Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live

SHIMO HATARI LAZIBWA

$
0
0
LILE Shimo hatari lililokuwa kero kwa watumiaji na kuripotiwa na Global TV Online juzi Jumatatu Mei 5, 2014 limezibwa kwa sehemu kubwa. Shimo hilo lilikuwa katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jirani na Kituo cha ITV, Mwenge jijini Dar es Salaam. Ungana na Global TV Online kushuhudia shimo hilo lilivyozibwa!

MZIGO MPYA UMEWASILI NDANI YA DUKA LA KIJANJA LA AKCLASSIC..!

$
0
0
 WALE WATAALAM WA MSASA WANA MALI MUPYAA!!, AK CLASSIC COSMETICS SASA WAMEWASHUSHIA MZIGO WA VITU VYA TOFAUTI KABISA!!  KUANZIA PRODUCTs ZA KUONDOA WEUSI WA KWAPANI,TIBA ZA CHUNUSI,PRODUCTs ZA KUNG'ARISHA NGOZI YAKO,DAWA ZA KUONDOA STRETCH MARKS,PRODUCT ZA KUKUZA NYWELE,KUONDOA WEUSI WA KWENYE MAPAJA!! ...NA  KUNA MADINI ZINGINE LUKUKI MAPYAAAAAA!!EM TUONGOZANE HAPA..

 KWA MAELEZO NA PICHA ZAIDI WATEMBELEE www.akclassic.blogspot.com
 KUWEKA ODA NA KUFIKISHIWA BIDHAA MPAKA ULIPO PIGA  0753-482909/0713-468393

Thanks in advance.






HII IMETOKEA LEO JIJINI MWANZA; MAHABUSU AVUA NGUO NA KUBAKI UCHI ILI KESI YAKE ISIKILIZWE

$
0
0
Inspector Henry (shati la bahari) akiwa na Inspector Veda (mwenye koti) wakisikiliza hoja za  Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu akiwa ameng'ang'ania mlingoti wa Bendera ya Taifa uliopo katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012.
Askari polisi wakiwalinda mahabusu wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, wakiwa wameng'ang'ania mlingoti wa Bendera ya Taifa huku mnoja akiwa mtupu mara baada ya kutoroka toka kwenye msafara wa mahabusu waliokuwa wakiingia mahakama ya wilaya ya Nyamagana na kisha mmoja wao kuvua nguo.
Inspector Henry akiwasihi mahabusu hao wawili wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, kuachia mlingoti wa Bendera ya Taifa na kurudi kwenye chumba cha mahakama kwaajiri ya taratibu za kesi.
Inspector Veda (mwenye koti) akichukuwa maelezo ya Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu akiwa ameng'ang'ania mlingoti wa Bendera ya Taifa uliopo katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Wilaya ya Nyamagana mkoa wa Mwanza, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012. akiwa na mwenzake Hamis Ramadani (30).
Ushawishi ukiendelea.
Mahabusu Thobiasi Warioba (aliye mtupu) pamoja na mwenzake Hamis Ramadhani katu katu waking'ang'ania mlingoti wa bendera ya Taifa huku wakishinikiza kuzungumza na waandishi wa Habari.
Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama.
Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari mahabusu hao walikubali kurejea chumba cha Mahakama.
Nje ya Mahakama kuelekea lango kuu.
Wananchi wamefurika viwanja vya mahakama.
Mashuhuda.
MAHABUSU wawili kati ya sita wanaotuhumiwa kwa kesi za mauaji, wameleta kizaazaa baada ya kujaribu kutoroka na kukimbilia kwenye mlingoti wa Bendera ya Taifa nakuing'ang'ania kisha kuvua nguo na mmoja wao kubaki mtupu.

Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 4:00 asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza, wakati mahabusu hao walipofikishwa kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao, lakini ghafla walipofika kwenye viwanja vya mahakama hiyo walitimua mbiyo kuelekea kwenye mlingoti wa Bendera hiyo ya Taifa na kuvua nguo.

Wananchi waliokuwa katika viwanja vya mahakamani hapo waliachwa midomo wazi na hali ya mshangao, mara baada ya mmoja kati ya hao wawili wakifanikiwa kuufikia mlingoti huo na kuvua nguo kisha kuanza kupiga kelele kwa kupaza sauti kudai haki itendeke.

 Tukio hilo pia lilishuhudiwa na watumishi wa Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Mwanzo, Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka ya jijini hapa (MWAUWASA), Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), na taasisi zingine zilizo jirani na majengo ya mahakamani hapo na wananchi waliokuwa wakisubilia kesi zao kutajwa.

Mahabusu hao sita waliojaribu kutoroka na kuishia kudhibitiwa vyombo vya dola, walitajwa kwa majina kuwa ni Thobiasi Warioba (35), aliyeamua kuvua nguo zote na kubaki mtupu eneo la mlingoti wa Bendera ya Taifa, ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji Na. 32/2012.
 
Watuhumiwa wengine waliojaribu kutoroka ni Hamis Ramadani (30), Anthony Petro (35), Marwa Mwita (38), na Chacha Wangwe (35), na mwingine ambaye hakufahamika majina yake mara moja, wote wanakabiliwa na kesi ya Jinai Na. 215/2013  na walikamatwa tangu mwaka 2011.
 
Wakiwa katika viwanja vya mahakama hiyo baada ya kudhibitiwa na askari polisi, mmoja wa mahabusu hao walisikika wakisema: “Haiwezekani, tangu mwaka 2011 tulipokamatwa hadi sasa kesi zetu hazijasikilizwa. Wengine tumebambikiziwa kesi.  “Tunaomba haki zetu, polisi mnatuonea, vyombo vya habari tunaomba mtusaidie  tumekaa muda mrefu bila kusikilizwa na hatujui hatma yetu tangu 2011 tulipo kamatwa tumechoka kukaa mahabusu, tunaomba kesi zetu zisikilizwe”.

Baada ya malalamiko yao, ndipo askari  mmoja aliyejitambulisha kuwa ni Inspekta Henry akiwa na wenzake sita waliokuwa wakiwadhibiti wasikimbie na kuwahoji kuhusiana na madai yao, huku askari hao wakiwataka kuondoka katika mlingoti huo na kumtaka Warioba avae nguo ili waweze kuingia mahakamani.

“Pamoja na maamuzi yenu haya, lakini mtambue mnavunja sheria na hili ni kosa jingine la jinai, hivyo ni vema mkaondoka kwenye mlingoti huu na kuingia mahakamani. Malalamiko yenu tumeyasikia na yatashughulikiwa,” alisema Inspekta Henry.

Mmoja wa maofisa waandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, ambaye alikataa kutajwa jina lake, alidai ushahidi wa kesi za watuhumiwa hao bado haujakamilika, na kwamba kesi zao haziwezi kusikilizwa na mahakama ya wilaya kwani haina uwezo na badala yake zitatajwa tu kisha kuhamishiwa Mahakama Kuu.

“Bado hiyo ni Criminal Case (kesi ya mauaji) au PI Case hivyo Mahakama Kuu haiwezi kuzungumzia hilo kwa sasa kwa kuwa utaratibu wa mahakama kuu ikisha kuwa tayari huitwa ‘Criminary Session Case’, ambapo sasa hupangiwa namba ya kesi na Jaji wa kuisikiliza,”  alisema.
 

CHANZO:GSENGO BLOG

PRESIDENT KIKWETE MEETS FORMER BRITISH PM GORDON BROWN AND MARK SUZMAN OF THE GATES FOUNDATION IN ABUJA, NIGERIA, TODAY

$
0
0
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with Rt. Hon. Gordon Brown (MP), UN Special Envoy for Global Education and Former British Prime Minister in the sidelines of the World Economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, May 7, 2014.


President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete in a bilateral meeting with Rt. Hon. Gordon Brown (MP), UN Special Envoy for Global Education and Former British Prime Minister in the sidelines of the World Economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, May 7, 2014.
President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete shakes hands with Mr Mark Suzman, President of Global Policy and Advocacy and Country Programmes of the Gates Foundation after holding bilateral talks in the sidelines of the World economic Forum on Africa in Abuja, Nigeria, today May 7, 2014.Photos by State House. 

SHIRIKA LA TAIFA LA HIFADHI YA JAMII NSSF LATOA SEMINA KWA WACHIMBAJI WADOGO WAMADINI MWANZA.

$
0
0
Naibu waziri wa wizara ya Nishati na Madini nchini Steven Masele ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi akizindua Mpango maalum na kufungua Semina kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.
Meneja kiongozi wa Mfuko wa Hifadhi ya jamii NSSF mkoa wa Mwanza akitoa maelezo ya awali na kutambulisha wadau mbalimbali walio hudhuria Semina kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza, ikiandaliwa na NSSF.
 "Mpango huu ni BIMA ambayo ukilipa utakusaidia katika huduma za matibabu wewe na familia yako lakini vilevile mwisho wa siku ukistaafu unachukuwa fedha kwaajili ya kuanza maisha mengine nje ya ajira, ikiwa ni sambamba na kukuwezesha katika suala la mikopo" Alisema Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la taifa la Hifadhi ya jamii NSSF Crescentius Magori.
Wadau wa NSSF wakinukuu pointi za msingi katika Semina ya wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.
"Serikali imetumia zaidi ya shilingi milioni 250 kuwakusanya wachimbaji wadogo ili waweze kuwa na vyama vyao, wapate kutambuliwa ili wapate kusaidiwa," kisha akaongeza  Rais wa Shirikisho la wachimbaji madini Chama cha wachimbaji TZ (FEMATA) John Bina kwa kusema "Napenda kuwahakikishienikuwa kwa sasa wachimbaji wadogo tumejipanga, Ile dhana ambayo watanzania wengi wamekuwa nayo kuwa siye wachimbaji wadogo ni watu wa kutangatanga au wakuzurura haipo!" 
Mameneja wa NSSF Makao Makuu Dar es salaam, Viongozi wa NSSF mikoa ya Mara, Geita, Shinyanga, Singida, Kahama na Mwanza pamoja na viongozi wa FEMATA na vyama mbalimbali vya wachimbaji wadogo wamekutana hapa.
Wadau NSSF.
Katika hotuba yake ya Ufunguzi kwa niaba ya Serikali na wizara Naibu waziri wa wizara ya Nishati na Madini nchini Steven Masele ameishukuru NSSF kwa kukubali kufanya kazi na wachimbaji wadogo.
Wanahabari wakisaka picha zenye mvuto za kutazamika.
"Niliamini kuwa itatuchukuwa muda mrefu kusafiri kuweza kujenga na kutengeneza kitu ambacho kitatambulika kitaifa kitakuwa na heshima inayostahili na kitatoa mchango unaostahili na kitashawishi wachimbaji wengine kuona kwamba hii ni Fursa ambayo hakuna yeyote yule anayeweza kuiacha ipite pembeni. Sasa wacha niwapongeze NSSF kwa kuwa wajanja kati ya mifuko mingine yote ya jamii na kuamua kuliangalia kundi hili ambalo nguvu yake ya baadaye italiongoza taifa kuwa na matajiri wake wa ndani nikimaanisha wawekezaji wa ndani wenye nguvu Mabilionea" alisema Masele.
Engo ya wadau washiriki wa semina kwa umakini.
Meza ya baadhi ya waratibu wa semina ya NSSF kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.
Kutoka meza kuu hadi kwa wadau washiriki wa semina ya NSSF kwa wachimbaji wadogo wa madini iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Serengeti, Victoria Palace Hotel Capripoint jijini Mwanza.
Naibu waziri Wizara ya Nishati na Madini Mhe. Steven Masele, akipata picha ya pamoja na Viongozi wa NSSF  pamoja na baadhi ya wanachama wa Chama cha wachimbaji wadogo wadogo wa madini (FEMATA). 

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA CHINA JIJINI ABUJA

$
0
0
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Waziri Mkuu wa China Mhe. Li Keqiang kwa mazungumzo oembeni ya Mkutano wa Uchumi Duniani kwa bara la Afrika jijini Abuja, Nigeria, Mei 7, 2014. 
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa China Mhe. Li Keqiang pembeni ya Mkutano wa Uchumi Duniani kwa bara la Afrika  jijini Abuja, Nigeria, Mei 7, 2014.

European Union Naval For Flag Ship F215 Brandernburg Visit Tanzania

$
0
0
European Union Naval Force Commander Task Force 465 Jurgen Zur muhlen at the centre Addressing the estimated guest during the Visit to Tanzania, and give thanks to Tanzania Government for good relationship.
Assistant Commander Tanzanian Naval Brigedier General Rogastian Laswai , give the word of thanks to European union Naval for flag Ship F215 Brandenburg for having Good relationship Between them and Tanzania and the Naval training that are organized by European Union Naval.
Untitled
European Union Naval Force Commander Task Force 465 Jurgen Zur muhlen at left side together with Assistant Commander Tanzanian Naval Brigedier General Rogastian Laswai during the gathering
Some Guest From Government of Tanzania, Delegation of European Union, Embassy of Federal Republic of Germany, invited Naval Force from Neighbor countries and other guest who join On Board inside Frigate Brandenburg

Rais Kikwete amteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Rished BADE kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).


Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni  Sefue, uteulzi huu unaanza tarehe 06 Mei, 2014.  Bwana BADE anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bwana Harry KITILYA ambaye alistaafu tarehe 14 Desemba,2013.


Kabla ya uteuzi huo, Bwana BADE alikuwa Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangu Septemba,2012 na baadaye kukaimu nafasi ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania tangia Bwana Kitilya alipostaafu.


Kabla ya kujiunga na Mamlaka ya Mapato Tanzania, Bwana Rished BADE amewahi kufanya kazi katika maeneo mbalimbali yaliyompa ujuzi na weledi mkubwa kwenye mambo ya fedha na mapato kama ifuatavyo:-


Ø  Oktoba, 1995 – Mei, 2000 – Mkaguzi wa Benki za Biashara, Benki Kuu ya Tanzania.

Ø  Juni, 2000 – Juni, 2001 – Credit Manager, Akiba Commercial Bank.

Ø  Juni, 2001 – Septemba,2001 – Chief Financial Officer, Akiba Banking Corporation.

Ø  Septemba, 2001 – Machi, 2006 – Chief Operating Oficer, Barclays Bank (Uganda).


Ø  Januari, 2007 – Desemba, 2009 – Chief Executive Officer, Barclays Bank (Tanzania)

Ø  Desemba, 2009 – 2012 – Chief Financial Officer, (East and West Africa Cluster) Barclays Bank Plc Emerging Markets.

Ø  Novemba, 2010 – Septemba, 2012 – Chief Executive Officer, Tanzania Mortgage Refinance Company.


Bwana Rished BADE ana Shahada ya Kwanza ya Bachelor of Commerce and Management ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (1995); Shahada ya Master of Commerce in Banking and Finance ya Chuo Kikuu cha Sydney (1999), na ni Certified Public Accountant (CPA).


Katika kumteua kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mheshimiwa Rais ana imani kubwa kwa elimu, uzoefu na weledi alionao, Bwana Rished Bade kwa kushirikiana na watumishi wenzake, atatoa mchango mkubwa kwa Taifa kwa kuzidi kuimarisha Mamlaka hiyo na kuboresha utendaji wake na hivyo kuongeza mapato ya Serikali kwa faida ya Taifa.

 “Mwisho”

Imetolewa na:


Premi Kibanga,

Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,

Ikulu - Dar es Salaam.


08 Mei, 2014


WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI WAPEWA SEMINA YA KUELIMISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MAY 7-2014 JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Julius Ningu akifungua mkutano na Wahariri wa vyombo vya habari May 7, 2014 jiji Dar es Salaam. juu ya utunzaji wa Mazingira na kuelekea maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani mapema mwezi wa Sita.
 Mwendesha mada  Bi. Singlunda, akielezea machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Julius Ningu.
 Mdau wa habari akichangia mada.
  Mdau wa habari akichangia mada.
 Afisa Mazingira Mwandamizi  Ofisi ya Makamu wa Rais, Ladislaus Kyaruzi, akisisitiza juu ya utunzaji wa mazingira.
 Afisa Elimu Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Matha Ngolowera akitoa ufafanuzi juu ya Tuzo ya Rais Dr. Jakaya Kikwete ya Upandaji wa Miti ambayo hutolewa mara moja kwa mwaka wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
 Wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari wakiwa kwenye mkutano huo.
 Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Fainahappy Kimambo (kulia), akisisitiza Jambo kuelekea siku ya Mazingira Duniani (kushoto), Mwendesha mada  Bi. Singlunda.
 Mdau wa habari akichangia mada.PICHA NA PHILEMON SOLOMON 

RAIS KIKWETE KATIKA MKUTANO WA DUNIA WA UCHUMI JIJINI ABUJA, NIGERIA

$
0
0
 World Economic Forum Founder and Chairman Prof. Klaus Shwab pins a WEF pin on President Dr Jakaya Mrisho Kikwete in the sidelines of  the World Economic Forum in Abuja.
 President Dr Jakaya Mrisho Kikwete in talks with the World Economic Forum Founder and Chairman Prof. Klaus Shwab in the side lines of  the World Economic Forum in Abuja.
 President Dr Jakaya Mrisho Kikwete in talks with the World Economic Forum Founder and Chairman Prof. Klaus Shwab in the side lines of  the World Economic Forum in Abuja.
 World Economic Forum Founder and Chairman Prof. Klaus Shwab speaks at the closing Plenary session of the Growth Africa Investment Forum at the World Economic Forum in Abuja. Listerning  from left arePresident Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Hon Daniel Kablan Duncan, the Prime Minister of Ivory Coast, President Goodluck Jonathan of Nigeria, Ms Amina Mohamed from the UN in charge of the Post-2015 goals initiative, President of Rwanda Hon. Paul Kagame, the Deputy Chairperson of the African Unity Hon. Erastus Mwacha, and the USAID Administrator, Dr Rajiv Shah.
  President Dr. Jakaya Mrisho Kikwete makes his contribution during the closing Plenary session of the Grow Africa Investment Forum at  the World Economic Forum on Africa in Abuja. Others from left are the Prime Minister of Ivory Coast, President Goodluck Jonathan of Nigeria, Ms Amina Mohamed from the UN in charge of the Post-2015 goals initiative, President of Rwanda Hon. Paul Kagame, the Deputy Chairperson of the African Unity Hon. Erastus Mwacha, and the USAID Administrator, Dr Rajiv Shah.
 President Dr, Jakaya Mrisho Kikwete listen to the Governor of the Bank of Tanzania Professor Benno Ndullu after  a High Level Meeting on the African Strategic Infrastructure Initiative in Abuja, Nigeria, on May 8, 2014. Others from left are Mr Erick Shitindi, Permanent Secretary in the Ministry of Labour and Employment, Dr Philip Mpango, Executive Director Planning Commission, Ambassador Celestine Mushy, Director Multilateral Cooperation, Dr Shaban Mwinjaka, Permanent Secretary in the Ministry of Transport and the Tanzania High Commissioner to Nigeria, Hon. Daniel ole Njoolay.
 President Dr, Jakaya Mrisho Kikwete attends a High Level Meeting on the African Strategic Infrastructure Initiative in Abuja, Nigeria,To his right are host President Goodluck Jonathan and H.E. Macky Sall, the President of Senegal.
President Dr Jakaya Mrisho Kikwete in talks with the USAID Administrator, Dr Rajiv Shah in the side lines of  the World Economic Forum in Abuja. STATE HOUSE PHOTO

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AWASILI WILAYANI IGUNGA MKOANI TABORA JIONI LEO,KUANZA ZIARA YA SIKU 10 MKOANI HUMO.

$
0
0
 Pichani Kulia ni  Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora,Ndugu Hassani Wakasubi akimpokea mgeni wake,Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana na Ujumbe wake alipowasili jioni ya leo katika kijiji cha Makomelo wilayani Igunga mkoani Tabora kwa ziara ya siku 10,ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi. 

 Ndugu Kinana akisalimiana na Wananchi mbalimbali waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Makomelo mapema leo jioni.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama ngoma ya kiasili iliondaliwa wilayani Igunga wakati wa mapokezi ya Ndugu Kinana, ambaye ameambatana na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye na viongozi mbalimbali wa chama hicho,mara baada ku kuwasili kijiji cha Makomelo Wilayani hummo jioni ya leo. 
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana mara baada ya kuwasili kijiji cha Makomelo Wilayani Igunga mkoani humo tayari kwa kuanza ziara ya siku 10 ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi. 
 Ndugu Kinana akipokelewa na vijana wa Green Gard tayari kwa kuvalishwa skafu na kukaribishwa wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh.Fatma Mwasa akiwa sambamba na viongozi mbalimbali wa CCM Wilaya na Mkoa wakisubiri kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana katika kijiji cha Makomelo Wilayani Igunga mkoani humo tayari kwa kuanza ziara ya siku 10 ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua miradi  ya Maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM,Kukagua maandalizi ya uchaguzi za serikali za mitaa pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.
  Baadhi ya wananchi mbalimbali waliojitokeza kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake alipowasili jioni ya leo Wilayani Igunga mkoani Tabora.
 Sehemu ya magari ya Wenyeji waliofika kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana jioni ya leo katika kijiji cha Makomelo,wilayani Igunga mkoani Tabora jioni ya leo.
 Ndugu Kinana akivalishwa skafu
 Ndugu Kinana na Ujumbe wakiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wilayani humo,kwa ajili ya kikao kupata taarifa ya maendeleo ya wilaya na mkoa sambamba na hali ya siasa.
Baadhi ya Viongozi mbalimbali wa Kamati ya Siasa na Mkoa wakiwa kwenye kikao hicho,ambapo Ndugu Kinana pia alizungumza nao.

WIKI YA ELIMU MKOA WA DAR ES SALAAM YAFANA, WANAFUNZI,SHULE ZA SERIKALI NA BINAFSI ZAFANYA VIZURI MITIHANI YA TAIFA MWAKA 2013

$
0
0
Picha na 1 (1)Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akiongea na wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari,wamiliki wa shule binafsi na wanafunzi wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoani Dar es salaam leo.Katika hafla hiyo washindi wa mitihani ya taifa kwa mwaka 2013 kutoka shule za msingi na sekondari za serikali na binafsi wametunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali kutokana na ufanisi wao katika utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).Picha na 2Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw.Raymond Mapunda akiongea na wadau mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za msingi na sekondari,wamiliki wa shule binafsi na wanafunzi wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoani Dar es salaam leo.Picha na 3 (1)Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za jijini Dar es salaam waliohudhuria hafla ya Siku ya Elimu mkoa wa Dar Es Salaam wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla hiyo.Picha na 4Wadau wa elimu wakiwemo wazazi, walimu wa shule za sekondari na msingi, wamiliki wa shule binafsi na viongozi mbalimbali wakishangilia mafanikio na ushindi wa mkoa wa Dar es salaam katika mitihani ya taifa ya shule za Msingi na Sekondari  kwa mwaka 2013 leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya Siku ya Elimu.picha na 5Mkurugenzi wa Shule ya shule ya Sekondari ya Tusiime ya jijini Dar es salaam Bw. Albert Katagira akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi (kulia) kufuatia shule yake kutoa wanafunzi bora katika ufaulu wa masomo katika mitihani ya taifa kwa ngazi ya taifa na mkoa wa Dar es salaam kwa shule binafsi.Picha na 6Mwalimu Stella Kasheba (kulia) kutoka shule ya Sekondari Zanaki akipokea cheti cha ushindi kwa niaba ya Mkuu wa shule hiyo kufuatia shule ya Sekondari Zanaki ya jijini Dar es salaam kutoa mshindi Bora wa Jumla kwa shule za sekondari za serikali katika mitihani ya taifa kwa mwaka 2013.Picha na 7Mwanafunzi Hussein Hemed Hussein wa Shule ya Msingi Tusiime akipokea cheti cha pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa jumla katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 kwa shule za Binafsi za jiji la Dar es salaam.Picha na 8Mwanafunzi Hussein Hemed Hussein wa Shule ya Msingi Tusiime akionesha  cheti cha pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa jumla kwa wavulana katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 kwa shule za Binafsi za jiji la Dar es salaam alichokabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi katika hafla ya Siku ya Elimu jijini Dar es salaam.Picha na 9Mwanafunzi Joyce Lymo wa Shule ya Sekondari Kanosa, Kinondoni akionesha  cheti cha pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa jumla kwa wasichana katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 alichokabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi katika hafla ya Siku ya Elimu jijini Dar es salaam.Picha na 10Wadau wa elimu wakiwemo wazazi, walimu wa shule za sekondari na msingi, wamiliki wa shule binafsi na viongozi mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoa wa Dar es salaam leo. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

SERIKALI YAKUSANYA TAKRIBANI SHILINGI BILIONI 3 KUTOKANA NA KUONGEZEKA KWA MAKUSANYO YA MRAHABA WA MADINI

$
0
0
IMG_4403
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bruno Mteta akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu mafanikio yaliyopatikana baada ya ongezeko la makusanyo ya mrabaha kwenye madini ya ujenzi kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Ukaguzi kutoka wakala huo Mhandisi Liberatus Chizuzu.

……………………………………………………………
Frank  Mvungi-Maelezo
SERIKALI imekusanya takribani shilingi bilioni 3 kutokana na  kuongezeka kwa makusanyo ya mrabaha uliotozwa katika madini ya Ujenzi katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani katika kipindi cha Juni mwaka 2011 hadi Novemba mwaka 2013.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bruno Mteta wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Mteta alisema awali kabla wakala huo haujaanza ukaguzi wa madini ya ujenzi kiasi kilichokuwa kikikusanywa ni shilingi milioni tatu tu kwa mwaka hivyo kwa sasa kiwango hicho kimefikia wastani wa Bilioni moja kwa mwaka.
Alisema ukaguzi umeimarishwa katika vituo vyote ambavyo wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara hiyo wanalazimika kupita na kuonyesha vibali vya kusafirisha madini hayo ambavyo ni vocha maalum zinazotolewa na wakala huo ili kudhibiti wale wanaokwepa kulipa mrabaha.
“Tumejipanga vizuri kuhakikisha kuwa kila anayetakiwa kulipa mrabaha katika biashara ya madini ya ujenzi anafanya hivyo kwa kuimarisha ukaguzi kupitia vituo vyetu vya Afrikana,Pugu,Chalinze na katika maeneo yote yaliyobainishwa kutumika katika uchimbaji wa madini ya Ujenzi” alisema Mteta.
Katika hatua nyingine Mteta alisema kuwa ni wajibu wa kila mchimbaji na mfanyabiashara wa madini kulipa mrabaha unaostahiki ambapo kifungu cha 87 (6) cha sheria ya Madini ya mwaka 2010 kinachotaka mrabaha ulipwe kwa kuzingatia thamani halisi ya madini (gross value)yanapofikishwa sokoni au kwa mtumiaji.
Naye Mkurugenzi wa udhibiti na Ukaguzi wa Uzalishaji na Biashara ya Madini  Mhandisi Liberatus  Chizuzu alitoa wito kwa wananchi hasa wafanyabiashara wa madini ya ujenzi kuzingatia sheria na kanuni za Madini ili kulisaidia Taifa kujenga uchumi  imara.
Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania TMAA kwa kushirikiana na Ofisi ya Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Mashariki ulianzisha matumizi ya hati za mauzo ya Madini ya Ujenzi katika ukaguzi wa uzalishaji na mauzo ya madini ya ujenzi Kanda ya Mashariki (Mikoa ya Dar es salaam na Pwani) ambapo matumizi ya stakabadhi hizo yameongeza pato la Serikali kwa kiasi kikubwa kutokana na makusanyo ya mrabaha kwa kiasi kikubwa.

BENKI YA CRDB KUFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA MEI 10 JIJINI ARUSHA

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk.Charles Kimei akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha. Benki ya CRDB itafanyaka mkutano wake Mkuu wa Mwaka Mei 10 katika ukumbi wa AICC jijini Arusha. (Na Mpiga Picha Wetu)

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk.Charles Kimei akionyesha kitabu cha taarifa ya mwaka 2013 cha benki ya CRDB katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Arusha. Katikati ni Katibu wa Benki hiyo, John Rugambo na Mkurugenzi wa Fedha, Fredrick Nshekanabo. Benki ya CRDB itafanyaka mkutano wake Mkuu wa Mwaka Mei 10 katika ukumbi wa AICC jijini Arusha. 

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk.Charles Kimei akiongea na Waandishi wa habari (Hawapo Pichani), kuhusu Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa benki ya CRDB utakaofanyika jijini Arusha. Katikati ni Naibu Mkurugenzi  wa Benki hiyo Bi.Esther Kitoka na Mkurugenzi wa tawi la Arusha Bi.Chiku Issa. Benki ya CRDB itafanya mkutano wake Mkuu wa Mwaka tarehe 10/05/2010 katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dk.Charles Kimei akiongea na Waandishi wa habari (Hawapo Pichani), kuhusu Mkutano Mkuu wa Wanahisa wa benki ya CRDB utakaofanyika jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi  wa Benki hiyo Bi. Esther Kitoka na Bw.John Rugambo ambaye ni Katibu wa Benki. Benki ya CRDB itafanya mkutano wake Mkuu wa Mwaka tarehe 10/05/2010 katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.

Walimu wapya Wilaya ya Handeni waanza kazi na machungu

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya Handeni, Dr Khalfany Haule.

WAAJIRIWA wapya wa fani ya ualimu wa shule za msingi katika Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga wameanza kazi kwa kuonja machungu ya madeni baada ya kutopewa stahili zao zote kabla ya kuanza kazi na kusambazwa kwenye vituo vyao vya kazi kwenye maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.

Wakizungumza na Thehabari.com kwa masharti ya kutotaja majina yao kwa kuhofia kunyanyaswa na uongozi wa juu wilayani hapo, walisema kuwa kwa mujibu wa makubaliano na taratibu walitakiwa kulipwa shilingi 245,000 ikiwa ni malipo ya fedha za kujikimu kwa siku saba yaani shilingi 35,000 kwa kila siku jambo ambalo halikufanywa.

Mmoja wa walimu hao walioanza kazi tangu Aprili Mosi, 2014 alisema walipoanza kazi walilipwa shilingi 140,000 tu na kuahidiwa kiasi kingine kumaliziwa ndani ya mwezi huo, ahadi ambayo haijatekelezwa ilhali wao wakiangaika na maisha ya ugenini fedha hawana na wamepigwa marufuku kufuatilia fedha halmashauri hadi hapo itakapotangazwa.

Alisema walitegemea kwa kuwa malipo ya kujikimu hawakupewa yote wangelipewa mshahara wa mwezi Aprili jambo ambalo nalo halikutekelezwa kwani wamejibiwa kuwa, eti hakuna fedha kwa sasa hadi hapo watakapojulishwa kwenye vituo vyao vya kazi.

"...Wakati tunaanza kazi (Aprili Mosi) tulipewa shilingi 140,000 badala ya Shilingi 245,000/- tuliahidiwa tungelipwa malipo yaliobaki ndani ya mwezi wa nne lakini hadi leo hatujalipwa na tumezuiwa kwenda kufuatilia wala kuulizia malipo, wametuma ujumbe toka halmashauri kwa walimu wakuu kuwa tusiende kufuatilia mshahara wa mwezi wa nne hadi hapo itakapotangazwa, jaribu kufikiria tunaishi vipi ugenini?," alisema mmoja wa walimu hao.

Aidha mmoja wa walimu hao alisema hali ya maisha walipopelekwa ni ngumu ilhali wakitakiwa kununua vitu vya msingi vya kuanzia maisha kama vile godoro, kitanda, vyombo vidogo vya ndani na vinginevyo jambo ambalo wengine walifanya na kuishiwa kabisa na fedha kidunju waliopewa.
"Ndugu mwandishi hebu wewe fikiria unawezaje kuishi ugenini kwa shilingi 140,000/- hujanunua godoro, kitanda na maji ndoo moja huku tunanunua shilingi 500, vyombo vya ndani huna unaishi vipi katika hali kama hii?," alisema mmoja wa walimu hao huku akionesha kusikitika.

Akizungumzia taarifa hiyo leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Handeni, Dk. Khalfany Haule alipopigiwa simu alioneshwa kushangazwa na taarifa hiyo na kudai atawasiliana na mwandishi wa habari baadaye, lakini alipotafutwa baadaye simu yake ilikuwa imezimwa. 

INAWEZEKANA SANA TU *MUST WATCH By NATHAN MPANGALA

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI NCHINI.

$
0
0

Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu  mfumuko wa bei nchini.

Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
 
Ofisi ya Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa mfumuko wa bei nchini  kwa mwezi Aprili umeongezeka ikilinganishwa na mwezi uliopita kutokana na kupanda kwa bei za bidhaa na huduma mbalimbali. 
 
 Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Aprili 2014 umeongezeka na kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia 6.1 za mwezi uliopita.
 
Amesema kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali kwa mwezi Aprili 2014 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na ile iliyokuwepo mwezi Machi huku kukiwa na ongezeko dogo la upandaji wa bei  kwenye baadhi ya bidhaa na huduma kwa mwezi huu ikilinganishwa na bei za mwezi uliopita.
 
 Ameeleza kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na migahawa kwa mwezi Aprili umeongezeka hadi asilimia 8.5 kutoka asilimia 7.9 za mwezi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi imeongezeka hadi asilimia 7.8 kutoka asilimia 7.2 za mwezi uliopita huku badiliko la fahirisi za bidhaa zisizo za vyakula likipungua hadi asilimia 4.9 kwa mwezi Aprili 2014 kutoka asilimia 7.2 iliyokuwepo mwezi uliopita.
  
Kwa upande wa  mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi,amefafanua  kuwa kumekuwa na ongezeko dogo la asilimia 0.7 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.6  kwa lililokuwepo mwezi Machi mwaka huu, huku fahirisi za bei za taifa zikiongezeka hadi kufikia 150.50 kwa mwezi Aprili 2014 kutoka 149.49 za mwezi Machi.
 
Amezitaja bidhaa zilizochangia ongezeko la fahirisi za bei nchini  kuwa ni pamoja na mchele, mahindi,unga wa Muhogo,Kuku wa kienyeji, dagaa,samaki wakavu, matunda, karanga na mihogo.
 
Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia ongezeko la fahirisi amesema ni pamoja mkaa wa kupikia, huduma za matibabu, mafuta ya dizeli,na gharama ya kusaga nafaka.
 
 Kuhusu uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma kwa mwezi Aprili Bw. Kwesigabo amesema kuwa  umepungua na kufikia shilingi 66 na senti 45.
 
“Kupungua kwa thamani ya Shilingi kunamaanisha kwamba, kama mtu alikuwa na uwezo wa kununua bidhaa kwa Shilingi 100 kwa mwaka jana, kwa kipindi hiki itampasa aongeze zaidi ili aweze kununua kitu kama kile kile mfano badala ya shilingi 100 inabidi atumie shilingi 134”
 

Kuhusu ulinganifu  mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana na kueleza kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya umeongezeka na kufikia asilimia 6.41 kwa mwezi Aprili 2014  kutoka asilimia 6.27 za mwezi Machi ,  huku  Uganda ikiwa na mfumuko wa asilimia 6.7 kwa mwezi huu ikilinganishwa na 7.1 za mwezi uliopita.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MFANYABIASHARA MAARUFU WA NIGERIA ALHAJ ALIKO DANGOTE JIJINI ABUJA

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na mfanyabishara maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote alipokutana naye jijini Abuja, Nigeria, May 8, 2014 pembeni mwa Mkutano wa Dunia wa Uchumi kwa Afrika. Alhaj Dangote ni mwekezaji mashuhuri duniani na hivi sasa anajenga kiwanda kikubwa cha saruji mkoani Mtwara.
Mfanyabishara maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bi. Juliet Kairuki wakati Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana kwa mazungumzo na mfanyabishara huyo maarufu wa Nigeria jijini Abuja, Nigeria, May 8, 2014 pembeni mwa Mkutano wa Dunia wa Uchumi kwa Afrika.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono baada ya mazungumzo na mfanyabishara maarufu wa Nigeria Alhaj Aliko Dangote alipokutana naye jijini Abuja, Nigeria, May 8, 2014 .PICHA NA IKULU

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LA MBUTU WILAYANI IGUNGA LEO.

$
0
0

 Meneja Mradi wa ujenzi wa Daraja la Mbutu,Injinia Makoye Luhuya akielezea maendeleo ya ujenzi wa daraja la Mbutu kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo,wilayani Igunga mkoani Tabora
 Ujenzi wa daraja la Mbutu ukiendelea kwa kasi
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiweka mbao wakati wa ujenzi wa daraja hilo ukiendelea,wilayani Igunga mkoani Tabora mapema leo asubui.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa  Meneja Mradi wa ujenzi wa Daraja hilo,Injinia Makoye Luhuya kuhusu ujenzi wa daraja la Mbutu, wilayani Igunga, leo Mei 9, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani Tabora. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (mbele) akishuka, baada ya kukagua ujenzi wa daraja la Mbutu, wilayani Igunga, leo Mei 9, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kuimarisha uhai wa chama na kusikiliza kero za wananchi mkoani Tabora. 

 Sehemu ya Daraja hilo Mbutu kama lionekanavyo pichani.

Wezi waiba miundombinu ya soko la Ngiu Makete

$
0
0
Katika hali ya kushangaza na kusikitisha, wezi wasiofahamika wameiba baadhi ya miundombinu ya soko la Ngiu wilayani Makete mkoani Njombe licha ya soko hilo kuwa na mlinzi.

Mwandishi wa blog hii ambaye amefika eneo la tukio mara baada ya kupenyezewa taarifa hizi na wananchi, ameshuhudia baadhi ya miundombinu haipo ikiwemo mifuniko yote ya chuma inayofunikia masinki ya vyoo, pamoja na mabomba ya kutiririshia maji ya mvua

Taarifa kamili na picha zote za tukio hilo zitakujia baadaye kidogo.
 Muonekano wa soko la Ngiu lililopo kata ya Iwawa, Makete mjini.
 Chemba ya choo cha soko hilo ikionekana baada ya wezi kuiba mifuniko yote mitatu ya kufunikia chemba hiyo .Na Edwin Moshi wa globu ya jamii, Makete
Viewing all 46396 articles
Browse latest View live




Latest Images