Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46366 articles
Browse latest View live

RAIS DKT. MAGUFULI AMPOKEA RAIS WA DRC MH. JOSEPH KABILA LEO

$
0
0

Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mh. Joseph Kabila wakipokea heshima za kijeshu muda mfupi baara ya Mh. Kabila kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere,  Jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mh. Joseph Kabila akikagua gwaride mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere,  Jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2016.
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli (wa pili kulia) na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mh. Joseph Kabila wakiangalia burudani ya ngoma, muda mfupi baara ya Mh. Kabila kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere,  Jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2016. Katikati ni Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan.

picha zaidi zitawajia baadae kidogo.

MAKAMU WA RAIS WA CUBA AMALIZA ZIARA YA SIKU TATU YA KIKAZI NCHINI

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akiagana na mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ambaye amemaliza ziara ya siku 3 ya kikazi nchini.

.....................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ameondoka nchini mchana huu baada ya kumaliza ziara ya kiazi ya siku tatu kwa mwaliko wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Lengo la ziara hiyo ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ni kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba hasa katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya,utamaduni,michezo na utalii.

Katika sekta ya utalii, Serikali ya Cuba imeahidi kuisaidia Tanzania katika kuendeleza utalii katika fukwe pamoja na kubadilishana uzoefu na wataalamu wa hapa nchini katika sekta hiyo ili kusaidia kuongeza pato la taifa kupitia shughuli za utalii nchini.

Aidha kwenye sekta ya viwanda Tanzania na Cuba zimekubaliana kushirikiana katika ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kutengenezea madawa ya binadamu nchini.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba Salvador Antonio Valdes Mesa ameagwa na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kuhitimisha ziara yake nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akimsindikiza mgeni wake Makamu wa Rais wa Cuba Mhe. Salvador Antonio Valdes Mesa ambaye amemaliza ziara ya siku 3 ya kikazi nchini.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

WANACHAMA WA PSPF WAPONGEZA HUDUMA ZA HARAKA NA BORA

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, (kushoto), akimsikiliza Mwanachama wa Mfuko huo, Margareth Mpunga, aliyefika kuhudumiwa wakati wa Wiki ya PSPF kwenye kitengo cha huduma kwa wateja makao makuu ya Mfuko jijini Dar es Salaam, Oktoba 4, 2016. Wakurugenzi na Mameneja wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu, waliungana nawafanyakazi wa kitengo hicho kuwahudumia wateja ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za wiki hiyo inayofikia kilele Oktoba 7
Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa wateja cha PSPF, Laila Maghimbi, (kushoto), akimuhudumia mteja ofisini kwake Oktoba 4, 2016
Judith Mtweve wa kitengo cha mawasiliano (call centre), akiwa kazini
Meneja wa Kitengo cha Hudma kwa Wateja, akimsikiliza mteja

Mkurugenzi Mkuu, akimsikiliza kwa makini mteja

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

WANACHAMA wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, wamepongeza uongozi wa Mfuko huo, kwa huduma bora na za haraka katika kuhudumia wateja.Hayo wameyasema Oktoba 4, 2016 wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, kwenye makao makuu ya Mfuko huo jengo la Jubilee Towers jijini Dar es Salaam.

“Nimefurahishwa na huduma zilizokuwa zikitolewa, kwani nilipofika nimepokelewa na kuhudumiwa haraka, sikuchelewa, kilichonileta ni kuwasilisha risiti za benki za michango yangu,” alisema Mwanachama wa PSPF kupitia mpango wa uchangiaji wa Hiari,(PSS), Hamid Maxan Haidary.

Hata hivyo mwanachama huyo alishauri, Mfuko ufanye juhudi kuelimisha umma hususan wajasiariamali kama yeye wajiunge nao kwani anahakika wengi watajiunga.

“Wafanyakazi wapelekwa huko kwenye kata, najua zipo juhudi kubwa za kufanya matangazo kwenye radio/tv, magazeti na mitandao ya kijamii, lakini sio vibaya wafike wenyewe mitaani kutoa elimu zaidi.” Alishauri.

“Mimi kama mtu mwenye kipato cha chini, nilikuwa Napata shida sana inapokuja swala la kuugua au kuuguliwa na watoto au mke wangu, lakini hivi sasa hilo sio tatizo tena kwangu, kwani kupitia bima ya afya ambayo nimepata baada ya kujiunga na PSPF, ninatibiwa bila wasiwasi.” Alifafanua Haidary.

Mwanachama mwingine wa Mfuko huo ambaye ni mstaafu, Peter Protus Mbele (64), alielezea kufurahishwa kwake na faida anayopata kutoka PSPF yeye kama mstaafu, ambapo licha ya kuchukua pensehni ya kila mwezi, ameweza pia kukopa fedha benki na hivyo kuboresha shughuli zake.

“Kwa ujumla nafurahia huduma za PSPF, nimeweza kupata mkopo benki, panatokea mara chache kuchelewa kwa palipo ya mwezi ya pensheni, lakini mimi nachukulia kama ni changamoto ya kawaida, kwani hata nyumbani mama anaweza kuchelewa kutayarisha chakula, pengine kwa sababu kuni ni mbichi au mkaa hauko vizuri lakini hatimaye chakula kinawiza na mnakula,” alisema.

Naye Devotha R. Kayumbe, aliusifu uongozi wa PSPF kwa kuwajali wateja. “Nimejisikia raha kuhudumiwa na Mkurugenzi Mkuu, hii inaonyesha jinsi watumishi wa umma wanavyowajibika na kwenda sambamba na kasi dhana ya Hapa Kazi Tu.”. Alisema Kayumbe.

Naye Naomi Albert Duma, ambaye alifika kwa nia ya kujiunga na Mfuko kupitia Uchangiaji wa Hiari, (PSS), alisema, ameridhishwa na huduma aliyopata kwani amehudumiwa kwa haraka na hakutegemea kama angechukua muda mfupi kumaliza kile kilichomleta.

“Nimefika kujiunga na PSS, tayari nimehudumiwa na sasa naondoka.”Alisema .

Akizungumzia Wiki ya Huduma kwa wateja, Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja cha PSPF, Laila Maghimbi, alisema, kila mwaka wiki ya mwanzo ya Oktoba Dunia huadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja. “Kuanzia Oktoba 3 hadi 7 tutakuwa tukiadhimisha wiki hii, kwa viongozi mbalimbali wa Mfuko, kupita maeneo mbalimbali ya nchi kuungana na wafanyakazi wa huko na kuhudumia wateja.” Alifafanua.


Meneja huyo alisema, katika wiki hii wateja pia watapata fursa ya kutoa maoni yao ili Mfuko uweze kuyafanyia kazi kwa nia ya kuboresha huduma, alisema.

Baadhi ya wakurugenzi na mameneja wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, waliungana na wafanyakazi wa kitengo cha huduma kwa wateja, ili kutoa huduma kwa wanachama waliofika kupatiwa huduma.Mkurugenzi mkuu alipata fursa ya kutoa huduma kwa muda wa dakika 35 na baadaye kutoa barua za pongezi kwa wafanyakazi bora watatu wa kitengo hicho.

Wafanyakazi hao ni pamoja na Afisa Huduma kwa wateja, January Buretta, Afisa Mwandamizi wa Uendeshaji, Hilda Mwema na Afisa Mkuu wa Matekelezo, Matilda Nyallu.

Alitolea mfano hapo makao makuu ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko, Adam Mayingu, naye aliungana na wafanyakazi wa kitengo chake kuhudumia wateja.

“Sambamba na kutoa huduma, lakini pia Wiki hii tutaitumia kuwatunukia wafanyakazi wetu bora katika kitengo hiki.” Aliongeza
Mkurugenzi Mkuu, akimsikiliza Mteja, Devotha Kayumbe,Meneja wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Laila Maghimbi, (kushoto), akimuhudumia mteja
Mkurugenzi Mkuu, akimkabidhi barua ya pongezi, Mmoja kati ya wafanyakazi watatu bora wa ,kitengo hicho, January Buretta, ambaye ni Afisa mwandamizi Huduma kwa wateja wa PSPF
Mkurugenzi Mkuu akimkabidhi barua ya pongezi, Afisa Mkuu wa Matekelezo, Matilda Nyallu
Mkurugenzi Mkuu akimkabidhi barua ya pongezi, Afisa Mwandamizi wa Uendeshaji, Hadija Mwema
Mkurugenzi wa Uendeshaji, wa PSPF, Neema Muro, (kulia), akifuatilia jinsi Afisa Uendeshaji Mkuu wa Mfuko huo, Zeinab Dau, (wapili kulia), wakati akimuhudumia mteja
Meneja Matekelezo wa PSPF, Francis Mselemu, (kushoto), akimuhudumia mteja
Mkurugenzi wa ukaguzi wa ndani, Sosthenes Mushema, (kulia), akimsikiliza kwa makini mteja aliyefika kuhudumiwa Oktoba 4, 2016
Afisa mwandamizi msaidizi wa nyaraka, Gwamaka Ngomale, (kushoto), akimuhudumia mteja
Wateja wakipatiwa huduma na wafanyakazi wa PSPF
Wafanyakazi wa PSPF, sehemu ya call centre wakitekeleza wajibu wao
Picha ya pamoja
Paulina Kagaruki, (kulia), Afisa uendeshaji, akimhudumia mteja
Isack Kimaro, (kushoto), akimuhudumia mteja
Afisa wa Uendeshaji wa PSPF, Elizabeth Shayo, akimuhudumia mteja Oktoba 4, 2016
Hadji Jamadary (kulia), akimuhudumia mkuu wa wilaya wa zamani Lephy Gembe, aliyefika kupata huduma za PSPF Oktoba 4, 2016
Afisa Mkuu Huduma kwa Wateja wa PSPF, Queen Edward, (kulia), akimuhudumia mteja

BANDA LA MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA (TFDA)LAVUTIA WENGI KATIKA MAONESHO YA WAJASILIMALI KANDA NYANDA ZA JUU KUSINI

$
0
0

Kaimu Meneja huduma kwa wateja na Elimu kwa Umma Ndugu Jemsi Ndege akitoa elimu kwa wajasilimali na wananchi waliofika katika banda la Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)Katika maonesho ya wajasilimali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yaliyoandaliwa na SIDO katika viwanja vya bustani ya jiji la Mbeya.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika Maonesho ya wajasilimali Kanda ya Nyanda za juu kusini katika viwanja vya busatni ya jiji la Mbeya wakiwa katika banda la Mamlaka ya Chakula na Dawa( TFDA)
Kaimu Meneja huduma kwa wateja na Elimu kwa Umma Ndugu Jemsi Ndege akitoa maelezo kwa mgeni rasmi aliyetembelea banda la TFDA ,Ndugu Chiwangu Nyasebwa ambaye alimuwakilisha katibu Tawala Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya zoezi la ufungaji wa maonesho hayo ya wajasilimali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mbeya,katika viwanja vya bustani ya jiji la Mbeya .
Mgeni rasmi katika Maonesho ya wajasilimali Ndugu Chiwangu Nyasebwa akizungumza mara baada ya kutembelea banda ya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ambao walishiriki katika maonesho ya wajasilimali kwa lengo la kutoa elimu juu ya ubora wa bidhaa zinazozalishwa na wajasilimali hao .

MJUMBE WA WAZIRI MKUU UINGEREZA NA WIZARA YA NISHATI NA MADINI WAJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI

$
0
0

Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (kushoto) akizungumza wakati wa mkutano huo. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James na katikati ni Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji nchini, Lord Hollick.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kulia) akizungumza wakati wa mkutano wa kujadili fursa za uwekezaji kwenye Sekta ya Nishati nchini hususan nishati jadidifu. Katikati ni Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji kwa Tanzania, Lord Hollick. Kushoto ni Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Sarah Cooke.
Wajumbe kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakifuatilia majadiliano ya fursa za uwekezaji na Ujumbe kutoka Serikali ya Uingereza. Kushoto ni Kamishna Msaidizi anayeshughulikia Umeme, Mhandisi Innocent Luoga akifuatiwa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji- Uwekezaji kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Declan Mhaiki.
Wajumbe wa mkutano uliokuwa ukijadili fursa za uwekezaji katika Sekta ya Nishati nchini wakiendelea na mkutano husika ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (katikati mbele). Upande wa kushoto ni Ujumbe kutoka Serikali ya Uingereza na kulia ni Wataalam kutoka Wizarani.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kulia) akimsikiliza Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji kwa Tanzania, Lord Hollick.
Ujumbe kutoka Serikali ya Uingereza ukiongozwa na Mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza, anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji nchini, Lord Hollick (kulia) aliyeambatana na Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke (wa pili kutoka kulia) wakijadiliana jambo.

WAFANYAKAZI WA WAKALA WA UFUNDI NA UMEME (TEMESA) WATAKIWA KUJITUMA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Bw.Senzo Gwanchele (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa viongozi na watendaji wa wakala huo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa idara ya ushauri wa kitaalam wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Eng. Manase LeKujan (wa pili kulia) akizungumza na viongozi na watendaji wa wakala huo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),Dkt.Musa Mgwatu (Katikati) akitoa maelekezo kwa viongozi na watendaji wa wakala huo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.
Viongozi na Watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), wakimsiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt.Musa Mgwatu (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.

…………………………………………………………

Na Theresia Mwami TEMESA.

Wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wameshauriwa kujituma kwa bidii katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Ushauri huo umetolewa leo na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt Musa Mgwatu alipokutana na watumishi hao kutoka katika Mikoa/vituo vya TEMESA vilivyopo nchi nzima katika kikao kazi kilichofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Dkt Musa Mgwatu amesema kuwa ana muda mchache tangu aanze kutekeleza majukumu yake na ameanza kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Wakala huu na kuahidi kupita katika vituo vilivyopo mikoani ili aweze kujifunza zaidi.

“Naahidi kushirikiana nanyi katika kuijenga TEMESA Mpya na naomba ushirikiano wenu na muwe wafatiliaji wa mambo kwani kazi zetu zinahitaji sana ufatiliaji wa kina” Alisema Dkt Mgwatu.

Ameongeza kuwa amepanga mikakati ya kuiimarisha TEMESA katika maeneo ya Matengenezo ya magari kwenye karakana za TEMESA, namna ya kuyatambua madeni ya TEMESA pamoja na utunzaji wa taarifa zake, utendaji kazi chini ya kiwango wa baadhi ya karakana, mawasiliano kati ya TEMESA makao makuu na mikoa au vituo vyake na utendaji kazi na watu au kampuni zilizosajiliwa.

Amesisitiza kuwa watumishi wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa dhana potofu iliyojengwa juu ya TEMESA kwa wateja wake, wajiimarishe katika utendaji kazi kwa kasi, ubora, weledi uadilifu, ufuatiliaji, na uwajibikaji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za uendeshaji TEMESA Bw. Senzo Gwanchele amesema kuwa kikao kazi hicho kimelenga kuondoa baadhi ya matatizo yanayojitokeza katika utendaji wa kila siku ikiwemo hoja mbali mbali za ukaguzi, ulipaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) pamoja na uzingatiaji wa sheria ya Ununuzi wa Umma.

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) hivi karibuni imepata Mtendaji Mkuu mpya ambaye amekuja na mikakati ya kujenga na kuimarisha TEMESA kwa kupambana na changamoto zinazoikabili Wakala kwa sasa.

DRC kuendelea kutumia zaidi bandari ya Dar es Salaam

$
0
0
 
RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo , Joseph Kabila akiungumza Ikulu leo.

………………………………………
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

RAIS wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo , Joseph Kabila amesema Serikali yake itaendelea kutumia bandari ya Dar es Salaam kupitishia mizigo yake ili kuendeleza ushirikiano na manufaa ya kiuchumi baina ya wananchi wa nchi hizo.

Akizungumza na waandsihi wa habari leo Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Magufuli, alisema kuwa nchi ya Kongo imekua ikitumia Bandari ya Dar es Salaam tangu hapo awali, na sasa wanatarajia kutumia bandari hiyo kwa kupitisha mizigo zaidi.

“Tunatarajia kufanya biashara zaidi na Bandari ya Dar er salaam kwa kupitisha mizigo kwa wingi, miaka ya nyuma tulikua na matataizo kidogo ila kwa sasa kuna kazi kubwa inafanyika ya kuboresha Bandari ya Dar es salaam na sisi tutaweza kupitisha mizigo yetu kwa wingi” alisema Rais Kabila.

Aidha Rais Kabila alisema kuwa katika mazungumzo yake na Rais Magufuli walijadili masuala mbalimbali ikiwemo hali ya usalama katika mipaka ya Kongo na uwekezaji.

Kwa upande wake Rais Magufuli, alisema kuwa katika kuboresha usafirishaji mizigo kwenda nchini Kongo, Bandari ya Dar es salaam imepunguza maeneo ya vituo vya kupima mizigo ambapo kwa sasa kuna maeneo matatu yenye vituo vya kupimia mizigo ambavyo ni Vigawanza, Manyoni na Nyakaliwa.

Ambapo pia Bandari hiyo imeongeza kipindi cha msamaha wa kuhifadhi mizigo bandarini kutoka nchini Kongo kutoka siku 14 hadi siku 30.

Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa biashara kati ya Tanzania na Kongo imendelea kuimarika hadi kufikia shilingi bilioni Tsh. 393.6 kutoka Tsh. Bilioni 23.1 kwa mwaka 2009.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo na Waziri wa Mafuta wa Kongo Mhe. Ngoyi Makena wametia saini mkataba wa makubaliano wa kutafuta mafuta katika ziwa Tanganyika.

Ziara ya Rais wa Kongo nchini inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia pamoja na kukuza maendeleo ya uchumi baina ya nchi hizo mbili.

BENKI YA CRDB YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA NCHI NZIMA

$
0
0


MKURUGENZI wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, amewataka wateja wa benki hiyo ndani na nje ya nchi kutumia vema fursa ya kutoa maoni ya namna ya kuboresha huduma ndani ya benki hiyo.

Mwambapa alitoa kauli hiyo jana wakati akizindua wiki ya huduma kwa wateja Duniani, ambako alizinadi Akaunti mbili za Dhahabu na Thamani, ambazo zimetajwa kuwa na faida na riba kubwa kwa wateja watakaofungua na kuzitumia.

Alibainisha ya kwamba benki yake imejipanga kupokea maoni yote kutoka kwa wateja ambayo yatachakatwa na kufanyiwa kazi ili kuboresha huduma zao kwa wateja ambao ndio mhimili mkuu wa mafanikio ya CRDB.

“Maazimio yetu mwaka huu yako chini ya kauli mbiu isemayo: Tunasikiliza, Karibu, Tukuhudumie. Matarajio yetu ni kuona wateja wakiibeba na kuitumia kauli mbiu hiyo kwa ustawi wa huduma za kibenki tunazowapatia,” alisema.

Aliongeza ya kwamba, benki yake imetumia takribani miaka mitano katika kuiweka kwa vitendo kauli mbiu ya CRDB isemayo: Benki Inayomsikiliza Mteja, hivyo sasa ni wakati wa kupokea mrejesho kutoka kwa wateja juu ya wapi wanakopaswa kuboresha.
Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay (kulia), akimsikiliza mmoja wa wateja wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kulia ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa na wa pili kushoto ni Mdhibiti wa tawi la Azikiwe, Bertha Mwakibete.
Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi (kulia), akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la PPF Tower, Cornell Meseyeck wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto ni Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Saugata Bandyopadhyay na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa.
Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa benki hiyo, Saugata Bandyopadhyay akisalimina na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi (kulia), wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko,Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa na Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la PPF Tower, Cornell Meseyeck wa pili kulia.
Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay (kushoto), akisalimia na mteja wa benki hiyo tawi la PPF Tower, wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.
Naibu Mkurugenzi Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay akisalimiana na wateja wa benki hiyo.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la PPF Tower, Cornell Meseyeck akitoa maelezo kwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Saugata Bandyopadhyay (kulia), alipotembelea tawi hilo kuonana na wateja pamoja na wafanyakazi wa tawi la PPF Tower wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja Duniani.
Ufafanuazi.
Jaji wa Mahakama Kuu Jaji Adam Mambi akikata utepe wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi la Mbeya.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la SAU Mwanza, Denis Moleko akikaribisha wateja.
Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Said Pamui akimuhudumia mteja.
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro mjini akifungua Wiki ya Huduma kwa Wateja katika tawi la Morogoro mjini.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawi la Inyeyeri Bujumbura Burudi wakiwa katika vazi rasmi wakati wa uzinduzi huo.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB tawila Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa Benki ya CRDB tawi la Moshi, Francis Molel akiwakaribisha wateja katika maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.

Imeandaliwa na Habari Mseto Blog

Rais Magufuli na Rais Kabila wafanya mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam

$
0
0

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuriwa na  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mhe. Joseph Kabila Kabange leo tarehe 04 Oktoba, 2016 wamefanya mazungumzo rasmi Ikulu Jijini Dar es Salaam na kisha kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari ambapo viongozi hao wawili wamekubaliana kuendeleza na kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kidugu na kihistoria katika nchi hizi mbili marafiki na majirani.


Katika Mazungumzo hayo Rais John Pombe Magufuli amemuhakikishia Rais Joseph Kabila Kabange kuwa Serikali ya Tanzania imechukua hatua kadhaa za kuimarisha huduma katika bandari ya Dar es Salaam na kupunguza vizuizi vya barabarani hadi kubaki vitatu ili nchi ya Kongo na nchi nyingine za kusini na magharibi mwa Tanzania ziitumie bandari hiyo bila vikwazo.


Dkt. Magufuli amesema Tanzania imejiwekea malengo ya kuhakikisha uchumi wake unakua kwa asilimia 7.2 na kwamba kutokana na hali hiyo anawakaribisha wafanyabiashara wa Kongo kuja kuwekeza nchini Tanzania na wafanyabiashara wa Tanzania kwenda kuwekeza nchini Kongo.


"Mhe. Rais Joseph Kabila Kabange takwimu zinaonesha nchi zetu zinafanya biashara kubwa kwani katika mwaka 2009 tulifanya biashara iliyofikia Shilingi Bilioni 23.1 na imekuwa ikikua mwaka hadi mwaka na hivi sasa tunafanya biashara yenye thamani ya shilingi Bilioni 393.6 kwa mwaka.

"Mimi ningependa kuona sisi ndugu na majirani tunafanya biashara zaidi, wafanyabiashara wa Kongo waje Tanzania kuwekeza na Serikali yangu itawaunga mkono" amesema Rais Magufuli.


Aidha, Rais Magufuli amezungumzia mikakati ya kuimarisha mawasiliano ya barabara na ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) ambapo Tanzania imetenga Shilingi Trilioni 1 kwa ajili ya kuanza ujenzi huo na kwamba hatua hiyo itarahisisha zaidi usafirishaji wa mizigo ya kwenda na kutoka Kongo kupitia bandari ya Dar es Salaam.


Kuhusu mradi wa ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania, Rais Magufuli amesema ni matarajio kuwa Kongo ambayo pia imegundua mafuta katika ziwa Albert itatumia bomba hilo kama ambavyo Tanzania pia inatarajia kulitumia kufuatia tafiti kuonesha uwepo wa mafuta katika maeneo ya ziwa Eyasi na Ziwa Tanganyika.


Kwa Upande wake Rais Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Mhe. Jospeh Kabila Kabange amemshukuru Rais Magufuli kwa mwaliko huu wa ziara ya kiserikali na amemhakikishia kuwa Kongo itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano wake na Tanzania kwa kuwa nchi hizi ni majirani na ndugu tangu enzi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.


Mhe. Kabila amesema Kongo inatambua umuhimu wa kushirikiana na Tanzania katika biashara na uwekezaji na kwamba amefurahishwa na hatua ambazo Serikali ya Tanzania imezichukua kuboresha huduma katika bandari ya Dar es Salaam ambayo ni tegemeo kwa usafirishaji wa mizigo ya Kongo Mashariki na sehemu nyingine za nchi hiyo.


Ameahidi kuwa pamoja na kuwahasisha wafanyabishara wa Kongo kuitumia bandari ya Dar es Salaam, Serikali yake itachukua hatua za kurekebisha kasoro zinazolalamikiwa na wafanyabiashara dhidi ya maafisa wa forodha wa Kongo waliopo hapa nchini.


Rais Kabila amezungumzia mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania akisema nchi yake pia imeamua kutumia bomba hilo kusafirisha mafuta yake iliyoyagundua katika ziwa Albert upande wa Kongo na pia juhudi zinazoendelea kupata mafuta katika ziwa Tanganyika na amesisitiza kuwa ili kufanikisha hilo ushirikiano ni muhimu.


Kuhusu hali ya usalama nchini Kongo, Rais Kabila amesema kwa asilimia 97 nchi hiyo ina usalama na kwamba ni maeneo machache tu ya mashariki mwa Kongo ndiko kuna vikundi vinavyoendesha vurugu.


"Mhe. Rais Magufuli hivi karibuni tutaanza mazungumzo ya kutafuta amani ya kudumu nchini Kongo, na lengo letu ni kuhakikisha nchi inakuwa na amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Desemba ama baada ya mwezi Desemba" amesema Rais Kabila.


Mhe. Rais Kabila amekubali kuupokea ujumbe wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Tanzania, Angola na Msumbiji ambao Mwenyekiti wa asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC - Organ Trioka) Rais John Pombe Magufuli ataituma hivi karibuni kwa ajili kufuatilia hali ilivyo nchini Kongo.


Baada ya mazungumzo rasmi na kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari, Rais Kabila anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la jengo la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) lililopo kando ya Bandari ya Dar es Salaam na jioni atashiriki dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli.





Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

04 Oktoba, 2016

NAIBU KATIBU MKUU WAZAZI TAIFA NAJMA MWITA GIGA AZINDUA OFISI MPYA YA WAZAZI MKOA MAGHARIBI KICHAMA.

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi Taifa Najma Mwita Giga akizungumza na viongozi wa CCM mkoa Magharibi Kichama baada ya kuzindua Ofisi ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa Magharibi, Mwera.

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Najma Mwita Giga akizungumza na viongozi wa CCM na Jumuiya ya Wazazi baada ya kuzindua Ofisi ya Jumuiya hiyo Mkoa Magharibi Mwera.
Viongozi waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia hotuba ya Naibu Katibu Mkuu wa Wazazi Najma Mwita Giga wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Jumuiya hiyo mkoa wa Magharibi.

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Najma Mwita Giga akimkabidhi Komputer na Printer Katibu Mkuu wa Wazazi wa Mkoa wa Magharibi kichama Mohd Abdi baada ya kuzindua Ofisi ya Jumuiya hiyo huko Mwera.

Picha na Salmin Said Nasor/Maelezo Zanzibar.

LUKUVI AKABIDHI BATI 2000 NA POWER TILA KWA MADIWANI WAKE WOTE JIMBO LA ISMANI

$
0
0

Katibu wa mbunge jimbo la Isimani Bw Thom Malenga kulia akimkabidhi diwani wa Mboliboli Khalfan Lulimi msaada wa bati kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miradi ya maendeleo katani kwake msaada huo umetolewa na mbunge Wiliam Lukuvi kwa kata mbali mbali kwa kutoa bati 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 44 na Power tila 15 kwa madiwani wote wa CCM jimboni mwake .
Diwani wa Mlolo Charles Nyagawa kushoto akikabidhiwa bati na katibu wa mbunge wa Isimani Thom Malenga .
Madiwani wakipokea bati
Diwani wa viti maalum Idodi Sophin Msekwa akipokea msaada wa badi

Diwani wa Mlenga akipokea bati


Diwani wa kata ya Malenga makali Flanzisca Kalinga akiwa akijiandaa kuendesha moja kati ya Power tila 15 zenye thamani ya Tsh milioni 105 zilizotolewa na mbunge wa jimbo la Isimani mkoani Iringa Wiliam Lukuvi kwa ajili ya madiwani wote 15 wa CCM jimboni mwake kama miradi yao pamoja na bati 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 44 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya maendeleo jimboni humu wa tatu kushoto ni katibu wa mbunge Lukuvi , Thom Malenga ambae alikabidhi kwa niaba ya mbunge Lukuvi akiwa na baadhi ya madiwani hao

Na MatukiodaimaBlog

MBUNGE wa jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi aametoa msaada wa bati 2000 ajili ya kukamilisha miradi ya kimaendeleo katika kata mbali mbali za jimbo hilo pamoja na kuwasaidia madiwani wote 15 wa chama cha mapinduzi (CCM) Power Tila vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 100.44

Lukuvi alisema amelazimika kukabidhi msaada huo wa power tila kwa madiwani wake ili kuwawezesha kiuchumi pia kusaidia kusukuma maendeleo katika kata zao kama kuwasaidia wananchi kutumia power tila hizo kuendeshea shughuli mbali mbali za kijamii zikiwemo za kilimo.

Kwani alisema kuwa power Tila hizo amezinunua zikiwa na kamili ya vifaa vyake vyote kama jembe la kulimia pamoja na tela zake kwa ajili ya kusafirishia mazao ama kufanyia shughuli nyingine za kijamii katika kata .

Akikabidhi msaada huo leo kwa niaba ya mbunge Lukuvi katibu wake Thom Malenga alisema kuwa kuwa lengo la msaada huo ni kusukuma mbele maendeleo ya wananchi wa jimbo la Isimani na kuwa msaada wa bati unakwenda katika kata zote ambazo zina miradi ya ujenzi wa shule ,nyumba za walimu na zahanati ambazo zilikuwa zikihitaji bati ili kumalizia ujenzi huo na kuwa bati zote ziliotolewa ni 2000 zenye thamani ya Tsh milioni 44

Wakati msaada huo wa power Tila umeelekezwa kwa madiwani 15 wa CCM waliopo katika jimbo hilo na kuwa kila power tila moja imegharimu kiasi cha Tsh milioni 7 na kwa powertila zote zimegharimu Tsh milioni 105 lengo kubwa la kutoa msaada huo ni kuwawezesha madiwani hao kuwa na vitega uchumi na kuongeza ari ya kuwatumikia wananchi wao .

Hivyo alisema kuwa kupitia msaada huo wa bati anaamini madiwani hao wakiwa ni wenyeviti wa kamati za maendeleo ya kata kuhakikisha wanasimamia vema miradi ya ujenzi inayoendelea katika maeneo yao na kwa upande wake mbunge ameamua kutoa msaada huo wa bati kama njia ya kuwapunguzia makali wananchi wake kwa ajili ya kuchangia pesa kununua bati hizo.

" Mheshimiwa mbunge amewaunga mkono wananchi kwa kazi waliyoifanya ya kusimamisha kuta za vyumba vya madarasa na zahanati na kwa ajili ya kuwaunga mkono bati amelazimika kununua "

Hata hivyo alisema kwa upande wa power Tila hizo alisema ni mradi binafsi wa madiwani wake kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wao hivyo kazi ya diwani na kusimamia shughuli za kimaendeleo na pale wananchi wanapohitaji msaada wa power tila hizo basi mwenye mamlaka nazo ni diwani mwenyewe na sio mradi wa kata wala kijiji .

Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Iringa na diwani wa kata ya Mboliboli Khlfani Lulimi akishukuru kwa niaba ya madiwani wenzake alisema kuwa msaada huo ni mkubwa kwao na zaidi wanampongeza mbunge wao kwa kuthamini kazi inayofanywa na madiwani na kuwa watahakikisha power tila hizo zinaleta chachu ya maendeleo katika maeneo yao.

Wakati diwani wa kata ya Malenga Makali FLanzisca Kalinga na diwani wa viti maalum tarafa ya Idodi Sophin Msekwa pamoja na kupongeza msaada huo walisema wanategemea kutumia power tila hizo kwa ajili ya kuwasaidia wanawake na watoto hasa ukizingatia kuwa kumwezesha mwanamke ni kuisaidia jamii nzima.

TEMESA WATAKIWA KUJITUMA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAO.

$
0
0
 Mkurugenzi wa idara ya ushauri wa kitaalam wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Eng. Manase LeKujan (wa pili kulia) akizungumza na viongozi na watendaji wa wakala huo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),Dkt.Musa Mgwatu  (Katikati) akitoa maelekezo kwa viongozi na watendaji wa wakala huo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Bw.Senzo Gwanchele (wa pili kushoto) akifafanua jambo kwa viongozi na watendaji wa wakala huo (hawapo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt.Musa Mgwatu  (Katikati) akitoa maelekezo kwa viongozi na watendaji wa wakala huo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.
 Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt.Musa Mgwatu  (Kulia) akisalimiana na watendaji wa Wakala huo, mara baada ya kufungua kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.
Viongozi na Watendaji wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), wakimsiliza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt.Musa Mgwatu (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa kikao kazi kwa watendaji hao, Jijini Dar es salaam.

Na Theresia Mwami TEMESA.
WAFANYAKAZI wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wameshauriwa kujituma kwa bidii katika kutekeleza majukumu yao ya kazi.

Ushauri huo umetolewa leo na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt Musa Mgwatu alipokutana na watumishi hao kutoka katika Mikoa/vituo vya TEMESA vilivyopo nchi nzima katika kikao kazi kilichofanyika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. 

Dkt Musa Mgwatu amesema kuwa ana muda mchache tangu aanze kutekeleza majukumu yake na ameanza kujifunza mambo mbalimbali kuhusu Wakala huu na kuahidi kupita katika vituo vilivyopo mikoani ili aweze kujifunza zaidi.

“Naahidi kushirikiana nanyi katika kuijenga TEMESA Mpya na naomba ushirikiano wenu na muwe wafatiliaji wa mambo kwani kazi zetu zinahitaji sana ufatiliaji wa kina” Alisema Dkt Mgwatu.

Ameongeza kuwa amepanga mikakati ya kuiimarisha TEMESA katika maeneo ya Matengenezo ya magari kwenye karakana za TEMESA, namna ya kuyatambua madeni ya TEMESA pamoja na utunzaji wa taarifa zake, utendaji kazi chini ya kiwango wa baadhi ya karakana, mawasiliano kati ya TEMESA makao makuu na mikoa au vituo vyake na utendaji kazi na watu au kampuni zilizosajiliwa.

Amesisitiza kuwa watumishi wanapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa dhana potofu iliyojengwa juu ya TEMESA kwa wateja wake, wajiimarishe katika utendaji kazi kwa kasi, ubora, weledi uadilifu, ufuatiliaji, na uwajibikaji. 

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za uendeshaji TEMESA Bw. Senzo Gwanchele amesema kuwa kikao kazi hicho kimelenga kuondoa baadhi ya matatizo yanayojitokeza katika utendaji wa kila siku ikiwemo hoja mbali mbali za ukaguzi, ulipaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) pamoja na uzingatiaji wa sheria ya Ununuzi wa Umma.

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) hivi karibuni imepata Mtendaji Mkuu mpya ambaye amekuja na mikakati ya kujenga na kuimarisha TEMESA kwa kupambana na changamoto zinazoikabili Wakala kwa sasa.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA ALAANI VIKALI MAUAJI YA WATAFITI KITUO CHA UTAFITI WA KILIMO CHA SELIAN CHA JIJINI ARUSHA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la 30 la Kimataifa la Wanasayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu(NIMR), lililoanza leo Oktoba 4 na kilelele chake kukoma Oktoba 6,2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
 
======  =======   =========

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amelaani vikali mauaji ya watafiti WAWILI wa kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Selian cha Arusha na dereva MMOJA waliokuwa kazi katika kijiji cha Mvumi Makulu wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo 4-Oct-2016 wakati akifungua kongamano ya 30 la Kimataifa la Wanasayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesema kuwa tukio hilo ni baya na amewahakikishia watafiti wanaoshiriki kongamano hilo kuwa serikali itachukua hatua stahiki kwa watu waliofanya kitendo hicho cha kinyama ili kukomesha tabia hiyo.

“Haiwezekani hata kidogo watu kufanya mauaji hayo ya kikatili na waachwe bila kuchukuliwa hatua kali za kisheria alisisitiza Makamu wa Rais”

Akizungumzia masuala ya utafiti, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali inatambua kazi nzuri inayofanywa na watafiti hao hivyo serikali itaendelea kutoa mchango wake wa hali na mali ili kuhakikisha watafiti hao wanafanya kazi zao kwa ufanisi unaotakiwa.

Makamu wa Rais pia amewahimiza wafadhili waendelee kusaidia watafiti hasa wanaofanya tafiti za afya nchini kwa sababu tafiti hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa namna ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali.

Amesema kuwa watafiti wanamchango mkubwa katika kuleta maendeleo kupitia matokeo ya tafiti zao nchini hivyo jitihada hizo ni muhimu zikaimarishwa ipasavyo.

Kongamano hilo la 30 la Kimataifa la Wanasayansi lililoandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu -NIMR- linajumuisha watafiti mbalimbali kutoka Ulaya,Afrika na Amerika.

Katika kongamano hilo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika zoezi utoaji wa tuzo kwa wanasayansi waliofanya tafiti mbalimbali za afya nchini.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam. 4-Oct-2016.

RC KAGERA AELEZA JITIHADA ZA SERIKALI KATIKA KUREJESHA HALI BAADA YA TETEMEKO

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWASILI KWA CHANJO NCHINI


NAIBU WAZIRI WA MALIASILI, ENG. RAMO MAKANI AONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA KUTUNDIKA MIZINGA KITAIFA MKOANI PWANI

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani akizungumza na wananchi katika viwanja vya Mwambisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa Mkoani humo. Naibu Waziri Makani ametoa wito kwa wananchi kutumia vizuri fursa ya maeneo ya misitu yaliyotengwa kwa shughuli za ufugaji nyuki kwenye ukanda wa wazi (buffer zone) kwa kutundika mizinga mingi na siyo kutumia maeneo hayo kwa shughuli nyingine za uharibifu wa mazingira kama uchomaji mkaa kwa kuwa kufanya hivyo kutasadia uhifadhi wa misitu na kuongeza uzalishaji bora wa mazao ya nyuki. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu, Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana (wa pili kushoto).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (katikati) akizindua Manzuki ya Makonga katika shamba la Miti Ruvu Kaskazini Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa yaliyofanyika Wilayani humo. Manzuki hiyo itatumiwa kama shamba darasa la kuwaelimisha wananchi juu ya ufugaji wa nyuki kwa njia za kisasa zitakazowezesha kuzalisha mazao bora ya nyuki. Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo, Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana (wa pili kushoto) na Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Daniel Isala (kushoto).
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) akitundika mzinga wa nyuki katika shamba la Miti Ruvu Kaskazini Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa Wilayani humo. Kushoto anaeshiriki nae ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana na kushoto kwa Mkuu wa Wilaya ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Eng. Ramo Makani (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana (kushoto) wakifunga mzinga wa nyuki baada ya kuutundika mapema jana katika shamba la miti Ruvu Kaskazini Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akitundika mzinga katika shamba la miti Mwakonga 2 Wilayani Kibaha jana. Prof. Silayo alisema kuwa kwa sasa Ofisi yake inasimamia jumla ya manzuki 92 zenye mizinga 7,129 ambazo zipo katika kanda 7 na mashamba ya miti manne. Aliongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2015/2016 jula ya mizinga 2,706 ilivunwa na kupata asali kilo 7,129 za asali na kilo 195 za nta. Katika salamu zake Prof. Dos Santos alisema kuwa Asali ya Tanzania imepimwa katika maabara nchini ujerumani na kugundulika kuwa ni asali bora isiyo na kemikali na pia nyuki wa Tanzania hawana magonjwa hivyo asali yake ni salama. Alitoa wito kwa wananchi kutumia fursa zilizopo kufuga nyuki kwa wingi ili kujiinua kiuchumi na kuendeleza uhifadhi wa mazingira nchini.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (kulia) akifunga mzinga huo baada ya kuutundika huku  akisaidiwa na moja ya mfanyakazi wa taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani (wa pili kushoto) akikagua miche ya miti katika shamba la miti Ruvu Kaskazini Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani jana wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa yaliyofanyika Mkoani humo. Shamba hilo lina jumla viriba vya miti milioni moja kwa ajili ya kupandwa katika shamba hilo na maeneo mengine nchini. Kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (wa tatu kulia) na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (kushoto).
 Naibu Waziri Makani akiangalia moja ya mche wa mti unaoota katika kitalu hicho.
Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani (wa tatu kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Grace Procucts Ltd inayojishuulisha na utengenezaji wa vipodozi vilivyochanganywa na asali, Dkt. Elizabeth Kilili jana wakati akaikagua mabanda ya maonesho kwenye viwanja vya Mwambisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani katika Maadhimisho ya Siku ya Kutundika Mizinga Kitaifa yaliyofanyika Mkoani humo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana.
Picha ya pamoja kati ya Naibu Waziri wa Maliasili, Eng. Ramo Makani (wa tatu mstari wa nyuma), Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Asumpta Mshana (wa nne mstari wa nyuma), Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Daniel Isala (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa (kulia), Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (kushoto) na Vijana wa "Skauti" baada ya kuwakabidhi zawadi za asali (mstari wa mbele) muda mfupi baada ya kufunga maadhimisho hayo katika uwanja wa Mwambisi Wilayani Kibaha Mkoa wa Pawani jana.
Naibu Waziri Makani akimkabidhi zawadi ya asali mmoja ya vijana hao wa Skauti. (Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii)

(Na Hamza Temba - Wizara ya Maliasili na Utalii-www.wizarayamaliasilinautalii.blogspot.com)

Kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu kuzalisha lita milioni 2 kwa mwaka.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa Mhe.Salvador Valdes Mesa(kushoto) na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu(katikati) wakimskiliza Meneja Teknolojia wa kiwanda cha Biotec Product Bi.Lourdes Gonzalez kinachozalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani. Picha na Daudi Manongi,MAELEZO .

Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Mlingi Mkucha wakati makamu uyo alipofanya ziara katika kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.Kushoto kwa makamu wa Rais wa Cuba ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu.

Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa akisalimiana na Meneja wa Kiwanda cha Biotec Product ambacho kinazalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria Bw.Alejandro Torres kilichopo Mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) Dkt Samuel Nyantahe akizungumza jambo wakati akimkaribisha Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa katika kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha akizungumza jambo mbele ya Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa wakati makamu uyo alipotembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.Katikati ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu.
Makamu wa Rais wa Cuba Mhe.Salvador Valdes Mesa akisisitiza jambo wakati alipotembelea kiwanda cha kuzalisha viuadudu wa kuua viluwiluwi wa mbu wanaoambukiza malaria mkoani Pwani.Kulia kwake ni Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akifuatiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
………………………………………………………….

Na Daudi Manongi,MAELEZO

Kiwanda cha Biotec Product kilichopo kibaha mkoani Pwani ambacho kinamilikiwa kwa ubia baina ya Serikali za Tanzania na Cuba kimekusudia kuzalisha lita milioni 2 za dawa za viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu waenezao ugonjwa wa malaria nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Cuba, Salvador Valdes Mesa katika kiwanda hicho.

“Kiwanda hiki kitasaidia katika vita yetu ya kupambana na malaria kwa kuwa ni miongoni mwa magonjwa yanayowasumbua Watanzania na Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika kuwatibu wagonjwa” alisema Waziri Ummy .

Waziri Ummy alisema dawa zinazotengenezwa kiwandani hapo zitaisadia tatizo hili na sekta ya Afya kwa kuwa uwezo wa Serikali ni kuzalisha lita milioni 2.5 kwa mwaka na wakati kiwanda hicho kinaweza kuzalisha lita milioni 2 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy alisema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa katika Watanzania 100, watanzania 14 wanapatwa na ugonjwa wa malaria. Aliongeza kuwa dawa hizo zina uwezo kuua viuadudu hivi katika hatua za mwanzo za kuzaliwa kwa mbu na hivyo uzalishaji huo utapoanza utasaidia kupunguza gharama za kutibu malaria, kununua vyandarua na dawa za kuua wadudu wa mbu.

Aidha Sekta ya Afya na Halmashauri zote nchini zitawajibika kununua dawa katika kiwanda hiki kwa sababu wao ndo wadau wakubwa wa sekta hii.

Kwa upande Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) Dkt Samuel Nyantahe alisema dawa zitazozalishwa kiwandani hapo zitauzwa katika nchi za Afrika Mashariki na Afrika nzima.

Akifafanua zaidi alisema Serikali ya Cuba imekubali kusaidia katika kutafuta masoko na hivyo wanategemea kujenga viwanda vingi vya aina hiyo ili kufanikisha adhma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuwa na viwanda.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alisema Mkoa huo umejipanga kuwa mkoa wa viwanda kwa kuwa una ardhi ya kutosha, na pia kiwanda hicho kinatarajia kutengeneza ajira kwa wananchi na hivyo kuwataka wawekezaji kuwekeza katika viwanda.

TAARIFA KWA WATAALAMU WA AFYA WANAOTARAJIA KUANZA MAFUNZO KWA VINTENDO (INTERNSHIP).

ISHA MASHAUZI NA LEYLA RASHID KUPAMBANA OKTOBA 22 DAR LIVE…

$
0
0


Jahazi na Mashauzi Classic kusindikiza

WAIMBAJI wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab kwa hivi sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid watapambana vikali Oktoba 22 ndani ya ukumbi Dar Live Mbagala.

Unaambiwa ni malkia wawili ndani ya jukwaa moja, ambapo Isha Mashauzi atathibitsha kuwa nyeye ni malkia wa masauti matamu huku Leyla akitaka kudhihirisha kwamba yeye ndiye malkia wa taarab.

Mratibu wa onyesho hilo Hajji Mabovu amesema bendi mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla.

Waimbaji hao wawili kwa pamoja wameuthibitishia mtandao huu kuwa wamefikia makubaliano ya kuonyeshana ubabe Jumamosi ya tarehe 22 mwezi huu.

Leyla Rashid amesema anamsikitikia sana Isha Mashauzi kwa kukubali kushiriki mpambano huo kwa vile kwasasa yeye (Leyla) ni maji marefu ambayo kamwe Isha hawezi kuyagoka.

Naye Isha Mashauzi ametamba kuvuna ushindi mkubwa na kuongeza kuwa Leyla ameingia choo cha kiume kwa kukubali mtanange huo.

WAZIRI MKUU ALAANI MAUAJI YA WATAFITI CHAMWINO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake mjini Dodoma, Oktoba 4, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake mjini Dodoma, Oktoba 4, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake mjini Dodoma, Oktoba 4, 2016. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amelaani kitendo cha wanakijiji kuwaua watumishi wa Serikali waliokuwa wakifanya utafiti wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Oktoba 3, 2016) wakati akizungumza na waandishi wa habari wa mkoa wa Dodoma ikiwa ni sehemu ya utaratibu wake wa kukutana na makundi mbalimbali.

Mauaji ya watafiti hao, Teddy Nguma, Jafari Mafuru na dereva wao Bw. Nicas Magazine yalitokea Oktoba Mosi, 2016 baada ya kushambuliwa na wakazi wa kijiji cha Makang’wa wilayani Chamwino mkoani Dodoma.

Amesema Serikali imesikitishwa na mauaji ya watu watatu wakiwemo watafiti wawili kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Seliani (SARI) kilichopo mkoani Arusha ambao walikuwa kazini kuchunguza sampuli za udongo ili kubaini kama matetemeko yataendelea kutokea.

“Kutokana na tetemeko lilitokea mkoani Kagera, Serikali iliamua kushirikisha watalaamu mbalimbali kufanya uchunguzi kuona kama tetemeko hilo ni endelevu au la katika maeneo mengine. Kitendo cha watu kujichukulia hatua mkononi na kukatisha uhai wa watumishi ambao walikuwa kazini hakikubaliki,” amesema

. Amesema watalaamu hao walifika katika Wilaya ya Chamwino na kufanya kazi kwa siku tano na siku ya sita ndipo walipoenda eneo la kijiji cha Iringa Mvumi kuendelea na kazi ambapo waliuawa wakiwa kazini.

“Serikali kupitia kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa inaendelea na uchunguzi wa kuwabaini watu waliofanya kitendo hicho’’ amesema. Hata hivyo, Waziri Mkuu amewatoa wasiwasi watumishi wanaohamia Dodoma kuwa Dodoma ni salama na kila anayekuja yupo salama. “Dodoma ipo salama na tunatarajia kila anayehamia hapa atakuwa salama na hata wakazi wa hapa wataendelea kuwa salama,’’ amesema.

Akizungumzia kuhusu migogoro ya ardhi inayojitokeza katika maeneo mbalimbali nchini, Waziri Mkuu amesema hali hiyo inajitokeza hivi sasa baada ya wananchi wengi kutambua thamani ya ardhi.

Amesema miaka ya nyuma watu wachache walitambua thamani ardhi hivyo kuchukua maeneo makubwa na kuyamiliki. Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa migogoro hiyo inamalizika kwa kuweka kuweka msisitizo kuwe mipango ya matumizi bora ya ardhi ikiwa ni pamoja na kupima ardhi yote na kutoa hati kwa wananchi.

“Tunataka ardhi yote ipimwe na kila mtu anayepewa ardhi apewe hati ya kumiliki na si vinginevyo’’ amesema. Wakati huohuo, Waziri Mkuu aliwaasa waandishi wa habari wawe makini na kazi yao na wajiepushe na upotoshaji kwenye taarifa wanazozitoa kwa wananchi.

Amesema vyombo vya habari ni kiungo muhimu baina ya Serikali na wananchi, hivyo aliwataka viongozi wote wa umma washirikiane na vyombo vya habari kwa kutoa habari za utekelezaji wa kazi za Serikali.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amepokea msaada wa sh. milioni 11.42 kutoka kwa taasisi na wadau mbalimbali mkoani Dodoma zikiwa ni kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17.

Michango aliyopokea leo imetolewa na Mzee Thakar Singh na familia yake sh. milioni 5; NSSF Dodoma (sh. milioni 1.2); Shirika la Bima ya Taifa tawi la Dodoma (sh. milioni moja); Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo (sh. milioni moja) na Ofisi Rais TAMISEMI (sh. milioni 2). Wengine ni TRA-Dodoma (sh. milioni moja); Dodoma FM (sh. 200,000) na Mwalimu Mstaafu, Mama Amina Mafuru aliyetoa sh. 20,000/-.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

S. L. P. 980,
DODOMA. JUMANNE, OKTOBA 04, 2016
Viewing all 46366 articles
Browse latest View live




Latest Images