
Wananchi wa kijii cha Rukoma kata ya Rukoma wakiwa wamekusanyika wakimsilikiza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara jioni ya leo Bukoba vijijini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 huku akihimiza uhai wa Chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 huku akihimiza uhai wa Chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Baadhi ya wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara katika kata ya Rukoma,Bukoba vijijini mkoani Kagera
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na ujumbe wake wakipokelewa katika uwanja wa Katoro,kwenye mkutano wa hadhara Bukoba vijijini mkoani Kagera jioni ya leo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Ndugu John Mongela akizungumza na wananchi na kuwaleza kuwa wasitishwe na mtu yeyote katika suala zima la kujiandikisa," asiwatishe mtu nendeni mkatumie haki yenu ya kikatiba mkajiandikishe katika daftari la wapiga kura katika kata ya Katoro Bukoba Vijijini na wala msiogope",alisema Mh.Mongella.
Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Mh Jason Rweikiza akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Katoro Bukoba Vijijini.
Wananchi wa Katoro wakimsilikiza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo wilayani Bukoba Vijijini mkoani Kagera.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Katoro jioni ya leo wilayani Bukoba Vijijini,mkoani Kagera.
Wananchi waliokusanyika katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Katoro wilayani Bukoba vijijini,mkoani Kagera jioni ya leo
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Katoro jioni ya leo wilayani Bukoba vijijini,mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto , Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Mh. Jason Rweikiza katikati na Novatus Nkwama Mwenyekiti wa CCM Bukoba Vijijini wakishiriki kufukia mabomba katika mradi wa maji unaotekelezwa na serikali katika kata ya Ibyera Bukoba vijijini wakati Katibu Mkuu huyo akiendelea na ziara yake katika jimbo hilo leo.Katibu Mkuu huyo yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 huku akihimiza uhai wa Chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye Kikao cha kupokea taarifa ya chama na serikali na kuzungumza na halmashauri kuu ya Wilaya,kabla ya kuendelea na ziara yake katika wilaya ya Bukoba Vijijini leo. Kinana amewataka viongozi wote kutokuwa na wagombea wao mioyoni katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, pia amewataka wapambe wa viongozi kuacha umbea wa kuuza maneno kutoka huku kwenda kule kwa sababu hali hiyo ni chanzo cha fitina miongoni mwa viongozi na wanachama.
Baadhi ya Wananchi wa Kemondo wakishangilia jambo
Wananchi wa Kemondo wakifuatilia yaliyokuwa yakijri kwenye mkutano wa hadhara,Bukoba vijijini mkoani Kagera.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika mji mdogo wa Kemondo,Bukoba Vijijini mkoani Kagera .
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika mji mdogo wa Kemondo, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa chama katika wilaya ya Bukoba Vijijini, mkoani Kagera.
Wananchi wakimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana na Ujumbe wake walipokuwa wakiwasili katika kijiji cha Rukoma,Bukoba vijijini mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Ofisi ya CCM ya Kijiji cha Rukoma, wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoka ndani ya Ofisi ya CCM ya Kijiji cha Rukoma aliyoindua leo, wilaya ya Bukoba Vijijini mkoani Kagera,kulai ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na kulia ni Mbunge wa Bukoba Vijijini Mh.Jason Rweikiza