Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiongea na viongozi wa mkoa wa Morogoro na baadhi ya watumishi wa Mkoa huo hawako pichani kuhusu madhumni ya kuanza ziara ya siku tatu mkoani humo pia kupokea taarifa ya masuala ya Afya na Maendeleo ya Jamii ya Mkoa jana huo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe akitoa ufafanuzi wa hali ya maendeleo sekta Afya na Maendeleo ya Jamii ya Mkoa wa Morogoro kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile kabla ya Waziri huyo kuanza ziara ya siku tatu Mkoani humo .

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jackob akitoa taarifa ya Mkoa wa Morogoro kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotombelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kupata taarifa ya Mkoa huo kabla ya kuanza ziara yake ya siku tatu Mkoani humo.

Baadhi ya watumishi wa Mkoa wa Morogoro wakifuatilia kwa makini maelezo na maagizo ya Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile alipotembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kabla ya kuanza ziara ya siku tatu Mkoani humo.
Picha Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
………………………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu- Morogoro
Serikali imetaka wazazi,walimu wakuu,watendaji wa kata na vijiji pamoja wale wote watakaousika na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto au kumpa mimba mwanafunzi kuwajibiswa kwa kusababisha watoto wa kike kushindwa kumaliza masomo yao na kusababisha wasichana walio mashuleni kushindwa kutimiza ndoto zao.
Hayo yalisemwa jana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile alipofanya ziara Mkoani Morogoro kupata taarifa ya Mkoa huo kwa lengo la kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa masuala Afya na Maendeleo ya Jamii Mkoani humo.
Akizungumzia hali hiyo Naibu Waziri Ndugulile alisema kiwango cha matukio haya ni kikubwa mno na kuagiza Mkoa huo kuanzisha Madawati ya Ulinzi na Usalama ya Wanawake na Watoto pamoja na vituo vya mkono kwa mkono (One Stop Centres) akisistiza kuwa haya ni maagizo ya serikali kama sehemu muhimu ya kupambana na vitendo vya ukatili nchini.
“Vituo hivi kwa nchi nzima ni kumi kwa hiyo akikisheni mnaanzisha Vituo hivi katika Mkoa wa Morogoro kwa kuwa ili ni agizo la serikali katika kuakikisha tunatokomeza vitendo vya ukatili”. Aliongeza Dkt.Ndugulile.
Akisoma taarifa ya Mkoa huo kwa Naibu Waziri Ndugulile, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Frank Jacob alisema kuwa mkoa wa Morogoro una jumla ya matukio 2,555 ya mimba za utotoni akiyataja matukio 1,160 kuripotiwa kutoka Dawati la Polisi mengineyo 895 kulipotiwa katika vituo vya Afya, mashuleni na jamii.
Aidha taarifa ya Mkoa kwa Naibu Waziri Ndugulile pia ilisema Mkoa wa morogoro una jumla ya kesi 268 zilizo mahakamani kuhusiana na vitendo vya ukatili lakini ni kesi 38 tu ambazo mashauri yake yametolewa hukumu lakini pia Mkoa huo una jumla ya matukio ya ukatili wa kijinsia 1,482 na kati ya matukio hayo watoto walioteandewa ukatili ni 819.
Aidha taarifa ya hali ya mkoa kuhusiana na vitendo vya ukatili iliyotolewa kwa Naibu Waziri Ndugulile imeutaja mkoa huo kuwa na idadi ya watoto 43.5 elfu walio katika mazingira hatarishi yakipelekea uwapo wa mashauri mbalimbali ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto katika sehemu mbalimbali za mkoa huo.
Naibu Waziri Ndugulile yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya siku tatu kuangalia hutoaji huduma za maendeleo ya Jamii lakini pia masula ya Afya ambapo alitembelea na kukagua makoa ya wazee funga funga, mradi wa umwagilia wa kikiji cha Wami Luiwindo Dakawa Wilayani Mvomero na kukagua hospitali za Mkoa na Wilaya.