Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 49567 articles
Browse latest View live

OLIMPIKI NA NGAO YA HISANI KUKUPA USHINDI MNONO

$
0
0

 

*Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!


WAKATI mashindano ya Tokyo Olimpiki 2020 yakielekea ukingoni, baadhi ya Ligi Soka barani Ulaya kuanza kutimua vumbi wikiendi hii na zingine kuanza wiki ijayo. Meridianbet, hatukuachi nyuma – zifaute Odds bora za wikiendi hii kama zilivyo;


Ijumaa hii, vijana wa Mexico watachuana na Japan katika mchezo wa kuwania medali ya shaba kunako mashindano ya Olimpiki. Timu hizi zilikua kwenye Kundi A zikimaliza hatua ya makundi katika nafasi ya 1 na 2. Kupoteza michezo ya nusu fainali dhidi ya Brazili na Uhispania, kunazifanya timu hizi kukutana kwenye kuwania mshindi wa tatu. Meridianbet tumekuwekea Odds ya 2.50 kwa Mexico.


Jumamosi itakua ni wikiendi ya kibabe! Fainali mbili kuchezwa ndani ya siku moja, unapiga pesa mchana na usiku. Hii ndio Meridiabet! 


Brazili uso kwa uso na Uhispania katika mchezo wa Fainali ya mashindano ya Olimpiki, bingwa wa mchezo huu ataondoka na medali ya dhahabu huku aliyefungwa akiondoka na medali ya fedha. Huku kuna mkongwe Dani Alves na Richarlson, kule kuna Marcos Asensio na Pedri, hapatoshi!! Odds ya 2.50 inakusubiri kwa Brazili.


Nchini Uingereza kutachezwa mchezo wa ufunguzi wa msimu mpya wa EPL. Kihistoria, mchezo wa Ngao ya Hisani ndio ishara ya kuanza kwa msimu mpya nchini Uingereza. Jumamosi hii, Leicester City atachuana na Manchester City baada ya kutwaa ubingwa wa FA na EPL msimu uliopita. Meridianbet tumekuwekea Odds ya 1.96 kwa Man City.


Jumapili tutatupia jicho kwenye wiki ya kwanza ya Ligue 1 kule nchini Ufaransa. Mabingwa watetezi – Lille watawafuata Metz katika mchezo wa kwanza wa kutetea ubingwa wao walioupata msimu uliopita. Lille wataweza kutetea ubingwa msimu huu? Meridianbet tumekuwekea Odds ya 1.79 kwa Lille.


Unapokuwa na Meridianbet, huna sababu ya kufikiria ushindi. Ndani ya Nyumba ya Ushindi, dau lako ni ushundi wako!


DK SERERA AKEMEA SIASA ZA UANAHARAKATI SIMANJIRO

$
0
0

 DK SERERA AKEMEA SIASA ZA UANAHARAKATI SIMANJIRO


Na Mwandishi wetu, Simanjiro

MKUU wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Dk Suleiman Serera, amewataka wanasiasa, viongozi na wananchi wa eneo hilo kuachana na siasa za unaharakati na kugeukia siasa za maendeleo.

Dk Serera ameyasema hayo alipotembelea na kukagua shule ya serikali ya msingi ya Bilionea Saniniu Laizer ya mchepuo wa kiingereza iliyojengwa na mchimbaji huyo maarufu wa madini ya Tanzanite.

Amesema maendeleo ya wilaya ya Simanjiro hayatapatikana endapo kutakuwa na siasa za uanaharakati badala ya kulenga kwenye malengo ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

Amesema kila mmoja akiimba wimbo wa maendeleo watafika mbali kwa maendeleo ila wakianza kuweka kipaumbele kwenye siasa hizo za uanaharakati hawatafika popote.

“Mimi nikiwa na kauli moja, mbunge akiwa na kauli moja, Mwenyekiti wa halmashauri na madiwani tukiwa na kauli moja ya maendeleo tutaifikisha mbali Simanjiro yetu,” amesema Dk Serera.

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Manyara, Kiria Laizer amesema baadhi ya watu wasio na nia njema wamekuwa wanamkatisha tamaa bilionea Laizer kwa maneno ya uzushi.

“Bilionea Laizer amekuwa akisaidia jamii ila kumekuwa na wakatishaji tamaa wanajenga hoja za fitina kwa lugha ambazo hawafanyi utafiti, zinazorudisha nyuma maendelo,” amesema Laizer.

Bilionea Laizer amesema shule hiyo imekuwa tumaini kwa jamii ya wafugaji na wakulima wadogo ila wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa walimu.

“Nitajenga bwalo la kulia chakula hivyo tunaiomba serikali ijenge bweni ili Esto wa wafugaji na wakulima waweze kulala na tuwabane wasome na kusaidia jamii baadae,” amesema bilionea Laizer.

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Silvanus Tairo amesema shule hiyo ilianza kujengwa madarasa mawili na hivi sasa imekamilisha madarasa yake.

“Tunampongeza mdau wetu wa maendeleo bilionea Laizer ambaye ameacha alama kubwa kwa kujenga shule hii ambayo ni ukombozi wa elimu kwani ni ya mfano kwa mkoa,” amesema Tairo.  

Teknolojia Kuboresha Maombi ya Leseni Huduma za Mawasiliano

$
0
0

 

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa utoaji wa leseni kwa njia ya Mtandao wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.Waziri wa Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa akizungumza kuhusiana na mapinduzi ya Sekta ya Utangazaji pamoja na Mfumo wa Uombaji leseni kwa njia ya Mtandao utapolea mapinduzi makubwa nchini.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dk.Faustine Ndugulile pamoja na Waziri wa Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa wakiwa katika uzinduzi wa Mfumo wa Uombaji leseni kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeanza kutumia Mfumo mwingine wa Maombi ya leseni kwa kundi la leseni kubwa; mfumo huo unamuwezesha muombaji wa leseni kuwasilisha maombi yake ya leseni kwa Mamlaka hiyo bila kulazimika kufika ofisini na kukutana ana kwa ana na maafisa wa leseni.

Mfumo huo laini wa maombi ya leseni (License Management System) unatarajiwa kuzinduliwa siku ya Jumamosi Tarehe 31 Julai mwaka huu na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile (Mb) akiwa sambamba na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Innocent Bashungwa Mawaziri ambao kwa pamoja wizara zao zinasimamia sekta za Mawasiliano na Utangazaji kupitia Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

Mfumo huo mpya wa maombi ya leseni kupitia tovuti ya TCRA ambayo ni www.tcra.go.tz utasaidia kuongeza ufanisi wa upatikanaji leseni kwa wateja wanaonuia kutoa huduma za Mawasiliano na utangazaji, kurahisisha mchakato wa mteja kupata huduma za leseni, utaokoa muda wa muombaji leseni, utaokoa gharama za ufuatiliaji kwa mwombaji mpya wa leseni au anaetaka kuhuisha leseni yake, utaongeza ufanisi kwa pande zote mbili yaani Mamlaka inayotoa leseni na mwombaji, utaongeza uwazi kwa kuwa utamwezesha mwombaji wa leseni kupata mrejesho moja kwa moja kwenye simu yake ya kiganjani au kupitia barua pepe juu ya hatua zote na maendeleo ya uchakataji wa leseni aliyoomba na kumwezesha Mwananchi kuendelea na shughuli za maendeleo badala ya kufuatilia leseni.

Makundi ya leseni yanayopatikana kwenye mfumo huu ambao mwombaji ataweza kuwasilisha maombi yake bila kulazimika kufika katika ofisi za TCRA ni pamoja na Leseni za pamoja ikihusisha leseni za Huduma ya Maudhui (Content Services), Huduma ya Mtandao (Network Services), Huduma ya Mifumo Tumizi (Application Services) na Miundombinu ya Mtandao (Network Facilities).

Leseni nyingine ni Leseni ya Huduma za Vifurushi na Vipeto, Leseni ya Mtumiaji wa Masafa, Leseni ya Matengenezo na Usimikaji, Leseni ya Uagizaji Nje na Usambazaji, Rasilimali za Utoaji Namba, Leseni ya Huduma za Posta kwa Umma na Leseni ya Vifaa Vilivyoidhinishwa.

Hatua ambazo mwombaji wa leseni husika atapaswa kufuata ni pamoja na kutembelea tovuti ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambayo ni www.tcra.go.tz kisha kugonga kiunga cha Utoaji Leseni na kisha kubofya kiunga cha Mfumo wa Kuomba leseni ambacho kitampeleka moja kwa moja kwenye ukurasa wenye fomu za kujaza ili aweze kupatiwa leseni anayohitaji kwa ajili ya kutoa huduma za Mawasiliano.

Hatua za maombi ya leseni za Mawasiliano kwa kundi la leseni kubwa (Individual License) zitasalia kama ilivyokuwa awali ambapo baada ya mwombaji kuwasilisha maombi yake kupitia Mfumo wa Maombi ya Leseni, itafuata hatua ya kutoa tangazo kwa umma kualika maoni ya wananchi juu ya mwombaji leseni, kisha tathmini kufanyika juu ya ombi lililowasilishwa, mwombaji kualikwa kutoa wasilisho la huduma ya Mawasiliano anayotarajia kuitoa na kisha hatua ya uidhinishaji leseni na hatimae mteja kupatiwa leseni.

Hatua hii inakuja ikiwa ni mkakati wa serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kurahisisha utaratibu wa upatikanaji huduma za leseni na kuweka mazingira rafiki zaidi kwa wawekezaji katika sekta ya Mawasiliano, sekta ambayo inatoa mchango chanya katika ukuaji wa maendeleo ya taifa.

BENKI YA NMB IKIKABIDHI MSAADA DAR KWA SHULE NA WASIOONA

$
0
0

 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija (mwenye skafu kushoto) akipokea sehemu ya msaada wa viti na meza za walimu toka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (kulia) hafla iliyofanyika Shule ya Sekondari Mchikichini jana jijini Dar es Salaam. Katika hafla hilo NMB ilikabidhi msaada wa Viti 190, meza 60 na Madawati 100 kwa Shule za Sekondari Kipunguni na Mchikichini, pamoja na Shule ya Msingi Kibaga zote za jijini Dar es Salaam.


 


Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija (mwenye skafu kushoto)  akikabidhi sehemu ya fimbo 500 za kuongozea wasioona zenye thamani ya shilingi milioni 14 kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Wasioona Tanzania (TAB), Bw. Omar Itambu na viongozi wa TAB jana jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na Benki ya NMB, wengine wanaoshuhudia ni maofisa waandamizi wa NMB (kulia).

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija (mwenye skafu kushoto) akikata utepe kuzinduwa sehemu ya msaada wa viti na meza za walimu zilizotolewa na Benki ya NMB kwa Shule za Sekondari Kipunguni na Mchikichini, pamoja na Shule ya Msingi Kibaga zote za jijini Dar es Salaam, kulia mwenye suti ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard. Msaada huo uliotolewa jana na NMB unasamani ya shilingi 14,700,000/-.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Ng'wilabuzu Ludigija (wa nne kulia) pamoja na Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard (wa tatu kulia) wakimkabidhi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Wasioona Tanzania (TAB), Bw. Omar Itambu sehemu ya fimbo 500 za kuongozea wasioona zenye thamani ya shilingi milioni 14 jana jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na Benki ya NMB, wengine wanaoshuhudia ni maofisa waandamizi wa NMB (kulia).
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Wasioona Tanzania (TAB), Bw. Omar Itambu (mwenye kipaza sauti) akiishukuru Benki ya NMB mara baada ya kupokea sehemu ya fimbo 500 za kuongozea wasioona zenye thamani ya shilingi milioni 14 jana jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na Benki ya NMB, wengine wanaoshuhudia ni maofisa waandamizi wa NMB (kulia).

SERIKALI KUSITISHA VIBALI VYA UAGIZAJI WA SUKARI IFIKAPO 2022-WAZIRI MKENDA

$
0
0

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kongamano la saba la wadau wa sekta ya kilimo kuhusu sera pamoja na kutathmini shughuli za kilimo nchini, leo tarehe 5 Agosti 2021 linalofanyika katika ukumbi wa Asante Estates uliopo katika eneo la Ntyuka Jijini Dodoma.Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kongamano la saba la wadau wa sekta ya kilimo kuhusu sera pamoja na kutathmini shughuli za kilimo nchini, leo tarehe 5 Agosti 2021 linalofanyika katika ukumbi wa Asante Estates uliopo katika eneo la Ntyuka Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo).

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kongamano la saba la wadau wa sekta ya kilimo kuhusu sera pamoja na kutathmini shughuli za kilimo nchini, leo tarehe 5 Agosti 2021 linalofanyika katika ukumbi wa Asante Estates uliopo katika eneo la Ntyuka Jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa
Afisa Mtendaji Mkuu wa Jukwaa la kuendeleza kilimo kusini mwa Tanzania SAGCOT akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kongamano la saba la wadau wa sekta ya kilimo kuhusu sera pamoja na kutathmini shughuli za kilimo nchini, leo tarehe 5 Agosti 2021 linalofanyika katika ukumbi wa Asante Estates uliopo katika eneo la Ntyuka Jijini Dodoma.



Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma

Serikali imesema ifikapo Mwaka 2022 itasitisha utoaji wa vibali vya kuagiza sukari nje ya nchi kwa makampuni ambayo ndio wazalishaji wa ndani wa bidhaa hiyo.

Upungufu wa bidhaa hiyo nchini hautokani na uhaba wa miwa bali unasababishwa na makampuni kushindwa kuongeza uchakataji wa miwa kutoka kwa wakulima.

Waziri wa Kilimo Mhe. Prof. Adolf Mkenda ameyasema hayo leo tarehe 5 Agosti 2021 katika ukumbi wa Asante Estates uliopo katika eneo la Ntyuka Jijini Dodoma aliposhiriki katika kongamano la saba la wadau wa sekta ya kilimo kuhusu sera pamoja na kutathmini shughuli za kilimo nchini.

“Baada ya mwaka huu Serikali haitotoa vibali kwa wawekezaji waliopewa viwanda vya sukari kuagiza sukari nje kwani tayari watakuwa wamefikia uwezo wa kuzalisha sukari toshelevu ikiwa ni pamoja na kukamilika kwa uanzishwaji wa viwanda vipya vya sukari hapa nchini”

Waziri Mkenda amesema kuwa zaidi ya Tani 350,000 za miwa ya wakulima katika Bonde la Kilombero mkoani Morogoro zinateketezwa kwa moto kutokana na kukosa soko la uhakika lakini viwanda haviongezi uwezo wa kuchakata miwa ili kuzalisha sukari ya kutosha.

Amesema kuwa zaidi ya Tani 40,000 zinaagizwa kutoka nje ya nchi jambo ambalo sio sahihi kwani viwanda vya sukari vilivyopo nchini vinapaswa kuongeza uwezo wao ili kuimarisha soko la wakulima jambo litakalopelekea nchi kutoagiza sukari.

Waziri Mkenda amesema kuwa mtu yeyote atakayeingiza sukari kiholela ni wasaliti wa nchi hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amesema kuwa kuna wimbi kubwa la ukosefu wa ajira hususani kwa vijana lakini viwanda vimeshindwa kuongeza uwezo wake wa kuzalisha sukari ili kuimarisha sekta ya ajira kwa wananchi.

Katika mkutano huo Waziri Mkenda ameipongeza serikali na mawaziri waliotangulia kuiongoza Wizara ya Kilimo kwa kusimamia vyema sekta ya kilimo ikiwa ni pamoja na kufanikisha kupunguza wimbi kubwa la uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi.

RC DKT SENGATI KUWA MKALI UFUATILIAJI WA RASIMALI FEDHA ZA MIRADI

$
0
0

 Na Anthony Ishengoma -Shinyanga

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amsema hatakuwa legelege katika kusimamia rasilimali fedha zinazotolewa na serikali au wananchi kwa ajili kutekeleza miradi ya maendeleo na hata sita kuchukua hatua kali kwa watendeji wabazilifu.

Dkt. Sengati alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bw. Joseph Mkude kusimamia miradi kwa karibu kwasababu katika Wilaya yake kuna shida ya wizi na uzembe na baadhi ya watendaji hawana dhamira ya kufanya kazi kwa lengo la kutoa matokeo makubwa.

Dkt. Sengati alisema hayo jana kwenye ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa iliyofika Shule ya Sekondari Ukenyenge Wilayani kishapu kukagua mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na ukarabati wa miundombinu chakavu ya shule hiyo.

Dkt. Sengati alitoa agizo hilo kufuatia ziara ya ukaguzi wa miradi chini ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Bw. Mabala Mlolwa kukataa taarifa ya Mkuu wa Shule aliyoitoa mbele ya kamati hiyo kuwa ukarabati wa chumba cha mahabara utagharimu kiasi cha shilingi milioni 30.

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Bw. Mabala Mlolwa aliutaka uongozi wa shule na watendaji wa Wilaya ya Kishapu kuhakikisha kiasi hicho fedha kinatumika vizuri na kukarabati vyumba vitatu badala ya chumba kimoja ili kazi itakoyofanyika iendana na thamani ya fedha.

Aidha Bw. Mlolwa alioji matumizi ya fedha na kuonya kuwa wananchi watakata tamaa ikiwa hatutamia kiasi hicho cha fedha kukamilisha vyumba vitatu na kuwataka wafanye kazi hiyo kama ambavyo michango ya kujitolea ya wananchi inavyofanya vizuri katika ujenzi wa baadhi ya vyumba vya madarasa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Modest Mkude alihaidi kwenda sambamba na watendaji hao kwa kuwa katika maeneo mengine fedha kama kama izo zimekuwa zikitumiaka vizuri hata kuongeza ofisi ya walimu katika kiasi hicho cha fedha kinachotolewa na serikali.

Mkude aliomba kupatiwa orodha ya bidha na bei zilizoainishwa kwa ajili ya ukarabati wa majengo hayo ili aweze kuzipatia kwa lengo la kujilidhisha na kuona baini tatizo liko wapi ili aweze kurekebisha mapungufu yaliyopo.

Aidha kiongozi huyo wa Wilaya alibainisha kuwa kama viongozi wangeachia suala hilo kupita bila kuoji kiasi kikubwa cha fedha kingebaki na kupata matumizi ambayo sio sawa nakuhaidi kulivalia njuga suala hilo.

Wakati huhuo Muhandisi wa Mkoa wa Shinyanga Francis Magoti aliongeza kuwa vifaa vionavyohitajika katika ukarabati wa mahabara hiyo ni vya kawaida na kumtaka muhandisi wa Wilaya Matoke Kyando kufanya kazi kwa karibu na shule hiyo kuhakikisha ufamisi unakuwa mzuri na unaoendana na thamani ya fedha.

Pamoja na kasoro hiyo kubainika pia ziara ya Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga pia haikufurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mwaweja na kuomba Mkuu wa Mkoa kupeleka timu ya wataalamu kufanya uchunguzi zaidi kujilidhisha na matumizi ya rasilimali katika mradi huo.

Ziara ya Kamati ya Siasa imehitimisha kazi yake ya kutembelea miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga ambayo imfanyika katika Halmashauri za Msalala, Kishapu, Ushetu, Kahama Manispaa, Halmashauri ya Shinyanga na Manispaa ya Shinyanga.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga Bw. Mabala Mlolwa akifungua maji ndani ya chumba ya cha mahabara ambacho kinafanyiwa ukarabati pamoja na kamati yake walipofika Shule ya Sekondari Ukenyenge kujionea maendeleo ya ukarabati wa mahabara hiyo jana Kishapu Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akisaidia kusogeza kifusi cha udongo kusaidia wanazengo wa Kijiji cha Mwamala wanaojitolea nguvu zao kuchimba shimo kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwamala Kishapu Mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Shinyanga Bw. Mabala Mlolwa akisaidia kusogeza kifusi cha udongo kusaidia wanazengo wa Kijiji cha Mwamala wanaojitolea nguvu zao kuchimba shimo kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo vya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mwamala Kishapu Mkoani Shinyanga.

PROFESA KABUDI: SERIKALI KUJENGA MAHAKAMU KUU KATIKA MIKOA TISA

$
0
0

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (katikati) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Viongozi wa Idara za Serikali ya Wilaya ya Ikungi wakati akikagua jengo linalojengwa la Kituo cha Polisi wilaya humo.Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Viongozi wa Idara za Serikali

Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi akikagua jengo linalojengwa la Kituo cha Polisi Wilaya ya Ikungi. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu.
Na Dotto Mwaibale, Singida
SERIKALI kuanza ujenzi wa Mahakama Kuu katika mikoa tisa nchini iliyobaki ukiwemo Mkoa wa Singida ili kuondoa tatizo la wananchi kusafari kwenda mikoa ya jirani kwa ajili ya kupata huduma za Kimahama.

Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi wilayani Ikungi mkoani hapa katika ziara yake ya kukagua Mahakama za wilaya na za Mwanzo pamoja na kuzungumza na wadau wa masuala ya Sheria.

Kabudi alisema alisema mpango wa ujenzi wa mahakama hizo utaenda pamoja na ujenzi wa mahakama za wilaya hasa kwenye wilaya ambazo hazina mahakama.

" Wilaya ya Ikungi nayo itaingizwa kwenye mpango wa ujenzi wa mahakama ya wilaya kwa sababu mpaka sasa haina mahakama ya wilaya ambapo wananchi wanafuata huduma za kimahakama mjini Singida,". alisema Profesa Kabudi.

Aidha Waziri Kabudi amewapongeza viongozi wa Wilaya ya Ikungi kwa kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama ya wilaya na kusema jambo hilo ni nzuri na linapaswa kuigwa na wilaya nyingine.

Akizungumzia kuhusu ukarabati wa mahakama za mwanzo nchini, Profesa Kabudi alisema utafanyika kwa awamu na kipaumbele kitatolewa kwenye Mahakama za Mwanzo ambazo zinahudumia idadi kubwa ya wananchi.

Unilever Yadhamini Mbio Za Watoto Rock City Marathon.

$
0
0

Kampuni ya Unilever Tanzania imekabidhi hundi yenye thamani Tsh milioni 20 kwa waandaaji wa mbio za Rock City Marathon ikiwa ni udhamini wa kampuni hiyo katika mbio za km 2.5 mahususi kwa ajili ya watoto. Mbio hizo  zinatarajiwa kufanyika Oktoba 24 mwaka huu, kwenye viunga vya Rock City Mall jijini Mwanza.

Hatua hiyo inatajwa kuwa ni muendelezo wa mkakati wa kampuni hiyo katika kushirikiana na jamii na serikali kwa ujumla katika kuhamasisha michezo nchini ili kuibua vipaji, kujenga afya pamoja na kukuza sekta ya michezo nchini.

Wakizungumza kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya hundi yenye thamani ya sh mil 20 kutoka kampuni ya Unilevel Tanzania kwenda kwa waandaaji wa mbio hizo kampuni ya Capital plus international (CPI), Mkurugenzi Mtendaji  wa Unilever Tanzania Bw David Minja pamoja na Mratibu wa mbio hizo kutoka CPI Bw Kasara Naftal walisema ushirikiano huo mpya ni ishara nzuri kwa mustakabari wa mchezo huo sambamba na ukuaji wa sekta ya utalii Kanda ya Ziwa.

“Tumeamua kudhamini tukio hili kwa sababu linawaleta pamoja watu kutoka nyanja mbalimbali katika maisha wakiwemo watoto ambao ni miongoni mwa wadau wetu wakubwa.,’’ alisema Bw Minja, huku akibainisha kuwa mbio hizo za km 2.5 kwa ajili ya watoto zitafahamika kama ‘Unilever Rock City Junior Challenge.’

Alisema ‘Unilever Rock City Junior Challenge’ inalenga kutoa fursa kwa watoto ambao ni miongoni mwa watumiaji wakubwa wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo ikiwemo sabuni ya OMO, sabuni ya Sunlight na mafuta ya kujipaka ya Vaseline ambao wataibuka washindi kwenye mbio hizo kuweza kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo vifurushi maalum vyenye bidhaa hizo.

“Kwa kuwa bidhaa zetu zinahusisha zaidi matumizi ya kifamilia nitoe wito kwa wazazi na wanafamilia kwa ujumla wajitokeze kwa wingi huku wakihamasisha watoto pia washiriki kwenye mbio hizi ili kuongeza ushindani. Unilever tunawahakikishia kwamba zawadi kwa watoto zitakuwa ni nyingi na za kutosha,’’ alisema.

Kwa upande wake Bw Naftal pamoja na kuishukuru kampuni ya Unilever kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na kampuni hiyo katika kuboresha mbio hizo, alisema kufuatia uwepo wa kampuni ya Unilever kwenye mbio hizo mwaka huu, inatarajiwa kwamba ‘Unilever Rock City Junior Challenge’ itakuwa ni moja ya kivutio kikubwa miongoni mwa matukio yanayotarajiwa kupamba mbio hizi.

Akifafanua zaidi kuhusu ‘Unilever Rock City Junior Challenge’ Bw Naftal alisema pia itahusisha utafutaji wa vipaji vya riadha kutoka kwenye baadhi ya shule za msingi jijini Mwanza kwa wanafunzi wenye umri wa miaka 5 hadi 10 ambapo washindi pamoja na kujipatia zawadi mbalimbali kutoka Unilever pia watapata tiketi zitakazowawezesha  kuchuana kwenye kilele cha mbio hizo.

“Tangu kuanzishwa kwa mbio hizi huu ukiwa ni msimu wa 12 sasa tumekuwa tukihusisha ushiriki wa watoto kwa namna mbalimbali. Ila mwaka huu tunaamini mbio za watoto zinakwenda kutikisa vichwa vya habari. Kupitia ushindani tunaoutarajia kwenye mbio hizi sasa tunaamini kwamba lengo letu la kuibua vipaji vipya vya riadha linakwenda kutimia…asanteni sana Unilever kwa kuwekeza kwa watoto’’ alishukuru.

Alisema maandalizi ya mbio hizo zinazotarajiwa kuhusisha washiriki zaidi ya 3000 wakiwemo wakimbiaji wa kimataifa, wakimbiaji kutoka mashirika mbalimbali, wanafunzi sambamba na watu wenye ualbino yanaendelea huku akitoa wito kwa washiriki kuendelea kujisajili kupitia njia ya simu na tovuti

Mratibu wa Mbio za Rock City Marathon Bw Kasara Naftal (Kushoto) akipokea mfano wa hundi yenye thamani Tsh milioni 20 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji  wa kampuni ya Unilever Tanzania Bw David Minja (Kulia) ikiwa ni udhamini wa kampuni hiyo kwenye mbio za km 2.5 mahususi kwa ajili ya watoto ambazo ni sehemu ya mbio za Rock City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 24 mwaka huu, kwenye viunga vya Rock City Mall jijini Mwanza. Katikati ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Unilever Tanzania Bi Lilian Kibbassa.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Unilever Tanzania Bw David Minja (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mratibu wa Mbio za Rock City Marathon Bw Kasara Naftal pamoja na Meneja Masoko wa Kampuni ya Unilever Tanzania Bi Lilian Kibbassa (Kulia)

 

Meneja Masoko wa Kampuni ya Unilever Tanzania Bi Lilian Kibbassa (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mratibu wa Mbio za Rock City Marathon Bw Kasara Naftal pamoja na Mkurugenzi Mtendaji  wa kampuni ya Unilever Tanzania Bw David Minja (Kulia)

Mratibu wa Mbio za Rock City Marathon Bw Kasara Naftal (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji  wa kampuni ya Unilever Tanzania Bw David Minja pamoja na Meneja Masoko wa Kampuni ya Unilever Tanzania Bi Lilian Kibbassa (Kulia)

 

 



 


BETWAY YATANGAZA KUINGIA TANZANIA

$
0
0

Hadhara Charles, mtaalamu wa kuchezea mpira akionesha ufundi wake wakati wa tukio la utambulisho wa kampuni ya Betway Tanzania. Uzinduzi umefanyika Agosti 11, 2021 jijini Dar es Salaam.

11 Agosti 2021 - Dar es salaam
Betway, kampuni ya kimataifa ya michezo ya kubashiri, wameingia rasmi katika soko la Tanzania. Lengo la kampuni hiyo ni kutoa huduma bora, za kipekee na rahisi kwa wapenzi wa michezo ya kubashiri nchini Tanzania ambao wanaweza kubashiri michezo ya ndani na ya kimataifa. 

Wakati kampuni inaanzishwa mwaka 2006, lengo la Betway lilikuwa ni kuleta ushindani katika tasnia ya michezo ya kubashiri. Kampuni imeendelea kukua mwaka hadi mwaka.

Hii imetuwezesha kuingia kwenye soko la Tanzania tukiwa na michezo mingi, yenye masoko tofauti ya kubashiri, mfumo wetu wa kubashiri Live na eSports ni wa kisasa zaidi. 

Tunajivunia kufanya kazi katika nchi ambazo sekta ya michezo ya kutabiri imeratibiwa, kwa sasa tuna leseni za kufanya kazi katika nchi 12 ikiwa ni pamoja na Kenya, Ghana, Afrika Kusini, Uganda, Zambia, Msumbiji na Nigeria. Tunayo matumaini makubwa kwamba uwekezaji wa kampuni yetu katika soko la Tanzania utapelekea Tanzania kuwa kitovu cha mafanikio ya michezo katika bara la Afrika. 

Katika kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea, tumeweka machaguo mbalimbali ambayo yanakidhi uwezo wa mtanzania wa kawaida. Wateja wanaweza kuweka pesa kwenye akaunti zao na kutoa pesa kwa urahisi na salama kwa kutumia njia mbali mbali za malipo. Kwa kusaidia wateja kuanza safari yao ya kubashiri, mteja mpya atapata Free Bet TSh 3,000 kwa kujisajili.

Kwa niaba ya serikali ya Tanzania, Mkurugenzi wa Idara ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Addo Komba ameikaribisha Betway nchini Tanzania na kuwahakikishia ushirikiano kutoka serikalini na kwa wadau wengine wa michezo.

“Ninafurahi kupewa heshima kuwa mgeni rasmi katika hafla hii muhimu sana ya kuikaribisha Betway nchini Tanzania. Serikali inafurahi kuona wawekezaji wapya kama Betway wanaingia Tanzania kwa nia ya kuunga mkono juhudi za maendeleo katika michezo. Betway ni kampuni kubwa ya michezo ya kubashiri kwa hivyo uamuzi wao wa kuja Tanzania ni ishara nzuri kwetu kwamba tunapiga hatua na wako tayari kutusukuma zaidi”, alisema Komba.

Mbali na kutoa burudani ya kusisimua uwanjani, pia tuna mipango kadhaa ya kusaidia jamii nje ya uwanja. Ni kwa mapenzi yetu ya michezo na nia ya maendeleo ya michezo tunauwezo wa kutoa msaada kwa jamii katika michezo yenye uhitaji. 

Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe alisema kwamba;
“Ni wakati mzuri katika sekta ya michezo ya kubashiri na tunaamini kwa uzinduzi wa bidhaa hii yenye ubora wa kimataifa kwenye soko, tunauwezo wa kuleta msisimko kwa wanaobashiri na mashabiki, wakati bado tunarudisha kwa jamii kupitia miradi mbali mbali ya michezo.”

Kama kampuni ya michezo ya kubashiri, ni jukumu letu kuhakikisha tunaweka mazingira rafiki kwaajili ya kubashiri kistaarabu.

Kuhusu Betway Group
Betway Group ni kampuni inayotoa huduma ya daraja la kwanza kwenye michezo ya kubashiri. Ilianzishwa mwaka 2006, kampuni inafanya kazi katika nchi mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda, Ghana, Afrika Kusini, Zambia, Msumbiji, Nigeria na Tanzania.
Betway inajivunia kuwapa wateja wake huduma bora za kubashiri, kuwaburudisha, kuwapa taarifa pamoja na kuhakikisha wanashiriki michezo ya kubashiri katika mazingira salama.
Kwa maelezo zaidi kuhusu Betway tembelea: www.betway.co.tz

Benki ya NMB kuwezesha wananchi kupata kwa haraka hati za umiliki Ardhi

$
0
0

 


Benki ya NMB imezindua huduma mpya ya mkopo wenye riba nafuu kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wenye kipato cha chini kutekeleza takwa la kisheria la kurasmisha makazi yao ijulikanayo kwa jina la ‘NMB Plot Loan.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ndani wa NMB, Benedicto Baragomwa aliyasema hayo wilayani Mbarali katika Mkoa wa Mbeya wakati wa Uzinduzi rasmi wa Programu ya Kitaifa ya Urasimishaji wa Makazi ambayo inatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Benki hiyo na Wizara ya Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi.

Alisema Benki ya NMB itawasaidia wananchi kulipia gharama zote za urasimishaji wa makazi/ardhihabari kuanzia upimaji wa viwanja mpaka uandaaji wa Hatimiliki na kwamba mwananchi atalipa kidogo kidogo ndani ya miaka miwili.

Alisema riba ya mkopo huo ni asilimia 10 na kwamba mwananchi atapatiwa hatimiliki baada ya kukamilisha urejeshaji wa mkopo wake katika benki hiyo.

“Tumeanzisha huduma hii kwa sababu kuna wananchi wamekuwa wakishindwa kurasmisha makazi yao kutokana na kukosa fedha za kulipia gharama za urasmishaji, wananchi wakisharasimisha makazi yao na kupatiwa hatimiliki watakuwa na sifa za kukopesheka na benki yoyote,” alisema Baragomo.

Alisema Mwananchi yeyote ambaye atakopeshwa mkopo huo atafunguliwa akaunti ya NMB bila gharama yoyote kwa maelezo kuwa fedha hizo zinapitia benki na hata marejesho yatapitia benki.

Akizindua Programu hiyo ya Urasmishaji wa makazi kitaifa, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliipongeza Benki ya NMB kwa kuanzisha huduma hiyo akidai kuwa itasaidia wananchi kupandisha hadhi makazi yao.

Alisema asilimia kubwa ya wananchi wanaishi kwenye makazi holela ambayo yamejengwa bila kufuata sheria na hivyo Serikali badala ya kuyabomoa imeamua kuyarasimisha ikishirikiana na Benki ya NMB ushirikiano ambao alisema haujawahi kutokea.

Lukuvi alisema kwa mujibu wa sheria kila mwananchi anatakiwa kujenga nyumba kwenye kiwanja kilichopimwa, chenye hatimiliki na lazima apate Kibali cha Ujenzi kitu ambacho alidai watanzania wengi hawatekelezi na hivyo kuwa na idadi kubwa ya makazi holela.

“Tulianza kutekeleza urasmishaji huu wa makazi mwaka 2013 lakini mpaka sasa tumefikia asilimia tano pekee nchi nzima, hii ilikuwa inasababishwa na wananchi wengi kukosa fedha za kugharimia, sasa hii huduma ya NMB Plot Loan itatusaidi kurasimisha makazi mengi zaidi,” alisema Lukuvi.

Hata hivyo alisema awali gharama za urasimishaji wa makazi ilikuwa Sh. 150,000 lakini sasa hivi Serikali imepunguza kiwango hicho na kufikia Sh. 130,000 na kwamba kwa sasa gharama hizo zitabebwa na Benki ya NMB na wananchi watalipa kidogo kidogo.

Alisisitiza kwamba kwa sasa mtu yeyote ambaye amejenga mjini ni lazima arasimishe makazi yake tofauti na wale wanaoishi maeneo ya vijijini ambao utaratibu utaendelea kuboreshwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera alisema zoezi hilo la urasmishaji wa makazi utasaidia kupunguza migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo yakiwemo yanayopakana na Hidahi.

Aliwataka wananchi kuchangamkia fursa ya mkopo huo ambao una riba ndogo na kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kurasmisha makazi yao huku akimhakikishia Waziri Lukuvi kuwa watashirikiana kukamilisha zoezi hilo.

Waziri wa Ardhi - William Lukuvi akizindua Mpango wa Kitaifa wa Urasimishaji Makazi/Ardhi uliofanyika katika Kijiji cha Igawa Wilayani Mbarali mkoani Mbeya, wengine katika picha kutoka kushoto, ni Mkuu wa Wilaya Mbarali -  Reuben Mfune, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya -Juma Homera, Kaimu Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Benki ya NMB -Benedicto Baragomwa, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi - Mary Makondo na Mkufunzi Chuo cha Ardhi - Dkt. Victoria Mwakalinga.

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi - William Lukuvi akipongezana na Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Benki ya NMB - Benedicto Baragomwa mara baada ya uzinduzi wa Mpango wa Kitaifa wa Urasimishaji Makazi katika Kijiji cha Igawa Wilayani Mbarali mkoani Mbeya.



Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi - William Lukuvi akimnyanyua mkono Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera ikiwa ni ishara kukamilisha kwa uzinduzi wa mpango wa Kitaifa urasimishaji makazi ambao umeanzia wilayani Mbarali mkoani Mbeya. Kulia ni Kaimu Mkaguzi Mkuu wa ndani wa Benki ya NMB Benedicto Baragomwa.
 

Dereva wa Bolt ajivunia mafanikio yake

$
0
0

 Na Mwandishi Wetu


Fabian Shao (32) anasema kuwa baada ya kuacha kazi ya udereva katika shirika moja la kimataifa na kuamua kujiajiri na kuwa dereva wa Bolt amepata mafanikio makubwa katika maisha yake.

Shao, ambaye ni mkazi wa Chanika Dar es Salaam ana mke na Watoto watatu, anasema kuwa amefanya kazi na shirika hilo ambalo akutaka liandikwe kwa miaka miwili lakini baada ya kuingia bolt amepata mafanikio makubwa pamoja na kuwa mjasiriamali kwa kufungua biashara.

Anaeleza kuwa hakuwa rahisi uamuzi aliochukua wa kuacha kazi pamoja na uamuzi wa kuchukua mkopo wa gari wa riba nafuu kwani mke wake hakuamini kuwa angeweza kufanikiwa.

Shao, anasema kuwa kilichomsukuma kuchukua mkopo ni kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu bila mkataba wa kidumu huku mshahara anaolipwa kutokidhi mahitaji yake na kushindwa kutimiza malengo yake.

Anasema kuwa ilifika wakati, kuwalipia ada Watoto wake ambao mmoja anasoma kidato cha kwanza na wapili darasa la tano na watatu darasa la tatu ilikuwa ngumu, kutokana na kipato kidogo na kukosa chanzo kingine cha mapato.

"Nilikuwa nafanya kazi katika shirika moja kubwa tu hapa Dar es Salaam, kama Dereva, nimefanya kwa Miaka miwili bila kuona nikisogea kimaendeleo ndipo nilipoamua kuacha kazi na kuchukua mkopo na kununua gari kwa ajili ya Bolt," amesema na kuongeza kuwa;

"Niliweka malengo na nimefanikiwa, ndani ya Mwaka mmoja nimemaliza mkopo, na kwa sasa nimenunua gari nyingine, Watoto wangu wana uhakika wa kusoma, nimefungua sehemu ya kuosha magari (car wash) na nimempa mtaji mke wangu wa kufuga kuku wa kisasa, kwakweli najivunia sana kuwa Dereva wa Bolt," amesema

Amewapa ushauri vijana kufanya kazi ya usafiri mtandaoni na Bolt kwani ni kampuni ambayo inawasaidia vijana kujikwamua katika maisha pamoja na kutimiza malengo yao.

Ameongeza kuwa utaratibu wa bolt waliouweka wa kuwajali madereva wake kwa kuwapa elimu ndio kitu kilichomvutia kwani wanakipa mwanga wa nini cha kufanya katika kazi yako ya udereva wa bolt.


Vodacom yakabidhi zawadi kwa mshindi wa promosheni ya Tusua Mapene

$
0
0

 



 Mshindi promosheni ya Vodacom wa zawadi kubwa ya Tusua Mapene Tsh 179,000,000, Ramadhani Ismail Bwaniki akikabidhiwa zawadi yake kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Bi Esther Alexander Mahawe katika hafla iliyofanyika uwanja wa katubuka mkoani Kigoma jana mchana.

MSIMU MPYA, VIBE JIPYA NDANI YA EPL NA LALIGA WIKIENDI HII

$
0
0

  *Burudika na Msimu Mpya wa Soka Ukiwa na Familia ya Meridianbet!

BAADA ya kukaa miezi 3 bila soka la vilabu barani Ulaya, hatimaye Agosti 13,2021 imefika na viwanja vyote kuanza kurindima kwa takribani miezi 8 ya msimu mpya wa soka 2021/22. VAR, vyenga vya kila aina, vita vya maneno ndani na nje ya uwanja – zote ni burudani za soka. Hakika, msimu mpya, vibe jipya! Tunaanza msimu mpya kwa namna hii;


Ijumaa hii, EPL itaukata utepe wa msimu mpya wa Ligi Soka nchini Uingereza kwa mchezo wa Brentford FC dhidi ya Arsenal. Wageni wa EPL – Brentford wataitupa karata yao ya kwanza dhidi ya vijana wa Mikel Arteta ambao hawatokua na michezo ya mashindano ya Ulaya baada ya kufanya vibaya msimu uliopita. Hii ni fursa ya timu hizi kuanza msimu huu kwa alama 3 muhimu kuelekea michezo 38 ya kukamilisha msimu. Meridianbet tumekuwekea Odds ya 1.95 kwa Arsenal.


Jumamosi kutachezwa mchezo wa mahasimu wa soka kwenye historia ya soka la Uingereza. Hapa ni Manchester United vs Leeds United ndani ya Old Trafford! Msimu uliopita, United alianza kwa kupoteza mchezo akiwa nyumbani. Lakini Leeds United alikula 6-2 alipocheza dhidi ya United pale Old Trafford, msimu huu itakuaje? Timu zote zimefanya usajili wa kutosha lakini dakika 90 zitaamua nyota ya nani itang’ara mbele ya mashabiki. Meridianbet tumekuwekea Odds Bora ya 1.54 kwa The Red Devils.


Pale Goodison Park, Rafael Benitez ataitupa karata yake ya kwanza akiwa kocha wa Everton kwenye mchezo dhidi ya Southampton. Benitez anakibarua cha ziada msimu huu, kuipata Imani ya mashabiki wa Everton ambao wengi wao wamepinga uamuzi wa klabu hiyo kumpatia mikoba ya Carlo Ancelotti. Ataweza kuwaonesha kuwa yeye ni mtu sahihi wa kuiongoza Everton licha ya kuwa aliwahi kuwa kocha wa Liverpool ambao ni mahasimu wakubwa wa The Toffees? Ifuate Odds ya 2.00 kwa Everton ukiwa na Meridianbet.


Macho ya wadau wengi wa soka la LaLiga na mashabiki wa FC Barcelona yatakua pale Nou Camp Jumapili hii. Barca watawaalika Real Sociedad kwenye mchezo wao kwanza bila Lionel Messi. Baada ya miaka 21, Messi ameondoka Nou Camp na sasa anapatikana kule Paris akiwa na Neymar Jr na Kylian Mbappe ndani ya PSG. Safari ya Barca bila nyota wao na nyota wa dunia yatakuaje? Mdhamini shujaa wako kupitia Meridianbet kwa kuifuata Odds ya 1.80 kwa Barcelona.


Wiki itaanza kwa mchezo wa Elche vs Athetic Bilbao kunako LaLiga Sentander. Msimu uliopita, timu zote zilikuwa zikidemadema kuokoa nafasi zao kwenye msimamo wa Liga hiyo, msimu huu wataanzaje na pengine watamaliza vipi? Mchongo upo Meridianbet, Odds ya 2.15 kwa Bilbao ipo kwa ajili yako.


Meridianbet, Nyumba Yenye Odds Bora na Bonasi Kubwa!


Karibu Dodoma Festival La Piga Hodi

$
0
0

Kamati ya Maandalizi ya karibu Dodoma Festival wakiwa na kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa wa WHUSM Mfaume Said katika picha ya pamoja.

Adeladius Makwega, WHUSM-Dodoma

Wasanii Mkoani Dodoma wameandaa tamasha linalofahamika kama Karibu Dodoma litakalo fanyika Oktoba 2021 ambalo lengo lake ni kutangaza miradi kadhaa ya kimkakati na ile isiyo kimkakati ya Serikali ya awamu ya tano na sita.

Wakizungumza katika kikao cha pamoja na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mji wa Serikali-Mtumba Jijini Dodoma kamati ya maandalizi imesema kuwa tamasha hilo litakuwa la kukata na shoka kwani litabeba kazi zote za Serikli ambapo miradi yote inyogusa jamii itaoneshwa.

“Tumejiandaa vilivyo na tunawajulisha Watanzania wote kuja kushuhudia tamasha hili ambapo Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo tumeiomba taasisi zake kama BASATA, COSOTA ziwepo ili kuweza kutoa huduma mbalimbali kwa watakaokuja kutazama tamasha hili letu.”Alisema Saimon Mwapagata ambaye ni msanii wa filamu nchini, akiwa mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo.

Tamasha hili litawakutanisha wasanii mbalimbali kama vile wa ngoma za asili, muziki wa kizazi kipya, filamu na vichekesho.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mfaume Said amesema kuwa wamefanya kikao  na kamti hiyo kwa pamoja wamekubaliana kuanza maandalizi ya kina kukamilisha tamasha la karibu Dodoma.

“Jambo hili ni la sekta yetu, tumelipokea, tumelijadili na tumekubaliana lifanyike Oktoba 2021 katika viwanja vya Nyerere Square.”

Mwenyekiti huyo kamati ya maandailizi aliambatana na katibu wake Eusted Rwegoshora na mjumbe Bi Wema Sekamba.


MBUNGE NEEMA LUGANGIRA ATEULIWA BALOZI WA COVID19

$
0
0

 




Mbunge Neema Lugangira  ameteuliwa kuwa Balozi wa harakati za kupambana na Ugonjwa unaosababishwa na Virusi vya Corona (Balozi wa UVIKO19 - COVID19).
MBUNGE wa Neema Lugangira ambaye pia ni Balozi wa Covid 19 akiwa na bango la kuhamasisha uvaaji wa barakoa na wananchi kuhakikisha wanachanja

 

MBUNGE wa Neema Lugangira ambaye pia ni Balozi wa Covid 19 wa kwanza kulia akiwa kwenye picha na Waziri wa Afya Maendeleo Jinsia Wazee na Watoto MBUNGE wa Neema Lugangira ambaye pia ni Balozi wa Covid 19 akifuatiwa na Msanii maarufu nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele 'Steve Nyerere' na Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini, Joyce Kiria.

Mbunge Neema Lugangira  ameteuliwa  Alhamisi ya Agosti 12 mwaka huu na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Dk. Dorothy Gwajima Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Mbunge Neema Lugangirq, wengine walioteuliwa ni Msanii maarufu nchini na Mwenyekiti wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao, Steven Mengele 'Steve Nyerere' na Mwanaharakati wa Kutetea Haki za Wanawake nchini, Joyce Kiria. 

Tangu janga la UVIKO 19 (COVID19) liingie nchini kwenye Wimbi la Kwanza hadi sasa Wimbi la Tatu, Mbunge Neema Lugangira ameonyesha kupambana na janga hilo huku akielimisha na kuhamasisha Watanzania kujikinga na kuchoma Chanjo ili kujikinga dhidi ya ugonjwa huu hatari duniani wa COVID19.

UFAFANUZI WA TAARIFA YA UPOTOSHAJI KUHUSU UTENDAJI KAZI WA TUME YA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0

 

Tume ya Utumishi wa Umma imeanzishwa chini ya Kifungu cha 9 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma (Sura ya 298 marejeo ya mwaka 2019), pamoja na majukumu mengine Tume ina jukumu la kupokea na kushughulikia rufaa kutoka kwa Watumishi wa Umma na Mamlaka za Nidhamu ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa dhidi yao,  kwa mujibu wa Kifungu cha 25 (1) cha Sheria hii na Kanuni ya 60 ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.

Tume ya Utumishi wa Umma inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa ya upotoshaji  kuhusu utendaji kazi wa Tume iliyotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” tarehe 12 Agosti 2021 kama ifuatavyo:-

1.    Kwa mujibu wa Kifungu cha 9(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma  Sura ya 298 (marejeo ya mwaka 2019), Tume inaundwa na Mwenyekiti na Wajumbe 6 ambao huteuliwa na Rais ambao pamoja na majukumu mengine wana jukumu la kisheria la kutolea uamuzi rufaa na malalamiko yanayowasilishwa mbele ya Tume. Aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 14(1) na (2) cha Sheria ya Utumishi wa Umma Sura ya 298 (marejeo ya mwaka 2019),   Tume ina Katibu ambaye ndiye Mtendaji Mkuu. Katibu na Wasaidizi wake (Sekretarieti) ndio watendaji wa kazi za kila siku katika Tume ya Utumishi wa Umma ambao wameteuliwa baada ya kukidhi sifa na vigezo katika nafasi walizo nazo.

2.    Pamoja na Sheria zilizopo, Tume inashughulikia rufaa kwa mujibu wa Mwongozo Kuhusu Mashauri ya Nidhamu na Rufaa kwa Watumishi wa Umma wa Mwaka 2009 ambapo rufaa hupokelewa, husajiliwa, huchambuliwa na kupitiwa na Kikao cha Menejimenti na hatimaye kuwasilishwa mbele ya Tume kwa uamuzi. Hatua ya mwisho ni Mrufani na Mrufaniwa kujulishwa kwa barua juu ya uamuzi unaotolewa na Tume. Utaratibu huu umewekwa ili kuimarisha utendaji kazi, kudhibiti upendeleo, rushwa na kuimarisha utoaji wa haki. Aidha, elimu kuhusiana na utaratibu huu imekuwa ikitolewa kwa wadau kupitia majukwaa mbalimbali.

3.    Tume katika kushughulikia rufaa na malalamiko haitoi uamuzi kwa shinikizo au ushawishi wa Mwajiri au Mamlaka ya Nidhamu yoyote ili kuwakandamiza watumishi wasipate haki zao. Tafsiri kuwa Tume ni chombo cha kulinda maslahi ya Waajiri na Serikali.  Tume inapenda kuufahamisha umma kuwa inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo.

4.    Rufaa na malalamiko yanayopokelewa Tume yenye vielelezo vilivyokamilika ndio yanayoshughulikiwa na kutolewa uamuzi kwa kadri yalivyopokelewa  (First in, First Out).

5.    Tume ya Utumishi wa Umma, inaomba umma kuupuuza upotoshwaji huu uliotolewa kupitia mtandao wa kijamii wa “Jamii Forum” na inatoa wito kwa umma na wadau wote kuwasiliana na Tume kwa ufafanuzi, maoni au suala lolote kuhusu Tume kupitia simu namba 0738166703, 0733 005 974  na barua pepe, secretary@psc.go.tz.

Imetolewa na:

 

John C. Mbisso

KAIMU KATIBU

TUME YA UTUMISHI WA UMMA

DAR ES SALAAM

 

13 AGOSTI, 2021


GSM HOME WAJA NA 'LIPA KIDOGO KIDOGO'

$
0
0
Pata bidhaa bora za GSM Home kwa mfumo wa kulipia kidogo kidogo

Kampuni inayoongoza kwa mauzo ya samani bora za majumbani na maofisini – kuanzia leo inawawezesha Watanzania wote kununua bidhaa zenye ubora wa kimataifa kupitia mfumo wa Lipa Kidogo Kidogo.

Akizindua huduma hiyo mpya ya Layby au ‘Lipa Kidogo Kidogo’ jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Biashara wa makampuni ya GSM, Bw. Allan Chonjo alisema kuwa mfumo huo wa ‘Lipa Kidogo Kidogo’ ni suluhisho sahihi kwa mahitaji ya wateja ambao wanataka bidhaa za kipekee za GSM kwa malipo nafuu zaidi, bila riba wala gharama ya maombi.

“Daima GSM tunawasikiliza na kuwajali wateja wetu. Ndio maana leo tunaanzisha mfumo mpya utakaowezesha mtu yeyote kuchagua na kulipia bidhaa na samani zetu za majumbani na maofisini kwa mfumo wa ‘Lipa Kidogo Kidogo,” alibainisha.

Kupitia mfumo huu, mteja anachagua bidhaa anayohitaji na kuingia katika makubaliano yanayompa uhuru wa kulipia kianzio cha asilimia 20, na kisha kama thamani ya bidhaa husika ni kati ya shilingi milioni moja na milioni tatu, atalipa salio ndani ya miezi mitatu, huku ikiwa thamani ya bidhaa ni zaidi ya milioni 3 atalipa salio ndani ya miezi 6.

“Sisi GSM Home tutakuhifadhia bidhaa alizochagua kwa uhakika na usalama hadi pale utakapokamilisha malipo yako. Sahau yale maumivu ya kupenda kitu na wakati bado unatafuta pesa ya kukinunua, unakuta kimenunuliwa tayari,” aliongeza.

Vile vile, kuanzia leo tarehe 13 Agosti hadi tarehe 15 Septemba, GSM Home wanaendesha promosheni kabambe itakayowawezesha wateja watakaofanya manunuzi ya TSH 500,000/= na zaidi kuzawadiwa vocha ya TSH 100,000/= wanayoweza kuitumia kufanya manunuzi zaidi kwenye maduka yote ya GSM - Max, Babyshop, Splash, Shoexpress, Anta Sports na Homebox.

Akizungumzia mfumo huo mpya wa ‘Lipa Kidogo Kidogo’ kutoka GSM Home, mteja aliyetembelea duka la GSM Home – Nuru Bakari aliwashukuru GSM kwa kuleta usawa katika manunuzi na kuongeza kuwa mfumo huo ni rafiki sana kwa wateja.

“Mfumo huu wa ‘Lipa Kidogo Kidogo’ utawasaidia sana Watanzania wasioweza kumudu gharama moja kwa moja, kwa kuwapa muda wa kujipanga na kuanza kulipia kidogo kidogo huku wakiwa na uhakika wa kuhifadhiwa bidhaa walizozipenda na kuzichagua. Inafurahisha kuwa unalipia bidhaa bila riba au gharama za maombi,” alisema.
Afisa Biashara Mkuu wa makampuni ya GSM , Allan Chonjo (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya  ya kununua bidhaa za GSM kwa kulipia kidogo kidogo "LAYBY - Lipa Kidogo Kidogo" ambapo mteja atachagua bidhaa anayohitaji na kuingia katika makubaliano yanayompa uhuru wa kulipia kianzio cha asilimia 20.  Kwa bidhaa ya thamani ya kuanzia milioni moja na tatu, mteja analipa salio ndani ya miezi mitatu, huku bidhaa yenye zaidi ya thamani ya milioni tatu atalipa ndani ya miezi sita. Kushoto ni Meneja wa Mauzo GSM, Fahad Mohammed.

MBUNGE KIRUMBA AKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA SHULE YA WASICHANA KISHAPU

$
0
0

Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (wa pili kushoto) akikabidhi Kompyuta kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga ili kuwajengea uwezo wa TEHAMA wanafunzi hao. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba amekabidhi vifaa vya TEHAMA zikiwemo Kompyuta 5 , Printa 1 pamoja na spika zake vyenye thamani ya milioni 15 kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga zisaidie kuwajengea uwezo wa TEHAMA wanafunzi hao.

Akikabidhi vifaa hivyo Jana Jumamosi Agosti 14,2021 Mhe. Kirumba amesema kuwa kompyuta hizo zitaenda kuwajengea uwezo wa TEHAMA wanafunzi na kuongeza ufaulu wa shule hizo.

Alisema Kompyuta hizo ni sehemu ya Computer 30 alizoomba kwa kushirikiana na Wabunge wenzake wa Mkoa wa Shinyanga na kutolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Mhe. Kirumba aliishukuru na kuipongeza Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara hiyo na taasisi yake ya UCSAF kwa kuthamini na kuisimamia vema ilani ya uchaguzi ambayo imezungumzia kuongeza matumizi ya TEHAMA na wao wanatekeleza kwa vitendo huku akizitaka shule zilizonufaika na vifaa hivyo kuvitunza na kuvitumia kuleta matokeo tarajiwa kwa walimu na wanafunzi wa shule hizo.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude alisema vifaa hivyo vya TEHAMA vitasaidia kuchochea ukuaji wa matumizi ya TEHAMA na kuwaandaa vijana na mabadiliko ya teknolojia duniani.

Mapema Jana Agosti 14,2021 Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Mhandisi Kundo Mathew alikabidhi vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya shule 6 za Sekondari zilizopo ndani ya Mkoa wa Shinyanga ikiwemo shule hiyo ya Kishapu Girls vyenye thamani ya shilingi Milioni 50 vilivyotolewa na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).

Makabidhiano hayo yalifanyika Mkoani Shinyanga kati ya Naibu Waziri huyo na Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Janista Mboneko, na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Shinyanga Nice Munisi ambapo jumla ya kompyuta 30 na printa 4 zilikabidhiwa rasmi.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo Mhandisi Kundo alisema kuwa Serikali kupitia UCSAF imeendelea kutekeleza mradi wa kupeleka vifaa vya TEHAMA katika shule za umma ili kuchochea ukuaji wa matumizi ya TEHAMA na kuwaandaa vijana na mabadiliko ya teknolojia duniani.

Pia alizungumzia mradi wa wasichana na TEHAMA unaotekelezwa na UCSAF ambao unalenga kuwawezesha na kuwajengea uwezo watoto wa kike katika TEHAMA ndio maana katika upelekaji wa vifaa vya TEHAMA katika shule za sekondari Mfuko huo unaangazia na Shule za Sekondari za wasichana.

“Wizara kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote tuna kipengele kingine cha kuwawezesha watoto wa kike na TEHAMA ili kuwajengea uwezo na hatimaye kutengeneza wataalam wa TEHAMA wengi zaidi nchini kwa sababu mpaka sasa wataalam wa TEHAMA wanawake ni wachache kuliko wa kiume lengo letu ni kwamba tunapoongelea 50 kwa 50 ionekane kwa vitendo", alisema Mhandisi Kundo.

Kwa Upande wa Mkuu wa Uendeshaji wa UCSAF Mhandisi Albert Richard alisema kuwa vifaa hivyo vya TEHAMA vilivyokabidhiwa katika Mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa jumla ya kompyuta 800 na printa 20 zinazoendelea kusambazwa katika ya shule za sekondari za umma ambazo zilianishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/22.
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (wa pili kushoto) akikabidhi Kompyuta kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga ili kuwajengea uwezo wa TEHAMA wanafunzi hao. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (wa pili kushoto) akikabidhi Kompyuta kwa ajili ya sshule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga.
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (wa pili kushoto) akikabidhi Printer kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga
Mbunge wa viti maalum wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Santiel Kirumba (wa pili kushoto) akikabidhi Printer kwa ajili ya shule ya Sekondari ya Wasichana Kishapu 'Kishapu Girls' mkoani Shinyanga
Zoezi la makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA likiendelea katika shule ya sekondari ya Wasichana Kishapu.
Zoezi la makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA likiendelea katika shule ya sekondari ya Wasichana Kishapu.
Zoezi la makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA likiendelea katika shule ya sekondari ya Wasichana Kishapu.
Wanafunzi wakifuatilia Zoezi la makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA katika shule ya sekondari ya Wasichana Kishapu.

Bia ya Serengeti Lite yazindua kampeni mpya ya ‘Take a Bite out of Life’

$
0
0
Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Serengeti Lite, imezindua kampeni mpya na ya aina yake inayojulikana kama “Take a Bite out of Life’, inayowahamaisha vijana na wateja wake kujiongeza, kufanya zaidi huku ikitoa fursa ya wenye vipaji kuonyesha uwezo wao na kuwaandaa kuwa wanachotaka.

Kampeni hiyo inalenga kuwafanya wateja wa Serengeti Lite kufurahia ladha ya kipekee ya bia hiyo ya Kitanzania, iliyotengenezwa Tanzania kwa ajili ya Watanzania huku wakionyesha vipaji na uwezo wao.

Kwa mujibu wa meneja mwandamizi wa chapa wa Serengeti Wankyo Marando, kampeni hiyo ni maalum kwa watu na vijana wenye uthubutu, wanaojiongeza na ambao pia wanaofanya zaidi na zaidi ili kufikia malengo waliyojiwekea bila woga wala kuangalia nyuma.

Kampeni hiyo itakayodumu kwa miezi mitatu, itahusisha mashindano ya kuwapata JD wakali na jumla ya washiriki 5,200 kutoka shehemu mbali mbali nchini watapewa jukwaa la kuonyesha vipaji vyao. Washindi watatu watapata zawadi ya DJs kits zenye thamani ya hadi shilingi milioni saba kila moja huku wakipewa nafasi za kufanya kazi kama ma DJ wa Serengeti Lite katika sehemu wanazoishi.

Washiriki ambao hawataweza kufika fainali, watapata zawadi mbali mbali kama baketi za bia, tisheti, kofia Pamoja na kupata jukwaa la kuonyesha vipaji vyao chini ya chapa ya bia inayoheshimika na kupendwa, Serengeti Lite

Kwa mujibu wa Wankyo, shindano ka kuwapata ma DJs wakali wanaochipukia lipo wazi kwa mtu yeyote mwenye umri wa miaka zaidi ya 18 na ambaye anaamini kuwa ana kipaji

“Mtu yeyote mwenye umri zaidi ya miaka 18 anaweza kushiriki kwenye shindano hili katika sehemu alipo kwa kuwa linafanyika nchi nzima. Matanganzo ya wapi linafanyika yatakuwa yakitolewa katika kila wilaya na mkoa kupitia magari ya matangazo, redio Pamoja na kurasa za mitandao ya kijamii za Serengeti Lite.

Ili kushiriki, washiriki watatakiwa kujiandikisha katika baa zitakazotangazwa na ambazo mashindano hayo yatafanyika na pia watatakiwa kuwa na orodha ya nyimbo watakazozicheza. Kutakuwa na mashindano kila wiki na mashindanao yatafanyika katika ngazi ya wilaya, mkoa na kitaifa ambapo washindi watatu watapatikana.

Wankyo alisema washindi watapatikana kwa kupigiwa kura ambapo majaji watakuwa na asilimia 60 ya kura zote na asilimia 40 itakuwa ni ya mashabiki. Mashabiki wanaweza kushiriki kwa kupihga kura moja kwa moja wakiwa eneo la tukio au kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za bia ya Serengeti Lite

Meneja huyo wa chapa aliwataka vijana kuchangamkia fursa hiyo itakayowapa nafasi ya kupiga hatua katika kile wanachokipenda,

Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa  Matiko Mniko (kati kati) akikuzindua rasmi kampeni ya ‘Take a Bite out of Life’  inayoendeshwa na Bia ya Serengeti Lite na ambayo inalenga kuvumbua vipaji vya Ma DJ chipukizi. Kulia na Meneja Mwandamizi wa Chapa kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti (Senior Brand Manager, mainstream beer) Wakyo Marando na kushoto ni mmoja wa majaji wa shindano hilo, DJ Zero. 

Mkuu wa kitengo cha Bia wa Kampuni ya Serengei Nandi Mwiyombella (kushoto) akifurahia bia ya Serengeti Lite kwa kugonganisha chupa na Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania Matiko Mniko (kati kati ), Meneja mwandamizi wa chapa wa kampuni hiyo Wankyo Marando  na  mmoja kati ya DJ atakayekuwa jaji katika shindano la kutafuta vipaji vya Ma DJ John Dilinga wakati wa uzinduzi wa  Kampeni ya 'Take Bite Out of Life' inayoendeshwa na bia ya Serengeti Lite. 

Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Bia ya Serengeti wakifurahi kujumuika pamoja muda mfupi bada ya uzinduzi wa  kampeni ya 'Take a Bite Out of Life' iliyofanyika jijini Dar es Salaam. Kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha vijana kuwa na uthubutu, kufanya zaidi na huku ikiwapa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kupitia mashindano ya kutafuta Ma DJ


NMB yatoa misaada ya Mil. 20/- kwa Shule Kimara, Sinza Magomeni

$
0
0
BenkiI ya NMB, kupitia Program ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), imetoa msaada wa viti na meza 150 kwa Shule Sekondari Saranga ya Kimara na Mashujaa ya Sinza, pamoja na mabati 175 kwa Shule ya Msingi Mianzini, iliyopo Magomeni Makurumla – zote wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 20.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika Shule ya Sekondari Saranga, ambako Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo, alimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hheri James, mbele ya Mbunge wa Ubungo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Kitila Mkumbo.

Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Bishubo alisema msaada huo ni sehemu ya utaratibu wao wa kila mwaka, ambako hutumia asilimia moja ya faida yao kwa mwaka uliotangulia, kurejesha kwa jamii kwa kusaidia utatuzi wa changamoto zinazoikabili Sekta za Elimu na Afya, pamoja na majanga.

Bishubo alibainisha kuwa, NMB inatambua, kuthamini na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha mazingira ya vijana na watoto wa Kitanzania kupata elimu bora, hivyo wao kama wadau, wanao wajibu wa kusapoti jitihada hizo kwa kusaidia kila penye uhitaji.

“Tangu Januari mwaka huu hadi sasa NMB imetumia Sh. Bilioni 1.3 kutoa misaada, ambapo kwa Mkoa wa Dar es Salaam Peke yakep benki imetoa misaada yenye thamani ya Sh. Milioni 207.9, kati ya hizo Sh. Mil. 144.5 katika elimu na Sh. Mil. 93 Sekta ya Afya,” alisema Bishubo.

Kwa upande wake, DC James, aliishukuru NMB, aliyoitaja kama sehemu ya familia ya maendeleo wilayani mwake kutokana na ushiriki wao wa mara kwa mara wa utatuzi wa changamoto katika elimu na afya, huku akiwataka walimu na wanafunzi kutunza misaada hiyo, ili idumu kwa muda mrefu.

“NMB wamekuwa wanafamilia wa maendeleo Ubungo, tangu siku naapishwa walikuwa na sisi, naanza kazi NMB ilikuwa pamoja na sisi, tuliposimama kuhangaika na changamoto za sekta ya elimu na afya, NMB iko pamoja nasi. Wao wako na sisi katika raha na shida.

Naye Waziri Mkumbo, aliishukuru NMB kwa namna inavyosaidia jamii inayoizuguka na kwa kuhakikisha wanaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili jamii.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo (kushoto), akikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James (katikati) na Mbunge wa Ubungo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo (wa pili kulia), sehemu ya msaada wa viti na meza 150 kwa Shule za Sekondari Saranga ya Kimara na Mashujaa ya Sinza, pamoja na mabati 175 kwa Shule ya Msingi Mianzini, iliyopo Magomeni Makurumla wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 20.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo (kushoto), akikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Khery James (katikati) na Mbunge wa Ubungo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo, sehemu ya msaada wa viti na meza 150 kwa Shule za Sekondari Saranga ya Kimara na Mashujaa ya Sinza, pamoja na mabati 175 kwa Shule ya Msingi Mianzini, iliyopo Magomeni Makurumla za wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 20.


Mkuu wa Kitengo cha Biashara za Serikali wa NMB, Vicky Bishubo (wa pili kushoto) na Kaimu Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Seka Urio, wakikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James, sehemu ya msaada wa viti na meza 150 kwa shule za Sekondari Saranga ya Kimara, Mashujaa ya Sinza, pamoja na mabati 175 kwa Shule ya Msingi Mianzini, iliyopo Magomeni Makurumla za wilayani Ubungo, jijini Dar es Salaam, vyote vikiwa na thamani ya Sh. Milioni 20. Katikati wanafunzi wa Shule ya Sekondari Saranga, Patrick Ndikwege na Vivian Valentino wakifurahia, hafla hiyo ilifanyika katika Shule ya Sekondari Saranga. Kulia ni Mbunge wa Ubungo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo, (Na Mpiga Picha Wetu).

……………………………………………………………………………
Viewing all 49567 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>