 4G, unaweza kufanya mambo mengi ambayo yanaweza kubadilisha kabisa dunia yako.Zuchu amekuwa mfano mzuri ambapo kupitia intaneti ameweza kuendeleza kipaji chake kwa kujifunza mambo mbalimbali ya muziki mtandaoni.

 Mbali na wasanii tamasha hilo lilihudhuriwa na viongozi kutoka Serikalini akiwamo Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mh.Tabia Mwita,Mkuu wa Mkoa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Magharibi. 

                 Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko wa Zantel, Aneth Muga akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ufunguzi wa tamasha la Zuchu Home Coming na Zantel jana katika viwanja vya Amani Zanzibar.Tamasha hilo lilihusisha wasanii mbalimbali wakiwamo wa Zenjifleva na Bongo Fleva.

VODACOM TANZANIA FOUNDATION YATAMBULIWA KWA KUBORESHA ELIMU KUPITIA TEKNOLOJIA

$
0
0

Mamlaka ya Elimu ya Tanzania (TEA) imetoa cheti cha kutambua mchango enedelevu wa Vodacom Tanzania Foundation (VTF) kwa ukuaji wa sekta ya elimu nchini. Kutambuliwa huku kunatokana na dhamira ya kampuni kutumia mtandao wake mpana kutimiza ahadi yake ya kutomuacha mtu yoyote nyuma kwa kuenga ushirikishwaji katika elimu kupitia teknolojia.

Elimu jumuishi ni moja ya misingi mikuu ya kampuni ambapo kupitia mipango inayoendeshwa kwa teknolojia, VTF inalenga kuleta usawa katika upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi na kuwapatia waalimu vifaa stahiki kwa kujenga upokeaji wa madarsa mtandaoni nchini. Foundation inafanya kazi kwa kushirikiana na serikali kupita Wizara ya Elimu kusaidia kufikiwa malengo ya kielimu ya taifa na kuendeleza kasi ya ufikiaji wa Lengo Endelevu(SDG) namba 4 linalolenga elimu bora ambapo, hadi sasa, Zaidi ya wanafunzi 100,000 wametumia jukwaa lisilo na gharama kupitia mradi wa Vodacom Tanzania Foundation uitwao E-Fahamu (awali ukijulikana kwa jina la Instant School).

Uwekezaji wa VTF kwenye elimu unatumia upana na ubora wa mtandao wa Vodacom unaolenga kujenga elimu bora na jumuishi nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango wa Foundation iliobebwa na kauli mbiu “Connecting for Good” inayohakikisha hakuna mtoto anayeachwa nyuma. Kupitia uwekezaji wake endelevu kwenye sekta hii, Foundation inasaidia lengo kuu la TEA kuleta elimu bora na sawa kwa wote. TEA ilianzishwa mwaka 2001 kusimamia Mfuko wa Elimu ulioanzishwa kwa lengo la kusaidia jitihada za serikali kwa kufadhili maendeleo ya elimu ya ngazi zote Tanzania bara na elimu ya juu Tanzania visiwani.

Mradi wa E-Fahamu unaonyesha uwezo mkubwa wa mtandao wa Vodacom na teknolojia kwa pamoja kujenga uchumi stahimivu kupitia uwekezaji makini ambapo tovuti zote zenye maudhui ya elimu hayatozwi kwa watumiaji ili kuwawezesha kufikia shule na vyuo bila gharama. “Tunajivunia kupokea heshima kubwa kama hii kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Heshima hii inaongeza azma yetu kuendelea kushirikiana na serikali kuleta elimu bure kwa wote.” Alisema Rosalynn Mworia, Mkurugenzi wa Foundation.

E-Fahanu ni jukwaa linalowapatia waalimu vifaa vinavyoboresha utoaji wa masomo na kuwapa wanafnzi maudhui mengi kuwawezesha kujifunza kwa kasi yao wenyewe na kuelewa vizuri zaidi yanayofundishwa darasani. Imejaza pengo linalotokana na upungufu wa vitabu kwa kutoa maudhui mengi kutosha bila gharama. Mradi unawasaidia waalimu kuwa na wakati rahisi Zaidi kupanga masomo yao kutokana na upatikanaji kwa haraka maelezo wanayohitaji. Mmoja wa waalimu hao ni Mwalimu Damian Mtono wa Shule ya Sekondari ya Mtakuja. “Nilikuwa napitia vitabu kuandaa notes kwa wanafunzi wangu, inachukuwa muda na juhudi nyingi na wengi wetu tumekuwa tukipata wakati mgumu kwa sababu kwanza inabidi kuvipata vitabu vyenyewe ambavyo viko vichache,” alisema Mwalimu Damian.

 “Instant Schools ilibadilisha kila kitu. Niliweza kupata maudhui kwa haraka na urahisi Zaidi kutokana na kutumia mpango huu nimekuwa mwalimu bora wa Bilojia wilayani wanafunzi wangu asili mia 71 wakipasi,” aliongezea.

Masomo ya sayansi kwa jumla yanaonekana kuwa magumu kuelewa lakini masomo yaliyko kwenye jukwaa la Instant Schools ni rahisi kusoma na kuelewa na yanaelezea kwa upana somo lote. Wanafunzi pia wanasifu faida za jukwaa. “Jukwaa la Instant Schools ni zuri kiasi kwamba natumia kuwafundisha wadogo zangu walioko madarasa ya msingi kwa sababu kuna vitabu na maudhui ya shule kuanzia chekechea hadi sekondari.” Alisema Happoiness Juma, wakai huo akiwa mwanafunzi wa shule ya Mtakuja.

Hadi sasa Zaidi ya shule 190 zinatumia jukwaa la Instant Schools. Mradi hu una mingine inayotekelezwa na VTF inafanikiwa kutokana na mtandao mpana wa Vodacom. Vodacom imedhamiria kusaidia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kutumia mtandao wake kupambana na changamaoto za kila siku zinazowakumba watu katika jamii. Hii inaendana na mkataba wa jamii wa kampuni kusaidia vipaumbele vya serikali. “Vodacom Tanzania ina minara Zaidi ya 2,000 ya 4G inayoleta mtanado wenye kasi Zaidi nchini. Hii pamoja na kuondolewa gharama kwa tovuti ya elimu inachochea kasi ya engo letu kuwafikia wanafunzi milioni moja ifikapo mwaka 2025,” alisema Rosalynn Mworia.

 “Tumeona mabadiliko makubwa, chanya kupitia mradi huu. Huu mradi unaboresha viwango vya elimu wanayopata wanafunzi, mabadiliko yanayoonekana kwenye ufahamu mkubwa wa maswala ya TEHAMA, kuongezeka kwa kujiamini, kufurahia Zaidi mafunzo na kuboreka kwa viwango mashuleni,” aliongeza.

E-Fahamu ni mradi pacha wa Instant Schools ulioanzishwa mwaka 2013 kwa ushirikiano kati ya Vodafone Foundation na UNHCR kuwapa wakimbizi vijana, jamii zinazowapokea na waalimu wao maudhui ya elimu kupitia mtandao. Kila shule inapata vifaa ikiwa ni pamoja na tablet ya mwalimu na kompyuta kwa wanafunzi. Vifaa vinawekewa maudhui ya nchini inayoendana na mitaala ya kitaifa. Zaidi ya kusaidia mafunzo ya msingi darasani, stadi wanazojifunza wanafunzi kupitia mradi huu zinaongeaz uwezo wao kupata ajira na kuwapatia fursa nyingi zaidi maishani.

Baadhi ya watoto walioko kwenye kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu, mkoani Kigoma wakitumia baadhi ya vifaa vya kujisomea vilivyotolewa na kampuni ya Vodacom Tanzania PLC kupitia Taasisi yake ya Vodacom Tanzania Foundation. Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) hivi karibuni ilitoa cheti kwa kampuni ya Vodacom kwa kutambua juhudi endelevu za kuunga mkono sekta ya elimu hapa nchini




CMSA YATOA HATIFUNGANI INAYOKIDIHI MATAKWA YA SHERIA ZA KIISLAMU

$
0
0
MAMLAKA ya Masoko ya mitaji na dhamana (CMSA) imetoa hati fungani inayokidhi matakwa ya sheria za Kiislam yaani Sharia Complicant Capital Market Product (Sukuk Wakala) ya Kampuni ya Imaan Finance ambapo hati za uwekezaji katika hati fungani zimetolewa rasmi.

Akisoma hotuba hiyo leo katika hafla hiyo kwa Niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA, Kaimu Mkurugenzi wa Sera,Utafiti na mipango wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), Alfred Mkumbo amewashukuru wageni waalikwa na wadau wote wa sekta ya fedha kwa kuweza kutenga muda kutoka kwenye ratiba zao na kuweza kuhudhuria hafla hiyo muhimu.

Amesema utoaji wa Hatifungani ya Sukuk Wakala ya Kampuni ya Imaan Finance Limited ni matokeo chanya ya ushirikiano wa wadau katika sekta ya masoko ya mitaji wenye lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, za kuhakikisha kwamba Sekta ya Fedha inawezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa Kampuni za wajasiriamali wadogo na wa kati.

Amesema hatua hiyo ni muhimu, kwani ina matokeo chanya katika ukuaji wa sekta binafsi, umma na uchumi wa nchi kwa ujumla.

" Utoaji wa Hatifungani hii ni matokeo ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) wenye lengo la kuziwezesha Kampuni mbalimbali kutumia fursa zilizopo katika masoko ya mitaji, ikiwa ni pamoja na kupata mitaji ya muda mrefu ya kugharamia miradi ya Maendeleo.

Hatua hii ni muhimu, kwani inatarajia kuongeza idadi ya wawekezaji katika masoko ya mitaji, na hivyo kuchangia utekelezaji wa Mpango Kabambe wa Taifa wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha (National Financial Sector Development Master Plan 2019/20 – 2029/30; Mpango wa tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22–2025/26 (The Third Five Year National Development Plan (FYDP III) wenye dhima ya “Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu”; na Mpango Jumuishi wa Huduma za Kifedha hapa nchini (National Financial Inclusion Framework)," Amesema.

Ameipongeza Bodi na Uongozi wa Kampuni ya Imaan Finance kwa kufanikisha uuzwaji wa Hatifungani ya Sukuk Wakala na hatimaye Hati za Uwekezaji katika Hatifungani hii zinatolewa rasmi.

Amesema kuwa CMSA iliidhinisha maombi ya Kampuni ya Imaan Finance Limited kuuza hatifungani yenye thamani ya Shilingi bilioni 2.0 kwa Mpango wa Uwekezaji binafsi yaani Private Placement kwa mujibu wa Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Sura ya 79; na Miongozo ya Masoko ya Mitaji na Dhamana ya Utoaji wa Hatifungani ya mwaka 2019, yaani “Capital Markets and Securities (Guidelines for the issuance of Corporate Bonds, Municipal Bonds and Commercial Papers), 2019”.

" Hatifungani hii imekuwa ya kwanza katika historia ya sekta ya fedha hapa nchini ambayo inayokidhi matakwa ya Sharia yaani Sharia Compliant Product.

Fedha zilizopatikana kupitia mauzo ya hatifungani hii zitatumika kutekeleza Mpango Mkakati wa kutoa mikopo kwa Kampuni zinazoendesha biashara zinazokidhi matakwa ya Sheria za Kiislam, itakayowezesha wawekezaji kugawana faida inayopatikana kwenye biashara (Profit Sharing)," Amesema.

Amesema dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ni kuona kuwa Sekta ya Fedha inawezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kutoa mikopo kwa gharama nafuu.

Kaimu Mkurugenzi wa Sera,Utafiti na mipango wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), Alfred Mkumbo (wa pili kushoto) akikabidhi kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA hati fungani inayokidhi matakwa ya sheria za Kiislam yaani Sharia Complicant Capital Market Product (Sukuk Wakala) ya Kampuni ya Imaan Finance kwa viongozi Waandamizi wa Benki ya KCB,kulia ni Kaimu MKurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Bi.Antonia Kilama pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma za Kiislam Amour Muro (pili kulia).Kushoto ni Afisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Imaan Financge Ltd,Faiz Arab pamoja na Mwenyekiti wa Bodi wa Wakurugenzi ya Kampuni ya Imaan Finance Ltd Aunali Fidahussein Rajabali.Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa Sera,Utafiti na mipango wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA), Alfred Mkumbo (wa pili kushoto) akikabidhi kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA hati fungani inayokidhi matakwa ya sheria za Kiislam yaani Sharia Complicant Capital Market Product (Sukuk Wakala) ya Kampuni ya Imaan Finance kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela,.Kushoto ni Afisa mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Imaan Financge Ltd,Faiz Arab pamoja na Mwenyekiti wa Bodi wa Wakurugenzi ya Kampuni ya Imaan Finance Ltd Aunali Fidahussein Rajabali (kulia) wakishuhudia tukio hilo.Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.





Sehemu ya wageni waalikwa mbalimbali waliofikwa kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam

SAFARI YA KUSAKA MAKOMBE IMEANZA KUNAKO MSIMU WA 2021/22

$
0
0

*Bashiri na Meridianbet, Uwe Miongoni Mwa Mabingwa!

WAKATI Ligi Kuu soka barani Ulaya zikiendelea, baadhi ya mashindano kuanza kushika kasi huku timu zingine zikiisaka tiketi ya kucheza mashindano ya Ulaya. EFL, UEFA, Europa na Uefa Europa League kuendelea wiki hii. Meridianbet mambo yapo hivi;


Jumanne hii, Watford atachuana na Crystal Palace kwenye mashindano ya EFL Cup. Hapa zinakutana timu mbili zinazocheza EPL, vita ya huku ni tofauti kidogo – kila timu kuisaka nafasi ya kusonga mbele kwenye mashindano haya. Meridianbet tumekuwekea Odds ya 2.45 kwa Watford.


Kwenye kuiwania tiketi ya Uefa, PSV kurudiana na Benfica jumanne usiku. Mchezo wa kwanza Benfica alishinda akiwa nyumbani, atafanikiwa kumuondoa PSV na yeye kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa? Mchongo mzima upo kwenye Odds ya 2.05 kwa PSV.


Jumatano utachezwa mchezo kati ya Shakhtar Donetsk vs Monaco, huu ni mchezo ambao AS Monaco wanaingia uwanjani wakiwa na deni ya goli 1 walilofungwa kwenye mchezo wa kwanza. Wataweza kulipa deni na hata kuwaondoa Shakhtar? Idhamini timu yako kupitia Meridianbet kwa kuifuata Odds ya 2.50 kwa Monaco.


Arsenal ataianza safari ya kuwania kombe la EFL dhidi ya West Bromwich Albion. Maisha ndani ya EPL yamewaendea kombo The Gunners kwenye michezo yao miwili ya mwanzo kwa kupokea vipigo mfululizo. Wataweza kuwapa matumaini mashabiki wao kwenye mashindano haya? Hapa kuna Odds ya 1.86 kwa Arsenal ndani ya Meridianbet.


Alhamisi hii kutakua na mchezo wa kuiwania nafasi ya kucheza mashindano ya Europa msimu huu. Hapa kuna mtanange kati ya CFR Cluj na Crvena Zvezda. Mchongo mzima upo ndani ya Nyumba ya Mabingwa- Meridianbet. Ifuate Odds ya 2.40 kwa Crvena Zvezda.


Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!

TUME YA MADINI KUIMARISHA USIMAMIZI MADINI UJENZI, VIWANDANI

$
0
0

 Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Medini, Mhandisi Yahya Samamba (kulia), akizungumza jambo kwenye Semina Elekezi kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula (katikati) na kushoto ni Kamishna wa Madini wa Tume ya Madini Janeth Ruben.


Asteria Muhozya na Tito Mselem Dodoma
IMEELEZWA kuwa, pamoja na mambo mengine, ili kufikia lengo la kukusanya Shilingi 650 Bilioni iliyopangiwa Wizara ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022, Tume ya Madini itaweka nguvu kubwa katika Usimamizi wa Madini ya Viwandani na Ujenzi ili yaweze kuchangia ipasavyo.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba Agosti 23, 2021 wakati akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Majukumu ya Tume ya Madini na hali ya upatikanaji na Utoaji wa Huduma katika Masoko kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Tume ya Madini zinaonesha kuwa, katika Mwaka wa Fedha 2020/2021 Madini ya Ujenzi yalichangia asilimia 2 na Madini ya Viwandani yalichangia asilimia 2.

Aidha, itakumbukwa kuwa, mapema mwezi Mei, 2021 mara tu baada ya Wizara kuwasilisha Bungeni Hotuba yake ya Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2021/22, Tume ya Madini iliwasilisha wizarani mapendekezo ya mkakati kuhusu namna ya kufikiwa kwa makusanyo hayo ambapo miongoni mwa yaliyopendekezwa ni pamoja na kuimarishwa kwa usimamizi katika madini ya ujenzi.

Akizungumzia hali ya utoaji na upatikanaji wa huduma katika masoko ya Madini Samamba alisema kuwa, tangu kuanzishwa kwa Masoko ya Madini mwezi Machi 2018, hadi kufikia Juni 2021, jumla ya Masoko ya Madini 41 na Vituo Vidogo vya Ununuzi 59 vimeanzishwa na kuongeza kwamba, kati ya masoko yaliyoanzishwa, 26 ni ya dhahabu, masoko 14 ni ya madini ya vito na soko 1 ni la Madini ya Bati.

‘’ Mhe. Mwenyekiti kati ya vituo 59 vya ununuzi wa Madini vilivyoanzishwa, vituo 55 ni vya ununuzi wa Madini ya dhahabu, vituo 2 ni vya ununuzi wa madini ya vito na dhahabu, 1 cha madini ya almasi na 1 cha madini ya vito,’’ alisema Mhandisi Samamba.

Akielezea hali halisi ya mapato katika masoko, Mhandisi Samamba aliieleza Kamati kuwa, tangu kuanzishwa kwa masoko hayo mwaka 2018 hadi kufikia mwezi Juni 2021, usimamizi wa masoko ya madini umeendelea kuimarika ambapo katika kipindi rejewa kilogram 32,592.84 za dhahabu, karatu 32,636.59 za Madini ya almasi na kilogramu 144,102.09 za Madini ya bati ziliuzwa kupitia masoko hayo.

Pia, aliongeza kuwa, karati 249,869.53 za tanzanite, kilogramu 3,461,183.27 na karati 47,029.11 za Madini ya vito mbalimbali ziliuzwa kupitia masoko hayo na kuipatia Serikali jumla ya shilingi bilioni 258.17.

‘’Mchango wa masoko kwenye mapato yatokanayo na Madini umeongezeka kutoka asilimia 2.62 mwaka 2018/19 hadi kufikia asilimia 26.44 mwaka 2020/21,’’ aliongeza Mhandisi Samamba.

Akizungumzia mchango wa masoko ya Madini kwa Mwaka wa Fedha 2020.2021, alisema masoko hayo yamechangia kiasi cha shilingi bilioni 145.23 sawa na asilimia 26.44 ya mapato yatokanayo na mrabaha na ada za ukaguzi ikilinganishwa na mwaka 2019/20 ambapo masoko hayo yalichangia kiasi cha shilingi bilioni 104.63 sawa na asilimia 21.28.

Aidha, akielezea matazamio katika Masoko ya Madini aliyataja baadhi kuwa ni pamoja na mapato yanayotokana na madini yanatazamiwa kuongezeka kutokana na kufutwa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa Madini yanayoingizwa ndani ya nchi, kurejea kwa mnada wa Madini ya vito Arusha ambako kunatarajia kuvutia uingizaji wa Madini ya vito na ununuzi kutoka nchi za nje na hivyo kuchochea mzunguko na mitaji ya wafanyabiashara wakubwa kuongezeka.

Vodacom yashirikiana na Samsung kuzindua simu mpya ya Samsung A22

$
0
0




Ili kuongeza wigo wa matumizi ya simujanja, kampuni ya teknolojia na mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC imeungana na kampuni ya Samsung kuzindua simu mpya aina ya Samsung A22, pichani Mkuu wa Mauzo na Usambazaji waVodacom Tanzania PLC George Lugata (Kushoto) na Meneja wa Samsung Tanzania Suleiman Mohamed wakionesha simu hiyo wakati wa uzinduzi. Ongezea simu hii inakuja na ofa maalum ya dakika za bure, MB na SMS, na inapatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini, lakini pia katika maduka ya Samsung.

MAHAKAMA YAMALIZA MGOGORO WA KANISA LA SILOAM

$
0
0

Mwandishi Wetu

Mahakama Kuu ya Tanzania imemaliza mgogoro wa muda mrefu wa Kanisa la Siloam, linalojulikana kama Siloam Ministry International, dhidi ya aliyekuwa mmoja wa Makuhani wa Kanisa hilo, Elisha Eliya Miaka1000 aliyewahi kujulikana kwa jina la Nathaniel Zabulon Rusumo. Kuhani huyu alikuwa amepora mamlaka ya Uongozi wa Kanisa hilo kinyume cha taratibu.

Mgogoro huo ulianza baada ya kifo cha Mwanzilishi na Kiongozi mkuu wa Huduma hiyo, Mtume na Nabii Nduminfoo Zebedayo Munuo, aliyefahamika kwa jina la Eliya Ad2 MunguwaMajeshi ambaye alitwaliwa na Mungu Novemba 16, 2014, ndipo Elisha Eliya Miaka1000 alijipa madaraka ya kumrithi kiongozi huyo bila kufuata utaratibu wa Katiba ya Huduma ya Siloam.

Kutokana na hatua hiyo ya kujipa madaraka hayo, Elisha Eliya Miaka 1000, alisababisha mgawanyiko wa waumini akashawishi baadhi wamuunge mkono ili wapore mali mbalimbali za huduma yakiwemo majengo ya ibada na kuondoka na sadaka kupeleka nyumbani kwake.

Serikali kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Msajili wa Vyama vya Jamii walijaribu kutatua mgogoro huo lakini E.E. Miaka1000 alikataa utengamano.

Kutokana na matukio hayo Bodi ya wa Wadhamini ililazimika kumshtaki Mahakama Kuu ya Tanzania, kupitia kesi ya madai namba 24 ya mwaka 2017.
Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyosomwa na Jaji Leila Mgonya Julai 23, 2021, baada ya kusikiliza kesi hiyo upande mmoja kwani mdaiwa hakufika mahakamani, ilikubaliana na maelezo ya wadai na ikatoa amri walizokuwa wakiziomba. 

Katika hukumu hiyo, Mahakama Kuu ilitoa amri za zuio la kudumu dhidi yake yeye Elisha Eliya Miaka1000, mawakala wake, watumishi wake na mtu yeyote atumikae kwa niaba yake kutokutumia na kutokusajili jina la The Pool of Siloam Church au Kanisa la Siloam mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia mahakama hiyo iliamuru kuwa Elisha Eliya Miaka1000 kwa kuwa hakuwa kiongozi wa Kikatiba ndani ya Siloam Ministry InternationaI haruhusiwi kufanya shughuli za kiutawala zikiwemo kuwateua au kuajiri makuhani au waumini na kuwahamisha kwa jina la The Pool of Siloam Church.

Vilevile mahakama hiyo ilimwamuru Elisha Eliya Miaka1000 au yeyote anayetumika kwa niaba yake kukabidhi mara  moja, maeneo, viwanja, majengo na mali zote za Siloam Ministry InternationaI walizokuwa wanazitumia kwa jina la Siloam Ministry InternationaI au The Pool of Siloam Church na kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Kwa mujibu wa maelezo ya wadai,  Siloam Ministry International (SMI)   ilianzishwa mwaka 2003 na kuongozwa na Mtume na Nabii N.Z Munuo, aliyefahamika pia kwa jina la Eliya Ad2 MunguwaMajeshi.

Huduma hiyo ilisajiliwa na Serikali ya Tanzania, Wizara ya Mambo ya Ndani kwa hati namba SO.12880 iliyotolewa Agosti 9, 2005, ambapo ilieneza Injili ya Yesu Kristo na kujenga makanisa maeneo mbalimbali nchini.

Tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo mwaka 2003 hadi mwanzilishi huyo alipotwaliwa na Mungu Novemba 16, 2014, huduma hiyo ilikuwa imeshakubalika ndani na nje ya nchi, ambapo kazi ilipanuka na kujenga vituo vya huduma katika mikoa mbalimbali nchini.

Kwa muda wote huo kabla ya kutwaliwa kwa mwanzilishi wake, kulikuwa na mshikamano, amani na heshima miongoni mwa waumini na viongozi na hapakuwepo na dalili zozote za uvunjifu amani katika kanda zote Saba za huduma hiyo zilizokuwa zimeanzishwa.

Mwaka 2007 aliingia katika huduma hiyo muumini aitwaye Nathaniel Zabuloni Rusomo ambaye baadae alijulikana kwa jina la Elisha Eliya Miaka1000 akiwa na matatizo mbalimbali ambapo aliombewa na kufunguliwa kisha akajiunga na huduma ya Siloam Bible School ambapo alifundishwa utumishi.

Wakati tayari akiwa kuhani wa kanda ya Dar es Salaam Miaka 1000 alisaliti kiapo cha utumishi, kwani baada ya kiongozi mkuu wa huduma hiyo kutwaliwa na kabla ya mchakato wa kumpata kiongozi mwingine, yeye alijivua safu ya ukuhani na akajipa cheo cha Mzeituni, Mpaka Mafuta, Mzee wa Siku, Wakili wa Mungu, mungu aliyetuma wote, baba wa uzao, baba halisi nk.

Mpaka aliacha kabisa imani aliyoikuta Siloam na aliazimia kupora thamani, uzuri na kibali cha kusanyiko la Siloam akiwa kwenye majengo ya Siloam.
Aliwapindua waumini kwa kuingiza mafundisho yaliyoacha maswali na hadithi za Kanisa Halisi la Mungu baba. E. E. Miaka1000 alitumia mbinu mbalimbali za kuvuruga safu za makuhani mikoani ambapo aliwashawishi waungane naye kusaliti maono ya mwanzilishi wa Huduma.

Ili kuhalalisha mapinduzi  hayo alitunga Katiba yake akitaka kusajili The Pool of Siloam Church lakini haikupitishwa na Serikali kwa kuwa hakuwa mmoja wa viongozi wa Kikatiba. Hivyo, alizalisha mzozo ili Serikali ifute usajili halali wa Siloam Ministry InternationaI.

Hata hivyo hilo nalo halikufanikiwa.
Hivyo yeye na kundi lake la waumini aliofanikiwa kuwashaiwishi katika vituo mbalimbali waliendelea kutumia mali na majengo ya SMI kufanyia ibada na kuondoka na sadaka.

Serikali, viongozi na makuhani waaminifu walijitahidi kunusuru mgogoro huo lakini Miaka 1000 alikataa utengamano kwa madai kuwa yeye ni mungu na hawezi kujadiliwa, kuhojiwa wala kushauriwa.MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemaliza mgogoro wa muda mrefu wa Kanisa la Sloam, linalojulikana kama Huduma ya Kimataifa ya Siloam (Siloam Ministry International) dhidi ya aliyekuwa mmoja wa makuhani wa kanisa hilo, Elisha Eliya aliyekuwa amepora mamlaka ya kanisa hilo kunyume cha taratibu.

Mgogoro huo ulianza baada ya kifo cha mwanzilishi wa kiongozi mkuu wa huduma hiyo, Mtume na Nabii Nduminfoo Zebedayo Munuo, kwa jina maarufu Eliya na Adam wa Pili au Munguwa Majeshi aliyetwaliwa na Mungu Novemba 16, 2014, ambapo Elisha Eliya ambaye alijipa madaraka ya kumrithi kiongozi huyo bila kufuata utaratibu wa Katiba yake.

Kutokana na hatua hiyo ya kujipa madaraka, Elisha Eliya maarufu kama Miaka 1000, kulisababisha mgawanyiko wa waumini ambapo aliwashawishi baadhi waliomuunga mkono na wakapora mali mbalimbali za huduma yakiwemo majengo ya ibada na kuondoka na ibada.

Pia Miaka 1000 alijaribu kutaka kubadili usajili wa huduma hiyo kwa jina la The Pool of Sloam Church Kanisa la Siloam lakini akakwama.

Kutokana na matukio hayo Bodi ya Wadhamini ililazimika kumshtaki Mahakama Kuu ya Tanzania, kupitia kesi ya madai namba 24 ya mwaka 2007.

Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyosomwa na Jaji Leila Mgonya Julai 23,2021, baada ya kusikiliza kesi hiyo upande mmoja kwani mdaiwa hakufika mahakamani, ilikubaliana na maelezo ya wadai na ikatoa amri walizokuwa wakiziomba. 

Katika hukumu hiyo, Mahakama Kuu ilitoa amri za zuio la kudumu dhidi Elisha Eliya, mawakala wake, watumishi wake na mtu yeyote atumikae kwa niaba yake kutokutumia na kutokusajili jina la The Pool of Siloam Church au Kanisa la Siloam mahali popote ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia mahakama  imeamuru kuwa Elisha Eliya, Miaka 1000 kwa kuwa hakuwa kiongozi wa Kikatiba SMI na haruhusiwi kufanya shughuli za kiutawala zikiwemo kuwateua au kuaji ri makuhani au waumini na kuwahamisha kwa jina la The Pool of Soam Churchht.

Vilevile mahakama imemuamuru Elisha Eliya Miaka 1000 au yeyote anayetumika kwa niaba yake kukabidhi mara  moja, maeneo, viwanja, majengo na mali zote za SMI walizokuwa wanazitumia kwa jina la SMI au The Pool of Siloam Charch na kulipa gharama zote za kesi hiyo.

Kaika kesi hiyo Bodi ya Siloam iliwakilishwa na mawakili tofautitotofati katika hatua mbalimbali akiwemo Jerome Msemwa, mon Ndunguru na Salha Mlilima aliyehusika katika hatua ya mwisho ya usikilizwaji wa ushahidi.

Mdaiwa, Miaka 1000 aliwakilishwa na ambaye alijitoa mwaka 2019 wakati kesi ikiwa katika hatua ya usuluhishi ambao ulikwama mbele ya Jaji John Mgetta, baada ya Miaka 1000 kukataa kwenda mahakamani kwa ajli ya usuluhishi.

Awali Miaka 1000 kupitia kwa wakili wake Sweetber Nkuba aliwasilisha maelezo yake ya utetezi wa maandishi,

Katika maelezo hayo alikana madai yote ya mdaia, akidai kuwa hakukaa kutii maelekezo ya Serikali na kwamba wala hapakuwepo na ukiukwaji wa Katiba ya Siloam kama ilivyoelezwa na mdai.

Zaidi alidai kuwa hapakuwepo na aina ypouote udhalilishaji kutokuwa na immani wala dhidi ya mdaiwa na kwamba mdai anapaswa kuthibitisha madai yake hayo.

Hata hivyo mamelezo hayo ya maandishi ya mdaiwa  yalitupiliwa mbali na Mahakama Machi 27, 2020 baada ya mdaiwa kutokufika mahakamani wakati wa usuluhishi, hivyo mahakama ikaamuru kesi kuendelea na usikilizwaji wa upande mmoja.

Katika usikilizwaji huo mdaiwa alithibitisha kesi yake kupitia kwa wakili mmoja tu Thebeti Eliya, Kuhani wa Siloam, ambaye ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa SMI.

Kwa mujibu wa maelezo ya wadaiwa, Huduma ya Siloam Ministry International (SMI)   ilianzishwa na kuongozwa na Mtume na Nabii N.Z Munuo, maarufu kama Eliya, Mungu wa Majeshi, mwaka 2003.

Huduma hiyo ilisajiliwa na Serikali ya Tanzania, Wizara ya Mambo ya Ndani kwa hati namba SO.12880 iliyotolewa Agosti 9, 2005, ambapo ilieneza Injili ya Yesu Kristo na kujenga makanisa maeneo mbalimbali nchini.

Tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo mwaka 2003 hadi mwanzilishi huyo alipotwaliwa na Mungu Novemba 16, 2014, huduma hiyo ilikuwa imeshakubalika ndani na nje ya nchi, ambapo kazi ilipanua na kujenga vituo vya huduma katika mikoa mbalimbali nchini na habari zake zilienea mpaka nje ya nchi.

Kwa muda wote huo kabla ya kutwaliwa kwa mwanzilishi wake, kulikuwa na mshikamani  amani na heshima miongoni mwa waumini na viongozi na hapakuwepo na dalili zozote za uvunjifu amani katika kanda zote Saba za huduma hiyo zilizokuwa zimeanzishwa.

Mwaka 2007 aliingia katika huduma hiyo muumini aitwaye Elisha Eliya Miaka 1000,  au Nathanile Zabuloni Rusomo akiwa na matatizo mbalimbali ambapo alifunguliwa aliombewa na kufunguliwa kisha akajiunga na huduma ya Siloam Bible School ambapo alifundishwa utumishi.

Wakati tayari akiwa kuhani wa kanda ya Dar es Salaam Miaka 100o alisaliti kiapo cha utumishi, kwani baada ya kiongozi mkuu wa huduma hiyo kutwaliwa na kabla ya mchakato wa kumpata kiongozi mwingijne, yeye alijivua safu ya ukuhani na akajipa cha Mzeituni, Mpaka Mafuta, Mzee wa Siku, Wakili wa Mungu, mungu aliyetuma wote, baba wa uzao, baba halisi nk.

Mpaka aliacha kabisa imani aliyoikuta Siloam na aliazimia kupora thamani, uzuri na kibali cha kusanyiko la Sloam akiwa kwenye majengo ya Sloam.

Aliwapindua waumini kwa kuingiza mafundisho yaliyoacha maswali na hadithi za Kanisa Halisi la Mungu baba. Miaka 1000 alitumia mbinu mbalimbali za kuvuruga kwa kutumia kanuni ya (kugawanya kisha kutawala) safu za makuhani mikoani ambapo aliwashawishi waungane naye kusaliti maono ya mwanzilishi wa SMI.

Ili kuhalalisha mapinduzi  hayo alitunga Katiba yake akitaka kusajili The Pool of Siloam Church lakini hakuweza kupitishwa na Serikali kwa kuwa hakuwa mmoja wa viongozi wa Kikatina. Hivyo alizalisha mzozo ili Serikali ifute usajili halali.

Hata hivyo hilo nalo halikufanikiwa japo alitumia njama za kiharamia kama zilizosababisha viongozi wa SMI kuwekwa rumande, kuwatishia maisha yao pamoja na makuhani waaminifu katika huduma ya SMI.

Hivyo yeye na kundi lake la waumini aliofanikiwa kuwashaiwishi katika vituo mbalimbali waliendelea kutumia mali na majengo ya SMI kufanya ibada na kuondoka na sadaka.

Serikali, viongozi na makuhani waaminifu walijitahidi kunusuru mgogoro huo lakini Miaka 1000 alikataa utengamano kwa madai kuwa yeye ni Mungu baba na hawezi kujadiliwa, kuhojiwa wala kushauriwa.

Mahakama katika uamuzi wake ilisema kwa kulingana na ushahidi ni jambo la ajabu ni kwa namna gani mdaiwa aliweza kujichukulia madaraka bila kufuata mchakato wa Kikatiba kama inavyotakiwa.

Mahakama hiyo ilisema kuwa kitendo cha mdaiwa kupora madaraka ya uongozo katika jamii iliyostaarabika ya kidini kama hiyo hakikubaliki na kwamba kwa kitendo hicho alisababisha mkakanyio na hali ya kutokuelewana na mgawanyiko miongoni mwa waumini na na viongozi kwa kuwaondoa katika kusudi la msingi la kuhubiri, kufundisha maelekezo ya Mungu na huduma kwa waumini.

Mahakama hiyo imeonya kwamba viongozi wa kidini hawapaswi kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani badala yake wahimize amani na umoja.

Mahakama hiyo imetoa wito kwa wana Siloam kurejea na kufanya kazi pamoja kama timu bila kujali tofauti zao zilizopita bali wajielekeze kwenye agenda yao kuu ya kuhubiri injili na kuwafundisha waumini matendo mema ambayo yanamvutia Mwenyezi Mungu.

Hivyo ilisema kuwa kutokana na maelezo hayo mahakama inaamua kuwa mdai anastahili amri alizoziomba na kwamba mdaiwa alivamia majengo ya Mdai na kuweka mabango katika makanisa ya mdai Dar es Salaam, Dodoma, Njombe, Arusha Manyara na mahali kwingineko nchini.


 

Nathanael Zabron Rusumo a.k.a Elisha Eliya Miaka1000(MDAIWA)

 

 


 

Viewing all 49473 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>