Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 996 | 997 | (Page 998) | 999 | 1000 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akiwa na mgeni wake Jaji Mkuu wa Australia Kusini, Mhe.Christopher Kourakis ambaye amemtembelea ofisini kwake mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu baina ya Mahakama ya Tanzania na Australia Kusini.
  jai2
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akiongea na waandishi wa habari juu ya ziara ya kikazi ya Jaji Mkuu wa Australia Kusini, Mhe.Christopher Kourakis (kushoto) yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Australia Kusini.
  jai3
  Jaji Mkuu wa Australia Kusini, Mhe.Christopher Kourakis (kushoto) akiwaeleza waandishi wahabari (hawapo pichani) mipango waliyokubaliana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) kushirikiana baina ya Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Australia Kusini mapema hii leo jijini dare s Salaam.
  jai4
  Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (kulia) akiongea na waandishi wa habari juu ya ziara ya kikazi ya Jaji Mkuu wa Australia Kusini, Mhe.Christopher Kourakis (hayupo pichani) yenye lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Australia Kusini,
  jai5
  Jaji Mkuu wa Australia Kusini, Mhe.Christopher Kourakis (kushoto) akiwaeleza waandishi wahabari (hawapo pichani) mipango waliyokubaliana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman (katikati) kushirikiana baina ya Mahakama ya Tanzania na Mahakama ya Australia Kusini mapema hii leo jijini dare s Salaam, kulia ni
  jai6
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mhe. Ferdinand Wambali (kulia) akiwa na mgeni wake Jaji Mkuu wa Australia Kusini, Mhe.Christopher Kourakis ambaye amemtembelea ofisini kwake mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu baina ya Mahakama ya Tanzania na Australia Kusini.
  jai7
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mhe. Ferdinand Wambali (kulia) akimuonesha baadhi ya ofisi za Mahakama Kuu ya Tanzania mgeni wake Jaji Mkuu wa Australia Kusini, Mhe.Christopher Kourakis (katikati) ambaye amemtembelea ofisini kwake mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu baina ya Mahakama ya Tanzania na Australia Kusini.
  jai8
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mhe. Ferdinand Wambali (kulia) akimueleza  mgeni wake Jaji Mkuu wa Australia Kusini, Mhe.Christopher Kourakis jinsi ya utendaji kazi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakati alipomtembelea ofisini kwake mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu baina ya Mahakama ya Tanzania na Australia Kusini.
  jai9
  Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Mhe. Ferdinand Wambali (kulia) akimueleza  mgeni wake Jaji Mkuu wa Australia Kusini, Mhe.Christopher Kourakis jinsi ya utendaji kazi wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakati alipomtembelea ofisini kwake mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu baina ya Mahakama ya Tanzania na Australia Kusini.

  ………………………………

  Na Lydia Churi- Mahakama ya Tanzania 
  Mahakama ya Tanzania inakusudia kushirikiana na Australia ya Kusini katika teknolojia za kuendesha mashauri mahakamani ili kutekeleza jukumu lake la msingi la kutoa Haki sawa kwa wote na kwa wakati.

  Akizungumzia ziara ya Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini Mheshimiwa Christopher Kourakis iliyoanza leo nchini, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amesema ziara ya kiongozi huyo inalenga kuimarisha na kujenga ushirikiano katika maeneo matatu likiwemo eneo la teknolojia ya kuendesha mashauri mahakamani.

  Alisema Australia ya kusini inaendesha mashauri mahakamani kwa kutumia teknolojia ya kisasa hivyo Mahakama ya Tanzania haina budi kuhama kutoka mifumo ya kuendesha mahakama kwa mkono kwenda kwenye teknolojia ya kidijiti.

  Alisema Mahakama inakusudia kuwapeleka wasajili na watendaji wa mahakama nchini Australia ya kusini ili wakajifunze mifumo hiyo kwa ajili ya kuanza kuitumia kuendeshea mahakama za Tanzania.

  Aliyataja maeneo mengine ya ushirikiano kuwa ni eneo la utoaji wa mafunzo kwa Majaji, Mahakimu na Wasajili wa Mahakama ya Tanzania huku akisema eneo la tatu ni la namna ya kuanzisha Kada mpya ya Wapiga Chapa Maalum wa Mahakama watakaokuwa wakitumia mashine ndogo inayochapa wakati mashauri yakiendelea Mahakamani.

  Akiielezea kada hiyo mpya, Jaji Mkuu alisema itawezesha kupatikana kwa nakala za mashauri ndani ya siku moja na kwamba watumishi hao ni tofauti na makatibu Muhtasi ambapo mishahara yao itakuwa ni mikubwa kuliko ile ya Makatibu Muhtasi.

  Naye Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini alisema Mahakama za nchini kwake zinaendesha mashauri kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kidijiti hivyo nchi yake itashirikiana na  Tanzania ili nayo iweze kuendesha mashauri mahakamani kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

  Akizungumzia kuhusu adhabu ya kifo kwa watuhumiwa wa kesi za mauaji nchini Australia ya Kusini, Mheshimiwa Kourakis alisema adhabu hiyo iliondolewa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo msukumo wa Haki za Binadamu.

  Alisema nchi yake pia ina mfumo ambapo endapo mtuhumiwa wa mauaji atakiri kosa ndani ya wiki sita basi atapunguziwa adhabu yake kwa asilimia 40. Aliongeza kuwa adhabu ya kifo nchini kwake ni kifungo cha maisha na endapo atakiri kosa atapunguziwa adhabu. Kiwango cha chini cha adhabu ya kifo ni kifungo cha miaka 20 jela.

  Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini leo ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini ambapo ametembelea Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu na pia anatarajia kutembelea Mahakama ya Zanzibar.

  0 0

    Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Anna Nguzo akisalimia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makala ambaye alikuwa mgeni rasmi katika Maonyesho ya 13 Wajasiriamali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yaliyofanyika katika Viwanja vya City Garden jijini Mbeya. PCHA NA KENNETH NGELESI.
   Kaimu Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Mbeya, Yohana Mwambilija, akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla (kulia) alipotembelea banda la shirika hilo wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya 13 ya  Wajasiriamali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
  Mkaguzi wa NSSF Mkoa wa Mbeya Bupe Mwantole akimkabidhi mwanachama mpya fomu ya kujiunga na NSSF wakati wa maonyesho ya 13 ya wajasiriamali jijini Mbeya.
   Afisa Masoko na Uhusiano wa NSSF,  Anna Nguzo akimkabidhi fomu mwanachama aliyefika katika banda la shirika hilo kwa ajili ya kupata huduma kwenye maonyesho ya 13 ya wajasiriamali  jijini Mbeya.
  Mkaguzi wa Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Mbeya wa (pili kulia) akimjazia fomu mteja aliyefika kwenye banda la shirika hilo wakati wa maonyesho ya 13 ya wajasiriamali jijini Mbeya. 
  Afisa Masoko na Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Anna Nguzo akitoa maelezo kwa watu waliopita katika banda la NSSF wakati wa maonyesho ya SIDO mkoani Mbeya.

  0 0

   Snura Mushi
   Msemaji wa Msanii Snura Baraka Nyagenda. akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salamm leo.
   Msanii Snura Mushi (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania. Kushoto ni Msemaji wake, Baraka Nyagenda.
  Mkutano na wanahabari ukiendelea.


   Na Dotto Mwaibale

  SERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeruhusu kupigwa kwa wimbo wa chura wa msanii Snura Mushi baada ya kuufunga kwa kuwa haukuwa na maudhui mazuri ya kitanzania.

  Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Snura Mushi alisema wimbo wake na video umeruhusiwa kupigwa baada ya audio ya chura kufanyiwa marekebisho na kuifanya kuwa katika maudhui ya kitanzania.

  Alisema ruhusa hiyo imetolewa kwa barua iliyoaandikiwa Septemba 26, 2016 yenye kumbukumbu HA.26/375/01'B'/137 ambayo gazeti hili lina nakala yake.

  Kupitia mkutano huo msanii Snura Mushi kwa mara nyingine aliomba radhi kwa watanzania na Serikali kwa ujumla kwa usumbufu walioupata kwa video yake ya kwanza na kuwaomba waendelee kuiona video mpya iliyorekebishwa baada ya kuifuta ya kwanza.

  0 0

  Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kagera Mhandisi Avitus Exavery akimuonesha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge uharibifu wa tanki la maji la shule ya sekondari ya Ihungo uliosababishwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mapema Septemba 2016.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge (wa nne kulia) akitembelea miundombinu ya maji iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mapema Septemba 2016.
  Baadhi maungio ya maji yaliyoharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera mapema Septemba 2016.
  Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge (kulia) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (kulia) leo mjini Bukoba kujionea uharibifu wa miundombinu ya sekta ya maji iliyosathiriwa na tetemeko la ardhi.


  Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu (kulia) akimkaribisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge (kulia) alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Bukoba kujionea uharibifu wa miundombinu ya sekta ya maji iliyosathiriwa na tetemeko la ardhi.
  …………………………………………………………

  Na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba.

  Serikali imeanza kurekebisha miundombinu ya maji iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi mkoani Kagera ili kuwapatia wananchi huduma ya maji safi na salama waweze kuendelea na kazi zao za kawaida za kila siku.

  Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu ofisini kwake leo mjini Bukoba kujionea uharibifu wa miundombinu ya sekta ya maji iliyosathiriwa na tetemeko la ardhi.

  “Ni lazima turudishe miundombinu ya maji ambayo imeharibiwa na tetemeko la ardhi ili kuwapatia wananchi huduma ya maji safi na salama, maji wanaweza kuyapata lakini yanaweza kuwa si salama, ni kukumu langu kuja kupita ili niweze kukagua kujua baada ya tetemeko hili bado maji ni salama au kuna mambo ya kufanya ili tuweze kuyashughulikia” alisema Waziri Mhandisi Lwenge

  Katika kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Kagera wanapata maji ya uhakika, Waziri Mhandisi Lwenge amesema kuwa ziara yake inalenga pia kuhakikisha azma ya Serikali ya kuwapatia wananchi maji ya uhakika.

  Mpango huo wa Serikali unalenga kuwapatia wananchi waishio mijini maji kwa kiwango cha asilimia 95 ambapo kwa wananchi waishio vijijini wanapata maji ya uhakika kwa asilimia 85 ifikapo 2020.

  Kwa wananchi waishio vijijini, Waziri Mhandisi Lwenge amesema kuwa kwa sasa wananchi wanapata maji kwa asilimia 60 hadi 70 wakati kwa ngazi ya kitaifa inaonesha wananchi hao wanapata maji kwa asilimia 72.

  Kwa upande wa sekta ya umwagiliaji, Waziri Mhandisi Lwenge amesema kuwa hali ya mvua nchni inazidi kupungua mwaka hadi mwaka.

  Waziri Mhandisi Lwenge amesema kuwa ili kuwa na uhakika wa chakula cha kutosha, Serikali pamoja na wananchi kuweka nguvu kwenye kilimo cha umwagiliaji ambacho ndio chenye uhakika wa kutatua changamoto ya uhaba wa chakula na upatikanaji wa maji.

  Katika kukabiliana na hali hiyo, Waziri Mhandisi Lwenge amsema kuwa Serikali imeanzisha Tume ya Umwagiliaji na kuainisha maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji ikiwemo mkoa wa Kagera ambayo yanaweza kutumika kwa kilimo cha umwagiliaji.

  Hatua hiyo ya Serikali itasaidia kujengwa kwa miundombinu ambayo itawasidia wananchi wanaoishi katika maeneo ya umwagiliaji waweze kufaidika kwa kilimo cha umwagiliaji ambayo ndio azma ya Serikali.

  Waziri Mhandisi Lwenge amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 kuwa na hekta milioni 1 za kilimo cha umwagiliaji ambapo kwa sasa zinalimwa hekta 461,0000 ambayo ni sawa na asilimia 1.6 ya eneo lote ambalo linaweza kutumika kwa umwagiliaji na kuutaja mkoa Kagera ni moja wapo ya maeneo ambayo yanafaa kwa kilimo cha umwagiliaji.

  Zaidi ya hayo, Waziri Mhandisi Lwenge amesema kuwa kulingana na jiografia ya mkoa wa Kagera, upo uwezekano wa kujenga mabwawa ambayo yatatumika kwa kilimo cha umwagiliaji, kufuga samaki, maji ya kunyweshea mifugo na kuweka rasilimali maji ambayo nchi nyingi duniani zimeanza kutegemea kilimo hicho ili kujihami na upungufu wa mvua.

  Akimkaribisha Waziri Mhandisi Lwenge, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu amesema kuwa katika sekta ya maji mkoani humo, miundombinu ya maji imeathirika na kuharibiwa na tetemeko la ardhi na kusababisha upatikanaji wa maji kwa wananchi kuwa si wa kuridhisha.

  Aidha, Mkuu huyo wa mkoa amemhakikishia Waziri wa maji na umwagiliaji kuwa maagizo na maelekezo yake aliyoyatoa yatasimamiwa na kutekelezwa ili kuwahudumia wananchi na maisha yao yaweze kuwa bora na kujiletea maendeleo.

  Katika ziara yake mkoani Kagera, Waziri Lwenge ametembelea maeneo miundombinu ya maji yaliyoharibiwa na tetemeko la ardhi, Mamlaka ya Maji Safi na Salama Bukoba, chanzo cha maji cha Bunena pamoja na tanki la maji la shule ya sekondari Ihungo lililoathiriwa tetemeko la ardhi.

  0 0

    Na Humphrey Shao, Dar es Salaam

  Baraza la mitahani nchini limeanzisha mfumo mpya wa Kutunza Kumbukumbu za Wanafunzi wa shule za Msingi (PREM), Utakaosadia uandikishwaji wa wanafunzi wote.

  Akizungumza na waandishi wa habari mapema jijini Dar es Salaam leo Afisa Habari wa Baraza la Mitihani nchini John Nchimbia, alisema kuwa mfumo huo utatoa namba Maalum ambayo itamtambulisha mwanafunzi katika ngazi zote za mitihani.

  “Mfumo huu utakuwa na faida nyingi sana pamoja na kusaidia katika uhamisho wa mwanafunzi kutoka shule moja kwenda nyingine ndani ya mkoa au nje ya mkoa hivyo kuondoa tatizo la wanafunzi hewa”alisema Nchimbi.

  Aliongeza kuwa mfumo huu utasaidia katika uandaaji na utoaji wa Takwimu za Wanafunzi katika ngazi ya shule Wilaya ,Mkoa mpaka Taifa.

  Alimaliza kw akusema kuwa Baraza limeanza kufanya majaribio ya Mfumo huu katika mikoa miwili ya Mwanza na Ruvuma na Ifikapo Disemba mfumo utaimarishwa ili Januari hadi Mei 2017 utumiwe nchi nzima kwa shule za msingi.

  0 0

   WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameahidi kukutana na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba mkoani Dodoma ili kuzungumzia namna ya kulikarabati na kulifanya liwe la kisasa.

  Amesema miongoni mwa mambo watakayoyajadili katika kikao hicho ambacho hakutaja siku ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara hasa kwa wanaouza bidhaa nje ya maduka.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Oktoba 5, 2016) wakati alipotembelea maduka hayo yaliyoko katika barabara ya One Way inayopita katikati ya barabara ya sita hadi ya 11 pamoja na soko la Sabasaba akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.

  Amesema Serikali tayari imeshahamia Dodoma hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kutumia fursa hiyo kwa kuboresha biashara zao ili waweze kumudu ushindani wa soko.

  “Wafanyabiashara lazima mboreshe biashara zenu, muongeze usafi zaidi na ikiwezekana muimarishe majengo yenu yawe ya kisasa zaidi kwani haiwezekani maduka ya Makao Makuu ya Nchi yawe katika hali hii,” amesema.

  Pia Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara hao wasiogope kwenda kukopa katika taasisi mbalimbali za kifedha kwa lengo la kujiongeza mitaji  na kupanua biashara.

  Amesema tayari alishatoa maagizo kwa wamiliki wa benki kuhakikisha wanawawezesha wajasiriamali wadogo kwa kuwapa mikopo, hivyo aliwataka wasiogope na badala yake wachangamkie fursa hiyo.


   IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  JUMATANO, OKTOBA 05, 2016

  0 0


  Kaimu Kamishna Generali wa Idara ya Uhamiaji ya Uhamiaji, Victoria Lembeli, akipokea Kombe la ushindi wa klabu Bingwa Taifa kutoka kwa Nahodha wa timu ya Uhamiaji , Neema Massawe wakati wa hafla ya kuwapokea wachezaji wa timu hiyo iliyofanyika katika Makao Makuu ya Idara hiyo jijini Dar es Salaam.
  .Wachezaji wa timu ya Idara ya Uhamiaji wakiingia katika Ofisi za makao makuu ya Idara hiyoKurasini jijini Dar es Salaam.
  Viongozi wa Ngazi ya juu wa Idara ya Uhamiaji wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo mara baada ya kumalizika kwa mkutano na waandishiwahabari. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.


  Na  Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
   
  WITO umetolewa kwa timu ya mchezo wa mpira wa pete ya Idara ya Uhamiaji nchini kuongeza juhudi katika michezo mbalimbali,katika suala zima la kuimarisha umoja na mshikamano uliopo nchini.

  Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu kamishna Jenerali wa uhamiaji nchini , Victoria Lembeli, alipokuwa akipokea kikombe cha ushindi wa Klabu bingwa Taifa kwa timu ya mpira wa pete

  “Hakika niwapongeze kwa ushindi mliopata kwani mmeweza kushindana katika ,mazingira magumu hivyo nilivyopata kusikia kuwa mmekuwa mabingwa sikuamini masikio yangu hivyo naomba muendelee na moyo huo huo kwa kuwa michezo ndio inadumisha umoja na mshikamano” anasema
  Kamishna Lembeli aliongeza kuwa mshikamano na juhudi katika michezo viatachangia kuongeza utashi wa kazi .

  Kwa uapande wake Nahodha wa timu hiyo ,Neema Massawe alisema kuwa wao kamatimu wamejipanga kushinda mishandano yote yaliyo mbele yao hili kuendelea kutetea nafasi walizonazo.

  Alitamba kuwa Uhamiaji ndio timu pekee inayofanya vizuri katika mchezo wa mpira wa pete hapa nchini hivyo tasisi nyingine za serikali na majeshi zinapaswa kujipanga na kujifua sana hili kufikia wao walipo.
  Aliongeza kuwa wameweza kucheza mashindano ya Klabu bingwa Taifa bila ya kufungwa hata mchezo mmoja na timu zote 12 jambo ambalo linathibitisha ubora wao

  0 0

  Muonekano wa kivuko kipya cha MV Kazi kikiwa katika hatua za awali za ujenzi wake. Kivuko hicho kinatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Kampuni ya Songoro wanaojenga kivuko kipya cha MV. Kazi, kinachojengwa katika yadi ya Bandari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutembelea na kujionea ujenzi wake. Kivuko hicho kipya kinatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa akiongea na mafundi wa wa Kampuni ya Songoro wanaojenga kivuko kipya cha MV. Kazi, kinachojengwa katika yadi ya Bandari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutembelea na kujionea ujenzi wake. Kivuko hicho kipya kinatarajiwa kukamilika mwezi Disemba mwaka huu.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), alipotembelea eneo la Kivukoni. Katikati ni Mkuu wa Kivuko upande wa Dar es Salaam, Eng. Lukombe King’ombe.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akiongea na mwanafunzi Arafat Kondo wakati alipotembelea kivuko cha MV. Kigamboni kujionea utendaji wake.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akishuka kwenye pantoni mara baada ya kukagua utendaji wa kivuko cha MV. Kigamboni.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akisikiliza taarifa ya matumizi ya mafuta kutoka kwa Mhandisi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) alipotembelea kivuko cha MV. Kigamboni.

  ………………………………………………………..

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameuagiza uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti ya kuongeza mapato katika vivuko vya MV. Kigamboni na MV. Magogoni kutoka Shilingi Milioni 14 ambazo zinakusanywa hivi sasa hadi kufikia Milioni 19 kwa siku.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kukagua vivuko hivyo na kuongea na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu Prof. Mbarawa amesema kuwa kipimo cha utendaji huo utafanyika ndani ya miezi minne ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wa vivuko hivyo na kuweza kufikia malengo.

  “Hatushindwi kutafuta mtu mwingine mwenye ujuzi na utendaji wa kazi uliotukuka, kama lengo la kukusanya milioni 19 halitafikiwa mkuu wa kivuko atafute kazi nyingine na tutafanya hivyo mpaka tuhakikishe tunapata atayeweza kukusanya kiwango hiki”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Prof. Mbarawa ameutaka Wakala huo kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa mapato katika vivuko hivyo na kuwa wa kieletroniki ili kudhibiti ubadhilifu unaofanywa na watumishi wasio waaminifu wakati wa utoaji huduma.

  Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amejionea maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV. Kazi nakusema kuwa kivuko hicho kitarahisisha usafiri kwa wakazi wa Kigamboni.

  Aidha, amemtaka mkandarasi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport kumaliza utengenezaji wa kivuko hicho ifikapo Mwezi Disemba mwaka huu ili watanzania wapate huduma bora za usafiri.

  Ameongeza kuwa Kampuni hiyo ihakikishe kuwa inasimamia upatikanaji wa injini za Kivuko hicho kwa wakati ili kusaidia ujenzi huo kukamilika kwa muda uliopangwa.

  “Nina imani na kasi mnayokwenda nayo, na nina uhakika Kivuko hiki kitamalizika kwa wakati naomba muwe waangalifu na kuhakikisha kwamba injini za kivuko hiki zinawasili mapema”, amesisitiza Prof. Mbarawa.

  Naye Mkurugenzi wa Karakana ya Dar es Salaam wa Kampuni ya Songoro Marine, Major Saleh Songoro amesema kuwa ujenzi wa Kivuko cha MV Kazi upo katika hatua nzuri ambapo kwa sasa wanakamilisha kazi ya kuchomea milango katika kivuko hicho.

  Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mgwatu amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa maagizo yote yatatekelezwa ikiwemo kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili Wakala huo.

  Dkt. Mgwatu amewataka wananchi kuwa na subira wakati kivuko cha MV. Kazi kinamalizika kujengwa kwani itapunguza kama sio kuondoa msongamano uliopo sasa katika maeneo ya Magogoni na Kigamboni.

  Ujenzi wa kivuko cha MV Kazi ulianza Mwezi Juni mwaka huu ambapo kina uwezo wa kubeba tani 170 sawa na watu 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.

  0 0

  East African Community Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko (right) holds talks with the Irish Ambassador to Tanzania and the EAC, H.E. Paul Sherlock, at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania. The two leaders discussed various issues including the status of the EAC-EU Economic Partnership Agreements (EPAs) and the Inter-Burundi Dialogue.

  EAC Secretary General Amb. Liberat Mfumukeko (left) with the Irish Ambassador to Tanzania and the EAC, H.E. Paul Sherlock, after they held bilateral talks at the EAC Headquarters in Arusha, Tanzania. They explored areas of collaboration in trade, investment, agro-processing, tourism and ICT.

  ……………………………………………………………………………

  East African Community Headquarters, Arusha, Tanzania, 5th October, 2016:

  The Secretary General of the East African Community, Amb. Liberat Mfumukeko, today received credentials from the Ambassador of the Republic of Ireland to the United Republic of Tanzania, H.E Ambassador Paul Sherlock, who has also been accredited to the EAC.

  In the Ambassador’s accreditation letter dated 30th August, 2016 addressed to the Secretary General of the EAC, the Irish Minister of Foreign Affairs, Mr. Charles Flanagan, appoints Amb. Paul Sherlock as the Irish representative to the EAC.

  The Secretary General warmly welcomed Amb. Sherlock to the EAC and briefed him on the current achievements in the pillars of the regional integration and development process. He said the Community had expanded tremendously within a short spell of time, which has necessitated the Community to review its institutional set-up and work on sustainable financing mechanism.

  Amb. Mfumukeko further informed his guest of the reforms he had instituted within the Organs and Institutions of the Community aimed at cost cutting and prudent financial management.

  In his remarks, Amb. Sherlock hailed the Secretary General for the good work he and his team were doing in deepening the regional integration agenda. He said achieving the Customs Union and the Common Market and moving towards a Monetary Union within such a short time for the Community was commendable

  Amb. Mfumukeko and the Irish envoy discussed several issues including the status of the EAC-EU Economic Partnership Agreements (EPAs) and the Inter-Burundi Dialogue. They also explored areas of collaboration in trade and investment, agro-processing, tourism and ICT.

  The Secretary General informed Amb. Sherlock that the EAC Secretariat was ready to mobilize and send an EAC Mission to Ireland to meet the Irish Chamber of Commerce and Industry, Tourism and Investment Agencies, and other stakeholders to concretize the specific areas of cooperation.

  Also present at the accreditation ceremony were Mr. Robert Hull, the Second Secretary at the Embassy of Ireland in Dar es Salaam, Deputy Secretaries General Mr. Charles Njoroge (Political Federation) and Hon. Christophe Bazivamo, and other senior officials at the EAC Secretariat.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembela Mtaa wa One Way mjini Dodoma Oktoba 5, 2016.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea eneo maarufu la biashara mjini Dodoma la Sabsaba Oktoba 5, 2016.

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitembelea eneo maarufu la biashara mjini Dodoma la Sabsaba Oktoba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu()
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembela Mtaa wa One Way mjini Dodoma Oktoba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  ……………………………………………………………………

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameahidi kukutana na wafanyabiashara wa soko la Sabasaba mkoani Dodoma ili kuzungumzia namna ya kulikarabati na kulifanya liwe la kisasa.

  Amesema miongoni mwa mambo watakayoyajadili katika kikao hicho ambacho hakutaja siku ni pamoja na kuboresha mazingira ya kufanyia biashara hasa kwa wanaouza bidhaa nje ya maduka.

  Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumatano, Oktoba 5, 2016) wakati alipotembelea maduka hayo yaliyoko katika barabara ya One Way inayopita katikati ya barabara ya sita hadi ya 11 pamoja na soko la Sabasaba akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo ya kutolea huduma za jamii mjini Dodoma.

  Amesema Serikali tayari imeshahamia Dodoma hivyo wafanyabiashara wanatakiwa kutumia fursa hiyo kwa kuboresha biashara zao ili waweze kumudu ushindani wa soko.

  “Wafanyabiashara lazima mboreshe biashara zenu, muongeze usafi zaidi na ikiwezekana muimarishe majengo yenu yawe ya kisasa zaidi kwani haiwezekani maduka ya Makao Makuu ya Nchi yawe katika hali hii,” amesema.

  Pia Waziri Mkuu amewataka wafanyabiashara hao wasiogope kwenda kukopa katika taasisi mbalimbali za kifedha kwa lengo la kujiongeza mitaji na kupanua biashara.

  Amesema tayari alishatoa maagizo kwa wamiliki wa benki kuhakikisha wanawawezesha wajasiriamali wadogo kwa kuwapa mikopo, hivyo aliwataka wasiogope na badala yake wachangamkie fursa hiyo.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila akipunga mkono wakati akipanda ndege kurejea nchini kwake mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu hapa nchini.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku tatu nchini na kurejea DRC.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakipunga mkono kuagana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila (hayupo pichani) katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) .
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Shekhe Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere mara baada ya kuagana na mgeni wake Rais wa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila. kulia ni mkuu wa Wilaya ya Ilala Sofia Mjema.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kabla ya kuondoka. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakati akimsindikiza katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kabla ya kuondoka. Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakati nyimbo za Taifa za mataifa yote mawili zikipigwa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakiangalia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikitoa burudani uwanjani hapo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na mgeni wake wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila wakiangalia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikitoa burudani uwanjani hapo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu akikagua mashine ya ukaguzi wa mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal One kuangalia ufanisi wa mashine hizo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu akiangalia ufanisi wa mashine za kukagulia mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal One na kukuta zinafanya kazi vizuri. Aliyekaa ni Mwendeshaji wa Mashine hizo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege TAA-Grace Jonathan.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati wakiangalia vikundi vya ngoma uwanjani hapo. PICHA NA IKULU

  0 0  Tukio lilianza tarehe Jumatatu 26/9/2016, ambapo Mwalimu Frank Msigwa, mwanafunzi kwa vitendo kutoka chuo kikuu cha  Dar Es  salaam ambapo alitoa assignment ya somo la kingereza kwa wanafunzi wa kidate cha tatu.

  Baada ya kusahihisha, aligundua kuwa kuna baadhi ya wanafunzi hawakufanya. Hivyo,tarehe Jumatano 28/9/2016,alikwenda darasani na kutoa adhabu wale ambao hawajafanya kazi yake.Alianza kwa kuwapa adhabu ya push-up,kisha kupiga magoti na baadae aliwapuga viboko viwili.Katika utekelezaji wa adhabu ile, mwanafunzi  Sebastian Chingulu alikataa kufanya  kutokana na kuumwa na goti.

  Baada ya kuigomea adhabu ile, Mwalimu Frank Msigwa na wenzake wawili, John Deo na Sanke Gwamaka, walimpeleka ofisini na kuanza kumshambulia kwa kipigo kama inavyoonekana kwenye video.Baada ya tukio hilo waalimu hao walitoweka shuleni hapo.Wakati wanamshambulia mwanafunzi huyo, kulikuwepo na Mwalimu mwingine aliyewasihi wasiendelee kumpiga kijana huyo na ndiye aliyerekodi tukio hilo.

  Serikali ya mkoa inaendelea kuwashikilia walimu kadhaa pamoja na Mwalimu Mkuu kwa mahojiano pamoja na kupata maelezo ya wanafunzi waliopata adhabu hiyo.Kuhusu mwanafunzi aliyepigwa,nawahakikishia kuwa serikali itawasaka popote walipo walimu  waliofanya tukio hilo na kufikisha katika vyombo vya dola ili wapate haki yao kisheria.
  Aidha mwanafunzi aliyepigwa anaendelea kupimwa na matibatibu.

  Hii ni taarifa ya awali, nitaendelea kutoa taarifa kwa kila hatua tunayoifikia. Ni Mimi,
   

  Amos G Makalla
  RC Mbeya

  0 0

    Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Shindano ya Miss Tanzania 2016 walipokutana kuzungumza kuhusu masuala ya urembo nchini na baadae kushiriki katika zoezi la upandaji miti Mjini Dodoma.
   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na washiriki wa wa Shindano ya Miss Tanzania 2016 na wadau wa Mashindano ya urembo nchini walipokutana kuzungumza kuhusu masuala ya urembo nchini na baadae kushiriki katika zoezi la upandaji miti Mjini Dodoma.

    Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akishiriki kupanda  miti wakati alipokutana na kuzungumza kuhusu masuala ya urembo nchini na baadae kushiriki katika zoezi la upandaji miti Mjini Dodoma
   Baadhi ya washiriki wa Shindano la Miss Tanzania 2016 wakipanda miti katika zoezi la upandaji miti lililofanyika Mjini Dodoma.

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa katika picha pamojja na washiriki wa Shindano la Miss Tanzania 2016 mara baada ya kufanya mazungumzo nao na  kushiriki zoezi la upandaji miti lililofanyika Mjini Dodoma.

  Picha na Kitengo cha Mwasiliano WHUSM.

  0 0

  Na: Genofeva Matemu - WHUSM

  Wadau wa tasnia ya filamu nchini wameipongeza Serikali kuwashirikisha katika mchakato wa uandaaji na ukamilishaji wa Sera ya filamu nchini.

  Hayo yamesemwa na wadau mbalimbali walioshiriki katika kikao cha kupitia uchambuzi wa hali halisi ya tasnia ya filamu kwa ajili ya maandalizi ya Sera ya filamu kilichofanyika mapema wiki hii.

  Akizungumza wakati wa kikao hicho Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa sekta ya filamu hapa nchini imekuwa ikisimamiwa na kongozwa na Sera ya Utamaduni ya mwaka 1997 lakini kutokana na kukua kwa tasnia ya filamu ilionekena kuwa kuna uhitaji wa Sera ya Filamu itakayo kuwa dira na mwongozo katika kukuza tasnia hiyo.

  Bibi. Fissoo amesema kuwa Bodi imekamilisha hatua ya uchambuzi wa hali halisi ya sekta ya filamu kwa kiasi kikubwa kwa kupitia machapisho mbalimbali pamoja na kuangaia mifano ya nchi zilizopiga hatua katika sekta ya filamu kama vile Afrika ya Kusini, Kenya, Nigeria pamoja na kuzingatia mchango mkubwa kutoka kwa wadau wenyewe ambao wamewezesha kupatikana kwa takwimu muhimu.

  Aidha Muigizaji wa filamu nchini Bw. Saidi Jangala amesema kuwa sera inayoandaliwa iweke maelekezo ya kuzingatia utengenezaji wa filamu zinazobeba historia ya Kitanzania kama vile historia ya Majimaji, pia sera hiyo ianishe mikakati mahsusi ya upatikanaji wa mitaji pamoja na kuipa kipaumbele michezo ya kuigiza kwani michezo hiyo ndiyo chachu kuu ya weledi katika uigizaji.

  Naye Msanii wa filamu nchini Bw. Chiki Mchoma ameiomba kamati ya kuanda sera ya filamu kuhakikisha sera inayoandaliwa inaelekeza wadau wa filamu kuandaliwa mifumo ya elimu pamoja na kuweka misingi ya kufilisi wanaojihusisha na uharamia wa kazi zao na kuwawajibisha wanaonunua kazi zitokanazo na uharamia.

  Hata hivyo mtaalamu wa Kiswahili Pro. Hermas Mwansoko ameitaka kamati ya kuandaa sera ya filamu kuhamasisha matumizi ya lugha ya Kiswahili kwenye filamu zetu kusaidia kuzitofautisha filamu za Kitanzania na zingine.

  Kukamilika kwa sera ya filamu nchini kutabadilisha kabisha taswira nzima ya sekta ya filamu hapa nchini kwani itatoa dira ama mwelekeo wa tasnia. Hii itawezesha kuongezeka kwa fursa za uwekezaji katika tasnia, kuweka mwongozo kuhusu motisha na fursa za mitaji, uzalishaji wa bidhaa bora zenye kuzingatia weledi pamoja na filamu kuangaliwa kama chombo cha kukuza uchumi kwa manufaa kwa Taifa na watanzania wote.

  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa  TIB Corporate Bank , Bw Frank Nyabundege (Kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa nchini, Bw Laurean Bwanakunu ambae taasisi yake ni mteja wa benki hiyo wakati wa hafla fupi ya  kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja Duniani iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dae es Salaam jana ili kutoa fursa kwa wateja wake kutoa mrejesho kuhusiana na huduma zinazotolewa na benki hiyo.
   Wafanyakazi wa  TIB Corporate Bank , wakimpokea mmoja wa wateja wakubwa wa benki hiyo,Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya PMM Estate (2001),  Dr Judith Mhina (kulia) alipohuduhuria  hafla fupi ya  kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja Duniani iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana ili kutoa fursa kwa wateja wake kutoa mrejesho kuhusiana na huduma zinazotolewa na benki hiyo.
   Meneja Uhusiano wa Benki ya TIB Corporate, Margareth Mulenga (kushoto) na Ofisa wa benki hiyo  Jane Magingi  (katikati)  wakisalimiana na mmoja wa wateja wakubwa wa benki hiyo,Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya PMM Estate (2001),  Dr Judith Mhina (kulia) alipohuduhuria  hafla fupi ya  kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja Duniani iliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam jana ili kutoa fursa kwa wateja wake kutoa mrejesho kuhusiana na huduma zinazotolewa na benki hiyo

   

  Katika kuadhimisha wiki ya Huduma kwa wateja Duniani,TIB Corporate Bank imekutana na wateja wake ili kujadili nafasi na mchango wa benki hiyo katika biashara huku ikitoa nafasi kwa wateja na wadau wa benki hiyo kutoa ushauri kuhusiana na huduma zake.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati hafla fupi iliyoambatana na mazungumzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Bw Frank Nyabundege alisema maadhimisho hayo ambayo ni ya kwanza kufanywa na benki hiyo tangu ianzishwe mwaka 2015 yametoa fursa kwa wateja wa benki hiyo kutoa mrejesho kuhusiana na huduma zinazotolewa na benki hiyo.

  “Maadhimisho haya ya wiki moja yalianza Octoba 3 mwaka huu na tunatarajia kuhitimisha Oktoba 7, kweli yamekuwa na manufaa makubwa sana kwetu kwa kuwa tumeweza kukutana na wateja pamoja na wadau wetu mbalimbali ambao wametumia fursa hii kutupatia mrejesho kuhusiana na huduma tunazotoa,’’ alibainisha.

  Bw Nyabundege aliongeza kwamba kwasasa benki hiyo imeboresha zaidi huduma zake ikiwemo suala la mikopo mikubwa na midogo huku akitoa wito kwa mashirika ya umma, watu binafsi na taasisi mbalimbali kujiunga na benki hiyo.

  “Kasi yetu inachochewa zaidi na kauli mbiu ya Mh. Rais John Magufuli ya ‘hapa kazi tu’ inayoenda sambamba na kuhimiza maendeleo ya viwanda na ndio maana miongoni mwa mwa huduma tunazotoa ni pamoja na mikopo kwa ajili ya viwanda,’’ alisema.

  Kwa mujibu wa Bw Nyabundege benki ya TIB Corporate kwa sasa ina wateja takribani 12,000 huku ikitarajia kuvutia zaidi makampuni na taasisi (corporate clients) kutumia benki hiyo, hatua aliyoitaja kuwa itafanikiwa kupitia uwepo wa huduma bora katika benki hiyo.

  Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa nchini, Bw Laurean Bwanakunu ambae taasisi yake ni mteja wa benki hiyo alisema aliipongeza benki hiyo kwa kutoa huduma bora huku akiahidi kuwashawishi mashirika mengine ya umma kujiunga na benki hiyo.

  “Binafsi nafarijika sana kuona kwamba taasisi yangu ambayo ni umma inafanya kazi na taasisi ya fedha ya umma tena kwa ufanisi mkubwa ndio maana naahidi kuwashawishi wenzangu ili waje kwa wingi kuunga mkono jitiahada za serikali katika kuboresha taasisi zake za fedha,’’ alisema.

  Ili kuwaongezea wigo wa kibiashara wateja wake, benki hiyo hivi karibuni iliingia mkataba wa ubia na Benki ya Posta Tanzania (TPB) unaoiwezesha benki hiyo kutoa huduma zake kupitia matawi makubwa 30 na madogo 30 ya benki ya Posta yaliyopo kote nchini.

  Hivi karibuni pia benki hiyo ilifungua tawi lake kwenye ofisi za Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ikilenga kusogeza huduma zake kwa ubora zaidi katika bandari hiyo.

  0 0

  Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) inaendelea na kongamano lake la kimataifa la Wanasayansi watafiti la 30 jijini Dar es Salaam.

  Miongoni mwa mambo mengi ambayo yanajadiliwa ni pamoja na namna ya kuweza kuhamasisha na kusaidia watoto wa kike nchini kuweza kusoma masomo ya sayansi na kuwapa hamasa za kuweza kutimiza ndoto zao kufikia malengo hayo.

  Wanawake wanasayansi watafiti walikutana na kujadili namna yakuweza kusaidia kuleta hamasa kwa watafiti chipukizi na wale walioko shulebni kuweza kuvutiwa na masomo ya sayansi na kusoma kwa bidii.

  Pichani juu ni Mwanasanasi Mtafiti Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Amani Tanga, Dk Theresia Nkya akielezea chagangamoto mbalimbali alizokumbana nazo na namna alivyoweza kuzikabili hadi kutimiza malengo yake.

  Mwisho wa mdahao huo watafiti hao kila mmoja aliweka ahadi yake kimaandishi jinsi ambavyo atasaidia kwa nafasi yake wale ambao wanachipukia na kutaka kuchukua masomo ya sayansi waje kuwa watafiti. 

  Aidha watafiti hao wanasayansi wanawake wametaka kuwepo na mikakati endelevu ya kuweza kuwasaidia wanasayansi chipukizi ili uhamasishaji unaofanyika mashu;leni kuwataka watoto wakike kusoma masomo ya sayansi uwe na mafanikio na kuleta tija. 

  Mwanasayansi Mtafiti kutoka NIMR Makao Makuu, Basiliana Emidi nae akitoa ushuhuda wake kwa yale aliyopitia na anayopitia na ushauri wake kwa wanasayansi wanawake chipukizi.
  Mwanasayansi Mtafiti Mstaafu, Dk Edith Lyimo nae alipata wasaa wa kuzungumza na kuelezea yale aliyokumbana nayo wakati akifanya tafiti mbalimbali na jisni alivyofanya kazi zake na wanaume miaka ya 1980. 

  Dk Nkya aliwataka wanasayansi watafiti chipukizi kuto kata tamaa na badala yake kuhakikisha wanafikia malengo yao kikamilifu.
  Tunu Mwinyimbegu (katikati) ni mmoja kati ya wasichana ambao wanandoto za kuwa wanasayansi watafiti licha ya kuwa alikuwa na vitu vingine alivyokuwa akifikiria kuvifanya katika maisha yake kama vile kuwa msanifu kurasa akieleza ndoto zake na watu wanaompa hamasa. Kulia ni Lucy Mrema na kustoto ni Mary-Angel Jimmy wote kutoka Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mahakama ya Makosa ya Jinai (MICT).
  Mary-Angel Jimmy wote kutoka Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Mahakama ya Makosa ya Jinai (MICT) akielezea ndoto zake za kuwa mwanasayansi na watu wanaomsukuma kutimiza ndoto hizo. 
   Watafiti mbalimbali wakifuatia mada katika mdahalo huo.
  Mkurugenzi Mkuu,Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Dkt Mwele Malecela akifuatilia kwa makini mjadala huo ambapo watafiti wa ngazi mbalimbali walikuwa wakielezea namna ambavyo wanakabiliana na chanagamoto katika kazi zao na jinsi walivyo weza kuvuka vikwazo na kufikia malengo yao.
   Wanafunzi Rozina Robert wa kidato cha sita mchepuo wa Sayansi (PCB) Shule ya Sekondari Tambaza (kulia) na Janeth Vegula wa kidato cha kwanza Sekondari ya Canossa wakifuatilia hamasa waliyokuwa wakipewa.
   Watafiti wakifuatilia
   Wanafunzi Rozina Robert wa kidato cha sita mchepuo wa Sayansi (PCB) Shule ya Sekondari Tambaza akielezea jinsi ambavyo anapenda masomo ya sayansi na anavyotaraji kuwa hapo badae.
   Janeth Vegula wa kidato cha kwanza Sekondari ya Canossa yeye anasema kuwa matarajio yake ni kuwa mfanyabiashara hivyo anataka kusoma biashara ila kwa hamasa aliyoipata hapo anaweza hamia huko maana anasema amefundishwa kucheza mziki kulingana na midundo yake.
   Caroline Senga yeye ni mwanafunsi wa masuala ya Saikolojia na yupo NIMR kwa mafunzo.
   Historia ya Mwanasanasi Mtafiti Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Amani Tanga, Dk Theresia Nkya iliwavutia wengi na kutaka kujua zaidi.
  Watafiti wakimsikiliza Dk Theresia Nkya.


  Mwisho kila mtafiti aliyeshiriki kwa nafasi yake aliahidi nini acha kufanya katika kusaidia wasichana wanaotaka kusoma sayansi na kuwa watafiti.

  0 0  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Oktoba, 2016 amezindua kiwanda cha kusindika matunda kinachomilikiwa na kampuni za kitanzania za Bakhresa katika eneo la Mwandege, Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.

  Kiwanda hicho ni miongoni mwa viwanda 13 vinavyomilikiwa na kampuni za Bakhresa vilivyopo Dar es Salaam na Pwani, kina uwezo wa kusindika tani 350 za matunda kwa siku, kimeajiri karibu wafanyakazi 1,000 na uwekezaji wake umegharimu takribani Shilingi Bilioni 261.

  Akizungumza baada ya kuzindua kiwanda hicho cha kwanza tangu aingie madarakani Rais Magufuli amempongeza Mwenyekiti wa kampuni za Bakhresa Bw. Said Salim Bakhresa kwa uwekezaji huo na amesema Serikali yake itamuunga mkono yeye na wawekezaji wengine ambao wanazalisha ajira na kulipa kodi ipasavyo.

  "Nawapenda wafanyabiashara wanaolipa kodi, nawachukia wafanyabiashara ambao hawalipi kodi, nawapenda wafanyabiashara wanaotengeneza ajira kwa watanzania, wewe umetengeneza ajira za watanzania, na umeendelea kutengeneza ajira kule mjini kwa wauza juisi na wengine, lakini pia unatengeneza ajira kwa wakulima.

  Mtu akitengeneza nanasi zake anajua kuna soko la kupeleka, mtu akilima maembe yake anajua kuna soko la kupeleka" amesema Rais Magufuli.

  Dkt. Magufuli ametoa miezi miwili kwa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) kupeleka umeme katika kiwanda hicho ili kupunguza gharama za uzalishaji zinazosababishwa na kutumia umeme unaozalishwa na majenereta.

  Pia ameahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizotajwa na mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni za Bakhresa Bw. Abubakar Said Salim Bakhresa zikiwemo kupatiwa gesi asilia kwa ajili ya kuendeshea mitambo ya kusindika matunda na urasimu unaosababishwa na wingi wa taasisi zinazodhibiti uzalishaji wa bidhaa.

  Aidha, Rais Magufuli ametoa wito kwa kampuni za Bakhresa kuwekeza katika uzalishaji wa sukari ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa bidhaa hiyo na amesema endapo kampuni hiyo ipo tayari Serikali itatoa eneo la kuzalisha miwa na kujenga kiwanda.

  Mapema akitoa taarifa juu ya hali ya viwanda katika mkoa wa Pwani, Mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo amesema pamoja na viwanda viwili vya kampuni za Bakhresa vilivyopo Mkoani Pwani, Mkoa huo unavyo viwanda vingine 88 ambavyo vinazalisha bidhaa na vingine vipo katika hatua mbalimbali za ujenzi, vikiwemo viwanda viwili vikubwa Afrika Mashariki na Kati ambavyo ni kiwanda cha uzalishaji wa vigae (Tiles) na kiwanda cha kuzalisha nondo na vyuma vya madaraja vitakavyokamilika ifika Desemba mwaka huu.

  Vingozi wengine waliohudhuria uzinduzi huo ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, Mbunge wa Mkuranga Mhe. Abdallah Ulega na Katibu Mkuu wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  06 Oktoba, 2016


  0 0


  0 0

  Na Salum Vuai, MAELEZO

  AGIZO lililotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kati Mashavu Sukwa Said kumtaka daktari na wauguzi wa kituo cha afya Unguja Ukuu kuhamia katika nyumba zilizoko kijijini humo limegonga ukuta.

  Mwandishi wa habari hizi aliyefanya ziara kijijini hapo, aligundua kuwa nyumba hizo mbili ambazo zimekamilika kiujenzi, hazina samani wala vifaa vyengine vya ndani kuwawezesha watendaji hao kuhamia kama walivyoagizwa na kiongozi huyo.

  Kwa mara ya mwisho, Mkuu huyo wa Wilaya alitoa agizo hilo Septemba 9, 2016 wakati alipokuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mabaraza ya vijana kwa shehia za Unguja Ukuu, akitaka ndani ya wiki moja, wafanyakazi hao wawe wameshahamia katika nyumba hizo.

  Wakizungumza na gazeti hili kwa sharti la kutotajwa majina yao, baadhi ya wauguzi walisema kuhamia katika nyumba hizo sio tatizo kwao kama zitakuwa na vifaa ikiwemo vitanda, makabati na vitu vyengine.

  “Sisi tuko hapa kufanya kazi ya kuwahudumia wananchi na tuko tayari kwa hilo lakini iko haja kwa kituo hichi kuwekewa mazingira mazuri, maana hakuna anayeweza kulala au kuweka vitu vyake sakafuni,” walisema.

  Aidha walisema, ingawa wanatakiwa kufungua kituo kwa saa 24 kwa ajili ya kutoa huduma za uzazi, wanashindwa kufanya hivyo kutokana na ukosefu wa dawa za msingi kwa ajili ya mama wajawazito kabla na wakati wa kujifungua.

  Alipoulizwa Mkurugenzi Kinga katika Wizara ya Afya Dk. Fadhil Mohammed Abdalla, alikiri kuwa nyumba hizo kwa sasa haziwezi kukalika kwa kuwa hazina samani ingawa ujenzi wake umekamilika kwa maeneo yote.

  Alisema kwa jumla kuna nyumba 13 hapa Unguja na tisa Pemba zilizojengwa sambamba na vituo vya afya katika maeneo mbalimbali mijini na vijijini kupitia mradi uliofadhiliwa na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Denmark (DANIDA), lakini haukujumuisha samani.

  Tatizo jengine, alitaja kuwa ni uhaba wa wafanyakazi, akisema katika hali ya kawaida, kila kituo kinahitaji watendaji wanane watakaofanya kazi kwa kupishana.

  Alisema daktari na muuguzi ni binadamu ambao hawawezi kutumika kwa saa 24, na kutokana na uhaba huo, utaratibu wa vituo vya afya ni kufunguliwa mapema asubuhi na kufungwa saa 9:30 mchana, tofauti na hospitali.

  “Katika hali kama hii inakuwa vigumu kuwashawishi wafanyakazi wetu kuhamia kwenye nyumba hizo, na pia tunakabiliwa na ukosefu wa fedha za kununua samani kwani zile zinazopatikana katika bajeti zinatumika zaidi katika ununuzi wa vifaa vya hospitali,” alifafanua.

  Kwa hivyo alisema, wizara imekuwa ikitafuta wafadhili wengine kuomba msaada wa kuweka vifaa katika nyumba hizo, ambapo hivi karibuni wamefanikiwa kupata samani kwa kituo cha afya Bumbwini Makoba Wilaya ya Kaskazini ‘B’.

  Aidha alisema, kimsingi nyumba hizo zimekusudiwa zikaliwe na wafanyakazi wa kitengo cha huduma za mama waja wazito na uzazi ambazo zinahitaji uangalizi wa saa 24.

  Kwa sasa, alisema ukosefu wa vifaa vya huduma hizo pamoja na samani za nyumba, unakwamisha mpango wa watendaji kuhamia katika nyumba hizo.

  Alitoa wito kwa wahisani wa ndani na nje, wakiwemo pia viongozi wa majimbo husika, kujitokeza kutoa misaada kwa ajili ya vituo vya afya na nyumba za wafanyakazi, ili kuwaondoshea usumbufu wananchi.

  Alisema azma ya serikali ni kuendelea kuwapatia wananchi wake huduma bora za afya kadiri hali ya kifedha inavyoruhusu, kwani inawategemea katika shughuli za kuleta maendeleo.

  IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO

  5 SEPTEMBA, 2016 .

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, George Simbachawene akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa maagizo kwa Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa kuwa waanze zoezi la kubainisha mipaka ya asili ya maeneo yote na kuyapima na kuhakikisha yana hati.Picha na Eliphace Marwa - Maelezo

  Na. Eliphace Marwa – Maelezo

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, TAMISEMI, George Simbachawene amewaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa waanzishe zoezi la kubainisha mipaka ya asili ya maeneo yote na kuyapima na kuhakikisha yana hati.

  Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Simbachawene amesema kuwa kuna tatizo kubwa la uvamizi wa maeneo ya Shule za Msingi, Sekondari, Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya, hospitali za mikoa na maeneo ya masoko.

  “Kwa kuwa uvamizi huu umefanyika katika maeneo mengi nchini hadi kufikia hatua ya kusababisha mwingiliano usiokubalika kati ya huduma zinazopaswa kutolewa na shughuli zinazofanywa na waliovamia maeneo hayo,” alisema Waziri Simbachawene.

  Akibainisha aina za uvamizi huo Waziri Simbachawene alitaja kuwa ni ujenzi wa nyumba za makazi ndani ya maeneo hayo, ujenzi wa vyumba vya kufanyia biashara kwa kuzunguka maeneo hayo pamoja na uporaji ardhi iliyotengwa na Serikali kwa matumizi ya ujenzi wa shule, Zahanati na Masoko.

  Waziri Simbachawene amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi hili kikamilifu kwenye malaka za Serikali za Mitaa zilizopo kwenye maeneo yao na zoezi hili litekelezwe ndani ya miezi mitatu.

  Aidha Waziri Simbachawene amesema kuwa maendelezo yote yaliyofanywa na yanayotarajia kufanywa hayaruhusiwi na kwa shule za msingi na sekondari zilizoko mjini Halmashauri zihakikishe zinajenga uzio kuzunguka shule hizo.

  “Wananchi waliovamia maeneo ya taasisi hizo waondoke wao wenyewe vinginevyo hatua za kuwaondoa kwa nguvu zitatumika,” alisema Waziri Simbachawene.

  Waziri Simbachawene alitoa wito kwa jamii zinazozunguka maeneo hayo kuhakikisha wanashirikiana na serikali kutoa taarifa kwa mamlaka za serikali za mtaa juu ya uvamizi huo kwa kuonesha alama za asili za mipaka ya maeneo hayo kabla ya kuvamiwa.

older | 1 | .... | 996 | 997 | (Page 998) | 999 | 1000 | .... | 1897 | newer