Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 49551 articles
Browse latest View live

RAIS MAGUFULI AWAJULIA HALI WAGONJWA WALIOLAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA CHATO PAMOJA NA MZEE ZEFANIA KANOGE PETRO (82) AMBAYE ALIMSHAWISHI KUINGIA KWENYE SIASA

$
0
0


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mzee Zefania Kanoge Petro 82 ambaye anapatiwa matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Chato mkoani Geita. Mzee Kanoge ndiye aliyemshawishi Mhe.Rais Dkt. Magufuli kuingia kwenye Siasa wakati alipokuwa akifanyakazi katika Mkoa wa Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muungano ya Chato wakati wakati alipowakuta katika Kiliniki wa Baba Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Chato wakisubiri kuchomwa Sindano za Chanjo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wazazi waliowapeleka watoto wao kupewa chanjo katika Kliniki ya Baba Mama na Mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Chato.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi mbalimbali pamoja na Madaktari wa Hospitali hiyo ya Chato mara baada ya kuwajulia hali wagonjwa pamoja na kutembelea Kliniki ya Watoto hospitalini hapo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafiwa katika msiba wa mzee Mariganya Ng’wenge aliyefariki tarehe 4/11/2019 na anatarajiwa kuzikwa kesho Choto mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwanunulia madaftari wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato Ladislaus , Daudi Petro na Shemila Mlegete mara baada ya kukutana nao katika eneo la Chato mjini wakati wakitokea shuleni kwao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika kaburi la Shangazi yake Salome Michael Nyahinga katika eneo la Chato wakati akitokea kuhani Msiba wa Mzee Mariganya Nghwenge katika eneo la Ginnery Chato mkoani Geita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza mkazi wa Chato Venance Magege wakati aliposimama kuwasalimia wananchi wa Chato mjini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanachi wa Chato mjini mara baada ya kusimama kuwasalimia wakati akitokea kuhani msiba wa mzee Mariganya Ng’wenge katika eneo la Ginnery  Chato mkoani Geita.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na wanafunzi wa Shule ya Msingi Chato Shemla Mlegete wakwanza kushoto, Ladislaus katikati pamoja na Daudi Petro mara baada ya kuwaona wakati akitoka akizungumza na wananchi wa Chato.
Picha ya Kumbukumbu- Marehemu mzee Mariganya Nghwenge aliyefariki juzi akiwa ameshikilia Mhogo mrefu alipokuwa akimuonesha Rais wa kwanza wa Tanzania Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere (haonekani pichani) mwaka 1967 katika eneo la Ginnery Chato mkoani Geita. Mzee huyo alikuwa akionesha namna gani alikuwa Mkulima bora katika kipindi hicho. PICHA NA IKULU

NBC yaendelea kuwapa mbinu za kibiashara wafanyabiashara jijini Dar

$
0
0
 Mkurugenzi wa Bima wa Benki ya NBC, Benjamin Nkaka (kulia) akisalimiana na wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Ubungo katika semina ya siku moja ilyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji za mbinu za kufanya biashara zao  jijini  Dar es Salaam jana.
 Meneja wa Kanda ya Dar es Salaam wa Benki ya NBC, Rachel Mwalukasa (kulia), akizungumza na wafanyabiashara wa maeneo ya Ubungo jijini humo jana kuhusu huduma na bidhaa zotolewazo na benki hiyo hususani wakati wa semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa kushirikiana na wadau muhimu kutoka taasisi mbalimbali zinazuhusika na masuala ya biashara.
 Mwakilishi kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Gwakisa Bapala (kulia), akizungumzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na baraza hilo wakati wa semina kuhusu mbinu mbalimbali za kufanya biashara iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati katika Ukumbi wa Hoteli ya Millenium Towers jijini Dar es Salaam juzi.

 Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa Kati na Wadogo wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo akizungumza katika semina ya siku moja ya  wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Ubungo  iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara zao  jijini  Dar es Salaam juzi.

 Meneja Ukuzaji wa Biashara wa NBC, Jonathan Bitababaje akichangia mada wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Benki hiyo ya wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa lengo la kuwawezesha kimafunzo kuhusu ukuaji wa biashara zao  jijini  Dar es Salaam juzi.

 Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakisikiliza kwa makini baadhi ya mada zilizokuwa zikitolewa katika Semina hiyo kutoka wadau mbalimbali wakiwemo Mamlaka ya Mapato (TRA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Makampuni (Brela), Chemba ya Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA),  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na wengineo.

Baadhi ya wafanyabiashara wa maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam wakisikiliza baadhi ya watoa mada katika semina iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wafanyabiashara hao juzi. 
Msaidizi wa Msajili Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), George Chuwa akizungumza wakati semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati wa maeneo ya Ubungo jijini Dar es Salaam jana.

SBL yatoa punguzo kubwa la bei kwa wateja wa vinywaji vikali

$
0
0

Watumiaji wa pombe kali zinazosambazwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), wana kila sababu ya kufurahi msimu huu wa sikukuu, baada ya kutangazwa kwa punguzo kubwa la bei kwa aina mbali mbali ya vinywaji vikali.

Ikiwa ni sehemu ya kuonyesha kuwajali katika msimu wa sikukuu, SBL jana ilizindua punguzo kubwa la bei kwa vinywaji vyake vikali ili kuwawezesha wateja wake kuwanunulia ndugu jamaa na marafikizawadi za  vinywaji vyenye ubora wa kimataifa kwenye sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya.

Akiongea na waandishi wa habari waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo kilichopo Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti alisema kampeni hiyo inalenga kuwahamasisha wateja wake kufurahia sikukuu pamoja na wawapendao kwa kuwanunulia pombe kali zinazosambazwa na kampuni hiyo kama Johnnie Walker, Captain Morgan, Ciroc, Smirnoff Vodka na nyinginezo kwa punguzo kubwa la bei.

“Kampeni hii ya kutoa zawadi, inaenda sambamba na wito wetu wa kunywa kistarabu ambapo tunawaelimisha wateja wetu kuepuka kutumia vilevi na kisha kuendesha vyombo vya moto,” alisema Ocitti.

Ni mwaka wa tano sasa kampuni ya SBL inaendesha ya kampeni ya unywaji wa kistarabu kwa kushirikianba na Jeshi la Polisi Kitengo cha Usalama barabarani pamoja na wadau wengine wa usalama barabarani.

Kwa upande mwinginre, Ocitti alizungumzia mwenendo wa kibiasahara wa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na upanuzi wa viwanda vyake vya Dar es Salaam na Moshi unaogharimu Pauni za Uingereza milioni 14. Upanuzi huo utakapokamilika,  utaiongezea kampuni hiyo uwezo wa uzalishaji kwa asilimia 34 zaidi.
  
“Upanuzi tunaofanya, unaonyesha nia yetu ya kupanuka na kuongeza upatikanaji wa bidhaa zetu pamoja na kutengeneza ajira zaidi. Upanuzi huu pia utaongeza mahitaji ya malighafi tunazonunua kutoka kwa wakulima wa ndani kwa ajili ya kutengeneza bidhaa zetu,” aliongeza.

Kampuni ya SBL imenunua tani 17,000 za ujazo za mahindi na uwele kutoka kwa wakulima wa ndani sawa na asilimia 70 ya jumla ya mahitaji yake yote ya malighafi kwa mwaka. SBL pia imelipa jumla ya shilingi 121bn/- kama kodi za aina mbali mbali kwa mujimu wa Ocitti.
 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Mark Ocitti, akizungumza na wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari waliotembelea kiwanda cha kampuni hiyo cha Dar es Salaam kujionea upanuzi mkubwa unaoendelea kiwandani hapo.


 


Meneja Afya na Usalama Mahali pa Kazi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) David Mwakalobo (kulia) akifafanua jambo kwa baadhi wahariri kutoka vyombo mbali mbali vya habari waliotembelea kiwanda cha Dar es Salaam kujionea upanuzi mkubwa unaoendelea kiwandani hapo.

Bilioni 205 za Dhihirisha “Utakimu” wa Biteko

$
0
0







Issa Mtuwa – “WM” Nzega

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema ataendelea kuongea kwa namba (takwimu) badala ya maneno huku akitamba kuwa wizara yake itavuka malengo ya makadirio ya makusanyo ya fedha zilizopangiwa na wizara yake kukusanya ambayo ni bilioni 475 katika mwaka wa 2019/20 huku akibainisha kuuwa ndani ya miezi 5 tu teyari wizara yake imeshakusanya bilioni 205.

Ameyasema hayo leo tarehe 7/12/2019 Wilayani Nzega alikokwenda kukabidhi Leseni 11 kwa vikundi 10 vya wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu. Ameongeza kuwa kuongea ongea hakusaidii zaidi ya kufanya kazi na ukifanya kazi acha namba zikusaidie kueleza unachokifanya.

Pamoja na kukabidhi leseni hizo, Biteko ametoa masherti kwenye eneo moja la uchimbaji aliloliwekea mashaka kuhusu usalama wake kutokana na hali yake huku akiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya chini ya mwenyekiti wake ambae pia ni Mkuu wa Wilaya Godfrey Ngupula kuhakikisha utaratibu wa usalama umezingatiwa kabla ya kuanza kuchimba.

Vikundi vilivyokabidhiwa leseni hizo ni pamoja na; Msilale Miners Group, Jimbo la Nzega Vijijini, Undomo Miners Group, Hapa Kwetu Group, Umoja wa Wachimbaji Mwanshina, Mkombozi Mining Group, Imalamakoye Miners Group, Salama Miners, Makalanga Minerals Group na Nzega Miners Association.

Biteko amesema uthubutu wake na viongozi wenzake wa wizara nzima ndio unaopelekea kuiweka sekta ya madini kwenye mwendo “mdundo” huku akiahidi yeyote anayetaka kurudisha nyuma mwendo huo hatokubaliana nae.

Ameongeza kuwa, mara kwa mara halali usiku kwa ajili ya kupokea simu za wananchi wakimpa taarifa za utoroshaji wa madini na taarifa mbalimbali. Hata hivyo amesema anakerwa na vitendo vya uchonganishi kwa kutoa taarifa za uongo huku akiwaomba wananchi kutoa taarifaa zenye ukweli na usahihi ili kulisaidia tafia.

“Madini haya si yangu mimi wala ya Rais John Pombe Magufuli, ni madini ya Watanzania na sote tunawajibu wa kuyalinda, kazi yangu ni kusimamia maekezo ninayopewa na Mhe. Rais na kuhakikisha sekta hii inachangia kwenye pato la taifa kama inavyostahili. Narudia tena, anae stahili sifa katika haya yote yanayofanyika kwenye madini sio Mimi Doto Biteko, anaye stahili sifa na pongezi zote ni Rais John Pombe Magufuli kwani yeye ndiye anaye elekeza na mimi ni msimamizi tuu wa kutekeleza yale anayo yaagiza.”. Alisema Biteko.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Leseni kutoka Tume ya Madini Mhandisi Yahaya Semamba amewaambia wanavikundi waliopatiwa leseni kuwa pamoja na kupatiwa leseni hizo wanapaswa kuzingati masherti ya leseni hizo na kwamba watakao kiuka watawafutia leseni yao. Miongoni mwa masherti hayo ni kuhakikisha ulipaji wa maduhuli ya serikali, kutunza mazingira, kuzingatia usalama na masherti mengine yote.

Akiongea kwa niaba ya wanavikundi wenzake waliokabidhiwa leseni Aluna Mgalula amemshukuru Waziri wa Madini na Mkuu wa Wilaya kwa kuwaondelea kero yao ya kupatiwa leseni. Ametoa ushuhuda wa namna alivyokuwa anamsumbua waziri Biteko kwa kumpigia simu hata usiku wa manane huku akipokea na kumsikiliza.

Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wilayani Nzega ametoa pongezi kwa serikali na wizara ya madini huku akimshukuru waziri Biteko kwa namna anavyo wasaidia wachimbaji wadogo katika kuwapatia maeneo mbalimbali na kuwafanya wachimbaji kuwa na utulivu katika kazi zao.

Waziri wa Madini Doto Biteko akikabidhi Leseni ya uchimbaji wa madini ya dhahabu kwa mmoja wa mwakilishi wa moja kati ya vikundi 10 vilivyo kabidhiwa leseni.

Equinor yafanya mahafali ya tano kwa wanafunzi iliyowafadhili

$
0
0

Mgeni rasmi Balozi wa Norway nchini Tanzania , Elisabeth Jacobsen akizungumza na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kwenye sherehe za mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliofadhiliwa kusoma na kampuni ya Equinor Tanzania kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering na Project Management UDSM. Wengine ni Prof. Ulingeta Mbamba wa UDBS, Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dkt. Mette Halvorsen Ottøy, Prof. Egil Tjland wa NTNU, Prof. Prof. Jon Kleppe wa NTNU na Mwakilishi wa bodi ya Norad, Erik Holtar 
Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dkt. Mette Halvorsen Ottøy akizungumza na wageni waalikwa jijini Dar es salaam kwenye sherehe za mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliofadhiliwa kusoma na kampuni ya Equinor Tanzania kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering na Project Management UDSM 
Prof. Ulingeta Mbamba wa UDBS akizungumza na wageni waalikwa 
Mwakilishi wa bodi ya Norad, Erik Holtar akipokea picha ya zawadi kwenye mahafali hayo 
Wahitimu wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi Balozi wa Norway nchini Tanzania , Elisabeth Jacobsen, Prof. Ulingeta Mbamba wa UDBS, Meneja Mkazi wa Equinor Tanzania, Dkt. Mette Halvorsen Ottøy, Prof. Egil Tjland wa NTNU, Prof. Prof. Jon Kleppe wa NTNU na Mwakilishi wa bodi ya Norad, Erik Holtar. 
Mhitimu wa shahada ya Uzamili, Anita Otto Ringia akiwa kwenye picha ya pamoja na Prof. Egil Tjland wa NTNU 
Mhitimu wa shahada ya Uzamili Beatrice Issara akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wahitimu wenzie kwenye sherehe za mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliofadhiliwa kusoma na kampuni ya Equinor Tanzania kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering na Project Management UDSM kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam 
Mhitimu wa shahada ya Uzamili, Pendaeli Mbise akiwa kwenye picha ya pamoja na Prof. Egil Tjland wa NTNU 

………………………………………………… 

Kampuni ya Equinor Tanzania inafuraha kufanya mahafali ya tano kwa wahitimu 14 waliowafadhili kwa kiwango cha Shahada ya Uzamili katika masomo ya Petroleum Geosciences, Petroleum Engineering and Project Management. 

Wahitimu hao wamefadhiliwa kupitia programu ya ufadhili ya Equinor Tanzania, inayofahamika kama ‘Angola Tanzania Higher Education Initiative’ (ANTHEI). Programu hiyo inayosimamiwa na Equinor inatoa ufadhili kamili kwa wanafunzi kumi kila mwaka kusoma Shahada ya Uzamili (MSc) katika masomo ya Petroleum Geoscience and Petroleum Engineering katika Chuo Kikuu cha Norwegian University of Science and Technology (NTNU), ambacho kinafanya kazi kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) 

Programu hiyo imetengenezwa katika muundo ambao wanafunzi wanasoma mwaka mmoja Norway na mwaka wa mwisho wa Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Kwa mujibu wa mkataba wa makubaliano uliosainiwa kati ya Equinor, Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam na NTNU, Programu hiyo ya msaada wa elimu chini ya Equinor, ulianza mwaka 2012 na unafikia mwisho mwaka huu. Jumla ya wahitimu 64 tayari wamefaidika na program hii, kwa na kubahatika kufanya kazi katika vitengo mbalimbali vya serikali pamoja na sekta binafsi. 

Akizungumza wakati wa mahafali hayo, Makamu wa Rais Mwandamizi ambaye pia ni Meneja Mkazi wa Equinor hapa nchini Dkt. Mette Halvorsen Ottøy, alisema, “Equinor inafuraha kufanya kazi kwa kushirikiana na vyuo vikuu ili kufikia lengo lake la kujenga uwezo ambalo ni jambo muhimu katika maendeleo ya sekta muhimu ya gesi nchini Tanzania. Lengo letu ni kuona watanzania wanapata mafunzo ili kuwa na sifa stahiki ili kutoa mchango wao katika ukuaji wa sekta hii kwa namna zote, moja kwa moja na isivyo moja kwa moja .” 

“Hapa Equinor tunatilia mkazo zaidi katika utendaji endelevu duniani kote. Mbinu ya Equinor ni kujenga mazingira endelevu ya shughuli zetu za msingi na kuchangia maendeleo pasipokuwa na kikomo mahali tunapofanya kazi,” aliongeza kusema Dkt. Mette. 

Wakati wa kipindi cha miaka sita ya Equinor kupitia programu yake ya uwezeshaji kumekuwapo na mafanikio ikiwa ni pamoja na maendeleo ya tafiti za Mafuta na Gesi, ambavyo vilipelekea uwepo wa Shahada ya Uzamili katika Fedha na Uhasibu kwenye Mafuta na Gesi (Master for Finance and Accounting in Oil and Gas -MFA-OG) vikitolewa kwa ushirikiano wa Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Stavanger. 

Halikadhalika Equinor imetoa msaada wa kiufundi katika Chuo Kikuu cha Barcelona pamoja na kuhakikisha uwepo wa Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Petroleum Geosciences kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Hii pia ilijumuisha mafunzo wa wakufunzi, ufundishaji kwa njia ya mtandao, na ujenzi wa maabara ya analojia 

Katika nyongeza ya ufadhili, mwaka huu Equinor imejenga maabara ya na kutoa mafunzo kwa mtu wa maabara katika Chuo Kikuu cha Teknolojia ya Uhandisi Dar es Salaam (UDSM), na kuwezesha ufundishaji wa Shahada ya Uzamili katika Uhadisi wa Petroli katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Vodacom kuwaunganisha Watanzania wengi zaidi kwenye intaneti katika msimu huu wa Sikukuu

$
0
0

Meneja wa Vodashop, Mlimani City, Dar es salaam, Vanessa Mlawi (Wapili kulia) na Afisa Mauzo Waziri Khalid (Wapili kushoto) wakizindua ofa ya msimu wa sikukuu inayowezesha fursa ya wateja kuunganishwa na uwapendao kupitia simu ya Smart Kitochi inayopatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini kwa bei nafuu ya TSH 45,000 tu. Hatua hii inalenga kuwezesha Watanzania wengi zaidi kuunganishwa na mtandao wa intaneti na kukuza matumizi ya kidigitali nchini kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na unaominika zaidi.
Meneja wa Vodashop, Mlimani City, Dar es salaam, Vanessa Mlawi (Kulia) na Mteja wa Vodacom Elvira Kamuzora (Kushoto) wakati wa uzinduzi wa ofa ya msimu wa sikukuu inayowezesha fursa ya wateja kuunganishwa na uwapendao kupitia simu ya Smart Kitochi inayopatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini kwa bei nafuu ya TSH 45,000 tu. Hatua hii inalenga kuwezesha Watanzania wengi zaidi kuunganishwa na mtandao wa intaneti na kukuza matumizi ya kidigitali nchini kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na unaominika zaidi. 
Meneja wa Vodashop, Mlimani City, Dar es salaam, Vanessa Mlawi (Kulia) na Afisa Mauzo Waziri Khalid (Kushoto) wakizindua ofa ya msimu wa sikukuu inayowezesha fursa ya wateja kuunganishwa na wapendao kupitia simu ya Smart Kitochi inayopatikana katika maduka yote ya Vodacom nchini kwa bei nafuu ya TSH 45,000 tu. Hatua hii inalenga kuwezesha Watanzania wengi zaidi kuunganishwa na mtandao wa intaneti na kukuza matumizi ya kidigitali nchini kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na unaominika zaidi. 



*************************************** 
 Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC inatoa fursa kwa wateja wake kutoa zawadi ya simu ya Smart Kitochi kwa ndugu, jamaa na marafiki wakati wa Msimu huu wa Sikukuu. 

Hatua hii ya kipekee inalenga kuwawezesha watanzania wengi kujiunga na matumizi ya digitali kama kampuni inayojiendesha kidigitali kwa lengo la kuongeza idadi kubwa ya watumiaji wa intaneti na kupata habari mtandaoni, kupitia mtandao Supa wa Vodacom wenye kasi na inaoaminika zaidi nchini kote. 

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa ofa hiyo katika Viwanja vya Igoma jijini Mwanza, Meneja Mauzo na Usambazaji wa Vodacom, George Lugata alisema, Wakati wa msimu huu wa Sikukuu Vodacom inatambua kuwa kuna umuhimu wa kutoa zawadi lakini pia kuwaunganisha wapendanao, ndiyo maana ya ofa hii. “Wakati wa msimu huu wa Sikukukuu. 

Vodacom inatoa fursa ya kipekee kusambaza upendo nchini kote kwa kumiliki au kumpa zawadi ya simu ya Smart Kitochi ndugu, jamaa na rafiki kwa bei nafuu kabisa ya Sh. 45,000 kutoka Vodacom. 

Katika maono ya kuipeleka Tanzania katika zama za kidigitali, Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kiasi kikubwa imewekeza katika miundombinu ya mawasiliano kupitia mtadao wake wa Supa Network wenye kasi na ambao unawafikia watanzania waliowengi kwa zaidi ya asilimia 92 katika viwango vya 3G, 4G na 4G plus nchi nzima. Hata hivyo jitihada hizi bado zinakwamishwa na uwepo wa matumizi madogo ya simu janja kwa watanzania walio wengi. 

“Tunataka kila mmoja apate uzoefu wa kutumia mtandao wetu wa Supa Network lakini pia afaidike na huduma ya intaneti. Pata Simu ya Smart Kitochi wewe na umpendaye na Vodacom watahakikisha kuwa unaunganishwa katika kipindi chote hiki cha msimu wa sikukuu kwa kukupa Data yenye GB 24, dakika 500 za muda wa maongezi na SMS 200 bure kwa muda wa miezi sita, vyote kutoka Vodacom. Pia utarejeshewa asilimia 10 kwa kila muamala utakaofanya kupitia MPesa, Naomba Watanzania wengi kujitokeza katika promosheni hii iliwaweze kuunganishwa katika huduma hizo muhimu,” alisema Lugata. 

Ikiwa na betri yenye nguvu ya 1400mAh ambayo inaiwezesha kukaa kwa muda wa masaa sita ya mazungumzo, Smart Kitochi inatumia laini mbili za simu, lakini pia ni chaguo sahihi kwa watanzania waliowengi katika soko la simu hapa nchini. 

Smart Kitochi ina apps maarufu kama Facebook, WhatsApp, YouTube, Instagram, Google Assistant na nyingine nyingi zitakazomuwezesha mtanzania kuwa katika jamii ya watumiaji wa intaneti. 

“Wateja wetu wanaweza kupata simu ya Smart Kitochi katika maduka yetu yote ya Vodashop nchi nzima, na kupitia katika magari yetu maalumu wakati wa msimu huu wa sikukuu, matamasha yetu yatafanyika katika mikoa mitano ambayo ni Mwanza, Arusha, Dodoma,
Mbeya na Dar es Salaam. 

Msimu huu wa Smart Kitochi unaambatana na matukio kadhaa ya kusisimua kama vile mashindano ya dansi, na burudani mbalimbali za katika mikoa hiyo mitano. Lengo la promosheni ni kuhakikisha kuwa tunawafikia watanzania wengi kwa kuwaunganisha katika maisha ya kidigitali,” 

Pamoja na ofa hii, Vodacom itakuwa ikifanya usajili wa laini za simu kwa alama za vidole. ‘Wateja wetu wanatakiwa kujitokeza kwa wingi kwa kuzingatia umuhimu wa zoezi hili. alisema Lugata

RAIS MAGUFULI PAMOJA NA MKEWE MAMA JANETH MAGUFULI WASALI MISA TAKATIFU DOMINIKA YA PILI YA MAJILIO KATIKA KANISA KUU LA EPIFANIA PAROKIA YA BUGANDO JIJINI MWANZA

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande leo tarehe 8/12/2019.

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande akihubiri katika Misa Takatifu ya Dominika ya pili ya Majilio iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza leo tarehe 8/12/2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wamejumuika pamoja na waumini wengine wa Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza katika Misa Takatifu ya Dominika ya pili ya Majilio iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza MhashamuRenatus Nkwande leo tarehe 8/12/2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikusanya Sadaka ya Ujenzi wa Kanisa katika Misa Takatifu ya Dominika ya pili yaMajilio iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na waumini wa Kanisa Kuu la Epifania Parokia ya Bugando jijini Mwanza katika Misa Takatifu ya Dominika ya pili ya Majilio iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza Mhashamu Renatus Nkwande leo tarehe 8/12/2019.
 PICHA NA IKULU

Vodacom yawapelekea ofa mbalimbali wakazi wa mkoa Kilimanjaro msimu huu wa sikukuu

$
0
0

Meneja wa Vodacom Kanda ya Kaskazini Brigita Stephen(kushoto) akizindua simu ya mkononi aina ya smart kitochi kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini yenye uwezo mkubwa wa internet ya 4G iliyozunduliwa Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wakiwa kwenye hafla ya  uzinduzi wa  simu ya mkononi aina ya smart kitochi kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini yenye uwezo mkubwa wa internet ya 4G iliyofanyika viwanja vya kituo cha mabasi Mjini Moshi.
Baadhi wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom wakifurahia uzinduzi wa  simu ya mkononi aina ya smart kitochi kwa Mikoa ya Kanda ya Kaskazini yenye uwezo mkubwa wa internet ya 4G iliyofanyika viwanja vya kituo cha mabasi Mjini Moshi


Rais Magufuli aweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa meli na chelezo pamoja na ukarabati mkubwa meli 2 Ziwa Victoria

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job Ndugai pamoja na viongozi wengine wakimsikiliza Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria Meja Abel Gwanafyo akitoa maelezo kuhusu miradi hiyo kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa Meli mpya ya M.V Mwanza (Hapa kazi Tu) wakati wakimsikiliza Msimamizi wa mradi wa ujenzi wa Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria Meja Abel Gwanafyo akitoa maelezo kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08,2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihotubia katika Sherehe za Uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job
Ndugai pamoja na viongozi wengine wakivuta kitambaa kuashiria uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria katika sherehe zilizofanyika eneo la
Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwachangia Kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza walipokuwa wakiimba kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Kwaya ya AIC Makongoro ya Jijini Mwanza walipokuwa wakiimba kwenye sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu),Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
Muonekano wa Chelezo inayojengwa katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Job
Ndugai pamoja na viongozi wengine wakiinua mikono juu kwa umoja na furaha mara baada ya uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria katika sherehe zilizofanyika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba
08, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkandarasi wa Ujenzi wa Meli mpya ya M.V Mwanza Bw. Dowan Kim kutoka kampuni ya STX Engine mara baada ya sherehe za uwekaji Mawe ya Msingi Miradi ya Ujenzi wa Meli Mpya ya M.v Mwanza (Hapa kazi Tu), Chelezo na ukarabati wa Meli za M.V Victoria na Butiama katika Ziwa Victoria zilizofanyika katika eneo la Bandari ya mizigo Igogo Jijini Mwanza. Disemba 08, 2019. 
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 08 Desemba, 2019 ameweka jiwe la msingi katika miradi ya ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu, Chelezo na ukarabati wa meli za MV Victoria na MV Butiama katika Ziwa Victoria.

Sherehe za uwekaji jiwe la msingi katika miradi hiyo zimefanyika katika Bandari ya Mwanza Kusini Jijini Mwanza na kuhudhuriwa na wananchi na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri na Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu, Wabunge, viongozi wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Wakuu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa, viongozi wa taasisi mbalimbali, viongozi wa Dini na viongozi wa vyama vya siasa.

Ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa Kazi Tu utakamilika Januari 2021 kwa gharama ya shilingi Bilioni 89.764 ambapo mpaka sasa umefikia asilimia 43.74 na unatekelezwa na kampuni za ukandarasi za Gas Entec Company Limitedna Kangnam Corporation za Jamhuri ya Korea kwa kushirikiana na Suma JKT. Kampuni hizi zimeshalipwa shilingi Bilioni 39.249.

MV MwanzaHapa Kazi Tu itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo, magari makubwa 3 na magari madogo 20, inatarajiwa kufanya kazi kati ya bandari za Mwanza, Kemondo, Bukoba na Musoma pamoja na kwenda nchi jirani za Kenya na Uganda na hivyo kukabiliana na adha ya usafiri kwa wananchi na mizigo katika Kanda ya Ziwa baada ya MV Bukoba kupata ajali ya kuzama majini mwaka 1996 na meli nyingine 4 kuharibika.

Ujenzi wa chelezo unafanywa na kampuni za STX Engine Company Ltd na Saekyung Construction Company Ltd, zote za Jamhuri ya Korea kwa gharama ya shilingi Bilioni 36.4 ambapo mpaka sasa ujenzi umefikia asilimia 68 na wakandarasi hao wameshalipwa shilingi Bilioni 32.85 sawa na asilimia 90 ya fedha zote.

Ukarabati mkubwa wa meli za MV Victoria na MV Butiama unafanywa na kampuni za KTMI Co. Ltdya Jamhuri ya Korea na kampuni ya Yuko’s Enterprises (EA) Co. Ltd ya Tanzania kwa gharama ya shilingi Bilioni 27.71 ambapo mpaka sasa shilingi Bilioni 11.57 zimeshalipwa na kazi imefikia asilimia 65 na 60 mtawalia. 

MV Victoria ina uwezo wa kuchukua abiria 1,200 na mizigo tani 200 wakati MV Butiama ina uwezo wa kuchukua abiria 200 na mizigo tani 100. Meli hizi zitakuwa zinafanya safari kati ya Bandari za Mwanza, Kemondo, Musoma, Bukoba na Nansio-Ukerewe. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) Bw. Eric Benedict Hamissi amesema ujenzi wa chelezo na ukarabati wa meli hizo ambao unafanywa kwa kiwango cha kuzirudisha kuwa meli mpya kabisa unatarajiwa kukamilika Machi 2020.

Bw. Hamissi amempongeza na kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa Serikali kufanya uwekezaji mkubwa wa mara moja ambao haujawahi kutokea tangu Tanzania ipate uhuru, ambapo katika kipindi kifupi cha miaka minne imewekeza shilingi Bilioni 152 katika usafiri kwa njia ya maji, na ameahidi kuwa MSCL itafanya kazi kwa juhudi na maarifa kuhakikisha uchukuzi kwa njia ya maji unaboreshwa ukiwemo mpango mkakati wake wa kuanzisha huduma za usafirishaji mizigo katika Bahari ya Hindi kati ya Dar es Salaam, Comoro, Madagascar, Shelisheli na maeneo mengine.

Mhe. Rais Magufuli amempongeza Afisa Mtendaji Mkuu wa MSCL Bw. Hamissi kwa mageuzi makubwa anayoyasimamia ambayo yameonesha mwelekeo mzuri wa kampuni hiyo ya Serikali ambayo kwa kipindi kifupi imefufua meli nne kati ya 14 zilizoachwa na Hayati Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere na amewapongeza wananchi wa Kanda ya Ziwa kwa kupata matumaini mapya ya kurejeshewa huduma za uhakika za usafiri kama alivyowaahidi wakati akiomba kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Amewapongeza Watanzania wote kwa kuchapa kazi na kulipa kodi zinazotumika kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo, na amesisitiza kuwa kutekelezwa kwa miradi hiyo ni uthibitisho kuwa Watanzania wanaweza hata bila kukopa au kupata ufadhili unaokuja na masharti magumu.

Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali itaendelea kutekeleza miradi mikubwa kwa kutumia fedha za Watanzania wenyewe ikiwemo mpango wa karibuni wa kujenga reli ya Mwanza – Isaka kwa kiwango cha kisasa (standard gauge), kukarabati meli nyingine 5 na ameahidi kuwa Serikali itatenga fedha kwa ajili ya kununua meli mpya itakayofanyakazi katika Bahari ya Hindi kuanzia bajeti ijayo.

Amempongeza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Aloyce Kamwelwe kwa kazi nzuri zinazofanywa na wizara hiyo zikiwemo ujenzi wa meli 3 katika Ziwa Nyasa, ukarabati wa MV Liemba utakaofanyika hizi karibuni, uanzishaji wa Wakala wa Huduma za Bandari (TASAC) na upanuzi wa Bandari za Dar es Salaam, Mtwara, Tanga, Kemondo, Bukoba na Nyamilembe.

Kesho tarehe 09 Desemba, 2019 Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Mkewe Mama Janeth Magufuli atakuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara yatakayofanyika kwa mara ya kwanza katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Mwanza
08 Desemba, 2019

Washindi wa wiki promosheni ya kishindo cha kufunga mwaka walamba mil.5

$
0
0
Meneja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Gwamaka Mwakilembe Akimkabidhi Mausel Magesa Mshindi Wa Milioni Tano katika promosheni ya kishindo ch kufunga Mwaka mkoani Mwanza Mapema wiki hii. 
Mkurugenzi Wa Tigo Kanda Ya Kaskazini Aidan Komba Akimkabidhi Elizabeth Makala Mshindi Wa Milioni Tano Katika Promosheni Ya Kishindo Cha Kufunga Mwaka Mkoani Arusha Mapema Wiki Hii.
Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazin Aidan Komba akimkabidhi Julita Kimaro Mshindi Wa Milioni Moja katika promosheni ya kishindo cha kufunga Mwaka mkoani Arusha Mapema wiki hii. 
Meneja wa Tigo kanda ya Ziwa Daniel Mainoya Akimkabidhi. Tegemeo Enos Mshindi Wa Milioni Tano katika promosheni ya kishindo ch kufunga Mwaka mkoani Mwanza Mapema wiki hii. 

NMB ILIVYOSHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 58 YA UHURU JIJINI MWANZA

$
0
0



Hivi ndivyo benki ya NMB ilivyoshiriki Maadhimisho ya siku ya Uhuru wa miaka 58 yanayoendelea leo katika uwanja  wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.



K-Finance yawaomba Watanzania kukopa kwa ajili ya kuendeleza biashara zao.

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya K-FINANCE inayotoa Mikopo na Ushauri wa Kibiashara kwa wafanyabiashara na watu binafsi Devotha Minzi(katikati), akiwapa Maelekezo Mwenyekiti wa tume ya Ushidani ,Prof.Humphrey Mushi(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa tume ya ushidani, John Mduma wakati wa maonyesho ya kusherekea Siku ya Ushindani duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Judith Minzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya K-FINANCE inayotoa Mikopo na Ushauri wa Kibiashara kwa wafanyabiashara na watu binafsi Devotha Minzi(katikati),akimpa maelekezo mteja(kulia) aliyetembelea banda hilo wakati wa Maonyesho ya siku ya ushindani Duniani yaliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa K-FINANCE Judith Minzi.
Afisa Mikopo wa Kampuni ya K-FINANCE,inayotoa Mikopo na Ushauri wa Kibiashara kwa wafanyabiashara na wateja binafsi Bernadetha Martini akimuelekeza jambo Mteja aliyetembelea bandao hilo wakati wa Maonyesho ya Siku ya ushindani wa kibiashara duniani katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam .


 Kampuni ya K-Finance ambayo hutoa huduma za kifedha na mafunzo ya kibiashara kwa wajasiriamali na kwa watu binafsi, imetoa wito kwa wafanyabiashara hapa nchini kujengea utamaduni wa kukopa na kupata ushauri wa kibiashara kwa ajili ya kukuza mitaji yao.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Judith Minzi wakati ya Maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja.

‘K-Finance ilianzishwa kwa lengo maalumu la kuwasaidia wafanyabiashara wadogowadogo ili kufanikisha matarajio yao kwa ukuaji wa biashara zao na hivyo basi, kukuza na kuchangia uchumi wa nchi. Ukuaji wa biashara sio tu kwa manufaa au kwa faida ya wajasiriamali wenye biashara hizo lakini pia kuna manufaa kwa uchumi kwa ujumla’ Minzi alisema.

Aliongeza kuwa huduma zitolewazo ni pamoja na mkopo wa muda mfupi kwa kiasi cha fedha kinachoanzia na shilingi milioni 1 hadi millioni 50 kwa ajili ya mahitaji binafsi na ya wajasiriamali wenye biashara zinazoendeshwa na zilizosajiliwa kwa taratibu za kisheria ambazo zinahitaji mkopo ili kuendeleza bishara hizo ikiwemo kulipia sehemu za uwekezaji mfano ardhi, fedha kwa ajili ya tenda, pamoja na fedha za kufanyia oda mbalimbali bila kusahau mikopo ya watumishi walioajiriwa katika sekta binafsi kuwapatia fedha za kujikimu, kulipia ada ya shule na kulipa bili mbalimbali. Mikopo inatolewa ndani ya masaa 48 baada ya makubaliano kukamilika na malipo ya mkopo ni kwa muda wa mwezi mmoja(1) mpaka miezi kumi na mbili(12).

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi wa K-FINANCE Devotha Minzi alisema kuwa tangu kuanzishwa kwa kampuni hiyo kumeleta matokeo chanya kwa jamii kwa kutoa huduma za kifedha kwa watu wenye kipato cha chini na cha kati kwa kuwapa mikopo inayowafaa kutokana na mahitaji yao na kuwasaidia kukua kiuchumi na kuwakomboa pindi wanapokuwa na hali ngumu.

K-Finance, imekuwa moja kati ya kampuni kubwa zinazotoa mikopo midogomidogo jijini, na inazidi kuwa kwa kasi mwaka hadi mwaka, alisema mwenyekiti huyo wa bodi huku akiongeza kuwa kampuni hiyo inatarajiwa kuandaa semina kwa ajili ya kutoa mafunzo ya kibiashara Januari 18 mwakani pale Hekima Garden kwa lengo la kuwajengea uwezo wajasiriamali katika kukuza biashara zao na kusihi wote kuhudhuria tukio hilo la kipekee

Benki ya DCB yaibuka kidedea tuzo za NBAA

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya mshindi wa kwanza katika kitengo cha mabenki madogo na ya kati ya Mwasilishi Bora wa Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) kwa Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji wa Benki ya Biashara ya DCB, Nelson Swai katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kulia kabisa ni Mkaguzi wa Hesabu za Ndani wa DCB, Samwel Stephano.
Mkaguzi wa Hesabu za Ndani wa Benki ya Biashara ya DCB, Samwel Stephano (kulia) akionyesha tuzo ya mshindi wa kwanza katika kitengo cha mabenki madogo na ya kati ya Mwasilishi Bora wa Hesabu zinazotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) mara baada ya kukabiodhiwa katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa DCB, Nelson Swai.

Benki ya Barclays yatwaa ushindi Tuzzo za NBAA

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shaban (wa pili kushoto), akikabidhi tuzo ya mshindi wa tatu katika kitengo cha mabenki makubwa ya Mwasilishi Bora wa Hesabu zinazotolewa na  Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) kwa Kaimu  Mkurugenzi wa Idara ya Fedha ya Benki yaa Barclays Tanzania, Bernard Tesha katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  Kulia ni Meneja wa Kitengo cha Usimamizi wa Fedha wa benki hiyo, Muhsin Kaye na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, Prof. Isaya Jairo. 
Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya Barclays Tanzania, Bernard Tesha (kulia), na Meneja wa Kitengo cha Usimamizi wa Fedha wa benki hiyo, Muhsin Kaye, wakionyesha tuzo ya mshindi wa tatu katika kitengo cha mabenki makubwa ya Mwasilishi Bora wa Hesabu zinazotolewa na  Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA) iliyoshinda benki hiyo mara baada ya kukaabidhiwa jijini Dar es Salaam h kwa Kaimu  Mkurugenzi wa Idara ya Fedha ya Benki yaa Barclays Tanzania, Bernard Tesha katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA SHEREHE ZA MIAKA 58 YA UHURU NA 57 YA JAMHURI KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri leo Jumatatu December 9, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli akipokea heshima baada ya kuwasili katika Uwanja wa CCMKirumba jijini Mwanza kuongoza Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 yaJamhuri leo Jumatatu December 9, 2019.
Muonekano wa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati waSherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri zilizoongozwa na RaisDkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu December 9, 2019.
Kikosi cha Makomando wa JWTZ wakioneshaumahiri wao wa kufanya zoezi la uokozi katika mfano wa Tukio laUtekaji.
Kikundi cha Sungusungu cha kutoka Kwimbamkoani Mwanza kikitumbuiza katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru waTanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza.
Baadhi ya Mawaziri wakiimba na kucheza wimbo wa Harmonize wakati wa sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM
Kirumba jijjini Mwanza.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuongoza Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri leo
Jumatatu December 9, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza. 
Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe
zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
 Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 

Wameondoka Majenerali wa Sekta Binafsi Tanzania

$
0
0

Na Paul R.K Mashauri

 Pichani juu kushoto ni Elvis Tables Musiba, Ali Mufuruki na pichani chini  kulia ni Sir. Andy Chande, Ruge Mutahaba pamoja na Dkt. Reginald Mengi enzi za uhai wao.



Miaka michache iliyopita tulimpoteza Elvis Tables Musiba aliyekuwa Mwenyekiti wa TPSF (Tanzania Private Sector Foundation). Mwaka jana tukampoteza Sir. Andy Chande aliyekuwa kiongozi wa sekta binafsi toka enzi za ukoloni. Mwaka huu tumewapoteza wafanyabiashara 3 wakubwa ambao walikuwa viongozi na watu muhimu sana kwa sekta binafsi Tanzania. Dr. Reginald Abraham Mengi aliyekuwa Mwenyekiti wa CTI (Confederation of Tanzania Industries) na TPSF, Ruge Mutahaba aliyekuwa mjumbe wa MOAT (Media Owners Association of Tanzania) na mjumbe wa TRA Stakeholders Forum na jana tumempoteza Mr. Ali Mfuruki aliyekuwa Mwenyekiti wa CEO Round Table.




Vijana wengi wamewaona na kuwasikia hawa watu "the generals" lakini wengi hawajui historia ya sekta binafsi Tanzania na mchango wao katika kuifikisha sekta binafsi hapo ilipo. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoeleza japo kwa kifupi mchango wao kwa sababu kwa namna moja au nyingine wote hawa kuanzia Sir. Andy Chande, Elvis Tables Musiba, Dr. Reginald Abraham Mengi, Mr. Ali Mfuruki na Ruge Mutahaba nimefanya nao kazi za sekta binafsi kwa karibu sana.


Sir. Andy Chande nilifanya naye kazi akiwa ni Mwenyekiti wa "boards" mbalimbali za taasisi kama MOI, IMTU, TRL nk. Na pia alikuwa mshauri katika "board" ya kampuni yangu mwenyewe. Ni bahati mbaya sana kwamba mwezi moja kabla ya kifo chake, mimi na Sir. Andy Chande tulipanga kukutana ili mimi Paul Mashauri nimfanyie "interview" ya namna sekta binafsi ya nchi hii ilivyokuwa kabla na baada ya uhuru. "Interview" ile ilikuwa itumike kama kipindi cha TV ili wengi zaidi wanufaike na uzoefu aliokuwa nao. Bahati mbaya Sir. Andy Chande alifariki kabla hatujakamilisha jambo hilo jema.

Elvis Tables Musiba nilifanya naye kazi akiwa Mwenyekiti wa TPSF na mimi nikiwa mjumbe wa kamati mbalimbali za sekta binafsi Tanzania. Tulisaidiana kuchangisha fedha"fundraising" kwa shughuli mbalimbali za kitaifa, na alitumia wakati huo kunisimulia mambo mengi sana.

Mr. Ali Mfuruki nilifanya naye kazi akiwa ni Mwenyekiti wa CEO Round Table na mlezi wa TRBN (Tanzania Responsible Business Network) chini ya UN Business Compact na mimi nikiwa ni mjumbe wa "secretariat" ya TRBN.

Dr. Reginald Abraham Mengi nilifanya naye kazi yeye akiwa ni Mwenyekiti wa CTI na mimi nikiwa ni mjumbe wa kamati ya SME ya CTI. Na Ruge Mutahaba nilifanya naye kazi wote tukiwa wajumbe wa TRA Stakeholders Forum.

Mara nyingi wote hawa walitumia muda wao mwingi kunisimulia vitu vingi sana wao wakiwa wakubwa kwangu kiumri na mimi nikiwa mdogo sana kwao. Wakati huo nilikuwa sijui kwanini wananiambia mambo yote hayo ya sekta binafsi kwa sababu kwanza nilikuwa mdogo sana na pili sikuwa na nafasi wala heshima kubwa kama walizokuwa nazo wao lakini jana baada ya kupata taarifa za kifo cha Mr. Ali Mfuruki nikagundua pengine walitaka siku moja niyasimulie hayo ili kizazi cha leo kipate kuelewa.

Wafanyabishara vijana, viongozi vijana katika serikali na wajasiriamali vijana wanaochipukia, lazima waelezwe kwamba historia ya sekta binafsi Tanzania haiwezi kuelezwa pasipo majina ya hawa wote niliowataja hapo juu. Lakini pia wapo wengine ambao wameshatutoka na wengine ambao bado wapo hai. Pia sitatenda haki nisipowataja japo baadhi yao.

 Hao ni pamoja na marehemu Mzee Mwakitwange, Dr. Reginald Abraham Mengi, Mzee Anorld Kileo, Dr. Juma Mwapachu, Elvis Tables Musiba, Mzee Iddi Simba na wengine ambao sikupata kuwafahamu. Hawa walikuwa waanzilishi wa TCCIA mwishoni mwa miaka ya 80 kabla ya baadhi yao kuondoka TCCIA na kuanzisha CTI. Kwanini waliondoka na TCCIA kuanzisha CTI? Hiyo ni mada nyingine ambayo inahitaji makala tofauti na hii.

Ukiondoa Mzee Mwakitwange ambaye alitangulia mbele za haki zamani kidogo, wengine wote akiwemo Mzee Anorld Kileo, Dr. Juma Mapachu na Mzee Iddi Simba nimepata kufanya nao kazi na kupata simulizi zao. Mzee Anorld Kileo ambaye alikuwa ni CEO wa TBL kwa muda mrefu sana na kiongozi wa TPSF yeye aliniita ofisini kwake na kunikalisha chini kwa masaa zaidi ya 3 akinieleza sekta binafsi ilipotoka na namna walivyopambana kuifikisha hapo ilipo. Ukurasa huu hautoshi kuandika historia yote ya ujasiriamali Tanzania ambayo vijana wengi wangependa kuijua lakini Dr. Juma Mwapachu aliandika kitabu chenye historia hii vizuri sana. Mimi nitagusia yale niliyoelezwa na hawa "generals" wa sekta binafsi Tanzania kwa kifupi sana.



1. Sir. Andy Chande, Mwanzilishi, Chande Mills

Sir Andy Chande alinieleza kwamba baada ya Uhuru wa nchi hii, Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius K. Nyerere alitaka kumteua kwenye baraza la mawaziri. Lakini akamwambia Mwalimu Nyerere, naomba uniache kwenye sekta binafsi. Mwalimu Nyerere aliheshimu mawazo ya Sir. Andy Chande. Lakini Mwalimu Nyerere akaamua kumteua Sir. Andy Chande kuwa mjumbe wa kamati ya uchumi na maendeleo mara tu baada ya Tanzania kupata uhuru. Kwa vijana wasiomfahamu Sir. Andy Chande huyu ndiye aliyekuwa mfanyabiashara wa kitanzania mwenye nguvu kubwa za kiuchumi wakati wa ukoloni na hata baada ya kupata uhuru. Aliendesha biashara ya kifamilia iliyoitwa Chande Mills ambayo baadaye ilitaifishwa na serikali mwaka 1967 wakati wa "Nationalization" na kuwa NMC (National Milling Corporation) kiwanda ambacho baadaye kilikuja kununuliwa na Bakhresa.


Sir. Andy Chande ndiye aliyekuwa mtanzania mwenye asili ya kiasia kuanza kutoa misaada kwa watu (philanthropism) kuanzia wakati wa uhuru mpaka alipofariki dunia miaka michache iliyopita. Kilichonishangaza kuhusu Sir. Andy Chande ni kwamba hata baada ya serikali kutaifisha biashara yake, bado aliendelea kutumia mtandao wake wa watu "network" akili na maarifa yake kuitumikia nchi. Sir. Andy Chande ananisimulia anasema, baada ya serikali kutaifisha biashara yake, Mwalimu Nyerere alimuita Ikulu, akamuuliza; Rafiki yangu Chande; unataka kwenda wapi baada ya serikali kuchukua biashara yako kwa manufaa ya umma?

Sir. Andy Chande akamuambia Mwalimu Nyerere; "sina pa kwenda". Mwalimu akamuambia "sasa kuanzia leo, wewe ndio utakuwa Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hii mpya inayomilikiwa na wananchi wote wa Tanzania. Sir. Andy Chande akajibu " sawa Mh. Rais". Na ikawa hivyo. Ingekuwa sisi vijana wa leo, rafiki yako ndiyo kiongozi wa nchi au DC au Mkuu wa mkoa au Waziri, anakufahamisha maamuzi ya serikali, tungeleta urafiki na mambo binafsi kwenye mambo ya nchi. Lakini Sir. Andy Chande alikuwa anajua kutofautisha ni wakati gani Nyerere, "rafiki" yake anaongea na ni wakati gani Nyerere, "Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu" anaongea. Alikuwa anajua mipaka yake.

Kutokana na uwezo wa Sir. Andy Chande, Mwalimu Nyerere alimpa uenyekiti wa "boards" nyingi sana ikiwa ni pamoja na TRL, ATC nk. Pia alikuwa Mwenyekiti wa "board" ya Kioo Ltd, Shaaban Robert Secondary School, IST, Barclays bank, Taasisi ya walemavu buguruni nk. Siwezi kuzimaliza zote ni nyingi mno.

Nilikuwa nyumbani kwake Upanga alipokuwa akisimulia haya. Nikamuuliza sasa uliwezaje kukubali kuwa Mwenyekiti wa "board" ya kampuni ambayo umeihangaikia miaka mingi na sasa si yako tena. Akasema mke wangu alinitia sana moyo. Lakini pili kwenye biashara usiweke mambo moyoni. Ukiweka mambo moyoni utakufa. Moyoni nikajisemea; Huyu kampuni yake aliyoisotea miaka mingi imechukuliwa. Tena siyo kampuni yenye mapato ya shilingi milioni 10 au bilioni moja. Unazungumzia mabilioni ya shilingi. Lakini bado maisha yakaendelea. Wewe umepoteza mteja mmoja unataka kufunga biashara. Kwanini? Hayo ni masomo ambayo nataka vijana wengi wayashike, kwamba;

I. Mke au mume wako ana mchango mkubwa sana katika maisha yako ya uongozi, biashara au ujasiriamali. Unapooa au kuolewa lazima uangalie mtu ambaye atakutia moyo wakati ukipitia changamoto za maisha kama ilivyokuwa kwa Sir. Andy Chande. Sio mke au mume ambaye atakukimbia ukifilisika au ukifilisiwa au ukishushwa cheo au ukifukuzwa kazi.

Wakati Sir. Andy Chande akiniambia haya, mke wake alikuwa ni mgonjwa na alikuwa anapata matibabu nchini Uingereza. Pamoja na umri wao mkubwa walipendana sana na kutiana moyo. Na mara nyingi nilipowatembelea niliona Sir. Andy Chande akimhudumia mke wake kwa hali na mali. Kipindi hicho pia Sir. Andy Chande naye hali yake ya kiafya haikuwa nzuri lakini hakuacha kufanya kazi. Alikuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali ya Uingereza na Canada. Sir. Andy Chande alikuwa rafiki mkubwa wa familia ya Malkia wa Uingereza-Qeen Elizabeth, Waziri mkuu wa Canada, na Marais wastaafu akiwemo Mh. Rais Ali Hassan Mwinyi, Mh. Rais Benjamin Mkapa na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

II. Somo la pili ni kwamba ukiwa mfanyabiashara au mjasiriamali, usiweke mambo moyoni, utakufa. Sir Andy Chande na Mwalimu Nyerere walikuwa ni marafiki wakubwa. Lakini maamuzi ya kutaifisha biashara ya Sir. Andy Chande hayakufanywa na mwalimu kama "mtu binafsi" ingawa yeye alikuwa ni mkuu wa nchi. Yalifanywa na serikali. Iwe yalikuwa ni maamuzi mazuri au mabaya, Sir. Andy Chande aliyapokea na kuyaunga mkono. Urafiki wao uliendelea na yeye aliendelea na maisha kama vile hakuna lililotokea.

Leo ukimkopa rafiki yako hela akakuambia hana hela za kukusaidia au hawezi kukupa ana mipango na hela alizonazo, una "mdelete" mpaka kwenye simu yako, "unamblock" facebook, "unamunfollow twitter, instagram na youtube". Ukimpigia simu rafiki yako asipopokea mara 2 au mara 3, unatuma ujumbe mfupi; "acha ujinga pokea simu" hata hujui kama yuko hospitali-ICU kalazwa au bafuni anaoga.


Uko wapi ujasiri wa akina Sir. Andy Chande katika kizazi cha leo? Iko wapi nidhamu ya akina Sir. Andy Chande katika kizazi cha wakati huu? Sir. Andy Chande ananiambia wakati akiwa na Chande Mills, mama Maria Nyerere alikuwa akienda kiwandani kuchukua mabaki ya mahindi kwa sababu alikuwa anafuga. Akasema mama Maria alikuwa hataki akifika kiwandani apewe "priority" wengine wasubiri. 

Alikuwa anapanga foleni kama wanawake wengine. Hata yeye alipojaribu kumshawishi ahudumiwe kwanza alikataa. Vijana wa leo ambao ni viongozi jifunzeni kitu hapa kutoka kwa mama Maria Nyerere. Wake au waume zenu wajishushe. Wasitake kupewa "priority" kwa sababu tu ni wake au waume wa viongozi. Akienda benki au saloon, mwambie na yeye apange foleni kama wengine. Ndio watu wakubwa "great people" wanavyoishi. Hawana makuu ingawa ni wakuu.



2. Elvis Tables Musiba, Mwenyekiti wa zamani, TPSF

Nikiwa mtoto mdogo nilikuwa nasoma vitabu vya Elvis Tables Musiba. Moja kati ya vitabu ambavyo sitopata kuvisahau ni kitabu kinachoitwa NJAMA. Kitabu kile cha kipelelezi kilikuwa kina "character" anaitwa Willy Gamba. Ulikuwa ukisoma vitabu vya Elvis Tables Musiba ni kama unaangalia sinema ya Rambo. Nakumbuka nilipokinunua kitabu kile sikulala usingizi mpaka nilipokimaliza. Willy Gamba alikuwa mtu hatari sana ndani ya ile simulizi. Na Elvis Tables Musiba alikwa ni gwiji na mwandishi mkubwa na mzuri sana. Kila ninapokutana na rafiki yangu Eric James Shigongo ambaye pia ni mwandishi wa vitabu namkumbuka Elvis Tables Musiba. Siku moja nitamuuliza Eric James Shigongo alipata wapi hamasa ya kuandika vitabu. Inawezekana alisoma pia vitabu vya Elvis Tables Musiba.

Nilipokutana na Elvis Tables Musiba nilishangaa kugundua kuwa alikuwa ana kipaji kingine cha biashara na uongozi. Wakati tunachangisha fedha kwa ajili ya kongamano moja katika sekta ya utalii, aliniita ofisini kwake Mirambo House karibu na ofisi za benki ya dunia. Tulikuwa tunahitaji kuchangisha kama shilingi milioni 100. Elvis Tables Musiba akamuomba katibu muhtasi wake amletee simu. Sikuelewa simu ya nini kwenye kuchangisha fedha. Nilitegemea tungeshirikiana kuandika barua na "proposals" za kuchangisha fedha. 

Lakini haikuwa hivyo. Simu ilipoletwa akaanza kazi. Alikuwa anatuuliza mnataka kampuni gani ituchangie fedha. Kwa hiyo kazi yetu ikawa ni kutaja majina ya makampuni na yeye anapiga simu. Nilishangaa kuona Elvis Tables Musiba hahitaji tumpe namba za simu. Alinyanyua simu na kupiga kila tulipotaja kampuni. Na alipopiga hakuongea na katibu muhtasi au mkurugenzi wa fedha. Aliongea na CEO, Director General au Mwenyekiti wa "board". Namba alizipata wapi? sijui. Lakini ndani ya saa moja tulikuwa na shilingi milioni 60.

Nikagundiua huyu si mtu wa mchezo. Ana "connections" za ajabu. Nikamuuliza hebu niambie haya mambo unayafanyafanyaje mbona kwangu mageni? Akasema "reciprocate". Hili ni neno la kiingereza linalomaanisha "rudisha wema'. Elvis Tables Musiba aliwasaidia wengi kufika pale walipo ikiwa ni pamoja na CEOs. Kumbuka amekuwa Mwenyekiti wa "boards" za kampuni nyingi. Wengi wa hawa CEOs ameshiriki kuwafanyia usahili kwa wao kuwa pale. Ndio maana haikumchukua muda kupata milioni 60. Alikuwa akiongea na watu ambao ni sehemu ya mchango wake katika maisha ya mafanikio yao. Hii ikanifanya nimdadisi zaidi. Nikamuuliza wewe ulianzaje biashara?

Akasema mtaji wangu wa biashara ulitokana na kuuza vitabu. Vitabu kama NJAMA ndivyo vilivyonitoa. Lakini nilipoanza biashara haikuwa rahisi. Mimi nilikuwa mtanzania wa kwanza "mswahili" kumiliki "Bureau De Change"-anasema Elvis Tables Musiba. Lakini siku moja nikiwa Musoma, nikasikia kwenye redio kwamba biashara yangu iko mikononi mwa serikali. Kidogo nipate kichaa. Lakini sikukata tamaa nikaanza upya. Akasema nyie vijana wa siku hizi mnalalamika mazingira magumu ya biashara. Nawashangaa sana. Tuulize sisi. Haikuwa rahisi kama mnavyofikiria. Kutoka kwa Elvis Tables Musiba nikajifunza yafuatayo;

I. Biashara ni mahusiano na watu. Elvis Tables Musiba kutumia saa moja kupata milioni 60 sio mchezo. Aliwekeza kwa watu. Leo hii kutafuta Tsh. 10,000/= ya luku ukikwama usiku wa manane na hauna salio kwenye simu ni shughuli pevu. Unaweza ukapiga namba zote kwenye simu yako usipate hata shilingi moja. Lakini Elvis Tables Musiba alitumia saa moja tu kupata shilingi milioni 60. Ina maana kila dakila alipata shilingi milioni 1.

II. Kipaji chako ndio mtaji wako. Badala ya kulalamika huna mtaji, angalia una kipaji gani? Elvis Tables Musiba alikuwa na kipaji cha kuandika hadithi. Ndicho kilichompa mtaji wa kuanzisha biashara. Eric James Shigongo aliwahi kuniambia pia, kwamba kipaji chake cha kuandika hadithi ndicho kilichomsaidia kuanzisha kampuni ya magazeti pendwa na kudumu mpaka leo (Global Publishers). Mifano ni mingi. Bila mpira Mbwana Samata angekuwa wapi? Bila mpira George Weah angekuwa Rais wa Liberia? badala ya kulalamika anza na kipaji chako? Mimi nilianza kwa kuandaa makongamano. Unaweza ukawa unaandaa harusi vizuri kila mtu anashangaa. Lakini bado unafikiri hicho siyo kipaji. Unafikiri kipaji ni "kuimba" tu! Mwenzako makongamano yalinipeleka mpaka Ikulu, yakanipa na mtaji wa kuanza.

III. Usikate tamaa. Elvis Tables Musiba anasema amefilisika mara nyingi katika maisha yake lakini alipambana akarudi tena kwenye mstari. Hakujinyonga. Baadhi ya biashara zake zilikwama. Lakini hakukata tamaa wala hakujenga chuki na watu. Kifupi, hakutafuta mchawi. Alianza upya na kusonga mbele. Alishirikiana na watu katika sekta binafsi na serikalini. Hiyo ndiyo roho ya "ujasiri wa mali" au "spirit" ya ujasiriamali au "entrepreneurship". Ni mlolongo wa kushindwa na kushinda, kushindwa na kushinda mpaka kieleweke.

3. Dr. Reginald Abraham Mengi, Mwenyekiti Mwanzilishi wa IPP Group na Mwenyekiti wa zamani wa CTI na TPSF

Dr. Reginald Abraham Mengi alinishirikisha mwanzoni kabisa wakati akianza kuandika kitabu chake cha "I Can, I Must, I Will". Nakumbuka alinipigia simu akasema njoo ofisini. Akaniambia nataka uwe sehemu ya team itakayonisaidia kukamilisha hili zoezi. Akaniomba nimtafutie vijana wengine wa kushirikliana na Prof. Msamali Nangoli, mwanazuoni wa Uganda aliyekuwa akiishi nchini Kenya, mwandishi wa kitabu maarufu kiitwacho "No More Lies About Africa". Prof. Msalami Nangoli alikuwa rafiki mkubwa wa Nelson Mandela, mpigania Uhuru na Rais wa kwanza wa serikali ya kidemokrasia nchini Afrika ya kusini. Akiwa gerezani, Nelson Mandela alikuwa akisoma makala za Prof. Msamali Nangoli, makala ambazo zilipitishwa gerezani kiujanja kama kifungashio cha chapati. Kumbuka akiwa gerezani, Mandela hakuruhusiwa kusoma hata magazeti.

Ili kukamilisha zoezi la kuandika kitabu cha Dr. Reginald Abraham Mengi chini ya uongozi wa Prof. Msamali Nangoli, nilipewa "tapes" za hotuba za Dr. Reginald Abraham Mengi nyingi sana (mabox kwa mabox) ili nizipitie. Pia tuliwahoji watu wengi waliofanya kazi na Dr. Reginald Abraham Mengi. Bahati mbaya sana katikati ya safari ya kumsaidia Dr. Reginald Abraham Mengi kuandika kitabu chake, Prof. Msamali Nangoli akafariki dunia na Dr. Reginald Abraham Mengi akasitisha zoezi kwa muda. Baadaye akapata namna nyingine ya kumalizia kitabu chake kizuri.

Tulipokuwa na Prof. Msamali Nangoli tulimshawishi sana Dr. Reginald Abraham Mengi kubadilisha "title" au jina la kitabu lakini alikataa. Sisi tulipendekeza kitabu chake kiitwe; Dr. Reginald Abraham Mengi-How I became Rich; Financially, Morally, Materially. Lakini hakutaka hata kutusikiliza. Baadaye nilikuja kugundua tulikuwa tunakosea sana kumshawishi abadilishe jina la kitabu cha "I Must, I Can, I Will". Kwanini?

Kwa sababu siku moja nikiwa nyumbani kwake Kinondoni, nilimuuliza. Kwanini "I Must, I Can, I will"?. Akasema kwa sababu maisha ya biashara yana changamoto sana. Akaniuliza Paul, kwani unafikiri changamoto za biashara Tanzania ni zipi. Moyoni nikasema sasa Dr. ananiuliza swali gani "simple" namna hii. Au anataka kupima uwezo wangu wa kufikiri? Nikamwambia kubwa ni 3. Kwanza Mitaji au "Capital", Pili Masoko au "Markets", Tatu Rasilimali Watu au "Human resource". Akasema umekosa. Akasema kwanza Roho Mbaya, Pili Chuki, Tatu Wivu. Nilichoka kichwa. Akasema ili ufanikiwe lazima ukabiliane na hizi changamoto 3 nilizokutajia kisha uunganishe na hizo za mitaji, masoko na rasilimali watu. Ndio maana ya "I Must, I Can, I Will". Lazima udhamirie kutoka moyoni kupambana na changamoto.

Dr. Reginald Abraham Mengi akasema tulipotoka ni mbali kuliko tulipo. Akasema nakumbuka wakati nimeanzisha biashara ya maji ya kunywa, nilienda kwenye maonyesho ya sabasaba kuonyesha biashara mpya ya maji. Akasema watu waliokuwa wakipita kwenye banda langu walikuwa wananishangaa sana. Wanasema "huyu mchaga anapenda sana hela". Mpaka anatuuzia maji? Kweli leo hii nchi hii tumefikia hatua ya kuuziana maji? Dr. Reginald Abraham Mengi akasema kwa hiyo unaweza ukaona "Kilimanjato Pure Drinking Water" imeshamiri ukafikiri ni lelemama. Haikuwa rahisi. Bora hawa ambao wanaanza kuuza maji leo. Sisi tulioanza tulipata shida. Kwa sababu hakuna aliyezoea kuuziwa maji. Lakini Paul ukweli ni kwamba huwezi kushindana na mtu aliyeanza. Aliyekutangulia amekutangulia tu!

Dr. Reginald Abraham Mengi akaendelea kusema zaidi ya hapo kujenga sekta binafsi haikuwa rahisi. Kumbuka historia ya nchi hii toka kipindi cha wakoloni. Toka enzi hizo biashara zilikuwa kwa matabaka. Wa kwanza pale juu ni wazungu, wa pili waarabu na wa tatu wahindi. Sisi wazawa wa "kiswahili" tulikuwa hatufikiriwi kabisa kuwa "matajiri". Kuna wakati nilinunua Mercedez Benz lakini nilikuwa naogopa kuliendesha. Kwa sababu mifumo ya kiuchumi ilikwishakamatwa na matabaka mengine. Kwahiyo unavyoona sekta binafsi imefika hapa ni mapambano kwelikweli. Mswahili kumiliki kiwanda miaka ya sabini na themanini na Mswahili kuwa kiongozi wa sekta binafsi ambayo haina waswahili wengi ulikuwa ni mtihani ambao ilibidi kuushinda. Haikuwa kazi rahisi. Mimi Paul Mashauri nimeona na kusimuliwa mengi pengine nahitaji kitabu kizima kuzungumza ya Dr. Reginald Abraham Mengi. Lakini kuna mafundisho machache nataka niyataje hapa;

I. Biashara si lelemama. Changamoto ni nyingi kuliko fursa. Lazima ubadilishe hizo changamoto ziwe fursa ili fursa ziwe nyingi kuliko changamoto. Hii haiwezekani pasipo kuwa na moyo mgumu "a iron heart". Kama unataka uache kazi uanze biashara ukifikiri ni mteremko jifikirie tena na tena na tena. Nakumbuka wakati nimemualika Dr. Reginald Abraham Mengi kuongea na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam alirudia hilo. Akasema; "safari ya mafanikio ni kama pambano la ngumi. Kuna makonde ya kuyakwepa, kuna makonde ya kuyazuia ambayo yakikupata yanasambaratisha uso wako au kukuua kabisa lakini kuna wakati ambao lazima ujibu mapigo ili ushinde pambano. Mh. Jokate Mwegelo, DC, Kisarawe, kipindi hicho akiwa chuoni, alikuwa "Moderator" katika tukio hilo. Anaweza akayakumbuka maneno haya.

II. Usiogope kuanzisha njia pasipo na njia. Usiogope kuwa wa kwanza kufanya jambo ambalo wengine wanasita kufanya. Maana yake ni kwamba "be the pioneer". Dunia tunayoishi iko hapa ilipo sababu ya "pioneers". Christopher Columbus angeogopa kusafiri kutoka Spain pengine America (New Land) ingechelewa sana kutambulika katika uso wa dunia. Hata wewe usiwe mtu wa kusubiri wenzako waanze. "Legends" sio wale wanao "copy na kupaste" Legends ni waanzilishi. Kuanza sio lazima iwe ni kwenye biashara. Hata kwenye familia yako unaweza ukawa wa kwanza kuwa "mbunge".


4. Mr. Ali Mfuruki, Aliyekuwa Mwenyekiti wa CEO Round Table

TRBN (Tanzania Responsible Business Network) ilipoanza niliombwa na Partner wa KPMG Ketan Patel pamoja na Partner wa Deloitte Joe Eshun niwe "Moderator" katika sherehe za uzinduzi wa TRBN pale Serena Hotel. Tulikuwa na CEOs zaidi ya 300. Mgeni rasmi alikuwa ni Mr. Ali Mfuruki, Mwenyekiti wa CEO Round Table. Baada ya ufunguzi nilikuwa na muda wa kutosha wa kuongea na Mr. Ali Mfuruki. 

Jambo moja Mr. Ali Mfuruki aliniambia ambalo sitolisahau ni kwamba lazima uwe na msimamo na lazima ukubali kupoteza baadhi ya vitu ikiwa ni pamoja na fedha kusimamia unayoyaamini. Akaniambia nyie vijana sasa hivi ndio mmekuwa mameneja kwenye makampuni na viongozi wa serikali na taasisi mbalimbali. Sasa wakati mwingine unakutana na kijana kwenye kampuni ambaye amepewa mamlaka, kijana ambaye unaweza kumzaa anataka akuzungushe, akunyanyase ili umpigie magoti. Mimi siwezi. Bora nikose hela kuliko kushusha heshima yangu.

Wapo vijana ambao wanamsikia Mr. Ali Mfuruki leo hii lakini hawajakutana na Mr. Ali Mfuruki na kuzungumza naye ana kwa ana. Sijui umesikia nini juu yake lakini Mr. Ali Mfuruki alikuwa na msimamo wa kipekee. Alikuwa anafikiria vizuri sana sio katika biashara zake tu hata kwa nchi. Ndio maana kifo chake kimetushtua kama Taifa. Unaweza ukawa unafikiria vizuri lakini kwa mambo yako binafsi na familia yako. Hilo ni jambo zuri na ndiyo jambo la pili baada ya kumfikiria Mungu. Lakini unapojiongeza na kufikiria Taifa na watu wengine ndani ya Taifa unakuwa wa tofauti zaidi. Ndivyo alivyokuwa Mr. Ali Mfuruki. 

Kuna siku nilikutana naye nikamuuliza Mr. Ali Mfuruki lini unaandika kitabu? Akaniambia nimeanza kuandika. Siku niliposikia ametoa kitabu, nikawahi bookshop Mlimani City kununua. Lakini baada ya kusoma kile kitabu nikagundua nilichofikiria kuwa kitakuwepo kwenye kitabu sicho. Mr. Ali Mfuruki hakuwa ameandika kitabu kuhusu yeye na mke wake na watoto wake. Alikuwa ameandika kitabu kuhusu uchumi wa viwanda. 

Huyo ndio Mr. Ali Mfuruki. Ndiyo sababu alidumu kama Mwenyekiti wa CEO Round Table kwa miaka mingi. Sio kwamba alipenda kuhodhi madaraka. Alikuwa ana uwezo kichwani. Na vyeo vingi alikuwa anakataa. Na pale alipokubali alijitoa kwa dhati. Amekuwa Mwenyekiti wa "boards" za Mwananchi Communications Ltd, amekuwa kwenye "board" ya Geita Gold Miming (GGM), Mwenyekiti wa "board" ya Vodacom nk. Waulize waliofanya kazi naye. Kile kilikuwa kichwa kingine.

Wakati fulani nilialikwa katika uzinduzi wa "Private Equity Fund" moja pale Golden Tulip Hotel. Alikuwepo Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waheshimiwa mawaziri na wafanya biashara. Mr. Ali Mfuruki alikuwa miongoni mwa waalikwa pia. Siku ile Mr. Ali Mfuruki aliongea kitu kikubwa sana. Akasema, wakati Marekani inataka kwenda mwezini miaka ya 60.

 Rais wa nchi hiyo J.F. Keneddy alitangaza kwamba Mmarekani yoyote atakayekuja na wazo au "idea" au "ubunifu" au "teknolojia" ambayo itaisaidia Taifa la Marekani kufika mwezini au kufika hatua moja mbele katika ndoto ya nchi kwenda mwezini, serikali ya Marekani italipa fedha kununua hilo wazo au huo ubunifu. 

Mr. Ali Mfuruki akasema; ili sisi kama Taifa tuweze kwenda mbele lazima kuwe na mbinu za kujenga "uhitaji" au "demand" ya ugunduzi na ubunifu "Creativity and innovation" . Akasema "kufikiria" ni kazi. Kugundua kitu ni gharama. Lazima ufanye "research" au "utafiti". Tukitaka watu wetu wawe wabunifu lazima tutengeneze mbinu za kumfikirisha mtu akijua kabisa kuwa nguvu zake hazitoenda bure.


Mr. Ali Mfuruki alikuwa haongei "nadharia". Sijawahi kumsikia akiongea "pumba". Kwa historia yake yeye ni mhandisi au "engineer" kwa lugha ya kiingereza. Mr. Ali Mfuruki Alipotoka nchini Ujerumani aliposomea, kuja nyumbani Tanzania kufanya biashara, aliona kuna fursa, kuna "demand" au "uhitaji" wa bidhaa za teknolojia hasa kompyuta. 

Kipindi hiki nchi ilikuwa imefunguka na serikali pamoja na makampuni binafsi yalikuwa yanabadilisha teknolojia kutoka katika mfumo wa kizamani wa "fax" na "typewriters" kuja kwenye matumizi ya kompyuta. Ndivyo kampuni yake ya Infotech Technologies Ilivyoanza. 

Huwezi kuzungumzia Teknolojia Tanzania pasipo kumzungumzia Mr. Ali Mfuruki ingawa amekuwa na biashara nyingi zaidi ya hiyo. Yeye ni baba katika eneo hili la TEHAMA hapa Tanzania pamoja na kwamba unapozungumzia ujio wa WoolWorth unamzungumzia Mr. Ali Mfuruki na hata unapozungumzia ujio wa Zuku unamzungumzia Mr. Ali Mfuruki. Nini cha kujifunza hapa;

I. Tunaishi katika dunia ya ubepari au "capitalism". Dunia ya "ubepari" na dunia ya ujamaa au "socialism" ni dunia 2 tofauti. Katika dunia ya ubepari mtu anaweza akakudhalilisha kwa sababu amekupa fursa. Mtu anaweza akataka umuabudu na umpigie magoti kwa sababu anakupa biashara. Mtu anaweza akakuvunjia heshima mbela ya mke na watoto wako kwa sababu bila yeye huwezi kupata mshahara. Haya ndiyo mambo ambayo Mr. Ali Mfuruki aliniambia hayataki. Akasema bora niwe "broke" au "masikini" kuliko kudhaliliswa. Alikuwa na msimamo.

II. Vijana wengi wanatamani kuheshimiwa kama Mr. Ali Mfuruki. Lakini hawajui kuwa heshima haiji kwenye kikombe cha chai. Inajengwa kwa jasho kubwa. Mimi Paul Mashauri ambaye nimekaa na hawa watu najua. Mimi Paul Mashauri ambaye nimetumika sana kwenye sekta binafsi nijaua. Ni kazi ngumu na inataka moyo. Kumbuka Mr. Ali Mfuruki ni mfanyabiashara. Ana biashara zinazomuangalia yeye. 

Na bado aangalie ya nchi. Sio jambo dogo. Kumbuka akifanya hivyo waziri ni sawa kwa sababu mwisho wa mwezi analipwa mshahara. Ni sehemu ya "job description". Lakini unapokuwa Mwenyekiti wa hizi taasisi za sekta binafsi unatumia akili zako na nguzu zako kama msaada na mchango kwa Taifa. Ingawa sina uhakika kama ukifilisika unapewa tena mtaji na Taifa. Ndio maana nasema inataka moyo. Ni vijana wangapi wako tayari kufanya hivyo? Kuacha biashara yako na watoto wako kuhangaikia ya wengine?

III. Mr. Ali Mfuruki alikuwa anafikiri vizuri "thinker" kwa sababu alikuwa anatumia muda mrefu sana kukutana na watu wa haiba tofauti, kusoma, kusafiri kupata "exposure" nk. Hakuna mtu alikuwa anamlipia tiketi ya ndege kusafiri. Alikuwa anajilipia mwenyewe. Leo unataka kuwa kama Mr. Ali Mfuruki unashinda instagram unasoma udaku. 

Hautaki kwenda kwenye kongamano lolote zaidi ya matamasha ya muziki na comedy. Kila tasnia ina utamaduni wake. Ukitaka kuketi katikati ya wakuu lazima ufikirie kama wakuu. Mr. Ali Mfuruki aliitwa na wakuu, alikaa meza moja na wakuu akiwemo Barack Obama, Rais Mstaafu wa Marekani sio kwa sababu alikuwa "handsome" mwenye "six packs" tumboni kuliko watanzania wote. La hasha! Alikuwa na madini adimu kichwani.


5. Ruge Mutahaba, Aliyekuwa Mkurugenzi au "Director" wa programs, Clouds Media Group

Niliposikia amefariki, nilisikitika sana. Kwa sababu miezi michache iliyopita kabla ya taarifa hizo nilimpigia simu. Nikamwambia kaka Ruge kuna kongamano la vijana na wazazi tunaandaa naomba uje uzungumze hasa na vijana. Akajibu akasema "count me in". Lakini miezi kadhaa nyuma, Ruge mwenyewe alinipigia simu. Akasema Paul wewe na mimi kama "speakers" lazima tufanye mambo ya kusaidia nchi. Akaniambia hebu andika "andiko" au "proposal" ya kusaidia Taifa letu kwa kutumia "speakers" kuhamasisha fikra mbadala hasa katika mambo ya msingi ya kitaifa. Nilikesha usiku ule nikaandika ile "proposal" na nikamtumia Ruge kwa email. Ile "propoal" niliipa jina la "Speakers Without Boarders".

Wengi walimfahamu Ruge Mutahaba kwenye "media" na "muziki" lakini Ruge Mutahaba alikuwa ni zaidi ya media na muziki. Ndio sababu alipofariki hata Rais wa nchi alitoa neno. Uwezo wa Ruge Mutahaba ulikuwa hauna shaka. Ubishi wake kwa kile alichokiamini ulikuwa si wa kitoto. Na utayari wake kujitoa kwa ajili ya wengine hauelezeki. Siweki chumvi na mimi sio mnafiki wala sisemi haya yote kwa sababu hayupo tena duniani. Niliyasema haya hata alipokuwa hai. 

Niliyasema ya Mr. Ali Mfuruki wiki iliyopita ambayo ni wiki moja kabla hajafariki. Sio wote wana moyo wa kusema nani aliwasaidia katika maisha yao lakini mimi nasema kwa sababu duniani hakuna mtu anayetoka bila msaada wa mtu mwingine. Hakuna kitu kama "self-made". Kusaidiwa sio lazima iwe pesa .Hata mwalimu wa shule ya msingi alikusaidia kujua kusoma na kuandika. Leo unasemaje kuwa wewe ni "self-made millionaire"? Humkumbuki hata mkeo au mumeo aliyekutia moyo ulipokata tamaa?

Ruge Mutahaba alinisaidia sana mimi na vijana wengine wengi. Yeye ndiye aliyenitambulisha kwa Azim Jamal aliye kuja kuwa rafiki yangu mkubwa katika "motivational speaking". Huyu ni mnenaji au "speaker", mwandishi wa vitabu au "author", mtaalam wa menejimenti au "consultant" na mfanyabiashara aliyebobea. Azim Jamal amefanya kazi na kuandika vitabu pamoja na wataalam na wanenaji "speakers" wakubwa duniani kama Brian Tracy. 

Kumlipa Azim Jamal kuzungumza kwenye tukio lako sio chini ya dola za Kimarekani milioni 10 au fedha za kitanzania zaidi ya shilingi milioni 20 ndani ya siku moja. Lakini kwa sababu ya urafiki na heshima ya Ruge Mutahaba, Azim Jamal alikuja kuzungumza kwenye tukio nililoandaa bila kulipwa hata shilingi moja. Baada ya hapo tulifanya kazi nyingi sana na Azim Jamal.

Pili wakati tunaanzisha gazeti la Familia, yeye ndiye aliyenipa matangazo ya bure. Alisema wewe unafanya kazi kubwa sana kuhamasisha vijana. Hakuna anayekulipa kwa kujitolea kwako. Malipo yako yatakuwa matangazo nitakayokupa Clouds FM. Kwa moyo ulionao ukitoka wewe, wengi zaidi watatoka. Ruge Mutahaba alilipa gharama ya kazi yangu kwa vijana. Si hayo tu, yeye pamoja na Joseph Kusaga ndio walionipa studio za Clouds TV kutengeneza sinema yangu iitwayo "Maisha Ni Siasa". 

Angalia sinema hii yote Youtube. Sio mimi tu, wako wengi aliowasaidia. Hata serikali inatambua nini Ruge Mutahaba alifanya katika nchi hii. Uzoefu wangu wa Ruge Mutahaba tukiwa wajumbe wa TRA Stakeholders Forum ulinidhihirishia uwezo wake wa kuangalia mambo kwa jicho la tatu. Ndio sababu alikuwa mbunifu sana. Kila tulipokuwa na kikao, Ruge Mutahaba hakuwa wa kwanza kuongea. Lakini alipopata nafasi ya kuongea, aliipindua pindua mada na wote tukaiona hoja husika kwa namna ambayo hatukuiona hapo kabla.

Kila nikimkumbuka Ruge Mutahaba nakumbuka mmoja kati ya vijana ambao walijiongeza. Ungeniuliza ni akina nani wanafanya sana kazi bila kuchoka ningekuambia ni Ruge Mutahaba. Binafsi sijui alikuwa anapumzika saa ngapi. Unakutana na kijana anasema anataka kuwa kama Ruge Mutahaba na bado analala saa 2 usiku na anaamka saa 2 asubuhi. Unataka kuwa kama Ruge yupi? Sijaona mimi mtu anafanya vitu vikubwa vya kitaifa na analala usingizi wa pono. Uliza wasaidizi wa Rais kama wanalala? Kama unajua huwezi kufanya kazi kwa bidii kubali kuwa wa kawaida. Usifikiri nazungumzia "utajiri". Hilo ni suala lingine.

Unaweza usiwe tajiri lakini bado ukawa si wa kawaida. Akina Dr. Martin Luther King Jr. na Nelson Mandela hawakuwa matajiri lakini pia hawakuwa wa kawaida. Lazima utofautishe kati ya kuwa "rich" au "tajiri" na kuwa "great". Hapa sizungumzii utajiri nazungumzia "greatness". Hata mwizi anaweka kuwa "tajiri" lakini inahitaji "akili nzuri", "kujitoa kwa wengine" na "kujituma" ili uwe "great" Vitu vinavyobadilisha jamii havihitaji mtu mzembe. Kama kusoma tu hii makala mpaka hapa umeshachoka unatamani iishe utaweza kuwa kama Ruge Mutahaba? Kuna mambo ya msingi ya kujifunza kutoka kwa Ruge Mutahaba;


I. Ubishi. Hakuna kitu kinakuja kirahisi. Mafanikio sio muujiza, yanafanyiwa kazi. Usifikiri Ruge Mutahaba alifika pale alipofika sababu ya "Clouds" kama media. Hatukatai ukweli kwamba alikuwa ni mmoja wa watu walioijenga Clouds Media Group. Kwanza, ulikuwa ukisikia Clouds FM iko hewani, sura mbili zinakuja kichwani kwako; Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. 

Hata isingekuwa "media" Ruge Mutahaba angefanya vitu vikubwa tu kwa sababu alikuwa ni "mbishi" asiyekubali kushindwa. Miaka 3 iliyopita nilimualika Ruge Mutahaba katika kongamano la Vijana lililoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC) pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO) pale Serena Hotel. Kongamano lilikuwa chini ya mradi wa kutoa mitaji kwa mawazo bora ya biashara kwa vijana "Ajira Yangu" Project ambayo niliisimamia.

II. Alipopewa nafasi ya kuzungumza, Ruge Mutahaba akasema "ukija kwangu na wazo au "idea" yako nakurudisha mara 3 au mara 4. Sio kwa sababu wazo lako ni baya. Nataka nione kama kweli wewe ni mbishi na uko tayari kupambana mpaka wazo lako lipate maisha. Vijana wa leo hawako hivyo. Wanataka mambo ya chapchap kama mabando ya internet. Hawana uthubutu. Wanaamini kwenye michongo na kushikwa mkono. Wanakata tamaa mapema. Hata wakija kwako uwe "mentor" wao wanakuja "kifursa zaidi". Wanataka uwe "mentor" wao na hapohapo uwape "hela". Hiyo sio "mentorship" hiyo ni "sponsorship". Sasa hatujui unataka nini? Unataka "mentorship" au "sponsorship"?Hawajui kuwa hata akina Ruge Mutahaba walipitia vikwazo lakini walikuwa wabishi.

III. Uwezo wa kufanya lolote unalolitaka. Nilisema hapo mwanzo kwamba wengi wanamjua Ruge Mutahaba kwa sababu ya "media", "muziki" na "matamasha". Ruge Mutahaba alikuwa zaidi ya hapo. Ruge Mutahaba alikuwa pia anandaa sinema. Nikiwa chuo kikuu Ruge Mutahaba alirekodi sinema inaitwa "Kelele". Yeye mwenyewe binafsi alikuwa nyuma ya kamera kuhakikisha sinema inarekodiwa vizuri. Ingawa sikumbuki kama aliwahi kuitoa ile sinema lakini nilichojifunza ni kwamba alijua anaweza kufanya kitu zaidi ya kimoja.

Kuna mikakati mingi sana na miradi mikubwa ya kitaifa mbayo Ruge Mutahaba alikuwa nyuma yake ingawa hakuonekana mstari wa mbele. Huyo ndiyo Ruge Mutahaba niliyemfahamu mimi. Leo hii unatamani siku moja upewe heshima aliyopewa Ruge Mutahaba lakini hujiulizi nini kitu cha tofauti unafanya? Zaidi ya kutoka bwenini, kwenda darasani kisha kwenda bwaloni kula ubwabwa nini kingine unafanya? Zaidi ya kutoka kazini na kwenda baa au kwenye harusi kula pilau, nini kingine unafanya?Unawezaje kuwa kama Ruge au zaidi ya Ruge kwa maisha ya pembe tatu?Unawezaje kufikia ndoto zako kwa maisha ya pembe tatu? Hata kama umeajiriwa. Usiku unafanya nini?

Tanzania imepoteza watu muhimu sana katika muda mfupi sana. Niliyoyataja hapa kwa hawa "generals" ni machache sana ukilinganisha na niliyoyafahamu na nisiyoyafahamu. Hawa watu walitumia vyema uwepo wao hapa duniani na uwepo wao katika hii nchi kuleta utofauti. Ni "generals" walioondoka lakini nchi bado ipo. Pamoja na utofauti wao, hawa wote wanasifa zinazofanana. Pamoja na mapungufu yao wote hawa wana faida zinazofanana.

1. Waliwekeza katika maarifa 2. Waliwekeza katika watu 3. Walitumia karama, vipaji na elimu zao kuleta utofauti na kulitumikia Taifa 4. Hawakuwa wepesi kukata tamaa hata walipopitia magumu katika ngazi za familia zao, maisha yao binafsi, biashara zao na kazi za kitaifa 5. Wameacha alama katika nchi hii, alama ambayo itaendelea kuishi ingawa wao hatunao tena. Amani ya bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nao, familia zao, ndugu zao, marafiki zao na watanzania wote kwa ujumla. 

Makala hii imeandikwa na Paul R.K Mashauri@hakimiliki 2019. Hairuhusiwi kuchapisha Makala hii au sehemu ya Makala hii pasipo idhini ya mwandishi. Wasiliana na mwandishi kupitia ceo@masterclassworldwide.co.tz 

Benki ya NMB yatwaa Tuzo ya NBAA kwa mwaka mwingine mfululizo.

$
0
0
BENKI ya NMB imetwaa tuzo maalum kutoka Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu(NBAA) kama Benki bora ya Taarifa za Kifedha zilizokaguliwa na kutambuliwa kimataifa kwa mwaka 2018,ilikoshinda benki kadhaa nchini.

Benki hiyo imetambuliwa kwa kufikia kiwango bora katika utayarishaji wa taarifa zake za kifedha, kulingana na mahitaji ya taarifa (viwango vya kuripoti za kitaifa na kimataifa).

Hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo ambayo kwa NMB, ni ushindi wa mara ya pili mfululizo, ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo NBAA ilisema taarifa za mahesabu za NMB zimeendelea kuwa bora kila mwaka, ubora uliowasukuma majaji kuwapa tuzo hiyo kwa mara nyingine.

Akizungumzia vigezo vilivyotumika kupata washindi, Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Mr.Pius Maneno, amesema walipatikana kwa kuangalia washiriki waliovuka asilimia 75 ya vigezo vilivyowekwa.

Naye Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Mr. Benedicto Baragomwa, amesema wao kama wataalam wa masuala ya fedha, wanatambua umuhimu wa kuandaa vitabu vya mahesabu vya Benki kwa njia na mifumo inayozingatia viwango vya kitaifa na kimataifa.

“Ushindi huu unadhihirisha namna ambavyo tumejikita katika kudumisha uadilifu wa hali ya juu kwenye uwasilishaji wa taarifa zetu za kifedha za mwaka,” alisema Baragomwa baada ya kupokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani.

Baragomwa alibainisha kuwa, wawezeshaji wa benki hiyo wameandaliwa katika misingi inayofuata na kuheshimu viwango vya kimataifa vinavyotambuliwa na IFRS, pamoja na mahitaji ya ndani.

Taarifa iliyotolewa na Benki hiyo imetoa shukrani kwa wafanyakazi na kujivunia mfumo bora wa Uongozi na utendaji hasa kitengo cha fedha. "Tuzo hii imepatikana nyuma ya mfumo uliopo wa utawala bora na michakato ya udhibiti ambayo inakuza uwazi wa taarifa za kifedha, uwajibikaji,ueledi na kiwango cha juu cha uadilifu wa takwimu. Hongera kwa kila mtu, haswa timu ya kifedha kwa kuongoza maandalizi ya Taarifa ya Fedha ya Benki ya NMB.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaabani, akimkabidhi Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, Tuzo ya Benki Bora katika utayarishaji wa ripoti za kifedha kwa mwaka 2019, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NBAA). Hafla ya kukabidhiwa tuzo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, akionesha Tuzo aliyoipokea ya Benki ya NMB kuwa Benki Bora katika utayarishaji wa ripoti za kifedha kwa mwaka 2018, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).
Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa utoaji tuzo.

MAHAFALI YA 30 YA TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

$
0
0

Bi. Pili Said Kassimu ambaye ni mmoja wa wahitimu wa ngazi ya Stashahada akipokea cheti kutoka kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa.

Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa akitoa hotuba wakati wa mahafali ya 30 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ambapo aliwataka wahitimu wakawe raia wema na kuitumia elimu waliyoipata ipasavyo kwa ajili ya manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. George D. Yambesi akitoa neno kwa wahitimu pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kutoa hotuba yake.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa (katikati) akiwa katika Meza Kuu na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bagamoyo pamoja na viongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni bagamoyo (TaSUBa). 

Wahitimu wakisikiliza hotuba kwa umakini kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye alikua ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa (hayupo pichani).

Mhitimu wa ngazi ya Stashahada Bw. David Nashoni akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake mbele ya mgeni rasmi ambaye alikua ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa.

 




Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kikitoa burudani wakati wa mahafali ya 30 ya Taasisi hiyo.

Benki ya CRDB na TTCL zaungana kuwasogezea Watanzania huduma za kifedha

$
0
0
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (wa pili kulia) akibadilishana nyaraka na Mkuregenzi wa T-Pesa, Lulu Mkude, baada ya kuingia makubalianao ya mpango wa pamoja wa kutoa huduma za SimBanking na T-Pesa utakaowawezesha wateja kupata huduma za kifedha kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi, katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji - TTCL, Mruta Hamis. Picha zote na Othman Michuzi.
Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (katikati) akishuhudia uzinduzi wa huduma ya kuhamisha fedha kati ya SimBanking na T-Pesa uliofanywa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili na Mkuregenzi wa T-Pesa, Lulu Mkude
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (aliyesimama) akizungumza jambo wakati akiongoza hafla hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. 
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB pamoja na wa TTCL wakifatilia hafla hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. 


Benki ya CRDB na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo wamezindua mpango wa pamoja kupitia huduma za SimBanking na T-Pesa utakaowawezesha wateja kupata huduma za kifedha kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema mpango huo unalenga katika kuwarahisishia wateja kuhamisha fedha kutoka akaunti za CRDB kwenda T-Pesa, kuhamisha fedha kutoka T-Pesa kwenda akaunti yoyote ya CRDB pamoja na kununua muda wa maongezi kupitia Simbanking.

“Lengo letu ni kuwapa wateja wetu uzoefu bora zaidi pindi watumiapo huduma ya SimBanking. Tunataka kuona mteja akiingia kwenye SimBanking USSD kwa kupiga *150*03# au SimBanking App aweze kumaliza mahitaji yake yote ya kifedha ‘One Stop Shop’ ikiwamo miamala ya T-Pesa,” alisema Raballa.

Raballa alisema ushirikiano huo na TTCL utataidia kusogeza huduma kwa watanzania wengi zaidi hususani maeneo ya vijijini. Takwimu zinaonyesha ni asilimia 60 ya watanzania ndio wameunganishwa na mfumo wa kifedha kupitia simu za mkononi, wakati ni asilimia 17 tu ya watanzania ndio wanaotumia huduma za kibenki.
“Benki ya CRDB inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha Watanzania wengi wanapata huduma za kifedha, hatua ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wetu wa taifa letu. Tunafurahi kushirikiana na TTCL katika kufanikisha azma hii "aliongezea Raballa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa T-Pesa, Lulu Mkude, alisema ushirikiano huo ni mafanikio makubwa kwa TTCL, kwani utawawezesha maelfu ya watanzania wote wa mijini na vijijini kupata huduma za kifedha za kwa urahisi.

Lulu alisema TTCL kuunganishwa kwa huduma ya T-Pesa na SimBanking kutawasiaidia wateja wa Benki ya CRDB kuweka pesa kwa urahisi kwenye akaunti zao kupitia T-Pesa lakini pia kuongeza salio au kuwatumia ndugu jamaa na marafiki fedha kwenye akaunti zao za T-Pesa.

''Kufurahia huduma mteja atatakiwa kuingia katika menu ya T-Pesa kwa kupiga *150*71#, na kisha kuchagua huduma ya SimBanking,” alisema Lulu Mkude, huku akisisitiza kwamba hivi sasa TTCL imejipanga vilivyo kusogeza mawakala wake wa T-Pesa karibu zaidi na wananchi hususani vijijini ambapo kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha

Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni usalama kwa Taifa -Mkuu wa Wilaya Mmanda.

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, Mtwara

 Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni usalama kwa Taifa kwani vitambulisho vya Taifa vinavyotumika katika usajili wa laini hizo ndio baadae watanzania tutatumbuliwa kwa kuwa na vitambulisho vya mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya uu Mtwara Evod Mmanda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa Uhamasishaji wa Wananchi kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Mmanda amesema changamoto kwa baadhi ya Wananchi wa Mtwara kupata vitambulisho ni kutokana na wanatoka nchi jirani ya Msumbiji hivyo lazima wafuate taratibu za Uhamiaji.

Amesema kuwa kila mtu ahakikishe anapata kitambulisho cha taifa ili aweze kusajili laini yake kwa alama za vidole kwani namba zitafungwa Desemba 31 na ambao hawatafanya namba hizo zisizosajiliwa zitafungwa na kugaiwa kwa watu wengine.

Amesema kuwa taarifa zilizosambaa katika mtandao ya kijamii kuwa zoezi la kuzima laini simu Desemba 31 kuwa limeongezwa ni kuzipuuza na kwamba zoezi liko palepale.

Aidha amesema kuwa katika kipindi hiki Wananchi waache kununua simu Mkononi kwani kuna watu wanaweza kufanya uhalifu na mwisho wa siku mtu akaingia katika matatizo.

Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko Amesema zoezi la usajili kwa Mkoa wa Mtwara lipo kwa Wilaya zote na kutaka Wananchi wajitokeze kupata kusajili laini za simu .

Amesema zoezi la kuzima simu liko palepale hivyo watu waache kupotosha zoezi hilo.Eseko Amesema kanda ya Mashariki wamezindua Uhamasishaji kumekuwa na matokeo makubwa kwa Wananchi kuhamasika katika kujisajili.

Afisa Usajili wa Mkoa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Gide Magila amesema changamoto wanayokutana nayo ni watu kusajili majina mara Mbili na wakati mwingine kusahau kumbukumbu walivyosajili.
 Foleni ya Wananchi wakiwa katika ufatliaji wa namba za vitambulisho vya Taifa.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na usajili wa laini za simu kwa alama  vidole katika uwanja wa Sabasaba mjini Mtwara. 

 Wananchi wakiwa katika foleni ya kuangalia namba za vitambulisho vya Taifa katika mfumo wa NIDA
 Afisa Msajili wa Mkoa wa Mtwara  wa Mamlaka ya a Vitambulisho vya Taifa (NIDA)Gide Magila  akitoa changamoto wanazokutana na Wananchi wakati usajili na uangaliaji majina katika mfumo.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda akizungumza na Wananchi wakati wa Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Mkoa wa Mtwara.
 Mabanda ya watoa huduma za simu kwa ajili ya kusajili laini za simu za  Wananchi kwa alama za vidole.
Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko akizungumza namna kanda ya TCRA inavyohamasisha Wananchi kusajili laini za simu kwa alama za vidole.
Viewing all 49551 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>