Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 46 | 47 | (Page 48) | 49 | 50 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Bwa.Ephrahim Mafuru akizungumza jambo mbele ya Wanahabari waliofika kushuhudia uzinduzi wa kampeni mpya ya bia ya Serengeti Premium Lager itakayoitwa "TUPO PAMOJA-KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO,ambayo inatarajiwa kufanyika nchi nzima katika maeneo mbalimbali.
  Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Bwa.Allan Chonjo akitoa ufafanuzi wa namna kampeni hiyo  "TUPO PAMOJA-KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO",itakavyofanyika, mbele ya Wanahabari waliofika kushuhudia uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika nchi nzima katika maeneo mbalimbali.
  Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,pichani kulia Bwa.Ephrahim Mafuru,pamoja na Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Allan Chonjo wakiandaa kufanya uzinduzi wa kampeni yao mpya ya kinywa cha Serengeti Premium Lager.Pichani kati anaeshuhudia ni Meneja wa Mahusiano ya ndani ya kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Iman Lwinga.
   Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,pichani kulia Bwa.Ephrahim Mafuru akitoa ufafanuzi mbele ya Wanahabari waliofika kushuhudia kampeni hiyo ambayo inatarajiwa kufanyika nchi nzima katika maeneo mbalimbali.
   Moja ya ratiba za shangwe hizo zitakapokuwa.
   Baadhi ya Wanahabari wakishuhudia uzinduzi wa kampeni mpya ya kinywaji cha Serengeti Premium Lager  "TUPO PAMOJA-KATIKA SHANGWE ZA MAFANIKIO",iliyofanyika mapema leo asubuhi.

  Meneja wa Mahusiano ya ndani ya kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Iman Lwinga akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo mbele ya Wanahabari,ndani ya moja ya ukumbi wa hotel ya JB Belmonte,Jijini Dar wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kinywaji chake cha Serengeti Premium Lager.Anaaefuatia ni Mkurugenzi wa Masoko wa SBL,Bwa.Ephrahim Mafuru,Meneja wa Kinywaji cha Serengeti Premium Lager,Allan Chonjo pamoja na Meneja Masoko Mosses Kebba 

  0 0

  Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknologia Dr. Hassan Mshinda akikata utepe kuashiria ufunguzi wa mashindano ya "INFOMATRIX AFRICA" yanayoshirikisha nchi zaidi ya 17, kulia kwake ni  Mkurugenzi mkuu wa shule za Feza Ibrahim Bicaku na kushoto kwake ni Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Balozi Ali  Davudoglu.
  Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknologia Dr. Hassan Mshinda akiangalia na kupata maelekezo ya ubunifu wa kiteknologia kutoka kwa moja ya washiriki wa "Infomatrix Africa" yaliyoandaliwa na shule za Feza.
   Mtoto Halid Yildirin(10)kutoka nchini Uturuki akionesha kifaa alichokibuni chenye uwezo wa kugundua na kuhamisha mabomu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine katika ufunguzi wa "Infomatrix Africa" yaliyofanyika jijini Dar es salaam
  Baadhi ya walimu wakijadiliana jambo kuhusu maksi za washiriki wa moja ya shindano katika hafla ya uzinduzi wa Infomatrix Africa

  0 0
 • 03/14/13--07:31: umealikwa.!


 • 0 0
 • 03/14/13--07:38: Burudika na Tigo
 •  Mtaalam wa bidhaa za burudani za Tigo Bi. Pamela Shelukindo akimkabidhi bw. Harold Hosea kamera ya digitali yenye thamani ya tsh. 800,000 aliyojishindia kwenye promosheni ya Burudani na Tigo. 
   Mtaalam wa bidhaa za burudani za Tigo Bi. Pamela Shelukindo akimkabidhi bw. Meritus Ishaballu kamera ya digitali yenye thamani ya tsh. 800,00 aliyojishindia kwenye promosheni ya Burudani na Tigo(huyo mwenye kofia babu).Promosheni ya Burudika na Tigo mtumiaji anatakiwa kutuma neno SHINDA,MAWILI,MAPENZI,AKIBA, na IMANI kwenda 15655 anakuwa ameingia kwenye droo ambayo atajishindia kamera ya digitali yenye thamani ya tsh. 800,000

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na mmoja wa wahadhiri Profesa Juma Mikidadi Mtupa (aliyeketi) Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro, Mama Mwantumu Malale, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Hamza Mustafa Njozi na wadau baada ya kuzindua rasmi jengo la Kitivo cha Sayansi la Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro leo Machi 14, 2013 mjini Morogoro. Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Mama Mwantumu Malale.
   
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua pazia kuzindua rasmi jengo la Kitivo cha Sayansi la Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro leo Machi 14, 2013 mjini Morogoro. Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Mama Mwantumu Malale.

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipunga mkono kuaga wanafunzi na wafanyakazi baada ya kuzindua rasmi jengo la Kitivo cha Sayansi la Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro leo Machi 14, 2013 mjini Morogoro. Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Mama Mwantumu Malale.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo juu ya ujenzi wa jengo la kitivo cha Teknohama toka kwa Bw. Hamza Mustafa Njozi  kabla ya  kuzindua rasmi jengo la Kitivo cha Sayansi la Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro leo Machi 14, 2013 mjini Morogoro. Kushoto kwake ni Mkuu wa Chuo hicho Mama Mwantumu Malale.

  =======  ======= =====

  HOTUBA YA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE KATIKA UFUNGUZI RASMI WA JENGO LA KITIVO CHA  SAYANSI KATIKA CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA  MOROGORO (MUM),
  TAREHE 14 MACHI, 2013, MOROGORO
   
  Mzee Kitwana Suleiman Kondo, Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF);
  Mheshimiwa Joel Bendera, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro;
  Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro;
  Profesa Hamza Mustafa Njozi, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro;
  Viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na Jumuiya mliohudhuria;
  Wageni waalikwa;
  Mabibi na Mabwana;
  Niruhusuni niungane na wenzangu walionitangulia kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehma, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha kukutana hapa.  Nakushukuru sana Mama Mwantumu Malale, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro na viongozi wenzako kwa kunialika kuja kujumuika nanyi katika siku hii adhimu ya ufunguzi wa jengo la Kitivo cha Sayansi katika Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro. Mmenipa heshima kubwa ya kuwa sehemu ya historia ya Chuo hiki.  Kwa kweli, nimefarijika sana kuona Chuo chetu kinazidi kupata mafanikio ya kutia moyo hasa ukizingatia ukweli kwamba kina muda mfupi tu tangu kuanzishwa kwake.
  Ndugu Mkuu wa Chuo;
  Natoa pongezi nyingi kwako, Makamu Mkuu wa Chuo na wale wote walioshiriki kubuni wazo la kuwa na jengo la Kitivo cha Sayansi na kufanikisha ujenzi wake.  Juhudi zao na moyo wao wa kupenda maendeleo ndio umetufanya sisi kujumuika hapa leo kushuhudia mafanikio haya. Hakika ni jambo la kujivunia. Pia, nawapongeza sana Wajenzi na Mhandisi Mshauri kwa kazi nzuri waliyofanya ya ujenzi wa jengo hili.  Sote tunaliona jengo lilivyojengwa vizuri na kwa namna yake linapendezesha mandhari ya Chuo. 
  Kwa namna ya pekee napenda kwa niaba yenu nitoe shukrani zangu za moyoni kwa taasisi ya Al-Barakah kwa kufadhili ujenzi wa jengo hili.  Asanteni sana kwa ukarimu wenu na upendo mkubwa mliouonesha kwa nchi yetu na watu wake. Naomba taasisi nyingine na watu binafsi waige mfano huu mzuri wa kusaidia miradi mbalimbali inayonufaisha jamii.  Tukumbuke ule msemo wa wahenga kuwa “kutoa ni moyo, usambe si utajiri”.
  Ndugu Mkuu wa Chuo;
  Mabibi na Mabwana;
  Kwa miaka mingi madhehebu ya dini  na mashirika ya dini yamekuwa washirika muhimu sana wa Serikali katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu.  Yamekuwa yanajihusisha na kutoa huduma kwa jamii kama vile afya, elimu na nyinginezo. Kwa ajili hiyo watu wengi sana nchini wamenufaika na wanaendelea kunufaika na huduma zinazotolewa na mashirika ya dini.
  Kwa miaka mingi  mashirika na  taasisi za madhehebu ya dini ya Kikristo ndiyo yaliyokuwa yakionekana kutoa huduma hizo. Kwa upande wa Waislamu, ukiacha Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan, mchango umekuwa mdogo sana. Ni jambo la faraja kubwa kuona Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF) ikionyesha njia.  Kwa kumiliki na kuendesha Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kwa ufanisi, MDF inatoa mchango muhimu katika kuendeleza elimu ya juu na maendeleo nchini.  Idadi kubwa ya wanafunzi waliofuzu masomo yao na waliopo katika Chuo hiki tangu kilipoanzishwa mwaka 2005 ni ushahidi tosha wa kazi nzuri inayofanywa na MDF.  Hongereni sana.  Tunawaombea kwa Mola mpate mafanikio makubwa zaidi miaka ya usoni kwa upande wa elimu na huduma nyingine muhimu.
  Ndugu Mkuu wa Chuo;
  Katika kipindi cha miaka saba sasa, Serikali yetu imeongeza sana uwekezaji katika upanuzi wa elimu  tangu ya awali hadi elimu ya juu.  Tumeamua kufanya hivyo kwa sababu vijana wengi waliokuwa wanastahili kupata elimu ya awali, msingi, sekondari, ufundi na elimu ya juu walikuwa hawapati. Tanzania ni kubwa kuliko Kenya na Uganda kwa eneo na idadi ya watu lakini ndiyo tuliokuwa na idadi ndogo ya wanafunzi kwa ngazi zote hizo.  Kwa mfano, mwaka 2005 idadi ya wanafunzi waliokuwa Chuo Kikuu nchini Kenya ilikuwa 108,407, Uganda 88,360 na kwa baadhi ya nchi za SADC kama vile Afrika Kusini idadi hiyo ilikuwa 717,973. Wakati wenzetu wakiwa na idadi hiyo, sisi tulikuwa na wanafunzi 40,719 tu katika vyuo vikuu nchini.  Hali ilikuwa hivyo pia kwa elimu ya sekondari.  Kenya ilikuwa na wanafunzi 925,341, Uganda 619,519 na Afrika Kusini 4,186,882 wakati Tanzania ilikuwa na wanafunzi 524,325 tu waliokuwa katika shule za sekondari.
  Tuliona hali hii haikubaliki hivyo tukaamua hatuwezi kuiacha iendelee.  Tukaamua kudhibiti. Tukachukua hatua tulizochukua za kupanua elimu katika ngazi zote.  Matokeo ya uamuzi huo ni kwamba vijana wanaopata fursa ya kupata elimu katika ngazi zote wamekuwa wengi kuliko wakati mwingine wo wote katika historia ya nchi yetu, tumewafikia na kuwapita majirani zetu. Kazi kubwa tunayoendelea nayo sasa ni kuwekeza katika kuimarisha ubora wa elimu waipatayo vijana wetu kwa kuongeza walimu, vifaa vya kufundishia, vitabu na huduma nyinginezo. Inshallah hata kwa dhamira yetu, hii njema Mola atatuwezesha. Mwanzo mgumu lakini hatma itakuwa nzuri.
  Ndugu Mkuu wa Chuo;
  Kufuatia juhudi hizo, idadi ya wanafunzi waliopo kwenye vyuo vikuu nchini imeongezeka sana, kutoka wanafunzi 40,719 mwaka 2005 hadi wanafunzi 166,484mwaka 2012. Kwa upande wa sekondari mwaka 2011 tulikuwa na wanafunzi milioni 1.79 na wenzetu wa Kenya walikuwa na wanafunzi milioni 1.77. Haya ni mafanikio makubwa.
  Serikali itaendelea kuwekeza  kwenye upanuzi wa fursa za elimu na ubora wake. Hata hivyo ushiriki wa wadau wengine kuunga mkono juhudi za serikali ni jambo muhimu sana.  Tumeweka  mazingira mazuri kwa wadau hao kufanya hivyo na mafanikio yanaonekana wazi. Kama nilivyokwishasema awali, mashirika ya dini yamekuwa wadau wa kutumainiwa na mchango wao uko wazi. Unajieleza wenyewe. Kwa mfano, katika vyuo vikuu 49 vilivyopo nchini, vinavyomilikiwa na umma ni 14tu. Vyuo vikuu 24 vinamilikiwa na mashirika ya dini na 11 na sekta binafsi.


  Ndugu Mkuu wa Chuo;
  Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa na muhimu unaotolewa na vyuo vikuu vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na sekta binafsi.  Ninyi mmekuwa washirika wazuri na wa uhakika katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya elimu katika nchi yetu.  Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono na kushirikiana nanyi ili kuwawezesha vijana na Watanzania wengi zaidi waweze kupata elimu. Uamuzi wa kufanya utaratibu wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu uhusishe wanafunzi wa vyuo visivyokuwa vya umma ni moja ya mambo mengi muhimu yanayofanywa na Serikali kuthibitisha usemi wangu huo.  
  Tulipoingia madarakani mwaka 2005 tulifanya mambo mawili muhimu kuhusu mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu.  Kwanza uamuzi kwamba, mikopo itolewe kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya umma na vile visivyokuwa vya serikali. Kabla ya hapo ilihusu vyuo vya umma pekee. Pili kwamba, kila mwaka tuongeze fedha zinazotengwa  kwa ajili ya Mfuko huo ili idadi ya wanafunzi wanaonufaika iongezeke. Tulikuta Mfuko ukiwa na  shillingi billioni 56.1 unanufaisha wanafunzi16,345 mwaka 2005. Tukaongeza kila mwaka na katika mwaka huu wa fedha (2012/13) tumetenga shillingi bilioni 345 zinazowanufaisha wanafunzi 98,772.
  Tutaendelea kuongeza fedha katika Mfuko huo ili wanafunzi wengi zaidi wanufaike na hata ifikie siku moja tuweze kuwakopesha wote bila ya kujali sifa ya uwezo wa wazazi au walezi kulipa ada.  Kwa kasi tuliyonayo na kwa jinsi tunavyozidi kufanikiwa katika kukusanya mapato ya serikali, naamini miaka michache ijayo tunaweza kufikia lengo hilo. Nawasihi Bodi ya Mikopo iwekeze katika  kuimarisha uwezo wa kuwafuatilia waliokopeshwa kulipa mikopo waliyopewa. Matamanio yangu ni kuwa fedha zilizotolewa zizunguke ili tupunguze kiasi kinachotolewa na bajeti ya serikali kila mwaka.   
  Ndugu Mkuu wa Chuo;
  Mabibi na Mabwana;
  Niruhusuni nitumie nafasi hii kukupongeza wewe Mkuu wa Chuo, Makamu Mkuu wa Chuo, Wahadhiri  na Jumuiya nzima ya Chuo Kikuu hiki  kwa kazi kubwa na nzuri muifanyayo ya kuendeleza na kuboresha Chuo. Tumeshuhudia ujenzi wa jengo nililolifungua leo. Tumeona mafanikio kwa upande wa ongezeko la idadi ya wanafunzi, walimu, wafanyakazi na fani zinazofundishwa katika kipindi hiki kifupi cha uhai wa Chuo hiki.
  Nimefurahishwa na kufarijika sana  kusikia kuwa ubora wa elimu inayotolewa hapa chuoni ni jambo linalopewa kipaumbele cha kwanza.  Jambo hili ni muhimu sana kulisisitiza kwani tunataka wahitimu wa Chuo hiki wafanane na wahitimu wa Chuo chochote kizuri nchini na hata duniani.  Ningependa kuona wahitimu wa Chuo hiki wanagombewa katika soko la ajira.  Hili ni jambo linalowezekana.  Kinachotakiwa  ni uamuzi wa Baraza na Seneti kuwa iwe hivyo na kuchukua hatua zipasazo.  Sina shaka kuwa mnaweza kufanya hivyo.  Hakika mnaweza, na sote kwa umoja wetu tunaweza.
  Ndugu Mkuu wa Chuo;
  Nimefurahi sana, pia, kusikia kuwa Chuo kinatoa mafunzo ya ualimu. Bila ya shaka mnaelewa kwa nini nafurahi. Tuna uhaba mkubwa wa walimu nchini hivyo Chuo cho chote kinachotoa mafunzo ya ualimu hunifurahisha.  Endeleeni kuimarisha mafunzo hayo ili Chuo chenu kitambulike na kukubalika nchini kwa sifa ya kutoa walimu wazuri.  Walimu wa kutoka Chuo hiki wawe wale wanaojua vyema masomo wanayofundisha, mahiri kufundisha na waadilifu.  Naomba pia mtoe kipaumbele cha juu kwa mafunzo ya ualimu wa masomo ya sayansi na hisabati.  Mkifanya hivyo, mtakuwa mnatoa mchango mkubwa katika jitihada za kupunguza uhaba wa walimu wa masomo hayo nchini.  Naamini kitendo cha kuzindua Jengo la Kitivo cha Sayansi, kilichofanyika muda mfupi uliopita kinatoa matumaini ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro kuchangia katika jitihada za kupunguza pengo la walimu wa sayansi nchini.  
  Ndugu Mkuu wa Chuo;
  Nimewasikia mkieleza kwa ufasaha changamoto kubwa na ndogo ambazo Chuo inakabiliana nazo.  Nawapongeza kwa dhati, wewe na viongozi wenzako kwa ubunifu wenu na hatua mnazochukua kuzikabili changamoto hizo.  Nawaahidi msaada na ushirikiano wangu na wa serikali kwa yale yaliyoko kwenye uwezo wangu na wa serikali katika kutafuta ufumbuzi kwa changamoto zinazowakabili.
  Nawapongeza kwa uamuzi wenu wa kutafuta vyuo vikuu rafiki vilivyoko katika nchi mbalimbali duniani mnavyoweza kushirikiana navyo.  Endeleeni kufanya hivyo kwani vyuo vikuu vingi duniani hufanya hivyo.  Hamtakuwa wa kwanza na wala hamtakuwa mnafanya jambo la kustaajabisha. Mnaweza,        mkipenda, kuwaomba Mabalozi wetu waliopo katika nchi mbalimbali duniani wawasaidie. Ni wajibu wao kufanya hivyo kwani kusaidia kusukuma maendeleo ya hapa nchini kutoka huko waliko ndilo jukumu lao la msingi. Vile vile, nimefurahishwa na mipango yenu ya baadaye ya kuwa na matawi katika mikoa mbalimbali nchini.  Hongereni kwa uamuzi wenu wa busara. Lazima Chuo kitanuke kwa maana ya kuwa kikubwa zaidi, makao makuu na kwa kuwa na vyuo vishiriki na shule au  vitivo sehemu mbalimbali nchini.
  Ndugu Mkuu wa Chuo;
  Kazi iliyo mbele yenu ni kubwa, hivyo ni vyema kuweka mikakati mizuri na mipango thabiti ya utekelezaji na ufuatiliaji wa dhamira yenu hiyo njema.  Rai yangu kwenu ni kuwaomba muwe wabunifu zaidi hasa katika kutafuta vyanzo vingine vya mapato vitakavyosaidia Chuo kujiendesha bila kutegemea ada peke yake.  Chuo kiangalie uwezekano wa kufanya shughuli zitakazowaingizia mapato kama vile kufanya shughuli za kutoa ushauri. Pia muangalie uwezekano wa kuwekeza wenyewe kwenye miradi ya kiuchumi au kwa kushirikiana na wawekezaji katika baadhi ya maeneo.
  Kuhusu nafasi mbili za ufadhili nilizopewa na Chuo kikuu cha Tun Abdul Razak cha Malaysia, nitafuatilia kujua  kilichoendelea na kinachoendelea. Je, nafasi hizo bado zipo?  Zikiwepo, nitawasiliana na wahusika waangalie uwezekano wa kuwapeni. Kama zimeshagawiwa basi tusubiri safari ijayo. Kwa  masuala ya ardhi na maombi mengine nimeyasikia, yaleteni tuangalie namna ya kusaidiana. 
  Ndugu Makamu Mkuu wa Chuo, na
  Wafanyakazi wote wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro;
             Napenda kuwakumbusha kuwa mnayo dhamana kubwa na wajibu mkubwa na wa kihistoria. Ule ukweli kwamba ni mara ya kwanza kwa Taasisi ya Waislamu wazawa kuwa na Chuo Kikuu inawapeni wajibu maalum wa kuhakikisha Chuo kinafanikiwa. Ni mtihani na changamoto ya aina yake kuthibitisha kuwa Waislamu nao wanaweza kuwa na Chuo kizuri na chenye kutoa elimu ya ubora wa hali ya juu.  Kwa sababu hiyo hamna budi kuhakikisha kuwa mna mipango mizuri ya kujenga Chuo cha hadhi na ubora wa hali ya juu.  Ihakikishwe kuwa mipango hiyo inatekelezwa kwa ukamilifu. 
             Aidha jumuiya yote inao wajibu wa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, maarifa na weledi ili dhima hiyo ya Chuo iweze kutimizwa kwa ukamilifu. Timizeni wajibu wenu ipasavyo ili jina la Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro likue haraka. Sifa yake isambae na kuvuma kote nchini. Chuo kifanye vizuri ili wanafunzi waone fahari kuwa wahitimu wa Chuo hiki. Chuo ambacho, wazazi wapende kuleta vijana wao kuja kusoma hapa. Kwa jinsi Mkuu wa Chuo alivyoeleza, mimi nina imani mnaweza, fanyeni kweli.


  Ndugu Wanafunzi wa Chuo cha Waislamu cha Morogoro;
  Naomba wote muone fahari ya kuwa wanafunzi katika Chuo cha kihistoria hapa nchini.  Nawasihi mjitume kwa kadri ya uwezo na vipaji mlivyopewa na Mwenyezi Mungu mfanikishe kile kilichowaleta.  Jifunzeni kwa bidii mfaulu vizuri ili mkihitimu muwe kielelezo kizuri cha mafanikio na ubora wa  Chuo  Kikuu Cha Waislamu cha Morogoro.  Muwe Mabalozi na kioo cha ufanisi wa Chuo hiki. Nawasihi mjiepushe na mambo yatakayowapunguzia muda au kuwaondoa katika shughuli ya msingi iliyowaleta hapa ya kujifunza mpate digrii katika fani mliyochagua mwenyewe kuisomea.  Vishawishi ni vingi na wapo watu wengi wanaopanga kuwashawishi mtumie muda wenu adhimu kufanya wanayoyataka wao ambayo mkishiriki huwatoa kwenye malengo na kutekeleza yao. Mambo ya dunia ya nje ya Chuo ni mengi huna budi kutambua lipi ufanye na lipi usifanye na kwa wakati gani! 
  Mwanafunzi wa Chuo Kikuu ni mtu mzima, si mtoto. Lazima ujue kuwa unawajibika kwa kila unaloamua na kutenda.  Amua kuwajibika vizuri. Fikiri kabla ya kutenda, changanua lipi ni lipi kabla ya kufanya uamuzi wa kile unachotaka kufanya.  Wakati wote uongozwe na busara na hekima na siyo jazba na ushabiki wa matakwa ya kundi.  Kama ni jema fanya na kama si jema usifanye.  Kwanza tambua wewe ni nani na uko hapa kwa ajili gani. Lazima ujue kuwa hatma ya yote uko peke yako.  Utafaulu au kufeli wewe.  Utapata shahada wewe na si mtu mwingine.  Hakuna ubia wa kufaulu au kufeli au kiwango cha kufaulu. It will always remain personal. Katika masomo unanufaika wewe.  Shirikiana na wengi lakini usisahau kujali maslahi yako.  Maslahi ya wengi yasiyojumuisha yako, yahoji vizuri kabla ya kuamua kushiriki au kufanya. Vinginevyo labda kama umeamua kujitoa muhanga, uwe shujaa. Hata kwa hilo, sijui utakuwa shujaa wa nani.
  Mabibi na Mabwana;
  Kabla ya kumaliza napenda kutambua na kumshukuru Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa na viongozi wa MDF kwa juhudi zao za pamoja zilizowezesha Chuo hiki kuwepo.  Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipowashukuru wananchi wanaokizunguka Chuo kwa ujirani mwema na wakazi wa Morogoro kwa ujumla kwa kukipokea vizuri na kuishi na wanajumuiya wa Chuo hiki kwa upendo mkubwa. Naomba muendelee na moyo na ushirikiano huo.
  Baada ya kusema hayo, nawashukuru sana kwa kunialika. Nawatakia kila la heri na mafanikio tele.
  Asanteni sana kwa kunisikiliza.

  0 0  Leo katika hafla iliyohudhuriwana waandishi wa habari, wageni na wadau mbalimbali Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni mpya na ya kipekee inayoenda kwa kauli mbiu ya TUPO PAMOJA.  Katika hafla hiyo iliyofana asubuhi ya leo pia ilihudhuriwa na wadau wa bia hii katika ishara ya kushereheka mafanikio na shangwe za bia hii.

  Akiongea na waandishi wa habari asubuhi la yeo, Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia Serengeti Bw. Ephraim Mafuru alisema kwamba, “ kwa miaka kumi sasa, tumeona na kushuhudia ukuaji na mafanikio makubwa”.  Bia hii inajulikana kwa kampeni ya ‘raha kamili kwa wengi wanaifahanu kama Chui.  Pia kwa udhamini wa Taifa stars ambao uliinua hadhi ya soka la Tanzania kwa kiwango kikubwa.  Kuna ufadhili wa Fiesta, ambao wote mnajua mchango Fiesta inatoa katika ukuaji wa tasnia ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini.  Aliendelea Bw. Mafuru


  Bia ya Serengeti ni bia ya kipekee ambayo ndio bia ya kwanza Tanzania yenye kimea halisi kwa asilimia mia.    Mwaka jana bia hii pia ilizindua muonekano mpya  wa nembo yake huku ikibaki na ladha ile ile.  Baada ya utafiti, Kampuni ya bia ya Serengeti na wadau wake, wamebaini kwamba watanzania wanahitaji  shangwe za mafanikio yao katika sekta mbalimbali zikiwemo za uchumi, kijamii, kimichezo na kadhalika.


  “Tunawakaribisha wote katika hafla mbali mbali ambazo tutaandaa ili kueneza kampeni hii ya Tupo Pamoja kama mlivyoona katika matangazo niliyowaonyesha, tutaleta shangwe popote mlipo., Alieleza meneja wa kinywaji hicho Bw. Allan Chonjo,  baada ya kuonyesha matangazo mbali mbali yatakovyokuwa katika vyombo vya habari.


  Hafla hiyo ya uzinduzi pia ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wa Kampuni ya bia ya Serengeti wakiwemo wasambazaji wa bia.  Kampeni hii inawatambua na kuwathamini  watanzania wote  kwa mafanikio yao katika sekta mbalimbali za maendeleo. 

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujeruman, Prof. Harald Draun, aliyeongozana na ujumbe wake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 14, 2013. Picha na OMR
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujeruman, Prof. Harald Draun, aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwa makamu Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Machi 14, 2013 kwa ajili ya mazungumzo.

  0 0  0 0


  UN Resident Coordinator of Tanzania Dr. Alberic Kacou giving out a speech during the Annually Ministerial Review, Regional Preparatory Meeting for Africa on “Innovation as Enabler for the Achievement of the Millennium Development Goals and Sustainable Development where he said technological advancements could be a critical way forward to face the new development challenges in the Post 2015 period.

  He added that this would also mean that we need to have innovative approaches to technology transfer, sharing knowledge and making use of them for the welfare of majority of global citizens.( All Photos by Zainul Mzige of Dewji Blog).
  Director General of World Intellectual Property Organization (WIPO) Dr. Francis Gurry giving out a statement during the opening of Regional Preparatory Meeting for Africa on “Innovation as Enabler for the Achievement of the Millennium Development Goals and Sustainable Development that any discussion on science, technology and innovation must consider the role played by intellectual property (IP) stressing that IP is an indispensable mechanism for translating knowledge into commercial assets, noting “IP rights create a secure environment for investment in innovation and provide a legal framework for trading intellectual assets.
  Sixty-ninth President of the Economic and Social Council His Excellency Mr. Nestor Osorio during one of the sessions of the the Annually Ministerial Review, Regional Preparatory Meeting for Africa on “Innovation as Enabler for the Achievement of the Millennium Development Goals and Sustainable Development who said Innovation is the essence of our modern society. Without harnessing its power, we will not be able to create healthy, educated or inclusive societies.
  United Nation Under- Secretary-General for Economic and Social Affairs Mr. Wu Hongbo, One of the speakers who elaborate concepts in the Annually Ministerial Review, Regional Preparatory Meeting for Africa on “Innovation as Enabler for the Achievement of the Millennium Development Goals and Sustainable Development.
  WIPO Member Staff.
  Director General of the National Institute for Medical Research in Tanzania Dr. Mwele Malecela.
  Some of Participants during the preparation of the Ministerial Review of the UN Economic and Social Council, which will take place in Geneva from 1 to 4 July 2013 held today in Dar es Salaam at the Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel.
  Tanzania Delegation including Acting CEO of Brella Ms. Leonilaa Kishebuka (centre) during the Meeting.
  Resident Coordinator Office's UN Tanzania Communication Team during the meeting.
  UN Resident Coordinator of Tanzania Dr. Alberic Kacou share a word with One of the Minister who attend the 2013 ECOSOC Annual Ministerial Review.
  UN Tanzania Communications Specialist Sangita Khadka (second left) and UN Communications Analyst Hoyce Temu exchanging views with United Nations Under-Secretary-General for Economic and Social Affairs, Mr. Wu Hongbo (right).
  Minister of Communications, Science and Technology Professor Makame. Mbarawa (left) with one of the Participant.
  UN Resident Coordinator of Tanzania Dr. Alberic Kacou chatting with the Senior Advisor Office of the Director General of WIPO Ms. Loretta Asiedu
  Brella and Ministry of Industry and Trade Secretariat Team which was assisting the International Delegation.  ***********
  A meeting bringing together over twenty African ministers, the President of the United Nations Economic and Social Council, the heads of the United Nations Department of Economic and Social Affairs (UNDESA) and WIPO, together with senior representatives of the private sector and civil society organizations has underlined the importance of science, technology and innovation to supporting development in Africa.

  WIPO Director General Francis Gurry, UN Under Secretary General Wu Hongbo, and President of the United Nations Economic and Social Council H.E. Mr. Nestor Osorio (Colombia), together with senior policy makers and enterpreneurs, met in Dar Es Salaam on March 14, 2013 to discuss the role of innovation for development. The meeting was held in preparation for the Annual Ministerial Review of the UN Economic and Social Council, which will take place in Geneva from 1 to 4 July 2013. They called on the United Nations and WIPO to support greater emphasis on science, technology and innovation as key to enabling sustainable development in Africa.

  Speaking earlier this week at the opening of a WIPO conference on innovation and intellectual property, Tanzanian President Jakaya Mrisho Kikwete said “Leveraging and protecting Intellectual Property (IP) such as patents, copyrights and other similar forms is a key factor of promoting socio-economic growth and development of nations.” He added “It encourages innovation, invention and development of new technologies. It promotes both domestic and foreign investment, facilitates technology transfer and increases agricultural and industrial production. It is an imperative, therefore, that countries must put in place effective IP policies and related laws.”

  “This meeting is a unique opportunity to define the key role that science, technology and innovation can play in achieving the development goals of the African continent,” Mr. Gurry said. “Any discussion on science, technology and innovation must consider the role played by intellectual property (IP).” He stressed that IP is an indispensable mechanism for translating knowledge into commercial assets, noting “IP rights create a secure environment for investment in innovation and provide a legal framework for trading intellectual assets. An investment in knowledge creation, and the maintenance of a robust and balanced IP system, should feature prominently in any strategy to ensure sustainable economic growth.”

  “With a fast approaching MDG deadline and transition to a post-2015 development era, innovation is a very timely topic. Innovation is needed to meet our common development goals; it is important in the final push for the MDGs and in unleashing the potential for sustainable development,” said United Nations Under-Secretary-General Wu Hongbo.

  ECOSOC President Néstor Osorio also stressed that “Innovation is the essence of our modern society. Without harnessing its power, we will not be able to create healthy, educated or inclusive societies”.
  The Ministerial meeting agreed on the following key priorities:
  -Innovation can bring benefits across all three pillars of sustainable development: economic, social and environmental, and is key to accelerating achievement of the Millennium Development Goals.

  -Discussions at ECOSOC must lead to a Ministerial Declaration that calls for much greater emphasis on the contribution that science, technology and innovation can make to achieving sustainable development in relation to the post 2015 development framework and implementation of the Rio+20 outcomes.

  - The global policy approach to technology and innovation must change to keep pace with changing models of innovation and the new geography of innovation. Innovation is increasingly open, global, networked and collaborative. The emergence of new innovation players in countries of the south creates new opportunites for Africa.

  -Technology and innovation partnerships for development must be multi-stakeholder and recognize the critical role of the private sector and harness the resources it offers. -Policymakers in Africa should redouble efforts to develop their legal and policy frameworks, including their intellectual property legislation and policy, so as to release the region’s untapped potential. Investments in education, research and development should be increased. Support in moving ideas to development and to market should be accelerated.

  -African countries need support to build their innovation infrastructure and the capacity to create domestic technology solutions to local development challenges, as well as to support the transfer, adaptation and dissemination of technology. Commitments of support should emerge from the ECOSOC Annual Ministerial Review.

  -ECOSOC should maximize its potential as a platform for multipe international efforts to support African countries on science, technolgy and innovation (STI) capacity building. It should identify mechanisms for greater coordination among providers of STI assistance. 

  0 0

  Bw. Andrew Mahiga akicheza mchezo wa foosball na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa michuano ya Foosball inayoendeshwa na kampuni ya Heineken Tanzania. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini Dar es Salaama ambapo michuano hiyo itafanyika katika baa tofauti za jijini Dar.
  Meza inayochezwa mchezo wa foosball.
  Warembo waliopamba uzinduzi huyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kazi yao ya kukaribisha wageni katika hafla ya Heineken Tanzania.
  Wageni waalikwa wakicheza mchezo wa Foosball katika hafla ya uzinduzi wa michuano ya Foosball inayoendeshwa na kampuni ya Heineken Tanzania.
  Kila mmoja akionyesha makeke yake ili aweze kushinda.
  Washindi wa mchezo wa Foosball, miiliki wa baa ya Triniti Bw. Jackie Verwey (kulia), Erica wakiwa pamoja na Mkurugenzi wa Heineken Tanzania, Bw.  Uche Unigwe mara baada yakushinda uzinduzi wa mashindano ya mchezo wa Foosball.
  Meza yenye kuchezea foosball

  0 0  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadik, Waziri wa Maji, Jumanne Maghembe, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantum Mahiza na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na viongozi wa Dawasa baada ya Makamu kutembelea na kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo wa Ruvu chini, jana Machi 14, 2013. 
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi Mji mpya wa Mabwe Pande (hawapo pichani) wakati alipofika katika mji huo jana Machi 14, 2013 akiwa katika ziara yake ya kutembelea na kukagua miradi ya Maji inayosimamiwa na Dawasa na kutembelea katika Mtambo wa Ruvu Chini kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo huo wa Ruvu chini. Kulia ni Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Saidik.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa miradi ya Maji, William Kazenga, kuhusu upanuzi wa mtambo wa Ruvu chini wa kusambaza maji, wakati Makamu alipofika eneo hilo jana Machi 14, 2013 kwa ajili ya kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo huo wa Ruvu chini. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa miradi ya Maji, William Kazenga, kuhusu upanuzi wa mtambo wa Ruvu chini wa kusambaza maji, wakati Makamu alipofika eneo hilo jana Machi 14, 2013 kwa ajili ya kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo huo wa Ruvu chini. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Ahmed Kipozi (wa pili kushoto) ni Waziri wa Maji na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea kukagua kazi zinazoendelea za upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu chini jana Machi 14, 2013 wakati Makamu alipofika eneo hilo jana. Picha na OMR

  0 0


  MSANII mahiri wa muziki wa Injili kutoka Afrika Kusini, Sipho Makhabane ametunga wimbo maalum kwa ajili ya mashabiki wake wa Tanzania.

  Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa amezungumza na msanii huyo na amemueleza kuwa amewaandalia zawadi Watanzania kwa ajili ya tamasha hilo.

  “Sipho amefurahi sana kumualika kwenye tamasha letu, amenihakikishia licha ya nyimbo zake za kawaida, lakini pia atakuwa na wimbo maalum kwa Watanzania, amesema anawapenda Watanzania na ameandaa wimbo mzuri ambao ana uhakika mashabiki wataupenda.

  “Mashabiki watakaokuja kwenye tamasha Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Machi 31 watapata fursa ya kumsikiliza msanii huyo pamoja na wimbo wake mpya ambao jina hakunambia lakini amesema ni zawadi nzuri kwa Watanzania,” alisema Msama na kuzitaja baadhi ya nyimbo za msanii huyo kuwa ni Moya Wami, Indonga, Akukhalwa, Over&Over, Nguy’zolo, Yizwa Nkosiseju, Hlalanami Nkosi Jesu, Yek’intokozo, Injabulo, Hlalanami Jesu, Makadunyiswe, Vuka Mphemlo, Mphefumlo na Moya Wami.

  Kuhusiana na maandalizi mengine ya tamasha hilo alisema yanaenda vizuri na kwamba mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kwamba ni matumaini yake mashabiki watajitokeza kwa wingi.

  Licha ya Sipho Makhabane, wasanii wengine wa nje ya Tanzania ambao tayari wamethibitisha kushiriki tamasha hilo ni , Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya na kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda inayotamba na albamu ya Mtegemee Yesu. Wasanii wa Tanzania waliothibitisha hadi sasa ni Rose Muhando, Upendo Nkone na John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili akimkabidhi mjumuisho wa michango Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude katika harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisimamia harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013. Kuume kwake ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi kwa watawa keki maalumu iliyopigwa mnada na kununuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni moja. Aliitoa keki hiyo kama zawadi kwa watoto yatima wanaolelewa na watawa hao.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude wakipokea keki maalumu iliyopigwa mnada na kununuliwa kwa zaidi ya shilingi milioni moja.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwakaribisha wachangiaji wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude wakiongea wakati wa harambee hiyo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha mmoja wa wachangiaji kupiga naye picha na kuchanga shilingi milioni moja wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013. 
  Sehemu ya waliohudhuria harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe iliyofanyika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013.

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali pamoja na kamati ya harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013. 

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Magadu mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2013 akiongozana na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro, Mhashamu Telesphor Mkude tayari kuhudhuria harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kigurunyembe. Zaidi ya Shilingi milioni 250 zilipatikana katika harambee hiyo, ikiwa ni zaidi ya lengo la kupata milioni 200 walilojiwekea. 

  PICHA NA IKULU.

  0 0  * Solomoni Mukubwa;Apania makubwa Tamasha la Pasaka mwaka huu

  KATIKA matamasha ya Pasaka mwaka 2010 na 2011 yaliyopambwa kwa muziki wa Injili kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam na mwaka 2012 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, nyoyo za mashabiki zilikongwa na waimbaji kochokocho waliotumbuiza.

  Lakini kivutio kikubwa walikuwa ni mwimbaji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya, Solomon Siaka Mukubwa na Rose Muhando, ambao mara kwa mara kelele za mashabiki zilisikika wakitaka kila mmoja aendelee kuwapa burudani. Mbali ya Rose Muhando na Mukubwa, wasanii wengine walioshiriki na kufanya vizuri ni Flora Mbasha na Upendo Nkone.

  Waimbaji wengine ni Bahati Bukuku, Jennifer Mgendi, Geraldine Oduor, Enock Jonas, na kundi la muziki wa Injili la Upendo la Kijitonyama, Dar es Salaam hayo ni matamasha ya mwaka 2010 na mwaka 2011 .Kwa mwaka jana waimbaji walioshiriki katika tamasha hilo ni  Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.


  Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani zilizokuwepo siku hiyo. Lakini Mukubwa na Rose ndio waliokuwa kivutio zaidi kutokana na kushangiliwa kwa nguvu. Mukubwa anasema hamasa aliyoipata miaka mitatu mfulululizo ndiyo inampa msukumo zaidi wa kuendelea kukonga nyoyo za mashabiki katika tamasha la mwaka huu.

  Tamasha la Pasaka mwaka huu litafanyika Machi 31 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.


  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama anasema kwa vile tamasha la mwaka jana lilikuwa la mafanikio makubwa, anaamini mwaka huu watavuka malengo yao. “Tamasha la mwaka huu Machi 31 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda naamini mashabiki wengi sana watajitokeza, mwaka jana mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Benard Membe,” anasema Msama.

  Anasema waimbaji mbalimbali wa ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kutumbuiza kwenye tamasha hilo, ambapo wa nje ya nchi ni Sipho Makhabane wa Afrika Kusini, Ephraim Sekeleti wa Zambia na Solomon Mukubwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) anayeishi Kenya, pamoja na kwaya ya Ambassadors of Christ ya Kigali Rwanda.

  Kwa upande wa wasanii wa hapa nchini watakaotumbuiza ni Upendo Kilahiro,  Rose Muhando, Upendo Nkone na John Lissu, kwaya ya Kinondoni Revival na kundi la Glorious Celebration.

  Anasema Tamasha la Pasaka litafanyika Dar es Salaam Machi 31 na  litaendelea Aprili mosi kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6 Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 

  Wasifu wa Mukubwa

  Mukubwa ni mlemavu wa mkono mmoja wa kushoto anaodai umekuwa katika hali hiyo kutokana na kudhuriwa kwa uchawi na mama yake wa kambo alipokuwa na umri mdogo.

  Katika mawasiliano ya msanii huyo na gazeti hili kwa njia ya mtandao hivi karibuni, msanii huyo anasema akiwa na miaka 12, alipata matatizo hayo kwa kutokea uvimbe wa ajabu na hakuna aliyejua tatizo lilikuwa nini, lakini walibaini kuwa ni mama yake wa kambo ndiye alimroga kutokana na wivu.

  Mukubwa aliyetamba na wimbo wa 'Mfalme wa Amani', anabainisha kwamba aliugua kwa miaka mitatu na alihaha huku na huko hospitalini hadi kwa waganga wa kienyeji kusaka tiba, lakini hakufanikiwa.Kwa mantiki hiyo, alifikia uamuzi wa kukatwa mkono kwa vile ulikuwa umeharibika.

  Mukubwa anasema mama yake huyo wa kambo alikiri kumroga baada ya kuokoka, hivyo alimsamehe. Hata hivyo, anasema mkono huo aliokatwa haumzuii kumuimbia Mungu.

  Mukubwa anasema alihamia Kenya kutokana na msaada wa mwimbaji wa nyimbo za Injili, marehemu Angela Chibalonza, aliyekuwa mshauri wake.

  Mukubwa amezaliwa kwenye familia ya watoto tisa, wanaume saba na wanawake wawili, yeye akiwa wa kwanza, alifunga ndoa na Betty Japhet, Machi mwaka 2010.

  Mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu hivi sasa anatamba na albamu yake mpya ya Usikate Tamaa.

  Nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ya Usikate Tamaa ni Usikate Tamaa, Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke Si Nguo, Moyo Tukuza Bwana, Chunga Ahadi Yako na Yesu Jina Zuri. Mukubwa amewahi kutoa albamu mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu.

  Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio.

  Albamu yake ya pili ya Mungu Mwenye Nguvu ina nyimbo za Mungu Mwenye Nguvu, Mkono wa Bwana, Mfalme wa Amani, Siku Moja, Tabia Ina Dawa na Roho Yangu Ikuimbie.


  0 0

  2

  3 4 5 6 7 9
  Hu Qingzhong akichora katuni kwa ajili ya kuingizw kwenye simu ya mkononi, katika Kituo Cha Vijana wajasriamali wasomi cha Chengdu, Machi 15, 2013.

  0 0

  Wakurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts Tanzania Limited, wakitoa heshima kwa mwili wa mamake, David Mgwassa. Benny Kisaka (kulia), Juma Pinto (kushoto) na Juma Mabakila.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi Tanzania, David Mgwassa akizungumza na baadhi ya waombolezaji waliofika kumfariji kwa kufiwa mamake mzazi Suzan  Mgwassa, Kijitonyama, Dar es Salaam. Mwili utasafishwa leo kwenda kwao Manda, Ludewa kwa mazishi.(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

  Mjukuu wa marehemu Suzan Mgwassa, Isaack Mgwassa 9kulia0 akijadiliana jambo na maaskofu wa Kanisa la Pentekoste wakati wa msiba huo.(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
                                                            Sehemu ya waombolezaji  Kwaya ya Kanisa la Pentekoste ikomboleza kwa nyimbo za injili wakati wa kuaga mwili wa marehemu Suzan
  David Mgwassa (wa pili kulia) akijadiliana jambo na maaskofu wa Kanisa la Pentekoste waliokwenda kuuombea mwili kabla kusafirishwa.(PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)


  David Mgwassa akifarijiwa na mmoja wa waombolezaji
  Mgwassa akifarijiwa na mmoja wa waombolezaji
  Waombolezaji wakipata mlo
  Mgwassa akizungumza na Abdul Sisco (kushoto)
  Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Teddy Mapunda (aliyevaa miwani) akishiriki kwenye msiba huo (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

  0 0

  Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Mh. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na wageni waalikwa pamoja na ujumbe wa wafanya biashara kutoka Ujerumani walioongozwa Balozi wa Ujerumani nchini Klaus –Peter Brandes katika hafla ya kuzindua Showroom ya magari ya kampuni ya Alliance Autos inayouza magari aina ya Volkswagon ambapo pamoja na mambo mengine amepongeza hatua hiyo na kusema serikali iko bega kwa bega na wafanya biashara wabunifu na pia kuuhakikishia ujumbe kutoka Ujerumani kuwa serikali imeweka mazingira bora ya kuwekeza hivyo wasisite kujitokeza.
  Mkurugenzi wa Biashara wa CFAO Motors Wayne Mcintosh (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp(kulia) wakifurahia hotuba ya Dkt. Mwakyembe.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp akizungumza wakati wa uzinduzi huo ambapo amesema kufuatia kupanuka kwa kampuni ya Alliance Autos na kuongezeka kwa wateja tumeonelea ni vizuri kufungua showroom mpya ya magari ya Volkswagon ambapo wateja wanaweza kuitembelea wakati wowote.
  Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kulia) akifurahia jambo wakati Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp (hayupo pichani) akisoma hotuba yake kwenye hafla ya uzinduzi wa Showroom mpya ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD. Kulia ni Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia wa Ujerumani. Kushoto ni Tender Manager wa CFAO Motors Bw. Marco Kahabi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof. Harald Braun (wa pili kushoto).
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof. Harald Braun akizungumza machache na wageni waalikwa ambapo amesema ziara ya Ujumbe kutoka Ujerumani imekuwa na mafanikio si tu kwa mazungumzo na Serikali bali kwa kufanikiwa kuhudhuria ufunguzi wa Showroom mpya ya magari ya Volkswagon ya kampuni ya Alliance Autos na kupata fursa ya kubadilishana mawazo na wafanyabiashara watanzania.
  Bw. Lionel Roux wa CFAO Paris Ufaransa akitoa salamu kwa wageni waalikwa wakati wa ufunguzi wa Showroom mpya ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos.
  Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja (kushoto), Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni (katikati) na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani, Prof. Harald Braun(hayupo pichani).
  Johns Wiseman wa Volkswagon Group katika uzinduzi huo.
  Tender Manager wa CFAO Motors Bw. Marco Kahabi (kulia) akiteta jambo na Mgeni rasmi Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harrison Makyembe. Wa pili kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Mh.Klaus Peter Brandes.


  Afisa Mauzo wa kampuni ya Alliance Autors Julius Guni akizungumza na vyombo vya habari akisema kuwa kampuni hiyo imeweza kutambulisha magari mapya aina ya Volkswagon amboyo yamefanyiwa ‘engineering’ ya Kijerumani hivyo ni magari madhubuti sana.
  Aidha amesema kupitia Chama cha Wauza Magari (TMTA) tunaitaka serikali kuhakikisha inaangalia sana suala la ushuru ili kila mtu aweze kuwa na uwezo wa kumiliki gari, hivyo tukishirikiana na makampuni mengine yanayouza magari kupambana tuweze kupata unafuu.
  Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni na mmoja wa wageni waalikwa wakikagua magari mapya aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos kwenye showroom mpya iliyozinduliwa jana jijini Dar na Waziri wa Uchukuzi Dr. Mwakyembe.
  Mkurugenzi Mshirika wa IMMMA Advocates Lawrence Masha akipata maelezo ya gari aina ya Volkswagon TIGUAN kutoka kwa Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni wakati wa hafla ya uzinduzi wa showroom hiyo.
  Meneja Mkuu wa Alliance Autos, wakala wa Volkswagen nchini, Alfred Minja (kulia) na Afisa Mauzo wa Kampuni ya Alliance Autos (T) LTD Bw. Julius Guni (katikati) wakibadilishana mawazo na mmoja wa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
  Picha juu na chini ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa showroom mpya ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos jijini Dar.
  Baadhi ya wageni waalikwa wakinywa na kufurahi baada wakati wa uzinduzi wa Show room mpya ya Kampuni ya magari aina ya Volkswagon ya Alliance Autos jijini Dar.
  Meneja Masoko wa CFAO Motors Tharaia Ahmed (kulia) akibadilishana mawazo na mmoja wa wateja waliohudhuria uzinduzi huo.
  Picha juu na chini ni Wakwetu Band ikiongozwa na Carola Kinasha kutoa burudani kwa wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa showroom mpya na ya kisasa ya magari aina ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos.
  Uzinduzi huo ulihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Ujerumani na Ujumbe wake.
  Afisa Mauzo wa Alliance Autos David Kritsos (katikati) na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo.
  Operations Manager wa Golden Tulip Bw. Aatish Ladwa(kushoto) na mmoja wa wageni waalikwa.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya CFAO Motors Roddy Sharp (kulia) akiongozana na Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya Ujerumani (kushoto) baada ya kuupokea Ujumbe kutoka nchini Ujerumani kunakotengenezwa magari aina ya Volks Wagon walipofika kushuhudia uzinduzi wa showroom mpya ya Kampuni ya Alliance Autos wauzaji wa magari ya Volkswagon. Kushoto ni Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Mh. Klaus Peter Brandes aliyeambata na ugeni huo.
  Waziri wa Nchi Mh. Anne Ruth Herkes wa Wizara ya Uchumi na Teknolojia ya Ujerumani akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika hafla ya uzinduzi wa Showroom mpya ya magari ya Volkswagon ya Kampuni ya Alliance Autos iliyopo Pugu/Nyerere road jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msaidizi wa Mkurugenzi wa CFAO Motors Mama Maria Petro akipokea wageni waalikwa.

  Warembo wa Volkswagon waliokuwa wakikaribisha wageni kwenye hafla ya uzinduzi wa showroom mpya ya Kampuni ya Alliance Autos iliyopo maeneo ya Pugu/Nyerere road jijini Dar es Salaam.

  0 0


  0 0
 • 03/15/13--23:43: kaazi kweli kweli.
 • Ukitaka kufaidi zaidi ingia http://www.nathanmpangala.blogspot.com/

older | 1 | .... | 46 | 47 | (Page 48) | 49 | 50 | .... | 1896 | newer