Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Serikali kuendelea kuagiza dawa ili kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa nchini

$
0
0
 
Na. Lilian Lundo – MAELEZO

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ikishirikiana na Bohari Kuu ya  Dawa (MSD) inaendelea kuagiza dawa ili kuhakikisha zinapatikana muda wote.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt.  Mpoki Ulisubisya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa ya hali ya upatikanaji wa dawa nchini.

“Kumekuwepo na taarifa zisizo na ukweli zilizotolewa na taasisi isiyo ya kiserikali inayofuatilia masuala ya afya nchini kwamba MSD inaupungufu mkubwa wa dawa ambapo taarifa hiyo inasema kuwa kuna makopo 173 ya dawa za  paracetamol nchi nzima, taarifa ambazo hazina ukweli wowote” alifafanua Dkt. Ulisubisya

Aidha ameeleza kuwa MSD imepokea makopo 10,000 ya vidonge vya paracetamol na kusambazwa katika vituo vyote vya kutoa huduma za afya nchi nzima.

Vile vile alisema kuwa MSD imesaini mkataba na mtengenezaji wa ndani kwa ajili ya kutengeneza makopo 138,000 ya dawa za  paracetamol yenye ujazo wa vidonge 1,000 ambazo zitaanza kupokelewa wiki ya kwanza ya mwezi Octoba mwaka huu na kusambazwa katika vituo vinavyotoa huduma za Afya nchini.

Hata hivyo alibainisha kuwa antibiotics na dawa za kupunguza maumivu (Ciprofloxacin, Ceftriaxone, Diclofenac, Co-trimoxazole, Amoxycyline, Doxycycline na Metronidazole) ambapo zilikuwa zikihitajika zaidi zimeshapokelewa na MSD na kupelekwa katika kanda zote za MSD kwa ajili ya kusambazwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Aliendelea kwa kusema kuwa, dawa za Miradi Msonge ambazo zinatibu na kuzuia magonjwa ya Malaria, UKIMWI, Kifua Kikuu, Ukoma, Kichaa cha Mbwa, Uzazi wa Mpango na chanjo mbalimbali zipo za kutosha kwenye Bohari.

Pia amesema kwa chanjo ambazo ziliripotiwa kutokuwepo zinatarajia kuwasili nchini kuanzia  Octoba 2, 2016, ambapo kwa wale waliotakiwa kupata chanjo hizo lakini hawakupata kutokana na ukosefu huo watataarifiwa ili kuweza kufika kwenye vituo vya afya na kupata chanjo hizo.

Akielezea juu ya hali ya upatikanaji wa dawa nchini Dkt. Ulisubisya alisema kuwa, kwa sasa upatikanaji wa dawa nchi ni asilimia 53 ambapo katika aina 135 za dawa muhimu, aina 71 za dawa hizo zinapatikana ghalani na nyingine zipo kwenye vituo vya kutolea huduma.

Dkt. Ulisubisya alisema kuwa hali ya upatikanaji wa dawa itaimarika zaidi Octoba mwaka huu ambapo Serikali inategemea kupokea kiasi kikubwa cha dawa pamoja na chanjo.

Burundi yawafuta machozi Wanakagera kwa tani 183 za vyakula.

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akikabidhiwa msaada na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) akiongea na wajumbe kutoka Burundi na Tanzania wakati wa kukabidhi msaada kutoka nchini Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Ujumbe wa Burundi uliongozwa na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine Nzeyimana (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kushoto (kushoto).
Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana akiongea na wajumbe kutoka Tanzania na Burundi wakati wa kukabidhi msaada kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Kushoto ni Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine Nzeyimana na wa kwanza kulia Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kushoto.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiwakaribisha wajumbe kutoka Burundi na Tanzania wakati wa mkutano kabla ya kukabidhi msaada kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Wa kwanza kulia ni Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana na katikati ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba.
Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana (katikati) akifafanua jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kushoto) mara baada ya kukabidhi ya kukabidhi msaada kutoka nchini Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya.
Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana (kushoto) akifafanua jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba (kulia) mara baada ya kukabidhi ya kukabidhi msaada kutoka nchini Burundi kwa lengo la kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu kushoto (kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana (wa kwanza kulia) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Suzan Kolimba (wa pili kulia)
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Suzan Kolimba akimaribisha Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Bw. Pascal Barandagiye mara baada ya kuwasili mpakani mwa Tanzania na Burundi katika eneo la Kabanga wilayani Ngara.
Viongozi kutoka Serikali za Tanzania na Burundi wakiwa katika picha ya pamoja na madereva wa malori yatakayosafirisha shehena ya vyakula vya msaada vilivyotolewa na serikali ya Burundi ili kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Wa nne kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt. Suzan Kolimba na Waziri wa Afrika Mashariki kutoka Serikali ya Jamhuri ya Burundi Bi. Leontine Nzeyimana (wa tano kutoka kushoto).
Viongozi kutoka Serikali za Tanzania na Burundi wakielekea kwenye eneo yaliposimama malori yaliyobeba shehena ya vyakula vya msaada vilvyotolewa na serikali ya Burundi ili kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera.

(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Ngara, Kagera)

…………………………………………………………

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO, Ngara, Kagera.

Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa tani 183 za vyakula mbalimbali kutoka Serikali ya Burundi kwa ajili ya kuwafuta machozi waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoni Kagera mapema mwezi huu na kuathiri maisha ya wakazi wa mkoa huo.

Makabidhiano ya msaada wa vyakula hivyo kutoka nchini Burundi yamefanyika mpakani mwa Tanzania na Burundi katika eneo la Kituo cha Ushuru cha Pamoja (OSBP) cha Kabanga wilayani Ngara ambapo Serikali ya Tanzania iliwakilishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu wakati Burundi iliwakilishwa na Waziri wa Afrika Mashariki Bi. Leontine Nzeyimana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Bw. Pascal Barandagiye.

Akikabidhi vyakula hivyo, Waziri Bi. Leontine amesema kuwa Serikali ya Burundi na Warundi wote walipatwa na mshtuko mkubwa na majonzi baada kusikia taarifa ya maafa yaliyowatokea ndugu zao wa mkoani Kagera.

“Kwa Kirundi tunasema, “Umubanyi niwe muryango” ikimaanisha jirani yako ni ndugu yako, kwa maana hiyo imekuwa ni wajibu kwa Serikali ya Burundi kuagiza wawakilishi wake ili waweze kufika hapa nchini Tanzania mkoani Kagera kuwaona ndugu zetu Watanzania na kuwapa pole”.

Waziri Bi. Leontine aliendelea kusema “Ndio maana tumekuja na kifurushi kidogo tu ili tuweze kuwaliwaza ndugu zetu waliofikwa na matatizo hayo” alisema Waziri Bi. Leontine

Waziri Bi. Leontine alivitaja vyakula hivyo kuwa ni pamoja na mchele tani 100, mahindi tani 50, sukari tani 30 na majani ya chai tani 03.

Akizungumzia suala la mahusiano ya Tanzania na Burundi, Waziri Bi. Leontine amesema kuwa udugu uliojengeka baina ya nchi hizo mbili na wananchi wake ni wa kihistoria, si wa leo au wa jana na kusema Serikali yake inadhamira ya kuendeleza udugu huo vizazi na vizazi huku akiamini Tanzania nayo ina dhamira hiyo hiyo.

Akitoa shukrani baada ya kupokea msaada huo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba ameishukuru Serikali ya Burundi kwa msaada waliotoa kwa Tanzania na kuongeza kuwa msaada waliotoa ni kielelezo cha mahusiano ya karibu na ya kidugu baina ya nchi hizo mbili na watu wake.

Pia Naibu Waziri Dkt. Suzan amewataka viongozi wa Serikali ya Burundi wafikishe salamu na shukrani za dhati za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunzinza na kuwathibitishia kuwa Tanzania itaendeleza uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi hizo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera ambao ndio umeathirika na tetemeko hilo Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ambaye pia ni Mkuu wa Ulinzi na Usalama wa mkoa huo ameihakikishia Serikali ya Burundi kuwa msaada walioutoa utawafikia walengwa kama ilivyokusudiwa.

Msaada huo uliotolewa na Burundi umekuwa ni mwendelezo wa misaada inayotolewa na nchi za Afrika Mashariki kwa Tanzania kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10 mwaka huu na kuathiri mikoa ya kanda ya ziwa.

Burundi imeungana na nchi za Uganda na Kenya kwa kutoa misaada kwa waathirika wa tetemeko hilo ambapo September 17 mwaka huu Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki 2 ambazo ni sawa na takribani Shilingi za Kitanzania milioni 437 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni na mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

DC KONGWA AMTUMBUA MENEJA WA MAMLAKA YA MAJI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi akizungumza wakati wa kikao cha Kumng'oa Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na salama Wilyani humo.
Watumishi wa Mamlaka ya Maji safi na salama WIlayani Kongwa wakizunguza na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe Deogratius Ndejembi.

Na Mathias Canal, Dodoma

Kushindwa kusimamia miundombinu ya maji na kupelekea kuwa na ugumu wa upatikanaji maji kwa kiwango kinachotakiwa ni miongoni mwa kadhia zilizopingwa wakati wa kampeni na Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ambaye ndiye Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kuahidi kuchagua wasaidizi watakaosimamia na kulimaliza jambo hilo mara baada ya kuingia madarakani.

Kwa kiasi kikubwa nchini Tanzania kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi wakitupa lawama kwa baadhi ya watendaji wa serikali ambao wamesababisha kudorora kwa uchumi na kuchagiza ugumu wa maisha kutokana na umbali wanaotumia kutafuta maji, huduma za afya sambamba na umbali wa shule za Sekondari na Msingi.

Kutokana na kadhia ya upatikanaji hafifu wa maji safi na salama Wilayani Kongwa imepelekea kukalia kuti kavu kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji safi na Salama Wilayani humo Ndg Kisha Bonga kutokana na kushindwa kusimamia majukumu yake ipasavyo ikiwemo kusababisha wafanyakazi wa Mamlaka ya maji kufikia maamuzi ya kuandamana.

Maandamano ya Wafanyakazi hao yalifanyika siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita yaliyoanzia Ofisi za Mamlaka ya Maji safi hadi ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kongwa wakiwa wamegoma kufanya kazi kutokana na kuchelewa kulipwa mishahara yao.

Katika malalamiko ya wafanyakazi hao yaliyopelekea kugoma kufanya kazi yanachagizwa na kudai mishahara ya zaidi ya miezi nane sasa (8) ikiwa ni muda wenye ishara ya kutolipwa mishahara yao tangu mwaka 2016 ulipochomoza mwanzoni mwa Januari mwaka huu.

Katika malalamiko yao pia wamemlalamikia Meneja huyo wa Mamlaka ya maji Ndg Kisha Bonga kwa kutumia lugha zisizo na staha kwa kuwataka waache kazi wale wote wanaoshindwa kuishi pasina kulipwa mshahara jambo ambalo linawafedhehesha watumishi hao.

Hata hivyo Dc Ndejembi akizungumza na wafanyakazi hao aliwataka kwa umoja wao kurejea Ofisini kwao na kuendelea na kazi huku akiahidi kulivalia njuga jambo hilo kwa kukutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ili wajue tatizo limeanzia wapi na kwa namna gani linaweza kutatuliwa.

Katika kutaka kutatua mgogoro huo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi alizuru katika ofisi ya Meneja wa Mamlaka ya maji kama alivyotoa taarifa kuwa angefika kukutana nae kwa pamoja washirikiane namna ya kutatua kadhia hiyo lakini Meneja huyo aliondoka na hakurejea tena tena jambo lililomlazimu kufanya kikao na wafanya kazi hao kwa kuanza kuomba kusomewa Mapato na matumizi ili kupata ahueni ya mahali pa kuanzia.

Mamlaka ya maji safi na salama Wilayani Kongwa inakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na moja (11,000,000) kwa mwezi fedha ambazo zingeweza kabisa kuwalipa wafanyakazi wote ambao kwa kila mwezi malipo ya mishahara yao haizidi milioni tano 5,000,000 hivyo kushindwa kufanya malipo hayo Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa huo ni uvivu na uzembe katika utendaji.

Fundi Mkuu wa Bomba Wilayani humo pamoja na Mkurugenzi huyo hawajawahi kupitisha hata mwezi mmoja bila kupata malipo ya mshahara wao jambo ambalo limemshangaza Mkuu wa Wilaya hiyo na hatimaye kufikia maamuzi ya kumsimamisha kazi Meneja wa Mamlaka ya maji Ndg Kisha Bonga kwa kupungua ufanisi wake katika utendaji.

Kutokana na maamuzi hayo Mkuu huyo wa Wilaya ya Kongwa kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhandisi Ngusa Izengo wamemteua Mhandisi Hamisi Ally kuwa kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji ili kusukuma gurudumu la utendaji kazi kusonga mbele.

Mara baada ya kukaimu nafasi hiyo Mhandisi Ally aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe Deogratius Ndejembi kutatua kero ya muda mrefu katika kata ya Chamkoroma kwa hujuma za wafanyabiashara wa maji kukata bomba na kuliunganisha ili wapate maji wao peke yao na hatimaye kuwauzia wananchi kwa shilingi mia nne kwa kila dumu la lita ishirini.

MKUU WA MKOA AZINDUA MIRADI YA MAJI KWA AJILI YA VIJIJI VYA SARANDA NA SUKAMAHELA NA KUPIGA MARUFUKU BIASHARA YA MKAA WILAYANI MANYONI.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akipampu maji katika kisima cha maji cha Kijiji cha Sukamahela kilichokarabatiwa na taasisi ya peace corps pamoja na wanakijiji wa Sukamahela, usambazaji wa maji kutoka katika kisima kwenda kijijini unafanywa na shirika la Wolrd Vision.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akipanda mti katika chanzo cha maji cha kijiji cha Saranda ili kutunza mazingira ambapo ukarabati na usambazaji wa maji kutoka katika chanzo hicho kwenda kijiji cha Saranda unafanywa na shirika la Wolrd Vision.



Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akizungumza na wakazi wa kijiji cha Sukamahela na kuwasisitiza kutunza mazingira na kuachana na biashara ya mkaa kwani huharibu mazingira kwa kukata miti kwa wingi.
Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe akipokea maelekezo ya kusimamia wananchi wake kutofanya biashara ya Mkaa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati wa kikao na wakazi wa kijiji cha Sukamahela, kushoto kwakwe ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Manyoni na anayefuata ni Meneja wa Wolrd Vision kanda ya kati Faraja Kulanga.

……………………………………………………………………..

Na Grace G. Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amepiga marufuku biashara ya mkaa wilayani Manyoni kutokana na ukataji miti hovyo unaoharibu vyanzo vya maji na kumwelekeza Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe kusimamia utekelezaji wa agizo hilo.

Mhandisi Mtigumwe ametoa agizo hilo katika vijiji vya Sukamahela na Saranda wilayani Manyoni wakati akizindua miradi miwili ya maji ambapo shirika la wolrd vision litatoa milioni 355 shirika la peace coarps limetoa shilingi milioni sita na wananchi wakichangia milioni mbili.

Amesema kumekuwa na tabia ya ukataji miti hovyo kwa ajili ya biashara ya mkaa hasa kwa halmashauri hiyo na kuwataka wananchi kuangalia ujasirimali mwingine huku wakiruhusiwa kukata mkaa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani tu.

Mhandisi Mtigumwe ameongeza kuwa kamati za miradi hiyo ya maji zinapaswa kusimamia moiradi hiyo na kutoa elimu ya uitunzaji wa mazingira kwa jamii inayozunguka miradi hiyo ili iweze kuwa endelevu.

Amesema kamati hizo zipange bei ya kuuzia maji itakayokuwa rafiki kwa wana jamii wote ili miradi hiyo iwanufaishe wananchi hao na kupata pesa ya kuendeshea jenerator na utunzaji wa miundombinu kwa pesa itakayokusanywa.

Mhandisi Mtigumwe amemshauri Mkuu wa Wilaya hiyo kusimamia mapato na matumizi ya pesa za miradi hiyo ya maji kutokana na kamati nyingine kufuja pesa za miradi ya maji kasha kuitelekeza bila ya kuiendeleza.

Meneja wa kanda ya kati wa shirika la World Vision Faraja Kulanga amesema tayari shirika hilo limeshatenga shilingi milioni 150 zitakazo tolewa kuanzia mwezi oktoba kwa ajili ya kutengeneza mifumo na maeneo ya kuchotea maji katika vijiji vya sukamahela na Saranda.

Kulanga amesema shirika hilo limeshakarabati mradi wa maji wa Saranda ambao tayari unatumika huku shirika likiendelea kukarabati miundombinu ya miradi hiyo na kuzisisitiza kamati za maji kumiliki na kuitunza miradi hiyo kwani wafadhili huondoka.

Naye mwenyekiti wa kamati ya maji kijiji cha Saranda Julius Kundule amesema kamati hiyo tayari ina shilingi milioni mbili kwenye akaunti huku wakiahidi kuitunza miradi hiyo.

Kundule ameongeza kuwa kamati hiyo itajitahidi kutunza miradi hiyo na kutoa elimu kwa wananchi juu ya uchangiaji wa maji ili kupata pesa kwa ajili ya ukarabati na utunzaji wa miundombinu kwakuwa wengi hudhani maji ni bure.

Wakazi wa vijiji vya Sukamahela na Saranda wameyashukuru mashirika ya world vision na peace corps kwa kukarabati miradi hiyo na kusogeza huduma ya maji karibu na makazi yao.

Wameongeza kuwa uboreshaji wa huduma hiyo ya maji utasaidia kupunguza muda wa kutafuta maji na hivyo kupata muda wa kutosha wa kujishughulisha na miradi ya maendeleo badala ya kutafuta maji.

MME NA MKE WATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI JIJINI DAR

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, linawashikilia watu wawili ambao ni Mme na Mke kwa tuhuma za matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha za moto katika maeneo tofauti tofauti jijini Dar es salaam.

Watuhumiwa hao ambao wametambulika kwa majina ya Bakari Abdallah (40) na Sihaba Omary (28) wakazi wa Vijibweni, Kigamboni walitiwa mbaroni mnamo tarehe 23 Septemba mwaka huu na Kikosi Maalum cha Jeshi hilo cha kupambana na ujambazi wa kutumia silaha.

Akizungumza mbele ya wanahabari, Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Kamishna Simon Sirro, alisema kuwa mnamo tarehe 26 Septemba mwaka huu Askari walifika nyumbani kwa watuhumiwa hao na kukuta bastola aina ya "BROWNING" yenye usajili namba CAR A081900 ikiwa na magazine mbili na risasi tano pamoja na simu aina ya Nokia Lumia ambayo inadaiwa kuwa iliporwa katika matukio ya unyang'anyi.

Watuhumiwa wote wawili wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya oparesheni ambazo zimefanyika maeneo mbalimbali na mafanikio yake leo jijini Dar es Salaam. ambapo Jeshi hilo lilifanikiwa kumtia mbaroni mtu mmoja kwa tuhuhuma za ujambazi wa kutumia silaha za moto.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro akionesha kwa wanahabari silaha zilizokamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro akionyesha gari aina ya Verosa likiwa limesheheni magunia saba za bangi leo iliyokamatwa hivi karibuni jiji Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha gari aina ya Noah ikiwa wan a magunia ya bangi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha namba za gari za bandia ambazo zimekuwa zikitumiwa na waharifu leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

NHC YAKABIDHI MASHINE ZA KUFYATULIA TOFALI KWA VIJANA BUKOBA

$
0
0
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (kushoto) akimkabidhi tofali Afisa Miradi wa Kikundi cha vijana cha Tuinuane cha Bukoba Mjini Christopher Vincent wakati wa makabidhiano ya mashine za kufyatulia matofali iliyotolewa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) yenye ubora unaofaa kujengea katika mazingira ya Bukoba kulingana na asili ya udongo na miamba ya mkoa wa Kagera.
nhc2
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na huduma kwa jamii Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bi.Susan Omari (kulia) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (kushoto) wakati wa kukabidhi mashine za kuengenezea matofali ya kisasa kwa vijana wa kikundi cha Tuinuane cha Bukoba Mjini yanayoendana na hali ya udongo na miamba ya mkoa wa Kagera leo mjini Bukoba.     
nhc4
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na huduma kwa jamii Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bi.Susan Omari (kulia) akitoa maelezo kwa vijana wa kikundi cha Tuinuane cha Bukoba Mjini yanayoendana na hali ya udongo na miamba ya mkoa wa Kagera leo mjini Bukoba.     
nhc5
Baadhi ya mashine zilizotolewa kwa vijana hao

WAFANYAKAZI WA AIRTEL WASHEREHEKEA SIKU YA WANAFAMILIA WET N WILD KUNDUCHI.

$
0
0
Watoto wa wafanyakazi wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, wakifurahia ndani ya bwawa la kuogelea katika  shamrashamra za siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Afisa Rasilimali wa watu, Mubaraka Kibarabara wa Kampuni ya Simu za Mkononi YA Airtel (kulia), akimpa zawadi Beatrice Nalingigwa baada ya kuibukas kidedea katika shidano la kuogelea katika  shamrashamra za siku ya wanafamilia wa Airtel jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya wafanyakazi na familia zao wa Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel wakichukua chakula kwa pamoja kuonyesha upendo na mshikamano wao ambao ni sehemu ya mafanikio ya kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.
 Mwanafamilia wa Airtel akiwapa chakula watoto ikiwa ni ishara ya upendo ulio ndani ya wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya Siku ya Wanafamilia wa kampuni hiyo jijini Dar es Salaam jana.

Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel Tanzania yasherehekea siku ya wanafamilia mwishoni mwa wiki hii Kunduchi Wet n Wild .

Ni muda muafaka kwa familia mbali mbali kuwezakujuana na  kujumuika kwa pamoja na kuweza kubadilishana mawazo na hata kufurahia mafanikia ya matunda waliyoyapata kwa mwa huu.

 Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya alisema ni desturi yao kuwa na siku maalumu kila mwaka ya kuwakutanisha wafanyakazi wao na familia zao ili pamoja na kushiriki michezo na mambo mengine ya kuburudisha nyoyo zao zao lakini pia huitumia siku hiyo kuzidi kuimarisha mshikamano miongoni mwao. "Umoja na mshikamano ni nyenzo muhimu mahali pa kazi, lakini pia ukiwa na mfanyakazi anayetoka katika familia iliyokosa utulivu, lakini pia mfanyakazi legelege hawezi kufanya kazi zake kwa ufanisi," akaongeza Bwana Foya.

Zaidi ya wafanyakazi na wanafamilia  600 walishiriki katika bonanza hilo na kushiriki michezo mbalimbali kama vile kucheza muziki, kuvutaka kamba, soka la baharini, wavu na kuogelea.  Baadhi ya watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania wakishindana.

MAKALA FUPI-SERIKALI YA BURUNDI YATOA TANI 183 ZA VYAKULA KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO


JUMLA YA WATOTO 4000 WANAZALIWA NA TATIZO LA KICHWA KIKUBWA NA MGONGO WAZI KILA MWAKA HAPA NCHINI TANZANIA

$
0
0

kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman Kiloloma akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Arusha
Gabriel Daqarro sehemu ambayo mtoto amefanyiwa upasuaji wa kichwa

Mkuu wa wilaya ya Arusha akiwasili katika hospitali ya Mount Meru iliopo jijini hapa Tayari kwakwenda kuangalia watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa

kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman Kiloloma akiwa anampa mkuu wa wilaya ya Arusha maelekezo ya picha inayoonyesha jinsi mtoto alivyokuwa kabla ya kufanyiwa upasuaji
mkuu wa wilaya ya Arusha mjini akimkabidhi pampas moja ya mama mzazi wa mtoto ambaye amefanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa ikiwa ni moja ya zawadi walizopatiwa na GSM Foundation

mkuu wa wilaya ya Arusha akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea watoto waliofanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa kikubwa



Na Woinde Shizza, Arusha

Jumla ya watoto 4000 wanazaliwa kila mwaka na tatizo la kichwa kikubwa na mgongo wazi na kati ya hao ni watoto 500 tu ndio wanafikishwa hospitalini kwa ajili ya upasuaji huku wengine 3500 awajulikani wanapopelekwa.

Hayo yamebainishwa leo na kaimu mkurugenzi Wa taasisi ya upasuaji mifupa na mishipa ya fahamu Dr.Othman Kiloloma wakati akiongea na waandishi Wa Habari Mkoani hapa.

Alisema kuwa wao kama taasisi ya moi walikaachini na kuona kunawatoto wengi ambao wanazaliwa na vichwa vikubwa lakini hawafiki hospitalini kwa ajili ya garama huku wengine wakiwa wanaamini imani za kishirikina kitu ambacho sivyo.

Alibainisha kuwa mpaka sasa wameshatembelea mikoa 13 ambayo ni awamu ya kwanza na wameshafanya upasuaji jumla ya watoto 167 ambapo kwa mkoa Wa Arusha wamewaona watoto 35 na wamewafanyia upasuaji watoto sita.

"Kila mwaka watoto 4000 wanazaliwa na kati yao 500 tu ndio wanafikishwa hospitali lakini watoto wanaobaki 35000 atujui wanaenda wapi au wanapelekwa wapi maana hospitalini awaji"alisema Kiloloma

Kwa upande wao wagonjwa waliofanyiwa upasuaji Wa kichwa Nasson Daniel 17 aliyelazwa katika wodi ya majeruhi wanaume no 3 pamoja na Aisha Amir Suleiman 17aliyelazwa wodi ya majeruhi wanawake wameiomba jamii wasiwafiche watoto wenye matatizo ndani wawatoe ili wakatibiwe kama walivyotibiwa wao.

Akizungumza kwa niaba ya wazazi wenye watoto waliofanyiwa upasuaji Emelda Buxay (36)amesema kuwa amewaomba huduma hii isogezwe karibu na jamii maana watoto wengi wenye matatizo kama haya wapo vijijini wanateseka na hawana msaada .

"Wazazi wenzangu haswa wakina mama sisi ndiyo tunakaa na watoto kwa mud a mrefu ndiyo tunaweza kugundua mabadiliko ya mtoto ,tusisikilize dhihaka za watu mtaani ambazo Mara nyingi watu wamekuwa wakisema pale wanapoona mtoto mwenye ulemavu wowote hebu tuchukue hatua tuwapeleke hospitalini,kama vile mtoto wangu Dorcus alivyofanyiwa upasuaji leo ni Siku ya tatu kichwa kinaendelea kupungua ,tusiwafiche watoto jamani "alisisitiza Emelda.

Naye mkuu Wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro alitoa wito kwa jamii hususa ni wazazi kutowaficha watoto wenye tatizo hilo kwani tatizo linatibika na mtoto anapona kabisa .

Alisema anapenda kuwashukuru madaktari hawa walioibua na kuangalia namna gani wanaweza kusaidia watoto hawa pamoja na shirika la GSM foundation ambao ndio waliothamini Huduma hii ya upasuaji bure ambapo alisema kwa upande wa Arusha jumla ya watoto 35 wameonwa huku watoto sita wakiwa wamekishwa fanyiwa upasuaji.

UWT ILIVYOCHANGIA MIFUKO YA SARUJI 200 KWA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA

NDEGE YA PILI YA BOMBARDIER Q-400 YAWASILI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikipata Saluti ya maji (Water Canon Salutation) mara tu baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ikiegeshwa karibu na pacha wake iliyofika wiki moja uliopita katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Katibu Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamriho na viongozi wengine wakielekea kwenye Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) ilipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Katibu Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamriho akisalimiana na nahodha wa  John Kuipers aliyeendesha Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) na kuiwasilisha salama katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa. Sherehe za uzinduzi rasmi wa ndege hizo umepangwa kuganyika kesho Jumatano Septemba 28, 2016 hapo hapo uwanjani.
Katibu Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamriho akikagua Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
Katibu Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamriho akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi pamoja na maafisa wengine wakiwa katika Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
Nahodha John Kuipers na Nahodha Owen Davies walioendesha Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) wakifurahia mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi wakitelemka baada ya kuikagua Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.
Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akimpa pongezi nahoda wa John Kuipers aliyeendesha aliyeendesha Ndege ya pili ya Bombadier Q400 iliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) mara ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Septemba 27, 2017 ikitokea Canada ilikotengenezwa.












CHADEMA IRINGA YASAIDIA ZAIDI YA WANAFUNZI MIA MBILI (200) KUENDELEA NA MASOMO

$
0
0
 Diwani wa  viti maalum CHADEMA Sara Mwajeka na  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igumbilo, Fredrick Asenga wakionyesha mfano wa sare za wanafunzi walizotoa msaada
 Naibu Meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igumbilo, Fredrick Asenga wakiwa tayari kukabidhi sare kwa wanafunzi
Hawa ni baadhi ya wanafunzi mia mbili (200) wanaoishi katika mazingira magumu wanatarajiwa kusaidiwa msaada wa pesa kwa ajili ya kununulia sabuni,nauli kila wiki na sare za shule ya msingi.
  NA FREDY MGUNDA,Iringa
 
ZAIDI ya wanafunzi mia mbili (200) wanaoishi katika mazingira magumu wanatarajiwa kusaidiwa msaada wa pesa kwa ajili ya kununulia sabuni na nauli kila wiki na wanawake walionda timu maalum ya kutoa msaada kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
 
Msaada huo unatarajiwa kutolewa kwa wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kutoka kata nne zilizoko manispaa ya Iringa ambazo ni Miyomboni, Igumbilo, Kitanzani na Ruaha na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 3.5
 
Akizungumza wakati wa kuwakabidhi msaada wa sare za shule,viatu na soksi wanafunzi hao, katika hafla fupi ya iliyofanyika katika shule ya msingi ya Igumbulo, Diwani wa   viti maalum CHADEMA Sara Mwajeka alisema kuwa wameamua kuwasaidia wanafunzi hao kwa lengo la kuwapatia elimu bora japo kuwa misaada hiyo haiwezi kumaliza shida zao.
 
Mwajeka aliongeza kuwa wanafunzi wenye mazingira magumu wanatakiwa kusoma ili taifa lipate wasomi wengi wenye tija ya kuisaidai nchi yao kuendelea kiuchumi.
 
“Mimi kama mama napata uchungu kuona wanafunzi wenye mazingira magumu wanasoma kwa taabu huku wana uwezo mkubwa darasani,hivyo tunajitaidi na kujikuna pale tunapoweza kuwasaidia wanafunzi nawaomba watu wenye uwezo kuwasaidia wanafunzi wote wenye mazingira magumu” alisema Mwajeka.
 
Kwa upande wake Naibu Meya wa manispaa ya Iringa Joseph Lyata aliwapongeza timu ya wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) manispaa ya Iringa kwa kutoa msaada huo ambao ni mkubwa kwa maisha ya wanafunzi wanaoishi kwenye mazingira magumu.
 
“Tanzania yetu kuna matajiri wengi sana lakini wanashindwa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu lakini wakimama hawa wamejitoa kwa kile walicho nacho kuwasaidia wanafunzi hao hivyo nami naunga mkono kuendelea kuchangia watoto hawa” alisema Lyata
 
Aidha Lyata aliwataka viongozi wa nchi kuwaangalia wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu ili kufuata na kumuenzi Mwalimu Nyerere kwa vitendo kwani alikuwa anapenda sana elimu ili wananchi waweze kuongeza ufahamu na kujua mbinu za kujitegemea na sio kuomba omba kila siku.
 
“Jamani kusaidia wanafunzi wenye mazingira magumu hawana idikadi ya vyama,dini wala makabila tunatakiwa kuwasaidia kutokana na uwezo wetu wa kifedha,mm nimekuwa mwalimu kwa muda mrefu na nayajua matatizo ya wanafunzi wenye mazingira  wanavyosoma kwa taabu ni aibu kwa taifa kama Tanzania kuwa wanafunzi wanaoteseka kama hawa” alisema Lyata.
 
Naye Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Igumbilo, Fredrick Asenga aliwashukuru timu ya wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Naibu Meya, Joseph Lyata kuwa kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo kwani wamewapunguzia na kuwaondolea aibu iliyokuwa inawakumba kutokana na umasikini wao.
 
“Wanafunzi hawa walikuwa wanavaa sare ambazo zilikuwa zimechanika na ilikuwa aibu kwa wanafunzi wengine lakini kwa msaada huu mmefanya wajisikie nao ni matajiri na najua sasa watasoma kwa bidii bila kujiangalia  wamekaaje hongereni sana na karibuni tena kuendelea kuwasaidia wanafunzi hawa” alisema Asenga.
 
Misaada hiyo imetolewa na timu ya wanawake wa chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) manispaa ya Iringa kwa lengo la kuwasaidia watoto wenye mazingira magumu wasome wakiwa na furaha kwa kuwa nao ni binadamu kama binadamu wengine.

Prof. Ndalichako aitaka Bodi mpya ya TCU kushughulikia matatizo Vyuo Vikuu

$
0
0
Na. Lilian Lundo - MAELEZO
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameitaka Bodi mpya ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) aliyoizindua leo jijini Dar es Salaam, kushughulikia kikamilifu changamoto zilizoko katika Tume hiyo.
Prof. Ndalichako ameiambia bodi hiyo kuwa amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kuhusiana na vyuo wanavyosoma, hivyo ni wakati wa bodi hiyo kufuatilia kwa ukaribu malalamiko hayo na kuyafanyia kazi.
“Tunaelewa kwamba wanafunzi ni watu wa kulalamika kila wakati, lakini yapo malalamiko ambayo yana tija na ni lazima yatatuliwe, kwa mfano malalamiko yanayohusu uvurugaji wa matokeo au taratibu zinazokuwa kandamizi kwa wanafunzi na walimu wa vyuo vikuu,” alifafanua Prof. Ndalichako.
Akitolea mfano wa taratibu kandamizi katika vyuo hivyo, Prof. Ndalichako amesema kwamba mwanafunzi anapopoteza kitabu cha chuo hulipishwa mara tatu ya gharama ya kitabu hicho huku mwanafunzi huyo akiwa ni mtoto wa masikini hali inayopelekea wanafunzi kutoazima vitabu wakihofia kulipishwa gharama kubwa pindi vitabu hivyo vitakapopotea.
Vile vile amesema kuwa kuna baadhi ya vyuo vimekuwa vikiwataka walimu kutoa taarifa ya kuacha kazi miezi mitano kabla ya kuacha kazi ambapo sheria mama inamtaka mwajiriwa kutoa taarifa ya kuacha kazi kwa mwajiri miezi mitatu kabla ya kuacha kazi.
Aliendelea kwa kusema kuwa taratibu hizo  zinawakandamiza  walimu kwani chuo kinapoamua kumfukuza kazi mwalimu humfukuza papo kwa hapo bila kumpa muda wa kujiandaa.
Pia amesema kuwa amepokea malalamiko kutoka kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Ifakara mwezi Mei mwaka huu kuhusiana na walimu wa chuo hicho kuvuruga matokeo yao, lakini chuo hicho akijatoa maamuzi juu ya walimu hao mpaka hii leo, hivyo kuwaacha wanafunzi kuendelea kubaki nyumbani bila kujua hatima yao.
Aliongeza kwamba TCU inamamlaka yote yakuvifuatilia vyuo vikuu vyote nchini pamoja na kuangalia utendaji kazi wa vyuo hivyo ikiwa unaendana na viwango vilivyowekwa.
Aidha, ameitaka TCU kufanya utafiti wa wanafunzi walioko vyuoni ili kubaini wanafunzi wasio na sifa kutokana na baadhi ya vyuo kuingiza wanafunzi kinyemela bila kupitia TCU au Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).
Vile vile, Prof Ndalichako ameitaka Bodi hiyo kutunga sheria ya Vyuo Vikuu itakayoipa meno tume hiyo kusimamia vyuo vikuu bila kuwa na pingamizi lolote.
Bodi hiyo itafanyakazi kwa kipindi cha miaka 3, kuanzia   Septemba 28 mwaka huu  hadi  Septemba 2019, ikiongozwa na Mwenyekiti Prof. Philip Jacob Mtabaji.
 

DFID YATOA MSAADA WA BILIONI 6.3 KUSAIDIA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI IHUNGO MKOANI KAGERA

$
0
0

.Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, ,Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari juu ya kupoka msaada wa Shilingi Bilioni 6.3 kutoka Idara ya Maendeleo ya Nje ya nchini Uingereza(DFID) ikiwa na sehemu ya kusaidia Shule zilizoathirika na tetemeko la Ardhi mkoani Kagera leo jijini Dar es Salaam kushoto ni Mkuu wa Idara ya DFID hapa nchini,Vel Gnanendran.
Mkuu wa Idara ya DFID hapa nchini,Vel Gnanendran akizungumza na waandishi wa habari juu ya Serikali ya Uingereza kutoa msaada wa Shilingi Bilioni 6.3 wenye lengo la kusaidia waathirika wa tetetmeko la ardhi hususan kwa shule zilizoathiriwa na tetemeko hilo,kulia ni Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi, ,Profesa Joyce Ndalichako.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.


Na: Frank Shija, MAELEZO.

MSAADA wa Shilingi bilioni 6.3 umetolewa na Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID) ili kufanikisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Ihungo iliyo haribika baada ya kuathiriwa na tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 Septemba mkoani Kagera.

Hayo yabainishwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kuhusu huo.

Profesa Ndalichako amesema kuwa msaada huo umetokana na ziara aliyoifanya tarehe 17 na 18 mkoani Kagera ambapo mwakilishi kutoka DFID nchini alishiriki katika zaiara hiyo na kutembelea shule zilizo haribika kutoka na tetemeko hilo.

“Baada ya bunge kuisha tarehe 17 na 18 nilifanya ziara ya kutembelea shule zilizoharibika kutokana na tetemeko, kwa bahati wadau wetu wa maendeleo DFID waliungana name kutembelea shule za Ihungo na Rugambwa kutokana ziara ile wameamua kutusaidia” Alisema Ndalichako.

Kufuatia ziara hiyo ambapo walijionea uharibifu mkubwa wa majengo ya shule ya Ihungo na nyumba za walimu wa Shule ya Sekondari ya Rugambwa, DFID waliguswa na athari walizozikuta na kuamua kusaidia ujenzi wa Shule ya Ihungo na nyumba 10 za walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Rugambwa.

Amesema kuwa msaada huo umelenga kujenga upya shule ya Sekondari ya Ihungo ikiwa ni pamoja na kujenga maabara ya kisasa na kununua samani zilizoharibika. Mpaka sasa wataalamu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wapo mkoani Kagera mabapo leo wanakabidhiwa shule hizo na Manispaa ya Bukoba ili waanze ujenzi wake unaotarajiwa kukamilika mwezi Januari mwakani.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Kimataifa nchini (DFID Tanzania) Vel Gnanendran amesema kuwa Serikali ya Uingereza imeguswa sana na athari zilizotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.

“Kwa niaba ya Serikali ya Uingereza tunatoa pole sana kwa Mhe. Rais Magufu na waathirika wote wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera kwa ni tukio lisilo pangwa”. Alisema Mkuu huyo. Vel amesema kuwa lengo kubwa la wao kutoa msaada huo ni kuhakikisha miundombinu ya shule zilizoharibika kujengwa haraka ili wanafunzi waweze kurejea mashuleni katika wakiwa katika hali ya kawaida.

“Tumeguswa sana na athari zilizotokana na tetemeko la Kagera, Serikali ya Uingereza kupitia ofisi ya DFID Tanzania imetoa msaada wa pound milioni 2.23 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 6.3 za Kitanzania”. Alisema Vel.

DFID ni idara iliyo chini ya Serikali ya Uingereza ambayo imekuwa ikisaidia masuala mbalimbali ya maendeleo katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.

TAARIFA RASMI KUTOKA IKULU YA UZINDUZI WA NDEGE MBILI ZILIZONUNULIWA NA SERIKALI KWA AJILI YA ATCL

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe akishuka kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam leo Jumatano Septemba 28, 2016.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Septemba, 2016 amezindua ndege mpya mbili aina ya Bombardier Dash 8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Uzinduzi wa ndege hizo za kisasa zilizotengenezwa nchini Canada, umefanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles, Mawaziri, Wabunge, Viongozi wa Wafanyabiashara, Taasisi mbalimbali na wadau wa usafiri wa anga.

Kabla ya kuzindua ndege hizo zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja, Rais Magufuli ameshuhudia makabidhiano ya mkataba wa ukodishaji wa ndege hizo kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kwa niaba ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) kwenda kwa Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho kwa niaba ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Taarifa ya ununuzi wa ndege hizo iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa ndege hizo ni mali ya Serikali na zitakodishwa kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa lengo kutoa huduma za usafiri wa anga ndani na nje ya nchi.

Imeongeza kuwa ndege hizo zimenunuliwa kwa kuzingatia kuwa zinafaa kufanya kazi katika mazingira ya Tanzania ikilinganishwa na ndege nyingine za jamii yake, na imetaja manufaa hayo kuwa ni pamoja na uwezo wa kuruka na kutua katika viwanja vya lami na visivyo vya lami, matumizi madogo ya mafuta, kuwa na injini zenye nguvu zaidi na kubeba mzigo mkubwa.

"Ni dhairi kuwa ndege hizi zitaimarisha mtandao wa huduma za usafiri wa anga kwa soko la ndani, lakini pia zitaongeza ushindani na kuleta unafuu wa bei kwa watumiaji wa usafiri wa anga, vilevile zitaimarisha sekta za biashara na uwekezaji na kuwezesha watalii kutembelea vivutio vya ndani ya nchi"ameeleza Balozi Kijazi.

Kwa upande wake Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa na kutimia kwa ahadi aliyoitoa ya kununua ndege mpya ili kufufua usafiri wa anga kupitia ATCL na ameahidi kuwa Serikali imeanza mazungumzo ya kununua ndege nyingine mbili zitakazofanya safari za ndani na nje ya bara la Afrika ambapo moja itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 160, na nyingine itakuwa na uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 240.

"Kwa sababu fedha za kununulia ndege hizo zote mbili kubwa zipo, tukinunua ndege ya kubeba watu 240 itakuwa inatoka hapa Dar es Salaam hadi Marekani bila kutua popote, itaondoka hapa Dar es Salaam mpaka China bila kutua popote ili watalii wanaotoka China, Marekani, Urusi, Ujerumani na nchi nyingine wasifikie nchi nyingine, watue hapa moja kwa moja na waangalie maliasili zetu tulizonazo, utalii wetu upande, na huo ndio mwelekeo wa nchi yetu tunaoutaka"amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa nchi na kuwapuuza watu wanaobeza juhudi hizo wakiwemo waliobeza ununuzi wa ndege hizo kwa kujenga hoja zisizo za msingi.

Aidha, Dkt. Magufuli ameitaka Bodi na Menejimenti ya ATCL kufanya kazi kwa weledi na ufanisi huku akiisisitiza kuondoa kasoro zote zilizosababisha kampuni hiyo kudorola ikiwemo kuchuja na kuwaondoa wafanyakazi watakaoshindwa kuendana na mwelekeo unaostahili, wasio waadilifu na waaminifu, wasaliti na wahujumu.

Rais Magufuli pia amewataka Watanzania wote wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi kusafiri kwa kutumia ndege hizo ili Kampuni ya ATCL ijiimarishe na iweze kujiendesha badala ya kutegemea ndege za Serikali.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Septemba, 2016

RC ARUSHA, MRISHO GAMBO AWAHIDI NEEMA WASANII WA MKOA WAKE

$
0
0

Na Woinde shizza,Arusha 

SHIRIKISHO la wasanii wa filamu jijini Arusha wameshukiwa na neema kutoka kwa Mkuu wa mkoa,Mh Mrisho Gambo kufuatia mkuu huyo kuwahidi kutatua matatizo yao.

RC Gambo ameahidi kuwasaidia wasanii wa filamu Mkoani hapa ambapo amewataka kufika ofisini kwake mapema kesho kwa ajili ya kuwasikikiza na kutatua kero zao.

Akizungumza  leo katika ufunguzi wa Mafunzo yaliyoandaliwa na jiji hilo ya siku mbili yenye lengo la kuwafundisha vijana ujasiriamali na jinsi ya kujikwamua katika umaskini Gambo aliwataka vijana kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na asilimia tano inayo toka serikalini.

" Tunaamini serikali yetu imekusudia kuwasidia wanyonge na wote wenye juhudi katika utafutaji hivyo ni vyema mkachangamkia fursa zitolewazo katika jamii yenu na mjiunge katika vikundi ambapo mtanufaika. alisema Gambo.

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la waigizaji wa filamu jijini Arusha(TDFAA) Isack Chalo alisema tasnia ya usanii mkoani hapo inakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo ukosefu wa Eneo la kufanyia mazoezi na Television ya mkoa ya kuonyesha kazi zao.

" Tunatamani kupata eneo la kufanyia shughuli zetu hususani mazoezi kwani tulizoea kufanyia shule ya msingi makubusho ambapo kwa sasa tumefukuzwa , hatuna sehemu ya Uhuru kufanyia mazoezi yetu" alisema Chalo.

Alisema walikuwa wamepanga kujenga Meru Village sehemu ambapo wangepata uwanja mpana wa kufanyia mazoezi lakini hadi sasa hawajafanikiwa kutokana na kukosa sapoti.

"Kama vile wasanii wa Dar es salam walivyopatiwa eneo kule Bagamoyo na sisi tunapenda tukumbukwe katika hili ili tuwe huru katika kufanya shughuli zetu pamoja na pia tuweze kutambulika" alisema.

Aliwataka wana Arusha kununua kazi za wasanii wa Arusha na wasiegemee tu upande mmoja wa filamu za Kikorea ( seasons) wakawasahau watu wa nyumbani jambo linalorudisha nyuma maendeleo ya wasanii Arusha na Tanzania kwa ujumla.

Naye Mmoja wa wasanii hao Experinsia Musa akisoma risala mbele ya Mkuu wa mkoa alisema pamoja na kupatiwa eneo la kujenga ofisi zao, bado wanakabiliwa na eneo la kilimo na ufugaji kwa wale wasanii wasiokuwa na ajira ili waweze kujiajiri kupitia kilimo na ufugaji.

Wasanii wa mkoa wa Arusha pia walitumia fursa hiyo ya kumkabidhi mkuu wa mkoa,Mrisho Gambo baadhi ya kazi zao ambazo wamezifanya ili na yeye azione na aweze kuwasadia zaidi.

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akiongea na wasanii wa mkoa wa Arusha waliohudhuria semina ya Ujasiriamali iliyofanyika leo katika viwanja vya shule ya msingi ya Arusha School iliopo jijini humu
Wasanii wa aina mbalimbali wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kwa makini

Kaimu Afisa maendeleo ya Jamii Jiji Tajieli Mahega akisoma risala fupi inayoelezea lengo la kuandaa mafunzo hayo kwa wasanii hao
Kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Rebeka Mongi akiwa anaongea na wasanii wa mkoa wa Arusha waliohudhuria mafunzo hayo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Arusha
 .

Muhimbili Yapokea Majokofu Sita Kutoka Auction Mart Leo

$
0
0
 Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Ageness Mtawa akipokea msaada wa majokofu sita kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Majembe Auction Mart Ltd, Sethi Moto. Majokofu hayo yatatumika kuhifadhi dawa katika wodi namba 16 Kibasila.  Kulia ni Meneja wa Jengo la Kibasila, Sister Leonarda Lodovick. 
stv2

(TFS) WASAINI MKATABA WA KUUZIANA MALIGHAFI YA MITI AINA YA MISINDANO NA MIKARATUSI NA KIWANDA CHA KARATASI CHA MUFINDI (MPM)

$
0
0
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Prof. Dos Santos (kulia) akizungumza katika hafla fupi ya kusainiana mkataba wa kuuziana Malighafi  ya miti aina ya Misindano na  Mikaratusi baina ya Wakala huyo na  kiwanda Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi ( MPM) yaliyofanyika jijini jana Dar es Salaam . ( Picha na Lusungu Helela, Wizara ya Maliasili na Utalii)
waka1
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Prof. Dos Santos (kulia)  na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi ( MPM) Jaswart Singhrai  wakisaini mkataba wa kuuziana Malighafi  ya miti aina ya Misindano na  Mikaratusi baina ya Wakala huyo na  kiwanda  hicho yaliyofanyika jana jijini  Dar es Salaam . ( Picha na Lusungu Helela, Wizara ya Maliasili na Utalii)
waka2
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) Prof. Dos Santos (kulia) akibadilishana hati ya mkataba wa kuuziana Malighafi  ya miti aina ya Misindano na  Mikaratusi na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi ( MPM) Jaswart Singhrai jana jijini Dar es Salaam.  ( Picha na Lusungu Helela, Wizara ya Maliasili na Utalii)

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuwa mgeni rasmi Mkutano wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya.

$
0
0
NA Beatrice Lyimo-MAELEZO

Dar es Salaam

WAZIRIwa Mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa 47 wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya utakaofanyika kuanzia Septemba 30 hadi   Octoba 2 mwaka huu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jumuiya hiyo Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry, Katibu Mkuu Msaidizi Abdurahman Ame alisema kuwa mkutano huo utafanyika eneo la kitonga, kata ya Msongola Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.

Alisema Jumuiya imeandaa mkutano huo kwa lengo la kuhamasisha amani katika jamii na kuwakumbusha waumini hasa wa kiislamu juu ya misingi sahihi ya dini ya kiislamu pamoja na kumjua na kutimiza haki ya Mwenyezi Mungu.

“Wajibu wa kiongozi wa dini ni kuandaa na kuhamasisha masuala ya dini, hivyo lengo la mkutano huo ni kuhamasisha amani katika jamii na pia kuwakumbusha waumini wa kiislamu juu ya kumjua, kuishi na kutimiza haki ya Mwenyezi Mungu hali itakayosaidia kuondokana na vitendo viovu,” alifafanua Katibu huyo.

Mbali na hayo, mkutano huo utabebwa na kaulimbiu isemayo “kuitambua amani ya jirani yako, huvunjilia mbali kuta zinazowatenganisha” ikiwa na ujumbe ya kwamba kuna haja ya kuelimisha jamii uzuri wa mafundisho ya dini kwa kutumia vitabu vitakatifu kupitia vyombo mbalimbali vya masasiliano.

Vile vile, Washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi zikiwemo Kenya, Uganda, Burundi, Malawi, Msumbiji na Uingereza wakiwemo viongozi wa vyama vya siasa, taasisi za kidini na za kijamii watashiriki katika mkutano huo.

Ahmadiyya ni jumuiya ya waislamu ya kimataifa iliyoenea katika nchi 209 duniani kwa lengo la kuleta uhuisho wa dini ya kiislamu kwa kutangaza kwa amani ujumbe sahihi wa Islam duniani kote.

NMB PROGRAMU YA SHULE DIRECT JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
 Mkuu wa shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa, Gebo Lugano akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa uzinduzi wa Proramu ya Shule Direct katika shule hiyo  ambayo itawasaidia wanafunzi kujifunza kwa kutumia Mtandao wa www.shule Direct.co.tz ambapo wanafunzi watajisomea masomo yao kupitia mtandao huo.

Wakati huo huo imezinduliwa akaunti ya ya NMB chipukizi akaunti kwaajili ya wanafunzi pamoja watoto wenye umri wa kuanzia miaka 14 kwaajili ya kujiwekea akiba ikiwa mprogramu hiyo imeanzia katika shule ya shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo.
Maneja mwandamizi wa amana, huduma za ziada na bima wa Benki ya NMB, Stephen Adil akizungumza na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa benki ya NMB waliohudhulia katika uzinduzi wa programu ya Shule Direct jijini Dar es Salaam leo katika shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa.
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa waliohudhulia katika kuzinduzi wa Shule Direct pamoja na NMB chipukizi akaunti ambapo baadhi ya wanafunzi wamefungua akaunti wakati huo huo.
 Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyarandu akizungumza wakati wa kuzindua Shule Direct ambapo wanafunzi watatembelea mtandao wa www.shuledirect.co.tz kwaajili ya kujifunzia masomo mbalimbali ambapo wanafunzi watatembelea mtandao huo  kwaajili ya kujifunza masomo mbalimbali. 
 Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde akizungumza wakati wa uzinduzi wa Shule Direct kwa wanafunzu wa shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo, amewaasa wa wanafunzi kusoma kwa kutumia mtandao wa www.shule.co.tz kwaajili ya kujifunza zaidi masomo yao na si kutembelea mitandao mingine ambayo haihusiana na masomo yao.
Pia amewaasa kujiwekea akiba zao kupitia akaunti ya Chupukizi ya NMB kwa pesa kidogokidogo wanazopewa na wazazi wao ili ziwafaidisha baadae na si kutumia pesa hovyo.
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde,  Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyarandu,  pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NMB pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa wakiangalia programu ya Shule Direct jinsi inavyofanya kazi.


 Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde,  Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyarandu na wafanyakazi wa NMB wapewa Maelekezo na Mtaalamu wa Kompyuta wa Programu ya Shule Direct, Erick Kondela wakati wa uzinduzi wa Programu ya Shule Direct katika shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa jijini  Dar es Salaam leo. 
Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyarandu akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa benki ya NMB na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde wakati walipotembelea Darasa la Shule Direct katika shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo.
 Mtaalamu wa Kompyuta wa Programu ya Shule Direct, Erick Kondela akiwasimamia baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo.
 Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Antony Mavunde,  Mkurugenzi wa Shule Direct, Faraja Nyarandu wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuzindua programu ya Shule Direct katika shule hiyo.
 Baadhi ya wanafunzi wakipokea zawadi baada ya kujibu maswali vizuri.
Picha ya Pamoja  baada ya kupata zawadi.

Baadhi ya wanafunzi wakifungua akaunti ya chupukizi ya NMB jijini Dar es Salaam leo.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images