MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti amesema wanalo jukumu la kuhakikisha huduma wanazitoa kwa ajili ya Watanzania zinakuwa salama wakati wote ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano za kuhamasisha kutumia njia za kieletroniki kwenye malipo ya fedha.
Corsaletti alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa huduma mpya inayojulikana kwa jina la Airtel Money Tap Tap ambayo inamuwezesha mteja wao anapotaka kununua mafuta kwa kutumia kadi ya Airtel badala ya kutoa fedha taslimu akiwa kituo cha mafuta.
Alisema wanahisi kwamba wanawajibu wa kufanya huduma zao kwa usalama, senye ufanisi na rahisi zaidi kwa wateja wao na kufafanua ni hatari kubeba fedha wakati wote maana ni rahisi kuhatarisha maisha.
Aliongeza hivyo ili kufanya jamii ya Watanzania inakuwa salama wakati wote imeona kuna haja ya kuwa na huduma hiyo ambayo itamuwezesha anayehitaji kununua mafuta kwenye vituo vya Puma vilivyopo maeneo mbalimbali ya Dar es salaam wanatumia kadi za Airtel kununua mafuta.
“Milango yetu iko wazi kwa ajili ya kuendelea kuboresha huduma zetu na kuna jambo lolote ambalo tunaweza kulifanya ili jamii yetu kuwa salama wakati wote.Hivyo kuna umuhimu wa kuwa na matumizi ya kadi ya Airtel katika kununua mafuta kwenye vituo vyetu vya Puma,”alisema.
Akifafanua zaidi kuhusu huduma ya Airtel Money Tap Tap, Corsaletti alisema chini ya utaratibu huo mtu yeyote aliyejisajili na huduma ya Airtel Money atakuwa na uwezo wa kulipia bidhaa za Puma katika vituo vyake vyote nchini kwa kutumia kadi ya huduma ya Airtel Tap Tap badala ya kutumia fedha kwa ajili ya huduma kama hizo.
“Kadi hii imeundwa kwa namna ambayo wakati wa kutumika kufanya malipo , hupunguza fedha kwa kiasi cha malipo kutoka katika akaunti ya Airtel Money ya mnunuzi kwenda kwenye akaunti ya muuzaji. “Kadi hii itakuwa inauzwa kwa bei ya Sh 2, 000 kwenye vituo vyote vya Puma Dar es Salaam na maduka yote ya Airtel Tanzania .Kuanzia mwakani kadi hii itakuwa pia inapatikana katika vituo vyote vya mikoani ambavyo vipo chini ya Puma,”alisema.
Alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa Puma Tanzania ina jumla ya vituo 46 nchini kote na kwa kuanza, vituo vyote vya Dar es Salaam vitakua vinatoa huduma hiyo, hali vituo vingine vilivyosalia vitaunganishwa hivi kuanzia mapema mwakani.“Lengo letu ni kuhakikisha kwamba aina yoyote ya biashara tunayofanya, inafanyika kwa namna ambayo mtumiaji wa mwisho anaridhika, na kubaki salama.
“Tunaamini hili kuwa jukumu letu kwa jamii popote wanapotumia huduma zetu. Kwa kutumia kadi hii ya Airtel Money Tap Tap, mtu hatahitaji kubeba tena hela tasilimu ili kupata huduma katika kituo cha Puma,”alisisitiza.
Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso wakionesha mikataba yao pamoja na kadi ya Airtel Money Tap Tap mara baada ya hafla hiyo fupi ya kutiliana saini ya makubaliano hayo,hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay,jijini Dar.
MENEJA Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso wakiasini mkataba wa makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Aiter Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay jijini Dar es salaam.
Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso wakibadilishana mikataba mara baada ya kutiliana saini makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Aiter Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay.
Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),wakati wa hafla fupi ya makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Aiter Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay jijini Dar es salaam. kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso
Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania Philippe Corsaletti kushoto akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso mara baada ya kumaliza kutiliana saini na kukabidhiana mikataba makubaliano ya uuzaji wa mafuta kwa kutumia kadi ya Airtel Money Tap Tap , Hafla hiyo ilifanyika katika kituo cha Mafuta cha Puma Oysterbay.
Meneja Rasilimali Watu wa Puma Tanzania Bi Loveness Hoyange pamoja na maofisa wengine wa kampuni hiyo na kampuni ya simu ya Airtel wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri katika hafla hiyo.