Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 677 | 678 | (Page 679) | 680 | 681 | .... | 1904 | newer

  0 0

   Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wapenzi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliojitokeza kwa wingi kwenye hafla fupi ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli kwa ushindi alioupata katika uchaguzi wa uliofanyika oktoba 25 mwaka 2015. 
   Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete (kulia)akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma Kinana(katikati) pamoja na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda wakati wa sherehe ndogo ya kushukuru wapiga kura walioipa CCM ushindi.
   Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
   Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwashukuru wananchi wote
  waliompigia kura kwenye uchaguzi wa Rais uliofanyika tarehe 25, oktoba
  ambapo aliibuka mshindi katika uchaguzi huo.
   Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kwa  wananchi waliojitokeza kumpongeza nje ya Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.
  Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akionyesha cheti alichokabidhiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya kushinda kiti cha Urais kwenye uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba mwaka 2015.
   Mama Samia Suluhu aliyekuwa Mgombea Mwenza akionyesha cheti chake cha Umakamu wa Rais kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja kumpongeza.
   Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akimtambulisha mke wake Janeth Magufuli mbele ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliokuja kumpongeza.
   Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais mteule wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli.
   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza kwenye hafla hiyo ya kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya Ofisi Ndogo CCM Lumumba.
   Rais Mteule Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa jiji la Dar es Salaam mara baada ya kumalizika hafla ya kuwasalimu na kuwashukuru kwa kumpigia kura zilizompa ushindi wa kiti cha Urais.
  Wakazi wa jiji la Dar es Salaam waliojitokeza kwa wingi kumpongeza Dk. John Pombe Magufuli nje ya ofisi ndogo CCM Lumumba.BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  02
  Rais Dk.Jakaya Kikiwete akizundua kampuni ya Soko la Bidhaa  katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam.
  05 
  Rais Dk.Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti na Bodi ya Kampuni ya Soko la Bidhaa wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo leo jijini Dar es Salaam.
  01
  Rais Dk.Jakaya Kikwete akizungumza wakati uzinduzi wa Kampuni ya Soko la Bidhaa iliyofanyika katikza ukumbi wa Serena jijini Dar es Salaam Oktoba 30, 2015.
  03
  Waziri wa Fedha na Uchumi,Saada Mkuya akizungumza na wakati uzinduzi wa kampuni ya Soko la bidhaa  jijini Dar es Salaam.
  04
  Sehemu wataalam mbalimbali wakiwa wamekekti katika uzinduzi wa Kampuni ya Soko la Bidhaa  jijini Dar es Salaam.  Rais Dk.Jakaya Kikwete amesema kuanza kwa kampuni ya soko la bidhaa kutasaidia wakulima kupata soko la uhakika na kukuza uchumi pamoja na kupata bima katika kilimo.
   Hayo ameyasema leo wakati uzinduzi wa Kampuni ya soko la bidhaa jijini Dar es Salaam,Dk.Kikwete amesema wakulima wamekuwa wakilima lakini masoko yao hayana uhakika na kilimo hakina tija.
   Amesema kuwa mfumo utasaidia wakulima kupata bei ya uhakika wa kuuza mazao yao na wanunuzi kufahamu bei ya soko la bidhaa wanayoihitaji.Dk.Kikwete ameitaka watu wanaofanya kazi kuwa waaminifu katika kuweza kuwafanya wakulima wanufaike na soko hilo kwa kuwaletea maendeleo ya kuendeleza na kuachana na kutafuta masoko ambayo mwisho wa siku wanauza kwa hasara.
   Aidha amesema soko la bidhaa litawaondolea wakulima ukopwaji ambao umekuwa ukiwakatisha tamaa na kushindwa kuendeleza kilimo chenye tija.Amesema wakulima wamekuwa wakifanya kazi zao za kilimo wakiwa na changamoto kubwa ya kukosa soko la uhakika na kufanya mazao kununuliwa na watu wachache kwa bei ya chini.
   Dk.Kikwete amesema wakulima wakiwa wana soko la uhakika kutafanya waweze kuingia katika bima kutokana na kilimo kuonyesha mwanga katika sekta hiyo.Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Soko la Bidhaa (TMX),Nasama Masinda amesema kuwa soko hilo wataanzia mazao ya Ufuta,Korosho pamoja na mpunga .
   Amesema wamejipanga katika kuhakikisha wanaweka uwazi wa soko katika bidhaa hizo kwa wanunuzi na wauzaji kuwa na bei inayoendana na soko.

  0 0

  Logo ya Zadia
  Jumuiya ya Wazanzibari Waishio Nchini Marekani (ZADIA), imekuwa ikifuatilia kwa karibu na makini zaidi zoezi zima la Uchaguzi Mkuu visiwani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. Kwa kiasi kikubwa mchakato wa uchaguzi ulifanyika kwa njia za amani na utulivu.

   Hata hivyo ZADIA imeshtushwa mno na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mh. Jecha Salim Jecha la kutangaza kuufuta Uchaguzi Mkuu Zanzibar na matokeo yake.
  Ama kwa hakika kitendo hicho hakikuwa cha busara na kinapelekea kurudisha nyuma maendeleao ya demokrasia Zanzibar, na vilevile hakiashirii mustakbali mwema kwa nchi yetu tuipendayo. 

  Wazanzibari wameelezea maoni na matakwa yao kwenye visanduku vya kupigia kura, na maoni na matakwa yao hayo yanapaswa kusikilizwa na kuheshimiwa.
  Kwa hivyo, ZADIA inatoa wito kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar, kumalizia mchakato mzima wa kuhesabu kura kwa majimbo yaliyobakia na kutoa matokeo ya mwisho ya Uchaguzi na kumtangaza mshindi ili kuiepusha Zanzibar yetu tuipendayo kuingia katika hali ya mtafaruku na mifarakano isiyokuwa na tija bali kuleta hasara.
  ZADIA pia inaungana na jumuiya zote za kimataifa ambazo zimetoa msimamo wao juu ya uchaguzi wa Zanzibar, hasa ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, ambao ni kiungo madhubuti kati ya Wazanzibari walioko Zanzibar na wenzao wanaoishi nchini Marekani.
  Aidha, tunapenda kumkumbusha Rais wa Zanzibar Mheshimiwa Dakta Ali Mohammed Shein kuwa Wazanzibari walimpa amana kubwa ya kuwaongoza, na kwa hivyo ni wajibu wake kuienzi amana hiyo kwa kuchukuwa hatua za kiungwana za kuitoa Zanzibar kwenye mgando huu wa kisiasa. Hali hii iliyopo sasa inaleta wasiwasi miongoni mwa raia na imekua ikiathiri maisha yao ya kila siku, na ikiachwa kuendelea huenda ikaathiri pia mustakbali maisha yao kwa jumla.
  ZADIA pia inamtolea wito Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake aliyonayo kuhakikisha Zanzibar inatoka kwenye mkwamo huu wa kisiasa na kwamba anaondoka madarakani akiiacha Zanzibar ikiwa katika hali ya amani na utulivu. Kwa kufanya hivyo atauthibitishia ulimwengu kuwa kweli Tanzania ni kisima cha amani.
  Na mwisho tunawaomba Wazanzibari, wapenzi wa Zanzibar, na Watanzania wote kwa ujumla popote pale walipo, wajitahidi kufanya mawasiliano na Jumuiya nyengine za Kimataifa ili ziingilie kati suala hili kabla nchi yetu haijaingia kwenye mtafaruku mkubwa wa kisiasa na kijamii na hata kupelekea kuhatarisha amani ya nchi yetu.
  Mungu Ibariki, Zanzibar.

  0 0

   Bwana Harusi Said akimnywesha Shampein mkewe Salma wakati wa sherehe ya ndoa yao iliyofanyika kwenye Uukumbi wa Best Choice uliopo Tabata jijini Dar es Salaam, jana usiku ambapo wanandoa hao walijiwekea historia ya ndoa yao kwa kusherehekea siku maalum ya utambulisho wa Rais mpya wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli aliyekabidhiwa hati ya utambulisho wa ama cheti cha ushindi kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu uliomalizika wiki iliyopita.

  Aidha wanandoa hao walifunga Ndoa Okt 27 huko Karatu mkoani Arusha.
   Bi Harusi Salma akimlisha Keki mumewe Said ikiwa ni ishara ya upendo.
   Bwana harusi na Bi Harusi,wakimkabidhi keki Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya sherehe yao, George John, ikiwa ni sehemu ya kumshukuru kwa kusheresha na kufanikisha sherehe hiyo.
   Mdogo wa Bi harusi akifanya yake ukumbini hapo...
   Bw na Bi Harusi wakiwa katika pozi.... KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

   Baadaye ilikuwa ni mwendo wa Kwaito kama hivi.....
  Baadhi wakishow love na maharusi....
   Kamati ikisonga kukabidhi zawadi kwa maharusi....
   Sebene la zawadi....
   Picha ya pamoja na wanakamati....
   Maneno ya shukrani.....
   Msanii wa muziki wa Injili, Mbasha, ambaye ni rafiki wa karibu na Bwana Harusi, akizungumza wakati wa sherehe hiyo, ambapo alimalizia na CCM oyeeeeeeeeeeeee, ukumbi ukaripuka oyeeeeeee
   Baada ya kuwapagawisha baadhi walishindwa kujizuia na kutoa skafu zao kibindoni na kumkabidhi mbasha kwa furaha......
   Msema chochote Mc, akimhoji mmoja wa wageni aliyefika kutoa zawadi maalum kwa maharusi..
   Mkono wa pongezi....
   Kamati kwa pamoja na maharusi.....
   Mama Mafoto akipata matukio ukumbini hapo....
  Mwisho wa siku ilikuwa na Twist kama hivi ama veeeeeepeeeeee.....
  . Picha na www.sufianimafoto.com

  0 0


  Mmoja wa Wakurugenzi wa Mtandao wa Asasi za Kiraia za Uangalizi wa Chaguzi (TACCEO), Hebron Mwakagenda (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Dar es Salaam leo mchana, kuhusu Polisi kudaiwa kufanya uvamizi na kuwakamata waangalizi, vifaa binafsi na vifaa vya Kituo cha Uangalizi wa Uchaguzi Mkuu wa 2015 katika kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mbezi jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urrio na Kaimu Mkurugenzi wa Utetezi wa LHRC, Anna Henga

  Kaimu Mkurugenzi wa LHRC, Imelda Urrio (wa tatu kutoka kushoto), akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kutoka kulia na Mwanasheria wa LHRC, Halord Sungusia, Mwakilishi wa Taasisi ya YPC, Maria Kayombo na Mwakiliashi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP),Melikizedeck Karol.
  Mkutano na waandishi wa habari ukiendelea.

  TACCEO yalaani kukamatwa waangalizi wa uchaguzi


  Na Dotto Mwaibale

  ASASI za Kiraia za Uangalizi wa Uchaguzi (TACCEO), pamoja na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), wamelaani kitendo cha kuvamiwa na Jeshi la Polisi, Oktoba 29, mwaka huu na lile la kukamata vitendea kazi na waangalizi wa uchaguzi  36.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo mchana, Kaimu Mwenyekiti wa TACCEO, Hebron Mwakagenda, alisema Jeshi la Polisi lilivamia kituo cha LHRC, kilichopo Mbezi na kudai kuwa, waliagizwa na mamlaka husika kuwakamata waangalizi  na vifaa vya kieletroniki vilivyokuwa vikitumika katika mchakato huo.

  Mwakagenda alisema polisi hao waliongozwa na Mkuu wa Upelelezi Wilaya  ya kipolisi Kawe, ASP Mgonja, ambapo  maofisa wa uangalizi walieleza kuwa, walipata taarifa kituo hicho kinakusanya na kunasambaza taarifa za matokeo zisizo rasmi.

  "Katika mchakato huo, polisi walikusanya vifaa vyetu na kukamata kompyuta za mezani 24, mpakato tatu na simu za mkononi za waangalizi 25," alisema Mwakagenda.

  Alisema baada ya tukio hilo, vifaa hivyo vilichukuliwa na kukabidhiwa kituo cha kati na baadaye kupelekwa makao makuu ya jeshi la polisi huku, baadhi ya waangalizi wakichukuliwa kwa ajili ya kutoa maelezo na baadaye kupata dhamani.

  Watu hao wametakiwa kurudi kituoni hapo Oktoba 30, mwaka huu kwa ajili ya kumalizia maelezo yao.

  "Mchakato huo la kurudi Oktoba 30, mwaka huu lilifanikiwa na kwa sasa waliambiwa warudi leo, kwa taratibu nyingine za kipolisi," alisema Mwakagenda.

  Mwakagenda alisema uvamizi huo uliofanywa na jeshi la polisi ni wa kudhoofisha ustawi wa demokrasia nchini kwani, wasababisha kuwatishia wananchi kushiriki katika mambo yanayohusu mchakato wa chaguzi nchini.

  "Katika hili ni kama wameondoa dhana nzima ya ushiriki kikamilifu wa sekta ya umma na binafsi   katika kutoa maoni ya kuboresha demokrasia na uchaguzi," alisema Mwakagenda.

  Aidha, Mwakagenda alisema uvamizi huo uliathiri  na kuwafanya wakashindwa kukusanya taarifa za mwisho za uangalizi wa matokeo na ukusanyaji wa maoni ya wananchi.

  "Uangalizi kwa kutumia tehama haujaanza mwaka huu kwani, tangu mwaka 2010 kulikuwa na utaratibu huu, mambo yaliyofanyika hivi sasa tunashindwa kuelewa tatizo ni nini," alisema.

  (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com

  0 0


  indexCHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo nchini (TASWA), kinatoa pongezi za dhati kwa Dk. John Magufuli kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Tanzania.

  TASWA imepokea kwa furaha ushindi huo wa Dk. Magufuli, ikiamini atawapa furaha wanamichezo katika masuala mbalimbali kama alivyofanya mtangulizi wake Rais, Jakaya Kikwete ambaye anamaliza muda wake wa kuwatumikia Watanzania kwa mujibu wa katiba na ataanzia pale mtangulizi wake alipoishia kuhusiana na michezo kwa ujumla.

  Kutokana na hali hiyo tunampongeza Rais Mteule Dk. Magufuli na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan, ambaye atakuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kushika wadhifa wa Makamu wa Rais hapa nchini.

  Tunaamini watakuwa tumaini kubwa la wanamichezo na tunaahidi kuwapa ushirikiano wa kutosha ili watekeleze majukumu yao ipasavyo upande wa michezo.Pia TASWA inawapongeza wadau wote wa michezo waliochaguliwa kwa nafasi mbalimbali za Ubunge na Udiwani na tunaamini ushindi wao utakuwa mwanzo mzuri katika kusaidia michezo hapa nchini.

  Tunawapongeza pia wale ambao si wanamichezo, lakini walitumia mgongo wa michezo na wanamichezo kutafuta uongozi wa kisiasa katika nafasi za Ubunge na Udiwani, wakiahidi watasaidia michezo. Nao tunawapongeza na tunasubiri utekelezaji wa ahadi zao.Wanasiasa ndiyo wanaounda Serikali, tena wao ndio wanaofanya uamuzi kutokana na nafasi zao. Watendaji ni wataalamu, na kazi yao ni kushauri au kutoa ushauri. Ushauri ni kitu kimoja, na ushauri kufanyiwa kazi ni kitu kingine pia.

  Hivyo basi tunaamini wanasiasa walioingia wakitokea kwenye michezo wanajua matatizo yaliyoko huko kwa kiasi kikubwa kuliko mwingine yeyote, hivyo wanaweza kusaidia kwa kiasi fulani mawazo ili michezo ipige hatua.
  Juma Pinto.Mwenyekiti TASWA

  0 0

  Aliyekuwa mgombea Ubunge jimbo la Moshi mjini,mfanyabiashara Davis Mosha akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Penfold kwa lengo la kuwashukuru wana CCM waliompigia kura.
  Baadhi ya wana CCM waliohudhuria mkutano huo.
  Mfanyabiashara Davis Mosha akitangaza uamuzi wake wa kutojihusisha tena na siasa,uamuzi uliosababisha wanaccm kushindwa kujizuia na kuanza kuangua vilio.
  Baadhi ya wana CCM wakilia kwa uchungu mara baada ya Davis Mosha kutangaza kutogombea tena Ubunge .
  Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Kilimanjaro,Michael Mwita alilazimika kwenda kumuomba kubadili uamuzi wake huo.
  Vilio havikuwa kwa wanawake peke yao hata wanaume walishindwa kuvumilia.
  Wengine walitishia kujinyonga mbele yake.
  Uamuzi wa Davis Mosha kuamua kutogombea tena Ubunge unatokana na kile alichodai kuwa baadhi ya viongozi wa CCM kushiriki kumuhujumu katika harakati za kuwania ubunge.
  Wengine sura zao zilibadilika zikawa tofauti na zile tulizozizoea.
  Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Moshi,Elzabeth Minde aliingilia kati kujaribu kuomba Mosha kubadili uamuzi wake huo bila ya mafanikio.
  Wanaccm wengine walilazimika kupanda jukwaani bado walizuiliwa.
  Wengine walizimia  na kupatiwa msaada wa huduma ya kwanza.
  Mosha aliondolewa uwanjani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi kutokana na wanachi walioonekana kutofurahishwa na uamuzi wake huo.
  Msafara wake ulisindikizwa na askari Polisi.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0

  1
  Waziri Mizengo Pinda akizungumza wakati alipozindua  Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuuu)
  2
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiliza mfugaji na mtalaamu wa masuala ya ufugaji nyuki na usindikaji asali, Bw. David Kaizilegi Kamala (kushoto) katika maonyesho ya ufugaji nyuki na usindikaji asali yaliyotangulia uzinduzi wa Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania alioufanya kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015.Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa  Kikosi Kazi cha uanzishwaji wa Chama hicho na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Parseko Konne. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Celestine Gesimba na Kulia kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa.
  3
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama sabuni, mafuta na vipodozi vinavyotengenezwa kwa kutumia mazo ya nyuki kaba ya kuzindua Chama cha Kuendeleza Ufugaji Nyuki Tanzania kwenye hoteli ya Morena mjini Dodoma Oktoba 30, 2015.

  0 0

   Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa  Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
   Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na Mwenyekiti wa Chama cha UPDP Taifa  Mhe. Fahmi Dovutwa katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
   Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mhe. Anna Mghwira  na wagombea wengine wakiwa  katika chumba cha VIP cha ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
   Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan wakiwa na  wagombea wengine wakielekea  ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
   Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan na Mhe Anna Mghwira na  wagombea wengine wakielekea  ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
   Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan na Mhe Anna Mghwira na  wagombea wengine wakielekea  ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  tayari kwa hafla ya kukabidhiwa hati ya Urais na Makamu wa Rais
   Viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi chini ya Jaji Damia Lubuva wakiwa tayari katika sehemu yao
   Meza kuu
   Mke wa Rais Mteule Mama Janet Mgufuli akisalimiana na Waziri wakuu wastaafu Mzee John Malecela na Jaji Joseph Sinde Warioba 
   Mama Janet Magufuli akisalimiana na Mama Salma Kikwete
   Rais Kikwete akisalimiana na Mama Janet Magufuli
   Mkrugenzi wa Uchaguzi Mhe. Kailima Ramadhani akisoma muhtasari wa ratiba
   Meza ya viongozi
   Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama 

   Sehemu ya viongozi wa  taasisi mbalimbali na wastaafu
   Viongozi wa Taasisi mbalimbali
   Viongozi wa Taasisi mbalimbali
   Viongozi wa Taasisi mbalimbali
   Viongozi wa Taasisi mbalimbali na wananchi waliohudhuria
   Viongozi wa Taasisi mbalimbali
   Viongozi mbalimbali
   Viongozi wa Taasisi mbalimbali
   Viongozi wa Taasisi mbalimbali
   Viongozi wa Taasisi mbalimbali za umma na binfasi
   Viongozi wa asasi mbalimbali za umma na binafsi
   Wananchi kutoka sehemu mbalimbali
  Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing akiwa ameketi na wananchi
   Sehemu ya wananchi na makada wa CCM
   Sehemu ya wananchi na makada wa CCM
   Sehemu ya wananchi na makada wa CCM
   Wanahabari
   Sehemu ya watumishi wa Tume ya Uchaguzi
   Sehemu ya watumishi wa Tume ya Uchaguzi
   Sehemu ya watumishi wa Tume ya Uchaguzi
   Wananchi toka sehemu mbalimbali
   Wanahabari na wananchi 
   Wananchi wakiwa na furaha
   Wananchi
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akisoma hotuba yake
   Wananchi wakimsikiliza Jaji Damina Lubuva

   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akisoma hotuba yake
   Viongozi wa dini  na wananchi wakisikiliza
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akisoma hotuba yake
   Vifijo toka kwa viongozi
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akisoma hati kabla ya kuikabidhi wa Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mhe Samia Suluhu Hassan
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akisoma hati kabla ya kuikabidhi wa Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mteule Mhe Samia Suluhu Hassan. Kulia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi Mhe. Kailima Ramadhani
   Wanahabari wa ndani na nje ya nchi wakirekodi tukio hilo la kihistoria
   Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akionesha hai ya Urais akiwa na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan, Jaji Damian Lubuva na Mhe Kailima Ramadhani
   Rais Mteule Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akionesha hai ya Urais akiwa na Makamu wa Rais Mteule Mama Samia Suluhu Hassan, Jaji Damian Lubuva na Mhe Kailima Ramadhani
   Viongozi wakishuhudia tukio hilo kwa furaha
   Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Lubuva akisoma hati ya Makamu wa Rais
   Makamu wa Rais Mteule Mhe Samia Suluhu Hassan akipokea hati  yake
    Makamu wa Rais Mteule Mhe Samia Suluhu Hassan akionesha  hati  yake
   Rais Mteule na Makamu wake mteule wakipongezwa baada ya kukabidhiwa hati
   Rais mteule akipongezwa na waliokuwa wagombea wa Urais wa vyama vingine
   Rais Mteule Dkt Magufuli akimuonesha Mhe Anna Mghwira cheti cha Urais
   Rais Kikwete akimpongeza Rais Mteule
   "...Cheti ndiyo hiki...." anasema Rais Mteule kwa Rais Kikwete
   Wakikionesha cheti kwa furaha
   "....Huyu ndiye our new boss..." anasema Rais Kikwete
   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais
   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais
   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais
   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais
   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais
   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais
   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais
   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais


   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais

   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais
   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais na kupeana mikono na Rais wa Zamani wa Nigeria Mhe Goodluck Jonathan

   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais kwa mabalozi
   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli akipita kuonesha cheti chake cha Urais
   Makamu wa Rais Mteule Mhe Samia Suluhu Hassan akipongezwa
   Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mhe Anna Mghwira akiongea kwa niaba ya wagombea wengine wa vyama mbalimbali  walioshiriki kwenye kugombea Urais
   Wanahabari
   Rais Mteule akimpongeza Mhe Anna Mghwira kwa hotuba nzuri
   Rais Mteule Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na viongozi wa tume na vyama vya siasa
   Wateule na Tume ya Taifa ya Uchaguzi


  0 0

   
   Mbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) akiwashukuru wananchi wa Kata ya Ndebezi katika jimbo hilo kwa kumpa kura za kishindo, madiwani na Dkt. John Magufuli aliyekuwa anawania kiti cha urais.
   
   Wananchi wa Kata ya Ntobo wakishangilia kwa furaha mara baada ya  Mbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) alipowasili eneo hilo kwa kutoa shukrani kwa wananchi hao kwa kumchagua katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.
  Akizungumza na wakazi wa Kata ya ChomaMbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) alisema ushindi wa kura 31,485 sawa na asilimia 67. 65 aliopewa na wana Manonga dhidi ya Ally Nguzo wa Chadema aliyepata kura 14,420 sawa na asilimia 30.96. Amesema atahakikisha anawapa wananchi hao ushirikiano, usimamizi na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakalibi. 
  Mke wa Mbunge Mteule Bi Sarah Abdallah akitoa shukrani kwa wananchi wa kata ya Choma kwa kazi nzuri waliyoifanya.
   Mbunge mteule katika Jimbo la Manonga wilaya ya Igunga mkoani Tabora , Seif Khamis Gulamali (CCM) akiwapungi amkono pamoj a na kuwashukuru wananchi wa kata ya Mwashiku kwa kuonesha upendo wa dhati baada ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo ilo
  Hakika ilikuwa ni siku ya furaha kwa wakazi wa jimbo la Manonga

  0 0

  Pr. Mwakabonga akiongoza ibada ya kumbukumbu ya marehemu Godfrey Mbiu Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekani na kuhudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wakiwemo wafanyakazi wa kituo cha utangazaji Sauti ya Amerika idhaa ya Kiswahili (VOA). Marehemu Godfrey Mbiu Mngodo aliaga Dunia Tarehe 11 Septemba, 2015 Dar es Salaam na kuzikwa Tanga. Godfrey Mbiu Mngodo amefanya kazi katika sehemu mbalimbali kama Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD), Voice of America, wizarani na kituo cha Channel Ten ameacha watoto 10 na wajukuu 14. PICHA NA KWANZA PRODUCTION/VIJIMAMBO
  Mmoja ya mtoto wa marehemu Michael Mngodo akiwa na mwanae Alvin wakifuatilia ibada ya kumbukumbu ya mpendwa baba yake marehemu Godfrey Mbiu Mngodo iliyofanyika siku ya Jumamosi Octoba 31, 2015 Columbus, Ohio nchini Marekani.
  Familia ya Mngodo ikifuatilia Ibada.
  Pr. Mwakaboma akifanya maombi kwa wanafamilia.
  Michael Mngodo akisoma wasifu wa mpendwa baba yake. Kulia ni mtoto wake Alvin.
  Ndugu, jamaa na marafiki wakifuatilia ibada. Kwa Picha zaidi bofya HAPA

  0 0

   Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazee wastaafu, Wakulima na Wafanyakazi  Zanzibar Mzee Ali Hassan Khamis akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hali ya nchi ilivyo sasa na kuwataka wananchi kusikiliza maelekezo yatakayotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Picha na Makame/Maelezo Zanzibar.

  RAMADHANI ALI /MAELEZO ZANZIBAR                    
  Jumuia ya Wazee wastaafu, Wakulima na Wafanyakazi  Zanzibar imewashauri wananchi  kuwa watulivu wakati huu na kusikiliza maelekezo yatakayotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  (ZEC) baada ya  Menyekiti wa Tume hiyo kufuta uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25.10.2015.

  Akitoa tamko  juu ya hali halisi iliyojitokeza  katika uchaguzi huo mbele ya waandishi wa Habari, katika Ukumbi wa Redio Swahiba Migombani, Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mzee Ali Hassan Khamis alikubali kuwa uchaguzi umevurugika  na lililobaki kwa sasa ni kusikiliza miongozo ya ZEC ili kusawazisha kasoro iliyotokea.Mzee Ali Hassan alisema  Tume ya Uchaguzi ndio ya kulaumiwa katika kuharibika kwa uchaguzi wa Zanzibar licha ya juhudi kubwa iliyofanya ya kusimamia uchaguzi huo katika hatua za awali.

   Alishauri kumalizwa  tatizo lililopo na wananchi wenye wa Zanzibar bila ya kushirikisha Jumuiya za Kimataifa kwani baadhi ya wakati  maamuzi yao yanakuwa katika ushabiki wa kisiasa.

  Amesema Jumuiya ya Wazee  wastaafu, wakulima na wafanyakzai inaunga mkono kurejewa kwa uchaguzi wa Zanzibar  na hatua hiyo sio jambo kigeni kwa Zanzibar kwa vile imewahi kutokea katika miaka ya siti.Mzee Ali Hassan aliwapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kushiriki vizuri katika uchaguzi huo kuanzia hatua ya kampeni na kupiga kura  katika misingi ya amani na utulivu.

  Aidha alimpongeza Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Magufuli kwa ushindi aliopata na kuwataka wananchi wote kumuunga mkono katika juhudi za kuleta maendeleo kwa wananchi wote.Aliwataka viongozi wa vyama vya siasa na wananchi kwa kujumla kusahau tofauti  zilizojitokeza wakati wa kampeni  na  wakati wa kupiga kura  na kuelekeza mawazo yao katika kujenga Tanzania mpya.

  0 0

  Na:George Binagi-GB Pazzo.
  Shule ya Msingi Green Hill iliyopo Ilala Mkoani Dar es salaam imekuwa miongoni mwa shule bora zilizofanya vizuri katika mtihani wa darasa la saba, uliofanyika mwezi Septemba mwaka huu kote nchini.


  Katika Matokeo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani nchini NECTA Dk.Charles Msonde, ufaulu wa Kitaifa mwaka huu umepanda kwa asilimia 10.85 kutoka asilimia 56.99 za mwaka jana, ambapo wanafunzi waliofaulu ni 518,034 kati ya 775,273 waliosahiliwa mwaka huu.


  Kwa upande wa Matokeo ya Msingi Green Hill, Matokeo yanaonyesha kuwa shule hiyo imeshika nafasi ya saba kati ya shule 56 katika Wilaya ya Ilala, nafasi ya 39 kati ya shule 634 katika Mkoa wa Dar es Salaam na nafasi ya 324 kati ya shule 16,096 Kitaifa.  Wahitimu wote 93 wa shule hiyo wakiwemo wa kume ni 45 na wa kike 48 wamefaulu mtihani wao kwa madaraja yote ya ufaulu jambo lililofanya shule hiyo kupokea pongezi mbalimbali kutoka kwa wazazi na walezi wa wahitimu hao kwa njia mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii.

  TAZAMA HAPA UFAULU

  0 0

  Na:George Binagi-GB Pazzo & Vesterjtz.

  Mbunge Mteule wa Jimbo la Nyamagana Mkoani Mwanza kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Stanslaus Shing’oma Mabula, amewahakikishia Machinga Jijini Mwanza kuwa wataendelea kufanya biashara zao katika maeneo mbalimbali ya katikati ya Jiji hilo kama yaliyotengwa na uongozi wa halmashauri.


  Mabula aliyasema hayo jana wakati akiwashukuru wakazi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa mbunge wao katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Mbugani, kufuatia uvumi unaoezwa mitaani kwamba machinga pamoja na mamantilie wataondolewa katikati ya Jiji la Mwanza kufuatia ushindi wake.


  “Mtu kaenda Makoroboi, Stand ya Tanganyika, Sahara, Soko la Igoma pamoja na maeneo mengine na kuwaambia Machinga na Mamantilie kuwa Mabula ameingia madarakani, cha moto mtakiona. Nataka msikilize kauli yangu leo kwamba sikuja kuitengua torati, nitaendelea kushirikiana na ninyi ili muwe bora, tena zaidi ya miaka mitano iliyopita”. Alisema Mabula.


  Katika hatua nyingine Mabula amewashukuru wakazi wa Jimbo la Nyamagana kwa kumuamini na kumchagua kuwa mbunge wao, kwani wakati akiwa  Mstahiki wa Jiji la Mwanza yeye pamoja na wanaccm wenzake walisemewa mambo mengi mabaya ambayo kimsingi hayakuwa na ukweli wowote.


  “Wamama walinyanyasika sana, walitemewa mate, walichaniwa nguo, walipondwa mawe, walitukanwa, walidharirishwa. Pia tulisemewa na kushuhudiwa uongo kila kona. Ninyi wenyewe mnakumbuka tuliambiwa tumevunja matorori, tumeiba maandazi , lakini nawashukuru maana wananchi wa Nyamagana walisema huyo huyo alieiba maandazi, kumwaga mchele na kuvunja matorori ndie atakuwa mtetezi wetu.

  Nae Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Miraji Mtatu, aliwashukuru Watanzania wote kwa kukichagua chama hicho kuanzia ngazi ya Madiwani, Wabunge pamoja na Rais ambapo Dkt.John Pombe Magufuli aliibuka na ushindi wa asilimia 58.46


  Katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita ya Octoba 25 kote nchini, Mabula aliibuka mshindi katika Jimbo la Nyamagana kwa kupata kura 81,017 na hivyo kumuondoa aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Ezekiel Wenje kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema aliepata Kura 79,280.


  0 0
 • 11/01/15--09:19: 2 of 5 SIKU YA MARUHANI
 • Na Swahilivilla blog. Washington D.C
  Jana ililkuwa ni "Siku ya Maruhani" nchini Marekani. Siku hii ijulikanayo kama "Halloween" husherehekewa kila tarehe 31 Oktoba, na ina historia ndefu.
  Siku ya Maruhani ilianzia huko barani Ulaya kiasi miaka 2,000 iliyopita ikifungamana na imani za kishirikina. Wazung walipoyavamia mabara ya Amerika walihamia pia na utamaduni mila, desturi, dini, na silka zao - na sema upendavyo. Miongoni mwa hayo ilikuwa ndiyo hii siku ya Maruhani ambayo jina lake la asili ni "Samhein".
  Sherehe za Maruhani  Photograph by treasuredragon/iStock.
  Tuyaachie ya historia kwa wanahistoria, lakini kwa ufupi hii iliaminika kuwa ni siku ambayo pepo, majini, maruhani, mazimwi na mizimu au mizuka ya watu waliokufa hurejea hapa duniani katika maeneo yao ya asili na kujichanganya na watu waliohai.
  Maudhui kuu ya siku hii ni kutisha, kuadhibu na mauti, ingawaje katika enzi zetu za leo imekuwa ni siku kuu ya watoto zaidi kuliko watu wazima. Sherehe zake hufanyika kuanzia familia, mitaa, makazini na hadi kufikia Ikulu yenyewe. Rejea kwenye toleo la jana la Swahilivilla uone Ikulu ya Marekani ilivyoadhimisha siku hii akiwepo rais Obama na familia yake.
   Wana maruhani wakiwa katika kwaride. (Photo Jefferson Siegel/New York daily news)
  Kama ambavyo kila siku kuu au sherehe huwa zinaaambatana na ada maalum ambazo zikikosekana basi siku hiyo huwa kana kwamba haijatimia, Siku ya Maruhani nayo pia ina ada na desturi zake. Na kama zilivyo sherehe nyingi hapa Marekani siku hii pia nayo imekuwa fursa ya wafanyabiashara kujipatia rizki zao.
  Mapambo: Shamra shamra za Siku ya Maruhani huanza mapema, pengine tangu mwezi wa Septemba kwa kuweka mapambo kwenye majumba, mabarabara na hata sehemu za kazi na biashara. 
  Na kama tulivyotangulia kusema, mapambo yote huwa yanalenga kwenye hali ya kutisha, kuadhibu na mauti. Miongoni mwa mapambo hayo ni buibui na nyumba zao, popo wakining'inia, mifupa na mabufuru ya vichwa vikiashiria watu waliokufa, panga, paka weusi, masanamu ya mizuka au mazombi na vimbwanga vyengine. Almradi kuonesha kuwa nyumba zimesibiwa na maruhani (haunted house). Si hasha ukapita vichochoroni ukakutana na kitu ukashtuka. Kwa ufupi ni kama vile tunavyoona kwenye picha za kutisha (scary movies).
  Halloween Live HD Image
  Maboga yaliotengenezwa kwajili ya Maruhani
  Maboga nayo ni sehemu muhimu katika Siku ya Maruhani. Hukaushwa, kutobolewa kwa mitindo maalum na kupakwa rangi na kuwa katika umbo la kutisha, kisha kutiwa mshumaa ndani. Boga hili maarufu huitwa kandili ya Jack 'O (jack-o’-lantern). Kiasili, mshumaa uliondani unaashiria roho iliyoko kifungoni ikiadhibiwa.
  Mavazi (Costumes): Inaaminika kuwa Wazungu wa kale huko Ulaya, walikuwa wakivaa mavazi ya kutisha katika siku hii ili kuwababaisha pepo, majini, maruhani na mazimwi wanapokuja, wadhani kuwa ni wenzao na hivyo kuwaacha na kutowadhuru. Kwa hivyo mpaka leo mavazi ya siku hii huwa ni ya kutisha, na watu hutembea kama mizuka, mazimwi (mazombi) au mtu aliyechagawa. 
  Makazini watu huruhusiwa kuvaa mapambo maalum ya kutisha almradi hayahatarishi usalama. Utawakuta watu wamejipaka masinzi, au rangi za ajabu ajabu mwilini, kuvaa masoksi usoni, kuvaa mavazi ya kivita na silaha zao na vikorobwezo vyengine. Baadhi ya sehemu za kazi hufanya mashindano maalum kuchagua mshindi wa mavazi bora ya siku hii.
  Trick-or-Treat
  Trick-or-Treat: Kama tulivyogusia hapo awali kuwa Siku ya Maruhani imekuwa ni siku kuu ya watoto zaidi kuliko watu wazima. Kwa hivyo, wakati wa jioni watoto wakiwa wamevalia mavazi yao ya kutisha hupita mitaani, nyumba hadi nyumba, kubisha hodi na kutoa mzaha wa vitisho (trick) kwa wenye nyumba iwapo hawatopewa zawadi (treat). 
  Mara nyingi hupewa zawadi ambayo zawadi maarufu ni peremendi au vitu vyengine vitamu. Baadhi ya watu huweka ishara maalum kwenye milango ya nyumba zao kuashiria kuwa zawadi zimejaa ndani, au huziweka mlangoni kama chano au tambiko kwa maruhani, na watoto wenye bahati ya kupita mwanzo hufaidika, na hivyo mwenye nyumba kunusurika na kitisho, au nyumba yake hunusurika isisibiwe.
  Kwa mujibu wa wanahistoria, inaaminika kuwa huko kale, majini na maruhani walipokuwa wakiingia mitaani siku hiyo huko Ulaya, watu walioshindwa kuwababaisha kwa mavazi yao, basi walikuwa wakiwapa zawadi au muhanga ili wawaachie na wasiwadhuru.
  Patry ya Maruhani (Photo: Aaron Favila, AP)
  Maparty nayo hufanyika, yakitawaliwa na michezo ya kuigiza ambayo maudhui zake kuu ni zile za kutisha, kuadhibu na mauti. Halkadhalika vipindi vya televisheni na redio pia hutawaliwa na maudhui ya Siku ya Maruhani zikiwemo nganu na picha za kutisha.
  Baadhi ya watu huitumia vibaya siku hii kwa kufanya vitendo vya kihalifu. Mpaka wakati tukiingia mitamboni bado hatujapata ripoti kamili ya vyombo vya usalama nchini Marekani kukhusu matukio ya kihalifu yaliyoripotiwa hiyo jana. Tuombe salama iwe hakuna mtu yoyote aliyedhurika.
  Lakini, ikiwa hakuna matukio yoyote mabaya yaliyotokea nchini humu, basi jinamizi la Siku ya Maruhani kwa mwaka huu litakuwa limeikumba Zanzibar. Kwani kinyume na Marekani na Ulaya ambako maruhani, majini, pepo na mazimwi hushuka kila mwaka, kwa Zanzibar hushuka kila baada ya miaka mitano. Na kwa vile hushuka kila baada ya muda huo, basi yakishuka huwa makali zaidi. Mwaka huu yameshuka yakiwa yamevalia mavazi ya kutisha, masoksi na masinzi nyusoni na silaha nzito nzito na vimbwanga vyengine yakibisha hodi milangoni na kusema "trick-or-trick". 
  Wazanzibari walikuwa wamezoea kuyapa peremendi, pipi na zawadi nyenginezo iwapo watashindwa kuvaa mavazi ya kuyababaisha ili yawaachie kuendelea kuishi angalau katika hali duni. Lakini mwaka huu Wazanzibari wamesema ng'o! Wamekataa kutoa chano, na kwa hivyo tayari yamevinjari kutaka kuwadhuru.
  Sherehe za hapa na pale zimekuwa zikiripotiwa, na vyombo vya khabari navyo vimekuwa vikitenga muda maalum kutangaza michezo ya kuigiza na nganu zenye maneno ya kutisha kama vile "hatutoi", "watarudi" na mengineyo. 
  Lakini Wazanzibari wamesimama kidete na wamekataa kutoa muhanga.
  Zanziba imekuwa nyumba iliyosibiwa na maruhani "haunted house". Ukipita mitaani siku hizi unaweza kumezwa na mazimwi, maruhani, majini au viumbe vyengine vya khatari, na roho za Wazanibari zimo kifungoni zikiadhibiwa bila kosa lolote lile. 
  Wamekuwa wakitoa muhanga na vyano kwa viumbe hao wa ajabu kwa miaka mingi mpaka khazina zao zimekauka, na sasa hawana walichobakiwa nacho ispokuwa imani zao thabiti kwa Mwenyezi Mungu na nyoyo za kizalendo.

  0 0

  Baadhi ya walimu wa Mkoa wa Manyara wakishikana mikono kwa lengo la kuonyesha umoja na mshikamano daima kwenye maadhimisho ya siku ya mwalimu ambapo kwa mkoa huo zilifanyika mji mdogo wa Mirerani.
  Mwenyekiti wa chama cha walimu nchini (CWT) Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Abraham Kisimbi akizungumza kwenye sherehe za siku ya mwalimu ambapo kwa mkoa huo zilifanyika mji mdogo wa Mirerani.
  Walimu wa Mkoa wa Manyara, wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro, Mahamoud Kambona wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya mwalimu ambayo kimkoa ilifanyika mji mdogo wa Mirerani.
  Mwenyekiti wa chama cha walimu nchini (CWT) Mkoani Manyara, Qambos Sulle akizungumza kwenye sherehe za siku ya mwalimu ambapo kwa mkoa huo zilifanyika mji mdogo wa Mirerani.
  Mwenyekiti wa chama cha walimu nchini (CWT) Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Abraham Kisimbi akizungumza kwenye sherehe za siku ya mwalimu ambapo kwa mkoa huo zilifanyika mji mdogo wa Mirerani.

  0 0
 • 11/01/15--10:07: STATE HOUSE STATEMENT


 • THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
  DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  Telephone:255-22-2114512, 2116898
  Website : www.ikulu.go.tz              

  Fax: 255-22-2113425  RESIDENT’S OFFICE,
        STATE HOUSE,
                1 BARACK OBAMA ROAD,  
  11400 DAR ES SALAAM.
  Tanzania.
   


  STATE HOUSE STATEMENT

  The State House has learnt, with regret, claims by the Secretary General of the Civic United Front (CUF) and its Presidential candidate in this year’s General Elections in Zanzibar, Honorable Seif Shariff Hamad, that he has been ignored and his request for an appointment with President Jakaya Mrisho Kikwete, to discuss the political situation in Zanzibar, turned down.


  The State House would like to categorically deny that it has received any request from Honorable Hamad for him to meet President Kikwete since voting day in Zanzibar on Sunday and subsequent nullification of the election process in Zanzibar by the Zanzibar Electoral Commission (ZEC) Chairman Jecha Salim Jecha on Tuesday.


  What President Kikwete has received, are complaints by CUF about some actions from some sections of the Police Force in Zanzibar and a request for him to facilitate a conversation between Honorable Hamad and the Chief of the Armed Forces (CDF) General Davis Mwamunyange.


  Subsequently, President Kikwete, who is also Commander-in–Chief, has instructed the Inspector-General of Police Ernest Mangu to investigate these claims by CUF and report back to him. Accordingly, he has also instructed his office to facilitate a conversation between General Mwamunyange and CUF officials. 


  The State House would like to confirm that President Kikwete is as concerned about the political and security situation in Zanzibar as every Tanzanian is, and has been working tirelessly and consulting widely over the last few days to find amicable and peaceful resolution to the situation in Zanzibar.


  While the matter remains firmly in the hands of an independent electoral body in Zanzibar, President Kikwete would like to express his readiness to do whatever is in his powers to regularize the situation in Zanzibar.

  ISSUED BY THE DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

  STATE HOUSE

  DAR ES SALAAM.

  31, OCTOBER, 2015

  0 0


  Mtoto Careen Modest Kassuw pichani, ana umri wa mwaka mmoja, amezaliwa ana tatizo la Moyo ukiwa na matundu mawili na valvu zake nyembamba  zimebana kiasi  hivyo analazimika kusafirishwa kwenda India kwa matibabu.

  Wazazi wa mtoto huyo wanaomba msaada wako wewe Mtanzania kwa atakayeguswa ili wafanikishe gharama za matibabu ya mtoto Careen ambayo ni Shilingi Milioni 30 zinahitajika ili kuokoa maisha yake.
  Ewe Mtanzania, ewe mzazi tunaomba mchango wako wa hali na mali, kwa atakayeguswa tunaomba utume mchango wako kwa mama mzazi wa mtoto huyo Eunice kwa namba0713 034866 au kwa namba 0715 083055
  Mungu awabariki wote mtakaochangia kwa njia moja au nyingine.

  0 0

  IMG-20151030-WA0039
  : Kipindi extended na bonyeza play hapa chini

  0 0

  Baraza la Mitihani Tanzania - NECTA limetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba iliyofanyika September 9 na 10 mwaka huu ambapo mikoa ya kanda ya ziwa imefanya vizuri ikilinganishwa na mikoa mingine nchini. 
  Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dk. Charles Msonde amesema jijini Dar es salaam kuwa  jumla ya watahiniwa 51,8034 kati ya 76,3602 wamefaulu sawa na asilimia 67.84, ambapo kati yao wasichana wamefaulu kwa asilimia 64.60 na wavulana asilimia 71.58 huku kiwango hicho cha kikiongezeka kwa asilimia 10.85 ukilinganisha na ufaulu wa mwaka jana wa asilimia 56.99. 

   Dk. Monde amezitaja shule zilizofanikiwa kuingia kumi bora kitaifa mwaka huu ni pamoja na shule ya Waja Springs ya Geita iliyoshika nafasi ya kwanza ikifuatiwa na Enyamai ya Mara na Twibhoki pia ya Mara katika nafasi ya tatu huku zikifuatiwa na shule nyingine 7 zote kutoka mikoa ya kanda ya ziwa. Shule ya Mwashigini ya mkoani shinyanga imetajwa kushika nafasi ya mwisho. 

   Katika hatua nyingine Dk. Msonde amezungumzia pia kukamilika kwa maandalizi ya mitihani ya kidato cha nne ambayo itafanyika kuanzia nov mbili hadi 27 mwaka huu na kuwataka wasimamizi pamoja na watahiniwa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu ili kuepuka kufutiwa mitihani hiyo.

   Kwa kuwa mitihani hiyo inafanyika tanzania bara na visiwani Dk Msonde amewatoa hofu watahiniwa wa Zanzibar ambako kuna hofu ya uvunjifu wa amani kutokana na masuala ya kisiasa kuwa mitihani hiyo itaendelea kama kawaida kwani suala la ulinzi limeimarishwa. 
  BOFYA jina la Mkoa kupata matokeo yake
  ARUSHADAR ES SALAAMDODOMA
  IRINGAKAGERAKIGOMA
  KILIMANJAROLINDIMARA
  MBEYAMOROGOROMTWARA
  MWANZAPWANIRUKWA
  RUVUMASHINYANGASINGIDA
  TABORATANGAMANYARA
  GEITAKATAVINJOMBE
  SIMIYU

older | 1 | .... | 677 | 678 | (Page 679) | 680 | 681 | .... | 1904 | newer