Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA MKOANI SINGIDA

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi mara baada ya kuwasili wilayani Manyoni na kupokea taarifa ya mkoa katika ukumbi wa Halmashauri Manyoni ikiwa siku ya kwanza ya ziara yake ya kuhamasisha na kukagua shughuli za kimaendeleo mkoani humo.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais )
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na vijana wa skauti mara baada ya kuwasili wilayani Manyoni, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Daniel Mtuka mara baada ya kuwasili wilayani Manyoni tayari kwa ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Singida

VIONGOZI WA CCM KAGUENI MIRADI-MAJALIWA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja vya  ofisi ya CCM ya mkoa wa Kigoma kuzungumza na  viongozi wa CCM, serikali na wabunge, Februari 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa CCM, Serikali na wabunge wa mkoa wa Kigoma kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM ya Mkoa wa Kigoma, Februari 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa CCM, Serikali na wabunge wa mkoa wa Kigoma kwenye ukumbi wa Ofisi ya CCM ya Mkoa wa Kigoma, Februari 16, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya viongozi wa CCM,Serikali na wabunge wa mkoa wa Kigoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Kigoma, Februari 16, 2019.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wajumbe wa Halmashauri Kuu za Mkoa na Wilaya za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wahakikishe wanakagua miradi mbalimbali inayotekelezwa kwenye maeneo yao na wajiridhishe kama inalingana na thamani halisi ya kiasi cha fedha kilichotumika.

Amesema iwapo viongozi hao hawataridhishwa na utekelezwaji wa mradi husika wasisite kuchukua hatua kwa kutoa taarifa katika ngazi huzika, lengo ni kuhakikisha miradi yote inakuwa na ubora na inalingana na thamani ya fedha iliyotolewa.

Ametoa maagizo hayo leo (Jumamosi, Februari 16, 2019) wakati akizungumza na viongozi wa CCM, wabunge pamoja na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Kigoma kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya CCM ya mkoa wa Kigoma.

Waziri Mkuu ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mlezi wa CCM mkoa wa Kigoma amesema ni muhimu kwa viongozi hao kujiridhisha na muenendo wa utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii katika maeneo yao zikiwemo za afya, maji, elimu na kilimo.

Amesema CCM itaendelea kuimarisha misingi ya utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi, hivyo amewataka viongozi wa CCM pamoja na viongozi wa Serikali washikamane ili malengo ya kuwaletea wananchi maendeleo yatimie.

“CCM ni chama imara chenye mipango inayotekelezeka na kilicholenga kuwaletea wananchi maendeleo na kushirikiana nao katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili na ndicho chama pekee chenye kuleta matumaini kwa Watanzania wote.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amewasisitiza wanachama na wapenzi wa CCM wasome katiba ya chama na kuzielewa kanuni, taratibu na sera ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Akisisitiza jambo hilo Waziri Mkuu amegawa nakala za katiba ya CCM kwa viongozi hao.

Awali, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu, Emmanuel Maganga alisoma taarifa ya mkoa huo, ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia zoezi la kuwasaka wahamiaji haramu linaloendelea kwenye mkoa huo.

Mkuu huyo wa mkoa amesema katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Desemba 2018 jumla ya wahamiaji haramu zaidi ya 4,135 walikamatwa kwenye msako uliofanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

DKT. MPANGO ATETA NA WAFANYAKAZI NA KUHIMIZA MAADIDLI NA UWAJIBIKAJI KAZINI

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na Watumishi wa Wizara hiyo na kuzungumza nao namna bora ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara ili kusukuma kasi ya maendeleo ya uchumi wa Taifa.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Mpango alisema Wizara ya Fedha na Mipango ni kitovu cha Serikali hivyo Watumishi wote wa Wizara wanawajibu wa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia nidhamu, maadili, sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa Umma ili kuongeza tija.

Amesema kila mtumishi anawajibu wa kufanya kazi kwa weledi, bidii na kushirikiana na kila mmoja katika nafasi yake ili kuboresha utendaji kazi na kukuza uhusiano mahala pa kazi.

Aidha Waziri Mpango aliwapongeza Watumishi wa Wizara hiyo kwa kazi wanazozifanya hususan kazi ya uandaaji wa Bajeti Kuu ya Serikali, Uchambuzi wa Sera za Taifa na uanzishwaji wa mfumo mpya wa ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki-GePG.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu amemhakikishia Waziri Mpango kuwa watatekeleza maelekezo yote aliyoyatoa kwa ukamilifu ili kuboresha utendaji kazi wa Wizara hiyo.


Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isidor Mpango (Mb) akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), katika kikao na Watumishi hao Jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Khatibu Kazungu akifafanua jambo wakati wa kikao na Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), Jijini Dodoma.

Mjumbe wa TUGHE Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Mariam Kihange, akichangia mada wakati wa kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo uliofanyika Jijini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Gisela Mugumira akifafanua jambo wakati wa kikao na Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani), uliofanyika katika ukumbi wa Kambarage Jijini Dodoma, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu wa Wizara hiyo, Bw. Alfred Dede.

Mwakilishi wa Kamishna wa Bajeti Bw. Sigsbert Kavishe akichangia hoja katika wa kikao na Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango, kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Khatibu Kazungu, kulia ni Kaimu Mhasibu Mkuu wa Serikali Bw. Victus Tesha Jijini Dodoma.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia kwa karibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika kikao cha Watumishi wa Wizara hiyo Jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WFM

Waziri wa Nishati, azindua Bodi mpya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutoa maelekezo

$
0
0
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Katika kikao hicho pia walihudhuria Watendaji wa Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kushoto kwa Waziri ni Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu.
Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Nishati, Raphael Nombo (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizungumza na Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambayo imezinduliwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambayo imezinduliwa na Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Katika kikao hicho pia walihudhuria Watendaji wa Wizara ya Nishati na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kulia kwa Waziri ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini, Michael Nyagoga kitabu cha Sheria ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005 ikiwa ni muongozo wa majukumu ya Bodi hiyo katika kusimamia Wakala huo.


Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, leo amezindua Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), na kutoa maelekezo mbalimbali kwa Bodi hiyo yatakayopelekea kazi ya usambazaji umeme vijijini kufanyika kwa kasi na ufanisi.

Kikao cha Waziri na Bodi hiyo kimefanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Mwinyimvua, Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Nishati, Raphael Nombo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga na watendaji wengine kutoka Wizara na REA.

Akizungumza na Bodi hiyo, Dkt Kalemani alieleza sababu mbalimbali za kuvunjwa kwa Bodi iliyopita tarehe 12 Novemba, 2018 kuwa ni kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kushindwa kusimamia vizuri Wakala wa Nishati Vijijini.

“ Leo tunawakabidhi majukumu yenu lakini suala la msingi ni kuwatumikia wananchi kwani tunawajibika kwao hivyo yaliyotokea kwenye Bodi iliyopita, yasitokee kwenye Bodi yenu”. Alisema Dkt Kalemani

Alitaja majukumu ya Bodi hiyo kuwa ni kusimamia Wakala wa Nishati Vijijini ili utekeleze majukumu yake kwa ufanisi na weledi na kusimamia shughuli za Wakala ili zifanyike kwa malengo na Dira ya Serikali ya kusambaza umeme katika Vijiji vyote nchini.

Aliongeza kuwa, majukumu mengine ya Bodi hiyo ni kusimamia Fedha za Mfuko wa Nishati Vijijini ili tija yake ionekane na kuitaka Bodi hiyo kutokuwa chanzo cha migogoro inayoweza kuchelewesha au kukwamisha kazi za Wakala.

Aidha, ameiagiza Bodi hiyo kuharakisha utekelezaji wa kusambaza umeme katika Vijiji, vitongoji na miradi mbalimbali ya kijamii na kuwasimamia ipasavyo wakandarasi wa umeme vijijini ili kazi zao ziende kwa haraka kwani wengi wao hawafanyi kazi zao inavyotakiwa.

Dkt. Kalemani amezindua Bodi hiyo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kumteua Bw. Michael Nyagoga kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo tarehe 14 Februari 2019.

Wajumbe wa Bodi hiyo ni Oswald Urassa, Mhandisi Styden Rwebangila, Francis Songela, Louis Accaro, Dailin Leonard, Henry Mwimbe na Dkt. Andrew Komba.

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUTUMIA WELEDI WALIONAO KUIELIMISHA JAMII KUHUSU AFYA YA UZAZI NA NDOA ZA UTOTONI

$
0
0

Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali Jijini Arusha wakifuatili kwa makini kongamano hilo lililowakutanisha kwa pamoja katika Ofisi ya Halmashauri ya wilaya ya Arusha
Mafunzo yakiendele juu ya maswala ya Afya ya uzazi chini ya vijana wenye umri wa miaka 18,ndoa xa utotoni, na mimba za utotoni.



Na. Vero Ignatus Arusha

Vyombo vya habari nchini vimetakiwa kutumia ujuzi na weredi katika kuelimisha jamii juu ya elimu ya uzazi kwa vijana chini ya umri miaka kumi na nane pamoja na kupinga vita ndoa za utotoni hali ambayo inapelekea vijana wengi kuacha kuendelea na masomo yao.

Akizungumza katika kongamano lililowakutanisha waandishi habari wa vyombo tofauti mkoani Arusha katika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Arusha Muuguzi mkuu wa mkoa Bi Getrude Anderson amesema lengo la kongamano hilo ili kuwapa elimu wandishi wa habari juu ya maswala ya afya ya uzazi ili waweze kutumia elimu hiyo katika kuwahabarisha jamii athari za mimba za utotoni, ndoa za utotoni pamoja na elimu ya uzazi wa mpango.

Aidha Bi Getrude amesema kupitia kongamano hilo waandishi wanauwezo mkubwa wa kutumia weledi na ujuzi walionao katika kuihabarisha jamii habari za afya zenye uhakika kwani elimu huwafikia walengwaa kwa kutumia vyombo vya habari.

“Tumeamua kuandaa kongamano hili kwa kuwaaitisha waandishi habari ili kuwapa elimu waandi hawa wa vyombo mbali mbali juu ya maswala ya uzazi kwa vijana kwani waandishi hawa wakianda vipindi mbali mbali vya elimu ya uzazi vijana wataelewa mambo ya wahusuyo lakini sio hivyo tu hawawezi kuanda habari zenye weledi bila kupata ujuzi kutoka kwetu sisi wataalam wa afya,tumewataka pia waanandae makundi mbali mbali ya waandishi wa habari mbali n kuwahabarisha pia wawafuate hukuo huko vijana wawape elimu” Alisema

Alisema kupitia waandishi watapata mafanikio ya kuwafikia jamii na vijana kwani vijana wengi hufutilia sana mitandao ya kijamii ya kijamii,na hufuatilia habari hivyo wanamategemeo kupitia kongamano hilo lililofanyika italeta mafanikio mazuri sambamba kuwashauri vijana kutengeneza vikundi,na vipindi mbalimbali vya ili kufikisha elimu kwa walengwa

Alisema siku ya leo 17 februari 2019 wameaandaa tamasha ambalo litawakutanisha vijana mbali mbali mkoani arusha ambapo Tamasha hilo lita fanyika katika viwanja vya kumbu kumbu la azimio la Arusha katika mnara wa Mwenge ambapo kutakuwa nafursa za upimaji wa afya kama vile upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi,virusi vya ukimwi na magonjwa mengineyo.,

Nae Mratibu wa mradi wa tupange pamoja Bwana Waziri Njau amesema lengo la kuwakutanisha waandishi habari ni kwa ajili ya kumtanisha kijana kwa kuandaa klabu mbalimbali na wameamua kuandaa matamasha ya vijana kupitia wandi habari ili kuwapa habari zenye weledi

WAZIRI LUGOLA AIPA POLISI WIKI MOJA KUFANYA UCHUNGUZI, KUWAKAMATA WATUHUMIWA WA MAUAJI YA WANAWAKE MTO WA MBU MKOANI ARUSHA

$
0
0
Na Mwandishi Wetu, MOHA-Monduli

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa wiki moja, Jeshi la Polisi kuhakikisha linafanya uchunguzi wa kina kwa kuwakamata watuhumiwa waliofanya matukio ya kikatili ya ubakaji na mauaji ya wanawake yaliyotokea Mto wa Mbu Wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha.

Akizungumza na wananchi wa Mji mdogo wa Mto wa Mbu, wilayani humo, leo, kutokana na matukio hayo, Waziri Lugola amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, kushirikiana na Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo, na kusimamiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, kuhakikisha uchunguzi wa kitelijensia unafanyika juu ya watu wanaohusika kufanya vitendo hivyo vya kikatili katika eneo hilo.

Lugola aliongeza kuwa, haiwezekani wananchi wa eneo hilo wawe wanaishi kwa wasiwasi, wanateswa, kuuawa na kudhalilishwa wakati Serikali ya Rais Dkt John Magufuli ipo, Polisi wapo, pamoja na wananchi wapo, kwa hatua hiyo lazima mauaji hayo yafikie kikomo.

"Ndugu wananchi Serikali ya Dkt Magufuli haiwezi kuchzewa hata kidogo, lazima tudhibiti hii taaruki, na tusipofanya hivi, hii hali itaendelea kushika kasi jambo ambalo Serikali haiwezi kukaa kimya,” alisema Lugola na kuongeza;

“Wakina mama wataisha kutokana na vitendo hivyo vya kikatili na lazima tuwe na uchungu sasa, Jeshi la Polisi lijipange vizuri kwa kufanya kazi ya weledi kwa muda wa wiki moja hakikisheni mnafanya kazi nzuri ipasavyo ili kuwatia mbaroni hao watuhumiwa na kufunguliwa mashtaka haraka iwezekanavyo,” alisema Lugola.

Lugola aliwatoa wasiwasi akina mama wa mji huo na kuwataka kuleta taarifa za siri kuhusiana na wahusika hao kwasababu hawatoki mbali bali katika mazingira hayo hayo wanayoishi.

“Mmependekeza mpige kura za kimya kimya kwa kuwa uwanjani mkiandika majina ya watuhumiwa, mkihofia mkipeleka taarifa Kituo cha Polisi kwa njia ya siri mnahofia mtakuja julikana, sijakataa njia mliopendekeza, lakini Polisi watafanya kazi hii ya kiitelejinsia hapa kwa umakini na watawakamata watuhumiwa,” alisema Lugola.

Lugola pia aliwataka wananchi hao kutoa ushirikiano wa kina kwa polisi hao wakati wanafanya kazi zao, pia aliwapa angalizo polisi hao wasije wakakurupuka wakati wanafanya uchunguzi huo, wasiwaonee wananchi, wahakikishe wanakua makini ili wasije wakawasumbua ambao wananchi ambao wanafanya shughuli zao za kibiashara.

Aidha, Mjumbe wa Kijiji cha Kigongoni, Kata ya Mto wa Mbu, Tarafa ya Manyara, Wilayani humo, Devotha Steven alisema wanaiomba Serikali iongeze nguvu katika kuwalinda wanawake wa Mto wa Mbu kwani vitendo vya kikatili vimekuwa vya kusikitisha na pia wanakosa amani popote wanapofanya shughuli zao za kutafuta ridhiki.

"Mheshimiwa Waziri, ninazungumza kwa machungu, kwanini tunateseka na Serikali ipo, tunaamini mtasambaratisha haya mauaji, nasema kwa uchungu yatima wanaongezeka, tunaomba tupige kura na wanachi waitwe kutoka tarafa ya Manyara na Makuyuni ili wahusika wapatikane na tunaomba ulinzi utolewe kwa wale wananchi wanaotoa siri walindwe," alisema Devotha.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga, alifurahia ujio wa Waziri huyo, na pia alimwomba kiongozi huyo kupitia Jeshi lake, wawakamate wahalifu hao ambao wanafanya vitendo vya kikatili, ili ukatili huo uweze kukomeshwa.

Waziri Lugola yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo anatembelea Wilaya zote za Mkoa huo akifuatilia utendaji kazi wa Taasisi zake zilizopo ndani ya Wizara yake.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimsikiliza Mjumbe wa Kijiji cha Kigongoni, Kata ya Mto wa Mbu, Wilayani Monduli, Mkoani Arusha, Devotha Steven, alipokuwa anaiomba Serikali iwakamate watuhumiwa wa mauaji ya wanawake katika Kata hiyo. Lugola ametoa wiki moja, Jeshi la Polisi mkoani humo kufanya uchunguzi wa kina na kuwakamata watuhumiwa hao. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akimpa maelekezo Kaimu Kamanda wa Polisi Arusha, Longinus Tibishubwamu (kushoto), kuwakamata watuhumiwa wa mauaji ya wanawake katika Kata ya Mto wa Mbu, Wilayani Monduli, Mkoani Arusha. Wapili kushoto ni Kamanda wa Polisi Wilaya ya Monduli, Gilbert Ngaizi, na wapili kulia ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Mto wa Mbu, Peter Ngoro.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kulia), akizungumza na Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mji wa Mto wa Mbu, wakati Waziri huyo alipohudhuria Sikukuu ya Maulidi iliyofanyika mjini humo, leo. Lugola aliwataka viongozi wa dini kuhubiri amani ili wananchi waache kufanya matukio ya uhalifu katika mji huo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS IKUNGI MKOANI SINGIDA LEO

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa huduma ya maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji Mtaturu (kushoto), Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi wakifurahia mara baada ya Makamu wa Rais kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliyampiti ambapo mradi huo wa maji utawahudumia wakazi 2628.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma kibao cha zahanati ya Kijiji cha Mang’onyi mara baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkoani Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa huduma ya maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Uliyampti tayari kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628.Makamu wa Rais yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku tano ambapo atakagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua maji kama ishara ya uzinduzi wa huduma ya maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Uliyampti tayari kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Uliyampiti, Ikungi ambapo mradi huo utawanufaisha wakazi 2628.Makamu wa Rais yupo mkoani Singida kwa ziara ya kikazi ya siku tano ambapo atakagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo

ATAKAYEDOKOA FEDHA ZA SERIKALI ATAZITAPIKA-DC MBONEKO

$
0
0



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko (pichani) amewataka watendaji wa serikali kutumia fedha zinazotolewa na serikali kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuepuka tamaa vinginevyo watakao kwenda kinyume watazitapika fedha hizo.

Mboneko ametoa kauli hiyo Februari 16,2019 wakati Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga (CCM) Mhe.Azza Hilal Hamad akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa kata ya Usule kuhusu shilingi milioni 146.6 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu katika shule ya msingi Masunula iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mkuu huyo wa wilaya alisema serikali haitasita kuwachukulia hatua za kisheria watu wote watakaobanika kutumia vibaya fedha za serikali. “Msithubutu kudokoa fedha za serikali, hakuna pesa ya serikali itapotea,ukidokoa utazitapika au tutakupeleka gerezani,fedha za serikali zinapokuja zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa,mnaponunua vifaa vya ujenzi nunueni kwa bei ya jumla na siyo reja reja”,alisema Mboneko. Aidha aliwataka wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo kwani serikali pekee haiwezi kufanya kila kitu huku akisisitiza kuwa kuna maendeleo yanaletwa na serikali lakini mengine yanatokana na wananchi wenyewe.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad alisema kupatikana shilingi milioni 146.6 zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili za walimu na madarasa mawili kunatokana na jitihada kubwa aliyofanya kama mbunge kuipigania shule ya Msingi Masunula ambayo imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba.

“Shule ya Msingi Masunula kwa miaka mitatu mfululizo 2016,2017 na 2018 imekuwa ikiongoza kwa shule za serikali kiwilaya na mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya darasa la saba…baada ya kulijua hilo, mimi nilisikitika na ninasikitika sana kusikia kwamba pamoja na jitihada kubwa za walimu wanazozifanya,eti walimu hapa shuleni hawana nyumba za kuishi lakini hata vyoo tu hawana”, “Hivi hawa walimu kwa kazi kubwa wanayoifanya kwa watoto wetu sisi tumeshindwa kujenga hata vyoo?,kweli ndugu zangu,kuna kitu gani hapa,yaani kabisa tunasimama tunasema shule yetu inaongoza kimkoa kwa ufaulu,kweli tuko sawa sawa kwa hili?”,alihoji Azza.

“Niliumia sana kuambiwa hakuna nyumba ya mwalimu hata mmoja,matokeo yake walimu wengine wanakaa Didia,nikaamua kulibeba na kwenda kulisemea kwa Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alipopita Tinde,nikaiomba serikali iangalie ya msingi Masunula na kwa sababu serikali yetu ni sikivu baada ya kuomba fedha Julai 2018,serikali imetuletea fedha shilingi milioni 146.6 mwezi Januari 2019”,alisema Azza.

Mh. Azza alieleza kuwa kati ya shule zote zilizopewa fedha,Masunula ndiyo shule iliyopewa fedha nyingi kama motisha kwa sababu ya matokeo mazuri na siyo vinginevyo. “Sasa ni jukumu letu wananchi kuhakikisha kuwa fedha tulizopewa twende tukajitolee,tukafanye nguvu kazi ili tuwe na uchungu,ni jukumu letu sasa kwamba tumepewa fedha ya kujenga nyumba mbili sisi tujenge tatu,kufanya kwenu vizuri itaonesha shukrani kwa serikali”,alisema.

“Nataka tuibadilishe Masunula,tuibadilishe kata ya Usule,Masunula ifanane na yale matokeo mazuri ya mtihani wa darasa la saba yanayosomeka kule, sasa siyo matokeo mazuri halafu wazazi hamtaki kuwaunga mkono watoto wetu,kwa sababu kama watoto wapo kwenye mazingira magumu,na walimu wanafundisha kwenye mazingira magumu na mazingira ndiyo haya,tukiwaboreshea mazingira matokeo yatakuwa mazuri zaidi,si mnaweza kusikia darasa la zima limefaulu!”,aliongeza Azza.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Masunula kata ya Usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kuwahimiza watendaji wa serikali na wananchi kutumia fedha zinazotolewa na serikali kwa malengo yaliyokusudiwa. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Masunula kata ya Usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM) akiwasisitiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo badala ya kusubiri serikali iwafanyie kila kitu.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wananchi wa kata ya Usule.

Wananchi wakimsikiliza Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM).

Mwananchi akiuliza swali kwa viongozi waliofika katika kata hiyo.
Wananchi wakiwa katika eneo la mkutano.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad (CCM) akikabidhi bati moja ikiwa ni sehemu ya mabati 20 aliyotoa kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Andrew Mitumba akimshukuru mbunge Azza Hilal kwa kutoa mabati 20.
Mwenyekiti wa kijiji cha Masunula Kiyenze Majinge (kwenye nguo ya bluu) akiwaongoza Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga, Azza Hilal Hamad na viongozi mbalimbali kwenda kuona eneo ambapo patajengwa nyumba za walimu pamoja na madarasa katika shule ya msingi Masunula.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Masunula Gadius Kuyerwa ( wa nne kutoka kulia) akionesha na kuelezea kuhusu eneo ambapo patajengwa nyumba za walimu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko(wa pili kulia) na diwani wa kata ya Usule, Amina Bundala wakioneshana eneo la ujenzi wa nyumba za walimu. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

MBUNGE AZZA HILAL ATEKELEZA AHADI YA MCHANGO WA MABATI UJENZI WA VYOO SHULE ZA MASUNULA NA USULE

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad ametekeleza ahadi ya kuchangia mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule zilizopo katika kata ya Usule halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Azza amekabidhi mabati hayo yenye futi 10,Februari 16,2019 kwa viongozi wa vijiji vya Masunula na Usule ikiwa ni ahadi aliyotoa Oktoba 15,2018, alipotembelea kata ya Usule na kuelezwa kuwa shule hizo zinakabiliwa na changamoto ya upungufu wa matundu ya vyoo.

Akizungumza wakati wa zoezi kukabidhi mabati lililoshuhudiwa pia na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Jasinta Mboneko, Azza alisema mchango wake huo ni sehemu ya kuboresha shule ya Masunula ambayo kwa miaka mitatu mfululizo (2016,2017 na 2018) imekuwa ikiongoza kwa shule za serikali mkoa wa Shinyanga katika matokeo ya darasa la saba. 

“Nilipewa malalamiko ya vyoo shule ya msingi Usule na shule ya msingi Masunula,nikaahidi kuchangia mabati 20,leo nimekuja kukamilisha ahadi yangu,hivyo nakabidhi mabati 10 yenye futi 10 kwa kila shule”,alisema. 

Mheshimiwa Azza aliwataka wananchi kuacha kufanya siasa kwenye masuala ya maendeleo huku akiwahamasisha wananchi kujenga vyoo kwenye nyumba zao. Diwani wa kata ya Usule Amina Bundala alimshukuru mbunge huyo kutekeleza ahadi yake na kuongeza kuwa tayari matundu 14 ya vyoo yamejengwa katika shule ya Masunula na sasa wanaendelea na shughuli ya kuezeka majengo ya vyoo hivyo. 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kusomesha watoto wao na kuachana na tamaa za kuwaozesha huku akiwataka kutumia fedha wanazopata kutokana na kilimo kujenga nyumba za kisasa. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa kukabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Masunula, Kiyenze Majinge (CUF). Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza wakati wa kukabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi moja kati ya mabati 20 kwa viongozi wa serikali za vijiji vya Masunula na Usule kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za Usule na Masunula.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi moja kati ya mabati 20 kwa viongozi wa serikali za vijiji vya Masunula na Usule.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza wakati Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule za msingi Masunula na Usule. 
Diwani wa kata ya Usule Amina Bundala akimshukuru mbunge Azza Hilal kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwapatia mabati 20 kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya vyoo. 
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza katika eneo ambapo pamejengwa vyoo vya shule katika shule ya msingi Masunula. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akieleza jambo katika eneo la ujenzi wa vyoo kwenye shule ya msingi Masunula. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KITUO CHA UTAFITI WA ZAO LA MICHIKICHI CHA KIHINGA MKOANI KIGOMA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama mbegu ya mchikichi inayoonyesha tabaka la mafuta wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Afisa Kilimo Mwandamizi na Mratibu wa Utafiti wa Kilimo mkoani Tabora na Kigoma, Dkt. Filson Kagimbo (kulia) wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. Wapili kushoto ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama mikungu ya mchikichi iliyochavushwa kitlaam ili kupata mbegu bora wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma, Februari 17, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



KILIMO WEZESHENI WATAFITI WA MICHIKICHI-MAJALIWA


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Kilimo iwawezeshe watafiti katika kituo cha Utafiti cha zao la michikichi cha Kihinga mkoani Kigoma ili waweze kuongeza kasi ya uzalishaji wa mbegu bora za zao hilo.

Amesema Serikali imeamua kuongeza nguvu kwenye zao hilo la michikichi, hivyo Wizara ya Kilimo haina budi kukiwezesha kituo hicho kwa lengo la kuzalisha mbegu bora zitakazosambazwa kwa wakulima.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Februari 17) wakati alipotembelea kituo cha Kihinga kwa ajili ya kukagua shughuliza uzalishaji wa mbegu za michikichi akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.

Amesema Serikali imeamua kulifufua zao hilo kwa lengo la kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini, ambapo kwa mwaka inatumia zaidi ya sh. bilioni 600 kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi.“Wizara ya Kilimo iwawezeshe watu wa utafiti ili waendelee na shughuli hiyo kwa kasi, iwaongeze watumishi kituoni hapa na ongezeni nguvu kwenye zao la michikichi kama yalivyofanya Mataifa mengine ya Costa Rica na Malaysia.”

Amesema wakulima wa zao hilo wanahitaji kupata mafanikio, hivyo kituo hakina budi kuongeza nguvu ya uzalishaji wa mbegu bora. Ili wafikie malengo amewasahauri washirikiane na taasisi binafsi zinazozalisha mbegu.

Pia Waziri Mkuu amesema chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Kihinga, kiendelee kutoa elimu na Wizara ya Kilimo ijenge majengo yake inayoyahitaji kwa ajili ya kufanyia shughuli za utafiti. Eneo la chuo linaukubwa kwa hekta 920.Kwa upande wake, Mratibu wa Utafiti wa Kilimo kwa mikoa ya Tabora na Kigoma, Dkt. Filson Kagimbo amesema michikichi iliyopo sasa inauwezo wa kuzalisha tani 1.6 ya mawese kwa hekta moja ambao kidogo na hauna tija.

Amesema mbegu wanazozizalisha zinalenga kumuongeza tija mkulima kwa kuwa zitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani nne kwa hekta, pia wanaendelea kuangalia vinasaba vya mbegu vilivyopo ili wazalishe mbegu bora zaidi.

“Tutakusanya vinasaba vyote vya mbegu tulivyonavyo na kuvitathimini na kuona uwezo wake na ikibidi tutaagiza kutoka nje ya nchi ili kuboresha zaidi.” Miche ya michikichi inachukua muda wa miezi 18 kutoka hatua ya uchavushaji hadi kusambazwa kwa wakulima.

Baada ya kumaliza shughuli ya ukaguaji wa uzalishaji wa mbegu kituoni hapo, Waziri Mkuu alikagua shamba la michikichi la Gereza la Kwitanga lenye ukubwa wa ekari 400 na kupanda mche kama ishara ya uzinduzi wa upandaji wa miche bora shambani hapo.Waziri Mkuu amesema Serikali imeamua kuongeza nguvu katika zao hilo na inategemea taasisi zake mbili za Jeshi la Magereza (Kwitanga) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT-Bulombora), ambazo zinamashamba makubwa ya michikichi.

Kadhalika Waziri Mkuu ameagiza elimu kuhusu kilimo cha zao la michikichi kuanzia hatua za awali hadi uzalishaji wa mafuta itolewe mashuleni ili wanafunzi waanze kupata ulewa na ifikishwe hadi kwa wananchi.

TBS YAWAFIKIA WANANCHI 14929 KANDA YA ZIWA

$
0
0
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limemaliza Kampeni yake kanda ya Ziwa ya kutoa Elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS na jinsi gani wajasiriamali wanaweza kupata Leseni ya TBS bure bila gharama yoyote.

Kampeni hiyo ya Elimu kwa umma imefanyika katika shule za msingi na sekondari, maeneo ya Soko,Stendi,Minadani na maeneo mengine ya wazi ambako
wananchi walijitokeza kupata elimu sambamba na ufahamu wa masuala mbalimbali yahusuyo Ubora wa Bidhaa.

Kwa upande wake Afisa Masoko Mwandamizi Bi.Gladness Kaseka amezidi kuwakumbusha Wananchi wote kuwa vita ya bidhaa hafifu sio ya TBS pekee bali ya kwetu sote,Kaseka alisema kampeni hii imeweza kuwafikia wananchi 14, 929 kati yao wajasiriamali 127,wanafunzi wa Sekondari na Shule ya msingi 3868 na wananchi 10,934.

Aliongeza pia wananchi wasisite kutoa taarifa kupitia mawasiliano waliyopewa pale wanapogundua uwepo wa bidhaa hafifu katika soko lao na kuhakikisha wananunua bidhaa zilizothibitishwa na TBS.

Vilevile Shirika lilipata fursa ya kutoa semina kwa wajasiriamali wanaojihusisha na bidhaa mbalimbali kama nafaka,sabuni, maziwa,asali na unga lishe,juu ya utaratibu wa kupata leseni ya kutumia alama ya ubora ya TBS na kuwa huduma hiyo inatolewa bure kwa wajasiriamali wadogo.Kampeni hii imefanyika kwenye ngazi ya wilaya ikiwamo wilaya ya Bukoba,Kahama,Tarime na Nyamagana.

Pichani ni Mhandisi Paul Ndege kutoka TBS akitoa Elimu kwa Wafanyabiashara, wafugaji na wananchi kam walivyokutwa mnadani Tarime
Elimu juu ya Udhibiti Ubora ikiendelea kutolewa Shuleni Sirari na Mhandisi Paul Ndege wa (Afisa udhibiti Ubora TBS, Tarime.)
Sehemu ya Wajasiriamali Wa Kahama waliohudhulia semina ya Siku moja kujifunza elimu ya Udhibiti Ubora Mkoani Shinyanga.
Pichani Bwn Evarist Mrema (Kaimu Mkuu TBS Kanda ya ziwa) akitoa elimu kwa wananchi na wafanyabiashara Wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza.
Pichani ni Afisa Uhusiano wa TBS Neema Mtemvu akigawa kipeperushi kwa Mkazi wa Bukoba, Mkoani Kagera mara baada ya kuelimishwa juu ya Utambuzi wa bidhaa hafifu
Pichani ni Afisa Masoko mwandamizi wa TBS, Gladness Kaseka akikagua bidhaa kwa mjasiliamali wa vitafunwa, maeneo ya Soko Kuu Bukoba Kagera.

GEREZA LA KWITANGA NA JKT BULOMBORA KUWA VITUO VYA KUZALISHA MICHE YA ZAO LA CHIKICHI KIGOMA.

$
0
0
Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma

WAZIRI mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema serikali imechagua gereza la kwitanga na kambi ya JKT Bulombora kuwa vituo vikubwa vya uzalishaji wa miche ya zao la chikichi.

Hayo ameyasema leo kwenye kambi ya bulombora wakati akiongea na wananchi pamoja na vijana wa JKT Bulombora wakati akiwa kwenye siku ya pili ya ziara yake kikazi.

Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa gereza la kwitanga kuongeza nguvu katika uzalishaji wa zao hilo ikiwa ni sambamba na kupanua mashamba na kuongeza askari wenye ujuzi wa kilimo cha zao la mchikichi.

"Wataalamu wowote kutoka duniani kote watakaotaka kujifunza kilimo cha zao la chikichi tutawaleta hapa Bulombora JKT na gereza la kwitanga pamoja na Ilagala haya maeneo yatatumika kama shamba darasa la zao hilo"alisema Majaliwa

Majaliwa amewataka viongozi wa Mkoa wa Kigoma pamoja na Wilaya zote na halmashauri ambazo zao la chikichi linastawi vizuri kutoa elimu na kuhamasisha wananchi jinsi ya kulima zao hilo kisasa ambapo mbegu(miche)ambapo wananchi watakuwa wanapewa bure kwenye halmashauri husika.

Alisema Wizara ya kilimo wanatakiwa kusimamia maeneo yote ambayo zao la chikichi linalimwa kisasa na wananchi.

"Nimefurahishwa na jitihada zinazofanywa na Jeshi la kujenga Taifa(JKT)kambi ya hapa Bulombora kwa kuandaa eneo lenye hekta zaidi ya 480 kwaajili ya kilimo cha zao la chikichi lakini hapa malengo yetu ni kulima hekta 2000,Gereza la kwitanga napo nimekuta wanasafisha shamba la hekta 450 na wao wanatakiwa kulima hekta zaidi ya 2000,tulime maeneo tunayo yakutosha"Alisema Waziri Mkuu.

Waziri mkuu amewataka wakulima wakubwa makampuni na taasisi binafsi kuja kuwekeza kigoma kwenye zao la chikichi kwenye vitalu vya mbegu bora,pia watapata maeneo ya kulima ili wawekeze kwenye kilimo chenyewe.

"Kwakweli tukifikia hatua hiyo nchi yetu ya Tanzania hatutakuwa na shida ya kuagiza mafuta ghafi toka nje ya nchi na dola zitabaki ndani"alisema Majaliwa.

Naibu waziri wa Kilimo Mgumba naye alisema tayari Wizara imeshatenga kwenye bajeti shilingi bilioni 10 kwaajili ya uendelezaji wa zao hilo,ambapo kwenye bunge lijalo.

"Mhe.Waziri Mkuu lakini hatuwezi kusubiria hadi hizo bilioni 10 hadi zipitishwe mwezi wa saba tumeanza kujibana matumizi yetu katika bajeti iliyopita ya mwaka jana,ili tuweze kutekeleza azma ya serekali ya kuendeleza zao la mchikichi nchini na kumaliza tatizo la mafuta"alisema Naibu waziri wa Kilimo

Alisema mpaka sasa wameshapeleka watumishi wawili waliobobea katika utafiti wa zao hilo katika kituo cha utafiti cha Kihinga na ndani ya wiki hii watakuja watafiti wengine 10 kutoka vyuo mbalimbali vya utafiti wa zao mchikichi na kwenda Kihinga.

Mbunge wa Jimbo la Kigoma kaskazini Peter Serukamba alimwambia Waziri Mkuu changamoto inayowakabili wakulima wa zao hilo ni upatikanaji wa mbegu bora,hivyo aliiomba serikali wakulima wapate mbegu bora na za kisasa pi matumizi hafifu ya teknolojia ya kilimo hicho.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipanda mche wa zao la chikichi katika shamba la JKT Bulombora ikiwa ni uhamasisha wa kulima zao hilo na kulifanya zao la kimkakati.
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia mstaafu Emanuel Maganga akipanda mche wa zao la chikichi kwenye shamba la JKT Bulombora katika kuhamasisha kulima zao hilo
 Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akizindua matreka mawili katika gereza la kwitanga ambayo yatatumika katika  shamba la Kwitanga kuendeleza za la chikichi
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama mikungu ya zao la chikichi iliyochavushwa kitaalam ili kupata mbegu bora wakati alipotembelea kituo cha utafiti wa michikicho cha Kihinga Kilichopo Wilayani Kigoma
 

WAZIRI MKUCHIKA ARIDHISHWA NA MAFANIKIO YA WALENGWA WA TASAF WILAYANI LIWALE.

$
0
0







Na Estom Sanga-Liwale

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,Mheshimiwa George Mkuchika amesema Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF- ni mojawapo ya vielelezo vya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015 inayoelekeza serikali na Wananchi kukabiliana na umaskini.

Waziri Mkuchika ameyasema hayo akiwa katika wilaya ya Liwale Mkoani Lindi ambako pamoja na mambo mengine anakutana na Walengwa wa TASAF ili kujionea namna Walengwa hao wanavyotumia fursa zilizoko kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini kujiletea maendeleo na kupunguza athari za umaskini miongoni mwao.

“kote nchini ninakofanya ziara kukagua shughuli za TASAF ninashuhudia mabadiliko makubwa katika maisha ya Walengwa jambo ambalo ni zuri na linapaswa kuendelezwa” amesisitiza Mhe. Mkuchika.

Aidha Waziri huyo ametaka Wataalam wa sekta mbalimbali nchini kote kuwa karibu zaidi na Wananchi na hususani Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini ili waweze kuboresha zaidi maisha yao na kunufaika na jitihada za serikali.

Akiwa katika kijiji cha Mbonde Katika wilaya ya Liwale Waziri Mkuchicha alitembelea baadhi ya kaya za Walengwa na kujionea namna wanavyotumia ruzuku itolewayo na TASAF katika kuboresha makazi kwa kununua mabati na kuezeka nyumba zao huku wengine wakianzisha shughuli za uzalishaji mali kama ufugaji wa kuku,bata, na kukuza shughuli za kilimo na hivyo kujiongezea kipato.

Kuhusu sekta ya afya,Waziri Mkuchika amekagua jengo la zahanati lililojengwa na TASAF kwa kushirikiana na Wananchi katika kijiji cha Mbonde zahanati ambayo imewaondolea wakazi takribani 400 adha ya kufuata huduma za matibabu mbali ya kijiji chao.Amewaasa Wananchi hao kulitunza jengo hilo ili waendelee kunufaika nalo.

Mapema Waziri Mkuchika akizungumza na Watumishi wa Umma waliopo katika Wilaya ya Liwale,aliwataka watekeleze majukumu yao kwa kuzingatia msingi ya uadilifu na kujituma ili kuondoa kero za wananchi huku akionya kuwa kamwe serikali haitawavumilia Watumishi wanaokiuka misingi ya utawala bora kwa namna yoyote ile. 


Waziri Mkuchika akipata maelezo ya namna jengo la zahanati lililojengwa na TASAF katika kijiji cha Mbonde, Wilayani Liwale mkoani Lindi linavyowanufaisha wananchi wa eneo hilo na vijiji vya jirani.
Waziri Mkuchika (mwenye shati jeupe)akiwa katika nyumba ya mmoja wa Walengwa (kulia kwake)katika kijiji cha Mbonde ,nyumba ambayo imezekwa kwa mabati baada ya kupata ruzuku kutoa TASAF.
Waziri Mkuchika akizungumza na Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaotekelezwa na Serikali kupitia TASAF katika kijiji cha Mbonde (picha ya chini).

Uzinduzi wa kampeni ya naweza na vodacom

$
0
0
 Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Bi. Harriet Lwakatare akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya 'NAWEZA NA VODACOM' inayowaelimisha wateja wake njia mbali mbali za kidijitali za kujihudumia na kutatua matatizo kwa haraka leo makao makuu ya kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi. Rosalynn Mworia.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania, Bi. Harriet Lwakatare akizungumza na wanahabari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya 'NAWEZA NA VODACOM' inayoelimisha wateja njia mbali mbali za kidijitali za kujihudumia na kutatua matatizo kwa haraka iliyofanyika leo makao makuu ya kampuni hiyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bi. Rosalynn Mworia na Mkuu wa Idara ya ufanisi kwa Wateja, Bi. Najenjwa Mbagga. 

SERIKALI YAZUIA SH. BILIONI 5.5 ZA UJENZI WA MRADI WA SOKO LA KISASA LA MAGOMENI DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (katikati) akisikiliza maelezo ya Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Justin Lukaza, kuhusu ramani ya Mradi wa Kimkakati wa Soko la Magomeni Jijini Dar es Salaam lenye ghorofa tatu ambalo limepewa kiasi cha Sh. bilioni 3.5, huku utekelezaji wa mradi huo ukiwa unasuasua.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (kushoto) akitoa maelekezo ya Serikali ya kuzuia Sh. bilioni 5.5 zilizosalia kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Kimkakati wa Soko la Magomeni Jijini Dar es Salaam kwa kuwa tangu fedha hizo zilipotolewa Mei, 2018 utekelezaji wake hauridhishi. Kulia ni Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Jastin Lukaza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) (wa pili kushoto), akionesha kushangazwa na kitendo cha Mkandarasi wa Mradi wa Kimkakati wa Soko la Magomeni Jijini Dar es Salaam kutokuwepo eneo la mradi. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Daniel Chongolo, wa pili kulia ni Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni Bw. Jastin Lukaza na watatu kulia ni Mwakilishi wa Mkandarasi wa mradi Bw. Sospeter Leonidas kutoka Kampuni ya GSI.
Mwenyekiti wa Soko la Magomeni Yusuph Waziri, akifafanua jambo mbele ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipotembelea na kukagua ujenzi wa mradi wa Soko la Kisasa la Magomeni, Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam



Na Peter Haule, WFM, Dar es Salaam


Serikali imezuia Sh. bilioni 5.5 ambazo zilipaswa kutumika kutekeleza mradi wa Kimkakati wa Soko la Magomeni, liliko wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es Salaam kutokana na kucheleweshwa kwa utekelezaji wa mradi huo licha ya kupewa fedha za kutosha kwa awamu ya kwanza.

Hatua hiyo imechukuliwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi huo unaotarajia kugharimu shilingi bilioni 9 na kukuta ujenzi wake unasuasua.

Dkt Kijaji alisema kuwa Serikali, imeipatia Manispaa ya Kinondoni shilingi bilioni 3.5 tangu mwezi Mei, 2018 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo ambao ungepaswa ukamilike ndani ya miezi tisa tangu kusainiwa kwa mkataba wa ruzuku hiyo lakini ameshangaa kutomkuta mkandarasi kwenye eneo la ujenzi.

“Serikali inasitisha kutoa kiasi cha Sh. bilioni 5.5 mpaka watakapo dhihirisha wako tayari kuwahudumia wananchi na kutekeleza dhamira njema ya Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ya kuwahudumia wananchi wake”, alieleza Dkt. Kijaji.

“Jana Manispaa ya Ilala wametuangusha kwenye usimamizi wa mradi wa Machinjio ya kisasa ya Vingunguti tumerejesha shilingi bilioni 3 Hazina na leo Manispaa ya Kinondoni nao wametuangusha na tunalazimika kuzizuia fedha hizo sh. bilioni 5.5 mpaka tujiridhishe na maendeleo ya ujenzi” alisisitiza Dkt. Kijaji

Awali, akitoa maelezo ya mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni, Mhandisi wa Manispaa hiyo Justin Lukaza, ameeleza kuwa Manispaa hiyo imeingia mkataba wa kujenga soko hilo litakalo kuwa na ghorofa tatu na Kampuni ya Group Six International na kwamba ujenzi ungekamilika katika kipindi cha miezi sita ijayo na kutofautiana maelezo na mwakilishi wa Mkandarasi ambaye alimweleza Dkt. Kijaji kuwa ujenzi huo ungechukua muda wa miezi 12.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Daniel Chongolo, amekiri kuwa kuna uzembe umefanywa na watendaji wa Manispaa ya Kinondoni uliosababisha mradi huo kuchelewa kuanza na kumwomba Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji ampe muda mfupi wa kurekebisha kasoro hizo.

Alisema kuwa tayari kuna hatua mbalimbali zilichukuliwa kwa maafisa waliofanya uzembe katika utekelezaji wa mradi hapo awali na hakujua kama bado kulikuwa na uzembe uliokuwa unaendelea baada ya kuchukua hatua hizo kwa sababu aliamini watendaji waliokabidhiwa kusimamia ujenzi wa mradi huo walijifunza kutokana na makosa ya wenzao walioondolewa kusimamia mradi huo

“Mimi nakubaliana na wewe (Naibu Waziri wa Fedha) kwamba kuna uzembe na kazi yetu sisi ni kuhakikisha tunarekebisha haya makosa na nichukue dhamana na tutawajika na watu hawa na nitalazimika kutumia dhana ya punda mwenye mzigo na mwenye punda anaye mchapa bakora ili punda aende” alisisitiza Bw. Chongolo

Baadhi ya wakazi wa Kinondoni, wameipongeza Serikali kwa ufuatiliaji wa miradi ya wananchi na kusikiliza kero zao wakitolea mfano wa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, na kwamba hatua hiyo inaleta uwajibikaji wa watendaji ambao walijenga mazoea ya kuzembea kwa makusudi kusimamia miradi ya wananchi na kuahidi kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuliletea Taifa maendeleo

Mradi wa Soko la Kisasa la Magomeni ni miongoni mwa miradi 22 iliyopewa ruzuku na Serikali katika Mpango wa Awamu ya Kwanza wa kuziwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kujitegemea kimapato ambapo zaidi ya shilingi bilioni 147 zilitolewa na Wizara ya Fedha na Mipango kwa ajili ya kutekeleza miradi hiyo.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA AFISA MWENDESHAJI MKUU WA KAMPUNI YA BARRICK GOLD CORPORATION (AFRICA NA MASHARIKI YA KATI) IKULU

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Bw. Willem Jacobs alipokutana naye kwa   mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 20, 2019.
 : Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga wakiwa katika   mazungumzo na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Bw. Willem Jacobs na ujumbe wake walipokutana Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Bw. Willem Jacobs baada ya  kukutana na kufanya naye mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 20, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Sheria na Katiba Profesa Palamagamba Kabudi na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Profesa Florens Luoga katika picha ya pamoja  na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ( kwa Afrika na Mashariki ya Kati) Bw. Willem Jacobs na ujumbe wake baada ya kukutana na kufanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo Februari 20, 2019.
PICHA NA IKULU

Dodoma Kupambana na Vifo vya Akina Mama na Watoto Wachanga

$
0
0
Na Adelina Johnbosco, MAELEZO- Dodoma 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge amezindua rasmi kampeni ya ‘JIONGEZE! TUWAVUSHE SALAMA’ jijini Dodoma, kampeni ambayo imelenga kumsaidia mama mjamzito kujifungua salama.Katika hotuba yake Mhe.Mahenge, amewataka viongozi wote kuwa washiriki na watendaji wa kampeni hii, ili kuhakikisha mama anakuwa salama kwa kutoa elimu ya uzazi popote kwa wananchi. 

Aidha, amesema lengo la tamko hili ni kuongeza kasi ya uwajibikaji katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga nchi nzima. 

‘’Tumeamua kuchukua kuchukua hatua hii muhimu kwa sababu, kifo cha mama mjamzito au anayejifungua au aliyejifungua na kifo cha mtoto mchanga aliyezaliwa havikubaliki,’’ alisema Dkt. Mahenge. 

Hata hivyo, amezitaja sababu kuu zinazosababisha vifo hivi kwa kina mama kuwa ni pamoja na kutokwa na damu nyingi kabla na baada ya kujifungua, kifafa cha mimba, kuchanika kizazi, upungufu mkubwa wa damu, kondo la nyuma kushindwa kutoka, matatizo yatokanayo na ugonjwa wa UKIMWI, uchungu pingamizi, matumizi ya dawa za miti shamba zinazoaminika kuongeza uchungu wa kujifungua na matatizo yatokanayo na kuharibika kwa mimba kwa njia yoyote ile. 

Dkt. Mahenge amesema kuwa sababu za vifo vya watoto wachanga ni pamoja na kushindwa kupumua kwa mtoto akiwa tumboni na mara baada ya mama kujifungua, matatizo yatokanayo na kuzaliwa njiti na matatizo ya ulemavu wa kuzaliwa nao (Congenital abnormalities). 

Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa takwimu zinaonesha kuwa Tanzania kwa mwaka 2017, vifo vya wanawake wajawazito 556 kwa kila vizazi hai 100,000 vilitokea, na lengo la Serikali ni kupunguza vifo hivi hadi kufikia 292 kwa vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2020. 

Ameongeza kuwa kwa mwaka 2017, vifo vya watoto wachanga ni 25 kwa kila vizazi hai 1,000 na lengo ni kupunguza hadi kufikia vifo 16 kwa kila vizazi hai 1,000 ifikapo mwaka 2020. 

“Kwa Mkoa wetu wa Dodoma, takwimu za miaka mitano mfululizo zinaonesha bado tunayo kazi kubwa ya kufanya ili kukabiliana na matatizo yanayojitokeza wakati wa ujauzito, kujifungua na baada ya kujifungua hasa unapoangalia namba halisi ya kinamama na watoto wanaofariki. Jumla ya wajawazito 309 walifariki, ambao ni sawa na mabasi 5 ya abairia 62 au waumini wa kanisa/msikiti mzima,’’ amebainisha Dkt. Mahenge 

Katika kuhakikisha huduma inaimarika, amesema tayari serikali imejenga na kukarabati kwa awamu miundombinu ya afya katika jumla ya vituo vya afya 22, kufadhili ujenzi wa hospitali tatu za wilaya katika Halmashauri ya Chemba, Chamwino na Bahi ambazo hazikuwa na Hospitali za Wilaya. 

Pia Serikali imeongeza bajeti ya dawa ambapo katika mkoa wa Dodoma bajeti ya dawa imeongezeka kutoka shilingi milioni 900 mwaka 2015/16 hadi shilingi bilioni 4.3 mwaka 2018/19. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mhe. Mwanahamis Mkunda, amesema amepokea kwa furaha kampeni hii na yuko tayari kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wananchi katika kuhakikisha elimu inamfikia kila mmoja ili tahadhari ichukuliwe kwa kipindi cha ujauzito. 

Naye, Mganga Mkuu wa Mkoa Dodoma, Dk. James Charles Kiologwe amesisitiza akina baba kuwa na ushirikiano na wake zao kipindi cha ujauzito, ikiwemo kuhudhuria kliniki, na kuwa waangalizi wao muda wote ili kuwasaidia inapotokea hali ya tofauti kiafya. 

Vile vile, ametoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Dodoma kutoa ushirikiano wa kuyachunguza magari ya kubebea wagonjwa na kuhakikisha yanafanya kazi inayopaswa, hii itasaidia wagonjwa ikiwemo kina mama kufikishwa hospitalini mapema. 

Dkt. Kiologwe amewataka wataalamu wa afya kufanya uchunguzi yakinifu ili kubaini mapema dalili zozote za hatari na kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za chanjo, ubora wa matibabu ya utotoni, ushauri kuhusu lishe bora, ikiwemo kutoa lugha nzuri kwa akinamama. 

Huu ni mwendelezo wa mapambano dhidi vifo vinavyotokea kwa akina mama wakati na baada ya kujifungua, pamoja na watoto wao, kwani serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na wadau wa Afya ya Uzazi na Mtoto, ilizindua kampeni hii mnamo tarehe 06 Novemba, 2018 hapa Jijini Dodoma, ikiwa ni pamoja na Wakuu wa Mikoa kusaini tamko la ahadi mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan. 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge

Usajili na Utambuzi wa Wanchi ni Bure

$
0
0

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) inapenda kuwakumbusha wananchi wote kuwa Huduma ya Usajili na Utambuzi wa Watu kwa ajili ya kupatiwa Kitam- bulisho cha Taifa inatolewa BURE. Mwananchi anatakiwa kufika katika ofisi za NIDA akiwa na nakala (Photocopies) za viambatisho vyake muhimu.

Waombaji wote wa Vitambulisho vya Taifa mnakumbushwa kuwa “Rushwa ni Adui wa Haki. Usikubali kudai, kutoa wala kupokea Rushwa.” Kitambulisho cha Taifa ni haki yako ya msingi na hakiuzwi.

Hakikisha unahudumiwa katika Ofisi au Vituo rasmi vya Usajili vya NIDA na Afisa wa NIDA na sio Vishoka wanaojipenyeza kwenye zoezi.

Ukiombwa Rushwa Toa Taarifa kwa Mawasiliano :-

Simu: 0800758888 au 0673 333 444 au 0759102010 au 0765201020, Barua: S.L.P 12324 Dar es Salaam, Barua pepe (email): nida.tanzania@nida.go.tz. Tembelea tovuti yetu: www.nida.go.tz, Facebook nidatanzania, twitter @nidaTanzania au twitter.com/nidatanzania

Imetolewa na:- Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

WAZIRI KAIRUKI AITAKA TIC KUIMARISHA HUDUMA ZA MAHALA PAMOJA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angella Kairuki akipata ufafanuzi kuhusu huduma za mahala pamoja kwa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa wawekezaji Bi Anna Lyimo, Waziri Kairuki alifanya ziara kwenye ofizi za TIC leo February 20, 2019
Mkurugenzi Mtendahi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Geoffrey Mwambe akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angela Kairuki alipotembelea kwenye ofisi hizo leo February 20, 2019
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angella Kairuki akitoa ufafanuzi wa jambo alipotembelea kwenye ofisi za kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Mapema February 20, 2019 ili kujionea baadhi ya kazi zinazofanywa na kituo hicho sehemu ya huduma za mahala pamoja
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Angella Kairuki akipata ufafanuzi kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Geoffrey Mwambe kuhusu huduma za mahala pamoja


Na Grace Semfuko-MAELEZO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji ) Angela Kairuki amekitaka Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC kupitia mfumo wa huduma za mfumo wa mahala pamoja kuboresha utoaji wa huduma kwa wawekezaji kupitia mfumo wa kielektroniki na kuwaagiza kuunganisha mfumo wa dirisha la uchakataji miradi (TIW) kwenye Kanda zote saba za kituo hicho Nchini ili kurahisisha mwenendo wa upatikanaji wa huduma kwa wawekezaji.

Kairuki alisema mfumo huo unasaidia kuondokana na urasimu,ucheleweshwaji na unarahisisha upatikanaji wa leseni,cheti na vibali ambao utasaidia kuongeza wawekezaji nchini ambapo kati ya kanda saba za TIC ni kanda moja tu ya Kaskazini ndio iliyoingizwa kwenye mfumo na kuagizwa kanda zingine ziharakishe mfumo huo ndani ya mwezi mmoja.

Waziri Kairuki aliyasema hayo February 20, 2019, baada ya kuzungumza na maafisa wanaotoa huduma ndani ya mfumo wa mahala pamoja na kufanya nao majadiliano juu ya namna ya kuboresha huduma hizo ambazo zinatolewa na taasisi 11 ndani ya jengo la TIC.

“Mfumo wa huduma za mahala pamoja ni mzuri sana, lakini tuhahitaji kuyafanyia kazi masuala kadhaa kwenye kila taasisi 11 zilizopo kwenye huduma za mahala pamoja ili kuondokana na changamoto ambazo zinachelewesha upatikanaji wa huduma za uwekezaji” alisema Kairuki.

Aidha aliwataka watendaji wa ardhi ndani ya kituo hicho kuweka vizuri takwimu za ardhi ya uwekezaji na kushughulikia changamoto za upatikanaji wa ardhi kwa wawekezaji ambao unasimamiwa na TIC.

Akiwa katika sehemu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Waziri Kairuki aliagiza watendaji hao kuuona umuhimu wa utoaji wa cheti cha utambulisho wa namba ya mlipakodi TIN kwenye Kituo hicho ili kurahisisha huduma kwa wawekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania TIC Bw. Geoffrey Mwambe alisema iwapo Serikali itawezesha taasisi zote zinazohusika na huduma za mahala pamoja kutoa huduma zake stahiki zinazohusu uwekezaji ndani ya ofisi za TIC itakuwa ni hatua kubwa katika uwekezaji.

“Taasisi zilizopo ndani ya mfumo wa mahala pamoja zinafanya kazi kubwa, tunachoomba sisi kama TIC ni kwamba huduma za taasisi hizo kwa wawekezaji zikamilike ndani ya TIC badala ya kwenda kwenye makao makuu ya ofisi hizo kufuata idhini ya vibali,leseni na vyeti husika kwa wawekezaji” alisema Mwambe.

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya huduma kwa wawekezaji Anna Lyimo alisema kwa sasa huduma za mahala pamoja zimekuwa na manufaa makubwa kwa wawekezaji kutokana na kuwapo kwa taasisi zote muhimu Kituoni na kwamba marekebisho yaliyotajwa na Waziri yatafanyiwa kazi mapema iwezekanavyo.

“Tumeyapokea maagizo ya Waziri na tutayafanyia kazi, ni maagizo yenye tija kwa kituo” alisema Kaimu Mkurugenzi Idara ya Huduma za Mahala Pamaoja wa TIC Anna Lyimo.

Huduma za mahala pamoja kwenye kituo cha uwekezaji Tanzania TIC zinajumuisha taasisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Baraza la Taifa la usimamizi na uhifadhi wa Mazingira (NEMC), Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (BRELA), Shirika la viwango Tanzania (TBS), Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na wenye ulemavu, Wizara ya Ardhi, Idara ya Uhamiaji,Wakala wa Usalama na Afya mahala pa kazi (OSHA), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA na Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA),

Makamu wa Rais afanya ziara wilayani Iramba mkoani Singida

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo na leo amefanya ziara katika wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Katika Wilaya ya Iramba Makamu wa Rais alitembelea kiwanda cha muwekezaji mzawa cha kusindika alizeti cha Yaza klichopo Ndago, pia alitembelea kituo cha afya cha Kinampanda na kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho pamoja na maboresho na ukarabati uliofanywa kwenye chuo cha Ualimu Kinampanda.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndago, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapongeza wananchi wa tarafa ya Ndago kwa kuwa mstari wa mbele katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.
“Serikali inakuja na mpango ama sheria ya Bima ya Afya ambapo kila mmoja atatakiwa kuwa na bima ya afya” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amewakumbusha wakazi wa Iramba kukumbushana juu ya ugonjwa wa ukimwi kwani kasi ya maambukizi yameongezeka hivyo kila mtu ajichunge mwenyewe na wazazi wachunge watoto kwani maambukizo yanaanzia vijana wenye miaka 15 mpaka 24.

Kuhusu uwezeshaji vijana, wanawake na walemavu, Makamu wa Rais amezitaka Halmashauri kutenga asilimia 10% kama matakwa ya kisheria yanavyosema.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais amewataka wananchi kuchagua viongozi wa serikali za mitaa na vitongoji wenye sifa.

“Sio tu kuhakikisha vitongoji na mitaa yote imerudi CCM ila kuchagua viongozi ambao wataendana na ajenda  ya maendeleo ya Serikali ya awamu ya tano”

Kwa upande mwingine naibu Waziri Ujenzi Mhe. Elias Kuandikwa amewataka wanafunzi wa kijiji cha Ndago kuweka mkazo katika masomo ya Sayansi kwani nchi yetu inaelekea kwenye uchumi wa kati ambapo viwanda vitakuwa vingi na vitahitaji wataalamu kwa wingi.
Wakati huohuo Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko amesema kuwa hiki ni kipindi pekee cha Watanzania kufaidika na madini yao haswa baada ya kufanyika madadiliko mbali mbali.

“leseni 40 zisizofanya kazi hapa na kupewa wachimbaji wadogo wadogo “.Alisema Waziri wa Madini. Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Iramba Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa niaba ya wananchi wa jimbo lake ambapo Serikali imetoa shilingi milioni 400 katika tarafa ya ndago kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya pamoja na gari ya wagonjwa.

Aidha Mbunge huyo amesema katika tarafa ya Ndago vijiji vinne ndani ya tarafa hiyo vimepata maji na wamejenga mabweni katika kila kata. 

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha kusindika alizeti cha Yaza katika kijiji cha Ndago, wilayani Iramba mkoa wa Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mhe. Mwigulu Nchemba (kushoto) mara baada ya kutembelea kiwanda cha kusindika alizeti cha Yaza katika kijiji cha Ndago, wilayani Iramba mkoa wa Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kutembelea kiwanda cha kusindika alizeti cha Yaza katika kijiji cha Ndago, wilayani Iramba mkoa wa Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Bw. Maulid Njau (kushoto) juu ya maboresho na ukarabati wa chuo cha ualimu Kinampanda, wilayani Iramba mkoa wa Singida. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live


Latest Images