Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

Wakorintho wapili kuzindua Mchepuko sio dili Tamasha la Krismasi

$
0
0
KWAYA ya Wakorintho Wapili ya Wilayani Mafinga mkoani Iringa inatarajia kuzindua albamu yake ya Mchepuko sio dili kwenye tamasha la Krismasi linalotarajia kufanyika Desemba 25 kwenye ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama albamu hiyo ina nyimbo nane ambazo zinafikisha ujumbe  wa neno la Mungu kwa jamii.Msama alizitaja nyimbo hizo ni pamoja na Tanzania, Mchepuko sio dili, Watenda mabaya, Ee bwana, Yahwe tunakuinua, Tuokoe baba, Dunia hii na Hana.

Aidha Msama alisema maandalizi ya kuelekea katika tamasha hilo yanaendelea vizuri, hivyo Watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kuelekea tamasha hilo.Aidha Msama alisema Watanzania walichukilie tamasha hilo kama sehemu ya kurudisha shukrani kwa Mungu baada ya kutupitisha katika kipindi kigumu cha uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika kwa amani na utulivu ingawa kulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani.

Msama alisema waimbaji wa Tanzania watakaosindikiza tamasha hilo ni pamoja na Rose Muhando, Upendo Nkobe, Joshua Mlelwa, Kwaya ya Wakorintho wapili.Wengine watakaopanda jukwaani siku hiyo ni Martha Mwaipaja, Jesca BM,  na Christopher Mwahangila, Sifael Mwabuka sambamba na Kwaya ya Yombo KKKT.

“Tumejipanga vilivyo na tamasha la Krismasi, hivyo tujiandae kupiga goti la kumrudishia Mungu Shukrani baada ya uchaguzi Mkuu ambao ulikuwa na mguso wa aina yake kutoka kwa vijana walioonesha kutaka maendeleo kutoka kwa serikali,” alisema Msama.

MAAFISA MAGEREZA NCHINI WAMETAKIWA KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil akihutubia kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza uliofanyika leo Desemba 16, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza,Ukonga jijini Dar es Salaam.
 Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza kutoka vituo mbalimbali hapa nchini wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kama wanavyoonekana.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akitoa maelezo ya awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza uliofanyika leo Desemba 16, 2015 katika Ukumbi wa Bwalo Kuu la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
 Meza Kuu wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza.




 Kamishna Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(wa kwanza kulia) akiteta pamoja na Makamishna wa Jeshi la Magereza kabla ya kumpokea mgeni rasmi(wa kwanza kulia) ni Naibu Kamishna wa Magereza Mstaafu, John Nyoka.

 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Mbarak Abdulwakil akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza (walisimama). Wa Pili tatu kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(wa tatu kulia) ni Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga(wa pili kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa(Picha zote na Lucas mboje wa Jeshi la Magereza).


Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.
MAAFISA wa Magereza nchini wametakiwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi kulingana na kauli mbiu ya Rais wa awamu ya tano, Dkt. John Magufuli.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, wakati akifungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza nchini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Mbarak Abdulwakil amesema kila kiongozi afanye kazi kwa bidii na maarifa ili utendaji wake ulete tija mahala pa kazi.

"Nadhani kila mmoja anafahamu kauli mbiu ya Mhe. Rais wa awamu ya tano ya "hapa kazi tu", na amekuwa akisisitiza kuwataka viongozi wenye dhamana na kila Mtanzania kufanya kazi kwa bidii na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani huu ni wakati wa kazi tu, " alisema.

Vile vile, Bw. Abdulwakil amewataka katika mkutano huo kujadili kwa kina mada maalum itakayowasilishwa na Kamishana Jenerali wa Magereza na kuweka mikakati ya kuongeza uzalishaji katika sekta za Kilimo, Mifugo na Viwanda.

"Kwa vile Jeshi la Magereza ni mdau mkubwa wa uzalishaji hasa katika sekta za Kilimo, Mifugo na Viwanda vidogo vidogo, nawaasa katika mkutano huu mjadili kwa kina na mapana hatimaye mtoke na mkakati wa namna mtakavyoongeza uzalishaji katika sekta hizo " alisema. 

Kwa upande wake, Kamishna Jenerali wa Magereza, John Minja amesema Jeshi la Magereza limejipanga vyema kutekeleza maelekezo mbalimbali ambayo yalitolewa na Rais wa Awamu ya tano, Mhe. John Magufuli ambayo ni pamoja na kuanzisha miradi ya kibiashara ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kuwahudumia wafungwa na mahabusu magerezani.

"Kuna mashamba 11 yametengwa ili kuzalisha kibiashara hivyo kuipunguzia Serikali mzigo na pia tumeainisha na miradi ya ufugaji" alisema Minja.

Kamishna Jenerali Minja amesema kuwa Jeshi hilo linakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwamo madeni ya Wazabuni, ukosefu wa Ofisi za Wakuu wa Magereza Mikoa, Migogoro ya Ardhi na wananchi wanaoishi jirani na vituo vya magereza pamoja na Msongamano wa wafungwa magerezani. 

Mkutano huu ni wa kwanza kufanyika tangu Uongozi wa Serikali ya awamu ya tano uingie Madarakani chini ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli mapema mwanzoni mwa mwezi Novemba, 2015.

Akizungumza kuhusu mkutano huo alisema ni mkutano wa kila mwaka kwa ajili ya kutathimini kwa pamoja utendaji wa Jeshi katika maeneo yote na kuweka mikakati ya kukabiliana na matatizo yaliyopo, kurekebisha dosari zilizojitokeza na kujiwekea malengo ya kuboresha utendaji wa kazi kwa ujumla katika mwaka ujao. 

Rais Magufuli apokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Waziri Mkuu wa Japan pamoja na Sudan

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mjumbe maalum wa Waziri Mkuu wa Japan Seiji Kiara Ikulu Jijini Dar es Salaam. Mjumbe huyo amekabidhi ujumbe wa maandishi kutoka kwa Waziri Mkuu wa Japan Mheshimiwa Shinzo Abe
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjumbe maalum wa Waziri Mkuu wa Japan Seiji Kiara mara baada ya kufanya nae Mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi Kamal Ismail, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya nje na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Sudan Mheshimiwa Omar Al Bashir.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjumbe maalum wa Rais wa Sudan Balozi Kamal Ismail aliyetumwa na Rais wa Sudan Mheshimiwa Omar Al Bashir.

WAZEE TAFF WAMWOMBA WAKIFAMBA AGOMBEE TENA NAFASI YA URAS

$
0
0
Msemaji wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Ahmed Olotu (mzee Chilo) akisoma waraka wa kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba kwa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kushoto ni Mzee Ramadhani Ditopile.
 Mzee wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Hamisi Kagaye (kushoto) akichangia mada wakati wa kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Bwana Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo. Kulia ni Mzee Ramadhani Ditopile. 
 Mmoja wa wazee wanaounda Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bi. Salome Nonge (kulia) akichangia mada wakati wa kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Bwana Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kushoto ni Mzee Ramadhani Ditopile na Mzee Ahmed Olotu maalufu kama mzee Chilo.


Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia tamko la Wazee wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) lililohusu kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). 
(Picha zote na Benedict Liwenga)

Na Skolastika Tweneshe na Tupokigwe Marco. ­­
WAZEE wa shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) hawajakubaliana na uamuzi wa Rais wa shirikisho hilo Bw. Simon Mwakifwamba kutogombea tena nafasi ya Urais katika shirikisho hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wazee wa Shirikisho hilo Bw. Ahmed Olotu maarufu kama Mzee Chilo amesema kuwa wao kama Wazee wakongwe katika Shirikisho hilo wamemuomba Rais huyo agombee tena wadhifa huo kwa mara nyingine ili aweze kumalizia mambo muhimu ya maendeleo katika tasnia ya sanaa.

“Sisi kama wasanii na Wazee wakongwe katika tasnia hii, bila kushurutishwa na mtu yeyote tunapinga uamuzi wake wakutotaka kugombea tena nafafasi hiyo .” Alisema Olotu.

Aidha, ameongeza kuwa, miradi kama TAFF Trust Fund, TAFF Creative Ltd na mingine mingi yenye kuhitaji umakini ambayo imehasisiwa chini uongozi wake inahitajika kumaliziwa kwani bado haijakamilika.

Kwa upande wake Bi. Salome Nonge (Mama Abdul) ameeleza kuwa, Bwana Mwakifwamba ndiye aliyesaidia kupatikana kwa Ofisi ya Wasanii pamoja na usafiri katika kazi zao.

“Binadamu hakosi kasoro ila kwa Mwakifwamba ni ndogo mno sasa hatutaki mtu mwingine aje.”Bi Salome alisema.

Naye Bi. Salumu Ally (Mkasi) ameeleza kuwa uongozi wa Mwakifwamba umesaidia wasanii kupata haki zao kama hati miliki zilizowezesha kupata maendeleo ya kiuchumi kupitia sanaa wanaoifanya.


Hata hivyo sanaa ya filamu inakuwa kwa kasi nchini pamoja na changamoto zilizopo ambapo juhudi katika kutengeneza kazi zenye ubora zitakazoleta ushindani katika soko la kitaifa na kimataifa bado zinahitajika.

MKUTANO MKUU WA TFF WAAHIRISHWA

$
0
0
Mkutano Mkuu wa kawaida wa Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) uliokuwa ufanyike Tanga ikiwamo shughuli ya uwekaji jiwe la msingi kwenye kiwanja cha TFF jijini Tanga sasa umeahirishwa kwa muda usiojulikana.

Mwishoni mwa mwezi Novemba 2015, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) mkoa wa wa Ilala ulitoa agizo la kufungwa na kuchukuliwa fedha kutoka kwenye akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) ili kulipa fedha zaidi ya shilingi bilioni 1.6, sehemu kubwa ikiwa ni malipo ya kutoka kwenye mishahara (PAYE) ya makoch Jan Poulsen, Kim Poulsen, na Jacob Michelsen na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye mchezo kati ya Tanzania na Brazil mwaka 2010.

Baada ya hatua hiyo TFF iliwasiliana na TRA na kuweka bayana kwamba deni la walimu (makocha) na mchezo dhidi ya Brazil lilistahili kulipwa na serikali na haikuwa sahihi kulielekeza TFF.

Aidha TFF ilieleza athari ambazo zingetokea iwapo amri hiyo (Agent Order) ingetekeleezwa kuwa ni pamoja na kusitishwa kwa ziara ya timu ya vijana chini ya miaka 15 (U15) katika nchi za Rwanda, Uganda na Kenya, kusimama kwa program za vijana na wanawake, Mkutano Mkuu, Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Kombe la Shirikisho.

Baada ya utekelezaji wa amri hiyo kuanza TFF ilifanya kikao na TRA na makubaliano ya kufungua akaunti yakafanikiwa. Hata hivyo akaunti zilifunguliwa zikiwa hazina fedha kwa kuwa zilishapelekewa Benki Kuu (BOT) na zoezi la madai haliwezi kukamilika kwa muda mfupi.

Baada ya hali hiyo kujitokeza, TFF ilifanya kila linalowezekana kuhakikisha Mkutano Mkuu unafanyika ikiwa ni pamoja na kutafuta ufadhili toka kwa wadau wake, lakini zoezi hilo limeshindikana katika muda mfupi uliopo na hivyo Shirikisho limeamua kuahirisha Mkutano Mkuu 2015 mpaka hapo hali itakaporuhusu.

TFDA Yafunga Kiwanda Bubu Kagera

RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEWA NA RAIS WA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA CNOOC KUTOKA CHINA

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya CNOOC kutoka Nchini China Cui Hanyun wakati alipofika Ikulu mjini Zanzibar leo na ujumbe aliofuatana nao.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Ujumbe wa Kampuni ya China National Offshore Oil Company ltd (CNOOC) ulifoka Ikulu Mjini Zanzibar kuonana na Rais, ugeni huo ukiongozwa na Balozi wa China nchini Tanzania Xie Yunliang (wa pili kulia) na Makamo Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya (CNOOC) Cui Hanyun (katikati) wengine ni viongozi wa juu wa kampuni hiyo.

[Picha na Ikulu.]

SHIRIKA LA NDEGE LA ETIHAD LACHANGISHA DIRHAM MILIONI MOJA KWA AJILI YA “WE CARE"

$
0
0
 Shirika la ndege likiwatunuku timu ya soka kutoka Serbia kama bingwa wa michuano ya kombe la dunia la mashirika ya ndege upande wa soka.
 Bendi ya vijana wenye ulemavu wa kusikia kutoka taifa la Falme za kiarabu wakiimba wimbo wa taifa la Falme za Kiarabu.
  Afisa mkuu wa biasaha wa Shirika la Etihad, Peter Baumgartner, akitumbuiza wakati wa tamsha.
 Dr Khawla Salem Al Saaedi, mwakilishi wa Rais wa shirika la kimataifa la umoja wa wanawake na afya, akiwazawadia timu kutoka Nepal kwa kushinda michuano ya kimataifa ya mavazi.

 Kamati ya Michezo na Jamii wakiwa na baadhi ya wahiriki wa michuano ya kimataifa ya mavazi.
 Kamati ya Michezo na Jamii wakiwa na baadhi ya wachezaji wa soka.
Abu Dhabi-based Fusion Arts ballet wakitoa burudani wakati wa tamasha. 

SHIRIKA la ndege la Etihad, ndege rasmi ya taifa za Falme za kiarabu, imefanikiwa kuchangisha kiasi cha dirhams milioni moja kwa ajili ya kusaidia kampeni ya “we care Yemen” hii ikiwa ni pamoja na kusaidia kukarabati shule mbili nchini Kenya kama sehemu ya mpango wa kila mwaka wa shirika hili la ndege la kuchangisha fedha kwa kushirikiana na shirika la Red Crescent kutoka nchi ya Falme za kiarabu pia. 

Mchango huu ulitangazwa wakati wa kufunga sherehe za kombe la dunia la mashirika ya ndege kwa upande wa mpira wa miguu na tamasha la vyakula na fashion, vyote vikiwa vimeandaliwa na kamati ya michezo na jamii ya shirika la Etihad, lilofanyika ukumbi wa kimataifa wa Al Forsan. 

Timu za soka kutoka mashirika 28 ya anga na ndege yalishiriki kwenye tamasha hilo lilokuwa na mashindano mbalimbali yakiwemo uchoraji wa henna, burudani ya mziki, ballet and michuano ya mavazi. Shirika la Etihad lilitoa zawadi kemkem ikiwepo safari kwenda kenya kwa mshindi wakwanza na wapili.

Makamu wa raisi wa shirika la Etihad masuala ya siasa za anga, Khaled Al Mehairbi, anayetumikia kama mwenyekiti wa kamati ya michezo na jamii, alisema “ Kama shirika la ndege la taifa ya Falme za kiarabu, tunapenda kuthibitisha dhamira yetu kwa jamii na kujitolea kwa wale wenye uhitaji. Tunayo furaha kushirikiana na UAE Red Crescent katika kutumikia and kusaidia jamii husika”.

“Tungependa kutoa shukrani za dhati pia kwa wageni, wadhamini and wauzaji walioshiriki kwa mioyo yao ya dhati kuchangia kampeni hii kwa mwaka 2015 ili kusaidia wale wenye uhitaji. Kwa pamoja tumetoa mwanga wa matumaini na nafasi ya maisha bora ya baadae kwa kaka na dada zetu waliopo Yemen na Kenya”

Sherehe za ufunguzi ziliongozwa na bendi ya taifa ya vijana wasio na uwezo wa kusikia. Tamasha hilo lilishuhudia burudani kutoka kwa “Sala the Entertainer”, mshindi wa mashindano ya X Factor 2015, na msanii kutoka Marekani, Dynasty. Burudani kutoka kikundi cha watoto waliocheza “Ballet” pia ilikuwa kivutio kikubwa katika tamasha hilo.

Michango ya hisani kwa Yemen ilikusanywa kupitia matukio mbalimbali ikiwemo mchango wa “Etihad gGuest Miles Online”, Kupitia timu ya soka ya Etihad, Mauzo ya vitu kutoka Etihad, mchango wa vifaa vya shule na mabegi mapya kwenda kwa watoto nchini Yemen kupitia wafanyakazi wa shirika la ndege la Etihad, na mchango wa fedha taslimu kwenye visanduku vya Emirates Red Crescent.

Mipango ya shirika kusaidia kampeni ya “We Care Yemen” na Kenya ni sehemu ya makubaliano ya awali juu ya ushirikiano wa kiubinadamu na kijamii baina ya shirika la ndege la Etihad na Emirates Red Crescent.

Tukio hili la kijamii lilihudhuriwa na mheshimiwa Khadija Issa Yusuf, Balozi wa kenya kwa nchi ya Falme za kiarabu, Bw. Humaid R Al-Shamsi, Naibu katibu mkuu kwa misaada ya kimataifa kutoka shirika la Emirates Red Crescent, Dr. Khalwa Salem Al Saaedi, mwakilishi wa Rais wa shirika la kimataifa la muungano wanawake na afya.

Wengine waliohuduria walikuwa katibu mkuu, Mheshimiwa Mariam Saif Al Qubasi, Mkuu wa sekta ya mahitaji maalumu kutoka Zayed Higher Organization (ZHO), Hamad Alhosani, Mtendaji mkuu wa TCA Abu Dhabi, na Mohammad Ali Khilji, meneja mkuu wa Axiom UAE. 

Shirika la ndege la Etihad liliwakilishwa na Peter Baumgartner, Afisa mkuu wa biashara, Khaled Al Mehairbi, Makamu wa Rais masuala ya siasa za anga, Ali Al Shamsi, Makamu wa Rais Abu Dhabi Hub, Oliver Iffert, Makamu wa rais uendeshaji masuala ya Ndege, na Geert Boven, Makamu wa Rais huduma wa Uwanja wa ndege.

Mwaka 2015, shirika la ndege la Etihad liliweza kuchangisha Etihad Guest miles, bidhaa za msaada na fedha taslimu yenye thamani ya zaidi ya dirhams milioni tatu.

Tamasha hili la siku mbili lilifanyika kwa kushirikiana na Emirates Red Crescent, baraza la michezo la Abu Dhabi, vyombo vya habari vya Abu Dhabi, ukumbi wa kimataifa wa michezo wa Al Forsan, Hoteli za Time, Shirika la wanawake la Joyful, kampuni ya maji ya Al Ain, Bottega Verde, Dusit Thani Abu Dhabi, Axiom UAE, Sebamed, Fusion Arts, Gabs, Pierre Fabre, Hoteli za Yas Viceroy, Novotel Al Bustan, Holiday Inn Abu Dhabi, Hoteli za One to One, Yas Waterworld, Maabara za dawa za Al Borg Medical, Al Jaber Optical, Mikura Pearls, Conrad Dubai, Absolute Dry, Zartux, and Hoteli ya Tilal Liwa.


Kuhusu Shirika la Ndege la Etihad
Shirika la Ndege la Etihad lilianza shughuli zake mnamo mwaka 2003 na hadi kufikia mwaka 2014, ilikuwa limeshabeba abiria takriban milioni 14.8. Kutoka makao makuu yake huko Abu Dhabi, shirika hili linasafiri au limetangaza mipango ya kuhudumia wasafiri na mizigo kutoka vituo 116 huko Mahariki ya kati, Afrika, Ulaya, Asia, Australia na nchi za Americas. Shirika lina ndege aina ya Airbus na Boeing takriban 120, Zaidi ya ndege 200 zikiwa zimewekea oda, zikiwemo Boeing 787s 66, Boeing 777Xs 25, Airbus A350s 62 na Airbus A380s tano.

Shirika la Etihad pia limewekeza katkia AirBerlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Jet Airways , Virgin Australia, pamoja na shirika lenye makazi Uswiss Darwin Airline, likifanya biashara kama Etihad Regional. Shirika la Ethihad, sambamba na airberlin, Air Serbia, Air Seychelles, Alitalia, Etihad Regional, Jet Airways na NIKI, pia hushiriki pamoja nkwatika washirika wa Etihad Airways, brand mpya inayowaleta kwa pamoja mashirika mengine ya ndege yenye uelewa sawa ili kutoa huduma bora zaidi kwa wateja, kuwapa wateja ratiba nzuri Zaidi na kuwazawadia wateja wakudumu.kwa maelezo Zaidi, tafadhali tembelea :www.etihad.com

MHAGAMA: AZITAKA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUTEKELEZA MAELEKEZO YA SERIKALI YA KUJIAANDAA NA KUKABILI MAAFA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akiangalia Sehemu ya mtaro wa maji katika eneo la Tegeta, Basihaya wilayani Kinondoni, Jijini Dar es Salaam leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akimsikiliza mkazi wa Tegeta, Basihaya Jijini Dar es Salaam, Jumanne Malongo alipokuwa akimueleza jinsi wembamba wa mtaro huo unavyosababisha maji kujaa katika makazi yao, leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda. 
 Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Manisipaa kinondoni, Ando Mwakunga akimueleza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), uharibifu wa “kalvati” katika eneo la Boko, Ununio Jijini Dar es Salaam, leo wakati Waziri huyo alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo. 

 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akiteta na Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brig. Jen, Mbazi Msuya juu ya ujenzi wa mtaro wa maji katika eneo la Mnyamani, Buguruni wilayani Ilala, Jijini Dar es Salaam leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge; Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Bibi Jenista Mhagama (Mb), akitoa maelekezo baada ya kutoridhishwa na ujenzi wa mtaro wa maji katika eneo la Mnyamani, Buguruni Ilala Jijini Dar es Salaam, kwa Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kumpatia taarifa ndani ya siku tano inayoeleza ni jinsi gani watakavyokamilisha ujenzi huo, leo wakati alipofanya ziara kuangalia jinsi wilaya hiyo ilivyojiandaa kukabili maafa ya Mvua zinazoendelea kunyesha jijini humo. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).

MO DEWJI FOUNDATION YATOA MSAADA WA MIL. 110/- KWA TAASISI INAYOWASAIDIA WATOTO WENYE KANSA YA TUMAINI LA MAISHA

$
0
0
IMG_8785
Meneja Mwendeshaji wa Taasisi ya MO Dewji, Francesca Tettamanzi (kulia) akikabidhi mfano hundi ya Shilingi Milioni 110 kwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Tumaini la Maisha inayohudumia watoto wenye kansa nchini, Gerard Mongera (wa pili kushoto) kwa ajili ya kusaidia watoto wenye kansa wanaopata matibabu yao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kushoto ni Ofisa anayesimamia utekelezaji wa Programu wa Taasisi ya Tumaini la Maisha inayohudumia watoto wenye kansa nchini, Lilian Ndyetabula.
IMG_8716
Meneja Mwendeshaji wa Taasisi ya MO Dewji, Francesca Tettamanzi (kulia) akitoa neno la ukaribisho kwa uongozi wa Taasisi ya Tumaini la Maisha inayohudumia watoto wenye kansa nchini na waandishi wa habari katika hafla fupi ya kukabidhi msaada wa fedha kwa ajili ya watoto wenye kansa iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za MeTL Group jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Mmoja wa Wakurugenzi wa Taasisi ya Tumaini la Maisha, Gerard Mongera na Wa pili kushoto ni Ofisa anayesimamia utekelezaji wa Programu wa Taasisi ya Tumaini la Maisha , Lilian Ndyetabula.
IMG_8726
Afisa Mahusiano wa Taasisi ya MO Dewji, Zainul Mzige (kulia) akisoma taarifa kuhusu madhumuni ya kuanzishwa kwa MO Dewji Foundation pamoja na kazi wanazofanya katika kusaidia jamii ikiwemo sekta ya Afya na Elimu.
IMG_8747
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Tumaini la Maisha, Gerard Mongera (kushoto) akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa MO Dewji Foundation na kuwaomba kuendelea kushirikiana nao wakati wa hafla ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 110 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye kansa wanaohudumiwa na taasisi hiyo.

IMG_8770
Pichani juu na chini baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za MeTL Group jijini, Dar es Salaam.

IMG_8723
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Taasisi isiyo ya kiserikali ya MO Dewji iliyo chini ya makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group) inayojishughulisha na kusaidia jamii imetoa msaada wa Shilingi Milioni 110 kwa taasisi ya Tumaini la Maisha ambayo inajihusisha na kuwasaidia watoto wenye kansa kupata matibabu pamoja kuwahudumia kwa kipindi chote wanachokuwa katika matibabu.

Akizungumzia msaada huo, Afisa Mahusiano wa MO Dewji Foundation, Zainul Mzige alisema kuwa MO Dewji Foundation imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kwa watoto ambao wanagundulika kuwa na kansa kuja Dar es Salaam kupata matibabu na msaada ambao wameutoa wanataraji kuwa utatumiwa vizuri na taasisi hiyo ili kuzidi kusaidia watoto.
Alisema wameshafanya kazi nyingi na Taasisi ya Tumaini la Maisha na wanawatambua katika utendaji wao wa kazi kusaidia watoto ambao wana kansa na msaada huo wa milioni 110 wanataraji utakuwa na faida kubwa kwa kutumika kusaidia watoto waliopo mikoani na hapa Dar ambao wanakutwa wakiwa na kansa na hivyo msaada huo utasaidia kuokoa maisha ya watanzania wengi.

“MO Dewji tumekuwa tukisaidia miradi mbalimbali ya kijamii na kama jinsi tunavyosaidia katika miradi hiyo na leo tunafuraha kutoa Shilingi Milioni 110 za kitanzania kwa Tumaini la Maisha tunaamini ni shirika linalotoa matumaini mapya kwa wagonjwa na familia zao,
“Tumekuwa tukishirikiana nao katika shughuli mbalimbali za kijamii tunafahamu ni jinsi gani wanavyosaidia watoto wenye kansa na kama jinsi tulivyokuwa tunashirikiana nao katika shughuli mbalimbali za kimatibabu na leo tunatoa msaada mwingine ili kuwawezesha kuzidi kuwasaidia watoto hao,” alisema Mzige.

Aidha Mzige alisema kuwa MeTL Group kupitia kwa MO Dewji Foundation wanatambua ni jinsi gani serikali imekuwa ikipambana na ugonjwa huo kwa kuwasaidia watoto wenye kansa na wao wanaahidi kuendelea kuwasaidia kwa kutoa misaada kwa watoto wenye kansa ili waweze kupata matibabu na kuokoa maisha yao.

Awali Afisa Mahusiano huyo alisema kuwa Rais na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji aliamua kuanza kuwasaidia watoto wenye kansa baada ya kukutana na mtoto wa miaka 7 aliyetambulika kwa jina la Zakia mwaka 2012 wakati akiwa mbunge wa Singida Mjini ambaye alikuwa akisumbuliwa na kansa ambayo ilikuwa imeshasambaa mwili mzima.

Mzige alisema Dewji baada ya kukutana na mtoto huyo alimchukua na kumpeleka hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu lakini walikuwa wameshachelewa kutokana na kansa kusambaa mwilini na hivyo mtoto huyo kupoteza maisha hali ambayo ilimfanya Dewji kujitoa kusaidia watoto wenye kansa ili waweze kupata matibabu na kwa mapema kabla kansa haijasambaa zaidi.

Nae Gerard Mongera ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Taasisi ya Tumaini la Maisha aliishukuru MO Dewji Foundation kwa msaada ambao wanaowapatia kwa kipindi chote ambacho wamekuwa wakishirikiana na kuitaja MO Dewji kama taasisi ambayo imekuwa ikiwasaidia zaidi hivyo kuwa na matarajio ya kuzidi kushirikiana.

Mongera alisema msaada umetolewa na MO Dewji Foundation utatumika kuwasaidia watoto hao kupata matibabu na chakula kwa watoto wanaoumwa kansa walio katika hosteli za taasisi hiyo na walezi wanaowasimamia watoto hao kwa kuwanunulia chakula na mahitaji mengine muhimu ambayo yanahitajika kwa watoto hao.

“Tumekuwa tukishirikiana kwa muda mrefu na MO Dewji Foundation na natumia fursa hii kuwashukuru kwa msaada wanaotupatia wamekuwa wakitusaidia kwa muda mrefu na tunawaomba wazidi kuwa na moyo huo wa kuwasaidia watoto wenye kansa ambao wengi wao wanatoka mikoani na kwa kusaidiana nao tunaamini tutaweza kuwasaidia watoto wengi zaidi,” alisema Mongera.

Mongera aliongeza kuwa tangu mwaka 2013 walipoanza kufanya kazi na MO Dewji Foundation wamefanikiwa kuokoa zaidi ya asilimia 50 ya maisha ya watoto ambao wamekutwa na kansa na kutumia fursa hiyo kuyaomba makampuni mengine pamoja na watu binafsi kujitokeza kuisaidia taasisi hiyo ili kuwa na uwezo zaidi ya kuwahudumia watoto ambao wanakuwa wanasumbuliwa na kansa.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO ATOA MWELEKEO WA UTENDAJI KAZI WA WIZARA

$
0
0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akizungumza na watendaji wa Wizara ya Ujenzi pamoja na Taasisi zake kuhusu ufanyaji kazi kwa uadilifu kwa kuzingatia maslahi ya jamii.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akitoa maelekezo kwa watendaji wa Wizara hiyo namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili na mikataba wanayoingia iwe kwa maslahi ya nchi.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akiweka sahihi katika kitabu cha wageni huku Katibu Mkuu wa aliyekuwa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi  na Teknolojia Bw. Yamungu Kayandabila akishuhudia.

 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Wizara ya iliyokuwa ya Uchukuzi wakati alipotembelea Wizara hiyo ambayo sasa imeunganishwa na Ujenzi na Mawasiliano.

Mwili wa marehemu Dotto Mzava wa Jamii Forums wasafirishwa leo kuelekea Same Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi

$
0
0
 Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Dotto Mzava likishushwa Kwenye gari maalum mara baada ya kuwasili katika kanisa la Wasabato Manzese uzuri kwaajili ya sala ya kuombea kabla ya Mwili kusafirishwa kuelekea Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
 Mchungaji wa kanisa la Adventist wasabato akiendelea na ibada wakati wa ibada ya kumuombea marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media Maxence Mello akitoa historia fupi ya Marehemu Dotto Mzava ambae pia alikua mmoja wa watumishi katika kampuni hiyo.
Baba Mkubwa wa marehemu Dotto Mzava akitoa maneno ya shukrani katika kanisa la Kisabato la Manzese Uzuri mara baada ya zoezi la misa kumalizika.
 Heshima za Mwisho zikiendelea kutolewa
 Majonzi na simanzi kwa ndugu wa marehemu
 Mmiliki wa Fullshangwe Blog,John Bukuku akitoa heshima za mwisho
 Heshima za mwisho zikiendelea kutolewa kwa mwili wa marehemu Dotto Mzava kabla haujasafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro kwaajili ya mazishi
 Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Dotto Mzava kabla ya Kusafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro kwa mazishi yanayotarjiwa kufanyika kesho
 Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media akitoa heshima za mwisho kabla ya mwili wa marehemu kusafirishwa Same Mkoani Kilimanjaro mapema leo
 Ibada ikiendelea
 Jeneza lenye mwili wa marehemu Dotto Mzava likipandishwa ndani ya gari tayari kwa safari ya kuelekea Same Mkoa wa Kilimanjaro leo kwaajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho
 Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kanisani
 Kwaya ya Angaza ikitoa huduma wakati wa ibada ya kumuombea marehemu Dotto Mzava
Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dotto Mzava wakiwa kanisani kwenye ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Wasabato la Manzese Uzuri kabla ya Mwili kusafirishwa kwaajili ya kwenda kupumzishwa katika nyumba yake ya milele huko Kwao Same Mkoa wa Kilimanjaro.Picha na Pamoja Blog

RAIS DKT. MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MKUU WA TAKUKURU

Article 24

TAMASHA LA MSAFARA LAFANA IFAKARA, VIJANA WENGI WAJENGEWA UWEZO WA KUTIMIZA NDOTO ZAO.

$
0
0

 Baadhi ya vijana wakiwa wanaendelea kufanya usafi maeneo ya Uwanja wa Taifa wa Ifakara eneo ambapo Tamasha hilo la Msafara lilifanyika.
 Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero Bw. Yahya Naniya(aliyevaa miwani) akiwa katika ushiriki wa kufanya usafi kaika uwanja wa Taifa wa Ifakara.

Vijana wengi wa Ifakara Wilayani Kilombero mkoani Morogoro wamepewa nasaha kutumia vipaji vyao kwa lengo la kutimiza ndoto zao ili maisha yao yaende sawa na kukuwa kiuchumi.
Mwenyekiti wa Programu ya Msafara James Isdore akizungumza  wakati wa uzinduzi wa programu ya msafara wilayani Kilombero kata ya Ifakara alisema asilimia kubwa ya vijana wenye umri kati ya miaka 14-15 wamekuwa wakijirudisha nyuma kutumia vipaji vyao kutimiza ndoto zao kwa sababu mbalimbali.

"Tumeamua kuja Ifakara kwa lengo la kuja kuinua vijana kupitia  programu hii ambapo programu hii kwa sasaa ipo katika majaribio inatarajia kuanza rasmi mwakani 2016 hadi sasa majaribio ya programu hii yameweza kufanyika katika mikoa miwili Dar es Salaam na Ifakara na matokeo yake tumeanza kuona ni makubwa mno katika kusaidia jamii ya vijana kutimiza ndoto zao na sio kukaa vijiweni kudidimiza ndoto zao"alisena Isdore

Alisema Programu hiyo inaendeshwa kwa kupitia mashirika matano yanayojishughulisha na masuala ya vijana yakiratibiwa na Shirika la Oxfam Tanzania.

  Veronica  Malwata ambaye ni Mkazi wa mji wa Ifakara alisema ndoto ya kipaji haiwezi kuja hivi  hivi bila kujituma hivyo vijana wanapaswa kupambanua wapi walipo na wanataka kwenda wapi.

 Ramadhani Lihapa ni mmoja wa vijana ambaye alifanikiwa kutimiza ndoto zake, alisema kijana  anapaswa kujitambua ananafasi gani katika jamii na kuona ni namna gani anaweza kufikia ndoto yake aliyekuwa anaiwaza siku nyingi.
 Mwenyekiti wa Maandalizi wa Msafara kutoka TYDC James Isdore akielezea maana ya msafara kwa wakazi wa Ifakara
  Baadhi ya wakazi wa Ifakara wakiendelea kusikiliza kinacho endelea 
Mbunge wa Kilombero Mh.Peter Lijuakali akielezea Historia ya Maisha yake na mpaka amefanikiwa kuwa Mbunge, na kuwasihi vijana wengine wasikate tamaa kwa sababu kila jambo lina wakati wake
 Baadhi ya watoto wa shule mbalimbali za Msingi katika mji wa Ifakara wakiwa katika Tamasha la Msafa
Suhaila Thawer kutoka Oxfam akiendelea kutoa utaratibu wa tamasha hillo.
 Kikundi cha young Feminist forums wakiwa wanatoa somo kwa vijana pamoja na burudani kwa njia ya ngonjera
 Mmoja wa wadau akiwa anatoa neno la kuwajenga vijana juu ya kujitambua lakini pia kuwajengea uwezo  vijana kuwa wafumbuzi na wabunifu ili waweze pata kujitambua
 Bi. Nusura Salum akitoa ushuhuda wake wa namna alivyo anza maisha yake kwa kuuza maandazi , kuwa mkulima na sasa mfanyabiashara mkubwa na alivyopitia katika safari yake ya mafanikio
 Mwanamuziki Chipukizi wa Bongo Fleva anayeishi Morogoro One Darin akitoa Burudani wakati wa Tamasha la Msafara
 Ramadhani Lyasa akielezea kwa ufupi jinsi alivyopitia changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutokusoma na kuwa alianza na kilimo na sasa ni mfanyabiashara
 MC Fadhiri akiendelea kutoa utaratibu wa wazungumzaji katika Tamasha la Msafara
 Bi. Veronica Malwata mkazi wa Ifakara akieleza jinsi alivyotaka kukata tamaa ya maisha baada ya kushindwa endelea na shule na baadae kujiinua kwa kuanza kufanya kazi katika moja ya Zahanati kama muhudumu na baadae alipelekwa shule ya uuguzi na sasa ni muuguzi katika Hospitali ya Ifakara.
 Kijana Narsis nae akitoa ushuhuda wake wa yale aliyopitia mpaka amefanikiwa kaika maisha.
 Baadhi ya waandaaji wa Msafara wakiwa wanatoa neno la Shukurani kwa wakazi wa Ifakara.
Baadhi wa wanavyuo wakiendelea kufuatilia Msafara. (Picha zote na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa Tanzania)


Waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa na Harakati za Kumkomboa Mwanamke

$
0
0

Baadhi ya waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa Wilayani Kahama wakiongea na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kwa ajili ya kujionea matokeo mbali mbali baada ya waraghabishi kuwasaidia wananchi hao kuchukua hatua katika kila jambo kwa maendeleo ya kijiji chao

Pichani nikihoji maswali kwa Dada Miriam Stefano (Aliyejishika tama ) ambaye amekuwa mchango mkubwa kwa kutoa elimu ya uzazi na mabadilko ya mwili kwa vijana wa kike katika baadhi ya shule za sekondari na msingi katika kijiji hicho

Picha ya pamoja nikiwa na waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa Wilayani na waandishi wa habari tuliopata bahati ya kutembelea kijiji hicho na kujifunza namna gani wameweza kuwa chachu ya maendeleo katika kijiji hicho


Na Krantz Mwantepele ,KAHAMA

Mkutano mkuu wa Kijiji cha Nyandekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga uliofanyika mwishoni wa mwezi wa tisa umeazimia kuwashikinikiza wazazi wa kijiji hicho kuwapeleka watoto wao shule Azimio hilo Pia limeelekezwa kwa vijana wanaokaa vijiweni kuwataka kushirki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na sio kukaa vijiweni pia kushiriki katika mikutano mbali mbali ya kijiji kujua maendeleo ya kijiji Iikihusisha mapato na matumizi. 


Mkutano huo umepitisha maazimio matano yanayolenga kurejesha nidhamu Na heshima kijijini Nyandekwa hatua hiyo imefikiwa Kutokana Na wananchi wa kijiji hiki kutoona umuhimu wao kuchukua hatua za kujikwamua kiuchumi na pia Kuwa na ujasiri wa kuhoji mapato na matumizi kwa ajili ya kijiji chao .

Hali hiyo inatokana na juhudi za dhati bila kukata tamaa zilizofanywa waraghabishi na watetezi wa haki za binadamu wa kijiji hicho akiwemo Miriam Stefano, Boniface Izengo , Matilda Peter ,Na Mwenyekiti Wa kitongoji cha Busolwa Bi Ana Alphonce kuwapa ujasiri na elimu ya uraia wananchi wenzao ili wawe chachu ya maendeleo.

Kwa mujibu wa bi Anna Alphonce ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha Busolwe aliweza kuongea na mtandao wa Mwanaharakati Mzalendo Blog alisema kupitia mikutano mbalimbali ya kijiji aliweza kutoa hamasa kwa wanawake na wanaume wa kijiji hicho kushiriki katika uchaguzi mkuu uliopita katika kusikiliza sera za viongozi na mwishowe kushiriki kupiga kura.Na kwa muda mfupi aliweza kufanikisha wanawake wengi kushiriki katika maamuzi ya kijiji pia kuwa na ujasiri wa kuhoji katika mikutano ya kijiji.

Wengi wa wanakijji ambao wamekuwa waraghabishi katika kijiji hiki waliweza kupata mafunzo haya ya uraghabishi ambapo waliweza kujua baadhi ya haki zao na kuwa na uajasiri wa kuhoji mapato na matumizi ya kijiji hicho ambapo mwanzoni walikuwa hawapati fursa hiyo kwa wakati .Waraghabishi hawa wamekuwa chachu ya maendeleo ya kijiji cha Nyandekwa katika sekta za kiuchumi ,kisiasa na kijamii kwa kuwaelimisha wanakijiji wenzao haki na wajibu wao kwa nafasi kubwa .

“Viongozi wa kijiji hiki hawakuweza kutupa mrejesho wa kila jambo linalofanyika kwa kijiji hcetu hasa katika mikutano ya kijiji na sisi tulipoanza kuhoji tulikosa ushirikiano kwao lakini mwishowe wananchi wengi waliona umuhimu wa kushirikishwa” alinukuliwa bw. Boniface Izengo mmoja wa waraghabishi wa kijiji hiki alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii.

Katika hatua nyingine mmoja wa waraghabishi wa kijiji hiki bi Matilda Peter amekuwa ni mmoja wa vijana wanaotoa elimu ya uzazi wa mpango kwa makundi rika ambapo hukutana na vijana hasa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari na kuwajuza kuhusu mabadiliko ya mwili yao na pia kuwashauri jinsi ya kuepuka maambukizi magonjwa ya ngono na mimba zisizotarajiwa.

Maazimio yaliyopitishwa kuwa ni vijana wanaokaa au kusimama ovyo barabarani na maeneo mengine bila shughuli maalum kuwajibishwa na pia kuweza kuwawezesha kuwashirikisha katika shughuli za kijiji hicho ikiwemo kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji kijijini hapo

Pia mkutano wa kijiji hiki uliazimia kuwa mapato na matumizi kuweza kujadiliwa kwa uwazi na pia kubandikwa katika mbao za matangazo hapo kijijini kuwezesha wananchi hao kuweza kusoma na kuelewa kila kinachoendelea kijijini kwao katika swala la maendeleo ya uchumi ..

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMTEMBELEA WAZIRI MKUU MSTAAFU JAJI WARIOBA

Wateja wa Airtel kushinda mamilioni ya pesa kupitia promosheni ya “Airtel MKWANJIKA”

$
0
0
Meneja uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando pamoja na Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga kwa pamoja wakizindua promosheni mpya ya “Airtel MKWANJIKA” itakayowawezesha wateja wote wa Airtel nchi nzima kujishindia mamilioni ya pesa taslimu kila siku.
Meneja Masoko wa Airtel Bi Anethy Muga akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa promosheni mpya ijulikanayo kama “Airtel MKWANJIKA” itakayowawezesha wateja wote wa Airtel nchi nzima kujishindia mamilioni ya pesa taslimu kila siku.
Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akielezea jinsi promosheni ya Airtel Mkwanjuka itakavyoendeshwa wakati uzinduzi wa promosheni hiyo itakayowawezesha wateja wa Airtel nchi nzima kujishindia mamilioni ya pesa hadi shilingi milioni 300.

TANZANIA NAMED FINALIST IN BEST TOURIST BOARD AFRICA CATEGORY FOR ANNUAL TRAVVY AWARDS.

$
0
0

By:  Geofrey Tengeneza.

Tourism sector in Tanzania is continuing to perform well at international arena after the country’s responsible organ for marketing Tanzania as a tourist destination Tanzania Tourist Board (TTB), being named one of three finalists in Destination:- Best Tourist Board Africa category for the 2015 Travvy Awards that recognizes the highest standards of excellence in the Industry today and honors travel companies, travel products, travel agencies, travel executives, travel agents and travel destinations. Other two finalist countries under the category are South Africa Tourism and Namibia Tourism Board.

Selection of the finalists is based on votes by travel agents. The final two winners in the respective categories are determined by the award-winning Travel Alliance editorial team.The Annual Travvy Awards will be presented by TravAlliancemedia at a Gala Awards night, New York City, January 6, 2016.

 “Tanzania is honored to be among the finalists for Africa. This is the result of the dedicated and pro-active work in the US market by Tanzania Tourist Board (TTB), together with The Bradford Group, TTB’s USA representative, and the strong support of Tanzania National Parks and Ngorongoro Conservation Area Authority as well as the Tanzania Embassy in Washington and the Tanzania Mission to the UN in New York.“ commented, the Permanent Secretary of the Ministry of Natural Resources and Tourism Dr. Adelhelm Meru 

He further said that In addition to Tanzania having some of the world’s most renown tourism icons, the Serengeti and the Great Animal Migration, Mt. Kilimanjaro, the Ngorongoro Crater as well as the hidden gems of the South, the Selous Game Reserve and Ruaha National Park, visitors from all over the world are also attracted to Tanzania because of its peace and tranquility, stability and prevailing democracy in the country that makes Tanzania a suitable place to stay for visitors.

This new development comes after recent developments where Tanzania mainland and Zanzibar were named by the US Travel and Leisure Magazine among the annual Best Places to Travel in 2016.Tanzania was also named among 52 places to go this year by the ‘New York Times’, the best African Destination to visit by the Fox News Channel, the best safari Country of Africa by SafariBookings.com and Tanzania’s Mt Kilimanjaro and Serengeti National Park being named two of the greatest parks in the World by National Geographic Magazine to mention just a few. Destination Tanzania has also received continuous positive coverage in the major travel publications and broadcast media.
 

Article 18

Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images