Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1822 | 1823 | (Page 1824) | 1825 | 1826 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Na Vero Ignatus, Arusha

  KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel ameagiza halmashauri zote nchini kutoa elimu kwa wafugaji umuhimu wa utumiaji mbegu bora zinazozalishwa kituo cha Taifa cha Uhimilishaji mifugo kwa njia ya chupa NAIC kilichopo Wilayani Arumeru,Mkoani hapa.

  Ametoa agizo katika ziara ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji, ambapo Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, ambapo Prof.Gabriel amesema ni kufuatia uwepo wa mwamko mdogo wa wafugaji katika utumiaji mbegu hizo.

  Amesema kuwa ili kuendana na uchumi wa viwanda ni lazima wafugaji nchi wabadilike na kutumia mbegu hizo ili kupata Ng'ombe wenye nyama bora,maziwa,ngozi na Kwato watakazokidhi malighafi za viwanda.

  Prof.Ole Gabriel amesema kwa kipindi cha mwaka jana waliweza kutoa mafunzo kwa wafugaji 58,000 kwa nchi nzima hali iliyosababisha kuzalisha Ndama 10,000 pekee licha ya kituo hicho kuzalisha mbegu 60,000 kwa wiki.

  "Idadi ya wagufaji waliopewa elimu ni ndogo na mwitikio wa utumiaji mbegu hizi hauridhishi kwa wafugaji wetu wakati kituo kinazalisha mbegu za kutosha kwa mahitaji ya wafugaji wote nchini,hivyo nawaagiza wataalamu wote watoke ofisini waende kwa wafugaji kutoa elimu juu ya utumiaji mbegu hizi,"alisema

  Aidha alitumia nafasi hiyo kuwataka wafugaji kuondokana na dhana potofu kwakutumia mbegu hizo ni kuharibu vizazi vya ng'ombe jambo ambalo sio sahihi ni kukinzana na maendeleo katika sekta ya ufugaji.

  Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega kuwa hali ya usambazaji wa mbegu hizo kwenye vituo vilivyopo kanda saba nchini hauridhishi kutokana na baadhi ya waataalamu kutotimiza wajibu wao wa utoaji elimu kwa wafugaji.

  "Serikali inauza mbegu hizi kwa ruzuku ili wafugaji wasiokuwa na uwezo waweze kumudu gharama ya Sh.5000,lakini kuna baadhi ya wataalamu wananunua mbegu hizi na kuziuuza kwa bei kubwa kati ya Sh.15,000 na Sh.40,000,"alisema

  Ametoa wito kwa wafanyabiashara binafsi wa mbegu za chupa kuacha kuagiza mbegu hizo nje ya nchi na kuuzia wafugaji mbegu hizo kati ya Sh.50,000 hadi 100,000.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Kilimo,Mifugo na Mjai,Mahmoud Mgimwa alisema utumiajo wa mbegu hizo utawezesha wafugaji kufuga kwa tija na kupata soko la uhakika la bidhaa za mifugo yao.

  "Kikubwa hapa wafugaji wabadilike kutoka kwenye ufugaji wa maea na kufuga kisasa kwa kutumia mbegu hizi za NAIC ili tushiriki uzalishaji wa malighafi za Viwanda vyetu vinavyoanzishwa kwa wingi nchini,"alisema.

  Hadi sasa kiruo hicho kina madume 28 ya aina zofuatavyo katika kituo hicho NAIC.Ng'ombe wa maziwa Ayrshine 6,Friesian7 na Jersey 2.Ngombe wa maziwa na nyama (Dual porpose) Simmental 2 na Mpwapwa 4,Ng'ombe wa nyama, Boran 4 na Binsmara2 na Teaser bull 1.

  Ngombe aliyeko tayari kwa ajili ya Uhamilishaji katika kituo cha NAIC
  KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel ameagiza halmashauri zote nchini kutoa elimu kwa wafugaji ili waweze kupata ngombe bora wa nyama, maziwa na ufugaji wenye tija
  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza na waandishi wa habari katika kutuo cha NAIC kilichopo Usariver Mkoani Arusha
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bungeya Kilimo,Mifugo na Mjai,Mahmoud Mgimwa
  Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo,Mifugo na Maji waliotembelea katika kituo hicho kujionea jinsi uhamilishaji
  Baadhi ya ng'ombe walipo katika kituo cha NAIC kwajili ya Uhimilishaji. Picha na Vero Ignatus.

  0 0
  0 0


  Na Woinde Shizza Globu ya jamii Arusha

  Timu ya mpira Wa miguu ya mkoani Arusha ijulikanayo kwa jina la Arusha United (wana utalii)Leo imetangaza rasmi kujitoa katika mashindano ya ligi daraja la kwanza Tanzania bara kwa kile kichodaiwa vurugu za Mara kwa Mara zinazotokea katika ligi hiyo.

  Akiongea na waandishi Wa habari mkurugenzi mtendaji Wa timu hiyo Otte Ndauka alisema kuwa timu hiyo imeamua kujitoa rasmi katika mashindano hayo kutokana na vurugu wanazofanyiwa Mara kwa Mara viwanjani wakati wakicheza michezo mbalimbali.

  Alisema kuwa timu yao ya Arusha United imefanyiwa vurugu katika mechi mbalimbali ikiwemo mchezo nambari 69 Wa ligi daraja LA kwanza uliochezwa mjini Tabora mnamo February 2 mchezo uliochezwa katika kiwanja cha All Hassan Mwinyi.

  "Mchezo huu tulienda tulifika sikumoja kabla kwa mujibu Wa sheria tulitakiwa kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo husikalakini jambo LA kusikitisha sana na lisilo lakiugwana viongozi Wa Rhino Rangers kwa kushirikiana na Meneja Wa uwanja walifanya kula jitiada kuhakikisha hatufanyi mazoezi,Aisha pia katika mechi ingine tuliocheza na kilabu ya Polisi pia tulifanyiwa vurugu na sio timu tu au wachezaji wanafanyiwa vurugu hapana lakini pia waandishi wetu wanapigwa na hata kunammoja aliaribiwa vifaa vyake vya Kazi" alisema Ndauka.

  Alisema kuwa matukio yote ambayo yametokea wameandika barua TFF kulalamika pamoja na Bodi ya ligi lakini hakuna uamuzi wowote Wa kinithamu ambalo wameuchukua hivyo ndio maana wameamua kujitoa katika ligi hiyo.

  Kuhusiana na swala La mikataba ya wacheza pamoja na Mali za klabu hiyo walisema kuwa bodi ya timu hiyo inakaa chini na wachezaji kujadili kuhusiana na mikataba hiyo pia wanampango Wa kuketi na bodi kujadili kuhusiana na Mali hizo.

  Akiongelea swala hilo Katibu Wa chama cha mpira Wa miguu mkoa Wa Arusha Zakayo Mjema alisema kuwa wao kama chama cha mpira Wa miguu Mkoa Wa Arusha awajapata taarifa yoyote kuhusiana na timu hiyo kujitoa
  Mkurugenzi mtendaji Wa timu ya Arusha United (WANAUTALII) Otte Ndauka 

  0 0
     0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

  Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema kuwa imeridhishwa na mtambo wa TTMS wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) unavyofanya kazi katika katika kulinda usalama wa Mawasiliano nchini.

  Akizungumza wakati Kamati hiyo ilivyotembelea Mamlaka Hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya PAC Naghenjwa Kaboyoka amesema kuwa wamejiridhisha katika mtambo huo kwa umerahisisha TCRA kufanya kazi kwa ufanisi katika kuweza kusaidia serikali kupata mapato.

  Amesema walikuwa na shaka kuhusiana na mtambo huo lakini wamejiridhisha kwa na kuondoa mashaka hayo kwa kamati na Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) nao wamejiridhisha na mtambo huo.

  Kaboyoka amesema TCRA imepiga hatua nzuri katika mawasiliano kwa kuwa na watendaji mahiri wa kuendesha mtambo huo.

  "Uzuri wa mtambo TTMS unasimamiwa na wazawa hii inaoyesha kuwa kila kinachofanyika kitakwenda sawa kuliko mtambo huo ungesimamiwa na watu wa nje"amesema Kaboyoka.Aidha amesema kuwa TCRA iendelee kudhibiti mawasiliano ikiwa ni pamoja na kwenda kukuza uchumi wa nchi.

  Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba amesema kuwa mtambo huo unaweza kukokotoa takwimu zote miamala ya fedha unavyofanywa na kampuni za simu kutoka na moja kwenda Mtandao mwingine.Amesema kazi nyingine ni kusimamia simu ndani na nje sambasamba na kutambua simu za ulaghai, uhakiki wa mapato na ubora wa mawasiliano.

  Amesema kuanza kwa mfumo huo umesaidia kupunguza simu za ulaghai kutoka asilimia 65 hadi kufikia asilimia 10 ikiwa ni pamoja kuongeza pato la Taifa kwa asilimia 9.8.
   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Mhandisi James Kilaba akizungumza na kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) ilipotembelea Mamlaka hiyo.
   Afisa wa Makumbusho wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Abdulrahman Milasi akitoa maelezo wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu PAC ilipotembelea Mamlaka hiyo katika Makumbusho ya vitu vilivyotumika zamani katika mawasiliano.
   Mwenyekiti wa Bodi ya TCRA Dkt Jonas Kilimbe akitoa maelezo kuhusiana na utendaji wa TCRA wakati Kamati ya PAC Ilipotembelea Mamlaka hiyo.
   Mhandisi wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA)Jumanne Ikuja akitoa maelezo katika gari la kuangalia masafa wakati Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali PAC ilipotembelea Mamlaka hiyo.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC)  Naghenjwa Kaboyoka akizungumza na waandishi wa habari wakati alipotembelea Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA).

  0 0


  Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika akitoa maelekezo kuhusu maazimio wakati wa kikao kazi cha siku mbili kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.

  Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika akifunga kikao kazi cha siku mbili kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro. 

  Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kutoka katika Wizara na Taasisi za serikali wakijadiliana maazimio wakati wa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
  Afisa Maendeleo ya Jamii Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Christina Mangwai akichangia mada wakati wa kikao kazi kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika katika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.
  Baadhi ya washiriki wa kikao kazi kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kutoka katika Wizara na Taasisi za serikali wakifuatilia mada wakati wa kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.


  Mkurugenzi Msaidizi, Idara wa Utawala, Mahakama ya Tanzania, Bi. Wanyenda Kutta akitoa mada kuhusu uzoefu wa taasisi yake katika masuala ya kijinsia kwenye kikao cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kilichofanyika kwenye ukumbi wa Glonency Hotel, mjini Morogoro.

  ………………….

  Taasisi za umma nchini zimetakiwa kuweka mazingira rafiki sehemu za kazi ili kuwezesha utekelezaji wa masuala ya kijinsia kwa ufanisi na hatimaye kufikia usawa wa kijinsia utakaokuwa na tija kwa maendeleo ya Taifa.

  Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Msaidizi, Sehemu ya Anuai za Jamii, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Leila Mavika wakati akifunga kikao kazi cha siku mbili cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia mahali pa kazi kilichofanyika mjini Morogoro kwa lengo la kuboresha mazingira ya utendaji kazi katika taasisi za umma.

  Bi. Leila amesema kuwa, mazingira rafiki ya ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi yanategemea menejimenti za taasisi za umma kutoa kipaumbele kwa masuala ya anuai za jamii kuwa ni sehemu ya shughuli za uendeshaji wa ofisi za kila siku.

  Bi. Leila ameainisha kuwa, ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia utafanikiwa iwapo kutakuwa na uelewa wa pamoja wa masuala ya kijinsia kwa watumishi wa umma na menejimenti zao ambao utasaidia kuepuka ubaguzi na unyanyapaa mahala pa kazi na kuongeza kuwa, taasisi za umma zikijenga majengo jumuishi yenye miundombinu inayofikika kwa urahisi na wadau wote hususan watu wenye ulemavu wa viungo, zitawezesha jinsia zote kupata huduma bora bila kikwazo cha aina yoyote.

  “Ni vema taasisi zikaweka mifumo thabiti itakayoweka mazingira rafiki, wezeshi na mifumo rejeshi inayotoa fursa kwa wananchi kutoa taarifa za masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na ukiukwaji wa maadili kwa ujumla” amesema Bi. Leila.

  Bi. Leila amezitaka taasisi zote za umma kuhakikisha kwamba, zinatenga bajeti kwa ajili ya ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi na kuyafanya masuala ya kijinsia kuwa ajenda ya kudumu katika vikao vya kitaasisi vya ndani na nje.

  Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa kikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Hamidi Mbegu amesema kuwa, kikao kazi hicho cha ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kitakuwa ni chachu ya kuboresha utekelezaji wa masuala ya kijinsia katika wizara yake na taasisi zote za umma.

  Aidha, Bw. Mbegu amesema, kikao hicho kimeazimia kuwepo mwongozo rasmi utakaowezesha utekelezaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi, ambao utasaidia uanzishaji wa madawati ya kijinsia sehemu za kazi ambayo yatarahisisha utekelezaji na ufuatiliaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi.

  Naye, Mshauri wa Masuala ya Jinsia wa Mradi wa SAUTI kutoka Shirika la Jhpiego, Bi. Grace Munisi amesema kuwa, serikali imekuwa ikishirikiana na mradi huo katika utekelezaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi kupitia udhamini wa warsha mbalimbali zinazosaidia kuwapa uelewa watendaji juu ya mahusiano ya kijinsia yanavyoweza kusababisha maambukizi ya virusi vya UKIMWI na kuepuka mila potofu zinazosababisha maambukizi ya Virusi vya UKIMWI sehemu za kazi na kwenye jamii kwa ujumla.

  Kikao kazi cha siku mbili kuhusu ujumuishwaji wa masuala ya kijinsia sehemu za kazi katika Taasisi za Umma kilijumuisha Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka katika Wizara, kwa lengo la kujadili fursa na changamoto za masuala ya kijinsia katika utumishi wa umma ili kuweka mikakati endelevu itakayofanikisha uwepo wa Usawa wa Jinsia mahala pa kazi utakaowezesha maendeleo endelevu.

  0 0

  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi mtoto cheti cha kuzaliwa baada ya kusajili watoto katika viwanja vya stand mjini Singida baada ya akizindua kampeni ya kitaifa ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Singida na Dodoma Machi 21,2019.
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi mzazi wa mtoto aliesajiliwa na kupata cheti cha kuzaliwa katika viwanja vya stand mjini Singida
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akimkabidhi mtoto cheti cha kuzaliwa baada ya kusajili watoto katika viwanja vya stand mjini Singida baada ya kuzindua kampeni ya kitaifa ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano kwa mikoa ya Singida na Dodoma Machi 21,2019.
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na wananchi mbalibali , wazazi na watoto waliopata vyeti vya kuzaliwa na watendaji wa RITA baada ya kuzindua usajili wa watoto kwa mikoa ya Singida na Dodoma katika viwanja vya stendi mjini Singida
  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akionyesha kitabu kinachotumika kusajili watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa baada ya kuzindua kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Singida na Dodomajini Singida leo

  ……………………

  Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amezindua kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Dodoma na Singida.

  Akizindua kampeni hiyo, Dkt. Mahiga ameitaka RITA kuhakikisha inatunza taarifa za watoto wanazozichukua kupitia mtandao wa simu na kuhakikisha zinapatikana pale zitakapohitajika.

  “Kuwasajili watoto hawa kwa kasi hii ni vizuri lakini kazi kubwa ni kuhakikisha taarifa hizo zinawekwa na kutunzwa kule zinakostahili na zinapatikana wakati wote”, alisema Dkt Mahiga.

  Amesema Serikali itaendelea kulinda haki za msingi za raia wake na ndio maana umeamua kutekeleza mpango wa Usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano kwa kuwa cheti cha kuzaliwa ni haki ya kila mtoto.

  Amesema cheti cha kuzaliwa ni alama na vitambulisho wa uraia wa kila mtu na kwamba Tanzania imeamua raia wake wote wawe na utambulisho wao.

  Akizungumza katika uzinduzi huo Mtendaji Mkuu wa RITA bibi Emmy Hudson amesema tangu kuanza kwa awamu ya kwanza ya kampeni hiyo jumla ya watoto milioni tatu wamesajiliwa na kupewa vyeti katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Simiyu, Geita, Njombe, Iringa, Songwe, Mara, Musoma, Lindi, Mtwara, Dodoma na Singida na inakadiriwa hadi kampeni hiyo itakapokamilika mwisho ni mwa mwezi huu zaidi ya watoto milioni tatu na nusu watakuwa wamesajiliwa.

  Awali akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi aliahidi kukusimamia Mkoa wa Singida ili uweze kufanya usajili kwa watoto zaidi ya lengo lililorekebishwa la watoto 280,000 ndani ya wiki mbili ambapo alisema hadi kufikia Machi 20 mkoa wake ulikuwa umesajili zaidi ya watoto 180,000

  Kazi ya usajili wa watoto hao inafanywa na wasajili wasaidizi ambao wamepewa Mafunzo maalum ya kuingiza taarifa za watoto kwa kutumia simu ya Mkononi na inafanyika katika vituo vyote vya afya na katika ofisi za kata ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.

  Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya stendi mjini Singida na kuhudhuriwa na viongozi na watendaji wa serikali kutoka mikoa ya Singida na Dodoma wadau wa maendeleo wa UNICEF, CANADA na kampuni ya TIGO ambayo imetoa simu na mtandao wa simu wake unaothmika kufanya usajili wa watoto katika mikoa hiyo nchini.

  0 0

  Across the globe, new technologies are rapidly replacing coins and notes, with variations among countries. According to the World Payment Report (2018), non - cash transaction global volumes continue to grow at a double-digit rate of 10.1% within an ecosystem of 482.6 billion people. 

  Multiple reports have also shown that the emergence of digital technologies is driving unprecedented change across African countries and Tanzania has joined the bandwagon of nations experiencing robust shifts in digital technology. These paradigm shifts include liberalisation of financial systems, improvements in infrastructure technology and innovations in payment systems. 

  Prior to Tanzania’s independence, people paid for goods and services using various currencies such as: The East African rupee, the Zanzibari rupee, the Zanzibari riyal, British East Africa Florin and the German East African rupee. Since the government issued its first Tanzanian shillings in 1966, the country has by and large been a cash-based economy where the majority of businesses and transactions operate on a cash basis only. The introduction of M-Pesa in 2008 revolutionized the payment/transaction landscape in Tanzania; coupled with the advent of the Internet of Things, the rise of e-commerce will disrupt the way business is conducted. 

  In the last decade, the country has seen ground breaking innovation of electronic payment methods ranging from mobile money, online banking, credit and debit cards, charge card e-wallet or QR scan to the Government e-Payment Gateway System (GePG). Recently, the Bank of Tanzania (BoT) launched an Instant Payment System (TIPS) which is set to create a shared platform for payments originating from different delivery sources to facilitate inter-provider payment for electronic systems and the use of digital financial services among payment service providers. The TIPS ecosystem includes traditional banking services, mobile money and telco network operators providing financial services. 

  According to the Tanzania Communication Regulatory Authority (TCRA), the use of mobile money in the country has recorded a robust growth in recent years, with the value of transactions averaging USD 1.6 billion per month, with over 45 million registered mobile money accounts. Mobile money platforms such as M-Pesa, continue to innovate and simplify the transfer of money across geographical boundaries as well as narrowing financial inclusion gap between men and women. 
  There has also been an increase in the uptake by businesses in the utilization of online payment solutions and the landscape continues to evolve, ensuring safety, security and convenience for consumers to transact online. Vodacom Tanzania limited has been on this journey since it launched M-Pesa in 2008, the platform has combined versatile digital products such as M-Pesa app, M- Pesa Mastercard, M-Pawa, and a newly launched Vikoba digital platform – M-Koba, all these platforms enable Vodacom universal customers to perform transactions without the need of cash, in a more safe and convenient way.

   “With the wider variety of payment options at consumers’ fingertips, the broader objective is to pursue the national cashless payments agenda, in which M-Pesa system will be a driving force in ensuring that over 60 percent of our transaction will be digitized by the M-Pesa cashless platform come 2025” said Vodacom Director of M-Commerce Epimack Mbeteni. 

  Tanzania is on the path to a cashless community and mobile companies like Vodacom are playing an integral role through the use of the digital technologies which allows all people, even in rural areas, to become a part of his cashless society though money transfers, e-payments to businesses and government agencies but also saving and access to loans. Going cashless is becoming increasingly popular among small and medium business all over the country who want to reap the benefits which include faster service, easier financial reconciliation, reduced risk of theft, and appeal to customers who don't carry cash. 

  A whole new suite of value-add services is possible when cash is replaced by electronic-based payment. This presents an opportunity for an inclusive cashless economy without the inconvenience of cash and geographical boundaries. Cash handling is expensive, and in today’s connected world, unnecessary. With 60% of transactions already taking place on mobile platforms, the future is undoubtedly cashless using mobile devices that over 40 million Tanzanians own.

  0 0

   Availability of clean water is still a challenge in many developing countries. According to the Ministry of Water and Irrigation, in Tanzania, only 64% of rural dwellers have access to clean water compared to nearly 80% of urban residents. Challenges such as access to clean water sources, poor management of the water sources and incomplete water projects still impede the public and private partner’s strides in achieving availability of sustainable water supply and management of water sources

  Various initiatives are underway to close the water supply gap and technology is playing a significant role to expedite the bridging process. Every March 22, the world commemorates the International Water Day, to commend the global efforts, partners and initiatives that ensure sustainable supply of water.

  Revolutionizing Remittance Recovery in Water (R3W), is a project funded by Human Development Innovation Fund (HDIF) in partnership with Catholic Relief Services (CRS), to empower communities in Tanzania by building their capacity to reduce water wastage and improve revenue collection. R3W launched a first in the country, electronic water machine called AQtab that is housed in a local kiosk and uses a smart card to monitor and utilize water more efficiently. 

  The project partnered with local water vendors such as Community Owned Water Supply Organizations (COWSOs), the Karatu Village Water Supply (KAVIWASU) and Endamarariek/Endabash Water Supply (ENDAWASU) and significantly ensured reliable and sustainable water supply in the communities. “Until mid-2018, 1,400 smart cards were disbursed to the community members and made a tremendous impact to the communities especially women whom prior to the invention, spent up to three hours waling to fetch water” said Engineer Ephraim Tonya, the Project manager.

  Gongali Nanofilter is another organization that provides safe and clean water to communities across Arusha. With an objective of redirecting the amount of time spent fetching water to productive economic activities, Dr. Askwar Hilonga, the founder of Nanofilter, innovated the tech and assembled 30 Nanofilter stations to provide sustainable supply of water in the communities outside Arusha town. 

  Also funded by Human Development Innovation Fund (HDIF), the project currently has 100 stations that have significantly bridge the water supply gap across Arusha and enabled the community members to invest their time in more productive economic activities such as small scale agricultural, and livestock keeping.

  Given the population growth and increase in water consumption, the Government is accelerating its partner’s efforts by implementing the Water Supply Development Plan (WSDP) which is on its second phase from 2014 to 2019 and also through implementing the right policies to enable successful water projects in Tanzania. 

  WSDP constitutes of programs intended to strengthen institutions in integrated water resources management and improve access to water supply and sanitation services across Tanzania. The Permanent Secretary of in the Ministry of Water and Irrigation, Professor Kitila Mkumbo recently affirmed scientists and innovators of the government’s support, assuring them that they will enact the right policies towards achieving the mutual objective of sustainable water supply in Tanzania.

  0 0  Ni ajabu namna ambavyo simu ya mkononi ilivyobadili maisha ya kila siku ya binadamu. Miongo kadhaa iliyopita, simu ilionekana kama kifaa cha anasa ambacho watu wachache wenye uwezo wa kifedha ndiyo walikuwa wanamiliki.
  Lakini leo hii, simu ya mkononi imekuwa ni kifaa muhimu ambacho asilimia kubwa ya binadamu hawawezi kufanya shughuli zao bila ya kuwa nacho. Simu haitumiki tena kwa matumizi ya kupiga na kupokea simu au kutuma na kupokea ujumbe mfupi wa maneno bali ni kifaa ambacho kinarahisisha shughuli kadha wa kadha za maisha ya kila siku ya binadamu.

  Kupitia simu ya mkononi mtu anaweza kupata huduma za intaneti - kutumia barua pepe, kupata habari, kuperuzi mitandao ya kijamii, huduma za kibenki, kulipia huduma tofauti, kufanya manunuzi ya bidhaa kwa njia ya mtandaoni, kusikiliza muziki, kutazama video, burudani na masuala chungu mzima ambayo yanazidi kuvumbuliwa kadri siku zinavyosonga mbele.

  Kutokana na umuhimu wa simu ya mkononi kumekuwepo na ongezeko kubwa la idadi ya watumiaji wa simu duniani. Kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwenye mtandao wa GSMA, watumiaji wa simu duniani wamefikia zaidi ya bilioni 5. Hii inamaanisha kwamba zaidi ya nusu ya watu duniani, ambayo ni zaidi ya bilioni 7.5, wanatumia simu katika shughuli zao za kila siku.

  Tanzania nayo haiko nyuma katika matumizi ya simu za mkononi. Ikiwa na watu zaidi ya milioni 54, idadi ya wananchi wanaotumia simu za mkononi inazidi kuongezeka kila mwaka. Hivi sasa, ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watumiaji wa simu za mkononi katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla.

  Kwa mujibu wa ripoti ya Takwimu za Mawasiliano iliyotolewa na TCRA ya kuanzia mwezi Oktoba mpaka Desemba 2018, inaonyesha kwamba idadi ya watumiaji wa simu wameongezeka na kufikia zaidi ya milioni 43 mwaka 2018 kutoka milioni 40 mwaka 2017. Hii ni sawa na ueneaji wa asilimia 81 ya Watanzania wanaotumia huduma za simu za mkononi nchini.  Ongezeko la umiliki na utumiaji wa simu za mkononi linasababishwa na sababu kadhaa zikiwemo; ongezeko la makampuni ya mitandao ya simu - ambayo yamepelekea unafuu kwenye upatikanaji wa huduma za mawasiliano, vifurushi vya mtandao wa intaneti pamoja na huduma za kifedha, ongezeko la makampuni yanayouza simu - ambayo yamepelekea simu za mkononi kupatikana kwa urahisi na bei nafuu miongoni mwa Watanzania wengi.

  Katika kuhakikisha watumiaji na wamiliki wa simu za mkononi wanazidi kuongezeka, Jumia imekuwa mstari wa mbele katika kurahisisha upatikanaji wake kwa kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi kwa njia ya mtandaoni. Njia hii itawapatia uwanja mpana wateja kunufaika kwa kuweza kuperuzi maelfu ya bidhaa za simu kutoka kwa wauzaji mbalimbali wa simu mtandaoni, kununua na kupelekewa mpaka mahali walipo.
  Kila mwaka, Jumia huwa na kawaida ya kuwa na kampeni kubwa ya mauzo ya bidhaa za simu pekee kwa muda wa wiki nzima! Wakati wa kampeni hii, wateja hufurahia mauzo ya simu za aina zote kwa gharama nafuu, kupatiwa punguzo kubwa la bei, vocha za bure za manunuzi, pamoja na kuzawadiwa zawadi lukuki pindi wanapofanya manunuzi yao ya kila siku.

  Zimebaki siku chache kabla ya kampeni hii kutangazwa na kuanza rasmi. Kwa sasa, unaweza kutembelea mtandao wa Jumia kujionea bidhaa zilizopo huku ukifuatilia kwa ukaribu kurasa zake za mitandao ya kijamii kupata taarifa mbalimbali. Usicheze mbali, kaa mkao wa kula!

  0 0


  Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Salama Aboud Talib (katikati) akionesha simu ya mkononi aliyokabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba (kuliye aliyeshika kipaza sauti) kama zawadi. 

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimwelekeza Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Salama Aboud Talib (kushoto) namna ya kufanya malipo ya bili ya maji Zanzibar kupitia T-Pesa. 

  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya mtandao wa Simu ya TTCL kulipia huduma za maji kupitia T-Pesa.
  Mkurugenzi wa Biashara na Huduma kwa Wateja wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Kazija Mussa Msheba (kushoto) akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya mtandao wa Simu ya TTCL kulipia huduma za ZAWA kupitia T-Pesa. Kwa makubaliano hayo sasa wateja wa ZAWA watakuwa wakilipa bili zao kupitia mtandao wa T-Pesa. 

  Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Salama Aboud Talib (katikati) akikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya mtandao wa Simu ya TTCL kulipia huduma za maji kupitia T-Pesa. Tukio hilo limefanyika sambamba na Maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Maji, yenye kauli mbiu 'Hakuna Atakae Achwa'. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba.
  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Waziri Waziri Kindamba (kulia) akimkabidhi zawadi ya simu ya mkononi Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Salama Aboud Talib (kushoto) kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya mtandao wa Simu ya TTCL kulipia huduma za maji Zanzibar kupitia T-Pesa. 


  Baadhi ya washiriki kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa matumizi ya mtandao wa Simu ya TTCL kulipia huduma za Mamlaka ya Maji Zanzibar kupitia T-Pesa wakifuatilia matukio anuai. Kwa sasa wateja wa ZAWA watakuwa wakilipa bili zao kupitia T-PESA.
  Baadhi ya wafanyakazi wa TTCL (kushoto) wakiwaelekeza washiriki namna ya kulipia huduma za ZAWA kupitia T-Pesa.
  Wateja wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) wakipata maelekezo namna ya kulipia bili kwa T-PESA.
  Picha ya pamoja na meza kuu mara baada ya hafla hiyo.

  0 0

  Hitimisho la Wiki ya Maji Duniani, Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka (DAWASA) wamewapa furaha wakazi wa Saranga na maeneo jirani kwa kuwapatia maji safi na salama. Akizungua wakati wa kuzindua mradi wa kuwasambazia maji wakazi wa Saranga Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori amesema kuwa amefurahishwa jinsi DAWASA walivyoweza kuwapa furaha wakazi hao wa Saranga kwa kuwapatia maji ambayo watakuwa wakiyapata masaa 24. Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es S  alaam Kisare Makori (kushoto) akimpongeza Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema kwa kuweza kufanikisha uwekaji wa bomba eneo la Saranga jijini Dar es Salaam. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
   Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori (kushoto) akimpongeza Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema kwa kuweza kufanikisha uwekaji wa bomba eneo la Saranga. Wengine wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori (kushoto) akizungumza na wakazi wa Saranga (picha ya chini) Kaimu Mkurugenzi wa miradi DAWASA Lydia Ndibalema akizungumza na wakazi wa Saranga jijini Dar es Salaam kuwaelezea jinsi walivyoweza kufanikisha kufikisha mradi huo.
  Meneja wa DAWASA- Kimara jijini Dar es Salaam Paschal Fumbuka akielezea jinsi mradi ulivyoweza kukamilika wakati wa hitimisho la wiki ya Maji Duniani iliyoanza Machi 16-22, 2019.
  Diwani wa kata ya Saranga Mhe. Haruni Mdoe akizungumza na wakazi wa Kimara Tembeni kata ya Saranga jijini Dar es Salaam.
   Mkuu wa Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam Kisare Makori (wa tatu kutoka kushoto) akikata utepe na Diwani wa kata ya Saranga Mhe. Haruni Mdoe kuzindua huduma hiyo.
  Tukio Lingine alilolifanya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Makori ni kuzindua eneo la Bomba la Kwanza lililowekwa kwa mkazi mmoja wa Saranga ili kuonyesha ishara ya usambazaji wa maji kwa wakazi hao.
  Wakazi wa Saranga wakijiandikisha mbele ya wenyekiti wa Serikali za mtaa ili waweze kupatiwa maji na DAWASA.
  Meneja wa huduma kwa wateja wa DAWASA Doreen Kiwango akiangalia zoezi la uandikishaji wateja wapya wakazi wa Saranga linavyoendelea.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwasilisha Taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na Taarifa kuhusu makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2019/2020 mbele ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) (hawapo pichani) wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Wizara kilichofanyika kwenye Ofisi za Bunge, Dodoma tarehe 22 Machi, 2019. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhan M. Mwinyi. 
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), Mhe. Mussa Azan Zungu akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) (hayupo pichani), wakati akiwasilisha taarifa kuhusu bajeti ya Wizara yake wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Wizara kilichofanyika Ofisi za Bunge, Dodoma tarehe 22 Machi, 2019. Wakati wa kikao hicho, Mhe. Zungu alitumia fursa hiyo kwa niaba ya Kamati, kumpongeza Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua ya kupeleka haraka misaada ya chakula na dawa kwa nchi za Malawi, Msumbiji na Zimbabwe baada ya kupatwa na maafa yaliyosababishwa na kimbunga kikali kilichozikumba nchi hizo. 
  Kikao kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama na Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kikiendelea 
  Sehemu ya Wabunge ambao ni Wajumbe wa Kamati hiyo wakifuatilia kikao 
  Sehemu ya Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye kikao na Kamati ya Bunge ya NUU 
  Wajumbe wa Kamati wakimsikiliza Mhe. Waziri (hayupo pichani) 
  Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kikao 

  Mjumbe wa Kamati akichangia hoja wakati wa kikao hicho 
  Sehemu nyingine ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara wakiwa kwenye kikao na Kamati ya Bunge ya NUU 
  Mjumbe wa Kamati akichangia jambo wakati wa kikao na Wizara 
  Mjumbe mwingine wa Kamati ya Bunge ya NUU akichangia hoja wakati wa kikao kati ya Kamati hiyo na Wizara 
  Mhe. Mbunge akichangia hoja

  0 0


  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Godwin Sharau kwa kushirikiana na madaktari kutoka Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kuziba tundu kwenye moyo wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku saba inayoendelea katika taasisi hiyo. Jumla ya watoto tisa wamefinyiwa upasuaji wa kuziba matundu na hali zoa zinaendelea vizuri
  Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Evarist Nyawawa kwa kushirikiana na madaktari wa Shirika la Open Heart International (0HI) la nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa kubadilisha valvu wakati wa kambi maalum ya matibabu inayoendelea katika taasisi hiyo. Jumla ya watu wazima watano wenye matatizo ya moyo wamefanyiwa upasuaji katika kambi hiyo ya siku saba na hali zao zinaendelea vizuri.
  Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Lilian Peter kwa kushirikina na wenzake wa Shirika la Open Heart International (OHI) la nchini Australia wakimuhudumia mtoto aliyelazwa katika chumba cha wagonjwa waliopo katika uangalizi maalum (ICU) wakati wa kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku saba inayofanywa katika taasisi hiyo. Jumla ya watoto tisa wamefanyiwa upasuaji na hali zao zinaendelea vizuri.

  Picha na: Genofeva Matemu – JKCI

  0 0


  Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Mkoa wa Tabora kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
  Mjumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Hamad Maalim akichangia jambo wakati Kamati hiyo ikipokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Mkoa wa Tabora kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)
  Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mheshimiwa Agrey Mwanri akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na makadirio ya mapato na matumizi ya kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ya Mkoa huo mbele ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa kwenye Ukumbi wa Msekwa Jijini Dodoma hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited (CSTC), Bw. Gerald Billet (kulia) wakifungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha CSTC kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuwasha mashine ya kuchakata muhogo wakati alipozindua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba na wa pili kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Frederick Clavier.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akibonyeza kitufe kuwasha mashine ya kuchakata muhogo wakati alipozindua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoni Lindi, Machi 22, 2019. Kulia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba na wa tatu kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Frederick Clavier.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua kazi ya uchakataji muhogo wakati alipofungua kiwanda cha kuchakata mhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe wakati alipofungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha mbalala kwenye jimbo la Mtama mkoani Lindi Machi 22, 2019. Wengine kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Hamida Abdallah, Naibu Waziri wa kilimo, Omari Mgumba, Kaimu Mkuu wa mkoa wa Lindi na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, Mwenyekiti wa CSTC, Gerald Billet, Balozi wa ufaransa nchini, Frederick Clavier, Mkurugenzi Mtendaji wa CSTC, Christophe Gallean na kulia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mfuko wenye unga wa muhogo wakati alipofungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kwenye kijiji cha Mbalala katika jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019. Wa pili kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Hamida Abdallah. Kulia kwa Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga na kushoto ni Shift Leader wa CSTC, Samwel Ponera
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzania Corporation Limkited (CSTC) baada ya kukifungua kwenye kijiji cha Mbalala katika jimbo la Mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashra, Joseph Kakunda na wa pili kulia ni Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye. Wa tatu kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi na Mkuu wa wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kufungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Cassava Starch of Tanzani Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala kwenye jimbo la mtama mkoani Lindi, Machi 22, 2019. Wa tatu kulia ni Balozi wa Ufaransa nchini, Frederick Clavier, wa pili kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Joseph Kakunda na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CSTS, Christophe Gallean. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  ………………………..

  *Awataka wakulima kuchangamkia fursa kwa kulima kwa wingi

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wananchi katika mikoa ya Lindi na Mtwara watumie fursa ya uwepo wa kiwanda cha kuchakata muhogo katika kijiji cha Mbalala, kata ya Nyengedi mkoani Lindi kwa kulima zao hilo kwa wingi ili waweze kujiongezea kipato.

  “Kama unataka pesa nenda kalime muhogo kwani kuna soko la uhakika na pia zao hili ni la muda mfupi na kilimo chake ni rahisi. Kwa sasa hatuna muda wa kukaa vijiweni vijana jiungeni katika makundi na muanzishe mashamba ya mihogo soko lipo tena mwenye kiwanda atawafuata hukohuko shambani.”

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Machi 22, 2019) wakati akifungua kiwanda cha kuchakata muhogo cha Kampuni ya Cassava Starch of Tanzania Corporation Limited (CSTC) kilichopo katika kijiji cha Mbalala, kata ya Nyengedi mkoani Lindi.


  Amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli la kuhamasisha ujenzi wa viwanda ni kusaidia katika kuongeza thamani ya mazao mbalimbali yanayolimwa na wakulima nchini kabla ya kuuzwa.” Mbali na kuongeza tija kwa wakulima pia viwanda vinatoa ajira nyingi”.

  Kadhalika, Waziri Mkuu amekipongeza kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo cha Naliendele kilichopo mkoani Mtwara kwa kazi nzuri ya utafiti wa mbegu za mazao mbalimbali wanayoifanya. Amesema kituo hicho ndicho kilichotafiti mbegu bora za muhogo zenye uwezo wa kuzalisha tani 20 hadi 50 kwa hekta.

  Kwa upande wake, Balozi wa ufaransa nchini, Balozi Frederic Clavier amesema Serikali ya Ufaransa ipo tayari kumuunga mkono Rais Dkt. Magufuli katika mkakati wake wa kukuza uchumi hadi kufikia uchumi wa kati kwa kupitia sekta ya viwanda ifikapo 2025.


  Amesema ujenzi wa kiwanda hicho ni ushuhuda tosha wa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ufaransa na kilimo ni miongoni mwa mikakati ya kuinua uchumi wa Tanzania.

  Nae, Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amewashukuru wawekezaji hao kwa uamuzi wao wa kujenga kiwanda cha kuchakata muhogo nchini kwa kuwa wamewezesha wakulima wa zao hilo kupata soko la uhakika na vijana wengi kupata ajira.

  Kwa upande wake,Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa msukumo alioutoa wa kuhamasisha ujenzi wa viwanda nchini kwa kuwa umechangia kuboresha maendeleo ya wananchi katika maeneo mbalimbali.

  Mbunge huyo amesema uwekezaji katika sekta ya viwanda umesaidia kupunguza changamoto ya ajira hususani kwa vijana. “Tunamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli kwa juhudi zake, kwani hatukutarajia kuwa na kiwanda katika eneo hili”.

  Awali,Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CSTC, Christophe Gallean alisema kiwanda hicho ambacho kilianza kujengwa mwaka 2012 kinazalisha unga wa muhogo wenye kiwango cha juu cha ubora na kinauza unga huo katika nchi za Afrika Mashariki, Kusini, Mashariki ya Kati, Ulaya na Marekani.

  Alisema kiwanda hicho chenye wafanyakazi zaidi ya 420 ambapo Watanzania ni asilimia 97 kina uwezo wa kuchakata tani 60 za muhogo mbichi kwa siku, ambao ni sawa na tani 25 za unga bora wa muhogo kwa siku.

  0 0

  Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha vijana bungeni, Zainabu Katimba, kulia, akizungumza na baadhi ya vijana wanaowakilisha makundi mbalimbali jijini Dar es Salaam, katika kongamano aliloandaa lenye dhamira ya kuangalia fursa za kiuchumi zinazoweza kufanyia na vijana kwa ajili ya kukuza uchumi wao. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung (FES), Andreas Quasten, ambayo wameshirikiana na Mbunge kuwezesha Kongamano hilo. Picha na Mpigapicha Wetu.

  Mbunge wa Viti Maalum anayewakilisha vijana bungeni, Zainabu Katimba, akizumgumza na waandishi wa habari hawapo pichani katika kongamano aliloandaa lenye dhamira ya kumuwezesha kijana katika hali ya kufanyia kazi changamoto zinazowakabili vijana nchini Tanzania. Kongamano hilo pia limeandaliwa kwa ushirikiano mkubwa wa taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung (FES). Picha na Mpigapicha Wetu. 


  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

  VIJANA mbalimbali nchini Tanzania, wameaswa kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi, ikiwamo namna bora ya kuungana vikundi ili kuomba fedha za Halmashauri ambazo zimekuwa zikikosa waombaji katika maeneo mengi, huku sababu kubwa ni uelewa mdogo juu ya upatikani wa fedha hizo zinazotolewa maalum ili kuwakomboa vijana kiuchumi. 

  Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalum, akiwakilisha vijana katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zainabu Katimba, katika kongamano la vijana aliloandaa kwa kushirikiana na taasisi yake ya WEZESHA, akishirikiana pia na Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung, ikikutanisha viongozi wa makundi mbalimbali jijini Dar es Salaam, nchini hapa. 

  Akizumgumzia changamoto hizo, mheshimiwa Katimba alisema kuwa wapo watu wanaoamini kuwa fedha hizo hazipo au zinatoka kwa watu maalum, bila kujua kwamba fedha hazitoki kwa watu mmoja mmoja na kinachotakiwa ni kuungana katika makundi na kuanisha vipengele vya kimkakati, jambo ambalo limekuwa halifanyiki. 

  “Mimi nawakilisha vijana kule bungeni, lakini pia tunaelekea kwenye bajeti mpya, hivyo naamini pamoja na mambo mengine, tukitoka kwenye kongamano hili la kuwezesha a, kuelimishana sambamba na kufungua milango ya kuiona fursa, naamini tutakuwa katika nafasi nzuri, zaidi uwezo wa vijana kuzichangamkia pia fedha za serikali katika Halmashauri zetu. 

  “Nimekuwa nikifanya makongamano haya kwa muda mrefu na dhamira yetu kubwa ni sisi vijana wenyewe kujitambua, kwa sababu tunapoweza kutumia fursa tunazokutana nazo mtaani, walau tunaweza kujikwamua kiuchumi na kulikomboa pia Taifa letu ambalo sera ya viwanda imeshika kasi na sisi vijana wenyewe ndio nguvu kazi ya Taifa kwa namna moja ama nyingine,”Alisema Katimba, ambaye pia ni mwasisi wa taasisi ya Wezesha. 

  Akizumgumzia kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Friedrich Ebert Stiftung (FES), Andreas Quasten, alimpongeza Mbunge wa Viti Maalum, Zainabu, kwakuwa karibu na vijana akisema anawawakilisha vizuri bungeni.
  “FES tunampongeza bi Zainabu kwa kufanya mambo mengi yanayohusu vijana, ambapo tunaamini kwa uwapo wake bungeni, unasaidia kuwezesha vijana, katika kipindi hiki ambacho idadi kubwa ya watu Tanzania ni vijana, huku wakiwa na changamoto nyingi ikiwamo ajira, ushiriki katika mambo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi. 

  “Sisi FES tutaendelea kushirikiana na makundi yote sambamba na serikali Kuu ili kuhakikisha kwamba changamoto hizo zinakwisha ili kuwafanya vijana na Watanzania wote wanaishi maisha vizuri, sanjari na uelewa mpana wa kutumia fursa endelevu za kiuchumi,”Alisema. 

  Katika kongamano hilo la siku moja lililofanyika katika ofisi Kuu za FES zilizopo Kinondoni, Morocco, jijini Dar es Salaam, vijana mbalimbali walichambua changamoto wanazokutana nazo mitaani, bila kusahau mwelekeo unaoatakiwa kufuatwa katika Bajeti Kuu ya Serikali itakayosomwa baadaye mwaka huu bungeni, jijini Dodoma.

  0 0


  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu (katikati) akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni (kushoto) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo kwa ukubwa wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita., Kulia ni Meneja wa shamba hilo, Edward Nyondo.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni (kushoto) alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo kwa ukubwa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita. Wengine ni watumishi pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa shamba la miti la Biharamulo ambalo mara baada ya kukamilika kwa kupandwa miti katika eneo lote litakuwa ndio shamba la pili kwa ukubwa kati ya mashamba 20 yanayomilikiwa na Wakala wa Hudumza Misitu Tanzania lililopo wilayani Chato mkoani Kagera.

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akipanda mti wakati alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita

  Mkuu wa wilaya ya Chato, Mhe. Mtemi Simeoni akipanda mti wakati alipoambatana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu alipotembelea Shamba la Miti la Biharamulo mara baada ya kukagua maendeleo ya miti iliyopandwa katika shamba hilo lenye ukubwa wa hekari 900 katika wilaya ya Chato mkoani Geita
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Constantine Kanyasu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya na watumishi wa Shamba la Miti la Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
  Baadhi ya watumishi wa Shamba la Miti la Biharamulo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika shamaba hilo hukuakiwasisitizan umuhimu wa kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi wanaoishi karibu na shamba hilo.
  (Picha na Wizara ya Maliasili na Utalii)
  …………………………. 

  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ametoa muda wa miezi mitatu kwa wananchi waliovamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba la miti la Biharamulo kuondoka mara moja kwa hiari yao bila shuruti kabla ya mwezi Juni mwaka huu. 

  Ametoa muda huo ili wananchi waliolima mazao mbalimbali yakiwemo mahindi na pamba waweze kuvuna mazao yao kabla ya kuanza kwa oparesheni maalum ya kuwaondoa, iliyopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu itakayofanywa na Wakala wa Huduma ya Misitu Tanzania ( TFS) kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo. 

  Mhe.Kanyasu ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kutembelea shamba la miti Biharamulo lililopo katika wilaya ya Chato mkoani Geita.
  Amesema Oparesheni hiyo haitasubiri taarifa ya Wizara tano inayoendelea kufanyiwa kazi kwa kuwa eneo hilo halihusiani na vile vijiji 366 vilivyokutwa ndani ya Hifadhi. 

  Amesema haiwezekani wananchi waliovamia eneo hilo waendelee kuachwa kwa kisingizio cha Kauli ya Rais aliyoitoa Januari 15 mwaka huu kuhusiana na vijiji 366 vilivyokutwa ndani ya maeneo ya Hifadhi. 

  Amebainisha kuwa wananchi waliovamia eneo hilo wameitafsiri visivyo Kauli hiyo na kuongeza kuwa baada tu ya tamko la Mhe. Rais , baadhi ya wananchi hata wale waliokuwa wakiishi katika maeneo mengine nje ya hifadhi waliendelea kuvamia na kuanza kujimilikishia maeneo makubwa wakidai kuhalalishwa na tamko la Rais. 

  Amefafanua kuwa taarifa inayoendelea kufanyiwa kazi na timu ya Mawaziri na Makatibu Wakuu kutoka Wizara tano imebainisha kuwa mpaka sasa zaidi ya vijiji 700 vimekutwa ndani ya Hifadhi badala 366 vilivyoripotiwa awali. 

  Kufuatia hali hiyo amesema baadhi ya wavamizi wa Hifadhi katika maeneo mbalimbali wataendelea kuondolewa bila kusubili kukamilika kwa zoezi linaloendelea kwa kuwa walieendelea kuvamia maeneo ya Hifadhi kwa kisingizio cha tamko la Rais huku maeneo hayo yakizidi kuharibiwa kwa miti kukatwa na shughuli nyingi za kibinadamu 

  Katika hatua nyingine, Mhe.Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ( TFS) kutenga Bajeti ya kugharamia operesheni ya kuwaondoa wavamizi ndani ya Shamba hilo. Ameitaka TFS kuendesha oparesheni za mara kwa mara ili wavamizi hao wajue Serikali ipo kazini kulinda rasilimali za Taifa muda wote. 

  Awali, Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mtemi Simeoni akizungumza katika ziara hiyo alisema kuwa baadhi ya wananchi kutoka nje ya wilaya hiyo wamekua wakivamia na kuanzisha shughuli za kibinadamu ndani ya Shamba hilo, suala ambalo ni kinyume cha sheria. 

  Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa wananchi katika maenro hayo wana mahitaji makubwa ardhi na kuiomba Wizara iangalie namna ya kuwasaidia hekari 5000 ili wapate maeneo ya kulima na kuchungia mifugo yao.
  Kwa upande wake Meneja wa Shamba hilo Bw. Thadeus Shirima amemweleza Naibu Waziri huyo kuwa hadi sasa zaidi ya hekari 900 zimepandwa miti licha ya Shamba hilo kukabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi pamoja na vitendea kazi.

  0 0


  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Balozi Tanzania Nchini Zambia Mhe.Balozi Hassan Simba Yahya, alipofika Ikulu Zanzibar leo 22-3-2019, kwa mazungumzo na Rais.(Picha na Ikulu)
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Mhe. Hassan Simba Yahya, alipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo leo 22-3-2019(Picha na Ikulu)
  /RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Balozi wa Tanzania Nchini Zambia Mhe. Balozi Hassan Simba Yahya, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu Zanzibar leo,22-3-2019.(Picha na Ikulu)

  0 0


  Serikali ya Marekani ilikabidhi vifaa vya kupimia maji kwa Bodi za Mabonde ya Maji Rufiji na Wami / Ruvu. Vifaa na huduma za ziada vitasaidia bodi kukusanya na kuchambua takwimu juu ya ubora na kiasi cha maji. Ufuatiliaji wa uboreshaji wa maji utasaidia wilaya kufanya maamuzi sahihi juu ya ugawaji wa maji ili kusimamia na kulinda rasilimali za maji kwa vizazi vijavyo.

  Mbali na vifaa vya kupimia maji, Bodi za Maji zilipata boti/mashua, kompyuta, redio, vifaa vya kukadiria umbali, na vifaa vya mtandao kwa shughuli za zinazofanyika katika eneo la mradi na ofisini. Wafanyakazi watafundishwa namna ya kutumia vifaa vya kupimia maji ya mtoni.

  Vifaa na huduma, vyenye thamani ya shilingi bilioni 2.3 za Kitanzania (dola 980,000 za Kimarekani), zilikabidhiwa na Shirika la WARIDI, na kufadhiliwa na Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID). WARIDI inaendeleza usimamizi wa rasilimali maji na kuboresha upatikanaji wa huduma za maji.

  “Kwa sababu maji yana jukumu muhimu katika kupunguza umasikini, kuboresha afya, na kuongeza uzalishaji, ni lazima yapewe kipaumbele cha juu serikalini na jumuiya ya wafadhili,” alisema Andrew Karas, Kaimu Naibu Balozi wa Ubalozi wa Marekani.

  Kupitia WARIDI, Serikali ya Marekani pia ilipatia Wizara ya Maji mwongozo wa matumizi ya kutathmini uwezo wa Jumuiya za Watumia Maji (WUAs), asasi za kijamii zinazohusika na usimamizi wa rasilimali za maji. WUA wana mamlaka ya kisheria ya kupata na kutumia vibali vya matumizi ya maji, kutatua migogoro ya matumizi ya maji, kulinda vyanzo vya maji, kuwakilisha maslahi ya watumiaji katika ngazi ya jamii, na kukusanya tozo za watumiaji wa maji kwa niaba ya Bodi za Mabonde za Maji.
   
   Kifaa kinaweza kutumika kwa ufuatiliaji wa mara kwa mara wa WUA na kutambua hatua za kuboresha utendaji. Ilianzishwa kupitia mchakato shirikishi unaohusisha wawakilishi kutoka Bodi ya Maji ya Bonde, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wizara ya Maji, na washauri wa ndani.

  Ili kuomba taarifa zaidi, tafadhali piga simu Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kupitia: +255 22 229-4000 au barua pepe: DPO@state.gov.

older | 1 | .... | 1822 | 1823 | (Page 1824) | 1825 | 1826 | .... | 1897 | newer