Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii
  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride la heshima katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza katika Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri leo Jumatatu December 9, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John PombeMagufuli akipokea heshima baada ya kuwasili katika Uwanja wa CCMKirumba jijini Mwanza kuongoza Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 yaJamhuri leo Jumatatu December 9, 2019.
  Muonekano wa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati waSherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri zilizoongozwa na RaisDkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu December 9, 2019.
  Kikosi cha Makomando wa JWTZ wakioneshaumahiri wao wa kufanya zoezi la uokozi katika mfano wa Tukio laUtekaji.
  Kikundi cha Sungusungu cha kutoka Kwimbamkoani Mwanza kikitumbuiza katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru waTanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika
  uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza.
  Baadhi ya Mawaziri wakiimba na kucheza wimbo wa Harmonize wakati wa sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM
  Kirumba jijjini Mwanza.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kuongoza Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri leo
  Jumatatu December 9, 2019.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na miaka 57 ya Jamhuri zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijjini Mwanza. 
  Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
  Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe
  zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
  Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika
  uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
  Rais wa Zanzibar Ali Mohamed Shein akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika
  uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
  Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
   Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiwasalimia wananchi katika maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara pamoja na Miaka 57 ya Jamhuri katika sherehe zilizofanyika katika
  uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 

  0 0


  Na Paul R.K Mashauri

   Pichani juu kushoto ni Elvis Tables Musiba, Ali Mufuruki na pichani chini  kulia ni Sir. Andy Chande, Ruge Mutahaba pamoja na Dkt. Reginald Mengi enzi za uhai wao.  Miaka michache iliyopita tulimpoteza Elvis Tables Musiba aliyekuwa Mwenyekiti wa TPSF (Tanzania Private Sector Foundation). Mwaka jana tukampoteza Sir. Andy Chande aliyekuwa kiongozi wa sekta binafsi toka enzi za ukoloni. Mwaka huu tumewapoteza wafanyabiashara 3 wakubwa ambao walikuwa viongozi na watu muhimu sana kwa sekta binafsi Tanzania. Dr. Reginald Abraham Mengi aliyekuwa Mwenyekiti wa CTI (Confederation of Tanzania Industries) na TPSF, Ruge Mutahaba aliyekuwa mjumbe wa MOAT (Media Owners Association of Tanzania) na mjumbe wa TRA Stakeholders Forum na jana tumempoteza Mr. Ali Mfuruki aliyekuwa Mwenyekiti wa CEO Round Table.
  Vijana wengi wamewaona na kuwasikia hawa watu "the generals" lakini wengi hawajui historia ya sekta binafsi Tanzania na mchango wao katika kuifikisha sekta binafsi hapo ilipo. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoeleza japo kwa kifupi mchango wao kwa sababu kwa namna moja au nyingine wote hawa kuanzia Sir. Andy Chande, Elvis Tables Musiba, Dr. Reginald Abraham Mengi, Mr. Ali Mfuruki na Ruge Mutahaba nimefanya nao kazi za sekta binafsi kwa karibu sana.


  Sir. Andy Chande nilifanya naye kazi akiwa ni Mwenyekiti wa "boards" mbalimbali za taasisi kama MOI, IMTU, TRL nk. Na pia alikuwa mshauri katika "board" ya kampuni yangu mwenyewe. Ni bahati mbaya sana kwamba mwezi moja kabla ya kifo chake, mimi na Sir. Andy Chande tulipanga kukutana ili mimi Paul Mashauri nimfanyie "interview" ya namna sekta binafsi ya nchi hii ilivyokuwa kabla na baada ya uhuru. "Interview" ile ilikuwa itumike kama kipindi cha TV ili wengi zaidi wanufaike na uzoefu aliokuwa nao. Bahati mbaya Sir. Andy Chande alifariki kabla hatujakamilisha jambo hilo jema.

  Elvis Tables Musiba nilifanya naye kazi akiwa Mwenyekiti wa TPSF na mimi nikiwa mjumbe wa kamati mbalimbali za sekta binafsi Tanzania. Tulisaidiana kuchangisha fedha"fundraising" kwa shughuli mbalimbali za kitaifa, na alitumia wakati huo kunisimulia mambo mengi sana.

  Mr. Ali Mfuruki nilifanya naye kazi akiwa ni Mwenyekiti wa CEO Round Table na mlezi wa TRBN (Tanzania Responsible Business Network) chini ya UN Business Compact na mimi nikiwa ni mjumbe wa "secretariat" ya TRBN.

  Dr. Reginald Abraham Mengi nilifanya naye kazi yeye akiwa ni Mwenyekiti wa CTI na mimi nikiwa ni mjumbe wa kamati ya SME ya CTI. Na Ruge Mutahaba nilifanya naye kazi wote tukiwa wajumbe wa TRA Stakeholders Forum.

  Mara nyingi wote hawa walitumia muda wao mwingi kunisimulia vitu vingi sana wao wakiwa wakubwa kwangu kiumri na mimi nikiwa mdogo sana kwao. Wakati huo nilikuwa sijui kwanini wananiambia mambo yote hayo ya sekta binafsi kwa sababu kwanza nilikuwa mdogo sana na pili sikuwa na nafasi wala heshima kubwa kama walizokuwa nazo wao lakini jana baada ya kupata taarifa za kifo cha Mr. Ali Mfuruki nikagundua pengine walitaka siku moja niyasimulie hayo ili kizazi cha leo kipate kuelewa.

  Wafanyabishara vijana, viongozi vijana katika serikali na wajasiriamali vijana wanaochipukia, lazima waelezwe kwamba historia ya sekta binafsi Tanzania haiwezi kuelezwa pasipo majina ya hawa wote niliowataja hapo juu. Lakini pia wapo wengine ambao wameshatutoka na wengine ambao bado wapo hai. Pia sitatenda haki nisipowataja japo baadhi yao.

   Hao ni pamoja na marehemu Mzee Mwakitwange, Dr. Reginald Abraham Mengi, Mzee Anorld Kileo, Dr. Juma Mwapachu, Elvis Tables Musiba, Mzee Iddi Simba na wengine ambao sikupata kuwafahamu. Hawa walikuwa waanzilishi wa TCCIA mwishoni mwa miaka ya 80 kabla ya baadhi yao kuondoka TCCIA na kuanzisha CTI. Kwanini waliondoka na TCCIA kuanzisha CTI? Hiyo ni mada nyingine ambayo inahitaji makala tofauti na hii.

  Ukiondoa Mzee Mwakitwange ambaye alitangulia mbele za haki zamani kidogo, wengine wote akiwemo Mzee Anorld Kileo, Dr. Juma Mapachu na Mzee Iddi Simba nimepata kufanya nao kazi na kupata simulizi zao. Mzee Anorld Kileo ambaye alikuwa ni CEO wa TBL kwa muda mrefu sana na kiongozi wa TPSF yeye aliniita ofisini kwake na kunikalisha chini kwa masaa zaidi ya 3 akinieleza sekta binafsi ilipotoka na namna walivyopambana kuifikisha hapo ilipo. Ukurasa huu hautoshi kuandika historia yote ya ujasiriamali Tanzania ambayo vijana wengi wangependa kuijua lakini Dr. Juma Mwapachu aliandika kitabu chenye historia hii vizuri sana. Mimi nitagusia yale niliyoelezwa na hawa "generals" wa sekta binafsi Tanzania kwa kifupi sana.  1. Sir. Andy Chande, Mwanzilishi, Chande Mills

  Sir Andy Chande alinieleza kwamba baada ya Uhuru wa nchi hii, Rais wa kwanza wa Tanzania Mwl. Julius K. Nyerere alitaka kumteua kwenye baraza la mawaziri. Lakini akamwambia Mwalimu Nyerere, naomba uniache kwenye sekta binafsi. Mwalimu Nyerere aliheshimu mawazo ya Sir. Andy Chande. Lakini Mwalimu Nyerere akaamua kumteua Sir. Andy Chande kuwa mjumbe wa kamati ya uchumi na maendeleo mara tu baada ya Tanzania kupata uhuru. Kwa vijana wasiomfahamu Sir. Andy Chande huyu ndiye aliyekuwa mfanyabiashara wa kitanzania mwenye nguvu kubwa za kiuchumi wakati wa ukoloni na hata baada ya kupata uhuru. Aliendesha biashara ya kifamilia iliyoitwa Chande Mills ambayo baadaye ilitaifishwa na serikali mwaka 1967 wakati wa "Nationalization" na kuwa NMC (National Milling Corporation) kiwanda ambacho baadaye kilikuja kununuliwa na Bakhresa.


  Sir. Andy Chande ndiye aliyekuwa mtanzania mwenye asili ya kiasia kuanza kutoa misaada kwa watu (philanthropism) kuanzia wakati wa uhuru mpaka alipofariki dunia miaka michache iliyopita. Kilichonishangaza kuhusu Sir. Andy Chande ni kwamba hata baada ya serikali kutaifisha biashara yake, bado aliendelea kutumia mtandao wake wa watu "network" akili na maarifa yake kuitumikia nchi. Sir. Andy Chande ananisimulia anasema, baada ya serikali kutaifisha biashara yake, Mwalimu Nyerere alimuita Ikulu, akamuuliza; Rafiki yangu Chande; unataka kwenda wapi baada ya serikali kuchukua biashara yako kwa manufaa ya umma?

  Sir. Andy Chande akamuambia Mwalimu Nyerere; "sina pa kwenda". Mwalimu akamuambia "sasa kuanzia leo, wewe ndio utakuwa Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hii mpya inayomilikiwa na wananchi wote wa Tanzania. Sir. Andy Chande akajibu " sawa Mh. Rais". Na ikawa hivyo. Ingekuwa sisi vijana wa leo, rafiki yako ndiyo kiongozi wa nchi au DC au Mkuu wa mkoa au Waziri, anakufahamisha maamuzi ya serikali, tungeleta urafiki na mambo binafsi kwenye mambo ya nchi. Lakini Sir. Andy Chande alikuwa anajua kutofautisha ni wakati gani Nyerere, "rafiki" yake anaongea na ni wakati gani Nyerere, "Rais wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu" anaongea. Alikuwa anajua mipaka yake.

  Kutokana na uwezo wa Sir. Andy Chande, Mwalimu Nyerere alimpa uenyekiti wa "boards" nyingi sana ikiwa ni pamoja na TRL, ATC nk. Pia alikuwa Mwenyekiti wa "board" ya Kioo Ltd, Shaaban Robert Secondary School, IST, Barclays bank, Taasisi ya walemavu buguruni nk. Siwezi kuzimaliza zote ni nyingi mno.

  Nilikuwa nyumbani kwake Upanga alipokuwa akisimulia haya. Nikamuuliza sasa uliwezaje kukubali kuwa Mwenyekiti wa "board" ya kampuni ambayo umeihangaikia miaka mingi na sasa si yako tena. Akasema mke wangu alinitia sana moyo. Lakini pili kwenye biashara usiweke mambo moyoni. Ukiweka mambo moyoni utakufa. Moyoni nikajisemea; Huyu kampuni yake aliyoisotea miaka mingi imechukuliwa. Tena siyo kampuni yenye mapato ya shilingi milioni 10 au bilioni moja. Unazungumzia mabilioni ya shilingi. Lakini bado maisha yakaendelea. Wewe umepoteza mteja mmoja unataka kufunga biashara. Kwanini? Hayo ni masomo ambayo nataka vijana wengi wayashike, kwamba;

  I. Mke au mume wako ana mchango mkubwa sana katika maisha yako ya uongozi, biashara au ujasiriamali. Unapooa au kuolewa lazima uangalie mtu ambaye atakutia moyo wakati ukipitia changamoto za maisha kama ilivyokuwa kwa Sir. Andy Chande. Sio mke au mume ambaye atakukimbia ukifilisika au ukifilisiwa au ukishushwa cheo au ukifukuzwa kazi.

  Wakati Sir. Andy Chande akiniambia haya, mke wake alikuwa ni mgonjwa na alikuwa anapata matibabu nchini Uingereza. Pamoja na umri wao mkubwa walipendana sana na kutiana moyo. Na mara nyingi nilipowatembelea niliona Sir. Andy Chande akimhudumia mke wake kwa hali na mali. Kipindi hicho pia Sir. Andy Chande naye hali yake ya kiafya haikuwa nzuri lakini hakuacha kufanya kazi. Alikuwa akiandika makala katika magazeti mbalimbali ya Uingereza na Canada. Sir. Andy Chande alikuwa rafiki mkubwa wa familia ya Malkia wa Uingereza-Qeen Elizabeth, Waziri mkuu wa Canada, na Marais wastaafu akiwemo Mh. Rais Ali Hassan Mwinyi, Mh. Rais Benjamin Mkapa na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

  II. Somo la pili ni kwamba ukiwa mfanyabiashara au mjasiriamali, usiweke mambo moyoni, utakufa. Sir Andy Chande na Mwalimu Nyerere walikuwa ni marafiki wakubwa. Lakini maamuzi ya kutaifisha biashara ya Sir. Andy Chande hayakufanywa na mwalimu kama "mtu binafsi" ingawa yeye alikuwa ni mkuu wa nchi. Yalifanywa na serikali. Iwe yalikuwa ni maamuzi mazuri au mabaya, Sir. Andy Chande aliyapokea na kuyaunga mkono. Urafiki wao uliendelea na yeye aliendelea na maisha kama vile hakuna lililotokea.

  Leo ukimkopa rafiki yako hela akakuambia hana hela za kukusaidia au hawezi kukupa ana mipango na hela alizonazo, una "mdelete" mpaka kwenye simu yako, "unamblock" facebook, "unamunfollow twitter, instagram na youtube". Ukimpigia simu rafiki yako asipopokea mara 2 au mara 3, unatuma ujumbe mfupi; "acha ujinga pokea simu" hata hujui kama yuko hospitali-ICU kalazwa au bafuni anaoga.


  Uko wapi ujasiri wa akina Sir. Andy Chande katika kizazi cha leo? Iko wapi nidhamu ya akina Sir. Andy Chande katika kizazi cha wakati huu? Sir. Andy Chande ananiambia wakati akiwa na Chande Mills, mama Maria Nyerere alikuwa akienda kiwandani kuchukua mabaki ya mahindi kwa sababu alikuwa anafuga. Akasema mama Maria alikuwa hataki akifika kiwandani apewe "priority" wengine wasubiri. 

  Alikuwa anapanga foleni kama wanawake wengine. Hata yeye alipojaribu kumshawishi ahudumiwe kwanza alikataa. Vijana wa leo ambao ni viongozi jifunzeni kitu hapa kutoka kwa mama Maria Nyerere. Wake au waume zenu wajishushe. Wasitake kupewa "priority" kwa sababu tu ni wake au waume wa viongozi. Akienda benki au saloon, mwambie na yeye apange foleni kama wengine. Ndio watu wakubwa "great people" wanavyoishi. Hawana makuu ingawa ni wakuu.  2. Elvis Tables Musiba, Mwenyekiti wa zamani, TPSF

  Nikiwa mtoto mdogo nilikuwa nasoma vitabu vya Elvis Tables Musiba. Moja kati ya vitabu ambavyo sitopata kuvisahau ni kitabu kinachoitwa NJAMA. Kitabu kile cha kipelelezi kilikuwa kina "character" anaitwa Willy Gamba. Ulikuwa ukisoma vitabu vya Elvis Tables Musiba ni kama unaangalia sinema ya Rambo. Nakumbuka nilipokinunua kitabu kile sikulala usingizi mpaka nilipokimaliza. Willy Gamba alikuwa mtu hatari sana ndani ya ile simulizi. Na Elvis Tables Musiba alikwa ni gwiji na mwandishi mkubwa na mzuri sana. Kila ninapokutana na rafiki yangu Eric James Shigongo ambaye pia ni mwandishi wa vitabu namkumbuka Elvis Tables Musiba. Siku moja nitamuuliza Eric James Shigongo alipata wapi hamasa ya kuandika vitabu. Inawezekana alisoma pia vitabu vya Elvis Tables Musiba.

  Nilipokutana na Elvis Tables Musiba nilishangaa kugundua kuwa alikuwa ana kipaji kingine cha biashara na uongozi. Wakati tunachangisha fedha kwa ajili ya kongamano moja katika sekta ya utalii, aliniita ofisini kwake Mirambo House karibu na ofisi za benki ya dunia. Tulikuwa tunahitaji kuchangisha kama shilingi milioni 100. Elvis Tables Musiba akamuomba katibu muhtasi wake amletee simu. Sikuelewa simu ya nini kwenye kuchangisha fedha. Nilitegemea tungeshirikiana kuandika barua na "proposals" za kuchangisha fedha. 

  Lakini haikuwa hivyo. Simu ilipoletwa akaanza kazi. Alikuwa anatuuliza mnataka kampuni gani ituchangie fedha. Kwa hiyo kazi yetu ikawa ni kutaja majina ya makampuni na yeye anapiga simu. Nilishangaa kuona Elvis Tables Musiba hahitaji tumpe namba za simu. Alinyanyua simu na kupiga kila tulipotaja kampuni. Na alipopiga hakuongea na katibu muhtasi au mkurugenzi wa fedha. Aliongea na CEO, Director General au Mwenyekiti wa "board". Namba alizipata wapi? sijui. Lakini ndani ya saa moja tulikuwa na shilingi milioni 60.

  Nikagundiua huyu si mtu wa mchezo. Ana "connections" za ajabu. Nikamuuliza hebu niambie haya mambo unayafanyafanyaje mbona kwangu mageni? Akasema "reciprocate". Hili ni neno la kiingereza linalomaanisha "rudisha wema'. Elvis Tables Musiba aliwasaidia wengi kufika pale walipo ikiwa ni pamoja na CEOs. Kumbuka amekuwa Mwenyekiti wa "boards" za kampuni nyingi. Wengi wa hawa CEOs ameshiriki kuwafanyia usahili kwa wao kuwa pale. Ndio maana haikumchukua muda kupata milioni 60. Alikuwa akiongea na watu ambao ni sehemu ya mchango wake katika maisha ya mafanikio yao. Hii ikanifanya nimdadisi zaidi. Nikamuuliza wewe ulianzaje biashara?

  Akasema mtaji wangu wa biashara ulitokana na kuuza vitabu. Vitabu kama NJAMA ndivyo vilivyonitoa. Lakini nilipoanza biashara haikuwa rahisi. Mimi nilikuwa mtanzania wa kwanza "mswahili" kumiliki "Bureau De Change"-anasema Elvis Tables Musiba. Lakini siku moja nikiwa Musoma, nikasikia kwenye redio kwamba biashara yangu iko mikononi mwa serikali. Kidogo nipate kichaa. Lakini sikukata tamaa nikaanza upya. Akasema nyie vijana wa siku hizi mnalalamika mazingira magumu ya biashara. Nawashangaa sana. Tuulize sisi. Haikuwa rahisi kama mnavyofikiria. Kutoka kwa Elvis Tables Musiba nikajifunza yafuatayo;

  I. Biashara ni mahusiano na watu. Elvis Tables Musiba kutumia saa moja kupata milioni 60 sio mchezo. Aliwekeza kwa watu. Leo hii kutafuta Tsh. 10,000/= ya luku ukikwama usiku wa manane na hauna salio kwenye simu ni shughuli pevu. Unaweza ukapiga namba zote kwenye simu yako usipate hata shilingi moja. Lakini Elvis Tables Musiba alitumia saa moja tu kupata shilingi milioni 60. Ina maana kila dakila alipata shilingi milioni 1.

  II. Kipaji chako ndio mtaji wako. Badala ya kulalamika huna mtaji, angalia una kipaji gani? Elvis Tables Musiba alikuwa na kipaji cha kuandika hadithi. Ndicho kilichompa mtaji wa kuanzisha biashara. Eric James Shigongo aliwahi kuniambia pia, kwamba kipaji chake cha kuandika hadithi ndicho kilichomsaidia kuanzisha kampuni ya magazeti pendwa na kudumu mpaka leo (Global Publishers). Mifano ni mingi. Bila mpira Mbwana Samata angekuwa wapi? Bila mpira George Weah angekuwa Rais wa Liberia? badala ya kulalamika anza na kipaji chako? Mimi nilianza kwa kuandaa makongamano. Unaweza ukawa unaandaa harusi vizuri kila mtu anashangaa. Lakini bado unafikiri hicho siyo kipaji. Unafikiri kipaji ni "kuimba" tu! Mwenzako makongamano yalinipeleka mpaka Ikulu, yakanipa na mtaji wa kuanza.

  III. Usikate tamaa. Elvis Tables Musiba anasema amefilisika mara nyingi katika maisha yake lakini alipambana akarudi tena kwenye mstari. Hakujinyonga. Baadhi ya biashara zake zilikwama. Lakini hakukata tamaa wala hakujenga chuki na watu. Kifupi, hakutafuta mchawi. Alianza upya na kusonga mbele. Alishirikiana na watu katika sekta binafsi na serikalini. Hiyo ndiyo roho ya "ujasiri wa mali" au "spirit" ya ujasiriamali au "entrepreneurship". Ni mlolongo wa kushindwa na kushinda, kushindwa na kushinda mpaka kieleweke.

  3. Dr. Reginald Abraham Mengi, Mwenyekiti Mwanzilishi wa IPP Group na Mwenyekiti wa zamani wa CTI na TPSF

  Dr. Reginald Abraham Mengi alinishirikisha mwanzoni kabisa wakati akianza kuandika kitabu chake cha "I Can, I Must, I Will". Nakumbuka alinipigia simu akasema njoo ofisini. Akaniambia nataka uwe sehemu ya team itakayonisaidia kukamilisha hili zoezi. Akaniomba nimtafutie vijana wengine wa kushirikliana na Prof. Msamali Nangoli, mwanazuoni wa Uganda aliyekuwa akiishi nchini Kenya, mwandishi wa kitabu maarufu kiitwacho "No More Lies About Africa". Prof. Msalami Nangoli alikuwa rafiki mkubwa wa Nelson Mandela, mpigania Uhuru na Rais wa kwanza wa serikali ya kidemokrasia nchini Afrika ya kusini. Akiwa gerezani, Nelson Mandela alikuwa akisoma makala za Prof. Msamali Nangoli, makala ambazo zilipitishwa gerezani kiujanja kama kifungashio cha chapati. Kumbuka akiwa gerezani, Mandela hakuruhusiwa kusoma hata magazeti.

  Ili kukamilisha zoezi la kuandika kitabu cha Dr. Reginald Abraham Mengi chini ya uongozi wa Prof. Msamali Nangoli, nilipewa "tapes" za hotuba za Dr. Reginald Abraham Mengi nyingi sana (mabox kwa mabox) ili nizipitie. Pia tuliwahoji watu wengi waliofanya kazi na Dr. Reginald Abraham Mengi. Bahati mbaya sana katikati ya safari ya kumsaidia Dr. Reginald Abraham Mengi kuandika kitabu chake, Prof. Msamali Nangoli akafariki dunia na Dr. Reginald Abraham Mengi akasitisha zoezi kwa muda. Baadaye akapata namna nyingine ya kumalizia kitabu chake kizuri.

  Tulipokuwa na Prof. Msamali Nangoli tulimshawishi sana Dr. Reginald Abraham Mengi kubadilisha "title" au jina la kitabu lakini alikataa. Sisi tulipendekeza kitabu chake kiitwe; Dr. Reginald Abraham Mengi-How I became Rich; Financially, Morally, Materially. Lakini hakutaka hata kutusikiliza. Baadaye nilikuja kugundua tulikuwa tunakosea sana kumshawishi abadilishe jina la kitabu cha "I Must, I Can, I Will". Kwanini?

  Kwa sababu siku moja nikiwa nyumbani kwake Kinondoni, nilimuuliza. Kwanini "I Must, I Can, I will"?. Akasema kwa sababu maisha ya biashara yana changamoto sana. Akaniuliza Paul, kwani unafikiri changamoto za biashara Tanzania ni zipi. Moyoni nikasema sasa Dr. ananiuliza swali gani "simple" namna hii. Au anataka kupima uwezo wangu wa kufikiri? Nikamwambia kubwa ni 3. Kwanza Mitaji au "Capital", Pili Masoko au "Markets", Tatu Rasilimali Watu au "Human resource". Akasema umekosa. Akasema kwanza Roho Mbaya, Pili Chuki, Tatu Wivu. Nilichoka kichwa. Akasema ili ufanikiwe lazima ukabiliane na hizi changamoto 3 nilizokutajia kisha uunganishe na hizo za mitaji, masoko na rasilimali watu. Ndio maana ya "I Must, I Can, I Will". Lazima udhamirie kutoka moyoni kupambana na changamoto.

  Dr. Reginald Abraham Mengi akasema tulipotoka ni mbali kuliko tulipo. Akasema nakumbuka wakati nimeanzisha biashara ya maji ya kunywa, nilienda kwenye maonyesho ya sabasaba kuonyesha biashara mpya ya maji. Akasema watu waliokuwa wakipita kwenye banda langu walikuwa wananishangaa sana. Wanasema "huyu mchaga anapenda sana hela". Mpaka anatuuzia maji? Kweli leo hii nchi hii tumefikia hatua ya kuuziana maji? Dr. Reginald Abraham Mengi akasema kwa hiyo unaweza ukaona "Kilimanjato Pure Drinking Water" imeshamiri ukafikiri ni lelemama. Haikuwa rahisi. Bora hawa ambao wanaanza kuuza maji leo. Sisi tulioanza tulipata shida. Kwa sababu hakuna aliyezoea kuuziwa maji. Lakini Paul ukweli ni kwamba huwezi kushindana na mtu aliyeanza. Aliyekutangulia amekutangulia tu!

  Dr. Reginald Abraham Mengi akaendelea kusema zaidi ya hapo kujenga sekta binafsi haikuwa rahisi. Kumbuka historia ya nchi hii toka kipindi cha wakoloni. Toka enzi hizo biashara zilikuwa kwa matabaka. Wa kwanza pale juu ni wazungu, wa pili waarabu na wa tatu wahindi. Sisi wazawa wa "kiswahili" tulikuwa hatufikiriwi kabisa kuwa "matajiri". Kuna wakati nilinunua Mercedez Benz lakini nilikuwa naogopa kuliendesha. Kwa sababu mifumo ya kiuchumi ilikwishakamatwa na matabaka mengine. Kwahiyo unavyoona sekta binafsi imefika hapa ni mapambano kwelikweli. Mswahili kumiliki kiwanda miaka ya sabini na themanini na Mswahili kuwa kiongozi wa sekta binafsi ambayo haina waswahili wengi ulikuwa ni mtihani ambao ilibidi kuushinda. Haikuwa kazi rahisi. Mimi Paul Mashauri nimeona na kusimuliwa mengi pengine nahitaji kitabu kizima kuzungumza ya Dr. Reginald Abraham Mengi. Lakini kuna mafundisho machache nataka niyataje hapa;

  I. Biashara si lelemama. Changamoto ni nyingi kuliko fursa. Lazima ubadilishe hizo changamoto ziwe fursa ili fursa ziwe nyingi kuliko changamoto. Hii haiwezekani pasipo kuwa na moyo mgumu "a iron heart". Kama unataka uache kazi uanze biashara ukifikiri ni mteremko jifikirie tena na tena na tena. Nakumbuka wakati nimemualika Dr. Reginald Abraham Mengi kuongea na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam alirudia hilo. Akasema; "safari ya mafanikio ni kama pambano la ngumi. Kuna makonde ya kuyakwepa, kuna makonde ya kuyazuia ambayo yakikupata yanasambaratisha uso wako au kukuua kabisa lakini kuna wakati ambao lazima ujibu mapigo ili ushinde pambano. Mh. Jokate Mwegelo, DC, Kisarawe, kipindi hicho akiwa chuoni, alikuwa "Moderator" katika tukio hilo. Anaweza akayakumbuka maneno haya.

  II. Usiogope kuanzisha njia pasipo na njia. Usiogope kuwa wa kwanza kufanya jambo ambalo wengine wanasita kufanya. Maana yake ni kwamba "be the pioneer". Dunia tunayoishi iko hapa ilipo sababu ya "pioneers". Christopher Columbus angeogopa kusafiri kutoka Spain pengine America (New Land) ingechelewa sana kutambulika katika uso wa dunia. Hata wewe usiwe mtu wa kusubiri wenzako waanze. "Legends" sio wale wanao "copy na kupaste" Legends ni waanzilishi. Kuanza sio lazima iwe ni kwenye biashara. Hata kwenye familia yako unaweza ukawa wa kwanza kuwa "mbunge".


  4. Mr. Ali Mfuruki, Aliyekuwa Mwenyekiti wa CEO Round Table

  TRBN (Tanzania Responsible Business Network) ilipoanza niliombwa na Partner wa KPMG Ketan Patel pamoja na Partner wa Deloitte Joe Eshun niwe "Moderator" katika sherehe za uzinduzi wa TRBN pale Serena Hotel. Tulikuwa na CEOs zaidi ya 300. Mgeni rasmi alikuwa ni Mr. Ali Mfuruki, Mwenyekiti wa CEO Round Table. Baada ya ufunguzi nilikuwa na muda wa kutosha wa kuongea na Mr. Ali Mfuruki. 

  Jambo moja Mr. Ali Mfuruki aliniambia ambalo sitolisahau ni kwamba lazima uwe na msimamo na lazima ukubali kupoteza baadhi ya vitu ikiwa ni pamoja na fedha kusimamia unayoyaamini. Akaniambia nyie vijana sasa hivi ndio mmekuwa mameneja kwenye makampuni na viongozi wa serikali na taasisi mbalimbali. Sasa wakati mwingine unakutana na kijana kwenye kampuni ambaye amepewa mamlaka, kijana ambaye unaweza kumzaa anataka akuzungushe, akunyanyase ili umpigie magoti. Mimi siwezi. Bora nikose hela kuliko kushusha heshima yangu.

  Wapo vijana ambao wanamsikia Mr. Ali Mfuruki leo hii lakini hawajakutana na Mr. Ali Mfuruki na kuzungumza naye ana kwa ana. Sijui umesikia nini juu yake lakini Mr. Ali Mfuruki alikuwa na msimamo wa kipekee. Alikuwa anafikiria vizuri sana sio katika biashara zake tu hata kwa nchi. Ndio maana kifo chake kimetushtua kama Taifa. Unaweza ukawa unafikiria vizuri lakini kwa mambo yako binafsi na familia yako. Hilo ni jambo zuri na ndiyo jambo la pili baada ya kumfikiria Mungu. Lakini unapojiongeza na kufikiria Taifa na watu wengine ndani ya Taifa unakuwa wa tofauti zaidi. Ndivyo alivyokuwa Mr. Ali Mfuruki. 

  Kuna siku nilikutana naye nikamuuliza Mr. Ali Mfuruki lini unaandika kitabu? Akaniambia nimeanza kuandika. Siku niliposikia ametoa kitabu, nikawahi bookshop Mlimani City kununua. Lakini baada ya kusoma kile kitabu nikagundua nilichofikiria kuwa kitakuwepo kwenye kitabu sicho. Mr. Ali Mfuruki hakuwa ameandika kitabu kuhusu yeye na mke wake na watoto wake. Alikuwa ameandika kitabu kuhusu uchumi wa viwanda. 

  Huyo ndio Mr. Ali Mfuruki. Ndiyo sababu alidumu kama Mwenyekiti wa CEO Round Table kwa miaka mingi. Sio kwamba alipenda kuhodhi madaraka. Alikuwa ana uwezo kichwani. Na vyeo vingi alikuwa anakataa. Na pale alipokubali alijitoa kwa dhati. Amekuwa Mwenyekiti wa "boards" za Mwananchi Communications Ltd, amekuwa kwenye "board" ya Geita Gold Miming (GGM), Mwenyekiti wa "board" ya Vodacom nk. Waulize waliofanya kazi naye. Kile kilikuwa kichwa kingine.

  Wakati fulani nilialikwa katika uzinduzi wa "Private Equity Fund" moja pale Golden Tulip Hotel. Alikuwepo Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mh. Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waheshimiwa mawaziri na wafanya biashara. Mr. Ali Mfuruki alikuwa miongoni mwa waalikwa pia. Siku ile Mr. Ali Mfuruki aliongea kitu kikubwa sana. Akasema, wakati Marekani inataka kwenda mwezini miaka ya 60.

   Rais wa nchi hiyo J.F. Keneddy alitangaza kwamba Mmarekani yoyote atakayekuja na wazo au "idea" au "ubunifu" au "teknolojia" ambayo itaisaidia Taifa la Marekani kufika mwezini au kufika hatua moja mbele katika ndoto ya nchi kwenda mwezini, serikali ya Marekani italipa fedha kununua hilo wazo au huo ubunifu. 

  Mr. Ali Mfuruki akasema; ili sisi kama Taifa tuweze kwenda mbele lazima kuwe na mbinu za kujenga "uhitaji" au "demand" ya ugunduzi na ubunifu "Creativity and innovation" . Akasema "kufikiria" ni kazi. Kugundua kitu ni gharama. Lazima ufanye "research" au "utafiti". Tukitaka watu wetu wawe wabunifu lazima tutengeneze mbinu za kumfikirisha mtu akijua kabisa kuwa nguvu zake hazitoenda bure.


  Mr. Ali Mfuruki alikuwa haongei "nadharia". Sijawahi kumsikia akiongea "pumba". Kwa historia yake yeye ni mhandisi au "engineer" kwa lugha ya kiingereza. Mr. Ali Mfuruki Alipotoka nchini Ujerumani aliposomea, kuja nyumbani Tanzania kufanya biashara, aliona kuna fursa, kuna "demand" au "uhitaji" wa bidhaa za teknolojia hasa kompyuta. 

  Kipindi hiki nchi ilikuwa imefunguka na serikali pamoja na makampuni binafsi yalikuwa yanabadilisha teknolojia kutoka katika mfumo wa kizamani wa "fax" na "typewriters" kuja kwenye matumizi ya kompyuta. Ndivyo kampuni yake ya Infotech Technologies Ilivyoanza. 

  Huwezi kuzungumzia Teknolojia Tanzania pasipo kumzungumzia Mr. Ali Mfuruki ingawa amekuwa na biashara nyingi zaidi ya hiyo. Yeye ni baba katika eneo hili la TEHAMA hapa Tanzania pamoja na kwamba unapozungumzia ujio wa WoolWorth unamzungumzia Mr. Ali Mfuruki na hata unapozungumzia ujio wa Zuku unamzungumzia Mr. Ali Mfuruki. Nini cha kujifunza hapa;

  I. Tunaishi katika dunia ya ubepari au "capitalism". Dunia ya "ubepari" na dunia ya ujamaa au "socialism" ni dunia 2 tofauti. Katika dunia ya ubepari mtu anaweza akakudhalilisha kwa sababu amekupa fursa. Mtu anaweza akataka umuabudu na umpigie magoti kwa sababu anakupa biashara. Mtu anaweza akakuvunjia heshima mbela ya mke na watoto wako kwa sababu bila yeye huwezi kupata mshahara. Haya ndiyo mambo ambayo Mr. Ali Mfuruki aliniambia hayataki. Akasema bora niwe "broke" au "masikini" kuliko kudhaliliswa. Alikuwa na msimamo.

  II. Vijana wengi wanatamani kuheshimiwa kama Mr. Ali Mfuruki. Lakini hawajui kuwa heshima haiji kwenye kikombe cha chai. Inajengwa kwa jasho kubwa. Mimi Paul Mashauri ambaye nimekaa na hawa watu najua. Mimi Paul Mashauri ambaye nimetumika sana kwenye sekta binafsi nijaua. Ni kazi ngumu na inataka moyo. Kumbuka Mr. Ali Mfuruki ni mfanyabiashara. Ana biashara zinazomuangalia yeye. 

  Na bado aangalie ya nchi. Sio jambo dogo. Kumbuka akifanya hivyo waziri ni sawa kwa sababu mwisho wa mwezi analipwa mshahara. Ni sehemu ya "job description". Lakini unapokuwa Mwenyekiti wa hizi taasisi za sekta binafsi unatumia akili zako na nguzu zako kama msaada na mchango kwa Taifa. Ingawa sina uhakika kama ukifilisika unapewa tena mtaji na Taifa. Ndio maana nasema inataka moyo. Ni vijana wangapi wako tayari kufanya hivyo? Kuacha biashara yako na watoto wako kuhangaikia ya wengine?

  III. Mr. Ali Mfuruki alikuwa anafikiri vizuri "thinker" kwa sababu alikuwa anatumia muda mrefu sana kukutana na watu wa haiba tofauti, kusoma, kusafiri kupata "exposure" nk. Hakuna mtu alikuwa anamlipia tiketi ya ndege kusafiri. Alikuwa anajilipia mwenyewe. Leo unataka kuwa kama Mr. Ali Mfuruki unashinda instagram unasoma udaku. 

  Hautaki kwenda kwenye kongamano lolote zaidi ya matamasha ya muziki na comedy. Kila tasnia ina utamaduni wake. Ukitaka kuketi katikati ya wakuu lazima ufikirie kama wakuu. Mr. Ali Mfuruki aliitwa na wakuu, alikaa meza moja na wakuu akiwemo Barack Obama, Rais Mstaafu wa Marekani sio kwa sababu alikuwa "handsome" mwenye "six packs" tumboni kuliko watanzania wote. La hasha! Alikuwa na madini adimu kichwani.


  5. Ruge Mutahaba, Aliyekuwa Mkurugenzi au "Director" wa programs, Clouds Media Group

  Niliposikia amefariki, nilisikitika sana. Kwa sababu miezi michache iliyopita kabla ya taarifa hizo nilimpigia simu. Nikamwambia kaka Ruge kuna kongamano la vijana na wazazi tunaandaa naomba uje uzungumze hasa na vijana. Akajibu akasema "count me in". Lakini miezi kadhaa nyuma, Ruge mwenyewe alinipigia simu. Akasema Paul wewe na mimi kama "speakers" lazima tufanye mambo ya kusaidia nchi. Akaniambia hebu andika "andiko" au "proposal" ya kusaidia Taifa letu kwa kutumia "speakers" kuhamasisha fikra mbadala hasa katika mambo ya msingi ya kitaifa. Nilikesha usiku ule nikaandika ile "proposal" na nikamtumia Ruge kwa email. Ile "propoal" niliipa jina la "Speakers Without Boarders".

  Wengi walimfahamu Ruge Mutahaba kwenye "media" na "muziki" lakini Ruge Mutahaba alikuwa ni zaidi ya media na muziki. Ndio sababu alipofariki hata Rais wa nchi alitoa neno. Uwezo wa Ruge Mutahaba ulikuwa hauna shaka. Ubishi wake kwa kile alichokiamini ulikuwa si wa kitoto. Na utayari wake kujitoa kwa ajili ya wengine hauelezeki. Siweki chumvi na mimi sio mnafiki wala sisemi haya yote kwa sababu hayupo tena duniani. Niliyasema haya hata alipokuwa hai. 

  Niliyasema ya Mr. Ali Mfuruki wiki iliyopita ambayo ni wiki moja kabla hajafariki. Sio wote wana moyo wa kusema nani aliwasaidia katika maisha yao lakini mimi nasema kwa sababu duniani hakuna mtu anayetoka bila msaada wa mtu mwingine. Hakuna kitu kama "self-made". Kusaidiwa sio lazima iwe pesa .Hata mwalimu wa shule ya msingi alikusaidia kujua kusoma na kuandika. Leo unasemaje kuwa wewe ni "self-made millionaire"? Humkumbuki hata mkeo au mumeo aliyekutia moyo ulipokata tamaa?

  Ruge Mutahaba alinisaidia sana mimi na vijana wengine wengi. Yeye ndiye aliyenitambulisha kwa Azim Jamal aliye kuja kuwa rafiki yangu mkubwa katika "motivational speaking". Huyu ni mnenaji au "speaker", mwandishi wa vitabu au "author", mtaalam wa menejimenti au "consultant" na mfanyabiashara aliyebobea. Azim Jamal amefanya kazi na kuandika vitabu pamoja na wataalam na wanenaji "speakers" wakubwa duniani kama Brian Tracy. 

  Kumlipa Azim Jamal kuzungumza kwenye tukio lako sio chini ya dola za Kimarekani milioni 10 au fedha za kitanzania zaidi ya shilingi milioni 20 ndani ya siku moja. Lakini kwa sababu ya urafiki na heshima ya Ruge Mutahaba, Azim Jamal alikuja kuzungumza kwenye tukio nililoandaa bila kulipwa hata shilingi moja. Baada ya hapo tulifanya kazi nyingi sana na Azim Jamal.

  Pili wakati tunaanzisha gazeti la Familia, yeye ndiye aliyenipa matangazo ya bure. Alisema wewe unafanya kazi kubwa sana kuhamasisha vijana. Hakuna anayekulipa kwa kujitolea kwako. Malipo yako yatakuwa matangazo nitakayokupa Clouds FM. Kwa moyo ulionao ukitoka wewe, wengi zaidi watatoka. Ruge Mutahaba alilipa gharama ya kazi yangu kwa vijana. Si hayo tu, yeye pamoja na Joseph Kusaga ndio walionipa studio za Clouds TV kutengeneza sinema yangu iitwayo "Maisha Ni Siasa". 

  Angalia sinema hii yote Youtube. Sio mimi tu, wako wengi aliowasaidia. Hata serikali inatambua nini Ruge Mutahaba alifanya katika nchi hii. Uzoefu wangu wa Ruge Mutahaba tukiwa wajumbe wa TRA Stakeholders Forum ulinidhihirishia uwezo wake wa kuangalia mambo kwa jicho la tatu. Ndio sababu alikuwa mbunifu sana. Kila tulipokuwa na kikao, Ruge Mutahaba hakuwa wa kwanza kuongea. Lakini alipopata nafasi ya kuongea, aliipindua pindua mada na wote tukaiona hoja husika kwa namna ambayo hatukuiona hapo kabla.

  Kila nikimkumbuka Ruge Mutahaba nakumbuka mmoja kati ya vijana ambao walijiongeza. Ungeniuliza ni akina nani wanafanya sana kazi bila kuchoka ningekuambia ni Ruge Mutahaba. Binafsi sijui alikuwa anapumzika saa ngapi. Unakutana na kijana anasema anataka kuwa kama Ruge Mutahaba na bado analala saa 2 usiku na anaamka saa 2 asubuhi. Unataka kuwa kama Ruge yupi? Sijaona mimi mtu anafanya vitu vikubwa vya kitaifa na analala usingizi wa pono. Uliza wasaidizi wa Rais kama wanalala? Kama unajua huwezi kufanya kazi kwa bidii kubali kuwa wa kawaida. Usifikiri nazungumzia "utajiri". Hilo ni suala lingine.

  Unaweza usiwe tajiri lakini bado ukawa si wa kawaida. Akina Dr. Martin Luther King Jr. na Nelson Mandela hawakuwa matajiri lakini pia hawakuwa wa kawaida. Lazima utofautishe kati ya kuwa "rich" au "tajiri" na kuwa "great". Hapa sizungumzii utajiri nazungumzia "greatness". Hata mwizi anaweka kuwa "tajiri" lakini inahitaji "akili nzuri", "kujitoa kwa wengine" na "kujituma" ili uwe "great" Vitu vinavyobadilisha jamii havihitaji mtu mzembe. Kama kusoma tu hii makala mpaka hapa umeshachoka unatamani iishe utaweza kuwa kama Ruge Mutahaba? Kuna mambo ya msingi ya kujifunza kutoka kwa Ruge Mutahaba;


  I. Ubishi. Hakuna kitu kinakuja kirahisi. Mafanikio sio muujiza, yanafanyiwa kazi. Usifikiri Ruge Mutahaba alifika pale alipofika sababu ya "Clouds" kama media. Hatukatai ukweli kwamba alikuwa ni mmoja wa watu walioijenga Clouds Media Group. Kwanza, ulikuwa ukisikia Clouds FM iko hewani, sura mbili zinakuja kichwani kwako; Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga. 

  Hata isingekuwa "media" Ruge Mutahaba angefanya vitu vikubwa tu kwa sababu alikuwa ni "mbishi" asiyekubali kushindwa. Miaka 3 iliyopita nilimualika Ruge Mutahaba katika kongamano la Vijana lililoandaliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu chini ya Baraza la Taifa la Uwezeshaji (NEEC) pamoja na Shirika la Kazi Duniani (ILO) pale Serena Hotel. Kongamano lilikuwa chini ya mradi wa kutoa mitaji kwa mawazo bora ya biashara kwa vijana "Ajira Yangu" Project ambayo niliisimamia.

  II. Alipopewa nafasi ya kuzungumza, Ruge Mutahaba akasema "ukija kwangu na wazo au "idea" yako nakurudisha mara 3 au mara 4. Sio kwa sababu wazo lako ni baya. Nataka nione kama kweli wewe ni mbishi na uko tayari kupambana mpaka wazo lako lipate maisha. Vijana wa leo hawako hivyo. Wanataka mambo ya chapchap kama mabando ya internet. Hawana uthubutu. Wanaamini kwenye michongo na kushikwa mkono. Wanakata tamaa mapema. Hata wakija kwako uwe "mentor" wao wanakuja "kifursa zaidi". Wanataka uwe "mentor" wao na hapohapo uwape "hela". Hiyo sio "mentorship" hiyo ni "sponsorship". Sasa hatujui unataka nini? Unataka "mentorship" au "sponsorship"?Hawajui kuwa hata akina Ruge Mutahaba walipitia vikwazo lakini walikuwa wabishi.

  III. Uwezo wa kufanya lolote unalolitaka. Nilisema hapo mwanzo kwamba wengi wanamjua Ruge Mutahaba kwa sababu ya "media", "muziki" na "matamasha". Ruge Mutahaba alikuwa zaidi ya hapo. Ruge Mutahaba alikuwa pia anandaa sinema. Nikiwa chuo kikuu Ruge Mutahaba alirekodi sinema inaitwa "Kelele". Yeye mwenyewe binafsi alikuwa nyuma ya kamera kuhakikisha sinema inarekodiwa vizuri. Ingawa sikumbuki kama aliwahi kuitoa ile sinema lakini nilichojifunza ni kwamba alijua anaweza kufanya kitu zaidi ya kimoja.

  Kuna mikakati mingi sana na miradi mikubwa ya kitaifa mbayo Ruge Mutahaba alikuwa nyuma yake ingawa hakuonekana mstari wa mbele. Huyo ndiyo Ruge Mutahaba niliyemfahamu mimi. Leo hii unatamani siku moja upewe heshima aliyopewa Ruge Mutahaba lakini hujiulizi nini kitu cha tofauti unafanya? Zaidi ya kutoka bwenini, kwenda darasani kisha kwenda bwaloni kula ubwabwa nini kingine unafanya? Zaidi ya kutoka kazini na kwenda baa au kwenye harusi kula pilau, nini kingine unafanya?Unawezaje kuwa kama Ruge au zaidi ya Ruge kwa maisha ya pembe tatu?Unawezaje kufikia ndoto zako kwa maisha ya pembe tatu? Hata kama umeajiriwa. Usiku unafanya nini?

  Tanzania imepoteza watu muhimu sana katika muda mfupi sana. Niliyoyataja hapa kwa hawa "generals" ni machache sana ukilinganisha na niliyoyafahamu na nisiyoyafahamu. Hawa watu walitumia vyema uwepo wao hapa duniani na uwepo wao katika hii nchi kuleta utofauti. Ni "generals" walioondoka lakini nchi bado ipo. Pamoja na utofauti wao, hawa wote wanasifa zinazofanana. Pamoja na mapungufu yao wote hawa wana faida zinazofanana.

  1. Waliwekeza katika maarifa 2. Waliwekeza katika watu 3. Walitumia karama, vipaji na elimu zao kuleta utofauti na kulitumikia Taifa 4. Hawakuwa wepesi kukata tamaa hata walipopitia magumu katika ngazi za familia zao, maisha yao binafsi, biashara zao na kazi za kitaifa 5. Wameacha alama katika nchi hii, alama ambayo itaendelea kuishi ingawa wao hatunao tena. Amani ya bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nao, familia zao, ndugu zao, marafiki zao na watanzania wote kwa ujumla. 

  Makala hii imeandikwa na Paul R.K Mashauri@hakimiliki 2019. Hairuhusiwi kuchapisha Makala hii au sehemu ya Makala hii pasipo idhini ya mwandishi. Wasiliana na mwandishi kupitia ceo@masterclassworldwide.co.tz 

  0 0

  BENKI ya NMB imetwaa tuzo maalum kutoka Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu(NBAA) kama Benki bora ya Taarifa za Kifedha zilizokaguliwa na kutambuliwa kimataifa kwa mwaka 2018,ilikoshinda benki kadhaa nchini.

  Benki hiyo imetambuliwa kwa kufikia kiwango bora katika utayarishaji wa taarifa zake za kifedha, kulingana na mahitaji ya taarifa (viwango vya kuripoti za kitaifa na kimataifa).

  Hafla ya kukabidhiwa tuzo hiyo ambayo kwa NMB, ni ushindi wa mara ya pili mfululizo, ulifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki ambapo NBAA ilisema taarifa za mahesabu za NMB zimeendelea kuwa bora kila mwaka, ubora uliowasukuma majaji kuwapa tuzo hiyo kwa mara nyingine.

  Akizungumzia vigezo vilivyotumika kupata washindi, Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA Mr.Pius Maneno, amesema walipatikana kwa kuangalia washiriki waliovuka asilimia 75 ya vigezo vilivyowekwa.

  Naye Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Mr. Benedicto Baragomwa, amesema wao kama wataalam wa masuala ya fedha, wanatambua umuhimu wa kuandaa vitabu vya mahesabu vya Benki kwa njia na mifumo inayozingatia viwango vya kitaifa na kimataifa.

  “Ushindi huu unadhihirisha namna ambavyo tumejikita katika kudumisha uadilifu wa hali ya juu kwenye uwasilishaji wa taarifa zetu za kifedha za mwaka,” alisema Baragomwa baada ya kupokea tuzo kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Shabani.

  Baragomwa alibainisha kuwa, wawezeshaji wa benki hiyo wameandaliwa katika misingi inayofuata na kuheshimu viwango vya kimataifa vinavyotambuliwa na IFRS, pamoja na mahitaji ya ndani.

  Taarifa iliyotolewa na Benki hiyo imetoa shukrani kwa wafanyakazi na kujivunia mfumo bora wa Uongozi na utendaji hasa kitengo cha fedha. "Tuzo hii imepatikana nyuma ya mfumo uliopo wa utawala bora na michakato ya udhibiti ambayo inakuza uwazi wa taarifa za kifedha, uwajibikaji,ueledi na kiwango cha juu cha uadilifu wa takwimu. Hongera kwa kila mtu, haswa timu ya kifedha kwa kuongoza maandalizi ya Taarifa ya Fedha ya Benki ya NMB.
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Amina Khamis Shaabani, akimkabidhi Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, Tuzo ya Benki Bora katika utayarishaji wa ripoti za kifedha kwa mwaka 2019, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NBAA). Hafla ya kukabidhiwa tuzo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. 
  Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa, akionesha Tuzo aliyoipokea ya Benki ya NMB kuwa Benki Bora katika utayarishaji wa ripoti za kifedha kwa mwaka 2018, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Hesabu (NBAA).
  Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha Benki ya NMB, Benedicto Baragomwa (wa pili kulia) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa utoaji tuzo.

  0 0


  Bi. Pili Said Kassimu ambaye ni mmoja wa wahitimu wa ngazi ya Stashahada akipokea cheti kutoka kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa.

  Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa akitoa hotuba wakati wa mahafali ya 30 ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) ambapo aliwataka wahitimu wakawe raia wema na kuitumia elimu waliyoipata ipasavyo kwa ajili ya manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Washauri ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) Bw. George D. Yambesi akitoa neno kwa wahitimu pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kutoa hotuba yake.
  Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa (katikati) akiwa katika Meza Kuu na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Bagamoyo pamoja na viongozi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni bagamoyo (TaSUBa). 

  Wahitimu wakisikiliza hotuba kwa umakini kutoka kwa Mgeni Rasmi ambaye alikua ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa (hayupo pichani).

  Mhitimu wa ngazi ya Stashahada Bw. David Nashoni akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake mbele ya mgeni rasmi ambaye alikua ni Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Mhe. Zainabu Kawawa.

   
  Kikundi cha ngoma kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) kikitoa burudani wakati wa mahafali ya 30 ya Taasisi hiyo.

  0 0

  Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (wa pili kulia) akibadilishana nyaraka na Mkuregenzi wa T-Pesa, Lulu Mkude, baada ya kuingia makubalianao ya mpango wa pamoja wa kutoa huduma za SimBanking na T-Pesa utakaowawezesha wateja kupata huduma za kifedha kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi, katika hafla fupi iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mauzo na Usambazaji - TTCL, Mruta Hamis. Picha zote na Othman Michuzi.
  Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa (katikati) akishuhudia uzinduzi wa huduma ya kuhamisha fedha kati ya SimBanking na T-Pesa uliofanywa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Benki ya CRDB, Stephen Adili na Mkuregenzi wa T-Pesa, Lulu Mkude
  Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu (aliyesimama) akizungumza jambo wakati akiongoza hafla hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. 
  Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki ya CRDB pamoja na wa TTCL wakifatilia hafla hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. 


  Benki ya CRDB na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) leo wamezindua mpango wa pamoja kupitia huduma za SimBanking na T-Pesa utakaowawezesha wateja kupata huduma za kifedha kwa urahisi kupitia simu zao za mkononi.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na Wakati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema mpango huo unalenga katika kuwarahisishia wateja kuhamisha fedha kutoka akaunti za CRDB kwenda T-Pesa, kuhamisha fedha kutoka T-Pesa kwenda akaunti yoyote ya CRDB pamoja na kununua muda wa maongezi kupitia Simbanking.

  “Lengo letu ni kuwapa wateja wetu uzoefu bora zaidi pindi watumiapo huduma ya SimBanking. Tunataka kuona mteja akiingia kwenye SimBanking USSD kwa kupiga *150*03# au SimBanking App aweze kumaliza mahitaji yake yote ya kifedha ‘One Stop Shop’ ikiwamo miamala ya T-Pesa,” alisema Raballa.

  Raballa alisema ushirikiano huo na TTCL utataidia kusogeza huduma kwa watanzania wengi zaidi hususani maeneo ya vijijini. Takwimu zinaonyesha ni asilimia 60 ya watanzania ndio wameunganishwa na mfumo wa kifedha kupitia simu za mkononi, wakati ni asilimia 17 tu ya watanzania ndio wanaotumia huduma za kibenki.
  “Benki ya CRDB inafanya kazi kwa bidii kuhakikisha Watanzania wengi wanapata huduma za kifedha, hatua ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi wetu wa taifa letu. Tunafurahi kushirikiana na TTCL katika kufanikisha azma hii "aliongezea Raballa.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa T-Pesa, Lulu Mkude, alisema ushirikiano huo ni mafanikio makubwa kwa TTCL, kwani utawawezesha maelfu ya watanzania wote wa mijini na vijijini kupata huduma za kifedha za kwa urahisi.

  Lulu alisema TTCL kuunganishwa kwa huduma ya T-Pesa na SimBanking kutawasiaidia wateja wa Benki ya CRDB kuweka pesa kwa urahisi kwenye akaunti zao kupitia T-Pesa lakini pia kuongeza salio au kuwatumia ndugu jamaa na marafiki fedha kwenye akaunti zao za T-Pesa.

  ''Kufurahia huduma mteja atatakiwa kuingia katika menu ya T-Pesa kwa kupiga *150*71#, na kisha kuchagua huduma ya SimBanking,” alisema Lulu Mkude, huku akisisitiza kwamba hivi sasa TTCL imejipanga vilivyo kusogeza mawakala wake wa T-Pesa karibu zaidi na wananchi hususani vijijini ambapo kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma za kifedha

  0 0

  Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii, Mtwara

   Usajili wa laini za simu kwa alama za vidole ni usalama kwa Taifa kwani vitambulisho vya Taifa vinavyotumika katika usajili wa laini hizo ndio baadae watanzania tutatumbuliwa kwa kuwa na vitambulisho vya mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

  Hayo ameyasema Mkuu wa Wilaya ya uu Mtwara Evod Mmanda kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa Uhamasishaji wa Wananchi kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

  Mmanda amesema changamoto kwa baadhi ya Wananchi wa Mtwara kupata vitambulisho ni kutokana na wanatoka nchi jirani ya Msumbiji hivyo lazima wafuate taratibu za Uhamiaji.

  Amesema kuwa kila mtu ahakikishe anapata kitambulisho cha taifa ili aweze kusajili laini yake kwa alama za vidole kwani namba zitafungwa Desemba 31 na ambao hawatafanya namba hizo zisizosajiliwa zitafungwa na kugaiwa kwa watu wengine.

  Amesema kuwa taarifa zilizosambaa katika mtandao ya kijamii kuwa zoezi la kuzima laini simu Desemba 31 kuwa limeongezwa ni kuzipuuza na kwamba zoezi liko palepale.

  Aidha amesema kuwa katika kipindi hiki Wananchi waache kununua simu Mkononi kwani kuna watu wanaweza kufanya uhalifu na mwisho wa siku mtu akaingia katika matatizo.

  Nae Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko Amesema zoezi la usajili kwa Mkoa wa Mtwara lipo kwa Wilaya zote na kutaka Wananchi wajitokeze kupata kusajili laini za simu .

  Amesema zoezi la kuzima simu liko palepale hivyo watu waache kupotosha zoezi hilo.Eseko Amesema kanda ya Mashariki wamezindua Uhamasishaji kumekuwa na matokeo makubwa kwa Wananchi kuhamasika katika kujisajili.

  Afisa Usajili wa Mkoa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Gide Magila amesema changamoto wanayokutana nayo ni watu kusajili majina mara Mbili na wakati mwingine kusahau kumbukumbu walivyosajili.
   Foleni ya Wananchi wakiwa katika ufatliaji wa namba za vitambulisho vya Taifa.
  Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na usajili wa laini za simu kwa alama  vidole katika uwanja wa Sabasaba mjini Mtwara. 

   Wananchi wakiwa katika foleni ya kuangalia namba za vitambulisho vya Taifa katika mfumo wa NIDA
   Afisa Msajili wa Mkoa wa Mtwara  wa Mamlaka ya a Vitambulisho vya Taifa (NIDA)Gide Magila  akitoa changamoto wanazokutana na Wananchi wakati usajili na uangaliaji majina katika mfumo.
   Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda akizungumza na Wananchi wakati wa Uhamasishaji wa usajili wa laini za simu kwa alama za vidole katika Mkoa wa Mtwara.
   Mabanda ya watoa huduma za simu kwa ajili ya kusajili laini za simu za  Wananchi kwa alama za vidole.
  Mwakilishi wa Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa TCRA Violet Eseko akizungumza namna kanda ya TCRA inavyohamasisha Wananchi kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

  0 0


   Moja ya mitambo ya kuzalisha umeme jua kutoka kampuni ya JUMEME iliyopo katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe. 
   Baadhi ya mafundi mitambo wa kampuni ya JUMEME, wakifunga mitambo ya umeme jua katika moja ya miradi ya kampuni hiyo huko kisiwani Ukara, Ukerewe mkoani Mwanza.  ZAIDI ya kaya 5,000 katika kisiwa cha Ukara kilichopo wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, zimenufaika na umeme jua unaozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya usambazaji umeme vijijini (JUMEME).


  Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni hiyo, Profesa Costa Mahalu katika hotuba yake kwa maofisa kutoka Umoja wa Ulaya na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), waliotembelea miradi ya umeme jua iliyopo wilaya hapo.


  Profesa Mahalu alisema kaya hizo zimenufaika kutokana na awamu ya kwanza ya mradi wa usambazaji umeme katika kisiwa hicho cha Ukara.

  “Awamu ya kwanza ya iliyopewa jina la "Uzalishaji umeme wa katika kukuza uchumi wa Tanzania’ imeonesha utofauti kutokana na faida za kiuchumi na kijamii zilizopatikana.


  “Kwa sababu mbali na kaya 5,000 kunufaika pia, wafanyabiashara wadogo na viwandani pia wameunganishwa. Lakini taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kijamii kama vile maji vijijini na hospitali zimeunganishwa,” alisema.


  Alisema huduma za JUMEME zimevifikia vijiji 20 kwenye visiwa 10 tofauti, na kuchochea uchumi wa eneo hilo jambo lililosaidia kuibua fursa nyingi za ajira.


  "Malengo ya muda mrefu kwa JUMEME ni kuendelea  kushirikiana na wazalishaji wadogo ikiwa ni pamoja na kuwekeza kwa waajiriwa wa eneo husika," alisema Prof. Mahalu ambaye pia ni Makamu wa Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT).


  Aidha, alisema kampuni hiyo imekuwa ikizingatia utoaji wa fursa za ajira kwa watanzania ili kuisaidia Serikali kukabiliana na uhaba wa ajira kwa vijana nchini.


  "Kila mmoja wa wafanyakazi wanaofanya kazi ya uhandisi katika miradi 12 ya JUMEME, ni Mtanzania. Kati ya watu 25 wanaounda timu ya kudumu ya JUMEME wenyeji ni 22, ambao hupewa upendeleo wa wazi linapokuja suala la kufanya kazi.


  “Kwa kuzingatia mafanikio ya awamu hii ya kwanza, tunatumaini kuwa na uwezo wa kutoa fursa zaidi za kazi kwa vijana wetu kwa kuendelea nao katika awamu ya pili, ya tatu na kuendelea zaidi katika miradi ya JUMEME. " alisema.


  Alisema ili kuongeza uweledi na ufanisi wa waajiriwa wazalendo, kampuni hiyo inaendelea kutoa mafunzo yanayowajengea uwezo wahandisi wa ndani na vijana wataalamu kwa madhumuni ya kuendesha gridi ndogo ndogo zinazoendelea kujengwa hapa nchini.


  Pia alisema lengo la JUMEME ni kutoa umeme wa uhakika na wa bei nafuu kwa wakazi husika hususani maeneo ambayo umeme gridi ya Taifa haiwezi kufika.


  “Lengo letu ni kufunga mifumo 300 ya uzalisha umeme utakaoweza kuingizwa kwenye ya gridi ya Taifa na kusaidia watu zaidi ya 1,000,000 ifikapo mwaka 2023 katika vijiji mbalimbali nchini Tanzania.


  Aliongeza kampuni hiyo ya JUMEME ilioundwa mwaka 2014  chini ya mradi wa "Micropower Economy roll out in Tanzania" na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU), inalenga kukuza, kujenga, na kuendesha gridi ndogo za umeme jua katika vijijini mbalimbali  nchini.  0 0


   
   
   
  Mtwara Jumatano 11 Disemba 2019

  Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezindua kampeini ya ‘Haachwi Mtu Nyuma Kamilisha Usajili mkoani Mtwara huku ikiwahimiza mwananchi wa mkoa kukamilisha usajili wa laini zao za simu kwa alama ya vidole kabla ya mwisho wa mwezi.

  Kampeini ya Haachwi Mtu Nyuma Kamilisha usajili ya laini ni ushirikiano wa makampuni yote ya simu za mkononi hapa nchini huku ikisimamiwa na TCRA kwa udhamini wa FSDT.

  Akizungumza Mtwara wakati wa kuzindua kampeini hiyo ya Haachwi Mtu Nyuma kamilisha usajili wako, Mmwakilishi wa TCRA Kanda ya Mashariki Viollet Essoko amesema changamoto zilizopo zimekuwa zikifanyiwa kazi na kusisitiza kuwa licha ya kuwekwa matangazo ya kuhamasisha umma haachwi mtu nyuma kamilisha usajili bado kuna wananchi wanasua sua kufuatilia michakato ya NIDA ili kupata namba na kusajili line zao za simu.

  Amesema idadi kubwa ya vijana wamekuwa wakipuuzia zoezi hilo huku watu wenye umri mkubwa wameonyesha kujitokeza kwa wingi kufuatilia vitambulisho vya nida lakini pia kusajili line zao za simu.

  Wakati huo huo, baadhi ya wakazi wa mkoa wa mtwara ambao bado hawajapatiwa vitambulisho vya taifa vya NIDA wameiomba mamlaka hiyo kuongeza watendaji na vitendea kazi ili kurahisisha zoezi hilo ambalo kwa sasa limekuwa na muamko mkubwa kwa wakazi wake.

  Wakazi hao wametoa ombi hilo kutokana na kukaa kwenye foleni ili kupata huduma hiyo kwa muda mrefu na hivyo kushindwa kufanya shughuli za kimaendeleo ipasavyo.

  Hata hivyo wakazi hao wameiomba mamlaka hiyo kuongeza watendaji sambamba na vitendea kazi ili zoezi hilo liweze kwenda kwa haraka hasa kipindi hiki ambacho idadi ya watu imeongezeka.

  Mapema akifungua zoezi hilo ambalo litadumu takribani wiki nzima katika wilaya zote za mkoa wa Mtwara Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evodi Mmanda amewataka wananchi kutopuuzia zoezi hilo ambalo umuhimu wake ni mkubwa.

  Amesema huwezi kuitwa Mtanzania kama huna kitambulisho cha NIDA na kuwataka watambue kuwa huduma muhimu zitapatikana tu kwa mtu mwenye kitambulisho cha nida na hivyo kuwasihi kukamilisha zoezi la nida na kupata usajili wa laini zao za simu.

  Zoezi la usajili wa laini za simu kwa kutumia alama za vidole linatarajiwa kukamilika disemba 31 mwaka huu.


  0 0

  Mhe. Innocent Bashungwa Waziri wa Viwanda na Biashara akiwa kwenye ziara ya kikazi mkoa Mwanza amekitembelea kwa mara ya pili kiwanda cha Mwatex (2001) LTD kilichobinafisiswa na Serikali kwa mwekezaji Amin Radhanin na chenye wafanyakazi 600.

  Kwenye ziara ya kwanza ya tarehe 30/09/2019 alitoa maelekezo kwa kiwanda kuhusu kuandaa mpango mkakati wa biashara wa kuendesha kiwanda lakini mpaka sasa huo mpango mkakati haujafika wizarani.

  Waziri baada ya kufika kiwandani hapo aliomba uongozi na menejiment nzima kutoka nje na mkutano ili kusikiliza kero na changamoto pia na maoni yao yatakayofanya kiwanda hicho kinafanye kazi kwa asilimia 100. 

  Amabapo kwa sasa kinafanya kazi asilimia 60 tofauti na matalajio ya serikali ya kiwanda kufanya kazi kwa asilimia 100 Waziri baada ya kusikiliza maona na kero za wafanyakazi ameagiza wizara kuunda kamati maalum ambayo itafika kiwandani kufanya uchambuzi wa uendeshaji wa kiwanda kwa kushirikiana na msimazi anaekiendesha kiwanda hicho na amewapa muda mpaka 01/01/2020 kamati hiyo iwe imeshamfikishia ripoti ya uchambuzi wa mwenendo wa kiwanda cha Mwatex Ripoti hiyo itaisaidia serikali kupata mwelekeo wa nini kifanyike ili kupata Mwatex iliyokuwepo enzi za Mwalimu Nyerere.

  Pia Waziri amesisitiza kuwa mkakati wa serikali ni kuona viwanda vyote vinafufuliwa na vinafanya kazi ili serikali iweze kutengeneza mnyororo wa thamani ya mazao yote hapa nchini.


  0 0

  Na.Catherine Sungura.Dodoma.

  Jumla ya sampuli 5106 zimefanyiwa uchunguzi katika maabara zikiwemo za masuala ya kijamii na kijinai katika mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati.

  Hayo yamesemwa na Meneja wa mamlaka hiyo kanda ya kati Musa Kuzumila wakati wa ziara ya maofisa habari wa wizara ya afya na taasisi zake wakati wa kutembelea mamlaka hiyo kujionea mafanikio yaliyofanywa katika kuboresha sekta ya afya nchini.

  Kazumila amesema kwamba tangu kuanzishwa kwa kanda hiyo miaka miwili na nusu sasa ,kanda yake imefanikiwa kupima sampuli hizo ambazo zimefanyiwa uchunguzi katika maabara na kuzitolea ushahidi mahakamani

  "Mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu inasimamia sheria na kudhibiti kemikali hivyo tumeweza kufanyia uchunguzi sampuli na hivyo kupunguzia wateja umbali na hivyo kusaidia wananchi kupata haki na kutoa ushahidi kwa wakati".Amesema Kazumila.

  Kwa upande wa vinasaba Kazumila amesema kati ya sampuli walizopokea jumla ya sampuli 36 zilizowasilishwa asilimia 90 zilikua zinaangalia uhalali wa baba wa mtoto.

  Hata hivyo amesema kwamba mamlaka hiyo imeweza kukagua maeneo yanayojihusisha na kemikali zipatazo 360 pamoj na kutoa vibali 139 za kuingiza na kusafirisha kemikali nchini kwa kanda ya kati.

  Kwa upande wa wajasiriamali wadogo wadogo mamlaka hiyo imewapatia mafunzo wajasiriamali 315 namna ya matumizi salama ya kemikali pamoja na kutoa elimu kwa wachenjuaji wa dhahabu wanaotumia kemikali aina ya sodium cyanide.

  Mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati inahudumia mikoa ya morogoro,iringa,dodoma,singida na tabora na ilianzishwa mwaka 2017.
  Meneja wa kanda ya kati ya mamlaka ya maabara ya mkemia mkuu wa serikali Musa Kazumila wakati akiongea na maofisa habari wa wizara na taasisi zake 

  0 0

   Baadhi ya abiria wakipakia mizigo katika boti za abiria katika Bandari ya Magarini wilayani Muleba mkoani Kagera.Bandari hiyo imeboreshwa kwa kujengwa kwa miundombinu yake ikiwemo majengo ya ofisi, vyoo na gati kwa ajili ya meli na boti kuegesha bandarini hapo.

   Baadhi ya abiria wakiingia ndani ya boti ya abiria kabla ya kuanza kwa safari kutoka Bandari ya Magarini kuelekea katika visiwa vingine vilivyomo katika Ziwa Victoria.

   Abiria wakiwa wamekaa ndani ya boti kwa ajili ya kuanza safari katika bandari ya Magarini.

   Mmoja wa wakazi wa Muleba akiwa katika bandari ya Magarini (aliyenyoosha vidole) akiwa amezungukwa na baadhi ya waandishi wa habari waliofika bandarini hapo kuangalia uboreshwaji wa miundombinu katka bandari hiyo.

   moja wa wananchi akielekea kupanda boti ya abiria katika bandari ya Magarini wilayani Muleba mkoani Kagera.
  Boti ya abiria ikiwa imeegesha ikisubiri kuanza kupakia abiria katika Bandari ya Magarini wilayani Muleba mkoani Kagera.  Na Said Mwishehe, Michuzi TV-Muleba


  WANANCHI wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera na hasa wanaoutumia usafiri wa meli na boti za abiria kufanya safari zao mbalimbali katika Visiwa vilivyomo ndani ya Ziwa Victoria wameipongeza Serikali Kuu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kwa hatua yake ya kuboresha miundombinu ya Bandari ya Magarini ambayo sasa imekamilika.


  Wakizungumza na Michuzi Globu ya Jamii pamoja na Michuzi TV, wananchi hao wamesema kuwa hakika Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Magufuli kupitia TPA umeonesha namna ambavyo umedhamiria kuboresha maisha ya watu kwa kuhakikisha huduma muhimu zinapewa kipaumebele na kwamba wao miundombinu ya bandari katika Ziwa Victoria ni muhimu kwani ndio njia rahisi ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine.


  Akizungumza leo kuhusu bandari ya Magarini, Mkazi wa eneo hilo Paul Stephen amesema kuwa wanathamini kazi inayofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari katika kuboresha miundombinu ya bandari hiyo ambayo kabla ya uboreshwaji wa miundombinu wananchi walikuwa wanapata huduma ya usafiri wa boti za abiria katika mazingira magumu.


  "Tunatoa shukrani kwa Serikali pamoja na Mamlaka ya Bandari kwa hatua hii iliyochukua ya kuboresha majengo , gati na ofisi za Bandari ya Magarini ambayo kwetu ni muhimu katika shughuli za kiuchumi.Tunaitegemea sana kwani ndio ambayo tunaitumia tunapotaka kufanya safari zetu za kila siku.Kwa uboreshaji wa miundombinu ambao umefanyika, tutaona manufaa yake na itakuwa chachu ya maendeleo kwetu,"amesema Stephen.


  Wakazi wengine wa eneo hilo wametoa ombi kuhusu kuangaliwa upya kwa ushuru ambapo walisema wanalipa Sh.600 wakati katika maeneo mengine bei ya ushuru kwa kila abiria ni Sh.200 au Sh.400.Hivyo ni matarajio yao Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari itasikia kilio chao kwa kushusha gharama za ushuru.


  Hata hivyo Meneja wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari katika Bandari za Ziwa Victoria Morric Mchindiuza amesema kuwa amesikia maombi ya wananchi hao kuhusu bei ya ushuru.Amesema kuwa katika bandari zote nchini gharama ya ushuru kwa kila abiria ni Sh.600 na kinachotokea kuna bandari bubu ambazo zenyewe zinatoza bei ya Sh.200 hadi Sh.400.


  "Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, tunao utaratibu ambao unatambulika kisheria kuhusu ushuru na tozo nyingine.Hili la ushuru wa abiria bandari zote nchini bei yake ni moja na hivyo kinachosemwa na wananchi ni ushauri ambao tumeuchukua na tutaufanyia kazi.Hata hivyo kama ambavyo tumekuwa tukielekeza kila siku bandari bubu zinakwenda mwishoni , hivyo bei ya ushuru itabaki ile inayotambuliwa na TPA,"amesema Mchindiuza wakati anafafanua kuhusu gharama za ushuru bandarini.


  Kuhusu bandari hiyo ya Magarini amesema kuwa kwa sasa ujenzi wa miundombinu umekamilika kwa asilimia kubwa na kilichobaki ni kuanza kutumika rasmi kwa majengo ya bandari hizo ingawa kwa upande wa gati imeanza kutumika.


  "Tumejipanga kuhakikisha tunaboresha miundombinu ya bandari zetu za Ziwa Victoria na ndio maana kila mahali ambapo tunakwenda utakuta aidha ujenzi umekamilika au unaendelea na mkakati wetu ni kuhakikisha usafiri wa meli unakuwa wa uhakika ili wananchi sasa waweze kusafiri kutoka eneo moja kwenda jingine,"amesema Meneja huyo.
  0 0

  Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu chake 

  MAMA Mzazi wa Samweli Suzana Senso akizungumza wakati wa uzinduzi huo
  Mkurungezi wa Fursa Bi Suma Mwaitenda kulia akimkabidhi kitabu hicho Samweli mara baada ya kufanya uzinduzi
  MAMA Mzazi wa Samweli Suzana Senso kushoto akimpatia nakala ya kitabu kilichoandikiwa na Mwanae Mtangazaji wa Kipindi cha Njia Panda cha Clouds FM Radio Dkt Isaac Maro wakati wa uzinduzi huo 
  Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake na mdogo wake Alan Michael Gimeno 

  Mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) katikati akiwa kwenye picha mara baada ya uzinduzi wa kitabu chake

  Jumamosi tarehe 7/12/2019 ilikuwa siku ya pekee wa mtoto Samwel Michael Gimeno (miaka 8) ambae alibahatika kuzindua kitabu chake cha kwanza ndani ya fursa ya Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Julius Nyerere International Conference Center 

  Kitabu cha BIBLIA YANGU kilizinduliwa na Mkurungezi wa Fursa Bi Suma Mwaitenda 

  Samwel amekuwa mtoto wa pekee kwenye familia ambae Mungu Ameweka kipaji cha kuandika na kuchora na Sisi kama wazazi wake tumeamua kumsaidia ili kuiishi ndoto yake maneno hayo yamesema na mama mzazi wa Bi Suzana Senso

  Kitabu cha kwanza cha Samwel kitakwenda Kuwa kinatolewa kwa watoto Yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu ikiwa sehemu ya samwel kurudisha kwa watoto wezake wanaoishi kwenye mazingira magumu ambao ni mara chache sana kupata kitabu kinzuri na chenye hadithi za kwenye Biblia kutokana na mazingira wanayoishi maneno hayo yamesemwa na baba wa Samwel Bw Michael Samwel Gimeno 

  KAMPENI KALAMU YANGU
  Ni maneno yatakayo kwenda kutumika kwenye kampeni samwel ambayo itakuwa nikutembelee vituo vya watoto yatima na watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na kuwagawia vitabu ili nao waweze kusoma sio tu kusoma kitabu tu ila pia kusoma kitabu kilichoandikwa na mtoto mwezao 

  Kampuni hii inaanza mwezi huu wa 12 hadi siku ya wapendanao tarehe 14/2/2020 ambapo samwel atakwenda kula na watoto wanaoishi kwenye kituo cha watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu ambacho tutakitaja siku zijazo na pia kuwagaia vitabu ya BIBLIA YANGU 

  Gharama ya kitabu itakuwa shilingi elfu 20,000 kuanzia 15/2/2020 baada ya kampuni ya KARAMU YANGU ukisha tarehe 14/2/2020

  Mama Samwel alisema Kwa sasa tunatamani kupata watu wa ku support kutoa nakala ya vitabu ambavyo tunatajia kuvigawa kwenye vituo vya watoto yatima Kwani hii kampeni haina mfadhili wa kufanya Ila ni wazazi tu ndio tunaifanya na tunatamani kuwafikia watoto wengi sana 
  Kwa yeyote atakae wiwa kuungana nasi kwenye Hii kampuni anaweza ku wasiliana Kupitia namba 0736 372138 

  Tukiwa kama wazazi wa Samwel tunapenda kuwashukuru Joel Kiiya ambae ni mentor wa Samwel, Bi Ezabel Simuyu ambae ndie ame design kitabu, photography wake Muki, Emanuel, Mkurungezi wa Fursa na wale waliotumia muda wao kufanikisha kitabu cha “BIBLIA YANGU” hadi kutoka.


  MUNGU AWABARIKI

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza na kuzindua kampeni maalum ambayo inayojulikana kama LIPA ADA kwa Airtel Money itakayotoa  suluhisho kwa  wateja wake kuweza kufanya malipo yoyote ya karo za shule ambapo kwa sasa wateja wataweza kulipa karo kwa kutumia akaunti zao za Airtel Money wakiwa popote katika  kipindi hiki cha msimu wa sikukuu na kuendelea.
  Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kutangaza kampeni hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money Isack Nchunda alisema kuwa LIPA ADA kwa kutumia Airtel Money itakuwa ni suluhisho kwa wazazi wengi ambao wamekuwa wakipoteza muda mwingi wa kwenda kupanga foleni benki ili kulipia watoto wao karo na vile vile itaendela kutoa hamasa kwa wateja wa Airtel kuendelea kutumia Airtel Money kulipia malipo mbali mbali ya bidhaa na huduma.
  ‘Kama mnavyojua, hiki ni kipindi cha wazazi na familia kuwa katika mapumziko, lakini pia muda huu wazazi huutumia kulipia karo za shule za watoto wao. Natoa wito kwa Watanzania kuendelea kutumia Airtel Money kwa malipo yao kwani ni njia rahisi, haraka na nafuu kwa malipo wakiwa popote wanaweza kulipa sio lazima kwenda bank na kupanga foleni, Nchunda alisema.
  Nchunda alisema kuwa Airtel imeamua kuja na kampeni ya LIPA ADA kwa Airtel Money kama njia mojawapo ya kutoa suluhisho ya kifedha kwa Watanzania. ‘Kama mnavyojua, kulingana na utafiti wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wa hivi karibuni kuonyesha kuwa zaidi ya Watanzania milioni 22.9 wanatumia huduma za kifedha kwa kutumia simu zao huku miamala yenye dhamani ya zaidi ya Trilioni 8 ikifanyika mpaka kufikia Juni 2019. Kwa miaka ya hivi karibuni, huduma za kifedha kwa simu za mkononi imebadilika kutoka huduma ya kawaida kama vile kununua muda wa maongezi mpaka kuwa moja ya huduma muhimu inayowezesha ukuaji sekta na  mzunguko wa fedha kila mahali.
  Jinsi ya kulipia Ada Kwa Airtel Money:
  • Piga *150*60# Ili kufikia Kwenye Menyu ya Airtel Money
  • Chagua 5: Lipia Bili
  • Chagua 4: Weka namba ya kampuni (Namba ya Malipo ya Shule)
  • Ingiza Kiasi cha pesa
  • Ingiza Namba ya Kumbukumbu (Jina la mwanafunzi na Kidato / Namba ya kitambulisho cha mwanafunzi )
  • Ingiza Namba ya siri
  Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema kuwa Airtel inajivunia kuwa kampuni ya simu za mkononi ambayo sasa inakuza kwa kasi mtandao wa huduma za kifedha hapa nchini.
  “Airtel tumejipanga na kujikita katika mipango yetu ya kuendelea kupanua wingo wa huduma zetu, Airtel kwa sasa tuna maduka ya Airtel Money branches Zaidi ya 1000 nchi nzima ikiwa ni moaja kati ya mpango yetu ya kuleta suluhisho za kifedha pamoja na kusambaza huduma na bidhaa zetu karibu na wateja. Dhamira yetu ni kuendelea kujenga mtandao imara na unaotegemewa’. Alisema Singano huku akiongeza kuwa huduma na bidhaa za Airtel kama vile kurundisha muamala uliokosewa, kubadilisha PIN, kusajili laini za simu kwa kutumia alama ya vidole zinapatikana kwenye maduka yote ya Airtel Money branches.
   Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda  akizungumza wakati wa kuzindua kampeni maalum inayojulikana kama LIPA ADA kwa Airtel Money itakayotoa suluhisho  kwa wateja wa Airtel Money kuweza kufanya malipo yoyote ya karo za shule  kwa kutumia akaunti zao za Aitel Money wakiwa popote katika kipindi hiki cha msimu wa Sikukuu na kuendelea Kushoto ni Meneja wa Airtel Jackson Mmbando

   
  Meneja wa Airtel Jackson Mmbando akifafanua jambo wakati wa kuzindua kampeni maalum inayojulikana kama LIPA ADA kwa Airtel Money itakayowawezesha  kwa wateja Airtel kuweza kufanya malipo yoyote ya karo za shule kupitia akaunti zao za Aitel Money wakiwa popote wakati msimu huu wa Sikukuu na kuendelea, hafla ya uzinduzi ilifanyika ofisi kuu ya Airtel  jijini Dar es Salaam jana.Katikati ni Mkurugenzi wa Airtel Money, Isack Nchunda na kulia ni Mkuu wa Kitengo cha lipa Ada kwa Airtel Money. Emmanuel Mwaisoloka
   

  0 0

  Msheheshaji  akimkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Bwana Hassan Khatib Hassan katika halfa ya kumkabidhi zawadi ya gari mshindi wa TIGO Chemsha Bongo #MshindiTigoChemshaBongo

  Tunashukuru jinsi kampuni ya mawasiliano ya TIGO inavyoleta hamasa kwa vijana kupitia miradi mbalimbali ya kuwainua. Leo tunakabidhi gari kwa mshindi wa TIGO Chemsha Bongo toka Zanzibar Bw. Shaban Hamis” 
  Mh. Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan
  #MshindiTigoChemshaBongo

  “Tunampongeza mshindi wa Tigo Chemsha Bongo Bw. Shaban Hamis aliejishindia gari aina Renault Kwid kutoka Tigo kampuni ambayo tunashirikiana nayo kwenye mambo mengi ya kimaendeleo”
  Aljazeera - Mwakilishi wa Jimbo Raha Leo #MshindiTigoChemshaBongo

  PICHA ADIMU ya mshindi wa TIGO Chemsha Bongo Bw. Shaban Khamis akiwa na “mke mdogo” katika gari yake mpya aina ya Renault KWID yenye thamani ya Tsh 23,000,000 (Zero Km)‬
  #MshindiTigoChemshaBongo 

  Mh. Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Hassan Khatib Hassan akikabidhi nyaraka za usajili wa gari aina ya Renault KWID yenye 0 Km (yenye thamani ya 23,000,000) kwa mshindi wa TIGO Chemsha Bongo Bw. Shaban Khamis akiwa na “mke mdogo” wake. 
  #MshindiTigoChemshaBongo

  NJOO KWEREKWE USHUHUDIE sasa hivi gari la mshindi wa TIGO Chemsha Bongo akiwepo na Mshindi mwenyewe Bw. Shaban Khamis #MshindiTigoChemshaBongo  GARI IMEFIKA salama nyumbani kwa Bw. Shabani Khamis wakapata na picha ya ukumbusho na familia. Tukumbuke hii ni Renault Kwid yenye thamani ya Tsh 23,000,000 (Zero Km)

  #MshindiTigoChemshaBongo

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa  TULab kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Lorah Madete akizungumza kwa niaba ya Wizara ya Fedha na Mipango wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Sera ya Jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dr. Paul Quarles Van Ufford akitoa salamu za UNICEF wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mtathimini kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Mr. Hong Vu akiendesha chemsha bongo wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi wakifurahia jambo wakati wa chemsha bongo kwenye kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Kutoka kushoto ni Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu, Mwenyekiti wa  TULab kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Lorah Madete pamoja na Mkuu wa Sera ya Jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dr. Paul Quarles Van Ufford wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida (katikati) akitoa maelezo mafupi kuhusu ESRF kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu (wa pili kulia) alipofika ofisini kwa mkurugenzi huyo kusaini kitabu cha wageni wakati wa kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Profesa Fortunata Makene(wa kwanza kushoto), Mkuu wa Sera ya Jamii kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto (UNICEF) nchini, Dr. Paul Quarles Van Ufford (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa  TULab kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dr. Lorah Madete (wa kwanza kulia).
  Baadhi ya wadau kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia, Taasisi za Elimu, Wahisani wa Maendeleo na Sekta binafsi walioshiriki kongamano la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya wadau wakishiriki kuchangia maoni wakati wa kongamano la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
  Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia, Taasisi za Elimu, Wahisani wa Maendeleo na Sekta binafsi walioshiriki kongamano la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana la kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
   
  Na Mwandishi Wetu
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk John Jingu amewataka watafiti wa programu ya Utafiti itakayoangalia huduma na ubunifu kwa watoto na vijana katika miji nchini Tanzania kutoa suluhisho la kudumu kuhusu mahitaji na usalama wa watoto na vijana ili kuwa na taifa lenye watoto wenye kujitambua.
   
  Alisema ingawa anatambua kwamba tafiti zikifika mwisho wataitwa kuelezwa matokeo lakini kutokana na haja ya kutafuta suluhu ya changamoto zilizopo kwa sasa ni vyema watafiti wakapata muda wa kueleza maendeleo ya tafiti zao na hasa matokeo ya awali kabla ya kufika mwisho.
   
  Alisema hayo katika kongamano la wadau la kujadili programu ya utafiti kuhusu vijana lililofanyika juzi kujadili namna bora ya kutatua changamoto zinazowakumba watoto na vijana katika miji. Programu hiyo inaandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) na Wizara ya Fedha na Mipango chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab).
   
  Kongamano hilo lilihudhuriwa na wadau takribani 40 kutoka Serikalini, Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Asasi za Kiraia, Taasisi za Elimu, Wahisani wa Maendeleo na Sekta binafsi.
  Alisema hali hiyo itasaidia Serikali kuchukua hatua mapema zaidi za kukabiliana na changamoto za watoto na hasa suala la malezi.
   
  Alisema kwa sasa kumekuwa na changamoto nyingi za malezi na hivyo kusababisha uwapo wa watoto wengi kwenye mazingira magumu na pia mitaani.
   
  Alisema utafiti unaokusudiwa ni utafiti wenye maana kubwa kwa kuwa unaangalia mazingira ya leo kwa manufaa ya taifa la kesho na kuondoa viashiria vya hatari katika malezi na hatima ya watoto wa Tanzania hasa wale wanaoishi mijini.
   
  Alisema watoto na vijana wanaoishi mijini wanakabiliwa na changamoto nyingi na ni wajibu wa jamii kuhakikisha kwamba changamoto hizo zinaondolewa kwa kuwepo kwa mbinu bora za kukabiliana na changamoto hizo, mbinu zenye manufaa na zinazowezekana.
   
  Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk Tausi Kida, akifafanua zaidi kuhusu warsha na programu ya tafiti inayoandaliwa na ESRF kwa kushirikiana na UNICEF alisema wanatengeneza programu hiyo kwa ajili ya kutanzua shida zinazowapata watoto na vijana wanaoishi katika miji.
   
  Alisema warsha hiyo iliyojumuisha watafiti na wadau kadha wa masuala ya utafiti imelenga kukusanya maoni kutoka kwa wadau ili kuweza kutengeneza programu mpya inayogusa masuala ya watoto na vijana katika miji yetu.
   
  Dk Tausi Kida, akifafanua zaidi kuhusu kongamano hilo, alisema kwamba utafiti huo utafanywa chini ya Maabara ya Ukuaji wa Miji Tanzania (TULab) na kusema  mipango miji ni suala muhimu kwa nchi ya Tanzania hasa wakati huu inapoelekea katika uchumi wa viwanda.
   
  Alisema wakati Tanzania inatarajia kuwa na watu milioni 45 wanaoishi katika miji ifikapo mwaka 2030, ikiwa ni nchi ya sita kwa kasi ya ongezeko la idadi ya watu Duniani ifikapo mwaka 2050 na hivyo ipo haja ya kuwa na sera madhubuti inayohusu ulinzi kwa watoto na vijana wanaoishi mijini.
   
  Alisema kutokana na serikali kutilia umuhimu wa masuala ya ukuaji wa miji katika Mpango wa Pili Miaka 5 wa Maendeleo  2016/17 – 2020/21 (FYDP II) kulianzishwa  TULlab mwaka 2017 ambapo sekretarieti yake ni ESRF wakati mwenyekiti ni Wizara ya Fedha na Mipango.
   
  Kazi ya TULab ni kuisaidia serikali  katika masuala ya ukuaji wa miji Tanzania. Kwa kuzingatia  tayari TULab imefanya tafiti na kuandaa Mpango Kazi kuelekea Maendeleo ya Miji.

  0 0


  Charles James, Michuzi TV

  MMOJA wa abiria waliokua wakishuka kwenye ndege katika uwanja wa kimataifa wa John Lennon, Merseyside January 1, 2018 alikua ni Virgil Van Djik.

  Beki huyu wa Southampton alikua akielekea kukamilisha usajili wake wa kujiunga na wababe Liverpool katika uhamisho ambao ulivunja rekodi ya mauzo kwa Klabu zote mbili.

  Ni usajili ambao pia ulimfanya Van Djik kuwa beki ghali duniani na kuingia katika rekodi za Dunia.

  Aliwindwa na Barcelona, Manchester zote mbili na Chelsea. Yeye mwenyewe alipaona Liverpool kama sehemu bora zaidi kwa kipaji chake na familia yake.

  Siku nne tu baada ya kutambulishwa na kukabidhiwa jezi ya dhahabu no4 alicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Everton na kufunga goli la pili na la ushindi.

  Toka hapo, Virgil amekua bora kwetu, ametushika sisi mashabiki, benchi la ufundi mpaka wachezaji wenzake. 

  Na Sasa anatajwa kama mchezaji bora kwenye Ligi Kuu ya England huku akiwekwa katika daraja la juu la mabeki bora duniani.

  Amechukua tuzo ya Mchezaji bora wa Ulaya lakini pia akishika nafasi ya pili nyuma ya Lionel Messi kwenye tuzo ya mchezaji bora wa Dunia.

  Sikudhani kama kuna siku mtu mmoja angekuja kumaliza tatizo letu la ulinzi.

  Nilifahamu fika ubora wa Van Djik lakini bado hakunifanya niamini ya kwamba tatizo sugu la ulinzi tulilokua nalo litakwisha baada ya ujio wake.

  Wengi walibeza ubora wake, wengine wakaponda kiwango cha fedha tulicholipa kumnasa. 

  Hivi unawezaje kumsajili kwa Pauni Milioni 75 beki asiye na rekodi ya mataji tena anaecheza timu kama Soton? Tulitukanwa sana na wapinzani.

  Mkurugenzi wa ufundi, Michael Edward na Jurgen Klopp ndio waliojua jinsi gani Van ni hodari linapokuja suala la ulinzi.

  Mwanzoni msimu ulivyokua ukianza alikua akipangwa na Joe Gomez. Gomez aliekua akionekana dhaifu akabadilika na kuwa jemedari hodari wa vita.

  Wengine wakamuita Joe kuwa ni John Terry mpya.. Akachukua hadi namba timu ya Taifa. Tu kwa sababu anacheza pacha na Van.

  Dejan Lovren haonekani akifanya makosa siku hizi kwa sababu anacheza na Le Commandment Field Marshall.

  Joel Matip takwimu zake za ubora ziliongezeka baada ya kuanza kupangwa kama pacha wa Van baada ya Dejan na Joe kuumia.

  Wote hawa wamebadilika kwa sababu ya mtu mmoja. Mabeki wa pembeni Andy Robertson na Anord Trent huwaambii kitu kuhusu mbabe huyu wa kati.

  Amewafanya kujiamini sana. Kama hujui Robertson na Trent Anord waliweka rekodi ya kuwa mabeki wanaotoa assist nyingi barani Ulaya msimu uliopita.

  Ubabe wa Van Djik umemfanya kila mmoja ndani yetu ajiamini..Golini Allison Becker hana presha, mabeki na viungo wote wanajua nyuma kuna kamanda yupo.

  Hata akina Salah na Mane wakifunga sasa wana uhakika magoli hayarudi maana kamanda yupo.

  Unataka kuujua Ubabe wa Van Djik? Kawaulize Spurs watakusimulia vizuri.

  Msimu uliopita game ya Liverpool ugenini White Hart Lane, Spurs walifanya shambulizi la kushtukiza dakika ya 84 langoni mwa Liverpool, Heung Son na Sissoko walikua wakija kwa kasi wakiwa wamebaki na Van Djik. 

  Yaani wawili dhidi ya mmoja na bado wakashindwa kufunga. Huyu jamaa anakaba watu wawili peke yake.

  Kumbuka chini yake msimu uliopita Liverpool walifungwa mchezo mmoja huku wakiwa timu iliyoruhusu magoli machache kwenye Ligi na kipa wao Allison Becker akiongoza kwa cleensheet akiwa nazo 20.

  Msimu huu mpaka sasa Liverpool ipo kileleni mwa Ligi ikiwa haijafungwa mchezo hata mmoja.

  Ndio namba nne wetu, mtazameni akikaba tunamtazama akifunga, anapiga pasi na anaongoza wenzake. Virgil Van Djik! Virgil Van Djik!

  UBINGWA WA LIVERPOOL

  Ebana huamini kama Liverpool ndio mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya England? Ugumu unakuja wapi mpaka ushindwe kuamini?

  Ukitazama namna ambavyo tunacheza utaona kabisa timu inahitaji kitu. Mechi zilizobaki zinatubeba kulinganisha na Manchester City ambao tunachuana nao.

  Tayari tumecheza michezo yote migumu kulinganisha na wapinzani wetu. Mpaka sasa tunapokaribia kumaliza mzunguko wa kwanza vigogo wote tumeshawamaliza.

  Ukiangalia jinsi ambavyo tunapata ushindi utakubaliana na Mimi kwamba ubingwa ni wa kwetu.

  Alex Ferguson alikua alisema ubingwa wa England unapatikana Machi na April..Akiwa na msemo wake wa Tricky Bum Time, lakini sidhani kama Klopp ataisubiri hiyo presha, mpaka kufikia mwishoni mwa Januari atakua ameshajua mbivu na mbichi.

  Tazama namna tunavyopata matokeo katika njia ngumu. Niliwaambia Njia ya mafanikio ya Liverpool ni ngumu siku zote.

  Hebu kumbukeni sare ya kibishi pale Old Trafford kwa United, ushindi dhidi ya Newcastle, Leceister, Spurs na hata Sheffield United utaona kabisa Liverpool ya msimu huu inacheza kibingwa sana.

  FALSAFA YA PEDIGREE

  Kuna kitu kinamea sana kwa sasa pale Anfield. Kinaitwa Pedigree. Klopp ni wazi ameamua kuacha alama isiyofutika kwetu.

  Na kama akifanikiwa kubeba taji la Ligi kuu basi hapana shaka atajengewa mnara wenye sura yake nje ya dimba letu.

  Oke. Pedigree ni nini? Hii ni ile hali ya kuwa na vitu vyenye muendelezo wa muda mrefu. Nitakupa mifano yake.

  Ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Spurs msimu huu ni muendelezo wa ubabe wetu mbele yao hasa katika uwanja wa Anfield.

  Ni lini umewahi kuiona Liverpool imara katika dimba lake la nyumbani kama hii ya Klopp? Jamaa hataki kabisa mchezo na ‘home’ anakubutua bila masihara.

  Liverpool ilikua na tatizo la kushinda michezo mikubwa na kupoteza dhidi ya zile ‘timu ndogo’. 

  Sasa toka tufungwe na Swansea msimu wa mwaka juzi hatujapoteza kwenye Ligi dhidi ya hizo mnazoziita timu ndogo. Hii nayo ni Pedigree. 

  Hata ukiangalia msimu uliopita ni Leceister City na West Ham pekee ambao angalau wameambulia sare. Wengine wote tumebutua.

  Pedigree nyingine ni hii ya kusajili wachezaji Kwa fedha nyingi. Ni wazi sisi ni miongoni mwa timu zinazoogopwa kwenye soko la usajili kwa sasa.

  Tuliwapiku Man city na Chelsea kuinasa saini ya Van Djik, tukaigaraza Man United kwa Fabinho, tukaipiga bao tena Man City kwa Naby Keita.

  Real Madrid waliangaika kumnasa Allison Becker lakini mwenyewe akachagua kuja kwetu. Hii Pedigree haikuwepo mwanzoni. 

  Jurgen Klopp kayafanya maisha yawe mepesi kwetu sasa.

  0683015145


  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

   Serikali imesema kuwa Soko la ajira rasmi  nchini ni dogo sana na  hivyo halikidhi mahitaji ya wahudumu wote kwa hali hiyo wahitimu hao wanatakiwa kukabiliana na changamoto ya Soko hilo kwa kuelekeza mawazo yao kwenye kujiajiri badala ya kuajiriwa.

  Hayo ameyasema Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Fedha na Mipango  Amina Shaban wakati akimwakilisha Waziri wa Fedha na Mipango katika mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa Kampasi ya Dar es Salaam na Mtwara yaliyofanyika katika Viwanja vya Kampasi jijini Dar es Salaam.

  Amesema kuwa kwa wale wahitimu wenye ajira msingi mkuu wa mafanikio ni kufanya kazi kwa kuzingatia sera,Sheria,Taratibu na Kanunu ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vishawishi au vitendo vya rushwa na ubadhirifu kwa kuwa vina madhara makubwa ya maisha ya mtu Mmoja moja na uchumi wa Taifa letu kwa ujumla.

  Shaban amesema elimu inayotolewa na TIA imejikita kwenye fani za Uhasibu ikiwemo Uhasibu wa Fedha za Umma, Ununuzi na Ugavi,Usimamizi  wa Biashara, Uongozi wa Rasilmali Watu pamoja na Masoko  hivyo fani hiyo ni nguzo muhimu katika kuendesha Uchumi wa Taifa hususani katika kusimamia mapato na matumizi ya Fedha za Umma.

  Naibu Katibu Mkuu huyo amesema sera yetu kwa sasa ni uchumi wa viwanda hivyo umahiri wa  wataalam wanaozalishwa  unatakiwa kuonekana ili kufanikisha azima ya serikali ya Tanzania ya Viwanda.

  Shaban amekazia katika kukabiliana na changamoto za Usimamizi wa Mapato na matumizi ya Fedha za Umma,mahitaji ya Soko ,Ushindani na Utandawazi hamna budi Taasisi ya Uhasibu nchini (TIA) Kuendesha Shughuli  kwa kutumia Teknolojia ya Kisasa ya kupeana na kubadilishana taarifa kwani watalaam wanaohitajika ni wenye weledi,maarifa na umahiri wa kutatua za changamoto na si kuongeza changamoto kwa Wananchi katika kupata huduma.

  Amesema kuwa TIA izingatie  umakini wa suala la umahiri katika mitaala ili kuweza kuwa na wataalam wenye uwezo wa kulifikisha Taifa kwenye uchumi wa Kipato cha kati kabla ya 2025.
  Mwenyikiti wa Bodi ya Wizara ya Fedha na Mipango Wakili Said Chiguma amesema kuwa waajiri wa sekta ya Umma na binafsi wamekuwa wakiona mafanikio kwa wahitimu wa TIA kuwa na sifa zilizotukuka katika kufanya kazi licha ya kuwapo kwa Vyuo vingi nchini na kufanya Chuo hicho kuendelea kuongeza idadi ya udahili kwa wanafunzi kusoma kwa  kila mwaka.
  Amesema Taasisi ina wanafunzi zaidi ya  19,000 katika Kampasi Sita za Kimkakati.

  Nae Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Luciana Hembe amesema kuwa wahitimu katika Chuo hicho wameweza kjfundishwa ujasiriamali ili kuweza kujiajiri katika kukabiliana na changamoto ya ajira nchini.
  Amesema Chuo kumekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakiksha wahitimu wanajiajiri katika maeneo Mbalimbali ya kuweza kukidhi mahitaji yao pamoja Taifa kunufaika na maarifa yao ya kujiajiri.

  Aidha amesema kuwa Baadhi wahitimu katika Taasisi hiyo wa miaka iliyopita wameweza kuanzisha Kampuni mbalimbali ambazo ziko katika Ushindani wa kibiashara na Kampuni zingine.
  Amesema wahitimu wa mwaka 2019 nao watumie ujuzi na maarifa yao katika kufungua milango ya ajira ya kujiajiri ili wasitumie muda mwingi wa kusubiri ajira katika sekta ya Umma na binafsi.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Shaban akizungumza katika Mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika katika Kampasi Dar es Salaam.
   Picha ya Pamoja na baadhi Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).
   Baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakifatilia Hutuba ya Mgeni Rasmi katika Mahafali ya 17 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika Viwanja vya Kampasi Kuu ya Jijini Dar es Salaam.
   baadhi ya Wahitimu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wakiwa katika mahafali ya 17 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika Viwanja vya Taasisi jijini Dar es Salaam.
   Mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Wizara ya Fedha na Mipango Thabit Dokodoko akitoa shukurani kwa Mgeni Rasmi katika mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliyofanyika Viwanja Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
   Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Amina Shaban akiwa katika picha ya pamoja na Meza Kuu mara baada ya kuhitimisha mahafali ya 17 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) yaliofanyika katika Kampasi Kuu ya Dar es Salaam.
   Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Luciana Hembe akitoa akizungumza na waandishi habari mara baada ya kuhitimishawa kwa Mahafali ya 17 ya Taasisi hiyo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
  Mwenyikiti wa Bodi ya Ushauri wa Wizara ya Fedha na Mipango Wakili Said Chiguma akitoa maelezo kuhusiana na uendeshaji wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika Mahafali ya 17 yaliyofanyika katika Viwanja vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha 

  Shirika la Hifadhi za Taifa{TANAPA} limezindua kampeni maalumu ijulikanyo kwe jina la ‘’Talii na TANAPA msimu huu wa sikukuu ya X mass na Mwaka mpya’’ kwa kushirikisha wasanii maarufu,warembo ,watangazaji maarufu na watu maarufu lengo ni kutaka kuhamashisha watanzania kutembele hifadhi za Taifa badala ya kwenda kutalii nje ya nchi katika kipindi hicho.

  Hayo yalisemwa na Kaimu Kamishina wa Uhifadhi wa TANAPA,Witness Shoo mbele ya waandishi wa habari kwa kushirikisha viongozi mbalimba wa uhifadhi,wasanii na watangazaji tukio lililofanyika katika Makao Makuu ya Shirika hilo Jijini Arusha..

  Shoo alisema kuwa lengo la TANAPA ni kutaka kila mtanzania kuwa mzalendo na nchini yake kwa kutembelea vivutio vilivyokuwa katika hifadhi 22 hapa nchini kwa kuvitembelea na kuwa balozi wakubwa wa kuvitangaza.

  Alisema kundi la kwanza la wasani,watangazaji na watu maarufu litaanza kufanya kampeni hiyo desemba 20 mwaka huu katika hifadhi sita ikiwemo Ruaha,Katavi,Mkomazi,Rubondo,Mikumi na hifadhi ya Gombe iliyopo Mkoani Kigoma.

  Kamishina huyo alisema katika Hifadhi ya Ruaha msanii Idrisa Sultan atakwenda kutalii katika mbuga hiyo na kuitangaza ndani na nje ya nchi katika mitandao ya kijamii kwani anawafuasi wengi katika mitandao ya kijamii hivyo anawajibu wa kutoa ujumbe kwa watanzania kuacha kukimbilia nje ya nchi kutalii badala yake watembelee hifadhi Taifa.

  Alisema msanii Mrisho Mpoto atakuwa katika Hifadhi ya Katavi,mrembo wa mwaka Nancy Sumary atakuwa katika hifadhi ya Mkomazi,mtangazaji kijana aliyejipatia umaarufu hapa nchini,Milard Ayo na Miss wa mwaka 2018 Elizaberth Makune watakuwa na jukumu la kuwakumbusha watanzania kutembelea hifadhi ya Robondo.

  Wengine ni pamoja na wasanii wa muziki wa Bongo flava Lulu Abas maarufu kwa jina la Lulu Diva atakuwa katika Hifadhi ya Mikumi na msani aliyetambulika kwa jina moja la Rubby atakuwa katika hifadhi ya Gombe.

  Naye Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kuwataka watanzania kuwa na tabia ya kutembelea mbuga za wanyama katika vipindi vyote vya sikukuu ya X Mass na Mwaka mpya na sikukuu nyingine kwa kutumia kiasi kidogo cha fedha na pia kuvitangaza vivutio hivyo kwa faida ya nchi.

  Shelutete alisema kuwa wasanii wa fani mbalimbali,watu maarufu na watangazaji watashirikishwa katika kampeni hiyo iliyolenga kumtaka mtanzania kupenda cha nchi yake na kuacha kujali vya nje .

  Naye Msanii Idrisa Sultan alisema kuwa katika maisha yake hajawahi kufika katika hifadhi ya Ruaha hivyo kwa fursa aliyopewa atahakikisha anaitangaza hifadhi hiyo kwa kadri awezavyo lengo ni kutaka watanzania kuwa wazalendo na kupenda cha kwao na kuacha ulimbukeni wa kikumbilia nje ya nchi kama Dubai na kungine kwa kutumia mamilionin ya pesa bila ya sababu za msingi.
  Kaimu Kamishina wa Uhifadhi wa TANAPA,Witness Shoo akizindua rasmi  kampeni ya Talii na TANAPA , ambayo mabalozi wake ni baadhi ya wasanii pamoja na watangazaji ndani ya ukumbi Wa ofisi za makao makuu ya shirika hilo.
  Mabalozi  Wa kampeni hiyo ambao ni wasanii Wa muziki ,vichekesho na watangazaji pamoja na baadhi ya wafanyakazi Wa TANAPA wakiwa katika   picha ya pamoja


  0 0

   
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Anne Makinda amesema kuwa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umejielekeza katika kumhudumia mtanzania wa kila aina kulingana na uwezo wake na sio kufanya biashara kama inavyoelezwa na baadhi ya watu.

  Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Vifurushi vya Bima ya Afya Bi. Makinda amesema kuwa NHIF kuanzisha vifurushi kwamba ni kufanya biashara si kweli bali ni kuhakikisha watanzania ambao nchi yao ipo huru na wana amani wapate pia amani ya huduma ya afya.

  “Mfuko huu ulianzishwa na Serikali, sio mfuko wa kufanya biashara, tunachukua hela za wanachama, ili wakatibiwe , unalipa 192,000 kwa mwaka halafu unaenda hospitali mara nne mara tano kwa mwaka kwa gharama zaidi ya pesa uliyowekeza, lengo letu ni kumhudumia mtanzania”-Bi Anne Makinda.

  “Ukitaka kwenda hospitali leo, kumuona daktari ni shughuli, hapo bado matibabu, sasa bima ya afya ni hela unayoweka ukiwa na uwezo, ukienda hospitalini utatibiwa kwa mamilioni hata usiowahi kuyatoa wewe, utatibiwa tu na hela yako ndogo uliyokata nayo wewe kwa mwaka mzima”-Alisema Bi. Anne Makinda

  Aidha Bi. Anne  Makinda amewataka watanzania kujiunga na Bima ya Afya hasa baada Mfuko huo kuja na vifurushi vya bima ya afya vinavyotoa wigo kwa watu wengi kujiunga kulingana na uwezo wake ili kusaidia Katika huduma za matibabu ambazo zimezidi kuwa kubwa kwa sasa.

  Akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Wilaya ya Chemba Bw. Simon Odunga ameupongeza mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kuja na mpango wa vifurushi kwani umejumuisha makundi tofauti katika jamii na kuwawezesha kila mmoja kujipimia kwa uwezo wake na hivyo kuwa na uhakika wa huduma za afya.

  Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Bw. Bernard Konga amesema katika wiki tatu tangu waanzishe mpango huu wa Vifurushi vya Bima ya Afya Idadi kubwa ya watanzania wamejitokeza kujiunga.

  “Ndani ya wiki tat utu tangu tuzindue vifurushi hivi idadi ya watanzania wanaojiunga na mfuko imekuwa kubwa ambapo mpaka sasa tumeshaunga watanzania zaidi ya elfu ishirini na idadi hii imeendelea kuongezeka siku hadi siku”-Alisema Bw. Konga

  Muwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Edward Mbanga amewataka watumishi wa NHIF kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kujiunga na vifurushi hivyo na kuachana na kelele zapembeni.

  Wawakilishi wa Vyama via BodaBoda na Machinga wamepongeza mango huo na kuahidi kuhamasisha wanachama wao kujiunga na mango huo kwani ni mkombozi kwa afya ya watanzania wote
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Anne Makinda akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya, leo Mkoani Dodoma
  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya Bw. Bernard Konga akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya leo Mkoani Dodoma, ambapo amesema katika wiki tatu tangu waanzishe mpango huu wa Vifurushi vya Bima ya Afya Idadi kubwa ya watanzania wamejitokeza kujiunga. 
  Mkuu wa Wilaya ya Chemba Bw. Simon Odunga akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya, ambapo aliwasisitiza watanzania kujitokeza kujiunga na vifurushi hivyo
  Muwakilishi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Edward Mbanga akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni ya uhamasishaji wa wananchi kujiunga na vifurushi vya Bima ya Afya, leo Mkoani Dodoma ambapo amewataka watumishi wa NHIF kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kujiunga na vifurushi hivyo na kuachana na kelele zapembeni.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Anne Makinda akiwapatia kadi za Bima ya Afya baadhi ya wakazi wa Dodoma waliojiunga na vifurushi vya bima ya afya leo Mkoani Dodoma

  0 0

    Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akifurahi pamoja na baadhi ya wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Kampuni  G4S Cash Solutions Tanzania, Hassan Nuru na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya G4S Secure Solutions Tanzania, Barry Hogg.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Abdallah Mwaduga katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Ofisa katika kitengo cha wateja binafsi wa NBC, Rehema Chonde.  
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kushoto), akisalimia na Mkurugenzi wa Kampuni ya Enterprises Business Department, Tony Wu huku Ofisa Fedha Mkuu wa Kampuni ya Huawei Technologies Tanzania, Mao Jinbao akiangalia katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

   Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NBC, Dk. Kassim Hussein (kulia), akisalimiana na baadhi ya wateja waliohudhuria  hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

   Mkurugenzi wa Wateja wa Makampuni wa Benki ya NBC, Linley Kapya (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi wa Fedha wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Abdallah Mwaduga katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Ofisa katika kitengo cha wateja binafsi wa NBC, Rehema Chonde.

   Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NBC, Dk. Kassim Hussein (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Anga Tanzania, Hamza Johari, huku Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe (katikati), akiangalia,  katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.            
  Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis ndunguru (katikati), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi (kushoto), huku Mwenyekiti wa Kampuni ya Chelsea Starway Group, Martin Mbwana akisikiliza, katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kutoa shukurani kwa mahusiano bora ya kibiashara kati ya NBC na wateja hao kwa mwaka 2019. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia), akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo wa Tawi la Mwanza, wakati wa ziara yake mkoani humo hivi karibuni.
   Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Marco Saguti (wa tatu kushoto), akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, wakati yeye na ujumbe wake walipomtembelea ofisini kwake katika ziara yao mkoani Kagera hivi karibuni.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (katikati), akipozi kwa picha na wafanyakazi wa benki hiyo wa tawi la Mwanza  wakati mkurugenzi huyo pamoja na ujumbe wake wakiwa katika ziara ya kikazi mkoani humo hivi karibuni. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (katikati), akipozi kwa picha na wafanyakazi wa benki hiyo wa tawi la Musoma wakati mkurugenzi huyo pamoja na ujumbe wake wakiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Mara hivi karibuni. 
  Meneja wa Benki ya NBC Kanda ya Ziwa, Japhet Mazumira (kulia), akizungumza na wafanyakazi wa benki hiyo wa Tawi la Mwanza wakati wa ziara ya Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi mkoani humo hivi karibuni.  

  0 0

  Katika kutambua afya ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya jamii, Benki ya NMB imekabidhi vitanda 15 vyenye jumla ya thamani ya milioni 45 kwa ajili ya chumba cha watoto wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum (ICU) katika hospitali za Muhimbili na Mloganzila za jijini Dar es Salaam.

  Akikabidhi msaada huo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Afisa Mkuu wa Mahesabu wa Benki ya NMB, Juma Kimori, alibainisha kwamba thamani ya vitanda vyote ni Sh. Milioni 45 huku  akifafanua kuwa kitanda kimoja cha ICU ya watoto kimegharimu Sh. Milioni 7.5 na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali kuboresha sekta ya afya.

  Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Zuhura Mawona, aliishukuru na kuipongeza NMB kwa msaada huo na kuiomba iendelee kutoa msaada zaidi kwa ajili ya chumba hicho maalum kwa watoto.

  “Tulipeleka maombi NMB na wametujibu hatuchoki, tunaendelea kuwaomba mtushike tena mkono, maana mahitaji ya vitanda katika chumba hicho muhimu cha kuokoa maisha ya watoto ni mkubwa, bado tunahitaji vingine saba mkiguswa tena mtukumbuke.

  “Kabla ya wodi hii kuanza watoto walikuwa wanachanganywa kwenye ICU za wakubwa na kule vitanda sio sawa na hivi tulivyopokea vya NMB hata sisi  wahudumu hatupati tabu sana kuvinyanyua wala mgonjwa haumii kila kitu kinasetiwa kwenye umeme asanteni sana NMB,” alisema Mawona aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.#NMBKaribuYako
  Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa Benki ya NMB, Peter Kimori akimkabidhi Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto; Mh. Ummy Mwalimu masada wa vitanda 15 kwa ajili ya chumba cha watoto wagonjwa waliopo kwenye uangalizi maalum(ICU) katika hospitali za Muhimbili na Mloganzila za jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto; Mh. Ummy Mwalimu na Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa Mahesabu ya Ndani wa Benki ya NMB, Juma Komori  wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao kutoka hospitali za Muhimbili na Mloganzila.

  0 0


  0 0

  Na Grace Gurisha


  MENEJA Mauzo na Masoko wa Kampuni inayojihusisha na uundaji wa mifumo mbalimbali ya kiteknolojia ya MD Technology, Mohamed Kaddy amesema wameleta  kifaa maalumu chenye uwezo wa kudhibiti wizi wa pikipiki na vyombo vya moto.

  Kaddy aliyasema hayo  jana  Desemba 14, mwaka huu, jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kifaa hicho, ambapo alisema kwa kutumia teknolojia hiyo,pikipiki ikiibiwa, itapatikana na mmiliki atapata taarifa kupitia simu yake ya mkononi.

  Meneja huyo alisema teknolojia hiyo ni rahisi, "Ukifunga kifaa cha kudhibiti wizi katika pikipiki yako,hata kama ikiibiwa usiwe na wasiwasi,itapatikana tu, lakini pia kama kuna mtu amesimama katika pikipiki yako utajulishwa”,.

  "Kifaa hichi maalumu kitafungwa katika pikipiki na kuunganishwa na simu ya mkononi ambapo mteja atapata taarifa zote za uendeshaji wa pikipiki katika simu yake ya mkononi na pia hata akipoteza simu yake anaweza kutumia simu ya mtu mwingine na kupata taarifa kifaa chake kilipo," alisema 

  Alisema mfumo huo husaidia kudhibiti udanganyifu wa madereva au marafiki katika matumizi ya umbali aliotumia kwa siku katika uendeshaji wa pikipiki,jambo litakalowawezesha wamiliki wa pikipiki kuwa na uhakika wa mapato, kwa zile zinazofanya usafiri wa abiria.

  “Mfumo huu utawasaidia wamiliki wa pikipiki kupata taarifa kwa haraka pale chombo chake kikitaka kuibiwa au kushikwa na mtu, pia mfumo huo utamsaidia mtu kuzima au kuwasha chombo mahali popote atakapokuwa, kama umeibiwa unauwezo wa kuizima pikipiki yako kabla haijafika mbali," alisema

  Alisema kifaa hicho tayari kimeshaanza kuuzwa kwa bei nafuu, hivyo madereva wajitokeze kwa wingi kununua ili kudhibiti wezi kutokana na wimbi la wizi wa Bodaboda linaloendelea hivi sasa.

  Pia, alisema wanafunga vifaa kwenye nyumba kwa mfumo wa kisasa ambapo hata mwizi atakapokwenda kuiba hata gundua kama kuna kifaa cha usalama kimefungwa kwa hiyo itakuwa ni rahisi yeye kukamatwa kwa sababu kifaa kitaonesha kuna mtu ameingia.
   Meneja Mauzo na Msoko wa Kampuni inayojihusisha na uundaji wa mifumo mbalimbali yabkiteknolojia ya MD Technology, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kifaa cha kisasa cha kuzuia wizi wa vyombo vya moto.

   Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya MD Technology, Brian Kessy akiwaeleza madereva wa Bodaboda faida ya kifaa hicho ambacho kitawasaidia katika suala nzima la ulinzi wa pikipiki zao
   Mtaalamu wa Mifumo kutoka MD Technology, Salum Mntitiwa akionesha jinsi ambavyo kifaa hicho kilivyofungwa na kuunganishwa na simu ya mkononi kinavyoweza kufanya kazi kwa kuliweka gari katika hali ya usalama,


  0 0   Wafanyakazi wa Kampuni ya mawasiliano ya  Vodacom wakiwa wamebeba bango lenye picha ya simu ya Smart Kitochi  wakati wa uzinduzi wa simu hiyo uliofanyika jijini Mwanza.
  Kaimu  mkuu wa mauzo wa Kampuni ya mawasiliano ya  Vodacom kanda ya Ziwa, Ayubu Kalufya akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa simu ya Smart Kitochi, uliofanyika jijini Mwanza.
  Wateja wa simu mpya za Smart Kitochi zenye uwezo wa 4G kutoka Vodacom wakipatiwa maelezo ya kuhusu simu hizo zitakazopatikana kwenye maduka ya Vodacom  nchini kote kwa bei ya shilingi 45,000/=  katika msimu huu wa sikukuu wakati wa uzinduzi wa simu hizo jijini Mwanza.

  Wateja wa simu mpya za Smart Kitochi zenye uwezo wa 4G kutoka Vodacom, wakijipiga selfie kwa kutumia simu hiyo baada ya kuinunua jijini Mwanza, wakati wa uzinduzi wa simu hiyo inayopatikana kwenye maduka ya Vodacom nchini kote kwa bei ya shilingi 45,000/= katika msimu huu wa sikukuu.