Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel

Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels

Showcase

Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 283 | 284 | (Page 285) | 286 | 287 | .... | 1897 | newer

  0 0

  0 0

  Kundi la Kwanza la Washiriki wa Kanda ya Kusini wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kupewa semina elekezi juu ya maswala mbalimbali kuhusiana na filamu na maisha kwa ujumla wakati walipofika katika ukumbi wa safari lounge kwaajili ya kushiriki kwenye shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika Mjini Mtwara leo.
  Baadhi ya washiriki kutoka Kanda ya Kusini wakiwa wamejitokeza katika usaili wa Kushiriki shindano la Tanzania Movie Talent katika Ukumbi wa Safari lounge uliopo Eneo la Maduka Makubwa, Mtwara Mjini wakiwa kwenye foleni tayari kwa shindano kuanza.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Proin Promotions wakiwabandika washiriki namba za ushiriki katika Shindano la Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika katika Kanda ya Kusini, Mkoani Mtwara leo.
  Washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents wakisubiri kuingia kwa majaji kwaajili ya kuanza kuonyesha Vipaji vyao vya kuigiza katika shindano la Kusaka Vipaji vya Kuigiza la Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika Kanda ya Kusini Mkoani Mtwara.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, asalimiana na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam leo Mei 9, 2014 kwa ajili ya kufungua Kongamano la siku mbili la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo linatarajia kumalizika kesho.

  Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Kongamano la siku mbili la Kampeni ya kudhibiti Ujangili na kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. Kongamano hilo lililofunguliwa leo Mei 9, 2014, linatarajia kumalizika kesho kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Hyat Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, akizungumza wakati wa Kongamano hilo.

  Baadhi ya washiriki wa Kongamano hilo, wakimsikiliza Makamu wa Rais Dkt. Bilal, wakati akihutubia kufungua rasmi Kongamano hilo, leo kwenye Hoteli ya Hyat Kilimanjaro jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Hofu ya kupoteza soko kwa makampuni ya kigeni yanayozalisha umeme dhidi ya makampuni ya kitanzania imetajwa kuwa chanzo cha vita dhidi ya kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).

  Chanzo cha uhakika kutoka Wizara ya Nishati na Madini kimetoa taarifa hiyo kwa gazeti hili jana kuwa kwa zaidi ya muongo mmoja, kampuni za kigeni zimekuwa zikipata faida kubwa kwa kuzalisha umeme na kuuza kwa bei ya juu nchini.

  Kampuni ya IPTL ambayo inamilikiwa na kampuni ya kizalendo, Pan African Power Solutions Tanzania Limited (PAP) iliishtua dunia mwishoni mwa mwaka jana pale ilipotangaza dhamira yake ya kushusha bei zake kutoka senti za Kimarekani 26 na 30 ya sasa mpaka senti za Kimarekani sita (6) na nane (8) kwa kila unit, pale itakapobadilisha mitambo yake kuweza kutumia gesi badala ya mafuta.

  Kwa sasa, makampuni mengine katika soko yanatoza kati ya senti za Kimarekani 38 na 60 kwa kila unit. “Watanzania wasidanganywe na taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari  kuwa IPTL ilinunuliwa na PAP bila kufuata sheria. Kuna kampeni ya kupakana matope kwa tamaa ya kuzalisha umeme kwa watanzania kutokana na biashara hii kuwa na faida kubwa katika sekta hii muhimu  kiuchumi ", chanzo hicho kilisema.

  Aidha, kampuni ya PAP katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana, imesema kuwa kampuni imeshtushwa na baadhi ya wawekezaji katika sekta hiyo pamoja na wanasiasa kuanzisha vita dhidi yao mara baada ya kutangaza kupunguza gharama za umeme.

  Uongozi wa kampuni hiyo umesema kuwa watanzania watafurahia gharama hizo za chini baada ya  utekelezaji wa mkakati wao wa utanuzi na ubadilishaji wa mfumo wa mitambo yao ambao utaongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme  kutoka mega wati 100 za sasa mpaka mega wati 500.

  Taarifa fupi iliyotolewa jana na katibu na mshauri wa maswala ya sheria wa IPTL/PAP, Bw Joseph Makandege, imesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikikumbana na changamoto ambazo zinajaribu kuzorotesha jitihada za uongozi mpya za kuleta mabadiliko ambayo yatapelekea kampuni hiyo kuanza kuzalisha umeme wenye gharama nafuu kwa watanzania wote.

  Taarifa hiyo imetolewa baada ya machapisho mbalimbali ya vyombo vya habari yanayoishutumu kampuni hiyo kutoa hongo kwa wajumbe wa kamati ya bunge ya nishati na madini kulinda matakwa yao au kuwalinda dhidi ya tuhuma mbali mbali wanazo husishwa nazo. 
  "Uongozi wa PAP katu haijapendezwa na jitihada za kuiangusha kampuni badala ya kushirikiana katika kuhakikisha kuwa tunazalisha umeme ambao utakuwa na manufaa makubwa kwa taifa hili na walaji wote nchi nzima.

  "Tukiwa kama kampuni ya ufuaji umeme, tunaelewa faida za kiuchumi zitokanazo na umeme wa gharama nafuu kwa mteja mmoja mmoja na kwa maendeleo ya kiuchumi ya nchi nzima. Kwa sababu hiyo ndiyo maana sasa tumeelekeza jitihada zetu katika kuona ni jinsi gani ya kuzaliza umeme wa gharama nafuu ambao utasaidia kuleta mabadiliko ya kiuchumi ya nchi hii, pasipo kuingia katika malumbano ambayo yataturudisha nyuma na kushindwa kutekeleza lengo letu la kuwekeza vilivyo katika sekta hii muhimu," ilisomeka taarifa hiyo.

  Bw. Makandege alisema kuwa kampuni yake imeamua kutafuta njia nzuri ya kuzalisha umeme wa gharama nafuu, ukilinganisha na wazalishaji wengine katika soko, sababu inaamini katika kutumia uwepo wake kuboresha maisha ya wateja wake na kuleta mabadiliko katika jamii inayoizunguka.

  "Uongozi mpya wa IPTL/PAP unaamini katika kuwapatia wateja wake matokeo yaliyo chanya. Njia pekee ya kulifanya hili ni kutoa bidhaa/huduma zenye gharama nafuu kwa wateja, licha ya wateja hao kuwa na viwango tofauti vya kimapato," alisema.
  Mbali na uzalishaji wa umeme, IPTL/PAP imekuwa ikijihusisha na shughuli mbali mbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kuwajengea vijana uwezo wa kifedha ili kuweza kuanzisha Saccos yao ambayo itawasaidia kujijenga kiuchumi.

  Kampuni hiyo pia imekuwa ikiunga mkono jitihada za serikali za kufikia malengo ya Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now) katika elimu kwa kutoa misaada mashuleni pamoja na taasisi za kijamii kama makanisa.

  0 0

  Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakitunishiana msuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba siku ya jumamosi ya may 10 picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com
  Bondia Mohamed Matumla akipima uzito.
  Mabondia Fransic Miyeyusho kushoto na Mohamed Matumla wakitunishiana msuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika katika ukumbi wa P.T.A Sabasaba siku ya jumamosi ya may 10 picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akifungua semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB iliyofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha jana. Kulia ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, anayeshughulika na Uendeshaji na Huduma kwa Wateja, Saugata Bandyadhiyay na Naibu Mkurugenzi Mtendaji Huduma Shirikishi wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka. (Na Mpiga Picha Wetu)
   Washiriki wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika Semina hiyo.
   Washiriki wa semina ya Wanahisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika Semina hiyo.

  Benki ya CRDB inatarajia kuuza Hisa zake katika Soko la Hisa la Nairobi, fursa ambayo itatoa wigo mpana zaidi wa biashara ya hisa za Benki hiyo katika soko la Afrika Mashariki.

  Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Dk. Charles Kimei wakati wa siku ya kwanza ya mkutano mkuu wa wanachama wote unaofanyika hapa jijini Arusha.

  Kimei alisema uuzaji wa hisa katika Soko la Hisa la Nairobi utafanya bei ya hisa za benki ya CRDB kupanda kutokana na ukweli kwamba katika soko la Dar es Salaam bei ya hisa zote ipo chini sana.

  Mfano kama ingeweza kufanyika mahesabu ya kitaalam, bei halisi ya hisa ya  CRDB  ingetakiwa iwe zaidi ya shilingi 500 badala ya 310 ya sasa. Na kitendo cha kuuza hisa kwenye soko la Nairobi ina maana wafanyabiashara wengi watavutiwa na wataweza kununua na kuuza hisa hizo.

  Pia ikizingatiwa ukweli kuwa sehemu kubwa ya wanahisa wa Benki ya CRDB ni wanahisa mmoja mmoja ambao huuza na kununua hisa zao kutokana na hali ya maisha inayowakabili kwa wakati Fulani.
   Kumbe kwa kuingia kwenye Soko la Nairobi ina maana kutakuwa na mchanganyiko na wafanyabiashara wakubwa.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akihututubia katika katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika  Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga, ambapo alisifu utenaji a Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Elibariki Kingu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo pamoja na  Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa uchapakazi wao. pamoja na ubunifu wa miradi mbalimbali ya kuwasaida vijana.
    Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM na Wananchi mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uwanja wa Sokoine mjini Igunga jioni ya leo,kwenye mkutano wa hadhara ambapo Katibu Mkutano wa CCM,Ndugu Kinana alihutubia.
   Katibu wa Itikdi n Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika katika  Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (pichani kulia) akimpokea aliyekuwa Katibu wa chama cha CUF Wilaya ya Igunga, Michael Maganga (aliyenyoosha kadi yake ya CUF juu), aliyeamua kukihama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Sokoine.
   Wakifuatilia mkutano wa hadhara wa CCM,kwenye uwanja wa Sokoine mjini Igunga leo jioni.
   Baadhi ya Wafuasi wa chama cha CCM na Wananchi mbalimbali wakifuatilia  yaliyokuwa yakijiri kwenye uwanja wa Sokoine mjini Igunga jioni ya leo,kwenye mkutano wa hadhara ambapo Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alihutubia.
    Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua shamba la alizeti la  ekali 25 la Kikundi cha Vijana katika Kijiji cha Iborogero, wilayani Igunga, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama , kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitazama mmea wa alizeti,wakati alipokwenda kagua shamba la alizeti la  ekali 25 la Kikundi cha Vijana katika Kijiji cha Iborogero, wilayani Igunga, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama , kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi.
  Sehemu ya shamba la alizeti la  ekali 25 la Kikundi cha Vijana katika Kijiji cha Iborogero, wilayani Igunga, wakati  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokagua wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama , kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi. 
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na baadhi ya Wananchi alipokuwa akiwasili mjini Igunga,kabla ya kuzindua mradi wa Vijana Saccos wa mjini humo mkoano Tabora.
  Katibu MKuu wa CCM,Ndugu Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa wakala wa uuzaji wa matrekta kwa wanavikundi,yanayouzwa na Vijana SACCOS LTD,ya Igunga,inayojumuisha vikundi mbalimbali vya wilaya hiyo,wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali pamoja na wananchi wilayani humo,Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Igunga,Mh.Elibariki Kingu.
  Ndugu Kinana akiwasha moja ya trekta mara baada ya kuuzindua uwakala wa zana za kilimo wa Vijana SACCOS LTD wilayani humo.
   Sehemu ya wananchi walikuwa wakishuhudia uzinduzi wa wakala wa uuzaji wa matrekta kwa wanavikundi,yanayouzwa na Vijana SACCOS LTD,ya Igunga,inayojumuisha vikundi mbalimbali vya wilaya hiyo

  0 0  “Ni kwa masikitiko makubwa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (ya Malawi) unauarifu umma kufariki dunia kwa Balozi Flossy Gomile-Chidyaonga baada ya kuugua kwa muda mfupi jijini Dar es salaam mchana huu”, imesema taarifa iliyotolewa na msemaji wa Wizara hiyo Quent Kalichero.

  “Tangu mwaka 2006 Marehemu Bi Flossy Gomile-Chidyaonga alikuwa Naibu Balozi wa Malawi London kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania mnamo Septemba mwaka 2011”, imesema taarifa hiyo na kuongezea kuwa taratibu za mazishi zitatangazwa baada ya taratibu kukamilika.

  MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MALI PEME PEPONI-AMEN  0 0

   Wananchi wakisubiri kesi zao zianze.

  Na Edwin Moshi wa Globu ya Jamii, Makete
  Watuhumiwa na walalamikaji mbalimbali wenye kesi zao katika mahakama ya wilaya ya Makete mkoani Njombe wameendelea kuonja tena machungu ya kuahirishiwa kesi zao leo Ijumaa Mei 09, kwa kile kilichoelezwa kuwa hakimu kushindwa kufika

  Wakisikika wakiongea mahakamani hapo wakiwa katika makundi makundi, wamesema hawakatai wao kuahirishiwa kesi zao ila zinapoahirishwa mara kwa mara kwa muda mrefu inawaumiza wananchi ukizingatia wengi wao wanatumia fedha nyingi ili kuweza kuhudhuria mahakamani
  Wakisikiliza taarifa ya kuahirishiwa kesi zao.
  "Hakimu wa wilaya sisi hatuna, hebu fikiria mara ya mwisho hakimu amefika hapa mwezi wa Februari akasikiliza kesi zetu vizuri tu, lakini tangu hapo tumekuwa tukiahirishiwa tu kesi kila tukija, na sababu tunaambiwa hakimu ametingwa na majukumu mengine, sasa jamani hii kero ni hadi lini" alisikika mmoja wa waliofika mahakamani hapo akizungumza

  Licha ya kuongezeka kwa kesi na huduma mbalimbali za kimahakama katika mahakama ya wilaya ya Makete, bado wilaya hiyo imeendelea kusota kwa kukosa hakimu wa mahakama hiyo hivyo hakimu kutoka mahakama ya Njombe hulazimika kuja kuendesha kesi katika mahakama ya wilaya ya Makete na mahakama yake ya Njombe

  Kutokana na jiografia ya Makete, mtu mwenye kesi katika mahakama ya wilaya kama yupo nje ya Makete mjini hulazimika kutumia gharama kubwa za kusafiri hadi kufika mahakamani kutokana na uhaba wa magari ya usafiri

  "Kwa mfano sisi tuliahirishiwa kesi juzi tarehe 30 Aprili tukaambiwa tuje leo, bado na leo ni kama yale yale tu, mimi naiomba serikali itupe hakimu wetu kwa sababu huyu hakimu anatoka Njombe na huko ana kazi za kimahakama yake pia sasa akitingwa si rahisi kuja huku" amesema mwananchi mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake

  Akitoa taarifa ya kuahirishwa kesi hizo hii leo Mkuu wa polisi wilaya ya Makete (OCD) Alfred Kasonde amewapa pole wananchi hao wenye kesi mahakamani hapo na kusema anawaomba wawe wavumilivu, na kesi zao zimeahirishwa hadi Mei 23 mwaka huu
  Wakiondoka baada ya kesi zao kuahirishwa.
  "Jamani naimani mmenisikia jinsi nivyokuwa nazungumza nao kwenye simu, nimewaeleza hali halisi lakini ndio hivyo tena, mimi nawaomba muwe wavumilivu yatakwisha tu, kila kitu kitakwenda sawa, naombeni mje kwa ajili ya kesi zenu tarehe 23 mwezi huu, poleni sana" amesema Kasonde

  1
  From left is Political Officer Delegation of the European Union Tom Vens, Rear Admiral Commander Task Force 465 Jürgen zur Mühlen , and the Chargé d´Affaires a.i. Hans Koeppel of the German Embassy in press conference for the role of EUNAVFOR, its cooperation with Tanzania and the recently signed European Union-Tanzania Transfer Agreement which allows to trial pirates, who are captured by European naval forces, in Tanzanians courts.
  2
  The Chargé d´Affaires a.i. Hans Koeppel from Embassy of Federal Republic of Germany welcomed the visit of the flagship as “an important sign of the common fight against piracy along the coast of the Indian Ocean”. He also talk about the aim of Task Force to fight against pirates with the countries bordering the coast of Indian Ocean including Tanzania.
  3
  Political Officer Delegation of European Union Tom Vens discuss about Europe day and Europe day , He also talk about the European Task Force that help security situation in the Earth lastly he discuss about good relationship between European Union and East African Community and Good Political relationship Between European Union and Tanzania.
  4
  Commander Force Force 465 Rear Admiral Jürgen zur Mühlen emphasized that the threat of piracy continues to exist. 10 days ago, the crew of Brandenburg boarded an Indian dhow which was formerly held hostage by pirates. The pirates fled from the captured dhow as EU naval forces intervened from the air and sea. “This event confirms that the piracy threat is still very real in the Indian Ocean. The deterrence and swift action by EU Naval Force once again denied the freedom of action to pirates”,
  IMG_0221
  Public Relation Officer of European Union Dormann addressing some issues during Press Conference.
  8
  9
  Different media During the Press Conference at Umoja House today.
  To Listen Click the Link down

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa jimbo la Nzega,Mh.Hamis Kingwangala mapema leo asubuhi katika kijiji cha Ziba,mpakani mwa Igunga na Nzega, wakati Ndugu Kinana na Ujumbe wake akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi, Siasa na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye mara baada ya kuwasili wilayani humo kuendelea na ziara yake ya siku 10 mkoani Tabora.Kinana amewasilia wilayani Nzega akitokea wilayani Igunga mkoani Tabora.
    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalaimiana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa,Hussein Bashe mara baada ya kupokelewa katika kijiji cha Ziba,mpakani mwa Igunga na Nzega mkoani Tabora.
  Mkuu wa Wilaya ya Igunga ambaye pia ni Kaimu mkuu wa Wilaya ya Nzega,Elibariki Kingu akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Nzega,Mh.Hamis Kingwangala mapema leo asubuhi wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipowasilia wilayani Nzega kuendelea na ziara yake ya siku 10 mkoani Tabora,kushotoo ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh Fatma Mwasa.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vijana wa Green Gard,kulia ni  Katibu wa NEC,Itikadi, Siasa na Uenezi CCM Taifa,Nape Nnauye
    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vijana wa Green Gard na viongozi mbalimbali wa Wilaya na Mkoa,katika kijiji cha Ziba mapema leo asubuhi.
    Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mbele wananchi wa kijiji cha Ziba mara baada ya kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Wilaya na Mkoa.
   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya mara baada ya kupokea taarifa fupi ya chama na Serikali,katika ukumbi wa RC mjini Nzega leo asubuhi. CCM Taifa,Nape Nnauye

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipokea maua muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ndjili jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) Augustin Matata Ponyo Mapon akimkaribisha na kuzungumza na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kuwasili katika mji mkuu wan chi hiyo Kinshasa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.Rais Kikwete baada ya atakutana na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila na kufanya naye mazungumzo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali na kumpa pole balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) Mh.Anthony Ngereza Chehe aliyelazwa katika hospitali ya Ngaliema Health Centre jijnii Kinshasa baada ya kuugua malaria.Rais Kikwete yupo jijini Kinshasa DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na Freddy Maro

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili(picha na Freddy Maro)
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa walipokutana kwa mazungumzo

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa  katika mazungumzo na mwenyeji wake Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Demokrasia ya  Kongo ikulu ya Kinshasa leo.Rais Kikiwete alikuwa nchini DRC kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha na Freddy Maro.

  Rais Jakaya Kikwete  amewasili mjini Kinshasa  Jamhuri ya Watu wa Kongo (DRC) usiku wa kuamkia leo kwa ziara ya kikazi akitokea nchini Nigeria ambapo amehudhuria Mkutano wa Viongozi kuhusu Uchumi barani Afrika.
   Akiwa Kinshasa, leo tarehe 10 Mei, Rais Kikwete amefanya  mazungumzo na Rais Joseph Kabila ambapo wanatarajia kuzungumzia uhusiano baina ya nchi  mbili hizi na hali ya kisiasa kwa ujumla katika ukanda wa Jumuiya ya ushirikiano wa Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). 

   Mara baada ya Mazungumzo haya Rais Kikwete ameondoka kuelekea Luanda , Angola kwa ajili ya mazungumzo na Rais Jose Dos -Santos.

     Wakati huo huo, Rais Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Rais Joyce Banda wa Malawi kufuatia kifo cha ghafla cha Balozi wa Malawi nchini  Tanzania Flossy Gomile-Chidyaonga kilichotokea tarehe 9 Mei jijini Dar-Es-Salaam. 

   "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa Balozi Chidyaonga, ni huzuni kwetu sote" Rais amesema na kumuelezea Balozi Chidyaonga kuwa alikuwa mcheshi na aliyependa kushirikiana na wenzake kwa moyo mkunjufu. 

   " Ni huzuni zaidi kwetu sote kwakuwa kifo chake kimetokea ghafla mno kwa  mtu tuliekua tunashirikiana naye kwa karibu katika juhudi za kukuza na kuimarisha mahusiano baina yetu" Rais amesema na kuongeza kuwa, kifo chake kimetokea wakati tunamhitaji zaidi na hivyo kusababisha pengo kubwa" 

   Rais amemuomba Rais Banda kufikisha salamu zake binafsi na za Watanzania kwa ujumla kwa familia ya marehemu, ndugu, Jamaa na Wamalawi wote kwa ujumla na kumuombea marehemu kwa mwenyezi Mungu, ampe mapumziko mema milele. 

   Imetolewa na; 
  Premi Kibanga, 
  Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi, 
  Kinshasa-DRC 10 Mei 14

  0 0  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo mapema Machi mwaka huu alikabidhiwa nishani ya kumbukumbu ya Profesa M.O. Oyawoye aliyewahi kuwa Profesa wa kwanza duniani kutoka Bara la Afrika katika masuala ya jiolojia huko nchini Nigeria. Profesa Muhongo alikabidhiwa nishani hiyo na timu ya wanajiolojia kwa kutambua mchango wake mkubwa barani Afrika na duniani kwa ujumla. Nishani hiyo alikabidhiwa balozi wa Tanzania nchini Nigeria Mhe. Daniel Ole Njoolay kwa niaba yake.
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiwa ofisini kwake huku akiwa amevaa nishani hiyo

  0 0

   Mwigizaji na Mchekeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Bongo Movie Unity, Steven Mengere 'Steve Nyerere' (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juzi baada ya kuteuliwa kuwa msimamizi wa mkuu Wasanii wa nje ya Bunge Maalum, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tanzania Kwanza nje ya bunge, Renatus Muadhi, na katikati ni Mwenyekiti wa Taasisis hiyo, Agustino Matefu.
   Mwigizaji na Mchekeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Bongo Movie Unity, Steven Mengere 'Steve Nyerere' (kushoto) akikabidhiwa mkataba wa kuwa msimamizi wa mkuu wa wasanii wa nje ya Bunge Maalum na Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Kwanza nje ya bunge, Agustino Matefu. Makabidhiano hayo yalifanyika juzi jijini Dar es Salaam.
  ---
  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
  WASANII wa Bongo Movie, muziki wa dansi, taarab, maigizo na tamthilia wametangaza kuzunguka nchi nzima wakiwa na kamati ya Tanzania Kwanza Nje ya Bunge Maalum la Katiba kwa lengo la kutangaza amani kwa vijana wa rika lote bara na visiwani.

  Baadhi ya wasanaii hao ni pamoja na Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ambaye ameteuliwa kuwa msimamizi mkuu wa uwakilishi kwa upande wa wasanii katika Tanzania kwanza nje ya Bunge maalum, Muungano huo uko chini ya Mwenyekiti Augustino Matefu.

  Akizungumza juzi na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Steve amesema kwamba ataungana na wasanii ambao wako katika vyama mbalimbali kama vile Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, NCCR, Mageuzi , Cuf na vyama vingine huku wote wakiwa na lengo moja tu la kuhimiza mchakato wa katiba uendelee huku wanasiasa wakizingatia kudumisha amnai na umoja wa Watanzania.

  Nyerere aliongeza kwa kusema kuwa yeye hakuwa na kipingamizi pindi alipoambiwa amechaguliwa kuwa miongoni mwa wasimamizi wa mpango huo ambao umewakutanisha vijana kutoka katika itikadi mbalimbali za vyama vya siasa.

  “Nilipoambiwa hili jambo niliweka itikadi zangu za chama pembeni na kuuvaa Utanzania kwanza ili kuunganisha fani zetu wote kwa pamoja na kuweza kuwahimiza wananchi wadumishe amani tuliyokuwa nayo nchini” alisema Nyerere. Aliongeza pia kwa kuwaomba viongozi wa dini masheikh na maaskofu wakiwemo mapadri wote kuungana nao wasanii hao katika kuhimizaani ya amani ya nchi.

  “Sisi wasanii tunapata riziki zetu kutokana na amani na utulivu uliopo nchini mwetu hivyo kila msanii na Mmtanzania aone ni jambo la fedheha kuiichezea amani ambapo siku ikipitea tutakwenda kuomba hifadhi katika nchi za jirani zilizopata uhuru na kufuata ushauri kutoka kwetu”.,

  Aliongeza kwa kusema kwamba ana imani kubwa watanzania watawaelewa pindi watakapokuwa katika ziara hiyo kuzunguka nchi nzima huku wakiwa na mabalozi watano kutoka kila nyanja ya sanaa ambazo ni muziki wa taarab, Hip Hop, Sanaa za maigizo, Michezo na tamthilia. Mkutano mkubwa unatarajiwa kufanyika Kibanda Maiti Zanzibar.

  0 0

   Jiwe kubwa Likiwa limeanguka toka mlimani na kuziba Barabara ya Vuga Kutoka Mombo kuelekea korogwe na Lushoto
   Baadhi ya wasafiri wakitembea kwa miguu baada ya kukwama eneo  Vuga  kwa takribani Masaa sita
   Kwa juu ni mlima ambapo jiwe hilo liling'oka na kudondoka hatimaye kuziba barabara hiyo kwa takribani masaa sita
   Abiria na madereva wakiwa wamekaa wakisubili mamlaka zinazohusikka wafike ili kutoa msaada wapate kuendelea na safari.
   Vyombo vya dola wakiwa wamefika eneo la tukio tayari kuweza kulisogeza jiwe hilo ili abiria na watumiaji wa barabara ya vuga kuendelea na shughuli zao
  Hayo ni baadhi ya mawe ambayo yanaonekana kwa juu ya barabara ya vuga inayounganisha kutoka mombo kuelekea lushoto.

  Hali ya usafiri kutoka mombo-korogwe kuelekea wilaya ya Lushoto mkoani tanga ilikuwa tete baada ya jiwe kubwa kuangua barabarani katika eneo la vuga road.Jiwe hilo lilisababisha wasafiri wa barabara hiyo kukwama kwa takribani masaa 6 bila magari kupita.Lakini hatimaye baadae vyombo vya usalama wakishirikiana na wanainchi waliweza kulitoa na hatimaye usafiri wa njia hiyo kurejea katika hali yake ya kawaida.

older | 1 | .... | 283 | 284 | (Page 285) | 286 | 287 | .... | 1897 | newer