Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

UN TANZANIA YAZINDUA RIPOTI YA MAENDELEO DUNIANI 2013 IKIONYESHA NCHI ZINAZOENDELEA 40 ZIMEPIGA HATUA KUBWA SANA YA MAENDELEO YA BINADAMU.

$
0
0
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akitoa hotuba ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 - Kuchomoza kwa Nchi za Kusini: Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai akisema kwa mujibu wa ripoti hii mwaka huu iaonekana kuwa Tanzania tumefanya vizuri na kiwango chetu kimeongezeka kama ngazi mbili ikilinganishwa na ripoti iliyopita.

Hata hivyo amesema kwa bado kuna mikoa mingi ambayo unapopima maendeleo kwa ujumla wake mikoa mingi ipo asilimia 20 hadi 30 ambapo hii inapima ujumla wa maendeleo katika Jamii. Bw. Lyimo amesema kwa sasa serikali ina mipangp mizuri ya kuisaidia mikoa hiyo, akitolea mfano kilimo kuwa kuanzia miaka ya 80 hatukuiangalia vizuri tulikuwa na taasisi za kilimo, mashirika ya maendeleo ya viwanda lakini katika kipindi hiki cha mageuzi tumepata matokeo mazuri.

Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Peniel Lyimo akikata utepe kuzindua rasmi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 ikiainisha Kuchomoza kwa Nchi za Kusini:Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai akiwa na Mratibu Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Sasa imezinduliwa rasmi.
Mratibu Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani ya mwaka 2013 ikiainisha Kuchomoza kwa Nchi za Kusini:Maendeleo ya Binadamu katika Dunia Anuwai ambapo amesema sera kabambe, zilizotengenezwa vizuri zinaweza kufanya mafanikio ya kimaendeleo ya binadamu kuwa endelevu katika miongo ijayo na kupanuka kufikia nchi nyingi zaidi zinazoendela.

Lakini pia Dkt. Kacou ameonya hatua za kubana matumizi zisizo na mtazamo wa mbali, zaweza kushindwa kushughulikia hali ya kukosekana usawa, na kukosekana kwa ushiriki wa maana wa jamii na kutishia maendeleo haya kama viongozi hawatachukua hatua za kurekebisha. Aidha amesema baadhi ya mataifa yanayoongoza kwenye nchi za Kusini yanajenga mwelekeo mpya wa kukuza maendeleo ya binadamu na kupunguza tofauti za kimaisha kwa kuweka sera bunifu ambazo zinasomwa na kuigwa sehemu nyingine duniani.


Mkurugenzi Mkazi wa UNDP nchini Tanzania Bw. Phillipe Poinsot akitoa neno la shukrani kwa wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo.

Baadhi ya Wakuu wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa nchini wakimsikiliza Dkt. Alberic Kacou (hayupo pichani) alipokuwa akisoma hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 iliyofanyika jijini Dar leo.


Mshauri wa Uchumi wa UNDP Bw. Amarakoon Bandara akiwasilisha ripoti hiyo na kuifafanua ambapo ameeleza kuwa Nchi za Kusini zinakabiliwa na changamoto ambazo pia inazikabili nchi zilizoendelea za Kaskazini, ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya wazee, shinikizo kwenye mazingira, tofauti za kimaisha katika jamii, kukosekana kwa uwiano kati ya maandalizi ya kielimu na nafasi za kazi na umuhimu wa ushirikishwaji umma na mengineyo, akisena hayo yanahitaji ufumbuzi wa kitaifa na kimataifa ikiwa nchi zinazoendelea zinataka kuendeleza kasi yao ya maendeleo.
Bw. Amarakoon amesema Ripoti hiyo inaonya kuwa namba ya watu walio maskini sana inaweza kuongezeka kufikia watu bilioni tatu ifikapo mwaka 2050, labda tu kama hatua za pamoja kimataifa zitachukuliwa kuzuia maafa ya kimazingira.
Mmoja wa mabalozi akiperuzi Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 baada ya kuzinduliwa rasmi.

Ripoti ya mwaka 2013 inasema kuchomoza kwa Nchi za Kusini ni changamoto kwa taasisi duniani kubadilika na kunaonyesha njia mpya ambazo nchi na maeneo yanaweza kufanya kazi pamoja kukabiliana na changamoto zinazofanana. Wakati taasisi kongwe haziendi na mabadiliko, taratibu mpya zinatokea, ikiwamo mitandao mipya ya ushirikiano ya kitaifa na kimataifa zikiwemo jumuiya za kibiashara, jumuiya za kiulinzi, benki za maendeleo na makubaliano ya nchi kwa nchi.
Baadhi ya Waheshimiwa mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini wakishuhudia uzinduzi wa Ripoti hiyo.
Mwakilishi wa UN Women Tanzania Bi. Anna Collins-Falk.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Mollel Raphael Leckshon akitoa maoni yake juu ya Ripoti ya Maendelo ya Dunia 2013 iliyozinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Prof. Delphin Rwegasira kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akichangia maoni yake baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa.
Wageni waalikwa na baadhi ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini katika uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013.
Mratibu Mkazi wa UN Tanzania Dkt. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na baadhi ya waheshimiwa mabalozi baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Dunia 2013.
Sangita Khadka wa Ofisi ya RCO (kushoto) na Stella Vuzo wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Dunia 2013 iliyozinduliwa rasmi jijini Dar leo katika Hoteli ya Serena.
Kansela wa Ubalozi wa Yemeni nchini Bw. Mohammed Abdulah Al-Dhaifi(kulia) akibadilishana business card na Mshauri wa Uchumi wa UNDP Bw. Amarakoon Bandara mara baada ya uzinduzi huo.
Picha Juu na chini ni Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wakiwapokea wageni mbalimbali wakiwemo Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wanafunzi wa vyuo vikuu, Maprofesa, na wadau wa taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi waliohudhuria uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo Duniani 2013 uliofanyika jijini Dar leo katika Hoteli ya Serena.(Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).

mdau atoa Mapendekezo ya Mfumo wa Elimu hapa nchini

$
0
0

Assalam akaykum
nimeona nichukue nafasi hii nitoe mapendekezo maana sijaona mwananchi kuchangia mawazo kutokana na matatizo yaliyopita ya mitihani Tanzania sasa kwa upande wangu nina haya naomba sana tena sana niwekee japokuwa ni marefu kidogo lakini nahisi ni jambo muhimu:

Mfumo wa Elimu Ningependekeza ungekuwa hivi:

Kuwepo na Tuition Resources (iwepo Online au hata maktaba zetu) ambayo itakuwa na mgawanyiko wa mambo makuu matatu (3) nayo ni haya:
 
1.      1. Syllabuses (Silabas)
2.      2. Lecture Guides (Muongozo wa Kusoma na kusomesha)
3.   3.    (a) Specimen question papers. (Sampuli ya Maswali) (b) Past Question papers and Answers.(Maswali na Majibu ya Mitihani iliyopita)
Mambo ya Nyongeza :
·         Kama kutakuwa na mabadiliko yoyote kwa mtihani ujao uelezwe hapa.(MFANO Masuala mangapi yanatakiwa yajibiwe yameongezeka au kupungua)
·         Kama kutakuwa na Mabadiliko au nyongeza  ya Syllabus vile vile ioneshwe hapa.
·         Ripoti ya Mtihani ambayo ieleze wapi wanafunzi walifanya uzuri na wapi bidii iongezwe na wapi walifanya vibaya.
·         Vidokezo vya kusoma (Reading Tips)
·         Listi ya Vitabu au website za kutafuta material zaidi (Reading lists)
·         Kuwepo na Manual au Mkusanyiko wote wa masomo  ambayo kama kutakuwa na mabadiliko yaelezwe kama nilivoorodhesha hapo juu wapatiwe wanafunzi kwa either bure au pesa kidogo walipie
·         Kuwepo na reward kwa wanafunzi walifanya vizuri na utambulisho mfano watolewe kwenye majarida maalum ya elimu ambayo yatasambazwa bure au hata kwa fee ndogo.
Ufafanuzi kidogo
 
1.       Sylubuses : Zioneshe mgawanyiko wa masomo ambao mwanafunzi akitoka atatoka na ujuzi mfano somo la Biologia
1.       Agriculture iwepo na core unit (masomo ya lazima) na optional zake asipandikizwe mwanafunzi mambo ya Anatomy au Biochemistry au biomechanics pamoja na masomo yanayohusu Agriculture, (information overload).
 
2.       Lecture guides: ambayo itagawika kwa:
(a) Learning outcomes (Mwanafunzi aelezwe umuhimu wa hicho unachomsomesha       
            kwanza kabla hata ya kwenda kwenye mada.
             (b)Indicative contents ( Ambazo zipo kwa number mfano  Somo la Human Resources  
             1.1Definition, 1.2.Work related stress ,1.3 Equality) Hii itamsaidia mtu kukumbuka   
              ambapo akijibu suala la mtihani kuwa topic hii ni topic ya 1.3. au 2.4.au hata  
             akitafuta material online yatamuonesha kuwa soma topic no.1.3 au 3.4 n.k
             (c)Examination tips (Muhimu sana unamueleza mwanafunzi atarajie swali la aina
                gani katika topic hii na jibu la aina gani ajibu)
 
3.        (a) Specimen Question papers ambazo zinakuwepo mwanzo wa mwaka kuonesha mwanafunzi atarajie masuala ya aina gani yatakuja katika mtihani sasa anajifanyia mara kwa mara kujibu maswali haya  kwa kutumia resources mbali mbali na pia zioneshe marks ambazo atapata kwa kila suala atakalojibu .
            (b)Maswali na majibu ya mtihani iliyopita,ni muhimu kwa kuwa unamjengea  
            mwanafunzi jinsi gani ya kujibu masuala au atarajie nini ,
 
Hitimisho
Wengi watasema mfumo wa maswali na majibu wanafunzi watakuwa hawasomi wata solve maswali tu,lakini sio kweli mfano yakiwepo maswali ya somo la Biologia tokea ya mwaka 2005 naamini kujibu mara kwa mara haya maswali yanakujengea confidence na ufahamu vile vile na mara nyingi elimu ni ile ile mambo madogo madogo tu yanaongezeka ambayo hata kwenye mitihani ya ulaya huwekwa kijiswali kidogo tu kimoja cha mark ndogo kutokana ni jambo jipya. Mfumo huu pia unatumika U.K mfano maswali ya interview unatakiwa uyasome na sio uwende interview kichwa kichwa, masuala ya driving lesson unakuwa na CD na vitabu ambayo kwenye mtihani wenyewe yanakuwa hayohayo.

Masuala ya uraia unapewa kitabu unasomeshwa hivo hivo hata masuala ya shule .
Sasa tuchukue mfano wa Driving lesson unajiona unajibu tu maswali lakini utakapoanza kuendesha je halikujii swali ulosolve ukaona aha nilisolve hili swali kuwa round about nikae upande gani sasa je si ujuzi huu?
 
Haya ndio nionayo mimi ila kila mtu ana mawazo yake
Ahsanteni.
Dr.Abdul AE 
University of Huddersfield 

COCA-COLA LAUNCHES COKE ZERO

$
0
0
 Coca-Cola Kwanza Managing Director, Basil Gadzios gives his remarks as Coke Zero is officially launched in Tanzania.
Coca-Cola Tanzania Brand Manager Maurice Njowoka speaks to the media at Coke Zero launch event in Tanzania held at Hyatt Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam.
 A section of invited guests follow attentively the official Coke Zero launch in Tanzania.
 Performance team entertains guests during Coke Zero launch in Tanzania. 
========  ========  =======

COCA-COLA LAUNCHES COKE ZERO



DAR ES SALAAM, Friday 15 March, 2013 – Coca-Cola in Tanzania has expanded its offering of the Coca-Cola range with the launch of Coke Zero. The company now offers regular Coke, Coke Light and Coke Zero in the Tanzanian market as part of its strategy to drive choice and variety to suit different consumer lifestyles and occasion needs.

Coke Zero is a zero-sugar cola with the same great taste as the original Coca-Cola; it is therefore another low calorie option. Coca-Cola Kwanza Managing Director, Basil Gadzios said “the brand gives variety-seeking consumers another unique, great tasting option in addition to Coca-Cola Light. Coca-Cola Zero is a sugar free soft drink sweetened with non-nutritive sweeteners”during the media launch at Hyatt Regency. It will be available countrywide in 500ml Plastic bottle.

Mr Basil added “This launch continues our commitment to providing our consumers with high quality products that fit their taste, occasion and lifestyle needs”.

The launch will be supported by a composite marketing campaign including TV, radio, outdoor, digital and sampling with the tagline “It’s Possible”. Basil said the tagline for Coke Zero advertising and activations originated from the cola’s impressive zero sugar qualities. 

Coca-Cola Brand Manager for Tanzania, Maurice Njowoka said “Coca-Cola Zero has a very different personality from any of our other brands. It’s fresh, edgy, bold and youthful offering consumers exciting surprises when it comes to marketing”. “We believe that Coca-Cola Zero’s taste and personality will appeal to young people who do not want to compromise on flavor or calories.”
The Brand Manager has appealed to consumers and the public to attend the Coca-Cola Zero consumer launch to be held at Coco Beach in Dar es Salaam on Sunday, March 17th, 2013 to celebrate and have an exciting feel of the product.  Apart from Dar es Salaam, Coca-Cola Zero consumer launches will also be done in Mwanza, Moshi and Arusha.

Coke Zero, as it is often referred to, was first launched in Atlanta in 2005 and has posted high sales for the last 5 years straight. Among more than 350 sparkling beverage brands launched since 2001, Coke Zero is one of only six to surpass one percent market share, and the only one to maintain it. 

The brand is available in more than 130 countries and continues to experience strong growth both in the U.S. and around the world -- making it the best-selling addition to The Coca-Cola Company's sparkling beverage portfolio since Diet Coke debuted in 1982. By using irreverent, humorous communication, the brand has established a strong connection with young adult males, a previously untapped market for diet soft drinks.


MADAKRI WA KICHINA WATOA HUDUMA VIJIJINI ZANZIBAR.

$
0
0

 Timu ya Madaktari bingwa kutoka China wakiwa na wenzao wa Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja,huko uzini Wilaya ya Kati Unguja.Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

 Daktari bingwa wa macho kutoka China akimfanyia uchunguzi mtoto Fatuma juma Mzee wa kijiji cha Uzini walipofika kutoa tiba na uchunguzi kwa wagonjwa mbalimbali,huko katika kituo cha Afya Uzini Wilaya ya Kati Unguja.
 Daktari bingwa kutoka China akimdadisi mgonjwa Madari Mgezu bada ya kumueleza matatizo yake yanayo msumbua walipofika kutoa tiba na uchunguzi kwa wagonjwa mbalimbali,huko katika kituo cha Afya Uzini Wilaya ya Kati Unguja.
Badhi ya wagonjwa waliofika katika kituo cha Afya Uzini wakisubiri kuonana na Madaktari bingwa wa China uliofika kutoa tiba na uchunguzi,huko katika kituo cha Afya Uzini Wilaya ya Kati Unguja.
=========   =======  ======
Madaktari wa Kichina watoa huduma vijijini Zanzibar.Na Salum Vuai-Maelezo Zanzibar 16/03/2013..


WANANCHI wa mbalimbali wa Wilaya ya Kati Unguja, wameelezea kuridhishwa kwao na huduma za uchunguzi wa kiafya na tiba zinazotolewa na madaktari wa kujitolea kutoka Jamhuri ya Watu wa China.



Wakizungumza na gazeti hili jana wakati wataalamu sita wa magonjwa mbalimbali kutoka China wakitoa huduma hizo katika kituo cha afya Uzini, wananchi hao walisema, mpango huo ni mzuri kwani unawapunguzia mzigo wa kufuata huduma mjini na kuchukua muda mrefu wakiwa nje ya vijiji vyao.



Hamad Juma, mkaazi wa Mgenihaji, alisifu ubora wa huduma zinazotolewa na madaktari hao, na kusema tiba zao ni mjarabu kwnai zimemsaidia sana kupata nafuu matatizo ya macho yanayomkabili.



“Kwa muda sasa nimekuwa nikitibiwa na madaktari kutoka China katika hospitali kuu ya Mnazimmoja badaa ya kuchomwa jichoni na kitu chenye ncha kali, na leo wamekuja hapa nami nimefuata sawa zaidi”, alifahamisha.



Naye Mtumwa Jabu Khamis, aliyempeleka mtoto wake mwenye matatizo ya kifua, alisema hatua hiyo ni muhimu na inafaa ifanyike kila kipindi kifupi ili kuwafikia wananchi walio wengi na ambao hawana uwezo wa kufuata huduma hizo mjini.



Akizungumzia ujio wa madaktari hao, Sheha wa shehiya ya Uzini Vuai Mgeni Vuai, alisema utaratibu unaofanywa na madaktari hao kupitia Wizara ya Afya, unawapa faraja wananchi wa vijijini, kwa kuwaondoshea usumbufu wa maradhi yaliyoficha na hatimaye kupatiwa tiba.



Alitoa wito kwa wananchi wanapopata taarifa za kufikiwa na madaktari bingwa wa maradhi mbalimbali, wasipuuze kwenda kufanyiwa uchunguzi, kwani huenda wakawa wanaishi na maradhi ambayo hayajajitokeza.



“Siku hizi kuna maradhi mengi, mengine hatuyajui mpaka tuchunguzwe, hivyo ni vyema kunapokuwa na huduma kama hizi, wananchi wafike ili kuchunguzwa na kuelezea matatizo ya kiafya waliyonayo ili yawahiwe mapema”, alisisitiza Sheha huyo.



Mapema, kiongozi wa timu ya madaktari hao Dk. Lu Jian Lin, alisema mpango huo unaofadhiliwa na Serikali ya China, unalenga kuwasaidia wananchi wa Zanzibar kuimarisha afya zao ili waweze kushiriki shughuli mbalimbali za kiuchumi.



Alieleza kuwa, serikali ya nchi yake inatambua uhaba wa madaktari unaozikabili hospitali na vituo vya afya vilivyoko vijijini, hivyo imeamua kwa makusudi kuandaa programu hiyo ya kupeleka huduma katika maeneo hayo Unguja na Pemba.



Aliwashauri wananchi kuchukua tahadhari ili kujiepusha na maradhi mbalimbali, kwa kula chakula bora, kufanya mazoezi ya mwili na kujenga utamaduni wa kuchunguza afya zao kila baada ya kipindi maalum.



Zaidi ya wananchi 250 kutoka shehia mbalimbali za Wilaya ya Kati, walipatiwa huduma hizo kwa kupimwa na kutibiwa maradhi ya macho, pua, kifua, masikio magonjwa ya akinamama na ya mifupa.    

Ajali:Basi la Ndenjela lilivyoteketea kwa moto mapema leo asubuhi likieleka Mbeya kutoka dar

$
0
0



Basi la Ndenjela likiwa linatoka jijini Dar kuelekea mkoani Mbeya  mapema leo asubuhi limeteketea kwa moto kama lionekanavyo pichani,maeneo ya Kibaha-Kongowe. 
kufuatia ajali hiyo ya kusikitisha hakuna mtu aliyepoteza maisha ispokuwa mizigo yote iliyokuwemo ndani basi hilo iliteketea kabisa.

KIFO NI HAKI YANGU

RAIS KIKWETE KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 25 YA HOSPITALI YA KAIRUKI, DAR ES SALAAM, LEO

$
0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, na viongozi wa hospitali ya Hubert Kairuki wakiwa katika picha ya pamoja na vijana waliozaliwa katika hospitali hiyo miaka 25 iliyopita leo Machi 16, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi tuzo kwa kutambua mchango wake mkubwa katika sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo Machi 16, 2013.
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Kumbukumbu ya  Hubert Kairuki, Mama Koku Kairuki akimkabidhi tuzo Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kutambua mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya afya nchini wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali hiyo leo Machi 16, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua rasmi hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki  wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013
 Baadhi ya viongozi wa dini waliohudhuria  sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim wakiangalia watoto wachanga waliotunzwa katika chumba maalum muda mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais Kikwete alipotembelea sehemu mbalimbali  za hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akiwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake leo Machi 16, 2013.

Msanii Mrisho Mpoto akiburudisha wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013.PICHA NA IKULU

CCM MKOA WA VYUO VIKUU latoa tamko lake.!

$
0
0

Mkoa maalum wa vyuo vikuu, kanda ya Dar es salaam, umefanya kikao cha kujadili mipango na mikakati mbalimbali ya kuimarisha Mkoa huo na Chama kwa ujumla. Pamoja na Ajenda hiyo, pia kikao hicho:-

·   Kimelaani vikali matukio ya kuvamiwa, kudhuru mwili na kuuawa kwa baadhi ya viongozi wa Dini na wanahabari. Mkoa umesikitishwa sana na tukio la kushambuliwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) na Mhariri Mtendaji wa New Habari 2006 Ndugu Absalom Kibanda.


·      Lakini pia, kimevitaka vyombo vya Dola kuwakamata, kuwashikilia na kuwachukulia hatua za kisheria wote waliothibitika kuhusika na matukio ya namna hiyo bila kuangalia Itikadi za Kivyama, Cheo ama Kundi. Na pia kuyataka makundi ya kijamii, wanaharakati na wanasiasa kuacha kuingilia/kuvuruga kwa namna yeyote taratibu za kisheria na kiusalama.


·    Pia, kuwataka wanausalama kumhoji kwa kina Dr Slaa juu ya tuhuma zake dhidi ya Kurugenzi ya Usalamawa Taifa (TISS) na kumtaka kuthibitisha madai yake kuwa baadhi ya watendaji wa taasisi hiyo muhimu na nyeti wanaripoti kwake kinyume cha utaratibu, kanuni na maadili ya taasisihiyo.


Kwani tuhuma hizo ambazo Dr Slaa amekuwa akizisema mara kwa mara tangu kipindi cha Kampeni za Urais Mwaka 2010 zimeanza kuaminika, lakini pia zimepelekea wananchi sasa kukosa imani na Taasisi hiyo na zaidi kupoteza imani juu ya uwezo wa serikali kuwalinda na kuwahakikishia Usalama wa maisha yao, ambapo ni jukumu la kikatiba la serikali.

Imetolewana:-

Daniel Zenda.

KatibuwaWilaya  Dar es salaam.


MBUNGE NA MWAKILISHI WA MAGOMENI ZANZIBAR WAGAWA SARE KWA WANAFUNZI WALIO FAULU

$
0
0
 Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin akimkadhi sare ya Skuli mwanafunzi Shida Muh'd Abdalla aliefaulu kuingia Darasa la 11 katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere Mjini Unguja
 Mbunge wa Jimbo la Nyerere Muhamad Amour Chombo akimkadhi sare ya Skuli mwanafunzi Abdilan Mzee aliefaulu kuingia Darasa la 11 katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere Mjini Unguja.
Mbunge wa Jimbo la Magomeni Muhamad Amour Chombo akitoa nasaha kwa wanafunzi,na pia kuwapongeza kwa kufaulu kwao kabla ya kuwazawadia sare za Skuli kwa kila mwanafunzi,huko katika Skuli ya Sekondari ya Nyerere Mjini Unguja.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.)

Twanga Pepeta kusindikiza utambulisho Miss Tabata 2013 Pasaka

$
0
0

Washiriki wa miss Tabata 2012 (picha na maktaba yetu).

Warembo watakaoshiriki kwenye kinyang’anyiro cha kumtafuta Miss Tabata 2013, watatambulishwa  siku ya sikukuu Pasaka katika ukumbi wa Dar Wes Park, Tabata.

Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga amesema jana kuwa utambulisho huo utasindikizwa na burudani kababembe kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta “Wazee wa Kisigino”. Kalinga alisema kuwa wapenzi wa urembo watapata fursa ya kuwaona warembo kabla ya fainali itakayofanyika Mei.

Utambulisho wa Miss Tabata 2013 imedhaminiwa na Konyagi, CXC Africa, Fredito Entertainment, Saluti 5 na Kitwe General Traders na kuandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts. Mratibu huyo alisema warembo 25 wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.

Washindi watano kutoka Tabata watafuzu kushiriki Miss Ilala baadaye mwaka huu. Anayeshikilia taji la Miss Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.

RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE MAALUMU TOKA KWA RAIS WA BOTSWANA LEO

$
0
0
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Botswana uliowasilishwa na  Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo Mhe Pandu Skelemi leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisoma ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Botswana uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi hiyo Mhe Pandu Skelemi leo Ikulu jijini Dar es salaam.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Botwana Mhe Pandu Skelemi baada ya kupokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa nchi hiyo leo Ikulu jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

SBL YAitikisa MITAA YA JIJI LA DAR ES SALAAM KATIKA amsha amsha za SHANGWE ZA MAFANIKIO YA BIA YA SERENGETI

$
0
0


Kampeni Kabambe ya kuitangaza Bia ya Serengeti Lager inayozalishwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) ijulikanayo kama TUPO PAMOJA KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO imelitikisa mitaa na vitongoji vya jiji la Dar es Salaam jana.

Huku pakiwa na burudani ya muziki ambayo iliashiria Shangwe za mafanikio, Msafara wa magari kadhaa ya Kampuni ya Bia ya SBL pamoja na Lori kubwa aina ya Scania Semitrailer likiwa limepambwa vilivyo na kuleta mvuto wa ajabu kwa Watanzania lilikatiza maeneo mbalimbali ya jiji.

Msafara huo wa kutoa Shukrani kwa Watanzania ndani ya jiji la Dar es Salaam ulianzia katika Kiwanda cha SBL Temeke kisha kwenda hadi Mwembeyanga hadi Saba saba.

Shangwe hizo ziliendelea hadi Taifa, Chang'ombe, Kamata, Msimbazi, kisha msafara huo ukaingia barabara ya uhuru, ukapita Ilala ukaja tokea Buguruni, ukaingia Barabara ya Mandela hadi Ubungo kisha ukapita Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, ukaelekea Sinza ukatokea Bamaga ukafuata barabara ya Bagamoyo hadi Victoria ukaingia Mwananyamala na kumalizia viwanja vya Biafra Kinondoni.

Aidha shangwe hizo zilikuwa zikiendelea katika maeneo kadhaa ya sehemu za starehe za Miti Mirefu, Kimara, Jambo park jet Lumo, Huduma Mbagala na Airtel Pub Banana.
Magari kadhaa ya Kampuni ya Bia ya Serengeti yaliongoza msafara huo.
Ni mwendo wa Shangwe tu ulikuwa ukiemdxelea kila kona Gari hilo lilipopita. Mbali na kampeni hii katika Mitaa ambayo imeanzia jijini Dar es Salaam na pia itasambaa mikoani pia Matangazo katikia vituo vya televisheni, Redio, Magazeti na Blogs yatakuwa yanatoka pamoja na mitaani.
 Magari mengine yalikuwa Nyuma na kupambwa na chapa mbalimbali za Bidhaa za kampuni ya SBL.
Tupo Pamoja katika Shangwe za Mafanikio.
PICHA ZOTE KWA HISANI YA http://mrokim.blogspot.com

Kwetu Pazuri kuzindua albamu Dar Pasaka

$
0
0


KUNDI la muziki wa kiroho la Ambassadors of Christ ‘Kwetu Pazuri’ la Kigali, Rwanda linatarajia kuzindua albamu yao mpya iitwayo Kaeni Macho Machi 31 mwaka huu Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha la Pasaka, Alex Msama alisema Dar es Salaam jana kuwa kundi hilo limemuhakikishia kwamba albamu hiyo itakuwa moto wa kuotea mbali na kuzitaja nyimbo zilizopo katika albamu hiyo kuwa ni Kaeni Macho, Mungu Wangu, Tugireurukundo, Ewe Ndugu, Tuombeane, Umwamini Yesu, Msalaba, Twawona, Okuswala na Huruma.

“Kundi hilo maarufu kwa jina la Kwetu Pazuri limefurahi sana kuja hapa Tanzania na wamenieleza albamu hiyo hawajawahi kuizindua hivyo ni baraka kubwa kwa Watanzania kupewa heshima hiyo,” alisema Msama na kuongeza kuwa kundi hilo pia litatumbuiza katika maonesho mengine ya mikoani. Kwa mujibu wa Msama hivi sasa kundi hilo linatamba na albamu ya Mtegemee Yesu na wamemuhakikishia kuwa watang’arisha tamasha la mwaka huu na wamejipanga vya kutosha kuhakikisha mashabiki wanapata burudani ya nguvu.

Alisema albamu yao hiyo ina nyimbo nane ambazo ni JY’ Ushima Uwite, Mtegee Yesu, Ndifuza Kugerayo, Iyana Iby’ Isi, Yesu Niwe Mungeri, Parapanda, Abasaruzi na Nenda. Licha ya kundi hilo, wasanii wengine wa nje ya Tanzania watakaotumbuiza tamasha hilo ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya. Wasanii wa Tanzania waliothibitisha hadi sasa ni Rose Muhando, Upendo Nkone, John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

WATANZANIA WAWAKILISHA VIZURI KATIKA MASHINDANO YA" INFOMATRIX AFRICA".

$
0
0

Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine na washindi wa mashindano hayo.

Washiriki wa Infotrix Africa walioiwakilisha vizuri Tanzania katika mashindano hayo yaliyomalizika wikendi hii.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa akiwakabidhi vyeti na hundi ya dolla 200 moja ya washindi wa medani ya fedha Sharon Hamis (wakwanza kushoto) na Fatma Jeddah (wapili kutoka kushoto) kutoka shule ya wasichana ya Feza.
 Washindi wengine wakikabidhiwa vyeti, Medali zao pamoja na Hundi baada ya kushinda.
 Baadhi ya washiriki kutoka shule mbalimbali za ndani na nje ya Tanzania wakiwa katika sherehe hizo ya kukabidhi zawadi kwa washindi.

WAziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa akijadili jambo na mkurugenzi wa shule za Feza Tanzania Ibrahim Bicakui katika hafla ya kutoa tuzo kwa washindi wa shindano la "Infomatrix Africa" lililoshikisha nchi 17 kutoka bara la Afrika.
 Wanafunzi kutoka shule mbalimbali zilizoshiriki mashindano hayo.

TAARIFA YA RIDHIWANI KIKWETE KUKANUSHA YALIYOANDIKWA DHIDI YAKE KATIKA MITANDAO YA JAMII

$
0
0

Ndugu zangu habari za wikiendi. Yapo mambo machache ningependa kuwashirikisha ili kuweka kumbukumbu sawa na pia kuzuia upotoshaji ambao unaweza kujitokeza siku za usoni iwe kwangu, kwako au kwa mtu mwingine.

Mojawapo ya mambo makubwa ambayo yamejitokeza siku za karibuni hasa katika suala la Teknolojia na habari ni jambo la sheria za faragha (privacy and privacy laws). Tumeshuhudia kufungwa kwa gazeti za News of The World, mali ya bilionea Rupert Murdoch wa Kimarekani baada ya kudhihirika alitumia wataalam wa teknolojia (hackers) kutafuta siri za watu mashuhuri kwa kuingia katika simu zao za mkononi kinyume cha utaratibu na sheria za faragha (Privacy Laws). Tumeshuhudia pia wahalifu hao hao wa mtandao wakifanya mengi kama kuvamia kwa mitandao ya makampuni makubwa kama Sony na mengineyo na hata katika mitandao hii ya kijamii upo wakati marafiki zako wanakwambia mbona umenitumia kitu kisichoeleweka, na baadaye kuja kugundua kwamba si wewe uliyefanya hivyo.

Tarehe 1, 8 na 9 mwezi huu wa Machi nilikuwa Dar es Salaam kwa shughuli zangu za kawaida kimaisha lakini ziko updates 5 zilifanyika hapa moja ikimhusu ndugu Absalom Kibanda. Ni ajabu kwamba baadhi ya waandishi tena waliojivika taji la usahihi katika uandishi waliiandika habari hiyo bila hata kuniuliza kwamba ni nini kinatokea. Tunajitahitahidi na kutamani kuwa na Taifa la waandishi makini na wenye kufuata maadili lakini wapo wanaoturudisha nyuma. Ni ajabu gazeti kuandika jambo lisilo la kweli huku wahusika wakiwa na kila uwezo wa kumfikia yule wanayedhani kwamba ameandika na kumhoji ili kuhakiki habari. Kazi ya uhariri ni kuhakiki. Ikiwa mtu atakimbilia kuandika jambo likuhusulo ambalo hana hakika nalo na alikuwa na kila uwezo wa kuwasiliana na wewe na kukuuliza lazima utajiuliza maswali mengi. Kwanza: Nini hasa lengo lake na pili ufahamu wake wa kile anachokifanya kwa maana ya taaluma yake katika kazi anayoifanya.

Napenda kuwaambia kwamba katika tarehe hizo mwezi huu wa Machi, wahalifu wa mtandao wakiwa eneo la Njiro na baadaye Kijenge mjini Arusha (Kila post ilionyesha eneo ilipotoka), (wakati huo mimi nikiwa Dar es Salaam) waliingia bila idhini kwa njia haramu (Hacking) katika anuani yangu ya Facebook na ku-post habari hizo tano. Sasa nimeliacha jambo hilo katika vyombo stahiki vya ulinzi na usalama ili kufuatiliwa kadiri ya taratibu zao.

Natoa wito kwa ndugu zangu waandishi kujitahidi kuhakiki habari kabla ya kuzipeleka katika vyombo vyao. Hii itasaidia 1. Wao kujenga heshima mbele ya jamii 2. Kufikisha kile hasa ambacho ni habari 3. Kuzuia mikanganganyiko isiyo ya lazima. Haya yakizingatiwa nadhani hata sintofahamu hizi za uandishi wa habari unaotokana na hisia na  vyanzo vumbi na  ufahamu mdogo wa jambo utaondoka na tutakuwa na jamii ambayo haki na uwajibikikaji wa wanahabari kwa jamii utaonekana kutendeka 

Niombe radhi kwa ndugu yangu, rafiki yangu na pia mwalimu wangu, Ndugu Absalom Kibanda kwa usumbufu wowote uliojitokeza ambao naamini watu wasio na nia njema walitaka kuutumia kuleta hisia tofauti katika jamii na pia kumpa pole kwa mara nyingine tena kwa maumivu yaliyosababishwa na ujangili huo. Namuombea kwa Mungu ampe unafuu mapema zaidi ili arudi katika meza yake kuendeleze harakati za kupambana na mchango wake katika kuleta maendeleo ya kweli kwa nchi yetu. Pili, pole pia kwa wote ambao kwa namna moja au nyengine walikwazwa na uzushi huo, kwa kuwa sina tatizo lolote na Bwana Kibanda na wala nisingependa lililomtokea limtokee yeye wala mtu mwengine yeyote. 

Ni imani yangu ya dhati kwamba vyombo husika katika nchi yetu havitasita kulitalifanyia kazi jambo hili na ukweli juu ya nini kimemtokea Bwana Absalom Kibanda utajulikana na kuwekwa bayana. 

Mwisho, shukrani kwa wote mlionipigia simu kuhusu hili, tuko pamoja na nawatakia kila la kheri katika shughuli za ujenzi wa Taifa letu hili la Tanzania ambalo msingi wake umejengwa katika haki, umoja, amani na kujali hali za watu wake.

Asanteni sana.

Ndugu yenu, 
Ridhiwani Kikwete,
Jumapili Machi 17, 2013.



TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL. 50 UCHIMBAJI VISIMA VYA MAJI MPWAPWA

$
0
0
 Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 50, Mhandisi wa Maji wa kampuni ya DRIMA __ Gound Woter Drilling, Melkion Mhagama kwa ajili ya uchimbaji wavisima 2 vya maji katika vijiji vya Iramba na Lukole Wilayani Mpwapwa hivi karibuni. Wanaoshuhudia ni Naibu Waziri wa Nishati  na Madini, George Simbachawene, Meneja wa TBL Kanda ya Kusini, James Bokela  na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpwapwa,Alexzanda Nyauringo.

Naibu Waziri wa Nishati  George Simbachawene akiwatambulisha Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Steve Kilindo na Meneja wa TBL Kanda ya Kusini, James Bokila.
 Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Christopher,Kangoye akifurahia jambo mbele ya wananchi wa vijiji hivyo alipokuwa akiongea nao wakati wa upokeaji wa
msaada wa sh. Mil 50  kwa ajili ya uchimbaji wa visima toka kampuni ya bia TBL
Wananchi wa vijiji hivyo wakifuatia jambo baada ya kupokea msaada huo.

wakazi wa jiji la arusha wakunwa vilivyo na ujio wa kinywaji cha Tusker Lite

$
0
0
Meneja wa bia ya Tusker Lite Bi. Anitha Msangi kielezea wadau jinsi bia ya Tusker Lite ilivyotengenezwa kwa vimelea asili na yenye wanga kidogo sana katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.

Wadau wa bia ya Tusker Lite na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti wakionyesha furaha na kuipokea bia ya Tusker Lite jijini Arusha katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.

Mama akifurahia zawadi ya glass za Tusker Lite baada ya kuibuka mshindi wa kucheza muziki katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.
Nyaki na Mama akishindana na nyaki kucheza muziki wakati wa hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.
  Nakaaya Sumari akifurahia jambo na MC katika hafla hiyo.
Mmoja wa wageni waalikwa ambaye mwanamuziki mkongwe wa muziki wa kizazi kipya jijini Arusha anayejulikana kwa jina la ”Mkoloni” akitoa neno lake kuonyesha hisia kuhusu ujio wa bia ya Tusker Lite, kushoto na JBC,na kulia mwisho ni Nakaaya Sumari katika katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.

Msanii wa Hip Hop kutoka jijini Arusha aitwaye JCB akitoa shukrani zake kwa Kampuni ya bia ya Serengeti kwa kuleta bia nzuri ya Tusker Lite katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.

 Wakazi wa jiji la Arusha wakifurahia ujio wa bia ya Tusker Lite katika hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.
Mwanamuziki wa Bendi ya Vibration ya jijini Arusha akiwaongoza mabalozi wa bia ya Tusker Lite kucheza pamoja na wadau wa jijini Arusha katika hafla hafla ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.
  Nyaki ambaye ni meneja mauzo kanda ya kaskazini akimtambulisha msambazaji mkubwa wa bia za Serengeti kanda ya kaskazini

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti wakishindani kucheza muziki wakati wa hafla ya uzinduzi wa bia ya Tusker Lite uliofanyika ka katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.


1.       Meneja wa bia ya Tusker Lite Bi. Anitha Msangi (mwenye gauni nyeusi) akiwa amepozi pamoja na wasanii wa jijini Arusha Nakaaya Sumari kushoto kwake na Peter kutoka Arusha na kushoto kwake ni Peter Ngassa mdau kutoka Dar Es Salaam katika hafla ya ya uzinduzi wa bia hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Kibo Palace jijini Arusha usiku wa ijumaa. Bia hiyo ya Tusker lite sasa imeanza kupatikana pia katika mikoa mingine ya Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya, Tanga na Moshi.

shindano la MISS UTALII TANZANIA 2012/13 lakumbwa na ukata wa bajeti, lasogezwa mbele mpaka machi MACHI 30, 2013

$
0
0

Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13, zilizo kuwa zimepangwa kufanyika 17,machi 2013  katika ukumbi wa Dar Live Dar es Salaam, zimesogezwa mbele hadi tarehe 30-3-2013,katika ukumbi utakao tangazwa badae. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano hayo nchini na Barani Afrika Erasto G., Chipungahelo, alisema kuwa sababu  ya kuahilishwa kwa fainali ni pamoja na upungufu wa bajeti ,uliosababishwa na baadhi ya wadhamini wakubwa walio ahidi kushindwa  kutimiza ahadi zao kama walivyo ahidi, hivyo kupelekea upungufu wa zaidi ya shilingi 170,000,000/= , kati ya bajeti ya shilingi 870,000,000/= zinazohitajika ili kukamilisha fainali hizo.

“Ili kulifanya shindano hili kwa ubora na kiwango cha kimataifa, tunahitaji sio chini ya shilingi 870 Milioni, ambapo hadi sasa tumefanikiwa kupata jumla ya shilingi 600Milioni, na tunaupungufu wa jumla ya shilingi 170 Milioni, ambao umesababishwa na baadhi ya wadhamini , kushindwa kutimiza ahadi zao kulikotokana na matatizo mbalimbali waliyo yapata ya kibiashara. Mashindano haya kama yalivyo mashindano mengine nchini na Duniani yanategemea udhamini kutoka kwa sekta binafsi na za umma, kwani gharama za kuyaendesha na kuyaandaa mashindano haya ni kubwa,ambazo haziwezi kulipwa wala kufidiwa kwa kutegemea viingilio vya getini”.

Hali hii imetulazimu kuahilisha fainali hizi hadi 30-3-2013,ili kupata muda wa kupata kiasi hicho cha fedha, na kukamilisha maandalizi kwa ubora na viwango vya kimataifa. Taratibu za kupata fedha hizo zinakaribia kukamilika kabla ya tarehe ya shindano kutoka kwa wadau wa utalii katika sekta binafsi na za umm. Kambi ya washiriki inaendelea katika hoteli ya Ikondelelo Lodge Dar es Salaam, ambapo kuanzia jumanne tarehe 19-3-2013 , washiriki wote wakiambatana na waandishi wa habari, wataanza ziara ya wiki moja katika hifadhi za Taifa za Mikumi,Saadani na Udzungwa, wakiwa katika hifadhi ya taifa ya Udizungwa washiriki watapanda milima ya udizungwa hadi katika kilele cha Maporomoko ya maji ya Sanje , ambayo ni kivutio kikubwa katika hifadhi hiyo.

Akizungumzia hali hii chipungahelo tumesikitishwa, na hali hii,tulijipanga na kujiandaa kwa makini,lakini bahati mabya mmoja wa wadhamini wetu amepata matatizo ya kibiashara,yote ni mipango ya mungu, na tunatambua kuwa washiriki wamekaa kambini kwa zaidi ya muda tulio kuwa tumeupanga,hivyo kutuongezea gharama, lakini baada ya kutafakari kwa kina tumeona kuliko kufanya shindano lililo chini ya kiwango, ni bora kuingia gharama zaidi za kambi ili tufanye shindano lenye hadhi na kiwango cha kimataifa na kuwa mfano kwa mashindano mengine nchini na Afrika kwa ujumla.Kwa washiriki ambao kwa sababu moja au nyingine hawatakuwa tayali kuendelea na kambi, basi milango iko wazi kwao na nafasi zao zitachukuliwa na washindi waliofuatia kutoka katika mikoa husika.

Sekta ya Utalii ni moja ya uti wa mgongo wa uchumi wa taifa,na sisi tunatangaza na kukuza utalii kitaifa na kimataifa,kwahiyo kwetu sisi ni ubora kwanza wa shindano na si bora shindano,bora hasara ya fedha kuliko hasara ya ubora wa shindano , ambalo ni alama ya urithi wa taifa.

Binafsi na kamati ya mashindano, hatutaki kuamini kuwa hii ni hujuma ,bali ni hali ambayo katika dunia ya biashara ya sasa, yeyote inaweza kumtokea, hivyo hatuna sababu ya kuchukua hatua za kisheria za kumshitaki mdhamini huyo, wala kumtaja katika vyombo vya habari,tumejiridhisha nae na kuamini bahati mbaya iliyo mtokea.

Tunawaahidi wadau na wapenzi wa mashindano haya kuwa dhamira,na nia ya kulifanya shindano hili kuendelea kuwa bora na lenye mafanikio makubwa kuliko jingine lolote nchini na Afrika iko pale pale, na hili litadhihirika hiyo siku ya tarehe 30-3-2013. Kwa wadau,wafanya biashara, makampuni binafsi na ya umma, hasa ya kizalendo tunaomba wajitokeze kutuunga mkono kwa kudhamini na kununua tiketi siku ya shindano. Kwa wale wasio tutakia mema basi wajiandae kuumbuka siku ya tarehe 30-3-2013.
Erasto G. Chipungahelo
Rais – Miss Tourism tanzania Organisation

SHINDANO LA MORO CARNIVAL LAANZA KUIBUA VIPAJI MJINI MOROGORO

$
0
0
 Majaji wa Shindano la Moro Carnival lililofanyika katika uwanja wa sabasaba, kutoka kulia ni Frado John, Msanii wa Muziki wa bongofleva Seleman Msindi 'Afande Sele', Wiliam Matajiri pamoja na mwanadada Adela Tilya.
 Jaji namba tatu Wiliam Matajiri akitoa maksi kwa mshiriki wa shindano la Moro Carnival.
 Jaji namba mbili Seleman Msindi 'Afande Sele' akitoa makisi kwa mshiriki.
Mshiriki wa muziki wa hip hop, akionyesha makali yake ya kuchana wakati wa shindano la Shindano la Moro Carnival lililofanyika uwanja wa sabasaba mjini Morogoro.
 Kijana Mafuvu akionyesha umahili wake wa kucheza katika Shindano la Moro Carnival ambalo lilikuwa likiwapambanisha vijana wa mji wa Morogoro kuonyesha vipaji vyao mbali mbali. Shindano hilo lililofanyika katika uwanja wa Sabasaba mjini Morogoro, Moro Carnival lengo lake ni kuvumbua vipaji wa kuwashindanisha na kuviendeleza vipaji kwa vijana wa mji wa Morogoro. Vipaji vilivyokuwa vikitafutwa ni vya kudansi, kuimba, wasanii wa muziki wa Hip Hop, Uchekeshaji n.k
Kikundi cha Moro Squid kikionyesha umahili wake wa kucheza katika Shindano la Moro Carnival.
 Watu waliojitokeza katika shindano hilo wakifuatatilia kwa makini mchuano.

kinywaji baridi cha Coca-Cola Zero chazinduliwa jijini dar.

$
0
0
 Mwanamuziki Madee akiimba sambamba na umati wa wapenzi wa muziki wakati wa uzinduzi wa kinywaji baridi cha Coca-Cola Zero uliofanyika Koko Beach juzi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

 Ommy Dimples akifanya vitu vyake wakati wa uzinduzi wa kinywaji cha Coca-Cola Zero katika ufukwe wa Coco.


Mwanamuziki nyota wa THT Linah (kulia), akicheza na mmoja wa mashabiki wake aliyepanda jukwaani wakati wa uzinduzi wa kinywaji cha Coca-Cola Zero uliofanyika Coco Beach jijini Dar es Salaam. 
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images