Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu azindua Bodi Mpya ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

$
0
0

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo (kushoto) akimuonyesha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) jengo linalojengwa katika Hospitali hiyo ambalo litatumika kuweka mashine zitumikazo kufanyia mionzi kwa jili ya wagonjwa wa saratani hospitalini hapo.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam, Bwana Diwan Msemo (kulia) akimueleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) baadhi ya majukumu wayafanyayo katika Hospitali hiyo alipowasili kufanya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini hapo, ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika hiyo mapema 17 Desemba, 2015.
Mama wa mgonjwa (kulia) akimueleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kushoto) juu ya changamoto za gharama za kupata matibabu wazipatazo wakati Waziri huyo alipofanya ziara katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyolenga kufanya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini hapo, ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika hiyo mapema 17 Desemba, 2015.
Muuguzi wa wagonjwa (kushoto) akimueleza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) juu ya changamoto za dripu wazipatazo wakati Waziri huyo alipofanya ziara katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyolenga kufanya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini hapo, ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika hiyo mapema 17 Desemba, 2015.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) akimjulia hali mama mgonjwa wakati alipowasili katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyopo Dar es Salaam kufanya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini hapo, ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika hiyo mapema 17 Desemba, 2015.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akitoa hotuba fupi wakati aliwaposili katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road iliyopo Dar es Salaam kufanya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini hapo, ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika hiyo mapema 17 Desemba, 2015.


Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria katika Mkutano wa Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Hospitalini Saratani ya Ocean Road iliyopo jijini Dar es Salaam uliofanyika 17 Desemba, 2015 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (hayupo pichani).
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar es Salaam 17 Desemba, 2015. (Picha zote na Benedict Liwenga)


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) akipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo (kushoto) mara alipowasili katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road ya Jijini Dar es Salaam kwenye Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road uliofanyika leo 17 Desemba, 2015.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo (aliyevaa suti) akimpeleka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia) katika chumba ambacho ukarabati wa mashine za matibabu zilizopata hitilafu ukiendelea katika Hospitali hiyo mara alipowasili hospitalini hapo mapema 17 Desemba, 2015.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akipatiwa maelezo toka kwa Mganga wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road juu ya matatizo ya kiufundi ilizozikumba mashine za matibabu hospitalini hapo wakati wa ziara yake ya Uzinduzi wa Bodi ya Taasisi ya Saratani ya ya hospitalini hapo uliofanyika leo 17 Desemba, 2015. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo
Baadhi ya Mafundi wakionekana kutengeneza mashine iliyopata matatizo wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu hospitalini hapo iliyolenga kufanya Uzinduzi ikiwemo kuangalia vitendea kazi na kero wazipatazo wagonjwa wenye matatizo ya saratani katika Hospitali ya Saratani ya Ocean Road.
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road, Bwana Diwan Msemo (kulia) akimpeleka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) kuangalia jengo ambalo litatumika kwa ajili ya mashine maalum za kufanyia huduma za mionzi kwa wagonjwa wa saratani katika Hospitali hiyo.


Na Shamimu Nyaki.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee Na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu leo amezindua Bodi Mpya ya Wadhamini ya Taasisi ya Saratani katika Hospitali ya Ocean Road Ambayo itasimamia programu za elimu ya afya kuhusu Saratani.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mhe. Ummy Mwalimu mbali na kutoa pongezi za uundwaji wa Bodi hiyo amewataka watendaji kuhakikisha wagonjwa wa Saratani wanapata huduma bora, ushauri wa namna ya kuzuia magonjwa ya Saratani, kufanya utafiti wa magonjwa ya Saratani kwa kushirikiana na wadau wengine wa ndani na Nje kwa kuwa Taasisi hiyo imeanzishwa ili kuwasaidia wagonjwa hao.

“Tumieni uzoefu wenu,vipaji vyenu, na taaluma zenu katika kutoa huduma kwa kuwa Taasisi hii inategemewa na watu wote”Alisema Mhe.Waziri.

Aidha Waziri huyo amewahakikishia watandaji wa Bodi hiyo kwamba atashirikiana nao kwa karibu zaidi katika kufanikisha ugojwa wa Saratani unatokomea au kupungua kwa vile Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) inaonyesha kuwa Tanzania ina jumla ya wagonjwa 33,884 lakini wanaopata huduma ni Wagojwa 3000 ambao ni sawa na asilimia 16 tu.

Mhe Ummy amesema atahakikisha Taasisi hiyo inatengewa fedha za kutosha ili iweze kutoa huduma na kupunguza tatizo la ugonjwa wa Saratani hapa nchini kwa kufanya tafiti muhimu Ktika maeneo tofauti na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ugojwa huo kwa vile wananchi wengi wanagundua ugonjwa huo ukiwa tayari umeshakuwa na athari kubwa.

Katika Hatua nyingine Mhe. Waziri Ummy amesikitishwa na kitendo cha Hospitali hiyo kukosa Dawa za kupunguza makali ya ugonjwa wa saratani kama vile damu,dripu ambapo wagonjwa hulazimika kutafuta huduma nje ya Hospitali hiyo tena kwa gharama kubwa ya Shilingi 800,000 wakati Sera ya Afya yaTaifa inasema huduma kwa wagonjwa wa Saratani hutolewa bure.

Kutokana na Ukosefu wa dawa hizo Waziri Ummy ameitaka Bohari kuu ya dawa (MSD) kuandaa maelezo kuhusu ukosefu wa Dawa za Saratani katika hospitali na waharakishe wanatafuta njia ya kupatikana kwa dawa hizo haraka ili wagonjwa Wapate huduma na kuwaagiza watendaji kuwashawishi wagonjwa na wananchi kwa ujumla kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ambao utawasaidia katika matibabu.

Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo ya Ocean Road Bw Hamisi Diyenga alitoa ufafanuzi kuhusu ukosefu wa dawa za kupunguza Makali ya ugonjwa wa Saratani kwamba umetokana na uhaba wa Bajeti,ukosefu wa Mashine za kutosha kwa ajii ya matibabu ya mionzi kwa wagonjwa kwakuwa silimia 90 ya wagonjwa wa Saratani wanatibiwa kwa mionzi.

Kaimu Mkurugenzi huyo amemueleza Waziri huyo wa Afya jitihada wanazozifanya kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wagonjwa kwamba wametenga shilingi Bilion 15 kwa ajili ya kununua mashine za kutoa huduma ya mionzi pamoja na kukarabati mashine ambazo zimeharibika.

“Huduma ya mionzi kwa wagonjwa wa Saratani ni muhimu sana katika kumpa nafuu hivyo tunalazimika kutoa kwa wale wanaohitaji huduma za dharura tuu” Alisema Mkurugenzi huyo.

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri aliwatembelea wagojwa waliolazwa,akakagua Mashine za mionzi pamoja na jengo linalojengwa kwa ajili ya kutoa huduma ya mionzi kwa wagonjwa wa Saratani ambapo huduma hiyo inapatikana hospitali ya Ocean Road pekee.

AMUUA MKE WAKE KISHA YEYE KUJINYONGA MBOZI MBEYA

$
0
0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi.


Na Mwandishi wetu,Mbeya,Jamiimojablog

Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanaume mmoja Mkazi wa kijiji cha Malolo Ndugu Chipunguli Mkisi (30) amemuua mke wake kwa kumkata panga kichwani kisha yeye mwenyewe kujiua kwa kujinyonga.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ndugu Ahmed Msangi amesema tukio hilo la aina yake limetokea Desemba 15 mwaka huu majira ya saa 7 mchana huko katika kijiji cha Malolo, Kata ya Msia, wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Mbeya.

Msangi amemtaja mwanamke huyo kuwa ni Neva Mwaweza (24) Mkazi wa Malolo ambaye ameuwawa na mumewe kwa kukatwa panga kichwani .

Kamanda Msangi amesema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi baada ya mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

inadaiwa kuwa baada ya tukio, mtuhumiwa alijinyonga kwa kutumia kamba kwenye mti umbali wa mita 100 kutoka nyumbani kwake.

Aidha mwili wa marehemu [mwanaume] ulikutwa ukiwa na majeraha kwenye vidole na kando kukiwa na panga na alikutwa na ujumbe uliokuwa na maneno “kuwa ameamua kumuua mke wake na yeye kujinyonga kutokana na mke wake kuwa na mahusiana ya kimapenzi na mwanaume mwingine aitwae kilasi nzowa”

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya vwawa. ambapo kwa mujibu Kamanda Msangi uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LAUNGANA NA COGNIZANT KUBORESHA HUDUMA KWA WAGENI WAKE DUNIANI.

$
0
0
SHIRIKA la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa za Falme za kiarabu na Cognizant (NSADAQ: CTSH), shirika linaloongoza kwa huduma za teknolojia ya habari, ushauri na biashara, leo wametangaza makubaliano ya kimkakati yatakayoendesha mabadiliko ya kidijitali pande zote za shirika hilo pamoja na washirika wake.


Chini ya mpango wao wa miaka mitatu wenye thamani ya mamilioni ya madola, Cognizant watawasaidia Etihad kufafanua mkakati wao wakidigitali na kutengeza dhana mpya ambayo itatumika katika kutoa huduma bora kwa wageni wao watakaosafiri popote na ndege za Etihad.

Kwa kuleta pamoja mikakati ya kidijitali, teknolojia, sekta na uzoefu wa ubunifu, Cognizant watafanya utafiti wa hali ya sasa ya biashara na teknolojia ya shirika la ndege la Etihad na kutumia utafiti huo kutengeneza mazingira ya kidijitali ya kiwango cha hali ya juu, itakachowezesha usambazaji kupitia idhaa nyingi, ugawaji wa wateja kwa kina zaidi na kubinafsisha ujuzi katika masoko.

Kwa kutumia taarifa mbalimbali na ufahamu wa mteja, Cognizant italiwezesha shirika la ndege la Etihad na washirika wake, kuelewa zaidi mahitaji ya wageni wake.

Kwa kuunganisha tafiti hizi na mazoea bora, michakato na teknolojia, shirika hilo litawapa wageni wake suluhisho, ofa zitakazoendana na kila mteja kwa mapenzi yake na itaboresha huduma zinazotolewa katika safari nzima kutokana na hali ya uaminifu wao na upendeleo wa mteja kama vile bidhaa na huduma, kuchagua wapendapo kukaa wakati wa safari, chaguo la mlo, safari kipindi cha sikukuu na kadhalika. Kwa shirika hili, hii inamaanisha kufungua mitiririko mipya ya mapato, kuongeza chapa na kutengeneza fursa nyingine za kibiashara.

Afisa Mkuu wa Biashara wa shirika la Etihad Peter Baumgartner, alisema, “Wageni wetu wamezidi kugeukia idhaa za kidijitali zaidi kujiunga nasi na hivyo tunatambua umuhimu wa kuwafikishia ubora wa kipekee na usio wa dosari katika sehemu zote tunazofikia. Ushirikiano wetu na Cognizant utatusaidia kufikia kiwango bora katika safari za kidijitali ambayo itawaburudisha wateja kuanzia kupanga safari hadi kununua tiketi, kwenye uwanja wa ndege na kwenye ndege, na itaboresha uaminifu wa wageni kwa kuwavutia na kuwashirikisha wageni katika njia mpya na za kisasa.”

Robert Webb ambae ni Afisa Mkuu Habari na Teknolojia wa shirika la Ndege la Etihad, alisema “Ushirikiano huu ni muhimu kwa mikakati yetu teknolojia na uvumbuzi ambayo hutuimarisha na washirika wetu katika kujipanga upya kuwapatia wageni wetu huduma bora katika safari zao ambayo inaendana wakati wa safari na tamati yake. Tumechagua Cognizant kwa sababu wanaongoza katika programu za kidijitali, uzoefu wa kidigitali kwenye huduma za usafiri, ukarimu na ushirikiano wa muda mrefu na shirika na pia ni viongozi katika dunia ya teknolojia.”

Afisa Mtendaji Mkuu wa Cognizant, Francisco D’Souza, alisema: “Tumefurahia kushirikiana na Etihad kutengeneza shirika la ndege lenye kuwapa kilicho bora wateja wake wakati wa safari zao kwa kutumia nguvu ya teknolojia ya kisasa. Kwa Cognizant, mfumo wa kidijitali’ inamaanisha kuwa na uwezo wa kuunganisha teknolojia, takwimu za kisayansi, vifaa, ubunifu na mikakati ya kibiashara kubadili mifumo na uzoefu.

 Ushiriki huu unaweka alama ya kuungana kwa mashirika mawili yenye kasi ya uongozi ambayo mikakati yao ya ukuaji inabebwa na uvumbuzi wa kidijitali. Timu ya kazi za kidijitali ya Cognizant inafurahia na kutegemea mengi kwa kusaidiana na shirika la ndege la Etihad pamoja na washirika wake ikiwemo kuleta udhibiti, urahisi na uwazi kwa msafiri wa kisasa. 

Muamko wa kidijitali utazidi kuimarisha shirika la Etihad katika kuwa na chapa yenye kiwango cha hali ya juu kwa kutoa huduma bora kwa wateja.

Kama sehemu ya ushirikiano huu, Cognizant itasimamia program za Etihad na kuziunganisha katika jukwaa jipya la kidijitali. Kituo cha ubora wa kidijitali itaanzishwa kuendesha uvumbuzi pamoja na washirika wakuu wa kiteknolojia wa Etihad.


TIGO YATOA DOLA 40,000 KUENDELEZA MIRADI YA WAJASIRIAMALI-JAMII

$
0
0

Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya dola za marekani 20,000 kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Bihage Edward kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam jana. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda (kushoto).
Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi cheti kwa kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Neema Shosho kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam jana. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda (kushoto).
Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya dola za marekani 20,000 kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Neema Shosho kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam jana. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda (kushoto).

Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitt (wa pili kulia) akikabidhi cheti kwa kwa mshindi wa shindano la Tigo Reach For Change, Bihage Edward kwenye hafla ya makabidhiano iliyofanyika Dar es Salaam jana. wanaoshuhudia ni Ofisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev (kulia) na Meneja Mkazi wa Reach For Change, Peter Nyanda (kushoto).


Dar es Salaam, -Kampuni ya Tigo ikishirikiana na shirika lisilokuwa la kiserikali la Reach for Change wametoa jumla ya dola 40,000 kwa washindi wawili wa shindano la ubunifu kwa wajasiriamali wanaotumia teknolojia ya kidijitali. Kila mshindi amepewa dola 20,000.


Shindano hilo ambalo ni la nne tangu lilipoanzishwa mwaka 2012, lina lengo la kuwawezesha wajasiriamali wanaobuni miradi ya teknolojia ya kidijitali inayosaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.


Washindi wa mwaka huu ni Neema Shosho ambaye kwa kupitia kampuni yake ya Afya Slices, amebuni mfumo wa teknolojia ya kidijitali unaotoa taarifa kuhusu lishe kwa watoto na Bihage Edward, aliyebuni mradi wa kutunza vifaa vya elimu kidijitali unaosaidia kutokomeza ajira kwa watoto na kusambaza taarifa kwa njia ya ujumbe mfupi kwa kutumia simu za mkononi na kutengeneza programu ya Mp3 mahsusi kwa kutoa uelewa kuhusu ajira kwa watoto kwa jamii nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Afisa Mkuu wa Biashara wa Tigo, Shavkat Berdiev alisema: “ni furaha kubwa kwetu kuwatangaza washindi wa mwaka huu wa shindano la ubunifu la Tigo Digital Change-Makers. Kwa muda wa miaka minne sasa shindano hili limewanufaisha zaidi ya watoto 10,000 nchini na tunaamini kuwa ongezeko la washindi wawili litaleta mabadiliko zaidi kwa watoto na kusaidia kuifanya Tanzania kuwa mahala pazuri pa kushi.


Berdiev alifafanua kwamba maisha ya kidijitali yanakuza teknolojia yenye mawazo ya kuleta mabadiliko endelevu. “Teknolojia ya kidijitali haibadilishi tu jinsi tunavyofanya biashara ila pia inasaidia kukuza biashara barani Afrika na vilevile kuleta mapinduzi ya jinsi ya kutatua matatizo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya kijamii kwa ujumla”, alisema Berdiev.

Huu ni mwaka wanne ambapo Tigo na shirika la Reach for Change wanazindua washindi wa shindano hili ambapo washindi huchujwa kutoka kwenye washindani vijana ambao wana mwamko wa kubuni miradi inayotumia ya kiditali ili kutatua matatizo mbalimbali ya vijana na watoto katika jamii ya Watanzania.Afisa Mkuu wa Biashara huyo alisifia kazi mbalimbali za washindi waliotangulia na kuwatia moyo wengine ili waendelee kubadilishana mawazo.

“Tumepata mafanikio makubwa sana katika kuwapa msukumo wajasiriali-jamii. Kwa sasa tunasasidia waleta mabadiliko saba ambao kati yao, watano wana miradi inayoshughulika na masuala ya kidijitali”. Kwa mfano, Carolyne Ekyariisma anafundisha masomo ya awali ya kompyuta ili kuwapa uwezo vijana wa kike wenye umri kati ya 10 na 18 ujuzi wa awali katika kutumia kompyuta na amefanikisha kuwapa ujuzi takribani wanafuzi 500 kwa mwaka 2014 pekee.

Mwingine ni Joan Avit ambaye amejikita katika kutoa elimu bora ya awali ya watoto kwa kuieneza kupitia njia ya michezo ya kidijitali inayojulikana kama Grapho Game Tanzania inayowasaidia watoto kujifunza kusoma kwa haraka na kwa makini na ameweza kuwasaidia watoto 900 kwa mwaka 2014 pekee kupitia mchezo huu. Naye Faraja Nyalandu anayeendesha mradi wa shule, alibuni maarifa ya elimu kudijitali ili kuwawezesha watoto na vijana kusoma kwa kupitia mtandao wa kompyuta na huduma za simu ya mkononi. Kwa kutumia nyenzo hizi aliweza kuwaweze sha zaidi ya watoto 7,300 mwaka 2014.


Vile vile, tunamuwezesha Thadei Msumanje ambaye amejikita katika kupunguza pengo lililopo kati ya watumiaji wa tehama mjini na vijijini ambapo ni watoto wachache tu wanao uwezo wa kutumia tehama mpaka sasa.

Kuna pia Leka Tingitana ambaye ni mtaalamu wa teknolojia; naye kabuni suluhisho la tatizo katika sekta ya afya ili kuinua mtandao wa wafanyakazi wa afya ambao wako mstari wa mbele katika kutoa huduma za afya kwa akina mama wajawazito”.


Balozi wa Sweden nchini Tanzania Bi. Katarina Rangnitt, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo aliahidi kutoa msaada na kuunga mkono juhudi za shindano hilo kupitia shirika la msaada la Swedish Development Cooperation Agency (SIDA), na kusema ataungana na Tigo ili kufanikisha shindano la kila mwaka la ubunifu wa miradi ya kidigitali unaofanywa na wajasiriamali-jamii wa kitanzania.


“Kwa miaka mingi sasa shirika la maendeleo la SIDA limekuwa mstari wa mbele kuunga mkono miradi mbalimbali ya maendeleo hapa Tanzania katika harakati za kupunguza umasikini uliokithiri miongoni mwa wananchi hasa vijana, watoto na akina mama”, alisema.

Alisema ya kwamba amefarijika mno kwamba sasa nchi yake itashirikiana na kampuni ya Tigo ambayo ni taasisi inayojituma kwa dhati katika kutekeleza malengo yake ya kuisaidia jamii hapa Tanzania kwa kubuni fursa mbalimbali za maendeleo ili kukusanya mawazo ya kuleta tija katika jamii ya watanzania.

Uongozi wa StarTimes waishukuru Serikali kwa ushirikiano mzuri inaowapa

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akimkaribisha ofisini kwake Makamu wa Rais wa Kampuni ya Star Times Tanzania Bi. Zuhura Hanif leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akielezea jambo wakati wa mazungumzo baina yake na uongozi wa Star Times waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang na Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue
 Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue afafanua jambo wakati wa mazungumzo baina ya wawakilishi wa  StarTimes na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (kulia) leo jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofangakielezea jambo wakati wa mazungumzo baina ya wawakilishi wa StarTimes na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya Kadi ya Krismasi aliyokabidhiwa kwa niaba ya uongozi wa StarTimes Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang. Katikati ni Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel akishukuru mara baada ya kupokea zawadi ya Kadi ya Krismasi aliyokabidhiwa kwa niaba ya uongozi wa StarTimes Tanzania na Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang (kushoto). Katikati ni Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel(mwenye tai) akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa StarTimes kwa kumtembelea ofisini kwake na kuipongeza Serikali kwa ushirikiano inaowapa katika kutekeleza wajibu wao kama wabia wa habari hapa nchini.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Bw. Assah Mwambene,Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang,Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania Bi. Zuhura Hanif
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel(katikati)akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa StarTimes Tanzania walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari –MAELEZO Bw. Assah Mwambene,Makamu wa Rais wa StarTimes Africa Bw. Eric Xue, Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. LEO Liofang na Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania Bi. Zuhura Hanif
Picha na Frank Shija,
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WHUSM

BANKI YA BARCLAYS WAZINDUA OFISI MPYA JIJINI DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Ramadhani Dau akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ofisi mpya kwenye ghorofa ya pili ya jengo la benki hiyo lililopo jengo la Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akiwa na baadhi ya wadau wa benki hiyo wakati wa kuzindua ofisi ya benki hiyo ghorofa ya pili ya benki hiyo.
Mwenyekiti wa bodi wa Benki ya Barclays hapa nchini, Ramadhani Dau  akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa ofisi ya benki hiyo  katika jengo la benki ya Barclays ghorofa ya pili leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akishuhudia wakati akifungua kitambaa hicho.
Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina akizungumza na wafanyakazi wa benki ya Barclays hapa nchini (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam.

 Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Barclays hapa nchini wakimsikiliza Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina.

Baadhi ya wanabodi ya benki ya Barclays wakimsikiliza Mkurugenzi mkuu mtendaji wa benki ya Barclays Tanzania, Kihara Maina mara baada ya kuzindua ofisi mpya leo jijini Dar es Salaam. 

WACHEZAJI WAPYA WENYE ITC RUKSA KUTUMIKA

$
0
0
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya marekebisho ya kanuni za usajili ambapo sasa mchezaji ambaye usajili wake utakuwa umepita kwenye mfumo wa mtandao wa Transfer Matching System (TMS) atapewa leseni na kuitumikia moja kwa moja timu yake mpya.

TFF itatoa leseni ya usajili wa mchezaji ambaye amethibitishwa kupitia mtandao wa TMS baada ya kuwepo nyaraka zote; mkataba uliomalizika, barua ya kuvunja mkataba, barua ya kuachwa (release letter), mkataba mpya na uthibitisho wa makubaliano kati ya klabu zinazohusika.

Licha ya mchezaji kupata leseni, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji bado itakuwa na mamlaka ya kushughulia upungufu, malalamiko ya kiusajili, pingamizi na uhalali wa kimkataba kati ya pande mbili (mchezaji na klabu).

Wachezaji wote wa kigeni waliosajiliwa kwa ajili ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) wanapaswa kulipiwa dola za kimarekani U$ 2,000 kwa kila mmoja kabla ya kupatiwa leseni na kuanza kuzitumikia klabu zao katika michuano ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho.

Pia TFF kupitia kamati ya sheria na hadhi za wachezaji inaweza kumruhusu kwa kipindi maalum mchezaji mwenye dosari acheze kwa leseni ya muda (provisional license) hadi dosari hizo kati ya klabu na klabu zitakapomalizwa. Iwapo dosari hizo hazitakuwa zimemalizwa, mchezaji anaweza kuzuiwa kucheza na klabu husika kuadhibiwa.


Timu zote za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili zinatakiwa kufuatilia TFF kujua wachezaji ambao hawana pingamizi na leseni za wachezaji waliopitishwa wanaweza kuanza kutumika kuanzia kesho tarehe 18/12/2015 na kwenye michezo ya kombe la Shirikisho (FA Cup) kama hawakuwa wamecheza raundi ya kwanza kwenye vilabu vya zamani.

WAZIRI MHONGO ATOA MWEZI MMOJA KWA TANESCO.


BOMOA BOMOA YATIKISA TENA WAKAZI WA BONDE LA MTO MSIMBAZI JIJINI DAR LEO.

$
0
0
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Manispaa za jiji la Dar es salaam zitafanya zoezi la kuondoa wavamizi maeneo yote ya Mabondeni, kingo za mito  na za Bahari, maeneo ya wazi, maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi zaidi ya 150 katika  jiji la Dar es salaam. Bomoa bomoa ya leo inaendelea katika Bonde la mto msimbazi.Mkuu wa Kitengo cha Sheria Balaza la Taifa la usimamizi wa mazingira Tanzania (NEMC), Manchale Heche akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juu ya zoezi la Bomoabomoa maeneo ya miundombinu na maeneo yote hatarishi nakuwataka wananchi waliojenga katika fukwe za bahari Kingo za mito na mikondo ya bahari kuhamisha mali zao mapema.
Wananchi wakitoa samani pamoja na vitu mbalimbali ndani ya nyumba zao ili kupisha ubomoaji wa nyumba zilizo maeneo hatarishi. 

Ubomoaji ukiendelea maeneo ya Mto msimbazi jijini Dar es Salaam. 
Wananchi pamoja na polisi (Wazee wa kazi) wakiangalia ubomoaji unavyoendelea bila vurugu.
Vijana wakiokota vitu mbalimbali katika maeneo yaliyobomolewa leo jijini Dar es Salaam. 

Wananchi wakiwa maeneo hatarishi ambayo yanasubiri kubomorewa. 
Uondoaji wa vyuma katika nyumba inayongoja kubomolewa. 

 Wazee wa kazi wakihakikisha usalama wa eneo ya ubomoaji. 
 Vitu mbalimbali vikiwa vimetolewa nje ili kupisha ubomoaji wa nyumba.

MREFA YAANDAA KOZI YA LESENI C

$
0
0
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa kushirikiana na Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA) wameandaa kozi ya makocha wa mpira wa miguu Leseni C, itakayofanyika jijini Mbeya kuanzia Disemba 21- 04 Januari, 2016.


Jumla ya makocha 46 kutoka katika kanda ya Nyanda za Juu Kusini wanatazamiwa kushiriki kozi hiyo ya wiki mbili, ambayo itaendeshwa na wakufunzi Kidao Wilfred na Salum Madadi.

Washiriki wa kozi hiyo ni Mussa Kasalika, Steven Viera, Golya, Mlekwa, Matokeo Sigalla, Ernest Nkandi, Felix A. Sosteness, Michael Mwamaja, Daniel Mwaisabila, Deus Nsheka, Albert Gama, Joseph Abiero, Simon Mwapili, Bahati Mwaipopo, Willy Ngailo, Charles Makwaza, Paul Msyahila, Osward Morris, Jacob Ndago, Castor Mahona, Ambilikile Albion, Jumanne Nsunye, Gowdin Mulenga.


Wengine ni Abel Shizya, Matatizo Abdallah, Michael Kasekenya, Thomas Kasombwe, James Wanyato, Rose Njobelo, Amos Chiwaya, Baraka Kibanga, Mohamed Dondo, Josephat Digna, Shabani Mwaibara, Lucas Kibaja, Yusuph Mlekwa, Joel Makitta, Josiah Steven, Rashid Kasiga, Charles Njango, Alex Lusekelo, Shabani Kazumba, Ismail Suleiman, Ibrahim Kasegese, Simon Bernard, Anthony Mwamlima, Christian Simkoko.

MHAGAMA; alitaka SHIVYAWATA kuondoa tofauti zao

$
0
0

44
Mkalimani wa lugha ya alama akifafanua mazungumzo kwa alama kwa baadhi ya wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wakati wa  mkutano wa shirikisho hilo na Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi (hayupo pichani), jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
43
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), (katikati) akimsikiliza  Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), Amon Mpanju wakati shirikisho hilo  lilipo kutana na Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi (wa kwanza kushoto), jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam, (wa tatu kulia), Naibu Katibu Mkuu Ofisi  ya Waziri Mkuu, Bibi. Regina Kikuli.
46
Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi, akiteta  jambo na mmoja wa wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) mara baada ya kukutana na wajumbe wa shirikisho hilo  jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
45
Baadhi ya wajumbe wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) wakifuatilia mazungumzo ya mkutano huo, wakati wa  mkutano wa shirikisho hilo na Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Dk. Abdalla Possi, jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………………….WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia, (Sera,Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), amelitaka Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) kuondoa tofauti zao ili kuweza kushirikiana na serikali ya awamu ya tano ambayo imedhamiria kuimarisha na kulinda haki za watu wenye ulemavu.
 “Mnapaswa kuhakikisha kuwa wale wote wanaoleta tofauti zenu kuwashughulikieni mapema katika vikao vyenu ili muweze kushirikiana na sisi katika kuhakikisha mnapata haki ya kulindwa , kuheshimiwa na usalama. Tunataka nchi yetu baada ya miaka mitano iwe katika historia nzuri kwa kuwajali watu wenye ulemavu”. Amesema.
 Ametoa wito huo wakati akizungumza na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) jana jioni (Jumatano, Desemba 16, 2015), katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Jijini Dar es Salaam.
 Bibi Mhagama alisema: “Tunapaswa tusimuangushe Rais Magufuli kwa imani aliyoionesha kwenu na kuteua Naibu waziri anayeshughulikia masuala yanayowahusu ambayo yanaratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu,” alisema.Awali akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa shirikisho hilo, Amon Mpanju pamoja na kumshukuru Waziri na Naibu Waziri anayeshughulikia (Watu wenye ulemavu) kwa kuitisha mkutano uliolenga kujadili vipaumbele vya watu wenye ulemavu nchini pamoja na nchi zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi alimuomba waziri huyo kuhairisha ili waweze kukamilisha uaiinishaji changamoto zao vizuri.
 “Tunaomba mheshimiwa waziri utupatie muda zaidi tuweze ili tuweze kuainisha vizuri zaidi changamoto zetu ambazo naamini Naibu waziri mwenye dhamana ya kushughulikia watu wenye ulemavu amabye pia tunaimani naye sana ataweza kubaini masuala yanayotuhusu na kuweza kuyatekeleza katika majukumu yake” alisema.
 Mkutano huo uliandaliwa na Naibu Waziri anayeshughulikia watu wenye Ulemavu Dk. Abdalla Possi, pia ulihudhuliwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu aliye wakilishwa na Naibu wake, Bibi. Regina Kikuli na Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu, Obey Assery.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto yatangaza Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Donan Mmbando  akieleza kuhusu Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya Waandishi wa Habari leo 17 Desemba, 2015.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Donan Mmbando akionyesha aina ya dawa zinazotakiwa kugawiwa kwa umma wakati alipotangaza Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele mbele ya Waandishi wa Habari leo 17 Desemba, 2015.




Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya kutangazwa kwa Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele iliyotolewa leo 17 Desemba, 2015 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
(Picha zote na Benedict Liwenga)


Na Shamimu Nyaki.
 
Serikali  kupitia Mpango wa  wa Taifa wa kudhibiti Magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo   imetangaza tarehe 19 hadi 23 mwezi huu kuwa itaanza zoezi la kugawa dawa kwa makundi yanayopaswa kupata dawa za magojwa hayo. 

 Tamko  hilo  limetolewa  na Katibu mkuu wa Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wazee,na Watoto  Bw. Donald  Mmbando   alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Magonjwa  ambayo hayapewi kipaumbele  ni Usubi,Vikope (Trakoma), Matende, Mabusha,Ngiri maji, na Minyoo ya tumbo  hivyo dawa hizo zitasaidia kupunguza tatizo.

Ameongeza kuwa zoezi hilo la ugawaji wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya Afya, Zahanati,Hospitali, shule za msingi na sekondari,sokoni,vituo vya usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali na Mashirika ya Umma na hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi  kupata huduma hiyo ambayo haina malipo yoyote.

Katibu Mkuu huyo  amesema  kuwa wahusika wakuu katika kupatiwa dawa hizo ni Watu wote kuanzia miaka mitano na kuendelea,isipokuwa watoto chini ya miaka mitano,wajawazito, mama    anaenyonyesha mtoto chini ya siku saba na Wagonjwa Mahututi.

“Tunataka kulinda afya zao na Uhai wao hivyo tunaomba wafuate maelekezo vizuri”.Alisema Bw Mmbando.

Aidha zoezi hilo litatekelezwa  katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma,Mtwara, Lindi na Pwani kwa ajili ya kujikinga  na kutibu  magonjwa hayo na Mikoa mingine iliyobaki  itafanya zoezi hilo  katika  ngazi ya  jamii na shuleni mwishoni mwa mwezi Januari kuendelea hadi Februari 2016.

Naye Mratibu wa Mpango  huo Dkt  Edward kirumbi ameeleza kuwa takwimu zainaonyesha kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele hapa nchini ni kubwa ambapo ugonjwa wa Usubi umeenea zaidi katika mikoa sita ikiongozwa na Dodoma, Ugonjwa wa Minyoo ya tumbo wagonjwa million 13, kichocho ,Matende na Mabusha tathmini za awali zinaonyesha mikoa 18  imeathirika kwa kuwa na wagonjwa million 12.

 Vile vile Dkt  Kirumbi ameeleza kuwa Magonjwa haya yamekuwa na athari kubwa hasa kwa kuathiri nguvu kazi ya Taifa hivyo wananchi wanapaswa kupata dawa hizo ambazo zitakuwa zinatelewa kwa mwaka mara moja  ili kukinga upungufu wa Damu, kuuwa vimelea vya ugonjwa huo, kupungua kwa magonjwa ya ngozi, na kuongeza virutubisho bora mwilini.

Hata hivyo jamii inapaswa kupewa elimu zaidi kuhusu Magonjwa haya kwa vile bado haijaelewa athari za magonjwa haya kwa  kiasi kikubwa hasa kwa maeneo ya vijijini ambayo ndio waathirika wakubwa.

Wauzao vyakula kiholela kupelekwa Mahakamani

$
0
0



Na Skolastika Tweneshe MAELEZO

Wafanyabiashara wameaswa kutoendelea na uuzaji wa vyakula na matunda yaliyomenywa katika maeneo yaliyo wazi na yoyote atakayeendelea kuuza atachukuliwa hatua kali za kisheria hii ni kutokana na kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Msemaji wa Manispaa ya Ilala Bw. David Langa alipozungumza na mwandishi kuhusu tamko la Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu kupiga marufuku uuzwaji wa vyakula au matunda yaliyomenywa katika maeneo ya wazi.

“Kwa mfanyabiashara yoyote tutakayemkamata tutamfikisha mahakamani na adhabu yake ni faini ya sh 30,000 au kwenda jela miezi mitatu au vyote kwa pamoja.” alisema Langa.

Aidha Bw. David Langa amesema katika ukutekelezaji wa suala hili watendaji wa kata wanahusika moja kwa moja kusimamia na kufuatilia kwa karibu operesheni hii, na kusisitiza sheria za Afya kuzingatiwa na kutokuwa na huruma kwa yeyote atakayevunja sheria.

Kumekuwa na uuzwaji wa vyakula na matunda yaliyomenywa jijini Dar es salaam hasa maeneo ya katikati ya jiji hivyo kuhatarisha afya za wananchi, ila Serikali kupitia halmashauri zake imeahidi kulitilia mkazo suala hili.

Huduma ya kugawa Dawa za Matende na Mabusha kuanza Disemba 19 Dar.

$
0
0
Na Shamimu Nyaki-Maelezo.

Serikali  kupitia Mpango waTaifa wa kudhibiti Magonjwa yasiyopewa kipaumbele leo   imetangaza tarehe 19 hadi 23 mwezi huu kuwa itaanza zoezi la kugawa dawa kwa makundi yanayopaswa kupata dawa za magojwa hayo.

 Tamko  hilo  limetolewa  na Katibu mkuu wa Wizara Ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wazee,na Watoto  Bw. Donald  Mmbando   alipokuwa anazungumza na waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kusema kuwa Magonjwa  ambayo hayapewi kipaumbele  ni Usubi,Vikope (Trakoma), Matende, Mabusha,Ngiri maji, na Minyoo ya tumbo  hivyo dawa hizo zitasaidia kupunguza tatizo.

Ameongeza kuwa zoezi hilo la ugawaji wa dawa litatekelezwa katika vituo vyote vya Afya, Zahanati,Hospitali, shule za msingi na sekondari,sokoni,vituo vya usafiri,pamoja na Ofisi za Serikali na Mashirika ya Umma na hivyo wananchi wanaombwa kujitokeza kwa wingi  kupata huduma hiyo ambayo haina malipo yoyote.

Katibu Mkuu huyo  amesema  kuwa wahusika wakuu katika kupatiwa dawa hizo ni Watu wote kuanzia miaka mitano na kuendelea,isipokuwa watoto chini ya miaka mitano,wajawazito, mama    anaenyonyesha mtoto chini ya siku saba na Wagonjwa Mahututi.“Tunataka kulinda afya zao na Uhai wao hivyo tunaomba wafuate maelekezo vizuri”.Alisema Bw Mmbando.

Aidha zoezi hilo litatekelezwa  katika mikoa ya Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma,Mtwara, Lindi na Pwani kwa ajili ya kujikinga  na kutibu  magonjwa hayo na Mikoa mingine iliyobaki  itafanya zoezi hilo  katika  ngazi ya  jamii na shuleni mwishoni mwa mwezi Januari kuendelea hadi Februari 2016.

Naye Mratibu wa Mpango  huo Dkt  Edward kirumbi ameeleza kuwa takwimu zainaonyesha kuwa magonjwa yasiyopewa kipaumbele hapa nchini ni kubwa ambapo ugonjwa wa Usubi umeenea zaidi katika mikoa sita ikiongozwa na Dodoma, Ugonjwa wa Minyoo ya tumbo wagonjwa million 13, kichocho ,Matende na Mabusha tathmini za awali zinaonyesha mikoa 18  imeathirika kwa kuwa na wagonjwa million 12.

 Vile vile Dkt  Kirumbi ameeleza kuwa Magonjwa haya yamekuwa na athari kubwa hasa kwa kuathiri nguvu kazi ya Taifa hivyo wananchi wanapaswa kupata dawa hizo ambazo zitakuwa zinatelewa kwa mwaka mara moja  ili kukinga upungufu wa Damu, kuuwa vimelea vya ugonjwa huo, kupungua kwa magonjwa ya ngozi, na kuongeza virutubisho bora mwilini.

Hata hivyo jamii inapaswa kupewa elimu zaidi kuhusu Magonjwa haya kwa vile bado haijaelewa athari za magonjwa haya kwa  kiasi kikubwa hasa kwa maeneo ya vijijini ambayo ndio waathirika wakubwa.

WATANZANIA WANNE WAPATA TUZO ZA UANDISHI WA FASIHI YA KISWAHILI AFRIKA

$
0
0
Afisa Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani)jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwandishi wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi na Mwandishi wa Ushairi la Kifaurongo, Christopher Budebah.
Mkuu wa Idara ya Fasihi ya Mawasiliano na Uchapishaji (TATAKI) WA wa chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwa na baadhi ya viongozi ya ALAF Limited. 
Mshiriki wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei  akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Mwandishi wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi akipokea ua kutoka kwa Meneja Huduma na Masooko Alaf ,Piyush Kanti Nath leo wakati wa kuwapongeza washindi wa uanishi wa fasihi za kiswahili Afrika.
Mwandishi wa kitabu cha Kolonia Santita, Enock Maregesi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusiana na tuzo aliyoipata katika uandishi wa wa kitabu cha Kolonia ya Santita.
Mwandishi wa Ushairi la Kifaurongo, Christopher Budebah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

KWA mara ya kwanza Lugha ya Kiswahili imeingia katika rekodi ya dunia kwa watanzania wanne kuchomoza katika tuzo ya waandishi ya Fasihi Afrika. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mshiriki wa Taaluma ya Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian Mtembei amesema lugha ya Kiswahili ya kujivunia kutokana na watanzania wenye lugha yao kuwa washindi.

Washindi wa tuzo hizo ni Enock Maregesi ambaye aliandika Kolonia Santita,Chiristophee Bubebah, Anna Manyaza aliandika Penzi la Damu, Mohamed Ghassani aliandika N’na Kwetu.

Walioshiriki katika tuzo hiyo walikuwa 65 na kuweza kuibuka watu wanne ambao ni washindi wakitokea nchini na sherehe hizo zilifanyika Nchini Kenya.

Amesema kwa lugha ya kifaransa na Kiingereza zimekuwa zikijitokeza kila mwaka kwa watu kuandika riwaya na mashairi lakini Kiswahili imekuwa ikisahaulika hivyo na kufanya Chuo Cornell Nchini Marekani iliamua kufanya hivyo kuwa watu kuandika Riwaya na Mashairi.

Katika tuzo hizo Kampuni ya watengenezaji wa Mabati ya Alaf ilizamini tuzo hizo na kutaka watu wajitokeze katika kuinua lugha ya Kiswahili duniani.



Afisa Masoko wa Alaf, Theresia Mmasy amesema kazi wataendelea kushirikiana na watanzania katika kukuza Kiswahili katika kudhamini tuzo hizo.

JAJI MARK BOMANI AMSHAURI MAALIM SEIF AKUBALI UCHAGUZI URUDIWE

$
0
0
Jaji  Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii 
JAJI Mkuu na Mwanasheria Mkuu Mstaafu, Mark Boman amesema kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja Zanzibar, Maalim Seif Hamad akubali uchaguzi urudiwe Zanzibar kwani kama alishinda atashinda tena kutokana na waliompigia katika uchaguzi ulifutwa watampIgia kura tena.

Boman ameyasema hayo leo jijini Dar eS Salaam , wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa Maalim kujitangazia kuwa ameshinda ni suala ambalo halikufuata utaratibu hivyo kutokana na mazingira hayo uchaguzi ufanyike ili kupata Rais wa Serikali ya Zanzibar.

“Kurudia uchaguzi Zanzibar ni jambo lisilo epukika lakini wakae na kuangalia dosari zilizojitokeza na kufuta uchaguzi lazima lishughukiwe kisheria bila kufanya hivyo kunaweza kuleta matatizo”amesema Jaji Mstaafu, Boman.

Amesema kuwa uchaguzi uliofanyika Zanzibar walitakiwa kukaa na kuona wapi walikosea katika kuondoa changamoto hizo ambapo ilikuwa ngumu kutokana na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha na wajumbe walishindwa kuafikiana.

Hata hivyo Boman ametaka suala la katiba lazima lishughulikiwe kuacha kwake ni aibu ya nchi kutokana na mabilioni ya fedha yametumika katika mchakato huo.


Amesema kuwa migogoro inayotokea ya ardhi na wafugaji pamoja wakulima inatokana na kutokuwa na katiba ambayo ndio ingekuwa suluhu ya utatuzi wa migogoro hiyo.

KAMATI YA URATIBU YA SHIRIKISHO LA VYUO ELIMU YA JUU YAANZA VIKAO VYA SIKU MBILI

$
0
0

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akiongoza kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akiongoza kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu, kulia ni Katibu Mtendaji Ally S. Hapi

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu Zainab Abdallah (MNEC) akijadiliana jambo pamoja na Daniel Zenda (katikati) na Ally S. Hapi wakati wa kikao cha Kamati ya Uratibu Taifa ya la Vyuo vya Elimu ya juu.
Wajumbe wa kikao wakichambua mambo mbali mbali.

Kamati ya Uratibu taifa ya Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu leo imeanza kikao cha siku mbili kinachofanyika makao makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es salaamchini ya Mwenyekiti wake bi Zainab Abdallah(Mnec). Viongozi wengine wanaohudhuria kikao hicho ni Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho Ndg. Hamid Mhina (Mnec), Katibu Mtendaji Ally S. Hapi, Katibu mtendaji Daniel Zenda, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa kutoka Shirikisho Joseph Chitinka,Katibu uchumi na Fedha Richard Luhende, katibu wa siasa na uenezi Fikiri Mzome na katibu wa uhamasishaji Mganwa Nzota.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

25 kuibuka washindi katika droo ya tatu ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" ya GAPCO

$
0
0
Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa kampuni ya GAPCO Tanzania, Jane Mwita (kati) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta kuwatafuta washindi wa droo ya tatu ya promosheni ya "Jaza Mafuta na Ushinde" inayoendeshwa na Kampuni hiyo kwa Wateja wake wa jijini Dar es Salaam,ambapo zaidi ya wateja 20 huibuka kidedea kila wiki. Kulia anaeshuhudia ni Mkaguzi wa michezo ya kubahatisha nchini, Chiku Saleh na Kushoto ni Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania, Caroline Kakwezi.

MAENDELEO YANALETWA NA WANANCHI WENYEWE ENDAPO WATATAMBUA JINSI YA KUTUMIA LASILIMALI ZAO.

$
0
0
Haihitaji kuwa na akili sana ili kuiona tofauti ya maisha kati ya miji iliyoendelea na vijijini. Hapa nazungumzia ushirikiano wa wakazi wa maeneo hayo mawili na viongozi wao wa serikali hasa kuanzia ngazi ya mtaa na kata.
Majadiliano yakiwa yanaendelea

Wakazi wengi wa mijini huwa wanabanwa na shughuli mbalimbali za kujitafutia kipato kiasi kwamba hukosa hata nafasi ya kuwafahamu viongozi wa serikali ya mtaa wao. Aina hii ya maisha hupelekea kuzaliwa kwa tabia mbaya zaidi, nayo ni kukosa muda wa kuhudhuria mikutano muhimu inavyofanyika katika mitaa yao.
Hali hii ni tofauti kwa vijijini ambapo wananchi wengi mwenendo wa maisha yao ya kila siku kutoka kwa viongozi wao kuanzia ngazi ya kijiji, kitongoji na kata. Kutokana na aina hii ya maisha inawafanya wawe na umoja, kuishi kwa ushirikiano na kufanya maamuzi kwa pamoja hasa juu ya rasilimali zao.
Katika miaka ya hivi karibuni wanakijiji wengi wanaoishi katika maeneo yenye rasilimali wametambua umuhimu wa kutunza na kutumia rasilimali zao vizuri kwa maendeleo yao na kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Lakini si kila sehemu hali ipo hivyo katika baadhi ya maeneo wanakijiji wamekuwa hawazitambui haki zao za msingi kutokana na uelewa mdogo.
Mwalimu kaziro Nyangisa akisoma moja ya mikataba
Mwime ni kijiji kilichopo katika kata ya Mwendakulima wilayani Kahama, mkoani Shinyanga. Wakazi wengi wa kijiji hiki ni wakulima wadogo wadogo, wafugaji na ni wachimbaji wa madini. 
Kijiji hiki ndicho kilichohifadhi mgodi maarufu wa dhahabu wa Buzwagi, uliochangia kwa kiasi kikubwa kupanda kwa hadhi ya kijiji hicho na kuwa mtaa. Hivyo kwa sasa Mwime ipo kwenye halmashauri ya mji kutokana na upatikanaji wa huduma muhimu karibia zote kuanzia huduma za afya, barabara, umeme na maji safi.
Awali kijiji cha Mwime kilikuwa kikimiliki leseni mbili za machimbo ya uchimbaji dhahabu ya Majimaji na Zanzibar. Wachimbaji wadogo wadogo walikuwa ndio walengwa wakubwa, ambapo walilipa ushuru kwa serikali ya kijiji. Na wao kunufaika na shughuli hizo ambazo zilikuwa zinawaingizia kipato.  
Uraghbishi umesaidia kupata Barabara nzuri
Ilipofika mwaka 2007 kampuni ya Pangea ilipata leseni ya kufanya utafiti na mwisho wa siku kuingia mkataba na serikali ya kijiji cha Mwime. Katika kipindi ambacho uwekezaji ulikuwa unafanywa katika eneo hilo ambalo sasa ni mgodi wa Buzwagi, kijiji kililipwa kiasi cha shilingi za kitanzania 12,000,000 kwa mwaka ikiwa kama malipo ya kusitisha uchimbaji katika eneo hilo.
Uraghbishi umesaidia kuleta umeme katika mtaa wa Mwime
Miaka miwili baadaye yaani mwaka 2009, ndipo kijiji kilipokabidhi rasmi leseni zake kwa kamishina wa madini na kuingia mkataba na Pangea (Barrick). Kwa mujibu wa kifungu namba 1.1 cha Makubaliano ya Nyongeza ya Mkataba baina ya Kampuni ya Madini ya Pangea (Barrick) na Kijiji cha Mwime; kampuni itakuwa ikikilipa kijiji kiasi cha Tsh milioni 60/- kila mwaka kwa kipindi cha miaka mitano na kisha pande mbili hizi zitakaa pamoja na kupitia kiwango hiki kwa kadri ya uzalishaji utakavyokuwa kwa nia ya kuboresha zaidi.
Hizi ni Nyumba mbili zilizojengwa kwa ajili ya walimu
Malipo haya yalitakiwa kuanza kulipwa kuanzia mwaka 2009 miaka miwili baada ya makubaliano kusainiwa tarehe 21 mwezi Aprili mwaka 2007. Ni mwaka 2012 malipo haya yamelipwa kwenye akaunti ya kijiji, kiasi hicho cha shilingi milioni 300/- ni malipo ya miaka mitano ya awamu ya kwanza; mkataba unatamka kila baada ya miaka 5 pande mbili (Kijiji na Mgodi) zitakaa kupitia kiwango hiki ili kuboresha kiwango hiki kutegemeana na uzalishaji.

Malipo haya yanafanyika, baada ya juhudi kubwa kufanywa na wananchi wa kijiji cha Mwime na viongozi wao katika kufuatilia fedha hizo. Na tatizo halikuwa upande wa mgodi wa Buzwagi, bali ni wananchi wa kijiji cha Mwime wenyewe kushindwa kuhimiza uongozi wao kuchukua hatua za kufuatilia suala hilo. Na hivyo kupita miaka miwili bila kitu chochote kufanyika kuanzia 2009 hadi 2011.
Hizi ni nyumba mbili  ambazo zimejengwa kwa ajili ya wauguzi

Kwa mujibu wa kifungu cha 1.2 cha Nyongeza ya Mkataba wa Makubaliano, fedha zitakuwa zinalipwa kupitia Bodi ya Wadhamini, ambayo inaundwa na wawakilishi wa kijiji, mgodi na serikali ngazi ya wilaya kama msimamizi.

“Lilitolewa tangazo kwa ajili ya watu kuomba nafasi ya kuwa wawakilishi wa kijiji kwenye Bodi, ila waliotakiwa ni wale walio chini ya miaka 60 na waliomaliza kidato cha nne. Nilipata hisia kwamba tangazo limebagua baadhi yetu wenye uwezo ila hatuna sifa walizozitaja,” anaelezea Maimuna Said mmoja wa waraghabishi wa kijiji hiko.

Wanakijiji wa Mwime pia wanafanya shughuli za kilimo na ufugaji
Hivyo wakati wa mkutano wa kijiji mwaka 2011 wanakijiji walitaka maelezo ya ziada kuhusu uundwaji wa Bodi ya Wadhamini pamoja na majukumu yake. Ndipo ilipojulikana kwamba tayari kuna watu wameshaomba nafasi hiyo na tayari wameshachanguliwa na zaidi Bodi hiyo ina mamlaka ya mwisho ya kuamua matumizi ya fedha itakazolipwa kijiji.
Uraghbishi huo ulipelekea kamati iliyokuwepo kuvunjwa na wanakijiji walioamua kuchagua viongozi wao wanaowataka na kupelekea kupata malipo yao vizuri na kufanyia maendeleo ya kijiji. Jitihada hizo zilimvutia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Lembeli kuchangia fedha kwa ajili ya kufungua akaunti ya kijiji ya maendeleo.
Sehemu ya fedha hizo (milioni 300/-) zilitumika katika kufungua miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na Tsh 78,000,000 kutumika kujenga nyumba mbili za kuishi wauguzi, kuvuta umeme kijijini hapo na kujenga barabara huku Tsh 7,000,000 zikitumika kulipa fidia kwa watu waliokuwa na miti na makaburi sehemu ambayo barabara hiyo ilipita.Mbali na hayo Tsh 1,800,000 zilitumika kuwalipa posho wafanyakazi wote walioshiriki kufanya kazi hiyo, yote hayo yaliweza kufanikiwa kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na walaghabishi.
Mgodi umesaidia hata wanakijiji kuwa na vitega uchumi vyao wenyewe
Waraghbishi mwalimu Kaziro Nyaingisa na mkulima Maimuna Said, wakirishirikiana na wanakijiji cha Mwime kupitia kamati iliyochaguliwa kupigania mkataba mpya na kampuni ya Accacia iliyowekeza kwenye mgodi huo baada ya Barrick. Katika mkataba mpya wa mwaka 2015/2016 umeongezeka kwa asilimia 50% kutoka Tsh 60,000,000 kwa mwaka mpaka kufikia Tsh 90,000,000 ambapo mpaka sasa fedha hizo zimeshaingia kwenye kamati na zinaendelea kutatua matatizo ya kijiji.Kama hiyo haitoshi, Uraghbishi huo umewafanya wawekezaji wa mgodi wa Accacia kutoa ajira za utunzaji wa mazingira kwa wanawake ambao wanaishi jirani na mgodi, huku wakitengeneza matundu ya vyoo vya kisasa 16 kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi Mwime. Wameahidi pia kuongeza idadi ya visima vya pete na nyumba za walimu.
Kutokana na waraghbishi kupaza sauti zao imewasaidia wanakijiji hasa raia wa kawaida kuwa na uwezo mkubwa wa kujitambua, kujua haki zao na uhalisia katika jamii. Wametambua nini maana ya uzalendo, umuhimu wa ushirikiano, watu kuishi kwa amani, na kufanya kazi bila woga.
Kupitia uraghbishi wanawake wamekuwa sio waoga tena katika kijiji cha Mwime, hiyo imesababisha mpaka vijiji vingine kama Kilago na Nyandekwa. 

(Imeandaliwa na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa)

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo atembelea kijiji cha magozi na kukagua vyanzo vya maji mto Ruaha

$
0
0

ric1
Kijiji cha Magozi chenye wakulima zaidi ya 1000 wanaolima mpunga kwa kutumia kilimo cha  umwagiliaji ambao unasababisha bwawa la mtera kukosa maji kutoka mto Ruaha kwa sababu za kilimo cha umwagiliaji. Pamoja na wakulima Hawa pia wapo wakulima  wa Mbalali mkoa wa Mbeya ambao wote kutokana na shughuli hizo za kilimo husababisha ufuaji umeme kukwama katika bwawa la  Mtera na Kidatu  mkoani Morogoro.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo kushoto anayezungumza na Richard Kasesela Mkuu wa wilaya ya Iringa  alitembelea  bonde hilo na kukagua shughuli za kilimo zinazoendelea katika bonde hilo na kusababisha upotevu wa maji katika mto Ruaha ambao unapeleka maji katika mabwawa ya kufua umeme Mtera, Mkuu wa wilaya ya Iringa ameitisha mkutano wa wadau wote  siku ya jumatatu tarehe  21 mwezi huu . ili kufanya majadiliano na kupanga mkakati wa Kuokoa bwawa la mtera.
ric2
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo akikagua eneo hilo na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela leo.
ric3
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo akizungumza na baadhi ya wakulima hao wakati alipokagua bonde hilo kulia anayemsikiliza ni Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela.
ric4
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mwijarubi Muhongo akizungumza na mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela wakati alipotembelea bonde la Usangu lenye shughuli za kilimo cha Umwagiliaji.
ric5
Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela akimwelezea jambo waziri wa Nishati na Madini wakati alipokagua bonde la Usangu katika kijiji cha Magozi chenye wakulima wa mpunga zaidi ya 1000.
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images