Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all articles
Browse latest Browse all 49395

RAIS MSTAAFU, ALLY HASSAN MWINYI MGENI RASMI MASHINDANO YA MAGARI.

$
0
0
 Rais wa Chama cha Mashindano ya Magari Tanzania,Nizar Jivani akizungumza kuhusiana na mashindano ya magari katika hoteli ya Southern Sun jijini Dar es Salaam,mashindano yatakayofanyika Juni 12 mwaka, kushoto ni Mkurugenzi wa mashindano ya magari,Satnder Birdi na  Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya gesi ya Oryx, Godfrey Frenarden.
 Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya gesi ya Oryx, Godfrey Frenarden, akizungumza kuhusiana na mashindano ya magari hayo na jinsi yatavyakuwa yanafanyiwa ukarabati baada ya mashindano hayo kulia ni  Rais wa Chama cha Mashindano ya Magari Tanzania,Nizar Jivani na  Mkurugenzi mkuu mtendaji  wa  Chama cha Mashindano ya Magari,Yusuf Ghor.
Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga akizungumza kuhusiana na watakavyokabiliana na usarama wa wananchi na Usalama wa barabarani wakati wa mashindano ya magari yatakayofanyika jijini Dar es Salaam na kumalizikia wilaya ya Kisarawe. Mkoani Pwani.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Oryx wakifuatilia kwa makini mkutano wa wadau wa Mashindano ya magari yatakayoanzia jijini Dar es Salaam.(Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.)

Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
 Rais mstaafu, Ally Hassan Mwinyi kuwa mgeni rasmi katika mashindano ya magari yatakayo fanyika Juni 12 hadi 14 mwaka huu kuanzia  katika hotel ya Sourthen Sun jijini Dar es Salaam na kuishia wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.

Hayo yamesemwa na Rais wa Chama cha Mashindano ya Magari Tanzania,Nizar Jivani wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Sourthen Sun jijini Dar es Salaam leo.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya gesi ya Oryx, Godfrey Frenarden amesema kuwa watakuwa wadhamini wa mashindano hayo ambayo yatafanyika Juni 12 mwaka huu.

Aidha Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Mohamed Mpinga amewaasa wananchi kuchukua tahadhari katika mashindano hayo na kukaa mbali na barabara ambazo zinaweza kutumiwa na waendesha magari kwani mashindano hayo hayatafuata foleni za hapa jijini Dar es Salaam.

Pia amesema kuwa wanaoendesha magari ya mashindano hayo lazima wachukue tahadhari na kujikinga wao wenyewe katika mashindano hayo kwami kila mtu alinde usalama wake binafsi.

Mashindano hayo yatahusisha nchi tatu ambapo kila nchi itakuwa na waendesha magari ya mashindano wawili  kwa kila nchi, ikiwa madereva wa Tanzania, Uganda na Kenya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 49395


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>