Baraza la sanaa la taifa limeteua majina matatu ya wabuni wa mavazi nchini Tanzania kuwa waamuzi wa shindano la wanamitindo bora wa mwaka wenye sifa za kipekee nchini Tanzania.
Uteuzi wa majaji hawa umezingatia sifa za cv za majaji sita zilizowakilishwa baraza la sanaa la taifa na hatima yake yakarudi majina matatu ambayo ni Asia Idarous,Gymkhana Hilall(paka wear) na Martin Kadinda.
Fainali za unique model 2012 zinafanyika ijumaa ya wiki hii tarehe 28 Desemba katika kumbi la maraha lililoko kule Oysterbay yaani naongelea New Maisha club ambapo wanamitindo 12 watapanda jukwaani kuwania taji hilo.
Burudani ya bendi mahili katika muziki Mashujaa band ikiongozwa na Chalz Baba watatoa burudani kali kwa mashabiki watakaohudhulia fainali hizo siku ya Ijumaa hii.pia msanii B-shop kwa mara ya kwanza ataonekana jukwaani. Ikiambatana na mashamushamu ya Costa siboka na burudani ya wanamuziki mbalimbali kwa kiingilio cha Tsh 15,000 tu.