Wafanyakazi TBL walivyoshiriki Kilimanjaro Marathon 2018
Idadi kubwa ya wafanyakazi kutoka kampuni ya TBL Group wameshiriki mbio za Kili Marathon zilizofanyika mkoani Kilimanjaro.Mashindano haya maarufu duniani yanadhaminiwa na kampuni hiyo kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premier Lager.
Mwaka huu TBL Group imekuja na ajenda ya kuwezesha na kuhamasisha upandaji mti katika maeneo yanayozunguka mlima Kilimanjaro ili kulinda mazingira,ambapo kwa kushirikiana na taasisi ya Kilimanjaro Project, inatarajia kupanda miti 100,000.
Uhamasishaji wa mradi huu umeanza kutekelezwa wakati wa mashindano ya Kili Marathon yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.