Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 995 | 996 | (Page 997) | 998 | 999 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio(kushoto) na Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) kwa pamoja wakisaini Mkataba wa Uwekezaji baina ya Taasisi hizo mbili katika Ukumbi wa Mkao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar salaam, Oktoba 4, 2016.
  . Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio wakibadilishana nyaraka mbalimbali za Makubaliano katika Mkataba huo kama inavyoonekana katika picha.
  Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio na Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) wakionesha nyaraka mbalimbali baada ya hafla fupi ya utiwaji saini wa Mkataba wa ujenzi wa Kiwanda kipya cha Viatu.
  Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Mfuko wa Jamii wa PPF wakifuatilia utiwaji saini wa Mkataba wa Uwekezaji.

  Kamishna Jenerali wa Magereza, CGP- John Casmir Minja(kulia) akizungumza katika hafla fupi ya utiwaji saini wa Mkataba wa wa Uwekezaji wa Kiwanda cha Viatu cha Gereza Karanga, Moshi baina ya Shirika la Magereza na Mfuko wa Jamii wa PPF(kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bw. William Erio, Oktober 4, 2016. 

  Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia utiwaji wa Mkataba huo kama inavyoonekana katika picha(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

  ………………………………………………………..

  Na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza,

  Jeshi la Magereza nchini kupitia Shirika lake la uzalishaji mali (Prisons Corporation Sole) limeingia Makubaliano na Mfuko wa Jamii wa PPF katika ujenzi na uboreshaji wa mradi wa Kiwanda cha Viatu cha Gereza Kuu Karanga – Moshi, Mkoani Kilimanjaro.

  Makubaliano hayo yamefanyika leo Jumanne 04 Oktoba, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano ulioko Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es salaam.

  Akizungumza na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wanahabari, Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Minja amesema uhirikiano huo unalenga kuliimarisha Shirika la Magereza ili liweze kujiendesha kibiashara pamoja na kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara.

  Kamishna Jenerali Minja ameongeza kuwa uwekezaji katika kiwanda hicho utalisaidia Jeshi la Magereza kufikia kiu ya kuzalisha bidhaa za ngozi zenye ubora wa hali ya juu na zinazochochea ushindani katika soko la ndani na nje.

  “Naamini uwekezaji huu wa Kiwanda kipya cha Viatu cha Karanga Moshi ni ishara tosha ya kuunga mkono dhamira ya dhati ya Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ya kutaka Tanzania mpya ya Viwanda inawezekana hivyo kutimiza malengo na Dira ya Taifa ya Uchumi wa Viwanda ifikapo mwaka 2025”. Alisema Kamanda Minja.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Jamii wa PPF, Bw. William Erio amesema kuwa PPF ipo tayari kwa dhati kushirikiana na Shirika la Magereza katika mradi huo wa ujenzi wa Kiwanda cha Viatu kwani yapo mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo ya ngozi hapa nchini.

  “Makubaliano haya yanahusisha ujenzi wa Kiwanda kipya cha viatu pamoja na uwekezaji wa mashine za kisasa za kutengenezea bidhaa za ngozi katika Kiwanda cha Viatu cha Karanga Moshi kinachomilikiwa na Jeshi la Magereza”. Alisema Bw. Erio

  Pia, aliongeza kuwa uwekezaji huo utawezesha Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama hapa nchini kununua sare za viatu na vifaa vingine vya bidhaa za ngozi zitakazozalishwa katika Kiwanda hicho badala ya kuagiza nje ya nchi.

  Mkakati wa Jeshi la Magereza hivi sasa ni kuendelea kuboresha maeneo mbalimbali pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo ili kuhakikisha kuwa linafikia ufanisi unaotarajiwa katika utekelezaji wa majukumu yake.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe,Mwigulu  Nchemba wakati alipofika kujitambulisha kwa Rais Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na kulu.]04/10/2016.
  mig2
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe,Mwigulu  Nchemba wakati alipofika kujitambulisha   Ikulu Mjini Zanzibar leo,[Picha na kulu.]04/10/2016.

  0 0

  Mwenyekiti wa Kikosi cha Kuzuia Magenzo Zanzibar (KMKM) Sports Club Kapteni Khatib Khamis Mwadini akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mbio za Kilomita 10 zitakazofanyika tarehe 29 mwezi huu kuanzia Makao Makuu ya kikosi hicho Kibweni na kumalizikia Uwanaja wa Maisara Mjini Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Chama cha riadha Zanzibar Abdulhakim Cosmas akitoa maelekezo juu ya mbio za Kilomita 10 zilizoandaliwa na Kikosi cha KMKM katika Mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Makao Makuu ya Kikosi hicho Kibweni.
  Mwandishi wa Habari wa Star TV Abdalla Pandu akiuliza swali wakati wa mkutano wa maandalizi ya mbio za kilomita 10 zilizoandaliwa na Kikiso cha KMKM.
  Mwenyekiti wa Kamati ya ufundi wa mbio za Kilomita 10 za KMKM Luteni Mlingi Mganga Bwire akijibu maswala yaliyoulizwa na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Kikosi hicho Kibweni Mjini Zanzibar.

  Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akifungua kikao cha pili cha bodi ya barabara kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
  Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kulia akifuatilia makabrasha ya kikao cha bodi ya barabara leo kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi,kulia ni Mbunge wa Jimbo la Mlalo(CCM)Rashid Shangazi,Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM)Adadi Rajabu

  Meneja wa Wakala wa Barabara nchini Tanroad Mkoani Tanga,Mhandisi Alfred Ndumbaro akiwasilisha taarifa ya mpango wa barabara kwenye kikao hicho
  Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe kushoto akibadilishana mawazo na Mbunge wa Jimbo la Handeni,Omari Kigoda kabla ya kuanza kikao cha pili cha bodi ya barabara
  Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM) kulia akiteta jambo na Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Korogwe,Daudi Gao kabla ya kuanza kikao cha bodi ya barabara picha ya kwanza ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM)Marry Chatanda akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso

  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM)Stephen Ngonyani alimaarufu Maji Marefu kulia akiteta jambo wakati wa kikao hicho kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM),Marry Chatanda
  Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso akiteta jambo na Mkuu wa wilaya hiyo,Zainabu Issa wakati wa kikao hicho
  Meneja wa Wakala wa Barabara nchini Tanroad Mkoani Tanga,Mhandisi Alfred Ndumbaro akifuatilia kwa umakini jambo katika kikao cha bodi ya barabara leo
  Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini,(CCM)Omari Kigoda kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe wakati wa kikao cha pili cha bodi ya barabara
  wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,(CCM)Stephen Ngonyani alimaarufu Maji Marefu akipitia maelezo ya makabrasha ya kikao cha bodi ya barabara aliyesimama kulia ni Mbunge wa Jimbo la Lushoto (CCM),Shabani Shekilindi kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe mji(CCM)Marry Chatanda na anayefuata ni Mbunge wa Jimbo la Mkinga (CCM)Dastan Kitandula

  Wajumbe wa Kikao cha Pili cha Bodi ya Barabara kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa,Mkuu wa wilaya ya Pangani,Zainabu Abdalla Issa na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso
  Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku katikati akisikiliza kwa umakini hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wakati akifungua kikao cha pili cha bodi ya barabara
  Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua akipitia maelezo kwenye kabrasha kabla ya kuanza kikao cha bodi ya barabara

  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi wakifuatilia kwa umakini kikao cha bodi ya pili cha barabara leo,Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0

  Mtangazaji wa kipindi hicho cha Take One kilichokuwa kinarushwa na Clouds TV-Zamaradi Mketema.

  Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa onyo kali kwa kituo cha Televisheni cha Clouds sambamba na kukifungia kwa kipindi kwa miezi mitatu kipindi cha Take One kinachorushwa na Kituo hicho.

  Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo Method Mapunda amesema sababu ya kukifungia kipindi hicho ni kutokana na ukiukwaji wa kanuni za utangazaji za mwaka 2005, kwa kumhoji na kurusha kipindi cha mtu kinachohamasisha biashara ya ngono, kuingilia faragha ya mtu na kutolinda maadili ya watoto.

  “Clouds tv inapaswa kukitathimini upya kipindi hicho kwa lengo la kupata njia bora ya kukiendesha na kupeleka mapendekezo TCRA kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kipindi hicho kufunguliwa,”alisema mapunda.

  Mahojiano yaliyopekea kipindi hicho kufungiwa ni kati ya mtangazaji wa kipindi hicho Zamaradi Mketema na Gift Stanford Maarufu kama ‘Gigy Money’ na yalirushwa Agost 09 saa 3.00 usiku na kurudiwa kesho yake saa 7.00

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkr John Pombe Magufuli akimshuhudia mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila akifunua pazia kuashiria kuwekwa kwa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016.PICHA NA IKULU.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkr John Pombe Magufuli akihutubia  katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016.
    Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila akihutubia katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016.
   Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila akipokea zawadi ya picha ya Bandari ya Dar es salaam kutoka kwa mwenyekiti wa Bodi ya TPA  Bw. Ignas Aloys Rubaratuka  katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la Jengo la ONE STOP CENTRE la Mamlaka ya bandari (TPA) jijini Dar es salaam leo Oktoba 4, 2016.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkr John Pombe Magufuli na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Mhe. Joseph Kabila katika sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi la wakipata maelezo toka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko.  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange ameweka jiwe la msingi la jengo la Kituo cha Pamoja cha Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambalo limejengwa kwa lengo la kuwaweka pamoja wadau wote wanaotoa huduma katika bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni juhudi za kuboresha huduma na kupunguza gharama kwa watumiaji wa bandari hiyo.

  Hafla ya uwekaji jiwe la msingi la jengo hilo refu kuliko yote Afrika Mashariki na kati imefanyika leo tarehe 04 Oktoba, 2016 na kushuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

  Akizungumza kabla ya kuwekwa jiwe hilo la msingi Rais Magufuli ameishukuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kuwa mteja mkubwa wa bandari ya Dar es Salaam na amesema aliamua jiwe la msingi la jengo hilo liwekwe na Rais wa Kongo kwa kutambua umuhimu wa nchi yake katika biashara ya bandari ya Dar es Salaam na pia undugu na urafiki wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizi mbili.

  Rais Magufuli amemhakikishia Rais Kabila kuwa kama ambavyo Serikali yake imechukua hatua kadhaa za kurekebisha kasoro zilizokuwepo katika bandari hiyo, itaendelea kujenga mazingira mazuri zaidi kwa wafanyabiashara wa Kongo kutumia bandari hiyo ikiwa ni pamoja na kudhibiti vitendo vya rushwa, kuongeza muda wa kutunza mizigo inayoshushwa kutoka siku 14 hadi siku 30, kuanzisha bandari kavu katika eneo la Ruvu mkoani Pwani na kuinua ari ya wafanyakazi wa bandari kutoa huduma bora.

  "Mhe. Rais Kabila bandari yetu ilifikia mahali pa kuandika rekodi ya kupotea kwa meli kwenye taarifa za bandari, kuna wakati hapa zilipotea meli 60, lakini pia mizigo ya watu ilikuwa inapotea na wafanyabiashara walikuwa wanaombwa rushwa.

  "Kuna baadhi ya wafanyakazi wa bandari waliifanya hii bandari kama mali yao, walikuwa wanaondoka na fedha za rushwa kwenye buti za magari, naomba nikuhakikishie kuwa haya hayatatokea tena, na yakitokea Mhe. Balozi wa Kongo upo hapa njoo unieleze mimi au mwambie Makamu wa Rais au Waziri Mkuu" amesisitiza Rais Magufuli.

  Dkt. Magufuli pia amempongeza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha ujenzi wa jengo hilo la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania na kwamba anaamini litasaidia kuimarisha biashara kati ya Tanzania na Kongo na nchi nyingine zinazotumia bandari ya Dar es Salaam.

  Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange amemshukuru Rais Magufuli kwa heshimu kubwa aliyompa yeye na nchi ya Kongo ya kuweka jiwe la msingi la jengo hilo na amesema kutokana na Tanzania kuchukua hatua madhubuti za kuimarisha huduma za bandari ya Dar es Salaam mizigo ya Kongo itapitia bandari hiyo.

  "Mhe. Rais Magufuli bandari hii ipo Dar es Salaam lakini bandari hii ni ya kwetu sote, mashariki ya Kongo inapakana na nchi nne za Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda lakini asilimia 50 ya mizigo inatoka Tanzania hususani katika bandari ya Dar es Salaam.
  "Nimefurahi pia kuwa katika juhudi za Tanzania kuboresha bandari pia mnaboresha barabara na bandari ndogo ndogo za ziwa Tanganyika, hili ni jambo muhimu kwa sababu sasa mizigo ya Kongo itasafiri kwa urahisi na wafanyabishara wa Kongo waliokuwa wameacha kutumia bandari ya Dar es Salaam watarudi" amesema Rais Kabila.

  Mhe. Joseph Kabila Kabange amesema katika miaka ya 70 na 80 Kongo ilikuwa ikizalisha shaba kiasi cha tani laki 1 lakini hivi sasa inazalisha hadi tani Milioni 1.2 na zote hizi zinategemewa kusafirishwa nje ya nchi kupitia bandari ya Dar es Salaam.

  Ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kununua ndege mbili aina ya Bombardier Q400 na ameunga mkono mpango wa kuanzisha safari za moja kwa moja kati ya Tanzania na Kongo huku akibainisha kuwa nchi yake pia itanunua ndege kwa ajili ya kuimarisha zaidi usafiri wa anga kati ya nchi hizi mbili.

  Mapema kabla ya Marais wote wawili kuzungumza, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mhandisi Deodatus Kakoko alisema jengo hilo lina ghorofa 35, urefu wa meta 157, ukubwa wa meta za mraba 65,115 na ujenzi wake unatarajiwa kukamilika tarehe 31 Desemba, 2016 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 130.

  Rais Kabila ambaye aliingia hapa nchini jana tarehe 03 Oktoba, 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu, jioni ya leo atahudhuria dhifa ya kitaifa katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam iliyoandaliwa kwa ajili yake na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam

  04 Oktoba, 2016
  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mhe. Dkt Kebwe Stephen Kebwe akipokewa na mkuu wa kitengo cha Kuboresha usalama wa jamii ( DCP) Godluck Mongi alipokwenda kufungua mafunzo ya upelelezi kwa askari wa polisi 100. ( katika ni Mkuu wa mafunzo wa Jeshi la Polisi DCP Ally Lugendo. Mafunzo hayo yanafanyika katika chuo cha polisi kidatu yamefadhiliwa na Taasisi ya Hanns Sidel. Picha na Tamimu adam- Jeshi la Polisi.

  ………………..

  Na Tamimu Adam- Jeshi la Polisi.

  Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe amefungua mafunzo ya upelelezi kwa askari 100 kutoka mkoa wa kipolisi kinondoni, mkoa ambao Jeshi la polisi nchini limeuchangua kuwa eneo la mfano katika kutekeleza mpango wa kuboresha usalama wa jamii uliozinduliwa katika viwanja vya Biafra kinondoni jijini Dar es salaam.

  Mafunzo hayo ya upelelezi ya miezi miwili yamefunguliwa katika chuo cha maafisa wa Polisi kidatu kilichopo mkoani morogoro yamefadhiliwa na taasisi ya isiyokuwa ya kiserikali ya Hanns Sidel inayotekeleza miradi mbalimbali hapa nchini.

  Akifungua mafunzo hayo mkuu wa mkoa huo, Dkt Kebwe alisema kuwa amefurahishwa na kitendo cha cha Jeshi la Polisi kuamua kuchangua mkoa wa Morogoro kufanyia mafunzo hayo na pia kumchagua yeye kuwa mgeni rasmi.

  Dkt Kabwe alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi ngumu wanayoifanya ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao na aliwataka askari wanaopata mafunzo hayo katika chuo cha maafisa wa polisi kidatu kutumia weledi na taaluma hiyo watakayoipta kutatua kero za wananchi zinazotokana na ucheleweshaji wa upelelezi .

  “ Nimefurahi sana kusikia kuwa mafunzo haya yanalenga kuharakisha upelelezi na kesi yoyote itakuwa inapelelezwa itakuwa imekamilika ndani ya siku sitini” alisema Dkt Kebwe.

  Mapema akitoa utangulizi wa mafunzo hayo, mkuu wa kitengo cha kinachoratibu utekelezwaji wa mpango wa Jeshi la Polisi wa kuboresha usalama wa jamii, Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Godluck Mongi alisema kuwa mafunzo hayo ya upelelezi yataleta mafanikio makubwa katika mkoa huo wa kinondoni kwa kuharakisha upelelezi wa kesi .

  Aliongeza kuwa lengo la maboresho hayo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2019 askari wote upelelezi wawe wamepata mafunzo hayo na hatimaye kupuza kero ya uhalifu katika mkoa wa kinondoni kwa asilimia 10%

  Naye mwakilishi wa Taasisi inayofadhili mafunzo hayo, Bw. Ombeni mhina alisema kuwa ufadhili wa mafunzo ya upelelezi kwa askari polisi 100 kutoka mkoa wa kipolisi kinondoni ni sehemu ya mpango wa Taasisi ya Hanns Seidel kuunga mkono jitihata za jeshi la polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kwa raia na mali zao kupitia mpango wa kuboresha usalama wa jamii unaoendelea kutekelezwa katika mkoa wa kipolisi kinondoni.

  Aliongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi sitini ambazo jumla ya miradi 100 inaendelea kutekelezwa ikiwa na lengo la kukuza demokrasia, amani na maendeleo duniani kote.

  Kwa upande wake mkuu wa chuo cha Polisi Kidatu kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Andrea Mwang’onda aliwataka wanafunzi wanaopata mafunzo hayo ya upelelezi kuzingatia kile wanachofundishwa na kufuata maadili yote ya uaskari wakati wote watakapokuwa katika mafunzo hayo.

  0 0

   Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi kushoto Seleman Jafo akipena mikono na Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu Wilaya ya Kisarawe,(UWAMAMI) baada ya hafla fupi ya kukabidhiana madawati 150 yenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 15.
   Naibu waziri ofisi ya Rais Tamisemi akizungumza na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kisarawe mara baada ya kupokea msaada wa madawati 150 kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kuondokana na tatizo la kukaa chini (PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

  NA VICTOR MASANGU, KISARAWE.
  NAIBU waziri ofisi ya rais  Tamisemi Selaman Jafo amewaagiza maafisa elimu wa shule za sekondari na msingi hapa nchini  kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea ya kushinda wakiwa wamekaa ofisini tu bila ya kujishughulisha na badala yake wanapaswa kuhakikisha wanakwenda katika maeneo ya kazi hususan ya vijijini kwa ajili ya kuweza kubaini changamoto mbali mbali  zinazoikabili sekta ya elimu ikiwemo upungufu wa madawati, vyoo pamoja na madarasa.

  Jafo ametoa agizo hilo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa madawati 150 kwa niaba ya serikali  katika halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani yaliyotolewa na umoja wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu (UWAMAMI) iliyofanyika wilayani humo.

  Alisema kwamba kuna baadhi ya maafisa elimu hawatambua majukumu yao ipasavyo hivyo  kutokana na agizo lililotolewa na  Rais Dr. John Magufuli la wanafunzi wote kusoma wakiwa wamekaa chini ya madawati atahahakikisha anawavalia njunga watendaji wote  watakaobainika wanakwamisha kwa makusudi  juhudi za serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo.

  “Kwa kweli kuna baadhi ya maafisa elimu wengine wana tabia ya kukaa tu mezani hawaendi kujishughulisha na kuangalia changamoto za vijijini, ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi na kuweka mikakati ya kuboresha sekta ya elimu hapa nchini kwa hiyo ninawaomba sana tucahpe kazi kwa bidii, ili tuweze kuleta maendeleo ya elimu,”alisema Jafo.

  Aidha Jafo baada ya kukabidhiwa msaada huo wa madawati  amebainisha kuwa licha ya utekelezaji wa agizo la rais la utengenezaji wa madawati  kwa halmashauri zote nchini kufikia kiwango cha asilimia 98 hadi sasa, lakini bado kuna  changamoto nyingine ya uhaba ma madarasa,matundu ya vyoo pamoja na nyumba za kuishi walimu.

  Kwa upande wake Katibu mkuu  wa umoja wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu Wilaya ya Kisarawe (UWAMAMI) Ally Kombe alisema wameamua kutoa  madawati hayo yaliyotokana na miti waliyoipanda na kuivuna   kwa lengo la kuweza kuunga juhudi za serikali katika kuhakikisha wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari wanasoma wakiwa kwenye madawati ili kuongeza kiwango cha ufaulu.

  Katibu huyo alifafanua kwamba msaada huo utaweza kuwa mmkombozi mkubwa wa wanafunzi wanaosoma katika wilaya ya kisarawe na kuwaomba wayatunze  kwa hali na mali madawati hayo ii yaweze kutumika katika vizazi vijavyo.
  Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe  Musa Gama amebainisha kuwa licha ya kupatiwa madawati hayo lakini bado wanakabiliwa na upungufu wa madawati mengine   404 hivyo kunahitajika juhudi za makusudi ili kuweza kuondoka na changamoto ya wanafunzi kusoma wakiwa katika mlundikano na baadhi yao kukaa chini ya sakafu.

  CHANGAMOTO ya kuwepo kwa  upungufu wa madawat katika shule za msingi na sekondari katika baadhi ya maeneo bado inaonekana kuwa ni tatizo licha ya agizo lililotolewa na Rais wa awamu ya tano Dr.John Magufuli ya kuziagiza halmashauri zote nchini kuhakikisha inataengeneza madawati ili wanafunzi waondokana na kero ya kusoma wakiwa wamekaa chini ya sakafu.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini  Profesa Justin Ntalikwa (mbele) akiongoza kikao cha kwanza cha kamati ya maandalizi ya  mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi katika  bandari ya  Tanga nchini  Tanzania. Kamati hiyo  inajumuishwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya  Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya  Fedha, Mamlaka ya Mapato  Tanzania (TRA) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (CAG). Lengo la kikao hicho  ni kujadili  maandalizi  ya ujenzi wa bomba hilo.
   Mratibu Miradi ya  Ubia wa Sekta Binafsi na Umma (PPP), Salum Mnuna  kutoka  Wizara ya Nishati na Madini (kulia) akielezea maandalizi ya  ujenzi wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi  Tanzania katika kikao hicho. Kushoto ni Mjiolojia Mkuu kutoka Wizara hiyo, Adam Zuberi.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa akisikiliza majadiliano yaliyokuwa yanaendelea.
   Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani) katika kikao hicho.
  Sehemu ya wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia maelekezo yaliyokuwa yanatolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Profesa Justin Ntalikwa (hayupo pichani) katika kikao hicho.


  0 0

  Na Jovina Bujulu-MAELEZO.

  Ni miaka 17 tangu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere afariki dunia. Ingawa amefariki lakini fikra zake bado zinaishi kama alivyowahi kusema mwanazuoni mmoja Seneta wa zamani wa Arkansas Bruce Holland “viongozi mahiri hawafi wanaishi milele kupitia fikra zao na maisha yao”.

  Kwa kuenzi mchango wa Mwalimu Nyerere kupitia fikra zake mnamo mwaka 2012 watatafiti watatu walibuni wazo la kufanya utafiti kuhusu fikra na falsafa za Mwalimu Nyerere, Wanazuoni hao ni Profesa Issa Shivji, Profesa Saida Yahaya Othman na Dkt. Ng’anzi Kamata.

  Wanazuoni hao walihitimisha utafiti huo kwa kuandika bayografia ya Mwalimu Nyerere ambapo walianzisha kavazi la Mwalimu Nyerere ambalo ni kituo huru kilichoanzishwa mwaka 2014 ndani ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH). Kavazi hilo lilizinduliwa mwaka 2015 na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa.

  Akizungumzia utafiti wa Bayografia (Wasifu) ya Mwalimu Nyerere, Dkt Bashir Ally ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Kavazi hilo alisema kuwa ingawa watu mbali mbali wameandika bayografia ya Mwalimu Nyerere, utafiti uliofanywa na wanazuoni hao watatu ni wa kwanza na wa kipekee uliofanywa kwa kina tofauti na Bayografia za watu wengine.

  Dkt. Bashir anaendelea kusema kwamba wanazuoni hao wanaendelea kukusanya taarifa mbali mbali za Mwalimu Nyerere, na nyaraka nyingi kutoka vyanzo mbali mbali na kuzihifadhi katika Kavazi.

  “Taarifa za nyaraka zinazohusu kazi na maisha ya Mwalimu zinazopewa uhai kwa kujadiliwa na kudadisiwa na watafiti wengine ndani na nje ya nchi hasa vijana kwa sababu zinabeba historia ya nchi”. anaongeza Dkt. Bashir.

  Kavazi la Mwalimu Nyerere limetafsiriwa kama ni mahali maalumu ambapo kumbukumbu za machapisho ya Mwalimu zimekusanywa na watafiti na kuhifadhi pamoja. Kavazi hilo linatoa fursa kwa watafiti kubuni fikra mpya zenye misingi ya fikra za Mwalimu Nyerere.

  Fikra hizo zinatumika kama nyenzo muhimu katika kufanya utafiti za kisayansi zitakazowezazesha nchi kupiga hatua za maendeleo kiuchumi kwa kuongeza ubunifu katika rasilimali kwa lengo la kuwanufaisha wananchi wote.

  Kavazi la Mwalimu ambalo linatumika kama kituo cha kuhifadhia na kuzipa uhai fikra zake limekwisha chapishwa machapisho matatu na mijadala mbalimbali.Machapisho hayo ni ushairi ambao Mwalimu Nyerere aliouandika katika miaka ya 1950 na 1960, uanazuoni wa Mwalimu na insha tatu za kifalsafa na mjadala wa Pan-African Nationalist or Nationalist Pan-Africa.

  Aidha, Kavazi la Mwalimu limefanya Mhadhara tarehe 28, mwezi Septemba, 2016 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Joseph Warioba ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu.Mhadhara huo ulihusu elimu ya juu katika maendeleo ya Afrika na uliambatana na ufunguzi wa hifadhi ya Nyaraka ya Mwalimu Nyerere na uzinduzi wa chapisho la 4 la kavazi.

  Akizungumzia shughuli za Kavazi la Mwalimu Dkt. Bashir anasema kwamba ni pamoja na kuhifadhi nyaraka zilizokusanywa na waandishi wa bayografia ya Mwalimu Nyerere ili zitumiwe na watafiti, kutoa nafasi ya mjadala ya kizuoni na kimkakati juu ya masuala muhimu ya maendeleo ya jamii, na kuandaa na kuendesha mafunzo ya nadharia na mbinu za utafiti wa masuala ya maendeleo ya jamii.

  Aidha, Dkt. Bashir anasema kwamba Kavazi la Mwalimu linatoa mafunzo kwa wanazuoni na wasomi chipukizi waliopo kwenye taasisi za elimu ya juu na asasi zisizo za kiserikali.“Kavazi limekwishafanya mafunzo kwa vijana ambayo yaliangalia rasilimali, dhana, na nadharia mbalimbali na mbinu za kiutafiti ambazo zinawapa maarifa na uwezo wa kuendeleza utafiti”. Anasema Dkt Bashir.

  Wafadhili wa Kavazi la Mwalimu ni pamoja na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambao walichangia fedha za awali, Taasisi ya Kijerumani ya Rossa Luxemburg na watu mbalimbali. Kavazi la Mwalimu limeanzisha mfuko maalumu (Endoworment Fund) ambao utazalisha fedha za kujiendesha, hata hivyo wananchi wanaombwa kuendelea kujitokeza kuchangia mfuko huo ili kukuza na kuendeleza kazi za Kavazi.

  Akizungumzia mapokeo ya Kavazi la Mwalimu Dkt. Bashir anasema ni mazuri kwa sababu viongozi mbalimbali wamekwisha tembelea Kavazi hilo wakiwemo Marais Wastaafu Mhe. Benjamini Mkapa, Mhe. Ally Hassan Mwinyi na Mkurugenzi wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Mzee Joseph Butiku na ujumbe wake.

  Viongozi wengine waliotembelea Kavazi hilo ni pamoja na Mawaziri Wakuu wastaafu Mhe Cleopa David Msuya, Jaji Joseph Sinde Warioba, Dkt Salim Ahmed Salim na wanasiasa mbalimbali wakiwemo waliofanya kazi na Mwalimu Nyerere ambao ni Mze Geroge Kahama na Mzee Kingunge Ngombale Mwiru familia ya Mwalimu Nyerere pamoja na wananchi mbalimbali.

  Alisifu ushirikiano wanaoupata kutoka Makumbusho ya Taifa, Taasisi ya Mwalimu Nyerere na baadhi ya vyombo vya habari kuwa umewawezesha kufanya kazi yao kwa ufanisi, hasa kukusanya nyaraka na taarifa za Mwalimu Nyerere.

  Naye Mkurugenzi wa Kavazi la Mwalimu, Profesa Issa Shivji ametoa wito kwa viongozi na wanasiasa mbalimbali waliofanya kazi na Mwalimu Nyerere kupeleka nyaraka zao katika Kavazi kwajili ya kuhifadhiwa na kufanyiwa tafiti mbali mbali.

  Dkt. Bashir anamalizia kwa kuwakaribisha wananchi kutembelea Kavazi ili kujisomea nyaraka na kazi za Mwalimu na kufahamu historia ya nchi yetu. Aidha anasema kuwa hakuna tozo yoyote kwa wananchi wanaokwenda kutembelea Kavazi hilo.

  Ama kweli Mwalimu Nyerere alikuwa Mwanafalsafa hodari na makini sana ambaye mawazo au falsafa zake zitakumbukwa vizazi hadi vizazi hasa suala la kutetea wanyonge, usawa wa binadamu na upendo kwa wote bila kujali itikadi, dini wala kabila la mtu.

  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu) Jenista Mhagama akifanya mazungumzo na Mke wa baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam, leo tarehe 5 Oktoba 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI-Afya Dkt. Zainabu Chaula akisalimiana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea Wizarani hapo mapema jana Oktoba 4.2016Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI-Afya Dkt. Zainabu Chaula akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya alipomtembelea ofisini kwake Wizarani jana Oktoba 4.2016.Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI-Afya Dkt. Zainabu Chaula akifuatiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki UlisubisyaPicha ya pamoja: Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI-Afya Dkt. Zainabu Chaula akifuatiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Mpoki Ulisubisya na Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Mh. Siaba Nkinga.

  0 0

   Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi akimkabidhi Underson Simon bendera ya Taifa ishara ya kumtaka akaitangaze vema Tanzania nchini Marekani.
  Underson Simon (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa TTB Bi devota Mdachi (wa pili kushoto) na baadhi ya maafisa aliofuatana nao katika ofisi za TTB muda mfupi baada ya kukabidhiwa bendera ya Tanzania na vielelezo mbalimbali vya utalii.

  Na: Geofrey Tengeneza 

  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imemtaka kijana wa kitanzania ambaye pia ni mchezaji wa mpira wa kikapu Underson Simon (19) kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii nchini Marekani kwa lengo la kuvutia watalii wengi zaidi kuitembelea Tanzania.

  Underson ambaye ni tunda la kituo cha Michezo cha Jakaya Mrisho Kikwete Youth Park cha jijini Dar es salaam amepata udhamini wa masomo kwenda kusoma shahada ya kwanza ya sayansi ya Kompyuta katika Chuo Kikuu cha Georgia University kilichoko Atlanta Georgia nchini Marekani. 

  Akizungumza wakati wa kumuaga Underson ofisini kwake jijini Dar esalaam, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi mchezaji huyo anayechipukia wa mpira wa kikapu nchini anayechezea timu mpira wa kikapu ya vijana (vijana Busketball Club) pamoja na kumtaka ajitahidi katika masomo yake, lakini pia amemtaka atumie fursa hiyo na ile ya kushiriki katika mashindano mbalimbali akiwa na timu yake ya chuo kikuu cha Georgia katika mchezo wa kikapu kuvitangaza vivutio vyetu vya utalii.

  “ Peperusha vema bendera ya nchi yetu na tumia kila jukwaa utakalopata ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii kuitangaza Tanzania kama eneo bora la utalii duniani” alisema Bi Mdachi na kuongeza kuwa TTB inakusudia kuanza mchakato wa kumpa heshima ya kuwa Balozi wa heshima wa Utalii wa Tanzania.

  Mkurugenzi huyo wa TTB alimkabidhi mchezaji huyo wa mpira wa kikapu nchini, bendera ya Taifa na vielelezo kadhaa vinavyoelezea utalii wa Tanzania ili visaidie kumjengea uelewa zaidi kuhusu vivutio vya utalii vya Tanzania.

  Kwa upande wake kijana huyo Underson Simon alielezea kufurahishwa kwake kupata nafasi hiyo lakini pia kutambuliwa na TTB kama mmoja wa wanamichezo wa kitanzania wanaoweza kuvitangaza vema vivutio vyetu vya  utalii nje ya nchi na hivyo kuchangia kukuza sekta ya utalii. 

  Naye mwalimu mwandamizi (kocha) wa mpira wa kikapu wa kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete Bw. Bahati Mgunda amesema kituo chake kinajivunia mafanikio hayo ya mmoja wa wachezaji wao kupata ufadhili huo wa masomo ambao umetokana hasa na umahiri wake katika mchezo huo. 

  Simon ameondoka saa 9.00 alfajiri ya leo kwa shirika la ndege la Uturuki kuelekea nchini Marekani tayari kujiunga na chuo kikuu hicho cha Georgia.


  0 0

  Na Lydia Churi- Mahakama ya Tanzania

  Mahakama ya Tanzania inakusudia kushirikiana na Australia ya Kusini katika teknolojia za kuendesha mashauri mahakamani ili kutekeleza jukumu lake la msingi la kutoa Haki sawa kwa wote na kwa wakati.

  Akizungumzia ziara ya Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini Mheshimiwa Christopher Kourakis iliyoanza leo nchini, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman amesema ziara ya kiongozi huyo inalenga kuimarisha na kujenga ushirikiano katika maeneo matatu likiwemo eneo la teknolojia ya kuendesha mashauri mahakamani.

  Alisema Australia ya kusini inaendesha mashauri mahakamani kwa kutumia teknolojia ya kisasa hivyo Mahakama ya Tanzania haina budi kuhama kutoka mifumo ya kuendesha mahakama kwa mkono kwenda kwenye teknolojia ya kidijiti

  Alisema Mahakama inakusudia kuwapeleka wasajili na watendaji wa mahakama nchini Australia ya kusini ili wakajifunze mifumo hiyo kwa ajili ya kuanza kuitumia kuendeshea mahakama za Tanzania.

  Aliyataja maeneo mengine ya ushirikiano kuwa ni eneo la utoaji wa mafunzo kwa Majaji, Mahakimu na Wasajili wa Mahakama ya Tanzania huku akisema eneo la tatu ni la namna ya kuanzisha Kada mpya ya Wapiga Chapa Maalum wa Mahakama watakaokuwa wakitumia mashine ndogo inayochapa wakati mashauri yakiendelea Mahakamani.

  Akiielezea kada hiyo mpya, Jaji Mkuu alisema itawezesha kupatikana kwa nakala za mashauri ndani ya siku moja na kwamba watumishi hao ni tofauti na makatibu Muhtasi ambapo mishahara yao itakuwa ni mikubwa kuliko ile ya Makatibu Muhtasi.

  Naye Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini alisema Mahakama za nchini kwake zinaendesha mashauri kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya kidijiti hivyo nchi yake itashirikiana na Tanzania ili nayo iweze kuendesha mashauri mahakamani kwa kutumia teknolojia ya kisasa.

  Akizungumzia kuhusu adhabu ya kifo kwa watuhumiwa wa kesi za mauaji nchini Australia ya Kusini, Mheshimiwa Kourakis alisema adhabu hiyo iliondolewa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo msukumo wa Haki za Binadamu.

  Alisema nchi yake pia ina mfumo ambapo endapo mtuhumiwa wa mauaji atakiri kosa ndani ya wiki sita basi atapunguziwa adhabu yake kwa asilimia 40. Aliongeza kuwa adhabu ya kifo nchini kwake ni kifungo cha maisha na endapo atakiri kosa atapunguziwa adhabu. Kiwango cha chini cha adhabu ya kifo ni kifungo cha miaka 20 jela.

  Jaji Mkuu wa Australia ya Kusini leo ameanza ziara ya kikazi ya siku tatu nchini ambapo ametembelea Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu na pia anatarajia kutembelea Mahakama ya Zanzibar.

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu taasisi za Serikali kutekeleza agizo la kuhuisha taarifa na huduma katika Tovuti zao mapema kabla ya mwisho wa mwezi huu katika mkutano uliofanyika Ofisi za Wakala ya Serikali Mtandao (EGA) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto.
  Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi hao leo jijini Dar es Salaam, kuhusu taasisi za umma kuhuisha taarifa katika Tovuti zao. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas akiwaonyesha waandishi wa habari mwongozo wa utengenezaji wa Tovuti za Serikali wakati wa mkutano wake na waandishi hao leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao Bibi. Susan Mshakangoto.
  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wao na Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas na Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala wa Serikali Mtandao (EGA) Bibi. Suzan Mshakangoto (hawapo pichani). Mkutano huo ulihusu kuzikumbusha Taasisi za umma kuhuisha taarifa katika Tovuti zao leo Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari, MAELEZO Bw. Hassan Abbas akielezea namna ambazo mitandao ya kijamii inavyo tumika kurahisisha kufikisha taarifa za Serikali kwa jamii na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu taasisi za umma leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Wakala ya Serikali Mtandao, Bibi. Susan Mshakangoto. Mkurugenzi huyo alitolea mfano wa akaunti ya Tweeter ya, Msemaji wa Serikali@ TZ_Msemaji Mkuu. Mwananchi anaweza kuifuata akaunti hiyo kwa kutafuta “Msemaji Mkuu wa Serikali on Twitter”.

  Picha na: Frank Shija, MAELEZO

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa na Askari Magereza wa Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga baada ya kulitembelea Oktoba  5, 2016. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taifa wa Parole Augusine Mrema, kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma na aliyekaa kushoto ni Mkuu wa Magereza wa mkoa wa Dodoma, SACP Kirumbi.
  gere2
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mofisa wa Magereza wakati alipotembelea Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga  mjini Dodoma Oktoba 5, 2016.
  gere3
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa na Askari Magereza wa Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga baada ya kulitembelea Oktoba  5, 2016. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taifa wa Parole Augustine Mrema, kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma  Jordan Rugimbana  na aliyekaa kushoto ni Mkuu wa Magereza wa mkoa wa Dodoma, SACP Kirumbi. Aliyekaa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme.
  gere4
  gere5gere6
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitoka kwenye Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga wakati alipolitembelea mjini Dodoma Oktoba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  gere8
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa na Askari Magereza wa Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga baada ya kulitembelea Oktoba  5, 2016. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taifa wa Parole Augustine Mrema, kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma  Jordan Rugimbana  na aliyekaa kushoto ni Mkuu wa Magereza wa mkoa wa Dodoma, SACP Kirumbi. Aliyekaa kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  gere9
  Askari Magereza wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kati alipowasilimia baada ya kutembelea Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma Isanga mjini Dodoma Oktoba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  gere10
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mofisa wa Magereza wakati alipotembelea Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga  mjini Dodoma Oktoba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Maofisa na Askari Magereza wa Gereza Kuu la Mkoa wa Dodoma la Isanga baada ya kulitembelea Oktoba  5, 2016. Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Taifa wa Parole Augusine Mrema, kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Dodoma na aliyekaa kushoto ni Mkuu wa Magereza wa mkoa wa Dodoma, SACP Kirumbi.
   
  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw. Jordan Rugimbana kuchunguza ni kwa nini Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Bw Antonino Kilumbi amekwenda kutengeneza madawati kwa watu binafsi  badala ya karakana ya Magereza kama  ilivyokusudiwa na Serikali.

  Magereza mkoa wa Dodoma ilipewa sh. milioni 24 na Serikali ili kutengeneza madawati 480 na kila moja lilitakiwa kugharimu sh. 50,000. Uongozi wa gereza hilo ulitengeneza madawati hayo kwa watu binafsi ambapo dawa moja limegharimu sh. 70,000.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Oktoba 5, 2016) wakati alipotembelea Gereza la Isanga mkoani Dodoma akiwa kwenye ziara ya kukagua maeneo yanayotoa huduma za jamii mjini hapa.

  Amesema kama gereza hilo halikuwa na uwezo wa kutengeneza madawati hayo kwa nini kazi hiyo wasingeipeleka kwenye taasisi nyingine ya umma, hivyo amemtaka Mkuu wa Mkoa Bw. Rugimbana kufuatilia ziada ya sh. 20,000 kwenye utengenezaji wa kila dawati inatoka wapi na inakwenda kwa nani.

  “Nimesikia kwamba mnawachangisha askari kiasi kilichoongezeka kwenye utengenezaji wa madawati hayo. Ni marufuku askari kutoa fedha mifukoni mwao kulipia shughuli za Serikali,” amesisitiza.

  Serikali imeandaa utaratibu wa kuwezesha taasisi zake zikiwemo za kijeshi kwa kuzipa kazi ya kutengeneza bidhaa na miundombinu mbalimbali ikiwemo madawati ili kuyaongezea tija aliongeza

  Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma Bw. Kilumbi amesema waliamua kupeleka kazi hiyo kwa watu binafsi kwa sababu hawana vifaa.

  Aidha, Waziri Mkuu amemtaka mkuu huyo wa magereza mkoa kuimarisha kitengo cha ufundi seremala na kuhakikisha anatumia vizuri nguvu kazi aliyonayo katika kuzalisha bidhaa mbalimbali.

  Kuhusu changamoto ya makazi kwa askari Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua na imeweka mkakati wa wa ujenzi na kwa upande wa askari Magereza wataanzia kwa mkoa wa Dodoma.

  Wakati huo huo Waziri Mkuu ametembelea maduka ya kuuzia bidhaa mbalimbali zikiwemo nguo katika maeneo ya soko la Sabasaba na Majengo.

   IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU
  S. L. P. 980,
  DODOMA.
  JUMATANO, OKTOBA 05, 2016

  0 0

  Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

  Serikali inaandaa mtaala wa kuongeza ustadi na ujuzi kwa watanzania  wanaofanya kazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati.

  Hayo yamebainishwa  leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Abdallah Kilima alipokuwa akikanusha habari iliyotolewa na Gazeti la Tanzania Mpya la Oktoba 04,Mwaka huu,Toleo namba 23 katika Ukurasa wa 4, lililokuwa na habari iliyosema “Watanzania wateswa nchini Oman na wengine hunyofolewa figo zao na kupewa ndugu wa  waajiri wenye mahitaji”.

  Kutokana na hayo Balozi Kilima  alifafanua kuwa habari hiyo haina ukweli wowote,isipokuwa ni maoni binafsi ya mwandishi  wa  gazeti hilo na hayawakilishi msimamo wa Serikali kuhusu masula ya wafanyakazi za ndani wakitanzania nchini Omani.

  Aidha, Balozi huyo amesisitiza kuwa nia ya Serikali ya kuanzisha mtaala huo ni katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakumba nazo watanzania wanaofanyakazi za ndani nchini Oman.

  “Serikali imeazimia kutumia Chuo cha Ufundi Stadi (VETA)  ili kutoa mtaala utakaosaidia kutoa mafunzo kwa maana ya utaratibu na utamaduni wa nchi wanazokwenda kufanyakazi, ili kusaidia  watanzania kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu kazi husika na changamoto zake kabla ya kukubali kufanyakazi hizo,” alisema Balozi Kilima

  Sambamba na hilo Serikali imeendelea kuwataka watanzania kufuata utaratibu kabla ya kwenda kufanyakazi katika nchi hizo kwa kutumia mawakala rasmi wa ajira walioandikishwa na mamlaka husika pamoja na kuwepo mkataba wa ajira unaotambuliwa na Mamlaka za nchi wanazookwenda  ili kuepuka usumbufu na changamoto wanazoweza kuzipata ikiwemo kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili.

  Balozi Mwilima ameongoza kuwa  katika kupata suluhisho la kudumu  katika  kuwasaidia watanzania kupata fursa za ajira nje ya nchi,Wizara kwa kushiririkiana na wadau  imeendelea kufanya jitihada  za kusaini Mikataba ya Ushirikiano katika Sekta ya ajira na kazi baina ya Serikali ya Tanzania na nchi mbalimbali.

  Watanzania  5600 wanakadiriwa  kufanyakazi katika kada za madaktari, walimu, wauguzi, wahadhiri, wapishi, wahudumu wa mashambani na bustani na watumishi wa nyumbani, na kati ya hao karibu watanzania 200 ndio wanaofanyakazi za ndani katika nchi za Mashariki ya Kati.

  0 0

   Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania,  Carter Luoh (kulia) akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Kushoto ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Bw. Gaspa Ngowi. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.
   Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Gaspa Ngowi (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luoh. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.
   Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo, Gaspa Ngowi akizungumza na wateja walipotembelea kitengo cha huduma kwa wateja wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.
   Meneja wa Ufundi wa StarTimes Tanzania, Yusuph Baracha (kushoto) akiwaelekeza wateja walipotembelea chumba cha kurushia matangazo ya chaneli mbalimbali zinazopatikana kupitia king’amuzi cha kampuni hiyo  wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Life.
   Baadhi ya wafanyakazi wa StarTimes Kitengo cha Huduma kwa Wateja wakiwahudumia wateja kupitia njia ya simu. Wateja wa StarTimes pamoja na waandishi wa habari walipata fursa ya kutembelea kitengo hicho pamoja na cha kurushia matangazo ya chaneli mbalimbali zinazopatikana kupitia king’amuzi cha kampuni hiyo  wakati wa hafla fupi kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja. Katika kuadhimisha wiki hiyo StarTimes imezindua chaneli mpya tatu ambazo ni ST Bollywood Africa, ST Bollywood na FOX Lif


  Na Dotto Mwaibale

  KATIKA kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja inayosherehekewa duniani kote na makampuni na taasisi mbalimbali katika wiki ya kwanza ya mwezi Oktoba, StarTimes wamewaletea wateja wake chaneli mpya ambazo zitanogesha zaidi burudani.

  Akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa StarTimes Tanzania, Carter Luoh amebainisha kuwa wanafanya jitihada za kutosha kuhakikisha mkoa yote nchini inafikiwa na huduma zake.

  “StarTimes inajivunia kuwa kinara katika huduma za matangazo ya dijitali nchini ikiwa na wateja zaidi ya milioni moja nchi nzima. Mpaka hivi sasa tumekwishaifikia mikoa takribani 17 ambapo hivi karibuni tumezindua huduma zetu mkoani Kigoma na tukiwa mbioni kuzindua na Mtwara pia. 

  Mbali na mikoa hiyo lengo kuu ni kuhakikisha kuwa nchi nzima inafikiwa na huduma zetu ambapo tutahakikisha tunasambaza maduka na ofisi zetu. Zote hizi ni jitihada za dhati ambazo kampuni iliahidi katika kuhakikisha kila nyumba ya mtanzania inafikiwa na huduma za matangazo ya dijitali. Hivyo basi tumekuwa tukijitahidi kukamilisha dhamira hiyo huduma na bidhaa zetu zinapatikana kwa bei nafuu ambayo hata mtanzania wa kipato cha chini anaweza kumudu.” Alisema Luoh

  “StarTimes inajivunia kuwa na watoa huduma takribani 300 ambao wapo tayari kuwahudumia wateja muda wote kupitia nambari 0764 700 800. Mbali na watoa huduma hao pia kupitia ofisi zetu na za mawakala wetu wateja pia wanahudumiwa katika ubora ule ule katika mikoa yote tunayopatikana. Pia tunayohuduma ya baada ya mauzo ambapo tunao mafundi waliotapakaa katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kuwafuata wateja walipo. Hii yote inadhihirisha na kwa namna gani tunavyowajali wateja wetu.” Alihitimisha Mkurugenzi huyo wa Uendeshaji

  Naye kwa upande wake Meneja wa Huduma kwa Wateja wa kampuni hiyo  Gaspa Ngowi ameongezea kuwa ndani ya mwezi huu wamewaletea wateja wao chaneli mpya ambazo ni ST Bollywood, ST Bolyywood Africa na FOX Life huku nyinginezo zikiwa njiani kuja rasmi.

  “Wiki hii ni maalumu kwa wateja wetu hususani katika kuonyesha kuthamini mchango wao katika kuunga mkono huduma zetu. StarTimes inapenda kusherehekea wiki ya huduma kwa wateja kwa kuleta chaneli mpya katika ving’amuzi vyake ambazo ni ST Bollywood, ST Bolyywood Africa ambazo zinaonyesha filamu kali na mpya za kihindi huku kukiwa na chaguo kwa mtazamaji kuchagua lugha anayoipenda ikiwemo Kiswahili; na FOX Life ambayo yenyewe inaonyesha filamu na mfululizo wa tamthiliya za runinga.” Alisema  Ngowi

  Meneja huyo wa Huduma kwa Wateja wa StarTimes alihitimisha kwa kusema kuwa, “Mbali  na chaneli mpya pia tumewaletea bidhaa za runinga na projekta ambazo ndani yake kuna ving’amuzi ambapo wanaweza kutazama chaneli na vipindi mbalimbali. Hivyo basi wateja wakae mkao wa kula ili kujipatia bidhaa hizi ziliunganishwa na mfumo wa dijitali moja kwa moja.”

  Katika kusherehekea wiki hii ya huduma kwa wateja, StarTimes imeadhimisha kwa kuwakaribisha wateja kutembelea ofisi zake ili kujionea jinsi wanavyoendesha shughuli zao.

  Wateja hao walipata pia fursa ya kutembelea kitengo cha huduma kwa wateja ambapo waliweza kuonana na kuzungumza moja kwa moja na watoa huduma hao, pamoja na chumba cha kurushia matangazo ya chaneli mbalimbali zinazopatikana ndani ya king’amuzi cha kampuni hiyo.

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu akikagua mashine ya ukaguzi wa mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal One kuangalia ufanisi wa mashine hizo.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu akiangalia ufanisi wa mashine za kukagulia mizigo katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) Terminal One na kukuta zinafanya kazi vizuri. Aliyekaa ni Mwendeshaji wa Mashine hizo kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege TAA-Grace Jonathan.   Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange leo tarehe 05 Oktoba, 2016 amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini na kurejea nchini kwake.

  Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Rais Kabila ameagwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

  Viongozi wengine walioungana na Rais Magufuli wakati wa kumuaga Rais Kabila ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mawaziri, Mabalozi wa nchi mbalimbali, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Paul Makonda na Viongozi wa Dini.

  Katika hatua nyingine, mara baada ya kuondoka kwa Rais Kabila, Rais Magufuli amefanya ukaguzi wa kushitukiza katika sehemu ya kukagulia mizigo na abiria ya uwanja huo upande wa Terminal One ambako Mwezi Mei mwaka huu alitembelea kwa kushitukiza na kubaini kuwa mashine za ukaguzi (Scanners) zilikuwa hazifanyi kazi.

  Mara hii Rais Magufuli amebaini kuwa mashine hizo zinafanya kazi, baada ya kujionea yeye mwenyewe uhalisia wa namna mizigo inavyokaguliwa.Hata hivyo amemuagiza Mkurugenzi wa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Bw. Paul Rwegasha kuwachukulia hatua za kinidhamu maafisa wawili  waliotoa taarifa za uongo pindi alipofanya ukaguzi wa kushitukiza mara ya kwanza.

  "Leo kweli mashine zinafanya kazi na mimi nimeona lakini wale walionidanganya mara ya kwanza nilipokuja, Mkurugenzi hakikisha unawachukulia hatua"amesisitiza Dkt. Magufuli.


  Gerson Msigwa
  Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
  Dar es Salaam
  05 Oktoba, 2016
   

older | 1 | .... | 995 | 996 | (Page 997) | 998 | 999 | .... | 1898 | newer