Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

JK NA LOWASSA WAJUMUIKA NA MAMIA YA WANANCHI MAZISHI YA BILIONEA MREMA ARUSHA

$
0
0
 Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akiweka shada la maua katika kaburi la Bilionea marehemu Maleu Mrema katika ibada ya mazishi yaliyofanyika jana katika hoteli yake ya Ngurudoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha(Habari Picha NA Pamela Mollel,Arusha)
Waziri Mkuu mstaafu,Edward  Lowassa akiweka shada la maua pamoja na mke wake  katika mazishi ya bilionea Maleu Mrema jana nje kidogo ya jiji la Arusha katika hoteli ya Ngurudoto
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Mrema katika ibada ya mazishi yaliyofanyika katika hoteli yake ya Ngurudoto iliyopo nje kidogo ya jiji la Arusha
 Baadhi ya wake za marehemu wakiweka udongo katika kaburi la mpendwa wao

 Waziri Mstaafu wa mambo ya nje Benard Membe akiweka shada la maua katika kaburi la Bilione Mrema

 Meneja mahusiano Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa)Pascal Shelutete akiweka shada la maua katika kaburi la Bilione Mrema.
 Watoto wa marehemu wakiwa wamebeba mashada ya maua

 Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete wakisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu,Edward  Lowassa katika mazishi ya bilionea Maleu Mrema leo nje kidogo ya jiji la Arusha katika hoteli ya Ngurudoto
 Baadhi ya wanakamati wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Mrema kuelekea katika eneo maalumu lililotengwa na familia kwaajili ya maziko
 Hapa watoto wakiwa wanaweka udongo katika kaburi la baba yao
 Wake wa marehemu wakiwa wanaingia katika eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya maziko
 Kulia ni Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete,katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo pamoja na
Abdulrahman Omari Kinana wakiteta jambo katika msiba wa Mrema
 Wake wa marehemu Mrema wakiwa katika huzuni kulia aliyevalia suti nyeusi ni baba mzazi wa Bilionea huyo
 Mh Abdulrahman Omari Kinana mara baada ya kuweka shada la maua
 Jeneza la marehe Bilionea Maleu Mrema likiwa linashushwa katika nyumba yake ya milele

Wanafamilia wakiwa katika picha ya pamoja na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete
Nyumba ya milele ya Bilionea Maleu Mrema

SERIKALI YAMALIZA SINTOFAHAMU YA TANI 3,700 ZA TUMBAKU

$
0
0

Serikali imefanikiwa kumaliza sintofahamu ilikuwepo baina ya wakulima na wanunuzi wa tumbaku mkoani Tabora juu ya uwepo wa tani 3,700 zilizokosa soko.

Tani 3,700 zilikuwa zimekosa wanunuzi kwa sababu hazikuwa na mkataba kati ya wakulima na wanunuzi na hivyo kuhitaji utatuzi wa haraka wa Serikali ili kuinusuru tumbaku hiyo.

“Tumefanikiwa kuongea nao na tutauza zile tani 3,700 kwa wanunuzi,” alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kuamsha shangwe ukumbi mzima.

Waziri Mkuu alitoa ahadi hiyo jana jioni (Jumatano, Agosti 9, 2017) wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku zaidi ya 600 wakiwemo wabunge, viongozi wa dini, chama na Serikali kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isike-Mwanakiyungi, mjini Tabora.

Aliwashukuru wanunuzi kwa kukubali kumaliza tatizo hilo kwani litaleta ari mpya kwa wakulima na kuwafanya wajipange vizuri kwa msimu ujao. “Makampuni ya ununuzi yatapita kwenye maeneo yenu, WETCU watafuatilia na tumekubaliana nao kuwa tutafanya kazi pamoja,” alisema Waziri Mkuu.

Kufuatia sintofahamu hiyo, wiki iliyopita, wakazi wa mkoa huo waliomuomba Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli aingile kati ili kuwanusuru na adha ya zao hilo kukosa soko. Naye akawaahidi wananchi hao kwamba suala hilo atalikamilisha Waziri Mkuu.

Mapema, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Bw. Aggrey Mwanri wakati akiwasilisha muhtasari wa taarifa ya mkoa huo alisema katika masoko ya tumbaku yanayoendelea, kuna tatizo la tumbaku kukosa  wanunuzi kwani hapakuwa na mkataba kati ya wakulima na wanunuzi.

“Tumbaku inayofikia kilo milioni 3.7 kwa sehemu kubwa ililimwa kwa ufadhili wa       WETCU Ltd, kwa fedha ambazo zilikuwa ziende APEX. WETCU walinunua pembejeo na kuwapa wakulima waliokuwa chini ya vyama sinzia, na sasa haina wanunuzi. Tunaomba ulisemee hilo ili tupate ufumbuzi wa suala hili,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Tabora ambaye pia ni mbunge wa Urambo, Mheshimiwa Margareth Sitta aliiomba Serikali ikubali kuliangalia suala hilo la tani za ziada 3,700 kwani wakulima wamejaza tumbaku majumbani mwao na kwenye maghala.

“Wakulima wetu wanahitaji kuuza hii tumbaku ili wapate fedha za kuanzia msimu ujao wa kilimo. Lakini pia tunaomba liangaliwe suala la upangaji madaraja ya tumbaku, wasaidiwe kukabili bei isiyotabirika na kutatua ukosefu wa soko la uhakika,” alisema Mama Sitta.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 10, 2017.

NMB yaendelea kung'ara Maonesho ya Nane Nane, Arusha na Morogoro

$
0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto - Dr. Hamisi Kigwangala akikabidhi kikombe cha ushindi kwa Meneja wa NMB kanda ya Mashariki – Aikansia Muro baada ya benki hiyo kuibuka mshindi wa kwanza kwenye Maonyesho ya Nane Nane Mjini Morogoro. Kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano wa NMB kwa serikali – Aneth Kwayu na kulia ni Meneja wa tawi la NMB Wami – William Kaitara. Meneja Mikopo wa NMB mkoa wa Arusha, Oscar Rwechungura (kushoto) akipokea kombe la ushindi wa kwanza kwa taasisi za fedha kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenesta Mhagama wakati wa kilele cha maonesho ya wakulima Nanenane uwanja wa Themi mkoa wa Arusha Naibu Waziri wa TAMISEMI – Suleiman Jafo akimkabidhi cheti cha ushindi Meneja wa NMB Tawi la Dodoma – Harold Lambileki baada ya benki ya NMB kuibuka mshindi wa Tatu katika sekta ya fedha kwenye maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini Dodoma. NMB inashiriki maonesho ya Nane Nane katika kanda saba na kutoa elimu juu ya huduma za mikopo kwenye sekta ya kilimo. Baadhi ya wafanakazi wa Benki ya NMB wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mgeni rasmi. Picha ya kumbukumbu baada ya ushindi.
 BENKI ya NMB imeendelea kufanya vizuri kwenye maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika kanda mbalimbali nchini. NMB Imeshika Nafasi ya kwanza kati ya taasisi za kifedha kwenye mikoa ya Arusha na Morogoro huku ikishika Nafasi ya tatu katika mkoa wa Dodoma. Benki ya NMB inashiriki katika maonesho ya Nane Nane maarufu kwa wakulima kwenye mikoa sita ya Lindi, Mbeya, Dodoma, Morogoro, Arusha na Mwanza. Miongoni mwa malengo ya NMB ni kuhakikisha inarahisisha zaidi na kuchochea maendeleo ya kilimo na kuwaendeleza wakulima nchini.  Wafanyakazi wa benki ya NMB wakifurahia kombe lao walilokabidhiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Kazi, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Jenesta Mhagama wakati wa kilele cha maonesho ya wakulima Nanenane uwanja wa Themi mkoa wa Arusha Naibu Waziri wa TAMISEMI – Suleiman Jafo akimkabidhi cheti cha ushindi Meneja wa NMB Tawi la Dodoma – Harold Lambileki baada ya benki ya NMB kuibuka mshindi wa Tatu katika sekta ya fedha kwenye maonyesho ya Nane Nane yanayoendelea mjini Dodoma. NMB inashiriki maonesho ya Nane Nane katika kanda saba na kutoa elimu juu ya huduma za mikopo kwenye sekta ya kilimo. Mgeni rasmi katika kilele cha Maonesho ya Nane Nane mkoani Mbeya, Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, MHE. George Simbachawene akimkabidhi zawadi mmoja wa waliotembelea banda la NMB katika maonesho hayo.

WADAU WA NISHATI KUTOKA UMOJA WA ULAYA NA TANZANIA WAKUTANA KUJADILI MFUMO WA NISHATI KATIKA MAJENGO MAKUBWA NCHINI

$
0
0





Mteja kutoka Simanjiro alipata fursa ya kutembelea banda la ALAF katika maonyesho ya nane nane kanda ya kaskazini Arusha, akaeleza ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya ALAF ambapo amewataka watanzania kupenda na kuthamini bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo kwa kuwa zinaubora wa hali ya juu(Habari picha na Pamela Mollel Arusha)




Afisa Masoko wa kampuni ya ALAF jijini Arusha Finias Wanguba akionyesha bati aina yaTekdek inayozalishwa na kampuni hiyo jijini Arusha,





















Meneja mauzo kanda ya kaskazini Edward William akionyesha aina ya mabati yanayopatikana katika kampuni yao




Wateja wakiwa katika banda la kampuni ya ALAFwakipewa maelezo juu ya ubora wa bidhaa hiyo












Kampuni ya ALAF inayozalisha na kusambaza mabati ya aina mbalimbali







Na Pamela Mollel,Arusha












Kampuni ya ALAF inayozalisha na kusambaza mabati ya aina mbalimbali ya rangi pamoja na bati maarufu simba dumu imekuwa ikihudumia watanzania kwa zaidi ya miaka 50.




Akizungumza katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini Afisa Mauzo wa kamapuni ya ALAF Finias Wanguba alisema kuwa mabati hayo yana ubora wa hali ya juu na bei zake ni za kawaida tu hivyo mwananchi yeyote anaweza kumudu kununua






Pia katika maonyesho hayo ya nanenane kamapuni hiyo imetoa punguzo la bei katika bidhaa zake






Mabati haya hupatikana kanda ya kaskazini Arusha,kanda ya kati Dodoma,kanda ya ziwa Mwanza,Nyanda za juu kusini Mbeya,Dar esaalam






Hata hivyo kiwanda cha ALAF ni kiwanda cha kwanza Tanzania kilicholeta teknologia ya bati la msauzi ambapo huzalisha bati na chuma






Kwa upande wake Mteja kutoka Simanjiro alipata fursa ya kutembelea banda la ALAF katika maonyesho ya nane nane Mkoa Arusha, alieleza ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya ALAF ambapo amewataka watanzania kupenda na kuthamini bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo kwa kuwa zinaubora wa hali ya juu





Mtoa mada kutoka Mradi wa Matumizi bora ya Nishati katika Majengo Makubwa Kutoka Umoja wa Ulaya,Margareta Zidar akizungumza na Wadau wa Nishati katika semina Maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini juu ya Matumizi ya Nishati katika Majengo Makubwa.
Mtoa mada kutoka Mradi wa Matumizi bora ya Nishati katika Majengo Makubwa Kutoka Umoja wa Ulaya, Lena Lampropoulou, akizungumza na Wadau wa Nishati katika semina Maalum iliyoandaliwa na Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini juu ya Matumizi ya Nishati katika Majengo Makubwa.
Wadau mbalimbali wa Masuala ya Nishati katika Majengo Makubwa wakiwa wanafuatilia mada katika Semina hiyo ya Nishati katika Majengo Makubwa
Wadau kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi Binafsi wakifatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano huo muhimu kwa ajili ya Nishati za Mjengo Makubwa
Wadau kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi Binafsi wakifatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano huo muhimu kwa ajili ya Nishati za Mjengo Makubwa
Wadau wa Masuala ya Nishati ya Majengo Makubwa kutoka nchini Tanzania na Ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya wakiwa katika picha ya Pamoja mara baada ya ufunguzi wa Semina yao ya masuala ya Nishati katika Majengo Makubwa iliyofanyika Serena Hotel Dar es Salaam.




















KAMPUNI YA ALAF YATOA PUNGUZO LA BEI BIDHAA ZAKE KATIKA MAONYESHO YA NANENANE ARUSHA

$
0
0
 Mteja kutoka Simanjiro alipata fursa ya kutembelea banda la ALAF katika maonyesho ya nane nane kanda ya kaskazini Arusha,  akaeleza ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya ALAF ambapo amewataka watanzania kupenda na kuthamini bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo kwa kuwa zinaubora wa hali ya juu(Habari picha na Pamela Mollel Arusha)
 Afisa Masoko wa kampuni ya ALAF jijini Arusha Finias Wanguba akionyesha bati aina yaTekdek inayozalishwa na kampuni hiyo jijini Arusha,




Meneja mauzo kanda ya kaskazini Edward William akionyesha aina ya mabati yanayopatikana katika kampuni yao
 Wateja wakiwa katika banda la kampuni ya ALAFwakipewa maelezo juu ya ubora wa bidhaa hiyo


Kampuni ya ALAF inayozalisha na kusambaza mabati ya aina mbalimbali 


Na Pamela Mollel,Arusha


Kampuni ya ALAF inayozalisha na kusambaza mabati ya aina mbalimbali ya rangi  pamoja na bati maarufu simba dumu imekuwa ikihudumia watanzania kwa zaidi ya miaka 50.
 
Akizungumza katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini Afisa Mauzo wa kamapuni ya ALAF Finias Wanguba alisema kuwa  mabati hayo yana ubora wa hali ya juu na bei zake ni za kawaida tu hivyo mwananchi  yeyote anaweza kumudu kununua

Pia katika maonyesho hayo ya nanenane kamapuni hiyo imetoa punguzo la bei katika bidhaa zake 

Mabati haya hupatikana kanda ya kaskazini Arusha,kanda ya kati Dodoma,kanda ya ziwa Mwanza,Nyanda za juu kusini Mbeya,Dar esaalam

Hata hivyo kiwanda cha ALAF ni kiwanda cha kwanza Tanzania kilicholeta teknologia ya bati la msauzi ambapo huzalisha bati na chuma

Kwa upande wake  Mteja kutoka Simanjiro alipata fursa ya kutembelea banda la ALAF katika maonyesho ya nane nane Mkoa Arusha,  alieleza ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya ALAF ambapo amewataka watanzania kupenda na kuthamini bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo kwa kuwa zinaubora wa hali ya juu.

'MARUFUKU VIONGOZI KUFANYA BIASHARA YA PEMBEJEO KAMA HAWANA MASHAMBA'.

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepiga marufuku viongozi wa Serikali kufanya biashara ya pembejeo na vishada kama hawana mashamba ya tumbaku.

“Kuna baadhi ya viongozi wa Serikali hapa mkoani wamejiingiza kwenye biashara ya vishada na uuzaji wa pembejeo. Hii ni dosari. Hatutaruhusu hili hata kidogo,” alisema.

Waziri Mkuu alitoa onyo hilo jana jioni (Jumatano, Agosti 9, 2017) wakati akizungumza na wadau wa zao la tumbaku zaidi ya 600 wakiwemo wabunge, viongozi wa dini, chama na Serikali kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Isike-Mwanakiyungi, mjini Tabora.

Alisema: “Kiongozi wa Serikali ni lazima uwe shamba na ulilime kisasa ili liwe ni shamba darasa kwa wakulima walio jirani nawe. Usifanye biashara ya pembejeo kana huna shamba. Nanyi viongozi wa AMCOS msikubali kuuza vishada vya viongozi wa Serikali, tukikukamata, utaenda jela.”

Alisema endapo viongozi wataamua kulima mashamba ya zao hilo, watalazimika kujiunga na vyama vya msingi (AMCOS) vya kwenye maeneo yao ili waweze kuuza kupitia huko kutokana na agizo la Serikali linalokataza makampuni kununua tumbaku bila kupitia kwenye vyama vya msingi.

Aprili 15, mwaka huu, akiwa katika ziara ya siku moja mkoani Tabora, Waziri Mkuu aliagiza wakulima wa kujitegemea (Indepenent Farmers) na wale wa kwenye vikundi (Associations) wote wauzie tumbaku yao kupitia kwenye vyama vya ushirika ili kuzuia utoroshaji wa zao hilo na wakulima wasio na madeni kulazimika kuwalipia wenzao.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 10, 2017.

SERIKALI KUDHIBITI USAFIRISHAJI WA FEDHA TASLIMU MIPAKANI

$
0
0

Washiriki wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni za Taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha tasilimu kutoka na kwenda nje ya nchi wakifuatilia kwa makini mjadala katika warsha hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni za Taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha tasilimu kutoka na kwenda nje ya nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wa warsha hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam

Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa Kanuni za taarifa za Usafirishaji na uingizaji wa fedha taslimu kutoka na kwenda nje ya nchi (Crossborder Declaration of Currency and Bearer Negotiable Instruments Regulations) ambapo wasafirishaji wa fedha taslimu na wasafiri wote wanaotoka au kuingia nchini, watatakiwa kutoa taarifa za fedha taslimu wanazosafirisha ikiwa fedha hizo zinalingana au zinazidi kiasi cha dola za kimarekani elfu kumi (USD 10,000).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili ya maandalizi ya utekelezaji wa Kanuni hizo, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU) Ndugu Onesmo H. Makombe alisema utekelezaji wa kanuni hizi, pamoja na mambo mengine utaiwezesha nchi kuwa na takwimu za usafirishaji fedha taslimu.

“Takwimu hizo zitakazosaidia pamoja na mambo mengine kubaini vitendo vya kihalifu, kupunguza utoroshaji wa mitaji na kuhakikisha kuwa tunapunguza kama siyo kumaliza kabisa usafirishaji wa fedha zitokanazo na uhalifu au/na fedha kwa ajili ya kufadhili ugaidi” alisema Bw. Makombe

Aidha kanuni hizo zimeweka adhabu zitakazochukuliwa dhidi ya wale watakabainika kutaka kupita na fedha zinazolingana au zinazozidi kiwango kilichowekwa bila kutoa taarifa au watakaotoa taarifa za uongo. Alizitaja adhabu hizo kuwa ni pamoja na kukamatwa kwa fedha taslimu walizonazo na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kama vile kufunguliwa mashtaka.

“Wahalifu pamoja na mambo mengine, wanapenda kusafiri na fedha taslimu kwani wanaogopa kutumia benki kutuma fedha kutokana na umakini unaoongezeka katika benki na udhaifu unaoweza kuwepo mipakani” Alisisitiza Bw. Makombe.Kamishna huyo amewaasa washiriki wa warsha hiyo kutekeleza jukumu hilo kwa uadilifu na uaminifu mkubwa ili kuziba mianya yote ambayo wahalifu wanaweza kuitumia kutimiza kusudi lao ovu na kuhatarisha usalama wa nchi.

Kutokana na umuhimu wa ushiriki wa wadau mbalimbali katika utekelezaji wa kanuni hizo warsha hiyo imejumuisha washiriki kutoka taasisi mbalimbali wengi wao wakiwa ni maafisa forodha.

Washiriki hao wametoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kikanda, Mamlaka ya Mapato Tanzania na vikosi vya ulinzi na usalama

Wengine ni Bodi ya Mapato Zanzibar, Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo-Zanzibar, Shirika la Posta, Benki kuu ya Tanzania, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka-Zanzibar, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka-Tanzania Bara Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania Bara na Zanzibar, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Idara ya uhamiaji na Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu.

MAFUNZO YA MFUMO MPYA WA TEHAMA KUANDA MIPANGO YA BAJETI ZA MAMLAKA ZA SERIKALI WAFUNGULIWA MOROGORO

$
0
0
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro, Clifford Tandari, akifungua mafunzo ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Tehama utakaotumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta zote za umma nchini, mkoani Morogoro jana. Mafunzo hayo yanafadhiliwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).Mkurugenzi Msaidizi wa Miundombinu ya TEHAMA, Ofisi ya Rais Tamisemi, Baltazar Kibola, akiwasilisha mada juu ya mfumo mpya wa Tehama ulioboreshwa ujulikanao kama ‘PlanRep’ utakaoanza kutumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta zote za umma, mkoani Morogoro jana. Mafunzo hayo yanafadhiliwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).
Meneja Mifumo ya TEHAMA kutoka Mradi wa PS3, Revocatus Mtesigwa, akizungumza na washiriki wa mafunzo ya namna ya kutumia mfumo mpya ulioboreshwa wa Tehama (hawapo pichani) utakaotumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa, mkoani Morogoro jana 
Washiriki wa mafunzo ya mfumo mpya ulioboreshwa wa Tehama utakaotumika kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka za Serikali za Mitaa na sekta zote za umma, wakifuatilia mada mbalimbali zinazotolewa na wataalam kutoka Tamisemi na Mradi wa PS3, mkoani Morogoro jana. Mafunzo hayo yanafadhiliwa Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID).

HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA YASHINDWA KUTEKELEZA AGIZO LA KAMATI YA LAAC

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi akimkabidhi mmoja wa madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba cheti cha mafunzo ya udiwani aliyopata na ambayo yatawawezesha madiwani wote kutambua majukumu pamoja na mipaka yao ya kazi.(Picha zote Na Jumbe Ismailly).
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi akisisitiza juu ya maafisa watendaji wa vijiji 30 walioiba fedha za chakula cha njaa kuhakikisha wanazirejesha ifikapo aug,30,mwaka huu na kupendekeza njia rahisi ya fedha hizo kurejeshwa kuwa ni kuanzishwa kwa Mahakama tembezi itakayomtembelea kila mdaiwa na kuuza mali alizonazo ili kulipia deni la chakula hicho cha njaa walizokula.

Na Jumbe Ismailly IRAMBA 

HALMASHAURI ya wilaya ya Iramba,Mkoani Singida imeshindwa kutekeleza agizo la kamati ya kudumu ya Bunge la kutenga asilimia kumi kutoka kwenye mapato yake ya ndani kwa ajili ya vikundi vya wanawake pamoja na vijana katika kipindi cha kuanzia mwaka wa fedha wa 2012/2013 hadi 2014/2015.

Kaimu Mweka Hazina wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba,CARROLINE DALULI aliyasema hayo kwenye taarifa aliyotoa kwenye mkutano wa Baraza maalumu la madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo lilipokutana kujadili hoja za Ukaguzi na Mpangokazi wa utekelezaji wa maoni yaliyotolewa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka 2015/2016.

“Kamati iliagiza Halmashauri kuchangia asilimia kumi kutoka kwenye mapato ya ndani kwa ajili ya wanawake na vijana kwa miaka hiyo iliyotajwa na kiasi kilichoonekana”alifafanua kaimu Mweka Hazina huyo.

Kwa mujibu wa Kaimu Mweka hazina huyo kwa mwaka 2012/2013,2013/2014 na 2014/2015 Halmashauri ya wilaya ya Iramba haijatekeleza agizo la kamati ya kudumu ya Bunge kwani hakuna fedha yeyote ile iliyotengwa na iliyopelekwa kwenye vikundi hivyo.

Aidha Daluli aliweka bayana pia kwamba kwa mwaka 2016/2017 Halmashauri hiyo imechangia shilingi milioni mbili,zikiwemo shilingi milioni moja kwa Mazega Kisimba na shilingi zingine milioni moja kwa kikundi cha Maendeleo Shelui na itaendelea kuchangia kadri fedha zitakapopatikana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Huduma za jamii wa Halmashauri hiyo,Hamisi Kinota akichangia hoja hiyo ya michango ya vikundi vya wanawake na vijana alisisitiza kwamba kutokana na uchangiaji wa Halmashauri hiyo unadhihirisha wazi kwamba Halmashauri haitaweze kuchangia michango hiyo kwa asilimia mia moja.

Hata hivyo Kinota huku akionyesha hofu ya utekelezaji wa agizo hilo la kamati ya kudumu ya Bunge alibainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2012/2013,2013/2014 na 2014/2015 kati ya shilingi milioni 109,819,388 zilizotarajiwa kutumika,ni shilingi milioni mbili tu ndizo zilizotolewa na hivyo kubakiza zaidi ya shilingi milioni 107,hali ambayo inaonyesha hakuna uwezekano kwa Halmashauri hiyo kumaliza deni hilo kwa asilimia mia moja.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi alishauri kwamba njia pekee ya kumaliza deni hilo la michango ya vikundi vya wanawake na vijana ni kuandika maandiko mbali mbali na kusambaza kwa wafadhili na kudai kwamba kuna watu wenye fedha walio tayari kuwasaidia wanawake na vijana.

“Mtakapopata hizo fedha najua mnaweza kupata hata zaidi ya shilingi milioni mia mbili,mtakapopata hizo fedha mtaaandika kwamba ni fedha ambazo ninyi wenyewe Halmashauri mmezitafuta kwa hiyo itakuwa ni sehemu ya mapato yenu na mtazipeleka kwa wanawake na vijana”alisisitiza Dk.Nchimbi.

Seven Opportunities in the Uganda-Tanzania Pipeline Project and How to Participate.

$
0
0
THE EAST African oil pipeline (or the Uganda-Tanzania pipeline is the talk of the town now. Not only in East Africa but all over the globe.
The construction of this pipeline is officially on. Social and resettlement planning services have been undertaking it in Tanzania.

The sad reality is that people don’t know about the business opportunities available in the project.
More and more people keep wondering what the opportunities emerging in this project are and how they can be part of it.
“Do they offer equipment or provide services?” they ask themselves.
If you are among these people seeking to do business in this projects but have no idea how to get started, then no need to worry.
This article shows you some opportunities available in the project and how you can participate so that you can reap a substantial profit.
The Tanzania-Uganda Pipeline Opportunities
  1. Pipes and connection supplies: One of the opportunities in this project is to supply and manufacture seamless tubes and pipes (LSAW) and also supplying steel pipes.
  2. Chemical Supplies: For the construction of the pipelines, there are a lot of specialty chemicals needed, from corrosion inhibitors additives to scale remover to chemicals that reduce paraffin build up. You cannot run a pipeline without these things, and you can get them from China really cheap. Which means your profit margin may increase by 30-50 percent.
  3. Pipeline equipment supplies: These cover all materials that are required in the pipeline transportation system. It includes fittings, valves, scraper traps, insulating flanges, flow tee, pumping station, etc.
  4. Civil engineering works: These include building construction work, construction and maintenance of roads, construction and maintenance of drainage system, etc.
  5. Pipeline inspection services.
  6. Food supply.
  7. Security services.
Are you ready to utilize opportunities in this project? Here is how to grab the opportunities:
1. Identify the decision makers and influencers in this Uganda-Tanzania pipeline project.
The first step in pursuing opportunities in the Uganda-Tanzania pipeline is determining who the decision makers are.
Decision makers are the people who can approve or disapprove your proposal.
No matter how big a company is, there are decision makers who can approve or disapprove documents.
This can be easily achieved by making a list of key players in the project and starting to build long term relationship with them.
2. Demonstrate your experience.
You should demonstrate that you are the right person to execute the project you’re proposing.
You should demonstrate your capability and your experiences in executing similar project.
“What if my business is small and new n the industry?” you may ask.
Well, the answer is pretty simple. You still have a chance to tap opportunities in the Uganda-Tanzania pipeline project.
If your business is small and new, and you don’t have any experience or working history to be taken as references to the service you want to render, you should consider going into a joint venture with an experienced contractor in the oil and gas industry in such bidding venture. However inexperienced, you still have a chance to participate in this work.
You have learned the opportunities in the East Africa pipeline project and you now know how to access them.
If you want to learn more about the opportunities in the Tanzanian oil and gas sector and how you can grab them, click here to know more.

WHC WAFUNGUA DIRISHA JIPYA LITAKALOWEZESHA WATUMISHI WA SEKTA BINAFSI KUWEZA KUNUNUA NYUMBA.

$
0
0
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Raphael Mwabuponde akifafanua jambo wakati wa kufungua dirisha jipya  litakalowezesha watumishi wa sekta binafsi  kuweza kununua nyumba zake kwa garama nafuu na kuwainua kiuchumi. katikati ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC),  Dkt. Fred Msemwa na kulia ni Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC),  Maryjene Makawia.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC),  Dkt. Fred Msemwa (Katikati)akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kufungua dirisha jipya  litakalowezesha watumishi wa sekta binafsi  kuweza kununua nyumba zake kwa garama nafuu na kuwainua kiuchumi. Kushoto  ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Raphael Mwabuponde na Kulia ni Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC),  Maryjene Makawia.
kulia ni  Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC),  Maryjene Makawia akizungumza na waandishi wa ahabari jijini Dar es Salaam leo. kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC),  Dkt. Fred Msemwa.

Kulia ni Afisa Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Irene Kasanda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC), Raphael Mwabuponde, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi Housing Company (WHC),  Dkt. Fred Msemw na Afisa Uhusiano na mauzo wa Watumishi Housing Company (WHC),  Maryjene Makawia.
Picha na Avila Kakingo, Blog ya Jamii.
 
Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.
WATUMISHI Housing Company (WHC),  wamefungua dirisha jipya  litakalowezesha watumishi wa sekta binafsi  kuweza kununua nyumba zake kwa garama nafuu na kuwainua kiuchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa WHC,  Dkt. Fred Msemwa, amesema, dirisha hilo ambalo litajumuisha Watumishi wote wale wa umma na wa binafsi, litawawezesha wafanyakazi wote kuwa na makazi bora kupitia umiliki wa nyumba kwani nyumba hizo wanaweza kuzitumia kwa kukopa kuanzisha miradi mbali mbali ya uchumi.

Amesema Watumishi hao wa sekta binafsi ambao nao wanapata fursa ya kununua nyumba hizo ni wale ambao hawako katika utumishi wa umma lakini wanachangia katika mifuko ya pensheni.

Ameongeza kuwa, wigo huo mdogo unatokana na mahitaji ya wengi kwani watu wengi ukitoa Watumishi wa umma ambao hapo awali ndio walikuwa na sifa ya kununua nyumba hizo,wanashida ya makazi bora na ya kisasa

"Kufuatia uamuzi huu, WHC sasa itakuwa ikiwahudumia Watumishi wa umma pamoja na wafanyakazi wengine walioko katika sekta binafsi ikiwa ni muendelezo wa juhudi za Serikali na mifuko ya hifadhi ya jamii katika kuwawezesha wafanyakazi wote kuwa na makazi bora na kuwainua kiuchumi kupitia umiliki wa nyumba", amesema Dkt Msemwa.

Naye Mkuu wa Kitengo cha mauzo na masoko wa WHC, Raphael Mwabuponde amewaalika watanzania wote wenye uhitaji wa nyumba hizo, kutuma maombi kwa kuchukua fomu katika tovuti ya WWW.whctz.org.
Ameongeza mpaka sasa bado kuna nyumba za kuuza zilizopo Bunji B, Gezaulole Kigamboni, Mkundi Morogoro, Mwanza Kisesa na Njedengwa Dodoma.

MASAUNI AFANYA MKUTANO NA ASKARI WA USALAMA BARABARANI NA MADEREVA BODABODA.

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza maswali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, wakati alipotembelea Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mjimwema, Wilayani Kigamboni   kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Gilles Muroto na anayefuatia ni Mkuu wa Utawala Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benadict   Kitalika.
 Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akimuonyesha eneo linapotakiwa kujengwa kituo cha Polisi Kibada, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya naibu waziri,wilayani Kigamboni, Dar es  Salaam.
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akikagua moja ya chumba cha mahabusu ndani ya kituo cha Polisi Mwasonga, wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya polisi wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa.
 Muonekano wa nje wa Kituo cha Polisi cha Mwasonga kilichopo wilayani Kisarawe, kikiwa katika hatua za mwisho kabla ya ujenzi wake kukamilika.
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na madereva bodaboda wakati wa ziara ya kikazi wilayani Kigamboni   ambapo aliwaasa madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani pindi wafanyapo shughuli zao ili kuepuka ajali.
 Muendesha Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Said Athumani, akimuuliza maswali   Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri huyo wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo.
Muendesha Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Fredrick Swai, akimuuliza swali   Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri huyo wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

WATANZANIA WAKARIBISHWA KUSHIRIKI MCHEZO WA KUBAHATISHA WA TATU MZUKA.

$
0
0

Mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Daniel Wilson akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa habari na Bahati nasibu ya Tatu Mzuka na kuwasii watanzania kutumia nafsi kushiriki katika mchezo huo ambao unaanzia kwa shilingi 500.
Mratibu wa Mawasiliano wa Mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka Sebastian Maganga, akizungumza hadi shilingi  na Waandishi  juu faida za mchezo huo na namna ya kucheza na kufanikiwa kupata Milioni 30.
Balozi wa Mchezo wa kubahatisha wa Tatu Mzuka,  Mc Ray Maharufu kama Chikunde  akizungumza juu ya yeye kuhusishwa na kampuni inayoendesha mchezo huo wa Tatu Mzuka.
Waandishi wa habari walioshiriki katika Mkutano huo na Waandishi wa habari na Kampuni ya mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka.
Kiongozi kutoka Mchezo wa Kubahatisha wa Tatu Mzuka, Mudy B akizungumza na Waandishi wa habari namna ya kushiriki kupitia simu zetu za Mkononi.

COKE STUDIO AFRIKA YACHANGIA KUPAISHA KAZI ZA WASANII NCHINI TANZANIA.

$
0
0
Baadhi ya wasanii wa Tanzania waliowahi kushiriki Coke Studio. *Imetangaza pia muziki wa Bongo Fleva Onyesho maarufu la muziki la Coke Studio Africa, ambalo hivi sasa limeingia katika awamu ya tano chini ya udhamini wa kampuni ya Coca-Cola, limechangia kwa kiasi kikubwa kutangaza wasanii wa Tanzania waliofanikiwa kushiriki na kazi zao nje ya nchi hususani wanaopiga muziki wa Bongo Flava. Kazi za wasanii zimejulikana kutokana na mtindo unaotumika katika onyesho hili la kuwakutanisha wasanii nguli kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo hufanya kolabo za pamoja ambazo zinarushwa kupitia vituo vya luninga na kufuatiliwa na wapenzi wengi wa muziki kupitia mitandao ya kijamii. Baadhi ya wasanii kutoka Tanzania ambao wameshiriki onyesho hili tangu lianzishwe ni Lady Jaydee, Diamond Platnumz, Vanessa Mdee, Alikiba, Joh Makini, Shaa, Fid Q, Ben Pol, John Makini, Shaa, Nahreel na msimu huu wa tano wapo Rayvanny, Izzo Bizness na Nandy. Misimu minne iliyopita ya Coke Studio Africa imekuwa na mafanikio makubwa katika kuutangaza muziki wa Bongo Flava barani Afrika. Wamejiongezea mashabiki, wamejifunza mambo mbalimbali kuhusu muziki kama burudani, muziki kama taaluma na muziki kama biashara na tena si tu kutoka kwa wasanii wenzao wa Afrika na Marekani pia. Vilevile wasanii wote ambao wamepita kwenye onyesho hili wameendelea kupata mafanikio makubwa ya kimuziki kutokana na kazi zao kuendelea kutamba na kukubalika kwa wengi ndani na nje ya Tanzania. Taarifa kutoka kampuni ya Coca-Cola iliyotolewa hivi karibuni imeeleza kuwa onyesho la Coke Studio Africa, ambalo umaarufu wake umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka msimu huu utakuwa na burudani za aina yake kutoka kolabo za wasanii nguli barani Afrika kuanzia Afrika Magharibi mpaka Afrika ya Kusini na litarushwa na vituo vya luninga kwenye nchi zaidi ya 30 barani Afrika.  
Tangia onyesho hili lianzishwe limekuwa kiungo kikubwa cha kuwakutanisha wanamuziki wa Afrika kufanya kazi kwa pamoja na kupiga muziki wenye vionjo kutoka sehemu mbalimbali za Afrika ikiwemo kuleta burudani kubwa kwa washabiki wa muziki wa kiafrika na kuwaunganisha waafrika hususani vijana kupitia muziki. Katika msimu wa Coke Studio Africa unaotarajia kuanza kurushwa kwenye luninga mapema mwezi ujao unashirikisha wasanii kutoka katika nchi za Kenya, Afrika ya Kusini, Uganda, Tanzania, Rwanda, Ethiopia, Nigeria, Ghana, Angola, Zimbabwe, Togo, Cote d’Ivoire, Madagascar, Mauritius, Msumbiji, DRC na Cameroon.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA BILL GATES NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI NCHINI

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa  tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. Bill Gates aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa  tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. ill Gates aliyemtembelea  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiagana na Mwenyekiti wa  tasisi ya Bill and Melinda Gates Foundation Bw. Bill Gates aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017. Pamoja nao ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (kulia), Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dk Charles Tizeba (wa tatu Kushoto), Msaidizi wa rais Masuala ya diplomasia Bi. Zuhura Bundala (kushoto)  pamoja na maafisa alioongozana nao Bw. Bill Gates

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akisalimiana na  Kaimu Balozi wa  Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwa katika mazungumzo na   Kaimu Balozi wa  Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea  Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akimsindikiza Kaimu Balozi wa  Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiagana na  Kaimu Balozi wa  Marekani nchini Bi. Immi Patterson aliyemtembelea na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 10, 2017.PICHA NA IKULU.

NEEMA KWA WENYE UHITAJI WA MIGUU BANDIA.

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda amefanikiwa kupata MIGUU YA BANDIA ya Kuhudumia wananchi MIA MBILI (200) itakayoweza kuwasaidia wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wenye mahitaji.

Miguu hiyo yenye thamani ya Shilingi Milion 600 hadi bilioni 1.2 ENDAPO watu wote 200 watahitaji miguu yote miliwi itatolewa bila BILA MALIPO (bure) kwa wananchi waliopata ajali na kushimdwa kupata miguu hiyo kutokana na kushindwa KUMUDU gharama za kununua miguu hiyo ambapo kwa MGUU mmoja unagharimu Milion TATU (3,000,000)

Mhe MAKONDA amewataka wananchi WOTE wenye UHITAJI wa miguu ya BANDIA NA ambao hawana UWEZO wa kumudu GHARAMA kufika ofisini ya mkuu wa mkoa siku ya Jumatatu Tarehe 14/08/2017 na Jumanne Tarehe 15/08/2017 kwaajili kukutana na wataalamu wa miguu watakaochukua VIPIMO kwaajili ya kutengenezewa miguu kulingana na maumbile yao.

"Nimepewa kazi ya MKOA kuhudumia MAKUNDI yote, nafahamu kwenye mkoa wangu wapo waliopata ajali na wengine wakavunjika miguu lakini PESA ya kupata miguu ya BANDIA ili waachane na magongo kwao imekuwa ni moja ya CHANGAMOTO, kutokana na sababu hiyo nimeona vyema nifikiri namna ya KUWASAIDIA wananchi ambao hawana UWEZO ili waweze kupata, nimefanikiwa kupata wadau watakaonipatia miguu ya kuhudumia wananchi 200" Nahii ni awamu ya kwanza ,Alisema Makonda.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
10/08/2017

TFS Kukusanya maduhuli kieletroniki

$
0
0
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imeanza utekelezaji wa ukusanyaji wa maduhuli kwa njia ya kielectroniki kufuatia marekebisho ya sheria ya fedha ya mwaka 2017 na maelekezo ya serikali ya awamu ya tano ambao umezitaka Taasisi za serikali kujiunga na mfumo wa ukusanyaji maduhuli uliosanifiwa na Wizara ya Fedha na Mipango unaoitwa Government electronic Payment Gateaway-GEPF.   
       
Akitoa ufafanuzi Mhasibu Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Bwana Peter Mwakosya amesema Mashamba yote na ofisi za Meneja (DFM's) za Taasisi hiyo zimeunganishwa katika mfumo huo.Aidha amesema kutokana na mazingira ya vizuia(checkpoints)  kutokidhi mahitaji ya mfumo huo na hasa kushindwa kuhifadhi vitendea kazi kama kompyuta na printa kwa sasa wakala inaendelea kuunganisha kwenye mfumo vizuia vyote kwa kutumia vifaa maalum (point of sales-POS). 
  Amebainisha kwamba vifaa hivi vitatumika kukusanya maduhuli na kuhakiki uhalali wa nyaraka zinazokaguliwa katika vituo vyote vya ukaguzi wa mazao ya misitu na nyuki kwa kipindi hichi ambacho tunaendelea kuunganisha vizuia kwenye mfumo moja kwa moja. 

Bwana Mwakosya amesisitiza Maduhuli yote yanayokusanywa kwenye vizuia yanawasilishwa Ofisi ya Meneja wa Misitu wa wilaya mapema ili yaingizwe kwenye mfumo pia amewakumbusha wateja wote wa Mazao ya Misitu na nyuki kuzingatia kwamba wanatakiwa kupata hati za madai (Bill) katika mfumo kabla ya kwenda kufanya Malipo. 

Aidha amewakumbusha wateja wa bidhaa za Misitu na nyuki kwamba stakabadhi zilizokuwazinatumika kabla ya mfumo huu (ERV) hazitaendelea kutumika katika vituo vilivyounganishwa na mfumo.

WAZIRI MKUU AMPA SIKU 15 MWEKA HAZINA WA SIKONGE, APATE MAELEZO YA KUTOKUSANYA MAPATO

$
0
0
*Ataka apate maelezo kwa nini ameshindwa kukusanya mapato

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amempa siku 15 Mweka Hazina wa Wilaya ya Sikonge, Bw. Evans Shemdoe ajieleze ni kwa nini ameshindwa kufikisha asilimia 80 ya makusanyo ya ndani.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo asubuhi (Alhamisi, Agosti 10, 2017) wakati akizungumza na watumishi na watendaji wa wilaya hiyo, mjini Sikonge.

“Nataka maelezo yakayoniridhisha ni kwa nini hamkufikisha asilimia 80 ya makusanyo ya halmashauri ambacho ni kiwango cha chini. Nzega TC wamefikisha asilimia 112, Kaliua wana asilimia 91, Nzega DC wana asilimia 80, ni kwa nini wewe umeshindwa kufikisha kiwango hicho?,” alihoji Waziri Mkuu.

“Ninataka nipate maelezo pia ni ipi mipango yenu ya kukusanya mapato kwa maeneo mliyoshindwa kufanya vizuri, na pia mmejipangaje kwa mwaka ujao wa fedha. Niyapate maelezo hayo ifikapo tarehe 25 Agosti,” amesema.

Alipopewa nafasi ya kujieleza, Bw. Shemdoe alisema wamefikisha asilimia 76.7 na wameshindwa kufikia lengo kwa sababu ya upungufu wa mvua katika msimu uliopita, hali ambayo ilichangia kushuka kwa mavuno ya zao la tumbaku miongoni mwa wakulima.

Hata hivyo, Waziri Mkuu aliwataka watumishi wa wilaya hiyo, washirikiane na watendaji na madiwani ili kuongeza mapato ya wilaya hiyo badala ya kuwaachia watendaji wa kata peke yao.

Jana, mara baada ya kupokea taarifa ya mkoa wa Tabora, Waziri Mkuu alizitaka Halmashauri tano kati ya nane za mkoa huo zitoe maelezo ni kwa nini zimeshindwa kufikisha asilimia 80 ya makusanyo kama ambavyo waliagizwa na Serikali.

“Halmashauri zilizovuka malengo ni tatu tu, Nzega TC, Kaliua na Nzega DC. Nataka taarifa za halmashauri zilizobakia ifikapo Agosti 25, wakijieleza ni kwa nini hawajafikia malengo ya ukusanyaji mapato yaliyowekwa ambayo ni asilimia 80,” alisema.

Taarifa ya mkoa huo inaonyesha makusanyo kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo:- Tabora Manispaa asilimia 64.1; Nzega Mji (asilimia 112); Nzega Wilaya (asilimia 80.8); Igunga (asilimia 64.6); Tabora (asilimia 77.3); Sikonge (asilimia 76.7); Urambo (asilimia 70.9) na Kaliua (asilimia 91.5).

Pia amezitaka Halmashauri zote zihakikishe zinafanyamakusanyo kwa kutumia mfumo wa kielektroniki. “Ukusanyaji wote wa mapato ni lazima ufanyike kwa mfumo wa kielektroniki. Halmashauri ambazo hazijafanya hivyo, zitumie makusanyo ya mwaka jana kununulia mashine za EFD. Hatutaki kuona risiti za kuandika kwa mkono zinatumika,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa mkoa wa Tabora uhakikishe wanapatikana watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika wilaya hiyo ili waweze kusaidiana na watendaji wa halmashauri hiyo kukusanya mapato.

“Hapa Sikonge naambiwa hakuna ofisi za TRA. Lazima tupate maafisa wa TRA katika kila Halmashauri ili watoe elimu na washirikiane na madiwani, watendaji wa vijiji na watumishi wa Halmashauri juu ya ukusanyaji mapato,” alisema.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
ALHAMISI, AGOSTI 10, 2017.

WAHALIFU 13 WAUAWA NA POLISI KIBITI

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Chini ni silaha  8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo. – Picha na Jeshi La Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,  IGP Simon Sirro  akionesha makasha ya risasi (magazine) ambazo  ni miongoni  mwa makasha 8 yaliyokuwa yakitumiwa na wahalifu  katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kushoto  ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na  Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. Katika tukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua wahalifu 13 ambao walikuwa wakifanya mauaji  Kibiti. – Picha na Jeshi La Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini,  IGP Simon Sirro  akielezea  baadhi ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu  13 waliouawa  katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti   ambapo  jumla ya  silaha 8 aina ya SMG,  risasi  158, pikipiki 2, pamoja na  begi la nguo  vilivyokuwa  vikitumiwa na wahalifu hao.  Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (CP) Robert Boaz.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro  akionesha silaha aina ya SMG ambayo ni miongoni mwa silaha 8  zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi  katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kulia  ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na  Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. – Picha na Jeshi La Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro  akiongea na wananchi wa Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti alipokuwa akitoka kukagua eneo la tukio walipouawa  wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi  katika eneo la Tangibovu. (Picha na Jeshi La Polisi.)

MASAUNI AKAGUA UJENZI WA VITUO VYA POLISI, AFANYA MKUTANO NA ASKARI WA USALAMA BARABARANI NA MADEREVA BODABODA

$
0
0
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akimuuliza maswali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, wakati alipotembelea Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mjimwema, Wilayani Kigamboni kukagua maendeleo ya ujenzi huo. Kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke, Gilles Muroto na anayefuatia ni Mkuu wa Utawala Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Benadict Kitalika 
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, akimuonyesha eneo linapotakiwa kujengwa kituo cha Polisi Kibada, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya naibu waziri,wilayani Kigamboni, Dar es Salaam.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akikagua moja ya chumba cha mahabusu ndani ya kituo cha Polisi Mwasonga, wakati wa ziara ya ukaguzi wa vituo vya polisi wilayani Kigamboni, jijini Dar es Salaam.Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa.
Muonekano wa nje wa Kituo cha Polisi cha Mwasonga kilichopo wilayani Kisarawe, kikiwa katika hatua za mwisho kabla ya ujenzi wake kukamilika.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na madereva bodaboda wakati wa ziara ya kikazi wilayani Kigamboni ambapo aliwaasa madereva hao kufuata sheria za usalama barabarani pindi wafanyapo shughuli zao ili kuepuka ajali.
Muendesha Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Said Athumani, akimuuliza maswali Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri huyo wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo. 
Muendesha Bodaboda wa Wilaya ya Kigamboni, Fredrick Swai, akimuuliza swali Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), wakati wa Mkutano ulioitishwa na naibu waziri huyo wakati wa ziara ya kikazi wilayani humo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images