CHAMA CHA TENNIS TANZANIA (TTA) KUANDAA TENA MASHINDANO YA
AFRIKA MASHARIKI (EAST AFRICAN JUNIOR ZONAL CHAMPIONSHIPS) KWA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 16, JANUARI 11-19 2015.
Chama cha Tennis Tanzania (TTA) kimepewa nafasi nyingine tena ya kuandaa mashindano ya vijana wa ukanda wa Afrika Mashariki (East Africa zonal championships) na yatafanyika kuanzia tarehe 11 hadi 19 Januari 2015. Nchi shiriki kwa mwaka 2015 ni Burundi, Comoros, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Seychelles, Sudan na Tanzania.
Tunategemea jumla ya washiriki wapatao 72 (pamoja na Tanzania). Tanzania itawakilishwa na vijana 22 ikiwa na team A na B.
TTA inajivunia kuanzishwa kwa mfumo wa renki unaotoa fursa kwa wachezaji kujikusanyia pointi kwenye orodha ya wachezaji wa tennis Tanzania. Hili limesaidia urahisi wa uchaguzi wa timu na kuepuka lawama za kupendelewa watu flani. Kila mchezaji wa chini ya umri 18 ana nafasi sawa ya kukusanya pointi kwa kushiriki mashindano yanayoandaliwa na TTA au watu binafsi yaliyoidhinishwa na chama. Timu ya Tanzania mwaka huu itawakilishwa na:
Boys | ||||
Categories | Jina | TTA Rank | Points | Club |
Under 12 | Deogratus Felex Ernest | 1 | 115 | AICC |
Yusuph Laurence Godwin | 2 | 100 | AICC | |
Kanuti Omary Alagwa | 4 | 30 | AGC | |
Under 14 | Hassan Hamisi Yambi | 1 | 125 | AICC |
Emmanuel Frank Temba | 3 | 30 | AGC | |
Ali Hamza | 4 | 30 | DGC | |
Adam Mwambungu | 3(12&U) | 80 | KJ | |
Under 16 | Frank Menard Mshana | 1 | 105 | AGC |
Emmanuel Mallya | 5 | 10 | AGC | |
Omary Hamisi Sulle | 4 | 10 | AGC | |
Hassan Mkajira | 2 | KJ | ||
Girls | ||||
Categories | First Name | Club | ||
Under 12 | Ester Paulo Nankulange | 1 | 140 | AGC |
Emiliana Katabalo | 5 | 15 | KJ | |
Maria Elisha Milanzi | 4 | 25 | AGC | |
Under 14 | Emiliana Stanslaus | 2 | 30 | KJ |
Shadya Maulid Kitenge | 12 | 5 | KJ | |
Jackline Kayuga | 2(12&U) | 75 | KJ | |
Under 16 | Adela Abraham Mollel | 1 | 32 | AGC |
Georgina Kemmy Kaindoah | N/A | N/A | N/A | |
Round Robin |
Kutokana na uhaba wa wachezaji wa kike kwenye kundi la umri wa chini ya miaka 16, nafasi moja itapiganiwa na wachezaji waliopo lakini hawajapata nafasi ya kushiriki mashindano ya ndani ili kupata pointi kwa mtindo wa mtoano (round robin).
TTA inafanya juhudi kuwataarifu wazazi wa watoto walioingia kwenye timu kwa ajili ya maandalizi. Timu ya Tanzania itasimamiwa na kocha Nico Jonas ambaye ni msimamizi wa High Performance Tennis (HPC) akishirikiana na Majuto Omari wote wakiwa ni makocha wa
level 2 kwa mujibu wa ITF.
Timu inatazamiwa kuingia kambini tarehe 27-12-2015 ambapo watapewa mafunzo mbali mbali pamoja na kufanya shindano la kujipima kabla ya mashindano yenyewe mwezi wa
kwanza.
TTA itafanya mkutano rasmi na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa mashindano
mwezi wa kwanza.
Kwa niaba ya uongozi mzima, tunawatakia sikuu njema ya krismasi.
Katibu Mkuu wa TTA.
MWISHO.
Kwa maelezo ya ziada wasiliana na:
1. Nico Jonas – Kocha Mkuu - +255 754 250 097.
2. Majuto Majaliwa – Kocha Mkuu msaidizi – 0718 849 889.
3. William Kallaghe – Maswala yote ya mashindano - +255 754 210 437.