Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live

Dkt. Chamuriho, MAB wakagua ujenzi Kiwanja cha ndege cha Songwe

$
0
0
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (wa pili kutoka kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB), Prof. Ninatubu Lema (wa pili kutoka kushoto), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Salim Msangi (wa kwanza kushoto) na wajumbe wengine wa MAB wakisikiliza maelezo yanayohusu jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa Songwe kutoka kwa wahandisi, walipotembelea ujenzi huo leo.
 Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Drk Leonard Chamuriho (kulia) akitoka ghorofa ya kwanza ya jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe, Mbeya, mara baada ya kufanya ukaguzi na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB). Wanne ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Salim Msangi.
 Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Ujenzi ya UNETEC, Roupina Jambazian (aliyenyoosha kidole), akitoa maelezo ya ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege ya Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi.
 Katibu Mkuu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (aliyechuchuma) akishika upana wa barabara ya kuruka na kutua ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe baada ya kupata maelezo kutoka kwa Wahandisi Washauri wa Kampuni ya UNETEC. Mhandisi Roupina Jambazian na Geofrey Asumenye (walioinama), baada ya kufanya ziara pamoja na wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya ndege (MAB) ya kukagua maendeleo ya ujenzi  wa miundombinu.
Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB) na Katibu Mkuu wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho (wa kwanza kushoto)  wakikagua barabara ya kutua na kuruka kwa ndege ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Songwe. Wa pili kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vyua Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi.

Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Serkta ya Uchukuzi), Dr. Leonard Chamuriho leo kwa kushirikiana na Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (MAB), wamefanya ukaguzi wa miundombinu ya barabara ya kutua na kuruka kwa ndege na jengo la abiria la Kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Songwe Mbeya.
Tayari ujenzi wa barabara ya kutua kwa ndege yenye urefu wa km. 3.3 umekamilika ambapo inaruhusu kutua kwa ndege zenye uwezo wa kubeba abiria kuanzia 90 hadi 300, ambapo ndege za mashirika mbalimbali ikiwemo ya ATCL, Precisions na Fastjet zimekuwa zikifanya safari zake mara kwa mara kwenye kiwanja hiho.
Kiwanja hicho kipi daraja la sita (category 6), ambapo mbali na ndege za abiria pia kinaruhusu kutua kwa ndege za mizigo ya mazao ya kilimo yakiwemo maua, matunda, nyama, mchele na maharage kupelekwa maeneo mbalimbali nchini na nje ya nchi.
Hatahivyo, pia kimekuwa njia kuu inayotumiwa na watalii na wageni wanaotembelea mbuga za wanyama za Ruaha na Kitulo, pia katika vivutio vingine kikiwemo Kimondo kipo Mbozi, Daraja la Mungu lipo Rungwe na Ziwa Ngozi lililopo juu yam lima baada ya shimo la volkano kujaa maji na kugeuka ziwa.
Ujenzi wa jengo hilo la abiria litakalokuwa na uwezo wa kuhudumia abiria milioni 1.5 kwa mwaka tofauti na jengo la awali linachukua abiria 500,000 pekee, unatarajiwa kumalizika baada ya miezi sita kutoka sasa.

TSN & TBC KUWAKUTANISHA PAMOJA WAGOMBEA URAIS TFF KATIUKA KIPINDI MAALUM

$
0
0
KAMPUNI ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) kesho Ijumaa (Agosti 11, 2017)wameandaa kipindi maalum kwa wagombea Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kitakachofanyika mjini Dodoma kuanzia majira ya saa 3 usiku.

Kipindi hicho maalumu kitarushwa mubashara kupitia TBC pamoja na ‘TSN Online’ kitawakutanisha wagombea urais; Ally Mayay, Fredrick Mwakalebela, Wallece Karia, Shija Richard, Iman Madega na Emmanuel Kimbe ikiwa ni saa chache kabla ya siku ya uchaguzi yaani kesho kutwa Jumamosi.

Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya kipindi hicho, Enock Bwigane alisema kuwa ili mpira wa miguu uendelee kukua nchini TBC na TSN iliona ni vyema ikawakutanisha wagombea kwenye jukwaa moja ili waweze kuwaambia wananchi ni kwa njia gani wataweza kuinua soka la Tanzania kama wakipewa dhamana hiyo.

Alisema, “Kuna takribani wapiga kura 130, wagombea urais ni sita lakini mmoja ndiye atakayeshinda na kuongoza shirikisho hilo kwa miaka minne kabla ya uchaguzi mwingine hivyo tumeona haja ya kuwakutanisha na kuwawezesha wananchi waweze kuwafahamu...

“…Naamini fursa ya kuwakutanisha na kuwapa nafasi ya kuwaeleza watanzania sera na mipango yao ya kuboresha soka ni jambo la msingi na ni haki yao ukizingatia kuwa leo ndiyo siku ya mwisho ya kampeni,” alisema Bwigane.

Naye Katibu wa kamati hiyo, Alfred Lasteck alisema kuwa TSN ikishirikiana na TBC inatambua nini watanzania wanataka kufahamu kuhusu mpira wa miguu na ndiyo maana imepanga kuwakutanisha wagombea ili waweze kuzungumza na umma kabla ya uchaguzi hapo kesho.

“Kuna zaidi ya Watanzania milioni 50 ambao wangependa kufahamu ni nini kitasaidia soka la Tanzania ili liweze kuendelea kutoka lilipo sasa hadi kufikia mafanikio.

“Hivyo ni nafasi ya kipekee kwa kila mtanzania kufuatilia matangazo mubashara yatakayorushwa na TBC1 pamoja na TSN Online kipindi kile ambacho wagombea wote wa Urais watakapokuwa wakielezea mipango yao kuhusu mpira wa miguu nchini,” alisema Lasteck.

WAFANYAKAZI WA TANESCO KUPITIA TUICO WAMPONGEZA RAIS MAGUFULI KWA KAMPENI YA "KA...TA" KWA KUONGEZA MAKUSANYO YA BILI ZA UMEME

$
0
0

Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO, Tawi la TANESCO, Bw. Hassan JM. Athumani, akizungumza wakati wa kutoa tamko la Wafanyakazi wa TANESCO kupitia chama chao cha TUICO kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kufuatia kampeni aliyoianzisha ya ukusanyaji wa madeni ya bili za umeme ijulikanayo kama "KA..TA". Tamko hilo alilitoa mbele ya wajumbe wa kamati kwenye ukumbi wa mikutano wa TANESCO makao makuu jijini Dar es Salaam, leo Agosti 10, 2017.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kupitia chama chao cha TUICO, wamemponegza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa mchango wake mkubwa katika kuendeleza sekta ya umeme nchini ambapo kampeni yake ya “KA..TA” imekuwa na mafanikio makubwa ambapo wale wadaiwa sugu sasa wanalipa madeni yao.

Akitoa salamu za pongezi kwa Rais leo Agosti 10, 2017, kwenye makao makuu ya TANESCO Ubungo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO, tawi la TANESCO, Bw.Hassan J.M Athumani, alisema, Mhe. Rais Magufuli, amewezesha TANESCO kukusanya madeni yake hata maeneo ambayo ilikuwa vigumu sana kulipa madeni.

“Wakati kampeni ya KA..TA ilipoanza mwezi Machi mwaka huu wa 2017, deni lilikuwa shilingi bilioni 275, kati ya hizo, taasisi za serikali pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), zilikuwa zinadaiwa shilingi Bilioni 180 wakati taasisi binafsi, zilikuwa zinadaiwa shilingi Bilioni 95.

Bw. Athumani alisema ZECO pekee tayari wamelipa shilingi bilioni 18, wakati taasisi za serikali yakiwemo majeshi wamelipa deni shilingi Bilioni 18 pia, huku wadaiwa binafsi (private) wamelipa shilingi bilioni 5 na hivyo kufanya deni lililolipwa kufikia Julai 2017, kufikia shilingi bilioni 41.

“Kampeni hii ya rais ya KA..TA, imewezesha TANESCO sasa kukusanya bili za umeme hadi asilimia 104 kwa mwezi kutoka asilimia 90 kwa mwezi kabla ya kuanza kwa kampeni hii.” Alifafanua Mkuu wa Fedha wa TANESCO Bw.Philidon Siyame

Ilipoanza kampeni ya KATA, mwezi Machi, 2016. Deni lilikuwa Bilioni, 275, Serikali na taasisi zake ilikuwa inadaiwa bilioni 180, ilikuwa ni taasisi za serikali wakati private ilikuwa 95 bilioni.

Hadi Julai tumekusanya Bilioni 41, ZECO imelipa bilioni 18, taasisi zingine za serikali zikiwemo zile nyeti, zimelipa bilioni 18., wakati private wamelipa bilioni 5.

Akieleza zaidi kuhusu mchango wa Rais katika kuliwezesha Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, kupeleka huduma za umeme kwa wananchi, Mwenyekiti huyo wa TUICO-TANESCO, Bw. Athumani, alisema Shirika kwa sasa limefanikiwa katika uanzishwaji na uendelezwaji wa miradi ya kimkakati kama vile mradi mkubwa wa ufua umeme kwa gesi asilia wa Kinyerezi II Megawati 240, ambapo Mheshimiwa Rais aliweka jiwe la msingi mara tu baada ya kuingia madarakani mnamo Machi 16, 2016 na unaendelea kwa kasi na ifikapo Mwezi Desemba mradi huu utaingiza umeme katika Gridi ya Taifa, pia upanuzi wa mradi wa Kinyerezi I (Kinyerezi I Extension) utakaotoa Megawati 185.

Aidha Mwenyekiti huyo amemsifu Rais, kwa kuliwezesha Shirika la Umeme nchini TANSCO kutekeleza miradi mikubwa ya umeme kwenye maeeno mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na mradi mkubwa wa usafirishaji umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka Mkoani Iringa hadi Shinyanga, Mradi mkubwa wa Gesi asilia wa Megawati 300 Somanga Fungu.

"Pia hivi karibuni ninyi ni mashahidi, serikali imesimamia uanzishwaji na uendelezwaji wa Mradi Mkubwa na muhimu kwa Taifa wa Rufiji Hydro Power Project wa Stieglers Gorge utakaofua zaidi ya Megawati 2,000 za umeme na kikubwa zaidi mradi huu utatekelezwa kwa fedha za ndani, kwa sisi wafanyakazi wa TANESC hiki ni kitu kikubwa sana na tuna kila sababu ya kumpongeza Mhe. Rais wetu." Aisisitiza.

Tunaamini kwa kasi hii umeme wa uhakika, Tanzania ya viwanda inawezekana. Alihitimisha kwa kusema.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO tawi la TANESCO, kutoka kushoto, Bw.Ahmed Mwinyi, ayewakilisha wafanyakazi upande wa uzalishaji umeme kwa njia ya mafuta (Themo Generation), Bw.Felix Lyimo, anayewakilisha wafanyakazi kutoak Kanda ya Dar es Salaam na Pwani na Bi.Asha Mtola, anayewakilisha wafanyakazi wanawake wa Shirika hilo wakisikiliza wakati tamko hilo likitolewa na Mwenyekiti wao. .
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt.Tito Mwinuka, (wapili kushoto), Naibu Mkurugenzi Mtendaji (uwekezaji), Mhandisi Khalid James, (wakwaza kushoto) na baadhi ya wajumbe wa TUICO, wakinakili yaliyokuwa yakisemwa na Mwneyekiti wa TUICO Bw. Athumani.
Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha (CFO), wa TANESCO ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya majadiliano ya TUICO, Bw.Philidon Siyame, (kushoto), Mwenyekiti wa TUICO-TANESCO, Bw. Hassan J.M Athumani, (katikati) na Kaimu Meneja Uhusiano TANESCO, Bi. Leila Muhaji, wakibadilishana mawazo baada ya mkutano huo.
Bi. Leila Muhaji akizungumza kwenye mkutano huo.
Bw.Siyame(kushoto) na Bw.Mwandu M. Chandarua, ambaye ni Katibu wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO-TANESCO 
Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya TUICO, Tawi la TANESCO, Bw. Hassan JM. Athumani, akizungumza wakati wa kutoa tamko la Wafanyakazi wa TANESCO kupitia chama chao cha TUICO kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kufuatia kampeni aliyoianzisha ya ukusanyaji wa madeni ya bili za umeme ijulikanayo kama "KA..TA". Katikati ni Katibu wa Kamati, Bw. Mwandu M.Chandarua, na Bw. Philidon Siyame.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji (uwekezaji), Mhandisi Khalid James(kushoto), akinakili, huku akiwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Mwinuka.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (wapili kulia), Naibu Mkurugenzi Mtendaji (Uwekezaji), Meneja wa Mradi wa Kinyerezi I, Mhandisi Simon Jilima, (wakwanza kushoto) na mjumbe wa TUICO, Bw.Ahmed Mwinyi, wakiimba wimbo maarufu wa wafanyakazi, (Solidarity Forever).

WAZIRI UMMY MWALIMU, WAZIRI SIMBACHAWENE NA BILIONEA BILLGATE WAZINDUA MFUMO WA MATUMIZI YA KIELEKTRONIKI KATIKA SEKTA YA AFYA

$
0
0
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam katikati ni Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates na kulia ni Waziri wa TAMISEMI Simbachawene.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akimkabidhi zawadi Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates wakati wa uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kushoto akionyesha kitabu cha mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam pamoja na Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates katikati na kulia ni Waziri wa TAMISEMI Simba Chawene.
Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya uliofanyika jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa sekta ya afya hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya unaosimamiwa na Taasisi ya Bilionea Billgate Bill & Melinda Gates uliofanyika jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates wa kwanza kushoto akisaini kitabu cha wageni wakati alipokutana na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa pili kushoto katika ofisi ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es salaam ili kuzindua mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa afya wa kwanza kulia ni Mwenyekiti mwenza wa Bill & Melinda gates foundation,bilionea Bill Gates na Katibu Mkuu Afya, Dkt. Mpoki Ulisubisya kushoto katika ofisi ndogo ya wizara hiyo jijini Dar es salaam ili kuzindua mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya.
Wadau mbalimbali wa sekta ya afya wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo pichani jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mpango wa mfumo wa matumizi ya kielektroniki katika sekta ya afya.

KATIBU WA CCM MKOA WA DODOMA AHIMIZA UMOJA,UPENDO NA USHIRIKIANO KATIKA KUITEKELEZA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Deogratius Ndejembi akizungumza na viongozi wa Chama na Serikali wa Tarafa ya Nzoisa wilayani humo katika semina ya kujenga uelewa wa namna ya kutekeleza majukumu yao kwa pamoja.
PICHA (2)
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Dodoma Jamila Yusuph akifungua semina hiyo kwa viongozi wa chama na serikali ngazi ya Tarafa ambapo amesisitiza ushirikiano,upendo na umoja katika kuitekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM iliyopo.
PICHA (3)
Baadhi ya viongozi wa Chama na Serikali wa Tarafa ya Nzoisa walioshiriki semina hiyo.
PICHA (4)
Katibu wa CCM mkoa wa Dodoma akiongoza viongozi wa Chama na Serikali wa wilaya ya Kongwa kuimba wimbo wa Chama katika semina hiyo,miongoni mwa viongozi hao yupo mkuu wa wilaya hiyo Deogratius Ndejembi,katibu wa CCM wilaya Mfaume Kizigo na mwenyekiti wa halmashauri White Zubeir.
…………………
Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma kimewakutanisha viongozi wa serikali na wa Chama ngazi ya Tarafa katika semina ya siku moja lengo likiwa ni kuwapa uelewa wa pamoja wakati wa  kutekeleza majukumu yao ya kazi.
Akifungua semina hiyo katika kata ya Nzoisa wilayani Kongwa Katibu CCM mkoa wa Dodoma Jamila Yusuph  amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa pamoja ili kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho kama ilivyoahidiwa.

Ili hilo litekelezeke amewaasa kujenga umoja na maelewano katika sehemu zao za kazi kwa kuelezana ukweli pale wanapoona kuna jambo haliendi sawa na kutatua kero za wananchi kama walivyoahidi.

Alisema viongozi wa Chama na Serikali wakiwa tofauti ilhali kazi ya kupeleka maendeleo kwa wananchi kutokana na Ilani iliyopo inapaswa kufanya kwa ushirikiano wanakuwa wanawakosea wananchi walioichagua CCM na kuiweka madarakani.

“Huwezi leo mtendaji wa kijiji au Kata unataka kukutana na wananchi lakini mwenyekiti wa CCM Kata au tawi hajui chochote,hujamshirikisha hapo tegemea mkutano wako kutofanikiwa maana Chama ndio kinakuwa na wananchi wakati wote na kina ushawishi,”alisema Jamila.

Aliwataka kufanya kazi kwa bidii ili yale anayoyafanya rais John  Magufuli yaweze kuonekana mpaka nchini kwa kuitekeleza Ilani kwa vitendo,kutatua kero na changamoto za wananchi,kutii sheria za nchi,kukemea kwa vitendo suala la rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.

Akizungumzia kuhusu uchaguzi ndani ya chama uliomalizika katika ngazi ya Kata amewataka wote walioshinda kuwaunganisha wana CCM popote walipo na waimarishe matawi na mashina.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kongwa Deo Ndejembi akizungumza katika kikao hicho aliwahimiza viongozi wa serikali kuitekeleza Ilani iliyopo na viongozi wa Chama wawasimamie ili kuhakikisha viongozi hao wanatimiza wajibu wao katika kutekeleza kile kilichoahidiwa kwa wananchi.

“Mwenyekiti wa Kata au Tawi lazima uulize lini mara ya mwisho kusomwa mapato na matumizi,lazima ujue mkutano umefanyika lini,bila ya kutatua kero za wananchi watanung’unika,watakuwa na nyongo na nyongo hiyo kuitema wataitema kwenye karatasi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020,

“Kuna watu wanasema mimi ni mkali,lakini jamani mfano wewe afisa elimu Kata,kuna mwalimu yupo mjini siku zote lakini hujui kama anafundisha,wananchi wanakereka na hali hiyo maana watoto wao hawafundishwi sasa nikae kimya?nikiuliza useme mi ni mkali?kwa kweli niiteni tu mkali lakini siwezi kukaa kuona mambo hayaendi halafu nikawa kimya,lazima kila kiongozi atekeleze wajibu wake na Ilani,”alisisitiza Ndejembi.

Naye katibu wa CCM wilaya ya Kongwa Mfaume Kizigo alisema lengo la kuwakutanisha pamoja viongozi hao ni kuhakikisha wanajenga nyumba ya CCM pamoja,kuepuka migogoro kati yao baada ya kila mtu kujua mipaka yake ya kazi na wanatarajia kuitoa katika tarafa zote zilizobaki ndani ya wilaya hiyo.

SERIKALI YAFUTA UMILIKI WA VIWANDA AMBAVYO HAVIJAENDELEZWA

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KATIBU MKUU WA JUMUIYA YA MADOLA MHE PATRICIA SCOTLAND IKULU JIJINI DAR ES SALAAM JIONI HII

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimlaki Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe Patricia Scotland Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Agosti 10, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe Patricia Scotland Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Agosti 10, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo  na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe Patricia Scotland Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Agosti 10, 2017 akiwa ameongozana na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro 
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na  Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe Patricia Scotland Ikulu jijini Dar es salaam jioni ya leo Agosti 10, 2017 akiwa kaongozana na  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro.

Picha na Ikulu

RAIS DK.SHEIN AZUNGUMZA NA BODI YA MIKOPO YA ELIMU YA JUU IKULU.

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na Uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu na Uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji, [Picha na Ikulu.] 10 /08/2017.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Maalim Kombo Hassan Juma (kushoto) alipokuwa akitoa maelezo na kuhusu Bodi yake wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,Bodi hiyo na Uongozi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu,wengine Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Said Hassan Saidi (katikati) na Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee,

Mkurugenzi wa Idara ya Mikopo ya Elimu ya Juu puia Katibu wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Nd,Iddi Khamis Haji alipokuwa akitoa taarifa ya Uongozi wa Wizara ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wengine (katikati) Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Maalim Kombo Hassan Jumaakifuatiwa na Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mhe.Said Hassan Saidi,[Picha na Ikulu.] 10/08/2017.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Elimu na Uongozi wa Baraza la Elimukatika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Elimu Bi.Sada Thani (kulia) alipokuwa akitoa taarifa yake wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,Bodi hiyo na Uongozi wa Baraza la Elimu,wengine ni Wajumbe wa Bodi,[Picha na Ikulu.] 10/08/2017.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Mitihani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), alipozungumza nao wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,Bodi hiyo na Uongozi wa Baraza la Mitihani,[Picha na Ikulu.] 10/08/2017.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Riziki Pembe Juma (wa pili kulia) alipokuwa kitoa mchango wake wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) kikao kilichojumuisha Bodi ya Wakurugenzi ya Baraza la Elimu na Uongozi wa Baraza la Elimu na Uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali,[Picha na Ikulu.] 10/08/2017.

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA MASHIRIKA YA KIPAPA YA VATICAN BABA ASKOFU PROTAS RUGAMBWA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya Sanamu ya  Bikira Maria wa Fatima kutoka kwa Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa aliyefika Ikulu jijini Dar es Salaam
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa wapili kutoka kushoto Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza na kumuaga mgeni wake Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa Ikulu jijini Dar es Salaam. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana  na  mgeni wake Rais wa Mashirika ya Kipapa-Vatican, Mhashamu Baba Askofu Protas Rugambwa Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

VIJUSO VYA MAGAZETI YA IJUMAA LEO AGOSTI 11,2017

Prince Amos - Kisha Nikaona (Official Music Video

WAFUGAJI LONGIDO WAANZA KUNUFAIKA NA UJENZI WA SOKO LA KISASA LA MIFUGO

$
0
0
Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido mkoani Arusha, Bw. Toba Nguvila (kushoto), akimweleza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (katikati) kabla ya kutembelea Soko la Kisasa Mifugo linalojengwa katika kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa, wilayani Longido, mkoani Arusha, linalojengwa kutokana na mkopo wenye masharti nafuu wa sh. Milioni 650 kutoka Benki hiyo. Kulia ni Afisa anayeshughulikia Dawati la Beni ya Maendeleo ya Afrika-AfDB kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Said Nyenge.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro akisikiliza maelezo ya mradi wa ujenzi wa Soko la Kisasa la Mifugo katika kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa, wilayani Longido mkoani Arusha, unaogharimu shilingi milioni 650, ikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu kutoka Benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, akisisitiza jambo baada ya kusikiliza maelezo ya mradi huo wa Soko la Kisasa la Mifugo linalojengwa katika kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa wilayani Longido mkoani Arusha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB, kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro (wapili kulia) akimweleza jambo Katibu Tawala wa wilaya ya Longido mkoani Arusha, Bw. Toba Nguvila, wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea na kukagua ujenzi wa Soko la Kisasa la Mifugo, linalojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 650 kupitia mkopo nafuu wa Benki hiyo kwa Serikali ya Tanzania.
Baadhi ya wafugaji wa kijiji cha Worendeke, kata ya Kimokouwa, wilayani Longido mkoani Arusha, wanaonufaika na uwepo wa soko hilo ambapo wameanza kuuza mifugo yao kwa faida kubwa badala ya kupeleka mifugo yao nchi jirani ya Kenya ambako walikuwa wakipata adha kubwa na faida ndogo kutokana na gharama kubwa walizokuwa wakitumia kufikisha mifugo yao nchini humo. (Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango) 
 
Benny Mwaipaja, WFM, LONGIDO-ARUSHA.

WAFUGAJI wilayani Longido Mkoani Arusha wameanza kunufaika na ujenzi wa soko la kisasa la mifugo linalojengwa na Serikali katika kijiji cha Worendeke kata ya Kimokouwa, kupitia mkopo wa fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB.

Baadhi ya wafugaji wamesema kuwa Soko hilo linalojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 650, limewaondolea adha kubwa waliyokuwa wakiipata walipokuwa wakiuza mifugo yao nchini Kenya kutokana na gharama kubwa ya kusafirisha mifugo kwenda huko pamoja na kulipa kodi na ushuru mbalimbali.

Wamesema kuwa kujengwa kwa somo hilo ni mkombozi mkubwa kwao na kwamba hali hiyo itasisimua uchumi wao kwa kuwa wafanyabiashara wa ndani na kutoka Kenya wamekuwa wakiwafuata kwenye soko hilo kununua mifugo yao hatua inayowafanya wapate faida kubwa.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Longido, Bw. Toba Nguvila, amesema kuwa soko hilo ambalo ujenzi wa miundombinu yake umekamilika kwa asilimia 85 limeanza kuiingiza Serikali mapato yake ambapo kwa wastani Halmashauri ya wilaya inakusanya wastani wa shilingi milioni 1 kwa siku.

“Asilimia 95 ya wakazi wa wilaya yetu ni wafugaji wa kimaasai ambao kwa kipindi kirefu wameteseka kusafirisha mifugo yao kwenda Kenya na kutopata faida kutokana na gharama kubwa ya kusafirisha, kupitisha mifugo kwenye maeneo ya watu hivyo kulazimika kulipa ushuru, halikadhalika kulipia tozo mbalimbali wakati wakisubiri kuuza mifugo yao” alieleza Bw. Nguvila

Alisema kuwa kuanzishwa kwa soko hilo litakalokuwa na miundombinu muhimu kama vile mizani ya kupimia uzito wa mifugo yao kabla ya kuiuza, si tu kwamba limesababisha wafugaji kupata faida kwa kuuza mifugo yao kwa bei nzuri ya soko, bali pia limeleta neema kwa wafanyabiashara wengine wadogo wakiwemo mamalishe.

“Akina mama wanafanyabiashara zao za kuuza chai na chakula huku kundi kubwa la vijana waliokuwa wakiuza bidhaa zao za kutembeza mikononi katika mpaka wa Kenya na Tanzania-Namanga, ambao wamejiajiri kwa shughuli za kushusha na kupakia mifugo kwenye malori” aliongeza Bw. Nguvila

Alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa mifugo inaongezewa thamani, mchakato wa kuanzisha kiwanda kikubwa cha kuchakata nyama kitakachokuwa na uwezo wa kuchakata mifugo 3,000 kwa siku kinatarajiwa kujengwa katika eneo la karibu na soko hilo kwa ajili ya kuuza nyama ndani na nje ya nchi

“Taratibu za kuanzishwa kwa kiwanda hicho zimekamilika na wakati wowote ujenzi wake utaanza hatua ambayo tunaamini watu wetu watanufaika zaidi na biashara ya mifugo kuliko ilivyokuwa hapo awali ikiwa ni juhudi za Serikali ya aAwamu ya Tano ya kuwahudumia wananchi wa hali ya chini ili kuboresha maisha yao” alisisitiza katibu Tawala huyo

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayesimamia nchi 7 za Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro, amesema Benki yake imefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa soko hilo litakalochochea uchumi wa wananchi.

Ameahidi kuwa Benki yake inafadhili ujenzi wa masoko mengi ya namna hiyo hapa nchini na nchini nyingine za Kiafrika ili nchi hizo ziweze kukuza uchumi wake na maisha ya watu wake kwa ujumla.

“Benki iko tayari kuendelea kusaidia eneo hili la ujenzi wa masoko ili kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi hivyo naushukuru uongozi wa mkoa wa Arusha na Wilaya ya Longido kwa kazi nzuri wanayoifanya kusimamia ujenzi wa soko hili na kwamba ujenzi wake utakamilika kwa wakati kama ilivyopangwa”Alisisitiza Dkt. Weggoro.

Benki ya Maendeleo ya Afrika-AfDB inafadhili ujenzi wa masoko kadhaa Tanzania Bara na Visiwani kupitia mkopo wenye masharti nafuu wenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 56 na unatekelezwa kupitia mpango wa kuendeleza miundombinu ya masoko, kuongeza thamani ya mazao na uboreshaji wa huduma za kifedha vjijini.

CHANGAMOTO ZA WASANII WA NYIMBO ZA INJILI ZAWEKEWA MIKAKATI YA KUTATULIWA

$
0
0








Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wasanii wa Nyimbo za Injili (hawapo pichani) wakati wa mkutano na wasanii hao kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare akifafanua jambo wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMWITA) Bw. Addo Novemba akiwasilisha changamoto zinazokabili muziki wa injili hapa nchini wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Mwanamuziki wa Nyimbo za Injili Bi. Christina Shusho akichangia hoja wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.
Waimbaji wa nyimbo za Injili wakitumbuiza wakati wa mkutano na wasanii wa nyimbo za Injili kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na viongozi kutoka serikalini pamoja na viongozi wa chama cha Muziki wa Injili Tanzania baada ya mkutano na wasanii hao kujadili changamoto zinazowakabili na namna ya kutatua changamoto hizo leo Jijini Dar es Salaam.

Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

…………………………….

CHANGAMOTO ZA WASANII WA NYIMBO ZA INJILI ZAWEKEWA MIKAKATI YA KUTATULIWA

Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Tarehe: 10/08/2017

Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe amekutana na wasanii wa nyimbo za Injili leo Jijini Dar es Salaam kusikiliza changamoto zinazoikabili tasnia ya muziki wa nyimbo za injili na kuweka mikakati ya kuzitatua changamoto hizo hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza wakati wa mkutano na wanamuziki wa nyimbo za Injili Mhe. Mwakyembe amesema kuwa serikali ina wajibu wa kufuatilia changamoto za tasnia ya muziki ukiwemo muziki wa injili na kuzitatua ili kuweza kukuza kazi za wasanii kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja na taifa.

“Muziki ni tasnia ambayo imewabeba vijana wengi hapa nchini, serikali ina wajibu wa kutetea, kulinda na kuhakikisha maslahi ya kazi za sanaa ikiwemo muziki wa injili inaheshimiwa na kulindwa” Amesema Mhe. Mwakyembe

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Chama cha Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bibi. Doreen Sinare amewataka Wasanii wa Muziki wa Injili kutoshawishiwa kutoa malipo yoyote katika vyombo vya habari ili nyimbo zao ziweze kuchezwa kwenye vyombo hivyo bali vyombo vya habari ndio vinapaswa viwalipa wasanii wakati wanapotumia nyimbo zoa.

Aidha Bibi. Doreen amewaomba waimbaji hao wa nyimbo za injili kutembelea ofisi za Bodi ya Filamu, Cosota na Basata ili waweze kupata ushauri wa namna ya kuandika mikataba bora na inayofaa wakati wa kutengeneza na kuandaa albamu za nyimbo za injili.

Naye Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMWITA) Bw. Addo Novemba amewataka Viongozi wa nyimbo za Injili Tanzania kuhakikisha kuwa wanafanya kazi bega kwa bega na serikali na kwa bidii katika kukuza, kuendeleza, na kulinda maslahi ya wanamuziki wa Injili.

Aidha Bw. Novemba ameiomba serikali kuhusisha wanamuziki wa nyimbo za injili katika matukio mbalimbali ya serikali na ya nchi kwani wasanii wa nyimbo za injili wamekua wakiimba nyimbo zinazojenga taifa na kuendeleza amani, upendo na ushirikiano wa nchi yetu.

KATIBU MTENDAJI BODI YA FILAMU AFUNGA SEMINA YA MAMENEJA WA USAMBAZAJI WA KAZI ZA FILAMU KUTOKA MIKOA 25 YA TANZANIA

$
0
0
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (katikati) akizungumza na mameneja wa usambazaji wa kazi za filamu (hawapo pichani) kabla ya kufunga semina elekezi kwa mameneja hao leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Barazani Entertainment Bw. John Kalage na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha uenezi Bw. Singo Mtambalike

Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Barazani Entertainment Bw. John Kalage (Kulia) alipotembelea ofisi hizo leo Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufunga semina ya mameneja wa usambazaji wa kazi za filamu kutoka mikoa 25 ya Tanzania.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (kushoto) akiteta jambo na viongozi wa Barazani Entertainment kabla ya kufunga semina ya mameneja wa usambazaji wa kazi za filamu kutoka mikoa 25 ya Tanzania leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni mkuu wa Mawasiliano kutoka Barazani Entertainment Bw. Jacob Steven na katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Barazani Entertainment Bw. John Kalage
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo (katikati) katika picha ya pamoja na viongozi wa Barazani Entertainment na mameneja wa usambazaji kazi za filamu baada ya kufunga semina elekezi kwa mameneja hao leo Jijini Dar es Salaam.

Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM

MAMA GRACA MARSHEL AZINDUA KITABU CHA WANAWAKE WALIOFANIKIWA KIUCHUMI AFRIKA

$
0
0
--

 Mke wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela , Mama Graca Marshel  akipiga makofi mbele ya Wanawake waliofanikiwa kiuchumi ambao wameandikwa katika kitabu  cha wanawake Afrika kuashiria uzinduzi wa Kitabu hicho katika Mkutano wa Advance Women Africa
 Mwandishi wa Kitabu cha Wanawake waliofanukiwa kiuchumi Afrika , Lisa O'Donoghue akifanya marejeo ya kitabu hicho kabla ya kuzinduliwa
 Mwandishi wa Habari kutoka Tanzania akitoa sori fupi ya Miasha na Mtoto wake , Ester Karin

 wanawake Mashuhuri nchini wakiwa katika mkutano huo wakijadili jambo kabla ya uzinduzi wa kitabu
  Mke wa Rais Mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela , Mama Graca Marshel , akiteta na Wanawake wajasiliamali nchini ambao  wameshiriki Mkutano wa Women Advance Afrika
 Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini
Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huo wakifatilia kwa makini

WAZIRI MKUU AWAONYA WATU WANAOCHUKUA DAWA KATIKA HOSPITALI ZA SERIKALI NA KUZIPELEKA KATIKA MADUKA YAO.

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia Wananchi wa Wilaya ya Sikonge Mjini leo Agosti.10.2017 katika viwanja vya Tasaf Waziri Mkuu yupo Mkoani Tabora kwa ziara ya Kikazi 


Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaonya wamiliki wa maduka ya madawa ya binadamu na watumishi wa sekta ya afya wanaochukua dawa ambazo zinapaswa kupelekwa katika Hospitali za Serikali ili kuwahudumia wananchi na kuziweka katika maduka yao.

Mhe. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana Wilayani Sikonge katika mkutano wa hadhara na wananchi katika Kiwanja cha TASAF.

Alisema kuwa vitendo hivyo ndivyo vimekuwa vikisababisha upungufu wa dawa katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali mbalimbali za Serikali na kufanya baadhi ya wananchi kuendelea kuteseka na maradhi kwa sababu ya kushindwa gharama za ununuzi wa dawa katika maduka ya watu binafsi.

Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa aliwaonya watumishi wa afya na wamiliki hao wenye tabia hizo kuacha mara moja endapo watabainika kuendesha vitendo hivyo watachukuliwa hatua kali.

Alisema kuwa Serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili kununua dawa ili zinasaidia kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi wake lakini kuna baadhi ya watumishi wa afya wasio waadirifu ambapo wamekuwa wakitorosha dawa na kuwauzia wamiliki wa maduka ya dawa na ksuababisha upungufu katika vituo vya Serikali.

Waziri Mkuu kuwa Serikali haiwezi kuwavilimia watumishi wa afya wasio waaminifu wanaochukua dawa na kuzipeleka katika maduka binafsi huku wakisababisha upungufu katika baadhi ya hospitali za umma.

Alisema kuwa hospitali ni lazima ziwe na dawa za kutosha ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameikabidhi Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tabora orodha ya watu wenye tabia ya kuwarubuni wakulima wa tumbaku na kununua katika mfumo ambao si rasmi na kisheria (soko huria) na kuwanyonya ili wahojiwe.

Alisema kuwa watu hao kwa muda mrefu ndio wamekuwa wakiwanyonya wakulima kununua tumbaku zao kwa vishanda na kuwa fedha ambazo zinazidi kuwakandamiza.

“Nina majina ya watu ambao wamekuwa wakipita kwa wakulima na kununua tumbakuza wakulima kwa njia ya vishada ….huku wakiwanyonya kwa kuwapa fedha kidogo nawataka waache mara moja.” Alisisitiza Mhe. Waziri Mkuu.

Aliongeza “leo siwataji majina yao lakini nakuachia Mkuu wa Mkoa ili wewe na Kamati yako ya Ulinzi na Usalama muwaite na kuwahoji na kisha ziwaonye wasiendelee na biashara hiyo, kama wanataka kuendelea na uuzaji wa tumbaku wahakikishe wanayopeleka sokoni ni ile waliolima wenyewe na sio ya kununua kwa wakulima”

Aidha Waziri Mkuu alitoa onyo kwa watumishi wa umma ambao wamekuwa na tabia ya kugonja wakulima walime tumbaku na wakisha kuvuna na kukausha wao wanakwenda kununua kwa ajili ya kuipeleka katika makampuni ya tumbaku.

Alisema mtumishi hakatazwi kulima kulima tumbaku bali atakiwi kununua tumbaku kutoka kwa mkulima.

Waziri Mkuu huyo aliwaagiza viongozi wa Mkoa wa Tabora kukamata watu wote wanajihusisha na ulanguzi wa tumbaku ya wakulima na kuongeza kuwa watakamatwa wakiwa na tumbaku ya ulanguzi ichukuliwe pamoja na chombo cha usafiri kinachotumika kusafirishia.

Alisema kuwa tumbaku yote inauzwa kupitia vyama vya msingi na kila mtu atauza tumbaku kwa kiwango alicholima.

DAWASCO YAANZA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI JUU YA MFUMO MPYA WA UTOAJI NA UPATIKANAJI WA TAARIFA MUHIMU

$
0
0
Mmoja ya waendesha bodaboda akimuuliza swali Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro juu ya matumizi ya mfumo mpya wa DAWSCO katika utoaji na upatikanaji wa taarifa.
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi Everlasting Lyaro akitoa elimu juu ya matumizi ya mfumo wa DAWASCO kwa kwa njia ya simu kwa watumiaji wa vyombo vya Moto hususani Bajaj na Pikipiki katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam. Mfumo huo umezinduliwa rasmi ili kutoa nafasi kwa wananchi kupata na kutoa taarifa sahihi za DAWASCO.
Mwendesha bajaji akihojiwana ITV juu ya matumizi ya mfumo mpya wa DAWASCO katika utoaji na upatikanaji wa taarifa.
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amewataka wananchi wa Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na hauna gharama zozote. Anasema ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata taarifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi, taarifa za lini mteja alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya malipo, lini mita yake ya maji ilisomwa na taarifa nyingine nyingi.
“Nawasihi wateja wetu na wananchi wote kupakua mfumo huu mpya katika simu zenu za mkononi ili kuweza kufurahia huduma zetu, hakuna gharama zozote ambazo utatozwa. Kupitia mfumo huu utaweza kupata taarifa zote muhimu za huduma ya majisafi zikiwemo taarifa za mivujo ya maji na ankara za maji za kila mwezi,”amefafanua Bi. Lyaro.
Amesema kwa sasa Wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika ufuatiliaji wa kuunganishwa huduma ya maji, bali kilichorahisishwa ni mteja kuweka taarifa zake sahihi kwenye mfumo huo na DAWASCO.

Mshindi wa Milioni 20 za Biko Kimara Suka akabidhiwa fedha zake

$
0
0
MSHINDI wa Shilingi Milioni 20 za Biko kutoka kwenye Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, Anthony Chitanda, amekabidhiwa fedha zake mapema jana katika benki ya NMB, Tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es Salam, sambamba na kupewa ushauri wa kifedha.

Chitanda aliibuka kidedea katika droo ya 30 ya Biko iliyochezeshwa juzi Jumatano na kuvuna Sh Milioni 20 zinazotolewa na waendeshaji hao wa Biko, mchezo wa kubahatisha unaoendelea kutingisha katika wilaya na mikoa mbalimbali ya Tanzania.


Akizungumza katika Makabidhiano hayo, Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles, alisema kwa kila anayecheza bahati nasibu yao, lazima ajiandae kulala masikini na kuamka tajiri.

Alisema ushindi wa Biko ni rahisi kwa wale wanaocheza kwa kutumia mitandao ya simu ya M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money ambapo namba ya Kampuni ni 505050 na kumbukumbu ni 2456, huku kianzio cha kuchezea Biko kikianzia Sh 1,000 na kuendelea.

“Mbali na kushinda Sh Milioni 20 kama alivyoshinda Chitanda na hatimae kumkabidhi fedha zake siku moja baada ya kushinda, pia Watanzania wanaweza kushinda zawadi za papo kwa hapo kuanzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja, huku wanaocheza mara nyingi zaidi kwa kufanya miamala kwenye simu zao wakiwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda zawadi za papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya Jumatano na Jumapili kwa ajili ya kuwania donge nono la Sh Milioni 20,” Alisema.

Naye Chitanda alisema kwamba fedha za Biko ni tamu inapotokea bahati ya ushindi, huku akisema amekubaliana na kauli mbiu ya Biko inayojulikana kama ushindi nje nje, kutokana na kuibuka kwake mshindi wa Sh Milioni 20 ambazo amekabidhiwa haraka.

“Nimekubaliana kwa kiasi kikubwa na kauli mbiu hii ya ushindi nje nje, maana awali nilijua sitaweza kushinda, lakini kwa kushinda kwangu, naomba niwaambie Watanzania wote waendelee kucheza Biko washuhudie nguvu ya Buku inavyozalisha mamilioni,” Alisema Chitanda.
Baada ya kukabidhiwa fedha zake pamoja na kupewa ushauri wa kifedha kutoka kwa wataalamu wa NMB, mshindi mwingine wa Biko wa Milioni 20 anatarajiwa kupatikana Jumapili hii kwenye droo ya 31.


Mshindi wa Biko droo ya 30, Anthony Chitanda, akionyesha shangwe zake baada ya kupokea fedha zake Sh Milioni 20 kutoka Biko kama sehemu ya ushindi wake.

Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Bahati Nasibu ya Biko, Hassan Melles kulia amkabidhi mshindi wao wa droo ya 30 Anthony Chitanda katikati katika benki ya NMB, Tawi la Bank House, Posta, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa wa NMB. Makabidhiano hayo yalifanyika jana mchana.
Mshindi wa droo ya 30 Biko Ijue Nguvu ya Buku, Anthony Chitanda kushoto akiwa na mke wake baada ya kukabidhiwa hundi ya fedha zake Sh Milioni 20 saa chache kabla ya kuelekea benki ya NMB, Posta jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukabidhiwa fedha zake jana.

NAIBU SPIKA WA BARAZA LA WAKILISHI ZANZIBAR AKUTA NA VITAL VOICES GROW MJINI UNGUJA

$
0
0
Image may contain: 1 person, sitting 
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni Hassan Juma  Akizungumza na Wanawake wa Kikundi cha Vital Voices Grow Kutoka Nchi za Kusini mwa Bara la Afrika Mjini Unguja.Kikundi cha Vital Voices Grow (VVGrow) kutoka Afrika Kusini  mwa Jangwa la Sahara (Sub-Saharan Africa) kwa mwaka 2015/2016  kimemtembelea Mheshimiwa Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni Hassan Juma katika ofisi zake mjini Unguja, Zanzibar.
Kikundi hicho kilichokuwa na ujumbe wa watu sita wakiongozwa  na mwenyeji wao Bi.  Shekha Nasser ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Shear Illusions na muasisi wa vipodozi vya Manjano walipata fursa ya kumtembelea Naibu Spika kwa lengo la kubadilishana mawazo kuhusu masuala ya kumuwezesha mwanamke kiuchumi.
Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mheshimiwa Bi. Mgeni Hassan Juma Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Wanakikundi hao.
Mheshimiwa Bi. Mgeni ni Mwanamke wa kwanza kushika wadhifa wa Unaibu Spika katika historia ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar. 
Katika ziara hiyo, VVGrow pia walipata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo wanawake na maendeleo ya kiuchumi kutoka kwa Bi. Mgeni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Wabunge Zanzibar (UWAWAZA). Pia ilikuwa ni fursa kwao kuonesha heshima yao kwa viongozi wa wanawake ambao wanaboresha ulimwengu na kuhamasisha usawa.
Kikundi cha VVGrow kiko mjini Zanzibar  kwa lengo la kujumuika na pia kutathmini na kujadili mawazo ambayo yatawasaidia kukua kwa wanakikundi wao binafsi na pia kukuza  biashara zao kwa kujenga ajira na kukuza uchumi.
VV GROW Fellowship ni fursa kwa wanawake ulimwenguni wenye ushindani mkubwa wa mafunzo ya mwaka mmoja wenye lengo la kusaidia wanawake wamiliki wa biashara ndogo ndogo na za kati katika mataifa ya Amerika Kusini na Caribbean, Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, na Afrika kusini mwa Sahara.

Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri,Mhe. Abdel Fattah Al Sisi anatarajia kufanya ziara ya Kitaifa wiki Ijayo.

$
0
0

Kufuatia mwaliko wa Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Abdel Fattah Al Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri atafanya Ziara ya Kitaifa nchini Tanzania wiki ijayo. Hii itakuwa ni ziara ya kwanza ya Mheshimiwa Abdel Fattah Al Sisi nchini Tanzania tangu Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli aingie madarakani. 

Lengo la ziara hii ni kuimarisha na kukuza zaidi mahusiano mazuri yaliyopo ya kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi mbili, ziara hii pia itatoa fursa kwa viongozi wetu kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi hizi mbili, ya kikanda na kimataifa.

Mheshimiwa Rais Al Sisi atawasili nchini kupokelewa na mwenyeji wake, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, Mheshimiwa Rais Al Sisi mchana atakuwa na mazungumzo (tete-a-tete) na mwenyeji wake kabla ya kushiriki mazungumzo rasmi (official talks) na baadae jioni Mheshimiwa Rais Al Sisi atahudhuria dhifa ya kitaifa itakayoandaliwa na mwenyeji wake. 

Tanzania na Misri zina mahusiano mazuri ya kidiplomasia ya muda mrefu ambayo yamezidi kuimarika hasa katika miaka ya karibuni. Ushirikiano huu unatokana na misingi ya mahusiano na mashirikiano ya karibu sana kati ya Marehemu Baba wa Taifa na muasisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kiongozi mashuhuri wa Misri na muasisi wa Jamhuri ya Taifa la Kiarabu ya Misri, Marehemu Gamal Abdel Nasser.

Uhusiano wa nchi hizi mbili umejengwa katika misingi ya ushirikiano na maelewano katika Nyanja za kijamii, kiuchumi, kisiasa, kiulinzi na kiusalama pamoja na medani za siasa za ushirikiano kimataifa, kutetea haki za binadamu, kuimarisha umoja na maendeleo ya Afrika, ukombozi wa Bara la Afrika na kupinga ukoloni, dhuluma na aina zote za ukandamamizaji duniani. Uhusiano huu umejengwa katika Nyanja zote za uhusiano katika sekta za huduma za kijamii na kiuchumi zikiwemo elimu, afya, kilimo, mawasiliano, usafiri, ulinzi na usalama na ushirikiano wa kimataifa.

Misri ni nchi ya pili yenye uchumi mkubwa Barani Afrika. Takwimu za mwaka 2016, zinaonesha kwamba pato la taifa (GDP) la Misri lilikuwa Dola za Kimarekani Billioni 266.213. Sekta kubwa kabisa katika uchumi wa Misri ni sekta ya huduma ( huduma za benki, mawasiliano, usafirishaji na utalii) ambayo inachangia takribani asilimia 52.5 kwenye GDP. Viwanda (manufacturing) inachangia asilimia 36.3, na kilimo asilimia 11.2.

Tanzania na Misri zinashirikiana katika ngazi za taasisi za serikali ambazo ni Taasisi ya Udhibiti wa utawala ya Misri (Administration Control Authority of Egypt) ambayo inashirikiana na Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa ya Tanzania (TAKUKURU), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Rufaa ya Mnazi mmoja zimesaini makubaliano ya Ushirikiano na Hospitali ya El Shatby ya Chuo Kikuu cha Alexandria nchini Misri, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kina mashirikiano ya kubadilishana wataalamu na usimamizi wa pamoja wa Shahada za juu za uzamili na uzamivu na Chuo Kikuu cha Azhar cha Misri, Jeshi la Wananchi wa Tanzania kupitia SUMA JKT wamesaini Makubaliano ya Ushirikiano na Kampuni ya Polyserve ya Misri .

Aidha, kutokana na takwimu za kituo cha Uwekezaji (TIC) kimesajili jumla ya miradi nane kati ya mwaka 1990 hadi 2017, miradi hii ina jumla ya thamani ya Dola za Kimarekani 887.02 na kutoa ajira zipatazo 953, uwekezaji huo ni katika maeneo ya Kilimo, viwanda(mbao, mbolea, madini, dhahabu na shaba) na sekta ya Huduma.

Hivyo ziara hii ina umuhimu mkubwa sana hasa katika wakati huu ambapo msisitizo wa Serikali ni katika kujenga uchumi wa viwanda.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam
11 Agosti, 2017.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima akiongea na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Mhe. Abdel Fattah Al Sisi itakayofanyika nchini wiki ijayo. 
Balozi Mlima akiendelea na mazungumzo yake na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.(hawapo pichani)
Viewing all 46340 articles
Browse latest View live




Latest Images