Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 49516 articles
Browse latest View live

SHINDANO KUBWA LA KUSAKA VIPAJI VYA KUCHEZEA MPIRA 'FREESTYLE FOOTBALL CHAMPIONSHIP' KUANZA HIVI KARIBUNI

$
0
0
IMG_20151022_190217
Tanzania Freestyle football championship (TFFC2016) ambalo ni shindano la kutafuta/kusaka vipaji vya kuchezea mpira yaani freestyle soccer/Freestyle Football wengi hupenda kuita hivyo ambalo linatarajiwa kuendeshwa kama vile mashindano mengine ya kutafuta vipaji kwa njia mbalimbali ikiwemo ile ya TV show.Waweza wasiliana nao kupitia anuani hapa +255 654 955 825/ +255 655 049 647
IMG_20151010_014924
IMG_20151010_022504

KAPUMZIKE KWA AMANI MAREHEMU ANNETH CHRISTIAN KAJURA

$
0
0
Mume wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mke wake Anneth Christian mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach - SalaSala Jijini Dar es Salaam na baadae maziko yalifanyika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
 Mmoja ya wanandugu akitoa heshima ya mwisho.
 Mume wa marehemu Anneth Christian akiweka mchanga katika kaburi la mke wake katika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
 Mama wa marehemu akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mwanae Anneth Christian mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwa marehemu Mbezi Beach - SalaSala Jijini Dar es Salaam na baadae maziko yalifanyika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
 Mume wa marehemu akiweka shahada la ua katika kaburi la mke wake katika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
 Mtoto wa marehemu akiweka mchanga katika kaburi la mama yake.
 Mama wa marehem akiweka mchanga katika kaburi la mwanae.
 Wanafamilia wakiweka maua katika kaburi la Anneth Christian.
Mwili wa Marehemu Anneth Christian ukiingizwa nyumbani kwake Mbezi Beach - SalaSala Jijini Dar es Salaam na baadae maziko yalifanyika Makaburi ya Kondo - Bahari Beach.
 Waombolezaji.

INTRODUCING Nonini ft Chege & Dj Pierra-Wanajishuku

$
0
0
Kenyan rap legend also known as Nonini MgengeTrue has been on a roll this Month. Barely a few weeks after he released Mchezo Na Ganji yet another Brand new Video dubbed "WANAJISHUKU" is here.

 “Wanajishuku” his latest track features TMK Wanaume’s Chege and Kenya’s number one deejay DJ Pierra Mackena. “Wanajishuku”  is Nonini’s second collaboration with a Tanzanian artist Chege after Kila Mmoja became a massive success in East Africa.  The chemistry between the two East African Artists is evident every time they bless a track together.

Wanajishuku audio was produced by R Kay Mwana Abuja and the Music Video directed by Willie Owusu and ProHabo.

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA WATAABIKA NA MAFURIKO KUTOKANA NA MVUA INAYOENDELEA KUNYESHA.

$
0
0
Miongoni mwa nyumba zilizopo Mtaa wa Kilimahewa Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza ambazo huathirika na kero ya Maji kuingia ndani pindi mvua zinapoanza kunyesha.

Pichani ni mmoja wa wakazi wa Kilimahewa akitoa maji ndani ya nyumba yake kutokana na mvua iliyoanza kunyesha majira ya saa kumi na mbili alfajiri hii leo. Hadi tunaenda hewani (saa 10:30 asubuhi) Mvua hiyo inaendelea kumiminika mdogomdogo.Picha na Loyce Nhaluke.

Mbali na Kilimahewa, Pia wakazi wa Mabatini Jijini Mwanza hukumbwa na kero ya Mafuriko wakati wa Mafuriko na kwa miaka mingi juhudi za kuwahamisha zimekuwa zikigonga mwamba linapokuja suala la kuwatafutia makazi mapya.Mara kadhaa mafuriko katika maeneo hayo yamekuwa yakisababisha athari mbalimbali ikiwemo vifo.
Maji hadi ndani, hakika ni hatari
Maji yakitolewa ndani
Kilimahewa Manispaa ya Ilemela
Binagi Media Group, Kwa Pamoja Tuijuze Jamii Whatsupp +255 (0) 757 43 26 94

BEI YA MADAFU HII LEO

TAMASHA LA UTALII NA AMANI KUFANYIKA ARUSHA

$
0
0

 mkurugenzi wa kampuni ya  Arusha Media  ambaye ni mmojawapo wa waandaaji wa tamasha hili Musa Juma katikati akiwa anaongea na waandishi wa habari kuhusiana na tamasha hilo
 Akizungumzia tamasha hilo na kutaja michezo itakayokuwepo  , Mkurugenzi wa  Alfredo Shahanga  Sports Promotion ,Alfredo Shahanga katika kati
 baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia mkutano huo
Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole   katikati akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari awapo pichani

 Na Woinde Shizza,Arusha
Tamasha la Utalii na amani, Arusha tourism Festival linatarajiwa kufanyika Novemba 22 katika jiji la Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari  Golden Rose hotel , Mratibu wa Tamasha hilo, Andrea Ngobole alisema, tamasha hilo limeandaliwa na taasisi ya Arusha Media na Alfredo Shahanga Sports  Promotion.

Alisema katika tamasha  hilo, kutakuwa na michezo michezo mbali mbali, ikiwepo soka, mashindano ya riadha ya Tourism Marathon, maonesho ya utalii na kongamano la utalii na amani."kauli mbiu ya tamasha hili ni Utalii wa ndani na amani sasa tunatoa wito kwa wadau mbali mbali kujitokeza kushiriki"alisema

Akizungumzia tamasha hilo, Mkurugenzi Alfredo Shahanga alisema, maandalizi yote muhimu yamekamilika.

Hata hivyo, alitoa wito kwa wadhamini zaidi kujitokeza  kudhamini ili kuhakikisha wakazi wa Arusha wanashiriki kuhamasisha utalii wa ndani na kuhubiri amani.
Naye mkurugenzi wa kampuni ya Arusha media ambaye pia ni mmoja wapo wa waandaaji wa tamasha hilo alitaja michezo ambayo itakuwepo ni pamoja na kukimbiza kuku,kuruka kamba,kukimbia na magunia ,riadha ambapo alisema kuwa kutakuwa na mbio za kilometa tano,half marathoni pamoja na full marathoni ambapo alieleza kuwa mbio za full marathoni zenyewe zitafanyika siku  december 13.

TANZIA

$
0
0
 MOHAMMED MBILILI ANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA RAFIKI KIPENZI NDUGU DAMAS D. MAGUZO (PICHANI )   KILICHOTOKEA TAREHE 01 NOVEMBA 2015  HOSPITALI YA MWANANYAMALA.

TARATIBU ZA MSIBA ZINAENDELEA NYUMBANI KWA BABA WA MAREHEMU HUKO MABIBO (GARAGE).

MWILI WA MAREHEMU UTASAFIRISHWA KESHO NOVEMBA 3 MWAKA HUU KUELEKEA SONGEA KWA MAZIKO.

KWA LOLOTE LILE UNAOMBWA UWASILIANE NA NAMBA HIZI ZIFUATAZO:

+255 665 62 40 52 / +255 624054 (BABA WA MAREHEMU)

CLEARING AGENTS  WOTE MNAOMBWA KUWASILIANA NA BABA WA MAREHEMU MAPEMA.

RAIS KIKWETE AMTEUA RAMADHAN KASWA KUWA KATIBU TAWALA WA MKOA LINDI

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua  Ndugu Ramadhan Kaswa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi kuanzia Oktoba  30, mwaka huu, 2015.

          Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Kaswa alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa Msaidizi,  Mkoa wa Tanga.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
2 Novemba, 2015



UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI NOVEMBA2,2015.

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni November 2, 2015.

SIMUtv: Baad ya kuburuzwa katika mechi za ligi kuu ,kocha wa timu ya Kagera Sugar akiri timu haiku sawa hivyo kupelekea matokeo mabaya
SIMUtv: Ligi ya mpira wa kikapu imeendelea kurindima  jiji Dar Es Salaam huku makocha wakitoa changamoto zinazokabili ligi hiyo;  https://youtu.be/3FnnqjPczrQ
SIMUtv: Fuatilia mada ya siku ya leo ambapo inaangazia kuhusu jeshi la zimamoto na uokoaji  pamoja na sheria za utendaji wa jeshi hilo; https://youtu.be/rO9rmNRojs0
SIMUtv: Kutana na kamishna wa iliyokuwa tume ya muafaka Zanzibar Asha Juma akizungumzia hali na muelekeo visiwani  Zanzibar katika mjadala;  https://youtu.be/I3p6Nk4cb-g

SIMUtv: Je vijna wa Kitanzania ana mtazamo gani baada ya uchaguzi mkuu uliyofanyika mwishoni mwa mwezi Octoba mwaka huu?; https://youtu.be/xGAkWu6I4e4

SIMUtv: Mvua kubwa ya mawe iliyoandamana na upepo mkali imesababisha athari kubwa kwa wakazi wa manispaa ya ya Sumbawanga; https://youtu.be/OX4pBAhg1mk

SIMUtv: Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Kigoma waipongeza serikali kwa kuanzisha mradi wa maendeleo ya jamii (TASAF); https://youtu.be/uJx7zFiZYbU

SIMUtv: jeshi la polisi ,viongozi wa dini waombwa kushirikiana  kuielimisha jamii kuhusu  uuzaji mafuta ya petrol katika makazi; https://youtu.be/b7xJTCMMR2Q

SIMUtv: Wazazi, walezi  nchini watakiwa kuwalea watoto wao katika misingi ya maadili na kuwajengea uzalendo kwa manufaa ya ulinzi wa taifa; https://youtu.be/GD9PZW6vhAo
SIMUtv: Wanafunzi wa kidato cha nne Tanzania, pamoja na wasimazi watakiwa kutojihusisha na udanganyifu ili kuepusha kufutiwa matokeo yao; https://youtu.be/oxtkjh_Oy0o
SIMUtv: Wanachama wa mtandao wa utetezi za haki za binadamu(THRDC) walaani uvamizi wa kituo cha TACCEO;https://youtu.be/YYd2kpBERYw

UWANJA WA KAITABA BUKOBA WAANZA KUWEKWA NYASI RASMI LEO.

$
0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba.

Uwanja wa Kaitaba Bukoba Umeanza kuwekwa nyasi bandia rasmi leo hii jumatatu 2 Novemba, 2015 na kutokana na maelezo ya wawekaji wamesema utachukuwa muda wa siku 14 tu. 

Wakaazi wa Mji wa Bukoba na Vitongoji vyake sasa kuanza kushuhudia kipute live bila Chenga katika Uwanja huo wa Kaitaba. Timu ya Kagera Sugar nayo inatarajiwa kurudi katika Uwanja huo ambao uutumia kama Uwanja huo ambapo mpaka sasa tangu msimu uliopita wamekuwa wakitumia Viwanja vingine kwa michezo yao ya Nyumbani na Ugenini pia. Uwanja huu umejengwa kwa 
ufadhili wa FIFA chini ya mpango wa misaada wa Goal Projects.

Uwekwaji Nyasi ukiendelea katika Uwanja wa Kaitaba leo hii.
Taswira ya Nyasi zenyewe za Bandia zikiwa zimetandazwa katika Uwanja huo wa Kaitaba uliopo Bukoba Mjini ambao hutumiwa na Timu ya Hapa Bukoba Kagera Sugar ambayo kwa sasa inaendelea kutumia Viwanja vya Ugenini.
Katibu wa KRFA Salumu Umande Chama ambaye pia ni Kiongozi kamati ya Waamuzi Nchini akizungumzia swala zima la Uwanja huo wa Kaitaba na Waandishi wa habari leo jumatatu 02 Novemba, 2015. Chama ameeleza kutokana na kasi iliyopo na kama Mafundi hawatakwama Uwanja huo utamalizika ndani ya Wiki mbili tuu.
Taswira kamili
Uwanja huo umeanza kuwekwa nysi rasmi leo na ndani ya siku 14 utamalizika na taratibu nyingine zitafuata na Timu ya Kagera itaanza kuutumia Uwanja huo. Uwanja huu sasa utakuwa umeongezeka katika Viwanja vilivyowekwa nyasi hapa Tanzania ikiwa ni pamoja na Uwanja wa Uwanja wa Uhuru uliopo Dar es Salaam, Uwanja wa Karume (Dar es Salaam) na Uwanja wa Gombani uliopo Pemba.

WAKAGUZI WATAKIWA KUZINGATIA WELEDI

$
0
0
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Bw. Gerald Mwanilwa akizungumza na Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy. Kushoto ni Bw. Slyvester Kibona, Mkaguzi Mkuu wa Nje wa Mkoa wa Morogoro. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Mkurugenzi wa msaidizi (Mafunzo) Bibi Felister Tirutangwa akizungumza wakati wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT) na Wizara ya Fedha wakifuatilia kwa umakini mafunzo  ya program ya TEAMMATE. Mafunzo hayo yanafanyika mkoani Morogoro kuanzia tarehe 02 hadi 06 Novemba, 2015.
Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy akizungumza na wanahabari kuhusu mafunzo hayo.

Mgeni rasmi wa mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka NAOT na Wizara ya Fedha, Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wanaohudhuria mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), Bw. Gerald Mwanilwa akizungumza na wanahabari kuhusu mchango wa Serikali ya Awamu ya Nne katika kuhakikisha uhuru wa CAG unapatikana.


Na Mwandishi wetu, Morogoro
Watumishi wa umma nchini wenye fani ya ukaguzi, wametakiwa kutumia weledi katika utendaji kazi zao hali itakayoongeza ufanisi katika usimamizi wa rasilimali za umma.

Wito huo umetolewa na Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Bibi Wendy Massoy wakati akifungua mafunzo ya program ya TEAMMATE kwa ajili ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na Wizara ya Fedha.

Bibi Massoy amesema, viwango vya ukaguzi Kimataifa vinahitaji mkaguzi kuhifadhi taarifa zake za ukaguzi vizuri ili kuwezesha mkaguzi mwengine kuweza kufikia hitimisho moja kulingana na kazi iliyofanywa na Mkaguzi mwengine.

“Programu ya TEAMMATE hutoa fursa kwa wakaguzi kwa kuwawezesha  kuhifadhi taarifa zake za ukaguzi vizuri hivyo kuwafanya kutii viwango vya ukaguzi Kimataifa vya ukaguzi,” alisema Bibi Massoy.

Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ameongeza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wakaguzi hao katika kazi yao ya ukaguzi.

“Nawasihi muweze kutumia fursa hii kujiendeleza na kutekeleza utaratibu wa kaguzi wa mwongozo kwa vile wengi wa hatua na taratibu wamekuwa umeboreshwa katika Teammate Programu.

Akizungumzia mchango wa Serikali ya Awamu ya Nne katika kuiboresha Ofisi ya CAG, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Gerald Mwanilwa alisema kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imechagizwa na uamuzi wa dhati wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kuimarisha taasisi za utawala bora, maadili na udhibiti, ikiwemo NAOT.

Bw. Mwanilwa aliongeza kuwa Rais alifanya hivyo kwa kuboresha sheria, kuongeza uhuru wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, kuongeza uwazi wa taarifa za Ofisi hiyo kwa kupeleka Ripoti za CAG kwa mara ya kwanza Bungeni pamoja na kuboresha mazingira ya kazi.

“Kwa mara ya kwanza Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliitisha vikao mbalimbali, kwa nyakati tofauti na Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa kusisitiza umuhimu wa kuzipitia na kuzifanyia kazi taarifa zinazotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Hii imeleta mwamko mpya katika kuona umuhimu wa ripoti hizi na kutumika katika kufanya maamuzi mbalimbali serikalini,” alisema.

Bw. Mwanilwa aliongeza Katika Uongozi wa Awamu ya Nne NAOT ilishuhudia uanzishwaji wa Sheria ya Ukaguzi wa Umma, ambapo serikali ilitunga Sheria ya Ukaguzi wa Umma ya Mwaka 2008 pamoja na kanuni zake za mwaka 2009. Sheria hii iliongeza wigo na uhuru wa Ofisi hii katika kutekeleza majukumu yake Kikatiba.

Kuhusu Bajeti ya uendeshaji wa NAOT, Bw. Mwanilwa aliongeza: “Rais Kikwete aliongeza Bajeti ya Ofisi ya Ukaguzi ambapo Serikali iliboresha utaratibu na mchakato mzima wa kupitisha bajeti ya Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali uliowezesha bajeti ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kuongezeka kwa asilimia 306% katika kipindi cha miaka mitano, kuanzia mwaka wa fedha wa 2008/9 hadi 2013/14.”

Jumla ya wakaguzi 65 kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi na kutoka 25 Wizara ya Fedha wanahudhuria mafunzo hayo ya siku tano yanayofanyika mkoani Morogoro.

VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAKUTANA

$
0
0
Msajili wa vyama vya siasa nchini,Jaji Mstaafu ,Francis Mtungi akiarisha mkutano wa vyama vya siasa ulioandaliwa kwa ajili ya kumuaga Rais Dk.Jakaya Kikkwete leo jijini Dar es Salaam.

.Mchambuzi wa wa Masuala ya Siasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,Dk.Benson Bana akizungumza na waandishi wa habari juu hali ya siasa nchini leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mgombea Urais wa TLP,Maxmillian Lymo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula( Kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Labour Patry (TLP), Agustino Lyatonga Mrema  (kulia ) na katikati Mgombea Urais, Maxmillian Lymo  jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti  Taifa  wa chama cha  (AFD)  Said Soud Said akifafanua jambo kwa wandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu  ya Jamii

UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI NOVEMBA 2,2015

$
0
0
Huu ni uchambuzi wa Habari toka vituo mbalimbali vya Televisheni Mchana Huu November 2, 2015.

Chama cha mapinduzi mkoani Lindi kimewataka watanzania kuungana pamoja katika kujenga nchi ili kusaidia utekelezaji wa Dkt. Magufuli.
Hali ya kisiasa Visiwani Zanzibar inaendelea shwari huku wananchi wakiendelea na shughuli zao za kila siku kama ilivyo kawaida. https://youtu.be/WcX-Npbsmbg

Mitihani ya kidato cha nne imeanza kufanyika leo nchini kote ambapo watahiniwa 448, 358 wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo. https://youtu.be/j79mEH18jcI
Raisi wa Misri Abdelk Fatah El Sisi atoa wito kwa watu kusubiri matokeo ya uchunguzi wa kubaini sababu ya kuanguka kwa ndege Ya Urusi. https://youtu.be/0KAV7il8mbA
Baadhi wa wanasiasa walioshindwa uchaguzi mwaka huu watakiwa kuwa na busara au kutumia njia ya amani ili kudai haki zao https://youtu.be/hztuHb6k9gY

Watanzania wametakiwa kuacha uvivu wa fikra na badala yake wajishughulishe kama wanataka maendeleo ya nchi yao https://youtu.be/zwzl7mk2-ug
Polisi  jamii mkoani mwanza imetajwa kuwa chachu ya amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa Tanzania; https://youtu.be/hZZe53utKOM
CCM Iringa yawataka wanachama wake kuwa watulivu hasa wale majimbo yao yaliyokuwa na dosari katika kipindi cha uchaguzi; https://youtu.be/uFtW2RiwDlQ
Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo jijini mwanza yasababisha ndege kutofanya safari zake  kwa mda kutokana na maji kujaa; https://youtu.be/k37x2D6UKBE


WATAALAM WA TAKWIMU KUTOKA OFISI ZA TAKWIMU BARANI AFRIKA

$
0
0
Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Afrika Kusini Risenga Maluleke akizungumza leo na waandishi wa habari kuhusu madhumuni ya mkutano wa watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika ambapo wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza leo na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa siku tano ambao umekutanisha watalaam wa takwimu kutoka nchi mbalimbali barani Afrika kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam. 
 Baadhi ya wakuu wa Ofisi za Takwimu kutoka barani Afrika wakifuatilia kwa makini majadiliano wakati wa mkutano wa kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu. Mkutano huo ni wa siku tano na unafanyika katika hoteli ya Golden Tulip iliyopo Jijini Dar es Salaam.
 (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO)

VIONGOZI wa Ofisi za Takwimu barani Afrika leo wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi hizo pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu katika nchi za Afrika.

Wakizungumza katika mkutano wa wataalam wa takwimu ulioanza leo Jijini Dar es Salaam, viongozi hao wamesema ili takwimu bora zipatikane kwa wakati, ni lazima kuwepo na mfumo bora wa uongozi pamoja na wataalamu waliobobea katika fani ya takwimu.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Dkt. Albina Chuwa amesema lengo la mkutano huo ni kujadili mfumo wa uongozi bora katika Ofisi za Takwimu pamoja na namna ya kuboresha mitaala ya ufundishaji wa masomo ya takwimu barani Afrika.

“Leo tupo hapa wataalamu wa takwimu kutoka zaidi ya mataifa 25 barani Afrika ili kujadili namna ya kuboresha mifumo yetu ya uongozi katika Ofisi za Takwimu pamoja na kujadili mbinu bora za kuimarisha utoaji wa mafunzo kwa watakwimu vijana hasa kupitia upya mitaala ya ufundishaji,” amesema Dkt. Chuwa.

Dkt. Chuwa amesema kuimarishwa kwa mfumo wa uongozi pamoja na kuboresha mafunzo kwa wakwimu kutasaidia katika ukusanyaji wa takwimu bora zitakazotumika katika kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wa Afrika ya Kusini, Risega Maluleke amesema mataifa mengi ya Afrika yanakabiliwa na changamoto kubwa ya kutokuwa na uwezo wa kujitegemea kifedha kitu ambacho hukwamisha upatikanaji wa takwimu kwa wakati.

Amesema licha ya changamoto hiyo, kwa kiasi kikubwa kazi ya ukusanyaji wa takwimu imekuwa ikifanyika kwa ufanisi mkubwa kutoka kwa watalaam hao wa takwimu na hivyo kupitia mkutano huu, wataweza kujadili namna ya kuboresha uimarishaji wa Ofisi za Takwimu.

Maluleke amesema ni vyema Serikali zikaziwezesha ofisi za ukusanyaji wa takwimu ili ziweze kujitegemea kibajeti na kuboresha utendaji kazi wake katika kuhakikisha takwimu bora zinapatikana kwa wakati muafaka.

Mkutano huo wa siku tano unatarajia kumalizika tarehe 06 Novemba, 2015 ambapo wataalam takribani 30 wamekutana kujadili Mfumo wa Uongozi Bora katika Ofisi hizo pamoja na Uboreshaji wa Mitaala ya Ufundishaji wa Masomo ya Takwimu katika nchi za Afrika.

TANGAZAO KWA WASAMALIA WEMA: MTOTO CAREEN ANAHITAJI MSAADA

$
0
0

Mtoto Careen Modest Kassuw pichani, ana umri wa mwaka mmoja, amezaliwa ana tatizo la Moyo ukiwa na matundu mawili na valvu zake nyembamba  zimebana kiasi  hivyo analazimika kusafirishwa kwenda India kwa matibabu.

Wazazi wa mtoto huyo wanaomba msaada wako wewe Mtanzania kwa atakayeguswa ili wafanikishe gharama za matibabu ya mtoto Careen ambayo ni Shilingi Milioni 30 zinahitajika ili kuokoa maisha yake.
Ewe Mtanzania, ewe mzazi tunaomba mchango wako wa hali na mali, kwa atakayeguswa tunaomba utume mchango wako kwa mama mzazi wa mtoto huyo Eunice kwa namba0713 034866 au kwa namba 0715 083055

Mungu awabariki wote mtakaochangia kwa njia moja au nyingine.

HANDENI MJINI KURUDIA KURA ZA MAONI KESHO

$
0
0
 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Sekretarieti, Makao Makuu ya CCM Ofisi Ndogo Lumumba.

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM iliyokutana leo, Novemba 02,2015 chini ya Mwenyekiti wa CCM,Rais Jakaya Mrisho Kikwete imejadili kwa kina mapendekezo ya wana CCM walioomba ridhaa ya kugombea ubunge katika jimbo la Handeni mjini.

 Kamati Kuu imetengua mapendekezo ya awali na kuagiza kurejewa kwa mchakato wa kura za maoni kwa wana -CCM wawili walioongoza kura za maoni za awali.

Wana- CCM hao watakaopigiwa kura za maoni tena kesho Novemba 03,2015 ni pamoja na Omari Abdallah Kigoda na Hamis Hamad Mnondwa.

Aidha Kamati Kuu imeteua wajumbe watatu kusimamia zoezi hilo ambao ni Dk. Maua Daftari, Dk.Emmanuel Nchimbi na Alhaji Abdallah Bulembo.

UKATILI WA KIJINSIA SOKO LA TEMEKE WAPUNGUA KWA ASILIMIA 70

$
0
0

 Mwezeshaji  Sheria katika Soko la Temeke Sterio, Batuli Mkumbukwa (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam  leo, kuhusu mafanikio waliyopata ya kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko hilo baada ya kupatiwa mafunzo na Shirika la Equality for Growth (EfG). Kushoto ni Mwezeshaji wa Sheria, Christina Simon na Augenia Gwamakombe.
 Mkuu wa Mgambo katika soko hilo, Onesmo Osward (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Mfanyabiashara wa matunda katika soko hilo, Isabela Juakali akichangia jambo kwenye mkutano huo.
 Mwezeshaji wa Sheria katika soko hilo, Augenia Gwamakombe (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
 Mfanyabiashara wa Soko hilo, Said, Mbonde (kulia), akizungumzia kupungua kwa ukatili wa Kijinsia katika soko hilo.
Wanawake wafanyabiashara katika soko hilo wakiwa kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

UKATILI wa kijinsia katika Soko la Temeke umepungua kwa asilimia 70 ukilinganisha na miaka mitatu iliyopo imefahamika.

Hayo yalibainishwa na Mwezeshaji wa Sheria wa soko hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika soko hilo, Christina Simon wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea soko hilo Dar es Salaam leo asubuhi kujua changamoto za ukatili wa jinsia katika soko hilo baada ya Shirika la Equality for Growth kutoa mafunzo ya namna ya kukabiliana na ukatili huo.

"Hivi sasa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika soko letu umepungua kwa kiasi kikubwa baada ya wanawake kujitanbua na kupatiwa mafunzi na shirika la EfG" alisema Simon.

Alisema awali matukio ya unyanyasi kila wiki walikuwa wakiyapokea kati ya matatu na zaidi lakini sasa kwa mwezi wanaweza kupokea tukio moja au lisiwepo kabisa.

Mwezeshaji wa Sheria, Taus Ali,  alisema katika soko hilo kulikuwa na unyanyasaji mwingi, lugha za matusi ambazo likuwa zimekithiri lakini hivi sasa hali hiyo haipo na kama ipo ni kwa kiwango kidogo hasa baada ya kuletewa mradi wa Mpe Riziki si Matusi na EfG.

Mfanyabiashara, Said Mbonde alisema hivi sasa unyanyasaji wa kijinsia kwenye soko hilo haupo kwani hapo awali kulikuwa na tabaka la kufanyabiashara kwani biashara aliyokuwa wanaifanya wanaume walikuwa hawaruhusiw kufanya wanawake lakini sasa kila mmoja wao anafanyabiashara hizo zikiwemo za udalali.

Mfanyabiashara wa matunda katika soko hilo, Isabela Juakali alisema tabia iliyokuwepo zamani ya mgambo kuwamwagia biashara zao wafanyabiashara ndogo ndogo hivi sasa haipo kabisa baada ya kuelewa na kufuata kanuni na maelezkezo ya utendaji kazi.

Mkuu wa Mgambo katika soko hilo, Onesmo Osward alisema siku hizi malalamiko ya mtu kutukanwa au kupigwa hayapo kabisa jambo lililoongeza utulivu na amani katika soko hilo.


Utambulisho wa kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili Washington DC

$
0
0
Jumamosi,Oktoba 31, Swahili Media Network LLC kwa ushirikiano na Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapa Washington DC walitambulisha kipindi kipya cha Televisheni cha Kiswahili JAMBO TV SHOW kitakachoonekana kwenye kituo cha Televisheni cha DCTV hapa Marekani.

Pia, Swahili Media Network inaandaa kipindi cha Radio cha Jambo America, kinachosikia kupitia WJFK ambayo ni radio-dada ya WPGC chini ya shirika la CBS Radios.

Ratiba kamili ya vipindi kutoka Swahili Media Network, itawajia hivi karibuni
Mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza (katikati) akizungumza na Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi waTanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme na baadhi ya waliohudhuria uzinduzi huo
Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Swahiba Mndeme (wa pili kushoto) ambaye pia alimuwakilisha Mhe Balozi Wilson Masilingi, akimsikiliza mwanzilishi wa Jambo Tv Show, Steven Mghaza
Steven Mghaza akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa kwa Mkuu wa Utawala na Fedha wa Ubalozi, na mwakilishi wa balozi kwenye hafla hiyo, Swahiba Mndeme,Kushoto ni Meneja mauzo wa CBC Radio R.J Trzaska, mratibu wa Mis Congo na msanii toka congo
Mshereheshaji wa siku hiyo, Grace Ssebo akikaribisha wageni.

Wasanii Adele na Frank wakiimba nyimbo za taifa za Marekani na Tanzania, wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo
Mwakilishi wa balozi, ambaye pia ni Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme, akisalimia wageni wakati wa utambulisho
Mkuu wa utawala na Fedha wa ubalozi, Swahiba Mndeme akitambulisha rasmi kipindi hicho

Meneja masoko wa CBC Radio hapa Washington DC R.J Trzaska
Mmoja wa washiriki wa Jambo Show Radio inayotayarishwa na Swahili Media Network, Sala Damali
Mwanzilishi wa Jambo Show Steven Mghaza akielezea kipindi hicho kwa wageni waalikwa
Meneja masoko wa CBC Radio hapa Washington DC R.J Trzaska akielezea umuhimu wa radio kwa jamii yetu na muelekeo wake
Mwakilishi wa Ubalozi wa Kenya, Joyce Gasugar, akitoa salaam







Mzee Magali akitumbuiza

Wasanii Frank Kesi na Adelle wakitumbuiza

Aunt Asha wa Kamona Bites akisalimia waalikwa

Ma Winnie wa Mitindo Night, akitambulisha fashion show yake
















Taarifa ya Utabiri Wa Mvua Za Vuli 2015

Vyuo Vikuu wampongeza Dkt. Magufuli

$
0
0
 Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Bi. Zainabu Abdallah akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa pongezi  kwa Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa niaba ya Shirikisho hilo leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Habari( MAELEZO).
Mwenyekiti wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (CCM) Bi. Zainabu Abdallah (katikati)akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) alipokuwa akitoa pongezi  kwa Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano Dkt. John Pombe Magufuli kwa niaba ya Shirikisho hilo leo jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Habari( MAELEZO). Kushoto ni Katibu Msaidizi wa Shirikisho hilo Bw. Daniel Zenda na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Frank Mvungi.Picha na Frank Shija.


Frank  Mvungi, MAELEZO
Rais mteule wa Jamhuri  Ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli amepongezwa kwa kushinda kiti cha Rais katika uchaguzi mkuu ulifanyika  oktoba 2015 ikiwa ni kielelezo cha utendaji bora alionyesha katika kuwatumikia watanzania kupitia nyazifa alizotumikia kabla ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa shirikisho la vyuo vikuu Chama cha Mapinduzi (CCM) Bi Zainab Abdallah wakati wa mkutano na waandishi wa Habari uliolenga kumpongeza Rais  mteule kwa tiketi ya chama hicho.

“Akifafanua Bi Zainab  amesema kuwa Rais Mteule Dkt. John Pombe Magufuli ameshinda kiti cha Urais kwa kuwa ndiye mtu pekee ambaye watanzania walikuwa wanamuhitaji ili aweze kuwaletea maendeleo kwa kuwa ni mchapa kazi na ameonyesha kwa vitendo dhamira hiyo katika utumishi wake kwa miaka yote iliyopita “alisisitiza Zainab

Bi. Zainab amesema kuwa Rais mteule Dkt. Magufuli anayo dhamira ya dhati yakuwaletea maendeleo watanzania ndiyo sababu hata kauli mbiu yake ililisisitiza  kuwa “hapa kazi tu” hivyo ni wajibu wetu kama watanzania kusisitiza umoja na mshikamano na kuondoa tofauti zetu ili tufanye kazi kwa bidii ili kujenga uchumi wa taifa.

Akizungumzia wasifu wa Rais Mteule Dkt. Magufuli; Bi Zainab  amesema kuwa ni mtu mwenye uzalendo,mwadilifu,mchapa kazi, na ambaye watanzania wote wanamkubali kuwa anao uwezo wa kuliongoza Taifa katika kipindi hiki.

Kwa upande wa Uchaguzi  mkuu Zainab  amesema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki  hali iliyowapa nafasi watanzania kuchagua viongozi wanaowataka  na kupelekea chama cha mapinduzi kuongoza katika uchaguzi huo  kutokana na utendaji madhubuti wa viongozi wa Chama na Serikali.

Pia Bi Zainab alitoa wito kwa watanzania kudumisha amani na umoja wa Kitaifa ulioasisiwa na Viongozi wa kwanza wa Taifa hili ili kufikia maendeleo ya Kweli.

Shirikisho la wanafunzi wa  vyuo vikuu Chama cha Mapinduzi (CCM)  limekuwa likihamasisha vijana kufanya kazi kwa bidii ili kujenga Taifa.
 


Viewing all 49516 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>