Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Benki ya KCB Tanzania yaandaa Futari kwa wateja wake wa Dar es Salaam

$
0
0
Benki ya KCB Tanzania leo jioni imeandaa Futari kwa ajili ya wateja wake katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, ikihudhuriwa pia na wajumbe wa bodi pamoja na wafanyakazi wa Benki.

Akiongea kwenye tukio hilo, Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya KCB Tanzania, Zuhura Muro, amesema benki imeamua kuandaa futari hiyo ili kujumuika na wateja wake kama hatua ya kuonyesha mshikamano na umoja katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

“Hapa Benki ya KCB, tunathamini na kutaambua wajibu wetu katika jamii hususani katika nyanja za elimu, mazingira na ujasiriamali.” Amesema Muro huku akiongeza kuwa benki imekuwa ikiwekeza katika masuala ya kijamii tangu ilipofungua milango yake nchini Tanzania mnamo mwaka 1997.

Amesema pia kuwa benki inaheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na ukweli kwamba, ni kipindi ambacho mwanadamu anajiweka karibu na Muumba kupitia sheria ya kufunga na kufanya maombi.

“Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni ukumbusho kwetu wote kujiweka karibu na Muumba wetu. Ni mwezi ambao pia unatukumbusha kufanya kilicho chema mbele za Mungu wetu. Ndiyo maana hapa KCB tumeamua kuandaa futari hii ili kujumuika na wenzetu.” Amesema Muro.

Muro pia ameongeza kuwa benki ina idara maalum inayojikita katika kutoa huduma kwa wateja wake wa imani ya Kiislam, idara inayojulikana kama "Sahl Banking" inayopatikana kwenye matawi yote ya KCB.

Muro ameongeza kuwa KCB ina jumla ya matawi 14 nchi nzima na ni taasisi ya kwanza ya kifedha nchini Tanzania kuanzisha Shariah Banking kwa ajili ya kuwahudumia wateja wake wa Kiisalam.

“Benki ya KCB imekuwa ikijidhatiti katika kuboresha huduma kulingana na mapendekezo mbalimbali ya wateja”. Kimario amesema huku akitolea mfano Shariah Banking ambayo inafuata muongozo wa Imani ya Kiislam katika nyanja ya kifedha.

Muro amewaomba wale ambao hawajajiunga na Benki ya KCB kufungua akaunti zao ili waweze kufurahia huduma bora na za kipekee zinazotolewa katika matawi yote ya KCB nchini.

Benki ya KCB Tanzania imekuwa ikiandaa futari za aina hii kila unapofika mwezi mtukufu wa Ramadhani kama hatua ya kuungana na jumuiya ya waislam wote nchini katika kutimiza funga zao.








UBA Tanzania yasherekea wiki ya Bara la Afrika

$
0
0
BENKI ya UBA Tanzania imeungana na nchi zingine za Afrika kwa kushehereke siku ya Afrika kama sehemu ya kumbukumbuku ya kila mwaka ya kuanzishwa kwa OAU na sasa AU ambao ulianzishwa Mei 25, mwaka 1963 

Kwa hapa nchini benki hiyo iliadhimisha siku hiyo UBA Tanzania, iliadhimisha siku hiyo kwa wafanyakazi wake kuvaa ngu za mitindo mbalimbali yenye kuonyesha uhalisia wa waafrika.

Akizungumzia siku hiyo Mkuu wa Kampuni ya Benki ya UBA Tanzania, Mussa Kitambi, alisema kuasisiwa kwa benki hiyo kunajumuisha historia ya Afrika kupitia mavazi, umoja na vyakula vya jadi.

“Siku ya Afrika (zamani ya Uhuru wa Afrika na Siku ya Uhuru wa Afrika) ni kumbukumbu ya kila mwaka ya msingi wa Shirika la Umoja wa Afrika (OAU) inayojulikana kama Umoja wa Afrika mnamo 25 Mei 1963. Inaadhimishwa katika nchi mbalimbali katika bara la Afrika , pamoja na duniani kote,” alisema Kitambi 

Katika kukumbuka siku hiyo shughuli mbalimbali zilifanyika kuvunja nazi, kukata keki na wateja, ngoma ya jadi na wafanyakazi, ngoma ya jadi na kikundi cha flash.
Mkuu wa Kampuni ya Benki ya UBA Tanzania, Mussa Kitambi, akipokea hati ya kutambuliwa kutoka kwa Waziri Mkuu wa Kassim Majaliwa, baada ya benki hiyo kusaidia futari kwa ajili ya watoto yatima 320 wa vituo sita vya Mkoa wa Dar es Salaam. Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Afrika.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya UBA Tanzania, Brendansia Kileo (wa pili wa kulia), akiwa na amembeba mtoto wa kituo kimojawapo cha yatima jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Afrika.
Wafanyakazi wa Benki ya UBA Tanzania, wakiwa katika mavazi ya kiasili ikiwa ni sehemu ya sherehe ya kumbukumbu ya nchi huru za Afrika
Wanyakazi wa Benki ya UBA Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja katika sherehe za wiki ya Afrika

United States Disburses Grants Worth $750,000 to Create Jobs for Rural Youth

$
0
0
Ms. Abella Bateyunga (right) from the Tanzani a Bora Initiative receives Advancing Youth grant for 209,057,674 TZ shillings. Ms. Bateyunga is accompanied, from left to right, by Mbeya Regional Commissioner, J. Chalamila; PO-RALG Minister, Selemani Jafo; USAID Mission Director, Andrew Karas; and USAID Private Sector and Youth Project Management Specialist Joyce Mndambi. (Photo: Courtesy of U.S Embassy).



USAID Mission Director, Andy Karas addresses a Feed the Future meeting in Mbeya on Wednesday. (Photo: Courtesy of U.S Embassy).

***********************************

Mbeya, Tanzania – On May 29, 2019, the United States Government disbursed grants worth a total of $750,000 to nine institutions that support job creation, entrepreneurship, leadership, and healthy living among youth.



The grants are supported by the Feed the Future Tanzania Advancing Youth activity, funded by the United States Government through the United States Agency for International Development (USAID), and are expected to create 950 jobs for youth in 700 new or improved youth-led enterprises across the regions of Iringa, Mbeya, and Zanzibar.

The Mission Director for USAID, Andrew Karas, and Honorable Suleiman Jafo, the Minister for the President’s Office Regional Administration and Local Government (PO-RALG), presented the grants to the local institutions.
During his remarks, Mr. Karas noted that “Investing in youth leadership in Tanzania is a priority for USAID and the Government of Tanzania. Tanzania is a young country, and its population is expected to double in the next 25 to 30 years. Deliberate efforts are needed by the government, private sector, and communities to ensure that the energy, talents, and
optimism of today’s youth, as well as the next generation, make Tanzania a place of promise and prosperity for all.”

The Advancing Youth activity encourages rural youth to engage in Tanzania’s agriculture sector and supports increased economic opportunities for young people aged 15–35 while promoting leadership and healthy lifestyles. Through its grants program, Feed the Future Tanzania Advancing Youth transforms challenges into opportunities for rural youth to drive and advance Tanzania’s economic growth.

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA NCHINI AKITOKEA AFRIKA KUSINI, NAMIBIA NA ZIMBABWE

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare kabla ya kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kurejea nyumbani akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Brigedia Jenerali Abdallah M. Alphonce na wafanyakazi wa ubalozi huo Bi. Alice Madele na Bi Joyce Makoye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare, kabla ya kupanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kurejea nyumbani akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Majenerali wa Jeshi akiwa na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019 baada ya kuhitimisha ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.
 Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa akipeana mikono na kuagana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhanga Mpina aliyeongozana na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019 .
Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa akipeana mikono na Ofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Bi. Joyce Makoye wakati wa kumsindikiza Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipohitimisha ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019. Wengine ni Bi Alice Madele pamoja na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini humo Brigedia jenerali Abdallah M. Alphonce 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019 baada ya kuhitimisha ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mhe. Dkt. Emmerson Mnangagwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Mugabe jijini Harare leo alhamisi Mei 30, 2019 baada ya kuhitimisha ziara yake ya Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi
.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi Diwani Athumani baada ya kutelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda.

Tigo yazindua ofa ya ‘Saizi Yako’ inayokidhi mahitaji ya kila mteja

$
0
0
Afisa Biashara Mkuu wa kampuni ya Tigo Tarik Boudiaf(kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na mchekeshaji Lucas Muhavile maarufu kama Joti (kati kati) Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko wa kampuni ya Tigo William Mpinga muda mfupi baada ya uzinduzi wa ofa mpya inayojulikana kama ‘Saizi Yako‘ uliofanyika jijini Dar es Salaam.

    Afisa Biashara Mkuu wa kampuni ya Tigo Tarik Boudiaf(kati kati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa mpya inayojulikana kama ‘Saizi Yako‘ uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo, Idara ya Huduma za Masoko William Mpinga na kulia ni Balozi wa kampeni hiyo Lucas Muhavile maarufu kama Joti.
    Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko wa kampuni ya Tigo William Mpinga (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa mpya inayojulikana kama ‘Saizi Yako‘ uliofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Afisa Biashara Mkuu Tigo Tarik Boudiaf akifuatiwa na Balozi wa kampeni hiyo Lucas Muhavile maarufu kama Joti
  Balozi wa Kampeni mpya ya Tigo inayojulikana kama ‘Saizi Yako’ Lucas Muhavile maarufu kama ‘Joti’ akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Afisa Biashara Mkuu Tigo Tarik Boudiaf na William Mpinga ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko wa kampuni hiyo.

Wateja wa Tigo sasa wana kila sababu ya kufurahi baada ya uzinduzi wa ofa mpya ya ‘Saizi Yako’ inayolenga kuwapatia huduma za intaneti, muda wa maongezi na SMS kutokana na mahitaji mahususi ya kila mteja kwa gharama nafuu.

Ofa hii ya ‘Saizi Yako’ ni ya kipekee sana kwa sababu inawapatia wateja ambazo ni mahususi kwa kila mteja hivyo kuwaridhisha wateja wa sasa na wa baadaye wakiangalia gharama wanayoitumia kulinganisha na huduma wanayoipata. Ofa hii pia inapatikana kupitia menyu iliyorahisishwa ili wateja waweze kuipata na kuinunua kwa urahisi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa ofa hii kutoka makao makuu ya Tigo, Dar es Salaam, Afisa Biashara Mkuu wa Tigo, Tarik Boudiaf, alisema kwamba lengo la kampuni hiyo ni kutoa ofa bora, zenye mahitaji yote ya mteja sehemu moja, kwa gharama nafuu, na zitakazo kidhi mapendekezo na mahitaji ya wateja wao.

“Tumezingatia tabia, mahitaji na mienendo ya wateja wetu kwa miaka mingi sasa. Na kinachotufanya tuwe wabunifu ni kwamba tunatambua kwamba kila mteja wetu ni wa kipekee. Hivyo, tumeamua kubuni ofa hii ya ‘Saizi Yako’ ambayo ina mahitaji yote ya mteja sehemu moja na inayozingatia mahitaji yao mahususi. Sasa tunatoa fursa kwa wateja wetu kuweza kupata ofa za kipekee kwa kuzingatia matumizi yao ya kila siku na kwa gharama nafuu,” alisema Boudiaf.

Boudiaf pia alieleza kwamba, kama mteja anatumia muda wa maongezi zaidi kuliko intaneti na SMS, basi atapata kifurushi bora cha muda wa maongezi. Na mteja akitumia zaidi intanet kuliko muda wa maongezi na SMS, mteja huyo atazawadiwa kifurushi bora cha intanet. Utaratibu huo huo utafuatwa pia kwa ajili ya SMS.

“Tunaamini kwamba ‘Saizi Yako’ itaendana na mahitaji, bajeti na maisha ya wateja wetu. Kuwapatia ofa ambayo wataweza kupata kila wanachohitaji sehemu moja, kwa ajili yao, pia inamaanisha kwamba, sisi kama Tigo, tunatambua na kufanyia kazi mahitaji ya wateja wetu yanayobadilika kila siku. Uelewa wetu wa wateja pia unajenga mahusiano yetu nao na kuwafanya watuthamini zaidi,” aliongeza Boudiaf.

Kufurahia ofa maalumu ya ‘Saizi Yako’, wateja wanaweza wakapiga *147*00# au *148*00# kwa urahisi na kuchagua ‘Saizi Yako’. Ofa hii pia itapatakina katika Tigo Pesa APP hivi karibuni.

SERIKALI KUSAIDIA UANZISHWAJI WA KITUO CHA KUATAMIA UBUNIFU NA BIASHARA CHA CHUO KIKUU MZUMBE

$
0
0

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akikagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akikagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa hosteli hizo.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akipata maelezo kutoka kwa msimamizi wa ujenzi wa hosteli hizo.Kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari baada ya waziri kukagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukagua ujenzi wa hosteli za wanafunzi.
Mwanafunzi anayesomea sheria akionyesha bidhaa zake wakati wa kufunga kambi ya ujasiriamali.
Bidhaa mbalimbali za wanafunzi wajasiriamali wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akipewa maelezo kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa chuo Kikuu Mzumbe juu ya kilimo cha kisasa.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akizungumza wakati wa kufunga kambi ya ujasiriamali chuoni hapo.
Mzungumzaji Mkuu wa Kambi ya Ujasiriamali ya Mwaka 2019, Ahmed Lussasi ambae ni mhitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Mwazilishi mwenza wa Kampuni ya MAXOM AFRICA, akizungumzia mafanikio aliyoyapata pamoja na changamoto zake.
Mkuu wa Shule ya Biashara Chuo Kikuu Mzumbe, Dk. Hawa Tundui (kushoto), akifuatilia hotuba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani),
Baadhi ya washiriki. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako, akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe wakati wa kufunga Kambi ya Ujasiriamali 2019.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka akimkaribisha Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, wakati wa ziara yake chuoni hapo mkoani Morogoro.
Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akisalimiana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Prof. Ganka Nyamsogoro.
Waziri wa Elimu, Sanyansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako, akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akitoa maelezo ya mradi wa ujenzi wa hosteli za wanafunzi chuoni hapo. Mhandisi wa ujenzi katika hosteli za Chuo Kikuu Mzumbe, Focus Odecho, akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa hosteli hizo.




Morogoro, Tanzania

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Joyce Ndalichako amesema Wizara yake iko tayari kusaidia kutafuta rasilimali kwa ajili ya kuanzisha kituo cha kuatamia Ubunifu na Biashara “Innovation and Business Incubation Centre “ cha Chuo Kikuu Mzumbe, ambacho kitatoa fursa kwa wanafunzi wanaosoma katika Chuo hicho na Vyuo vingine na vijana wengine wenye mawazo ya kiubunifu, ujasiriamali na biashara, kuyaboresha mawazo na shughuli zao za kiubunifu ili ziweze kuwa biashara kamili.

Waziri Ndalichako amesema hayo katika kilele cha kambi ya ujasiriamali ya Chuo Kikuu Mzumbe iliyofanyika katika Kampasi yake Kuu Morogoro ambapo amepongeza hatua hiyo ya kuanzishwa kwa kambi hiyo ambayo ni mara ya tatu inafanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2017, huku akisema utaratibu huo ni tafsiri sahihi na kwa vitendo ya agenda ya Kitaifa ya kujenga Uchumi wa Viwanda.

“Nimefurahi sana leo kuona bidhaa na ubunifu wa hali ya juu hapa na kusikia kuwa Kambi hii imeendelea kuvutia watu wengi, wakiwemo wanafunzi, baadhi ya wafanyakazi na watu wengine kutoka jamii zinazotuzunguka, utaratibu huu utakuwa na faida ya muda mrefu kwa Chuo kwani wahitimu wenu watakuwa wameiva kinadharia na kivitendo, na wenye uwezo wa kujiajiri na kutengeneza ajira”.

Ndalichako amevitaka vyuo vingine kuiga mfano huu ambao unatoa fursa ya kukitangaza Chuo ambapo watanzania wataweza kujionea namna ambavyo fani mnazofundisha kama Uongozi wa Biashara, Ujasirimali, Uchumi na Mipango, TEHAMA, na zingine zinavyotayarisha wahitimu ambao wana mawazo ya kibunifu na ujasiriamali na mtazamo wa kibiashara.

Ndalichako amewataka Chuo Kikuu Mzumbe kuhahakisha kupitia kituo hicho atamizi kinawezesha wabunifu wao kushiriki katika mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU), kwa lengo la kuhamasisha ubunifu nchini yanayoratibiwa na Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.

Akizungumza katika kilele hicho Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Lughano Kusiluka amesema kambi hiyo inashirikisha wanafunzi wa Mzumbe na wengine, wahitimu wa Mzumbe ambao ni wajasiriamali. Ameongezea pia kuwa kupitia kambi hiyo wanafunzi wenye mawazo ya kibiashara pia hukutanishwa na wafanyabiashara walibobea na ili kupata uzoefu. Kusiluka ameahidi kusimamia uanzishwaji wa haraka wa kituo atamizi kwani kitasaidia kukuza mawazo ya kibunifu kuwa biashara kubwa nchini zitakazo changia pato la Taifa.

Nae mzungumzaji Mkuu wa kambi ya Mwaka 2019. Ndugu Ahmed Lussasi ambae ni mhitimu wa Chuo kikuu Mzumbe na Mwazilishi mwenza wa kampuni ya MAXOM AFRICA, kampuni inayofanya vizuri katika biashara, amesema anapongeza wazo la kituo atamizi na ameiomba Serikali kulipa kipaumbele , kwani biashara yao ilianza kwa kulelewa katika kituo atamizi na hatimae kukua. Lusassi kama mmoja wa wahitimu amekitaka Chuo kuwa na mfumo mzuri wa kushirikisha wahitimu wake katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya Chuo hicho.

Katika kambi hiyo Ndalichako amezindua bidhaa mbalimbali zilizobuniwa na wanafunzi wabunifu na wajasiriamli katika chuo hicho, ikiwa ni pamoja na kitabu kilichoandikwa na mwanafunzi wa Chuo hicho. Kwa mwaka 2019 wanafunzi 48 wameandikisha mawazo yao ya kibunifu ili yaweze kuboreshwa.

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia

Kampuni ya GreenWastePro yahamasisha wananchi kutumia mifuko mbadala

$
0
0
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakionyesha aina mifuko (vibebeo) ambayo haipaswi kutumika kuanzia leo Juni 01, 2019 baada ya kuanza kwa katazo la Serikali la uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko hiyo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kampuni ya huduma ya usafi ya "GreenWastePro Ldt" imewahimiza wananchi na wafanyabiashara wote nchini kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ni adui wa mazingira na badala yake kujikita kwenye matumizi na biashara ya mifuko mbadala isiyohatarisha mazingira.

Meneja wa kampuni hiyo Kanda ya Ziwa, Salim Madafa ametoa rai hiyo leo jijini Mwanza baada ya zoezi la kuhamasisha katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki na uzinduzi rasmi wa matumizi ya mifuko mbadala. Kampuni ya GreenWestPro ni miongoni mwa wadau wa mazingira walioshiriki kwenye zoezi hilo.

"Mifuko ya plastiki imekuwa na athari kubwa katika uchafuzi wa mazingira, mitaro kujaa maji kutokana na mifuko hiyo kuziba hatua ambayo hukwamisha kazi yetu ya uzoaji taka hivyo nitumie fursa hii kuwahimiza wananchi kutumia mifuko mbadala na kuachana na mifuko ya plastiki" amesisitiza Madafa.

Baadhi ya wafanyabiashara wadogo waliokuwa wakisalimisha mifuko ya plastiki katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza, wameomba Serikali kusaidia uzalishaji wa mifuko mbadala kwa wingi na kusambazwa katika maeneo yote huku ikiuzwa kwa bei nafuu hadi shilingi hamsini (Tsh. 50) kama ilivyokuwa mifuko ya plastiki, tofauti na hivi sasa ambapo inauzwa kuanzia shilingi mia mia tatu (Tsh.300).
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakionyesha aina ya mifuko ya plastiki ambayo imepigwa marufuku kutumika ikiwa ni sehemu ya kampuni hiyo kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala na kuachana na matumizi ya plastiki ambayo ni hatari kwa mazingira.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (kushoto) akikusanya mifuko ya plastiki iliyozuiliwa matumizi yake kutoka kwa baadhi ya akina mama wajasiriamali katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (kushoto) amesema mifuko ya plastiki ilikuwa ikisababisha uchafunzi wa mazingira hivyo wananchi wahamasike kutumia mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.
Mmoja wa wafanyabiashara wadogo katika eneo la "Market Street" jijini Mwanza akiendelea na uuzaji wa mifuko mbadala.
Gari la kisasa la kampuni ya usafi ya GreenWastePro linalotoa huduma ya ukusanyaji uchafu katika Mitaa mbalimbali jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wadogo waliojitokeza kupata elimu kuhusu matumizi ya mifuko mbadala kwenye zoezi la kuhamasisha katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki lililofanyika jijini Mwanza.
Baadhi ya wananchi na wafanyabiashara wadogo jijini Mwanza wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu katazo la kuzalisha, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki na badala yake wajikite kwenye matumizi ya mifuko mbadala.
Wananchi na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro wakiwa kwenye zoezi hilo.
Baadhi ya wafanyabiashara wadogo pamoja na viongozi wa dini jijini Mwanza wakifuatilia wakifuatilia maelezo mbalimbali kuhusu katazo la kuzalisha, kusambaza na kutumia mifuko ya plastiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya GreenWestPro Kanda ya Ziwa wakiwapungia mikono wananchi baada ya kutambulishwa kwenye zoezi la kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala ambapo kampuni hiyo ni miongoni mwa wadau muhimu wa usafi na utunzaji wa mazingira.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu jijini Mwanza (kushoto), akimuonyesha Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati) aina ya mifuko mbadala ambayo tayari ameanza kuiuza sokoni hapo.
Mmoja wa wafanyabiashara katika Soko Kuu jijini Mwanza (kushoto) akieleza kuhusu upatikanaji wa mifuko mbadala na hivyo kuwatoa hofu wananchi kuhusu upatikanaji wa mifuko hiyo jijini Mwanza.
Meneja wa kampuni ya usafi ya GreenWastePro Kanda ya Ziwa, Salim Madafa (wa pili kulia) akiteta jambo na wadau wa mazingira jijini Mwanza wakati wa zoezi la kuhamasisha matumizi ya mifuko mbadala na kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki.
Ujumbe muhimu unaohamasisha matumizi ya mifuko mbadaya ambayo ni rafiki kwa mazingira kutoka kampuni ya GreenWestPro inayohusika na usafi na utunzaji wa mazingira kwa sasa ikifanya shughuli zake katika mikoa ya Mwanza, Dodoma na Dar es salaam.
Tazama Video hapa chini

AZAM FC YAUNGANA NA SIMBA KIMATAIFA

$
0
0
*Ni baada kuifunga Lipuli fainali za ASFC

TIMU ya Azam FC imefuzu michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika msimu ujao baada ya kuifunga Lipuli FC bao 1-0 kwenye fainali za Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Mbali na kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika, timu ya Azam imeondoka na kitita cha sh. milioni 50, medani pamoja na kombe.

Fainali hizo zimefanyika leo (Jumamosi, Juni 1, 2019 katika uwanja wa Ilulu, Manispaa ya Lindi ambapo ushindi huo unaifanya Azam FC kuungana na Simba kuliwakirisha Taifa kwenye michezo ya Kimataifa itakayoanza Novemba mwaka huu.

Mshambuliaji wa Azam Obrey Chirwa ndio aliyeiwezesha timu yake ya Azam kuibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya kufunga bao la ushindi katika kipindi cha pili.


Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, timu ya Lipuli FC iliyong’ara kwa kutawala mchezo kwenye kipindi cha kwanza, ilishindwa kutumia nafasi nyingi ilizozipata kuifunga Azam.

Mbali na timu ya Lipuli kuwa mshindi wa pili katika mashindano hayo, pia timu hiyo imetoa mchezaji bora wa mechi ya fainali, Paul Ngalema pamoja na mfungaji bora wa mashindano hayo Seif Rashid.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, JUNI 1, 2019.

Mshambuliaji wa Azam, Donald Ngoma akichanja mbuga kuelekea lango la Lipuli huku akizongwa na mlinzi wa Lipuli Haruna Shamte katika mechi ya fainali ya mashindano ya Shirkisho la Azam kwenye uwaja wa Ilulu mjini Lindi Juni 1, 2019. Azam ilioshinda 1-0. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkiuu)


MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA WAAHIDI KUSIMAMIA HAKI YA WANACHAMA WAKE

$
0
0

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii


MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), umewataka watoa huduma katika vituo vya afya na hospitali nchi nzima walio katika orodha ya mfuko huo kutowanyanyapaa wanachama wake.

Kauli hiyo imetolewa leo wakati wa kikao kazi kati ya watumishi wa mfuko huo na Wahariri wa vyombo vya habari nchini kilichofanyika ukumbi wa Idd Nyundo uliopo katika Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya Wahariri pamoja na kujadili masuala mbalimbali, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bernard Konga amesema anachofahamu vituo vyote vinavyotoa huduma za afya kwa wateja wa mfuko huo wanaelewa taratibu zilizokuwepo na amesisitiza kila mwanachama anayo haki kupata huduma kulingana na aina ya kadi aliyonayo.

Ameongeza kuwa alishawahi kupokea malalamiko katika baadhi ya hospitali, lakini baada ya kufuatilia kwa sasa kila kitu kipo sawa huku akieleza unajua mfuko wao una wateja wengi, kama wataamua kuacha kufanya kazi hospitali yoyote basi itapoteza watu kwa kiasi kikubwa.

Amesema ndio maana wameweka wazi kwa yeyote anayeonesha kunyanyapaliwa au kutendewa kinyume na taratibu za huduma za kiafya atoe taarifa kwetu tutalishughulikia ndani ya muda mfupi.

Pia Konga amesema lipo tatizo la wizi au ubadhirifu katika baadhi ya watoa huduma. "Mifuko mingi ya bima ya afya duniani inalalamikia wizi unaofanywa kati ya wanachama kudanganya watoa huduma kuwema bili kubwa ya matibabu kinyume na bili halisi au watumishi wasio waaminifu wa NHIF kuuibia mfuko,".

"Zipo kesi nyingi tunazifuatilia kwenye baadhi ya hospitali. Lakini kwa sasa tunafanya utafiti. Tukishajipanga tutalimaliza hili tatizo.Lakini pia lipo tatizo la wanachama kuendelea kuwa na wategemezi waliopitisha umri wa miaka 18. Tunaamini huyo anatakiwa kuwa katika utaratibu mwingine wa uchangiaji. Ndiyo maana tyliamua kupeleka huduma za bima ya afya kwa wanafunzi ambapo wanalipia Sh 50,400 kwa mwaka," amesisitiza Konga.

Awali akiwasilisha mada kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, Mkurugenzi wa Wanachama wa NHIF, Mbaruku Magawa amesema wamekuwa wakikipa fedha nyingi katika vituo vyote vilivyo kwenye utaratibu wao ili kuhakikisha wanachama wanapata huduma stahiki.

"Mfano kwa mwaka 2018/19 tumelipa jumla ya Sh Bilioni 339.06 kwa vituo vya afya 7,400 nchini. Hapo zikiwemo hospitaki za mikoa, wilaya, Zahanati na Hospitali ya Taifa," amesema Magawa.

Amebainisha kwamba mfuko huo ulioanzishwa mwaka 2001 kwa Sheria Sura namba 395 umetimiza miaka 18. Ambapo hadi sasa kuna wanachama 16,969,943 sawa na asilimia 32 ya watanzania wote.

Wanajipanga kuhakikisha watanzania wengi zaidi wanajiunga na mfuko huo ili kupata huduma za afya kwa wakati na gharama nafuu. Hasa ikizingatiwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanaongezeka siku hadi siku.

Akitolea mfano, takwimu za mfuko zinaonyesha mwaka 2014/15 idadi ya wagonjwa waliotibiwa magonjwq yasiyo ya kuambukizwa walikua 286,806.

Na kwamba ndani ya miaka minne idadi imeongezeka maradufu ambapi takwimu za mwaka 2017/18 zinaonyesha kuna wagonjwa 1,574,803 waliotibiwa kupitia NHIF wakisumbuliwa na maradhi yasiyo ya kuambukiza.

Wakati huo huo NHIF imeahidi kuwa karibu na wanachama wake kwa kutoa taarifa za mara kwa mara kupitia vyombo vya habari ikiwemo elimu juu ya umuhimu wa kuwa na bima ya afya lakini pia kuzisaidia baadhi ya hospitali zisizo na uwezo wa kuwa na vifaa tiba kwa kuwapa mikopo ili wanachama wao wapate huduma popote ndani ya nchi.

Akitoa shukrani kwa watumishi wa mfuko huo kwa niaba ya wahariri wa vyombo vya habari nchini,Celina Wilson kutoka Gazeti la Uhuru amesema wahariri kupitia kikao hivyo ameongeza uelewa na ufahamu kuhusu mfuko wa Taifa wa Bima ya afya huku akieleza wahariri watahakikisha wanakuwa makini katika kuandika habari za mfuko huo.

"Tunawahakikishia Wahariri tutatumia kalamu zetu na vyombo vyetu vizuri katika kuandika habari zinazohusu afya.Kuna mengi ambayo tumeyafahamu kupitia kikao hiki,kikubwa tuendeleee kushirikiana na wahariri tupo tayari,"amesema Wilson.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Bernard Konga akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini leo jijini Dar es Salaam
Mmoja ya wahariri akizungumza wakati wa kikao kati ya wahariri wa vyombo vya habari nchini na maofisa wa NHIF .Kikao hicho kimefanyika leo jijini Dar es Salaam
Mhariri kutoka Gazeti la Uhuru Celina Wilson akitoa neno la shukrani kwa uongozi wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya(NHIF) baada ya kufanyika kikao leo jijini Dar es Salaam.
Maofisa wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya wakawa katika picha ya pamoja na Wahariri wa vyombo vya habari nchini

RAIS MSTAAFU MWINYI AKABIDHI ZAWADI WASHINDI WA MASHINDANO YA KUHIFADHI KURANI KIKWAJUNI

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akimkabidhi zawadi Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Kurani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi.Mashindano hayo yamefanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Mjiini, Twalib Ali Twalib akikabidhi msaada wa vitabu vitakavyoenda katika madrasa mbalimbali Visiwani Zanzibar kwa Mgeni Rasmi katika Mashindano ya Kuhifadhi Kurani, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, wakati wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani yaliyofanyika leo Visiwani Zanzibar.Wakwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni na anayefuatia ni Mwakilishi wa jimbo hilo, Salehe Nassor Jazzera

Mshindi wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Juzuu Kumi na Tano, Abdallah Hassan, akibeba zawadi ya televisheni aliyokabidhiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi (watatu kushoto), wakati wa fainali za mashindano yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi, Visiwani Zanzibar.Wakwanza ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, akimkabidhi zawadi Mshindi wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani Juzuu Tano, Asia Abdallah wakati wa fainali za mashindano hayo yaliyofanyika leo, katika Viwanja vya Mapinduzi, Visiwani Zanzibar.Wakwanza ni Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni, Mhandisi Hamad Masauni.
Mshiriki wa Mashindano ya Kuhifadhi Kurani katika Jimbo la Kikwajuni, Thureiya Abdallah akisoma Kurani wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Mapinduzi Visiwani Zanzibar.

BENKI YA EXIM YAFUTURISHA WATEJA WAKE WA TANGA NA MTWARA

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evodi Mmanda akizungumza na wageni walikwa pamoja na wateja wa benki y Exim Mkoani Mtwara waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo na kati wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Andrew Lyimo akizungumza na wageni waalikwa pamoja na wateja wa benki hiyo jijini Tanga wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo mwishoni mwa wiki.
Sheikh mkuu wa Mkoa wa Tanga, Sheikh Ally Luwuchu akizungumza na wageni walikwa pamoja na wateja wa benki ya Exim jijini Tanga waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wageni waalikwa pamoja na wateja wa benki ya Exim wakipata chakula walipohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo jijini Tanga mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim wakifuturu pamoja na wageni waalikwa pamoja na wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo jijini Tanga mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Benki ya Exim tawi la Mtwara Bw Ramadhani Magera (katikati) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki
Meneja wa Benki ya Exim tawi la Mtwara Bw Ramadhani Magera (kushoto) akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Sheikh Nurdin Mwangochi akizungumza na wageni walikwa pamoja na wateja wa benki ya Exim Mkoani Mtwara waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa benki hiyo mwishoni mwa wiki

NMB YATOA NAFASI KWA WATU WATANO WENYE ULEMAVU KUJIFUNZA MAMBO MBALIMBALI

$
0
0
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV 

Benki ya NMB imetoa nafasi tano kwa watu wanaoishi na ulemavu kujifunza masuala tofauti ndani ya benki hiyo katika Idara zake mbalimbali kwa kipindi cha awali cha miezi mitatu. 

Benki hiyo imetoa nafasi hizo wakati wa uzinduzi wa mpango maalum ujulikanao kama 'All Inclusive' kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Taasisi ya CEFA inayojihusisha na watu wenye Ulemavu pamoja na Hospitali ya CCBRT ya Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Rasilimaliwatu kutoka Benki hiyo, Emmanuel Akonaay amesema wametoa nafasi hizo kwa kuangalia ujuzi,mafunzo na elimu zao ambapo watapata nafasi ya kupata mafunzo kwa vitendo katika idara tofauti za benki hiyo.

Akonaay amesema NMB inaamini uwezo wa mtu uko kwenye kipaji na sio muonekano wake wa nje, amesema wametoa nafasi hizo kwa kwa watu wa jamii hiyo kuonyesha vipaji na baadae kutoa ajira kwao pale kutakapokuwa na uhitaji.

Kwa Upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Taaluma ndani ya Rasilimali watu kutoka Benki ya NMB, Joanitha Rwegasira amesema wamepokea Watu 25 watakaopata mafunzo hayo katika masuala ya Kifedha na masuala mbalimbali yakibenki. 

Naye Mmoja wa Watu wanaopata mafunzo hayo, Mwanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Faudhia Kitenge amesema amepata nafasi yakujifunza masuala mbalimbali ya utendaji wa kibenki.

Faudhia ametoa wito kwa Taasisi nyingine kutoa nafasi kama hizo kwa Watu wenye Ulemavu ili kutoa nafasi kwa kundi hilo kuonyesha vipaji na uwezo kwa jamii.

Mwakilishi kutoka Taasisi ya CEFA, Mratibu Mkuu wa Uwezeshaji Kiuchumi, Gerald Mpangala ametoa wito kwa Taasisi mbalimbali kutoa mafunzo kama hayo kwa kuwapa Watu hao wenye Ulemavu mafunzo mbalimbali ikiwemo ya Kiuchumi, amewataka Wanafunzi watano waliopata nafasi hiyo kwenye Benki ya NMB kutumia ipasavyo nafasi hiyo kufunza.
Mtaalamu Mwandamizi wa Vipaji, Mafunzo na uendelezaji wa benki ya NMB, Edith Mwiyombela, kizungumza wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya Makao makuu ya benki hiyo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu, Emmanuel Akonaay akifafanua jambo wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu  iliyofanyika mwishoni mwa wiki Makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkuu wa Kitengo Cha Taaluma ndani ya Rasilimali Watu, Joanitha Rwegasira Mrengo akieleza jambo kwenye ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya  jijini Dar es Salaam.
Mtaalamu Mwanadamizi Uajiri wa Benki ya NMB, Eleanor Maseke akitoa ufafanuzi wa jambo wakati wa ziara ya mafunzo iliyoandaliwa na Benki ya NMB kwa kushirikiana na Chama Cha Waajiri Tanzanja (ATE), Taasisi ya CEFA na CCBRT kwa wahitimu wenye ulemavu waliyoifanya katika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja.

Tangazo la Utoaji wa Hati Fungani kutoka Benki ya NMB.

QNET YAFUTURISHA MKOANI DODOMA

$
0
0

Watoto wa vituo mbalimbali kumi vya kulelea watoto wenye uhitaji mkoani Dodoma, wakipata futari iliyoandaliwa na Kampuni ya QNET jana. Hafla hiyo ilihudhuriwa na zaidi ya watoto 200 kutoka vituo hivyo na kuongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Mustapha Shaaban, Wawakilishi wa QNET na wawakilishi toka Bakwata.
…………………… 

QNET INASHEREHEKEA ARI YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KWA KULETA FARAJA KWA WENYE UHITAJI NA KUSAIDIA JAMII AFRIKA IKIWEMO TANZANIA

QNET YAUNGANA NA YATIMA JIJINI DODOMA KWA KUANDAA FUTARI KWA ZAIDI YA WATU 200
kampuni ya biashara ya mtandao duniani, sambamba na tamaduni zake na jitihada za kusaidia jamii, kusambaza upendo, huruma na ukaribu kwa kutoa msaada na kuleta faraja kwa jamii nyingi zisizo na uwezo barani Afrika. Katika zoezi ambalo lilifanyika katika nchi zote ambako kampuni hii inaendesha shughuli zake barani Afrika, QNET sambamba na wawakilishi wake wa kujitegemea (IRs), mawakala na wafanyakazi imeleta faraja, tumaini na tabasamu kwenye nyuso za wengi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani. 

Kampuni ya QNET inaendeshwa na falsafa ya RYTHM – Jiinue Kusaidia Wanadamu (‘Raise Yourself to Help Mankind’) imeandaa kampeni hii ya mwaka kusaidia kuboresha maisha ya familia na watoto wengi wasio na uwezo kwa kuwapatia mahitaji muhimu kama vile chakula, vinywaji na msaada wa kifedha kwa madhumuni ya elimu na kibinadamu. 

Hafla ya Futari Jijini Dodoma imewaleta pamoja zaidi ya watoto yatima 200 kutoka katika wilaya kumi za mkoa huo. Pamoja na hafla hiyo ya Iftar kampuni ya QNET imetoa zawadi za mbuzi, kilo 100 za mchele, kilo 50 za unga, kilo 25 za maharage, kilo 25 za sukari na lita 20 za mafuta ya kula kwa kila vituo kumi vya watoto yatima mkoani humo. 

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Shaaban alitoa wito wa amani na kuihamasisha jamii kuiga mfano uliofanywa na QNET katika kusherehekea mwezi mtukufu wa Ramadhani. Sheikh Shaaban ameipongeza kampuni ya QNET kwa kutayarisha Iftar kwa vituo vya watoto yatima Jijini Dodoma, chaguo ambayo inaunga mkono mkakati wa serikali ya kuhamisha makao yake Jijini humo. Pia alishukuru kampuni ya QNET kwa moyo wa msaada na ushirikiano hasa katika mwezi huu wa Ramadhan. 

Akiongea katika hafla hiyo, mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi Mwanahamisi Mukunda alisema ‘Tendo hili la Iftar imesaidia serikali ya mkoa katika utekelezaji wa majukuku yake pamoja na kuwaangalia watoto yatima’.
Hafla ya Iftar Jijini Dodoma iliudhuriwa pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Dodoma, wawakilishi wa baraza la kislamu Tanzania-BAKWATA, viongozi wa dini la kislamu wa mkoa pamoja na wawakilishi wa kampuni ya QNET. 

Katika nchi za Senegali, Cameroon, Kenya, Niger, Mali, Burkina Faso, Togo, Guinea, Ivory Coast na Ghana, QNET imetoa magunia ya mchele, magaloni ya mafuta ya mboga, vinywaji baridi, vifaa vya usafi na fedha taslimu kwa yatima, jamii za waisiliamu, vituo vya kutoa msaada wa kielimu na ofisi ya misaada ya Imamu mkuu. 

Biram Fall, Meneja Mkuu wa QNET Kanda ya Afrika chini ya jangwa la Sahara, wakati akitoa maoni kuhusu CSR ya Ramadhani ya QNET kwa mwaka huu, alisema: 

“QNET imekuwa ikifanya hivi kwa miaka mingi. Kampeni ya kutoa msaada katika kipindi cha mwezi wa Ramadhan ni moja ya njia tunazotumia kuzifikia jamii kusaidia watu. Kadri tunavyoendelea katika biashara yetu, tunaamini katika kusambaza faraja na utoshelevu unaokuja pamoja nao. Kwa kweli ni muhimu sana, inatia moyo na inakamilisha jitihada za QNET. 
Inawezesha watu, 
inaonyesha upendo kwa jamii na pia inahamasisha wafanyakazi wetu na Wawakilishi wetu wa Kujitegemea (IRs), kadri wanavyoshiriki wao binafsi katika kuboresha maisha ya wengine. Malengo yetu ya kibiashara pia ni kuhusu kutengeneza fursa kwa watu, kufanya maisha ya watu kuwa bora na kuwawezesha watu kuwasaidia waweze kuishi maisha ya ukamilifu. Tunaita hiyo kuwa ni kuishi kikamilifu” 

Mwaka jana, Kituo cha Uwajibikaji wa Mashirika kwa jamii cha Afrika ya Kusini kiliitunukia QNET kuwa kampuni bora ya mwaka ya kimtandao ya uwajibikaji kwa jamii (E-Commerce CSR Company of the Year) kwa uwajibikaji wake katika kusaidia jamii na kuleta mabadiliko bora.

TPB BENKI YAMWAGA MIKOPO KWA WAJASIRIAMALI MKOANI TANGA

$
0
0
 MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la Benki ya Posta kwenye maonyesho ya saba ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini Tanga kulia ni MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga (RAS) Mhandisi Zena Said
Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga Edward Bukombe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Banda la TPB Benki kushoto ni MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana 

MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana aliyevaa koti jeusi akizungumza na wageni mbalimbali waliotembelea banda lao kwenye maonyesho hayo
 MENEJA wa Tawi la Benki ya Posta (TPB) la Tanga Jumanne Wagana kulia akisalimiana na kiongozi wa TCCIA Mkoani Tanga wakati wa maonyesho hayo
 Maafisa wa Benki ya Posta Tawi la Tanga (TPB) kulia wakimsikiliza mmoja wa wakazi wa Jiji la Tanga aliyetembelea Banda lao
MENEJA wa Tawi la Benki ya TPB la Tanga Jumanne Wagana kushoto akimkabidhi zawadi kiongozi wa TCCIA ambao ndio waandaaji wa maonyesho hayo


WAJASIRIAMALI wadogo na wa kati wapatao 3400 mkoani Tanga wamenufaika na mikopo kutoka Benki ya Posta (TPB) wenye thamani ya Bilioni 9.1 ambao umewawezesha kujikwamua kiuchumi.

Hayo yalisemwa na Meneja wa Benki ya Posta (TPB) tawi la  Tanga Jumanne Wagana wakati wa maonyesho ya Biashara ya kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwahako Jijini hapa.

Alisema kwamba mikopo hiyo ilitolewa pia kwenye vikundi mbalimbali, watumishi wa umma na wazee waastaafu kwa mkoa mzima wa Tanga.

Aidha alisema wakati wanaanza kutoa mikopo hiyo mwaka jana waliweza kuitoa kwa wateja 3000 ambao ulikuwa na thamani ya sh.bilioni 8 huku wakiweka lengo la kuwafikia wateja wengi zaidi.

Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo ni baadhi ya wateja kushindwa kurudisha mikopo hiyo kwa wakati huku wengine wakiwa na mikopo zaidi ya mmoja.

Hata hivyo aliwataka wateja wao kuendelea kutumia huduma zao mara kwa mara kwa sababu mikopo yao wanatoa kwa riba nafuu na huduma nzuri zinazowajali wateja wao.

Naye kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella ambaye alitembelea banda hilo aliipongeza Benki hiyo kwa kuwawezesha wakazi wa mkoa huo kunufaika na mikopo ambayo imekuwa mkombozi kwao.

Alisema kwamba mikopo hiyo inasaidia kwa kiasi kikubwa kuchochea wafanyabiashara na wajasiriamali kukuza kipato chao na hivyo kupata mafanikio .

UJUMBE MARIDHAWA KUTOKA DAWASA: USAFI WA MAZINGIRA NI UTU

TAASISI ZA FEDHA ZATAKIWA KUCHANGAMKIA VIWANDA VYA USINDIKAJI MAZIWA

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo, Profesa Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) akizungumza jambo na Afisa Utafiti wa benki ya NMB, Mboka Mwanitu na Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro (kushoto) wakati wa Wiki ya Maziwa kitaifa iliyofanyika jijini Arusha.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina akizungumza jambo na Meneja Mwandamizi wa idara ya Kilimo biashara NMB Oscar Rwechungura pamoja na wafanyakazi wa NMB kwenye banda la benki hiyo wakati wa Wiki ya Maziwa kitaifa iliyofanyika jijini Arusha.
Afisa Utafiti wa benki ya NMB makao makuu, Mboka Mwanitu akiwasilisha mada juu fursa za mikopo inayotolewa na benki hiyo kwenye sekta ya Maziwa wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Maziwa kitaifa iliyofanyika jijini Arusha.
 

Mwandishi Wetu, Arusha.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo,Profesa Elisante Ole Gabriel amezitaka taasisi za fedha nchini kuchangamkia fursa ya soko la usindikaji wa maziwa ambalo linahitaji uwekezaji wa kimkakati kutokana na sehemu ndogo ya maziwa yanayotoka kwa wafugaji ndiyo yanayosindikwa.

Profesa Ole Gabriel ametoa rai hiyo katika kongamano la 10 la Wiki ya Maziwa kitaifa nchini kuwa kiwango cha maziwa kwa mwaka ni takribani lita 2.7 bilioni wakati kiwango cha maziwa kinachosindikwa ni lita 56 milioni pekee hatua inayomnyima mapato mazuri mfugaji.

“Nitoe wito kwa taasisi za fedha kuchukua fursa hii muhimu kwa kuwekeza kwa nguvu kwenye mnyonyoro wa thamani ili kuyapa thamani maziwa yetu,ipo fursa kubwa ambayo itawasaidia wafugaji na taasisi zenu kupata faidi,”alisema Ole Gabriel

Kongamano hilo limewaleta wadau kutoka mikoa mbalimbali na nje ya nchi linajadili namna ya kuongeza uzalishaji bora wa maziwa na namna ya kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa mbegu bora za uhamilishaji,malisho ya mifugo,masoko ya maziwa na uhaba wa viwanda vya usindikaji wa maziwa.

Mweneyekiti wa Bodi ya Maziwa nchini,Lucas Malunde alisema viwanda zaidi vinahitajika kwaajili ya kuongeza kiwango cha maziwa yaliyosindikwa ambayo yanamhakikishia faida mfugaji na mtumiaji wa maziwa.
Alisema kiwango cha matumizi ya maziwa kwa mtu mmoja hapa nchini kipo chini kiasi cha lita 49 kwa mwaka wakati lengo ni kumwezesha kila mtu kutumia lita 200 kwa mwaka.

Afisa Utafiti wa benki ya NMB, Mboka Mwanitu alisema benki hiyo imetenga kiasi cha Sh 500 bilioni “for AVC” na tasnia ya maziwa kwa ujumla na hadi sasa wapo wajasiriamali walionufaika kwa kuchukua mkopo wa Sh 30 bilioni na hii imetokana na kuongezeka kwa mahitaji ya maziwa nchini.

Alisema mikopo yao imejielekeza kwenye kupata mbegu bora za ng’ombe,kuwa na vituo bora vya kukusanyia maziwa ,vifaa vya kisasa vya usindikaji wa maziwa,malisho na huduma za chanjo na matibabu .

GGM, TACAIDS kuzindua Kilimanjaro Challenge kwa lengo La kukusanya fedha za kutokomeza Ukimwi

$
0
0
Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) inatarajia kuzindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2019), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2019 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini.

Kilimanjaro Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko alisema takwimu zilizotolewa na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), zimeonesha kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 % mwaka 2011/ 2012 hadi asilimia 4.7% mwaka 2016/17.

Alisema mwaka wa 2016, inakadiriwa kuwa watu milioni 1.5 nchini wanaoishi na VVU na UKIMWI hadi sasa watu 225 wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa siku. Ugonjwa huu umewaathiri zaidi vijana na watoto yatima zaidi. Tunahitaji kubadilisha hali hii.

Aidha, aliongeza kuwa lengo la kukusanya fedha ni kuweza kusaidia serikali ya Tanzania katika jitihada zake kufikia sifuri tatu. Sifuri katika maambukizi mapya, sifuri ya unyanyapaa, sifuri katika vifo vitokanavyo na UKIMWI.

“TACAIDS kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na wadau wengine kwa kupitia mpango huu wa Kili Challenge tunapenda kutoa mchango na ushirikiano wetu kwa Taifa ili kutunisha mfuko utakaowezesha kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huu. Tuna matumaini ya kujenga timu imara yenye hamasa ya kupambana na janga hili.

“Tunatoa wito kwa makampuni na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, wajitokeze ili tusaidiaane kutunisha mfuko wa Kili Challenge na mwishowe kufikia malengo yetu ya kuhakikisha tunakuwa na kizazi kisicho na maambukizi ya VVU/ UKIMWI,” alisema Dkt. Leonard Maboko.

Makamu wa rais miradi endelevu wa kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo alisema shughuli hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 4 Juni mwaka huu na kuzinduliwa na Waziri wa Uwekezaji Angellah Kariuki ambapo atafanya zoezi la ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka jana 2018 zilizopatikana baada ya wadau mbalimbali kupanda na kuendesha baiskeli na kuzunguzuka Mlima Kilimanjaro.

Alisema kuna tatizo linaloikabili jamii sasa ambapo baadhi yao wanawatenga na kukataa kuishi na watu wenye maambukizi ya VVU/ UKIMWI, kutokana na tatizo hilo Mgodi wa Dhahabu wa Geita, umeamua kuwekeza katika mradi huu kwa kuuwezesha kuwa mradi wa kitaifa na si wa GGM

“Huu ni mwaka wa 18 sasa tangu Kili Challenge ianze. Pia zaidi ya watu 800 kutoka pande mbalimbali za dunia wameshiriki. Taasisi zaidi ya 40 zimefaidika kutokana na utunishaji wa mfuko huu kwa sababu taasisi ambazo hazina fedha za kuendesha kampeni na shughuli mbalimbali za mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI zimekuwa zikifaidika na mfuko huu. Pamoja na mambo mengine, watoto waliopoteza wazazi wao sasa wanaweza kutabasamu tena kutokana na uangalizi pamoja na upendo wanaoupata kutokana na mfuko huu.

“Tunapenda pia kutambua ushirikiano wa kampuni na taasisi mbalimbali kama vile ACACIA, AKO, Mantrac, NSSF, PUMA, TOYOTA, Prime Fuels, Coastal Aviation, Airtel, Capital Drilling, PPF, Serena Hotel, Geita Power Limited, SGS na wadau wengine tunaoshirikiana nao. Tunawashuruku kutokana na ushirikiano wenu katika mapambano dhidi ya VVU/ UKIMWI hivyo, tunaweza kufurahia mafanikio haya kwa kuwa na mradi endelevu,” aliongeza Simon Shayo.

Balozi wa Kili Challenge ambaye pia ni mwanamuziki maarufu nchini Tanzania, Mrisho Mpoto alisema jamii inapaswa kuacha kuwa tegemezi kwa sababu ina uwezo wa kujisimamia kwa kutumia vyombo vya habari, na watu wenye ushawishi mkubwa na kwa pamoja; UKIMWI unaepukiki.

Makamu wa rais miradi endelevu wa kampuni ya AngloGold Ashanti, GGM, Simon Shayo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu uzinduzi wa zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2019), na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2019 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini. Uzinduzi huo unafanyika Juni 4 mwaka huu. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko.

UZINDUZI WA MASHINDANO YA UMITASHUMTA YAMEFANYIKA JIJINI ARUSHA CHINI YA UDHAMINI WA TTCL

$
0
0

Kutoka katikati ni Afisa Utamaduni Jiji la Arusha Benson Maneno,aliyepo kulia kwake ni Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet
Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Arusha katika katika uzinduzi rasmi wa michezo ya UMITASHUMTA.
Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet akimkabidhi mpira Afisa Utamaduni Jiji la Arusha Benson Maneno kama ishara ya uzinduzi rasmi wa mashindano hayo.
Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Ngarenaro Nuru Jofrey Mungure mchezaji wa mpira wa miguu ameihakikishia shule yake kuwa watafanya vizuri hadi kufikia ngazi ya Taifa.
Mwanafunzi Salha,Mashaka Rajabu kutoka shule ya msingi Ngarenaro amewaomba wazazi wavumbue vipaji vya watoto wao wasivifike kwani michezo ni Afya na Ajira.
Mwanafunzi kutoka shule mojawapo katika Jiji la Arusha anayecheza mpira wa mikono Handball



Na.Vero Ignatus,Arusha.

Halmashauri ya Jiji la Arusha imeingia ubia na Shirika la simu la TTCL ,Mkoani Arusha,katika maswala ya mashindano ya michezo kwa vijana katika shule za Msingi UMITASHUMTA

Benson Maneno ni Afisa utamaduni katika Jiii la Arusha amesema Michezo hiyo imedhaminiwa na TTCL katika msimu wote wa mashindano ambapo yataanza kesho june 4 na kushirikisha vijana 500 lakini katoka mchujo watachukua vijana 100 peke yake ambao watawaingiza katika timu ya mkoa wa Arusha

Maneno amesema Halmashauri ya Jiji la Arusha imejipanga kikamilifu kwa mashindano hayo kuhakikisha inafanya vizuri ambapo tamebeba kauli mbiu isemayo "Michezo na TTCL Rudi nyumbani kumenoga"

Kwa upande wake Meneja wa TTCL mkoa wa Arusha na Manyara,Brown Japhet amesema kampuni hiyo imeguswa kusaidia sekta ya michezo katika.Jiji la Arusha kwa kuwa michezo ni sehemu ya ajira na wanamichezo wengi duniani wanamafanikio makubwa kutokana na michezo.

Amesema kupitia michezo hiyo kampuni ya TTCL itajitangaza Kitaifa na kimataifa na amewataka wananchi kutumia fursa hiyo kuitangaza kampuni hiyo ya kitanzania inayoungwa mkono na serikali.

Katika hafla hiyo likiendana na ugawaji wa line za simu za TTCL kwa washiriki ambapo wamepata fursa kujipatia kama sehemu ya wadau muhimu katika kulitangaza kampuni hilo .

Benki ya Exim Sasa Mdau Rasmi Uchangiaji Wa Damu Nchini

$
0
0
Benki ya Exim Sasa Mdau Rasmi Uchangiaji Wa Damu Nchini
Kilimanjaro; Juni 3, 2019: Benki ya Exim Tanzania pamoja na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) wameingi kwenye makubaliano rasmi ya utekelezaji wa pamoja wa mpango wa uchangiaji wa damu utakaohusisha matawi yote ya benki hiyo hapa nchini. 

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa benki hiyo ya uwajibikaji kwa jamii unaofahamika kama ‘Exim Cares’ 

Ushirikino huo umezinduliwa rasmi leo katika tukio la uchangiaji wa damu lililoandaliwa na benki hiyo kwenye tawi lake lililopo barabara ya Old Moshi katika Manispaa ya Moshi, mkoa wa Kilimanjaro ikiwa ni urasmishaji wa jitihada za benki hiyo kwa kipindi cha miaka minane mfululizo katika uchangiaji wa damu hapa nchini,. 

Akizungumzia mpango huo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Staniley Kafu alisema unaenda sambamba na kauli mbiu ya benki hiyo inayosema “Exim kazini leo kwa ajili ya kesho” na kwamba unalenga kuchangisha damu na kutoa elimu ya umuhimu wa kuchangia damu katika mpango wa taifa.
“Kampeni hii ni sehemu ya uthibitisho kuwa benki ya Exim iko makini kutafuta njia za ubunifu za kuhudumia wateja wake na muhimu zaidi, inajitolea kuhakikisha inashiriki kuleta mabadiliko chanya katika jamii.’’ Alisema Kafu. 

Akizungumzia kuhusu makubaliano hayo na NBTS, Kafu alisema benki hiyo itawezesha mpango na utekelezaji wa uchangiaji damu kwenye kambi nane (8) za uchangiaji damu katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, Tanga, Mtwara na Zanzibar huku ofisi ya Mpango wa Taifa Damu Salama wakisimamia masuala yote ya kitabibu katika mpango huo. 

“Zaidi benki ya Exim kwa kushirikiana wadau wote wa mpango huu wakiwemo Mpango wa Taifa Damu Salama , Wizara ya Afya na wadau wa habari tutahusika na kuratibu mikakati ya uelemishaji na uhamasishaji wa wananchi ili waweze kujitokeza kwa wingi katika suala hili muhimu kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya kuchangia damu Duniani.’’ Alisema Kafu 

Kwa upande wake Menaja wa NBTS Kanda ya Kaskazini Dk Edson Mollel alisema ofisi hiyo inahitaji kukusanya chupa (units) 526,000 za damu ili kukidhi mahitaji ya kila mwaka kwa nchi nzima ambapo kiasi kilichpatikana mwaka jana ilikuwa ni chupa 307,835 sawa na asilimia 58 ya mahitaji. 

“Mwaka huu lengo nikukusanya chupa 357,000 za damu na kupitia maadhimisho ya mwaka huu pekee tumejipanga kukusanya chupa 41,920 na ndio maana tunaridhishwa sana wanapojitokeza wadau kama benki ya Exim ili kutuunga mkono…uhitaji wa damu ni mkubwa.” 

“Hatua hii ni mfano wa kuigwa kwa kuwa benki ya Exim na wafanyakazi wake wanakuwa sehemu ya jamii wanayoihudumia kwa ukaribu zaidi na pia wanathibitisha rasmi mioyo yao ya kujitolea kwa hali na mali kwa jamii wanayoihudumia,’’ alisema 

Benki ya Exim imeendelea kuonyesha uwajibikaji wake katika kusaidia sekta ya afya kupitia mipango mbalimbali na miradi ya kijamii. Katika miaka minane iliyopita benki imechangia zaidi ya lita 100 za damu katika Benki ya damu taifa

Meneja wa Benki ya Exim Kanda ya Kaskazini Bw Amos Lyimo (Kushoto) pamoja na Meneja wa benki hiyo tawi la Moshi mkoani Kilimanjaro Bw Masood Abutwalib (Kulia) wakichangia damu ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa uchangiaji damu kila mwaka kupitia matawi yake yote hapa nchini kwa ushirikiano na Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS).Anaewahudumia ni mtaalamu wa afya kutoka NBTS Bi Marygoreth LaswaiTaarifa kwa vyombo vya habari

Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Exim Tawi la Moshi pamoja na wateja wa benki hiyo wakiendelea taratibu za uchangiaji wa damu uliofanyika kwenye kwenye viunga vya tawi la benki hiyo Manispaa ya Moshi leo.

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images