Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

Kongamano la wadau wa mafuta na gesi kuhusu sera ya uzawa lafanyika jijini Dar es salaam

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na mwakilishi mkazi wa Benki ya dunia Bi. Bella Bird, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa,Mkurugenzi wa Shirika la TradeMark East Afrika Bw.John Ulanga na kamishna Msaidizi wa umeme kutoka wizara ya nishati na madini Mhandisi John Luoga.
get3
Mwakilishi mkazi wa Benki ya dunia Bi. Bella Bird akizungumza na wadau wa mafuta na gesi kuhusu  sera ya uzawa katika mradi wa Liquidfied natural gas (LNG) uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam.
get4
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani akizungumza na wadau wa mafuta na gesi kuhusu sera sera ya uzawa katika mradi wa Liquidfied natural gas (LNG)uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam.
get5
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani akizungumza na wadau wa mafuta na gesi kuhusu sera sera ya uzawa katika mradi wa Liquidfied natural gas (LNG)uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam.
get1
Mwakilishi mkazi wa Benki ya dunia Bi. Bella Bird (kushoto) akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani(kulia) wakati walipokutana kuzungumzia masuala ya mafuta na gesi katika sera ya mzawa katika mradi wa Liquidfied natural gas (LNG)uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam.
Picha na Daudi Manongi,MAELEZO
get2
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa akizungumza na akizungumza na wadau wa mafuta na gesi kuhusu sera sera ya uzawa katika mradi wa Liquidfied natural gas (LNG) uliofanyika katika ukumbi wa mwalimu nyerere jijini Dar es Salaam.


CHADEMA YAFANYA UTEUZI WA NAFASI YA KATIBU WA WILAYA YA ARUSHA

$
0
0

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Arusha Mjini kupitia kikao chake cha Kamati ya Utendji kilichofanyika tarehe 24/09/2016 kimefanya uteuzi wa nafasi ya Katibu wa Wilaya kwa kumteua ndugu STEVEN URASSA kuwa Katibu wa Wilaya na kuchukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na aliyekuwa Katibu wa Wilaya Ndugu Lewis Emmanuel Kopwe kwa kukoma uongozi kwa kujiuzulu kwa hiari yake ( Ibara ya 6.3.4 (a) ) Uteuzi huu utaanza tarehe 26/09/2016 mara baada ya makabidhiano ya Ofisi kufanyika.

Kabla ya Uteuzi huu ndugu STEVEN URASSA alikuwa Mwenyekiti wa Kata ya Ngarenaro na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa TCA katika Kata ya Ngarenaro.

Uteuzi huu ni kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA Toleo la 2006 ( Kama ilivyoboreshwa 2014 ) Ibara ya 6.3.5 Kuziba nafasi wazi za Uongozi (a) (b) (c) Uteuzi huu pia umezingatia KANUNI ZA UENDESHAJI KAZI ZA CHAMA SURA YA KUMI ; 10.0 MAADILI YA VIONGOZI, SIFA MAHUSUSI ZA VIONGOZI NA MAADILI YA WANACHAMA.
Tunaomba apewe ushirikiano wote katika kutekeleza majukumu yake.

Imetolewa na;
Kitengo cha Habari na Mawasiliano

CHADEMA WILAYA YA ARUSHA MJINI

SMMRP YAENDELEA KUBORESHA MAJENGO OFISI ZA MADINI

$
0
0

Mwakilishi wa kampuni ya ukandarasi ya Malcom Investment Co Ltd (mwenye tshirt ya bluu) waliojenga jengo hilo, akikabidhi ufunguo kwa Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali watu wa Wizara ya Nishati na Madini Bibi Joyceline Lugora (katikati) wakati wa kukabidhi jengo hilo kwa kanda ya madini kusini mkoani Mtwara hivi karibuni.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (aliyeshika ufunguo) baada ya kupokea kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali watu wa Wizara ya Nishati na Madini, Joyceline Lugora (katikati) tayari kuanza kulitumia jengo hilo kabla ya kuzinduliwa rasmi hivi karibuni.
Msanifu Majengo wa SMMRP, Joseph Ringo,( mwenye shati nyeusi) akijaribu moja ya kifaa kinachotoa sauti kuashiria hatari pindi hitilafu au dharura ya moto itakapotokea katika jengo
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka,(kulia) akifungua mlango kukagua baadhi ya vyumba katika jengo hilo wakati wa makabidhiano hayo.
Taswira ya mbele ya mwonekano ya jengo la ofisi ya madini kanda ya kusini mkoani Mtwara.
Taswira ya muonekano wa upande wa kulia wa jengo hilo la Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini mkoani Mtwara.
Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka,(kulia) na Mkurugenzi Msaidizi Rasilimali watu wa Wizara ya Nishati na Madini Joyceline Lugora wakitia sahihi nyaraka za kukabidhiwa jengo la Ofisi ya Madini Kanda ya Kusini mkoani Mtwara wakishuhudiwa na Msanifu Majengo wa SMMRP, Joseph Ringo (katikati)
 
Zuena Msuya, Mtwara

Mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) ulio chini ya Wizara ya Nishati na Madini, umekabidhi Jengo la kisasa kwa Kanda ya Madini Kusini ambalo linatarajiwa kurahasisha utendaji kazi kwa kutumia mfumo wa teknolojia ya kisasa.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi jengo hilo mkoani Mtwara hivi karibuni, Msanifu Majengo wa SMMRP, Joseph Ringo alisema kuwa, ujenzi wa jengo hilo umefadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia mradi huo kwa lengo la kuboresha Sekta ya Madini nchini.

Ringo alisema kuwa, jengo hilo ambalo litatumika kama kituo cha Kisasa cha Madini (Center for Excellence) limeunganishwa katika mfumo wa kisasa wa TEHAMA kwa kuhifadhi taarifa pamoja na kumbukumbu mbalimbali za kidijitali za madini za Wizara pamoja na taasisi zilizo chini yake na endapo itatokea tatizo katika mfumo huo itakuwa ni rahisi kupatikana.

Alifafanua kuwa, jengo hilo limeunganishwa na mfumo wa kisasa wa TEHAMA, Ofisi za watendaji wa wizara, maktaba ya kisasa ya kuhifadhia taarifa za madini yanayopatikana katika ukanda wa kusini pamoja na uwepo wa vyumba maalumu vyenye vifaa kwa ajili ya kutolea mafunzo kwa wachimbaji wa madini.

Aidha, Ringo alifafanua kuwa, mradi wa SMMRP umelenga katika kuboresha miundombinu hasa ya majengo kwa kuweka mifumo ya kisasa pamoja na kuimarisha shughuli za rasilimali madini katika Ofisi za Kanda na Mikoa nchini.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini, Mhandisi Benjamin Mchwampaka alisema kuwa hivi sasa jengo hilo litawasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi kwakuwa lina uwezo wa kukidhi miundombinu yote ya wafanyakazi. Vilevile, amewataka wafanyakazi watakaokuwa wakitumia jengo hilo kuitunza na kulinda miundombinu ya jengo hilo.

Jengo hilo limebuniwa na Kampuni ya OGM Architects Consultants na kujengwa na kampuni ya ukandarasi ya Malcom Investment Co Ltd.

TAOMAC wamkabidhi Waziri Mkuu Majaliwa Jumla ya Shilingi 404.8 Milioni kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la Kagera

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wane kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha Waagizaji Wakubwa wa Mafuta (TAOMAC) baada ya kupokea hundi ya fedha kiasi cha sh. Milioni mia nne na nne na laki nane (404,800,000) pamoja na mifuko ya simenti 1000 kutoka chama hicho kwa ikiwa ni mchango wa wanachama wa chama hicho kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoani Kagera. Wengine ni pamoja na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ,Charles Mwijage (wa kwanza kulia)

========  ======= ========

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea fedha kiasi cha sh. Milioni mia nne na nne na laki nane (404,800,000) pamoja na mifuko 1000 ya simenti kutoka kwa Chama cha Waagizaji Wakubwa wa Mafuta TAOMAC ikiwa ni mchango wa wanachama wa chama hicho kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni mkoani Kagera.

Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Waziri Mkuu Majaliwa pamoja na kuwashukuru watu binafsi, taasisi na mashirika yaliyojitoa kwa hali na mali katika kuwasaidia waathirika wa janga hilo, pia aliwahakikishia kuwa misaada wanayoitoa itawafikia walengwa huku akibainisha kuwa serikali imejipanga kuzuia kila aina ya wizi au ubadhilifu wa misaada hiyo.

“Tayari tumechukua hatua kwa wahusika wote waliojaribu kucheza na misaaada hii. Niwahakikishie tu kwamba serikali ipo makini kwenye misaada na michango inayoendelea kutolewa kwa kuwa ni jukumu lake kufanya hivyo kwa kuwa mnapotoa misaada hii maana yake kuna sehemu mmejinyima,’’ alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TAOMAC Bw Salum Bisarara alisema mchango huo ni mwitikio wa ahadi walioyoitoa kwenye mkutano ulioitishwa na Waziri Mkuu Majaliwa na kufanyika Ikulu Septemba 13 nakuhusisha wadau mbalimbali nchini kwa kusudio la kuchangia waathirika wa tetemeko hilo.

“Katika kikao kile Wanachama wa TAOMAC tuliahidi mambo mawili, kwanza wanachama wenzetu watatu ambao ni GBP, OILCOM na MOIL waliahidi kuchangia kwa kuchukua jukumu la kuzijenga upya shule mbili za sekondari zilizoathirika ambazo ni shule ya IHUNGO na ya NYAKATO. Gharama za ujenzi huo tutajulishwa baada ya kukamilika tathmini,’’

“Pili wanachama waliosalia tuliahidi kukutana na kuchangisha fedha ili zisaidie waathirika wa tetemeko kwa njia mbalimbali ikiwemo kutengeneza upya miundo mbinu iliyoharibika hasa zahanati, hospitali, barabara na madaraja, ahadi ambayo tunaikamilisha leo,’’ alisema.

Katika mchango huo jumla ya Sh. Milioni mia mbili na arobaini na nne (244,000,000) tayari zilikuwa zimeingizwa kwenye akaunti maalumu ya kuchangia waathirika hao huku kiasi cha sh milioni mia moja na sitini ((160,000,000) kikiwa ni hundi halisi za kampuni wananchama ambazo zilikabidhiwa kwa mhasibu ofisi ya Waziri Mkuu.

Aliyataja makampuni yalichongia kuwa ni pamoja na Mogas Tanzania Ltd, National Oil (T) LTD, Barrel Petrol Energy, ATN Petroleum Company LTD, Petroafrica (T) Ltd, TSN Oil, Delta Petroleum, Engen Petroleum, Agusta Energy, Petrofuel, Genera Petroleum, Sahara, TIPER, Hass Petroleum, Lake Oil, Dalbit Petroleum, Camel Oil, Gapco, Oryx Oil Company na Puma Energy.

Aidha, wanachama wa chama hicho walimuahidi Waziri Mkuu kuwa wataendelea kuunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa taifa letu huku wakiishukuru serikali kwa kuwashirikisha katika kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo.

BENKI KUU YA TANZANIA YASEMA PATO LA TAIFA LIMEONGEZEKA KWA ASILIMIA 7.9

$
0
0

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandshi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya ukuaji wa pato la taifa kwa robo na nusu ya mwaka 2016. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mabenki, Kenedy Nyoni.
Kaimu Meneja Kitengo cha Mahusiano kwa Umma wa BoT, Victoria Msima, akimkaribisha Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu (wa pili kushoto), kuzungumza na wanahabari kuhusu ukuaji wa pato la taifa kwa robo na nusu mwaka 2015 Dar es Salaam leo.
Taswira ya meza kuu katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja Kitengo cha Mahusiano kwa Umma, Victoria Msima,Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mabenki, Kenedy Nyoni, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Beno Ndulu na Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti wa Sera za Kiuchumi, David Kwimbere.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.


Na Dotto Mwaibale

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema ukuaji wa pato la Taifa umeongezeka kwa asilimia 7.9 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 5.8 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015.

Hayo yamebainishwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizungumza na wanahabari kuhusu ukuaji wa pato la Taifa kwa robo na nusu mwaka 2016.

Profesa Ndulu alisema shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kasi ya juu zaidi katika kipindi hicho ni usafirishaji na uhifadhi wa mizigo ikiwa ni asilimia 30.6, uchimbaji wa madini kwa asilimia 20.5, mawasiliano na habari asilimia 12.6 na sekta ya fedha na bima kwa asilimia 12.5.

Alisema ukuaji wa sekta ya uchukuzi na uhifadhi wa mizigo umetokana na kuongezekea kwa usafirishaji wa abiria kwa njia ya barabara na gesi asilia ambao umekua kwa zaidi ya nusu ukilinganisha na robo ya pili ya mwaka 2015 kwa asilimia 9.4.

"Kwa upande mwingine, ukuaji wa sekta ya uchimbaji wa madini na gesi umechangiwa zaidi na kuongezeka kwa uzalishaji wa gesi ambao umekua kutoka mmSFt3.7,793 kwa mwaka 2015 mpaka mmSFt3 11,267 kwa mwaka 2016" alisema Ndulu

Profesa Ndulu alitaja sekta nyingine ambayo imefanya vizuri ililinganishwa na kipindi kama hicho kwa mwaka 2015 kuwa ni sekta ya kilimo ambayo imekua kwa asilimia 3.2 kwa robo ya pili ya mwaka 2016 wakati mwaka jana ilishuka kwa asilimia 1.9.

Aidha sekta ya fedha na bima imekua kwa asilimia 12.5 kwa robo ya pili ya mwaka 2016 ikilinganishwa na asilimia 10.0 kwa robo ya pili ya mwaka 2015.

Akizungumzia ukuaji wa pato la Taifa alisema katika nusu ya mwaka 2016 yaani Januari hadi Juni 2o16 kasi ya ukuaji wa pato la taifa imeongezeka na kufikia asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2015.

UPDATES MUHIMU KUHUSU MKUTANO WA KIDEMOKRASIA WA ACT WAZALENDO

$
0
0
1. Mkutano wa Kidemokrasia utafanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

2. Chama kimetuma mialiko kwa vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa.
3. Chama kimetuma mialiko kwenye Asasi Mbalimbali za Kiraia
4. Tumepata pia wageni wawili wa Kimataifa waliothibitisha kuhudhuria, Vital Kamerhe, Spika wa Zamani wa Bunge la Kongo na Kiongozi wa Chama cha UNC (Chama Kikubwa Zaidi cha upinzani nchini Kongo) & Ababu Namwamba, Kiongozi wa Chama cha Labour cha Kenya. Wote (Wakishirikiana na Deus Kibamba, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba) watawasilisha mada juu ya Mapambano ya Kudai Katiba ya Wananchi kwa kutupa uzoefu kutoka kwenye nchi zao.

5. Mkutano huu pia utakuwa jukwaa maridhawa la kufanya mjadala mpana kuhusu nchi na chama. KC, Mwenyekiti na Prof. Kitila watawasilisha mada mbalimbali juu ya nchi na chama. Meya wa Kigoma atatueleza nini tunachofanya kubadilisha maisha ya watu kwenye Manispaa yetu ya Kigoma-Ujiji.
Wenu,
Ndugu Ado Shaibu, Mwenezi, 0653619906

WAZIRI NAPE AKUTANA NA BALOZI WA SPAIN NCHINI.

$
0
0
 Waziri wa Habari, Utamaduni,  Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda kuhusu kusaidia kuendeleza sekta ya Utamaduni na Michezo leo Septemba 30,2016 wakati Balozi huyo alipofika ofisini kwa Waziri  Jijini Dar es Salaam kukabidhi moja ya mradi wa Utamaduni uliokuwa ukifanywa na serikali ya Spain katika Bonde la Ufa la Olduvai Gorge Mkoani Manyara.
Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda (kushoto) akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye kuhusu kuendeleza mradi wa kujenga Shule ya Mpira wa Miguu Kigamboni kama ilivyokuwa katika mkakati wa awali alipofika Ofisini kwa waziri Jijini Dar es Salaam  Septemba 30, 2016 kumkaribisha kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya Utamaduni yaliyoandaliwa na nchi ya Spain yatakayofanyika Makumbusho ya Taifa.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akisoma mradi wa Utamaduni uliokuwa ukifanyika Olduvai Goerge mkoani Manyara baada ya kukabidhiwa na Balozi wa Spain nchini Bw. Felix Costales Artieda (kushoto) Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016.

WAZIRI MKUU APOKEA MICHANGO YA SH. MILIONI 190.

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akipokea hundi ya shilingi milioni 80 kutoka kwa Balozi wa Pakistan nchini, Amir Khan  (wapili kushoto ukiwa ni mchango  kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani  Kagera. 
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye hoteli ya Kyatt Regency jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na  kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea hundi ya Shilingi milioni 50 kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Tasisi ya Aga khan nchini, Amin Kurji (kulia) ukiwa ni mchango kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Makabidhiano hayo yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Septemba 30, 2016. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Augustine Mahiga na wapili kulia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea jumla ya sh. milioni 190 kutoka kwa balozi wa Pakistan nchini Mhe. Amir Khan, Kaimu Balozi wa China Mhe. Gou Haodong na Taasisi ya Aga Khan.

Fedha hizo zimetolewa ili kusaidiia  wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa.

Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika leo (Ijumaa, Septemba 30, 2016) kwenye Hotel ya Hyatt Regency jijini Dar Es Salaam ambapo Waziri Mkuu aliwashukuru kwa michango hiyo na alitumia fursa hiyo kuwaomba wale walioahidi kutoa michango wakamilishe ahadi zao.

“Ninawaomba wale walioahidi kutoa michango wakamilishe ahadi kwa kuzileta ofisini kwangu au kutuma kupitia akaunti ya maafa iliyofunguliwa katika Benki ya CRDB yenye Namba. 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz,” amesema.

Amesema watu walio mbali na benki watumie namba za simu zilizotolewa mahsusi kwa ajili ya kupokea michango ya maafa hayo ambazo ni 0768-196-669 (M-Pesa), au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616 (Tigo Pesa).

Akikabidhi hundi kwa Waziri Mkuu, Balozi wa Pakistan, Mhe. Amir alisema wanaamini mchango huo wa sh. milioni 80 walioutoa utasaidia kuwapunguzia uchungu wananchi wa Kagera kutokana na athari zilizosababishwa na tetemeko la ardhi.

Kwa upande wake Kaimu Balozi wa China Mhe. Haodong alimweleza Waziri Mkuu kwamba wameshtushwa na tukio hilo na tayari walishawapeleka madaktari na wataalamu wengine mkoani Kagera na leo walikuwa wanakamilisha ahadi yao ya kutoa mchango wa sh. milioni 60.
Naye Muwakilishi Mkazi wa Taasisi za Aga Khan nchini, Amin Kurji  alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 50.                               

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM
IJUMAA, SEPTEMBA  30, 2016.

BASATA YAMPONGEZA MUSTAFA HASANNALI KWA KUSHINDA TUZO YA UBUNIFU WA MAVAZI

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lenye dhamana ya kufufua, kukuza na kuendeleza Sanaa nchini linapenda kuchukua nafasi hii kumpongeza msanii na mbunifu wa Mavazi Mustafa Hassanali kwa kushiriki kinyanga’anyiro cha Tuzo ya Mavazi ya Afrika Mashariki Kenya 2016 (Kenya Fashion Awards 2016) yaliyofanyika tarehe 03/09/2016 na kupata tuzo ya Mbunifu Bora wa Mwaka wa Afrika Mashariki.

Baraza linathamini mchango mkubwa wa Mbunifu huyu wa mavazi katika kuendeleza tasnia ya ubunifu, kwa kuanzisha Jukwaa la mavazi Afrika Mashariki na Kati, Swahili Fashion week na maonyesho mengine ya mavazi.

Aidha tuzo hii itakuwa chachu kwa ustawi wa tasnia ya ubunifu wa mavazi kwa kuwa imedhihirisha ubora wa kazi za sanaa za Kitanzania katika soko la Kimataifa. Baraza litaendelea kushirikiana na wabunifu wenye maono na bidii katika kukuza na kuendeleza sanaa nchini ili kuhakikisha sekta ya sanaa inasonga mbele kwani ni ukweli usiopingika kuwa tasnia ya sanaa ina mchango mkubwa katika kutoa ajira kwa watanzania wengi hususan vijana.

Baraza linatambua mchango wa Bwana Mustafa Hassanali katika kukuza maendeleo ya ubunifu na amekuwa akitoa fursa kwa wabunifu wengine wa Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Baraza linathamini na linatoa pongezi kwa Bwana Mustafa Hassanali kwa kazi nzuri anayoifanya.

SANAA NI KAZI TUIKUZE, TUILINDE NA KUITHAMINI

Godfrey L. Mngereza
KATIBU MTENDAJI, BASATA


 
 
 

MAKAMU WA RAIS KUONGOZA UPANDAJI MITI KESHO JIJINI DAR

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya jamii

MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa upandaji miti Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema upandaji wa miti unaanza kesho hivyo kila mwananchi wa Dar es Salaam anatakiwa kupanda mti mmoja ikiwa ni kwa ajili ya ustawi wa afya.

Amesema kuwa upandaji miti utafanywa katika Wilaya yaTemeke kwa kupanda miti katika barabara ya Kilwa na baada kupanda miti atakagua miundombinu ya maji kwa ajili ya kumwagilia miti katika Wilaya Ilala pamoja na Kinondoni.

Makonda amesema miti hiyo itakayopandwa ni faida ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa ajili hewa na pamoja na vivuli vya kupumzika.Aidha amesema kila mwananchi lazima afanye jitihada za kupanda miti ikiwa ni pamoja watendaji wote wa mitaa na kata kuhamasisha wananchi kupanda miti.

Hata hivyo amewataka mashabiki wa yanga na simba kupanda miti kabla ya kuanza mpira kati timu hizo.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza leo na waandishi habari juu ya upandaji miti utaozinduliwa kesho,jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii)

TRA YAKUSANYA ASILIMIA 92 YA MAPATO MWEZI AGOSTI.

$
0
0


Na Ally Daud-MAELEZO

MAMLAKA ya mapato nchini (TRA) imefanikiwa kukusanya asilimia 92 sawa na shilingi milioni 84.618 kwa mwezi Agosti mwaka huu ikiwa ni katika kutimiza lengo la kukusanya bilioni 1 na kuendelea kila mwezi kwa Mkoa wa kodi Ilala.

Hayo yamesemwa na Afisa Elimu na Huduma wa TRA Mkoa wa kodi Ilala Bw. Zakeo Kowero katika semina iliyofanyika jijini Dar es salaam kati ya mamlaka hiyo na watendaji wa kata na Serikali za Mitaa wilaya ya Ilala kuhusu maswala ya ukusanyaji kodi bora na sahihi kwa maendeleo ya Wilaya na nchi kwa ujumla.

Bw. Kowero amesema kuwa kiasi hiko kimekusanywa kwa mwezi agosti kufuatia malengo waliojiwekea kama Wilaya na kuhakikisha wanapiga hatua zaidi ya hapo ili kuhakikisha mapato yanapatikana kwa wingi kwa maendeleo ya nchi.

“tumejiwekea maelengo ya kukusanya mapato kuanzia shilingi bilioni moja na kuendelea kwa mwezi lakini tumefanikiwa kukusanya milioni 84 ikiwa ni katika kutimiza malengo yetu na tunaimani ya kufanya vizuri kwa watendaji wetu wamejipanga kwa utendaji na uadilifu katika ukusanyaji mapato” alisema Bw. Kowero.

Mbali na hayo Bw. Kowero amesema kuwa semina hiyo ya kukutana na watendaji hao inalenga kutatua kwa wakati kero za na matatizo ya walipaji kodi ikiwa pamoja na kutumia mashine za EFD kwa usahihi katika ukusanyaji kodi wao.

Aidha Bw. Kowero ameongeza kuwa katika semina hiyo inawaelimisha watendaji hao kuweza kuimarisha uhusiano mzuri kati ya TRA na walipa kodi ili kuhakikisha wanafatilia kwa urahisi madeni ya wasiolipa kodi kwa wakati muafaka.

Afisa huyo wa Elimu na huduma TRA Mkoa wa kodi Ilala amewataka wanaokwepa na wasiolipa kodi wajisalimishe wenyewe ili kuweza kulipa madeni wanayodaiwa kabla mkono wa sheria haujaanza kuwatafuta.

KESHO NI SIKU YA KUPANDA MITI KITAIFA,PANDA MTI KWA AFYA YA MAZINGIRA NA NCHI YAKO

TFS YASAIDIA MADAWATI 12,000 MKOANI MWANZA

$
0
0

Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii , Eng. Ramo Makani( kushoto) akimkabidhi madawati Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela ( kulia) ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000, wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo( Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii).

Baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa jana na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000 .
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamekaa kwenye madawati mara baada ya makabidhiano yaliyofanyika Mkoani Mwanzan jana na Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongela ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe . ( Picha na Lusungu Helela- Wizara ya Maliasili na Utalii)


Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imekabidhi madawati 12,115 mkoani Mwanza ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa bungeni mwanzoni mwa mwaka huu na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ya kutengeneza madawati 20,000. Makabidhiano hayo baina ya TFS na Serikali yalifanyika kitaifa kwenye Uwanja wa chuo cha Mafunzo ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi.

Naibu wa Waziri wa Wizara hiyo , Ramo Makani alitoa mwezi mmoja kwa uongozi wa TFS kuhakikisha unakamilisha kutengenenza madawati 7,885 yaliyosalia kabla ya novemba mwezi huu .‘’ Pamoja na kufikia asilimia 61 ya lengo, nawaomba TFS muhakikishe idadi iliyobaki ya madawati inakamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao’’ Alisema Makani.

Akizungumza kabla ya kukabidhi madawati hayo, Mtendaji Mkuu wa TFS, Prof. Dos Santos Silayo bila kutaja gharama iliyotumika alisema ofisi yake imechelewa kufikia asilimia 100 ya kutengeneza madawati 20,000 kutokana na kuwa na changamoto ya ucheleweshwaji wa taratibu za uvunaji mbao katika baadhi ya misitu.

TFS tumetekeleza agizo hili kwa kulenga ngazi za chini kabisa za mfumo wa utendaji wa Wakala ambao ni wilaya. Hivyo katika kugawa idadi ya utengenezaji madawati wa kanda ilizingatia idadi ya wilaya kwa kila kanda’’ alisema Prof. Silayo. Waziri Makani alisema madawati hayo yatagawiwa katika mikoa ya Simiyu., Kagera, Mara,Geita na Mwanza ambayo itapokea madwati 2,580 yaliyokwisha tengenezwa.

Akizungumz kwa niaba ya Wakuu wa Mikoa ya Tanzania Bara, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela aliwapongeza TFS na kuahidi kuyatunza madwati hayo ili yatumike kwa muda mrefu kwa manufaa ya wanafunzi.

WIZARA YA AFYA YAUPONGEZA MKOA WA SINGIDA KWA KUTOA HUDUMA ZA KIBINGWA KATIKA NGAZI YA HALMASHAURI..

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe (katikati) akizungumza na wagonjwa, kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki na kushoto ni Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara ya afya Dokta Magreth Mhando.
 Wagonjwa waliofanyiwa operesheni ya macho na madaktari bingwa wakizungumza na Mkuu wa Mkoa (hayupo).
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe (katikati) akizungumza na mgonjwa (hayupo pichani), kushoto kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki.
 Wagonjwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa alipowatembelea na kuona huduma za mkoba za kibingwa zikiendelea kutolewa, wagonjwa hao walikuwa wakisubiri kuonana na daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe akitembelea na kukagua huduma wanazopatiwa wagonjwa wa huduma za kibingwa katika hospitali ya Mt calorus Mtinko, kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki na kushoto ni Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara ya afya Dokta Magreth Mhando.
.Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J Mtigumwe akisikiliza maoni ya wagonjwa waliokuwa wakisubiri kupata huduma za kibingwa kushoto kwake ni  Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki na  anayefuata wa kwanza ni Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara ya afya Dokta Magreth Mhando.

Grace Singida.

Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee imeishauri mikoa yote ya Tanzania bara kuiga mfano wa mkoa wa Singida wa kuanzisha huduma za kibingwa za mkoba kwa ngazi za wilaya ili kuwafikia watanzania wengi wenye uhitaji.

Mkurugenzi wa tiba kutoka wizara hiyo Dokta Magreth Mhando ametoa ushauri huo katika hospitali ya Mtakatifu Calorus Mtinko Singida Vijijini alipotembelea kujionea awamu ya pili ya zoezi la huduma za kibingwa za Mkoba. Dokta Mhando amesema kumekuwa na huduma za kibingwa za mkoba ila hazikufanyika vizuri kama ambavyo mkoa wa Singida umekuwa ukifanya na kutoa pongezi za Wizara kwa Mkuu wa mkoa na Mganga mkuu wa mkoa kwa ubunifu huo.

Amesema huduma za kibingwa za mkoba zimekuwa zikiratibiwa na taasisi au hospital kubwa kama Muhimbili ambapo madaktari bingwa wamekuwa wakitoa huduma kwa ugonjwa fulani na kwa ngazi ya hospitali za Mkoa tofauti na zoezi linaloendelea Mkoani Singida la kutoa huduma za kibingwa kwa magonjwa mbalimbali.

Dokta Mhando ameongeza kuwa kutokana na uhaba wa madaktari bingwa nchini wizara imetenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha madaktari na kuwashauri waajiri ambao ni makatibu tawala wa mikoa na wakurugenzi wa halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kuwasomesha madaktari hao kwakwuwa wizara pekee haitaweza.

Amesema utaratibu ni kuwa na madaktri bingwa angalau watano kila Mkoa lakini mikoa mingi haina idadi hiyo huku akiongeza kuwa lengo la kutembelea zoezi hilo Singida nikujionea hali halisi na sio kusubiria taarifa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew John Mtigumwe mara baada ya kutembelea wodi zote na kuzungumza na wagonjwa waliopata huduma za kibingwa amemtaka Mganga Mkuu wa Mkoa kuongeza muda wa kutoa huduma hiyo kutoka siku tano hadi nane kutokana na wingi wa wagonjwa waliojitokeza.

Mhandisi Mtigumwe amesema huduma hiyo inasaidia kutambua magonjwa na kuyatibu kabla hayajawa sugu lakini pia gharama zikiwa nafuu kutokana na kusogezwa kwa ngazi za halmashauri. Ameongeza kuwa lengo la ofisi yake ni kuhakikisha huduma za kibingwa za mkoba zinapelekwa kwa kila halmashauri na endapo zoezi likikamilika na kukiwa na uhitaji mkubwa kuna uwezekano mkubwa wa kurudia zoezi hilo.

Mhandisi Mtigumwe amesema kuelekea Tanzania ya viwanda afya bora ni muhimu na wazalishaji wakubwa ni wananchi wa ngazi za chini hivyo huduma hiyo itasaidia kuimarisha afya ili waweze kuzalisha bidhaa kwa wingi na zenye ubora.

Amesema kwa wale wagonjwa watakaopewa rufaa kwenda nje ya Mkoa utaratibu utaangalia wa kuwapatia usafiri wa Mkoa ili kuwapeleka hasa wale wasiojiweza. Naye Mganga Mkuu wa Mkoa Dokta John Mwombeki amesema kwa muda wa siku tano wagonjwa zaidi ya 800 wameonana na madaktari bingwa huku idadi ikitarajiwa kuongezeka kutokana nakuongezwa kwa siku za klutoa huduma.

Dokta Mwombeki amesema wagonjwa wengi wanaofika wanatoka maeneo mbalimbali hasa maeneo ya kijijini na wenye hali duni ya maisha hivyo zoezi hilo limesaidia wananchi hasa wwenye kipato cha chini. Amesema madaktari bingwa wanaotoa huduma za kibingwa za mkoba ni madaktari bingwa wa magonjwa ya akina mama, watoto, macho, meno, magonjwa ya ndani na daktari bingwa wa upasuaji.

Wagonjwa waliopata huduma wameushukuru uongozi wa mkoa kwa kubuni utaratibu wa kuwafuata wagonjwa karibu ili kuwapatia huduma za kibingwa kwakuwa inawasaidia kupata matibabu mapema kabla magonjwa hayajawa sugu na kushauri huduma iwe endelevu angalau kila mwaka.

KATUNI


KESHO NDIO KESHO,PATAKUWA HAPATOSHI UWANJA WA TAIFA

$
0
0


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

SHAMRA SHAMRA za mechi ya watani wa Jadi baina ya Yanga na Simba zinazidi kupamba moto kwa kila upande kujinadi kwa kila namna. Mechi hiyo inayotarajiwa kuchezwa kesho kwenye dimba la Uwanja wa Taifa saa 10, ukichezeshwa na Mshambuliaji wa beji ya FIFA, Martin Sanya akisaidiwa na Frank Chacha na Mpenzu huku mezani akiwa Hery Sasii. 

Mechi hiyo itakayoanza kutumia mfumo mpya wa kadi za kieletroniki umekuwa na hamasa kubwa sana kwa mashabiki na wengi kujitokeza kuchukua kadi hizo. Yanga wakiwa njiani kuingia Dar es salaam wakitokea Pemba walipoweka kambi ya wiki moja, Simba tayari wameingia jijini na asubuhi ya leo kufanya mazoezi mepesi kwenye uwanja wa Gymkhana. 

Timu hizi zimeweza kukutana mara 96 na tayari Mabao 196 yakiwa yamefungwa huku katika mechi tano tano za mwisho Yanga ameshinda mara mbili, Simba ikishinda mara moja na sare mbili. Yanga Ikiwa haijabadilisha benchi la ufundi pamoja na kikosi kwa muda mrefu wanakutana na Simba ambayo imebadilisha asilimia kubwa ya wachezani na benchi la ufundi. 

Lakini siku ya Jumapili, michezo itakuwa mitano ambako Mbeya City itaikaribisha Mwadui kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya; Majimaji itakuwa mwenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro. Mbao na JKT Ruvu Jmwatakuwa kwenye Uwanja wa Mabatini huko Mlandizi wakati Kagera itaikaribisha Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.

PPRA YAKABIDHI RIPOTI YA UKAKUZI KWENYE UNUNUZI WA UMMA MWAKA 2015/2016

$
0
0

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akikabidhiwa Ripoti ya ukaguzi kwenye Manunuzi ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Balozi DKT. Matern Lumbanga. Makabidhiano yaliyofanyika Wizarani jijini Dar es Salaam, Septemba 30, 2016

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Balozi DKT. Matern Lumbanga (kushoto kwa waziri wa Fedha na Mipango aliyekaa katikati), akifafanua jambo kabla ya kukabidhi Ripoti ya ukaguzi kwenye Manunuzi ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2015/2016.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Balozi DKT. Matern Lumbanga (kushoto), akifafanua jambo kabla ya kukabidhi Ripoti ya ukaguzi kwenye Manunuzi ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2015/2016. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA-Dkt. Laurent Shirima.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, akizungumza baada ya akukabidhiwa nakala za Ripoti ya ukaguzi kwenye Manunuzi ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2015/2016 na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Balozi DKT. Matern Lumbanga (Kulia). Makabidhiano yamefanyika Wizarani Jijini Dar es Salaam, Septemba 30, 2016.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Balozi DKT. Matern Lumbanga (kushoto), akitoa taarifa aya ripoti hiyo mbele ya waandishi wa Habari (Hawapo Pichani) kwenye makao Makuu ya Mamlaka hayo, Jijini Dar es salaam, Septemba 30, 2016. Kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dkt. Laurent Shirima na kushoto kwake ni Wajumbe wa Bodi hiyo Dkt. Leonard Chamriho ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) na Dkt. Edmund Mndolwa.
Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango baada ya kupokea Ripoti ya Ukaguzi wa Manunuzi ya Umma kwa mwaka wa fedha 2015/2016. Waziri Mpango aliwataka kufanya kazi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kukuza uchumi na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 kwa kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma.
(Picha zote na Wizara ya Fedha na Mipango).

UKAWA YASITISHA TENA MAANDAMANO YA UKUTA

$
0
0

Mwenyekiti  wa Chama cha CHADEMA Taifa,Mh.Freeman Mbowe


Na Anthony John,Globu ya Jamii


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  kimesitisha  shughuli  zote  za maandamano na mikutano nchi nzima,kwa kudai kuwa ukuta ni fikra endelevu na si mpango wa siku moja.


 Hayo yamesemwa leo na  Mwenyekiti  wa Chama hicho Taifa,Mh.Freeman Mbowe wakati  akizungumza  na Waandishi  wa Habari,Makao Makuu ya Chama hicho jijini Dar es Salaam.


Mbowe amesema kuwa wataendelea Kujipanga katika kulinda  Haki yao ya kidemokrasia kama ambavyo katiba ya vyama vya siasa inavyosema,kuwa ni haki yao ya kidemokrasia.

‘’Mapambano  ya  kisiasa si tukio la siku moja ni tukio endelevu na kwa hiyo tarehi Mossi ,Oktoba ambayo ilikuwa ni siku mbadala ya maandamano maalum,hivyo kwa niaba ya kamati kuu imeona kuna umuhimu  wa kusimamisha maandamano maalumu na mikutano nchi nzima ilikupisha mbinu nyingine mbalimbali’’amesema Mbowe

TANESCO YAFANYA KIKAO CHA UJIRANI MWEMA NA VIONGOZI WA JAMII INAYOZUNGUKA VITUO VYA KUFUA UMEME WA GESI VYA KINYEREZI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

SHIRIKA la Umeme nchini TANESCO na viongozi wa dini, vyombo vya dola na viongozi wa Serikali za Mitaa sita inayozungu vituo vya kufua umeme wa Gesi asili vya Kinyerezi jijini Dar es Salaam, wamekubaliana kuweka mikakati ya pamoja kuhakikisha jamii inashiriki katika ulinzi wa miundombinu ya umeme.

Makubaliano hayo yamefikiwa leo Septemba 30, 2016, kwenye kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC, viongozi wa dini, viongozi wa serikali za mitaa na vyombo vya dola ili kujadili namna bora ya kulinda miundombinu ya umeme kwenye vituo hivyo.

“Umeme wa Gesi ni umeme salama kabisa, hata hivyo ni wajibu wetu kushirikiana pamoja kuhakikisha miundombinu ya umeme huu wa Gesi inatunzwa na kulindwa,”, Meneja wa Kituo cha Umeme Kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge alianza kwa kusema wakati akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao hicho.

Tumeona tuitane hapa leo ili tujadiliane pamoja namna bora ya kuhakikisha umeme huu utokanao na Gesi ambao Serikali imeiingia gharama kubwa, miundombinu yake inalindwa na nyinyi viongozi mnao wajibu mkubwa wa kuwafikishia ujumbe wananchi wanaoishi maeneo yanayozunguka mitambo hii. Alisema Mhandisi Busunge.

Akitoa mada juu ya Mambo yanayoweza kusababisha uharibifu wa miundombinu ya umeme wa Gesi na hasara inayoweza kulikumba taifa na jamii kwa ujumla, Mkuu wa Usalama wa TANESCO makao makuu, Misana Gamba alisema, “Lazima tutambue kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa vituo hivi na fedha hizi ni za walipa kodi wa Tanzania, kwa hivyo ni wajibu wetu sote na sio TANESCO pekee kuhakikisha tunalinda miundombinu hii kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo,” alisema Gamba

Akifafanua zaidi, Mkuu huyo wa usalama alibainisha mambo ambayo jamii inapaswa kuelewa kuwa ni hatari dhidi ya miundombinu ya umeme ambayo ni pamoja na kuwasha moto, kulima au kuchimba mchanga, mmomonyoko wa udongo, wezi wa vyuma, uvuvi haramu, kujenga, kufanya biashara au kuendesha magari makubwa sehemu ambayo miundombinu hiyo ya umeme wa Gesi inapita.

Mkuu huyo wa usalama wa TANESCO alisema, hatari inayoweza kutokea endapo mambo hayo yatafanywa ni pamoja na kurudisha nyuma jiyihada za Serikali katika kuwaletea umeme wananchi, lakini pia hatari ya kulipuka kwa mitambo hiyo ambapo madhama makubwa yanaweza kuwakumba wananchi.

Meneja wa Kituo cha kufua umeme kinyerezi I, Mhandisi Lucas Busunge, akifungua kikao cha ujirani mwema kati ya TANESCO, TPDC na viongozi wa jamii inayozunguka Vituo vya kufua umeme wa Gesi vya Kineterezi jijini Dar es Salaam Septemba 30, 2016.
Mkuu wa Kitengo cha Usalama, TANESCO Makao makuu, Misana Gamba


Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji (aliyesimama), akizungumzia umuhimu wa viongozi wa mitaa kushirikiana na TANESCO katika kuelimisha umma, kutunza miundombinu ya umeme.

Afisa Usalama wa TANESCO makao makuu, Fidelis Almasi, akielezea namna viongozi wanavyoweza kushiriki katika kuelimisha wananchi umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme na athari za zitokanazo na uharibifu wa miundombinu hiyo kwa jamii na serikali.

Akichangia kwenye mazungumzo hayo, Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, ambaye ndiye alikuwa muendesha kikao, alisema, Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, imekuwa ikitoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kutunza miundombinu ya umeme kwa faida ya Watanzania wote, na hatua ya kikao hicho ni mwendelezo wa utoaji elimu na kuwataka viongozi hao kuwa mabalozi katika maeneo yao, kwenye nyumba za ibada, ili kusudi wananchi wengi waelewe umuhimu wa kuunza miundombinu ya umeme ambayo kimsingi ni mali ya Watanzania wote.

Naye afisa mwandamizi wa usalama Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Elias Muganda, alitahadharisha juu ya shughuli za kiuchumi kwenye eneo linakopita bomba la Gesi na ksuema hiyo ni hatari. “Kwa sasa kuna mabomba mawili yenye Gesi tayari, ambayo yako umbali wa mita 2 kwenda chini, yakipata mgandamizo unaosababishwa na magari makubwa kupita juu yake inaweza kupelekea leakge na kusababisha Gesi kuvuja na matokeo yake kila mtu anayajua ni moto.” Alifafanua

Akatoalea mfano wa mabomba yaitwayo Carthodic Protection, ambayo huzuia kutu, lakini tayari kuna watu wanang’oa vyuma hivyo na hii inaweza kusababisha kutu na mabomba kutoboka,alitahadharisha, Muganda.

Wakichangia mazungumzo hayo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kanga, Shamte Mlanzi Mkali, alitoa wito kwa viongozi wenzake wa Mitaa, kila wanapokutana kwenye vikao, moja ya ajenda ya kuzungumza ni pamoja na usalama wa mitambo ya Gesi.Hata hivyo viongozi wengi walionyesha umuhimu wa TANESCO kutoa ajira kwa vijana waishio maeneo ya jirani na mradi ili waweze kuona manufaa ya moja kwa moja ya ujio wa mradi huo.

Mambo yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho ni pamoja na ulinzi wa miundombinu ya Gesi iwe ni moja ya ajenda za vikao vya Serikali za Mitaa, na iwe marufuku kwa mtu kupita au kukatiza eneo la Mitambo bila ya kibali maalum, uwepo utaratibu wa kuwaalika viongozi wa TANESCO/TPDC kwenye vikao vya Serikali za Mitaa kama itahitajika.

Maazimio mengine ya kikao hicho kilichomuhusisha pia Mkuu wa upelelezi wa Kituo cha Sitakishari-Ukonga, SSP, Hassan Okello, ni pamoja na kampuni za ulinzi kwenye eneo la mitambo zijulikane kwa viongozi wa Serikali za mitaa yote inayozunguka eneo la mradi.

Mitaa iliyoshiriki kwenye kikao hicho ni pamona na Mtaa wa Kanga, Kibaga, Kinyerezi, Kichangani, na Kifura.
Mhandisi Busunge
Mkuu wa upelelezi, Kituo cha polisi Sitakishari-Ukonga, MrakibuMsaidizi wa Polisi, (ASP), Hassan Okello, akiwatoa hofu viongzoi hao kuhusu kutunza siri wanapotoa taarifa za wahalifu na uhalifu na kwamba yeye binafsi yuko tayari siku zote kuhakikisha usalama kwenye eneo hilo unazingatiwa
Afisa Usalama Mwandamizi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini, (TPDC), Eliasi Muganda, amesema, mabomba mawili ya gesi tayari yana gesi  na yako umbali wa kina cha mita 2 kutoka uso wa ardji na hivyo hayahitaji mgandamizo kutoka juu kwani ni hatari yanaeza kupata nyufa na kuvujisha Gesi.

Afisa Elimu wa Kata ya Kinyerezi, Mwalimu Mercy Mtei, (kulia), yeye amesema, atawashirikisha walimu na wanafunzi kueneza ujumbe kwenye jamii
Sheikh Juma Swaleh wa Msikiti wa Othman Bin-Afan wa Kinyerezi
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kichangani, Niyukuli Leonard (kulia)
Mchungaji Jacob Msami, akizungumza
Ustaadhi Ally akizungumza
Mchungaji Ariel Mungereja wa Kanisa la EAGT, Kinyerezi
Afisa Usalama wa Kituo cha Kinyerezi I, Furaha Munisi, akifafanua mambo mbalimbali ya kiusalama ambayo viongozi hao wanapaswa kuyachukua na kuwaelimisha wananchi
Picha ya pamoja baada ya kikao

WAREMBO 30 MISS TANZANIA WATINGA KAMBINI LEO, WAPEWA SOMO LA AWALI NA MISS TANZANIA WA SASA

$
0
0
Baadhi ya Washiriki watakaowania Taji la Miss Tanzania 2016 wakiwa katika picha pamoja muda mfupi baada ya kuwasili kambini. Jumla ya Washiriki 30 kutoka kanda mbalimbali nchini wameingia Kambini leo Septemba 30, 2016 tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.
Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazima akizungumza na Warembo alipokutana nao leo Septemba 30, 2016 kwenye Hoteli ya Regency, Jijini Dar es salaam. ambapo jumla ya Washiriki 30 wameingia kambini leo tayari kwa maandalizi ya Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa Mwezi ujao.


Baadhi ya Washiriki wa Miss Tanzania 2016 wakimsikiliza kwa makini Mrembo anaeshikilia Taji la Miss Tanzania kwa sasa, Lilian Kamazim.
 Warembo wakifanyiwa Usaili na viongozi wa Miss Tanzania.
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images