Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all articles
Browse latest Browse all 49404

WIZARA YA ARDHI YAFANYA MABADILIKO KATIKA KODI YA ARDHI

$
0
0
Na Georgina Misama…MAELEZO…Dodoma


Serikali imekusudia kufuta milki za ardhi kwa wamiliki wanaokikuka masharti ya umiliki ikiwemo kutokulipa kodi ya ardhi kwa wakati.

Hayo yamesemwa na waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (MB) leo Bungeni Dododma wakati akiwasilisha makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yake kuwa huo ni mmoja wa mikakati ya Wizara yake katika kuimarisha uwezo wa kukusanya kodi.
Mhe. Lukuvi amesema baada ya Wizara yake kurekebisha viwango vya kodi inazokusanya inatarajia kukusanya shilingi bilioni 70 kwa mwaka.

Pamoja na kusudio hilo, Mhe. Lukuvi amesema mikakati mingine ambayo Wizara yake imedhamiria kuitekeleza ili kufikia lengo hilo ni pamoja na kutumia njia za kielektroniki kukusanya kodi ya pango la ardhi, ada na tozo mbalimbali.

Mikakati mingine ni kuhakikisha wamiliki wa mashamba na viwanja wanalipa kodi ya ardhi kupitia Benki, kushirikiana na Wizara ya Fedha kurejesha asilimia 30 ya makusanyo kwa wakati kwenye halmashauri kwa lengo la kuchochea ukusanyaji wa kodi ya ardhi kwa njia ya matangazo kwenye magazeti, redio, luninga na vipeperushi kulipa kodi kwa wakati.

Katika hotuba hiyo, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetangaza kuhuisha viwango vya kodi, ada na tozo mbalimbali ili wananchi wa kima cha chini waweze kulipa ada, tozo na kodi hizo.

Katika uhuishaji huo kwa mfano, kodi ya pango la ardhi imepunguzwa kwa wastani wa asilimia 30 na viwango vya vingine vinavyomgusa mwananchi wa kawaida kwa asilimia 50 au zaidi. 

Viwango vya tozo ya mbele (premium) itapunguzwa kwa asilimia 50 kuanzia mwaka wa fedha 2015/16 na tozo nyingine za sekta ya ardhi kwa asilimia 30. Makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo yamepitishwa leo jioni.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 49404

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>