Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

DKT. MWANJELWA AWAPA WIKI MOJA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA MKINGA

$
0
0
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wilayani Mkinga, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 
Baadhi ya watumishi wa umma wilayani Mkinga wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akiteta jambo na Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said, kabla ya kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla ya kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 
Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said (kushoto) akimkaribisha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji, kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 
Afisa Utumishi Mwandamizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Baraka N. Nangosongo akitoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi kwa watumishi wa umma wilayani Mkinga wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 



Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said kuhakikisha watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga wanaoishi nje ya vituo vya kazi kuhamia wilayani Mkinga ndani ya siku saba ili kutoa huduma bora kwa wananchi na kwa wakati. 

Agizo hilo amelitoa wilayani Mkinga wakati wa kikao kazi na watumishi wa halmashauri hiyo, alipowatembelea kuhimiza uwajibikaji kabla ya kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wilayani humo kwa lengo la kukagua na kujiridhisha kuhusu utekelezaji wa miradi ya TASAF wilayani humo. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema, watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga wanaoishi nje ya vituo vya kazi na kutumia rasilimali za serikali, ni dhahiri kuwa wanatumia vibaya rasilimali za umma hivyo wanafanya kosa kwa mujibu wa Kanuni, Sheria na Taratibu za Utumishi wa Umma. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesisitiza kuwa, ni marufuku kwa mtumishi wa umma yeyote nchini kuishi nje ya kituo cha kazi, kwani kitendo hicho kinawanyima haki ya msingi wananchi wanaohitaji huduma katika Taasisi za Umma kutokana na watumishi wengi kuchelewa kufika kazini kwasababu ya kuishi nje ya vituo vyao vya kazi. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amehoji uwepo wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga na wakuu wake wa Idara kushindwa kushughulikia tatizo hilo la watumishi kuishi nje ya vituo vya kazi, na kumtaka Mkurugenzi huyo kuhakikisha anashirikiana na menejimenti yake kushughulikia suala hilo kwa wakati na kuongeza kuwa, iwapo tatizo hilo litaendelea kuwepo wilayani humo, itakuwa ni ishara tosha kwamba, wamedhihirisha kutokuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yao. 

Mhe. Dkt. Mwanjelwa amewataka watumishi wa umma wilayani humo kuzingatia nidhamu ya kazi na kutochezea fursa waliyonayo ya kuutumikia umma na kuongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuwa na utumishi wa umma wenye viwango na unaomjali mwananchi pindi anapofuata huduma katika taasisi za umma. 

Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Tanga na Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kushughulikia ubadhirifu wa fedha uliopo katika Kituo cha Afya cha Kiwegu na kutaka apatiwe mrejesho mapema iwezekanavyo. 

Kwa upande wake, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Bi. Zena Said amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga na Maafisa Utumishi kuhakikisha ifikapo Februari 21 mwaka huu, watumishi wote wanaoishi nje ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga wawe wameshahamia wilayani Mkinga. 

Bi. Said amemshukuru Dkt. Mwanjelwa kwa kuwahimiza watumishi wilayani Mkinga kuvaa mavazi yenye staha na kumtaka kila mtumishi wa umma wilayani humo kuzingatia Waraka wa Mavazi Na. 3 wa Mwaka 2007. 

Kuhusiana na ubadhirifu wa fedha katika Kituo cha Afya cha Kiwegu, Bi. Said amemuahidi Dkt. Mwanjelwa kutekeleza maelekezo aliyoyatoa kwa wakati kwa kufanya ufuatiliaji ili kutatua tatizo hilo. 

Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) anaendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Tanga yenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi kwa umma, ikiwa ni pamoja na kukagua na kujiridhisha na utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na TASAF mkoani humo. Mpaka sasa ameshatembelea Halmashauri ya Mji wa Tanga, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza na Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga.

Mshindi wa Milioni 188.5 za M-BET kuichangia Yanga

$
0
0
Mkazi wa Njombe, Frank Kayombo (24) ameshinda Sh.188,484,550 kwa kubashiri kiusahihi Mchezo wa Perfect 12 unaondeshwa na kampuni ya M-Bet. Kayombo ambaye  shabiki wa timu za Yanga na Manchester United ya Uingereza  amekuwa mshindi wa kwanza wa droo ya M-BET kwa mwaka huu, Meneja Masoko wa Kampuni ya M-BET Tanzania, Allen Mushi alisema kuwa  M-Bet inaendelea kuwa nyumba ya mabingwa kwa kubadilisha maisha mbalimbali ya watanzania.

Mushi alisema kuwa serikali imejipatia Sh38 millioni ikiwa ni kodi ya ushindi asilimia 20 na  kuchangia pato la taifa. Alisema kuwa droo yao ya Perfect 12 inazidi kutoa washindi na kuchangia maisha kwa Watanzania ambao wamekuwa wakijishindia mamilioni ya fedha kila wakati.

“Huu ni mwanzo wa mwaka na tayari M-BET imetoa mshindi wa mamilioni ya fedha ambaye ataweza kujiendeleza kimaisha  na vile vile kuchangia taifa lake. M-Bet tunajivunia kuwa kampuni pekee ambayo mpaka sasa imewafaidisha watu wengi kupitia michezo yake, naomba Watanzania kuendelea kubashiri na kampuni michezo yetu kwa njia ya mitandao, simu ya mkononi na mengineyo,” alisema Mushi.

Kwa upande wake, Kayombo alisema kuwa alitumia Sh 1,000 na kubahatika kushinda droo hiyo ya kwanza ambapo atatumia fedha hizo kwa ajili ya kujiendeleza, kufungua miradi na vile vile kununua nyumba. Kayombo ambaye ni mfanyabiashara ya miamala ya fedha kwa njia ya simu, alisema kuwa ndoto yake kubwa ni kupata maendeleo makubwa katika biashara zake na kuweza kuisaidia familia yake.

“Nina furaha sana kupata kiasi hiki cha fedha ambacho kwa kweli ni kikubwa ukilinganisha na kiasi nilichotumia kubashiri, Naona mwanga wa maisha yangu na familia kwa ujumla. Naishukuru M-BET kwa kuonyesha uaminifu kwangu na kwa washindi wengine,” alisema Kayombo.

Mshindi huyo pia alisema atatumia kiasi cha fedha alizoshinda kuichangia timu yake ya Yanga kupitia namba maalum iliyotangazwa kwenye vyombo vya habari. “Naipenda Yanga na kiasi ambacho nitawapa timu yangu kinabakia kuwa siri,” alisema. Kaimu Msimamizi wa Kitengo cha Michezo ya Kubahatisha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Philipo Haule aliipongeza M-BET kwa kuendelea kuchangia pato la Taifa.
Mshindi wa droo ya kwanza  ya mwaka huu ya Perfect 12 ya kampuni ya M-BET Frank Kayombo (wa pili kushoto) kutoka mkoa wa Njombe  akipokea mfano wa hundi ya Sh milioni 188.5 kutoka kwa meneja Masoko wa M-BET, Allen Mushi (wa pili kulia). Wengine katika picha ni Afisa wa Michezo ya Bodi ya Kubahatisha Catherine Lamwai (wa kwanza kulia) na Philipo Haule afisa kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

SEKTA YA AFYA ISIWE KIKWAZO KWA WANANCHI KUPATA MATANGAZO YAO MAPEMA.

$
0
0
Na WAMJW - DSM

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameagiza Sekta ya Afya kutokuwa kikwazo kwa wananchi kupata Matangazo ya kuzaliwa kwa watoto kwa ajili ya kupata cheti cha kuzaliwa kwa muda mfupi.

Ameyasema hayo leo, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala jijini Dar ea salaam.

Dkt. Ndugulile amesema kuwa Hospitali hiyo ni lazima ichukue juhudi za makusudi, ikiwemo kuongeza wafanya kazi ili kuhakikisha kwamba Watoto wote wanaweza kupata matangazo yao ndani ya Wiki moja, jambo litaloepusha usumbufu kwa Mwananchi ambao unaweza kuepukika.

" Sisi kama sekta ya Afya, tusiwe kikwazo, vya Mwananchi kupata haya matangazo, na hili nimeliona nimeshatoa maelekezo juu ya hili, na ndani ya wiki moja nategemea kwamba tatizo hili litakuwa limetatuliwa" Alisema Dkt. Ndugulile

Dkt. Ndugulile akiongeza kuwa Matangazo haya ni ya muhinu sana katika mchakato wa kupata vyeti vya kuzaliwa, hivyo Mganga Mfawidhi ni lazima aweke mikakati thabiti ikiwemo kuongeza watu ili kuhakikisha kuanzia sasa matangazo yawe yanatoka ndani ya masaa 24. 

Kwa upande mwingine Dkt. Ndugulile amesema kuwa katika kupambana na changamoto ya msongamano wa watu katika Hospitali hiyo, Serikali imeboresha zaidi ya vituo vya Afya 350, huku zikijengwa Hospitali za Wilaya 67, na Hospitali za mikoa 2, ili wananchi waweze kupata huduma katika ngazi ya chini kabla yakufikia katika Hospitali za Rufaa.

"Kama Serikali tunachofanya ni kuboresha vituo vya Afya karibia 350, tunajenga Hospitali za Wilaya 67, na Hospitali za Rufaa za Mikoa 2, hivyo tunatarajia hizi Hospitali zinkianza kufanya kazi na huduma za upasuaji zikianza kupatikana kule, huu msongamano utaamia kule" alisema Dkt. Ndugulile

Mbali na hayo Dkt. Ndugulile amewapongeza watu wote wenye VVU kujitokeza kupata matibabu, huku lengo la Serikali ni kufikia 909090, yaani 90 watu wote walio na Virusi vya Ukimwi waweze kufikiwa na kupimwa, 90 ya pili ni kuhakikisha waliopimwa waweze kuanzishiwa dawa papo kwa papo, na 90 ya tatu ya walioanzishiwa dawa waweze kufubaza virusi vyao vya Ukimwi, yote ni kuhakikisha ifikapo 2030 pasiwe na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.

Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dkt. Mkungu Daniel mesema kuwa Hospitali hiyo inapokea Mwananchi zaidi ya 2000, huku akisisitiza kuwa Hospitali hiyo ipo katika hatua yakujenga jengo ambalo litabeba jumla ya vitanda 150 kwaajili ya mama na mtoto ili kupambana na changamoto hiyo ya msongamano.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na moja kati ya wazazi waliopeleka watoto wao kupata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiangalia daftari la matibabu kutoka kwa moja kati ya wazazi waliopeleka watoto wao kupata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati wa ziara yake ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akifanya ukaguzi katika chumba cha kuhifadhia Dawa wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akimsalimia moja Kati ya Wazee waliofika kupata huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika Hospitali hiyo.

KWA MARA YA KWANZA TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA SUMBAWAGA,MSAMA ATHIBISHA

$
0
0
Kampuni ya Msama Promotions,inayoratibu tamasha la Pasaka nchini imetangaza kulipekeka tamasha hilo kwa mara ya kwanza kwa wakazi wa Sumbawanga,mkoani Rukwa. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam , Msama amesema wakazi wa Sumbawanga wamekuwa wakihitaji huduma ya tamasha hilo kwa muda mrefu, hivyo ameahidi kuikata kiu ya wakazi wa mji huo kwa namna ya kipekee kabisa.

“Sumbawanga wamekuwa wakilalamika muda mrefu kuhusu kutokupelekewa Tamasha hilo, Mwaka huu kwa Mara ya kwanza tutapeleka Tamasha kwa wakazi wa Sumbawanga, wakae tayari kupokea ujio wa Tamasha lililobeba utofauti” amesema Msama. 

Amesema katika Tamasha la mwaka huu kutakuwa na utofauti mkubwa, ambapo ameeleza kuwa wapo waimbaji wapya ambao hawajawahi kuja nchini, na kuongeza kuwa kwa Mwaka huu waimbaji wote watakaopata nafasi watalazimika kuimba kwa kutumia Band (LIVE) na si CD (PlayBack) kama ilivyozoeleka. 

“Tumeongeza Waimbaji wapya ambao hawajawahi kuja nchini, waimbaji ambao hawataweza kuimba live kwakweli watatusamehee bure,itakuwa vigumu kupokea ushiriki wao kwenye tamasha hilo,tunafanya yote hiyo kuhakikisha tamasha la Pasaka 2019 linakuwa lenye utofauti mkubwa ,n ahata wapenzi wa muziki huo waone utofauti mkubwa na si vinginevyo”aliongeza Msama. 

Akizungumzia kauli ya tamasha hilo,Msama ametaja kuwa ni “ Umoja na Mshikamano hudumisha amani ya nchi yetu” alisema na kuongeza kuwa ni lazima Watanzania tukubali Mungu ametupa Rais mzuri na mchapa kazi,tutamuombea kokote tutakaposimama na ninawaomba Watanzania kwa ujumla wetu tumuombee Rais wetu. 

Tamasha hilo la Pasaka linatarajiwa kufanyika April, 21, 2019 katika Viwanja vya Posta Kijitonyama ambapo ameahidi Tamasha hilo kuwa lenye utofauti Mkubwa ukilinganisha na Matamasha yote yaliyopita.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,inayoratibu tamasha la Pasaka Alex Msama akizungumza na baadhi ya Waandishi wa habari leo Ofisini  kwake,Kinondoni jijini Dar wakati akiendelea kutoa ufafanuzi kuhusu maandalizi ya tamasha la pasaka,ikiwemo kutangaza kulipeleka tamasha hilo kwa mara ya kwanza mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions,inayoratibu tamasha la Pasaka Alex Msama akifafanua jambo mbele ya Waandishi wa habari leo Ofisini  kwake,Kinondoni jijini Dar  kuhusu maandalizi ya tamasha la pasaka 2019,ikiwemo kutangaza kulipeleka tamasha hilo kwa mara ya kwanza mjini Sumbawanga,mkoani Rukwa. 
Mmoja wa Waandishi wa habari  kutoka ZBC akiuliza swali  kwa Mwandaaji wa tamasha la Pasaka,Alex Msama.

 Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama alipokuwa akizungumza nao leo kuhusu maandalizi mbalimbali ya tamasha la Pasaka

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI UTOAJI WA TUZO YA KISWAHILI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia akiwasili wakati wa hafla ya utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Mabati –Cornell ya Fasihi ya Afrika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia akihutubia wakati wa hafla ya utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Mabati –Cornell ya Fasihi ya Afrika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia akimkabidhi cheti cha ushindi wa tuzo ya Fasihi Bw. Jacob Ngumbau Julius wakati wa hafla ya utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Mabati –Cornell ya Fasihi ya Afrika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia akimkabidhi   tuzo ya ushindi katika Fasihi Bi. Zainab Alwi Baharoon wakati wa hafla ya utoaji Tuzo ya Kiswahili ya Mabati –Cornell ya Fasihi ya Afrika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa wamiliki wa viwanda kurudisha fadhila kwa jamii ikiwemo kuwekeza katika lugha ya Kiswahili.

Makamu wa Rais ameyasema hayo leo kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo ya Kiswahili ya Mabati-Cornell ya Fasiji ya Kiafrika iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

“kwa hakika hii lugha haiwezi kupiga hatua bila kuwekewa uwekezaji wa dhati utakaojumuisha Serikali, sekta binafsi na asasi za kiraia”alisema Makamu wa Rais. Makamu wa Rais alisisitiza kuwa maendeleo yeyote ya Taifa hayawezi kufikiwa bila kuwa na lugha ya mawasiliano inayounganisha watu wa ndani ya nchi na hata nje ya nchi.

Tuzo hizi zimedhaminiwa na kampuni ya kutengeneza mabati ya ALAF Limited Tanzania pamoja na mshirikika wake kampuni ya Mabati Rolling Mills,Kenya kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Aidha, Serikali imeendelea kuwatafutia walimu wetu wa Kiswahili fursa mbalimbali za ajira ikiwemo kuwapeleka nchi jirani pamoja na kuzishawishi nchi hizi kukifanya Kiswahili kuwa lugha rasmi. 

Makamu wa Rais ametoa rai kwa waandaaji kuangalia namna ya kuhamasisha washiriki kutoka nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika.Makamu wa Rais alionyesha umahiri wake pale alipoamua kughani moja ya beti kutoka kwa mshahiri maarufu mkongwe Mzee Haji Gora.

Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais alisisitiza jamii kuienzi lugha ya Kiswahili kwani imekuwa kiungo muhimu baina ya familia na koo mbali mbali hapa nchini.Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Uwekezaji alisema matumizi ya lugha rahisi yanachagia kukuwa kwa maarifa na uelewa mahala pa kazi.

Washindi wa tuzo ya Kiswahili mwaka huu ni Bi. Zainab Alwi Baharoon na Bw. Jacob Ngumbau Julius.Wakati huohuo Makamu wa Rais alizindua kitabu cha washindi wa mwaka 2017, Bw. Ally Hilal na Doto Rangimoto .

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbali mbali na wadau wa Kiswahili kutoka sehemu mbali mbali duniani.

TRA TANGA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUTUMIA MASHINE ZA EFD,WANUNUZI NAO WATAKIWA KUDAI RISITI.

$
0
0
Meneja Mkuu wa Mkwabi Super Market Kawkab Hussein kulia akizungumza na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kushoto wakati wa ziara yake kwa walipakodi wanaotumia mashine na EFD na wasiokuwa nazo ili kubaini changamoto na kuziboresha
 Meneja Mkuu wa Mkwabi Super Market Kawkab Hussein kulia akizungumza na Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kushoto wakati walipoingia kwenye duka hilo
 Meneja Mkuu wa Mkwabi Super Market Kawkab Hussein kulia akimuonyesha Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure namna wanavyotumia mfumo wa EFD Mashine kutoka huduma zao kwa wateja wao kushoto wakati walipoingia kwenye duka hilo
  Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kulia akimuonyesha Mfanyabiashara Yusuph Tayabani kitu kwenye risiti wakati wa ziara hiyo
  Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kulia akitoka kwenye mmoja ya duka ambalo alilitembelea wakati alipowatembelea walipakodi wanaotumia mashine na EFD na wasiokuwa nazo ili kubaini changamoto na kuziboresha
  Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure katikati akiwa na maafisa wengine wa TRA mkoani Tanga wakitoka kwa duka la kuuzia gesi wakati wa ziara hiyo
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure


MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) Mkoani Tanga wamefanya ziara ya kutembelea walipakodi waliokuwa na mashine za EFD na wasiokuwa nazo ili kuweza kubaini changamoto zao na kuweza kuboresha huduma zao.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Meneja wa TRA Mkoani Tanga Specioza Owure alisema baada ya kutembelea walipakodi hao wameona wapo walikuwa wanastahili kuwa na mashine za EFD lakini hawana hivyo kuwaachia barua za kwenda kununua mashine hizo.

Alisema pia wamelazimika kutoa barua za wito kwa baadhi yao ili waweza kufika ofisi za mamlaka hiyo kwa ajili ya kuona kumbukumbu za mauzo na manunuzi ili kuona kama wanastahili kwa na mashine za EFD

Meneja huyo alisema kwamba ni muhimu sana kwa wafanyabiashara kuendelea kutumia mashinde za EFD ikiwemo kuwataka wanunuzi nao kudai risiti wakati wanapofanya manunuzi.

“Lakini pia tumewaelimisha walipa kodi athari za kutokutoa risiti na kutokutumia mashine za EFD na kwamba usipotoa risiti adhabu yake ni milioni tatu mpaka nne na nusu huku kwa wale wasiodai risiti adhabu yake inaanzia elfu 30 hadi milioni 1.5 au kifungo kisichozidi miaka mitano”Alisema.

Awali akizungumza katika ziara hiyo Meneja Mkuu wa Mkwabi Super Market Kawkab Hussein alisema umuhimu wa mashine hizo ni mkubwa kwani unarahisisha kufahamu mauzo ya siku na pia kuchangia maendeleo ya nchi .

Hussein alisema pia mfumo huo unawafanya wafanyabiashara kutokuibiwa kutokana na kila anayenunua bidhaa anapata risiti na hivyo kuwa rahisi kuweza kujua mauzo ya siku husika lakini pia kuchangia maendeleo ya nchi.

Hata hivyo alisema kwamba changamoto kubwa ambayo wanakumbana n ayo ni mtandao wa hizo mashine wakati mwengine unasumbua lakini pia ni ghali sana inabidi wapunguze maeneo ya mauzo yao unatakiwa ununua sita au zaidi ya hapo kama utaboreshwa mfumo vizuri unawasaidia kuweza kutambua mauzo.

Mamlaka hiyo iliwatembelea maduka mbalimbali yakiwemo ya dawa,vituo cha kuuzia mafuta cha Ratco,Super Marketi ya Mkwabi na maduka ya kuuza bidhaa za jumla za vyakula.

NAIBU WAZIRI JAWESO ATOA WIKI TATU KWA MKANDARASI KUKAMILISHA MRADI WA MAJI WA SAWALA

$
0
0

Naibu waziri wa maji Juma Aweso ametoa wiki tatu kwa kampuni ya mavonoa’s kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa
NAIBU waziri wa maji Juma Aweso akimbana mkandarasi wa kampuni ya mavonoa’s kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa



NA FREDY MGUNDA,IRINGA.


NAIBU waziri wa maji Juma Aweso ametoa wiki tatu kwa kampuni ya mavonoa’s kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala uliopo jimbo la Mufindi kusini katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Akizungumza mbele ya wananchi,wabunge na wafanyakazi wa halmashuri hiyo,waziri Aweso alisema kuwa amekuwa akipokea malalamiko mengi ya mkandasi huyo ambaye amekuwa hana mahusiano mazuri na viongozi wa halmashauri hiyo.

“Mimi niseme ukweli nakupa wiki tatu kuhakikisha unamalizia ujenzi wa mradi wa maji wa Sawala la sivyo utaniona mbaya na mimi ni mkali kweli kwa wakandasi wamepewa kazi na serikali na wanashindwa kutekeleza mradi kama ambavyo mkabata ulisema hivyo nakupa wiki tatu kuhakikisha wananchi wanapata maji” alisema Aweso

Aweso alisema serikalia ya awamu ya tano haita kubari kumuanda mkandarasi yeyote Yule aliyepewa kazi na serikali anashindwa kukamilisha mradi wakati fedha amepewa,mkandarasi huyo atachukuliwa hatua za kisheria haraka sana kwa kuwa saizi hakuna mtu kutumia vibaya pesa za serikali kama ilivyokuwa huko nyuma.

“Walizoea kuzichezea pesa za serikali miaka ya huko nyuma kwa sasa hakuna mkandarasi tayeweza kuichezea serikali ya awamu hii kwa kuwa sisi wateule wa Rais wetu Dr John Pombe Magufuli hakuna anayekubari kutumbuliwa kisa wakandarasi kufanya vibaya kwenye miradi waliyopewa” alisema Aweso

Aidha naibu waziri Aweso aliwatoa hofu viongozi wa halmashuri ya wilaya ya Mufindi kuhusu mkandarasi huyo kuwa akishindwa kutekeleza mradi huo ndani ya wiki tatu hizo basi sheria itachukua mkoando wake.

“Mkuu wa wilaya,mbunge,mkurugenzi na mwenyekiti wa halmashauri niwahakikishieni kuwa nitatakuja tena tarehe mbili mwezi wa tatu hapa kuja kuangalia kuwa huu mradi umefikiwa wapi na makubariano yetu ameyatekeleza mkandarasi huyu” alisema Aweso

Awali mkuu wa wilaya ya Mufundi Jamhuri William alimueleza naibu waziri kuwa mkandarasi huyoamekuwa anaidharau serikali kwa kuwa mara kwa mara ameandikiwa barua na serikali ya wilaya lakini hajawahi kujibu hata mara moja kitendo kinachoashiria dharau.

“Huyo mkandarasi amekuwa anatusumbua sana maana tunamuita mara kwa mara hataki kuitika wito wetu hivyo hizo ndio dharau kubwa kiasi kwamba anashindwa hata kuendelea kutekeleza mradi huu ambao wananchi wanategemea kuwa mkombozi wao” alisema Jamhuri William

Mkuu wa wilaya alisema kuwa atamkamata na kuwa ndani mkandarasi huyo kwa kuwa anachelewesha kuteleza mradi huo wa maji na kusababisha wananchi kuichukia serikali kwa kusema kuwa wametoa ahdi hewa kitua ambacho sio kweli.

“Mheshimiwa naibu waziri hapa Sawala tunashindwa hata kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya huu mradi wa maji ambao mwazoni wananchi walijenga imani kubwa wakati wa kusainiana mkataba wa kutekeleza mradi huu” alisema Jamhuri William

Akitoa malalamiko hayo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Festo Mgina alimwambia naibu waziri wa maji Juma Aweso kuwa hamhitaji tena huyo mkandarasi kwa kuwa amekuwa kikwazo cha kuleta maendeleo ya wananchi kwa kushindwa kutekeleza mradi huo wa maji.

“Huyu kwetu ni kero kubwa mno mheshimiwa naibu waziri wa maji,sisi kama halmashauri hatupo tayari kufanya kazitena na huyu mkandari kwa ujeuri wake na kushindwa kuiheshimu sekali ya wilaya kwa kushindwa kumtua ndo mwanamke” alisema

Nao baadhi ya wananchi walijitokeza hapo walimwambia naibu waziri kuwa mkandarasi huyo hafanyi kazi ipasavyo kwa kuwa amesikia waziri unakuja ndio na yeye ameanza kazi jana tu ya kukarabati tenki hili la maji ili ukifika uone kama yupo anafanya kazi wakati sio kweli.

Hata hivyo naibu waziri Juma Aweso alimalizia kwa kusema kuwa ifikapo tarehe mbili mwezi wa tatu mradi huo uwe umekamilika na wananchi waweze kupata maji na kufanikisha adhima ya Rais ya kumtua ndoo mwanamke.

TANTRADE YAMWAGA FURSA KWA WAZALISHAJI WA KAHAWA,VIUNGO,CHAI,CHIA, UFUTA NA MATUNDA YA KUUZA NJE YA NCHI


WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KANGI LUGOLA AMPONGEZA MKUU WA WILAYA YA MERU

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Alphaxard Lugola(MB akishikana mkono na Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakiwa pamoja na baadhi ya viongozi wa wilaya na Mkoa wa Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arumeru JerryMuro akionyesha moja ya gari la Polisi aina Land Rover Defender, alililifanyia ukarabati wilayani hapo mara tu alipoanza kazi mwaka jana 2018


Na. Vero Ignatus, Arusha

WAZIRI wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola(MB) amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry C. Muro, kwa juhudi alizozifanya za Kukarabati Gari ya Polisi aina Land Rover Defender, ambalo lilikuwa halitumiki kwa miaka mingi kutokana na kuchakaa na kuwa chuma chakavu, ambapo ukarabati huo umegharimu zaidi ya Tshs. Milioni 19. 

Mhe. Kangi Alphaxard Lugola amesema juhudi zilizofanywa na Mhe. Jerry C. Muro, kuwezesha ukarabati wa Gari hiyo ambayo imekarabitiwa na wadau wa maendeleo wa Wilaya ya Arumeru, kutasaidia kuimarisha Ulinzi katika maeneo ya Mamlaka ya Mji Mdogo wa Ngaramtoni. 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe. Jerry C. Muro, amesema Kwa kipindi cha miezi mitano alichotumikia wananchi wa Arumeru, amemua kutatua changamoto za vifaa vya kutendea kazi Kwa jeshi la Polisi ikiwemo kukarabati Magari yote ya Jeshi la Polisi Wilaya ya Arumeru, kwa kuwashirikisha wadau, badala ya kusubiria fedha kutoka Serikali Kuu.

SBL YAWAKUTANISHA WANAWAKE KUADHIMISHA SIKU YA WAPENDANAO

$
0
0
Wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Moshi, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya maazimisho ya siku ya wapendanao duniani ‘Valentine’s Day’ ambapo SBL imeazimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wanawake kujadili mchango wao katika ukuaji wa kampuni hiyo.
. Mwenyekiti wa wanawake wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Anitha Rwehumbiza akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wapendandanao duniani (Valentine’s Day) ambapo SBL imeazimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wanawake kupitia jukwaa liitwalo ‘SBL spirited women’ ili kutambua mchango wao katika utendaji kazi wa kampuni hiyo.
Wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL), Moshi, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya maazimisho ya siku ya wapendanao duniani ‘Valentine’s Day’ ambapo SBL imeazimisha siku hiyo kwa kuwakutanisha wanawake kujadili mchango wao katika ukuaji wa kampuni hiyo.

Katika kuadhimisha siku ya wapendano duniani maarufu kama ‘Valentine’s Day’ Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Ltd (SBL) imewakutanisha wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao katika utendaji kazi wa kampuni hiyo. 

Akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Alhamisi Februari 14, 2019 Mwenyekiti wa wanawake wa SBL, Anitha Rwehumbiza amesema lengo kubwa ni kuwainua wanawake ndani na nje ya ofisi kupitia jukwaa maalumu lijulikanalo ‘SBL spirited women’. 

Hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya kampuni hiyo yaliyopo Chang’ombe jijini hapa pamoja na matawi yaliyopo mikoa ya Mwanza na Moshi. 

“Lengo ni kuwainua wanawake katika nyanja tofauti sio tu katika kazi lakini pia nje ya ofisi na kwa mwaka huu tumeona tujumuike pamoja tuonyeshe upendo wetu kwa wanawake wote wa Serengeti na kuwashukuru wanawake kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kuendeleza kiwanda chetu,” amesema Rwehumbiza. 

Rwehumbiza amesema katika siku hiyo ya wapendanao kampuni ya Serengeti inawakumbusha watanzania kuzingatia unywaji wa kiistaraabu. 

“Kwa wateja wetu tunawashukuru sana kwa kuwa pamoja na sisi kwasababu uwepo wetu unategemea zaidi wafanyakazi na vilevile wanywaji wetu wakubwa,” amesema 

Wanawake hao walionyesha umaridadi kwa kuvaa mavazi ya rangi nyekundu ambayo huvaliwa katika siku hiyo na kukabidhiwa kinywaji maalumu kijulikanacho kama ‘Baileys’ kinachotengenezwa na kampuni mama ya Diageo na kusambazwa na kampuni ya bia Serengeti.

Wakandarasi watakaodanganya Serikali na Wananchi kuchukuliwa hatua

$
0
0
Na Teresia Mhagama

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, ameeleza kuwa, mkandarasi yeyote anayesambaza umeme vijijini, ikitokea amewadanganya wananchi na Serikali kwa kutotekeleza majukumu yake kadri ya makubaliano, atachukuliwa hatua za kinidhamu.

Dkt. Kalemani aliyasema hayo akiwa wilayani Gairo mkoani Morogoro ambapo alifika katika Kijiji cha Kibedya kwa ajili ya kukagua kazi usambazaji umeme na kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi.

“Nilipanga kuja hapa mwezi Disemba mwaka jana na ndipo Mkandarasi huyu akaamua kuleta umeme hapa, lakini sikuja na yeye akasimamisha kazi, hivi leo nimekuja kukagua na kukuta nyumba nyingi bado hazijaunganishiwa umeme na nguzo zimelala badala ya kutumika kusambazia watu nishati hii muhimu,” alisema Dkt Kalemani.

Kutokana na hilo, Dkt. Kalemani alitoa agizo kwa Mameneja wa TANESCO wa mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa wakandarasi wa umeme vijijini wanasambaza umeme katika maeneo yote waliyopangiwa vinginevyo Mameneja hao wajiondoe wenyewe kwa kushindwa kusimamia kikamilifu mradi huo.

“ Ili kutekeleza mradi huu kwa kasi, naendelea kusisitiza agizo la Serikali kuwa kila mkandarasi lazima awe na magenge matano ya kazi katika eneo lake, ili kutorudisha nyuma juhudi za Serikali za kuwasambazia umeme wananchi,” alisema Dkt Kalemani.

Akiwa katika Kijiji hicho, Dkt Kalemani aliwasha umeme ambao unatumiwa na wateja wa awali waliounganishwa na kutoa siku 13 kwa Meneja wa TANESCO, Wilaya ya Gairo kuwasambazia umeme wananchi waliosalia ambao tayari wameshalipia huduma ikiwa ni pamoja na vitongoji vya Kijiji hicho.

Aidha, amewataka Mameneja wa TANESCO nchi nzima, kuwafuata wananchi katika maeneo yao ili kutoa huduma kwani Serikali imewapa vitendea kazi kama magari ili kuwasogezea huduma wananchi badala ya wananchi hao kufuata huduma katika ofisi za TANESCO ambazo nyingine ziko mbali na wananchi hao..

Kwa upande wake, Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby, aliishukuru Serikali kwa juhudi zake za kusambaza umeme vijijini kwani Vijiji vyote katika Wilaya ya Gairo vipo katika mpango wa kusambaziwa umeme na tayari vingine vimeshaunganishwa na nishati hiyo.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa huduma ya umeme katika Kijiji cha Kibedya wilayani Gairo mkoa wa Morogoro. Wa pili kulia ni Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby na wa Pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Nchembe.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani (katikati) akizungumza na wataalam wa TANESCO pamoja na mkandarasi anayesambaza umeme vijijini wilayani Gairo mkoani Morogoro wakati alipofika katika Kijiji cha Kibedya wilayani humo kukagua kazi ya usambazaji umeme. Wa Pili kushoto ni Mbunge wa Gairo, Ahmed Shabiby.
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akizungumza na baadhi ya wananchi katika Kijiji cha Kibedya wilayani Gairo wakati alipofika kukagua mradi wa usambazaji umeme vijijini wa Awamu ya Tatu.

UTAFITI WAONESHA UBORA WA KURIPOTI HABARI UKO CHINI

$
0
0
*Habari nyingi ni za matukio, za kuikosoa Serikali haziandiki

Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii

RIPOTI ya matokeo ya Utafiti kuhusu Ubora wa Maudhui ya vyombo vya habari Tanzania kwa mwaka 2018 unaonesha ni nadra kwa vyombo vya habari kuandika au kutangaza habari zenye kuikosoa Serikali huku pia ikionesha kuwa ubora wa kuripoti habari uko chini na nyingi ni za matukio.

Pia ripoti hiyo inonesha kumekuwepo na dhana kwamba vyombo vya habari vinaripoti zaidi habari zinazotoka katika miji mikubwa ikiwemo ya Dar es Salaam,Dodoma, Mwanza, Mbeya,Arusha,Mjini Magharibi na Kusini Pemba.

Kwa mujibu wa watafiti wa utafiti huo ambao ni Christoph Spurk kutoka Switzerland na Abdallah Katunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Spurk Media Consulting Ltd wamesema vyombo vya habari vinawajibu mkubwa wa kuhamasisha maendeleo kwa kutoa habari zenye weledi, maslahi kwa umma na zenye kuwasamamia wenye mamlaka kuhakikisha wanatenda kulingana na taratibu zilizowekwa.

Hata hivyo wamesema wajibu huo muhimu unaweza kutimizwa na kuendelezwa pale tu vyombo vya habari vinapoweza kuripoti kwa kufuata vigezo vya kitaaluma na kwamba utafiti huo wa ubora wa vyombo vya habari Tanzania mwaka 2018 umechambua ubora wa vyombo vya habari kwa kutazama namna vinavyoripoti habari zao kwa kutumia vigezo maalumu ambavyo vimekubaliwa na wadau wa vyombo hivyo.

Akifafanua zaidi, Mtafiti Abdallah Katunzi amesema jumla ya sampuli 1886 ambazo zinajumuisha habari, makala na maoni kwa upande wa magazeti, habari na vipindi vya redio na televisheni pamoja na posti za blogu na mtandaoni kutoka vyombo vya habari 25 Tanzania Bara na Zanzibar na kwamba vyombo hivyo vinajumuisha magezeti saba , redio za kitaifa tano, redio za mikoani saba, televisheni za kitaifa tatu, televisheni ya mtandaoni moja, blogu moja na mitandao moja.

"Kwa ujumla matokeo yanaonesha ubora wa kuripoti kwa vyombo vya habari nchini uko chini kwenye vigezo vingi vilivyotazamwa kwa upande wa vigezo vya kitaaluma zaidi ya 1/3 ambapo asilimia 36 ya sampuli yote iliyochambuliwa imetumia chanzo kimoja cha habari na kwamba habari habari nyingi za waandishi ni zao la habari za matukio kwa asilimia 60 ikiwa ni ongezeko la asilimia nane ukilinganisha na matokeo ya utafiti wa mwaka 2017, ingawa kuna tofauti kubwa kati ya aina ya habari na vyombo vya habari,"amesema Katunzi.

Ametoa mfano kuwa za magazeti ni zao la habari za matukio kwa asilimia 72 wakati makala zinazozalishwa kwa kutegemea jitihada ya vyombo husika ni kwa asilimia 85 na kwamba upande wa televisheni asilimia 78 ya habari ni zao la habari za matukio wakati asilimia 90 ya vipindi vinazalishwa nje ya mfumo wa kufuata matukio.

Pia amesema kuna tofauti kubwa miongoni mwa vyombo vya habari, gazeti la Jamhuri lililofanya vizuri kwa mwaka 2018 habari zake zinatokana na jitihada za wahandishi kutafuta habari hizo kwa asilimia 63 wakati gazeti la The Gurdian ni asilimia 19 pekee.

Katunzi amesema kuwa ukitazama vigezo vya ukamilifu wa habari matokeo pia siyo mazuri kwa wastani ni asilimia 23 tu ya habari ,vipindi na makala zilizochambuliwa ndio zilikuwa na maelezo ya kwanini habari hizo zimeandikwa(root causes).Wakati asilimia tisa pekee ya sampuli yote ndio imeweza kutoa usuli(back ground) wa habari zilizoandikwa.

Kwa upande wa habari kueleweka kwa walengwa , amesema hali inaridhisha kwani asilimia 56 ya kazi zote zilizochambuliwa zina muundo mzuri wa waandishi huku zikiunganisha sehemu mbalimbali za habari kwa mtiririko mzuri.Hata hivyo bado kuna changamoto kwa vyombo vya habari kuelezea takwimu kwa namna ambayo inamsaidia msomaji au msikilizaji kuzielewa takwimu hizo ni asilimia 25 pekee ya kazi zote ndio imeweza kuelezea takwimu kwa kumrahisishia mlengwa kuzielewa.

Kuhusu maadili, amesema asilimia 42 ya sampuli yote imeshindwa kuwapa nafasi watuhumiwa kujieleza ikilinganishwa na asilimia 60 za mwaka 2017 , magazeti yamezingatia kigezo hicho kwa asilimia 50 huku redio na televisheni kwa asilimia 33 mutawalia. "Kuna tofauti kubwa kati ya redio au televisheni na magazeti na chombo kimoja kimoja cha habari.Kwa ujumla magazeti yamefanya vema kwenye vigezo vingi ukilinganisha na televisheni na redio, magazeti kwenye vigezo vyote kwa asilimia 33.2.

Pia amesema utafiti unaonesha kuwa ni vyombo vya habari vichache ndio vinaandika habari za kukosoa utendaji wa Serikali na katika eneo hilo ni Jamii Forums ndio inamaudhui ya kukosoa utendaji wa serikali.

Kupita utafiti huo inapendekezwa ili kuimarisha ubora wa vyombo vya habari inapendekezwa vyombo hivyo vitumie matokeo ya tafiti hiyo na hasa vikijikita kwenye maeneo ambayo havijafanya vizuri au viko chini ya wastani.Hata hivyo vyombo vya habari vinapaswa kujiimarisha kwenye maeneo kama ujumuishaji wa usuli kwenye habari.

"Sababu za kuandikwa kwa habari husika na kuongeza idadi ya habari ambazo zitachochea utendaji kazi wa Serikali ili kuvisaidia vyombo vya habari kujitathimini vyenyewe, utafiti wa mwaka 2018 umeboresha pima kadi ya ubora wa habari ambayo kwa sasa  redio za mikoani inaonesha matokeo kwa kila kigezo kwa kulinganisha na wastani na alama ya juu.Pia utafiti huu umetayarisha pima kadi nyingine ambayo inaonesha nafasi ya kila chombo,"amesema Katunzi.

NAIBU WAZIRI NISHATI AWATAKA WANA-PWANI WACHANGAMKIE UMEME WA REA

$
0
0
Na Veronica Simba – Pwani 

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani, hususan wanaopitiwa na Mradi wa Umeme Vijijini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kuchangamkia fursa hiyo kutokana na unafuu wa gharama zake.

Alitoa rai hiyo jana, Februari 15, 2019 kwa nyakati tofauti akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme, kuwasha umeme na kuzungumza na wananchi katika wilaya za Rufiji na Kibiti.

Alisema, gharama za uunganishaji umeme wa REA kwa kila mwananchi ni shilingi 27,000 tu lakini pindi mradi huo utakapoisha muda wake, gharama za uunganishaji zitakuwa kubwa zaidi. 

Hivyo, aliwaasa wananchi kutumia fursa hiyo ipasavyo kwa kujitokeza kwa wingi kulipia ili waunganishiwe.Aidha, Naibu Waziri aliwataka wananchi walio katika maeneo ambayo miradi mbalimbali ya umeme ilikwishapita na hawakufikiwa, kutulia kwani iko miradi mingine itakayotekelezwa katika maeneo yao hususan mradi wa ujazilizi (Densification).

Akifafanua, alisema, hakuna mwananchi au eneo ambalo litaachwa pasipo kupelekewa huduma ya umeme; ndiyo maana serikali kupitia Wizara ya Nishati, inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayolenga kuyafikia maeneo yote na kuhakikisha wananchi wote wanapata umeme, zoezi linalofanyika hatua kwa hatua.

Vilevile, Naibu Waziri Mgalu aliutaja mradi mkubwa wa umeme wa maji ya mto Rufiji maarufu kama Stiegler’s, ambao tayari mkandarasi amekabidhiwa rasmi kuanza kuujenga; kuwa utakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Pwani ambao ndiyo mkoa unaoubeba mradi husika.

Akiwa wilayani Rufiji, aliwataka kuzitumia fursa zitakazotokana na utekelezaji wa mradi wa umeme wa Rufiji katika eneo lao kwa kuwa wabunifu ili kujiongezea kipato kupitia shughuli mbalimbali.“Mradi wa Stiegler’s utaanza na ni fursa kwenu wana-Rufiji. Rai yangu tujipange kutumia fursa hizo. Rufiji hii itakuwa nyingine.”

Akiwa katika Kata ya Ngarambe, Naibu Waziri alitoa taa zinazotumia nguvu ya jua (solar), kwa wauguzi wa Zahanati za Ngarambe na Tapika wilayani Rufiji, ili kusaidia utoaji huduma kwa wagonjwa, wakati wakisubiri kufikiwa na huduma ya umeme. Pia, alitoa msaada wa mashuka katika Zahanati hizo.

Kwa upande wao, viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Kibiti na Rufiji, viongozi wa Halmashauri na Mbunge wa Kibiti, walipongeza jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na Serikali ya Awamu ya Tano, kupitia Wizara ya Nishati, katika kuhakikisha maeneo mbalimbali yanafikiwa na huduma ya umeme.

Waliomba jitihada hizo ziendelee kwa kasi ili kuyafikia maeneo yote hususan ya vijijini.Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Mgalu aliambatana na viongozi na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, TANESCO na REA. Alitembelea vijiji vya Ngarambe, Azimio, Umwe, Kitembo na Mkupuka.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), akiwakabidhi wauguzi wa Zahanati za Ngarambe na Tapika wilayani Rufiji, vifaa mbalimbali zikiwemo Taa zinazotumia umeme jua (solar) ili kuboresha utoaji huduma kwa wagonjwa. Naibu Waziri alikuwa katika ziara ya kazi wilayani humo Februari 15, 2019.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kata ya Ngarambe, wilayani Rufiji, Mkoa wa Pwani, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 15, 2019.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akisalimiana na watumishi mbalimbali wa Halamshauri ya Wilaya ya Rufiji, alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, akiwa katika ziara ya kazi, Februari 15, 2019.
 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (kulia), akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo (mwenye fulana ya njano), alipomtembelea ofisini kwake, Februari 15, 2019 akiwa katika ziara ya kazi wilayani humo. Wengine pichani ni baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo pamoja na wataalamu kutoka wizarani, REA na TANESCO.
Mmoja wa wakazi wa Ngarambe wilayani Rufiji, akitoa maoni yake kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme, mbele ya Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu (hayupo pichani); wakati wa ziara yake wilayani humo, Februari 15, 2019.

 Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu (mwenye kilemba cha pinki) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, maafisa kutoka wizarani, REA na TANESCO. Naibu Waziri alikuwa katika ziara ya kazi wilayani humo, Februari 15, 2019.

IKUPA ARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MASUALA YA WATU WENYE ULEMAVU WILAYANI KONGWA

$
0
0
NA OWM (KVAU) - KONGWA

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu, Mhe. Stella Ikupa ameridhishwa na utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu katika Wilaya ya Kongwa.

Hayo ameyasema wakati wa ziara yake katika wilaya hiyo kuangalia hali ya utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.

Akitoa pongezi hizo, Naibu Waziri, Ikupa alisema kuwa ushirikishwaji wa kundi hilo maalum ni jambo la msingi katika kuhakikisha haliachwi nyuma kwenye nyanja mbalimbali za maendeleo.“Endeleeni kuwajali na kuweka mipango thabiti yenye kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapata haki sawa kama wengine,” alisema Ikupa. 

Pia, aliipongeza wilaya ya kongwa kwa kusaidia Watu wenye Ulemavu kuhudhuria maadhimisho mbalimbali ya Kitaifa yanayofanyika hapa nchini.
“Matukio hayo yamekuwa yakiwapa hamasa kubwa na kuona fursa ambazo zinaweza kuwasaidia kujikwamua kiuchumi,” alieleza Ikupa

Aidha, Mhe. Ikupa alitoa rai kwa Watu wenye Ulemavu kuwa wabunifu na kuweza kutambua fursa kutokana na mazingira waliyopo na kuzitumia kujiongezea kipato.

Hata hivyo, Naibu Waziri Ikupa alihimiza uboreshwaji wa miundombinu rafiki zitakazowesha kundi hilo, kuelimisha jamii juu ya haki za watu wenye ulemavu, uundwaji wa kamati za kuhudumia kundi hilo maalum na kuwapatia taarifa watu wenye ulemavu kuhusu fursa za mikopo zinazotolewa na halmashauri, ajira na upatikanaji wa dawa, mafuta ya wenye ualbino na vifaa saidizi. 

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi alimshukuru Mhe. Ikupa kwa kufanya ziara Wilayani humo, na kuahidi kuendelea kutoa huduma kwa kundi hilo maalum ikiwemo asilimia 2 ya mapato ya ndani ya halmashauri zinatengwa na kutoa mikopo kwa Vikundi vya Watu wenye Ulemavu, pia kuhakikisha kamati za Watu wenye Ulemavu zinaundwa katika kila Kijiji na kufanya kazi kulingana na miongozo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri, Ikupa alitembelea Kituo cha Utengamao kilichopo Mlali na Shule maalum Kongwa Kitengo cha Viziwi. Pia alitembelea Wilaya ya Mpwapwa, Shule ya msingi Chazungwa na Mpwapwa Sekondari ambazo zina wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (wa kwanza kutoka kulia) akizungumza kuhusu masuala ya Watu wenye Ulemavu alipofanya ziara Wilaya ya Kongwa kukagua utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi akitoa taarifa ya utekelezaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa.
Mwalimu wa Shule ya msingi Kongwa, Kitengo Maalum cha Viziwi, Bi. Anitha Massawe akiwafafanulia wanafunzi wenye uziwi kwa lugha ya alama maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) alipotembelea shule hiyo.
Daktari wa Mazoezi ya Viungo kutoka Kituo cha Utengamao Mlali, Dkt. Nshashuku Joseph akimwelezea Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa aina ya mazoezi wanayoyatoa kwa Watoto wenye ulemavu wa viungo. (katikati) ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Deogratius Ndejembi.
Baadhi ya wazazi wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia (Wenye Ulemavu) Mhe. Stella Ikupa (hayupo pichani) alipotembelea Kituo cha Utengamano kilichopo Mlali, Wilaya ya Kongwa.

MKUU WA WILAYA YA KIGAMBONI ATEMBELEA MRADI WA VISIMA, AITAKA DAWASA KUVIKAMILISHA KWA WAKATI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa sita toka kushoto) na viongozi wengine alioambatana nao akimsikiliza Kaimu meneja miradi ya DAWASA, Ramadhani Mtindasi (wa nne kushoto) wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya Visima ilayosimamiwa na DAWASA. Picha na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

 Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni atembelea mradi wa visima unaotekelezwa unaotekelezwa na Mamlaka ya MajiSafi na MajiTaka (DAWASA) katika Wilaya yake huku akiitaka mamlaka hiyo kumaliza miradi hiyo kwa wakati. Akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza ziara yake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri amesema ipo haja ya kumaliza miradi kwa wakati ili kuweza kuwapa wananchi huduma stahiki.

 "Niwashuruku DAWASA kwa kutenga baadhi ya miradi na kuisimamia mpaka ikamilike kwa asilimia 100, ili sasa tunavyotatua changamoto za wananchi tujue kwamba Kimbiji, Gezaulole na Vijibweni hakuna tatizo la maji ili tuendelee na miradi mingine kuliko kuwa na miradi mingi alafu rasilimali ni chache alafu tunaendelea kuibua miradi mingine tunakuwa na viporo ambavyo havijakamilika", Amesema Msafiri Amesema Kigamboni kuna changamnoto kubwa ya miradi ya maji na umeme, kukamilika kwa wakati jambo ambalo linaweza kukwamisha ujenzi wa viwanda kwani kwa sehemu kubwa viwnada vinategemea maji na umeme wa uhakika. 

 "Leo tumeanza kutembelea miradi ya maji, hasa miradi inayotekelezwa kwenye ngazi ya Taasisi ambazo hazipo chini ya Manispaa ya Kigamboni na tumetembelea miradi mbalimbali na miradi mingi ni ya muda mrefu kwa mfano mradi wa Kimbiji wenye visima 12, kwa sasa DAWASA wameona wajielekeze kwenye baadhi ya visima, wamechukua visima viwili wamalize kabisa waendelee na usambazaji wa maji kwa wananchi watu waendelee kupata maji", Amesema Msafiri. Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri, akiwa ofisini kwake pamoja na maafisa wa DAWASA kabla ya kuanza ziara. Ameongeza kuwa "Lakini tuna mradi mwengine kama ule wa Geza Ulole, Maradi ule ni wa muda mrefu sana, Tafrisi yake ni nini kama taasisi, kumbe wanaweza kutenga fedha kwa ajili ya miradi ya mipya yenye changamoto ya kibajeti lakini tungetumia fedha hizo kufanya marekebisho", 

 Naye Mratibu wa Miradi kutoka DAWASA, Charles Makoye, amesema Mradi wa Gezaulole ulijengwa zamani na ndio kilikuwa chanzo kikuu cha maji kwa eneo la Gezaulole, Kibungomo na Mjimwema. "Chanzo kikuu cha mradi huu ambao umejengwa mwaka 1970 ni kisima kilichopo eneo la Gezaulole chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita 28, 000 elfu klwa saa na kilikuwa kikitumia pampu ya dizeli" Amesema Makoye. 

 meongeza kuwa Mradi huo ulikarabatiwa na DAWASA baada ya kuacha kufanya kazi kwa zaidi ya 18. Amesema ukarabati wa mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la maji kwa maeneo ya Gezaulole, Mbwa Maji na Kibungumo maeneo ambayo hayana mfumo rasmi wa maji pia Dawasa inatekeleza mradi wa maji wa Vijibweni unaoendela kujengwa ambapo Gharama kuuz a ukarabati wa mradi huo ni Tsh. 683,173,200.00.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa tatu toka kushoto) akiwaa na viongozi wengine alioambatana nao wakimuangalia Kaimu meneja miradi ya DAWASA, Ramadhani Mtindasi akionja maji yaliyo matika moja ya kisima wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya Visima ilayosimamiwa na DAWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa tatu toka kushoto) akiwa na viongozi wengine alioambatana nao wakimsikiliza Kaimu meneja miradi ya DAWASA, Ramadhani Mtindasi (wa nne kulia) wakati alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya Visima ilayosimamiwa na DAWASA.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (wa tatu toka kushoto) akipata maelezo toka kwa  Msimamizi wa Miradi ya Majitaka Wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) Mhandisi Charles Makoye (wa kwanza kushoto) juu ya mradi wa maji Gezaulole ambao ulijengwa toka mwaka 1970 na sasa DAWASA wameamua kuukarabati ili kutoa huduma ya maji.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa DAWASA Ole juu ya mradi wa maji utakaovuka bahari kwa upande wa Kigamboni kwenda Kijichi na kuwapatia wakazi wa Kigamboni Majisafi na Salama.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri akiongea na wanahabari kutoa ufafanuzi juu ya masuala mbali mbali ya maendeleo, changamoto zinazoikabiri wilaya hiyo mara baada ya kumaliza kufanya ziara ya kukagua maendeleo ya miradi mbali mbali.

KUMBILAMOTO AKUTANA NA WAJANE NA WALEMAVU ZAIDI YA 200 NA KUGAWA MIKATE

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Wajane zaidi ya  200 na Makundi ya watu wenye ulemavu kutoka kata ya Vingunguti wamekutana katika ukumbi wa Mashujaa Vingunguti jijini Dar es Salaam Kujadili Changamoto zao zinazo wakabili na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali.

Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti na Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala,ambae ndio chachu ya mkutano huo na mwanzilishi wa makundi hayo amewataka wakazi hao ambao wako katika kundi maalum kudumisha upendo na mshikamano katika Vikundi walivyoanzisha ili waweze kukopesheka.

Kumbilamoto amesema kumekuwa na ufinyu wa taarifa za fursa za watu wenye makundi maaalum kutokana na wao kujitenga na jamii inayowazunguka na kujiona wanyonge ,hivyo kupitia vikundi hivyo walivyounda wataweza kukaa pamoja na kupokea taarifa mbalimbali na fursa zinazopatikana kutoka katika taasisi za ndani na nje ya nchi.

"Iwe rahisi mtu kukufata nyumbani kwako kwa kuwa wewe mjane akakupa mkopo au fursa iliyopo mahali, lakini kupitia vikundi hivi mtaweza kukopesheka na Halmashauri yenu pamoja na mabenki kwa Halmashauri imetenga fungu maalum kwa ajili ya Vijana Walemavu na Wanawake ambalo mkopo wake auna riba hivyo ni vymea mkachangamkia fursa hii kwa kusajili vikundi vyenu na kukopa mapesa ya Rais Magufuli"alisema Kumbilamoto.

Aidha katika kusanyiko hilo kumbilamoto aliweza kugawa mikate miwili miwili kwa kila mjane na mlemavu waliofika katika mkutano huo kama kifungua kinywa kwa siku ya kesho.
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto akizungumza na kundi la Wajane na Walemavu wa kata ya Vingunguti
Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Vingunguti kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),Omary Kumbilamoto akigawa Mikate kwa Wanawake wajane na watu wenye ulemavu.
Sehemu ya Wanawake Wajane na Watu Wenye ulemavu waishio Vingunguti wakisubiri neno kutoka kwa Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto.

WAZIRI MKUU AWASILI KIGOMA KWA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU NNE.

$
0
0
Na  Editha Karlo wa blog ya jamii,Kigoma.

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania mhe Kassim Majaliwa amewasili leo Mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku nne.

Lengo la ziara yake imeelezwa kuwa ni kuweka msisitizo katika ufufuaji na uendelezaji wa zao la chikichi ikiwa ni pamoja na kukagua vitalu vya mashamba ili kuliboresha zaidi zao hilo.

Aidha katiaka ziara yake,Waziri Mkuu atatembelea katika Wilaya ya Kigoma Uvinza,Kibondo na Kakonko,sambamba na kuitembelea kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilayani kibondo na kuzungumza nao.
 Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege kigoma
 Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma
 Waziri mkuu akifurahi pamoja na kikundi cha ngoma cha akina mama
 Waziri mkuu Kassimu Majaliwa akiwasalimia wananchi waliofika kumlaki katika uwanja wa ndege wa kigoma, baada ya kuwasili kwaajili ya ziara ya kikazi.

Taasisi ya MISA Tanzania yawapiga msasa wanahabari Kanda ya Ziwa

$
0
0
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Internews imeandaa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Simiyu, Mara na Mwanza ili kuwajengea uwezo kuhusu sheria mpya za vyombo vya habari na haki ya upatikanaji taarifa. 

Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia leo Februa 16, 2019 yanafanyika Bariadi mkoani Simiyu ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini Tanzania ambayo yamekuwa yakitolewa na MISA Tanzania.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkufunzi wa mafunzo hayo, Sengiyumva Gasirigwa (kulia) akiwasilisha mada kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika utetezi wa haki za binadamu.
Mafunzo hayo yanagusia sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya mwaka 2016, Sheria ya Taifa ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma za Mitandao ya Kijamii ya mwaka 2015 pamoja na Kanuni zake.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Clonel Mwegendao (kulia) kutoka SACHITA FM iliyopo Tarime mkoani Mara akieleza matarajio yake ambapo amesema anatarajia kutambua sheria mpya za habari, changamoto zake na namna ya kukabiliana nazo.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Edna Elisha (kulia) kutoka Jembe FM ya Jijini Mwanza amesema mafunzo hayo yatamjengea uelewa mpana kuhusu sheria ya huduma za habari na hivyo kutimiza vyema majukumu yake.
Mshiriki wa mafunzo, Hellen Mteremko kutoka City FM Mwanza akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki Raphael Okelo wa Gazeti Majira kutoka Bunda mkoani Mara akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Dinna Maningo akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki, Derick Milton wa Gazeti Mtanzania mkoani Simiyu akieleza matarajio yake baada ya mafunzo hayo.
Mshiriki wa mafunzo hayo, Machunda Nicholaus wa Sibuka FM mkoani Simiyu akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki, Hassan Ramadhan wa Star TV Jijini Mwanza akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mshiriki, Neema Evance wa Azam TV mkoani Simiyu amesema sheria yoyote mpya inakuja na changamoto zake hivyo mafunzo hayo yatamjengea uwezo kutambua sheria mbalimbali za vyombo vya habari na namna ya kukabiliana na changamoto hizo.
Washiriki wa mafunzo hayo.
Afisa Utawala na Fedha kutoka taasisi ya MISA Tanzania, Andrew Marawiti (kushoto) akiteta jambo na Afisa Habari na Utafiti wa taasisi hiyo, Neema Kasabuliro (kulia).
Tazama BMG Online TV hapa chini

LUGOLA ATOA ONYO MAGARI YA POLISI KUBEBA, KUSINDIKIZA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Arumeru 

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku na kutoa onyo kali kwa magari ya polisi nchini kutumika kubeba au kusindikiza dawa za kulenya. 

Lugola amesema wapo baadhi ya polisi wanatuhumiwa kufanya matukio ya kubeba bangi, mirungi pamoja na dawa aina mbalimbali za kulenya hapa nchini wakitumia magari ya Jeshi la Polisi ambapo ni kinyume cha sheria. 

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Soko la Ngaramtoni wilayani Arumeru, Mkoani Arusha, jana, mara baada ya kukabidhiwa gari la polisi lililokarabitiwa na Kampuni ya Friedkin Conservation Fund (CFC) ya hapa nchini kwa gharama ya shilingi milioni 15, amesema kitendo hicho kinalifedhehesha Jeshi la Polisi ambalo linatakiwa kuwa mfano wa kukabiliana na uhalifu. 

Kutokana na tabia mbaya hiyo walionayo baadhi ya polisi nchini wasiokua waadilifu, Waziri Lugola amesema polisi yeyote akikamatwa kushiriki kufanya tukio hilo hata muonea huruma kamwe, ataondolewa katika nafasi hiyo na kushtakiwa. 

“Polisi wakikamatwa wanasindikiza au kubeba dawa za kulevya, polisi hao tutawafukuza kazi pamoja na kuwashtaki, gari hili la polisi ambalo limekarabatiwa na Taasisi hii, litumike vizuri kwa kupambana na wahalifu na siyo vinginevyo,” alisema Lugola. 

Aidha, Mbunge wa Viti Maalum wa CCM Wilayani humo, Amina Mollel alimlalamikia Waziri Lugola akisema ndani ya Wilaya hiyo kuna kesi ambazo zinachukua mda mrefu katika vituo vya polisi kwa kisingizio cha upelelezi kuwa haujakamilika hasa kesi za ubakaji ambapo alitoa namba ya faili mkutanoni hapo. 

“Mheshimiwa Waziri, licha ya kuwa Polisi wanafanya kazi vizuri wilayani hapa Arumeru lakini kuna tatizo la kesi mbalimbali zinachukua muda mrefu katika vituo vya polisi hasa kesi za kubaka, na kuwafanya wananchi kuchelewa kupata haki zao, kesi inachukua miezi sita bado ipo katika upepelezi, huo muda ni mrefu sana” alisema Amina. 

Hata hivyo, Waziri Lugola kutokana na tuhuma hiyo, alimuagiza Mkuu wa Polisi wilayani humo (OCD) kutafuta faili la kesi zilizotajwa na Mbunge huyo ili aweze kumletea katika mkutano huo kabla ya kumaliza mkutano huo. 

Baada ya kutoa agizo hilo, OCD alileta faili hilo katika mkutano huo, na kumkabidhi Mkuu wa Wilaya hiyo, ambaye pia ndio Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Jerry Murro, ili aweze kumkabidhi Waziri Lugola na aweze kutoa maelekezo zaidi. 

Waziri Lugola yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ambapo anatembelea Wilaya zote za Mkoa huo akifuatilia utendaji kazi wa Taasisi zake ambazo zipo ndani ya Wizara yake.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na wananchi katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Soko la Ngaramtoni, Wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha, leo, akitoa onyo kwa baadhi ya Polisi nchini wenye tabia ya kubeba, kusindikiza dawa za kulevya kwa kutumia magari ya Jeshi la Polisi. Kulia ni Mbunge wa Viti Maalum kutoka Arusha, Amina Mollel. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akipokea ufunguo wa gari la Polisi namba PT 0747, kutoka kwa Kampuni ya Friedkin Conservation Fund (FCF), Mratibu wa Shughuli za Kudhibiti Ujangili, William Mallya (kulia) ambayo ilikarabati gari hilo la Kituo cha Polisi Usa-River, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Lugola mara baada ya kulikabidhi gari hilo kwa Jeshi la Polisi wilayani humo, alitaka gari hilo litumike vizuri kubebea watuhumiwa na sio kubeba au kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Jerry Muro
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akilikagua gari la Polisi namba PT 0747 ambalo limekarabatiwa na Kampuni ya Friedkin Conservation Fund kwa ajili ya Kituo cha Polisi Usa-River, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Lugola alikabidhiwa gari hilo na pia naye akalikabidhi kwa Jeshi la Polisi Wilaya hiyo na kuagiza litumike vizuri kubebea watuhumiwa na sio kubeba au kusindikiza dawa za kulevya. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto, akimwelekeza jambo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro (katikati), wakati Waziri huyo alipokuwa anaelekea kupokea madarasa yaliyojengwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Shule ya Msingi Usa-River, Wilayani humo, Mkoa wa Arusha. Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, James Mchembe. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

NUKUU ZA NDG. HUMPHREY POLEPOLE KWENYE KIKAO NA WAFANYABIASHARA WA MIFUGO WILAYA YA LONGIDO

$
0
0

16 Februari 2019

1. "Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi imefanikisha ujenzi wa kiwanda cha nyama hapa kinachoendelea kujengwa kitakuwa kinapokea Ng’ombe 50 na Mbuzi 2000 kwa siku bidhaa zote za mifugo zitatengenezwa hapa na wanufaika wa msingi ni wananchi wote, huo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM” Ndg. Polepole

2. "Tunataka Serikali yetu ipate mapato kutokana na biashara ya mifugo na mapato hayo yawe ya haki, mapato yasiwe yana mgandamiza mfanyabishara na yatakayo kuwa rafiki kwa wafanyabishara” Ndg. Polepole

3. "Nasi kama Chama tunasema kulipa kodi hakuna mjadala lakini lazima kodi hiyo iwe inayozingatia haki” Ndg. Polepole

4. "Hapa kuna wafanyabishara wanapitisha mifugo kwenye njia za magendo na sababu  mmesema ni kodi kubwa ila wengine ni kwa sababu ya ukorofi wao tu wakuto tii sheria” Ndg. Polepole

5. "Tumezungumza na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Naibu Waziri wake na Katibu Mkuu wa Wizara  Chama kimeelekeza waje hapa Longido wazifanyie kazi changamoto zenu na ndani ya siku mbili kutoka leo Naibu Waziri atakuwa hapa” Ndg. Polepole

6. "Naye Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi atafika hapa kesho kuwasikiliza tunataka suala la usumbufu barabarani kwa wafanyabiashara wa mifugo nalo liishe, Serikali yetu ni sikivu tunaamini litakwisha” Ndg. Polepole

7. "Msimamo wetu kama Chama tozo hizi kwa wafanyabiashara wa mifugo zipungue ziwe rafiki kwa wafanyabiashara, wao wapate faida na Serikali ipate faida, wao wawe matajiri na Serikali iwe vizuri kimapato ilete maendeleo makubwa kwa wananchi” Ndg. Polepole

8. "Lengo letu kama Chama tunataka kila changamoto iliyokatika uwezo wa binaadam kutatuliwa tuitatue” Ndg. Polepole

Imetolewa na,
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

 
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images