Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all articles
Browse latest Browse all 49632

FOMU YA KUOMBA HATI MPYA PALE YA ZAMANI INAPOPOTEA.

$
0
0

Na Bashir Yakub.

Ni fomu namba 3 katika kanuni za Sheria ya usajili wa ardhi .Inatokana na kifungu cha 38 cha Sheria ya Usajili wa Ardhi Sura ya 334. Fomu hii kazi yake ni kuombea hati mpya ya ardhi baada ya ile uliyokuwa nayo mwanzoni kupotea. Hati, sawa ilivyo kwa vitu vingine vyote inaweza kupotea, kuibiwa au kuharibiwa. Mazingira ya matukio haya yote yameandaliwa majibu na sheria za ardhi. Fomu hii namba 3 ni rasmi kwa waliopoteza hati na hivyo kutaka kupata hati mpya.

Fomu hii hutakiwa kujazwa na mhusika yaani yule ambaye jina lilikuwa linasomeka kwenye hati iliyopotea. Kama lilikuwa likisomeka jina la kampuni basi wale waliokuwa wamesaini ile hati iliyopotea awali ndio wasaini na kujaza fomu hii. Anaweza kuwa mkurugenzi wa kampuni ama katibu wa kampuni.

Msimamizi wa mirathi pia anaweza kujaza na kusaini fomu hii ikiwa jina lililo kwenye hati iliyopotea ni la mtu ambaye sasa ni marehemu. Isipokuwa sasa kwa msimamizi wa mirathi ni lazima awe na fomu za kuthibitisha kuteuliwa na kuthibitishwa na mahakama kuwa msimamizi wa mirathi. Ikiwa msimamizi wa mirathi ni zaidi ya mmoja basi wote watajaza fomu hii ya kuomba hati mpya na watasaini .

KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com

Viewing all articles
Browse latest Browse all 49632

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>