Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 48893 articles
Browse latest View live

MSHINDI WA PROMOSHENI YA BETI NA KITOCHI MERIDIANBET

$
0
0

Kila mmoja ana ndoto kubwa ya kumiliki vitu vizuri, lakini vikwazo vya Maisha na bajeti kubana hukwamisha ndoto ya wengi kumiliki vitu wanavyovitaka, kwa kulitambua hili kampuni ya Meridianbet waliamua kurahisha mipango yako, kwenye promosheni ya shinda TV ukibeti na kitochi.

 Ilichukua siku kadhaa mpaka kumpata Bingwa wa kubeti na kitochi mwanafamilia wa Meridianbet anayejulikana kwa jina la Alex mkazi wa Jiji la Dar Es Salaam aliyejishindia TV mpya inch 55. Beti na kitochi ya Meridianbet inaendelea kutimiza ndoto ya kila mtu.

 

Kila mtu huwa ana yule mtu mmoja anayemuamini kwa kutoa taarifa za michongo, Alex kwa alipata taarifa ya promosheni hii ya Meridianbet kutoka kwa marafiki zake, hivyo marafiki ni muhimu Zaidi kwenye Maisha.

 

Unapotaka kufanya jambo huwa kuna sababu, hata bingwa wa kubeti na kitochi ni mpenzi wa michezo na hiyo ilimfanya yeye kubeti meridianbet, alienda mbali Zaidi na kusema siku ya kwanza alishinda, na wewe una nafasi ya kushinda jaribu bahati yako meridianbet mabingwa wa michezo ya kubashiri pia wana kasino mtandaoni.

 

Vuta picha unapigiwa simu na kupewa habari njema, huwa unakuwa kwenye hali gani, na je pale unapokabidhiwa jambo lako? Alex anasema kuwa promosheni ya beti na kitochi imempatia TV kubwa ambayo hakuwa kuwaza ni lini ataipata, lakini kwa dau lake dogo tu la kuanzia TZS 250/= limetimiza ndoto yake.

 

“TV hii itasaidia familia yangu, ukizingatia kombe la dunia linaendelea hivyo nitakuwa nangalia mechi nyingi kwa raha na ubora Zaidi, nawashukuru Meridianbet kwa zawadi hii kubwa kwenye Maisha yangu”- Mshindi wa promosheni ya beti kitochi- shinda TV 

 

 Moja ya sababu ya Bingwa huyu kuwa mwanafamilia ya Meridianbet ni uwezo wa kurudisha dau lako uliloweka “Cash Out/ Turbo”kama unaona mkeka wako upo kwenye hali mbaya ya kuchanika.

 

“Kujaribu sio kitu kibaya kila mtu ana nafasi ya kubashiri meridianbet na kushinda, ukiangalia kama nchi yetu kuna ile kitu kupotosha, hakuna kitu kibaya hususani kubeti kwa malengo sio tatizo”

 

“Watu wanapaswa kubeti kupitia Meridianbet, kwani mimi nimeshawahi kubashiri na kampuni nyingi, lakini kampuni ya meridianbet wako vizuri ina machaguo mengi sana ya kubeti, kitu ninachokipenda ni ule uwezo wa kurejesha hela yako ‘Turbo’ pindi unapoona mechi haiendi vizuri una nafasi ya kuchukua pesa yako hata kwa kiasi kidogo”- Alex



UFUNGAJI WA MAFUNZO YA ULINZI WA MTANDAO KIST

$
0
0

 

 

Mkurugenzi kutoka Kitengo cha Usalama wa Mitandao katika Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhandisi Stephen Wangwe amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la udukuzi wa taarifa katika mitandao jambo ambalo linapelekea matatizo makubwa kwa Taasisi na watu binafsi  ikiwemo upotevu wa fedha.

Alizungumza hayo, wakati wa ufungaji wa mafunzo mafupi ya ulinzi wa mifumo ya kompyuta na kuzuia wizi wa mitandao, yaliyofanyika katika Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), Mbweni Zanzibar.

Alisema kumekuwa na tovuti nyingi zinazotumwa katika mitandao ya kijamii ambayo wananchi wengi bila kufahamu hufuata na kujiunga na tovuti hizo, na hatimae hupelekea kudukuliwa taarifa zao, hivyo amewataka wananchi kuwa makini katika utumiaji wa mitandao.

Katika hatua nyengine, Mkurugenzi Wangwe amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kuyatumia vyema katika kuisaidia serekali, pamoja kuhakikisha wanaweka mbele uzalendo wa nchi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia(KIST), Bi Latifa Ufuzo amesema mafunzo hayo yatawaimarisha na kuwajengea uwezo wataalamu wetu wa ndani na nje ya Taasisi katika ulinzi wa mifumo.

Alieleza kuwa, ipo haja ya kujenga misingi imara ya kuhakikisha kila kitengo cha Tehama kinakuwa na ulinzi wa kutosha ambapo miongoni mwa misingi hiyo ni kupatiwa mafunzo ya ulinzi wa mifumo na kompyuta.

Nae Mkufunzi wa Mafunzo hayo Bwana Yussuf Kileo amesema bara la afrika lina kazi kubwa ya kuhakikisha mifumo inapata ulinzi wa kutosha kwani matukio mengi hutokea Afrika, ikiwemo uporaji wa fedha kupitia mitandao.

Amesema miongoni mwa sababu zinazopelekea uporwaji wa fedha katika mitandao ni uwekezaji wa fedha katika mitandao ambayo hata wamiliki wake hawafahamiki.

Hivyo aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kuineza elimu walioipata ili jamii iweze kujilinda na uhalifu unaofanywa na wadukuzi wa mitandao.





 

TANZANIA KUNUFAIKA NA DOLA BILIONI 1 KUTOKA KOREA

$
0
0

 


Na. Peter Haule, WFM, Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Korea kwa kutenga kiasi cha dola za Marekani bilioni 1 zitakazotolewa kwa njia ya mkopo nafuu kwa Tanzania kupitia Mfuko wa  Shirika la Maendeleo ya Kiuchumi (EDCF), kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi miaka mitano

Dkt. Nchemba ametoa shukrani hizo jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri anayesimamia uratibu wa masuala ya Sera wa Korea Mheshimiwa Moon-Kyu Bang, alipokutana na kufanya mazungumzo naye akiwa katika ziara ya kikazi nchini.

“Septemba mwaka 2022, Tanzania na Korea tulisaini makubaliano yatakayoiwezesha Tanzania kupata mkopo wenye riba nafuu wenye thamani ya dola za Marekani  bilioni moja ambapo Tanzania itakopa mkopo huo kwa riba ya asilimia 0.01 kwa mwaka na kuulipa kwa kipindi miaka 40 ambacho kimeambatana na kipindi cha neema cha miaka 15.” alisema Dkt. Nchemba

Dkt. Nchemba aliishukuru Korea kwa kuahidi pia kusaidia utekelezaji wa miradi miwili mipya ukiwemo mradi wa maji na usafi wa mazingira mkoani Iringa wa Iringa na ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni-Zanzibar, ambayo italeta manufaa makubwa kwa wananchi.

Alisema kuwa Wizara na Serikali kwa Maelekezo na mwongozo wa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, ipo tayari kushirikiana na timu ya Serikali ya Korea na wawakilishi wa Benki ya Exim nchini kuweza kukamilisha kwa haraka taratibu zote za kitaalamu ili miradi hiyo iweze kutekelezwa.

Aidha Dkt. Nchemba, amezikaribisha Kampuni za Jamhuri ya Korea kuwekeza nchini ukiwemo uwekezaji wa ubia katika miundombinu wezeshi ikiwemo ya barabara, nishati, afya, usafiri wa majini na Tehama.

Dkt. Nchemba alisema kuwa Serikali ya Tanzania ina fursa nyingi za uwekezaji kwa kuwa ni lango la nchi nchingi zikiwemo za Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika na pia ina mazingira bora ya uwekezaji na ufanyaji biashara.
 
Pia alibainisha kuwa ushirikiano kati ya Tanzania na Korea ni wa kirafiki na kindugu, ikizingatiwa kuwa Serikali ya Korea iliwezesha Tanzania kupata fedha za kutekeleza miradi mingi ukiwemo mradi wa ujenzi wa daraja la Tanzanite jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake    Waziri Ofisi ya Uratibu wa Sera wa Jamhuri ya Korea, Mhe. Moon-Kyu Bang aliahidi kuwa mradi wa kuboresha usambazaji maji na mazingira wa Iringa uamuzi wake wa kuutekeleza utafanyika mwishoni mwa mwaka huu na utekelezaji utaanza mara moja ilihali mradi wa Hospitali ya Rufaa ya Binguni  Zanzibar, taratibu za kitaalam zitakamilishwa ndani ya miezi sita ili utekelezwe. 

Vilevile ameeleza kuwa Korea inampango wa kuongeza zaidi ya marambili kiwango cha bajeti ya kutoa misaada kwa Afrika hadi kufikia mwaka 2030, hivyo ameitaka Tanzania kuandaa miradi ambayo itatekelezwa katika mpango huo utakapoanza ikiwemo miradi ya ubia na Sekta binafsi katika maeneo ya barabara, reli na mingine.

Mhe. Bang aliipongeza Serikali kwa kutekeleza mradi wa kimkakati wa reli ya kisasa ambao amesema ni kubwa na utasaidia kuinua uchumi wa nchi na nchi Jirani na kuahidi kuwa atazishawishi kampuni kutoka nchini mwake kushiriki katika mradi huo kwa njia ya utaratibu wa ubia kati ya umma na sekta binafsi.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiipongeza Korea kwa kutoa misaada na mikopo yenye mashariti nafuu kwa Tanzania, wakati wa mkutano kati yake na Waziri Ofisi ya Uratibu wa Sera wa Korea, Mhe. Moon-Kyu Bang (hayupo pichani), jijini Dodoma, kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Emmanuel Tutuba.

Waziri Ofisi ya Uratibu wa Sera wa Korea, Mhe. Moon-Kyu Bang (katikati) akiteta jambo na baadhi ya wajumbe alioambatana nao katika mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), uliofanyika jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM)
Waziri Ofisi ya Uratibu wa Sera wa Korea, Mhe. Moon-Kyu Bang (katikati) akiteta jambo na baadhi ya wajumbe alioambatana nao katika mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (hayupo pichani), uliofanyika jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Emmanuel Tutuba (wa nne kushoto) akizungumza jambo wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Waziri Ofisi ya Uratibu wa Sera wa Korea, Mhe. Moon-Kyu Bang (hayupo pichani), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa nne kulia) na Waziri Ofisi ya Uratibu wa Sera wa Korea, Mhe. Moon-Kyu Bang (wa tano kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Korea na Tanzania baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao, jijini Dodoma.Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiagana na Waziri Ofisi ya Uratibu wa Sera wa Korea, Mhe. Moon-Kyu Bang, baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao, jijini Dodoma.

MIAKA 61 YA UHURU NA ONGEZEKO LA WATANZANIA MILIONI 61

$
0
0


Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Nickson Simon (kushoto), Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Mwanana Msumi (katikati) na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe(kulia) wakiwa wameshika keki kama ishara ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa nchi yetu.Keki hiyo ilikatwa na kulishwa viongozi mbalimbali pamoja wananchi walioshiriki kwenye Mdahalo ulioandaliwa na Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali.


Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kisarawe Eva Stesheni(kushoto) akiweka vijiti kwenye vipande vya keki.Katikati ni Mkuu wa wilaya hiyo Simon Nickson akitoa maelezo kuhusu keki hiyo na kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Zuberi Kizwezwe.

Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Nickson Simon(kushoto) akimlisha keki Katibu Tawala wa wilaya hiyo Mwanana Msumi(kulia) kama ishara ya kusherehekea na kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika.Tukio hilo la kukata keki limefanyika baada ya kumalizika kwa mdahalo ulioandaliwa na Mkuu wa wilaya hiyo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali wakati wakiadhimisha siku hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon(kushoto) akimlisha keki Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo Zeuberi Kizwezwe.Kisarawe imeadhimisha siku ya Uhuru kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kuanzia Desemba 1 na leo Desemba 9 wamehitimisha kwa kufanya mdahalo ngazi ya wilaya.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Zuberi Kizwezwe akizungumza wakati wa Mdahalo uliondaliwa na Mkuu wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya kiutamaduni wakati Taifa likiadhimisha miaka 61 ya uhuru wake

Ofisa Ustawi wa Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Mwandili Rangi akitoa ufafanuzi kuhusu hali ya mahusiano ya kwenye ndoa ndani ya Wilaua hiyo wakati wa mada ya kuzungumzia mahusiano na unyanyasaji wa kijinsia.Wengine kwenye picha hiyo ni Mkuu wa wilaya hiyo Nickson Simon(katikati) na Kamanda wa Polisi Eva Stesheni (kulia).


Baadhi ya washiriki wa mdahalo uliondaliwa na Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Simon Nickson ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 61 ya Uhuru wan chi yetu ambapo kwenye mdahalo mada mbalimbali zilijadiliwa.

Watalii sasa kuwasiliana wakiwa kileleni Mlima Kilimanjaro

$
0
0

Waziri Nape akifungua kitambaa kuangalia njia ya kuelekea kileleni cha Mlima Kilimanjaro mara baada ya hafla ya kuelekea Uzinduzi wa Huduma ya Intaneti katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro iliyofanyika Marangu Gate mkoani Kilimanjaro. 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (wa pili kulia waliosimama) akishuhudia Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) pamoja na Shirika la TTCL wakisaini Hati ya Makubaliano(MoU) ya ushirikiano katika hifadhi ya Mlima Kilimanjaro. Kulia wanaosaini ni Kamishna Mhifadhi Mkoa wa Kilimanjaro, Dkt. Emilian Kihwele na Mkurugenzi Mkuu Shirika la Mawasiliano Tanzania, Mhandisi Peter Ulanga (kushoto).
Waziri Nape akiangalia njia ya kuelekea kileleni cha Mlima Kilimanjaro mara baada ya hafla ya kuelekea Uzinduzi wa Huduma ya Intaneti katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro iliyofanyika Marangu Gate Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Wahandisi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL (waliosimama) waliofanikisha ujenzi wa miundombinu ya Mawasiliano mpaka Kilele cha Mlima Kilimanjaro, mara baada ya hafla ya kuelekea Uzinduzi wa Huduma ya Intaneti katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro iliyofanyika Marangu Gate Mkoani Kilimanjaro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakutugenzi ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL, Bi Zuhura Snare Muro akizungumzia jinsi Bodi yake itakavyoendelea kuleta mageuzi katika sekta ya Mawasiliano nchini wakati wa hafla ya kuelekea Uzinduzi wa Huduma ya Intaneti katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro iliyofanyika Marangu Gate Mkoani Kilimanjaro.

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) limefanikiwa kufikisha huduma za mawasiliano ya Intaneti kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro, ikiwa ni juhudi za kuunga mkono Serikali kutangaza vivutio vya utalii nchini.

Akizungumza katika hafla ya awali kuelekea uzinduzi wa mawasiliano ya Data Katika Kilele cha Mlima Kilimanjaro uliofanyika Makao Makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ameipongeza TTCL kufanikisha mradi huo wa kuweka mawasiliano katika Mlima Kilimanjaro.

Alisema kukamilika kwa mradi huo kunaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kusimika huduma za mawasiliano katika kilele cha Mlima kilimanjaro, jambo ambalo litaongeza kasi ya kuutangaza mlima huo duniani na kuvutia idadi kubwa ya watalii kuutembelea.

"Leo ni siku muhimu kwa Shirika letu la TTCL na Tanzania tunapokwenda kushuhudia tukio la kihistoria la uzinduzi wa intaneti katika kilele cha Mlima Kilimanjaro, utakaofanyika pia rasmi kwenye kileleni cha mlima Desemba 13, 2022 tukiwa huko kileleni," alisema Mhe. Nnauye.

Jumla ya kilometa 44.7 za njia ya Mkongo wa Mawasiliano zimejengwa kuanzia Kituo cha Marangu hadi kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro, uwekezaji ambao umefanikisha vituo vyote vilivyopo katika Mlima Kilimanjaro kupata mawasiliano ya intaneti na simu za mezani.

"Tangu kuzinduliwa kwa huduma za mawasiliano katika vituo vya awali, watalii wanaopanda mlimani wameanza kuzungumza na ndugu, jamaa na marafiki wakiwa mlimani na kuelezea uzuri wa vivutio vyetu jambo ambalo linaendelea kuutangaza utalii nchini, licha ya kurahisisha shughuli za huduma kwa watalii zinazofanywa na taasisi mbalimbali katika Mlima Kilimanjaro," alisisitiza Waziri Nnauye.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Eng. Peter Ulanga alisema uwepo wa huduma hiyo ya mawasiliano katika Mlima Kilimanjaro itaboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa watalii mlimani, pia wanapopata dharura yoyote wakiwa safarini.

Aidha aliongeza uwepo wa huduma za mawasiliano utaimarisha shughuli za ulinzi na usalama kwa watalii wakiwa mlimani kupitia mamlaka husika jambo ambalo ni kivutio cha kuchocheza na kuvutia watalii wengi kuutembelea.

"Mkakati wa Shirika wa miaka mitano ni kuhakikisha huduma za mkongo zinawafikia wananchi katika makazi yao, maeneo ya biashara, maofisini na sehemu za vivutio vya utalii wetu, TTCL inatambua umuhimu wa utalii nchini hivyo tutaongeza nguvu kutoa huduma za mawasiliano kupitia mkongo katika maeneo mengine ya utalii ili kuchochea shughuli za utalii nchini," alibainisha Eng. Ulanga.

VETA Kipawa yajivunia wahitimu kuajiriwa kabla ya kuhitimu

$
0
0

Picha ya pamoja na mgeni rasmi  na Wafanyakazi wa Chuo cha Tehama VETA Kipawa  kwenye mahafali ya 11 ya Chuo hicho.
Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Angelus Ngonyani akizungumza katika mahafali ya 11 ya Chuo  Cha Tehama VETA Kipawa yaliyofanyika kwenye chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Tehama VETA Kipawa Mhandisi Sospeter Mkasanga akitoa maelezo kuhusiana mafunzo yanayotolewa na Chuo hucho jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wazazi katika Mahafali ya 11 ya Chuo cha Tehama  VETA Kipawa Everister Ndunguru akitoa Rai kwa wahitimu wa chuo hicho jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kipawa Albert Otieno akizungumza kuhusiana na umhimu wa chuo hicho kwa wakazi wa Kipawa kwenye mahafali ya 11 Chuo cha Tehama VETA Kipawa , jijini Dar es Salaam.


Picha za pamoja za wahitimu na mgeni rasmi kwenye mahafali ya 11 ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa.

*Mkurugenzi VETA Kanda aagiza kufanya tafiti kwenye mahitaji

Na Mwandishi wetu.
 CHUO cha Tehama VETA Kipawa kimesema kuwa sekta ya Tehama nchini inakua kwa kasi hivyo vijana wanafursa ya kupata mafunzo na ujuzi katika eneo hilo na kuweza kutoa mchango kwa taifa na kwa mtu mmoja mmoja.

Hayo aliyasema Mkuu wa Chuo cha Tehama Kipawa Mhandisi Sospeter Mkasanga wakati wa mahafali ya 11 ya Chuo hicho yaliyafanyika kwenye viwanja vya VETA Kipawa jijini Dar es Salaam.

Mhandisi Mkasanga amesema kuwa Chuo hicho kimeanzisha kozi bobevu kwa ajili ya Tehama kwa wanafunzi kusoma kitu kimoja tu ambapo inafanya kuwa mahiri kwenye ujuzi wa eneo husika.

Mhandis Mkasanga amesema kuwa wakati wa sasa ni fursa kwa vijana wa kitanzania kosoma kozi bobevu kutokana na uchumi unabadilika ambao unahitaji kuwa na mifumo ya Tehama katika kurahisisha kufanya kazi za watu 100 basi kufanya watu 50 na soko la Tehama liko wazi.

Hata hivyo amesema kuwa vijana wanaosoma Chuo cha VETA kipawa asilimia 70 wanahitimu wakiwa na kazi ya mkononi na hiyo inatokea pale tu wanapokuwa wamekwenda kwenye mafunzo ya vitendo.

Aidha amesema kuwa Chuo kinaendelea kutafuta mashine ya za kisasa za kujifunzia kutokana na teknolojia yake kubadilika kila wakati hivyo kunahitaji kwenda sambamba na Teknolojia.

Akizungumza mgeni rasmi katika mahafali ya 11 ya Chuo cha VETA Kipawa Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Angelus Ngonyani amesema kuwa VETA Kipawa wanahitaji kufanya tafiti katika soko la Tehama pamoja na kufanya kozi bobevu kuwa na vijana wengi zaidi kutokana mahitaji yaliyopo katika nchi.

Ngonyani amesema kuwa VETA kipawa katika kufikia maendeleo kunatakiwa ushirikiano na wadau mbalimbali ikiwemo na wenye viwanda ambao vijana waliopata elimu ya ufundi wanatakiwa kwenda huko.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa katika eneo la kilichopo Chuo Albert Otieno amesema kuwa wananchi kuwa chuo VETA Kipawa ni mkombozi kwa vijana katika kupata elimu ambayo kwa sasa ndio mahitaji kwenye soko.

TANTRADE YAIFUNGULIA MILANGO TCA

$
0
0


Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)

Latifa Khamis na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser pamoja na wageni waalikwa wakitembelea mabanda kujionea Tasnia ya Vipodozi inchi inavyoendelea katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.  Na Khadija Kalili 

 MKURUGENZI Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa Khamis amesema kuwa kuwa kuanzia sasa serikali itafanya kazi na Chama Cha Vipidozi Tanzania (TCA) ikiwa ni katika kuhakikisha wanalinda afya za watumiaji wa vipodozi na sekta ya urembo na watanzania wote kwa ujumla.

Mkurugenzi huyo amesema hayo leo Desemba 10, 2022 wakati alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam ambapo alimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji. 

Amesema enzi za kupenda na kithamini vipodozi au bidhaa kutoka nje ya nchi zimepitwa na wakati. "Hivyo nachukua fursa hii kuwapongeza sana kwa Tamasha hili la aina yake huku nikiwataka muongeze kasi katika uzalishaji wa vipodozi visivyo na viambata vyenye sumu na nina waahidi kuwa Tantrade tutawapa fursa ya kujitangaza kitaifa na kimataifa.

Nawakaribisha TCA mtukimbilie muda wowote na milango iko wazi kwa ajili yenu huku nikiwaahidi kuwa tutawatafutia masoko nje ya nchi kwani hii ni fursa kubwa katika kuitangaza nchi kimataifa katika nyanja ya biashara pia kuanzia mwakani tutawapa fursa ya kuonesha bidhaa zenu kwenye maonesho ya Viwanda Tanzania pamoja na makongamano mbalimbali ya biashara kwa kuwaunganisha na wadau mbalimbali kwa kupitia muamvuli wa TCA."

"Tasnia hii ya vipodozi ina wigo mpana ambao umeongeza ajira na kukuza uchumi kwa vijana na kinamama wa hapa nchi, Wanawake shikamaneni na mnyanyuane kiuchumi ikiwa ni kwenye kuongeza kipato katika familia zenu.  Amesema Latifa Khamis 

Kwa Upande wa Mwenyekiti wa TCA, Shekha Nasser ameweka wazi kuwa inaonesha kuwa wanawake wengi hasa wakaazi wa Wilaya ya Kinondoni ni wahanga wa kunyonyoka kope kutokana na kubandika  kope za bandia huku wakitumia gundi ambazo zimewapatia madhara.

Pia amewaasa wanawake kujenga Utamaduni wa kutumia vipodozi vya asili visivyo na madhara huku akisema endapo watatumia mafuta ya mnyonyo yanayoyengenezwa ni mwanachama wao Nzalakado yatasaidia kuziotesha kope hizo. Bi Shekha ameiomba serikali iweze kuwapunguzi kodi kwenye bidhaa za urembo ikiwemo saluni na kuwekwe muongozo ambao utakua ni rafiki kwenye kulipa kodi kwa kupitia chama hicho TCA kilizinduliwa miaka mitatu iliyopita Jijini Dar es Salaam ambao ni muunganiko wa wadau wenye kuuza na kutengeneza vipodozi nchini.
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa Khamis akizungumza leo Desemba 10, 2022 alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam akimwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji. 
Mwenyekiti wa TCA na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser akizungumza leo Desemba 10, 2022 uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.





Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa Khamis na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser pamoja na wageni waalikwa wakitembelea mabanda kujionea Tasnia ya Vipodozi inchi inavyoendelea katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade)
Latifa Khamis na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser pamoja na wageni waalikwa wakipata maelekezo walipotembelea mabanda kujionea Tasnia ya Vipodozi inchi inavyoendelea katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.



Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Picha ya Pamoja.

Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Latifa Khamis na Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya MANJANO FOUNDATION, Shekha Nasser pamoja na wageni waalikwa wakiwa katika Picha za pamoja katika uzinduzi Tamasha la siku moja 'Vipodozi Day' lililofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI KOMGAMANO LA UHIFADHI WA MAZINGIRA NA UTUNZAJI WA VYANZO VYA MAJI MKOANI IRINGA

$
0
0

-Wanahabari kuwa sehemu ya kuelimisha kuhusu uharibifu wa mazingira


Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv

Makamu wa Rais Dk.Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni Rasmi katika Kongamano la Kujadili kukauka Mto Ruaha litakalofanyika Desemba 19 mkoani Iringa.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari, Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) Habib Mchange amesema kuwa kongamano hilo linalenga kujadili kukauka mto Ruaha ikiwa wanahabari ni sehemu ya kuhakikisha wanatumia karamu ya kuelimisha madhara ya wananchi kufanya shughuli za kibinadamu.

Mchange amesema mabadiliko ya Tabianchi ni mabadiliko ya Tabia za wanadamu hivyo wanahabari ni nguzo katika kuhakikisha masuala ya mazingira linasimamiwa pamoja sheria ziheshimiwe.

Amesema mito inayoingiza maji kwenye bonde la Usangu inatiririsha maji wakati wote lakini mto Ruaha haina maji kabisa.

Amesema kuwa mara ya kwanza Mto Ruaha ulikauka 1994 ambapo serikali ilichukua hatua ukatiririka kwa muda tena ukakauka 2005 hadi sasa unakauka ambapo sasa ni wakati wa waandishi kuchukua karamu.

Aidha amesema kuwa kongamano hilo litaaziamia nini kifanyike katika kufanya mto Ruaha irudi kwenye kutiririsha maji

Mto Ruaha ndio inayochangia umeme kwa asilimia 15 kwenye bwawa la Mtera na tegemeo kwa bwawa la nyerere hivyo mgao wa umeme watu hawajui.

Amesema mgao wa umeme ulipoanza ni matokeo ya mto Ruaha kukauka ambapo miradi ya umeme ndio ikaanza ikiwemo mradi wa IPTL 2005 ukaanza.

Kwa upande wa Ofisa Mawasiliano wa MECIRA, Hamisi Mkotya,amesema kuwa wanahabari wana wajibu wa kupaza sauti kusemea jambo hilo kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika mambo mengine ili kupambana na uharibifu huo wa mazingira na vyanzo vya maji.

“Unapoharibu mazingira au vyanzo vya maji, haumkomoi mtu, unajikomoa wewe mwenyewe. Kuna shughuli za binadamu zinafanyika kiholea au isivyo halali na kuharibu mazingira na vyanzo vya maji. Kuna kilimo kinafanyika kiholela, ufugaji wa kuingiza mifugo katika maeneo ambayo hayaruhusiwi, kwa hiyo yote hayo, rasilimali zinavyoharibika, taifa linapata hasara, lakini tunaathirika sisi sote",amesema Mkotya .

Nae Mjumbe wa MECIRA na Mdau mkubwa wa mambo ya Uhifadhi nchini,Mwandishi mkongwe wa Habari, Manyerere Jackton amebainisha kuwa wajibu wa wanahabari ni kujipambanua badala ya kuwa sehemu ya watu wanaolalamika, kutumia kalamu zao kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira hayo.

“Mazingira yanapo athirika hayachagui mtu, sisi wote tunaathirika. Leo hii kuna mgawo wa umeme, watu wote wanaathirika bila kujali itikadi ya mtu, kwa hiyo tumeona sisi kama wanahabari tulete mabadiliko chanya katika suala hili la kutunza na kuhifadhi mazingira yetu kwa sababu tunao wajibu huo wa kushirikiana na serikali kuelimisha jamii,”alisema Manyerere.


Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari ,Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) Habib Mchange akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) leo Desemba 11,2022 jijini Dar es Salaam kuhusu kufanyika kwa kongamano kubwa litakalohusisha Wahariri na Wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya Digitali, Blog, Redio, Televisheni, na Magazeti; Mawaziri, Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini, Mashirika ya umma, Mashirika ya kimataifa, na Wadau mbalimbali wa uhifadhi na utunzaji wa mazingira kujadili na kutafuta suluhu ya hali inayoendelea ya uharibifu wa mazingira nchini, litakalofanyika katika ukumbi wa Chuo kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa,ambapo mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango. PICHA ZOTE NA MICHUZI JR (MICHUZI MEDIA).


Mjumbe wa MECIRA na Mdau mkubwa wa mambo ya Uhifadhi nchini,Mwandishi mkongwe wa Habari, Manyerere Jackton akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kwa Waandishi wa Habari ikiwemo kuwakumbusha wajibu wao wa kujipambanua badala ya kuwa sehemu ya watu wanaolalamika, kutumia kalamu zao kuelimisha umma kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira hayo.

 Ofisa Mawasiliano wa MECIRA, Hamisi Mkotya akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani) akiwaomba Wanahabari kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha wanapaza sauti na kusemea jambo hilo la uharibifu mkubwa wa mazingira kama ambavyo wamekuwa wakifanya katika mambo mengine ili kupambana na uharibifu huo wa mazingira na vyanzo vya maji.




 MCHENGERWA AFAGILIA TAMASHA LA BATA MSITUNI

$
0
0

-Ni lilofanyika Msitu wa Vikindu, Mkuranga asema Matamasha kama haya yanatakiwa kufanyika Tanzania nzima

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amefurahishwa na Tamasha la Bata Msituni ambalo liliandaliwa na Chinobychino Travel kwa kushikiriana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ambapo amesema kuwa matamasha kama hayo yanatakiwa kufanyika Tanzania nzima ili watu wafurahi.

Mhe. Mchengerwa alisema hayo wakati akizindua Tamasha hilo lililofanyika Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia Pugukazimzumbwi Safu ya Vikindu uliochini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS). Alisema Watanzania wanafanya kazi sana hivyo baada ya majukumu yao ni muhimu kupumzika na hivyo matamasha kama hayo ni muhimu sana.

Aidha, Mhe. Mchengerwa aliwapongeza waandaaji kwa kuwa na ubunifu huo mkubwa na kuwasihi waendelee kuandaa matamasha hayo zaidi huku wakiwahusisha mamlaka husika.

Mgeni Rasmi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa akizungumza na wananchi ambapo alipongeza ubunifu huo na kusisitiza kuwa matamasha kama haya yanatakiwa kufanyika Tanzania Nzima, alizungumza hayo wakati wa Tamasha kubwa la Bata Msituni Lililofanyika katika Msitu wa Vikindu Safu ya  Pugu Kazimzumbwi

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir akitoa salamu za shukurani kwa muitikio Mkubwa wa watu waliofika katika Tamasha la Bata Msituni lililofanyika katika Msitu wa Vikindu safu ya  Pugu Kazimzumbwi  uliochini ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS)



Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa akitoa burudani ya nguvu huku watu wakifurahia wakati wa Tamasha kubwa la Bata Msituni ambalo lilifanyika katika msitu wa Vikindu Safu ya Pugu Kazimzumbwi  ambao Msitu huo upo chini ya Wakala wa Misitu Tanzania TFS


Wanamwita Chui, Rayvan hapa akiwa anakiwasha wakati wa Tamasha la Bata Msituni ndani ya Msitu wa Pugu Kazimzumbwi Safu ya Vikindu Mkuranga , Msitu huo upo chini ya wakala wa Misitu Tanzania TFS


Ukisikia piga kigoma mpaka unaamka ni hiki sasa Mgeni Rasmi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa, hapa akaona hapana ikabidi aungane na wanabata msituni kufurahia Tamasha kubwa la Bata Msituni huku Kigoma kikiendelea. (Picha na Fredy Njeje Mdau wa Utalii)
 

GGML YAWAAGA WAHITIMU WA MAFUNZO TARAJALI

$
0
0

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo tarajali kutoka GGML wakiwa na vyeti vya kuhitimisha mafunzo waliyoyapata kwenye kampuni hiyo kwa mwaka 2021/2022



Na Mwandishi Wetu.

Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imewaaga wahitimu 26 wa mafunzo tarajali waliokuwa wakifanya mafunzo katika kampuni hiyo kwa mwaka 2021/2022.

GGML hutekeleza programu ya mafunzo tarajali kila mwaka kwa kushirikiana na ofisi ya Waziri Mkuu inayohusika na ajira, vijana, na watu wenye ulemavu pamoja na Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) na Chama cha Waajiri Nchini (ATE). Hii ni mojawapo pia ya mkakati wa kampuni ya GGML kunufaisha jamii ya Tanzania kutokana na shughuli za uchimbaji dhahabu.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga wahitimu hao mkoani Geita, Meneja Mwandamizi anayesimamia kitengo cha Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo kutoka GGML, Dkt Kiva Mvungi amewapongeza wahitimu hao kwa kufikia hatua hiyo muhimu katika fani walizozisomea.

“Tunawapongeza kwa kupata fursa hii. Kampuni yetu imekuwa ikitoa nafasi hizi kila mwaka na wahitimu wengi wa vyuo vikuu wamekuwa wakituma maombi yao. Kwa ambao mlichangamkia fursa za ajira zilipotangazwa, tunawapongeza kwa kuwa wafanyakazi wa kudumu wa kampuni hii. Kwa ambao bado hamjapata ajira, endeleeni kutuma maombi yenu kila GGML inapotoa nafasi za kazi,”

Dkt Mvungi alisisitiza, “Kukamilisha programu hii ni mwanzo sasa wa kuonesha ukomavu wenu mnapoitwa katika udahili wa kazi. Asimilia kubwa ya vijana waliopitia programu hii wameajiriwa na makampuni mbalimbali, bila shaka nanyi mtaajiriwa pia hapa GGM au kwingineko. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa sekta ya madini hapa nchini inapata wafanyakazi wenye uzoefu.”

Kwa upande wake Mhandisi Ruth Mugurusi ambaye ameajiriwa katika kitengo cha ulipuaji cha GGML ameshukuru kupata fursa hiyo akiwa katika mchakato wa kuhitimu mafunzo yake.

“Mimi ni Mtanzania ambaye naishukuru sana GGML kwa kunipatia fursa hii. Baada tu ya kuhitimu masomo yangu ya Chuo Kikuu, nilituma maombi na kuanza mafunzo haya. Namshukuru Mungu nikiwa katika kipindi cha mafunzo haya, zilitangazwa nafasi na mimi na wenzangu tukatuma maombi na kufaulu usaili na leo hii hatimaye tumeajiriwa na GGML. Nawashauri wahitimu wengine wa mafunzo haya, waendelee kutuma maombi yao kila nafasi zinapotangazwa kwa kuwa GGML ni kampuni inayotoa fursa kwa watu wote wakiwemo wanawake,” alisema Mhandisi Mugurusi.

Tangu programu hii ianze mwaka 2009 hadi hivi sasa jumla ya wahitimu 168 wamenufaika ambapo kati ya hao wasichana ni 58 na wavulani ni 110. Asilimia kubwa wameajiriwa na GGML katika vitengo vya uchenjuaji dhahabu, uhandisi, ufundi, ulipuaji na uchimbaji madini na baadhi yao wameajiriwa katika makampuni mengine ndani na nje ya nchi.


WADAU WA BAHARI KUTOKA NCHI 15 WANOLEWA, TASAC WAAHIDI KURIDHIA MKATABA WA KIMATAIFA WA BAHARI

$
0
0

 KATIKA kuhakikisha mazingira ya Bahari na maji yanatuzwa wadau wa mazingira kutoka nchi mwanachama 15 wa Afrika wameshiriki katika Warsha ya siku tatu kwaajili ya kukuza uelewa wa pamoja juu ya Mkataba wa kimataifa wa Utunzaji wa Mazingira ya Bahari.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya uchukuzi) Dkt. Ally Possi akizungumza katika warsha hiyo leo Desemba 12 jijini Dar es Salaam amesema kuwa Mwitikio wa nchi mwanachama umekuwa mkubwa na ni jambo ambali dunia imeanza kuipa kipaumbele mkataba wa kimataifa kwaajili ya kulinda mazingira ya bahari ili kuhakikisha viumbe vitakavyo zaliwa majini vinakuwa hai.

Akizungumzia kuhusiana na Hali ya bahari kwa sasa amesema kuwa Mazingira ya Bahari kwa sasa ni manzuri lakini tahadhari mbalimbali lazima zitolewa kwaajili ya Vizazi vya vijavyo.

"Ifahamike kuwa vyanzo vya maji hususani bahari vinasimamia sera ya uchumi wa bluu, sasa bahari inapochafuka na inapoharibiwa kimazingira, sera ya uchumi wa bluu inakuwa ngumu kwani kwa sababu ya viumbe ambavyo vinafanyika kuwa uchumi vitapotea pamoja na vyombo vya usafiri majini vitaharibika na kushindwa kufanya kazi inayotakiwa."
Amesema Dkt. Possi

Amesema kuwa mkutano huo utatilia mkazo wa uridhiaji wa itifaki ya sheria ya bahari kwaajili ya kuendeleza uelewa mpana wa wadau wote.

Washiriki wa mkutano huo ni Wafanyakazi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania
(TASAC), Bandari, Taasisi ya Bahari ya Dar es Salaam (DMI) wa wawakilishi wa Nchi 14 za Afrika.

 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge amesema Shirika hilo limekasimiwa mamlaka ya kudhibiti mazingira ya majini na Maji yanayotokana na uchafunzi wa vyombo vya Usafiri Majini hivyo madhumuni ya warsha hiyo ni uelewa wa pamoja wa Jinsi ya kudhibiti maji, kusimamia masuala ya usafiri majini.

.....kwa kukaa sana yale maji inawezekana kuna viumbe ambavyo vinazaliwa na yale maji yaliyokuwa kwenye meli hakishushwa baharini katika maji ya kitaifa au eneo lolote la bahari kunauwezekano wa kushushwa na viumbe wengine ambao wamezaliwa baada ya yale maji kukaa muda mrefu

Hivyo basi yale maji yakishushwa yanaweza kuzalisha viumbe wengine ambavyo vitakuwa hatarishi kwa uendelevu viumbe ambao wapo baharini na tunavihitaji.

Amesema uchumi wa bluu unaweza usifikiwe kama maji yanakuwa hayadhibitiwi. Kwahiyo hatutaufikia uchumi wa bluu kama mikataba hii hatutairidhia na kuzingatia ni jinsi gani tunaweza kujikinga na hivyo viumbe ambavyo vinaweza kuzalishwa.

Shirika la Kimataifa la Bahari linatoa elimu kwa Taasisi mbalimbali zinazohusika na masuala ya usafiri kwa njia ya maji, taasisi zinazohusika na masuala ya bahari zimeshiriki warsha hiyo ili kuwa na uelewa wa pamoja ili mkataba utakaporidhiwa na kutengeneza kanuni za Kutumika hapa nchini.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Usalama na mazingira baharini kutoka Wizara ya Ujenzi na uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Stela Katondo amesema kuwa maji yanahobebwa na meli yanasaidia meli pale ambapo inakuwa haina mzigo pia ikiwa na mzigo mdogo yanapunguzwa au kuongezwa ili kuweka uzito sawa katika meli na Maji hayo watu wenye meli wamekuwa wakiyamwaga baharini jambo ambalo sio zuri.

"Maji hayo yanaviumbe na mimea ambayo sio asili ya huku kwetu kwa hiyo ikitokea yanamwagwa baharini yatakuwa na viumbe wavamizi wataleta namna tofauti ya kimazingira Shirika la Kimataifa la Bahari (IMO) liliona umhimu wa kuweza kudhibiti hali hiyo kwa sababu kimazingira sio sawa, kinachotakiwa ni kuto kumwagwa baharini kama nchi mwanachama wa IMO tunatakiwa kuridhia mkataba huo ili kuweza kusimamia kuwa haitakiwi ukifika bandarini kumwaga maji inatakiwa kwenda kumwagwa katika kati ya habari ili yasiweze kuleta shida katika eneo letu la mazingira ya maji.

Amesema Kwa Tanzania Sasaivi tupo katika hali nzuri kwa sababu tumeshaanza kuridhia mkataba pia amesema Kama wizara wameshatoa maoni na mapendekezo kwa wadau mbalimbali wanaohusika na mkataba huu. Na mpaka sasa wameshaanza kupokea maoni yao.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya uchukuzi) Dkt. Ally Possi akizungumza na waandishi wa habari mara baada kufungua warsha ya Siku tatu kwa wadau wa Bahari leo Desemba 12 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Kaimu Abdi Mkeyenge akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 12, 2022.
Mkurugenzi wa Usalama na mazingira baharini kutoka Wizara ya Ujenzi na uchukuzi, Sekta ya Uchukuzi Stela Katondo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Desemba 12, 2022.
Baadhi ya wadau wa habari kutoka nchi 15 wakiwa kwenye warsha ya siku tatu wakijadili itifaki ya usimamizi wa habari na mazingira.

WASANII WAZIJUE FURSA ZA KIPATO KATIKA MUZIKI

$
0
0

 

Mkuu wa TuneCore Magharibi na Afrika Mashariki, Chioma Onuchukwu, alizungumza juu ya haja ya kufundishwa upya kwa wasanii kuelewa fursa za mapato katika tasnia ya muziki, ikiwa ni pamoja na haki za uchapishaji na mapato ya mrabaha, wakati wa mjadala wa jopo lililomalizika hivi majuzi 2022. toleo la Kongamano la Muziki Barani Afrika kwa Ushirikiano, Mabadilishano na Maonyesho (ACCES) jijini Dar es Salaam, Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita. Mkutano huo wa kila mwaka huwaleta pamoja wasanii, mawakala wa watalii, mameneja, lebo, wakala wa usambazaji na wadau wa tasnia ya muziki kwa mfululizo wa warsha na vikao vya kubadilishana mawazo, kugundua vipaji vipya na kuharakisha uundaji wa sekta ya muziki iliyochangamka barani Afrika.


Chioma Onuchukwu alijumuika katika kikao hicho na watendaji wengine wa tasnia ya muziki ambao ni pamoja na Karabo Senna, Meneja Mkuu wa Leseni na Mauzo - SAMRO (Afrika Kusini); Mamby Diomandé, Mkuu wa Live and Brand - Universal Music Africa (Ivory Coast); Thando Makhunga Mkurugenzi Mkuu - Sheer Publishing Africa katika Downtown Music Services (Afrika Kusini) na Lerato Matsoso Meneja Mahusiano ya Wadau na Uanachama - CAPASSO (Afrika Kusini) kujadili Mito ya Mapato Isiyotumika kwa Watayarishi wa Muziki barani Afrika.

Katika maelezo yake, alitaja hakimiliki na uchapishaji kama baadhi ya njia muhimu zaidi za mapato barani Afrika ambazo hazijatumiwa. Alihusisha hili na ukosefu wa uelewa wa upande wa biashara ya sekta hiyo.

"Kuna habari nyingi zinazopatikana kuhusu kuchuma mapato kwa muziki wako, kwa hivyo wasanii wanapaswa kuwa na ufahamu bora wa matarajio ya mapato ya muziki. Kama msanii, unapaswa kuendelea kutafuta fursa za kuongeza mapato ya muziki na kukuza thamani ya chapa yako. Kuna habari nyingi zinazopatikana kwenye majukwaa kama vile mitandao ya kijamii, tovuti za muziki, na hata kutoka kwa wataalamu katika biashara ya muziki. Wanamuziki wengi hawana habari kuhusu vipengele hivi vya tasnia ya muziki, jambo ambalo linazuia maendeleo yao kuelekea kujenga kazi yenye faida kubwa” - Chioma Onuchukwu, Mkuu wa TuneCore Afrika Mashariki na Magharibi.

TANGAZO LA AJIRA

$
0
0

 


Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania hivi karibuni alitangaza nafasi za ajira kwa vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), waliopo kwenye makambi na nje ya makambi wenye elimu ya kidato cha Nne, Astashahada, Stashahada, Stashahada ya juu na Shahada kulingana na sifa zilizoainishwa katika tangazo hilo.

Sifa za Waombaji.
a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.

b) Awe amehitimu mafunzo ya JKT/JKU

c) Awe amehitimu kidato cha nne kuanzia mwaka 2016 na kuendelea mwenye umri kuanzia miaka 18 hadi 25.

d) Wahitimu wa Shahada, Stashahada ya juu na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 30.

e) Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA).

f) Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa serikali.

g) Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.

h) Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.

i) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo)

j) Awe na urefu usiopunguwa futi tano(5.5) kwa wanaume, na futi tano inchi tatu (5’3”) kwa wanawake.

k) Awe hajawahi kutumia madawa ya kulevya.

l) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.

m) Awe hajaajiriwa na taasisi nyingine ya serikali.

n) Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.

o) Waombaji watakaofaulu usaili ndio watakaochaguliwa.

p) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa

q) Kwa mwenye elimu ya Astashahada, Stashahada, Stashahada ya juu na Shahada awe na fani zilizoainishwa kwenye (kiambatisho ‘A’).

Kama ilivyoelekezwa katika tangazo hilo, mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 27/12/2022. Kwa waombaji wahitimu wa kidato cha nne wenye sifa tajwa hapo juu waliopo Mkoa wa Mbeya walete maombi yao moja kwa moja ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya iliyopo Forest ya zamani barabara ya mahakama kuu kwa hatua zaidi za kiofisi.

Pia kwa mwananchi yeyote mwenye mashaka na mwenye uhitaji wa uelewa kuhusu tangazo hili afike ofisi ya kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya kwa maelekezo zaidi.

Aidha nitoe rai kwa wazazi, walezi na vijana waombaji wa ajira hizi kuhakikisha wanafuata taratibu za uombaji wa ajira hizi ili kuepuka matapeli au wadanganyifu ambao wanaweza kuwalaghai kwa kuwataka kutoa kiasi fulani cha fedha.

Utaratibu wa kutuma Maombi.

i. Waombaji wote waandike barua za maombi wao wenyewe kwa mkono (Handwriting) bila kusahau namba zao za simu, kivuli cha kitambulisho cha NIDA au namba ya NIDA kwa ambao bado hawajapata kitambulisho, cheti cha kuzaliwa, cheti cha elimu ya kidato cha nne na cheti cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kwa anuani:-

Mkuu wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu ya Polisi,
S.L.P 961,
DODOMA.

K.K
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya,
S.L.P 260
MBEYA.

Kwa maelezo zaidi niwatake waombaji wote kutembelea tovuti ya Jeshi la Polisi Tanzania www.policeforce.go.tz

Imetolewa na,
Benjamin E. Kuzaga,
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya.

WATANZANIA TUTUNZE RASILIMALI ZA MISITU-MAJALIWA

$
0
0

 


*Akabidhi hundi mbili zenye thamani ya shilingi bilioni 4.27 zilizotokana na hewa ukaa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka Watanzania watunze rasilimali za misitu kwa kuwa zinafaida kubwa kwa Dunia, Taifa na mwananchi mmoja mmoja.


Amesema kuwa katika vipindi tofauti Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza juu ya umuhimu wa kuhifadhi misitu nchini, hivyo kila mmoja ahakikishe anazingatia suala hilo.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Desemba 12, 2022) alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Kagunga Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi baada ya kukabidhi hundi mbili zenye thamani ya shilingi bilioni 4.27. Fedha hizo zilizotolewa na taasisi ya CARBON TANZANIA kwa wananchi wa vijiji vinane na Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika zimetokana na mauzo ya hewa ya ukaa awamu ya sita.

“Fedha hizi mmezipata kutokana na tabia yenu nzuri ya utunzaji wa misitu, endeleeni kuitunza misitu hii ili tupate mvua za kutosha. Pia, tumieni mvua hizi zinazoendelea kunyesha kwa kupanda mazao mbalimbali.”

Mheshimiwa Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini waendelee kuweka mikakati ya kuwaelimisha wananchi kuhusu utunzaji wa mazingira. “Kila mtumishi wa umma kwenye eneo lake ahakikishe moja ya agenda iwe uhifadhi wa mazingira.”

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka halmashauri zote zenye miradi ya hewa ukaa zifuatilie mikataba inayosainiwa baina ya makampuni na vijiji kwa ajili ya mauzo ya hewa hiyo. “Mikataba hii ni lazima tuijue, wanasheria wetu lazima muifuatilie.”

Waziri Mkuu amewataka wana-Vijiji watumie fedha wanazozipata kutokana na mauzo ya hewa ya ukaa kwa maslahi ya wananchi wote. “Wakurugenzi fuatilieni kama mipango ya wanavijiji ina maslahi kwa wananchi wote, jengeni miundombinu ya umma, posho isichukue nafasi kubwa.”


WAZIRI MKUU AAGIZA HOSPITALI YA KATAVI IANZE KUTOA HUDUMA

$
0
0

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, Dkt. Patrice Serafin ahakikishe ifikapo Januari Mosi , 2023 hospitali hiyo iwe imeanza kutoa huduma kwa wananchi.

 

Waziri Mkuu Kassim ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Disemba 12, 2022) baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambayo inatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 12.4 itakapokamilika na imefikia asilimia 92 ya ujenzi.

 

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Meneja wa TANESCO mkoa wa Katavi kuhakikisha ifikapo Disemba 23, 2022 awe amefikisha huduma ya umeme katika hospitali hiyo.

 

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia kutoa shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali hiyo.

 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi amesema kukamilika kwa hospitali hiyo kutawezesha kulaza wagonjwa 170 na hivyo kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kwa jamii.

 

Ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mheshimiwa Dkt. Samia imeanza kuweka huduma ya kipimo cha CT-SCAN katika hospitali zote za mikoa. “Kwa mara ya kwanza Katavi watapata huduma ya kipimo cha CT-SCAN katika hospitali hii.” 

 

Naye, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia amedhamiria kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.

 

“Dhamira hii njema ya Rais Dkt. Samia tunaiona na ndio maana hapa manispaa ya Mpanda kunajengwa vituo vya afya vitano na vipo katika hatua ya umaliziaji, pia ametoa shilingi milioni 150 kwa ajili ujenzi wa zahanati”


KAMPENI YA NMB MastaBata ‘KOTE KOTE’ YAZIIDI KUPASUA ANGA

$
0
0

 

Meneja Mwandamizi Biashara za Kadi Benki ya NMB, David Ngusa (kulia) na Meneja wa NMB Tawi la Bank House, Seka Urio (kushoto) wakimkabidhi tiketi ya kuhudhuria tamasha la Fullmoon Party visiwani Zanzibar, Elihuruma Minja (katikati), mshindi wa droo ya nne ya Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote’ inayohamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu.

***************

Kampeni ya NMB MastaBata ‘Kote Kote,’ inayoendeshwa na Benki ya NMB, imezidi kupasua anga baada ya zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 10.5 kutolewa kwa washindi 76 jana, hivyo kufanya jumla kuu ya zawadi kufikia zaidi ya Sh. Mil. 96.5 kati ya Sh. Mil. 350 zilizotengwa.

Washindi 76 walipatikana wakati wa droo ya tano iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambako pia washindi wa pikipiki wa droo ya nne na washindi wa safari ya Zanzibar iliyolipiwa kila kitu na NMB, walikabidhiwa zawadi na tiketi zao.

Katika droo hio iliyochezeshwa chini ya Ofisa wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT), Salim Bugufi, ilishuhudiwa David Kaaya akiibuka mshindi wa bodaboda yenye thamani ya Sh. Mil. 3, huku washindi wengine 75 wakijinyakulia Sh. 100,000 kila mmoja.

Katika hafla hiyo, Elihuruma Minja na Grace Mponeja walikabidhiwa tiketi za safari ya kwenda Zanzibar (wao na wenza wao), ambako watahudhuria tamasha la Zanzibar Full Moon Party, huku Hamza Hamood akikabidhiwa pikipiki aliyoshinda katika droo iliyopita.

Akizungumza kabla ya droo hiyo, Meneja Mwandamizi Biashara za Kadi NMB, David Ngusa, alisema tayari zawadi zenye thamani ya Sh. Mil. 86 zilishatolewa kwa washindi mbalimbali waliopatikana katika wiki nne za kampeni hiyo inayofanyika kwa msimu wa nne sasa.

“Ni kampeni inayohamasisha matumizi ya kadi badala ya pesa taslimu ‘cashless,’ ambayo ni salama na nafuu zaidi, ambako tumetenga zaidi ya Sh. Mil. 350 kuwazawadia wateja wetu wanaotumia kadi za NMB mastercard kwa kutumia POS, Online au Lipa Mkononi (QR Code).

“Kila wiki tunakabidhi Sh. Mil. 7.5 kwa washindi 75, huku tukitoa pikipiki moja. Lakini pia tuna droo za mwezi, tunakowazawadia Sh. Mil 1 washindi 49, sambamba na bodaboda mbili, na droo ya fainali itazawadia safari za Dubai kwa washindi saba na wenza wao kwa siku nne,” alisema Ngusa.

Kwa upande wake, Bugufi alibainisha kuwa usimamizi wa droo za NMB MastaBata uko chini ya GBT, ambayo ni taasisi tanzu ya Serikali yenye jukumu hilo, hivyo kuwataka Watanzania kufanya matumizi yasiyo ya pesa taslimu ili kuwania zawadi mbalimbali za kampeni hiyo.

Baada ya kukabidhiwa tiketi zao za kwenda Zanzibar kuhudhuria Tamasha la Full Moon Party linalofanyika katika fukwe za Kendwa Rocks, Elihuruma na Grace waliishukuru NMB kwa fursa adhimu ya utalii wa ndani waliyoipata mwishoni mwa mwaka wao na wenza wao.

KAMATA ODDS BOMBA ZA NUSU FAINALI WC 2022?

$
0
0

Michuano ya kombe la dunia imefikia patamu sana, hatua ya Nusu Fainali timu zilikuwa 32 na hatimaye sasa zimesalia timu 4, mbili zikitoka bara la Ulaya, moja Amerika Kusini na Moja ni kutoka Afrika. Argentina vs Croatia, Morocco vs Ufaransa. Mchanganuo wa ODDS kubwa na bomba Meridianbet upo kama ifuatavyo.

 

Machaguo spesho ya Meridianbet Mechi hizi.

 

ARGENTINA V/S CROATIA- 13 Disemba 2022

 

Kiwango cha ushindi: Argentina ashinde kwa tofauti ya goli 1 =3.55, Croatia 6.20, Croatia ashinde kwa tofauti ya goli 2=15, Argentina 5.60, Sare ina ODDS ya 3.40

 

Mfungaji wa muda wowote: Messi 2.12, Modric 7.58, Molina Nahuel 13.64, Bruno Petkovic 5.42

 

Mfungaji wa Kwanza: Lionel Messi 4.10, Luke Modric 18, Nikola Vlasic 17, Nahuel Molina 30, Mateo Kovacic 35

 

Njia ya Ushindi: Croatia ashinde muda wa kawaida 4.20, kwa penati 11, Argentina ashinde kwenye penati 11, muda wa kawaida 1.76, muda wa nyongeza 9.00, Croatia ana Odds ya 19

 

Idadi ya kadi: Argentina apate chini ya kadi 2=2.55, kadi 2=3.00, kadi 3=4.10, kadi 4+ 5.40 kumbuka mechi iliyopita ya robo fainali alipata kadi za njano 9, kwenye nusu fainali dhidi ya Croatia lolote linaweza kutokea. Bonyeza hapa kubeti.

 

Idadi ya jumla ya kadi kwa timu zote: chini ya kadi 4=268, kadi 4=3.98, kadi 5=4.22 au ukiona mechi imekuwa ya nguvu sana weka idadi ya kadi 10 unapata odds 30, hizi odds kubwa na bomba unazipata kwenye machaguo spesho ya meridianbet.

 

UFARANSA V/S MOROCCO 14 Disemba 2022

 

 

Kufuzu Fainali: Ufaransa ana odds ya 1.25, Morocco ana 4.20

 

Goli la Mwisho: Ufaransa afunge goli la mwisho kwenye mechi 1.48, Morocco awe wa mwisho kufunga goli 3.60

 

Kiwango cha ushindi: Ufaransa ashinde kwa toafauti ya goli 1=1.50, goli 2=4.70, goli 3=5.60 kwa upande wa Morocco, ashinde kwa toafauti ya goli moja= 8.20, goli mbili kamili=23. Kwenye mechi hii ushindi wa mabao yeyote unawezekana, kwa timu kama Ufaransa yenye Mbappe, Giroud, Dembele au Morocco yenye Hakim Ziyech, Sofiane, Achraf Hakim inakosaje mabao mechi hii. Bofya hapa kubashiri sasa.

 

Mfungaji wa muda wowote: Olivier Giroud ana odds ya 2.71, Sofiane Boufal 7.33, Rabiot Adrien 7.51, HakimZiyech 6.95, Tchouameni Aurelien 8.65, Mbappe 2.21

Njia ya Ushindi: Ufaransa ashinde goli moja tu baada ya muda wa kawaida ana odds ya 1.50, goli 2 kwa Morocco=6.20, Goli moja baada ya muda wa nyongeza 8.20, goli moja la penati ina 13. Morocco ashinde bao 2 baada ya penati 13. Bonyeza hapa kuona na kubashiri.

 

 

Pia Meridianbet wana kasino mtandaoni ambayo ina michezo mingi sana, kama vile AVIATOR, TITAN DICE, TITAN ROULETTE na mingine mingi. Kushiriki mchezoni ni rahisi sana.

 

CHEZA HAPA

 

WAKUFUNZI MASUALA YA WENYE ULEMAVU WANOLEWA STADI ZA MAISHA

$
0
0
 Na: Mwandishi Wetu – MWANZA
 
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imeendelea kutoa elimu ya Stadi za Maisha kwa wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu ili kuwezesha vijana wenye Ulemavu nchini kuelewa njia sahihi za kushughulikia changamoto na mahitaji yao.
 
Akizungumza, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo mkoani Mwanza, Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka ofisi hiyo, Dkt. Mwiga Mbesi ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya vijana nchini ikiwemo kuwapatia mafunzo ya stadi za maisha yatakayo wawezesha kujitambua, kuhimili mihemko, kutatua matatizo na kufanya maamuzi.
 
“Vijana ndio nguvu kazi ya taifa na serikali inatambua mchango mkubwa walionao katika kukuza uchumi wa nchi, hivyo Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu ilianzisha programu ya stadi za maisha ili kuwezesha vijana kujitambua,”
 
Ameeleza kuwa, vijana wenye Ulemavu wapo kwenye hatari zaidi ya kukabiliwa na matendo mbalimbali ya ukatili, hivyo mafunzo hayo yatajikita katika kuhakikisha elimu ya stadi za maisha inajumuishwa kwenye afua na programu za kushughulikia changamoto za vijana wenye Ulemavu.
 
Ameongeza kuwa, awali mwongozo huo wa stadi za maisha umetumika katika kuwajengea uwezo wawezeshaji wa kitaifa wa stadi za maisha 142 kwa kushirikiana na mamlaka za mikoa na serikali ambao wameweza kutoa mafunzo kwa waelimishaji rika 16,390 katika mikoa yote Tanzania bara. Waelimishaji rika hao wametoa mafunzo kwa vijana wapatao 655,600.
 
“Wakufunzi 26 mliopo katika mafunzo haya kama kila mmoja wenu atatoa elimu kwa waelimishaji rika 100 wenye ulemavu tutaweza kuwa na waelimishaji rika 2600, hivyo waelimishaji rika hao wakiweza pia kuwafikia vijana 50 kila mmoja tutakuza uelewa na elimu wa stadi za maisha kwa vijana 130,000 wenye Ulemavu,”
 
Amefafanua kuwa, Wawezeshaji wa kitaifa hivi sasa wapo 379 ikiwemo Maafisa vijana wa halmashauri (185), Maafisa Vijana wa Mkoa (26), Wakufunzi na watendaji kutoka taasisi zanazoshughulikia Watu wenye Ulemavu (26) ambapo idadi ya wawezeshaji hao watatoa mafunzo kwa waelimishaji rika na pia watatoa mafunzo kwa vijana ili ifikapo 2023 vijana wapatao 2,960,000 waweze kunufaika na mafunzo hayo.
 
Vile vile, Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa mwaka 2017 Ofisi ya Waziri Mkuu ilianza kufanya mapitio ya Mwongozo wa stadi za maisha wa mwaka 2009 lengo ikiwa ni kuhakikisha masuala mapya yaliyojitokeza katika duru za kitaifa, kikanda na kitaifa kwa ajili ya maendeleo ya vijana yanahuishwa kwenye Mwongozo.
 
Aidha, amewataka wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu kuhakikisha elimu ya stadi za maisha inawafikia vijana wenye ulemavu ili waweze kujitambua, kuwa na uthubutu na kufanya maamuzi sahihi.
Pia, amewataka vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ikiwemo mikopo inayotolewa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana unaoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na mikopo inayotolewa na halmashauri 4% kwa Vijana, 4% Wanawake na 2% kwa Watu wenye Ulemavu.
 
Naye, Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Rasheed Maftah alieleza kuwa, mafunzo watakayopatiwa wakufunzi na watendaji kutoka kwenye taasisi zinazoshughulikia masuala ya Watu wenye Ulemavu yatawezesha kuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto zinazokabili Watu wenye Ulemavu nchini.
 
Kwa upande wa washiriki wa mafunzo hayo wameshukuru kupata elimu hiyo na wameahidi kutoa elimu hiyo kwa walengwa ili waweze kuwezesha kundi hilo kujitambua na kuona umuhimu walionao katika ujenzi wa maendeleo ya taifa.


Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, Dkt. Mwiga Mbesi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Stadi za Maisha kwa wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu yaliyofanyika leo Disemba 12, 2022 koani Mwanza.

Afisa Maendeleo ya Vijana Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bi. Diana Kasonga akitoa elimu wakati wa mafunzo hayo.Afisa Maendeleo ya Vijana Mkuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Godfrey Massawe akitoa elimu wakati wa mafunzo hayo.Mwezeshaji Bw. Robert Semkiwa (aliyesimama kushoto) akifafanua jambo kuhusu stadi za maisha kwa wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu. Kulia ni Mwezeshaji wa Stadi za Maisha kitaifa, Bi. Rhoda Kagogo (aliyesimama).Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma kwa Watu wenye Ulemavu, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Rasheed Maftah akieleza jambo wakati wa mafunzo hayo kuhusu Stadi za Maisha kwa wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu yaliyofanyika mkoani Mwanza.

Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, Dkt. Mwiga Mbesi (hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa mafunzo ya Stadi za Maisha kwa wakufunzi na watendaji wa masuala ya Watu wenye Ulemavu yaliyofanyika mkoani Mwanza.



AKO TANZANIA WAKABIDHI VYOO VIPYA KAMBI YA CHOKAA

$
0
0

 

Na Mwandishi wetu, Simanjiro


SHIRIKA lisilo la kiserikali la AKO Ujerumani kupitia Tawi lao la AKO Tanzania Community Support limekabidhi mradi wa vyoo vya kisasa kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kambi ya Chokaa Kata ya Naisinyai, Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara.

Mkurugenzi wa AKO Tanzania Community Support Hilda Kimath akizungumza wakati wa kuvikabidhi amesema vyoo hivyo vimetumia kiasi cha shilingi milioni 68.

Kimath amesema vyoo hivyo vina matundu 14 vitakavyotumiwa na wasichana matundu nane na wavulana matundu sita.

"Kwenye matundu nane vya wasichana kipo kimoja cha walemavu na matundu sita ya wavulana kipo kimoja cha walemavu pia," amesema Kimath.

Diwani wa kata ya Naisinyai, Taiko Laizer amelishukuru shirika la AKO Tanzania kwa kuwajengea wanafunzi hao vyoo hivyo kwani wameisaidia serikali kutimiza wajibu wake.

Afisa elimu vifa na takwimu wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Abdalah Hamis amewataka walimu na wanafunzi kuhakikisha wanatunza miundombinu ya vyoo hivyo ili vidumu muda mrefu.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Praxeda Tarimo amesema AKO Tanzania kabla ya kujenga vyoo hivyo pia wametoa misaada mbalimbali ikiwemo ujenzi wa darasa la awali.

“Pia AKO Tanzania wamesaidia ujenzi wa majiko ya wanafunzi wa darasa la awali na shule ya msingi pia wamefanikisha maji shuleni, chakula kwa wanafunzi, printa na mashine ya photocopy,” amesema Tarimo.

Mwanafunzi wa darasa la sita wa shule ya msingi Kambi ya Chokaa, Christina Julius amesema wanawashukuru AKO Tanzania kwa kuwajengea vyoo hivyo kwani vya awali vimechakaa.

“Sasa hivi tunajisitiri vyema tukiwa faragha na pia tumetengewa eneo maalum la kubadili taulo za kike kwa wale wasichana wakubwa waliopevuka,” amesema.






 

WAZIRI MKUU KUFANYA ZIARA MKOA WA RUKWA

$
0
0

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) atafanya ziara ya kikazi ya siku tatu (3) mkoani Rukwa kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo , kuongea na wananchi pamoja na watumishi wa umma.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mheshimiwa Queen Sendiga leo kwa waandishi wa habari imesema Mheshimiwa Majaliwa atawasili mkoani Rukwa tarehe 14 Desemba,2022 na atahitimisha ziara yake tarehe 16 Desemba 2022 ambapo atetembelea Wilaya tatu za Nkasi,Kalambo
na Sumbawanga.

Sendiga alibainisha kazi zitakazofanyika kuwa ni: Kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Shule ya Sekondari Paramawe- Nkasi,kutembelea mradi wa jengo la upasuaji na jengo la huduma za dharura (EMD) Hospitali ya Wilaya Nkasi,Kuweka jiwe la msingi jengo la Utawala Halmashauri ya Wilaya ya
Kalambo, Kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya Matai-Kasesya na Kukagua ujenzi wa Chuo cha Ualimu Sumbawanga.

Wito umetolewa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye maeneo yatakayotembelewa na Waziri Mkuu.Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Queen Sendiga akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Sumbawanga kuhusu ujio wa Waziri Mkuu atakayewasili tarehe 14 Desemba 2022 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.(Habari na Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa) 

Viewing all 48893 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>